Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

CHADEMA Yaandaa Vijana 4,000 wa Kuzuia mkutano wa CCM......Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Ahojiwa na Jeshi la Polisi

$
0
0
BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limeendeleza msimamo wake wa kuzuia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, uliopangwa kufanyika Julai 23, mwaka huu mjini Dodoma.

Katika kuhakikisha linatimiza azma yake hiyo, baraza hilo limesema wanachama wake wapatao 4,000 wamejiandaa kushiriki kwenye shughuli hiyo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, baada ya kuhojiwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi, Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick ole Sosopi, alisema kuna vijana watakaotoka sehemu mbalimbali ili kuzuia mkutano wa CCM.
 
Sosopi alisema Bavicha watakwenda Dodoma kuzuia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM kwa kile walichodai kusaidia Jeshi la Polisi kutekeleza amri yake ya kuzuia mikutano ya kisiasa hadi 2020.
 
Alisema pia kuna watu wamejitolea kutoa magari kwa ajili ya kuwabeba vijana hao ili kuwafikisha Dodoma kuunga mkono agizo la polisi.
 
Sosopi pia aliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kutokana na kauli zao za vitisho walizozitoa dhidi ya Bavicha hivi karibuni.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Julai 4, mwaka huu, Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamad Shaka, aliionyaBavicha wasiende Dodoma kuzuia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM kwa kuwa watatumia kila mbinu kuwazuia ili kulinda heshima ya chama chao.
 
Sosopi alisema wao hawataki matatizo wala vurugu bali wanachofanya ni kutii agizo la polisi kwa unyenyekevu.
 
"Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu kwani Rais alipopiga marufuku mikutano ya kisiasa hadi 2020, CCM walichekelea wakiamini kuwa Chadema tumekomolewa lakini iweje sasa Jeshi la Polisi likubali kuruhusu mkutano wao wakati Chadema hata mikutano ya ndani tunazuiliwa?
 
"Hatutanii hata kidogo na wala CCM wasidhani kuwa hatutakwenda Dodoma lakini tunaliomba Jeshi la Polisi litende haki juu ya kauli za uchochezi kwani nilitegemea viongozi wa UVCCM wangekamatwa na jeshi hilo lakini tunaokamatwa ni sisi tu," alisema Ole Sosopi.
 
Akizungumzia suala la kuhojiwa na polisi jana, Ole Sosopi alisema alikuwa kituoni hapo kuhojiwa kwa kosa analodaiwa kufanya Juni 18, mwaka huu la kutoa kauli za uchochezi.
 
Sosopi alikamatwa mara ya kwanza Juni 26, mwaka huu mkoani Iringa na kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam na
kuhojiwa kwa kosa hilo katika shughuli ya mahafali ya wanachama wa Chadema waliomaliza vyuo vikuu.
 
Sosopi alisema baada ya kuhojiwa jana na polisi, anatakiwa kuripoti tena kituoni hapo Julai 18, mwaka huu.
 
Akizungumzia suala la Sosopi, mwanasheria wake, Frederick Kihwelo alisema Sosopi aliripoti kituoni hapo kwani anakabiliwa na tuhuma ya kutoa lugha ya uchochezi.
 
Alidai lengo la mteja wake ni kuhakikisha polisi wanatenda haki bila upendeleo kwani kazi yao kubwa ni kulinda usalama wa raia na mali zao
 
Alisema baada ya kuhojiwa na polisi jana, atatakiwa kufika tena kituoni hapo Julai 18, mwaka huu wakati huu upelelezi unafanyika na ushahidi kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaki ya Jinai (DPP) ili aamue kama kuna kesi ya kujibu au la.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yazungumzia hatma kura ya maoni ya katiba mpya

$
0
0

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inatarajia kukamilisha mchakato wa katiba inayopendekezwa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, aliyama hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kutembelea banda la tume hiyo katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Alisema katiba inayopendekezwa itaweka maoni ya wananchi juu ya mapendekezo ya tume huru ya uchaguzi wanayoitaka na hivyo uchaguzo ujao utakuwa katika mfumo huo.

Jaji Lubuva alisema ili kufanyika kwa kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa, ni lazima kwanza Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na NEC zikutane ili kufanya marekebisho ya sheria ya taifa ya uchaguzi.

"Ni matumaini yetu na tungependa sana kuona kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu ujao 2020, tuwe tumeshapata katiba mpya ambayo itatupa muongozo wa uchaguzi mkuu huo," alisema.

Alisema ili kupata tume ya uchaguzi ambayo itakuwa huru, itatokana na kupatikana kwa katiba mpya ambayo mchakato wake unatarajiwa kumalizikia kwenye kura ya maoni.

Hata hiuvyo, Jaji Lubuva alisema tume iliyopo ni huru kwa sababu haiingiliwi na mtu yoyote isipokuwa kinachosabisha isionekane huru ni mfumo wake wa kuteuliwa kwa makamishna nane na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama.

"Tume iliyopo ni huru na haki kwa sababu kazi zetu haziingiliwi na yeyote na hata uchaguzi tulioufanya mwaka jana ulikuwa huru na haki isipokuwa watu walishaaminishwa tume siyo huru, " alisema Jaji Lubuva na kuongeza:

“Wanachokitaka Watanzania ni kuona wanakuwa na tume huru ya maandishi pamoja na isiyoingiliwa na yeyote. Nchi yetu ina tume huru na haki, ni tofauti na nchi nyingine ambazo zipo kwenye maandishi tu lakini si huru.”

Juzi Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima alisema uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura utafanyika mwaka wa fedha wa 2017/18.

Alisema kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa inaweza kufanyika kabla au baada ya uboreshaji wa daftari hilo.
 
Hata hivyo, alisema daftari hilo litaanza kiboreshwa mara baada ya sheria ya uchaguzi kufanyiwa marekebisho na kupitishwa.

Watu Waliokufa Katika Ajali ya City Boy Wafikia 32

$
0
0
Idadi ya watu waliokufa katika ajali iliyohusisha mabasi mawili ya Kampuni ya City Boy imeongezeka na kufikia 32 baada majeruhi aliyekuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) kufariki dunia.

Ajali hiyo iliyohusisha mabasi hayo wakati moja likitokea Dar es Salaam kuelekea Kahama mkoani Shinyangana lingine likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam, ilitokea saa tisa Jumatatu katika eneo la Maweni, Kata ya Kintiku Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Akizungumza jana Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,  Dk Ibehzi Ernest alisema kazi ya kutambua miili ya marehemu hao bado inaendelea.

Alisema hadi jana miili ya watu 25 waliokufa kwenye ajali hiyo ilikuwa imetambuliwa na ndugu zao. Dk Ernest ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Ajali, Upasuaji na Mifupa alisema kati ya maiti 25 zilizotambuliwa 12 zimechukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi.

“Wengine wametibiwa na kuruhusiwa tumebaki na majeruhi watano ambao hali zao zinaendelea vizuri,” alisema. 

Kwa siku nzima ya juzi na jana watu walikuwa wakipishana kuwatambua ndugu zao katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Dodoma. Kutokana na miili kuharibika, ndugu hao walikuwa wakirudi mara mbili kuangalia. 

Gesi Ya Kupikia Kuagizwa kwa Pamoja Kuanza Septemba

$
0
0
Serikali itaanza kutumia mfumo wa uagizaji wa pamoja wa nishati ya gesi ya kupikia (LPG), kama inavyofanyika kwa mafuta ya ndege, petroli, dizeli na mafuta taa ifikapo Septemba mwaka huu. 

Akizungumza wakati wa semina ya wadau wa sekta ya mafuta kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, Mkurugenzi wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Godwin Samuel alisema mpango huo utasaidia kupunguza gharama na bei ya gesi hiyo inayoanza kutumika kwa kasi majumbani. 

Samuel alisema mpango huo pia utaongeza udhibiti wa mapato ya Serikali katika sekta hiyo inayoshika kasi nchini. 

Kuhusu uagizaji wa mafuta ya ndege, petroli, dizeli na mafuta ya taa, Mkurugenzi huyo alisema mchakato unaendelea kuboresha mfumo wa sasa kwa kukusanya maoni na mapendekezo ya wadau yatakayotumika kubadilisha taratibu zilizopo ifikapo Novemba, mwaka huu mikataba ya sasa itakapomalizika.

“Tunakusudia kuongeza ushindani wenye tija katika uagizaji wa pamoja wa mafuta ya ndege, petroli, dizeli na mafuta taa kwa kuongeza idadi ya kampuni kulinganisha na kandarasi zilizopo zinazofikia kikomo ifikapo Novemba mwaka huu,” alisema Samuel. 

Kuhusu elimu kwa wadau, Mkurugenzi huyo alisema Ewura inalenga kuwawezesha kujua na kuzingatia mabadiliko yanayotokea katika sekta na biashara ya mafuta ili kuwezesha kila upande kutimiza wajibu kulingana na sheria, kanuni na taratibu. 

“Changamoto zinazoikabili sekta na biashara ya mafuta hayawezi kutatuliwa na Ewura pekee bali ni kwa ushirikiano wa wadau wote,” alisema.

Breaking News : Orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri na Majiji walioteuliwa leo na Rais Magufuli

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo July 07 2016 amefanya uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.


Uteuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe ambapo kati ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa, 65 wameteuliwa kutoka orodha ya wakurugenzi wa zamani na 120 ni wakurugenzi wapya.
 
Orodha ya wakurugenzi walioteuliwa kulingana na mikoa yao ni kama ifuatavyo;
 
ARUSHA
⦁ Arusha Jiji – Athumani Juma Kihamia
⦁ Arusha DC – Dkt. Wilson Mahera Charles
⦁ Karatu DC – Banda Kamwande Sonoko
⦁ Longido DC – Jumaa Mohamed Mhiwapijei
⦁ Meru DC – Kazeri Christopher Japhet
⦁ Monduli DC – Stephen Anderson Ulaya
⦁ Ngorongoro DC – Raphael John Siumbu
 
DAR ES SALAAM
⦁ Dar es salaam Jiji – Siporah Jonathan Liana
⦁ Kinondoni Manispaa – Aron Titus Kagurumjuli
⦁ Temeke Manispaa – Nassibu Bakari Mmbaga
⦁ Ilala Manispaa – Msongela Nitu Palela
⦁ Kigamboni Manispaa – Stephen Edward Katemba
⦁ Ubungo Manispaa – Kayombo Lipesi John 
 
DODOMA
⦁ Dodoma Manispaa – Dkt. Leonard M. Masale
⦁ Kondoa DC – Kibasa Falesy Mohamed
⦁ Kondoa Mji – Khalifa Kondo Mponda
⦁ Mpwapwa DC – Mohamed Ahamed Maje
⦁ Kongwa DC – Mhandisi Ngusa Laurent Izengo
⦁ Chemba DC – Semistatus Hussein Mashimba
⦁ Chamwino DC – Athuman Hamis Masasi
⦁ Bahi DC – Rachel Marcel Chuwa
 
GEITA
⦁ Bukombe DC – Dionis Maternus Nyinga
⦁ Chato DC – Mhandisi Joel Bahahari
⦁ Geita DC – Ally Abdallah Kidwaka
⦁ Geita Mji – Modest J. Apolinaly
⦁ Mbogwe DC – Mahwago Elias Kayandabila
⦁ Nyang’wale DC – Carlos K. Gwamagobe
 
IRINGA
⦁ Iringa Manispaa – William Donald Mafwele
⦁ Mafinga Mji – Saada S. Mwaruka
⦁ Mufindi DC – Riziki Salas Shemdoe
⦁ Iringa DC – Robert Mgendi Magunya
⦁ Kilolo DC – Aloyce Kwezi
 
KAGERA
⦁ Biharamulo DC – Wende Israel Ng’ahala
⦁ Bukoba DC – Abdulaaziz Jaad Hussein
⦁ Bukoba Manispaa – Makonda Kelvin Stephen
⦁ Karagwe DC – Godwin Moses Kitonka
⦁ Kyerwa DC – Shedrack M. Mhagama
⦁ Missenyi DC – Limbe Berbad Maurice
⦁ Muleba DC – Emmanuel Shelembi Luponya
⦁ Ngara DC – Aidan John Bahama
 
KATAVI
⦁ Mlele DC – Alex Revocatus Kagunze
⦁ Mpimbwe DC – Erasto Nehemia Kiwale
⦁ Mpanda DC – Ngalinda Hawamu Ahmada
⦁ Mpanda Manispaa – Michael Francis Nzyungu
⦁ Nsimbo DC – Joachim Jimmy Nchunda
 
KIGOMA
⦁ Buhigwe DC – Anosta Lazaro Nyamoga
⦁ Kakonko DC – Lusubilo Joel Mwakabibi
⦁ Kasulu DC – Godfrey Msongwe Masekenya
⦁ Kasulu Mji – Fatina Hussein Laay
⦁ Kigoma Ujiji – Manispaa – Judethadeus Joseph Mboya
⦁ Kigoma DC – Hanji Yusuf Godigodi
⦁ Kibondo DC – Shelembi Felician Manolo
⦁ Uvinza DC – Weja Lutobola Ng’olo
 
KILIMANJARO
⦁ Manispaa ya Moshi – Michael Nelson Mwandezi
⦁ Hai DC – Yohana Elia Sintoo
⦁ Siha DC – Valerian Mwargwe Juwal
⦁ Same DC – Shija Anaclaire
⦁ Mwanga DC – Golden A. Mgonzo
⦁ Rombo DC – Magreth Longino John
⦁ Moshi DC – Emalieza Sekwao Chilemeji
 
LINDI
⦁ Kilwa DC – Bugingo I. N. Zabron
⦁ Lindi DC – Samwel Warioba Gunzar
⦁ Lindi Manispaa – Jomaary Mrisho Satura
⦁ Liwale DC – Justine Joseph Monko
⦁ Nachingwea DC – Bakari Mohamed Bakari
⦁ Ruangwa DC – Andrea Godfrey Chezue
 
MANYARA
⦁ Babati Mji – Fortunatus Hilario Fwema
⦁ Hanang DC – Bryceson Paul Kibasa
⦁ Mbulu DC – Festi Fungameza Fwema
⦁ Mbulu Mji – Anna Philip Mbogo
⦁ Simanjiro DC – Yefred Edson Myezi
⦁ Kiteto DC – Tamim Kambona
⦁ Babati DC – Hamis Iddi Malinga
 
MARA
⦁ Manispaa ya Musoma – Fidelica Gabriel Myovela
⦁ Bunda DC – Amos Jeremiah Kusaja
⦁ Bunda Mji – Janeth Peter Mayanja
⦁ Butiama DC – Solomon Kamlule Ngiliule
⦁ Musoma DC – Flora Rajab Yongolo
⦁ Serengeti DC – Juma Hamsini Seph
⦁ Rorya DC – Charles Kitanuru Chacha
⦁ Tarime DC – Apoo Castro Tindwa
⦁ Tarime Mji – Hidaya Adam Usanga
 
MBEYA
⦁ Busokelo DC – Eston Paul Ngilangwa
⦁ Chunya DC – Sofia Kumbuli
⦁ Kyela DC – Mussa Joseph Mgata
⦁ Mbarali DC – Kivuma Hamis Msangi
⦁ Mbeya DC – Ameichiory Biyengo Josephat
⦁ Mbeya Jiji – Zacharia Nachoa Ntandu
⦁ Rungwe DC – Loema Isaya Peter
 
SONGWE
⦁ Momba DC – Adrian Jovin Jungu
⦁ Tunduma Mji – Valery Alberth Kwemba
⦁ Mbozi DC – Edna Amulike Mwaigomole
⦁ Ileje DC – Haji Mussa Mnasi
⦁ Songwe DC – Elias Philemon Nawela
 
MOROGORO
⦁ Gairo DC – Agnes Martin Mkandya
⦁ Kilombero DC – Dennis Lazaro Londo
⦁ Ifakara Mji – Francis Kumba Ndulane
⦁ Kilosa DC – Kessy Juma Mkambala
⦁ Morogoro DC – Sudi Mussa Mpili
⦁ Morogoro Manispaa – John Kulwa Magalula
⦁ Mvomero DC – Florent Laurent Kyombo
⦁ Ulanga DC – Audax Christian Rukonge
⦁ Malinyi DC – Marcelin Rafael Ndimbwa
 
MTWARA
⦁ Mtwara DC – Omari Juma Kipanga
⦁ Mtwara Mikindani Manispaa – Beatrice Dominic Kwai
⦁ Masasi Mji – Gimbana Emmanuel Ntayo
⦁ Masasi DC – Mkwazu M. Changwa
⦁ Nanyumbu DC – Hamis Hassan Dambaya
⦁ Newala DC – Mussa Mohamed Chimae
⦁ Newala Mji – Andrew Frank Mgaya
⦁ Tandahimba DC – Said Ally Msomoka
⦁ Nanyamba Mji – Oscar Anatory Ng’itu
 
MWANZA
⦁ Mwanza Jiji – Kiomoni Kibamba Kiburwa
⦁ Ilemela Manispaa – John Paul Wanga
⦁ Kwimba DC – Pendo Anangisye Malabeja
⦁ Magu DC – Lutengano George Mwalwiba
⦁ Misungwi DC – Eliud Leonard Mwaiteleke
⦁ Ukerewe DC – Tumaini Sekwa Shija
⦁ Buchosa DC – Crispian Methew Luanda
⦁ Sengerema DC – Magesa M. Boniphace
 
NJOMBE
⦁ Njombe Mji – Iluminata Leonald Mwenda
⦁ Makambako Mji – Paul Sostenes Malala
⦁ Makete DC – Francis Emmanuel Namaumbo
⦁ Njombe DC – Monica Peter Kwiluhya
⦁ Ludewa DC – Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija
⦁ Wanging’ombe DC – Amina Mohamed Kiwanuka
 
PWANI
⦁ Bagamoyo DC – Azimina A. Mbilinyi
⦁ Chalinze DC – Edes Philip Lukoa
⦁ Kibaha DC – Tatu Seleman Kikwete
⦁ Kibaha Mji – Jenifer Christian Omolo
⦁ Kisarawe DC – Mussa L. Gama
⦁ Mafia DC – Erick Mapunda
⦁ Mkuranga DC – Mshamu Ally Munde
⦁ Kibiti DC – Alvera Kigongo Ndabagoye
⦁ Rufiji DC – Salum Rashid Salum
 
RUKWA
⦁ Kalambo DC – Simon Ngagani Lyamubo
⦁ Sumbawanga DC – Nyangi John Msemakweli
⦁ Sumbawanga Manispaa – Hamid Ahmed Njovu
⦁ Nkasi DC – Julius M. Kaondo
 
RUVUMA
⦁ Mbinga DC – Gumbo Samanditu Gumbo
⦁ Mbinga Mji – Robert Kadaso Mageni
⦁ Namtumbo DC – Christopher Michael Kilungu
⦁ Nyasa DC – Oscar Albano Mbuzi
⦁ Songea DC – Simon Michael Bulenganija
⦁ Madaba DC – Shafi Kassim Mpenda
⦁ Tunduru DC – Abdallah Hussein Mussa
⦁ Songea Manispaa – Tina Emelye Sekambo
 
SHINYANGA
⦁ Kishapu DC – Stephen Murimi Magoiga
⦁ Msalala DC – Berege Sales Simon
⦁ Shinyanga DC – Mark Emmanuel Malembeka
⦁ Kahama Mji – Anderson David Msumba
⦁ Shinyanga Manispaa – Lewis Kweyemba Kalinjuna
⦁ Ushetu DC – Michael Augustino Matomola
 
SIMIYU
⦁ Bariadi DC – Abdallah Mohamed Malela
⦁ Bariadi Mji – Melkizedek Oscar Humbe
⦁ Itilima DC – Mariano Manyingu
⦁ Maswa DC – Fredrick Damas Sagamiko
⦁ Busega DC – Anderson Njiginya
⦁ Meatu DC – Said F. Manoza
 
SINGIDA
⦁ Ikungi DC – Rustika William Turuka
⦁ Iramba DC – Linno Pius Mwageni
⦁ Mkalama DC – Martin Msuha Mtanda
⦁ Manyoni DC – Charles Edward Fussi
⦁ Itigi DC – Luhende Pius Gerald
⦁ Singida DC – Rashid Mohamed Mandoa
⦁ Singida Manispaa – Kizito L. Brava
 
TABORA
⦁ Igunga DC – Revocatus Lubigili Kuuli
⦁ Kaliua DC – John Marco Pima
⦁ Nzega DC – Jacob James Mtalitinya
⦁ Nzega Mji – Phillimon Mwita Magesa
⦁ Sikonge DC – Simon Saulo Ngatunga
⦁ Tabora Manispaa – Bosco Addo Ndunguru
⦁ Urambo DC – Magreth Nakainga
⦁ Tabora -Uyui – Hadija Maulid Makuani
 
TANGA
⦁ Tanga Jiji – Daudi R. Mayeji
⦁ Korogwe DC – George John Nyaronga
⦁ Korogwe Mji – Jumanne Kiangoshauri
⦁ Muheza DC – Luiza Osmin Mlelwa
⦁ Handeni Mji – Keneth K. Haule
⦁ Handeni DC – William Methew Mafukwe
⦁ Pangani DC – Sabas Damian Chambasi
⦁ Mkinga DC – Mkumbo Emmanuel Barnabas
⦁ Bumbuli DC – Peter Isaiah Nyalali
⦁ Kilindi DC – Clemence Andagile Mwakasenda
⦁ Lushoto DC – Kazimbaya Makwega Adeladius
 
Wakurugenzi wote walioteuliwa wametakiwa kufika Ikulu Jijini Dar es salaam siku ya Jumanne July 12 2016 saa tatu asubuhi kwa ajili ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma.

Uteunzi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Watenguliwa

Rais Magufuli Amteua Deogratius Ndejembi Kuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Kongwa Mkoani Dodoma

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016 amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi anachukua nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. John Ernest Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.

Uhamisho wa Bw. John Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya Mhe. Rais Magufuli kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi.

Bw. Deogratius John Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma siku ya Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Julai, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya July 8


Majambazi Yateka Kijiji Kwa Masaa Matatu Mkoani Kagera

$
0
0

MAJAMBAZI wanne wamevamia kijiji cha Benaco kilichopo katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kwa muda wa saa tatu ambapo wamefanikiwa kupora Sh milioni 2.4 na simu ambazo hazikujulikana idadi yake kwa mfanyabiashara mmoja wa huduma ya M-Pesa.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kagera ambaye pia ni ofisa upelelezi wa polisi mkoa huo, Abel Mtagwa, alisema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana ambapo majambazi hao walikuwa na silaha moja ya kivita aina ya SMG.

Alisema kuwa wakati majambazi wakijiandaa kuondoka eneo hilo walimpiga risasi mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Gankabo Wilayani Kibondo mkoani Kigoma aliyetambuliwa kwa jina la Nelson Simon (15) na kumjeruhi mguu wake wa kulia. Mwanafunzi huo amelazwa katika hospitali teule ya Murgwanza iliyopo wilayani humo.

Edward Lowassa ashiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge mstaafu, Beatrice Shelukindo

$
0
0
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amekuwa miongoni mwa mamia ya waombolezaji walioshiriki maziko ya mbunge wa zamani, Beatrice Shelukindo (58) yaliyofanyika nyumbani kwa wazazi wake katika kata ya Olorien Jijini Arusha jana.

Viongozi wengine waliohudhuria maziko hayo yaliyotanguliwa na ibada ni pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhani, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda.

Pia maziko hayo yalihudhuriwa na wabunge na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mkoa wa Tanga na Arusha, Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Kalisti Lazaro na viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali. 

Ibada ilifanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro ambako Askofu mstaafu, Simon Makundi, alisema Beatrice hakuwa fisadi na alitoa mchango mkubwa kwa familia, dini, taifa na Afrika Mashariki.

“Jiulize wewe una mchango gani hata katika familia yako, dini yako, taifa hili na hata kwa Afrika Mashariki?” Alihoji Makundi.

Aliwataka mamia ya waombolezaji wakipewa nafasi, heshima na vyeo serikalini au katika kampuni yo yote kuitunza heshima hiyo kwa kufanya kazi kwa uadilifu na kuwa na hofu ya Mungu.

Beatrice aliyezaliwa mwaka 1958 amefariki akiwa na umri wa miaka 58, jambo ambalo askofu mstaafu alisema hiyo ni neema ya Mungu.

Alisisitiza kuwa Beatrice alifanya kazi za utumishi serikalini na ubunge kwa uadilifu mkubwa na kupata heshima na serikali, dini na jamii na ndiyo maana aliweza kuhitimisha heshima hiyo hadi mwisho. Askofu Makundi alisema alipata bahati ya kuzungumza naye kabla ya mauti.

Sheikh Ponda Issa Ponda Ponda afurahia Magufuli kurejesha mali za Waislamu

$
0
0
Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda amempongeza Rais John Magufuli kutokana na ahadi yake ya kurejesha mali za Waislamu. 

Lakini Sheikh Ponda hajakubaliana na kitendo cha Rais kutoa fedha taslimu kwa ajili ya kuchangia safari za Hija, akisema mkuu huyo wa nchi angezungumza na wahusika ili kujua matatizo ambayo fedha hizo zingesaidia. 

Sheikh Ponda amesema ahadi hiyo ya Rais ni ya kuungwa mkono kwa kuwa inaonyesha kujali masilahi ya wananchi, hususan Waislamu. 

Juzi, akihutubia Baraza la Idd el Fitr jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema atawasaidia Waislamu kurejesha mali zao na kumpongeza Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Abubakar Zubeir kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kurejesha mali hizo kabla hata hajapewa cheo hicho. 

“Nakumbuka wakati nikiwa Waziri wa Ardhi, kabla hujawa Mufti, pamoja na viongozi wa Bakwata na wengine, ulifika ofisini kwangu ukieleza jinsi mali za Waislamu zilivyokuwa zinadhulumiwa. 

"Ninafamu pamekuwa na hiyo tabia ya baadhi ya viongozi wenye mali kuwatumia viongozi wa Bakwata na dini nyingine katika kuwarubuni na kuingia ubia. Mali hizo baadaye huwa zinapotea kabisa,” alisema. 

“Tujitahidi kwa nguvu zote kusimamia mali hizi zisije kuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani. Tunapenda wawekezaji, lakini wanachokiahidi hawatekelezi. Haiwezekani. 

“Haiwezekani na wala haikubaliki kwa watu kwa ujanja wao na wakati mwingine kwa kutumia wanasheria wao kukalia mali za Waislamu. Mali za Waislamu lazima zirudi na za Wakristo zirudi ili amani iwepo.” 

Sheikh Ponda alisema kwa kauli hiyo, Rais Magufuli ametambua juhudi ambayo wamekuwa wakizifanya katika kupigania mali za Waislamu, kama ilivyokuwa katika kupigania kiwanja cha Chang’ombe hadi kusababisha kesi dhidi yake na wenzake. 

“Utakumbuka, tulikuwa na kesi kuhusu kiwanja cha Waislamu kule Chang’ombe, katika hatua za awali tulishindwa, lakini baadaye tukakata rufaa na kushinda. Ndiyo sababu ya kuunga mkono kauli hii ya Rais,” alisema Sheikh Ponda. 

Akizungumzia msaada wa Rais Magufuli kwa ajili ya Hija, alisema hiyo ni ruzuku muhimu, lakini Rais angekaa na Waislamu wamweleze mambo ambayo ni muhimu zaidi ili uwekezaji wake uwe na manufaa zaidi. 

Alipoulizwa ni mambo gani ni muhimu zaidi, Sheikh Ponda alisema ni masuala ya elimu na afya ambayo Serikali ikisaidia baadaye yatapunguza mzigo mkubwa kwake

Serikali Yazifungua Minyororo ofisi za Nimrod Mkono

$
0
0
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jana imezifungua ofisi za Kampuni maarufu ya uwakili ya Mbunge wa Butiama, Nimrod Mkono, ikiwa ni siku chache baada ya kuzifungia kwa madai kuwa kampuni hiyo inadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.

TRA waliwasili katika jengo la ofisi hizo zilizoko katika jengo la Bank ya Exim iliyoko jijini Dar es Salaam (ingawa ilikuwa sikukuu), pamoja na Kampuni ya udalali ya Yono na kuzifungua ofisi hizo mbele ya Nimrod Mkono na binti yake.

Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amekiri kufunguliwa kwa ofisi hizo. Kayombo amesema kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuwepo kwa makubaliano kati ya pande mbili na ahadi ya kufanya malipo iliyowekwa na mkono.

“Ni kweli muda upo tuliokubaliana lakini hatutaki uwe katika vyombo vya habari, kutokana na nia ya dhati aliyoonesha Mkono ndio maana tumekubaliana nae,” Kayombo anakaririwa.

Hatua hiyo imefikiwa huku kukiwa na taarifa kuwa ingawa Mkono amefungiwa ofisi zake akidaiwa kodi ya shilingi bilioni 1, yeye anaidai Serikali takribani shilingi bilioni 9 kwa kazi alizofanya ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Mvutano wa CCM na CHADEMA Walitikisa Jeshi la Polisi.........BAVICHA Yaandaa Zaidi ya Vijana 5000 Kuzuia Mkutano, Polisi Mara Yasema Wanacheza Ngoma ya Kitoto

$
0
0

Mvutano wa kisiasa baina ya vijana wa CCM na CHADEMA  kuhusu katazo la mikutano ya vyama vya siasa umezidi kukua huku jeshi la polisi likitarajiwa kutoa tamko kuhusu hali hiyo.

Hali hiyo ya jino kwa jino imejitokeza  zikiwa zimebakia siku 16 kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa CCM July 23, ambao Baraza la Vijana la CHADEMA ( BAVICHA )  limesema litawasaidia polisi kuuzuia.

Tayari BAVICHA limetangaza kuandaa vijana 5000 kutoka sehemu mbalimbali nchini kwenda kuzuia mkutano huo utakaotumika kumkabidhi Rais John Magufuli uenyekiti wa chama hicho.

Jumatatu iliyopita, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka aliionya Bavicha wasiende Dodoma kuzuia mkutano wa CCM kwa kuwa watatumia kila mbinu kuwazuia ili kulinda heshima ya chama chao. 

Shaka alisema mkutano huo utafanyika kama ulivyopangwa, hivyo Bavicha kama kweli ni vidume wa mbegu wajitokeze ili wakione cha mtema kuni. 

Shaka alisema UVCCM wako tayari kuidhihirishia dunia kwa kuwatia adabu Bavicha na kuonya wasijaribu kufanya jambo lolote linalotishia kuhatarisha usalama au ustawi wa maendeleo ya kisiasa ya CCM kwa saa, siku, wakati na mahali popote. 

Shaka aliwataka Bavicha kuacha siasa za mikwara, vitisho, kutishia usalama na amani ya nchi kwa kujifanya vijogoo wakati hawana lolote wanaloweza ama kuzuia, kujenga au kubomoa. 

Alipoulizwa kuhusu mvutano huo, Msemaji wa Polisi nchini, Advera Bulimba alisema jeshi hilo litatoa taarifa na ufafanuzi kuhusu zuio la mikusanyiko ya vyama vya siasa leo. 

Sintofahamu ilivyoanza 
Utata huo uliibuliwa na amri ya Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi Makao, Nsato Mssanzya ya kuzuia mikutano na maandamano yote ya vyama kwa madai kwamba vyanzo vyake vya kiintelejensia vilibaini kuwapo kwa uwezekano wa kutokea kwa vurugu. 

“Jeshi la polisi nchini linapiga marufuku maandamano na mikutano yote ya hadhara kuanzia Juni 7, mwaka huu hadi hapo hali ya usalama itakapotengamaa." Ilisema sehemu ya taarifa ya jeshi la polisi


Baada ya katazo hilo, jeshi hilo lilitawanya mikutano ya ndani ya Chadema, yakiwamo mahafali ya vijana wa chama hicho (Chaso) yaliyopangwa kufanyika Dodoma kwa madai ya kuwapo mlipuko wa ugonjwa usiofahamika. 

Hatua hiyo ya polisi ilikuja baada ya Chadema kutangaza mpango wa kuzunguka nzima kueleza masaibu ya kidemokrasia yanayokikumba na baadaye CCM kutangaza kupita katika maeneo hayo ‘kufuta nyayo”.

Katibu wa Bavicha, Julius Mwita alisema mpaka jana tayari vijana 5,000 walikuwa wakijiandaa kwenda Dodoma; “kushirikiana na polisi kuwafundisha CCM kuheshimu amri zinazotolewa na viongozi. "

"Tumeandaa vijana 5,000 kutoka mikoa 19 nchini ambao wamejitolea kwa nauli zao kwenda Dodoma kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha mkutano wa CCM haufanyiki.” 

Watembelea Butiama 
Katika hatua nyingine, viongozi wa Chadema juzi walitembelea kaburi  la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere huko Butiama, wakisema walikwenda kumshtaki Rais Magufuli kwa kuminya demokrasia. 

Mwenyekiti wa Bavicha, Pastrobas Katambi alisema chama hicho kinatambua jitihada zilizofanywa na Mwalimu Nyerere katika kukuza na kuendeleza ustawi wa jamii ya kidemokrasia nchini.

“Tunapenda kuwaambia watawala kwamba amani ni tunda la haki na ni muhimu utawala ukaheshimu misingi ya kikatiba iliyoachwa na Baba wa Taifa,” alisema Katambi. 

Kauli za CCM, Chadema 
Naibu Katibu Mkuu Chadema, John Mnyika alisema anabariki maandalizi ya mpango na kitendo kinachotarajiwa kufanywa na Bavicha ili kuwepo na usawa wa kidemokrasia. 

“Kama ni ruhusa iwe kwa wote na kama zuio liwe kwa wote, haina maana Chadema wazuiwe lakini CCM waendelee na mikutano yao ya kisiasa,” alisema Mnyika. 

Kaimu Katibu wa CCM, Mkoa wa Dodoma alisema mkutano huo ni wa kitaifa na wala si wa mkoa na kushauri atafutwe Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka. 

“Sisi tunatekeleza maagizo tunayopewa na si vinginevyo,” alisema. Ole Sendeka hakupatikana na simu yake ilikuwa inaita bila kupokelewa. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema mkutano wa CCM ni wa ndani wala hakuna tatizo lolote kwa kuwa mikutano ya ndani inaruhusiwa na kuwa jeshi hilo litawalinda wanaCCM. 

Kuhusu Jeshi hilo kuzuia mikutano ya Chadema, Mambosasa alisema walizuia bendera na si vinginevyo na kuwa alitoa taarifa ikiwa kamili lakini waandishi walipotosha. 

Manyara wajiandaa
Zaidi ya vijana 560 wa Mkoa wa Manyara, wamejiandikisha tayari kuelekea Dodoma kwa ajili ya kuwasaidia polisi kuzuia mkutano wa CCM ili kuunga mkono agizo la kupigwa marufuku mikusanyiko ya kisiasa.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Francis Massawe aliwataka vijana hao kuachana na mpango huo wa kitoto kwani wao wamejipanga kushughulika na watu wanaotaka kuanzisha vurugu. 

Kamanda Massawe alisema endapo kuna kundi linataka kukwamisha mkutano halali wa CCM wa kumchagua mwenyekiti wao, wasubiri hadi mwaka 2020 ndipo wafanye na kwamba polisi hawatakubali hilo litokee. 

“Hao vijana wanacheza ngoma ya kitoto ambayo haikeshi kwani wanaingilia majukumu ambayo siyo yao, uchaguzi wa CCM hauna ubishi lazima ufanyike na hakuna wa kuzuia, hao wanacheza kombolela,” alisema. 

Msimamo wa Zitto
Akizungumzia uamuzi wa Bavicha, Kiongozi wa ACT Wazalendo ambacho pia mitano yake imezuiwa, Zitto Kabwe alisema haoni tatizo kuhusu suala hilo kwa kuwa wanafanya siasa, hivyo haoni kama ni njia mbaya.

Zitto alisema chama chake hakiwezi kusema moja kwa moja kuwa kinaunga mkono uamuzi wa Bavicha lakini wao watakwenda mahakamani kupinga hatua ya Serikali kuzuia uhuru wa vyama vya siasa kufanya mikutano yao. 

Riwaya:Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard) - Sehemu ya 11

$
0
0
...Jeneza la mwalimu John lilikuwa tayari limefunuka, Mwalimu John aliinuka ndani ya Jeneza na kusimama wima cha kwanza alichofanya ilikuwa ni kunyanyua kinywa chake na kumuita mkewe mpenzi kwani ndiye aliyekuwa akimfikiria kila sekunde. " Mke wanguuuuu... Niko hai..usilie" Mwalimu John alisema kwa sauti kuu, huku furaha ikiwa imefurika moyoni mwake kwani hakuamini kama kweli ameurudia uhai.

Akiwa katika furaha hiyo isiyo na kikomo mwalimu John akatahamaki sana baada ya kuona umati wote uliokuwa ukiomboleza kwaajili yake ukikimbia. Watu walikimbia kwa fujo huku hofu ikiwa imewatamalaki. Cha ajabu hata mke wa Mwalimu John pia alikimbia kama swala anayekabiliana na mnyama mkali.

Hakuna aliyesalia kwenye eneo lile, vumbi lilitimka na kuwaaga waombolezaji wote ambao mpaka wakati ule hakuna aliyejua kilichotokea. "Maajabu haya! Maiti kafufuka? Kweli dunia IPO ukingoni" alisikika mwanamume mmoja ambaye alikuwa amejikwaa mguu baada ya kukimbia kwa muda mrefu.Alihema kwa nguvu huku akizitafuta nguvu zingine za kukimbilia. Ghafla akahisi kuna Mtu kasimama nyuma yake

" Vipi kuna mini kwani?" Ilisikika sauti ile ambayo ilipenya vyema masikioni mwa mwanaume yule. Akageuka kutazama anayeuliza, Mwanaume yule alitetemeka sana baada ya kukutana USO kwa uso na Mwalimu John. Akainuka haraka na kuziendeleza mbio zake.

Mwalimu John alikuwa haelewi ni kwanini watu wote wanakimbia, na yeye akaingiwa na hofu akaanza kukimbia akijua labda kuna jambo la hatari linakuja. Alizipiga mbio kuelekea nyumbani kwake ili akajihifadhi haraka iwezekanavyo.

Mwalimu John alipofika mtaani kwao, kila MTU alikimbilia ndani na kujifungia. Ndipo alipozidisha juhudi na kuongeza mwendokasi akidhani hatari inamkaribia. Mwalimu John alifika nyumbani kwake, alipofika getini ghafla geti likafungwa. Akastaajabu sana kwani hakufikiria kuwa mkewe badala ya kumpokea kwa shamrashamra alimfungia mlango.

"Nifungulie mke wangu!" Alisema Mwalimu John huku akipigapiga mlango, na kwakuwa mlango haukufungwa vyema ukajifungua. Mwalimu John aliingia ndani huku akihema sana.
"Mamaaaaa!"
Zilisikika kelele ndani ya nyumba ya Mwalimu John, ndugu wote walipiga kelele.
"mke wangu! Hunitaki!?" Mwalimu John aliuliza kwa sauti ya kutia huruma, huku akimsogelea mkewe.
"Ushindweee!" Mkewe alifoka.
"Mke wangu nishindwe Mimi? Leo unaniambia nishindwe kwani Mimi pepo?" Mwalimu John alizidi kutia huruma.
Aliinamisha kichwa chini, kwa bahati macho yakatua mwilini mwake. Mwalimu John alishtuka kupita kiasi, akajiogopa na akatamani kujikimbia.
 
"Nooooooooo!"


Mfumuko wa bei wa Taifa waongezeka hadi asilimia 5.5

$
0
0
Mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Juni, 2016 umeongezeka hadi asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 mwezi uliopita kutokana na kuongezeka kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephaim Kwesigabo amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kumesababishwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi.

“Mfumuko wa bei umesababishwa na kuongezeka kwa bei za vyakula kama vile mahindi ambayo yameongezeka kwa asilimia 3.2, unga wa muhogo kwa asilimia 2.4, samaki wabichi kwa asilimia 3.8, maziwa mgando kwa asilimia 4.3, maharage mabichi yaliyomenywa kwa asilimia 6.1, kitunguu swaumu kwa asilimia 12.5, njegere kwa asilimia 6.2, viazi mviringo kwa asilimia 2.5, mihogo mibichi kwa asilimia 6.7, magimbi kwa asilimia 4.5, na ndizi za kupika kwa asilimia 2.7,” amesema Kwesigabo.

Amesema bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na huduma ya kinywa na meno ambayo imeongezeka kwa asilimia 13.8, mafuta ya dizeli kwa asilimia 2.4 na mafuta ya petroli kwa asilimia 4.3.

Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa mwezi Juni, 2016 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.5 ongezeko sawa na mwezi uliopita.

Aidha amesema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka wa bidhaa za vyakula majumbani na migahawani umeongezeka hadi asilimia 8.3 mwezi Juni, 2016 kutoka asilimia 7.2 mwezi Mei, 2016. Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.47 mwezi Juni, 2016 kutoka 103.00 mwezi uliopita.

Kwesigabo amesema uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 96 na senti 65 mwezi Juni, 2016 kutoka mwezi Disemba, 2015.

Waziri Muhongo : Serikali Ya Uganda Kujenga Kiwanda Cha Kuchakata Mafuta Ghafi Na Kuwa Safi

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema Serikali ya Uganda itajenga Kiwanda cha kuchakata mafuta ghafi na kuwa masafi (refinery)katika eneo la Kabaale katika wilaya ya Hoima nchini humo.

 Profesa Muhongo amesema hayo baada ya kutembelea eneo hilo nchini Uganda wakati wa vikao vya kujadili michakato ya ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Kabaale - Hoima nchini humo hadi katika bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Vilevile amesema kuwa Serikali ya Uganda imetoa jumla ya 40% ya hisa za (refinery) hiyo kwa Serikali 5 za Afrika Mashariki kabla ya Sudani kusini kujiunga.

Katika hisa hizo Tanzania imekaribishwa na kutengewa 8% za kununua hisa hizo zenye thamani ya US$150.4 Millioni. Aidha Prof. Muhongo ameishauri Serikali na Sekta Binafsi kushirikiana kununua hisa hizo.

Katika hatua nyingine ujumbe wa Tanzania na ule wa Uganda juu ya ujenzi wa bomba la mafuta umetembelea eneo la ziwa Albert na kujionea visima vilivyochorongwa tayari kwa uzalishaji wa mafuta ghafi (crude oil).

Ambapo inakadiriwa kuwepo kwa mapipa bilioni 6.5 ya akiba (reserve) na yanoyoweza kuchimbwa ni mapipa bilioni 2 (recoverable). 

Ujenzi wa Bomba la mafuta kutoka Kabaale Uganda hadi Tanga (The East African Crude Oil Pipeline ) utagharim dola za Marekani Bilioni 3.55 na litakuwa na urefu wa kilometa 1,443, na litakuwa na uwezo wa kusafirisha mapipa 200,000 kwa siku.

Waziri Mkuu Asitisha Vibali Vya Uvunaji Mbao

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesitisha utoaji wa vibali vya uvunaji wa mbao kutoka katika mashamba nane ya miti ya kupandwa yanayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
 
Serikali  kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii inamiliki mashamba ya miti ya kupandwa 18, na kati ya hayo uvunaji umekuwa ukifanyika katika mashamba nane ambayo ni
  1. Sao Hill (Mufindi),
  2. Buhindi (Sengerema),
  3. Meru/Usa (Arumeru),
  4. West Kilimanjaro (Hai),
  5. Shume (Lushoto),
  6. North Kilimanjaro (Rombo),
  7. Kiwira (Rungwe) na
  8. Kawetire (Mbeya Vijijini).
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Julai 8, 2016) na kufafanua kwamba usitishaji huo unalenga kutathmini taratibu, kanuni na vigezo sahihi vinavyotakiwa kutumika katika kugawa malighafi kutoka kwenye mashamba hayo.
 
Amesema wadau wote wa viwanda vinavyojikita katika malighafi ya misitu na hususan wamiliki wa viwanda vya kupasua mbao wanashauriwa kuwa watulivu wakati utaratibu huu ukifanyiwa mapitio na umma utatangaziwa rasmi pindi uboreshaji huo utakapokamilika.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya July 9

TCRA yaipiga Clouds Tv adhabu kwa Kurusha kipindi chenye maudhui ya ushoga.

$
0
0
MAMLAKA ya mawasiliano nchini (TCRA) imetoa onyo pamoja na kuutaka uongozi wa Clouds TV kuomba radhi Watanzania kupitia taarifa zake za habari ndani ya siku tano mfululizo kuanzia jana.

Adhabu hiyo ilitolewa jana na kamati ya Maudhui ya TCRA, baada ya baadhi ya wananchi hususani watazamaji wa kipindi cha ‘Take One’ kilichorushwa 28 Juni mwaka huu ambacho kilidaiwa kueleza masuala ya mapenzi ya jinsia moja (Ushoga), kulalamikiwa kwamba kilikiuka maadili ya taifa.

Wakati akisoma tamko la adhabu hiyo, Joseph Mapunda, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wajumbe wa kamati kutafakari maelezo ya utetezi yaliyotolewa na uongozi waClouds TV.

“Tumetafakari kwa kina maelezo ya utetezi yaliyotolewa na clouds tv kuhusu kipindi chake cha Take One kilichorushwa hewani tarehe 28 June 2016 ambacho kilikiuka baadhi ya kanuni za maadili ya utangazaji,” alisema Mapunda.

Aliongeza kuwa “kutokana na kipindi hicho kuwakwaza pamoja na kuwasababishia usumbufu wananchi hususan watazamaji kwa kuwasilisha mada inayozungumzia masuala ya mapenzi ya jinsia moja (ushoga), Clouds TV inatakiwa kuwaomba radhi watanzania wote na watazamaji.”

Alisema taarifa ya kuomba radhi itoke siku tano mfululizo katika taarifa zao za habari ya saa moja na nusu na ya saa tano usiku kuanzia siku ya kusomwa hukumu, na kwamba uthibitisho wa taarifa hizo upelekwe TCRA siku ya Jumatano tarehe 13 Julai 2016 kabla ya saa kumi jioni.

“ Hatua ya pili, Clouds Tv inatakiwa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza na kuhakikisha inazingatia kanuni zote za utangazaji nchini katika kutekeleza majukumu yake ya utangazaji,” alisema na kuongeza.

“Kamati inawaonya vikali Clouds tv kwa kukiuka kanuni za huduma za utangazaji (maudhui) ya mwaka 2005, namba 5(b), 5(c), 5(d) na 15(c) 16(2) uamuzi huu umetolewa leo, haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu iko wazi ndani ya siku 30 tangu siku uamuzi unapotolewa.

Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa Clouds Media Group alisema baada ya kutafakari tamko la adhabu atatoa msimamo wake kama watakata rufaa au la.

“Tunaweza tukarudi nyuma na kusema tufanye kazi ya kukata rufaa, kwa sababu tunaamini na mimi nina simamia msimamo wangu kwamba tunapoambiwa tunalinda maadili ya kitaifa, kupinga jambo lolote baya ni kulinda maadili ya kitaifa,” alisema na kuongeza.

“Sasa ukiambiwa kwamba ulipinga kwa namna ya ulivyo pinga ni tofauti kidogo labda inaweza ikasaida kutengeneza mjadala mkubwa wa kujiuliza maadili tunayotakiwa kuyalinda ni yapi.”

Mutahaba alisema“Lakini moja kati ya kitu tunachokiona kina utofauti ni kuna baadhi ya mambo yamezungumzwa ambayo sikumbuki kabisa kama yako kwenye kipindi, kwa hiyo sijui wamezitolea wapi.”

Alisema kuwa ushoga ni tatizo na kwamba lazima alikemee na ataendelea kulikemea.

“Kwa ajili ya kosa la kutaja neno shoga katika kipindi cha njia panda mwaka 2000, miaka minne iliyopita kwenye gazeti tulivyosoma neno ushoga tukatozwa faini ya mil 5, haiwezekani miaka kumi na sita inapita kutaja neno shoga kila siku mtu anapewa adhabu,” alisema

Dereva wa Basi la City Boy Asomewa mashitaka 30 ya Kuua

$
0
0
MMOJA wa madereva waliosababisha ajali ya mabasi ya City Boy Jumatatu iliyopita katika kijiji cha Maweni wilayani Manyoni, Jeremiah Semfungwe (34), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida akikabiliwa na makosa 30 ya kuua bila kukusudia.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Joyce Minde, ilidaiwa kuwa mshitakiwa Semfungwe alitenda makosa hayo Julai 4 mwaka huu saa 8.15 mchana wakati akiendesha basi T. 247 BCD mali ya Kampuni ya City Boy kwa kuligonganisha na basi T.331DCE.

Wakili Mkuu Mfawidhi wa Serikali, Zakaria Ndaskoi alidai kuwa siku ya tukio mshitakiwa ambaye ni dereva na mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, bila kukusudia, alisababisha vifo vya abiria 30 kinyume na Kifungu 195 na 198 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Toleo la Kwanza.

Wakili wa mshitakiwa, Francis Kitope aliiomba mahakama impe mteja wake dhamana kwa kuwa chini ya Kifungu 148 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kosa hilo linadhaminika.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Ndaskoi alipinga hoja hiyo kwa kudai kuwa kwa kufanya hivyo usalama wa mshitakiwa utakuwa hatarini kwa kuwa ndugu wa marehemu na majeruhi bado wana hasira kutokana na ajali hiyo kuwa bado “mbichi”.

Aidha, Ndaskoi ambaye alikuwa akisaidiana na Petrida Muta aliendelea kudai kuwa majeruhi 54 wa ajali hiyo hali zao bado ni mbaya na hatma yao haijulikani hivyo si vyema mshitakiwa kupewa dhamana na kwamba mshitakiwa mwingine, dereva Boniface Mwakalukwa ametoroka.

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka juu ya kesi za mauji na ameswekwa rumande hadi Julai 21 kesi yake itakapotajwa tena.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images