Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Programu za vyuo vikuu ambazo hazijasajiliwa na TCU na NACTE kufutwa

$
0
0
Na: Lilian Lundo -Maelezo
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Bi. Maimuna Tarishi ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)   kufuta programu zinazotolewa na vyuo vikuu hapa nchini ambazo hazijafanyiwa tathmini wala kusajiliwa.

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga maonyesho ya kumi na moja ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Julai 20 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

“Wakati mwingine najiuliza inakuwaje chuo kinafundisha programu ambayo haijatathminiwa wala kusajiliwa na TCU au NACTE, ni lazima tuwe makini kwani tunahitaji elimu bora katika vyuo vyote nchini bila kuangalia kama ni cha Serikali au ni Binafsi,” alifafanua Bi. Tarishi.

Aliendelea kwa kusema kuwa, TCU na NACTE wanajukumu ya kuzifuta programu hizo na kuanzisha programu zenye uhitaji mkubwa kama vile shahada ya mafuta na gesi, Kompyuta na Ualimu wa Sayansi ambapo wataalamu katika maeneo hayo wamekuwa wakihitajika zaidi katika kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano inajikita zaidi katika uanzishwaji wa viwanda.

Aidha Bi. Tarishi amewataka TCU na NACTE kudahili wanafunzi wenye vigezo vinavyohitajika na kusisitiza kuwa ni bora kuwa na wanafunzi wachache katika vyuo vikuu kuliko kuwa na wanafunzi wengi ambao hawana sifa.

Wakati huo huo Mkuu wa Kitivo cha Biashara Chuo Kikuu cha Zanzibar Salehe Mwinyi amesema kuwa wanafunzi wengi wamejitokeza kutembelea banda la Chuo hicho kutaka kujua pogramu zinazotolewa na wengi wao wameonyesha nia ya kujiunga katika Chuo hiko.

Vile vile Mwinyi amesema kuwa mwaka huu idadi ya wanafunzi waliotembelea maonyesho hayo ni wengi zaidi kutokana na eneo lililochaguliwa kufikika kwa urahisi kutoka pande zote za jiji la Dar es Salaam ukilinganisha na mwaka jana ambapo yalifanyika viwanja vya Saba Saba na kutembelewa na idadi ndogo ya wanafunzi na wazazi.

Kwa upande wake, Fadia Suleiman mwanafunzi anayetegemea kujiunga na Chuo Kikuu mwaka huu, amesema kuwa maonyesho hayo yamemsaidia kwa kiasi kikubwa kujua ni programu gani asome kutokana na ufaulu wake wa kidato sita.

Maonyesho ya  Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ambayo huandaliwa na TCU hufanyika kila mwaka yakitoa fursa kwa Vyuo Vikuu vya ndani na nje ya nchi kutoa elimu kwa wazazi na wanafunzi wanaotegemea kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka husika juu ya programu zinazotolewa na vyuo hivyo pamoja na kutoa ushauri ni programu gani mwanafunzi asome kwa kuangalia ufaulu wake.

Kikwete Aongoza Kikao Cha Halmashauri Kuu Ya Taifa Ya CCM Mjini Dododma Leo .......Ampa Tahadhari Rais Magufuli

$
0
0

JAKAYA Kikwete, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) anayemaliza muda wake amemtahadharisha mwenyekiti mtarajiwa wa Chama hicho John Magufuli kwa kumweleza kuwa uenyekiti ndani ya CCM siyo lelemama kwani wajumbe wasipoelewa wanachokitaka.

Mbali na kumpa tahadhari hiyo pia alikiri kuwa mwaka jana chama hicho kilikumbwa na misukosuko mingi ambayo ingeweza kukifanya chama hicho kuanguka kwani kilikuwa na mafisi wengi ambao walikuwa wakisubiri mkono udondoke ili washibe

Ametoa kauli hiyo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho ambayo ajenda ilikuwa moja tu ya kujadili na kupitisha jina la mwenyekiti ambalo litapelekwa katika mkutano mkuu kwa lengo la kupigiwa kura.

Kikwete amesema ..."CCM ilikuwa ivunjike wakati wa kipindi kigumu cha uchaguzi wa mwaka jana lakini tunamshukuru Mungu kwa kuwa tumeweza kukaa imara na kukitafa chama kutovunjika.

“Tunasema kikao kama hiki hatumwi mtoto tunakuja wenyewe kikao cha leo ni kikao cha kihistoria, kwa mamna mbili kwanza ni kikao changu cha mwisho, nikija kwenye NEC ni pale mtakapo nialika lakini tulikubaliana kwamba wazee hao wameishatumikia vya kutosha na tuwaache wapumzike utaratibu wa hapo nyuma ukimaliza uenyekiti unakuwa mjumbe wa kudumu wa kamati kuu na halmashauri kuu.

“Siku moja Mzee Mkapa akasema bwana mbona sisi wazee mnatusumbua sana mnatuita kila siku na sisi tumeishakuwa wazee tunakaa mpaka saa saba usiku kwa hivi sasa tuacheni, ndipo niliposema hatuwezi na tukaamua kuunda baraza la wazee.

“Tukaona hatuwezi kuwaita kila siku lakini tunawatengenezea baraza la wazee ambalo ni baraza la ushauri kimsingi linahitajika kwa jambo muhimu sana kama ilivyo kuwa mwaka lakini nilijadiliwa nikaambiwa JK hataki wazee lakini nikasema huo ni uamuzi wa busara kabisa” amesema Kikwete.

“Kuna maswala makubwa ya chama chetu na uhai wake kama ilivyokuwa mwaka wa jana, eeee chama chetu kilikuwa kimekaa katika msukosuko mkubwa mnaingia hapa watu wanaimba hiki wanaimba kile mjadala mkali lakini nikasema tutavuka tu maadamu tupo ndiyo changamoto ya uongozi.

“Na maadamu CCM haikuvunjika mwaka wa jana haitavunjika tena, maana mafisi yalikaa hapa yanasubiri mkono udondoke lakini haukudondoka na maadam haukudondoka mwaka wa jana CCM haidondoki,”amesema Kikwete.

Amesema rais atakuwa mwenyekiti na wakati mwingine kuna wakati kikao kinakuwa kigumu kwani wajumbe wanataka kutendewa haki wa wasipopata haki zao wanakuwa wakali sana.

Amesema halmashauri kuu ni kikao Muhimu cha uongozi pale ambapo hakuna mikutano ya chama amesema kamati kuu ni kikao cha kusimamia shughuli muhimu za chama na NEC ni kikao cha juu cha kutoa viongozi.

Amesema wajumbe wa vikao ni wepesi sana kusifia lakini wanakuwa wakali sana pale ambapo mambo yanaenda vibaya hivyo kiongozi ni lazima kumsikiliza na kujua nini ambacho wajumbe wanataka.

Amesema wajumbe hao wanakuwa wakali kwa kuwa wanataka mambo ndani ya chama yaende vizuri ili nao ndani ya chama waweze kujivunia.

Mbali na hayo amesema wajumbe wanatakiwa kushirikiana na mwenyekiti mpya ili kukifanya chama kuweza kusonga mbele zaidi.

Ripoti ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam Baada ya Kumalizika kwa zoezi la uhakiki wa silaha......Pia Wamezungumzia Kiasi Walichokusanya Ndani ya Siku 6

$
0
0
Jeshi la Polis kanda Maalumu jijini Dar es salaam limekamata watuhumiwa sugu 1,065 kwa makosa mbalimbali yakiwemo unyang’anyi wa kutumia nguvu, wizi wa maungoni, wapiga debe, wavuta bangi, kikosi cha mbwa mwitu, watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti tofauti katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na kamishina wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro alipokua akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo, Sirro alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumekuja baada ya kufanya operesheni kali katika maeneo mbalimbali jijini humo.

Aidha pamoja na kufanikisha zoezi hilo kwa watuhumiwa hao,jeshi hilo pia wamekamata lita 952 za pombe aina ya gongo,bangi puli 227, kete 210, na misokoto144 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Katika hatua nyingine ,kikosi cha kupambana  na wizi wa simu cha polisi kimefanikiwa kuwatia hatiani watuhumiwa watatu(3) kwa makosa ya uporaji wa simu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa kinondoni,watuhumiwa hao ni Richard Augustino (18), Abdallah Chande (36),Abdallah Said (22) wote wakazi wa jijini  Dar es salaam.

Hata hivyo kamanda Sirro aligusia  zoezi zima la uhakiki wa silaha na kusema kuwa lilienda vizuri na watu walijitokeza kwa wingi japo kuna changamoto kadhaa zilizojitokeza

Kamanda  Sirro amesema  idadi ya watu waliojitokeza kuhakiki silaha kwa wilaya zote tatu ni 11,602 na jumla ya silaha 14107 zilihakikiwa.

Pia kasema Jumla ya silaha 66 zilisalimishwa kutokana sababu mbalimbali ikiwamo mmiliki wa silaha kuwa na umri mkubwa na kushindwa kumudu silaha. Zoezi la uhakiki wa silaha limeiingizia Serikali mapato kiasi cha Mil 198.8

Jeshi hilo kupitia kikosi cha usalama barabarani kanda maalumu ya Dar es salaam limeweza kujikusanyia kiasi  cha shilingi 562,860,000/= kutokana na ukamataji wa makossa mbalimbali ya usalama barabarani kuanzia tar 15/7/2016 hadi 21/7/2016.
  1.    Idadi Ya Pikipiki Zilizokamatwa  -1,413
  2.      Idadi Ya Magari Yaliyokamatwa  –17,349
  3.      Daladala Zilizokamatwa           -7220
  4.      Magari Mengine (Binafsi Na Malori)- 10,129
  5.      Jumla Ya Makosa Yaliyokamtw-  18,762
6. Bodaboda Waliofikishwa Mahakamani Kwa Makosa Ya Kutovaa Helmet Na Kupakia Mishkaki   ni 49

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya July 23

Kamati Kuu ya CHADEMA kukutana kwa dharura Dar es Salaam

$
0
0

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), itakutana kwa dharura, jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe, ambapo pamoja na masuala mengine, itapokea taarifa na kujadili hali ya siasa nchini.

Katika siku za hivi karibuni, taifa limekuwa likipitia katika majaribu makubwa, ikiwa ni pamoja na uvunjifu mkubwa wa sheria na taratibu za kuongoza nchi unaofanywa waziwazi na mamlaka za juu/viongozi waandamizi wa nchi kupitia kauli na matendo mbalimbali kiasi cha kuwashtua Watanzania ambao wangependa kuona nchi yao ikiendeshwa katika misingi ya uwajibikaji wa kisheria na demokrasia.

Katika kikao hicho cha siku mbili, Julai 23-24, mwaka huu, Kamati Kuu pia itapokea taarifa na kujadili kabla ya kufanya maamuzi kuhusu mipango mbalimbali inayoendelea ya kukipanga chama ili kiendelee kufanya shughuli zake kwa ufanisi hususani kinapokwenda kuimarisha misingi kuanzia ngazi ya kitongoji nchi nzima, kupitia usimamizi wa kanda 10 za chama.

Imetolewa  Ijumaa, Julai 22, 2016 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA

Askari Polisi Auawa Kwa Kupigwa Risasi akiongoza magari usiku Kijitonyama Dar es Salaam

$
0
0

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Mensah wa Kituo cha Polisi Oysterbay ameuawa usiku wa kuamkia leo  kwa kupigwa risasi akiwa kazini eneo la Sayansi Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku huu na chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.

“Tukipata chanzo itakuwa tayari upelelezi wetu umetimia, hivyo kwa sasa tunalifanyia kazi ili kubaini wahusika wa mauaji hayo,” amesema Fuime.

Uamuzi wa Bodi ya Mikopo kuhusu Wanafunzi ambao hawajarejesha mikopo yao hadi leo

$
0
0

Mnamo mwezi Machi, 2016, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa notisi ya siku 60 ikiwataka wanufaika wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao.  

Aidha, taarifa hiyo pia iliwataka waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao na makato ya marejesho.  Baada ya kipindi hicho kumalizika, kipindi cha notisi hiyo kiliongezwa ambacho pia kimekwisha.

Kufuatia hatua hiyo, Bodi inapenda kuwataarifu wanufaika wote wa mikopo kwamba kuanzia wiki ijayo itaanza kutangaza majina ya wale wote ambao hawajaweza kujitokeza na kuanza kurejesha mikopo yao. 

Zoezi hili litajumuisha pia waajiri ambao hawajawasilisha taarifa za waajiriwa wao.  Hatua hiyo itafuatiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaoshindwa kutimiza matakwa hayo kwa mujibu wa kifungu cha 19A (1) cha sheria Na. 9 ya mwaka 2004.

Hivyo basi, wanufaika wa mikopo wanahimizwa kuanza kulipa madeni yao na waajiri kuwasilisha taarifa za waajiriwa au kufika kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ili kupata Ankara za madeni yao kabla ya zoezi la kutangaza majina halijafanyika. Marejesho yanaweza kufanyika kupitia Akaunti:

A/C No. 2011100205 – NMB

A/C No. 01J1028467503 – CRDB

A/C No. CCA0240000032 – TPB

Ni muhimu kuzingatia taarifa hii ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza kutokana na hatua zitakazochukuliwa.

Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

Vigogo wote Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Watumbuliwa MAJIPU

$
0
0
SERIKALI imemuondoa katika nafasi yake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Gerald Kamwenda na wakurugenzi wenzake, katika jitihada za kufumua na kusuka upya shirika hilo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ametangaza hatua hiyo ya serikali jana alipokutana na vyombo vya habari na kuongeza kuwa, watumishi wengine 41 wamehamishwa vituo vya kazi.

Alifafanua kuwa hatua hizo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lililotaka kufumuliwa na kusukwa upya kwa TFS ili kuongeza ufanisi.

Kutokana na hatua hiyo, Waziri Maghembe alisema Profesa Dos Santos Silayo ameteuliwa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TFS, wakati Kamwenda anahamishiwa Chuo cha Viwanda vya Misitu kilichopo Moshi.

Aidha, Mwanaidi Kijazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Raslimali za Misitu na Nyuki, yeye amekwenda kuwa Mhifadhi Mkuu Amani Nature Reserve na nafasi yake inachukuliwa na Zawadi Mbwambo.

Waziri Maghembe alisema Mohamed Kilongo aliyesimamishwa kazi Januari 5, mwaka huu uchunguzi umeonekana hana hatia na hivyo anaendelea kuwa Mkurugenzi Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu.

Alisema Wizara imeamua Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Gladnes Mkamba ahamishiwe Idara ya Mipango makao makuu na nafasi hiyo kuteuliwa Dk Ezekiel Mwakalukwa, kuwa Kaimu Mkurugenzi.

Aidha Monica Kagya aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Ufugaji Nyuki, anakuwa Mtafiti Mwandamizi Idara ya Nyuki (Tawiri). Alisema Kagya ni mtaalamu wa masuala ya nyuki, hivyo atahamishiwa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori, ili ashughulikie utafiti wa masuala ya nyuki.

Pia alisema katika Idara ya Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa anakuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Herman Kerayo ambaye anahamishiwa Idara ya Mipango Makao Makuu.

Profesa Ramadhan Kideghesho, yeye anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo cha Mweka wakati Mabula Misungwi aliyekuwa Meneja Mradi Selous, anakwenda Chuo cha Wanyamapori Pasiansi na nafasi yake inachukuliwa na Jaffary Lyimo, huku Robert Mande akipelekwa kuwa Kaimu Mkurugenzi msaidizi Uzuiaji Ujangili.

Waziri Maghembe alisema Majjid Ally ameteuliwa kuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Leseni, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Haji Mpya ambaye amehamishiwa Shamba Jipya Songea kuwa Ofisa Misitu Alisema Julai 18, mwaka huu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikutana na viongozi na watumishi wa Wizara hiyo na watendaji wakuu na watumishi wa TFS na kuagiza kufumuliwa na kusukwa upya kwa wakala huo.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu alitaka kuondolewa kwa utitiri wa vituo vya ukaguzi na kuwekwa vituo vichache na kuondolewa kwa ofisi za makontena yanayotumiwa na ofisi ya TFS, badala yake watumishi wanaofanya ukaguzi wasimame mahali pa wazi ili kuondoa mianya ya rushwa na kuweka uwazi katika utendaji.

Ujumbe wa Diamond kwa bintiye Wazua Gumzo......Kamwambia "Ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana"

$
0
0
Diamond Platnumz si mgeni kwenye jumbe tata kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini ujumbe wake mpya kwa bintiye, Tiffah umesababisha mjadala mkubwa.

Akiweka picha ya binti yake huyo ambaye mwezi ujao anatimiza mwaka mmoja, Diamond aliandika: Buff day Girl! my little Pumpkin😍 My Miss World 👸 @princess_tiffah kua mama, nikupe Raha ya Dunia na ujifaidie Ustar wako….. ila dah ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana #KIDOGO tu, Maana ntalificha wapi hili sura langu.”

Maneno: Ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana #KIDOGO tu’ ndiyo yaliyosababisha povu la haja.


Twinsrebeccita: Hivi mtoto hajafikisha hata miaka miwili ushaanza kufikiria masuala yake ya ngono!!!! Maneno ya bure kwako, usitumie utupu wa mwanao kutangaza biashara yako.

Precioushamis: Mungu auTunze usichana wako /ujana wako tiffah, kinywa cha baba yako kishindwe kwa jina la yesu amina

Jahmolbiggz: Daym 😁 did u just wrote that? Any real Dad out there won’t even think of writing such words to her dota.. Shit is Crazy

Madimwashiti: @princess_tiffah never follow your parents foot steps. U need more prayer. @diamondplatnumz better pray for this little girl coz what goes around comes around. Many many little SIMBAS out there want spare you dear. That is my own thoughts. Think about it NASSEB

Neyesu Daniel: Diamond ww sio baba mwema! Utaanzaje kumwambia bint ako ivo!? Umenikera mbna unakosa madil ya kiafrika?? Acha izo bna kama ww una njia ambazo si nzur bc mfunze mwanao akue vema!

Rajabu Mussa: Tena atakua amefuata Tabia Za Huku na huku(kwa maza n baba) maana kote kote hakuna mwenye afazali…….ukila nawe utaliwaaaaa japo #Kidogo

Tuzo Hella: Atii aliwe kidogooo!!! Labda wakati anaandika hiyo post hakuwa poa!!alionja kidogo ile kitu ya Arusha inarushanga akili,coz diamond hukogi na akili mingi sasa alifikiri nn kuandika hayo maneno hayo!!eti mtt akulwe kidogo kweliii!!!! D your not serious

Unaounaje ujumbe huo?

Maamuzi ya Wizara ya Elimu kuhusu wanafunzi Wa Vyuo Vikuu wanaotakiwa kwenda Field na na Hatima ya mikopo yao ya Field

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kufunguliwa Kwa Mfumo Wa Udahili Wa Pamoja (CAS) Unaoratibiwa Na NACTE Na Kutangazwa Kwa Majina Ya Waombaji Udahili Waliochaguliwa Kujiunga Na Kozi Za Cheti Na Diploma

$
0
0
Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) umefunguliwa tena kuanzia tarehe 22 Julai 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizo wazi baada ya Baraza kuchagua waombaji udahili waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni  tarehe 5 Agosti 2016 saa sita usiku.

Waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kukamilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016, wanaarifiwa kuanza kuwasilisha maombi ya udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) ili kujaza nafasi zilizo wazi. Waombaji wanahimizwa kutumia muda huu wa nyongeza ili kuwasilisha maombi.

Baraza linapenda pia kuwaarifu waombaji udahili na umma kwa ujumla kuwa vikao vya Kamati za kuidhinisha majina ya waombaji udahili kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) vilipitisha orodha ya majina  ya wenye sifa za udahili kulingana na nafasi za udahili kwa kila kozi zitolewazo na vyuo husika kati ya tarehe 18 Julai 2016 na 21 Julai 2016. 

Majina ya waombaji waliochaguliwa kwa kila kozi itolewayo na chuo husika yamekabidhiwa vyuoni kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS). 

Waombaji waliochaguliwa nao wamearifiwa kupitia kurasa (profile) zao binafsi au kwa kubofya hapa. Waombaji ambao hawakuchaguliwa wamejulishwa sababu zilizowafanya wasichaguliwe kupitia kurasa (profile) zao pia.  

Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza waliowasilisha maombi yao kupitia NACTE, Baraza linapenda kuwaarifu kuwa, mashauriano kati ya NACTE na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yanaendelea kufanyika ili kufanikisha udahili wa waombaji wa kozi za Shahada ya Kwanza kama Serikali ilivyoagiza.

Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 22 Julai, 2016

Mo Dewji kugawa nusu ya mali zake kwa Watu Masikini

$
0
0

MKURUGENZI Mtendaji wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL Group), Mohammed Dewji, ameungana na matajiri wakubwa duniani, kutangaza azma ya kugawa nusu ya mali zake kusaidia jamii.

Taarifa kutoka mtandao mashuhuri duniani wa Forbes, imesema kuwa Dewji, ambaye ni bilionea kijana kuliko wote barani Afrika, ameingia katika kundi la matajiri hao ambao wametoa ahadi ya kutoa nusu ya mali zao, kusaidia jamii.

“Baada ya kushuhudia umasikini mkali wakati nikilelewa, siku zote nimekuwa nikijisikia kuwajibika kutoa kwa ajili ya jamii yangu,” amesema Dewji katika barua yake ya kutangaza ahadi hiyo, ambayo ameiweka wazi kwa waandishi wa habari.

Alishukuru wazazi wake kwa kumuunga mkono na kumjengea moyo wa kusaidia jamii na kipekee katika wajibu wake kwa dini yake ya Uislamu wa kutoa na kujali wahitaji na jamii.

Bilionea huyo anakuwa Mtanzania wa kwanza kuungana na matajiri duniani, Bill Gates na Warren Buffett katika kutangaza nia hiyo tangu 2010 na kushauri watu wengine wenye uwezo kujitolea kwa ajili ya jamii.

Kundi la matajiri waliokwisha kutangaza nia hiyo ya kutoa sehemu ya mali zao kwa jamii, limeshafikia 155 kutoka nchi 17, ambapo Juni mwaka huu, kundi hilo linalotambuliwa kwa jina The Giving Pledge, lilitangaza kupata wajumbe wapya 17.

Wajumbe wa mwanzo wa kundi hilo ni pamoja na Eli Broad na mkewe Edythe, John Doerr na mkewe Ann pamoja na mmoja wa wamiliki wa Facebook, Mark Zuckerberg na mkewe, Priscilla Chan.

Mtandao mashuhuri wa Forbes, umemkadiria Dewji kuwa anamiliki mali zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.1, akiongoza kundi la makampuni ya METL nchini Tanzania, linalojihusisha na biashara za viwanda vya nguo, vinu vya unga na viwanda vya mafuta ya kula, huku kinywaji chake cha Mo Cola, kikiuzwa bei rahisi kuliko kununua Coca-Cola.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 1 & 2

$
0
0

Ningependa Kukushukuru Mpenzi Msomaji, Uliyekuwa Nasi Katika Simulizi Ya Kwanza Ya Mwanafunzi Mchawi

Hiyo Riwaya bado inaendelea na ndo kwanza imefikia patam. Wakati tukiendelea na Riwaya hiyo, tumeona tusikuache mtupu, tukaamua kuja na hii mpya huku ukiendelea na ile ya mwanzo ambayo huwekwa kila baada ya siku moja.
 ***************

Mtunzi:Eddazaria G.Msulwa
Ni siku ya jumamosi kama kawaida wanafunzi wote wa shule tunayosoma tunakwenda viwanjani kucheza michezo mbali mbali kama mpira wa miguu na michezo mingine ambayo wanacheza wasichana waliopo katika shule yetu ambayo niya bweni yenye mchanganyiko wa wasichana na wavulana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na nishule ya mtu binafsi(PRIVET SCHOOL) iliyopo katoka mkoni Arusha.

Kama kawaida yangu ya kuwa shabiki wa timu ya darasa langu la kidato cha tano ninachosoma ninaendelea kutazama mechi tunayocheza na kidato cha tatu hadi wakati huu tumeshafungwa goli mbili kwa moja huku dakika zikiwa zinakimbia kuelekea ukingoni huku mashabiki wa kike wa kidato cha tano wakiendelea kuwapa moyo wachezaji wetu waliopo uwanjani

“Oya Eddy mcheki yule manzi pale”
“Yupi?”
“Yule aliyevaa sweta jeupe”
“Ana nini?”
“Cheki alivyo bomba majamaa kibao wamemtokea wamepigwa chini”
“Yupo kombi gani?”
“HKL”
“Ndio maana angekuwa huku tulipo sisi wala asingekuwa mzuri”

“Hembu acha pumba zako Eddy”
“Kweli John unadhani angekuwa science unadhani angekuwa hivi wewe si unawaona wakina Matha walivyo kauzu class hadi kuwatongoza mtu unashindwa”

Tukajikuta tukikatisha mazungumzo baada ya mchezaji wetu mmoja kufunga bao la kukomboa jambo lililoturudishia furaha hata ya kuwepo uwanjani.

Kabla hata ya dakika mbili mbele mchezaji wetu yule yule akafunga bao jingine kupitia mpira wa kona uliopigwa na akaudumbukiza nyavuni kwa kichwa na kuamsha shangwe za wanafunzi wote wa kidato cha tano na kuwafanya mashabiki baadhi kuingia uwanjani huku wakishangilia kwa furaha kwani tayari dakika zilisha kwisha.

Mimi na rafiki yangu John tukabaki nje ya uwanja huku sura zetu zikiwa na furaha kupita maelezo

“Wee dada jamaa anakuita hapa”.John alimuita yule msichana tuliyekuwa tunamjadili dakika kadhaa zilizopita.

Akatuangalia kwa dharau yeye na rafiki zake kisha wakaongea maneno ya kunong’onezana na kuanza kucheka kicheko kilichotufanya tuwe kimya kama tumemwagiwa maji ya baridi.

Safari ya kurudi shuleni ikaanza kwani kiwanja chetu cha mpira kipo eneo la nje ya eneo la shule.Tukiwa tumeongozana na kundi la wasichana wa kidato chetu wakiimba nyimbo za ushindi mimi na John tukawa na kazi ya kumfwatilia yule msichana ambaye kusema la ukweli amejaliwa uzuri unaweza kusema alipewa siku yake ya pekee katika uumbwaji wake

Tukafika hadi kwenye duka la shule ambapo yule msichana alikwenda na rafiki yake ambaye kidogo naye anavutia japo si sana.Kutokana hatukuwa na lengo la kufika katika duka hilo kwa aibu tukajikuta tukinunua mifuko miwili ya pipi za Big boom

“Claudia ile hela siioni”Yule msichana alizungumza huku akiwa anajipapasa papasa kwenye mifuko ya sketi yake huku akionekana kuwa na wasiwasi wa hali ya juu kwani tayari walishakunywa soda pamoja na kula keki za watu

“Hebu tazama vizuri”
“Kweli si unaona mifuko yote haina hela jamani sijui imeangukia wapi”

Nikawatazama kwa huruma kisha nikatoa waleet yangu mfukoni iliyotuna kwa wingi wa pesa nikamuuliza muuza duka ni kiasi gani cha pesa anachowadai akaniambia nikawalipia na chenchi iliyobaki nikamwambia muuza duka awapatie.

Tukaanza kuondoka kabla hatujafika mbali Claudia akatuita na tukasimama wakaja katika lile eneo tulilosimama huku rafiki yake ambaye ndio aliyetufanya twende pale dukani kwa kumfatilia akaawa analia

“Samahani kaka zangu tunawashukuru”

“Haina shida vitu vya kawaida,Eddy twende zetu”

“Ngojeni kwanza”

Claudia alizungumza huku akimshika John beda aliyeanza kugeuka na kutaka kuanza kuondoka katika eneo tulilo kuwepo

“Mbona huyo mwenzako analia”

 “Amepoteza pokety money yake ndio kwanza ametoka kuipokea leo mchana kwenye basi”

“Mmmm poleni”

John alizungumza kwa maringo na kuanza kuondoka ikanilazimu mimi kubaki kwani roho ya huruma ilianza kunitawala huku wakati wote nikimtazama yule msichna ambaye bado sikulitambua jina lake

“Amepoteza sh ngapi?”

“Eti Salome umepoteza shii ngapi?”

“Elfu themanini na tano”

Nikakaa kimya kama dakika mbili nikifikiria nini nifanye,nikajikuta nikiitoa wallet yangu mfukoni na kuesabu noti tisa za elfu kumi kumi kisha na kuzitoa na kumpa Salome taratibu akazipokea huku akiwa haamini tukio linalo tendeka kwa wakati huo.

“Zitakusaidia saidia siku mbili tatu”

“Asante sana kaka yangu”

“Powa ukiwa na shida utakuja darasa la PCB ndio ninaposoma”

Nikawapa na mfuko wa pipi nilio nunua kisha nikaondoka huku moyoni mwangu nikijifariji kuwa tayari nimesha fanikiwa katika hatua ya kwanza ya kumpata mtoto mzuri.

Tukafika bwenini tukaoga kujiandaa na sikukuu ya wanafunzi ambayo hufanyika kila mwisho wa mwenzi wakati wa usiku katika ukumbi wa shule.

Sikukuu hii hutoa fursa ya wanafunzi kuonyesha vipaji vyao mbali mbali.Tukapitia katika cantin ya shule na tukanunua chakula kisha tukaelekea kwenye ukumbi uliojaa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza ahadi cha sita

Shughuli zikaanza huku wanafunzi mbali mbali wakionyesha vipaji vyao huku wakishangiliwa na wanaofanya vibaya huzomewa.Ukumbi ukakaa kimya huku tukiwasubiria washiriki wa shindano la umiss wa shule kupita mbele yetu huku majaji wakiwa ni waalimu wetu wa michezo pamoja na wanafunzi baadhi.

Wakaanza kuingia mmoja mmoja huku wakiwa wamependeza,nikajikuta ninanyanyuka kwa furaha huku nikipiga makofi hii ni baada ya kumuona Salome akiwa katika msururu huo wa mamisi waliochanganyika vidato mbali mbali.

Wakajipanga mbele ya majaji na kuanza kuulizwa maswali mmoja baada ya mwingine kwa lugha ya kingereza.Ikafika zamu ya Salome kuulizwa swali wanafunzi wote wakakaa kimya kumsikiliza atakacho kijibu

“SALOME CAN YOU TELL US WHAT IS LOVE?”(Salome unaweza kutuambia upendo ni nini?)

“Love is force of nature however much we may want to,we can not command,demand or disapper love,any more than we can and in adition love cannot  be bought,sold or trade.You cannot make some one to love you.Thanks”(Upendo ni hali ya msukumo wa kihalisia kwa jinsi tunavyo hitaji.Hatuwezi kulazimisha,kukomalia au kutawanya upendo kwa kadri tunavyoweza na kwa kuongezea Upendo hauwezi kununuliwa kuuzwa au kubadilishana.Hauwezi kumfaya mtu kukupenda wewe.Asante”)

Ukumbi mzima ukapiga makofi kasoro mimi kwani nikajikuta sentensi ya mwisho ya Salome ikijirudia rudia akilini mwangu “YOU CAN CANNOT MAKE SOMEONE TO LOVE YOU”(Huwezi kumfanya mtu kukupenda).Wakatoka ukumbini kwa wimbo walio ingilia kupisha mambo mengine kuendelea huku tukisubiri matokeo kutoka kwa majaji wetu.

Muda wa matokea ukawadia huku washiriki waote wakisimama mbele yatu.Jaji mmoja akaanza kutangaza nafasi kuanzia ya tatu na ya pili huku nafasi ya kwanza akimkabidhi mgeni rasmi ambaye ni mmiliki wa shule kuitangaza huku wakiwa wamebakia washiriki wanne.Tukakaa kimya kusubiria ni nani atakaye nyakua taji kwa mwaka huo

“NA MSHINDI WETU NI……………………..SALOME ALEX EDWARD”

Ukumbi mzima ukanyanyuka na kuanza kupiga makofi ikiwemo mimi huku John akinisukuma sukuma kila wakati huku akinionyeshe jinsi Salome alivyopendeza na kuzidi kuvutia kwenye macho ya wengi.Akaanza kuvalishwa vitu wanavyo valishwa mamisi pale wanapashinda huku akikabithiwa uwa kubwa na mgaeni rasmi.

Muongoza shindano MC akamuomba Salome amchague mtu wa kwenda kucheza naye mziki kwa dakika tano.Salome akachukua kipaza sauti na sote tukakaa kimya kumsikiliza ni nani atapata bahati hiyo ya kuitwa mbele ya ukumbi huo.Salome akatizama tizama na macho yake akaelekea sehemu tuliyokaa sisi.Akanyoosha kidole chake watu wote wakaangalia tulipo sisi

“Eddy hichi kidole ni chako”.John alizungumza huku akinisukuma sukuma kwa kutumia bega lake.Nikanyanyuka kidogo ila Salome akatingisha kidole chake kwamba si mimi ni jamaa aliyekaa kiti cha nyuma yetu ambaye ni kaka mkuu wetu.

Jamaa akanyanyuka kwa furaha huku wezake nyuma wakimtuma akamchezee Salome hadi alainike.Mimi na John tukabaki kama watu wasio amini huku mimi roho ikianza kuniuma kupita maelezo na kumfanya John kuachia msunyo mkali adi watu wa pembeni yetu wakamtazama na kuanza kucheka

“Mademu wengine bwana was**e kama nini”John alizungumza huku akiendelea kutoa misunyo.Jamaa kama alivyoagizwa na wezake akawa anazidi kumshika shika Salome mwili wake huku wanafunzi wakishangilia kwa furaha na kuzidi kunifanya niichukie sikukuu hiyo

“John twende zetu tukalale”Tukanyanyuka kwenye viti vyetu kutokana na mlango wa kutokea upo mbele tukalazimika kupita mbele ya ukumbi huku macho yangu yaliyojaa hasira yakimtazama Salome ambaye naye alinitazama kwa sekunde kadhaa kisha akayapeleka macho yake sehemu nyingine.Tukashuka kwenye ngazi za ghorofa lenye ukumbi wa shule.Kabla hatujafika chini mwanafunzi mmoja akatuita.

==>Endelea nayo <<kwa kubofya hapa>>

Serikali ya Kenya yamtimua Koffi Olomide Kwa kumpiga mnenguaji wake wa kike

$
0
0

Serikali ya Kenya mapema leo imechukua uamuzi wa kumtimua mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Koffi Olomide kufuatia tukio alilolifanya jana la kumpiga mnenguaji wake wa kike katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Taarifa za kuaminika kutoka jijini Nairobi zimeeleza kuwa Koffi Olomide alikamatwa na polisi jana majira ya saa nne usiku alipotoka kufanya mahojiano na Citizen TV.

Mwanasheria wa Koffi Ollomide, Prof George Wajackyah amesema kuwa tangu walipokamatwa jana usiku walitunzwa kama wanyama na kwamba Serikali ya Kenya imewatimua na kuwarudisha Congo hata bila kuwa na passport zao.

Alisema walitimuliwa kwa nguvu na kusindikizwa leo asubuhi hata bila kupewa nafasi ya kwenda mahakamani Jumatatu kama walivyokuwa wanatarajia.

Koffi Olomide alitua nchini humo jana akitarajia kufanya tamasha kubwa leo lakini limeota mabawa.

Jeshi la mitandao ya kijamii la Wakenya ambalo linatajwa kuwa na nguvu zaidi Afrika Mashariki hasa kupitia twitter kuanzia jana lilimshambulia vikali Koffi Olomide kwa hatua yake ya kumtwanga teke mnenguaji wake jijini Nairobi, katika tukio ambalo lilinaswa kwenye kamera.

Ntahakikisha Serikali inahamia Dodoma :Rais Dkt.Magufuli.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  amesema katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha Serikali inahamishia makazi yake mjini Dodoma.

Amesema hayo leo, wakati alipokuwa  akihutibia wajumbe  wa Chama cha Mapinduzi(CCM) katika Mkutano Mkuu Maalumu  wa  Chama hicho uliofanyika  mjini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti.

“Nitahakikisha katika awamu ya uongozi wangu, Serikali inahamia Dodoma, najua viongozi wengine wote nao watanifata, kwa kuwa sasa miundombinu ya Dodoma inaweza kukidhi mahitaji yote” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi nane ya uongozi wake chini ya Serikali ya Awamu ya Tano  ameweza kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuanza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Akiongelea maeneo ya utekelezaji katika kipindi chake Dkt. Magufuli alisema kuwa mpaka sasa Serikali imefanikiwa kusimamia suala la utoaji wa elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari nchini na kuwezesha udahili kuongezeka zaidi tofauti na miaka iliyopita.

Aidha Dkt. Magufuli alisema kuwa Serikali yake pia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa mapato ya serikali hali itakayosaidia kuimarisha utoaji wa huduma muhimu za jamii.

Aidha, Serikali ya Awamu ya Tano imeagiza  ndege mbili mpya zinazotarajiwa kuwasili nchini Septemba mwaka huu,

Rais Dkt. Magufuli aliongeza kuwa Serikali yake kwa kushirikiana na Serikali ya Uganda wamefanikiwa kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima katika ziwa Alberti nchini Uganda kwenda bandari ya Tanga ambapo mafuta hayo yatasafirishwa sehemu mbalimbali duniani na bombahilo  litazalisha zaidi ya ajira 20,000.

Vile vile, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali yake imeweza kurudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma  na kuweza kuondoa watumishi hewa waliokuwa na waliokuwa wamefikia 12,500,na  kuongeza kuwa kwa mwaka huu Serikali imetenga fedha za matumizi jumla ya shilingi trilioni 29.5, ambapo asilimia 40 ya fedha hizo zitapelekwa katika kutekeleza  shughuli za maendeleo.

Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ulihudhuriwa na wajumbe zaidi 2,000  ulimpitisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mshindi na Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kura 2398  kati ya kura 2398 zilizopigwa ikiwa ni sawa na asilimia 100.

Rais Magufuli anakuwa  Mwenyekiti wa awamu ya Tano baada ya  kupokea uongozi huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho anayemaliza muda wake Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka 10.

Picha za Rais Magufuli Alivyochaguliwa Kuwa Mwenyekiti Mpya wa CCM Kwa Kura Zote

$
0
0
Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake Dkt Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli wakiwapungia mkono Wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum mara baada ya matokeo kutangazwa rasmi na Dkt John Pombe Magufuli kuibuka kwa kura zote za ndio zipatazo 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika.
Mwenyekiti Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akimkumbatia Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka kumi.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake leo,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi mbalimbali vya chama cha Mapinduzi (CCM),Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyepigiwa kura na Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum na kuibuka na kura zote za ndio kutoka kwa Wajumbe 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika
Makamu Mwenyekiti-Zanzibar Dkt Shein akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10,pichani katikati anaeshuhudia ni Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dkt Jakaya Kikwete 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrhamani Kinana akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka 10.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh William Mkapa akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho 
Wake wa viongozi wakishangilia baada ya Mwenyekiti Mpya wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho 

Alichokiandika Zitto Kabwe baada ya Rais Magufuli kupewa uenyekiti wa CCM

$
0
0
Jana July 23 2016  Rais John Pombe Magufuli alikabidhiwa rasmi nafasi ya uenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM   baada ya kupigiwa kura za ndio 2398  kutoka kwa wanachama wa chama hicho ambapo hakuna kura hata moja ya hapana wala iliyoharibika

Baadhi ya viongozi wakiwemo wa vyama vya upinzania walishiri akiwemo mwenyekiti wa TLP Augustino Mrema, lakini wapo pia waliotamani kufikisha hisia zao kuhusu tukio hilo na mmojawapo ni mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kupitia account yake ya facebook aliandika maneno haya…

"Napenda kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama hicho. CCM imeendelea kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila baada ya muda

"Jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na barani Afrika. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona umuhimu wa Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu.

"Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais." –Zitto Kabwe

Alichokisema Rais Magufuli Baada ya Kuchaguliwa Kuwa Mwenyekiti wa CCM

$
0
0
MWENYEKITI wa tano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli, amewaomba wanachama wa chama hicho kumuombea kwa Mungu ili apate uvumilivu wa mtangulizi wake, Mwenyekiti mstaafu, Jakaya Kikwete.

“Mzee Kikwete wewe una moyo wa uvumilivu. Sina hakika kama mimi ninao uvumilivu kama wako...umetupa fundisho kubwa sana,” alisema Magufuli wakati akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa kwa kura asilimia 100 kuwa Mwenyekiti wa chama hicho.

Katika kuonesha tofauti yake na Kikwete katika uvumilivu, Magufuli alikumbusha changamoto aliyokutana nayo Kikwete, wakati alipoingia katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mwaka jana, kupeleka mapendekezo ya majina ya wagombea watano wa urais waliokuwa wamepitishwa na kikao cha Kamati Kuu, ili wapigiwe kura.

Ndani ya kikao hicho wakati Kikwete, wajumbe wa Kamati Kuu na wa Baraza la Wazee la Ushauri wakiingia, baadhi ya wajumbe wa kikao hicho walikiuka utaratibu wa siku zote wa chama hicho, kwa kuimba kuwa na imani na mmoja wa wagombea wa urais, Edward Lowassa, ambaye jina lake lilikatwa katika kikao cha Kamati Kuu.

Kupotezwa  
“Siku ile umeingia ukumbini, watu wakawa wanaimba kuwa wana imani na mtu mwingine, siku hiyo hiyo robo au nusu yao wangepotea...sifahamu, umetoa fundisho kwa sisi vijana kwamba saa nyingine uvumilivu ni kitu muhimu,” alisema akimaanisha kama hali hiyo ingemkuta yeye ndiye Mwenyekiti, hayo ndiyo yangetokea.

Kutokana na uvumilivu aliouonesha Kikwete katika mkutano huo, Magufuli aliwataka wanachama hao wa CCM kumuombea kwa Mungu, ili apate angalau nusu ya uvumilivu wa Kikwete, ili katika uongozi wake mambo yaende salama.

Kuzushiwa JK
Alimsifu Kikwete kwa kutumia hekima ya uvumilivu, kwa kuwa kiongozi huyo mstaafu, amesemwa mambo mengi, akazushiwa na hata kutukanwa kutokana na hatua, uamuzi na vitendo vyake Magufuli.

“Umesemwa mengi, umetukanwa mengi na umezushiwa mengi kwa ajili yangu, lakini kwa upendo wako na kwa kumtegemea Mungu, ukakaa kimya...sina cha kukulipa, bali nitafanyia kazi Watanzania na hasa wana CCM kwa nguvu zote,” alisema Dk Magufuli.

Alitoa mfano wa Kikwete kuzushiwa alikuwa akikataa kumkabidhi Dk Magufuli uenyekiti wa CCM kwa kufuata desturi ya chama hicho, akasema Mwenyekiti huyo mstaafu amemshawishi mara nne, lakini yeye ndiye aliyekuwa akikataa.

“Nakumbuka umeniambia mara nne, ya kwanza ulikuja kuniambia nikakukatalia bosi wangu, ulinipigia simu na mimi nikawa naanzisha mjadala mwingine. Nakupa pole na unisamehe sana kwa kuwa kukukatalia kulisababisha utukanwe,” alisema Rais Magufuli.

Serikali Dodoma
Kabla ya kumaliza hotuba yake, Magufuli alitangaza ahadi kwa wanachama hao, kuwa amebakiza miezi minne na miaka minne kabla ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitano na kusema kabla ya kumaliza kipindi hicho, atakuwa amehamishia serikali yote Dodoma.

Magufuli alisema kwa sasa miundombinu ya Dodoma inawezesha serikali kuhamia huko, kwa kuwa barabara za kutoka Makao Makuu hayo ya serikali kwenda sehemu mbalimbali nchini, zinapitika kwa lami.

Mbali na barabara, alisema pia huduma kwa ajili ya maisha ya watu nazo zinapatikana kwa kuwa mkoa huo una uzoefu wa kuhudumia wabunge, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na mikutano mingine, huku mkoa huo ukiwa na Chuo Kikuu cha Dodoma, ambacho ndio kikubwa kuliko vyote nchini.

Alisema, akihamia yeye katika Ikulu ya Chamwino ambayo alisema ina kila huduma anayohitaji, anatarajia Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri na serikali nzima itamfuata.

Babu wa demokrasia
Magufuli alisema CCM ndio chama kilicholea demokrasia hapa nchini na kinaendelea kutoa ulezi huo na kufafanua kuwa chama hicho ndio babu na bibi wa demokrasia; baba na mama wa demokrasia na kaka na dada wa demokrasia kwa vyama vyote nchini.

Alisema kwa kuwa Serikali anayoiongoza inatekeleza Ilani ya chama hicho, hivyo chama hicho ndio mabosi wa mabosi wote serikalini na kuonya kuwa ambaye hataki hilo, ataondolewa.

Kupendekezwa kwake
Awali wajumbe wa Mkutano huo Mkuu Maalumu wa CCM wapatao 2,398 walimpigia kura ya kumchagua Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Kikwete ndiye aliyesoma pendekezo la NEC kwa wajumbe wa mkutano huo kuhusu mgombea wa nafasi hiyo.

“Madhumuni ya mkutano huu ni kuchagua mwenyekiti mpya. Sisi katika Halmashauri Kuu tunampendekeza kwenu Mheshimiwa Dakta John Pombe Joseph Magufuli ashike nafasi hiyo,” alisema Kikwete saa 7:10 na kauli yake hiyo kupokelewa kwa shangwe, vifijo na vigelegele.

Akimwelezea Magufuli, Kikwete alisema ana imani isiyo na hata chembe ya shaka kuwa atafanya kazi hiyo vizuri, kwa sababu ya imani na mapenzi yake makubwa kwa chama hicho na Watanzania.

Alisema Magufuli ametumikia Taifa na wananchi kwa miaka mingi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa, katika wadhifa mbalimbali aliokuwa nao. Alisema Magufuli amekuwa mbunge na waziri kwa miaka 20, ambapo miaka 10 wakati wa serikali ya Rais Benjamin Mkapa na mingine 10 wakati wa serikali yake.

Alisema pia Magufuli amekuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya na mkoa, mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya na mkoa na mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa kwa miaka 20, hivyo anakijua mno chama.

Kikwete alisema Magufuli ameongoza nchi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa katika kipindi kifupi cha miezi 8 tangu alipochaguliwa, hivyo sasa anafaa kuvaa kofia zote mbili.

“Kichwa chake sasa kinatosha avae kofia zote mbili - ya urais na uenyekiti wa chama. Nawaomba wajumbe wote tumuunge mkono. 

“Tumpe kura zote za ‘Ndiyo’ na isipotee hata moja,” alisema Kikwete ambaye ameng’atuka baada ya kuongoza Chama tangu Juni 2006. 

“Mimi naondoka na bila shaka yoyote namwachia Chama Cha Mapinduzi Rais Dakta John Pombe Joseph Magufuli. Nakiacha Chama Cha Mapinduzi katika mikono salama na nina hakika kitapata maendeleo makubwa ya haraka,” alisema.

Kura zatangazwa
Kazi ya kupiga kura na kuzihesabu ilipokuwa ikiendelea, viongozi wakuu wa CCM na wastaafu baada ya baadhi yao kupiga kura, waliondoka kwa ajili ya mapumziko.

Baada ya mapumziko, walirejea ambapo baada ya salamu za wageni na baadhi ya wanasiasa waliorejea CCM baada ya kukimbilia upinzani kumalizika, Kikwete alisoma matokeo.

Akitangaza matokeo hayo, Kikwete alisema kura zilizopigwa zilikuwa 2,398, zilizoharibika sifuri na hivyo kura halali zikawa 2,398. 

Kikwete aliendelea kuwa matokeo yameonesha kuwa, kura za Hapana ni sifuri na kura za ndio ni 2,398, na hivyo Magufuli amepitishwa na wajumbe wa CCM kwa nidhamu ya juu ya kumpa asilimia 100 ya kura.

Makamu wenyeviti
Awali, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema mkutano mkuu huo usio wa kawaida, unafanyika kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (103) (4) cha Katiba ya CCM na ajenda yake ni kumchagua mwenyekiti mpya, kufuatia uamuzi wa Kikwete kung’atuka, akitekeleza utamaduni wa chama kuachiana madaraka, ili kumpisha Rais John Magufuli.

Aidha, alisema kwa mujibu wa Kifungu 7 (105) (5) (a) cha Katiba hiyo, unapofika wakati wa uchaguzi kazi mojawapo ya mkutano mkuu ni kuchagua makamu wenyeviti. 

Lakini, alisisitiza makamu wote wawili wa sasa, muda wao haujamalizika kikatiba na utamalizika mwezi Novemba 2017 “Makamu wote wawili hawajamaliza muda wao. Muda wao utamalizika Novemba 2017, hivyo hakuna sababu ya kuwachagua tena. Hapa leo tunachagua mwenyekiti peke yake,” alitangaza Kinana.

Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Bara ni Phillip Mangula na upande wa Zanzibar ni Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais wa Zanzibar Dk Shein , mawaziri wakuu wastaafu Mizengo Pinda, Cleopa Msuya, Dk Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba, John Malecela, Makamu wa Rais mstaafu Mohamed Gharib Bilal na makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Yusuf Makamba na Wilson Mukama.

Kinana Ajiuzulu..........Achaguliwa Tena mbele ya Mkutano Mkuu Kuwa Katibu Mkuu wa CCM

$
0
0
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo kwa Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais John Magufuli, lakini Rais amekataa barua yake hiyo.

Badala yake, Rais Magufuli amemtaka Kinana na manaibu katibu wakuu wawili na sekretarieti nzima ya chama hicho, kuendelea na kazi. 

Hayo yalisemwa na Rais Magufuli wakati akitoa hotuba ya kushukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu Malumu wa CCM, mjini hapa.

“Nimepata barua ya Kinana ya kujiuzulu nafasi yake pamoja na wakuu wa idara za sekretarieti. Nimeamua Kinana na sekretarieti yote waendelee kuwepo. 

“Kama kutakuwa na haja baadaye nitaitisha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na siyo leo,” alisema Magufuli, akiwatangazia wajumbe hao wa kikao cha Mkutano Mkuu, ambacho ni kikao cha juu cha chama.

Alisema kwa kuwa mkutano huo ndiyo wenye uamuzi wa mwisho kuhusu masuala ya chama, hivyo anawauliza wajumbe kama wamekubaliana na pendekezo lake hilo la Sekretarieti ya chama iendelee.

“Nawauliza wajumbe mnaafiki?” Ambapo wote kwa kauli moja walisema; “Ndiyo.” Magufuli alisema kulikuwa na watu waliokuwa wamejipanga kuchukua nafasi hizo za sekretarieti, lakini “sasa imekula kwao”. Hakutaja watu hao.

Akiongeza kuwa; “Nitaendelea kuwa na Kinana na nina imani yeye na sekretarieti nzima watasimamia vizuri mambo kadhaa niliyoagiza yasimamiwe haraka.”

Magufuli alisema CCM ni chama cha aina yake duniani, kwa kuwa kila upande kuna fursa ya ushauri kutoka kwa wazee wastaafu (huku akiwataja kwa majina), jambo linalofanya kazi iliyo mbele yake kuwa nyepesi.

Rushwa
Akizungumzia kuhusu utendaji wa chama na upitiaji wa muundo wa chama, Magufuli alionya kuwa katika uongozi wake mwanachama atakayetumia fedha kuomba uongozi, hatapita.

Alikumbusha wakati wa kuomba udhamini ili ateuliwe kugombea urais kupitia CCM, kwamba alifika Iringa akakuta Wilaya moja wanachama wote wamenunuliwa, akalazimika kwenda vijiji vya mbali kupata wadhamini.

Magufuli alisema rushwa aliyosema iko ndani ya chama hicho, imekuwa ikiwanyima haki wanachama wengine kugombea na matokeo yake, vyeo vimekuwa vikishikwa na watu wenye fedha na kuacha watu muhimu kwa sababu hawana fedha.

Vyeo kufutwa
Aidha, aliahidi kuongeza maslahi ya wafanyakazi wa chama hicho lakini akaonya kuwa kuna baadhi ya vyeo ambavyo haoni kama vina tija katika siasa za sasa, ambavyo anafikiria kuviondoa.

Alitoa mfano wa makamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), walezi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), washauri wa Jumuiya ya Wazazi na chipukizi, ambao alisema wengi ni wa umri wa kuanzia miaka nane mpaka 15, ambao wanapaswa kuwa shuleni.

Mwenyekiti huyo pia alisisitiza umuhimu wa mwanachama mmoja cheo kimoja na kuonya kuwa hapendi kuona mawaziri, ndio wajumbe wa NEC, ndio makamanda wa vijana na kusema hali hiyo inawanyima cheo wanachama wengine.

Mali za chama 
Kuhusu mali za chama hicho, aliagiza sekretari hiyo nayo kuzifuatilia, kuziorodhesha na kuhakiki mali ipi inaingiza mapato yapi na yanakwenda wapi. 

Kuhusu ada za wanachama wanaozidi milioni 8.7, ambao Mwenyekiti mstaafu, Jakaya Kikwete alisema kama kila mmoja angelipa ada ya Sh 1,200 kwa mwaka, chama hicho kingepata zaidi ya Sh bilioni nane na kuondokana na ukata wa kutegemea ruzuku, Magufuli aliagiza uhamasishaji wa kulipia ada ufanywe na malipo yawe kwa njia ya kielektroniki.

Kinana 
Akizungumza baada ya kurejeshwa madarakani, Kinana alisema baada ya kuandika barua hiyo ya kujiuzulu na hata kuzungumza na Magufuli, amejikuta akigonga mwamba na hivyo anajipanga kuomba tena kupumzika.

Alisema alipokuwa akifanya kazi, kuna wakati alidhani yuko mwenyewe lakini Mwenyekiti Kikwete, alimpigia simu na kumwambia kuwa anamuunga mkono, jambo lililomtia moyo.

Lowassa na Sumaye Wapewa MAKAVU Ndani ya Mkutano wa CCM .........Mpendazoe Ahamia CCM, Mrema Alalama Kuitwa CCM B

$
0
0

VIGOGO mashuhuri wa Chadema waliowahi kuwa mawaziri wakuu; Edward Lowassa na Frederick Sumaye, jana waligeuka gumzo ndani ya Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kumchagua Rais John Magufuli, kuwa Mwenyekiti wa tano wa chama hicho.

Gumzo hilo, lilianzishwa na Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba, alimpomtaka Askofu wa Kanisa la Ufufuko na Uzima, Josephat Gwajima, asimpotoshe Magufuli ili yasije yakampata ya Sumaye, ambaye sasa anachezea mchangani Kibaha.

Sumaye mchangani
“Hata akina Sumaye hawakuunda vyama vyao. Bado wanahangaika; na sasa Sumaye anacheza mchangani Kibaha,” alisema Makamba.

Sumaye ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu na NEC ya CCM, kwa sasa anawania uongozi wa Kanda ya Pwani katika Chadema. Kabla ya kusema kuwa Sumaye anahangaika na siasa za mchangani, Makamba alimtaka Gwajima kuacha uongo na kusingizia viongozi wa CCM.

Makamba aliyepewa nafasi ya kumuombea kura Rais John Magufuli kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, alisema anamtia moyo Magufuli asiogope kuongoza chama, kwani hataongoza peke yake bali wapo wanachama wengi watakaomsaidia kazi hiyo.

“Wewe siyo wa kwanza kukataa kazi hii. Hata watangulizi wako Kikwete na Benjamin Mkapa nao walifanya hivyo hivyo,“ alisema Makamba ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

Makamba alisema hata manabii na mitume wengi, kama Haruni, Mussa, Yona au Yunus na Yeremia walifanya vivyo hivyo, walipopewa utume au unabii na Mungu, kwani waliogopa kufanya kazi hizo lakini, alisema mara zote Mungu aliwaagiza kuwa wasiogope kuwa manabii na mitume, kwani atatia maneno kwenye vinywa vyao.

Aidha, Makamba alitaka viongozi wa dini mfano Askofu Gwajima, waache kumfitini Kikwete eti kwamba alikuwa hataki kumpa uenyekiti Magufuli.

“Askofu Gwajima alikuwa anasingizia kuwa Jakaya kiongozi wetu mpendwa hataki kukupa uenyekiti. Alikuwa akikuhimiza kuwa kama hataki uunde chama chako. Huu ni uongo. Gwajima amemaliza uongo wote,” alisema Makamba na kumuomba Magufuli asisikilize uongo wa kiongozi huyo wa kiroho.

Makamba alimtaka Askofu Gwajima atambue kuwa hata baadhi ya wana-CCM waliojiengua mwaka jana, hawakuunda vyama vyao badala yake wameangukia pua.

Aliwataka wajumbe wa mkutano huo, kumpa kura zote za ‘Ndiyo’ Rais Magufuli, kisha Makamba akaanza kutumia uhodari wake wa misemo, methali, mafumbo na aya za Biblia na Kurani Tukufu.

“Mzigo wa chama ulikuwa umebebwa na Mkwere Kikwete ambaye sasa anaondoka; na kwa kuwa kuna msemo kuwa ‘mzigo mzito mpe Mnyamwezi au Msukuma, nawaomba wajumbe wote sasa mzigo wa chama tumpe Msukuma Magufuli,” alisema na kauli yake hiyo ilishangiliwa na wajumbe.

Lowassa na ufisadi
Akielezea aina ya kiongozi anayetoka CCM na anayeingia, Makamba alisema kuwa anayetoka, Kikwete ni mpiganaji wa ufisadi, kwa kuwa alifikia hatua ya kumtosa rafiki yake Edward Lowassa, kuwa hafai kuwa Rais kwa kuwa anatuhumiwa kwa ufisadi.

Alisema kada wa chama hicho anayeingia baada ya Kikwete, Dk Magufuli yeye ndiye muasisi wa Mahakama ya Mafisadi, ambayo tayari imeshaanzishwa kwa Sheria ya Bunge. Kwa mujibu wa Makamba, Kikwete ni kiongozi aliyepiga vita umasikini na anapoondoka, anayeingia Dk Magufuli msimamo wake ni asiyefanya kazi na asile.

Kumchinja Kobe
Naye mmoja wa vigogo wa Chadema aliyerejea CCM, Fred Mpendazoe, alikuja na dhana ya namna ya kumchinja kobe, akifananisha na utaratibu uliotumika, kukata jina la Lowassa katika majina 38 ya wagombea urais.

Mpendazoe alisema Kikwete alifanya ‘timing’ sana kushughulikia ufisadi ndani ya chama hicho, kwa kuwa kati ya makada hao 38 waliokuwa wakiwania urais, baadhi akiwemo Lowassa walikuwa na tuhuma za ufisadi na kukatwa kwa majina yao, kulifanyika kwa wakati sahihi.

Kuachana na nzi
Mpendazoe pia alisema Wasambaa walimfundisha msemo mmoja kwamba, mtu akitaka asifuatwe na nzi, anatakiwa atupe mzoga na kuongeza kuwa, hatua ya wagombea wenye tuhuma za rushwa kutupwa, CCM ilitupa kibudu.

Kwa mujibu wa Mpendazoe, kuhamia Chadema kwa Lowassa, kulisababisha chama hicho na Ukawa waliomuunga mkono, kupoteza ajenda, kwa kuwa walimpokea mtu waliyezunguka nchi nzima wakimtuhumu kwa ufisadi tena wakisema wanao ushahidi.

“Walipompokea Lowassa, nikasema basi mchezo umekwisha wamepoteza ajenda,” alisema Mpendazoe huku akishangaa kitendo cha Ukawa kudai demokrasia imekuwa ikibanwa.

Gia angani
Mpendazoe alisema anashangaa kusikia Magufuli anabana demokrasia na kuhoji kati ya chama kilichotangaza nafasi ya urais na kuruhusu wagombea 38 kugombea, huku mchujo ukifanyika hadharani na kilichompata mgombea kwenye chopa (helikopta), ni kipi chenye demokrasia?

Akifafanua zaidi, Mpendazoe alisema Chadema ilimpata mgombea wake angani ndani ya helikopta, na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe alipokwenda katika vikao, akasema chama hicho kimebadilisha gia angani.

“Nilihoji iweje uamuzi huo ufanyike bila vikao,” alisema na kuongeza kuwa kilichofanyika kilikuwa sawa na biashara na kuhoji kwa nini chama hicho kisisajiliwe Brela (Ofisi ya Msajili wa Makampuni) ili kufanya biashara.

CCM B
Naye Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alihoji yeye kuitwa CCM B, baada ya Rais Magufuli kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole na kusema inakuwaje yeye aliyetoka katika chama hicho mwaka 1995, apewe jina hilo.

Alisema kama kupewa cheo na Magufuli, ndio sababu ya kuitwa CCM B, basi hata Mbunge wa Vunjo, James Mbatia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, ni CCM B kwa kuwa aliteuliwa kuwa Mbunge na Rais Jakaya Kikwete.

Mrema alisema kama kuitwa kwake CCM B ni kutokana na kutoka ndani ya CCM; basi Lowassa na Sumaye ni CCM A, kwa kuwa wao wametoka mwaka jana wakati yeye ametoka tangu 1995.

Haeleweki
Naye Magufuli alisema alimshangaa Rais mstaafu Benjamini Mkapa, kwa kumteua mtu mmoja kuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 mfululizo, wakati waliofanyakazi na Waziri Mkuu huyo, akiwamo yeye waliona kuwa ni mtu asiyeeleweka. Waziri Mkuu wa Mkapa, alikuwa Frederick Sumaye.

Kauli hiyo ya Magufuli, ilitanguliwa na ya Kikwete, ambaye alishangaa kuona mtu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, sasa anagombea uenyekiti wa Kanda.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images