Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kauli ya serikali kuhusu kuhamishwa kwa stendi ya mabasi Ubungo Jijini Dar es Salaam

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapiga marufuku mawakala wanaotoza faini za kuegesha magari vibaya katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Ubungo hadi hapo yatakapotengenezwa maeneo rasmi kwa ajili ya maegesho ya magari.

Makonda alitoa kauli hiyo jana wakati alipofanya ziara kujionea hali halisi ya kituo hicho.

Alisema haiwezekani mawakala wakaendelea kutoza faini za maegesho ambayo si sahihi wakati katika eneo hilo hakuna maeneo maalumu kwa ajili ya maegesho ya magari.

“Nataka maeneo rasmi yakishatengwa ndipo muanze kutoza faini, mmekuwa mkiwasumbua wananchi hawajui wapi ni sehemu ya maegesho na wapi si sehemu ya maegesho wekeni alama ndipo muanze kuwatoza,” alisema Makonda.

Licha ya kutoa kauli hiyo, Makonda pia alimtaka Mkurugenzi wa Jiji kabla ya kumalizika wiki hii kuhakikisha kituo hicho kinawekwa taa ili kuondoa usumbufu wanaokutana nao abiria na wananchi hasa wakati za usiku.

"Lakini kabla ya wiki hii haijaisha nataka kuona taa zote za ubungo zinawaka, sitaki kuviona vifusi katika eneo hili la stendi na baada ya siku 20 nitarejea kujionea utekelezaji wake kama umekamilika"  Alisema  Makonda

Katika hatua nyingine, Makonda alisema kuwa serikali ipo katika mpango mwisho wa kuihamishia stendi hiyo kutoka ubungo kwenda Mbezi mwisho.

"Shahuku yangu ni kuwa na stendi tofauti na tuliyonayo, nataka Dar es salaam iwe na stendi ya kimataifa na tayari tunalo eneo kule mbezi ambapo halmashauri ya jiji tayari ipo kwenye mchakato wa kukamilisha ujenzi huo.

"Nataka kuihamisha hii stendi ya ubungo ili tuepukane na kero ya kukutana na mabasi ya mwendo kasi kwakuwa nayo ni moja ya changamoto, duniani kote maroli  yakiingia katikati ya mji hutumika kubeba mikate ajabu Dar es salaam maroli yanabeba ngano na makontena"


Serikali Yalifunga gazeti la Mseto kwa miezi 36

$
0
0

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifungia kwa miezi 36  gazeti la “MSETO”. Amri ya kulifungia  Gazeti hilo imetolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 242 lililotolewa tarehe 10 Agosti, 2016. Uamuzi huo umetolewa kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 Sura ya 229, kifungu 25(1).

Kifungu hicho kinasema “Waziri akiona kwamba kwa ajili ya manufaa ya umma au kwa ajili ya kudumisha amani na usalama inafaa afanye hivyo aweza kutoa amri na kuitangaza kwenye Gazeti la Serikali ambayo itaeleza kwamba gazeti lililotajwa katika amri hiyo litakoma kutolewa tangu siku (ambayo katika fungu hili itaitwa ''tarehe ya kuanza kutumika'') itakayotajwa katika amri hiyo”

Uamuzi huo unazuia gazeti la Mseto kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.

Aidha, hatua hii ya kulifungia gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Septemba, 2012 hadi Agosti,  2016  kumtaka Mhariri wa gazeti kuacha kuandika habari za upotoshaji, uchochezi na za uongo na zisizo zingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari bila mafanikio.

Kutokana na hali hiyo, Serikali kwa masikitiko makubwa, imelazimika kuchukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo wa kuandika na kuchapisha habari ya uongo na kughushi kwa kutumia nyaraka mbalimbali za Serikali kwa nia ya kumchafua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wa Serikali kwa lengo kutaka  kumchonganisha na wananchi ambao wamekuwa na matarajio makubwa kwa uongozi wa Awamu ya Tano.

Pamoja na makosa mengine, hivi karibuni gazeti lao katika toleo Na. 480 la tarehe 4 hadi 10 Agosti, 2016 lilichapisha na kusambaza makala na barua ya kugushi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) yenye kichwa cha habari kisemacho  “Waziri Amchafua JPM” Amhusisha na rushwa ya uchaguzi mkuu, ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano.

Kwa mujibu wa vyombo vya uchunguzi vya Serikali, imebainika kwamba nyaraka hiyo imeghushiwa na wahariri na walipotakiwa kuleta uthibitisho wa nyaraka waliyotumia katika gazeti lao, walishindwa kuleta vithibitisho hivyo

Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari ambayo ukizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote. Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo.

Serikali ya Tanzania imeridhia mikataba mbalimbali ya Kimataifa inayoanisha uhuru na mipaka ya habari kama vile Tamko la Kimataifa la haki za Binadamu la mwaka 1948, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa, na Mkataba wa Afrika juu ya Haki za Binadamu na Watu 1981.

Mikataba na matamko hayo kwa pamoja licha ya kuanisha uhuru wa habari ambao Tanzania imeruhusu kwa kiwango kikubwa pia, imeweka ukomo wa uhuru huo kwa kukataza habari za uongo, uzushi na uchochezi.

Ninapenda  kusisitiza kwamba Serikali itaendelea kujenga uhusiano mzuri na wa kirafiki kati yake na wadau wa sekta ya habari. Aidha ninasisitiza tena wadau wa sekta hii kuzingatia Sheria, kanuni na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari ili kujenga heshima ya tasnia ya habari na kulinda amani ya nchi yetu.

Mhe. Nape M. Nnauye (Mb,)
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Mahakama Kuu yatengua hukumu ya awali ya kuwafutia shtaka la utakatishaji fedha aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Kitilya na wenzake

$
0
0


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua uamuzi uliotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Emmilius Mchauru wa kufuta shtaka la kutakatisha Dola Milioni 6 za Kimarekani baada ya kuona liliondolewa kinyume cha sheria!

Kesi hiyo inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) (pichani kati) Harry Kitilya na wenzake dhidi ya mashtaka manane ikiwamo la kutakatisha fedha na walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Aprili Mosi Mwaka huu. 

Akisoma uamuzi huo Jaji Edson Mkasimongwa alisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili mahakama yake imeona Hakimu Mchauru wa Mahakama ya Kisutu alikosea kuliondoa shtaka hilo na kwamba shtaka la kutakatisha fedha litabaki kama lilivyofunguliwa katika hati ya mashtaka.

"mahakama ya Kisutu ilikosea kisheria kulifuta shtaka la 8 na ninaamuru kurejesha kumbukumbuku ya jalada la kesi hii kwa ajili ya kuendelea kusikilozwa" alisema Jaji Mkasimongwa.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania 1996 Shose Sinare na Sioi Solomon ambao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mchauru.

Awali, jopo la mawakili wa utetezi liliwasilisha maombi ya kuliondoa shtaka la nane ya kutakatisha fedha na mahaka?a ya Kisutu ilikubali na kuliondoa.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Osward Tibabyekomya ulowasilisha nia ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam alitupilia mbali rufaa hiyo baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kwamba mahakama yake haina mamlaka ya kusikiliza rufaa ya kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha.

Upande wa Jamhuri ulikata rufani katika Mahakama ya Rufani Tanzania.

Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jopo la Majaji watatu ikiongozwa na Bernad Luanda,Salum Masati na Aristoclas Kaijage liliamuru jalada la kesi hiyo kurejeshwa mahakama kuu na  kupangiwa jaji mwingine wa kusikiliza rufaa ya Jamhuri.

Jalada hilo lilipangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Mkasimongwa.

Rais Magufuli Ahutubia Maelfu Ya Wananchi Wa Jiji La Mwanza Uwanja Wa Furahisha Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa mkoa wa Mwanza na maeneo ya kanda ya ziwa katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha eneo la Kirumba jijini humo. 

Umati wa wananchi ukiwa umefurika kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Agosti 12

Taarifa Toka IKULU Kuhusu Maagizo ya Rais Magufuli Aliyoyatoa Jana Jijini Mwanza

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuchunguza na kuchukua hatua za kurejesha mali za Chama Kikuu cha Ushirika cha  Nyanza ambazo zilinunuliwa na kutwaliwa na watu binafsi kwa njia za ujanja ujanja.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo tarehe 11 Agosti, 2016 alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Dkt. Magufuli alisema Serikali yake haipo tayari kuwafumbia macho watu wachache waliovifilisi vyama vya ushirika vya wakulima kwa kujimilikisha mali za ushirika yakiwemo majengo, viwanda na mashamba na ametaka mali hizo zirudishwe mikononi mwa wananchi.

"Hata kama walichukua miaka 20 iliyopita, vyombo vya dola vichukue hatua na mali hizo zirudishwe kwa umma" Alisema Rais Magufuli.

Katika Mkutano huo Rais Magufuli pia alisema Serikali itafanya oparesheni kubwa ya kuteketeza Makokoro katika ziwa Victoria ikiwa ni juhudi za kukabiliana na tatizo la uvuvi haramu uliosababisha kupungua kwa samaki na kuathiri shughuli za uvuvi na usindikaji wa minofu ya samaki katika viwanda.

Alibainisha kuwa lengo la kuchukua hatua hiyo ni kuwezesha samaki wengi kuzaliana ili lengo la Serikali la kujenga viwanda vya kusindika mazao ikiwemo viwanda vya kusindika minofu ya samaki lifanikiwe.

Kabla ya kuhutubia mkutano huo Rais Magufuli aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la waenda kwa miguu la Furahisha linalokatiza barabara ya Uwanja wa Ndege kwenda katikati ya Jiji la Mwanza.

Daraja hilo litakuwa na urefu wa meta 46, upana wa meta 3.6 na kimo cha meta 5.5 na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Mwezi Desemba Mwaka huu kwa gharama ya Shilingi Bilioni 6.455

Akizungumzia ujenzi huo Rais Magufuli alimtaka Mkandarasi anayejenga Daraja la Furahisha kukamilisha kazi hiyo Mwezi Desemba Mwaka huu kwa mujibu wa mkataba, na pia ameagiza Mkandarasi aliyekuwa akifanya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuendelea na kazi hiyo ndani ya wiki moja kwa kuwa Serikali imejipanga kumlipa fedha za kazi hiyo.

Pia Dkt. Magufuli ameahidi kuongeza fedha katika ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Katikati ya Jiji la Mwanza hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza ili barabara hiyo ifike hadi uwanjani badala ya kuishia eneo la Pasiansi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Mwanza

11 Agosti, 2016

NMB Yazindua Tawi Katika Jengo La Rock City Jijini Mwanza

$
0
0
Benki ya NMB imeendelea kutanua mtandao wa matawi yake nchini ili kuwa karibu zaidi na wateja wake. Mwishoni mwa wiki iliyopita, NMB ilizindua tawi jipya la NMB Rock City lililopo ndani ya jengo jipya la kibiashara la Rock City jijini Mwanza.

Tawi hili linafanya jumla ya matawi ya NMB kwa Mwanza mjini kufikia matano na 28 kwa kanda nzima ya ziwa ni imani ya NMB zinduzi huu unaleta tumaini jipya kwa wateja wa NMB jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla. 

Huduma zinazotolewa na tawi hili jipya ni pamoja na kufungua akaunti, mikopo, huduma ya fedha za kigeni, huduma za kuweka na kutoa fedha.

Katika kuhakikisha kuwa NMB inahudumia makundi mbalimbali ya wateja wake kulingana na mahitaji yao ya kifedha, wiki iliyopita, benki iliendesha mkutano wa Klabu ya Biashara uliowakutanisha pamoja zaidi ya wateja 300 wanaohudumiwa na matawi ya NMB ya jijini Mwanza.

 Baadhi ya faida zilizopatikana katika mkutano huo ni pamoja na mafunzo ya jinsi ya kukuza biashara, elimu ya mlipa kodi, jinsi ya kutunza daftari la biashara na njia mbalimbali za kuboresha biashara.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela (katikati) akikata utepe kuzindua tawi la Rock City Mall la benki ya NMB jijini Mwanza, wa tatu kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB Bi Magreth Ikongo na wa tano kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ineke Bussemaker.

Meneja wa NMB kanda ya ziwa- Abraham Augustino akiongea katika mkutano wa klabu ya biashara uliofanyika jijini Mwanza wiki iliyopita. Zaidi ya wateja 300 walihudhuria mkutano huo ambapo pamija na mambo mengine walipata mafunzo ya jinisi ya kukuza biashara, elimu ya mlipa kodi na njia mbalimbali za kuboresha biashara.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurungezi ya NMB- Margaret Ikongo akizungumza katika mkutano wa Klabu ya Biashara jijini Mwanza.

PICHA: Rais Magufuli Akiweka Jiwe La Msingi Daraja Wa Waenda Kwa Miguu La Furahisha Pamoja Na Upanuzi Wa Barabara Ya Mwanza Airport

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kuhakikisha kuwa ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu na upanuzi wa Barabara ya Makongoro jijini Mwanza unakamilika ifikapo disemba mwaka huu.

Aidha amesema upanuzi wa barabara ya Makongoro uliokuwa ujengwe kati ya Furahisha hadi Pasiansi Km 2.8 sasa utaendelezwa hadi kufikia uwanja wa ndege.

Akizungumza jana  mara baada ya kuweka jiwe la msingi la daraja la watembea kwa miguu na upanuzi wa barabara ya Makongoro Mh. Dkt. Magufuli alisema kasi ya ujenzi wa barabara jijini Mwanza uendane na ujenzi wa uwanja wa ndege ili kuwezesha mkoa wa Mwanza kuwa kitovu cha nchi za maziwa makuu.

“Nakuagiza Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  uhakikishe kuwa barabara na daraja la watembea kwa miguu Furahisha vinakamilika mwezi desemba na mkandarasi wa uwanja wa ndege anaanza kazi mara moja”.
Alisisitiza Rais Dkt. Magufuli.

Alisema nia ya Serikali yake ni kununua meli mbili na kujenga daraja kati ya Kigongo na Busisi ili kuboresha huduma za usafiri katika Ziwa Victoria.

Naye Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale alimtaka mkandarasi anaejenga daraja la waenda kwa miguu na barabara ya Makongoro kuhakikisha ujenzi wake unakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Zaidi ya shilingi bilioni 6.4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo utakaopunguza msongamano wa magari na ajali katika barabara ya makongoro jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Mbunge wa Sumve Richard Ndassa wakipiga makofi mara baada ya tukio la uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na Upanuzi wa barabara ya Mwanza-airport.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya namna daraja la Furahisha litakavyokuwa mara baada ya kukamilika.

Viongozi Wa Shirika La Jinsia Moja ( LGBT VOICE) Matatani......Naibu Waziri wa Afya Awataka Wafike Wizarani Leo Bila Kukosa

Shibuda aibukia mkutano wa Rais Magufuli Mwanza.....Awapa Neno UKAWA

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda jana alijitokeza katika mkutano wa Rais Dkt. John Magufuli katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza na kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa namna ambavyo anatatua kero za wananchi.

Akihutubia maelfu ya wakazi wa Mwanza na maeneo jirani waliojitokeza kumsikiliza Rais Dkt. Magufuli , Shibuda alivitaka vyama vingine vya siasa nchini kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuwa kazi anayoifanya ni kwa ajili ya watanzania wote.

"Mheshimiwa Rais Magufuli endelea kuwahudumia watanzania na nikuambie sijawahi kuona mchongoma unang’olewa kwa upepo au sijawahi kuona utelezi wa mlenda unamwangusha mtu mzima" - Alisema Shibuda.

Shibuda alisema vyama vya UKAWA vinapaswa kutambua kwamba Rais Dkt. Magufuli ni mtu mzuri ndiyo maana aliwasaidia kumaliza mgogoro wa uchaguzi wa Meya Jijini Dar es Salaam hivyo watambue mchango wake kwa taifa .

Aidha Shibuda alimuomba Rais  Magufuli kwamba akipata muda aende akamweleze vizuri matatizo yanayowakabili wakulima nchini.

Rais Magufuli Akerwa na Uozo Uliopo Ndani ya CCM.......Aagiza Jiji la Mwanza Lisiwatoze Kodi Wafanyabiashara Wadogowadogo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuna mambo ya hovyo ambayo yapo ndani ya Chama cha Mapinduzi ambayo yanahitaji kuhojiwa na kupatiwa majibu yenye tija.

Aikihutubia maelfu ya wananchi jana waliojitokeza kumsikiliza katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza Dkt. Magufuli alisema anafahamu kwamba ndani ya CCM kuna mambo ya hovyo na mfano ni uwanja wa CCM Kirumba na majengo mengine ya CCM ambayo ukiuliza maduka na ofisi zinazozunguka majengo hayo mapato yake yako wapi huwezi kupata majibu ya kuridhisha.

"Ninyi wananchi wa Mwanza na wanachama wa CCM hojini haya na atakayewauliza mwambieni ni mimi Mwenyekiti wa CCM nimesema muwaulize, nataka chama ambacho mali zake zinajulikana kwa sababu ukienda kuwauliza mnakusanya shilingi ngapi kwa chumba kimoja wanaweza kukuambia ni elfu 50 kumbe wanaingiza laki 5" Alisema Rais Dkt. Magufuli

Rais Magufuli alisisitiza kwamba anaitaka CCM ya Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius Nyerere siyo CCM ya watu ambao mchana wapo CCM na usiku wapo vyama vingine, wanaofanya hivyo ni bora wahamie huko moja kwa moja.

Aidha katika hatua nyingine Rais Dkt. Magufuli ameagiza uongozi wa Jiji la Mwanza kutowatoza ushuru wajasiriamali wadogo wadogo kwa kuwa wanatakiwa wanufaike na taifa lao na pia wamachinga waachwe mjini kwanza hadi hapo watakapo andaliwa mazingira mazuri ya kufanyia biashara yatakayokuwa na wateja.

Serikali: Hatuna ushahidi wa kuzihukumu shule za Feza, Hivyo Hatuwezi Kuzifunga

$
0
0

SERIKALI imesema haina ushahidi wa kutosha kuzitia hatiani shule za Feza nchini zinazodaiwa kumilikiwa na mmoja wa wananchi wa Uturuki anayetuhumiwa kujihusisha na ugaidi na kuitaka Serikali ya Uturuki kuwasilisha taarifa zenye ushahidi wa kutosha kuhusu tuhuma hizo.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga.

Alisema walipokea madai kutoka Ubalozi wa Uturuki nchini kuwa shule hizo zinamilikiwa na mmoja wa wananchi wa nchi hiyo anayejihusisha na ugaidi.

Balozi Mahiga alisema katika madai ya ubalozi huo, shule hizo ni miongoni mwa miradi inayomilikiwa na mtuhumiwa huyo na kwamba, baadhi ya walimu wake hutumia mbinu za kigaidi kufundisha wanafunzi.

Akijibu tuhuma hizo, Balozi Mahiga alisema serikali kabla ya kutoa kibali kwa mwekezaji au mfanyabiashara yeyote kuendesha shughuli zake nchini, vyombo vya usalama nchini, hufanya upelelezi wa kina na wamejiridhisha kwamba wafanyabiashara wa Uturuki waliopo nchini wanafanya biashara halali.

“Ni kweli tumepokea tuhuma kutoka kwa Ubalozi wa Uturuki nchini kuhusu shule za Feza kwamba ni sehemu ya makundi ya kigaidi, lakini hatuwezi kuzitia hatiani shule hizo hadi tuletewe ushahidi wa kutosha,” alisema Balozi Mahiga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule za Feza, Habib Miradji alisema shule hizo ni za asasi iliyosajiliwa kisheria na Serikali ya Tanzania hivyo ni mali ya Tanzania na endapo kuna kitu au tatizo ni lazima wawasiliane na serikali na watafika kukagua ili kama kuna lolote baya hatua zichukuliwe.

Aidha alisema kwamba shule hazijafungwa.

Rais Magufuli atua Jijini Dar, Apokelewa kwa Shangwe na nderemo

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia kuwasalimia wanaCCM waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, jijini Dar es salaam akitokea jijini Mwanza. 

Vyama 10 Vya Upinzani Vyaungana Kuupinga UKUTA Wa Chadema

$
0
0

VIONGOZI wa vyama vya siasa wanaounda Klabu ya Viongozi wamesema hawaungi mkono maandamano yaliyopangwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika kulinda amani ya nchi.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Fahmi Dovutwa alisema uamuzi wa kutounga maandamano hayo imefikiwa kwenye kikao cha viongozi wa vyama wa siasa wa klabu hiyo waliokutana jana kujadili hali ya siasa nchini.

“Vyama vya siasa tumekutana leo (jana) ili kufanya tafakari juu ya hali ya siasa nchini hususan tamko la Chadema la kufanya maandamano na hatimaye mikutano sehemu mbalimbali. Pia tumezingatia tamko lililotolewa na Serikali na Rais John Magufuli la kutaka amani ya nchi idumishwe, hivyo hatuungi mkono maandamano,” alisema.

Alisema pamoja na kutounga mkono, viongozi hao wanataka kufanyika kwa mkutano ambao utashirikisha vyama vyote vya siasa nchini ili kupata muafaka ambao utaepusha nchi kuingia katika malumbano na misuguano.

“Tarehe waliyopanga kufanya hayo maandamano ni maadhimisho ya Siku ya Majeshi Duniani kote, hivyo wanajeshi watakuwa na shughuli zao ambazo zinaweza kuleta taswira ya jeshi kuingilia maandamano, lakini jambo la msingi ni kurudi kwenye meza ya mazungumzo kwa vyama vyote,” alisema Dovutwa.

Vyama vilivyohudhuria mkutano huo ni Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Alliance For Tanzania Farmers Party (AFP), Chama cha Democratic (DP), D-Makini, JAHAZI Asilia, Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD), United Peoples Democratic Party (UPDP), ADA-TADEA na Chama Cha Kijamii (CCK). 

Hivi karibuni, Chadema ilitoa tamko la kufanya maandamano na mikutano nchi nzima katika kampeni waliyoiita Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA).

Azma ya Chadema inakuja baada ya siku kadhaa za Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano kwa sababu za kiusalama. 

Hata hivyo, Rais Magufuli alipiga marufuku maandamano hayo kwa lengo la kutaka amani ya nchi idumishwe na kuelekeza mikutano ya hadhara ya wabunge walioshinda ifanywe kwenye majimbo yao.

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 30

$
0
0
Mtunzi:ENEA FAIDY
....Dorice aliendelea Julia huku matone yake ya machozi yakiwa damu. Ghafla akajikuta ana uwezo wa ajabu ambao hajawahi kuufikiria kuwa nao hata siku moja. Alijibadilisha sura na kuwa kiumbe wa kutisha, macho yalikuwa kama ya paka, uso wake ukawa mweusi tii kama mkaa, kucha zake zikawa ndefu sana na meno yake mawili yalichomoza nje ya kinywa chake. Mansoor alicheka kicheko kikali cha kutisha huku sauti ya kicheko chake ikiambatana na mwangwi. Radio zikapiga mfululizo Dorice akatoweka ghafla na kumuacha Mansoor.

Pete aliyokuwa amevalishwa Dorice ilimpa uwezo mkubwa na wa ajabu. Alipata uwezo wa kupotea na kujibadilisha kadri atakavyo lakini sharti kubwa alilotakiwa kufanya ilikuwa ni lazima arudi tena kwa Mansoor baada tu ya kumaliza kazi yake inayompeleka duniani.

Dorice alikuwa ametokeza katika eneo lenye Giza Giza lilitawaliwa sauti za wadudu. Palikuwa na utulivu mkubwa sana , kwani eneo lile halikukaliwa na mtu yeyote zaidi ya ndege, wadudu na wanyama wadogo wadogo. Dorice alibaki anajishangaa, alijiuliza amefika vipi eneo lile akiwa peke yake bila Mansoor.

"Ina maana nimekuwa na nguvu za kijini?" Alijiuliza Dorice. Ghafla upepo mkali ukapuliza eneo lile, Dorice alitazama huku na kule ili kujua nani alikuwa mgeni wake kwa wakati ule. Ghafla Mansoor akajitokeza akiwa anacheka kicheko cha kutisha sana kisha akapiga hatua za taratibu kumsogelea Dorice.

"Kwanini umefika huku?" Aliuliza Mansoor kwa ghadhabu.
"Sijui nimefikaje" alijibu Dorice.
"Muda wako wa kuondoka kwenye himaya yangu bado Dorice, nilikuwa na jaribu kukupa ladha ya vile utakavyokuwa baada ya wakati kutimia" alisema Mansoor.
"Kwahiyo unataka nirudi?"
"Ndio.. Tunarudi wote".

"Hapana Mansoor sitaki kurudi tena Kule" alisema Dorice.
"Ni lazima urudi maana bado sijakupa maelekezo"
"Hayo maelekezo nipe hapa hapa"
"Haraka haraka ilimfanya chura apate ngozi ya mabaka"
"Hata hivyo siwezi kurudi".

Yalizuka mabishano makali baina ya Dorice na Mansoor kwani Dorice hakutaka kurudi kwenye himaya ya Mansoor tena. Alitaka aachwe huru na arudi kwao, lakini mkongwe ni mkongwe tu licha ya mabishano Yale Mansoor aliibuka mshindi baada ya kumchukua Dorice kinguvu kwa kutumia uwezo mkubwa wa kijini alionao. 

Katika eneo walilokuwepo ukatokea upepo mkali na kuwavuta wote wawili kisha ndani ya muda mfupi walijikuta wametokea katika himaya ya akina Mansoor. Dorice alikasirika sana.


Tahadhari Dhidi Ya Matapeli Kwa Waombaji Wa Mikopo HESLB

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwatahadharisha  waombaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017 na umma kwa imepokea taarifa kuwa kuna watu wasio waaminifu ambao si watumishi wa Bodi huwapigia simu baadhi ya waombaji kwa lengo la kuwatapeli.

Taarifa hizo za kitapeli zimekuwa zikisambazwa katika siku za hivi karibuni kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zikiwataka baadhi ya waombaji wa mikopo au wadhamini wao kutuma fedha (Tshs 39,000/-) kwa namba ya simu 0716463190 ili fomu zao za maombi ya mikopo zilizowasilishwa Bodi zirekebishwe kwa kuwa zimeonekana zina makosa na hivyo hawatapata mikopo.

Namba inayotumika kusambaza taarifa hiyo au kupiga simu kutoa taarifa hizo ni 0764640325 na mtu anayepiga anajitambulisha kwa jina la Charles Amos.

Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale walioomba mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kuwa taarifa hizo si za kweli. Mtu huyo ni tapeli na si mtumishi wa Bodi ya Mikopo.

Iwapo waombaji watapigiwa simu na matapeli hao, watoe taarifa kwa vyombo vya dola kwa hatua zaidi.

Aidha, Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu waombaji wa mikopo kuwa utaratibu wa Bodi kuwasiliana na waombaji wa mikopo ambao fomu zao za maombi hubainika kuwa na upungufu haujabadilika. Mara baada ya kazi ya ukaguzi wa fomu kukamilika, Bodi ya Mikopo itatoa taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo tovuti yake (www.heslb.go.tz) na kuwaalika waombaji kufanya marekebisho.

Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya Bodi iliyotajwa hapo juu.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
IJUMAA, AGOSTI 12, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Agosti 13

Mwanamke abakwa, auawa na kutupwa kichakani

$
0
0

MWANAMKE anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40, amekutwa amekufa katika mazingira yanayoonesha kwamba alibakwa kabla ya kuuawa na kutupwa kichakani.

Mwili wake ulionekana Agosti 10, mwaka huu saa 7.30 mchana katika Kijiji cha Iringa Mvumi, Kata ya Mvumi, Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amesema kwamba wanamfanya msako waliotenda unyama huo ili wawafikishe katika mkondo wa sheria.

Alitoa mwito kwa wakazi wa Kijiji cha Iringa Mvumi na vijiji vya jirani kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwafichua wahalifu hao ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Wakati huo huo, Mahakama ya Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma imemtupa jela miaka 30 mkazi wa Kijiji cha Mlali Iyengu, Mkengela Mchechele (27) baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 11.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kongwa, Mary Senapee pamoja na kumtupa jela miaka hiyo, pia aliamuru mtuhumiwa kuchapwa viboko 12 na akitoka jela alipe fidia ya Sh milioni moja.

Mzee Yusuph ameacha muziki na kumrudia Mungu

$
0
0
Mfalme wa muziki wa taarabu mzee Yusuph maarufu kama "mfalme wa taarabu" amefunguka na kusema kuwa sasa ameamua kuachana na muziki huo na kumrudia Mungu huku akiwataka watanzania pia kumrudia Mungu.

Akiongea jana baada ya kumaliza swala ya Ijumaa kweneye msikiti wa Ilala Bungoni (Masjdi Taqwa) Mzee Yusuph alisema kwa taarifa za awali watanzania wanatakiwa kutambua kuwa yeye ameachana na muziki na sasa amemrudia Mungu na kuwataka kuwa na subira kwani atatafuta siku maalum yeye kutangaza suala hilo ambapo atafunguka kwa kirefu zaidi kwanini ameamua kufanya maamuzi hayo.

"Ni kweli nimeamua kuachana na muziki na sasa nimemrudia Mungu, nawaomba watanzania wengine pia wamrudie Mungu, nitatafuta siku ambayo nitaongea kwa kirefu zaidi juu ya suala hili, hivyo watanzania watambue tu nimeachana na muziki sasa" alisema Mzee Yusuph.

Hii ni mara ya pili kwa mzee Yusuph kutangaza kuacha muziki kwa mara ya kwanza ilikuwa mwaka jana, alitangaza kuacha muziki na kuingia kwenye siasa lakini hakuweza kufanya vizuri kwenye siasa na kurudi tena kwenye muziki.

Chadema Yaanza Kugawa Vifaa vya Operesheni UKUTA

$
0
0
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani kimeanza kugawa vifaa zikiwemo bendera kwa ajili maandalazi ya Umoja wa Kupinga Udikteta ( Ukuta) ambayo yanatarajia kufanyika Septemba mosi mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Kanda ya Pwani wa Chadema, Casimir Mabina, alisema kuwa bendera hizo zitaanza kupeperushwa kuanzia kesho kutwa kwa ajili ya kuunga mkono azimio la Kamati Kuu ya kufanyika oparesheni Ukuta.

Alisema oparesheni Ukuta ni lazima ifanyike nchi nzima na kwamba hawako tayari kuona ukandamizaji wa demokrasia unaoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano ambayo imeonyesha viashiria vya utawala wa kidikteta.

Alisema Rais John Magufuli, anajaribu kuua demokrasia ya vyama vingi kwa kukataza na kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani huku CCM ikiendelea na mikutano yake kama kawaida.

“Tumeona jinsi Rais alivyopiga marufuku wapinzani kukutana kwenye mikutano ya hadhara huku akiwatishia kuwa wakikaidi atawashughulikia na kweli amewaamuru polisi watekeleze amri hiyo ya kuwakamata viongozi wa Chadema na kuwafungulia mashtaka,” alisema

Aliongezea kuwa mbaya zaidi Jeshi la Polisi linazuia hata mikutano ya ndani ya vyama vya upinzani na makongamano na hata mahafali ya wanafunzi wenye itikadi za upinzani licha ya kutambua kuwa mikutano ya ndani haiwezi kuleta uvunjifu wa amani kwa walio ndani ya ukumbi.

Alisema licha ya kwamba Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli. amekataza mikutano hiyo kufanyika chama tawala, kinafanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali kwa kisingizio cha shughuli za serikali.

Mabina alisema juzi CCM ilisema itakuwa na maandamano kutoka uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ya kumpokea Rais Magufuli hadi Makao Makuu ya CCM yaliyopo Lumumba.

“Tunahoji haki ya kufanya siasa ni kwa CCM tu na siyo kwa vyama vingine? Hili jambo hatuwezi kukubali Jeshi la Polisi lituambie inakuwaje vibali vinatolewa kwa CCM halafu upinzani tunyimwe tunasema lazima tufanye oparesheni Ukuta ya kupinga ukandamizaji wa demokrasia,” alisema Mabina

Naye Katibu wa Wabunge wa Upinzani Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Viti Maalum, Anatropia Theonest, alisema lengo la oparesheni ya Ukuta ni kupinga ukandamizaji unaofanywa na serikali.

Alisema wana haki ya kikatiba ya kufanya mikutano bila kuzuiliwa kama ambayo wamefanyiwa na ndio maana wameanza kugawa bendera kwa ajili ya kujiandaa na oparesheni hiyo.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images