Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mrema Akataa Kurudi CCM........Ataka TLP na CCM Viungane Kuanzisha UKAWA Mpya

$
0
0
Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema amesema pamoja na Rais John Magufuli kufanya kazi vizuri, hawezi kurejea CCM na badala yake amependekeza vyama hivyo viwili viunde ushirikiano wao kama ilivyo kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani, pia amesema kuna haja ya suala la maandamano na mikutano ya kisiasa kuundiwa kanuni ili kuondoa malalamiko ya vyama vya upinzani kuzuiwa kutekeleza haki hiyo ya kikatiba.

Mrema, ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Msamaha kwa Wafungwa (Parole), alitoa kauli hiyo jana wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds FM.

Alikuwa ameulizwa na mmoja wa wasikilizaji wa kipindi hicho kwa nini asirejee CCM kama anaridhika kuwa Rais Magufuli anatekeleza yale ambayo alitaka yafanyike lakini hayakufanyika hadi akaamua kuisaliti Serikali ya Awamu ya Pili na kuihama CCM na kwenda NCCR-Mageuzi kabla ya kuanzisha chama cha TLP.

Mrema alijibu swali hilo kwa kuanza kueleza historia yake na mambo aliyofanya wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika kupambana na uhalifu na kwamba alipoona anatofautiana na Serikali aliamua kujitoa.

Alisema CCM chini ya Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli inafanya vizuri kwa kutekeleza yale aliyokuwa akiyataka wakati akiwa waziri.

Alisema Rais Magufuli anatoa ushirikiano kwa kila mtu, hivyo atakuwa bega kwa bega kumsaidia kiongozi huyo aliyedai anatekeleza majukumu yake kwa uwazi.

“Hiyo Ukawa nyingine siipendi kwa sababu haijui inataka kufanya nini.”

Mrema, ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP mwaka 2010 hadi 2015, alisema ataendelea kumwamini Rais Magufuli kutokana utendaji kazi wake kazi mzuri, ikiwamo kupambana na ufisadi, kazi ambayo alisema anapenda aone ikifanyika.

Akizungumzia uamuzi wa Rais Magufuli kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa, Mrema alisema agizo hilo ni sahihi kwa sababu hakuna haja ya mikutano wakati uchaguzi ulishapita.

Lakini alipoulizwa kama Serikali ingezuia mikutano na maandamano wakati alipoihama CCM mwaka 1995, Mrema, ambaye alivuta hisia za wengi wakati huo alisema katika kipindi hicho Rais hakuwa Magufuli.

Alisema kama Magufuli angekuwa ni Rais wakati huo na anatekeleza hayo aliyokuwa anataka, angekubaliana na uamuzi wa kuzuia maandamano.

Magufuli: Nitaigeuza Ikulu Kuwa Jumba la Makumbusho

$
0
0

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli amesisitiza kutekelezwa kwa mpango wa serikali kuhamishia makazo yake mkoani Dodoma ndani ya kipindi cha miaka mitano ya utawala wake huku akitangaza kuigeuza Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam kuwa sehemu ya maonyesho.

Aidha, Rais Magufuli amesema majengo ya wizara mbalimbali yaliyopo karibu na mwambao wa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam yatauzwa kwa wawekezaji mbalimbali ili yageuzwe hoteli za kitalii na fedha zitakazopatikana zitatumika kuustawisha mji wa Dodoma ambako serikali inahamia.

Magufuli alitangaza mpango huo jana wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa chama hicho muda mfupi baada ya kutembelea ofisi yake ya kichama iliyopo ndani ya jengo la Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli alisema wale wanaosema kuwa amesema atauza Ikulu baada ya kuhamia Dodoma wanapotosha ukweli kwa sababu serikali haina mpango huo.

“Wengine wanasema Ikulu itauzwa.. jengo la Ikulu litabaki pale, litakuwa jengo la maonyesho… wizara na majengo mengine yaliyo jirani na bahari yatauzwa ili tupate fedha za kuiendeleza Dodoma,” alisema Magufuli.

Serikali Kuhamia Dodoma
Alisema Serikali inahamia Dodoma ili Dar es Salaam ipumue na ili viongozi wakitaka kuja waje kwa ajili ya kutembea lakini shughuli zote za Serikali zitakuwa zimehamia mkoani humo.

Aidha, Rais Magufuli aliwashangaa watu wanaokejeli mpango wake wa kuhamishia Serikali Dodoma na kubeza kwa kudai kuwa haiwezekani.

“Suala la kuhamia Dodoma limeanza tangu mwaka 1973. Nimesoma darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu, nikamaliza bado hatujahamia… hatuwezi kujenga Serikali kwa mchakato, mchakato umekwisha, nimesema ndani ya miaka minne na miezi minne iliyobaki, nitahikikisha tutakuwa tumeshaondoka Dar es Salaam,” alisisitiza.

Alishangaa pia watu wanaohoji kwamba watapata wapi makazi iwapo Serikali itahamia mkoani humo na kuhoji kuwa mbona wakati wa Bunge watumishi hao hao huwa wanakwenda kwa wingi na wanapata makazi.

“Wakati wa Bunge, zaidi ya watu 300 huwa Dodoma, mawaziri, manaibu na makatibu wakuu, wanakaa na wanatosha… kwa nini hili wanahoji watakaa wapi,” alisema.

“Nazifahamu ofisi zote ukitoka Hoteli ya Kilimanjaro mbele kuna ofisi ya Takwimu, Wizara Ardhi, Utumishi zote zimetazama baharini… tutatangaza zabuni watu wanaotaka kujenga hoteli watanunua huko kote kuwe eneo la kitalii, tukipata fedha tutaweka makandarasi kujenga Dodoma. Hakuna kinachoshindikana, kinashindikana kwenye akili zetu,” alisema.

Aidha, alisema awali wakati wakitangaza kwenda Dodoma, kulikuwa hakuna miundombinu, maji, umeme wala barabara lakini sasa kila kitu kipo na mipango ya kuiboresha Dodoma ipo.

Alisema Dodoma ikijengwa miji mingine itakuwa na utalii utaongezeka kwa sababu huo (Dodoma) ni mji ambao upo katikati ya nchi.

“Kutoka Dodoma kwenda Arusha ni saa moja na nusu na maeneo mengine hii itasaidia watu wa mikoa mbalimbali kuja kuwekeza Dodoma na wamachinga nao watakuja,” alisema.

Rais Magufuli aisifia ‘Sizonje’ ya Mrisho Mpoto, ategua fumbo la mashairi yake

$
0
0

Utunzi mahiri wa mashairi na ughani uliotukuka wa Mrisho Mpoto, umeligusa sikio la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameeleza kuwa shabiki mkubwa wa kazi za msanii huyo hususan wimbo wake ‘Sizonje’. 
 
Akizungumza na Mpoto jana, muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Magufuli alimueleza msanii huyo kuwa anazifahamu vizuri kazi zake na kwamba anaupenda sana wimbo wake wa ‘Sizonje’ huku akichambua baadhi ya mistari iliyomo kwenye beti za wimbo huo. 
 
Mpoto alikuwa msanii pekee aliyeongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es  Salaam, Paul Makonda, Wakuu wote wa Wilaya za Dar es Saalam pamoja na viongozi wengine waliofika katika uwanja huo wa ndege kumpokea Mkuu huyo wa nchi.
 
“Nasikiliza sana nyimbo zako, ila huu wimbo wako wa Sizonje nimeuelewa sana na nausikiliza kila siku, kwangu umekuwa kama wimbo wa taifa. Mwanzoni nilipata tabu kuuelewa lakini sasa hivi… aaaah, nimeuelewa vizuri sana. Halafu Sizonje namjua, nimtaje?,” yalisikika baadhi ya maneno ya Rais Magufuli kwa Mrisho Mpoto. 
 
Akielezea tukio hilo lililoleta msisimko wa aina yake uwanjani hapo, Mpoto alisema kuwa baada ya kumsikia Rais ameanza kuusifia wimbo wake alishtuka na kujawa na furaha ya aina yake kwani kwa msanii ni jambo la thamani kubwa kusifiwa kazi yake na Mkuu wa Nchi.
 
Alisema kuwa pamoja na kuusifia wimbo huo, Rais alionesha kuufahamu vizuri zaidi baada ya kuanza kuipitia baadhi ya mistari na kuahidi kumfumbulia fumbo lililofichwa kwenye wimbo huo watakapokutana tena. 
 
“Unapopata thamani kutoka kwa Mkuu wa Nchi inaleta faraja sana," amesema Mpoto. "Kwahiyo, mheshimiwa Rais leo kuniambia kwamba yeye ni shabiki wa kazi zangu na kwamba anapenda sana wimbo wa Sizonje, na akafunguka kwa mistari ‘minane’ ya Sizonje ikiwa ni pamoja na ile inayosema ‘huyu mgeni anayepitia madirishani wakati milango ipo!’ Na akaniambia siku tukikutana ataniambia vile vyumba vitatu kwanini havifunguki,” aliongeza.
 
Msanii huyo amemshukuru Rais Magufuli kwa kuthamini mchango wake katika sanaa kwakuwa anaamini kuthaminiwa ni hitaji kubwa la kila msanii. 
 
“Kwakweli leo ni siku yenye furaha sana. Najisikia furaha sana. Asante sana mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli. Umenifanya nimekuwa na siku nzuri sana,” Mpoto alifunguka kwa furaha. 
 
Mwaka huu mwanzoni, Mrisho Mpoto aliachia audio na video ya ‘Sizonje’ aliomshirikisha Banana Zorro ambapo kwa muda mfupi tu, wimbo huo uligeuka kuwa mkubwa na kufanya vizuri. Kutokana na ufanisi wa kazi zake, Mpoto ameendelea kukubalika akipata mikataba ya ubalozi wa mashirika na taasisi kubwa nchini ikiwa ni pamoja na mfuko wa pensheni wa PSPF.
 
Mpoto ambaye mwaka jana alipewa tuzo ya heshima ya WASTA ya nchini Kenya kutokana na mchango wake katika lugha ya Kiswahili, amejipatia heshima kubwa kutokana na utunzi  mahiri wa nyimbo za awali, zikiwemo Nikipata Nauli, Adela, Chocheeni Kuni, Samahani Wanangu, Waite, Njoo Uichukue na zingine.

Agizo la Rais Magufuli Laanza kutekelezwa mgodi wa Geita

$
0
0

Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani Geita la kuwagawia wananchi mabaki ya mawe maarufu kama Magwangala kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita GGM umeanza kutekelezwa.

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo yupo katika ziara ya kikazi katika mgodi huo kwa kutafuta sehemu ambayo wachimbaji watayaweka na kuyachenjua kwa ajili ya kuyagawa kwa wananchi.

Akiongea mara baada ya ziara hiyo Mhe. Muhongo amesema kuwa agizo la Rais lilikuwa ni baada ya wiki tatu lakini kwa kuwajali wananchi wa eneo hilo wameamua kuanza zoezi hilo mapema kwa ajili ya utekelezaji wa agizo la rais.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Emanuel Kiunga, amesema kuwa serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na wabunge wa mkoa huo na baadhi ya viongozi wametafuta maeneo ya kuweka Magwangala hayo kwa ajili ya kuyahifadhi.

Wakizungumzia maeneo hayo yaliyotengwa kwa ajili ya zoezi hilo baadhi ya wabunge wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa viti Maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Upendo Peneza, na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Musukuma wamesema serikali lazima iwe makini na mawe hayo pamoja na kuwajali wananchi wa maeneo yaliyotengwa.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 17 & 18

$
0
0


Mtunzi: EDDAZARIA G.MSULWA
 ....Nikabaki nimesimama huku sielewi ni kitu gani nifanye nikageuka kiunyonge na kukutana na daktari tuliyemkuta jana usiku akiwa anatembea mwendo wa kasi sikujua ni wapi anapoelekea ikanibidi nimsimamishe.
“Daktari vipi”
“Salama mdogo wangu nakomba tuzungumze baadaye mimi ngoja niondoke hali imeshakuwa mbaya”
“Sijakuelewa dokta?”
“Kuna waziri wa afya amekuja hapa tayari dokta mkuu ameshapigwa chini wewe nakuomba tuondoke kama vipi njoo tuzungumze nyuma huku”

Nikatoka huku nikicheka kimoyo moyo na kusema laiti angejua huyo mtu anaye mkimbia ni mama yangu wala asingezungumza na mimi.
“Ehee kijana shida yako ni nini?”
“Dokta jana nilileta mgojwa hapa mida wa usiku alipatwa na….”

“Ohooo nimekumbuka huyo mgonjwa wako tumemsafirisha kuelekea katika hospitali ya K.C.M.C”
“Hali yake ikoje?”
“Si nzuri sanaa na kama tungembakisha hapa angetufia bure…..Kijana hebu nakuomba uniache niende kwani huyo mama namuona anakuja huku”

Dokta alizungumza huku akichungulia chungulia kupitia mlango tulio tokea nje huku akianza kupiga hatua za haraka kuelekea kwenye njia ya kichochoro iliyopo karibu na Zahanati hiyo.Nikarudi ndani huku nikiwa nawaza ni nini nifanye ili mama aweze kunielewa kama ni kuenda shule niende siku hiyo hiyo.Mama akamaliza kuzungumza na madaktari pamoja na manesi aliowakuta.

“Ehee wee huyo mgonjwa wako yupo wapi?”
“Wamesema wamemuamisha hospitali”
“Nani kasema?”
“Waulize hao madokta hapo”
“Eti kuna mgonjwa aliletwa jana amepata ajali?”
“Ndio muheshimiwa”

“Ahaa bahati yako haya jamani tekelezeni yale niliyo waambia ni bora mupoteze kazi nyingi kuliko kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa vifo vinavyosababishwa na uzembe wenu na kuanzia sasa hivi Kiongozi mkuu atakuwa huyo hapo bwana nani vile?”
“Bwana John Henry”

“Ok bwana John ndio atakuwa kiongozi wenu kwa muda hadi pale wizara itakapo leta mtu daktari mwengine sawa jamani.”Madaktari na Manesi wakamuitikia mama kisha akaagana nao pamoja na wananchi kisha tukaingia ndani ya gari na safari ya kurudi nyumbani ikaanza.Tukafika nyumbani mida ya saa saa nane mchana.Wakanishusha getini kisha mama akaelekea kwenye mishuhuliko yake.Mida ya jioni mama akarudi huku akionekana amechoka nikamsalimia na moja kwa moja akaenda chumbani kwake na kulala.Nikakaa nyumbani kwa siku mbili na bila ya kuzungumza na mama kuhusiana na swala la kurudi shule.

“Eddy shule unakwenda lini?”
Mama aliniuliza baada ya kupita mbele yake nikitokea nje huku yeye akiwa amekaa sebuleni akitazama taarifa ya habari ya saa mbili usiku
“Mama nakusikilizia wewe?”
“Unanisikilizia mimi hivi unaakili kweli mwanangu?”
“Sasa mama kuzungumza hivyo ndio mimi sina akili?”
“Nakuona bado unaakili za kitoto.Sasa anaye soma ni mimi au wewe?”

“Ila kumbuka mama wewe ndio uliye niruduisha nyumbani”
“Nilikurudisha ili akili yako ikae sawa.Na sijui hiyo PCB yako unaisoma vipi?”
“Mama mimi Genius”
“Mmmm genius uwe wewe,kesho shule na uondoke na gari ya kwanza uwahi kufaika shuleni?”
“Mama siwezi kusafiri ijumaa”
“Pumbavu wewe usiniletee ujinga nimekuambia kesho alfajiri nikitoka kwenda kazini ninakuacha ubungo sawa”
“Ila mama hizi safari zako za kushtukiza huwa sizipendi kama nini”
“Upende usipende kesho shule”

 Kama alivyozungumza mama safari ya kurudi shule ikaanza na akaniacha stendi ya mabasi ya Ubungo mida ya saa kumi na moja asubuhi kisha yeye akaelekea ofisini kwake sikujua ni kwanini siku hiyo amewahi sana kwenda ofisini.Nlicho kifanya ni kutafuta nyumba ya wageni(gest house) iliyo karibu na stendi kwa bahati nzuri nikapata chumba nikaingia na kulala hadi mida ya saa tatu asubuhi kisha nikarudi stendi na safari ikaanza kwa kutumia basi Dar Express na katika siti niliyokaa nipembeni yangu kuna msichana amavalia baibui ninja na ni ngumu kuweza kuiona sura yake.

Hatukusemeshana chochote kiasi kwamba safari nzima kila mtu akawa kimya,kwa bahati mbaya tukakuta ajali ya roli mbili zimegongana maeneo ya Wami kiasi kwamba ikatuchukua muda mrefu kukaa barabarani tukisubiria gari hizo kuja kuondolewa kutokana zimeifunga barabara na hapakuwa na uwezekano wa magari kupita.

“Aisee hii ajali inatuchelewesha”
Msichana niliye kaa naye alizungumza na kunifanya nimtazame kwa muda kisha nikamjibu.
“Wee acha tuu yaani nilisaa la tatu tumekaa hapa na hiyo foleni hapa hadi tuimalieze ni shughuli”
“Ndio tatizo la nchi yetu kukitokea jambo kama hili basi wahusika wataanza kujivuta vuta usishangae hapa tunakaa zaidi ya masaa kumi”

“Kweli na hapa mtu huwezi kusema utahairisha safari kwani nyuma yetu kuna foleni mbele huko ndio usiseme”
“Kuna biashara zangu nilitaka kuziwahi ila hapa nimesha chelewa itanilazimu kulala Arusha kitu nilichokuwa sijakipanga kabisa”

“Ulitaka urudi leoleo?”
“Ndio ila kwa hali hii nahisi hapa kuna kulala”
“Wewe ni mfanya biashata?”
“Ndio ninachukua mizigo ya nguo za wanawae na watoto kutoka Dar na kwenda kuuza Arusha”
“Ahaa hivi hiyo biashara inalipa?”
“Ina lipa pale mtu unapokuwa mchacharikaji ila ukiwa goigoi utaiacha kazi…..Vipi wewe uanashughulika na nini?”

“Mimi ni mwanafunzi nipo kidato cha tano”
“Ahaaa ila si hamjafunga bado?”
“Ndio ila mimi kuna matatizo kidogo yalinipata ndio nikarudi nyumbani ila sasa hivi kidgo nipo powa”
“Soma bwana sisi wengine tulikimbia shule na sasa hivi tunazunguka zunuka na dunia”
“Sawa ila hata wanao soma pia wanaangaika na dunia”

“Ni kweli ila huwa ninawashangaa sana wale wanaosoma na kutaka kuajiriwa.Wanashinda kutumia elimu walizonazo katika kubuni miradi itakayo waingizia pesa wanakazi ya kukaliaa kuhangaika na vijibahasha vyao kwenye maofisi ya watu na mbaya zaidi unakuta mshaara anaolipwa ni waajabu sana”

“Yaani wee acha tuu mdoi maana mimi katika maisha yangu sijapanga kuja kuajiriwa nahitai nijiajiri mimi mwenyewe”
“Ukiwa na nia na malengo utaweza hakuna kinacho shindikana chini ya jua”

 Gafla tukasikia mlipuko mkubwa ukitokea katika magari ya mbele ya magari yetu na ikatulazimu tushuke kwenye gari haraka kwenda kuangalia ni nini.Tukakuta moshi mwingi mweusi ukisambaa angani na huku magari mawili ya mbele ikiwemo roli la mafuta lililopata ajali yakiteketea kwa moto mwingi.Watu waliopo kwenye magari ya karibu na magari hayo yanayowaka moto wakaanza kukimbia kurudi nyuma  tulipo sisi na kusababisha msongamano mubwa wa watu wanao jaribu kuziokoa roho zao.
“Huu moto utakuja tuu huku”

Msichana alizungumza huku akiwa anafunua kitambaa kilicho iziba sura yake na kujikuta nikimeza fumba kubwa la mate na kubaki nikimtazama jinsi alivyojaliwa uzuri wa sura kiasi kwamba nikajikuta nashindwa kumjibu kitu
“Vipi mbona unanishangaa?”
“Ha…haaa pana”

Kabla sijajibu chochoye gari nyingine mbili zikashika moto na kuanza kuteketea na kwa mahesabu ya haraka haraka gari letu ni la nane kutoka katika gari nne zinazoteketea kwa moto.Polisi wa kikosi cha barabarani wakaanza kuwaomba watu kurudi nyuma kwani hali sio nzuri na muda wowote magari mengine yanaweza kufwata katika kuungua kwa moto.Nikaingia ndani ya basi na kuchukua begi langu la nguo pamoja na pochi kubwa ya msichana huyo kisha nikashuka na tukajumuika na watu wengine kurudi nyuma huku tukizipisha gari za zima moto kufanya kazi yao.

“Kaka unaitwa nani?”
“Ninaitwa Eddy wewe je?”
“Mimi ninaitwa Sheila”
“Una jina zuri”
“Hahaaaaa wapi mbona jina la kawaida”
“Ebwaane ehee hapa safari inaweza ikaahiriswa?”
“Sijui tusubirie matoke kwa maana hapa hali imeshakuwa mbaya”

==>Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>

Jukwaa la Wahariri lapinga Gazeti la Mseto kufungiwa

$
0
0

 Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepokea kwa mshituko taarifa za kufungiwa kwa miezi 36 gazeti la Mseto kwa kutumia kifungu cha 25(1) cha Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa na mwenyekiti wake, Theophil Makunga, TEF imesema, “hatukubaliani na wala hatuungi mkono utaratibu huu wa Serikali kufungia au kufuta vyombo vya Habari.”


Katika maelezo ya Waziri, Nape Nnauye anasema tangu Mwaka 2012 wamekuwa wakiwaonya Mseto bila gazeti hilo kubadilika.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Halihalisi, Saed Kubenea amekana kupata maonyo kutoka Serikalini.

"Sisi TEF tunapinga utaratibu wa Serikali kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka na Hakimu katika kesi inazohusika.

"Tunataka mchakato wa kubadili Sheria ikaanzisha chombo cha kitaaluma cha kusimamia wanahabari na vyombo vya habari uende haraka kwa nia ya kumaliza kadhia hii.

"Serikali imeahidi muda mrefu kubadili Sheria hii mbaya ya Magazeti lakini miaka yote utekelezaji umekuwa sifuri.

"Tunasisitiza kuwa hatukubaliani na wala hatuungi mkono utaratibu huu wa Serikali kufungia au kufuta vyombo vya Habari.

"Kwa upande mwingine tunapenda kuvitahadharisha vyombo vya Habari katika matumizi ya nyaraka ili kuepuka kuingia katika migogoro na Serikali, Jamii au mtu mmoja mmoja." Amesema Makunga

"Pamoja na taarifa hii, TEF itafanya uchunguzi na uchambuzi wa adhabu iliyotolewa kwa Gazeti la Mseto pamoja na habari iliyosababisha gazeti hilo kufungiwa, kwa manufaa ya waandishi wa habari na vyumba vya habari." Amesema Makunga

Zaidi ya Wavuvi 9 Waliokuwa Wakifanya Uvuvi Mto Kagera Wafariki Katika Mazingira ya Kutatanisha

$
0
0

ZAIDI ya wavuvi tisa waliokuwa wakifanya shughuli zao za uvuvi ndani ya mto Kagera wamefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha kwa nyakati tofauti.

Akisoma taarifa ya Wilaya kwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchini Lameck Mwigulu Nchema,Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa kanali mstaafu Shaabani Lissu alisema kuwa wavuvi hao wanatokea katika mialo ya Rubwela,Kanyika,katwe na Ruko katika ziwa ngoma.

Alisema matukio hayo ya vifo vya utata yameanza kutokea kuanzia mwezi wa pili mwaka huu wakati wavuvi hao wanapoenda kuvua ndani ya mto Kagera unaotenganisha nchi ya Rwanda na Tanzania.

"Mara nyingi wavuvi wakienda kuvua ndani ya Mto Kagera huwa hawarudi,huwa wanatekwa na kuuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni askari wa nchi jirani ya Rwanda"Alisema Mkuu huyo wa Wilaya

Alisema hivi karibuni wavuvi wawili walienda kuvua ndani ya mto Kagera na mmoja aitwaye Emanuel Kahonda alipigwa risasi na kufariki dunia huku mwenzake Yoha Misago akinusurika katika tukio hilo na kukimbia na kwenda kutoa taarifa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

"Mhe.Waziri ni juzi tu kuna mvuvi alipigwa risasi ndani ya mto Kagera hata msiba kwake bado upo, mwenzake aliyeshuhudia na kufanikiwa kuwatoroka wauaji hao yeye kunusurika ndiyo alikuja kutoa taarifa ofisini kwangu"alisema

Naye mwenyekiti wa mwalo wa Kitwe Ustadhi Hakimu alimthibitishia Waziri kuwa wavuvi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kuuwawa kikatili na askari wa nchi jirani ya Rwanda.

"Hapa kijijini kuna wajane wengi,waume zao walikuwa wakienda kuvua samaki ndani ya mto Kagera hawarudi,wanadai tunavua samaki kwenye maji yaliyopo nchi mwao,na mto kagera wameufanya wao peke yao,Tunaomba utusaidie Mhe.Waziri hili tatizo liishe

Upande wa kule kwao kuna misitu sana na huwa wanajificha humo,yaani wakikuona tu wala hawakusemeshi wanakupiga risasi tu humo humo majini,na maiti zimekuwa zikipotelea mtoni humo humo"alisema Mwenyekiti huyo.

Naye waziri wa mambo ya ndani ya nchini Mwigulu Nchemba aliiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kyerwa kukutana na viongozi wa mialo ili wapate taarifa rasmi ya chanzo cha matukio hayo na kuipatia wizara ili waweze kutoa tamko rasmi juu ya mauaji hayo ya wavuvi.

"Hali hii imenistua sana,hatuwezi kuruhusu watanzania wenzetu wawe wanauwawa kikatili kiasi hiki,nikipata taarifa rasmi nitafuatilia jambo hili hata kwa kuwasiliana na wenzetu ili nijue kama ni msimamo wa serekali yao au ni uhalifu"alisema Nchemba.

Mkurugenzi wa Bunda apokea madawati 90 kutoka kwa Mbunge Ester Bulaya

$
0
0


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jimbo la Bunda, Mkoani Mara Bi. Janeti Mayanja amepokea madawati 90 yalitolewa na Mbunge wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bi. Ester Bulaya, ambapo hapo awali  madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo walikataa kupokea madawati hayo baadaya ya kuwa yameandikwa  jina la mbunge huyo pamoja na kuwa yamenunuliwa na fedha za Mfuko wa Jimbo.

Akizungumza leo kwa njia ya simu, Mkurugenzi  Mayanja alisema kuwa  amepokea madawati hayo jana  Agosti 12  kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo Ester Bulaya baada ya kufutwa jina lake, ambapo madawati hayo tayari yamewasilishwa katika shule tatu zilikuwa na uhaba.

“Tulifanya kikao na Mbunge Bulaya na tukakubaliana kuwa ni vyema majina yake yakafutwa katika madawati hayo kwa vile yalinunuliwa kwa fedha  za Mfuko wa  Jimbo, lakini endapo mbunge atapenda kutupa madawati atakayonunua kwa  fedha zake binafsi  na kuandika majina yake hapo tutapokea kwa vile bado kuna tunauhitaji katika jimbo letu” alisema Mkurugenzi Mayanja

Alifafanua kuwa fedha zilizotumika  kununua  madawati hayo zilikuwa ni  fedha za Mfuko wa  Jimbo zinazotokana na ruzuku ya Serikali ambazo matumizi yake hupangwa na Ofisi ya Mbunge.

Madawati hayo 90 yalisambazwa katika shule tatu za Msingi zilizopo katika Jimbo la Bunda zilizokuwa na uhaba wa madawati  ambazo ni  Nyatwali, Nyerere na Ligamba,  zilizopewa madawati 30 kwa kila moja.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Agosti 14

Mrema ataka mateja wasitupwe jela

$
0
0

MWENYEKITI wa Bodi ya Taifa ya Parole, Augustine Mrema ameshauri waathirika wa dawa za kulevya kupelekwa hospitalini kupata tiba badala ya polisi kuwakamata na kuwapeleka mahabusu au gerezani ambapo huko hujazana bila kupata msaada wowote.

Aidha, amesema atamwomba Rais John Magufuli kumrejesha kazini Mwalimu wa Sekondari, Emmanuel Roman ambaye alifukuzwa kwa ajili ya utumiaji wa dawa hizo, lakini hivi sasa ameacha baada ya kupata tiba na ushauri nasaha.

Mrema alitoa ushauri huo jana Dar es Salaam alipokutana na waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya katika Ukumbi wa Friends Corner, Manzese katika Manispaa ya Kinondoni.

Alisema anapopelekwa gerezani mtumiaji wa dawa za kulevya atakuwa hajasaidiwa, kwani atazidi kuharibikiwa badala ya kurekebishwa.

“Ni marufuku kukamata vijana wadogo wanaotumia kete. Sio kama nahamasisha waendelee kutumia ila wakikamatwa wapelekwe hospitali za Muhimbili, Mwananyamala na Temeke ambako kuna vituo vyao. “Ukianzisha operesheni ya kukamata wezi bila kujua historia zao inawezekana ni waathirika wa dawa za kulevya, ambao wanapoanza kutumia kuacha ni kazi sana hivyo wanalazimika kuiba ili wapate hela ya kununua dawa hizo,” alisema mwanasiasa huyo mkongwe aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Kwa upande mwingine amevitaka vyombo vya usalama kushughulikia wafanyabiashara wakubwa wa dawa hizo maarufu kama `Mapapa wa dawa za kulevya’, badala ya kuhangaika na hao wanaotumia ili kudhibiti hali hiyo.

“Hili nitalifikisha kwa Rais nimwambie taifa lako linaangamia, vijana wanaharibika kutokana na dawa za kulevya, hivyo awashughulikie mapapa wanaoleta dawa kutoka Iran, kwani wanajulikana kwa majina na wengine wanachukua na kusambaza mtaani,” aliongeza.

Alisema kutokana na janga la dawa za kulevya kuzidi kuwa kubwa nchini, atamwomba fedha Rais Magufuli za kuwasaidia waathirika hao kuunda vikundi vya kuzalisha mali.

Pia ameshauri waathirika hao ambao wameacha watumike kukomesha wizi katika Jiji la Dar es Salaam kwa kuwakamata mateja ambao wanawajua.

Naye Mwalimu Romani alianza utumiaji wa dawa za kulevya mwaka 1998 akiwa sekondari na aliendelea kutumia hadi alipohitimu kidato cha sita na kwenda chuo cha ualimu, kisha kuanza kazi ambayo aliachishwa kwa kutoonekana kazini kwa muda.

Awali, mwathirika wa dawa za kulevya ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kompyuta katika Hospitali ya Mwananyamala, Yusuph Mizito akisoma risala kwa niaba ya wenzake, alisema wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa vituo vya tiba, kwani kwa nchi nzima vipo katika Jiji la Dar es Salaam pekee.

Alisema watumiaji wa dawa hizo ambao wameamua kuacha dawa za kulevya husafiri kupata huduma Dar es Salaam ambako vituo hivyo vipo Mwananyamala, Muhimbili na Temeke.

Papa Francis Awatembelea Makahaba

$
0
0
PAPA Francis Kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki Duniani amekaa kwa zaidi ya saa moja na makahaba waishio nchini Italia ambao walisafirisha kutoka nchi mbalimbali duniani.

 Papa mwenye umri wa miaka 79 amekua akikemea vitendo vya kusafirisha wanawake kutoka taifa moja kwenda lingine ili kuwatumikisha katika biashara za ngono.

Akiwa na wanawake 20 waishio katika moja ya jengo linalomilikiwa na Kanisa Katoliki katika Mji Mkuu wa Italia kiongozi huyo alizungumza na wananwake hao akitaka kujua namna walivyoingia biashara hiyo haramu.

Wanawake hao wenye umri unakadiriwa kuwa kati ya miaka 30 walitekwa na mwanamme mmoja. Miongoni mwao wapo wanaigeria saba, waromania sita na wanawake wanne kutoka Albania, huku wengine watatu katika kundi hilo wakitoka Italia, Tunisia na Ukraine.

Aidha, wamekiri sababu kubwa inayopelekea kwenda huko kuwa ni ajira ambapo wafanyabiashara Italia na nchi nyingine kutoka mataifa ya Ulaya huwachukua kwa kuwaahidi kuwapa kazi na wakifika huko hulazimishwa kufanya ukahaba.

Papa Francis amewatia moyo makahaba hao wenye nia ya kuachana na biashara hiyo, amewataka wawe “thabiti” wakati wanapoanza maisha mapya kwa usaidizi wa kituo cha Papa Yohana wa pili.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete atoa Tamko la Tathmini ya Jumuiya ya Madola la Uchaguzi Mkuu wa Zambia

$
0
0

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete leo ametoa tamko la Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola  la Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika tarehe 11 Agosti, 2016 kuchagua Rais, Wabunge, Mameya, Madiwani na Kura ya Maoni ya Katiba. 

Rais Mstaafu Kikwete yuko nchini Zambia kufuatia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kumteua kuwa Mwenyekiti wa Timu hiyo yenye waangalizi wa kimataifa 17 kutoka nchi za Jumuiya ya Madola.

Kwa mujibu wa tamko hilo, Jumuiya ya Madola imejiridhisha kuwa zoezi la upigaji kura, usimamizi wa kura na uhesabuji kura vituoni kwa ajili ya umeendeshwa kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni bora za uendeshaji wa chaguzi.

 Tamko linasema, dosari na hitilafu zilizojitokeza hazikuwa kubwa kiasi cha kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu huo.

Amewapongeza wananchi wa Zambia kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa amani na kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka. 

Amewasihi viongozi wa kisiasa wa Zambia, wagombea na vyama vya siasa kuheshimu maamuzi wa wananchi na pale inapojitokeza upande wowote kutoridhika na matokeo, zitumike njia za amani na kisheria za kutafuta ufumbuzi.

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 31 ...

$
0
0


...Doreen alimsikiliza kwa Umakini mama Pamela ili ajue ni swali gani analotaka kuuliza. Mama Pamela alikaa vyema kisha akakohoa kidogo na kumtazama Kwa makini Doreen.
"Niulize Tu mama" alisema Doreen.

"Hivi ni kitu gani unapenda nikufanyie ili moyo wako ufurahi? Maana nimependa sana heshima na adabu uliyojaaliwa." Alisema mama Pamela.
"Kiukweli mama Mimi napenda sana unitafutie shule.. Ili niweze kusoma na kufikia malengo yangu" alisema Doreen.
"Shule tu? Wala usijali wiki ijayo nitakuwa tayari nimetafuta shule kwa ajili yako.."
"Nitafurahi sana mama..."
"Unapenda shule ya kutwa au bweni?"
"Yoyote tu itanifaa" alisema Doreen.
Suala lile lilimfurahisha sana Doreen, aliendelea kuishi kwa kunyenyekea sana ndani ya nyumba ile, lakini katika ulimwengu mwingine alikuwa ni mtu jeuri na katili kwa familia ile. Kila Mara aliliwinda sana titi la Pamela, alitamani kulipata kwa udi na uvumba lakini kwa bahati mbaya ilikuwa vigumu kulipata. Alitumia kila namna lakini bado hakuelewa sababu ya kushindwa kulipata titi la Pamela.

Hasira zilimuwaka sana Doreen pale alipoingia chumbani kwa Pamela usiku na kutaka kumkata titi lake. Alikuta Pamela amelala usingizi mzito sana, akampulizia dawa ili usingizi ule uzidi kuwa mzito zaidi kisha akamsogelea taratibu akiwa ameshikilia panga Kali lililofungwa kaniki nyeusi na nyekundu. Doreen alitamka maneno ambayo aliyajua mwenyewr kisha akamfunua shuka Pamela na kusogeza kisu chake karibu na titi la Pamela. Hakuwa na hofu kama kazi yake haitofanikiwa kwani alikuwa anajiamini na alikiamini kile alichokifanya. Lakini kwa bahati mbaya sana kila alipotaka kumgusa Pamela na upanga ule, Doreen hakuona chochote kitandani pale. Alijaribu tena na tena lakini bado hali ikaendelea kuwa vile vile. Doreen alikasirika sana, akatupa chini upanga ule mlio wake ukamshtua Pamela usingizini.
Doreen alishtuka sana baada ya Pamela kushtuka usingizini,  akakimbia haraka na kujibanza kwenye kona moja ya chumba kile kisha akatamka maneno Fulani ya kichawi halafu akatulia kimya.
Pamela aliangaza macho huku na kule chumbani mle lakini hakuona kitu, akainuka kitandani na kuwasha taa kisha akaangalia kila sehemu ya chumba kile lakini hakuona chochote. Akatoka na kwenda msalani, alipokuwa anajisaidia haja ndogo akahisi kuna mtu anamfuata nyuma yake Pamela alishtuka na kuogopa sana kisha akakumbuka jambo muhimu la kufanya kama alivyoambiwa na baba yake. Pamela akasali kwa sauti ya chini na kwa imani kubwa sana kisha akajisaidia na kurudi kitandani, akalala bila kuzima taa.
Doreen alikasirika sana baada ya kumkosa Pamela kwa Mara nyingine. Akaamua kurudi chumbani kwake kupitia  kona ile ile aliyokuwa amejibanza.

Rais wa Zamani wa Zanzibar afariki Dunia leo, Rais Dkt. Magufuli atuma salamu za rambirambi

$
0
0

Rais wa awamu ya pili wa Zanzibar na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi (1972-1984), Mzee Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu. 

Mzee Aboud Jumbe amefikwa na mauti hayo nyumbani kwake Kigamboni, Jijini Dar es salaam. Rais wa Jamhuri wa Muungano amemtumia Salaam za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa msiba huu mzito
 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Agosti 15


Rais Dkt. Ali Mohamed Shein akitoa taarifa rasmi ya kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya pili Mzee Aboud Jumbe.

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, ametoa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Pili, Mheshimiwa Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.

Katika taarifa hiyo aliyoitoa jana kupitia vyombo vya habari, Alhaj Dk. Shein kwa masikitiko makubwa aliwaarifu wananchi kuwa jana tarehe 14 Agosti 2016, Mzee Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia, msiba ambao umetokea nyumbani kwake Mji Mwema, Dar es Salaam.

Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa Marehemu Mzee Aboud Jumbe ni Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Pili, ambaye vile vile alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Marehemu Mzee Aboud Jumbe amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na umri wake.

Kwa taarifa ya Alhaj Dk. Shein, maziko ya marehemu yatafanyika leo tarehe 15 Agosti 2016 saa 7.00 mchana ambapo maiti yake itasaliwa katika Masjid Mshawar, Mwembeshauri na kuzikwa nyumbani kwake Migombani.

Aidha, Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa kufuatia mchango na juhudi kubwa ambazo Marehemu Mheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi alizichukua katika uhai wake kwa kuitumikia, kuiongoza na kuijenga Zanzibar pamoja na nafasi yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nchi yetu imekabiliwa na msiba mkubwa kwa kifo cha kiongozi huyu mahiri”alieleza Alhaj Dk. Shein katika taarifa hiyo.

Kutokana na msiba huo mkubwa Alhaj Dk. Shein alitangaza rasmi siku saba za maombolezo, kuanzia leo tarehe 15 Agosti 2016 ambapo katika kipindi hicho chote bendera zote  zitapepea nusu mlingoti.

Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa utaratibu wa maziko utafuata wasia ambao mwenyewe marehemu aliutoa wakati wa uhai wake.

“Tunaungana na Wanafamilia wote katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Naomba kutumia nafasi hii kutoa mkono wa pole kwa wafiwa wote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie kauli thabit marehemu mzee wetu na amlaze pahala pema peponi, Amin. Inalillahi wainnailaihi rajiun” Alieleza Alhaj Dk. Shein katika Taarifa hiyo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Spika wa Bunge Job Ndugai Awaalika Wapinzani Kwenye Meza ya Mazungumzo ili Kumaliza Tofauti Zilizopo

$
0
0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amekiri bunge hilo kusambaratika na kuwa vipandevipande kutokana na vurugu za mara kwa mara zilizopelekea wabunge wa upinzani kususia vikao hivyo anawaalika wabunge hao kwenye mazungumzo.

Ndugai, ambaye kipindi kirefu cha Bunge la Bajeti lililomalizika hivi karibuni, alikuwa India kwa matibabu, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza kwenye kipindi cha Funguka kinachorushwa na televisheni ya Azam.

Ndugai alisema ili bunge lifanye kazi yake yake, linahitaji kuishinda changamoto iliyopo ya bunge kutokuwa kitu kimoja, huku akielezea wazi kuwa chanzo kikuu kinachosababisha bunge hilo kusambaratika ni pamoja na "u-vyama" kuzidi na wabunge kutojali maslahi ya taifa.

Sababu nyingine aliyoitaja Ndugai, ni ugeni wa wabunge ambapo kila unapofanyika uchaguzi sehemu kubwa ya wabunge huwa ni wageni hivyo wengi wao wanakuwa hawajaelewa kanuni na tamaduni za kibunge.

Alisema yanayotokea sasa kwa kiasi kikubwa siyo mageni, yalikuwepo tangu wakati wa bunge la 10. 

"Hali hii imeanza zamani kidogo tangu enzi za spika Makinda, wabunge walikuwa wakitoka nje, wakigomea vikao, wakiadhibiwa n.k. Ugumu ambao tunaupata ni kwamba kila baada ya uchaguzi wanakuja wabunge wengi wageni ambao hawajui mambo mengi na mfano ni bunge hili ambapo karibu 70% ya wabunge ni wapya" Alieleza Ndugai na kuongeza kuwa hata suala la kumsusia Rais anapokwenda kuhutubia bungeni, limewahi kutokea katika bunge lililopita.

Pamoja na hayo, Spika Ndugai alisema kuwa hakuna kanuni inayomzuia mbunge kutoka nje ya bunge kwa kuwa ni haki yake 

"Hakuna kanuni inayomkataza mbunge kutoka nje, ni sehemu ya demokrasia yao, lakini hii ya sasa imezidi, ni jambo lisilopendeza... maana watanzania wamewatuma kwenda kuwakilisha hoja zao, wanapotoka inakuwa haipendezi".

Aliwasihi wabunge wa Upinzani kurudi bungeni na kueleza mambo yaliyowaudhi ili wakae wajadili na watafute ufumbuzi badala ya kuendelea kususia. 

Alisema "Wabunge kutoka nje ni jambo ambalo halipendezi hata kidogo, nisingependa niendelee kuliona.

"Nawaomba katika bunge lijalo kama wanahisi tunakosea watueleze, na sisi tuwaeleze wanakosea wapi ili twende sawa"

Kuhusu malalamiko ya wapinzani dhidi ya Naibu Spika, alikiri kupokea malalamiko hayo kupitia kwa mbunge james Ole Millya, na yeye aliyawasilisha kwenye kamati husika lakini hoja zote ambazo walikuwa wakizilalamikia zilizonekana hazina uthibitisho, hivyo maamuzi ni kwamba Naibu Spika Dkt Tulia Ackson hana hatia yoyote.

Kuhusu hoja ya Naibu Spika kuendelea kukalia kiti kwa muda wote Ndugai anasema " Uongozi ndiyo unapanga nani akae pale, sioni tatizo la mtu kukaa kwenye kiti kwa muda mrefu, lakini kama mtu anakosea, zipo fursa za kupeleka jambo kwenye kamati badala kulalamika bila kufuata kanuni"

Alisema haoni tatizo la Naibu Spika na hajui ni mambo gani amewaudhi ila anadhani kinachowasumbua wapinzani ni hisia za jinsi Naibu Spika alivyopatikana

"Wabunge wa upinzani wanapitia changamoto nyingi kabla ya kuingia Bungeni, wengi wao wanahangaika sana kupata ubunge hadi kufikia hatua ya kulala sana selo (polisi) kwaiyo namna ya 'kudeal' nao inahitaji uvumilivu kidogo. Naibu Spika siyo mbunge wa jimbo, na wao wamezoea mbunge wa jimbo ambaye anafanana nao, Naibu Spika ni mbunge wa uteuzi kwahiyo wanahisi anafanya kazi kwa kufuata maelekezo kutoka nje ya bunge au anatumikia mabwana wawili jambo ambalo siyo kweli. Pia adhabu zilizokuwa zinatolewa zinawafanya wahisi wanaonewa kila wakati"

Pia Spika alikemea tabia ya baadhi ya wabunge wa CCM kutumia muda mwingi bungeni kurusha vijembe kwa wabunge wa upinzani

"Kwa wabunge wa chama tawala siyo jambo zuri kurusha vijembe, tukienda bungeni nitakaa nao, na nitawaeleza kuwa siyo jambo jema kuwa na bunge la vijembe, nawaasa tubadilike, tuheshimiane ... matusi kelele vijembe kanuni haziruhusu na haipendezi"

Kuhusu mwenendo wa baadhi ya wabunge kutoheshimu kanuni, Ndugai alisema "Kanuni zimetungwa kwa watu wazima, lakini tatizo wabunge wanaokuja sasa hivi wengi ni vijana, na wako chini ya kiwango cha kanuni. Bado sijajua nini cha kufanya ili hali hii isiendelee, kwenye bunge la katiba angalau kulikuwa na kitu kinaitwa kamati ya maridhiano, nafikiri inabidi tuige kitu hicho tupate watu hata wastaafu watakaokuwa wanakaa kuyaweka mambo haya sawa"

Kuhusu sakata la Lugumi, Ndugai alisema kuwa kamati ndogo iliyoundwa kufuatilia suala hilo itatoa taarifa yake katika mkutano ujao wa bunge.

Kuhusu uamuzi wa serikali kuzuia Bunge LIVE, Ndugai alisema uamuzi huo ni mzuri na anauunga mkono kwa kuwa unasaidia kupunguza vurugu kwa wabunge.

Kuhusu suala la posho za wabunge Naibu Spika alisema kuwa posho za wabunge wanazolipwa sasa, ni za kawaida na siyo kubwa kama watu wanavyodhani huku akiunga mkono uamuzi wa wabunge kukatwa kodi kwenye kiinua mgongo.

Ofisi za Bunge kuhamia Dodoma Septemba mwaka huu

$
0
0

Ofisi za Bunge zilizopo Jijini Dar es salaam zinatarajia kuhamishiwa Dodoma mwezi Septemba mwaka huu, ikiwa ni utekelezaji wa agiza la Rais Magufuli la kuhamishia shughuli za serikali Dodoma.

Taarifa hiyo imetolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai jana na kusema kuwa kwa bunge suala la luhamia Dodoma siyo gumu kwa kuwa tayari makao makuu yake yako Dodoma.

Alisema tayari alikwishatoa maagizo kwa ofisi yake kuhakikisha kuwa kufikia mwezi Septemba kila kitu kinachofanyika Dar es salaam kifanyike Dodoma isipokuwa mambo  machache.

"Nimeagiza ofisi yangu ihamie dodoma mara moja kuanzia Septemba hii, watumishi wa bunge karibu wote watahamia Dodoma, masuala ya malipo yataangaliwa baadaye, kwa sasa ni kuhamia dodoma tu, ofisi tunazo huko" Alisema Ndugai

Kama sehemu ya mwanzo wa utekelezaji wa azma hiyo, tayari ofisi ya bunge imetangaza kufanyia Dodoma vikao vyake vyote vya kamati za bunge tofauti na ilivyokuwa umepangwa mwanzo na ilivyozoeleka kufanyikia Dar es salaam.

Mbunge wa CUF akamatwa kwa uchochezi

$
0
0

MBUNGE wa Tanga Mjini, Mussa Mbaruku (CUF), amekamatwa.

Mbunge huyo alikamatwa juzi na Jeshi la Polisi na kuhojiwa kwa zaidi ya saa sita kwa tuhuma za kufanya mikutano ya hadhara na kutoa lugha za uchochezi za kutomtambua Meya wa Jiji la Tanga, Mustapha Selebosi (CCM).

Taarifa za awali zinasema kuwa, mbunge huyo kabla ya kutiwa mbaroni, alipelekewa barua ya kuhitajika katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul kwa mahojiano zaidi.

Taarifa hizo zinasema kuwa, baada ya mbunge huyo kuitikia wito huo, aliwekwa chini ya ulinzi na kuanza kuhojiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti Chama cha Wananchi (CUF), Mkoa wa Tanga, Rashid Jumbe, alithibitisha mbunge huyo kukamatwa na kusema wakati wa tukio alikuwa na madiwani wa chama hicho.

“Inasemekana alikamatwa na madiwani kwa tuhuma za kutaka kufanya mikutano ya hadhara ya kuwashukuru wananchi kutokana na ushindi walikipa chama chetu.

“Juzi walianza kufanya mikutano hiyo kwenye Kata ya Mwanzange jijini Tanga ambayo ilihudhuriwa na mbunge na jana walifanya mkutano wao kwenye eneo la Madina, Kata ya Msambweni.

“Baada ya kumalizika kwa mikutano hiyo, ndipo asubuhi mbunge huyo alikamatwa na jeshi hilo na kutakiwa yeye na madiwani wasiendelee na mikutano hiyo kwa madai kuwa ni ya kichochezi,” alisema Jumbe.

Naye Kamanda Paul alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi ili azungumzie tukio hilo, alisema alikuwa kwenye kikao.

CUF yampiga chini rasmi Profesa Lipumba

$
0
0


ALIYEKUA Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ametoswa rasmi kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Agosti 21 mwaka huu, kupitia Mkutano Mkuu Maalumu.

Hali hiyo imebainika baada ya kuteuliwa kwa majina ya watu tisa kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo ya uenyekiti, huku jina la Profesa Lipumba likikosekana katika orodha hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Shaweji Mketo, pia majina manne yameteuliwa kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti likiwamo jina la Dk. Juma Duni Hajji ambaye anatetea nafasi yake.

Mwishoni mwa mwaka jana, Dk. Hajji  alijiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo aliteuliwa kuwa mgombea mwenza wa urais akiwa na Edward Lowassa aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa).

Katika taarifa hiyo, Mketo alisema nafasi nyingine zinazowaniwa kwenye uchaguzi huo ni pamoja na nafasi nne za wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa  wa Kanda ya Nyanda za juu Kusini ambapo mjumbe yeyote anaweza kugombea kutoka kanda hiyo na nafasi moja ya mjumbe kutoka Kanda ya Kati ambapo mjumbe yeyote wa Mkutano Mkuu Taifa kutoka kanda hiyo anaweza kugombea.

Alisema nafasi moja ya mjumbe kutoka Kanda ya Ziwa ambayo ni ya mwanamke anaweza kugombea mjumbe yoyote na nafasi moja kutoka Kanda ya Kaskazini ambapo  mjumbe yeyote kutoka kanda hiyo pia anaweza kugombea.

Aliyataja majina tisa ya wanaowania nafasi ya mwenyekiti na taaluma zao kwenye mabano kuwa ni pamoja na Abdul Omary Zowo (Mhandisi wa Ndege za Kivita), James Mahangi (Maabara), Joseph Rhobi (Fundi Seremala), Juma Nkumbi (Mtaalamu wa Kompyuta), Salum Barwany (Fundi Magari), Selemani Khatibu, Twaha Taslima (Mwanasheria), Zuberi Kuchauka (FTC Mechanical) na Riziki Mngwali (Usuluhishi wa migogoro).

Mketo alisema, majina manne ambayo yanawania nafasi ya makamu mwenyekiti na taaluma zao kwenye mabano ni pamoja na Dk. Juma Ameir Muchi (Daktari), Juma Duni Hajji (Mchumi), Mussa Hajji Kombo na Salim Abdallah Bimani.

Alisema, Mkutano Mkuu Maalumu wa kupitisha majina hayo unatarajiwa kufanyika Agosti 21 mwaka huu, jijini Dar es Salaam ambao utaweza kuziba nafasi zilizoachwa wazi

Alisema kuwa chama hicho kilitoa utaratibu wa uchukuaji wa fomu hizo za kuomba nafasi za uongozi ambapo wagombea walitakiwa kwenda kwenye ofisi za  makatibu wa wilaya kwa ajili ya kuchukua fomu hizo, hali iliyosaidia kufanikisha zoezi hilo.

Alisema kutokana na hali hiyo, siku ya mwisho ya kuwasilisha taarifa za wagombea hao kwenye ofisi za makatibu wa wilaya ilikua Agosti  10 mwaka huu.

“Naomba niwashukuru wanachama na viongozi wetu katika ngazi zote nchini kwa kuhamasisha wanachama wenzao ambao wameweza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya uongozi ndani ya chama.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images