Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

VIDEO: Masanja akitoa adhabu kwa wanaochelewa kuoa, kaanza na MC pilipili

$
0
0
Mchekeshaji kutoka kwenye kundi la Original Komedi, Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja Mkandamizaji ambae August 14 2016 alifunga ndoa na mchumba wake aitwae Monica ameifanya hiki kichekesho kifupi akiwa na MC pilipili akitoa adhabu kwa wanaochelewa kuoa.

==> Tazama video hapo chini

Dk. Tulia afunguka, asema Ukawa walimtukana tusi kubwa

$
0
0

SIKU mbili baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuahidi kufanyika maridhiano kati ya uongozi wa Bunge na wabunge wa upinzani katika kikao kijacho kinachotarajiwa kuanza Septemba 6, mwaka huu, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson amesema hataki kuwasikia wabunge wa upinzani wala kuwawaza.

Kauli hiyo ya Naibu Spika huenda ikazidi kutonesha kidonda hasa baada ya Bunge la Bajeti lililofanyika Mei mwaka huu kuacha majeraha kutokana na wabunge wa upinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kususia vikao vyote vilivyoendeshwa na kiongozi huyo.

Juzi wakati akihojiwa kupitia kipindi cha Funguka kinachorushwa na Kituo cha Luninga cha Azam, Spika Ndugai,  alisema anatafuta mbinu ya kuweka sawa mambo hayo kwa kufanya maridhiano  ikiwemo kushirisha maspika wastaafu.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania juzi katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Dk. Tulia alisema hapendi kuwawazia wabunge hao wa upinzani.

“Kwa kuwa Spika yeye kazungumza siwezi kucomment chochote kwa sababu sipendi kuwawazia wabunge hao,”alisema.

Alipoulizwa kwamba ni kwanini migogoro ilizidi wakati yeye akiwa anaendesha vikao, alisema alichokuwa anafuata ni kanuni na kwamba malalamiko hayawezi kukosekana.

“Nashangaa wengine wanasema kuendesha vikao ni mpaka uwe na uzoefu…unajua zile kanuni hata ukipewa uendeshe wewe ukishazielewa hazihitaji uzoefu wowote. Kulalamika kuwa nawapendelea ni jambo la kawaida.

“Kwa mfano siku iliyotokea vurugu wakati wabunge wa upinzani wanadai kutorushwa matangazo ya Bunge live, aliyekuwepo kwenye kiti alikuwa ni mwenyekiti ambaye ni mzoefu wa siku nyingi na ni yeye aliyepeleka majina yao kwenye Kamati ya Maadili, sasa sidhani kama hiyo ni hoja,”alisema Dk. Tulia

Alieleza kushangazwa kwa kitendo cha wabunge wa upinzani katika barua yao waliyomwandikia Spika kwamba hawana imani naye, huku akihusishwa na fedha zilizorejeshwa serikalini.

“Katika ile barua walieleza sababu nyingine kuwa hawana imani na mimi, wakanihusisha na zile Shilingi bilioni 6 zilizorejeshwa serikalini wakati sheria na utaratibu upo wazi kwa sababu Spika au Naibu Spika hauhisiki na masuala ya fedha bali anayehusika ni Katibu wa Bunge.

“Kwa hiyo ni jambo la kushangaza kwamba Naibu Spika karudisha fedha, mimi si mshika mafungu lakini pia ni namna watu walivyopokea huwezi kuwazuia wanavyokuwazia,” alisema.

Akizungumzia kauli ya Spika Ndugai kwamba kwa kuwa Bunge la 11 lina wabunge wapya wengi na kwamba kuwaongoza kunahitaji uvumilivu mkubwa alisema: “Nisingependa kuongelea kauli ya Spika…lakini uvumilivu wa mtu kutakiwa akae hadi mara 11 halafu ameendelea kusimama ni uvumilivu gani huo?,” alihoji.

Pamoja na mambo mengine alisema wakati wabunge wanawake wa Ukawa walipojitoa kwenye  Chama cha Wabunge Wanawake (TWPG), alitukanwa tusi kubwa lakini alinyamaza.

Mei 5, mwaka huu wakati akichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria, Mbunge wa Ulanga Mashariki, Gudluck Mlinga (CCM), alidai kuwa ili kuwa mbunge wa viti maalumu Chadema lazima uwe ‘baby’ wa mtu.

“Laiti ungeona Hansard tusi walilonitukana siku ile, actually Mlinga hajatukana lakini ulisikia nikilalamika mahali kwamba nimetukanwa? wao wanaongee vibaya…watukane, mimi bado ni kiongozi wao na siwezi kuanza kuwakasirikia itakuwa sasa nashindwa kuwaongoza mimi ni kama mzazi wao,” alisema Dk. Tulia.

Alisema kitendo cha watu kudai kwamba anafanya upendeleo bungeni ni changamoto ya kawaida, kwa sababu hata katika mabunge ya Jumuiya ya Madola malalamiko ya aina hiyo yapo.

“Pale bungeni  wako wabunge 389, hawa ni wengi sana wote hawawezi kupata nafasi ya kuongea. Kwa mfano uliomba nafasi jana ukapewa ukaomba leo, hata ukisimama mara 11 katika hali ya kawaida huwezi kupewa kwa sababu wako wengi ambao hawajachangia.

“Kama kiongozi naona ni sehemu mojawapo ya kusimamia jamii ni changamoto na itaendelea kuwepo kwa miaka mitano,”alisema Dk. Tulia.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 21 & 22

$
0
0


Mtunzi:EDDAZARIA G.MSULWA


    Madam Mery akaniwahi kunishika shati na kuanza kuniomba niache vurugu,mkuu wa shule akanyanyuka kwa hasira na kunisogelea na kunizaba kofi lililopelekea nikazidi kupadwa na hasira,Madam Mery akaendelea kuning’ang’ania kwa nguvu zake zote ila kutokana na nguvu nilizo nazo nikajitoa mikononi mwa madam Mery na kumfwata mkuu wa shule na kuanza kumrushia ngumi zisizo na idadi na uzuri zaidi kipindi nipo mdogo baba yangu alikuwa akinifundisha mbinu za kuweza kupigana kiasi kwamba hadi ninakua mkubwa swala zima la kupigana kwangu ni lakawaida.Waalimu wa kiume waliopo eneo la shule wakaja kutuzuia japo kuwa mkuu wa shule ni mzee kidogo ila na yeye alijitahidi kunipa makonde kadhaa yaliyo niingia vizuri sehemu mbali mbali za mwili wangu
 
“Eddy nakuomba uwe mpole kumbuka hapa tupo shule”
Madam Mery alizungumza kwa upole huku nikiondolewa eneo la tukio na waalimu wapatao wanne na kwajinsi nilivyo na nguvu na iliwalazimu kutumia nguvu nyingi katika kunizuia kwenda kuendeleza ogomvi na mkuu wa shule
“Wewe kijana mshenzi sana hujafunzwa huko kwenu hadi unapigana na mume wangu na nitahakikisha shule huna wewe mpumbavu mkubwa weee”
 
Mke wa mkuu wa shule alizungumza maneno yaliyozidi kunipandasha hasira laiti angejua mumewe kitu alicho toka kukifanya jana usiku wala asinge zungumza ujinga anao uzungumza
“Sawa waalimu wangu nimewaelewa ngoja mimi niondoke zangu naombeni muniachie”
 
   Nilizungumza kwa upole na kuwafanya waalimu wa kiume walio nishika kuniachia taratibu na huku wakiniomba niondoke sehemu ya eneo la shule.Kwa haraka nikamsukuma mwalimu wa mbele yangu akaanguka chini nikapata nafasi ya kukimbilia eneo alilopo mkuu wa shule na nikamchomoa katikati ya watu wanao mpa pole na kumpiga kabali moja takatifu iliyotupeleka hadi chini ardhini na watoto wa mjini wenyewe tunaiita kabala ya mbao na kuwafanya walinzi na waalimu wa kiume kuanza kuushika mkono wangu na kuanza kuuvuta kwa nguvu ili kuyanusuru maisha ya mkuu wa shule.Wakafanikiwa kunichomoa huku mwili wangu ukiwa umejaa jasho jingi huku misuli ya mwili mzima ikiwa imetuna kiasi kwamba mtu aliyezoea kuniona kwenye mazingira ya kawaida atabisha kuniona kwenye hali ya hasira niliyo nayo sasa na atasema sio mimi
 
Mke wa mkuu wa shule akaanza kumfuta futa mumewe mchanga kwenye uso wake kiasi kwamba baadhi ya wanafunzi wakaanza kumcheka kwa jinsi anavyo tisha sura kwa kuchafuka.
 
“Oya Eddy tutakuchukulia hatua za kisheria sisi kama shule”
“Tea na wewe mwalimu wa nidhamu ninakumind kama nini sasa na wewe ingia kwenye kumi na nane zangu……Wewe unajua huu ugomvi umetokea wapi au unazungumza zungumza kumpa bichwa huyo choko wenu sifa……”
Nikasimama kwenye sehemu iliyopo juu na kuwafanya watu wote wanitazame kwa umakini huku wakinisikiliza akiwemo mkwe wa mkuu wa shule
 
“Huyo mzee wenu anahabari za kiseng* sana….Kazi yake ni kuwachukua wanafunzi wa kike na kwenda nao kwenye mahoteli makubwa na kufanya nao mapenzi.Ushahidi ninao na kama mwalimu yoyote atake bisha nitautuma kwenye wizara ya elimu tuone kama hii shule haito fungiwa”
Nilizungumza na kumuona Salome akijikatiza katikati ya wanafunzi na waalimu na kuja kupanda sehemu niliyo simama mimi huku akionekana kuwa na asira kali.Nikamtazama kwa jicho kali kiasi kwamba akatulia na kuzidi kuwafanya wanafunzi kuzidi kuongezeka wakitokea mabwenini na madarasani wakitaka kujua ni nini kinacho endelea
 
“Hapa nina gazeti linaelezea mambo ya huyo mzee aliyo yafanya jana usiku isitoshe alitaka kuniua kwa kunipiga na bastola ila kwa bahati mbaya akampiga mpenzi wangu na sasa hivi ninavyo zungumza amelazwa hospitalini”
Minong’ono ya wanafunzi ikaanza kutawala eneo tulilopo na nikaanza kazi ya kuwanyamazisha wanafunzi wezangu na kumfanya mkuu wa shule kuzidi kunitumbulia mimacho ya hasira na kila alipotaka kuondoka mke wake akawa anamzuia asiondoke
 
“Ngoja niwasomee habari ya hili gazeti na mukiwa amuamini nitawawekea video au picha za huyo mzee muone mambo mauvu anayo yafanya…….Kichwa cha habari cha hili gazeti kanasema HEAD MASTER AUA KISA MAPENZI habari ukurasa wa pili ianasema hivii….Mkuu wa shule moja jina tunalihifadhi anajiukuta akiangukia kwenye mikono ya polisi baada ya kumpiga risasi”
 
Nikapunguza sauti ya kulisoma gazeti kwani kitu kilicho andikwa kwenye gazeti kilianza kunichanganya kidogo na nikazidi kukisoma kimya kimya bila mtu kusikia
“Binti mmoja na kumuua kabisa.Muobgozaji wa filamu hiyo inayoitwa SCONGA LOVE imeshirikisha wasanii wengi maarufu kutoka nje na ndani ya mipaka ya Tanzania.Star wa filamu hiyo ambaye amecheza kama mkuu wa shule inasemekana ameweza kuziteka hisia za wasanii wezake alio wafanya nao kazi.Muandishi wetu alikutana na msanii huyo na mahojiano yalikuwa hivi”
 
Nikanyanyua macho yangu na kuwatazama wanafunzi na watu wengine wakisubiria niwasomee kilicho andikwa ndani ya gazeti hilo.Gafla sauti ya Salome ikaanza kusikika kwa sauti ya juu na kunifanya nimtazame
 
“Huu ndi mwisho wa manyanyaso ya wasichana wa kike kwenye hii shule…..Waalimu wengi hapa shule hututumia sisi kama vituliza nyeg* japo wana wake zao na wengine magirl friend zao……Mfano mzuri ni mimi.Jana asubuhi nilimuomba mwalimu wa zamu Pass(Ruhusa) ya kwenda kununua matumizi yangu binafsi kabla sijatoka getini mkuu wa shule akaomba anipe lipfti kwenye gari lake hadi mjini.Sikuwa na hiyana zaidi ya kukubali kutokana tumememzoea kama baba yetu wa kimwili na kiroho”
 
Salome alizungumza huku machozi yakimwagika na kunifanya na mimi niungane na wanafunzi wengine kumsikiliza kwa umakini wa hali ya juu
“Basi tukiwa ndani ya gari alipandisha vioo vyake vya gari lake na kuanza kunitongoza huku akidai atanipa kila nitakacho taka ikiwemo kunivujishia mitihani ya nusu mwaka kwa sisi A LEVEL……….Nilikataa na mwenzangu akazidi kuliendesha gari lake kwa kasi na sikuweza kushuka kwani hata mjini kwenyewe alinipitisha na tukafika kwenye moja ya hoteli na akanitolea bastola na kuniambia endapo nitakataa kushuka ndani ya gari ataniua.Sikuwa na ujanja zaidi ya kufanya kama alicho niagiza.Tukapitliza moja kwa moja kwenye chumba na head master akanilazimisha nifanye naye mapenzi bila kinga…….Na isitoshe aliniingilia kinyume na maumbile”
 
Mwili mzima ukafa ganzi nikabaki niemeduwaa huku wanafunzi wengie wakianza kutokwa na machozi wakimuonea haruma Salome.Ukelele mkali ukasikika katikati ya wanafunzi na ni mke wa mkuu wa shule alizidi kupiga makelela huku akiongea kichaga na kumpiga piga mumewe kwenye kifua
 
“Baba Evance mtoto wa watu umeshamuua wewe si unajijua kuwa sisi ni waadhirika ni kwanini sasa umefanya hivyo baba Evance”
Salome baada ya kuyasikia maneno ya mke wa mkuu wa shule akalegea mwili wake na kabla hajafika chini nikamnyaka na kumlaza taratibu na vilio vya wanafunzi wa kike vikaanza kutawala huku wengine wakidai wametembea na mzee huyo bila kinga na nimiongoni mwa wanafunzi walio ambukizwa virusi vya ukimwi.Waalimu wa kiume wakaanza kumchukua mwalimu mkuu na kumuingiza ndani ya gari la shule na wakaondoka kwa kasi katika eneo la shule kwani wanafunzi walianzisha vurugu za kuwarushia mawe
 
“NANI YUPO PAMOJA NAMI”
Wanafunzi karibia wote wakanyoosha vidole juu akiwemo rafiki yangu John ambaye alikuja wakati wa mwisho mwisho wa tukio na ninavyo mjua alikuwa ametoroka.Wanafuzni wakaanza kurusha mawe kwenye ofisi za waalimu na kuvunja vioo,nikamnyanyua Salome nikisaidiwa na wezake na tukamuingiza ndani ya gari langu huku  John akiingia kwenye siti ya upande wangu huku akijichekesha chekesha.Nikawasha gari na kwa kasi ya hali ya juu nikanza kufwata njia ilipo elekea gari la shule kutokana katika eneo hiko kuna njia moja tu ya kutokea.Kwa mwendo kasi wa gari langu nikaanza kuliona gari alilopanda mkuu wa shule kwa mbali likikata kona kusoto kushika njia ya kuelekea porini kwenye migomba mingi
 
“Eddy na huyo Salome tunakwenda naye wapi?”
“Huko huko”
“Huko huko wapi akitufia mtoto wa watu itakuwaje?”
“Potelea pote ila cha msingi nilazima mkuu wa shule alipe kwa hili”
“Eddy mtu mwenyewe mbona kama haemi”
“John hembu niachie kelele”
Johnalizungumza kimasihara kiasi kwamba ninaona anazidi kunichanganya,Simu yangu mfukoni ikaanza kuita na ninamba ngeni ndio inayo ingia ikanilazimu kuipokea na kuweka loudspeaker
“Eddy mume wangu uko wapi?”
Ilikuwa ni sauti ya Sheila ikizungumza kwa upole
“Baby usijali ninakuja…hii namba ni ya nani?”
“Ni namba ya nesi nimemuomba”
“Umeshakula baby?”
“Ndio mume wangu……nakuomba ndani ya dakika kumi uwe umefika hapa la sivyo nitameza vidonge nijiue kabisa”
“Mke wangu usiseme hibyo”
“Nasema hivyo kutokana nina hamu na wewe na ninahisi upo na mwanamke mwengine”
“No baby naomba usinifikirie vibaaya”
“Sawa ila fanya hivyo nakuesabia dakika mume wangu”
“Sawa”
 
Nikakata simu na kuzidi kuongeza kasi ya gari langu hadi nikafanikiwa kulipita gari alilopo mwalimu mkuu kisha nikalisimamisha gari langu gafla kitendo kilichomfanya dereva wa gari alilopanda mwalim mkuu kunikwepa na kugonga mti mkubwa uliopo pembeni ya barabara nagari lao likasimama kiasi kwamba ndani ya dakika mbili hapakuwa na mtu yoyote aliye shuka kutoka ndani ya gari lao.Nikashuka na kuitoa simu yangu na kuanza kurekodi tukio moja baada ya jengine hadi ninafika kwenye gari la shule nikamkuta dereva wa gari hilo akiomba msaada wa kutolewa ndani ya gari hilo hii nibaada ya kubanwa na mskani wa gari kwenye kifua.Kitu kilicho nishagaza sikuweza kumuona mwalimu mkuu wala waalimu wengine wa kiume walio toroka eneo la shule
 
“Mkuu wa shule yupo wapi?”
“Ni…liwas…shusha…..njiani”
“Wapi?”
“Kul…e kwenye shamb…..a la migomba”
“Fuc*”
Nikamuacha derava akiendelea kubanwa na mskani wake na nikaingia ndani ya gari huku John akifwatia kwa nyuma na kuingia ndani ya gari na kufunga mkanda
“Eddy si tungemsaidia jamaa wa watu”
“Siwezi kusaidia mijitu mipumbavu kama yeye”
“Kwa nini?”
“Hii vita yeye haimuhusu kilicho mfanya aingilie ni nini?”
“Eddy kuwa na roho ya kibinadamu yule jamaa yupo powa sana huwa……”
 
“JOHN KAMA UNATAKA KUMSAIDIA SHUKA NDANI YA GARI LANGU NA UENDE UKAMSAIDIE”
Nilizungumza kwa sauti kali iliyo jaa hasira kiasi kwamba John akastuka na kukaa kimya,Nikageuza gari na kabla sijafika umbali kutoka lilipo gari la shule lilipo pata ajali nikasimamisha gari
“Eddy nishushe nikamsaidie jamaa wa watu”
“Powa shuka”
John akashuka ndani ya gari na mimi nikaendelea na safari ya kurudi mjini huku gari nikiliendesha kwa mwendao wa kasi ili nimuwahi Sheila aliye nipa dakika la sivyo anaweza kufanya kitu kibaya cha kujiua.Kitendo cha kufika hospitli nayo simu yangu ikaita kwa namba ile aliyo nipigia Sheila kwa mara ya kwanza nikaipokea
“Eddy mume wangu hutaki kuja eheee?”
“Nipo hapa nje”
“Kweli?”
“Ndio mke wangu”
“Sawa”
 
Nikamuita nesi mmoja na kumuonyesha Salome tuliye mlaza siti ya nyuma na kumuomba amtoe na kumfanyia huduma ya kwanza.Nikapitiliza moja kwa moja hadi chumba alicholazwa Sheila na kumkuta akiwa ana wasi wasi
“Baby mbona umechelewa”
Nikaanza kumuadisia Sheila kuanzia mwanzo wa tukio hadi mwisho wa tukio lilivyo tokea ila nilimficha juu ya uwepo wa Salome kwenye hospitali hiyo
“Sasa huyo mkuu wa shule yeye yupo wapi?”
“Sijui yupo wapi na mbaya zaidi jana alipo toka kufanya tulio la kukupiga risasi polisi wakamuachia huru”
“Mmmm mume wangu ninakuomba umpotezee”
“Siwezi kufanya hivyo yule mzee anatabia chafu na isitoshe anawaambukiza wanafunzi wa kike HIV kimakusudi”
“Weeee”
 
“Ndio hapa shule wanafunzi wengi wa kike nimewaacha wakili na nahisi ametembea na wengi sana”
“Mmmm kweli huyoo si mtu wa kuacha uraiani.Sasa wewe kama wewe umeamuaje?”
“Hi video nitaituma kwa mama kisha atajua nini cha kufanya”
“Ngoja kwanza ukimtumia mama yeye akikuuliza ulifwata nini hotelini utamjibuje?”
“Nitajua cha kumuambia mimi mama yangu hana neono”
“Mmm mimi ninakushauri usimtumie ni bora ukaituma kwa huyo waziri wa elimu”
“Umesha kula?”
 
“Ndio na wamenichoma sindano ya kukausha kidonda”
“Wamekuchomea wapi hiyo sindano”
“Kwenye makalio”
“Kwahiyo wamekushika mpododo?”
“Bwana Eddy hembu acha utani wako”
“Ngoja nikachukue msosi tangu jana tulipo kule njiani hadi sasa hivi sijaweka kitu mdomoni”
“Sawa mume waangu ila usichelewe kurudi”
Nikamnyonya lipsi Sheila na kutoka nje chumba na kwenda alipo lazwa SALOME na kukuta madaktari wakimshughulikia
“Dokta amepata tazizo gani?”
“Amepata mstuko wa moyo”
“Mmmm kwahiyo itakuwaje?”
 
“Ndio tunamshuhulikia kuurudisha moyo wake kwenye hali yake ya kawaida”
“Sawa dokta kila kitakocho endelea unijulishe kwenye hii namba”
“Sawa”
Nikamuachia daktari namba yangu ya simu kisha nikatoka na kwenda kwenye mgahawa wa karibu na hospitali na nikaagiza chakula na kuanza kula taratibu huku nikitafakari ni nini nifanye juu ya ushaidi wa kumkamata mkuu wa shule.Tv(Luninga) iliyopo kwenye mgahawa Chaneli Ten ikaonyesha habari iliyo wafikia kwa wakati huo(BREAKING NEWS) na kunifanya niache kula na kuitazama kwa umakini.Nikashuhudia jinsi askari wakijitahidi kutuliza fujo zinazo endelea shuleni kwetu huku ofisi za waalimu zikiwa zinateketea kwa moto 

====> Endelea Nayo <<kwa Kubofya  Hapa>>

Waliomzushia kifo Ndesamburo watiwa mbaroni

$
0
0
Polisi wamewatia mbaroni watu watano wanaodaiwa kusambaza taarifa kwenye mitandao ya  jamii kuwa Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo amefariki dunia.

Miongoni mwa waliokamatwa na kuhojiwa na polisi na simu zao kushikiliwa kwa uchunguzi, ni wanachama wa Chadema na maofisa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).

Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa  jana alisema kuwa, uzushi huo kuwa Ndesamburo amefariki dunia, ulisambazwa zaidi kupitia makundi ya WhatsApp.

“Tarehe 29/7/2016 mzee Ndesamburo alifika polisi na kutoa taarifa kuwa katika mitandao ya jamii kuna taarifa na picha yake, inasambazwa kwa kasi kuwa amefariki dunia,” alisema Mutafungwa na kuongeza: 

“Picha hiyo ilikuwa na maneno RIP (Rest in Peace), wakimaanisha apumzike kwa amani. Tulifungua jalada na kitengo chetu cha Cyber Crime (makosa ya kimtandao) kiliingia kazini.”

Alisema watu mbalimbali walihojiwa na polisi wanaendelea kazi hiyo pia watu watano walikiri kupokea ujumbe huo na kuusambaza.

Kamanda Mutafungwa alisema wanaendelea na uchunguzi wa kisayansi kumpata mtu aliyeanzisha ujumbe huo, ambao ulisababisha usumbufu  kwa Ndesamburo na familia yake.

Wanaoendelea kuhojiwa ni Ofisa Usalama wa Kampuni ya Kilimanjaro Airport Development (Kadco) na msimamizi wa waongoza ndege wa Fast Jet Uwanja wa Kia.

Wengine ni wanachama watatu wa Chadema, ambacho Ndesamburo ni Mwenyekiti wake wa Mkoa Kilimanjaro. Katibu wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Basil Lema alithibitisha kuhojiwa kwa wanachama wake na kwamba, anaamini mwanzilishi wa taarifa hiyo ya uzushi hajakamatwa.

Mabasi ya mikoani kugoma Jumapili

$
0
0

CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) kimesema kitasitisha huduma ya kusafirisha abiria kwenda mikoa yote nchini Jumapili ili kufanya ukaguzi wa mabasi yake, hatua ambayo itakuwa sawa na mgomo.

Aidha, Taboa imesema inapinga uamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) kutangaza kuyafungia mabasi yote ya kampuni ya City Boy badala ya moja ambalo lilisababisha ajali mkoani Singida hivi karibuni.

Julai 4, mabasi mawili ya kampuni hiyo yaligongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30 wilayani Manyoni mkoani Singida.

Taboa imesema pia itaipeleka serikali mahakamani kutokana na kufungiwa kwa mabasi hayo kwani kwa mujibu wa sheria, aliyetakiwa kulifungia ni waziri mwenye dhamana na si Sumatra kama ilivyofanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kumaliza kikao cha dharura cha wamiliki wa mabasi ya mikoani, Katibu wa Taboa, Enea Mrutu, alisema hawatakatisha tiketi kuanzia Jumapili ili kujipa muda wa kukagua mabasi yao kama yana uwezo wa kufanya safari ama la.

"Tumeamua kwa pamoja kuwa, kwa sababu tayari tumeshafanya 'booking' ya abiria, kuanzia Agosti 21 mwaka huu, tuanze kufanya ukaguzi wa mabasi yetu kote nchini ili yale ambayo hayana sifa yakae pembeni na yale yanayostahili kusafirisha abiria yafanye hivyo, kuliko utaratibu huu wa serikali wa kuyafungia yote bila kujali gari lililohusika kwenye ajali," alisema Mrutu.

Aidha alisema wanapinga vikali agizo la Sumatra la kuyafungia mabasi 60 ya kampuni 12 kwa makosa ya kusababisha ajali na wanataka mabasi yanayohusika pekee ndio yafungiwe.

Alizitaja kampuni zilizofungiwa mabasi yake kuwa ni Mohamed Trans, City Boy, Ota High Class, Kisbo Safari, Kisbo Express, Lubonelo na Kanda Safari.

Mrutu pia alisema kikao kicho kilipinga azimio la serikali kutaka mabasi yanayoenda masafa marefu kama mikoa ya Mwanza na Mbeya kutumia siku mbili na badala yake yatumie siku moja kama ilivyokuwa awali.

Alitaja azimio la tatu kuwa ni kufunga mfumo maalum wa udhibiti wa magari (Car Track System) ambao utaunganishwa na ule wa Sumatra ili kuliona gari lilipo kwa lengo la kudhibiti ajali.

Aidha, Mrutu alisema wamekubaliana mabasi yote yatatembea kilometa 80 kwa saa moja na 50 pale inapohitajika kama kwenye matuta ili kuepuka ajali.

Alisema wamekubaliana pia dereva atakayehusika kutembea zaidi ya mwendo waliokubaliana, afukuzwe kazi na kumchukulia hatua stahiki.

"Kama magari yetu tutayafanyia ukaguzi na pia kufunga kifaa cha kulionyesha basi na kupunguza mwendo, hakuna haja tena ya kutaka tusafiri zaidi ya siku moja... maeneo wanayoona kuna hatari ya usalama ni bora yakasubiriana na askari wakayasindikiza mpaka yanapokwenda," alisema.

Aliendelea kueleza kuwa wamekubaliana Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, awahakikishie hakuna askari atakayedai mabasi hayo rushwa.

Mrutu alisema wamekubaliana mabasi yasikaguliwe kila kituo ili kuepuka kupoteza muda wakati wakisafiri kwenda mikoani ambako kunasababisha madereva kutembea mwendo kasi ili kuokoa muda waliopoteza njiani.

Viongozi wa Dini Waingilia Kati Oparesheni UKUTA

$
0
0

SERIKALI na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wametakiwa kukaa chini kutafuta suluhu ya mvutano unaoendelea kuhusu operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta) ili kuepusha vurugu kutokea nchini maandamano hayo yatakapofanyika.

Rai hiyo ilitolewa na Taasisi ya Maridhiano inayoundwa na viongozi mbalimbali wa dini jijini Dar es Salaam jana.

Lengo la taasisi hiyo ni kuishauri serikali na kutafuta suluhu na viongozi wa Chadema walioanzisha operesheni hiyo.

Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Mchungaji Osward Mlay, alisema ili kuepuka machafuko yanayoweza kutokea wakati wa kutekeleza operesheni hiyo Septemba mosi, mwaka huu huku Jeshi la Polisi likisema litauvunja Ukutani vyema pande zote mbili zikajadiliana na kupata mwafaka.

"Hakuna jambo lililoshindikana mezani. Sisi kama taasisi ya maridhiano, tunaiomba serikali ikae mezani na viongozi wa Chadema ili kumaliza tofauti," alisema.

Mchungaji Mlay aliongeza kuwa sababu ya kuwashawishi Chadema na serikali kufanya maridhiano ni kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha amani ya nchi inadumu na kuondokana na dhana ya viongozi wa dini kutafuta usuluhishi pindi machafuko yanapotokea.

Alisema wana jukumu la kuwashauri viongozi wote wa serikali pale wanapohisi kunaweza kutokea uvunjifu wa amani na kwamba hawako tayari kukaa kimya pindi wanapoona ishara ya vitendo hivyo kama lilivyo lengo lao.

Mchungaji Mlay pia aliitaka Chadema kusitisha maandamano waliyopanga kufanya na badala yake wakae mezani kuona namna wanavyoweza kudai demokrasia kwa amani badala kutumia njia ya maandamano.

Pia alivishauri vyombo vya dola kuongoza nchi kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosimamiwa na Katiba ya nchi bila kukandamiza demokrasia.

Alisema wananchi pia wanapaswa kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani kama kufanya maandamano yasiyo na tija kwa taifa ili kusitokee vurugu zinazoweza kuhatarisha amani ya nchi.

Naye Sheikh Mohamed Hariri, alisema wanategemea serikali na Chadema watatafuta suluhu badala ya kusubiri machafuko yatokee.

NSSF Yaburuzwa Mahakamani

$
0
0

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limeburuzwa mahakamani na wakazi 87 waliokopeshwa nyumba za mradi wa shirika zilizoko Kijichi jijini Dar es Salaam, wakiiomba lisiwabugudhi hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa. 

 Kesi hiyo imefunguliwa na wakazi hao katika Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, wakilalamikia Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF na Kampuni ya Majembe Auction Mart. Kesi hiyo ilipangwa kutajwa jana mbele ya Jaji Penterine Kente. 

 Wakili wa walalamikaji hao, Benito Mandele, amewasilisha maombi mahakamani hapo kutaka itoa amri ya kutokubugudhiwa na mazingira ya makazi hayo yabaki kama yalivyo hadi kesi yao ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi. 

Katika kesi ya msingi, mbali na NSSF, mlalamikiwa wa pili ni Majembe ambaye hakufika mahakamani. Wakili Mandele alidai kuwa alipeleka wito wa mahakama katika ofisi yake iliyoko Mwenge, lakini hakufanikiwa kumpata kwa kuwa amehamisha ofisi eneo hilo. 

Jaji Kente alisema mahakama inatoa hati nyingine kwa ajili ya mlalamikiwa wa pili ili afike mahakamani kusikiliza kesi dhidi yake. Kesi ya msingi itasikilizwa Oktoba 17, mwaka huu, na maombi ya kutokubughudhiwa yatasikilizwa Agosti 24, mwaka huu.

Wakazi hao kupitia kwa wakili wao, waliamua kukimbilia mahakamani kufungua shauri hilo, baada ya kushindwa kupata ufumbuzi wa madai yao katika Taasisi ya Usuluhishi kutokana na walalamikiwa kutofika. 

Ilidaiwa kuwa wakazi hao waliamua kwenda katika taasisi ya usuluhishi kutokana na mkataba wao kuwataka kufanya hivyo kabla ya kuamua kwenda mahakamani. 

Kwa mujibu wa hati ya madai, wakazi hao wanadai kwamba mlalamikiwa wa kwanza (Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF), ameshindwa kutekeleza makubaliano kwa mradi huo kukosa huduma za kijamii. 

Aidha, wanadai nyumba hizo hazina ubora hali iliyowalazimu wengi wao kutumia fedha zao kufanya ukarabati. 

Wanadai kuwa kutokana na hali hiyo, baadhi ya wakazi wameshindwa kulipa fedha ambazo wanatakiwa kulipa kila mwezi, hivyo Majembe walifika na kuwapatia notisi na kuwatangazia kuwaondoa. 

Wakazi hao wanaiomba mahakama hiyo, kuiamuru bodi hiyo kurejea mikataba, kutambua majukumu ya msingi ya kila upande na nyumba ziwe za kuwawezesha kuishi na kuwe na huduma za kijamii. 

Katika maombi, wakazi hao wanaiomba mahakama hiyo kutoa amri ya hali ilivyo kwa wakazi hao katika makazi hayo ibaki kama ilivyo mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Kiongozi Mkuu Wa Madhehebu Ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin (Tus) Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 17 Agosti, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb(TUS) Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga ambapo Rais Magufuli ameipongeza Jumuiya ya Dawoodi Bohra kwa juhudi kubwa inazofanya katika kutoa huduma za kiroho na pia kushiriki katika maendeleo.

Dkt. Magufuli amewakaribisha wana Jumuiya hiyo kuwekeza hapa nchini hususani katika sekta ya viwanda na pia amewakaribisha katika Maadhimisho ya Jumuiya ya Dawoodi Bohra duniani yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam Mwezi Oktoba 2016.

"Tanzania ni nchi nzuri, tumekuwa na ushirikiano mzuri sana na wenzetu wa Jumuiya ya Bohra, hivyo njooni mfanye biashara na Tanzania,  tumepanga katika kipindi cha mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 Tanzania iwe nchi ya viwanda, kwa hiyo tunawakaribisha kuja kuanzisha viwanda vya kutosha" Amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri inayofanywa na Serikali yake ya awamu ya Tano, na pia ameahidi kuwa Jumuiya ya Dawoodi Bohra ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika maendeleo.

Aidha, Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb amemkabidhi Rais Magufuli hundi ya Dola la Marekani Elfu Hamsini na Tatu (USD-53,000) sawa na Shilingi Milioni 116 za Kitanzania kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati ya wanafunzi kwa shule mbalimbali hapa nchini na pia amekabidhi hundi ya Dola za Marekani Elfu Ishirini na Moja (USD-21,000) sawa na Shilingi Milioni 46 kwa ajili ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amepokea barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi Mhe. Brahim Ghali iliyowasilishwa na Mjumbe Maalum wa Rais huyo ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Bachir Moustapha Sayed.Pamoja na kupokea barua hiyo Rais Magufuli amesema Serikali yake ya Awamu ya Tano itaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake na Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi na pia itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi wa Saharawi kupata haki ya kuamua hatma yao.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
17 Agosti, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha  Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wakwanza kushoto.(Katikati ni mkalimani)
 Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin akimuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuchangia madawati kwa kutoa hundi yenye thamni ya dola za Kimarekani (USD 53,000) kwa ajili ya utengenezwaji wa madawati.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuchangia madawati kwa kutoa hundi yenye thamni ya dola za Kimarekani (USD 53,000) kwa ajili ya utengeezwaji wa madawati. Wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir watatu kutoka kushoto na Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum wa kwanza kushoto.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir,  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na viongozi wengine wa BAKWATA na wa madhehebu ya Bohora.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir pamoja na viongozi wengine wa Madhehebu ya Bohora.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin kabla ya kuondoka Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuagana na  mgeni wake Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe uliotoka kwa Rais wa Saharawi na kuwasilishwa kwake na Mjumbe Maalum Bachir Moustapha Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

Vyuo vikuu vilivyopokea fedha ambazo wanafunzi hawapo vyuoni vyapewa siku saba kurejesha fedha hizo

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof.  Joyce Ndalichako ametoa siku saba kuanzia Agosti 17, 2016 kwa vyuo vikuu kurejesha fedha zilizopokea ambazo ni za wanafunzi ambao hawapo chuoni.

Prof.  Ndalichako ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya taarifa la zoezi la uhakiki wa wanafunzi wanufaika wa mikopo vyuo vya Elimu juu.

Prof.  Ndalichako amesema kuwa uhakiki wa wanafunzi hao umefanyika katika vyuo 31 kati ya vyuo 81 vilivyopo nchini.

Katika utafiti huo wanafunzi 2,192 wameshindwa kuhakiki majina yao, hivyo kushindwa kuthibitisha uwepo na uhalali wa wanafunzi hao.

“Mikopo ya Wanafunzi hao imesitishwa na kwa wale ambao ni wanafunzi halali lakini walishindwa kujihakiki itabidi waombe tena mkopo,” alifafanua Mhe. Ndalichako.

Ameendelea kwa kusema kuwa, kwa mwaka wa fedha 2015/16 wanafunzi hao hewa wameigharimu Serikali kiasi cha shilingi 3,857,754,460.

Kutokana na mambo yaliyobainika Serikali imechukua hatua zifuatazo
  1. Vyuo vikuu ambavyo vimepokea fedha za wanafunzi ambao hawapo chuoni vinatakiwa virejeshe fedha hizo ndani ya siku saba kuanzia August 17 2016
  2. Vyuo vya elimu ya juu vinaagizwa kuweka mfumo mzuri wa uhifadhi wa kumbukumbu za wanafunzi kuanzia usajili, matokeo ya majaribio na ya mitihani na namba za akaunti za benki ambapo fedha za mikopo hilipwa.
  3. Vyuo vikuu vinaagizwa kuwasilisha bodi ya mikopo, kwa wakati taarifa zote za kitaaluma na za kibenki za wanafunzi ili kuiwezesha kufanya marekebisho stahiki katika kumbukumbu zao na kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
  4. Bodi ya mikopo inapaswa kuchambua na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa za wanafunzi kama zilivyopelekwa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
  5. Hatua kali za kinidhamu zichukuliwe na kuingiza mara moja mabadiliko ya taarifa za waafunzi kama zilivyopokelewa kutoka vyuoni ili kuepusha ulipaji wa fedha kwa wanafunzi wasiostahili.
  6. Vyuo viweke utaratibu mzuri wa kudhibiti malipo kwa wanufaika wa mikopo ili kuepuka kufanya malipo kwa wanafunzi hewa.
  7. Wakuu wa vyuo ‘VCs’ na Principals’ waweke mfumo wa kuhakiki usahihi wa matokeo ya wanafunzi yanayotumwa bodi ya mikopo na watawajibika kwa usahihi wa taarifa zinazowasilishwa kwani zoezi la uhakiki limebaini kuwepo kwa usdadanganyifu mkubwa kwenye matokeo ya wanafunzi; wapo ambao hawakufanya mtihani au waliofeli lakini wameandikiwa PASS ili waendelee kupata mikopo.
  8. Uchunguzi zaidi utafanyika kwa miaka iliyopita ili kubaini fedha za mikopo ambzo zimelipwa kwa watu wasiostahili. Hatua hii inatokana na matokeo ya uchunguzi ambao umebaini kuwa wapo baadhi ya wanafunzi waliohitimu tangu mwaka 2013 lakini wameendelea kupokea fedha na wengine waliofukuzwa kwa kushindwa masomo tangu mwaka 2013/14 lakini bado wamelipwa hadi mwaka 2015/16.

Makubaliano ya Simba na MO Dewji kuhusu kuiendesha Simba katika mfumo wa hisa

$
0
0
August 15 2016 kamati ya utendaji ya Simba ilikutana na mfanyabiashara na mkurugenzi mtendaji mkuu wa makampuni ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL) Mohammed Dewji  ambaye aliomba kununua asilimia 51 ya hisa za Simba kama mfumo ukibadilika na kuanza kuendeshwa klabu hiyo kwa hisa, leo August 17 Simba wametoa makubaliano yao walioafikiana katika kikao chao cha pamoja.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Apokea Madawati Toka Kwa Balozi Wa Kuwait Nchini.

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa sh. milioni 12 kutoka mashirika ya misaada ya Kuwait kwa ajili ya kununulia madawati ili kupunguza tatizo hilo nchini. Pia amepokea madawati 100 kutoka ubalozi wa Kuwait na taasisi ya Direct Aid ya nchi hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo leo (Jumatano, Agosti 17, 2016), Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Bw. Jasem Al Najem amesema msaada huo ni michango kutoka mashirika ya misaada ya nchi yake ambayo yanatoa huduma mbalimbali hapa nchini.

“Tumejipanga kukamilisha ahadi ya madawati 600, tunaendelea kuwasiliana na wenzetu wa Kuwait Fund, na mashirika mengine. Kwa sasa tunachangia madawati, baadaye tutakwenda kwenye ujenzi wa madarasa, hata ikibidi tutaenda kwenye ujenzi wa shule,” alisema.

Balozi Najem amesema wanatoa misaada hiyo ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Magufuli za kutaka wanafunzi wote wakae kwenye madawati.

Akitoa shukrani mara baada ya kupokea msaada huo, Waziri Mkuu alimshukuru Balozi wa Kuwait kwa moyo wao wa kujitolea ikizingatia kuwa ni wiki tatu tu zilizopita alikwishatoa msaada mwingine wa madawati kwenye shule ya msingi Chamazi, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.

Aliyashukuru pia mashirika ya misaada kupitia Ubalozi huo, ambao wametoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati. Ametoa wito kwa mabalozi wengine, sekta binafsi na wadau wa maendeleo watoe michango zaidi ili yapatikane madawati ya kutosha.

Mashirika yaliyotoa michango hiyo ni African Relief Organisation (hundi ya sh. milioni 6), Al Furqaan Islamic Centre (hundi ya sh. milioni 6), Taasisi ya Direct Aid (madawati 50 ya shule za Msingi) na ubalozi wa Kuwait (madawati 50 ya shule za sekondari).

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.

JUMATANO, AGOSTI 17, 2016.

Wakuu Wa Shule Za Msingi 68 Kuvuliwa Vyeo Vyao Jijini Dar Es Salaam.

$
0
0

WALIMU wakuu wa shule 68 wa shule za Msingi wanatakiwa kuvuliwa  na kunyang'anywa vyeo vyao kwa kosa la udananyifu wa takwimu za wanafunzi  hewa tangu elimu itangazwe kuwa bure.

Hayo yamesemwa na  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum  Hapi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. 

Amesema kuwa walimu wakuu hao wametakiwa kuvuliwa vyeo vyao na kuwapa walimu wengine kwa kosa la kutoa takwimu za wanafunzi hewa 3462 wa shule za  msingi 68 za Wilaya ya Kinondoni. Pia hatua kali za Kisheria zitachukuliwa kwa dhidi ya walimu wakuu wa shule hizo.

Pia Hapi amemwomba Katibu Tawala wa Mkoa kuwavua vyeo wakuu wa shule 22 wa shule za Sekondari 22 za Manispaa ya Kinondoni na Ubungo kwa kosa la kutoa takwimu za uongo na kuweka wanafunzi hewa.

Wakuu wa shule za Msingi hao wamekuwa na wanafunzi hewa 2534  kutoka shule 22 za Sekondari za Manispaa ya Kinondoni na Manispaa ya Ubungo.

Wakuu wa shule hizo wameisababishia Serikali kupoteza zaidi ya shilingi milioni 60 kwa kupeleka fedha za kuwahudumia wanafunzi wanaosoma katika shule hizo.

Baadhi ya shule za sekondari zilizokutwa na wanafunzi hewa ni Boko wanafunzi 74, Bunju B155, Goba Mpakani 42 na Hananansifu wanafunzi 154. Na shule za Sekondari ni Msisiri B wanafunzi hewa 395, Upendo 273 na Ubungo Msewe 267.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Agosti 18

Wenye Akaunti ‘ FEKI ’ Mitandaoni Kukiona-TCRA

$
0
0

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa Nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia majina na taarifa za uongo.

James Kilaba Kaimu Mkurugenzi wa TCRA amesema, vitendo vya watu kujisajili katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi, ni kosa kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kilaba ameyasema hayo jana, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na Kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa nchini (TZ-CERT).

“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” alisema Kilaba.

Kampeni hiyo ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao, itafanyika kupitia matangazo ya redio, televisheni, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo katika mitandao ya kijamii itajulikana kama, “Darasa mtandao”.

“Miongoni mwa mambo ambayo tutawafundisha wananchi ni kutoweka wazi taarifa zao binafsi zote katika mitandao, kubadili na kutunza neon la siri (password), kutojibu ujumbe unaosema umeshinda bahati nasibu na mengineyo mengi,” alisisitiza Kilaba.

Polisi Watuhumiwa Kufanya Vurugu, Kubambika Kesi

$
0
0
WATU wanaosadikiwa kuwa ni polisi mkoani Shinyanga wanadaiwa kuanzisha vurugu baada ya kuagiza chipsi na kukataa kuzilipa, kisha kuanza kuwapiga wauzaji na kuwabambikizia kesi.

Tukio hilo linaelezwa kuwa lilitokea hivi karibuni katika eneo la Mshikamano, kata ya Ngokolo, katika Manispaa ya Shinyanga majira ya usiku, wakati askari hao wakidaiwa kwenda kwa muuza chipsi kwa ajili ya kununua.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Salumu Saidi ambaye ni muuza chipsi aliyedai kufanyiwa vurugu, alisema askari hao walikuwa zaidi ya wanne, lakini wawili ndio walioomba wakaangiwe chipsi.

“Wakati naweka chipsi katika chombo cha kukaangia walianza kula kabla ya kuiva na nilipotaka kuweka mayai waliniambia niongeze kwa madai kuwa ni ndogo na ndipo nilipokataa kwa kuwa kipimo ni hicho, lakini walikataa kulipa,” Saidi alisema.

Alidai kuwa baada ya mzozo kuibuka, mteja mmoja aliyekuwa ndani ya duka lililopo karibu na biashara hiyo, aliwasili na kuulizia kuhusu malipo huku akiwa amelewa na kuanzisha vurugu, lakini ghafla gari la Polisi lilifika kwenye eneo hilo na kumbeba hadi kwenye kituo cha Polisi alikofunguliwa kesi ya unyang’anyi wa kutumia nguvu.

Kwa upande wake, muathirika mwingine wa tukio hilo, Dotto Machunda ambaye ni muuza matunda katika eneo hilo, alisema aliona vurugu katika maeneo ya Darajani na baadaye kuona polisi katika kibanda chake ambao walianza kumpiga na kisha kuondoka na kurejea kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi.

“Niliambiwa nivue mkanda na kuwekwa ndani kuunganishwa kwenye makosa, lakini mpaka leo hii sijapata matibabu, niliwaomba PF3 nikatibiwe walikataa wakati nipo ndani na nilipotoka walininyima pia. Nilipokwenda hospitali ya mkoa kutibiwa waliniambia kwa kuwa nimepigwa mpaka PF3, mpaka sasa sijapata matibabu,” alisema Machunda.

Mwenyekiti wa Mtaa lilipotokea tukio hilo, Victor Ochieng, alikiri kujua tatizo hilo na kwamba alikwenda kwenye eneo la tukio kupata maelezo ya wananchi wake kisha kufika Kituo cha Polisi kujua kinachoendelea.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huu, Muliro Jumanne, alikiri kupokea taarifa lakini alieleza kuwa alizozipata zilihusu askari wao kuvamiwa na wananchi.

Alisema hata hivyo uchunguzi unaendelea kubaini wahusika wa tukio hilo ili sheria ichukue mkondo wake, kwa sababu hakuna anayeruhusiwa kufanya vurugu hata kama ni polisi.

Mbaroni kwa Kuua na Kufukia mwili Chooni

$
0
0
POLISI mkoani Kilimanjaro inawashikilia watuhumiwa watano kwa tuhuma za kumuua kwa kukusudia mwanamke Neema Ndewera (65), kwa kumchoma kisu shingoni na sikio la kulia.

Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Willbrod Mutafungwa, watuhumiwa hao walifanya tukio hilo la kinyama Julai 10, mwaka huu ambapo baada ya tukio hilo walifukia mwili wa marehemu kwenye shimo la choo cha nje ya nyumba yake.

Alisema Ndewera alikuwa akiishi peke yake katika kata ya Mbokomu, ambako Juni mwaka huu aliaga anasafiri kwenda Arusha kuwaona watoto wake, ambapo alimuomba jirani yake Michael John kuwa mwangalizi wa mifugo yake ambayo ni mbuzi wawili, ng’ombe mmoja na kuku.

Alisema mwanzoni mwa Julai, alirudi nyumbani kwake na kukuta mbuzi na kuku wameuzwa, hali iliyomlazimu kumuuliza John kuhusu suala hilo ambalo hakupewa majibu ya kuridhisha. 

Mutafungwa alisema kutokana na hali hiyo Julai 10, John akishirikiana na watuhumiwa wenzake, wote kwa pamoja walimuua Ndewera ili asiwashtaki kwa wizi wa mifugo.

Alisema baada ya tukio hilo watuhumiwa hao waliuza ng’ombe aliyebaki kwa Sh 400,000 kisha kugawana fedha, ambapo walidanganya kuwa Ndewera anaumwa na amesafiri kwenda Dar es Salaam kwa mtoto wake kwa matibabu.

Alisema Agosti 12, Polisi ilipata taarifa hizo kutoka kwa raia wema, ambapo walifika eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umefunikwa kwenye shimo la choo ukiwa na kisu shingoni, ambapo uchunguzi ulifanywa na madaktari na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu.

Kamanda aliwataja watuhumiwa wa tukio hilo ni John (24) fundi ujenzi, Nevance Reginald (46), Mussa Issa (23), Fausta Naftari (29) na Magreth John (53), wote wanne wakijishughulisha na kilimo.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wenzake 8 Wafikishwa Mahakamani

$
0
0

ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu na maofisa wengine saba waandamizi, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka 27 yakiwamo ya matumizi mabaya ya ofisi na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni 1.2.

Washitakiwa wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Kibiashara, Avelin Momburi, Meneja wa Fedha na Uhasibu, Benamini Mwakatumbula, Meneja wa Bajeti na Milki, Joseph Makani, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima na Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond.

Wengine ni Xavery Kayombo ambaye wadhifa wake haukutajwa, na Astery Ndefe ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers Company Limited. Washitakiwa hao pia wanakabiliwa na mashitaka yanayohusu kutumia nyaraka zenye kusudio la kudanganya na kula njama za kutenda kosa.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage, washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote dhidi ya mashitaka hayo kwa sababu wanashitakiwa chini ya Sheria ya Uhujumu Uchumi. Wote waliamuriwa kurejeshwa mahabusu hadi Agosti 31, mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.

Uchunguzi wa kesi hiyo kwa mujibu wa waendesha mashitaka, wanaoongozwa na Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Awamu Mbangwa haujakamilika. 

Hakimu alisema kwamba suala la dhamana litaamuriwa na Mahakama Kuu, kwa kuwa kiwango cha fedha katika kesi hiyo kinazidi Sh milioni 10.

Lakini alisema atatoa uamuzi kuhusu dhamana kwa washitakiwa Mobuli na Makani kesho kwa sababu ya hoja kwamba wawili hao hawakabiliwi na mashitaka ya uhujumu uchumi, kama washitakiwa wengine. 

Jopo la waendesha mashitaka linawajumuisha pia Leonard Swai, Janeth Machuria, Joseph Kiula na Fatma Waziri.

Waendesha mashitaka walidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2010 na 2015, wakiwa watumishi wa umma, Maimu na Mwakatumbula walitumia vibaya madaraka yao kwa kuidhinisha kwa Kampuni ya Gotham International Limited malipo ya Dola za Marekani milioni 5.175 pamoja na Sh milioni sita.

Serikali Kuchunguza Mali za Vigogo 500.........Wamo Wabunge, Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi

$
0
0

WAKATI takribani asilimia 20 ya viongozi wa umma kwa mwaka 2011 hadi mwaka jana hawakuwasilisha matamko ya mali zao kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa wakati, mwaka huu serikali imetangaza kuhakiki matamko ya mali za viongozi 500.

Aidha, serikali hiyo imebainisha wazi kuwa haitowafumbia macho viongozi, watakaoshindwa kuwasilisha matamko ya mali zao kwa mujibu wa sheria, ikiwemo viongozi watakaowasilisha matamko ya mali yatakayobainika kuwa na udanganyifu.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki wakati akifungua warsha ya wadau, kujadili taarifa ya matokeo ya utafiti kuhusu hali ya maadili nchini Dar es Salaam jana.

Kairuki alikiri kuwa hata katika tafiti nyingine ndogo, zilizofanyika kuhusu hali ya maadili nchini pamoja na takwimu kubadilikabadilika, lakini zilibainisha kuwepo kwa viongozi wasiowasilisha matamko yao ya mali na wengine kutowasilisha kwa wakati.

Alisema taarifa hiyo ya utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi nchini kwa miaka mitano kuanzia 2011 hadi mwaka jana, ilibainisha kuwa pamoja na kuwepo kwa mwamko wa viongozi kuhusu suala zima la maadili, bado asilimia 20 ya viongozi hao wa umma hawakuwasilisha matamko yao ya mali kwa wakati.

“Tumepokea taarifa hii na imetutia hamasa kwa kweli, tumeona asilimia 20 hawarejeshi kwa wakati matamko yao, hawa ni wengi sana ikizingatiwa kuwa ni viongozi, tunatoa onyo hakuna atakayefumbiwa macho endapo atakiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kwani atachukuliwa hatua stahiki za kisheria,” alisisitiza.

Alisema kwa kawaida endapo kiongozi asipowasilisha tamko la mali zake hadi ifikapo Desemba 31, huhojiwa na Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, lakini pia inapothibitika kuwa alikiuka kwa makusudi sheria hiyo ya maadili ya viongozi huchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema mwaka huu, kuna jumla ya viongozi wa umma 15,624 kati ya hao viongozi 500 tayari wameshatengewa fedha kwa ajili ya mali zao kuhakikiwa na endapo fedha zitapatikana idadi hiyo inaweza kuongezeka na kufikia 1,000.

“Miaka ya nyuma tulikuwa tunahakiki kwa mwaka viongozi 100 hadi 200, safari hii tumejipanga kuanza na viongozi 500. Lakini katika hili tunaomba wananchi nao watusaidie kuhakiki mali za viongozi hawa wa umma kwani sheria inawa ruhusu kufanya hivyo, ili kuweza kubaini viongozi wadanganyifu,” alisema.

Akiwasilisha matokeo ya utafiti huo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Profesa Kessy aliyefanya utafiti huo kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi, alisema lengo la utafiti huo ni kuangalia hali halisi ya maadili nchini kuanzia viongozi hadi kwa wananchi.

Wasanii wanne wa Orijino Komedi Wakamatwa na Kuhojiwa Polisi....Masanja Mkandamizaji Aendelea Kusakwa

$
0
0

Wasanii wanne wa kundi la vichekesho la Orijino Komedi akiwamo meneja wao wamekamatwa na kuhojiwa na jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kosa la kuwa na sare za polisi. 

Juzi, jeshi hilo lilitoa onyo kwa mtu ama kikundi chochote kuacha kutumia mavazi yanayofanana na sare zinazovaliwa na majeshi ya ulinzi na usalama nchini na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria. 

Kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai, sura ya 16 na marejeo yake ya mwaka 2002, kifungu cha 178 (1) na (2) kinachozungumzia makosa dhidi ya sare za majeshi ya ulinzi na usalama, kinabainisha kuwa ni kosa kisheria kwa mtu yeyote ambaye siyo mtumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuvaa mavazi yanayotumiwa au kushabihiana na sare za majeshi hayo bila kibali kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo, Hezron Gyimbi alisema wasanii hao walikamatwa juzi saa 10 jioni baada ya kusambaa kwa video kwenye mitandao ya kijamii wakiwa wamevalia sare hizo kwenye sherehe ya harusi ya Emmanuel Mgaya maarufu ‘Masanja’. 

Gyimbi aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Lucas Lazaro (Joti), Alex John (McRegan) na Isaya Gidion (Wakuvanga) na Sekioni David (Seki) ambaye ni meneja wao. 

Alisema sare walizokutwa nazo watuhumiwa hao ni za kazi za kawaida za jeshi la polisi hilo ikiwamo kofia, filimbi, shati, suruali, cheo na mkanda. 

“Tunaendelea kuwachunguza zaidi kama wana vitu vingine vya jeshi la polisi na tunataka kujua kuwa sare hizi wamepa- ta kibali kwa nani na uhalali wa kuwa nazo,” alisema Gyimbi. 

Alisema jeshi hilo linaendelea kumtafuta Masanja ili kujibu tuhuma zinazomkabili. Kaimu kamanda huyo alisema watuhumiwa hao walihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi kuanzia juzi saa 10 jioni hadi jana jioni huku na dhamana zao zilikuwa wazi. 

Tundu Lissu Atumia Dakika 120 Kupangua hoja Mahakamani ........Alikuwa akimtetea Ester Bulaya dhidi ya wafuasi wa Wasira

$
0
0

Tundu Lissu, ambaye ni wakili wa Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya jana alitumia muda wa saa mbili kupangua maombi ya wananchi wanne wanaopinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu yaliyompa ushindi mteja wake. 

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa tena baada ya Mahakama ya Rufaa kufuta uamuzi wa Mahakama Kuu uliotupilia mbali hoja za kupinga matokeo hayo, ambazo ziliwasilishwa na wafuasi wanne wa aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo, Steven Wasira (CCM). 

Jaji Mohamed Gwae wa Mahakama Kuu, alitupilia mbali kesi hiyo baada ya kukubali pingamizi la Lissu kuwa wafuasi hao hawakuwa na haki ya kisheria kufungua kesi hiyo. 

Wakazi hao wa Bunda wanadai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki kutokana na kugubikwa na vitendo vya rushwa, mgombea wanayemuunga mkono kunyimwa fursa ya kuhakiki matokeo na pia kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kupigia kura.

Jana, Lissu, ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na wakili wa kujitegemea, alitoa majibu ya utetezi mbele ya Jaji Lameck Mlacha kuanzia saa 4.10 asubuhi na kukamilisha saa 6.02 mchana wakati shauri hilo lilipoahirishwa kwa muda hadi saa 8:00 mchana kutoa fursa kwa mawakili wa upande wa wadai, Constantine Mutalemwa kujibu. 

Lissu alidai kuwa waleta maombi wameshindwa kutoa hoja mahususi kuonyesha ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi wanazodai ulikuwepo katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana. 

Wakili Lissu pia alidai kuwa walalamikaji ambao ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malegele, pia wameshindwa kuonyesha madhara waliyopata kama wapigakura kuishawishi mahakama kutengua matokeo yaliyompa ushindi Bulaya dhidi ya mwanasiasa huyo mkongwe. 

“Waleta maombi wanadai uchaguzi haukuwa huru na haki, idadi ya wapigakura kutofautiana kwa kila kituo na uwepo wa vitendo vya rushwa, lakini hawabainishi wazi nani mhusika wa mambo wanayoyalalamikia na madhara waliyopata kwa nafasi yao ya wapigakura,” alisema wakili Lissu. 

Alisema vitendo vya rushwa katika uchaguzi ni kosa kubwa linaloweza kusababisha kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi mzima, lakini walalamikaji wana wajibu wa kumtaja mhusika wa vitendo hivyo ili kuipa mahakama fursa ya kutafsiri vyema sheria na kutoa haki. 

“Lakini madai ya juujuu tena ya jumla kuwa aliyetoa rushwa ni wakala wa mteja wangu, hayakubaliki mbele ya macho ya sheria kwa sababu mtu huyo hajulikani na jukumu la kuthibitisha madai ni la mleta maombi na uthibitisho huo haumo kwenye hati yao ya maombi,” alidai Lissu. 

Aliomba maombi hayo yafutwe kwa hoja kwamba wadai hawajataja vifungu vinavyoipa mahakama haki na mamlaka ya kuyasikiliza na kuyaamua.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images