Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

TCRA Yavipiga Faini ITV, Clouds Tv na Clouds Fm Radio Kwa Kukiuka Maadili ya Utangazaji

$
0
0

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevipa onyo na kuvipiga faini vituo viwili vya televisheni na kimoja cha redio kwa kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo ni ITV, Clouds Tv na Clouds Fm Radio, vyote vya jijini Dar es Salaam, ambavyo kwa ujumla vimepigwa faini ya Sh milioni 19.

Akitoa uamuzi uliofikiwa na Kamati ya Maudhui ya TCRA, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Mapunda alisema vituo hivyo vilibainika kukiuka Kanuni za Huduma za Utangazaji na kuvitaka kuwa wasimamizi wazuri wa vipindi vyao.

Mapunda alisema kamati hiyo imekipa onyo na kukipiga faini ya Sh milioni 10 kituo cha televisheni cha ITV kwa makosa mawili; la kwanza ni kupitia kipindi chake cha Kumekucha cha Juni 15, mwaka huu kati ya saa 1:00 na 1:30 asubuhi ambacho mtangazaji alifanya mahojiano na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kuhusu mwenendo wa Bunge la Bajeti, na Mchungaji Msigwa alitamka maneno ya kashfa dhidi ya Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

“…mtangazaji hakuchukua jitihada za kumwomba Mheshimiwa Peter Msigwa kufuta lugha ya matusi aliyoitumia, bali alionekana akifurahia na kuendelea kumuuliza maswali mengine,” alisema Mapunda.

Katika kosa la pili, Mapunda alisema kituo hicho kilikiuka kanuni katika taarifa ya habari ya Juni 23 kati ya saa 1:00 na 2:00 asubuhi, kilitangaza taarifa ya msichana wa miaka 16 aliyebakwa na kupewa ujauzito na walitumia utambulisho wa msichana huyo kwa jina na shule anayosoma.

Katika utetezi wake, Mwakilishi wa ITV, Stephen Chuwa alikiri kuwa Mchungaji Msigwa alitoa maneno ya kashfa na hakutembea katika ahadi yake ya kutomkashifu mtu.

Aidha alisema kama mtangazaji angemuomba kufuta kauli, mjadala ungekuwa mkubwa zaidi. Alisema watachukua hatua za kumwomba radhi Dk Tulia kutokana na kashfa hiyo.

Kwa upande wa Kituo cha Clouds Tv, kituo hicho kimepewa onyo na kupigwa faini ya Sh milioni nne ambazo wanapaswa kulipa ndani ya siku 30 kuanzia siku ya hukumu.

Mapunda alisema kituo hicho kupitia kipindi chake cha Hip Hop, kilichorushwa kati ya saa 8:00 mchana na 12:00 jioni, kilirusha video ya nyimbo za Asanteni kwa Kuja wa Mwana FA na Break It Down wa Lil Bebbie, ambazo zinadhalilisha utu wa mwanamke.

Aidha, Clouds Fm pia imepewa onyo na kupigwa faini ya Sh milioni tano kwa vipindi vyake vya ‘Power Breakfast’ na Jahazi kwa walikiuka kanuni za utangazaji.

Alisema katika kipindi cha Jahazi cha Mei 9, kilichorushwa kati ya saa 10:00 hadi 12:55 jioni, watangazaji walisikika wakishabikia taarifa ya mtu kufanya ngono na mbuzi, ambako walieleza kuwa mtu huyo na mbuzi ni kama mtu na mpenzi wake, jambo lililoonesha wanahamasisha vitendo hivyo.

Aidha, Mei 18, mwaka huu katika kipindi cha Power Breakfast, kilichorushwa kati ya sa 12:00 na 4:00 asubuhi baada ya kusoma taarifa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhusu kupandikizwa kwa sehemu za siri za kiume kwa mtoto wa miaka mitatu, aliyezaliwa akiwa hana na kulelewa kama mtoto wa kike.

Serikali Yatoa Siku 14 kutatua changamoto za watumishi Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)

$
0
0
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa siku 14 kwa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mifupa (MOI) kuangalia matatizo yaliyopo na kuyafanyia tathmini, huku akisisitiza kambi za upasuaji zirejee na zianze kazi mara moja ifikapo Agosti 13, mwaka huu.

Alisema bodi hiyo itakapokaa na kurudisha majibu kwake atafanya maamuzi likiwamo suala la uteuzi wa mkurugenzi wa taasisi hiyo, akisema imekaimiwa kwa kipindi kirefu na sasa ni wakati wa kumpata wa kuishikilia.

“Kitu kinachonisumbua kichwa kwa sasa ni kuhusiana na kambi za upasuaji, naomba zianze kazi mara moja, wanaoteseka ni wananchi wa hali ya chini maana baada ya kufutwa kambi za upasuaji ikaanzishwa kambi ya upasuaji wa watu wanaolipia, wasiojiweza wanahudumiwa vipi?” alihoji.

Kauli ya Ummy imekuja baada ya kikao cha ndani alichokifanya jana na wafanyakazi wa taasisi hiyo, ambao walitoa malalamiko mbalimbali kuhusu utendaji wa taasisi, stahiki zao pamoja na malalamiko mengine waliyoyaandika kwenye makaratasi na kuwasilisha kwake.

“Baada ya kuwaambia muandike kwenye vikaratasi, nimegundua kwamba mlishindwa kusema wazi ila molari ya wafanyakazi ipo chini na baada ya kusoma kwa makini nimegundua hakuna ushirikiano wa kutosha,” alisema Ummy.

Ummy alisema katika kutatua changamoto kadhaa ndani ya taasisi ataanza kwa kupeleka CT Scan mpya, lakini pia bajeti ya vifaa tiba kiasi cha Sh3 bilioni.

Aliunga mkono wazo la madaktari wa taasisi hiyo ambao walimtaka kupeleka muswada bungeni wa kupitisha sheria ya malipo ya kuchangia huduma katika mfuko wa Trauma Fund kwa watu wote wanaotumia vyombo vya usafiri ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaopata ajali.

“Naunga mkono hoja hii, lakini siwezi kuisemea moja kwa moja mpaka ipate baraka kutoka Baraza la Mawaziri, maana ninachokitaka ni kusaidia maskini wasiojiweza ambao ndiyo hao kila siku wanagongwa na pikipiki na magari, ndiyo wahanga wa hizi ajali,” alisema Ummy.

Akizungumza kwa msisitizo, Ummy alisema lengo lake kubwa ni kuhakikisha sekta ya afya inakuwa bora kwa kipindi chake atakachokuwa waziri wa afya huku akiahidi kushughulikia kero mbalimbali za wafanyakazi walizoziwasilisha kwake.

Akizungumza awali Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa (MOI) Dk Othman Kiloloma alisema wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo motisha na posho kwa wafanyakazi.

Alisema deni la MOI limekuwa sababu ya Taasisi kukosa vifaa na vitendanishi kwa wakati kutokana na wasambazaji wengi kushindwa kuhudumia.

Dk Kiloloma alisema mwaka 2014 wakati anapokea Taasisi hiyo kama Kaimu Mkurugenzi alikutana na deni kubwa la stahiki za wafanyakazi kiasi cha Sh4 bilioni pamoja na deni upande wa Saccos kiasi cha Sh500 milioni na kwa sasa wamefanikiwa kulipia Sh600 milioni.

Alisema jengo jipya la MOI bado linahitaji kiasi cha Sh20.6 bilioni ili kukamilisha vifaa vinavyohitajika ikiwemo samani muhimu.

“Tatizo kubwa tunalopambana nalo hivi sasa ni jengo jipya la MOI, ambalo bado hatujakabidhiwa mpaka sasa, kwanza lina upungufu mkubwa ikiwemo lifti kutokufanya kazi, jengo zima ili likamilike linahitaji kiasi cha Sh8.6 bilioni,”alisema Dk Kiloloma. 

Wafanyakazi wafunguka 
Wakitoa malalamiko yao kwa Waziri, wafanyakazi hao walizungumzia mambo makubwa manne likiwemo la stahiki ya mishahara yao na malipo, uchakavu wa vifaa tiba, maendeleo ya rasilimali watu na mrundikano wa wagonjwa.

Pamoja na mambo mengine wafanyakazi hao walilalamikia suala la kutopandishwa vyeo, kutopanda kwa mishahara na malipo ya ziada kuwa hayatoshelezi, huku wengine wakifanya kazi kwa miezi sita bila malipo.

Mmoja wa wauguzi wa MOI, Mwajabu Ali alisema vitanda vilivyopelekwa na Rais John Magufuli baada ya kuzuiwa kwa mchapalo, vimekuwa na upungufu mkubwa ikiwemo kukosa matairi, jambo ambalo linaleta ugumu wa utoaji wa huduma.

Alisema jengo hilo jipya limekuwa na matatizo ya lifti, hivyo inakuwa kazi kubwa kumsafirisha mgonjwa kutoka wodini mpaka kumfikisha katika chumba cha upasuaji au kipimo.

“Tunafanya kazi katika mazingira magumu, vitanda havina matairi, lifti mbovu, hakuna maji, oksijeni za ukutani hakuna, tunatumia mitungi ambayo hata hivyo ni mizito sana kuibeba,”alisema Mwajuma.

Mtaalamu wa usingizi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi MOI, Lucas Magwisa alisema wauguzi wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na stahiki zao kuwa tofauti na madaktari ambao hata hivyo kazi nyingi wanazifanya wao. 
Kaimu Mkurugenizi wa MOI Dkt. Othman Kiloloma akizungumza mbele ya watumishi wa Taasisi ya mifupa muhimbili (MOI) hawapo pichani kabla ya kumkaribisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  hayupo pichani wakati alipokwenda kusikiliza changamoto za watumishi hao jijini Dar es salaam.

Matabibu Mbadala waomba kibali kuishtaki Serikali kuwafutia usajili

$
0
0

MATABIBU wanne wa Tiba Asilia na Mbadala akiwemo mmiliki wa Kliniki ya Sure Herbal, Simon Rusigwa wamewasilisha maombi ya kuomba ruhusa ya kufungua kesi ya kupinga uamuzi wa kufutiwa leseni za kutoa huduma za kitabibu.

Wamewasilisha maombi hayo katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, dhidi ya Baraza la Tiba Asilia na Mbadala, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Mbali na Rusigwa, matabibu wengine waliowasilisha maombi hayo kupitia kwa Wakili Dk Lucas Kamanija, ni Abdallah Mandai wa kliniki ya Mandai Herbalist, Fadhili Kabujanja wa Fadhaget Sanitarium na John Lupimo wa Lupimo Sanitarium.

Maombi hayo yalitakiwa kusikilizwa jana mbele ya Jaji Ama–Isario Munisi wa mahakama hiyo, hata hivyo kabla ya kuanza kusikilizwa, Serikali iliwasilisha pingamizi la awali ikidai kuwa maombi hayo hayakufuata misingi ya kisheria.

Katika pingamizi hilo serikali inadai kuwa maombi hayo yana kasoro kwa kuwa waombaji hawajapita njia zote zinazotakiwa wazifuate ndipo waende mahakamani pia wanadai maombi hayana miguu ya kusimamia kwa kuwa hati ya viapo vya walalamikaji vina upungufu ya kisheria.

Baada ya kuwasilishwa kwa pingamizi, Jaji Munisi aliahirisha shauri hilo hadi kesho saa 8 mchana, ambapo alizitaka pande zote zinazohusika ziwepo ili kusikiliza pingamizi hilo.

Katika maombi yao, matatibu hao wanadai, wameamua kupeleka maombi hayo mahakamani, kwa kuwa wanaamini walifutiwa leseni bila kufuata taratibu za kisheria.

Wamedai wanaamini uamuzi uliochukuliwa umetolewa bila kupitia Kamati ya Maadili ya Baraza la Tiba Asilia na Mbadala, huku wakidai kuwa huo si uamuzi bali zilikuwa tuhuma mpya, lakini hawakupewa nafasi ya kusikilizwa.

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 29

$
0
0

MTUNZI:ENEA FAIDY

.....MR Aloyce alizidi kumkazia macho mkewe akahisi ni mrembo zaidi ya Mama Eddy yule anayemfahamu yeye. Halafu alikuwa na madaha sana kuzidi vile alivyomzoea. Wasiwasi ukamtanda akilini make na kumfanya asimwamini sana mwanamke yule kuwa ndiye mkewe halisi.

"Mbona unaniangalia sana? Umemisi busu langu nini?" Aliuliza Mama Eddy.
"Hapana wala usijali"
"Ok kama wewe hukumiss basi Mimi nilimisi sana kiss lako mpenzi".

Alisema Mama Eddy huku akimsogelea Mr Aloyce kwa ukaribu zaidi na kumshikashika kidevu kwa mahaba. Mr Aloyce alionesha kutojali mguso ule aliopapaswa na mikono laini ya mkewe. Hakuelewa ni sababu zipi zilizomfanya asimjali mwanamke yule kwa kiasi kile ila moyo wake ulikuwa mzito sana.

"Baby mbona hivyo...? Embu usiwashe gari kwanza mpaka unibusu" alisema Mama Eddy kwa sauti iliyojaa mdeko wa kimahaba. Mr Aloyce hakutaka kukiri udhaifu, akaachia usukani na kusogeza mdomo wake karibu na mdomo wa mkewe kisha akambusu.

Busu lile lilimpa nafasi nzuri sana Mama Eddy ya kupenyezapenyeza mpaka kuingiza ulimi wake mdomoni kwa Mr Aloyce. Kisha wakabadilishana mate yao kwa mahaba. Lakini wakati tendon hilo likiendelea, Mwanamke yule alimwachia vitu Fulani Mr Aloyce bila yeye mwenyewe kujua. Na ilikuwa ni dawa Kali ya kumfanya Mr Aloyce amwamini mwanamke yule kuwa ndiye mkewe halisi wakati hakuwa yeye. Alikuwa ni mwanamke kutoka himaya ya akina Doreen na alitumwa nyumbani kwa Mr Aloyce ili afanye kazi muhimu sana aliyotumwa.

Kwa vile alivyomfanyia Mr Aloyce, alifanikiwa kuziteka akili za Mwanaume yule. Baada tu ya busu lile la huba, Mr Aloyce alijkuta akimpenda sana mwanamke yule akijua ndie Mkewe halisi na kumbe haikuwa hivyo. Wasiwasi wake ulifutika kichwani mwake, pendo la dhati likatawala moyoni mwake.

"Tuondoke mume wangu" alisema mama Eddy kwa sauti ya upole iliyojaa huba huku akiwa ameachia tabasamu pana usoni mwake.

"Usijali mke wangu.. Nilikukumbuka sana... Nina imani hata mwanetu anakusubiri kwa hamu sana." Alisema Mr Aloyce huku akishikilia vizuri usukanu na kuondoa gari kwa kasi sana.

Mr Aloyce aliendesha gari kwa kasi ya ajabu na baada ya masaa machache tu waliwasili eneo la Ipogoro Iringa kisha wakaelekea nyumbani kwao.

Walifika getini wakapiga honi geti lilifunguliwa. Mr Aloyce aliegesha gari pembeni kisha akashuka kwa furaha kubwa, na baada ya hapo akaelekea upande wa pili wa gari yake na kumfungulia mkewe huku tabasamu mwanana likiwa limechanua mdomoni mwake.

"Shuka malkia wangu... Tumeshafika kwetu.." Alisema Mr Aloyce huku mwanamke yule anayefanana kwa kila kitu na Mama Eddy akishuka kwa madaha kisha akamkumbatia Mr Aloyce na kumbusu. Wakati yote hayo yakiendelea Mlinzi alikuwa pembeni yao akishuhudia penzi la zamani lililochipua upya tena kwa kasi ya ajabu.

"Mh bosi naona mama Amerejea.." Alisema mlinzi kimzaha.
"Ndio.."alijibu Mr Aloyce kwa furaha.
"Baby nataka kuongea jambo na mlinzi wetu naomba utuache kidogo.." Alisema Mama Eddy.
"Ok ila kuwa makini tu nisije kupinduliwa na houseboy.." Alisema Mr Aloyce na kuondoka zake huku akimsisitiza mkewe asichelewe.

Baada ya Mr Aloyce kuondoka pale, Mwanamke yule alimsogelea mlinzi na kumtazama kwa ghadhabu Kali. Hali hiyo ilimtisha sana mlinzi na kumfanya ajiulize maswali mengi ambayo alishindwa kujijibu mwenyewe.

Waziri Mbarawa azindua treni ya pili Dar

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amezindua treni ya pili ya abiria jijini Dar es Salaam, inayofanya safari zake kuanzia kituo kikuu cha stesheni hadi Pugu.

Akizungumza mara baada ya kuzindua treni hiyo Waziri Mbarawa amesema kuwa serikali imejipanga usafiri huo kuwa endelevu ili kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Waziri Mbarawa amesema treni hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 1500 kwa wakati mmoja itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa msongamano na kuwahisha shughuli za maendeleo kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

Aidha waziri Mbarawa amesema kuwa takribani magari 46 yanayobeba abiria 35 yatakuwa yamepungua kutokana na treni hiyo ambayo licha ya changamoto zilizokuwepo ameahidi kushughulikia ili usafari huo uweze kudumu kwa muda mrefu.

Mwigulu Nchemba Awaonya Polisi Wanaowabambikiza Kesi Raia

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba amewaambia askari wa jeshi la Polisi mkoani Katavi kufanya kazi kwa taratibu na sheria bila kumuonea mtu yeyote hasa wanyonge.

Waziri Mwigulu ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kutembelea makazi ya watanzania wapya pamoja na kuzungumza na askari wa jeshi la polisi, Magereza pamoja na Uhamiaji.

Mhe. Mwigulu amesema kuwa Askari hao waondokane na tabia ya matukio ya kuwabambikizia kesi raia kwa maslahi binafsi na kuwaonea na kusema kuwa serikali kali ya awamu ya tano haitamfumbia macho askari atakayebainika kufanya hivyo.

Aidha Waziri Mwigulu amechukua fursa hiyo kuwapa hamasa Askari hao kwa kusema kuwa serikali itawaboreshea maslahi yao kadri bajeti itakavyoruhusu ili waweze kufanya kazi kwa weledi zaidi.

Gazeti la Mseto latakiwa kumwomba radhi Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Ngonyani ndani ya Siku 7

$
0
0

 Na: Abushehe Nondo - MAELEZO
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi. Edwin A. Ngonyani amelitaka gazeti la Mseto kumuomba radhi na kumlipa fidia ya shilingi bilioni moja kutokana na kuandika habari ya kumchafua.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake Waziri Ngonyani amesema kuwa Gazeti hilo la tarehe 4 Agosti 2016 liliandika habari yenye kichwa cha Habari “Waziri amchafua JPM” ikimuhusisha na upokeaji wa fedha kutoka moja ya Kampuni ya Madini wakati akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico).

“Nimewaandikia notisi ya siku saba ikiwataka waombe radhi na kunilipa fidia, na wasipofanya hivyo hatua stahiki kuwapeleka mahakamani akiwemo Mwandishi Josephat Isango, Mwanahalishi Publisher na Mchapaji wa gazeti hilo”. Alisema Mhandisi Ngonyani.

Mhandisi Ngonyani amesema kuwa habari hiyo siyo ya kweli na mwandishi ametumia nyaraka za kughushi ikiwemo barua iliyoandikwa tarehe 24 Julai  na kutiwa saini yake akiwa Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO wakati ukweli ni kwamba tarehe hiyo yeye alikuwa ni Mkurugenzi kamili na siyo Kaimu kama barua hiyo inavyosomeka.

Ameongeza kuwa habari hiyo imewachafua watu wengi ikiwemo familia yake, wapiga kura wake wa jimbo la Namtumbo ambao walijitoa katika kumsaidia wakati wa kampeni na hali kadhalika zimemchafua Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumhusisha na fedha kutoka kwa wawekezaji wa nje kwa kuwaahidi kuwa mitaji yao nchini itakuwa salama.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli alishasema kama kuna mfanyabiashara yeyote aliyechangia kuingia kwake ikulu ajitokeze na hakuna aliyefanya hivyo, Iweje leo mtu tu anaibuka na kuandika habari za kugushi? ”. Aliongeza.

Aidha Naibu Waziri huyo ametumia fursa hiyo kuwataka waandishi wa habari nchini kuwa waangalifu pindi wanapoandika habari za kutunga kwa kutotumia majina halisi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na kanuni za uandishi wa hadithi (Habari za kutunga).

“Waandishi wa habari mnatakiwa kufuata maadili ya kazi yenu kwa kuandika habari zenye ukweli ili kuliepusha taifa kuingia katika machafuko na  migogoro isiyo ya lazima” Alisema Naibu waziri huyo.

Washitakiwa 572 wapatikana na hatia kutokana na makosa ya rushwa

$
0
0


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Mwaka ya utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna Valentino Mlowola Ikulu jijini Dar es Salaam April 11,2016.Picha na Ikulu.
****
Hussein Makame-Maelezo
Jumla ya washitakiwa 572 wamepatikana na hatia kufuatia tuhuma za rushwa zilizowakabili katika mahakama mbalimbali nchini katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna Valentino Mlowola katika taarifa iliyotolewa kwa niaba yake na Afisa habari wa taasisi hiyo Mussa Misalaba.

Taarifa hiyo inaonesha kuongezeka kwa idadi ya washitakiwa waliopatikana na hatia ambapo mwaka 2010 washitakiwa 61 walitiwa hatiani wakati hadi kufikia Desemba 2015 mahakama iliwatia hatiani washitakiwa 188.

Alisema katika mwaka 2015 (Januari-Desemba) jumla ya matukio ya rushwa 5,000 yaliripotiwa na aina ya rushwa iliyoripotiwa mara nyingi ni matumizi mabaya ya madaraka.

Taarifa hiyo inaonesha kuwa katika kipindi hicho cha miaka 6 kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, kesi mpya 1,691 zilizofikishwa mahakamani zikiwemo kesi 227 zilizofikishwa mwaka 2010, kesi 193 (2011), kesi 288 (2012), kesi 343 (2013), kesi 256 (2014) huku kesi 384 zikifikishwa mahakamani mwaka 2015.

Aliongeza kuwa kesi zilizokuwa zinaendelea mahakamani kuanzia mwaka 2010 hadi 2015 zilikuwa 3,321 huku washitakiwa walioachiwa huru na mahakama katika kipindi hicho wakiwa 646.

Kwa upande wa kesi za rushwa zilizoondolewa mahakamani kutokana na sababu mbalimbali kuanzia mwaka 2010 hadi 2015 zilikuwa 162 kati ya hizo mwaka 2010 zilikuwa kesi  30, mwaka 2011 kesi 26 na mwaka 2012 kesi 24.

Kwa mwaka 2013 kulikuwa na kesi 17 zilizoondolewa mahakamani,wakati mwaka 2014 zilikuwa kesi 33 huku mwaka 2015 zikiwa kesi 32.

Mbali na kesi hizo, Kamishna Mlowola alisema kuanzia mwaka 2010 hadi 2015 kesi 54 zilikatiwa.

Kamishna Mlowola alimtaka kila mwananchi kutekeleza jukumu lake la kikatiba na kisheria katika kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa nchini.

Kifungu cha 39 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 kinatamka kuwa “kila mtu anayefahamu kutendeka kwa kosa au anafahamu kusudio la mtu mwingine kutenda kosa chini ya Sheria hii anatakiwa kutoa taarifa TAKUKURU”.

“Hivyo, tunamsihi kila Mtanzania asijiingize katika vitendo vya rushwa na asinyamaze anapofahamu kutendeka kwa vitendo hivyo au hata kuwa na wasiwasi na mali zinazomilikiwa na mtu yeyote.” Alisema.

Alifafanua kuwa njia mojawapo nyepesi ya kuifikia TAKUKURU ni kupiga simu bure kwenda namba 113 au *113# (USSD) na kutoa taarifa za rushwa kwa muda wote wa saa 24.

Akizungumzia jinsi ya kukabiliana na vitendo vya rushwa, Kamishna Mlowola alisema ni wajibu kwa kila mwananchi kuzuia rushwa kwa kujijengea uelewa wa taratibu za eneo analokwenda kupata huduma na kupambana na rushwa kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa vinavyotokea au vilivyotokea ili hatua za kisheria zichukuliwe. 

Rais Magufuli Aanza Ziara Yake Mkoani Mwanza.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wanakwaya wa UWT Kisima cha maji Chumvi mara baada ya kuhutubia wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu Mstaafu wa Shule ya Sekondari Sengerema Wilson Fumbuka Mbanga ambaye walifundisha naye shule hiyo tokea mwaka 1982-1985 mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara Sengerema Mkoani Mwanza.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kumaliza kuwahutubia.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Busisi wakati akielekea Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya kivuko cha MV. Misungwi wakati akielekea mkoani Mwanza. 
PICHA NA IKULU.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Agosti 11

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akabidhiwa mpango wa kuhamia Dodoma

$
0
0
MKOA wa Dodoma wakishirikiana na Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu (CDA) wametekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kuandaa na kuwasilisha mapendekezo ya awali ya namna serikali itakavyohamia Dodoma.

Aidha, imeelezwa kuwa kuanzia sasa Waziri Mkuu ataweka hadharani maelekezo ya wizara na watumishi kuhamia Dodoma.

Hayo yamebainishwa katika mahojiano yaliyofanyika jana  na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Waziri Mkuu wakati akizungumza na viongozi wa serikali, taasisi, watendaji na wananchi wa Mkoa wa Dodoma alielezea azma ya serikali kuhamia Dodoma na kutoa siku 14 kwa Mkoa na CDA, kuwasilisha mapendekezo ya awali kwa namna serikali itakavyohamia Dodoma.

Akitoa siku hizo kwa Serikali ya Mkoa wa Dodoma kukaa na taasisi zake, hususani CDA kuandaa na kutoa mpango kazi wake, Majaliwa alisema,“Ndani ya siku 14 nipate proposal (mapendekezo) ya kwanza namna mtakavyotekeleza, naagiza kiundwe kikosi kazi chini yenu kitakachowajumuisha makundi yote. Baada ya siku 14 nipate mpango wenu.”

Madenge alisema kwamba Mkuu wa Mkoa huo, Jordan Rugimbana yuko Dar es Salaam alitarajiwa kuwasilisha mpango kazi huo kwa Waziri Mkuu na kwamba muda wowote Waziri Mkuu atatangaza utaratibu wa kuhamia Dodoma.

“Tumeandaa mpango kazi kulingana na maelekezo ya waziri mkuu na mkuu wa mkoa amekwenda kukabidhi mpango huo,” alisema Katibu Tawala Dodoma.

Akizungumzia taarifa za baadhi ya wizara kuanza kuhamia huko, Katibu tawala huyo alisema kwamba kama mkoa hawana taarifa za wizara na watumishi kuanza kuhamia Dodoma.

“Tunasubiri maelekezo ya waziri mkuu, baada ya mpango kazi kukamilika utawekwa hadharani mambo yote ya serikali kuhamia Dodoma,” alisema Madenge. 

Akifafanua zaidi, alisema anachojua yeye mpango unakabidhiwa Ofisi ya Waziri Mkuu na na wizara zitajipanga kwa mujibu wa maelekezo ya Waziri Mkuu Majaliwa.

Mkoa wa Dodoma umekuwa katika hekaheka za kutekeleza maagizo ya serikali ya kuhamia Dodoma, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba huduma muhimu kama upatikanaji wa viwanja zinakwenda kwa taratibu zinazotakiwa.

Ili kuondoa mhemko na udalali wa viwanja unaoweza kupandisha bei na pia kuzuia vurugu, mkuu wa mkoa amepiga marufuku uuzaji wa viwanja ndani ya mji wa Dodoma. Sababu kubwa ya kupiga marufuku kunatokana na kundi la madalali kutoka mikoa mbalimbali kuvamia mji.

Kupokewa kwa mpango kazi huo ni moja ya hatua za kukamilisha uhamiaji wa serikali Dodoma, ambapo hatua nyingine ni kwa serikali kuwasilisha bungeni muswada wa kuitambua Dodoma kama makao makuu ya nchi ili uthibitishwe kisheria.

Muswada huo utawasilishwa katika Bunge linaloanza Septemba 6, mwaka huu.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema muswada huo wa sheria ya serikali kuhamia Dodoma, utapelekwa bungeni ili azma ya Rais John Magufuli na serikali yake uwe na nguvu kisheria, baada ya Rais Magufuli kutangaza hivi karibuni kuwa ndani ya miaka minne na ushee iliyobaki ya kumaliza muhula wake wa kwanza wa urais, Serikali ya Awamu ya Tano itakuwa imehamia katika mji wa Dodoma, ambao mwaka 1973 ulitangazwa kuwa Makao Makuu ya Tanzania.

Taarifa Toka IKULU Kuhusu Ziara ya Rais Magufuli Jijini Mwanza Iliyoanza Jana

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 10 Agosti, 2016 ameanza ziara ya siku mbili katika mikoa ya Geita na Mwanza baada ya kumaliza mapumziko mafupi nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.

Jijini Mwanza Rais Magufuli alipokelewa na maelfu ya wananchi waliokuwa wakisimamisha msafara wake tangu alipoingia kupitia kivuko cha Busisi - Kigongo na baadaye kupita Usagara, Buhongwa, Mkolani, Nyegezi, Mkuyuni na Igogo ambako pamoja na kuwahakikishia kuwa Serikali yake imejipanga kukabiliana na kero mbalimbali za wananchi na kuwaletea maendeleo, amesitisha agizo la Jiji la Mwanza la kuwataka wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga kutofanya biashara zao katikati ya Jiji ifikapo tarehe 20 Agosti, 2016.

Pamoja na kusitisha agizo hilo, Dkt. Magufuli amewaagiza viongozi wa Jiji la Mwanza na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kutafuta na kuandaa maeneo ambayo wafanyabiashara hao watayatumia kwa ajili ya kufanyia biashara zao.

"Na mtakapowatafutia maeneo ya biashara wapelekeni sehemu ambazo ni nzuri, msiwapeleke sehemu ambazo hazina biashara, hawa wamachinga wanaendesha maisha yao kwa kutumia biashara hizi" Amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewahakikishia wananchi wa Mwanza kuwa Serikali imeanza kufanya usanifu na upembuzi yakinifu ikiwa ni maandalizi ya kuanza ujenzi wa daraja kubwa litakalounganisha eneo la Busisi Wilayani Sengerema na Kigongo Wilayani Misungwi ili kuondoa adha ya wananchi kuvuka eneo hilo kwa kutegemea vivuko, na pia itahakikisha inanunua meli moja katika ziwa viktoria kama ilivyoahidi.

Kabla ya kuingia Jijini Mwanza Rais Magufuli alihutubia mkutano wa hadhara katika Mji wa Sengerema na pia alizungumza na wananchi wa Sima Wilayani Sengerema na Kasamwa Wilayani Geita ambako aliwahakikishia kuwa Serikali yake itaongeza msukumo katika kutatua tatizo la uhaba wa maji katika maeneo hayo kwa kusambaza maji ya kutoka ziwa Viktoria huku akiwataka viongozi halmashauri husika kutumia rasilimali za halmashauri kutatua tatizo hilo la maji katika maeneo ambayo hayatapitiwa na mradi mkubwa wa maji ya kutoka ziwa Viktoria.

Katika hatua nyingine Mhe. Rais Magufuli amewaagiza viongozi wa Mikoa ya Mwanza na Geita kutafakari sababu zilizosababisha kufa kwa Chama Kikuu cha Ushirika cha NYANZA na viwanda vya kuchambua pamba (Ginneries) ili kupanga namna ya kuvifufua.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo  alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kasamwa kilichopo Wilayani Geita na ameahidi kuwa Serikali yake ipo tayari kuunga mkono juhudi za wakulima kwa kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yao ikiwemo zao la pamba.

Rais Magufuli atakamilisha ziara yake ya siku mbili leo tarehe 11 Agosti, 2016 kwa kuweka jiwe la msingi katika Daraja la watembea kwa miguu na kuzungumza na wananchi wa Mwanza katika Uwanja wa Furahisha.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Mwanza

10 Agosti, 2016

Mtuhumiwa Auawa Ndani ya Kituo cha Polisi

$
0
0

MKAZI wa Kwere wilayani Babati Mkoa wa Manyara, Mohamedy Pagweje (29), amepigwa na kufa na mtu anayedaiwa kuwa hana akili timamu aliyewekwa naye katika chumba cha mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Mkoa wa Manyara, kilichopo wilayani Babati.

Hata hivyo, ndugu wa Pagweje ambaye ni fundi ujenzi wa eneo hilo, wamekataa kuuchukua mwili kwa maziko wakitaka kujua ukweli wa kifo chake baada ya kupigwa akiwa mahabusu katika Kituo cha Polisi cha Babati.

Mama mzazi wa kijana huyo Hadija Pagweje, akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Raymond Mushi, alisema alimkabidhi mtoto wake kituoni hapo saa 8:00 mchana juzi akiwa salama.

Alisema alimfikisha mwanawe kituoni hapo baada ya kijana huyo kulewa pombe na kutishia kujiua kutokana na kutolipwa fedha za ujenzi kutoka kwa askari aliyemjengea nyumba. Askari huyo ametajwa kwa jina moja la Justine.

“Nilimwacha hapa kituoni mahali pa usalama na kuwaomba askari wa zamu wanisaidie maana kijana wangu amekunywa pombe nyingi, anatishia kujiua kwa madai kuwa amekosa haki yake. Nilifanya hivyo nikijua kituo cha polisi kina usalama ili angalau pombe ziishe, jioni nimchukue,” alisema.

Alipokwenda kupeleka chakula polisi walimtaka arudi tena saa 12:00 jioni, aliporudi kituoni hapo alishangaa kuona baadhi ya watu wakimshangaa na kumjulisha kuwa kijana wake amepigana na mahabusu mwenzie na kuwa amepelekwa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Babati ya Mrara kwa matibabu.

Alisema alipokwenda katika hospitali hiyo alikutana na askari ambaye alimfahamisha kuwa mtoto wake alikuwa amefariki dunia. Baba wa marehemu Amiri Shabani alisema alipata taarifa ya kifo cha kijana wake saa 1:00 usiku juzi baada ya kuelezwa kuwa mtoto wake alikufa akiwa anadai Sh 200,000 kutoka kwa askari huyo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Francis Massawe alikiri kutokea kwa tukio hilo, saa 8:00 mchana Agosti 8, mwaka huu ambapo alisema mama wa marehemu alimpeleka kituoni hapo kijana wake Pagweje, fundi ujenzi akidai kuwa alikuwa akimletea fujo na alifunguliwa mashtaka ya kutishia kuua.

Alipoingizwa mahabusu alipigana na mahabusu mwenzake Bura Malireh (19) mkulima na mkazi wa Gijedaboung Kata ya Mamire wilayani humo, ambaye ilidaiwa alikuwa mgonjwa wa akili.

Afungwa jela miaka mitatu kwa kumuibia mkewe dhahabu

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemhukumu Hussein Janga kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa dhahabu zenye thamani ya Sh5 milioni mali ya mkewe, Saida Mwakitete.
 
Pia, mahakama hiyo imemtaka mshtakiwa huyo kumlipa mkewe Sh5 milioni ambazo ni thamani ya dhahabu aliyoiba.
 
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Said Mkasiwa alisema ameridhishwa na mashahidi watatu wa upande wa mashtaka waliotoa dhidi ya mshtakiwa huyo.
 
Alisema upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi watatu ambao wamethibitisha shtaka hilo pasi na kuacha shaka.
 
“Kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapa nimejiridhisha pasi na kuacha shaka hivyo mshtakiwa ninamtia hatiani kama alivyoshtakiwa,’’ alisema Hakimu Mkasiwa na kuongeza:

“Hivyo Mahakama imekuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na kosa la kuiba seti moja ya dhahabu yenye ya Sh5 milioni.” 

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
 
Akijitetea kwa nini asihukumiwe kifungo hicho, Janga aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa madai kuwa hali yake ya kiafya siyo mzuri. Aliomba apewe kifungo cha nje.
 
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Janga alitenda kosa hilo Oktoba 27, 2014 katika maeneo ya Upanga wilayani Ilala. Alidaiwa kuiba dhahabu ambayo ni cheni ya shingoni, cheni ya mkononi na hereni mali ya mkewe.
 
Inadaiwa kuwa wawili hao walidumu katika ndoa kwa mwezi mmoja.

Aliyekuwa Akiibia Serikali Milioni 7 Kwa Dakika Akwama Kupata Dhamana

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetupilia mbali maombi ya kufutwa kwa shitaka la utakatishaji fedha katika katika kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 14 inayomkabili, mfanyabiashara Mohammed Yusufali ‘Choma’ na mwenzake.
 
Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri alitoa uamuzi huo jana baada ya kupitia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili katika kesi hiyo.

 Kutokana na uamuzi huo, washitakiwa wataendelea kusota rumande hadi kesi itakapokwisha kwa kuwa kisheria mashitaka ya utakatishaji wa fedha hayana dhamana.
 
Katika kesi hiyo Choma aliyewahi kutajwa kujipatia Sh milioni saba kwa dakika moja kwa njia ya udanganyifu katika mapato ya serikali, pamoja na mfanyabiashara Samuel Lema, wanakabiliwa na mashitaka 222 ya kula njama, kutakatisha fedha, na kuisababishia serikali hasara hiyo kwa kukwepa kulipa kodi.
 
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mashauri alisema Mahakama imetupilia mbali maombi hayo yaliyowasilishwa na upande wa utetezi kwa kuwa haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
 
Alisema mahakama inakubali kuwa hati ya mashitaka inayowahusu washitakiwa hao haina makosa, hivyo Mahakama haiwezi kubadili hati hiyo kwa kuwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
 
Aidha aliongeza kuwa, kama upande wa utetezi ungekuwa na nia ya kutaka kufutwa kwa shitaka hilo ungewasilisha maombi hayo tangu awali. Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 18, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
 
Katika hoja za ombi hilo, Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa aliomba shitaka hilo kufutwa kwa kuwa lina mapungufu kisheria na kuongeza kuwa si kila kosa la wizi na kughushi ni utakatishaji fedha, bali makosa yanayofuata baada ya vitendo hivyo yaani kuficha chanzo au asili ya upatikanaji wa fedha hizo ndiyo kosa la utakatishaji.
 
Alidai maelezo ya kwenye shitaka la 221 hayajengi kosa la utakatishaji fedha hivyo aliiomba mahakama ifute shitaka hilo ili waendelee na mashitaka mengine.
 
Upande wa Jamhuri uliiomba mahakama itupilie mbali ombi hilo kwa kuwa halina msingi kisheria na shitaka hilo lina maelezo ya kutosha kujenga kosa la utakatishaji wa fedha.

Hatimaye Dk Mwaka ajisalimisha Polisi

$
0
0

Siku chache baada ya Polisi wa Dar es Salaam kutangaza kumsaka mmiliki wa iliyokuwa kliniki ya tiba asilia ya Foreplan, Juma Mwaka ‘Dk Mwaka’ kwa agizo la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangallah, tabibu huyo ameamua kujisalimisha polisi.

Dk Kiwangallah alitoa agizo hilo siku sita zilizopita baada ya kutembelea kliniki hiyo kwa mara ya pili. Dk Mwaka alijisalimisha jana saa nne asubuhi katika Kituo cha Kikuu cha Polisi, jijini Dar es Salaam na kuhojiwa kwa saa kadhaa kabla ya kuachiwa kwa dhamana. 

Msako wa Dk Mwaka unachagizwa na madai ya ukiukwaji wa agizo la Serikali la kuendelea na utoaji wa tiba licha ya kufungiwa. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdani alisema jana kuwa baada ya kujisalimisha muda huo, alihojiwa na kuachiwa kwa dhamana lakini akatakiwa kuripoti leo kwa mahojiano zaidi. 

“Kuhusu kupelekwa mahakamani, ni mpaka jeshi la Polisi litakapomaliza kukusanya ushahidi na kumkabidhi DPP ambaye atautumia kufungua kesi,” alisema.

CCM, AG na IGP 'Wagoma' Kushiriki Kikao cha Kujadili UKUTA Wa Chadema Kilichoitishwa na Tume ya Haki na Utawala Bora

$
0
0

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, hawakutokea kwenye mkutano ulioandaliwa na Tume ya Haki na Utawala Bora jijini Dar es Salaam jana.

Mkutano uliokuwa na lengo la kumaliza mvutano ulioibuka kati ya vyombo vya dola na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mvutano huo unatokana na amri ya Rais John Magufuli, ya kupiga marufuku kufanyika kwa maandamano na mikutano ya vyama vya siasa hadi mwaka 2020.

Rais Magufuli, hata hivyo, ameruhusu viongozi waliochaguliwa kama madiwani na wabunge kufanya mikutano kwenye maeneo waliyopigiwa kura.

Kupinga amri hiyo, Chadema kimeamua kuitisha maandamano na mikutano ya wanachama na wafuasi wao nchi nzima yatakayofanyika, Septemba mosi, mwaka huu katika operesheni waliyoipa jina la `Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania’ (Ukuta).

Baada ya kuibuka kwa mvutano huo, uliosababisha Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kukamatwa na Jeshi la Polisi na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi, tume hiyo iliwaita IGP Mangu, Kinana, Masaju, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, Katibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji na Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia (TCD), Daniel Loya.

Hata hivyo, IGP Mangu, Kinana na Masaju hawakuhudhuria mkutano huo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa walitoa udhuru.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga, alisema jijini jana kuwa wametoa mapendekezo matatu ambayo yanapaswa kufuatwa na pande zote zinazovutana.

Alisema mapendekezo yao yamelenga kutoa nafasi kwa mahakama kuamua kesi zilizofunguliwa.

Nyanduga aliyataja mapendekezo hayo kuwa ni Jeshi la Polisi na Chadema kusitisha matumizi ya lugha au maneno yenye viashiria vya uvunjifu wa amani, haki za binadamu na utawala bora kwa kuwa lugha hizo hazikidhi matakwa ya sheria.

Alisema wamependekeza Jeshi la Polisi linapaswa kutokutumia maneno "tutawashughulikia wote watakaokaidi amri" kwa kuwa tume inaamini kuwa matumizi ya maneno hayo yanaweza kusababisha matumizi mabaya ya mamlaka ya jeshi hilo.

“Ni katika mazingira haya, tume imepata wasiwasi kuwa endapo matamko haya yataachiwa yaendelee, yana viashiria vya machafuko na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu unaoweza kutokea,” alisema Nyanduga.

Alisema pendekezo lingine ni Chadema kurekebisha msamiati wa mikutano wanayopanga na kuondoa neno udikteta katika mikakati yao ya kisiasa.

Akifafanua kuhusu pendekezo hilo, Nyanduga alisema Tanzania ni nchi yenye taasisi za kidemokrasia na inaheshimu utawala wa sheria na ndiyo sababu Chadema wamekwenda mahakamani.

Alisema Chadema na Jeshi la Polisi wanapaswa kuheshimu mahakama na kuacha kutoa matamko ambayo yanaendelea kuongeza joto kuhusu uwapo au kutokuwapo maandamano na mikutano ya Septemba Mosi, mwaka huu.

Nyanduga alisema pendekezo la tatu ni Chadema kusitisha maandamano yake ili kutoa nafasi kwa mahakama kufanya kazi yake kwa umakini bila shinikizo la muda kuanzia sasa hadi Septemba Mosi.

Alisema kutozingatiwa kwa mapendekezo hayo kutasababisha kutokea kwa uvunjifu wa haki za binadamu na jambo hilo likitokea, wahusika wote watawajibishwa.

Alisema tume ina mamlaka ya kujadili hoja hizo mbili kwa kuzingatia mamlaka iliyonayo chini ya Ibara 130 (1) (g) na (h) ya Katiba ya nchi, kuhusu kutoa ushauri na kutafuta maelewano kati ya viongozi wa serikali na Jeshi la Polisi kwa upande mmoja na uongozi wa Chadema.

Nyanduga aliongeza kuwa mkutano wa jana ulikuwa na lengo la kuzungumzia tamko la Jeshi la Polisi la kuzuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa isiyo ya kiutendaji na tamko la Chadema kuhusu Ukuta.

“Ofisi ya AG, IGP na CCM tuliwaalika, lakini walitujibu kuwa hawataweza kuhudhuria kwa kuwa wana udhuru, hivyo tulikutana na Chadema, Ofisi ya Msajili na TCD (Kituo cha Demokrasia Tanzania), na kukubaliana kutafanyika kikao kuhusu umuhimu wa kudumisha amani nchini,” alisema Nyanduga.

Julai 27, mwaka huu, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alitangaza kuzinduliwa kwa Operesheni Ukuta kwa lengo la chama hicho kufanya mikutano nchi nzima ifikapo Septemba Mosi mwaka huu, baada ya amri ya Rais Magufuli na Jeshi la Polisi kuzuia kufanyika kwa mikutano ya kisiasa na maandamano nchini.

Mashinji Afunguka
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Mashinji, alipotafutwa ili kueleza juu ya mapendekezo ya tume, alisema anashangaa kuambiwa kwamba kuna masuala yaliyojadiliwa kwa kuwa kikao hakikufanyika jana.

“Mbona hicho kikao hakijafanyika? "alihoji. "Kulikuwa na mvutano kwamba kifanyike ama kisifanyike kwa sababu akidi haikutimia, nashangaa kusikia kuna maazimio yamepitishwa.

“Hiyo inaonyesha kabisa ni njama za hao watu ili ionekane kuna kikao kilifanyika, kikao kisingeweza kufanyika kwa sababu hawakuwapo Kinana, IGP, wala AG,” alisema Dk. Mashinji.

Alisema anachojua yeye ni kwamba, wao wanaendelea kama kawaida na maandalizi yao ya mikutano ya hadhara na maandamano nchi nzima hiyo Septemba 1, mwaka huu.

Maalim Seif ahojiwa juu ya tuhuma za ufisadi

$
0
0

MAMLAKA ya Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), imemhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya kuwahusisha baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na tuhuma za ufisadi.

Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma cha ZAECA, Abubakari Mohamed Lunda, alisema jana kuwa Maalim Seif alihojiwa na Mkurugenzi wa ZAEC, Mussa Haji Ali, ili athibitishe tuhuma hizo.

Lunda alisema tuhuma zilizotolewa dhidi ya watendaji na viongozi ni nzito ndiyo maana mamlaka hiyo imeamua kuchunguza ukweli wake kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake.

Lunda alisema kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kuchunguza jambo lolote ambalo linahusu maslahi ya Zanzibar katika kupambana na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi.

“Tayari mamlaka imemhoji Maalim Seif ili kutafuta ukweli juu ya tuhuma alizotoa za kuwapo viongozi wanaomiliki fedha chafu na mali nje ya nchi,” alieleza Lunda.

Alisema nia ya kumhoji Maalim Seif ilikuwa kupata ukweli wa tuhuma alizotoa dhidi ya viongozi na watendaji aliowatuhumu kwa kumiliki fedha chafu na mali nje ya nchi.

Hata hivyo, Lunda alisema mpaka sasa hafahamu mkurugenzi amegundua kitu gani baada ya kufanyika kwa mahojiano hayo huku akisisitiza kuwa ZAECA imetimiza wajibu wake wa kupokea na kuchunguza taarifa mbalimbali wanazopata kupitia wanasiasa, vyombo vya habari na wananchi.

Lunda pia alisema kuna majalada 20 yamekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee kwa ajili ya hatua za kisheria kuchukuliwa.

Alisema majalada hayo yanahusisha kesi mbalimbali zikiwamo za rushwa ya uchaguzi zilizotokea wakati wa kura ya maoni ya kuwapata wagombea wa ubunge na uwakilishi kupitia CCM mwaka jana.

Alisema kitendo cha majalada kukaa muda mrefu kwa DPP bila ya kufunguliwa mashtaka mahakamani si jukumu la ZAECA kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

"Ni jukumu la Mkurugenzi wa Mashtaka wa Zanzibar (DPP)," alisema.

Akizungumza na waandishi wa habari, Aprili 10 mwaka huu mjini Zanzibar, Maalim Seif, ambaye ni Makamu wa kwanza wa Rais wa zamani wa Zanzibar alituhumu kuna viongozi na watendaji wa visiwani humo wanamiliki fedha chafu na mali nje ya nchi.

Alisema kuwa fedha hizo zilipatikana kwa njia za ufisadi na kutaka jumuiya ya kimataifa kufuatilia akaunti za vigogo hao na watendaji nje ya nchi kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake.

Maalim Seif alidai kuwa haihitajiki tochi kuwamulika viongozi wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi na kutaka mamlaka za dola kufanya uchunguzi dhidi ya vigogo hao na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 15 & 16

$
0
0

 Mtunzi:EDDAZARIA G.MSULWA

.....Nikaongeza hatua za haraka kwenda kumsaidia Manka,nikamkuta anatokwa na damu nyingi katika paji la uso wake huku mguu wake mmoja ukiwa umebanwa katika siti,Nikajitahidi kuitoa siti iliyombana Manka hadi nikafanikiwa kisha nikamuweka kando kwenye barabara na kwenda kutazama majeruhi wengine akiwemo Mwalimu Mayange.


Nikachungulia chungulia ndani ya gari na ila sikuona mtu yoyote anayeomba msaada kwani ukimya mkubwa ulitawala ndani ya gari na kutokana na giza jingi nikajua moja kwa moja watu waliomo ndani ya gari watakuwa wamefarika dunia ua kupoteza fahamu.

  Nikarudi barabarani kumtazama Manka na kukuta hali yake inazidi kuwa mbaya nikamnyanyua na kwenda naye ndani ya gari na kumkuta dereva akiwa amekaa kwenye siti niliyokuwa nimekaa mimi huku akiwa kama amepigwa na bumbuazi kiasi kwamba hawezi kufanya kitu chochote huku jasho jingi likimtoka japo ndani ya gari letu aina ya VX G8 lina  Air condition(A.C) ya kutosha.Nikamuingiza Manka ndani ya gari na kumuweka siti ya nyuma kisha na mimi nikaingia kwenye upande wa dereva na kuwasha gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi,nikafika kwenye moja ya zahanati na kumkuta daktari mmoja na nesi ambao wapo zamu ya usiku.

Nikamtoa Manka ndani ya gari na kumuweka kwenye kitanda cha matairi kilichotolewa na nesi kisha wakamuingiza ndani ya chumba na kuniomba nisubiri nje na kunihitaji nikatafute PF3 ya polisi ili hata kama kuna hali yoyote itajitokeza juu ya Manka wao wasihusike kwa chochote.Nikarudi kwenye gari na kumkuta dereva nje ya gari akiwa amejiegemeza kwa unyonge huku akionekana kuwa na wasi wasi mwingi.

“Oya kuna kituo cha polisi hapa karibu”
Nilimuuliza dereva na kumuacha akiwa ananitazama kama hajalisikia swali langu nililo muuliza
“Oya broo mbona kama umesizi ni wapi kwenye kituo cha polisi ambacho ninaweza kupata huduma yao?”
“Hapo mbele”
“Wapi?”
“Labda Mombo kule nyuma tulipotoka kwani bado tupo Mombo”
“Powa ingia kwenye gari”

 Nikawasha gari na kuanza safari ya kurudi kule tulipotoka na safari hii gari nillizidi kuliendesha kwa kasi ili kuwahi kupata alichoniagiza daktari.Nikajikuta nikifunga breki za gari gafla na kusimama hii ni baada ya trafki mmoja kunisimamisha katika sehemu waliyo pata ajali Manka na ndugu zake na kukuta kuna askari wengine wakiendelea na vipimo vya ajali imetokea tokea vipi huku kukiwa na watu watatu wakiwa wamelazwa kando ya barabara na huku wakiwa wamefunikwa na mashuka maalumu ya polisi na baadhi ya wananchi wakiwa wanashangaa shangaa ajali.“Dreva washa taa ya ndani au ushuke ndani ya gari”.

Nikawasha taa ya gari na nikamuona trafki akishtuka nikajichunguza na kugundua kuwa chati langu la shule kidogo lina damu.Trafki aliye nisimamisha akaniomba tena nishuke ndani ya gari  huku bunduki yake akiishika vizuri na sikuwa mbishi nikashuka huku funguo nikiingiza mfukoni.“Ninaomba leseni yako na kadi ya gari”.

Nikaanza kujipapasa kama ninatifafuta leseni yangu kwenye mifuko yangu japo najua kuwa sina leseni ya aina yoyote kwenye mfuko wangu zaidi ya wallet yangu yenye kitambulisho cha shule na pesa za matumizi.

“Afande nahisi nimeishahau leseni yangu kwenye gari”
“Mbona shati lako limejaa mijidamu.Lete funguo za gari”
Nikamkabidhi trafki funguo za gari na kwaishara akaniomba niende kumchukulia leseni yangu na kumuacha akimnong’oneza mwenzake.Nikafungua mlango wa gari na kumkuta dereva akiwa na wasiwasi mwingi
“Oya kaka hivi una leseni yoyote hapo ulipo?”
“Ninayo ya kwangu”
“Siwezi kutumia ya kwako?”
“Huwezi kwani ina picha yangu”.


Kitwanga Akutana Uso Kwa Uso na Rais Magufuli

$
0
0
Rais John Magufuli jana alikutana ana kwa ana na rafiki yake, Charles Kitwanga ikiwa ni siku 80 baada ya kumvua cheo cha Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kosa la kuingia bungeni kujibu maswali akiwa amelewa. 

Wawili hao walikutana kwenye Jimbo la Misungwi ambako Rais alisimama akitokea Wilaya ya Sengerema ambako alihutubia wananchi. 

Rais alitengua uteuzi wa Kitwanga Mei 20, wakati sakata la utekelezwaji mbovu wa mkataba wa Sh37 bilioni baina ya Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises likivuma kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano. 

Lakini jana, hali ilionekana ya kikazi zaidi wakati Rais alipofika kwenye jimbo hilo. Kitwanga, ambaye ni mbunge wa Misungwi mkoani Mwanza, alitumia nafasi hiyo kukutana na Rais kwa mara ya kwanza hadharani, kuwasilisha kero za wananchi wake, hasa ya maji. 

Katika tukio hilo lililovutia hisia za waliokuwepo, Rais aliuthibitishia umma kuwa yeye na Kitwanga ni marafiki wa muda mrefu, alipokuwa akijibu ombi la mbunge huyo la kutaka Serikali itatue kero ya maji eneo la Usagara na Misungwi. 

“Kitwanga ni rafiki yangu. Tayari Serikali imepanga kutumia zaidi ya Sh8 bilioni kutekeleza mradi mkubwa wa maji maeneo ya jimbo la Misungwi, ikiwemo Usagara,” alisema Rais Magufuli akiwa amesimama kwenye gari lililofunuliwa upande wa juu. 

Katika sakata la Lugumi, wabunge walitaka suala lijadiliwe baada ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kubaini kuwa kampuni hiyo ilishindwa kufunga mashine za kielektroniki za kuchukulia alama vidole kwa mujibu wa mkataba. 

Mkataba huo ulisainiwa mwaka 2011 lakini hadi CAG alipokuwa akifanya ukaguzi mwaka jana, ni vituo 14 tu kati ya 118 vilivyokuwa vimefungwa mashine hizo, huku Lugumi Enterprises ikiwa imelipwa Sh36 bilioni ambazo ni zaidi ya asilimia 90 ya fedha za mkataba huo. 

Kitwanga alihusishwa na sakata hilo kutokana na dhamana yake na pia kuwa na hisa kwenye kampuni ya Infosys, ambayo ni wakala wa kampuni ya Dell inayozalisha kompyuta, kuhusishwa kutoa vifaa hivyo. 

Hata hivyo, Juni 22, Kitwanga aliwaambia waandishi wa habari nyumbani kwake kuwa Infosys haina uhusiano wowote wa kibiashara na Lugumi.

Jitihada za wabunge, hasa wa upinzani kutaka kuzungumzia suala hilo zilikwama kwa maelezo ya kutaka kusubiri ripoti ya kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza suala hilo. 

Ripoti hiyo iliwasilishwa mwishoni mwa vikao vya Bunge la Bajeti na haikujadiliwa baada ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kusoma maagizo ya Bunge kwa pande zinazohusika kwenye mkataba. 

Kabla ya suala hilo kuzuiwa kujadiliwa, wabunge walikuwa wakidai kuwa Rais na Kitwanga ni marafiki wa karibu na baadaye mitandao ya kijamii ikasambaza mkanda unaoonyesha jinsi walivyokuwa wakijadili suala la Magufuli kuchukua fomu ya kugombea urais. 

Kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Magufuli alimnadi Kitwanga kwa kueleza kuwa anamfahamu kwa kuwa walisoma wote na ni rafiki yake. 

Kabla ya kwenda Sengerema kwa kivuko jana, Rais alihutubia wilayani Sengerema ambako aliendelea na onyo lake dhidi ya watu anaosema wanataka kuvuruga amani.

Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mnadani mjini Sengerema, Rais Magufuli aliwataka wenye lengo la kuvuruga amani kumsubiri amalize kipindi chake cha uongozi kwa sababu hatawapa fursa hiyo. 

“Wapo wanaotumia taasisi za kisiasa na kidini kujaribu kuvuruga amani ya nchi. Hawa hatutawapa fursa hata kidogo kwa sababu amani ya nchi ikivurugika hakuna hata mmoja atakayebaki salama; sote tutaangamia,” alisema Rais Magufuli 

Aliwakumbusha wakazi wa Sengerema jinsi walivyowapokea wakimbizi kutoka nchi jirani ya Rwanda miaka ya tisini wakati taifa hilo lilipoingia kwenye mauaji ya kimbari yaliyoishia kwa watu zaidi ya milioni moja kupoteza maisha.

 “Tunayo mifano hai ya mataifa yaliyochezea amani na kusambaratika. Rwanda ilipitia njia hiyo kabla ya kusimama upya.Zipo Libya na Somalia ambazo hadi sasa zimegawanyika vipande vipande,” alisema Rais Magufuli. 

Aliwataka Watanzania kulinda kwa udi na uvumba amani na utulivu ulioasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na viongozi wengine, kwa kuwapiga vita wanaovuruga amani hata kama ni ndugu, jamaa, marafiki, wanachama au waumini wenzao. 

Rais anaendelea kutoa onyo hilo wakati Chadema ikiendelea kusisitiza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho ya kuitisha mikutano ya hadhara nchi nzima kuanzia Septemba Mosi, ikiwa ni sehemu ya kampeni itakayoendeshwa na Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), ambayo tayari baadhi ya wakuu wa mikoa wamepiga marufuku.

Chadema inadai kuwa uamuzi wa Rais kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na kudhibiti wanasiasa kuhudhuria mikutano hiyo nje ya maeneo yao, ni kukiuka Katiba, Sheria ya Vyama vya Siasa, Kanuni za Maadili za Vyama vya Siasa na haki za binadamu.

Kuhusu vita dhidi ya ufisadi, Rais pia aliahidi kuongeza kasi kupitia mtindo wake wa kutumbua majipu, huku akilishukuru Bunge kwa kupitisha sheria itakayosaidia vita hivyo pamoja na kupitisha bajeti ya Sh2 bilioni ya kuanzisha Mahakama Maalumu ya Rushwa. 

Akizungumzia suala la chakula nchini, Rais John Magufuli amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha maeneo yao yanazalisha chakula cha kutosha, akionya kuwa Serikali haitatoa chakula cha msaada kwa watakaokumbwa na njaa kutokana na uzembe na uvivu. 

Rais alisema kazi ya kulisha familia ni jukumu la wakuu wa familia na kuongeza kuwa kila familia ina wajibu kulima na kuhifadhi chakula cha kutosha mahitaji ya kipindi chote cha mwaka. 

“Kazi ya Serikali ni kutoa huduma kama barabara, dawa na mahitaji mengine ya kijamii, lakini si msaada wa chakula kwa watu wavivu,” alisema Rais Magufuli. 

Kuhusu usafiri wa Reli ya Kati, Rais alisema tayari Serikali imetengeneza zaidi ya Sh1 trilioni kwa ajili ya mradi wa kubadili reli hiyo kuwa katika viwango vya kimataifa. 

Alisema serikali pia inakusudia kununua meli mpya ya abiria itakayokuwa ikifanya safari Ziwa Victoria yenye uwezo wa kubeba abiria 1,000 na tani 800 ya mizigo. 

Pia alisema Serikali imeweka mikakati ya kukabiliana na uvuvi haramu kwenye Ziwa Victoria, ambalo lilikuwa likitoa fursa za ajira kwa watu zaidi ya milioni 6 katika nyanja mbalimbali, fursa ambazo alisema zimepungua maradufu kutokana vitendo vya uvuvi haramu. 

Rais Magufuli, ambaye atatumia ziara yake kukagua miradi ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa daraja la juu la waenda kwa miguu eneo la Furahisha pamoja na upanuzi wa barabara ya Ghana-Pasiansi kutoka njia mbili za sasa hadi nne, leo anatahutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Furahisha, Kirumba jijini Mwanza.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images