Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Awafutia Kesi Ya Rushwa Kangi Lugola na Wenzake

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewaachia huru wabunge watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya kuomba rushwa ya Sh milioni 30. 

Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage aliwaachia huru washitakiwa hao baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kuwasilisha hati ya kuwafutia mashitaka.

Wabunge hao na majimbo yao katika mabano ni Kangi Lugola wa Mwibara mkoani Mara maarufu kama ‘Nyoka wa Shaba,’ Suleiman Saddiq ‘Murad’ (Mvomero – Morogoro) na Victor Mwambalaswa (Lupa – Songwe). 

Awali Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi akisaidiwa na Wakili Emmanuel Jacob kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), waliieleza mahakama kuwa kesi hiyo imetajwa kwa ajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Kishenyi alidai mbali na kutaka kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao, DPP anaomba kuwafutia mashitaka yao kwa kuwa hana nia ya kuendelea na mashitaka dhidi yao.

Baada ya maelezo hayo, Wakili wa Utetezi, Mpale Mpoki aliiomba mahakama itoe agizo ili apewe maelezo ya mlalamikaji. Hakimu Mwijage alisema, mahakama imekubali ombi la DPP hivyo kuanzia sasa wabunge hao wapo huru.

Aidha, alisema wakili Mpoki anatakiwa afanye juhudi kwenda katika ofisi za DPP ili kupata taarifa hizo, kinyume cha hapo mahakama haiwezi kutoa amri kwamba apatiwe maelezo hayo.

Baada ya washitakiwa hao kuachiwa huru, ndugu na marafiki wa wabunge hao waliokuwa wamefika mahakamani, walianza kuangua kilio cha furaha. 

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake, Lugola alisema watakaa na wanasheria hao ili wajue nini cha kufanya kutokana na udhalilishaji waliofanyiwa na Takukuru.

"Tumesikitishwa sana na kitendo cha Takukuru walivyotufikisha mahakamani na kutushitaki kwa kashfa ya rushwa na dunia nzima imetambua, lakini tangu tufike mahakamani mioyo yetu ilimtanguliza Mungu na leo (jana) Mungu ametoa majibu,” alisema Lugola.

Alisema walikuwa wanajua kuwa kesi hiyo ni ya kutunga na ilijaa siasa kwa kuwa awali Takukuru ilisema upelelezi umekamilika, lakini hawakuwa na ushahidi na ndio maana wameamua kuifuta.

Kwa mara ya kwanza wabunge hao walipandishwa kizimbani, Aprili mosi mwaka huu wakidaiwa kuwa Machi 15 mwaka huu, kati ya saa mbili na saa nne usiku, katika Hoteli ya Golden Tulip, Kinondoni jijini Dar es Salaam, kwa pamoja wakiwa kama wabunge na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), waliomba na kushawishi kupewa rushwa ya Sh milioni 30.

Inadaiwa waliomba fedha hizo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Gairo, Mbwana Magotta, kama kishawishi cha kutoa mapendekezo ya hati safi kwa halmashauri hiyo, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Kupandishwa kizimbani kwa wabunge hao kulitokana na kashfa ya rushwa iliyomsababisha Spika wa Bunge, Job Ndugai kupangua wenyeviti na makamu wenyeviti kwa kuwaondoa kwenye kamati walizokuwa wanaziongoza. Mabadiliko hayo yaliwagusa pia wabunge 27, ambao baadhi yao wanadaiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Waziri Mkuu Atoa Siku Moja Kwa Manispaa Ya Morogoro Kutangaza Maeneo Kwa Ajili Ya Wafanyabiashara Wadogo

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku moja kwa uongozi wa Manispaa ya Morogoro kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na kuyatangaza kesho ( leo ).

“Mbali na kutenga maeneo pia nawaagiza muwasaidie wafanyabiashara hawa kuunda vikundi kulingana na aina ya biashara wanazozifanya ili kuwawezesha kupata mikopo kwa urahisi kutoka katika taasisi za fedha” alisema.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi Msamvu unaojengwa kwa ubia kati ya Manispaa ya Morogoro na Mfuko wa Pensheni wa LAPF.

Awamu ya kwanza ya mradi huo inatarajiwa kufunguliwa Agosti 12 mwaka huu utakuwa ni kituo cha mabasi cha kwanza cha kisasa Tanzania ambapo Waziri Mkuu amezitaka halmashauri zote zilizoko makao makuu ya mikoa nchini kuiga mfano huo.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kulipongeza Baraza la Madiwani la Manispaa ya Morogoro na LAPF kwa kubuni mradi huo wa kisasa utawezesha abiria kupata taarifa ya basi lilipo na muda litakapowasili kituoni hapo hivyo kupunguza udanganyifu kutoka kwa mawakala wasiokuwa waaminifu.

Kwa upande wake Meneja wa mradi huo Stanley Mhapa alisema mradi huo umegharimu sh. bilioni 40 ambapo Manispaa inamiliki asilimia 40 ya hisa na mfuko wa LAPF unamiliki asilimia 60.

“Mafanikio ya mradi huu ni pamoja na kuiwezesha Manispaa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka sh 350,000 kwa siku hadi kufikia sh. milioni 1.7 kwa siku,” alisema.

Mhapa alisema mradi huo utakapokamilika utatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za kibenki, vibanda vya biashara, sehemu za chakula, ofisi na sehemu ya mapumziko ya abiria na vibanda vya kukatia tiketi.

Waziri Mkuu Awataka Wafugaji Wakubwa Kujiandaa Kufuga Kisasa

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wafugaji wenye mifugo mingi nchini kujiweka tayari kwa ajili ya kuhamia kwenye maeneo yatakayotengwa na Serikali katika ranchi mbalimbali nchini ili waweze kufuga kisasa.

Pia aliwataka wafugaji hao kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya maeneo hayo ikiwemo ujenzi wa visima vya maji na majosho ili ufugaji wao uwe na tija.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Agosti 03, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika nyama cha Nguru Hills Ranch kilichoko wilayani Movomero.

Hata hivyo Waziri Mkuu alisema kitendo cha wafugaji hao kuhamia katika ranchi kitawezesha mifugo yao kuwa na ubora kwa sababu aina ya ufugaji wa sasa ya kutembeza mifugo umbali mrefu inasababisha ufugaji wao kuwa na tija ndogo.

Akizungumzia kuhusu uwepo wa kiwanda cha kuchakata nyama wilayani Mvomero Waziri Mkuu alisema kitamaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji kwa kuwa wafugaji watapata fursa ya kuuza mifugo yao kiwandani hapo.

“Uwepo wa viwanda katika maeneo yetu utatuwezesha kupunguza matatizo tuliyonayo katika maeneo yetu ikiwemo suala la migogoro kati ya wafugaji na wakulima. Viwanda ndiyo vitakavyotuondoa kutoka katika uchumi wa chini hadi wa kati,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi na Mshauri wa kiwanda cha Nguru Hills Ranch, Dunstan Mrutu alisema kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 300, mbuzi na kondoo 1,500 kwa siku kinatarajiwa kufunguliwa mwezi Desemba mwaka huu.

Mkurugenzi huyo alisema takriban asilimia 80 ya nyama itafungashwa na kuuzwa nje ya nchi  hasa Uarabuni kwa sababu nyama ya mbuzi ya Tanzania imebainika kuwa na mvuto maalum katika nchi hizo.

“Mbali na uwekezaji huu wa kiwanda cha nyama pia tunatazamia kuwekeza katika mnyororo wa thamani kuanzia kusindika ngozi inayotoka kiwandani hadi kuzalisha viatu, mikanda na bidhaa zote za ngozi na kupunguza uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi,” alisema.

Mrutu alisema nia yao ni kuitikia wito wa Rais Dk. John Magufuli wa kutaka viwanda vizalishe viatu nchini kuanzia vya majeshi na wananchi wote ambapo wamepanga kuanzia mwakani wataanza kuuza bidhaa hizo.

Aliongeza kuwa uwepo wa kiwanda hicho utatoa fursa kwa wafugaji na wakulima kuuza majani, mifugo na mazao ya chakula kama mtama, mahindi, ambapo tayari wameanza kuhamasisha jamii za wafugaji na wakulima wa Mvomero, Ngerengere na sehemu zinazozunguka eneo la kiwanda kuchangamkia fursa hiyo.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mvomero kufanya mapitio ya mashamba ili kujua wamiliki wake na kama hawajayaendeleza wachukue uamuzi wa haraka wa kuyatwaa na kuyarudisha mikononi mwa Serikali.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akijibu ujumbe uliokuwa katika mabango yaliyobebwa na wananchi wa kijiji cha Maji ya Chumvi wilayani Mvomero waliosimamisha msafara wakati ukitokea kwenye kiwanda cha nyama.

Freeman Mbowe Amtembelea na Kumjulia Hali Spika wa Bunge, Job Ndugai

$
0
0
Kiongozi wa Kambi rasmi  ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.Spika wa Bunge amerejea nchini hivi karibuni kutoka nchini India alipokwenda kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe aliyemtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Kiongozi wa Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe aliyemtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mhe Freeman Mbowe  akiagana  na Spika wa Bunge  Mhe. Job Ndugai alipomtembelea Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Bunge)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi siku ya Vijana Kitaifa.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi siku ya Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Simiyu Oktoba 14 mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.

Mhe Mavunde alibainisha kuwa Kauli mbiu ya Siku ya Vijana mwaka huu ni “Tokomeza umasikini kwa uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija”.

Akifafanua kuhusu kauli mbiu hiyo Mhe. Mavunde alisema lengo la kauli mbiu hii ni kuzihimiza nchi wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha kikamilifu Vijana katika shughuli za uzalishaji na kuhakikisha kuwa panakuwepo na matumizi sahihi ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini na Nishati ili kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 2030.

Akizungumzia maadhimisho hayo Kitaifa Mhe . Mavunde alisema kuwa vijana watapata fursa ya kushiriki shughuli mbalimbali kama makongamano,matamasha,michezo,maonnyesho ya Kazi za Vijana,Shughuli za kujitolea na maandamano ya amani.

“Tanzania tutasherekea siku ya Vijana Duniani Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na kilele kitakuwa tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe hii itaenda sambamba na Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.” Alisisitiza Mhe. Mavunde.

Wazo la kuwa na siku ya Vijana Duniani lilitolewa katika Mkutano wa Vijana wa Kimataifa mwaka 1991 Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya kutafuta njia ya kuchangisha fedha za kusaidia mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo mwaka 2000 nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku ya Vijana Duniani kulingana na mazingira yake kwa kuzingatia kauli mbiu ambayo huandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA Harry Kitilya na Wenzake wafungua kesi ya kikatiba Wakupinga Kunyimwa Dhamana

$
0
0

Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake watatu wanaokabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha katika kesi mbili tofauti wamefungua kesi ya kikatiba wakipinga kunyimwa dhamana. 

Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomon, wanaoshtakiwa katika kesi moja na nyingine ya utakatishaji fedha inayomjumuisha, Gidion Wasongo wamefungua kesi hiyo Mahakama Kuu. 

Mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wa pili ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkurugenzi wa Mashtaka ( DPP). 

Kesi hiyo ya kikatiba namba 14 ya mwaka 2016, Kitilya na wenzake wanapinga kifungu cha 148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kinachozuia dhamana kwa mashtaka ya utakatishaji fedha.

Wanadai kuwa kifungu hicho kinakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, Ibara ya 13 (b).

Ibara hiyo inazuia mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo. 

Pia, wanadai uamuzi wa kuwafungulia shtaka la utakatishaji fedha haukuwa wa haki, bali ulikuwa na nia mbaya ya kuwanyima dhamana.

Kesi hiyo imepangwa kuanza kutajwa leo mahakamani hapo, kabla ya kuendelea na taratibu nyingine za usikilizwaji wa hoja za  msingi za wadai hao. 

Wakati Kitilya, Sinare na Sioi wakikabiliwa na shtaka hilo katika kesi moja, Wasongo anakabiliwa na shtaka hilo katika kesi tofauti yeye na wenzake wengine akiwamo aliyekuwa Mhasibu wa TRA, Justice Katiti. 

Hata hivyo, licha ya kesi hiyo ya kikatiba, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kutoa uamuzi wa rufaa dhidi yao Agosti 9, ambayo DPP anapinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wa kuwafutia shtaka la utakatishaji fedha. 

Katika kesi ya msingi, Kitilya na wenzake wanakabiliwa na mashtaka manne ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, kujipatia fedha Dola za Marekani 6 milioni kwa njia za udanganyifu na kutakatisha fedha kiasi hicho, ambalo liliwafanya wakose dhamana. 

Hata hivyo, ilikuwa ni furaha kwao baada ya Mahakama hiyo baadaye kuwafutia shtaka hilo, kutokana na juhudi za mawakili wao, Dk Ringo Tenga, Majura Magafu na Alex Mgongolwa kulipinga kuwa halijakidhi vigezo vya kisheria kuitwa kosa la utakatishaji fedha. 

Lakini DPP hakukubaliana na uamuzi huo wa Mahakama ya Kisutu, hivyo alikata rufaa Mahakama Kuu, lakini Mahakama Kuu katika uamuzi uliotolewa na Jaji Moses Mzuna ilitupilia mbali rufaa hiyo pamoja na mambo mengine akieleza kuwa hapakuwa na haja kukata rufaa kwa uamuzi huo. 

DPP hakukubaliana pia na uamuzi huo wa Mahakama Kuu, hivyo alikata rufaa Mahakama ya Rufani na akashinda na mahakama hiyo iliamuru Mahakama Kuu isikilize upya rufaa ya DPP.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla Apiga Marufuku mikutano ya Operesheni UKUTA iliyotangazwa na Chadema

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amepiga marufuku mikutano ya Operesheni Ukuta iliyotangazwa kuratibiwa na Chadema kuanzia Septemba Mosi. 

Akizungumza katika kikao cha kazi kilichoshirikisha kamati ya ulinzi na usalama mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri, Makalla alitangaza kupiga marufuku mkutano wowote utakaofanyika chini ya utaratibu unaoitwa Operesheni Ukuta. 

“Bila shaka wananchi wa Mbeya wanataka amani na kazi, hivyo ni marufuku kufanyika mkutano wowote wa kisiasa unaoandaliwa kwa kushirikiana na watu wengine kutoka nje ya mkoa,” alisema Makalla aliyewahi kuwa mbunge na mweka hazina wa CCM.

Alifafanua kuwa wabunge na madiwani akiwamo Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) wa Chadema wanaweza kufanya mikutano yao bila wasiwasi katika maeneo yao.

 Makalla alisema vyombo vimewekwa tayari kuwashughulikia kwa nguvu zote watakaokaidi maagizo yanayotolewa na kutoa mwito kwa vijana wa mkoa huo kuwafichua watu wenye njama zozote zikiwamo za kuwahamasisha kufanya maandamano au mikutano. 

Polisi yadai kukamata vijana 
Wakati Makalla akipiga marufuku Operesheni Ukuta, Polisi mkoani Mbeya wameeleza kuwakamata vijana wawili wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema kwa tuhuma za kuandaa na kusambaza ujumbe wa sauti wenye kauli za kutaka ofisi za CCM zichomwe moto. 

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Dhahir Kidavashari alidai kwamba vijana hao waliandaa na kusambaza ujumbe huo Julai 29 ukiwataka vijana wenzao ambao ni wanachama wa chama hicho kwenda kuchoma moto ofisi za CCM mahali walipo. 

Kidavashari alidai kwamba ujumbe huo unahamasisha vijana kufanya uhalifu huo wakati wowote kabla ya Septemba Mosi na baada ya hapo ilimradi nchi iwe kwenye machafuko. 

“Baada ya kufuatiliwa na kumkamata, mtuhumiwa wa kwanza alipekuliwa na kukutwa na simu ambazo zilitumika kusambaza ujumbe huo.Pia kupitia mtuhumiwa huyo tulifanikiwa kumpata mtuhumiwa mwingine.”

Tundu Lissu Akamatwa na Jeshi la Polisi Akiwa Singida.....Msigwa Ahutubia Iringa, Adai Serikali Imekurupuka Kuhamia Dodoma

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amekamatwa na polisi muda mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Ikungi, Singida. 

Wakati Lissu akiwa mikononi mwa polisi, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa jana alifanya mkutano wa hadhara na kusema hakuna wa kumpangia cha kuzungumza kwenye mikutano yake. 

Kukamatwa kwa Lissu 
Lissu, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema ndiye aliyetoa taarifa za kukamatwa kwake kwenye mtandao akisema: “Wakubwa sana salaam. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida.

" Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki. Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer (RCO) wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander (RPC) Singida nikamatwe apparently (dhahiri) kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam.

 “Kwa hiyo niko nguvuni na ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa kunipeleka. It’s likely (inawezekana) nitasafirishwa Dar usiku huu. In fact (hakika) ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi. Kwa vyovyote itakavyokuwa, there’s no turning back. There’s no shutting up (hakuna kurudi nyuma, hakuna kunyamaza). 

"Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa, whether in freedom or in jail (niwe huru au jela)... Aluta continua!. "

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka  alithibitisha kukamatwa kwa Lissu lakini alikataa kutoa sababu za hatua hiyo. 

Chadema jana jioni ilitoa taarifa kuhusiana na kukamatwa kwa Lissu ikisema: “Tunaweza kuthibitisha kwa vyombo vya habari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama Mh. Tundu Lissu anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.” 

Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene ilibainisha kuwa Polisi walimkamata jana jioni baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara alioufanya Ikungi jimboni kwake na kueleza kuwa viongozi wa chama hicho mkoani humo walikuwa polisi kuhakikisha anapata haki zake kama inavyostahili na kwamba ofisi ya katibu mkuu inafuatilia kwa ukaribu kujua sababu hasa ya kushikiliwa kwake na kutoa msaada wa haraka kadri itakavyohitajika. 

Lissu amekuwa kwenye misukosuko na Jeshi la Polisi mara kadhaa na kwa siku za karibuni alikamatwa na kufikishwa mahakamani akituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kwenye gazeti la Mawio. 

Sambamba na kesi hiyo, Lissu alikamatwa na polisi kwa madai ya kutoa maneno ya uchochezi baada ya kupata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 

Msimamo wa Msigwa 
Mkoani Iringa, Msigwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kwanza wa kibunge tangu alipochaguliwa uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa, alisema hakuna wa kumpangia hoja za kuzungumza kwenye mikutano yake. 

Juzi, mbunge huyo alipewa barua na Jeshi la Polisi iliyoeleza kuwa imempa kibali cha kufanya mikutano hiyo, lakini ikimuwekea masharti mbalimbali likiwamo la kutozungumzia viongozi wengine na badala yake ajikite kwenye shughuli za maendeleo na kuchukua maoni ya wananchi anaowawakilisha. 

Pia, alitakiwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu kutoka nje ya Mkoa wa Iringa au eneo lolote lililo nje ya mamlaka atakayeruhusiwa kuzungumza. 

Lakini jana akihutubia alisema:“Ninaona watu wote mna nyuso za hofu na mimi nimekuja kuwaondoa hofu …hakuna mtu mwenye mamlaka ya kunipangia cha kuzungumza, sipo hapa kwa matakwa ya polisi … mimi nipo kwa matakwa ya kisheria na ninazungumza kwa mamlaka mliyonipatia.

 “Pia Katiba inaeleza wazi mad raka na kinga ya Mbunge… mbunge anayo haki ya kuitisha na kufanya mkutano wa hadhara kwa mjibu wa sheria.” 

Kuhusu Rais kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, Msigwa alisema hakubaliani na hatua hiyo kwa madai kuwa kufanya hivyo ni ukiukaji wa Katiba ya nchi na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ambavyo nchi inayoongozwa chini ya utawala wa kidemokrasia inapaswa kuvifuata.

 “Ninamuunga mkono na ninampongeza Rais John Magufuli kwa kupambana na ufisadi, anapinga rushwa… lakini siungani naye kwa kitendo chake cha kukandamiza demokrasia nchini na niwaombe wananchi wa Iringa kuungana na mimi kumpinga mtu anayekandamiza demokrasia nchini,” alisema. 

Kuhusu Serikali kuhamia Dodoma, mbunge huyo ambaye pia ni waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje, alikosoa uamuzi huo akisema hajawahi kuona katika mipango yote iliyowasilishwa na Serikali bungeni inayoelekeza hilo.

“Serikali ilileta mpango wake wa miaka mitano, mwaka mmoja na Bajeti, hivi vyote vinaletwa bungeni na baada ya kujadiliwa na kupitishwa, vinatungiwa sheria ili viweze kutekelezwa hivyo vipaumbele vyake ni lazima vifiti kwenye mipango hiyo,” alisema Msigwa na kuongeza:

 “Lakini katika vyote vitatu vya mwaka huu, mpango wa miaka mitano, mwaka mmoja na hata katika bajeti ya mwaka huu sijaona mahali popote palipoandikwa kipaumbele cha Serikali ni kuhamia Dodoma.” 

Msigwa alisema kuhamisha Serikali ni gharama kubwa na kuwataka wakazi wa Iringa na maeneo mengine kuhoji suala hilo kama ndicho kipaumbele cha maendeleo na mahitaji yao. 

Alisema wamejipanga kufanya shughuli za maendeleo ikiwamo miradi ya barabara, kuboresha huduma za afya, usafi wa mazingira na miundombinu. 

Mkutano huo ulihudhuriwa na madiwani wa halmashauri hiyo wakiongozwa na Mstahiki Meya, Alex Kimbe.


RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 26

$
0
0
 MTUNZI: ENEA FAIDY
....BI CAROLINA alipiga hatua za taratibu kuelekea sebuleni lakini hali iliyokuwemo ndani mle ilizidi kumshangaza kwani alisikia harufu Kali na mbaya ya kitu kuungulia. Alifika sebuleni lakini hakukuta Mtu yeyote, akaamua kwenda jikoni.

Alipoingia jikoni tu, alipiga chafya tatu mfululizo kutokana na moshi mzito ulioambatana na harufu Kali sana uliotawala jikoni mle. Aliisogelea mpaka sehemu ya kupikia akagundua moto uliwashwa na kuna kitu kilichomwa. Akaangalia sufuria zote lakini hakukuta kitu chochote, akabaki na mshangao.
"Doreen!" Aliita Bi Carolina akiwa ameshika mkono kiunoni.
"Abee mama!" Sauti ya Doreen ilisikika kutoka chumbani.
"Njoo huku jikoni"

Bila ya kuchelewa Doreen alifika jikoni kule na kumkuta Bi Carolina akiwa ameshika kiuno akimsubiri kwa hamu amuulize kilichotokea.
"Abee mama" aliitikia Doreen kwa adabu sana.
"Nini kimetokea huku jikoni?"
"Nisamehe mama... Nilitaka kupika.. Ila kwa bahati mbaya nikaunguza kwani sijui kutumia jiko la gesi." Alijitetea Doreen huku akitia huruma sana.

"Ulitaka upike nini asubuhi yote hii?"
"Nili...nilikuta maziwa.. Nyama kwenye friji nikataka nipike.."
"Mara maziwa mara nyama.. Mbona sikuelewi? Haya ulipikia sufuria gani?" Bi Carolina alishindwa kumuelewa Doreen ila kutokana na ugeni aliokuwa nao hakuweza kumfokea sana kwa kuhofu kuwa atajisikia vibaya.
"Nilichukua nyama... Sufuria ilipoungua sana nikaamua kuiosha.." Alisema Doreen akidai kutetemeka kwa woga.
"Sawa ila usirudie tena.. Nitakufundisha jinsi ya kupikia jiko la gesi.."
"Sawa mama" alisema Doreen kwa sauti ya upole iliyojaa hekima ya viwango vya juu.
"Sawa mwanangu nenda kaendelee na kazi zako"

Doreen alitoka jikoni mle na kuelekea chumbani kwake. Alichukua kimfuko cheusi kidogodogo kisha akafungua na kuutoa ungaunga mweusi. Kisha akaweka kiganjani na kusogelea kila kona ya chumba kile na kuupuliza kwa midomo yake. Alifanya hivyo mpaka unga ule ilipoisha, akasogelea kitanda chake na kukaa.

"Hapa sasa nimemaliza kazi... Mpaka huo moshi uishe nitakuwa nimefanikiwa kabisa." Alisema Doreen akitabasamu kwani ule moshi uliotapakaa ndani mle ulisababishwa na Doreen. Alikuwa amechoma dawa ambayo ingewafanya wakaaji wa nyumba ile kumpenda Doreen kupita kiasi, na wasingeweza kumfukuza hata iweje mpaka pale atakapoamua kuondoka yeye mwenyewe.

Aliangalia SAA yake ya mkononi ilikuwa tayari ni saa nne na nusu asubuhi. Doreen alisikia sauti ya Bi Carolina ikimwita. Akatii wito na kumfuata Bi Carolina.
"Abee mama" aliitikia kwa heshima.
"Umeoga?"
"Bado"
"Kaoge unywe chai."
"Sawa mama"
Doreen alitoka sebuleni pale na kwenda bafuni kuoga. Alipomaliza alipaka mafuta na kuvaa tena nguo alizokuwa amevaa kabla ya kuoga kisha akaenda sebuleni. Akamkuta Bi Carolina akiwa amekaa huku akitazama televisheni.
"Mbona umevaa nguo chafu?"
"Sina zingine"

"OK.. Baadae tutaenda Mwanjelwa ukatafute nguo za kuvaa.. Sasa hivi nenda ukanywe chai.." Alisema Bi Carolina.
"Sawa mama.. Vipi kuhusu Dada Pamela?" Aliuliza Doreen.
"Atakuja si muda mrefu.. Ameniambia yupo njiani. Baada ya kumwambia hivyo ghafla mlango ukagongwa . Akaingia msichana mmoja mrefu kiasi, mweupe, matiti yenye ukubwa kiasi, kiuno chembamba kama sindano na makalio makubwa kama milima miwili iliyopangana vyema. Wote walishtuka kidogo.
"Ah Pamela kumbr ulikuwa jirani tu.. Tumekuongelea sasa hivi hapa.."

"Sikuwa mbali"
"Karibu sana" alisema Bi Carolina wakati huo Pamela alikuwa akiketi sofani na kuweka pembeni mkoba wake. Kwa muda wote huo Doreen alikuwa akimtazama Pamela katika maeneo ya kifuani.
"Shkamoo Dada Pamela" alisalimia Doreen
"Marhaba hujambo? Wewe ndo Doreen?"
"Ndio.." Aliitikia Doreen huku akimgeukia mama Pamela "kumbe una mtoto mzuri namna hii?" Alisema.
Bi Carolina na Pamela walicheka tu.
"Huyu ndo mwanangu mpenzi... Yuko peke yake kama Tanzanite..." Alisema Mama Pamela huku akicheka.
Doreen aliwaacha wakiendelea na mazungumzo kisha yeye akaenda chumba cha kulia chakula (dinning). Moyoni mwake alifurahi sana kwani kwa uzuri aliokuwa nao Pamela titi lake lilifaa sana kwa kazi ya Doreen.

==> Endelea Nayo <<Kwa Kubofya Hapa>>

Tahadhari Kwa Wakenya : Uchawi Ni Utumwa.

$
0
0
                             Na. THEOFLIDA  WA  YESU.
Naanza  kwa  kuwasalimu  kwa  JINA  LA  YESU. Jina  lililo  Kuu  kupita  majina  yote. 
 
Wiki  kadhaa  zilizo  pita, niliandika  waraka  wangu   kwa  watanzania  na  kuusambaza   kupitia  blogs  na  mitandao  mbalimbali   kuhusu  athari  za  kujihusisha  na  masuala  ya  waganga  wa  jadi  . 

Katika waraka  huo   niliwatahadharisha  watanzania  kutojihusisha  na  WAGANGA  WA  TUNGULI  kwa  sababu WAGANGA  WA  TUNGULI  ni   WACHAWI NA MAWAKALA  WA  SHETANI   walio  vaa  kofia  ya  utabibu.

Katika  waraka  huo  niliwaelezea  watanzania  jinsi  nilivyo  shawishika  kutafuta  msaada  wa  maisha  yangu   kwa  MGANGA  WA  TUNGULI  aitwae  MUNGU  WA  KABILI  na  kujikuta  nikipata  matatizo  makubwa  ambayo  hata  hivyo  yalipelekea  kunikutanisha  na  YESU  ambae  ameniokoa.

Katika  waraka  huo nili  sahau  kueleza  mambo  makuu  mawili yafuatayo:

Kwanza  nilisahau  kuweka  mawasiliano  ya   MUNGU  WA  KABILI   ayatumiayo pindi  anapokuwa  nchini  KENYA ili  kuwa  tahadharisha  wakenya  wasipige  namba  hiyo  wala  wasijaribu  kutafuta  msaada  kwenye  namba  hiyo, kwa  sababu  mtu  huyo  ni  WAKALA  WA  SHETANI  alie  jificha  kwenye  kivuli  cha  UGANGA...

Wengi  walio  jaribu  kutafuta  msaada  kwa  MUNGU  WA  KABILI  wamejikuta  wakiishia  kuunganishwa  na  UTAWALA  WA  KUZIMU  ambao  umewapelekea  kujikuta  katika  matatizo  makubwa  kama   niliyo  yapata  mimi.

Nimeona  vyema  kuwatahadharisha  wakenya, kwa  sababu  mungu  wa  kabili  hufanya  kazi  zake  Tanzania  na  Kenya.  Anapokuwa  Tanzania, namba  yake  huwa  ni + 255  744  000  473  na  anapokuwa  Kenya , namba  yake  huwa  ni  + 254    704  71 61 59.
 
Hivyo  basi   Ndugu  zangu Wakenya , hii ni  tahadhari  yangu  kwenu. Nimeweka  namba  hizo  hapo  juu  kama  alama  ya  MPINGA  KRISTO  ambayo  watu  wote  wenye  hofu  ya  Mungu  wanapaswa  kuepukana  nayo..

Nimeongozwa  katika  namna  ya  rohoni, kuanza  kufanya  kampeni  ya  nguvu  dhidi  ya  roho  ya  kuhusudu  masuala  ya  UGANGA, UCHAWI  NA  USHIRIKINA  na  nitajikita  zaidi  katika  mapambano  dhidi  ya  MGANGA  WA  JADI  AITWAE  MUNGU  WA  KABILI.
 
Ninaanza  kwa  kupambana  na  MUNGU  WA  KABILI  kwa  sababu, kwa  miaka  zaidi  ya  mitatu  ambayo  nimekuwa  nikishirikiana  na  MUNGU  WA  KABILI,  nimeweza  kujua  kuwa  yeye    ndio   MKUU  WA  WAGANGA  NA  WACHAWI  WOTE  WA  AFRIKA  MASHARIKI  NA  KATI , na  watu  wenye  hekima  wanasema  katikati  ya  kundi  la  kondoo  MPIGE  RUNGU  MCHUNGAJI, NA  KONDOO  WOTE  WATATAWANYIKA.

Naamini  nikimsambaratisha  mungu  wa  kabili, basi itakuwa  rahisi  kwa  waganga  wengine  kwa  sababu  wote  ni  kama  wafuasi  wake  tu.

Katika  kampeni  yangu  hii  ya  kiroho, nimeanzisha  blogu  iitwayo  SHUHUDA  ZA  AJABU  ambayo  inapatikana : www.shuhudazaajabu.blogspot.com.
 
Nitakuwa  nikitoa  shuhuda  za  mambo  mbalimbali  ya  kichawi  niliyo fundishwa  na  MUNGU  WA  KABILI  na  jinsi  unavyo  weza  kujiepusha  nayo  kwa  kutumia  Jina  la  Yesu.

Najua  kazi  hii  itainua  uadui  mkubwa  dhidi  yangu, kwa  sababu  hakuna  kitu  wachawi  wanakichukia  kama siri  zao  kutolewa  hadharani, lakini  kwa  Jina  la  Yesu, nitapambana  vita  hii  na  nitaishinda.
 
 MUNGU  WA  KABILI  na  jeshi  lake  watajaribu  kushindana  na  mimi  lakini  hawatashinda.( YEREMIA 1:19.)
 
Shuhuda  nitakazo  zitoa, zitakuwa  na  mafundisho  mazuri yatakayo  kupa  faida  , kama  Mungu  anavyo  sema katika  kitabu  cha ISAYA  48  kwamba  " MIMI  NI  MUNGU  NIKUFUNDISHAE  ILI  UPATE  FAIDA'.

Ushuhuda  huu  utakufanya  umjue  shetani  vizuri kama  wasemavyo  watu  wenye  hekima  " MJUE  ADUI  YAKO  KAMA  UNAVYO   IJUA  NAFSI  YAKO"

JAMBO  LA  PILI  na  la  msingi  ambalo  sikuweza  kulielezea  kwa  kina  katika  waraka  wangu  wa  kwanza  ni  namna  ambavyo  MUNGU  WA  KABILI  alinifundisha  uchawi  na  uganga...

Nianze  kwa  kurudisha  kumbukumbu  zenu  nyuma. Kama  mlifatilia  vizuri  waraka  wangu  mtakuwa  mnakumbuka  kuwa, kwa  kutumia  uchawi  nilio  pewa  na  MUNGU  WA  KABILI, nilifanikiwa  kuteka  na  kudhulumu  mali  za  mwanaume  mume  wa  mtu   aitwate " K". 

Mali  hizo  zilikuwa  ni  pamoja  na  maduka  mbalimbali  ya  biashara  ambayo  nilimkabidhi  mdogo  wangu  ayasimamie.

Kutokana  na  usimamizi  wa  hovyo  ulio fanywa  na  mdogo  wangu, maduka   hayo  yakaanza  kufilisika  taratibu. Hali  hii  ilinifanye  niende  kuomba  msaada  wa  MUNGU  WA  KABILI.

Mungu  wa  Kabili  akaniambia  kuwa  mimi  siwezi  kufanikiwa   kupitia  biahsra  yoyote  hata  iweje.  Mungu  wa  Kabili  akaniambia  , Nina  nyota  ya  Uganga " kwa  hiyo  ninatakiwa  kuwa  mganga.

Sikuwa  na  jinsi  zaidi  ya  kukubaliana  nae  kwa  sababu  nilishamfanya  kuwa  kama  muungu  wa  maisha  yangu. Nilitii  na  kufuata  kila  alicho  kisema.

Ikapangwa  siku  rasmi  ya  mimi  kusimikwa  uganga  kisha  baada  ya  kusimikwa uganga ndipo nianze kufanya  kazi  ya  kuwaagua  watu  wenye  shida, tabu  na  matatizo  mbalimbali  ya  kimaisha.

Zoezi  la  kunisimika  uganga  rasmi  lilikamilika  ambapo nilikabidhiwa  nyenzo  za  uganga  pamoja  na  jina  la  kazi, baada  ya  hapo, mungu  wa  kabili  akaniambia, nitaanza  kufundishwa  uganga, lakini  akasema, kabla  ya kuujua  uganga  ninatakiwa  kuujua  kwanza  uchawi, kwa  nadharia  na  vitendo. Hapo ndipo ninaposema  siku zote  kuwa  MCHAWI  NA  MGANGA  LAO MOJA.

mungu  wa  kabili  aliniambia ' UCHAWI  NI  SAYANSI  YA  SIRI  YENYE  MRENGO  WA  UFISADI  ( YANI  MLENGO  WA  UHARIBIFUI ) Ilihali  UGANGA  NI  SAYANSI  YA  SIRI YENYE UWEZO  WA  KUPAMBANA  ATHARI  ZA   NGUVU  YA SAYANSI  YENYE  MLENGO  WA  UFISADI.
 
mungu  wa  kabili  akaniambia, ili  niwe na  uwezo  wa  kupambana  na uchawi  ni  lazima  kwanza  niufahamu  uchawi  vizuri kwa  nadharia  na  vitendo , kisha  baada  ya  hapo  nitafundishwa  kuhusu  mbinu  za  kupambana  na  uchawi  ambao kwa  mujibu  wa  mungu  wa  kabili, ndio  huo  uganga  wenyewe..
 
Nilifundishwa  vitu  sana  katika  uchawi, kuanzia  jinsi  ya  kuroga  ukoo  mzima, kufanya  watoto  wasikue, kutengeneza  ukimwi  wa  kichawi, kuvunja  ndoa, kutengeneza  radi, nyoka, simba n.k, kusafiri  na  aina  tatu  za  ungo  wa  kichawi, kutengeneza  na  kuzuia  mvua, kuchukua  misukule, kutengeneza  magonjwa  mbalimbali  kwa  watu, mimea  na  mifugo, kutengeneza  chuma ulete, kutengeneza  majini,kuingia  mikataba  na  majini & mizimu, kuwafunga  watu  vifungo  vya  kichawi  vya  aina  mbalimbali  nakadhalika....
 
==> NITAENDELEA   KUSIMULIA  KESHO.  Nitakuwa  nikisimulia  kila  siku  kupitia  blogu  ya  hapa  MPEKUZI  pamoja  na  blogu  yangu  iitwayo  WWW.SHUHUDAZAAJABU.BLOGSPOT.COM.
 
MUNGU  AKUBARIKI  SANA..AMEN

Kiama cha madereva walevi na wazembe Chawadia........Serikali yazindua mkakati wa mambo 14 kukabiliana na ajali

$
0
0
Na Jonas Kamaleki-Maelezo
Serikali yajipanga kupunguza ajali za barabarani kwa kiwango cha takribani asilimia 10 hapa nchini ili kupunguza vifo na majeruhi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Yusuf Hamad Masauni  kuwa baraza la Usalama Barbarani linakerwa sana na kadhia ya ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.

“Kukithiri kwa ajali za barabarani kwa siku za hivi karibuni, umewezesha Baraza kuibuka na Mkakati wa Miezi Sita (6) unaolenga katika kukabiliana na ajali za barabarani nchini, mkakati huu ni wa muda mfupi kuanzia mwezi Agosti, 2016  hadi Februari 2017 tutakapokaa na kutathmini matokeo yake”, alisema Masauni.

Masauni amesema ajali za barabarani zimewaacha watoto wakiwa yatima  na kuwafanya akina mama kuwa wajane, hivyo  juhudi za makusudi inabidi zifanywe ili kupunguza kama sio kuondoa kabisa ajali hizo.

Ametaja vyanzo vikuu vya ajali za barabarani nchini kuwa ni pamoja na Makosa ya Kibinadamu, mazingira ya barabara na ubovu wa vyombo vya moto.

Naibu waziri huyo amesema takwimu za ajali barabarani katika miaka mitatu tangu 2012 ajali ziliongezeka toka 23,578 hadi 23, 842 kwa mwaka 2013, vifo vilikuwa 3,969 kwa mwaka huo hadi kufikia 1,043 mwaka 2013.

Vifo hivyo vilipungua hadi kufikia 3,760 mwaka 2014, upungufu huo ulitokana na usimamiaji madhubuti wa Sheria na kanuni za Usalama barabarani pamoja na juhudi zilizofanya na Baraza kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa Masauni, Mkakati uliozinduliwa unalenga kudhibiti makosa yanayosababisha madhara makubwa na ambayo husababisha kuongezeka kwa ajali za barabarani.

Ameyataja mambo hayo kuwa  ni:
 1. Udhibiti wa madereva walevi na kuendesha kwa uzembe.

2. Udhibiti wa mwendokasi kwa madereva na wamiliki wa magari; kuwa na madereva wenza

3. Uendeshaji magari bila sifa/leseni ya udereva na bima

4. Udhibiti wa usafirishaji wa abiria kutumia magari madogo yenye muundo wa tairi moja nyuma kwa mfano; Noah, Probox

5. Kudhibiti ajali za pikipiki za magurudumu mawili ‘bodaboda’ na magurudumu matatu

6. Abiria kufunga mikanda ya usalama wanapotumia vyombo vya usafiri

7. Kuyabaini na kuyadhibiti maeneotete na hartarishi ya ajali za barbarani ‘black spots/kilometers’

8. Kuangalia uwezekano wa kufanya marekebisho ya sheria za usalama barabarani.

9. Kuanza kwa mfumo wa nukta ‘point system’ kwenye leseni za udereva.

10. Kutoa mafunzo ya msasa yanayolenga katika kuimarisha utendaji wa askari wa usalama barabarani.

11. Kuhakikisha kuwa waendesha bodaboda wanafikiwa na kupewa mafunzo yaa uhakika juu namna na jinsi ya kuzitumia barabara kwa usalama zaidi.

12. Kudhibiti rushwa na kuwaadhibu watoaji na wapokeaji wa rushwa katika barabara zetu nchini.

13. kuwahusisha wamiliki wa magari ya abiria na ya mizigo, katika kuutekeleza mkakati.

14. Mkakati mwingine waliouweka ni kuwa Dereva ukikamatwa unapelekwa rumande na baadae mahakamani kujibu shitaka litakalokuwa linakukabili.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya August 5

Polisi Wamnyima Tundu Lissu Dhamana, Atupwa Rumande

$
0
0

JESHI la Polisi, kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemnyima dhamana, Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kumaliza kuhojiwa katika kituo kikuu cha polisi.

Baadhi ya viongozi waliofika kumwekea dhamana  ni pamoja na  Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema, Edward Lowassa Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu wa Chama hicho, aliyefika saa 12:14 jioni akiungana na viongozi na wanachama wa chama hicho.

Baada ya kufika Lowassa wanachama na wafuasi wa Chadema waliokuwa nje ya ofisi hizo za polisi walianza kuimba wimbo wa kumuita rais, rais, rais ikiwemo na kauli mbiu ya maarufu ya Peoles power.

Mara baada ya kufika alipokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliyekuwa amepanda gari moja na Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob waliokuwa nje ya geti.

Viongozi hao waliokuwa nje baada ya kuzuiwa kuingia ndani na polisi waliongozana na Lowassa kuomba kuingia lakini walizuiwa hali iliyofanya wachukue uamuzi wa kuondoka.

Kiongozi aliyeruhusiwa kuingia alikuwa ni Meya wa Dar es Salaam, Isaya Mwita.

Akizungumzia kuhusu hilo, Peter Kibatala mwanasheria wa Lissu alisema kwamba mahojiano kati ya jeshi hilo na mtuhumiwa yalianza saa 9:30 hadi saa 12:30.

“Katika maelezo ya polisi wanasema kwamba wakati Lissu akitoka mahakamani juzi kwenye kesi yake  alitamka maneno ya uchochezi, lakini haya yote yanahitaji ushahidi,” alisema Kibatala.

Wakili huyo alisema kwamba polisi baada ya kumaliza mahojiano na wao wakiwa wameandaa utaratibu wa dhamana walikataliwa hadi leo Ijumaa atakapofikishwa mahakamani.

Aliyesambaza Ujumbe Asakwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida,   Thobias Sedoyeka  ametangaza kumsaka mtu aliyesambaza ujumbe ambao amaedai “una ishara zote za uchochezi” unaoonyesha umeandikwa na Lissu   baada ya kukamatwa na jeshi hilo.

Alisema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kina kwenye mitandao ya  jamii kuhusu ujumbe huo.

Ujumbe huo ambao pia umenukuliwa na jeshi hilo katika taarifa yake, ulieleza jinsi polisi mkoani Singida walivyomkamata Lissu baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara   huku akihamasisha watu kutokubali kunyamazishwa na “Udikteta Uchwara”.

“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kwenye mitandao ya  jamii kuhusu ujumbe mfupi wa maneno uliosambazwa katika mitandao hiyo baada ya kukamatwa kwa Lissu ukiwa na ishara zote za uchochezi…,” alisema Sedeyoka na kuongeza:

“Katika uchunguzi huo endapo mtu yeyote atabainika kutuma taarifa hiyo basi Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za  sheria zinazostahili ikiwamo kumkamata na kuwafikisha mahakamani mara moja.”

Ujumbe huo ulisomeka, “Wakubwa sana salamu. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida. Nimemaliza kuhutubia mkutano  wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya jimbo la Singida Mashariki.

“Mara baada ya kushuka jukwaani nilifuatwa na RCO wa mkoa aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kuniarifu kuwa ameelezwa na RPC nikamatwe. Wakati huohuo, kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam kwa hiyo nipo nguvuni ninasubiri maelekezo ya wanapotaka kunipeleka…

“Its likely (kuna uwezekano) nitasafirishwa Dar usiku huu. Infact ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi. Kwa vyovyote itakavyokuwa ‘there is no turning back’ (hakuna kurudi nyuma), there is no shutting up (hakuna kufunga mdomo). Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa.

“Whether in freedom or in jail as long as I have a voice to speak with. (Nikiwa huru au kifungoni ilimradi nina sauti ya kuzungumza) sitakubali kunyamazishwa na Dikteta Uchwara. Msikubali kunyamazishwa na Dikteta Uchwara. Aluta continua!!!! From Tundu Lissu”.


Kamanda Sedoyeka  alisema endapo itathibitishwa kuwa Lissu ndiye aliyeandika na kusambaza ujumbe huo ataingia tena matatani kwa kukamatwa na kuchukuliwa hatua za  sheria kama lilivyoeleza jeshi hilo.

Hiyo ni mra ya tatu kukamtwa kwa mbunge huyo kwa kipindi cha miezi michache na    amekwisha kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za uchochezi.

Kesi ya kwanza ni ile iliyodaiwa ametoa lugha ya uchochezi katika habari iliyochapishwa na gazeti la Mawio na kesi ya pili ni   ya kutoa maneno ya uchochezi kwa kumwita Rais Magufuli ‘Dikteta Uchwara’

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania asimamishwa kazi kwa uzembe

$
0
0

Waziri wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege ATCL Kapten Johnson Mfinanga na Mkurugenzi wa Uendeshaji Kapten Sadick Muze kwa kosa la kumchagua rubani asiye na sifa kwenda kupata mafunzo Canada.

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Mbarawa amesema marubani watano walichaguliwa kwenda nchini Canada kwa ajili ya kupata mafunzo ya kurusha ndege mpya zitakazoingia nchini mwezi Septemba kama alivyoahidi Rais Dkt. John Magufuli.

Waziri ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya za shirika la ATCL alitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi huyo kuchagua marubani watano wenye sifa kwa ajili ya kwenda kupata mafunzo nchini Canada ambapo kati ya watano waliochaguliwa mmoja amebainika hana vigezo hivyo ameamua kuwasimamisha viongozi hao kutokana na uzembe.

Aidha waziri Mbarawa amewataka watendaji wa serikali kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kanuni za kazi na mtumishi atakayefanya kinyume hatasalimika kuwajibishwa.

Babu Atiwa mbaroni kwa kumbaka mjukuu wake

$
0
0

JESHI la Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka 12.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa, aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba aliyebakwa ni mwanafunzi wa darasa la tano na ana umri wa miaka 12.

Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, mtuhumiwa huyo ambaye ni mlinzi, Philipo Stephano , alikamatwa Agosti 2 mwaka huu, saa tisa mchana katika maeneo ya Soweto, Kata ya Soweto, Manispaa ya Moshi mkoani hapa.

“Yule mtoto ambaye jina lake tunalihifadhi, alibakwa na babu yake mzaa mama yake, mkazi wa Soweto.

“Kabla ya mtuhumiwa kufanya tendo hilo, alimwambia mjukuu wake huyo amwelekeze na alipokubali, alimpeleka katika eneo analolinda na kumfanyia unyama huo.

“Baada ya uchunguzi wa daktari, ilithibitika mwanafunzi huyo alibakwa na kusababishiwa maumivu makali katika sehemu zake za siri.

“Kwa hiyo, mtuhumiwa tumemkamata na tunaendelea na upelelezi kabla hatujampeleka katika vyombo vya sheria,” alisema Kamanda Mutafungwa.

Mwenyekiti wa mtaa adaiwa kumpa mimba mwanafunzi

$
0
0

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sangabuye, kata ya Igombe wilayani Ilemela mkoani Mwanza anayejulikana kwa jina la John Mayala anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumtorosha na kumpa ujauzito mwanafunzi.

Mwanafunzi huyo amefahamika kwa jina la Lucy Daudi, anayesoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Sangabuye ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 14 hadi 17.

Aidha jeshi la polisi pia linamshikilia mama mzazi wa mwanafunzi huyo aitwaye Agnes Kadilana mwenye umri wa miaka 48 mkulima, mkazi wa Sangabuye kwa kosa la kushindwa kutoa ushirikiano kwa polisi pindi alipohojiwa kuhusiana na tukio hilo.

Inadaiwa kuwa mama huyo alishiriki katika kumtorosha binti yake kwenda kuishi kinyumba na mtuhumiwa baada ya kupewa fedha.

Mama huyo amedai kuwa binti yake aliamua mwenyewe kuacha shule kwa madai kuwa shule imemshinda. "Yeye mwenyewe alisema hawezi kusoma, akasema ajifunze cherehani, sasa sijui" Amesema mama huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo hususani wanaume wenye tabia ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi pamoja na wasichana wenye umri chini ya miaka 18 kuacha mara moja kwani ni kinyume cha sheria bila kujali kama palikuwa na makubaliano au la.

Vyama 9 Vya Siasa Kufutwa

$
0
0

Vyama tisa vya siasa kati ya 22 vyenye usajili wa kudumu vipo hatarini kufutwa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo na matakwa ya kisheria yaliyoviwezesha kupata usajili wa kudumu. 

Hatua ya kufutwa vyama hivyo, vikiwamo baadhi visivyo na ofisi za kudumu (vyama vya mfukoni) itafikiwa ikiwa vitashindwa kujieleza kutokana na makosa ambayo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imebaini katika ukaguzi uliofanyika hivi karibuni Bara na Visiwani. 

Jukumu kubwa la Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni kusimamia, kuboresha, kuendeleza na kudumisha demokrasia ya vyama vingi hapa nchini majukumu ambayo yanatokana na Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi Na. 7 ya mwaka 2010. 

Majukumu mengine ya ofisi ya msajili ni kusajili vyama vya siasa na kuvifuta vyama ambavyo havikidhi matakwa ya sheria hiyo na kusimamia ugawaji wa ruzuku ya Serikali kwa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria.

 Akizungumza ofisini kwake jana, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi alisema uhakiki uliofanywa na ofisi yake katika vyama hivyo upande wa Bara na Visiwani umebaini kasoro nyingi zikiwamo za ukiukaji wa masharti ya usajili.

 “Katika uhakiki uliofanywa na ofisi yangu tumebaini kasoro mbalimbali ambazo kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ni miongoni mwa vigezo muhimu vinavyoangaliwa ili chama kiwe na sifa ya kusajiliwa,” alisema. 

“Kasoro tulizozibaini ni nyingi na baadhi ya vyama kutokana na mapungufu waliyo nayo huhitaji kutoa nafasi tena….unaweza kuvifuta hapohapo.” 

Msajili hakutaka kutaja majina ya vyama hivyo ambavyo tayari vimeandikiwa barua lakini alitaja makosa kuwa baadhi havina ofisi za kudumu Tanzania Bara na Visiwani au upande mmoja na vingine havina anuani ya posta. 

“Unakuta chama fulani kina ofisi labda Zanzibar lakini hakina ofisi Bara,” alisema Jaji Mutungi. Alisema vyama vingine havina viongozi wa kitafa kutoka pande mbili za Muungano na pia havina bodi ya wadhamini iliyosajiliwa kwa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita) kama sheria inavyohitaji. 

Katika ukaguzi huo, Msajili alibaini pia kasoro nyingine kuwa ni kukosekana kwa orodha ya wanachama wa chama husika jambo alilosema nalo ni muhimu kila chama kuwa na orodha ya idadi ya wanachama wake. 

Vilevile, baadhi ya vyama hivyo vimeshindwa kuonyesha akaunti ya fedha ya chama hali inayotia shaka namna vinavyojiendesha.

Mahabusi waliojaribu kutoroka watiwa mbaroni

$
0
0

Mahabusi wawili kati ya saba waliotoroka chini ya ulinzi wa askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro, wametiwa mbaroni na kuhukumiwa kutumikia vifungo jela.

Kutoroka kwa mahabusi hao kulisababisha askari 10 mkoani Kilimanjaro waliokuwa wakiwalinda kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.

Mahabusi hao ni Lucas Akaro (26) ambaye alijisalimisha kwa uongozi wa Gereza la Karanga na Charles Malenge (24), aliyekamatwa na Polisi akiwa amejificha nyumbani kwake.

Wakati wakitoroka, Akaro alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo cha udaktari KCMC, Baneti Materu (22) na Malenge  ya unyang’anyi.

Mahabusi hao walifikishwa kortini jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Joachim Tiganga na kukiri shtaka moja kati ya mawili yaliyokuwa yakiwakabili.

CUF wadai wanasubiri Maalim Seif akamatwe, kurejea leo

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad anatarajiwa kurejea leo kutoka ughaibuni alikoenda kwa ziara ya takribani wiki tatu huku jeshi la polisi likijiandaa kumfikisha Mahakamani.

Hivi karibuni, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu alieleza kuwa Jarida la Mashtaka dhidi ya Maalim Seif liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa Zanzibar, kutokana na kile alichodai kuwa aliwachochea wafuasi wake kufanya fujo kupitia vikao vya ndani vya chama hicho.

IGP Mangu alieleza kuwa uchaguzi wa Oktoba 25 na ule wa Marudio vilifanyika kwa amani na utulivu lakini matatizo na vitendo vya uvunjifu wa amani vilianza kuonekana tangu mwanasiasa huyo aliyegombea Urais kuanza kufanya mikutano hiyo ya ndani akiwahamasisha wafuasi wake kutoshirikiana na Serikali iliyopo madarakani.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Makame amethibitisha kuwa tayari jalada hilo liko kwa DPP na kwamba upelelezi unaendelea.

Akizungumzia mpango huo wa Jeshi la Polisi, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF, Shemeji Mketo aliwaambia waandishi wa habari kuwa chama hicho kimekuwa kikisubiri polisi watekeleze azimio lao hilo ndipo wataeleza msimamo wao.

“Acha wamkamate na sisi tunalisubiri hilo… wakimkamata ndipo tutasema nini tunafanya,” alisema Mketo.

Aidha, Mketo alisema kuwa Maalim Seif atakapowasili atazungumza na waandishi wa habari kuelezea kuhusu ziara yake, nchi alizokwenda na mambo aliyoyafanya.

Tundu Lissu afikishwa tena Mahakamani

$
0
0

HATIMAYE Jeshi la  Polisi Jijini Dar es salaam limemfikisha rasmi kizimbani Mwanasheria Mkuu wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo Singida Mashariki wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Tundu Lissu ambaye alikamatwa Juzi mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara Ikungi, Singida na kusafirishwa usiku, kulazwa Chamwino Dodoma na kufikishwa Dar jana saa saba mchana alilazwa rumande kabla ya kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mchana wa leo.

Akionekana mwenye kujiamini, Lissu amewasili Mahakamani Kisutu akitokea mahabusu ya Kituo kikuu cha Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam saa nane na dakika arobaini na nane (14:48) akiwa kwenye gari yenye namba za usajili  T 517 BET Corolla na akisindikizwa na ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Muda wowote kuanzia sasa, atapandishwa kizimbani ili kusomewa mashitaka ambayo yanatajwa kuwa huenda yakawa ni ya uchochezi kufuatia kauli aliyoitoa mahakamani hapo 02 Agosti Mwaka huu wakati akitoka katika kesi nyingine ya uchochezi inayomkabili.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images