Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Amuapisha Mrisho Gambo Kuwa Mkuu Wa Mkoa Wa Arusha.......Pia Kakutana Na Rais Mstaafu Wa Benki Ya Maendeleo Ya Afrika (Afdb) Dkt. Donald Kaberuka Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya tukio la Kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wa kwanza (kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa  na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo wa kwanza (kushoto).
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Augusti 20

Vigogo 2 wa NIDA wapata dhamana......Wengine Kuendelea Kusota Rumande

$
0
0

VIGOGO wawili wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) wanaokabiliwa na mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 1.2 wameachiwa kwa dhamana.

Washitakiwa hao ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara, Avelin Momburi na Mkurugenzi wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Joseph Makani.

Hata hivyo, washitakiwa wengine akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Dickson Maimu na wenzake watano wanaendelea kusota rumande.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Respicius Mwijage alitoa uamuzi huo jana kwa kuwa washitakiwa hao wawili hawaguswi katika mashitaka yaliyofunguliwa chini ya Sheria ya Uhujumu Uchumi.

Alisema anakubaliana na hoja za upande wa utetezi zilizowasilishwa na Wakili Johnson Jamhuri kuwa mashitaka yanayowakabili washitakiwa hao yana dhamana na hayahitaji kuombewa dhamana hiyo Mahakama Kuu.

Hakimu Mwijage alisema, washitakiwa wanatakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya Sh mil 200, pia wawasilishe hati zao za kusafiria na hawatakiwi kwenda nje ya Dar es Salaam bila kibali cha mahakama.

Watakaochakachua Mitihani Kidato cha Nne Kukiona

$
0
0
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema haafiki uchakachuaji kwenye mitihani na kusema wakuu wa shule watakaobainika kufanya udanganyifu huo hawatapona.

Profesa Ndalichako alisema hayo kwenye kikao kati ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Maofisa Elimu wa Mikoa, Wakuu wa shule kongwe na wakuu wa shule zilizoungua moto.

Alisema ikiwa imebaki miezi mitatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kufanya mitihani aliwataka wakuu wa shule kujipanga kupata ufaulu mzuri.

“Bado siafiki suala la uchakachuaji kwenye mitihani wanafunzi waachwe wafanye mitihani wenyewe na si kupitia kamati za ufundi, sasa Wizara inaangalia ubora wa elimu na wakuu wa shule watakaokiuka agizo hilo watachukuliwa hatua,” alisema.

Alisema pia matokeo ya mitihani ya shule za sekondari ya mwaka jana yalimhuzunisha sana lakini anaamini wakuu wa shule watajipanga kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri zaidi.

“Nilipokuwa Baraza la Mitihani nilisema nisiulizwe kutokana na matokeo kuwa mabaya lakini sasa niko Wizara ya Elimu siwezi kukwepa hilo tena,” alisema.

Waziri Ndalichako alisema watabadilisha mfumo wa namna maofisa elimu watakavyofanya kazi zao ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule za serikali na kuwataka wakuu wa shule na maofisa elimu kila mmoja ajipange.

Aidha alisema mkuu wa shule ni mdhibiti wa taaluma katika eneo lake na hatakiwi kumuogopa mtu anayemuongoza. Waziri huyo pia alisema katika mtihani wa kidato cha sita uliopita shule 100 za kwanza shule za serikali zilikuwa tatu na kuwa nafasi ya 53 ndio ilishikwa na Ilboru ya Arusha.

“Mpaka namba 100 shule za serikali ni tatu tu, sio kitu cha kawaida hapa ndio mahali pa kuzungumza kama serikali tunashindwa kuonesha mfano tuachie sekta binafsi,” alisema

Tundu Lissu Aibwaga Serikali Mahakamani

$
0
0
Serikali imeendelea kupigwa mweleka katika kesi ya uchochezi dhidi ya mshitakiwa Tundu Lissu baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutupa pingamizi la Wakili wa Serikali wakitaka wakili Peter Kibatala kujitoa kumtetea mwanasiasa huyo. 

Lissu, ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema alipandishwa kizimbani Agosti 5, na kusomewa mashtaka matatu, mawili kati yake yakiwa ni ya uchochezi na moja la kuidharau mahakama. 

Pigo la kwanza la upande wa mashtaka ni pale Lissu alipopangua hoja na kufanikiwa kupata dhamana, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza. 

Jana ilikuwa ushindi mwingine kwa upande wa utetezi, baada ya Mahakama kutupa pingamizi la upande wa mashtaka lililotaka Kibatala ajitoe katika jopo la mawakili wanaomtetea Lissu. 

Upande wa mashtaka ulioongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, uliweka pingamizi hilo kwa maelezo Kibatala ni shahidi wao kwa kuwa alikuwapo siku na mahali wakati Lissu akitoa maneno yanayodaiwa ya uchochezi. 

Wakili Kibatala ambaye ni kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Lissu, alipinga hoja za Serikali za kutaka ajitoe katika kesi hiyo, mvutano ambao ulisababisha kesi hiyo kuahirishwa mara mbili. 

Wakili Kibatala alipinga kuwa hakuna kifungu cha sheria kinachomzuia wakili kumtetea mteja wake kwa sababu tu ya kushuhudia akitoa maelezo yake Polisi. 

Akitoa uamuzi wa pingamizi hilo la Serikali, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha anayesikiliza kesi hiyo, hakukubaliana na hoja za upande wa Jamhuri (mashtaka) na hivyo akalitupa pingamizi hilo. 

Hakimu Mkeha alikubaliana na hoja za wakili Kibatala kuwa hakuna kifungu chochote cha sheria kinachomzuia kumtetea Lissu. 

Alisisitiza kuwa Kibatala ataendelea kuwa wakili wa Lissu katika kesi hiyo na kwamba kama upande wa mashtaka ukimhitaji awe shahidi wao utalazimika kumuomba. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 19.

Mfanyabiashara Moshi Ajimwagia Petroli na Kujipiga Kiberiti

$
0
0
lnawezekana likawa tukio baya lililoacha gumzo na simanzi baada ya mfanyabiashara wa mjini Moshi, Romani Shirima (74), kujiua kwa kujilipua kwa petroli nje ya nyumba yake.

Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli na kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake. 


Ingawa hakuna taarifa rasmi ya nini kiini cha mfanyabiashara huyo kuchukua uamuzi huo mgumu ulioacha maswali mengi, lakini baadhi walidai ni msongo wa mawazo uliotokana na madeni. 

Hili ni tukio la pili kwa mfanyabiashara mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro, kwani miaka kadhaa iliyopita, mfanyabiashara anayemiliki hoteli eneo la Marangu alijilipua kwa petroli akiwa katika gari lake. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema  jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa 11.25 asubuhi maeneo ya Mjohotoni. 

Alisema, mfanyabiashara huyo ni mmiliki wa shule ya sekondari ya Merinyo iliyopo mjini Moshi, na kusema kuwa aliamka asubuhi nyumbani kwake na kujimwagia mafuta hayo na kisha kujilipua na kiberiti. 

Kamanda Mutafungwa alisema chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika ingawa kuna maneno yanayoongelewa na watu, lakini hawawezi kuyachukua moja kwa moja na kwamba jeshi hilo linachunguza ili kubaini chanzo chake.

Taarifa za tukio hilo la aina yake zimekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na vitongoji vyake, hasa njia aliyoitumia kukatisha uhai wake.

Waziri Mkuu Ziarani Katavi

$
0
0

MAPOKEZI makubwa yanamsubiri Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anayetarajiwa kuwasili leo mchana mjini Mpanda kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Katavi inayoambatana na kutembelea, kukagua miradi kadhaa ya maendeleo na kuhutubia mikutano ya hadhara.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa juu wa kitaifa kutembelea mkoa wa Katavi tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani, ziara ambayo itamfikisha pia katika mkoa jirani wa Rukwa.

Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Katavi, Lauteli Kanoni amesema ziara ya Waziri Mkuu mkoani humo itaanza leo na kutarajiwa kuhitimisha ziara yake Agosti 23, mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba, Waziri Mkuu atawasili leo mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Mpanda kisha ataelekea Ikulu Ndogo ambako atasomewa taarifa ya mkoa na kuzungumza na watumishi wa serikali katika viwanja vya ikulu ndogo.

Siku itakayofuata atakwenda katika Kijiji cha Majalila, kunakojengwa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na kutembelea mradi wa maji kijijini humo kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara.

Kwa mujibu wa ratiba yake, anatarajiwa kuhutubia mikutano ya hadhara katika kijiji cha Ndui kilichopo kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba na katika uwanja wa Azimio, Manispaa ya Mpanda.

Aidha, Agosti 22, mwaka huu Waziri Mkuu atafanya ziara ya siku moja katika wilaya ya Mlele ambapo atawahutubia wananchi wa Inyonga katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kabla ya kuelekea katika Kijiji cha Majimoto, Halmashauri ya Mpimbwe atakapokagua ujenzi wa daraja la mto Kavuu na baadaye kuhutubia mkutano wa hadhara.

Waziri Mkuu Majaliwa anatarajiwa kufanya majumuisho ya ziara yake Agosti 23, mwaka huu katika ukumbi wa Idara ya Maji mjini Mpanda kabla ya kuelekea wilayani Nkasi kuanza ziara ya siku tatu mkoani Rukwa.

Tanzania kuachana na nguo za mitumba ifikapo mwaka 2018

$
0
0

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Serikali imeazimia kuachana na biashara ya kuingiza nguo za mitumba kutoka nje ya nchi ifikapo mwaka 2018.

Maazimio hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika uzinduzi wa mafunzo ya uanagenzi ya ushonaji nguo katika kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Company, Ltd.

Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana kwamba ifikapo mwaka 2018 soko la Afrika Mashariki halitaingiza nguo za mitumba kutoka nje. 
 
 Ameongeza kuwa kwa kutekeleza azimio hilo Serikali imeandaa  mafunzo ya kuhakikisha vijana wengi wanapata stadi za kushona nguo nchini ili kuwawezesha kufanya kazi katika viwanda vilivyopo na vitakavyojengwa kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zetu wenyewe na kuacha kutegemea bidhaa kutoka nje.

“Tumejipanga kutekeleza azimio hili na kwa kushirikiana na kiwanda hiki tunategemea kutoa mafunzo ya uanagenzi kwa vijana 2,000 kwa mwaka katika stadi za kubuni mitindo, kukata, kushona na kumalizia nguo” alisema Mhe. Jenista.

Aidha Waziri huyo amewapongeza washiriki wa mafunzo hayo kwani mafunzo hayo yatawasaidia kuendana na viwango vya soko la kimataifa na mahitaji ya soko la nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika kubuni mitindo, kukata na kushona nguo zenye ubora wa kimataifa.

“Imani yangu kuwa wataalamu waliopo katika kiwanda hiki watawapa ujuzi wa kutosha na wengine wataweza kupata ajira katika kiwanda hiki tumieni fursa hii mliyoipata ni ya pekee kwani mmebahatika kuwa miongoni mwa wanafunzi wa kwanza kupata mafunzo chini ya Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini. 
 
Mhe Jenista amesisitiza kuwa mafunzo hayo yatawezesha vijana kupata ajira katika Viwanda, kujiajiri na hata kutoa ajira kwa wengine hivyo vijana watumie fursa hiyo kutengeneza mtaji na kujiunga katika vikundi vitakavyowawezesha  kufungua viwanda vidogo vidogo vya kutengeneza nguo na kuendelea kukuza ujuzi waliopata.

Pia Waziri Jenista ametoa wito kwa viwanda vingine kushirikiana na Serikali kukuza ujuzi kwa vijana kupitia mafunzo ya uanagenzi na kuwahakikisha kuwa Serikali itaendelea kuwawezesha Vijana kupata mafunzo ya aina hiyo.

“Napenda niwahakikishie kuwa Serikali iko bega kwa bega nanyi, fungueni viwanda vingi sehemu mbalimbali katika nchi yetu, sisi kama Serikali tutashirikiana kwa pamoja kuhakikisha rasilimali watu ya kuendesha viwanda hivi inapatikana”

Mbali na hayo Serikali inayo mipango na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya viwanda na kuwa na uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Serikali iliingia makubaliano na kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Co. Ltd kutoa mafunzo ya uanagenzi kwa vijana 2,000 kwa mwaka katika stadi za kubuni mitindo, kukata, kushona na kumalizia nguo .Jumla ya vijana 1,089 waliomba nafasi ya kupata mafunzo hayo yatakayoendeshwa kwa awamu tatu na kwa sasa jumla ya vijana 430 wanapata mafunzo hayo.

Waziri Mkuu Majaliwa Amtembelea Jaji Warioba, Pia Awajulia Hali Spika Wa Bunge, Mh. Job Ndugai Na Mzee Malecela

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Oysterbay jijini Dar es salaam Agosti 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) na kewe Fatma Mganga Ndugai wakati wakati walipokwenda nyumbani kwa Spika Salasala jijini Dar es salaam Agosti 19, 2016 kumjulia hali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakiagana na Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia) na mkewe Fatma Mganga Ndugai (wapili kushoto) wakati walipokwenda nyumbani kwa Spika, Salasala jijini Dar es salaam Agosti 19, 2016 kumjulia hali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomjulia hali jijini Dar es salaam Agosti 19, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomjulia halijijini Dar es salaam Agosti 19, 2016.

Kuweni makini na matapeli wa ardhi Dodoma - Mabula

$
0
0

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amewataka wananchi mkoani Dodoma kuwa makini kabla ya kununua ardhi kwa kuhakikisha wamepita kwenye ofisi za serikali ili kuepuka utapeli.

Akizungumza katika kipindi cha NIPASHE kinachorushwa na Radio One, Mabula amesema kutokana na serikali kutangaza kuhamia Dodoma, ardhi imeanza kuuzwa sana hivyo wananchi wawe makini kwa kuzingatia taratibu na wasiishie kwenye ofisi ndogo za mitaa kwani kama watakuwa hawana ramani wanaweza kununua eneo ambalo limepangiwa shughuli nyingine.

“Wananchi waende Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) ndiyo itawapa ramani za viwanja vya maeneo na shughuli ambazo zinaonekana kwenye ramani tofauti na hapo mtu anaweza kununua ardhi ambayo ni halali na kuepuka ghadhabu ambayo inaweza kuja kutokea baadaye” Amesema Mabula.

Aidha hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu CDA, Pascas Muragili alisema tayari mamlaka hiyo imeshafanya kazi ya kuupanga mji huo hivyo wananchi watakaotoka katika maeneo mbalimbali wawe makini wasije kuuziwa ardhi kinyemela jambo ambalo litawaletea usumbufu na kupoteza fedha zao.

Wizara ya Elimu Yatafuna Mabilioni Kuandaa Hafla HEWA na Malipo HEWA ya Jengo Dodoma

$
0
0

Madudu mengine yameibuliwa katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknlojia baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serilali (PAC) kupitia taarifa za Manunuzi na za kihasibu za wizara hiyo wakati sakata la wanafunzi hewa likiendelea kufukuta.

Kamati hiyo imebaini kuwa shilingi bilioni 1.2 zilitumika kwa ajili ya kuandaa hafla ya harambee ya Wizara hiyo nchini Marekani, tukio ambalo hata hivyo halikufanyika.

Kwa mujibu wa maelezo ya wizara hiyo, harambee hiyo ilitarajiwa kukusanya zaidi ya dola milioni 3 za Marekani ambazo ni sawa na shilingi bilioni 6 za Kitanzania.

Wajumbe wa PAC walihoji matumizi ya fedha hizo. Hivyo, Gerald Mwaja ambaye anahusika na mipango alilazimika kutoa majibu ambayo hata hivyo yalionekana kutowaridhisha wajumbe wa Kamati hiyo.

Alisema kuwa fedha hizo zilitumika kwa ajili ya mradi huo ambao ulikuwa na malengo matatu, kati ya malengo hayo lengo moja la kufanya harambee hiyo lilishindwa lakini malengo mengine mawili yalifanikiwa.

“Mradi wenyewe ulikuwa na malengo matatu; kuongeza matumizi ya teknolojia ya Mawasiliano, kuja na mbinu za kufundishia na pia kukusanya fedha kwa awamu,” alisema.

Alisema malengo mawili yaliyotimia ni kuongeza matumizi ya teknolojia ya mawasiliano pamoja na mbinu ya kufundishia.

Katika hatua nyingine, PAC imebaini kuwa Wizara hiyo ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 2.1 na kuingia mkataba na Kampuni ya Ujenzi ya Magereza mwaka 2014 kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa tatu la ofisi za wizara hiyo Mkoani Dodoma lakini jengo hilo halijajengwa hadi sasa.

Mbunge wa Vwawa (CCM), Josephat Asunga alisema kuwa wamebaini kuwa sheria ya manunuzi ya umma haikufuatwa na kwamba mkandarasi alilipwa kiasi shilingi milioni 780.6 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo hata kabla ya mkataba kusainiwa.

Aliongeza kuwa hakukuwa na maelezo yoyote yanayoonesha kulikuwa na mshindani katika zabuni hiyo huku fedha nazo zikilipwa kwenye akaunti ya mtu aliyetajwa kwa jina la Mang’ula badala ya akaunti ya kampuni ya Magereza.

Pia, Asunga alieleza kuwa kabla ya ujenzi kuanza mwaka 2015, Wizara hiyo ilibadili mpango wa kujenga jengo hilo kwa ghorofa tatu na kuwa jengo la ghorofa nne litakalogharimu shilingi bilioni 4.4.

“Baada ya Rais Magufuli kuagiza kuwa wote tunahamia Dodoma, wamebadilika wanasema hawajapata eneo la ujenzi wakati walishasema awali wamepata eneo,” alisema Asunga.

Aliyekuwa waziri wa Waziri wa Elimu wakati huo, alieleza kuwa hakufahamishwa lolote kuhusu ujenzi wa jengo hilo na kwamba hata muhtasari wa mpango huo hakupewa kwa ajili ya kushauri.

“Mimi kama Waziri sikujua kinachoendelea katika ujenzi wa jengo, na hata briefing (muhtasari) ilikosekana ili niweze kushauri,” alisema.

Akijibu maswali hayo, Afisa Manunuzi wa Wizara hiyo, Audifasy Myonga alikiri kuwa utaratibu wa manunuzi haukufuatwa na kwamba kulipaswa kuwa na mshauri mwelekezi ili kutimiza matakwa ya Sheria.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Hillary Aeshi aliagiza kupitiwa upya kwa mchakato wa zabuni ya Jengo la ofisi ya wizara hiyo mjini Dodoma na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji kwenye ofisi ya Katibu wa Bunge kabla ya Septemba Mosi mwaka huu.

CCM wataka Maalim Seif azuiwe kuhudhuria matukio ya kitaifa

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Serikali kumpiga marufuku Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kuhudhuria hafla na matukio ya kitaifa kutokana na kitendo alichokifanya hivi karibuni kwenye msiba wa Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Aboud Jumbe.

Maalim Seif alikataa kumpa mkono Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein kufuatia msimamo wa chama hicho wa kutoshirikiana na Serikali Visiwani humo, wakipinga kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 na Kufanyika kwa Uchaguzi wa Marudio uliompa ushindi wa kishindo Dkt. Shein baada ya CUF kuususia.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai alisema kuwa ni muda muafaka sasa kwa Serikali kumzuia kushiriki matukio ya kitaifa. Alisema CCM imefadhaishwa na kitendo alichokifanya Maalim Seif na kuwataka watu wote kukilaani.

“Nawaomba watu wasiendekeze sakata hili kwa sababu linamdhalilisha Maalim,” alisema Vuai. “Hatukutarajia kiongozi kama Maalim kufanya kitendo kama kile,” aliongeza.

Hili ni tukio la kwana kwa Maalim kugoma kumsalimia Dkt. Shein. Awali, Dkt. Shein alimtembelea Maalim Seif na kumjulia hali katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam na walizungumza vizuri wakiombeana heri.

Bi Shakila kuzikwa leo, ni baada ya kufariki ghafla Jana Ijumaa

$
0
0

Muimbaji mkongwe wa muziki wa Taarab nchini, Bi. Shakila Said, atazikwa Jumamosi hii. Bi. Shakila alifariki ghafla jana Ijumaa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Rais wa shirikisho la muziki Tanzania, Addo November, muimbaji huyo alifariki ghafla mara baada ya kumaliza kuswali nyumbani kwake, Mbagala Charambe jijini Dar es Salaam. 

Kwa mujibu wa mwanae, Shani, mama yake alianguka na kupoteza maisha na kwamba hakuwa akiumwa. Mazishi yake yanafanyika kwake Mbagala.

Bi Shakila aliwahi kuwika na nyimbo kadhaa ukiwemo ule maarufu, MACHO YANALIA MOYO UNACHEKA aliouimba akiwa na bendi ya JKT miaka ya 90.

Mwaka 1960, aliolewa akiwa na umri wa miaka 11 tu na kuachana akiwa na mtoto mmoja kabla ya kuolewa tena na mwanaume aliyedumu naye kwa miaka 18 na kuzaa naye watoto watano kabla ya mumewe kufariki mwaka 1975.

Alikuja kuolewa tena na mwanaume mwingine aliyezaa naye watoto watano kabla ya kuja kuolewa tena mara ya nne na mwanaume aliyezaa naye watoto wawili. 

Alipokuwa na mimba ya mtoto wake wa mwisho, Shani, mume wake alimwacha. Shani alizaliwa mwaka 1993 na hapo ndipo alidai alichukia wanaume na kuamua kuishi mwenyewe.

Pamoja na kustaafu kazi JKT, Shakila aliendelea kufanya muziki na miaka miwili iliyopita alikuwa akirekodi album yake Mama na Mwana ambayo ingekuwa na nyimbo nane.

BASATA Yatoa Salamu Za Rambirambi Kufuatia Kifo Cha Msanii Shakila

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Msanii wa muziki wa taarab Bi. Shakila Said kilichotokea ghafla nyumbani kwao Mbagala jijini Dar es Salaam jana Ijumaa ya tarehe 19/08/2016.

Shakila ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa na mchango mkubwa katika kukuza muziki wa taarab nchini hasa katika kubuni kazi za Sanaa za muziki mbalimbali ambazo zilikuja kupata umaarufu mkubwa. Moja ya kazi alizobuni na kupata umaarufu mkubwa ni pamoja na 'Macho yanacheka' na 'kifo cha mahaba'.

Mchango wake katika muziki wa taarab hasa katika kubuni na kutunga nyimbo zenye ubora, ujumbe na maadili kwa jamii hautasahaulika kamwe. Ni mwanamuziki aliyeacha misingi katika sekta ya muziki na alijitolea kwa kiasi kikubwa katika kuufikisha muziki wa taarab mahali ulipo leo.

Baraza, wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia marehemu Shakila hasa katika kupenda kujitolea muda mwingi katika kukuza muziki wa taarab na sekta ya muziki kwa ujumla.

Baraza linatoa pole kwa ndugu wa marehemu, shirikisho la muziki, wasanii na wadau wote wa Sanaa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen

Picha: Jeshi la Polisi Likifanya Mazoezi ya Utayari wa Kukabiliana na Uhalifu na Wahalifu Nchini

$
0
0
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wa wakiwa moja ya maozezi yao ya kupasha viungo kabla ya kuanza mazoezi ya kutuliza ghasia.


Askari Polisi wa kikosi maalum cha polisi (CRT) wa mkoa wa Iringa wakiwa katika mazoezi ya utayari wa kukabiliana na matukio yoyote yatakayojitokeza katika maeneo mbalimbali.
Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa mikoa mbalimbali wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kupambana na matukio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu katika maeneo mbalimbali.
Askari wa vikosi vya kutuliza ghasia wa wakiwa na magari yao wakati wa mazoezi ya utayari wa kutuliza ghasia na kukabiliana na matukio yoyote ya uhalifu na wahalifu.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Lindi wakifanya mazoezi magumu ya kijiweka tayari kukabiliana na matukio yoyote yatakayojitokeza ikiwemo watu wasiotii amri za Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kutofuata sheria za nchi.
Askari Polisi wa vikosi vya kutuliza ghasia  wa mikoa ya Lindi, Iringa, kanda maalumu ya Dar es salaam na mikoa mengine wakipokea maelekezo mbalimbali wakati wa mazoezi ya tayari katika kukabiliana na matukio mbalimbali ya uhalifu na wahalifu (Picha zote na makao makuu ya Jeshi la Polisi.)

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 32 na 33

$
0
0
Mtunzi:ENEA FAIDY

.... Shule ya sekondari Mabango ilikuwa na utulivu wa hali ya juu tangu Doreen alipoondoka shuleni pale. Licha ya kwamba kulikuwa na upungufu wa walimu lakini hali ilikuwa shwari kabisa. Wanafunzi waliendelea na masomo yao kama kawaida huku wakimshukuru Mungu kwa kuwaondolea mbaya wao aliyeisumbua shule ndani ya muda mfupi tu.

Majira ya saa saba mchana katika shule ile alifika Mwanaume mmoja wa makamo akiwa ameambatana na  mwanamke mmoja mwembamba mrefu. Wanafunzi wa shule waliokuwa karibu waliweza kugundua kuwa mwanamke yule bila shaka alikuwa ni mama yake Dorice kwa jinsi walivyofanana.  Nadia Joseph aliyekuwa anapita eneo lile la ofisi aliwasalimia kwa heshima kisha akasimama kidogo huku akitafakari jambo alilotaka kuzungumza.
"Samahani mama.. We ni ndugu yake Dorice.." Aliuliza Nadia huku akitabasamu.

"Ndio.. Ni mama yake mzazi.." Alijibu mama yule.
"Oh mmefanana sana... Vipi lakini hajambo?" Aliuliza Nadia akiwa anatabasamu lakini swali lile lilikuwa kama mwiba mkali moyoni mwa Mama Dorice kwani ujio wake pale shuleni ilikuwa ni kumfuata Dorice na kupata taarifa zake kwani ulipita muda mrefu sana bila mawasiliano yoyote.
"Kwani Dorice hayupo hapa shule?" Aliuliza Mwanaume aliyeambatana na Mama Dorice kwa mshangao. Na huyo alikuwa ni mjomba wa Dorice.

"Ah! Unataka kuniambia hayupo nyumbani?" Alishangaa Nadia lakini ndani ya muda mfupi alitokea madam Amina eneo lile hivyo Nadia aliamua kuondoka ili kukwepa adhabu.
Madam Amina aliwasogelea wageni wale na kuwasalimu. Kisha akawakaribisha ofisini. Bila kuchelewa wageni wale waliambatana na Mwalimu Na kuingia ofisini.
"Karibuni sana.. "
"Asante.. Sisi ni wazazi wa Dorice na tumekuja hapa kuuliza binti yetu anaendeleaje?"
"Dorice.. Alikuwa kidato cha nne?" Aliuliza mwalimu.
"Ndio!"

"Mmh! Mbona aliacha shule na tuliwapigia simu mkasema amefika"  alisema Mwalimu  Amina kwa mshangao. Kauli ile iliularua moyo wa mama Dorice na kumfanya achanganyikiwe sana, maana hakuna simu aliyopigiwa wala Kuambiwa chochote kuhusu mwanae.
"We mwalimu umechanganyikiwa? Mbona kama hujielewi eti?" Mama yule wa kinyaturu aliinuka kitini na kuanza kumfokea mwalimu.
Mwalim Amina aliamua kujitetea kwani hali ya hewa ilianza kuchafuka ofisini mle. "Tunamtaka mwanetu.. Mmemtorosha nyie? Au mmemuua?" Alizidi kucharuka mama Dorice.

Mwalimu Amina alikumbuka mbali, akakumbuka siku ambayo Dorice alipotea kisha wakapewa taarifa za upotevu wa mwanafunzi huyo. Barua ya maelezo iliandikwa kisha walimu wakapiga simu kwa wazazi wa Dorice. Lakini kwa bahati mbaya sana simu ilipokelewa na  jini Mansoor kwa namna ya ajabu sana. Na jini huyo aliongea sauti ya Mama Dorice na kuwafanya walimu wajiaminishe vizuri kuwa waliongea na mama Dorice lakini kumbe haikuwa hivyo na hakuna aliyejua siri hiyo zaidi ya Mansoor pekee.

"Mama tena nilipiga simu Mimi.. Na ulikubali mwanao aache shule.." Alijitetea madam Amina lakini hakueleweka.
Wazazi wa Dorice waliondoka kwa hasira sana shuleni pale huku wakiwa hawajui binti yao alienda wapi. Roho iliwauma sana lakini hawakuwa na jinsi. Waliondoka na gari yao waliokuwa wamekodi ikawafikisha kituo cha mabasi Iringa mjini.
 
Walishuka ili watafute sehemu ya kula chakula kwani hawakula chochote tangu asubuhi kisha wakate tiketi, ghafla kwa mbali sana Mama Dorice alimwona msichana kama Dorice. Alijifuta macho yake na kutazama vizuri akamtazama vizuri binti yule.
"Kaka Dorice yule pale"
"Yuko wapi?" Kaka yake alishtuka sana.
"Pale mbele kwenye watu wengi.. Tumfate haraka.." Alisema Mama Dorice akiwa tayari ameanza kupiga hatua kuelekea kule alipo msichana yule.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Agosti 21

Jela miaka 30 Kwa Kumbaka Mwanafunzi wa Miaka 9

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilayani Urambo mkoani Tabora, imemuhukumu Deus Barnaba(45) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumkuta na hatia ya kumnajisi mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye umri wa miaka tisa.

Akitoa hukumu hiyo mwishoni wa wiki iliyopita, Hakimu Mkazi, Baptista Kashusha, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka hivyo kumuona mshitakiwa ana hatia.

Alisema adhabu hiyo iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kufanya vitendo hivyo. Hakimu Kashusha alisema mashahidi nane walioletwa mahakamani hapo walithibitisha kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo.

Mashahidi hao ni pamoja na daktari aliyempokea mlalamikaji na kutoa fomu namba tatu (PF3) iliyoonesha kuwa binti huyo aliumizwa katika sehemu za siri.

Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, ,Joseph Mbwana, alieleza mahakama hiyo kuwa Machi 27, mwaka huu, majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha Mwangaza wilayani Urambo, Deus alimnajisi binti mwenye umri wa miaka tisa na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri.

Aidha, aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili kukomesha matendo ya ubakaji kabisa kwani mtuhumuwa anaonekana ni mtu mwenye akili timamu, alifanya hivyo kwa makusudi tu. 

Hata hivyo, mshitakiwa huyo aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwakuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na ana wazazi, mke na watoto wanaomtegemea.

Janga la Watumishi Hewa: Waziri Asema Wameongezeka na Kufikia 16,127, Ripoti Rasmi Kukabidhiwa Kwa Rais Magufuli Agosti 26

$
0
0
TAARIFA rasmi ya mwisho ya utekelezaji wa kuwaondoa watumishi hewa serikalini na taasisi zake zote, itawasilishwa kwa Rais John Magufuli Ijumaa wiki ijayo na kwamba hadi sasa wameshabainika watumishi hewa 16,127 na wameondolewa kwenye mfumo wa utumishi.

Aidha, mbali ya serikali kuokoa Sh bilioni 16.15 kwa mwezi huu wa Agosti baada ya watumishi hewa hao kuondolewa kwenye mfumo wa utumishi, ambao kama wasingeondolewa fedha hizo zilikuwa ziwalipe mshahara, posho na malipo mengine, waajiri 145 hawajawasilisha taarifa kuhusu uhakiki wao.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la kuwataka waajiri wote wa umma na serikali, kuwaondoa watumishi hewa.

Akifafanua taarifa hiyo, Kairuki alisema Agosti 26, mwaka huu watamkabidhi rais taarifa rasmi ya utekelezaji wa agizo hilo huku akiwataka waajiri 145 ambao hawajawasilisha taarifa za ama uwepo wa watumishi hewa au la, kuhakikisha wanaziwasilisha taarifa hizo kabla ya Ijumaa wiki ijayo.

“Tunawapa muda hadi Ijumaa wiki ijayo wawe wamewasilisha taarifa za kama wana watumishi hewa au la na sisi Agosti 26, mwaka huu ndio tunamkabidhi rais taarifa rasmi ya mwisho ya utekelezaji wa agizo alilotoa,” alisema Kairuki akizungumzia hatua ya Rais Magufuli kuagiza uhakiki huo Machi mwaka huu.

Akielezea hatua zilizochukuliwa hadi sasa na waajiri hao, Kairuki alisema nchi ina jumla ya waajiri 409 wa serikali na taasisi mbalimbali za umma, na kati ya waajiri hao, hadi sasa waajiri 264 ndio waliowasilisha taarifa za utekelezaji wa agizo hilo.

Alisema kati ya waajiri hao 264 waliowasilisha, waajiri 63 wamethibitisha hawana watumishi hewa, huku waajiri 201 wakibaini uwepo wa watumishi hewa kuanzia mmoja na kuendelea.

“Tumepokea taarifa za utekelezaji wa agizo la rais alilitoa Machi 15, mwaka huu na hadi sasa waajiri 264 kati waliotekeleza agizo hilo, 201 wamebaini wana watumishi hewa,” alisema Kairuki.

Akizungumzia hatua zitakazochukuliwa baada ya kufikia tarehe ya mwisho wa kupeleka taarifa hizo, Kairuki alisema jukumu lao ni kuzipokea na kukabidhi mamlaka ya uteuzi ambayo ndiyo iliagiza na ambayo ndiyo itaamua hatua za kuchukua.

Sambamba na hilo, Kairuki alisema hadi sasa jumla ya watumishi hewa 606, wameanza kuchukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo mashauri yao kupelekwa polisi na hivi sasa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), wanafanya uchunguzi na hatimaye watuhumiwa hao wafikishwe kwenye vyombo vya juu vya sheria.

Aidha, maofisa utumishi 233 waliohusika kwenye malipo ya mishahara hewa mashauri yao, wamefikishwa kwenye mamlaka husika kwa uchunguzi, ilhali watatu wamefukuzwa kazi, huku wizara ikiendelea kufanya uchunguzi kwenye taasisi 75 za umma ili kujiridhisha kuhusu suala la watumishi hewa.

Kuhusu waajiri 145 ambao hawajawasilisha taarifa za uhakiki wa watumishi wao, Kairuki alisema zimo taasisi, wakala, bodi, mabaraza, vyuo, hospitali, ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa, tume na mamlaka kadhaa ambazo hazijawasilisha taarifa zao.

Kwa upande wa mabaraza nchini, Kairuki alisema mabaraza mbalimbali 10 hayajawasilisha taarifa za uhakiki wa watumishi na baadhi yao ni kama vile Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), Baraza la Elimu ya Ufundi (Nacte), Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Aidha, jumla ya vyuo vya umma 25 nchini havijawasilisha taarifa zao za uhakiki wa watumishi hewa na baadhi yao ni Dodoma (Udom), Chuo KIkuu Huria (OUT), Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Chuo cha Diplomasia, Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (Duce), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Upande wa Bodi mbalimbali ambazo hazijawasilisha taarifa zao jumla yake ni 10 na baadhi ya bodi hizo ni pamoja na Bodi ya Korosho Tanzania, Bodi ya Tumbaku, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Bodi ya Utalii na Bodi ya Maziwa.

Pia zimo hospitali teule za rufaa tatu ambazo ni Hospitali ya CCBRT, Hospitali ya Rufaa Bugando na Hospitali ya Rufaa KCMC na kwamba katika hospitali kama hizo zilizowasilisha taarifa zake, wamebainika na kuondolewa watumishi hewa 4,000.

Kwenye taasisi za Umma na Wakala ambazo hazijawasilisha taarifa zao jumla ziko 30 na baadhi yao ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mfuko wa Pembejeo za Kilimo, Makumbusho ya Taifa, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Madini la Taifa (Stamico), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Wakala wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).

Pia zipo Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa 12 ambazo baadhi yake ni Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Dodoma, Dar es Salam, Mbeya, Pwani na Kagera; kwa upande wa mamlaka zipo sita ambazo ni Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA).

Aidha, zipo tume 10 ambazo hazijawasilisha taarifa zake na baadhi yake ni Tume ya Pamoja ya Fedha, Tume ya Atomiki, Tume ya Elimu Taifa, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

Pia zipo Mamlaka za Serikali za Mitaa 38 zikiwemo Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Manispaa ya Iringa, Nyamagana, Halmashauri ya Mji, Kasulu, Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi.

Taarifa: Makamu wa Rais, atoa onyo kwa watendaji waochochea uharibifu wa mazingira

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mkutano wa kazi na watendaji wa ofisi yake ya Idara ya Mazingira kujadili kwa kina namna ya kukabiliana na hali tete ya uharibifu wa mazingira unaoendelea nchini.

Katika mkutano huo uliofanyika leo, Ikulu, Dar es salaam ambao ulihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba, Makamu wa Rais ameawaagiza watendaji wa idara hiyo waache kukaa ofisini na badala yake waende kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema hali ya uharibifu wa mazingira ikiachwa iendelee kama ilivyo inaweza ikasababisha madhara makubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla, hivyo ni muhimu kwa makundi yote wakiwamo wataalam wa mazingira na wadau wa maendeleo kuelekeza nguvu zao katika kukabiliana na tatizo hilo.

Alisema baadhi ya watendaji wamekuwa ni sehemu ya uharibifu wa mazingira na kuonya wataobainika kufanya vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali ili kukomesha tabia hiyo.

Baadhi ya watendaji waliotoa taarifa kuhusu hali ya mazingira nchini wamekiri kuwa hali ya uharibifu wa mazingira siyo nzuri hasa kwenye mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Manyara, Geita, Singida na Kilimanjaro.
Inakadiriwa kuwa takribani hekta 400,000 za misitu zinaharibiwa kila mwaka hali ambayo inapelekea baadhi ya wanyama kutoweka.

Watendaji hao wameiomba serikali iongeze bajeti ya kutosha ili waweze kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi.

Makamu wa Rais ametumia siku ya mapumziko ili kujadiliana na kuweka mipango na mikakati ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini. Mkutano huo wa kazi unaendelea tena hapo kesho.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
20/8/2016
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images