Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Afungua Duka la MSD Ruangwa, Kuhudumia Hospital 524

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefungua duka la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika Hospitali ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia hospitali 524 katika mikoa ya Lindi, Mtwara na wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Akizindua duka hilo leo (Jumamosi, Julai 16, 2016) Waziri Mkuu amesema duka hilo litaendelea kuboresha huduma za upatikanaji wa dawa kwa gharama nafuu  katika hospitali, vituo vya afya na zahanati katika wilaya ya Ruangwa pamoja na mikoa na wilaya za jirani.

Duka hilo ni la sita kufunguliwa tangu Mhe. Rais Dk. John Magufuli alipotoa agizo kwa MSD kufungua duka la dawa ndani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo mengine yako katika mikoa ya Mwanza (Sekou Toure), Arusha (Mount Meru), Mbeya (karibu na hospitali ya mkoa) na Geita (hospitali ya wilaya ya Chato).

“Duka hili litasaidia kufikiwa kwa malengo ya Serikali ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wakati na kwa gharama nafuu, hivyo nawaomba mlitumie duka hili,” amesema.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa benki ya NMB, kikosi cha SUMA JKT na MSD kwa kufanikisha ujenzi wa duka hilo ambalo litaimarisha upatikanaji wa dawa kwa uharaka.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema kuanzishwa kwa duka hilo kutaongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa gharama nafuu , hivyo kuondoa usumbufu kwa wagonjwa  wa kwenda kuzitafuta katika ya mbali na kwa bei kubwa.

“Nitoe mfano wa tofauti wa bei za dawa kati ya maduka yetu na mengine, dawa ya sindano ya diclofenac tunauza sh. 250 huku mitaani ni sh. 1,000 hadi 1,500 , ampliclox dozi moja MSD sh. 1,500 mtaani sh. 3,500 na Ciprofloxacin MSD sh. 100 na mtaani sh. 500 hadi 1,000,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema lengo la maduka hayo si kuuza dawa reja reja, nia yao ni kuziuzia hospitali, vituo vya afya na Zahanati ili wagonjwa wanapokwenda huko kupatiwa huduma wasikose dawa kwa wakati.

Akizungumzia kuhusu gharama za ujenzi wa duka hilo Bwanakunu mesema umegharimu sh.milioni 59 ambapo kati yake MSD imetoa sh. milioni 29 na benki ya NMB imetoa sh. milioni 30.

“Mbali na gharama za ujenzi MSD tumenunua na kufunga vifaa vya TEHAMA kwa sh milioni 17 na mtaji wa dawa wa sh. milioni 37, ambapo imetenga sh. milioni 100 kwa ajili ya dawa za duka hilo.

Amesema duka hili litaendeshwa na kusimamiwa na MSD kwa muda wa mwaka mmoja na kisha wataikabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa ajili ya kuliendeleza ambapo litaisaidia katika kuiongezea mapato.

Breaking News: Matokeo Ya Kidato Cha Sita(ACSEE) Na Ualimu (DSEE Na GATCE) 2016 Yametangazwa.....Bofya hapa Kuyaangalia

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya July 17

Tume ya vyuo vikuu(TCU) yatoa ufafanuzi kuhusu alama za kudahiliwa vyuoni

$
0
0
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza utaratibu mpya kwa watahiniwa wa mwaka mpya wa masomo wa 2016/2017 wanaochukua shahada, huku wanafunzi wengi wakiwa hatarini kukosa nafasi kwa kukosa sifa na vigezo.

Utaratibu huo mpya umekuja ikiwa ni miezi miwili sasa tangu kutumbuliwa kwa watendaji wa tume hiyo kutokana na kudahili wanafunzi wasio na sifa na kusababisha kupewa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Sifa hizo ziliwekwa mapema wiki hii katika tovuti ya TCU na kurudiwa jana. Taarifa hiyo inaonyesha kutolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Eliuta Mwageni.

Akizungumza na  mwandishi wetu kwa njia ya simu jana, Ofisa Habari Mwandamizi wa TCU, Edward Mkaku, alithibitisha taarifa ya utaratibu huo mpya.

Mkaku alisema utaratibu huo umetolewa baada ya mwaka jana kutumika mfumo wa wastani wa pointi (GPA) ambao Januari, mwaka huu, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, aliagiza ufutwe na kurudishwa ule wa madaraja (division) uliotumika siku zote.

“Mfumo wa udahili uliotumika mwaka jana ulikuwa ni GPA na mwaka huu utatumika mfumo wa divisheni, ndiyo maana utaratibu huo ukawekwa,” alisema Mkaku.

Moja ya sifa zinazotakiwa katika udahili wa mwaka huu wa masomo (2016/2017), ni wahitimu wa kidato cha sita waliomaliza kabla ya mwaka 2014 kuwa na ufaulu wa (D mbili) pointi 4.0.

Mchanganuo ulionyesha kuwa pointi hizo zinatokana na ufaulu wa A = 5; B= 4; C= 3; D = 2; E = 1.

Taarifa hiyo ilionyesha kuwa ili wahitimu wa kidato cha sita kwa mwaka 2014 na 2015 wawe na sifa za kudahiliwa, watatakiwa kuwa na alama za ufaulu wa (C mbili ) pointi 4.0 kupitia mchanganuo wa A = 5; B+ = 4; B = 3; C= 2; D = 1.

Pia tovuti hiyo ilionyesha kuwa wahitimu waliomaliza kidato cha sita kwa mwaka huu, watahitajika kuwa na ufaulu wa alama (D mbili) 4.0 kupitia mchanganuo wa A = 5; B = 4; C= 3; D= 2; E = 1.

Mbali na sifa hizo, watakaodahiliwa ni wale ambao pia watakuwa  na utambulisho wa sifa za kielimu za kidato cha nne ambazo ni kuanzia alama nne za D na kupanda juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B+, ikiwa A =75-100, B+ = 65-74, B=50-64, C=40-49, D=35-39, F= 0-38.

Sifa nyingine zinazotakiwa ni wenye cheti cha NVA daraja la tatu pamoja na ufaulu wa si chini ya alama nne za D za kidato cha nne au sifa nyingine zinazokaribiana na hizo, ikiwa ni pamoja na zinazotambuliwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) au Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Pia watahiniwa hao watatakiwa kuwa na angalau GPA ya 3.5 kwa stashahada (NTA) daraja la sita au wastani wa B kwa cheti cha ufundi (FTC) katika mchanganuo wa alama A=5, B=4, C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+ kwa wenye stashahada za ualimu, au wastani wa daraja la B+ kwa kitengo cha afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyingine au cheti na stashahada nyinginezo.

Sifa nyingine zinazoangaliwa katika udahili huo ni kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye stashahada zisizokuwa za NTA.

Pamoja na hayo, TCU ilisema hakutakuwa na usajili wa mafunzo ya awali pamoja na yale ya UQF6 yaliyozuiwa kuanzia mwaka wa masomo wa 2016/2017.

Taarifa ya tovuti hiyo iliendelea kusema kuwa maombi yote ya usajili wa wanafunzi hao wanaotaka kuchukua shahada yanatakiwa kupitia TCU pekee.

“Kwamba tume hiyo imeamua kuwa kuanzia mwaka 2016/2017, maombi yote ya usajili kwa makundi yote yanayoanzia aya ya 3.0 kwenda juu wataunganishwa na TCU pekee na walio chini ya hapo hawatahusika na tume hiyo,” ilisema taarifa hiyo.

Pia TCU ilisema taarifa hiyo ni kwa mujibu wa kipengele cha 5(1)(c)(i) cha katiba ya vyuo vikuu, kifungu cha 346 cha sheria nchini.

“Msingi wa kubadili viwango vya kujiunga na elimu ya juu ni kutokana na kuwepo maoni kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya uwezo wa wahitimu wanaojiunga na vyuo vikuu mbalimbali,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Mei, mwaka huu, Profesa Ndalichako aliwasimamisha kazi Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya, kwa kushindwa kuisimamia tume hiyo kutokana na kuwapo kwa wanafunzi wasiokuwa na sifa, kisha wakadahiliwa katika vyuo vikuu na kupata mkopo.

Wengine aliowasimamisha kazi ni Mkurugenzi wa Ithibati na Udhibiti Ubora, Dk. Savinus Maronga, Mkurugenzi wa Udahili na Nyaraka, Rose Kiishweko na Ofi sa Msimamizi Mkuu wa Taarifa, Kimboka Stambuli.

Pia Mei mwaka huu, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Idrisa Kikula, alitangaza kuwasimamisha masomo zaidi ya wanafunzi 7,000 wa kozi maalumu ya stashahada ya ualimu ambao hawakuwa na sifa.

Alipozungumzia sakata hilo Juni, mwaka huu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais Dk. John Magufuli, aliwaita wanafunzi hao kuwa ni vilaza, na kwamba idadi kubwa ya waliofukuzwa hawakuwa na sifa stahiki za  kudahiliwa kusoma kozi hiyo.

Sauti: Augustino Mrema azungumzia hatua ya Rais kumteua na hatma yake ndani ya TLP

$
0
0
Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party, Augustino Lyatonga Marema amezungumzia hatua ya Rais Magufuli kumteua kuwa Mwenyekiti wa Parole Taifa na kuwa ni ipi hatma yake ndani ya TLP.

Kumsikiliza Mrema akiongea, bonyeza hapo chini

Kapteni wa JWTZ Apanda Kortini Kwa Kutishia Kuua

$
0
0
KAPTENI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), Henrick Mahenge (34) mkazi wa Mliman City, Dar es Salaam, juzi alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashitaka ya kujaribu kumuua askari wa usalama barabarani.

Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan, Wakili wa Serikali, Grace Mwanga alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai 12, mwaka huu maeneo ya Mnazi Mmoja wilayani Ilala. Mwanga alidai kuwa mshitakiwa alijaribu kumuua askari wa usalama barabarani WP 5177 Clesensia Makanyaga.

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo.

Hata hivyo, Mwanga alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kwamba hali ya mgonjwa haijulikani hivyo aliomba mahakama izuie dhamana hadi watakapopata uhakika kuhusu hali ya mgonjwa.

Mshitakiwa alipopewa nafasi ya kuelezea kilichotokea, alidai hakutishia kuua na kwamba yeye ndiye alifanyiwa fujo na kuchaniwa nguo zake na kwamba alimuona mshitakiwa baada ya tukio na kwamba hakupata taarifa kuwa mlalamikaji yupo hospitali.

Hakimu Hassan alisema kuwa dhamana ipo wazi kwa wadhamini wawili kutoka taasisi zinazotambulika na kuwataka wakaguliwe kwanza kujiridhisha.

Alisema pia mshitakiwa arudishwa rumande hadi Julai 19 mwaka huu watakapojiridhisha na wadhamini pamoja na kujua hali ya mlalamikaji.

Bavicha wabadili mbinu.....Tarehe 20 Kutua Tena Dodoma

$
0
0
BARAZA la Vijana wa Chadema (Bavicha) limepanga kufanya mkutano wa Kamati ya Utendaji ya baraza hilo Julai 20, mwaka huu mkoani Dodoma ambao utatoa mwelekeo wa kupigania demokrasia.

Aidha, limewataka vijana wa chama hicho nchi nzima kuwa watulivu na kutii agizo la Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe wakati wakisubiri maamuzi ya kikao hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrobas Katambi alisema, baraza hilo linaona kama jeshi la polisi halitendi haki kwa kuruhusu mkutano wa CCM, jambo alilosema ni ukandamizaji wa demokrasia.

“Kikao chetu cha Kamati ya Utendaji tulikuwa tumekiahirisha baada ya polisi kuzuia, lakini sasa tunafanya tena kwa tarehe ileile ambayo ni Julai 20 mjini Dodoma ambapo tulipanga kufanya mwanzo,” alisema.

Aidha, Katambi alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu hana budi kujiuzulu iwapo mkutano huo wa CCM utafanyika kwa kuwa atakuwa ameshindwa kusimamia kauli ya jeshi hilo lakini pia ya Rais John Magufuli.

Alisema baada ya Mbowe kuwazuia wasiende Dodoma wameamua kuja na mpango wa pili ambapo hawatakwenda Dodoma lakini hawataruhusu mkutano wa CCM ufanyike hadi serikali itakapotoa kauli ya haki sawa za kidemokrasia kwa kila chama.

Katibu Mkuu wa baraza hilo, Julius Mwita alisema, hawaoni kama kufanyika kwa mkutano wa kamati ya utendaji kutaathiri kwa namna yoyote usalama wa wanachama au mkutano wa CCM.

Alisema tayari hata IGP anajua kuwa watafanya mkutano wao mjini Dodoma lakini watampa taarifa ukumbi utakaofanyika mkutano huo baada ya kuupata na kukubaliana na mwenye ukumbi.

Majaliwa: Uamuzi wa Serikali wa kufuta tozo tano katika zao la korosho uko pale pale.

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Serikali wa kufuta tozo tano kati ya tisa alizokuwa anakatwa mkulima wa zao la korosho uko pale pale na unatarajiwa kuanza kutumika katika msimu mwaka huu hivyo ameitaka Bodi ya Korosho kusimamia uamuzi huo.

“Watendaji wa Serikali katika ngazi mbalimbali mnatakiwa kuhakikisha kwamba maelekezo haya yanafuatwa. Malengo yetu ni kumpunguzia mkulima mzigo wa tozo nyingi alizokuwa anakatwa,” alisema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Julai 16, 2016) wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya mkoa Mtwara pamoja na taarifa ya kuondolewa kwa baadhi ya tozo katika zao la korosho zilizowasilishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego.

Alisema Serikali iliamua kuzifuta tozo hizo baada ya kubainika kuwa zilikuwa zikiwanyonya wakulima hali iliyosababisha wauchukie mfumo wa stakabadhi ghalani.

“Kuanzia mwaka huu Serikali imeamua mfanyabiashara yeyote wa korosho hana budi kuanza kulipa malipo ya awali kabla ya kuingia kwenye mnada ili tuwe na uhakika wa kununua korosho hizo na kuwalipa wakulima kwa wakati,” alisema.

Akizungumzia kuhusu changamoto ya kushuka kwa uzalishaji wa korosho Waziri Mkuu aliutaka mfuko wa wakfu wa kuendeleza zao hilo ufanye utafiti wa kubaini sababu ili waweze kutafuta namna ya kuipatia ufumbuzi.

“Nitakuja kukutana na viongozi wa mfuko waniambie wanafanya nini na wamefanya nini miaka mitatu iliyopita na wana mpango gani huko mbele tunakokwenda kama hakuna mpango tutauangalia mara mbili mbili kwani wana fedha nyingi lakini hata mbegu hawapeleki kwa wakulima,” alisema.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliitaka Bodi ya Korosho kuhakikisha kila msimu wakulima wanapata pembejeo bora na zinawafikia kwa wakati ili waweze kupata mazao ya kutosha.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 17, 2016

Mtoto aliyewekewa ‘mashine’ kwenye moyo aanza mazoezi

$
0
0
Mtoto Happiness John Mkazi wa Seliani Arusha aliyefanyiwa upasuaji kwenye moyo na kupandikiziwa kifaa cha kusaidia kudhibiti mapigo ya moyo (pacemaker), ameanza mazoezi. 

Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto, Sulender Kuboja aliyeshiriki upasuaji huyo alisema jana kuwa hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri na wameanza kumfanyia mazoezi mepesi. 

Dk Kuboja alisema kwa kawaida mgonjwa yeyote aliyefanyiwa upasuaji anapaswa kufanyiwa mazoezi mepesi na kwamba kwa mtoto, mazoezi anayofanyiwa ni ya kukaa, kusimama na kutembea kidogo. 

“Hali yake inaonekana kuendelea vizuri sana... nimetoka kumfanyia vipimo muda mfupi uliopita kifaa kile kinafanya kazi vizuri na maendeleo yake yanaridhisha sana,” alisema Dk Kuboja. 

Alisema mtoto huyo anaweza kuongea na hata kula chaku- la, hali aliyosema inaonyesha nafuu nzuri kwake. 

Mama mzazi wa mtoto huyo, Elitruda Malley alisema anaridhishwa na maendeleo ya afya ya mwanaye kwa kuwa tangu afanyiwe upasuaji huo juzi, hali yake imeonekana kuimarika kwa haraka. 

Mama huyo alisema tangu awekewe kifaa hicho, mwanaye amekuwa mchangamfu, hali aliyosema inamtia moyo na kumpa matumaini makubwa. 

“Ingawa yupo kwenye oxygen, lakini namshukuru Mungu kwani anaonekana anapata nafuu nzuri, anatabasamu na kuongea vizuri kabisa na ana furaha sana, shauku yake ni apone ili aende shule kama watoto wengine,” alisema Malley. 

 Aliongeza kuwa mtoto huyo amekuwa akila vizuri na kumpa moyo kwani mwili wake unaonekana kuwa na nguvu na afya nzuri. 

Madaktari wapo karibu wakifuatilia afya ya mtoto kwa ukaribu, wanampa chakula, wanamfanyia mazoezi ya kukaa na kushuka chini, anaonekana kuwa na nguvu na mwenye maendeleo mazuri. "

Alisema jambo linalompa faraja ni kuona jinsi madaktari wote wanaomuhudumia mtoto huyo wanavyofanya kazi hiyo kwa upendo na bidii. 

Juzi, kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ilifanikiwa kumpandikiza mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitano kifaa cha kusaidia kudhibiti mapigo ya moyo (pacemaker) kinachoendeshwa kwa betri. 

Hayo ni mafanikio ya pili kwa taasisi hiyo ya kisasa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati baada ya Mei 24 na 25, mwaka huu kufanikisha operesheni kwa wagonjwa 18 bila kuusimamisha moyo.

Taarifa: Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).
 
Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Nyamajeje Calleb Weggoro ambaye muda wake umemalizika.
 
Uteuzi huu umeanza tarehe 16 Julai, 2016.
Kwa mujibu wa sheria ya Mamlaka ya usafiri wa anga ya mwaka 1977 Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mwenyekiti akitoka Tanzania Bara, Makamu Mwenyekiti hutoka Tanzania Zanzibar na kinyume chake.
 
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kedmon Andrew Mnubi kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).
 
SACP Kedmon Andrew Mnubi pamoja na makamishna wengine 59 ambao Rais Magufuli amewapandisha vyeo kuanzia tarehe 16 Julai, 2016 watakula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kesho jumatatu tarehe 18 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam saa tatu asubuhi.
 
Rais Magufuli atakuwepo wakati Makamishna wote 60 wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi ambalo litaendeshwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
 
Wote wakaohudhuria tukio hili wanatakiwa kufika Ikulu kabla ya saa mbili na nusu asubuhi na wataingia kupitia lango kuu la mashariki (lango la baharini).
 
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
17 Julai, 2016

Taarifa kamili kuhusu habari ya Rais Magufuli kumteua Jerry Murro kuwa msaidizi wa mawasiliano ya Rais Ikulu

$
0
0

Baada ya taarifa kuenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Rais John Pombe Magufuli amemteua Jerry Murro ambaye alikuwa afisa habari wa Yanga kuwa msaidizi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, kurugenzi ya mawasiliano imekanusha habari hizo na kusema kuwa sio za kweli.

Barua iliyoandikwa kutoka Ikulu imesema ‘kuna taarifa zimesambazwa zikisema kuwa Rais Magufuli amemthibitisha Gerson Msigwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu huku msaidizi wake akiwa ni aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga Jerry Murro, taarifa hizo sio za kweli na wananchi wazipuuze'

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya July 18

Waziri Mkuu Apiga Marufuku wanafunzi kutumia viberit na mishumaa mabwenini

$
0
0
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku matumizi ya viberiti, mishumaa na hita za kuchemshia maji kwa wanafunzi wa bweni ili kuepusha majanga ya moto na atakayekutwa, atachukuliwa hatua kali.

“Kuna tabia ya baadhi ya wanafunzi hasa wa masomo ya fizikia kutengeneza vifaa vya kienyeji vya kuchemsha maji mabwenini, jambo hili ni la hatari kwani linaweza kusababisha ajali ya moto, hivyo ni marukufu kwa mwanafunzi kutumia vifaa hivyo,” alisema.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari Lindi, yaliyoungua moto usiku wa kuamkia Julai 10, mwaka huu.

Katika ajali hiyo shule imeathirika kwa asilimia 34 baada ya vyumba tisa vya madarasa, jengo lenye matundu 26 ya vyoo na jengo la maabara ya kemia na fizikia yameungua na kusababishia hasara ya Sh milioni 682.78.

Waziri Mkuu alisema kwa namna ambavyo majengo hayo yameungua, ni vema yakavunjwa na kujengwa upya. Aliwataka kutumia nafasi hiyo kujenga jengo la ghorofa ili kutumia eneo dogo kwa kujenga madarasa mengi.

Pia alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi kuhakikisha fedha zitakazopatikana katika harambee hiyo, zinatumika kama ilivyokusudiwa.

Harambee ilihudhuriwa na mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego na wadau wa maendeleo na wanafunzi waliosoma shule hiyo akiwemo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amezitaka taasisi mbalimbali nchini kufunga vifaa vya kuzimia moto katika majengo yao kwa ajili ya kuvitumia pindi ajali za moto zinapotokea.

Kikwete Akubali Ombi La Mheshimiwa Rais Fikipe Nyusi Wa Msumbiji Kushiriki Mazungumzo Ya Amani Nchini Humo

$
0
0
Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi.

Ujumbe huo uliwasilishwa jana jijini Dar es Salaam na Mjumbe Maalum wa Rais Nyusi Meja Jenerali Mstaafu Mariano de Araujo Matsinhe ambaye aliongozana na Mshauri wa Diplomasia wa Rais Nyusi Kanali Manuel Mazuze, Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mheshimiwa Monica Patricip Clemente Mussa na Afisa wa Ubalozi wa Msumbiji nchini Rachide Usualle.

Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na  ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi

Maalim Seif Kitanzini.....Jeshi la Polisi Lasema Litamkamata na Kumshitaki kwa Uchochezi Zanzibar

$
0
0
MKUU wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu amefunguka kuhusu mambo juu ya utendaji wa jeshi hilo na kueleza kuwa wakati wowote litamburuza mahakamani Katibu Mkuu wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad kwa kuhamasisha uchochezi visiwani Zanzibar.

Amebainisha kuwa jeshi hilo, kamwe halikandamizi wala kuonea chama chochote cha siasa, kwani limekuwa likitekeleza wajibu wake kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo.

Akizungumza katika mahojiano yaliyofanyika kwenye kipindi cha Funguka, kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Azam jana, IGP Mangu alisema hali ya siasa Zanzibar ilikuwa shwari katika chaguzi zote mbili na kwamba machafuko na vurugu vilianza kutokea baada ya uchaguzi wa pili.

Alisema vurugu hizo zilianza baada ya kubainika kuwa Maalim Seif, alikuwa akifanya mikutano ya ndani na mingine ya chini kwa chini na wafuasi wake katika maeneo ya Kaskazini na Kusini.

“Kwa sababu ilikuwa ni mikutano ya ndani, Polisi hatukuona tatizo na wala hatukumzuia, tuliona ni mwananchi anataka kuzungumza na wafuasi wake, tukasema mwache aongee nao tu,” alisema IGP Mangu.

Alisema baadaye jeshi hilo liligundua kuwa kiongozi huyo wa CUF, alikuwa anawachochea wananchi waichukie serikali iliyopo madarakani na wapinzani wao ambao ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwafanyia uhalifu.

Alisema baada ya vikao hivyo vya Maalim Seif, visiwani humo kukaanza kuibuka matukio ya vurugu kama vile mashamba kuchomwa moto na mazao kung’olewa.

“Haya mambo hayakutokea kabla ya vikao vya Seif, yalitokea baada ya vikao vyake,” alifafanua mkuu wa polisi.

Alisema wafuasi hao walichochewa, kiasi cha kususa hadi shughuli za kijamii, kama vile misiba na wakati mwingine ilifikia hatua ya kususa kuwauzia bidhaa wafuasi wa CCM.

“Tukasema kama wameona kugeuza biashara zao siasa, basi waendelee tu. Biashara inadumu kwa sababu unatengeneza faida, sasa kama umeamua kuchagua wa kumuuzia ni shauri yako. Hawa tuliwaacha kwa sababu tuliona hawana makosa,” alisema.

Hata hivyo, alisema jeshi hilo kamwe halikuwanyamazia wahalifu waliochoma na kung’oa mazao kwenye mashamba ya wenzao, eti tu kwa kigezo cha ufuasi wa chama au siasa.

“Hawa tuliwakamata na wapo wengine tunaendelea kuwatafuta, watakapoacha ndio hatutawatafuta. Wale wahalifu ndio tunaowatafuta. Pengine kwa sababu ya siasa wanadhani Polisi tunawaonea wananchi tunawakamata bila sababu. Sasa hawa watu tunawaoneaje wakati tunawapeleka mahakamani?” Alihoji.

Maalim Seif kuhojiwa 
Alisema kutokana na matukio hayo, tayari Maalim Seif amehojiwa na jalada lake halijaamuliwa, lipo kwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) Zanzibar. “Lakini pia tunataka tumpeleke mahakamani kumshitaki kwa makosa aliyofanya ya kuchochea fujo,” alieleza.

Alisema kazi kubwa ya Polisi kwa sasa si kujiingiza kwenye siasa au kupatanisha pande mbili zinapokwaruzana, bali kazi yake ni kuhakikisha inadhibiti na kuwakamata wahalifu.

Alisema endapo vyama viwili vinavyolumbana visiwani Zanzibar, vitaamua kuchukua hatua za kisheria kumaliza tofauti zao, polisi haina tatizo, lakini endapo vyama hivyo vitachukua hatua za kijinai au kukomoana, jeshi hilo halitokaa kimya.

“Kazi ya polisi iko wazi, tunakamata tunapeleleza na kupeleka mahakamani umma unatuona tunachofanya hatuna cha kuficha,” alisisitiza.

Maandamano na mikutano
Akizungumzia madai ya jeshi hilo kukandamiza demokrasia na wapinzani kwa kudhibiti shughuli za siasa nchini, IGP Mangu alisema hakuna mwanasiasa au chama chochote, kilichozuiwa kufanya shughuli zake, ikiwemo mikutano.

Alisema kinachotakiwa ni kwa mwanasiasa au chama hicho, kupeleka maombi yake Polisi kwa mujibu wa sheria na baada ya jeshi hilo kufanyia tathmini maombi hayo, endapo yataonekana hayana tatizo yataruhusiwa kuendelea.

Alisema endapo jeshi hilo linazuia shughuli za kisiasa, hutokana na uchunguzi au tathmini lililofanya na kujiridhisha kuwa shughuli husika si salama na inatishia usalama wa raia.

“Unajua unapozungumzia masuala hayo tuwe makini kidogo, kwa sababu hapa kuna watu wa aina mbili kuna wanaofanya siasa na sisi watendaji tunaotekeleza sheria. Ila sisi pia hatuko juu ya sheria, kama kuna mahali tunakiuka upo utaratibu wa kutushughulikia,” alisisitiza.

Alisema hata katika suala la kuzuia shughuli za kisiasa, kama vile mikutano na maandamano endapo, kuna chama au mwanasiasa anahisi kuwa jeshi hilo, halikutenda haki au limeenda nje ya mstari, taratibu zinamruhusu kukata rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais na Mahakama.

Hata hivyo, alisema jeshi hilo halifanyi jambo lolote nje utaratibu wa kisheria, akifafanua, “lakini sisi hatuwezi kujiingiza kwenye siasa kwa sababu sisi sio wanasiasa, pia hatuwezi kuzuia wanasiasa kulumbana kwa sababu ni uwanja wao wa kulumbana. Sasa kama tulitoa maelekezo fulani basi ujue tulikuwa tunatekeleza sheria na utaratibu uliopo.”

“Sidhani kama sisi tunakandamiza upinzani, tunachofanya sisi ni kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na watu wako huru kama wanafikiri tumeenda nje ya mipaka yetu wakatuchukulie hatua,” alisisitiza.

Alitoa mfano wa matukio yaliyozuiwa na Polisi kwa sababu za kiusalama kuwa ni pamoja na mkutano wa mahafali wa Dodoma, ambao ulifanyika siku moja na mkutano wa mahafali uliofanyika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam ambao wenyewe haukuzuiwa. Yote ilikuwa mikutano ya wanafunzi wafuasi wa Chadema.

“Kama sisi tuna sera ya kuzuia, mbona wa Karimjee hatukuuzuia? Dodoma kulikuwa na sababu na imeelezwa na viongozi wa Dodoma. Hii si sera yetu, usichukulie mkutano mmoja kuzuiwa basi ndio yote nchi nzima imezuiliwa. Haiwezekani,” alifafanua.

Alisema sheria inazungumzia wanaohitaji kufanya mkutano au kufanya maandamano, wanatoa taarifa kwa mkuu wa polisi wa hilo eneo, na mkuu huyo ataangalia kama mazingira yanaonesha hakuna tatizo, mkutano utaendelea, kama kuna tatizo atauzuia.

“Sasa ni wapi sisi tumefanya kitu ambacho ni kinyume na tunaonekana tunakandamiza upinzani? Na ikumbukwe kuwa kuna mikutano baadhi iliombwa tukaizuia kwa sababu kipindi hicho kulikuwa na kelele za mauaji Mwanza, Sengerema, Tanga mpaka tunahojiwa Polisi mko wapi,” alisema.

Alisema wakati Polisi ikihojiwa kuhusu dawa ya mauaji, baadhi ya vyama viliwasilisha maombi ya maandamano.

“Hivi kweli? Kwanza mauaji yenyewe mtindo wake ni mpya unajuaje kama wanaoomba wangeenda nao kuvamiwa? Lazima tuchukue tahadhari,” alisema na kuongeza kuwa Polisi imepewa jukumu la kisheria kuhakikisha panakuwepo na amani. 

“Sasa tunapochukua hatua kuhakikisha kuna amani, naomba tuvumiliane. Msione kuna amani, basi mkajua ipo tu na ni ya kudumu, mjue kuna wengine wameumia kuhakikisha hiyo amani inakuwepo. Lazima iwe hivyo ndio utaratibu wa kuongoza nchi, sisi hatubagui wala kukandamiza chama chochote,” alieleza IGP Mangu.

Matumizi ya nguvu
IGP Mangu alisema si kweli jeshi hilo limekuwa likitumia zaidi nguvu katika kudhibiti vurugu na kubainisha kuwa nguvu hutumika, pale tu inapobainika kuwa upande wa pili unaodhibitiwa nao unatumia nguvu.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa Polisi nchini imekuwa ikitekeleza wajibu wake vyema bila kukandamiza wala kutumia nguvu, kwani hata taasisi ya kimataifa iliyofanya tathmini juu ya utendaji wa jeshi hilo katika uchaguzi mkuu nchini ilibainisha kuwa jeshi hilo lilifanya vyema.

Polisi na rushwa 
Akizungumzia tuhuma zinazorushiwa Jeshi la Polisi kwamba kuna baadhi ya askari wake, wanatuhumiwa kwa rushwa, alisema askari hawana mamlaka ya kula rushwa na kujilimbikizia mali halafu wasiguswe na mtu.

“Hili haliwezekani. Kwa hiyo nasema bado wananchi wanaweza wakasaidia kama kweli wanazo taarifa za Polisi na zitafanyiwa kazi. Kama hawaamini kama sisi wenyewe hatuwezi kudhibitiana, vipo vyombo vingine vinaweza kufanya hivyo,” alisema.

Hata hivyo, alisema wapo askari Polisi wenye maisha mzuri kwa maana ya nyumba na magari, ambao wamepata mali hizo kupitia taasisi mbalimbali za mikopo ikiwemo Saccos ya Polisi, ambayo ndio kubwa nchini.

“Askari polisi kumiliki gari nzuri si kosa, la msingi amepataje hilo gari, kama kuna polisi ana mali au gari isiyo na maelezo tuleeteni, polisi hazuiliwi kuwa na gari nzuri. Siku hizi kuna taasisi nyingi zinakopesha anaweza kukopa,” alisisitiza.

Kashfa ya Lugumi
Akizungumzia suala la kashfa ya mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd inayomilikiwa na mfanyabiashara Said Lugumi, IGP Mangu alisema suala hilo lilichukuliwa na Bunge na kufanyiwa uchunguzi hivyo, matokeo ya uchunguzi hawezi kuyazungumzia.

Alisema anachoweza kukizungumzia ni maelekezo ambayo jeshi hilo limepatiwa na Bunge, ambayo ni kukamilisha yale ambayo hayajakamilishwa.

“Tunaendelea kuchukua hatua za kukamilisha.Kuhusu uchunguzi kazi ilifanywa na Bunge kwa anayetaka anaweza kuwasiliana na Bunge na kupatiwa matokeo kwa kuwa naamini Bunge linawakilisha wananchi, taarifa zao ziko wazi,” alisema.

Ajali ya Lori Yaua Watatu Dodoma Wakitoka Mnadani

$
0
0
WATU watatu wamekufa baada ya kufukiwa na mizigo wakati lori walilokuwa wamepanda kutoka Mnada wa Mgaga wilayani Bahi mkoani Dodoma, kupasuka tairi na kupinduka.

Ajali hiyo iliyotokea katika Kijiji cha Chifutuka saa 11 jioni juzi, pia ilisababisha majeruhi 19 ambao wamekimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Mayala Towo alilitaja lori lililohusika kuwa ni aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T 689 BEG.

Alisema lori hilo lilipofika eneo la Chifutuka wilayani Bahi, tairi lake la mbele lilichomoka na kupinduka.

“Gari hilo lilichomoka tairi ya mbele na kusababisha kupinduka kisha mizigo kuwaangukiwa watu waliokuwepo katika lori hilo ambapo watu watatu wamekufa na majeruhi 19 walipelekwa katika Hospitali ya Mkoa,” alisema Towo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Zainabu Chaula alisema juzi saa mbili usiku walipokea majeruhi 19 na maiti watatu.

Dk Chaula alitaja waliokufa kuwa ni Isdori Thomas Motto (38), Michael Msongela (29) na Elias Masimo Petro (51) wote wakazi wa Dodoma.

Daktari huyo alisema majeruhi 12 walitibiwa na kuruhusiwa huku wengine wakilazwa wodi namba 10, 8 na 11 kwa ajili ya uangalizi zaidi. 

Aliwataja waliolazwa kuwa ni Muoni Magege (40) mkazi wa Dar es Salaam, Suzy, Samweli (16), Frida Chipaga, Chausiku Mohammed (38), Josephine Sakiru (43), Selemani Salum (35) na Elias Petro (51) wote wakazi wa Dodoma.

Akisimulia ajali hiyo, mmoja wa majeruhi ambaye amelazwa katika Wodi Namba 8, Chausiku Mohammed mkazi wa Chinangali mjini Dodoma, alisema walipanda lori hilo lililokuwa likitoka mnadani na kwamba alichokiona ni kuchomoka kwa tairi la lori hilo, hivyo gari kupinduka na wao kufunikwa na mizigo iliyokuwepo katika lori hilo.

“Mimi nilienda mnadani kwa ajili ya kununua mazao, kama unavyojua malori ya minadani yanabeba kila kitu hadi mizigo sasa sisi kilichotuumiza ni mizigo kwani ilitulalia na mimi kama unavyoona nimeumia huu upande wote wa kulia na hapa katika mkono wangu,” alisema Chausiku.

Seleman Salum aliyelazwa Wodi Namba 11 mkazi wa Uwanja wa Ndege, alisema ajali hiyo ilisababishwa na kuchomoka kwa tairi la mbele na kupinduka. Alisema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11 jioni karibu na Kijiji cha Chifutuka wilayani Bahi.

UVCCM wawasaka BAVICHA Dodoma....Waandaa vijana 3000 Kuimarisha Ulinzi

$
0
0

Umoja wa Vijana CCM, wametua mjini Dodoma ambapo Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unatarajiwa kufanyika wiki hii huku wakiwatafuta wajumbe wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) ambao awali walipanga kuzuia kufanyika kwa mkutano huo.

Akiwa katika Ofisi za UVCCM – Dodoma jana, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu aliwaambia waandishi wa habari kuwa amefika mjini hapo pamoja na mambo mengine kusimamia ulinzi wa chama na viongozi wa chama hicho lakini hawaoni BAVICHA.

“Nipo hapa kwa muda mrefu kwa ajili ya kuongoza shughuli za ulinzi wa chama na viongozi wetu, kama Mtendaji Mkuu na mtoa maelezo ya itifaki. Kwa bahati mbaya kwa muda wote sijaona dalili wala harufu ya BAVICHA. Hii inadhihirisha kwamba kusema na kutenda ni vitu tofauti,” alisema Shaka.

Aliongeza kuwa wamejipanga vizuri na wameandaa vijana 3,000 maalum watakaofanya kazi ya kulinda mkutano huo uliolenga kufanikisha kumkabidhi Uenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kwa mujibu wa katika ya chama hicho tawala.

Aliwahakikishia usalama wajumbe wa Kamati Kuu akiwataka kuwa na amani kwani wataingia na kuondoka mjini humo wakiwa salama.

Juzi, BAVICHA walitangaza kurudi mjini Dododoma kwa lengo la kufanya Mkutano wao wa Kamati ya Kiutendaji baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuwataka kusitisha adhma ya kutaka kuzuia kufanyika kwa mkutano wa CCM.

Hatima ya Abdulrahman Kinana mikononi mwa Rais Magufuli..

$
0
0
HATIMA ya nani atakuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ipo mikonini mwa mwenyekiti mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli, ambaye sasa yupo mbioni kukabidhiwa mikoba ya chama hicho.

Nafasi hiyo kwa sasa inashikiliwa na Katibu Mkuu anayemaliza muda wake, Abdulrahman Kinana, ambaye ameshika nafasi hiyo tangu Novemba, 2012.

Jana Msemaji wa CCM, Christopher ole Sendeka, alisema hadi sasa maandalizi yanakwenda vizuri na tayari wajumbe wataanza kuwasili mjini Dodoma mapema wiki hii, kwa ajili ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Julai 23, mwaka huu.

“Suala la nani ni Katibu Mkuu litaamuliwa na mwenyekiti mpya Dk. John Magufuli, baada ya kukabidhiwa chama na Rais mstaafu Jakaya Kikwete. Tunataraji wajumbe 2,465 watahudhuria na hata wakipungua basi ni kidogo,” alisema

Msemaji huyo wa CCM alisema kuwa baada ya Julai 23, kutakuwa na kikao cha Halmashauri Kuu ambacho ndicho kitaamua juu ya mapendekezo ya mwenyekiti mpya kama anabadili sekretarieti au laa.

“Kwa sasa Katibu Mkuu bado ni Kinana hivyo sasa hapo ndipo kuna kitandawili ambacho kitateguliwa na mwenyewe Rais Magufuli kama ataendelea na aliyepo sasa au atakuja na mtu mwingine,” alisema Sendeka.

Alipoulizwa kuhusu kuibuka kwa kundi la watu wanaompinga Rais Magufuli, asipigiwe kura kwa ajili ya kukabidhiwa chama, alisema hakuna kitu kama hicho zaidi ya taarifa hizo kuenezwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Suala la kuwepo kwa watu kumpinga Rais Magufuli asikabidhiwe chama si geni, ingawa hadi sasa hatujaweza kumfahamu mwanachama yeote anayeendesha mpango huu.

“Mambo haya nahisi kuna kikundi cha watu kinajifurahisha katika mitandao ya kijamii hivi inawezakana vipi wajumbe walewale waliomchagua Magufuli awe mgombea wa CCM eti leo hii wageuke na kumpinga?

“… hili si kweli na si geni kama unakumbuka hata mwaka 2002 wakati mzee Benjamin Mkapa anawania uenyekiti kwa mara ya pili mambo kama haya yalijitokeza na wale waliokuwa wanatajwa walikanusha na haohao ndiyo wakawa mstari wa mbele kuhakikisha wanatafuta kura za kutosha,” alisema Sendeka.

Hata hivyo hadi sasa bado Kinana amekuwa akipewa nafasi ya kuendelea kuwa katibu mkuu ingawa mwenyewe amekuwa akitajwa na watu wake karibu kuwa anahitaji kupumzika.

Polisi wachimba mkwara
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, Mrakibu Mwandamizi wa jeshi hilo mkoani hapa Mayala Towo,  alisema polisi wamejipanga kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa kisima cha amani wakati wote na baada ya Mkutano Mkuu wa CCM.

“Amani itakuwepo wana Dodoma na Watanzania wasiwe na wasiwasi ukija na nia mbaya tutakachokufanya utawasimulia wenzako kwani kwetu amani ni wajibu wetu,” alisema Mayala.

Alitoa angalizo kwa wale watakaopokea na kuwaweka wageni katika nyumba zao ambao lengo lao ni kufanya  fujo kuwa jeshi hilo litawachukulia hatua kali za kisheria.

“Usiwe sehemu ya tatizo, kama unampokea mtu na kumweka kwako ili aje afanye vurugu wa kwanza kuchukuliwa  hatua utakuwa wewe mwenye nyumba,” alisema.

Askofu Gwajima Aibuka.......Azungumzia Sakata lake Kanisani, Msaidizi wake Akanusha Kanisa Hilo Kufungiwa

$
0
0
KIONGOZI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, amefunguka kwa kuelezea safari yake aliyoifanya nje ya nchi hivi karibuni, baada ya taarifa mbalimbali kudai kuwa alilikimbia Jeshi la Polisi.

Akiongoza ibada kanisani kwake, Ubungo, jijini Dar es Salaam jana, Askofu Gwajima alisema aliondoka nchini kwenda Japan Juni 15, mwaka huu, kwa ndege ya Emirates.

Akitoa mahubiri katika ibada jana, Gwajima alisema alifika mjini Osaka Juni 16 na kuanza mkutano wa kuhubiri injili na siku zilizofuata alikwenda katika miji mbalimbali.

Askofu Gwajima ambaye aliingia kanisani hapo saa 5:00 asubuhi na kuanza kuhubiri dakika 15 baadaye, asubuhi alitumia muda wa saa tatu hadi saa 8:20 kumaliza mahubiri yake.

Baada ya kuanza kuhubiri, alielezea safari hiyo kwa kutaja miji aliyekwenda ikiwamo Nagoya alikohubiri kwa siku mbili, Karuizawa, Ibaraki, Hiloshima na Yanakochi.

“Safari yangu ilikuwa ya mafanikio sana. Tulisafiri salama na kuzunguka miji mbalimbali na tulirudi Jumatatu ya wiki iliyopita,” alisema Askofu Gwajima.

Kadhalika, katika mahubiri hayo, Gwajima aliwakumbusha waumini wa kanisa hilo kuhusu kuhama kwa kanisa hilo, kwa kuwatajia siku ya mwisho ya kumalizia michango kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jipya kuwa ni Julai 30, bila ya kutaja sehemu ambayo kanisa hilo litahamia.

Hata hivyo, Askofu Gwajima wakati wote wa mahubiri, hakuzungumzia suala la kuhojiwa kwake na Jeshi la Polisi.

Wakati huo huo, mwandishi alizungumza na Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze, kuhusu tetesi za kufungiwa kwa kanisa hilo na kusema taarifa hizo si za kweli bali ni maneno ya mitaani.

“Hayo maneno si ya kweli. Si umeona ibada imeendelea kama kawaida na Askofu amehubiri? Maneno ya mtaani usiyalete kanisani,” alisema Bihagaze.

Julai 12, mwaka huu, Kikosi cha Polisi cha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) kilimkamata Askofu Gwajima wakati akitokea Japan kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya.

Baada ya kukamatwa, alipelekwa moja kwa moja Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuhojiwa, akidaiwa alitoa maneno ya uchochezi mwezi uliopita.

Jeshi la Polisi lilikuwa likimtafuta Askofu Gwajima baada ya kusambazwa mkanda kwenye mitandao ya kijamii unaodhaniwa una sauti yake.

Katika mkanda huo, Gwajima anapendekeza Rais mstaafu Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake, ambayo kwa sasa Rais Magufuli anayashughulika kwa staili ya utumbuaji majipu.

Pia Gwajima alisikika akimshauri Rais John Magufuli, kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) iwapo watakataa kumkabidhi uenyekiti na kwamba apeleke muswada bungeni, kuondoa kinga ili rais ashtakiwe kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani.

Tangu kusambaa kwa mkanda huo, Jeshi la Polisi lilikuwa likipiga kambi katika moja ya nyumba za Askofu Gwajima, iliyoko Mbezi Salasala jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kupiga kambi, jeshi hilo halikufanikiwa kumkamata na baadaye ilielezwa kuwa amekwenda nje ya nchi kuhubiri.

Jukwaa Huru la Wazalendo Lalaani Maamuzi ya Meya wa Dar es salaam

$
0
0

Siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kutoa agizo la msako wa nyumba hadi nyumba ili kuwabaini watu wasio na kazi maalum, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita aliibuka na kudai agizo hilo ni batili na haliwezi kutekelezeka kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Jukwaa Huru la Wazalendo kwa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia kwa Mwenyekiti wake Andrew Kadege wamelaani vikali kitendo kilichofanywa na Meya wa Dar es Salaam, Isaya Mwita kwa kufanya harakati za siasa badala ya zile za kuwaletea wananchi maendeleo huku akiwapotosha kwa makusudi wananchi na kuwataka kukaidi agizo la Makonda.
 
Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania limewataka wananchi wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kutoa ushirikiano mara zoezi la kuwatambua wakazi katika kaya litakapoanza rasmi ili kupata takwimu sahihi kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla hususan katika kipindi hiki ambapo serikali inataka kuanza ugawaji wa Sh. Milioni 50 kusaidia maendeleo ya kaya.

Hata hivyo jukwaa limemtaka meya kutokuendelea na tabia ya kuwalaghai wanainchi kutoshiriki katika shughuli za maendeleo kwani ndio sehemu yao ya kujikwamua kiuchumi  na kuondoa umasikini unaowakabili watanzania kwa ujumla.

Jukwaa limeongeza  kuwa hatua hiyo ya mkuu  wa mkoa  wa Dar es salaam ya kutaka kuwatambua  wanainchi wa  mkoa wake wa Dar es salaam katika ngazi  ya kaya ni kutaka  kujua  jinsi gani ya kuweza kupanga na kuwahudumia kama ilivyo katika majiji  ya London,Paris na Berlin inavyofanyika.

Jukwaa huru limechukua nafasi hiyo kuwaomba na kuwashauri wanainchi wote popote litakapo fanyika  zoezi hilo  kushirikiana na serikali kikamilifu kwani ni kwa manufaa ya wanainchi wenyewe na taifa kwa ujumla ili kuweza kuinua uchumi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images