Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Zitto Kabwe Amjibu Rais Magufuli

$
0
0

Kauli ya Rais ya Kuzuia Vyama vya Siasa Kufanya Shughuli za Siasa kwa Miaka Mitano ni Tangazo la Vita dhidi ya Demokrasia na Mfumo wa Vyama vingi Nchini

Tumepokea kwa MSHTUKO na masikitiko makubwa kauli ya Rais kwamba vyama vya siasa havipaswi kufanya siasa isipokuwa wakati wa Kampeni na kupitia bungeni. 

Kimsingi kauli ya Rais ni kauli yenye nia ya kuvunja Sheria ya Vyama vya siasa inayolinda uwepo wa mfumo wa vyama vingi na kuhimiza vyaMA vya siasa kufanya shughuli za siasa katika msimu wote ili kuthibitisha uhai wao.

Tunaichukulia kauli ya Rais kama tangazo la vita dhidi ya demokrasia na uhai wa vyama vingi nchini. Chama chetu kitaitisha vikao vya dharura kujadili hali ya siasa nchini na namna ya kukabiliana na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya demokrasia nchini mwetu.

Tunatoa wito kwa vyama vyote vya siasa vinavyoamini katika misingi ya demokrasia nchini kukutana haraka na kujadili namna ya kuunganisha nguvu pamoja katika kupigana vita mpya ya kulinda demokrasia nchini mwetu.

Aidha, tunatoa wito kwa wananchi wote na taasisi za kiraia kusimama imara katika kulinda demokrasia. Tunasisitiza kuwa ushahidi wa kisayansi duniani kote unaonyesha kuwa huwezi kuua demokrasia bila kuua juhudi za maendeleo. Tusiruhusu mtu yeyote mwenye mamlaka kuua demokrasia nchini mwetu.

Hatua zozote za kuua demokrasia ni kuua Umoja, Amani na Mshikamano wa wananchi na Taifa, ambayo ndiyo misingi ya maendeleo ya nchi yetu kijamii, kisiasa na kiuchumi. 

Tunatoa wito kwa wananchi wote kushikamana na kusimama imara katika kipindi hiki kigumu ili kulinda demokrasia.

Zitto Kabwe, MB
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Alhamisi, 23 Juni 2016.

Serikali Yamiliki Hisa Za TTCL Kwa Asilimia 100

$
0
0
Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) Dkt. Injinia Maria Sasabo akiishukuru kampuni ya Bharti Airtel kwa kuuza hisa 35 ili Serikali iweze kuendeleza mikakati yake ya kuimarisha TTCL. Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL (wa kwanza kulia) na Bwana Lawrence Mafuru, Msajili wa Hazina (wa kwanza kushoto) wakifuatilia tukio hilo.
********
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imefanya makabidhiano ya hati ya kuiwezesha Serikali Kumiliki Hisa za Kampuni ya TTCL kwa asilimia 100 ambapo hisa ailimia 35 zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Bharti Airtel.
 
Utiaji saini huo umefanyika baina ya Bwana Larewnce Mafuru, Msajili wa Hazina na Bwana Christian Manuel De Faria, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Afrika.
 
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2016 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kushuhudiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Dkt. Injinia Maria Sasabo, Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL na Dkt. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
 
Kabla ya tukio hilo la leo, Serikali kupitia TTCL ilikuwa ina miliki hisa hizo kwa alisimia 65 na Bharti Airtel kwa asilimia 35.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, 
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Serikali Yakanusha Madai Kuwa Haina Mpango wa Kuwapanga Vijana Waliohitimu Kidato cha Nne kwenda kidato cha Tano

$
0
0

Serikali imekanusha madai ya  kuwepo kwa taarifa ya kuwa haina mpango wa kuwapanga vijana waliohitimu kidato cha nne kwenda kidato cha tano kwa sababu mbalimbali.

Akiongea leo Bungeni Mjini Dodoma, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa taarifa hizo ni za uvumi na serikali kwa sasa ipo katika mchakato wa upangaji wa majina hayo na wakati wowote mwisho mwa mwezi majina yatakuwa yametolewa.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema moja ya sababu za kuchelewa kwa matokeo hayo ni pamoja na wizara kubadili mfumo wa GPA, kwenda Division hivyo mchakato huo ndio unafanywa na serikali ili wanafunzi wote wapate madaraja yao na waweze kupangiwa shule.

Mhe. Majaliwa amesema suala la upangaji halikuwa kwa kidato cha tano peke yake bali pia wale wanaokwenda vyuo mbalimbali na kusema kuwa baada ya kukamilika watatoa majibu yao wiki mbili kabla ili wazazi waweze kujiandaa kuwapeleka watoto mashuleni.

Magufuli: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Pumzika Kwa Amani.......Wewe upo Salama, Usisikilize kelele za Nje

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kwamba serikali itawalinda wastaafu nchini wakiongozwa na viongozi wakuu wa umma ili wawe na heshma yao ndani ya jamii.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kukabidhiwa ripoti ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa tume ya taifa ya uchaguzi.

''Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wewe pumzika kwa raha zako , upo salama watachonga wee lakini mimi kama Rais wa awamu ya tano nipo tayari kuwalinda watumishi wote wastaafu kwa kuthamini mchango wao ndani ya taifa hili''

Aidha Rais Magufuli amesisitiza kwamba uchaguzi nchini umemalizika hivyo vyama vyote vya siasa viongeze nguvu baada ya miaka mitano ili apimwe na wananchi waliomchagua kama ametekeleza ahadi zake.

''Niwaombe wanasiasa wenzangu uchaguzi umekwisha, kama ni wabunge jielekezeni bungeni, kama ni madiwani jielekezeni kwenye maeneo yenu, sitakubali mtu yeyote anikwamishe katika kutimiza ahadi zangu kwa wananchi'' Amesema Rais Magufuli.

Kuhusu tume ya uchaguzi kukabiliwa na changamoto lukuki Rais Dkt. Magufuli amesema fedha za tume hiyo ilizobakiza kiasi cha shilingi bilioni 12 na kuzirudisha serikalini, serikali imeruhusu fedha hizo zitumike kujenga jengo la tume hiyo ili kuondokana na gharama za kupangisha jengo wanalotumia kwa sasa.

Aidha akikabidhi ripoti hiyo kwa Rais Magufuli, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva amesema uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ulikuwa huru na wa haki na hata waangalizi wa nje wengi wamepongeza uchaguzi huo.

Alex Msama Amwangukia Mwakyembe Kumuomba Radhi Baada ya Gazeti la DIRA Analolimiliki Kuchapisha Habari Zenye Utata

$
0
0
MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba,  Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki.
 
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari.

Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo.

Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe.

Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo.

“Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari,  ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe, ninachukua nafasi hii kumuomba radhi nikiwa mmiliki wa gazeti hilo,” alisema Msama.

Aidha Msama alisema hatua nyingine anayochukua ni kumsimamisha kazi mhariri wa gazeti hilo, Mussa Mkama kwa kuwa alishindwa kufanya kazi yake kwa umakini ya kuhakikisha habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi wa habari na weledi.

Alisema Mkama alipaswa kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya hivyo kwa hiyo anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za kinidhamu zitafuata.

“Mimi ni mfanyabiashara sijui mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini atasimamia yale aliyofundishwa chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae pembeni kwanza,” alisisitiza Msama.

Ameahidi kuwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania litakalotoka Juni  27, kwa ukubwa uleule atamuomba radhi Waziri Mwakyembe.

Hivi karibuni  Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo  iliyochapishwa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la Juni 20 na la Juni 23 mwaka huu zililenga kumchafua na kuahidi kuwa atalishtaki kupitia habari hizo mbili.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya June 27

Rais Magufuli Alitaka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA Liombee Taifa Amani

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI amewahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- waendelee kuombea amani katika taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.
 
Kauli hiyo ya Rais imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN kwa niaba ya Rais katika tafrija ya futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania- BAKWATA- katika uwanja wa shule ya sekondari ya KINONDONI MUSLIM jijini Dar es Salaam.
 
Rais Magufuli amesema jamii yeyote inayolelewa na kukua katika misingi ya kufuata maandiko ya Mwenyezi Mungu ni vigumu kujiingiza kirahisi katika vitendo vinavyomchukiza Mungu vikiwemo vitendo vya uhalifu.

Rais MAGUFULI pia amewatakia kheri waumini wote wa dini ya kiislamu kote nchini katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
 
Kwa upande wake, Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh ABUBAKAR ZUBEIR ameipongeza serikali kwa hatua inazochukua katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa nchini na kusisisita kuwa Viongozi wa BAKWATA na wataendelea kushirikiana na serikali katika kukemea vitendo viovu katika jamii kama hatua ya kuhakikisha vitendo vya uhalifu vinakoma hapa nchini.

Mufti wa Tanzania pia ametoa rai kwa waislamu wote nchini wadumishe umoja,upendo na mshikamano miongoni mwao katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya mfungo kama kitabu kitukufu cha QUR’AN kinavyoelekeza.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais. 

Afariki Dunia Baada ya Kunywa GONGO Kupita Kiasi

$
0
0

MKAZI wa Mondo katika Kijiji cha Kitumba wilayani Magu, Wilson Magola (45), amekufa baada ya kunywa pombe haramu ya gongo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa, tukio hilo lilitokea Juni 23, mwaka huu, saa 8:00 mchana kitongojini humo.

Msangi alieleza kuwa, baada ya kufika nyumbani kwa Daudi Mtula anayeuza gongo kwa siri Magola alikunywa pombe hiyo kupita kiasi akaishiwa nguvu na kupoteza maisha.

“Mtu huyo pia alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa,” Kamanda Msangi alisema na kuongeza kuwa, baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitoroka na kuuacha mwili wa marehemu nyumbani kwake.

Alisema kuwa Polisi inamtafuta kwa ajili ya kumchukulia hatua za kisheria. 

“Tulipata taarifa kutoka kwa raia mwema na tulipofika nyumbani kwa mtuhumiwa tuliupata mwili na tayari umekwishafanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa familia kwa ajili ya maziko,” alisema.

Alitoa wito kwa wananchi kuiunga Polisi mkono kudhibiti biashara ya pombe hiyo haramu.

CHADEMA Watafakari Hatua za Kuchukua Baada ya Rais Magufuli Kutaka Siasa Zifanywe 2020 ( wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao )

$
0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani kimesema kinatafakari hatua gani ya kuchukua baada ya Rais John Magufuli kutaka siasa za nguvu zifanywe wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao, kauli inayotafsiriwa kuwa ni kupiga marufuku shughuli za kisiasa. 

Rais alitoa kauli hiyo mapema wiki iliyopita wakati akipokea taarifa ya Uchaguzi Mkuu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kuisisitizia juzi wakati wa hafla ya kuzindua mpango wa polisi wa kuboresha huduma za usalama wa jamii. 

Akizungumza jana ofisini kwake jijini Dar es Salaam, katibu wa Chadema wa kanda hiyo, Casmir Mabina alisema wamefikia azimio la kupinga unyanyasaji na ukandamizaji kwa vyama vya siasa unaofanywa na Serikali ya Dk Magufuli. 

Mabina alisema Rais Magufuli anavunja Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 ambayo inaviruhusu vyama vya siasa kuendesha shughuli mbalimbali za kisiasa. 

Alisema vyama haviwezi kukaa kimya mpaka mwaka 2020 wakati kazi yao ni kukutana na wananchi. 

“Tunamshauri Rais Magufuli aache kutawala nchi kwa woga na ubabe ... afuate misingi ya Katiba na sheria, na kuwaongoza Watanzania badala ya kuwatawala,” alisema Mabina. 
 
Mabina aliongeza kuwa Jeshi la Polisi liache kutumiwa na Serikali kufinyanga sheria za nchi na kukandamiza upinzani kwa kutumia vibaya Sheria ya Jeshi la Polisi, kifungu cha 43 (3) kwa kusingizia habari za ‘kiintelijensia’ na ‘hali ya uvunjifu wa amani’. 

Mwenyekiti wa Chadema wa Kanda ya Dar es Salaam Kuu, Mwita Waitara alilalamikia kitendo cha mameya wa Dar es Salaam kunyimwa vibali vya kwenda nje ya nchi kutafuta fedha ili kusaidia maendeleo ya halmashauri zao. 

Alisema fedha za safari hizo zinatolewa na washirika wa maendeleo, lakini Serikali imekuwa ikizuia safari hizo kwa kisingizio cha kubana matumizi. 

Alisema safari nyingine za nje ni muhimu kwa sababu zinawawezesha mameya kukutana na wadau wa maendeleo ili kupata misaada. 

 “Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob alikuwa na safari ya kwenda Afrika Kusini kukutana na mameya wengine duniani, lakini alizuiliwa kwa maelekezo. 

"Hatuwezi kuendelea kama tutashindwa kukaa na wenzetu ili kujifunza mambo ya maendeleo,” alisema.

Mwita alidai kuwa huo ni mpango wa Serikali kudhoofidha halmashauri zinazoongozwa na upinzani ili wasiweze kufanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kufanywa na CCM. 

Alisema yeye pia alizuiliwa kwenda Marekani akiwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii. 

Ushauri mwingine ulitolewa na mwenyekiti wa Kanda ya Ilala, Dk Makongoro Mahanga ambaye alimtaka Rais kufuata Katiba kwa sababu aliapa kuilinda na kuitetea kwa masilahi ya Taifa. 

Dk Mahanga alimtaka Rais akumbuke ahadi mbili alizozitoa wakati wa kampeni na wakati anaapishwa, ambazo ni kuilinda Katiba na kuwaletea wananchi maendeleo. 

“Kinachowaogopesha CCM ni upinzani kupata kura zaidi ya milioni sita wakati wa uchaguzi. Wanajua kwamba wanaweza kuchukua nchi, ndiyo maana wameanza kudhibiti vyama vya siasa ili visiwe na nguvu,” alisema Dk Makongoro ambaye aliwahi kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo

$
0
0
Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo kuanzia jana. 

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema Rais amemteua Dk Charles Mlingwa ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Siha kujaza nafasi hiyo. 

Mulongo anakuwa mkuu wa mkoa wa pili kutimuliwa kazi na Rais Magufuli baada ya Anne Kilango Malecela aliyekuwa Shinyanga.

Hata hivyo, tofauti na Kilango ambaye alitimuliwa kutokana na kutoa taarifa potofu kuhusu watumishi hewa mkoani mwake, Ikulu haikutoa sababu za kutenguliwa kwa uteuzi wa Mulongo.

Mulongo ameondolewa madarakani miezi sita baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dk Faisal Issa baada ya kutofautiana na Mulongo wakati huo akiwa mkuu wa mkoa huo.

Baada ya kumwondoa Dk Issa na nafasi yake kujazwa na aliyekuwa Kamishna wa Polisi, Fedha na Utawala (CP) Clodwig Mtweve, miezi miwili baadaye Rais alimbadilisha Mulongo kituo cha kazi akimhamishia Mara.

Alipoulizwa jana jinsi alivyoipokea hatua hiyo iliyochukuliwa dhidi yake Mulongo alisema: “Sina taarifa rasmi.” 

Kabla kuhamishiwa Mara akitokea Mwanza, Mulongo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Alishika nafasi hiyo baada ya kupandishwa cheo akiwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.

Dk. Mbassa wa Chadema afariki dunia akiwa usingizini

$
0
0

ALIYEKUWA Mbunge wa   Biharamulo Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Anthony Mbassa alifariki dunia jana usiku  akiwa usingizini nyumbani kwake.
 
Taarifa zilizopatikana kutoka Biharamulo na kuthibitishwa na Msemaji wa familia, Pendo Ngonyani, zilieleza kuwa kifo cha Dk. Mbassa kilifahamika alfajiri ya jana.
 
Alisema  watoto walipokwenda kumuamsha hakuamka hali iliyowalazimu    kumuita mama yao ambaye aliwasiliana na madaktari wa Hospitali ya Biharamulo na kuthibitishwa kuwa alikuwa amefariki dunia.
 
Dk. Mbasa ambaye alikuwa mbunge   mwaka 2010 baada ya kushinda uchaguzi mkuu, hakurejea kwenye ubunge baada ya kuangushwa na mshindani wake, Oscar Mkasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2015.
 
Akizungumzia kifo hicho, Pendo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) Mkoa wa Kagera, alisema Dk. Mbassa alifariki dunia akiwa usingizini.
 
Pendo alisema  haijafahamika  sababu ya kifo chake ingawa familia imedokeza inataka uchunguzi ufanyike   kubaini sababu ya kifo hicho.
 
Kwa mujibu wa maelezo ya familia,   juzi mkewe akiwa kazini, yeye (Dk. Mbasa) alitoka na kurudi  jioni saa   12 na kuacha gari lake nyumbani na kwenda ambako   hakujajulikana.  Alirudi nyumbani   saa 5.00 usiku akiwa akionekana kuwa amelewa.
 
“Nimeelezwa kuwa baada ya kuacha gari alitoka kwa mguu kuanzia hiyo saa 12 na kurejea   yumbani saa 5.00 usiku.  Haijajulikana alikwenda wapi  lakini alirejea akiwa amekunywa alikuwa akihangaika na ilidhaniwa ni hali ya pombe, ndiyo hivyo asubuhi alikutwa akiwa amefariki dunia.
 
“Leo alikuwa na safari ya kwenda Bukoba   kuwasiliana na mawakili wake kwa ajili ya kushughulikia madai ya fidia ya  Sh milioni 60 za gharama za kesi namba 5/2010, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo hilo, Oscar Mkasa,” alisema.
 
Alisema kinachosubiriwa hivi sasa ni ndugu na jamaa   kupanga utaratibu wa maziko.

Waziri Mkuu alia na mauaji dhidi ya raia

$
0
0

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amekemea matukio ya mauji yanayoendelea nchini na kusema kuwa hakuna dini inayofundisha vitendo hivyo viovu.
 
Alisema serikali inawaomba viongozi wa dini nchini kuendelea kushirikiana nayo kutoa elimu kwa waumini wao kama njia ya kukomesha mauaji dhidi ya watu wasiokuwa na hatia nchini.
 
Akizungumza  Dar es Salaam jana katika fainali ya mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Koran nchini,   alisema   ni wajibu kwa Watanzania kushikana   kulinda amani ya nchi.
 
“Napenda nigusie mambo machache ambayo nimeyaona; ni hivi karibuni nchi yetu ilingia katika mtihani ambao wengi wenu kupitia vyombo vya habari mliarifiwa juu ya kuuawa kwa waumini wema waliokuwa wakifanya ibada ndani ya msikiti kule mkoani Mwanza.
 
“Katika siku za hivi karibu kumekuwa na matukio mabaya mbele ya macho yetu na nchi yetu imefika mahala hadi watu wanafuatwa majumbani na kuchinjwa  jambo ambalo kwetu sisi kama Serikali tuna kazi ya kulinda uhai wa kila Mtanzania.
 
“Linapotokea suala kama hili hatuwezi kula wala kulala mpaka tuone juhudi za dhati katika kukomesha unyama wa aina hii,” alisema Majaliwa.
 
Alisema Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama inaendelea kushughulikia tatizo hilo kwa umakini na akawataka Watanzania kuendelea kutoa ushirikiano.
 
Akizungumzia utendaji wa Serikali ya awamu ya tano, alisema watendaji wengi ni wapya  huku akiomba kukoselewa  inapokosea jambo ambalo litasaidia kujenga Serikali imara  na yenye mshikamano.
 
Mashindano hayo ya kuhifadhi Koran yalihusisha washiriki 21 kutoka mataifa mbalimbali duniani huku kijana, Rashid Ally (8) kutoka   Tajikistan akiibuka mshindi wa kwanza.

Meli ya mizigo yazama Bahari ya Hindi

$
0
0

MELI ya Mizigo ya Mv. Happy iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda  Zanzibar  imezama katika Bahari ya Hindi ikiwa imebeba mbao zaidi ya 1090 na magunia 450 ya viazi mviringo.
 
Hata hivyo,  mabaharia 12 ambao ni wafanyakazi katika meli ya mizigo  ya hiyo wamesalimika kufa maji  kwa vile meli hiyo  haikuzama yote  katika eneo la Kizingo  kisiwani Zanzibar.
 
Tukio hilo lilitokea jana alfajiri kisiwani Unguja. Mkuu wa Operesheni baharini, Msilimiwa Idd,  alisema tukio hilo lilitokea saa 8.00 usiku baada ya meli hiyo kuyumba kutokana na dhoruba kali ya upepo.
 
Alisema ilipotimu saa saa 9.00usiku nahodha wa meli hiyo alipoona hali imezidi kuwa mbaya akaelekea katika Kisiwa Mchanga  ambako alijikuta akikwama kwa vile upande mmoja wa meli ulikuwa unapitisha maji.

Aliyeondolewa Ukuu wa wilaya Lushoto ajitetea,adai hakubebwa.

$
0
0
Siku moja baada ya Rais John Pombe Magufuli kutangaza upya nafasi za wakuu wapya wa wilaya nchini, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Lushoto mwenye umri mdogo kuliko wenzake ambaye jina lake limeondolewa katika orodha hiyo Mariam Juma,amedai kuwa nafasi aliyokuwa ameipata sio kwamba alichaguliwa kwa upendeleo,na badala yake elimu ndio iliyosababisha kupata hadhi ya kumuwakilisha Rais wa awamu ya nne.
 
Amezungumza hayo na wazazi,viongozi wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,pamoja na viongozi wa serikali ngazi ya wilaya katika harambee ya kuchangia maendeleo katika chuo cha mafunzo ya ujasiriamali kilichopo vuga wilayani Lushoto.

Awali akielezea shughuli zinazofanywa katika Chuo maalum cha kujifunza ujasiriamali ikiwemo kutengeneza mizinga ya nyuki kwa kutumia udongo wa mfanyanzi,elimu ya mazingira pamoja na kilimo cha mboga mboga ili kuwapunguzia vijana changamoto za maisha,Mkuu wa chuo hicho Mchungaji Yohana Mmaka amesema elimu ya ujasiriamali imekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwawezesha vijana kujitambua.

Kufuatia hatua hiyo,diwani wa kata ya Vuga wilayani Lushoto Jumaa Dhahabu,ameiomba serikali kuu kuwahisha mafungu ya fedha za shughuli za maendeleo katika halmashauri ya wilaya hiyo,kufuatia miradi tofauti ikiwemo ujenzi wa maabara iliyoanzishwa na rais wa awamu ya nne kusitishwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kumuwakilisha Rais Magufuli Kesho Botwasana

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo Juni 27 kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini  mwa Afrika wa Double Troika ya Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama (SADC Double Troika Summit)   utakaofanyika kesho Juni 28, 2016.

Mhe. Waziri Mkuu anamuwakilisha Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Gaborone (GICC).

Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Botswana Mhe. Lt. Jen. Seretse Khama Ian Khama ambaye ni SADC, utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Lesotho. Mkutano huu   utatanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu ambao utafanyika leo.

Pia mkutano huo utahudhuriwa na Marais wa Afrika Kusini, Mwenyekiti aliyetoka (outgoing chair) wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama Mhe. Jacob Zuma , Mhe. Jacinto Filipe Nyusi, Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama.

Wengine ni Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Robert Mugabe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe na Mwenyekiti anayeondoka wa SADC.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Aziz Mlima na Maofisa wengine waandamizi.

Kitwanga Akabidhi Rasmi Ofisi Kwa Waziri Mwigulu Nchemba, Jijini Dar Es Salaam Leo.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto meza kuu) akimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga alipokuwa anazungumza na Waziri huyo pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano ofisini humo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili kulia) alipokuwa anazungumza kabla ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (wa tatu kulia) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) mara baada ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (katikati) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto), aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga wakifurahi jambo mara baada ya Waziri Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano katika tukio lililofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (wa pili kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. 
 
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Watuhumiwa wa Mauaji Jijini Mwanza na Tanga Wauawa Dar es Salaam

$
0
0
MTU mmoja anayedaiwa kuhusika katika mauaji yaliyotokea katika Msikiti wa Rahma, jijini Mwanza ameuawa.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam leo limeeleza kumuua Salum Saidi Muhangwa (30) kwa madai ya kuwa miongoni mwa waliofanya mauaji kwenye msikiti huo.

Akizungumza na wanahabari Simon Siro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema, mtu huyo ameuawa leo asubuhi wakati akijaribu kuwakimbia polisi kupitia dirishani.

“Baada ya kufanya mauaji kule Mwanza na kikundi chake walikimbilia huku Dar es Salaam, taarifa za raia wema zimetuonesha jambazi huyo alikua anaishi Buguruni,” amesema.

Mauaji hayo yalifanyika tarehe 19 Mei mwaka huu katika msikiti huo uliopo kwenye Kata ya Mkolani wilayani Nyamagana ambapo watu watatu, waumini wa msikiti huo waliuawa wakati mwingine mmoja  akijeruhiwa.

Kamanda Sirro amesema, mtu huo baada ya kugundua kuwa askari wamezunguka jengo alilokuwemo, alijaribu kujihami kwa kuwarushia askari bomu la mkono ambapo askari walifanikiwa kumpiga risasi ya mguu hatimaye kufariki wakati akipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

“Tunashukuru askari hawakufanywa lolote katika tukio hilo na tunashukuru kwa sababu wapo makini,”amesema Kamanda Sirro.

Hata hivyo amesema, mtu huyo amefanya matukio mengi pale Mwanza yakiwemo kufanya unyang’anyi katika vituo vya M-Pesa, Tigo Pesa, uchinjaji watu msikitini pamoja na maduka makubwa.

“Kuna timu yake imebaki hapa Dar es Salaam lakini tuwahakikishie wana Dar es Salaam kwamba, tutawakamata na haki itatendeka lakini wakikaa vibaya wasilaumu serikali.

“Kwa sababu silaha wanazozitumia hawajanunua madukani, wanakaa nazo visivyokua halali wabadilike wawe raia wema itawasaidia lakini kwa staili hii niwaambie wataacha familia zao kwa sababu ukamataji wa mtu mwenye silaha sisi ndio tunajua namna ya kukamata,”amesema.

Katika tukio jingine, Jeshi hilo limefanikiwa kumkamata jambazi sugu aliyefahamika kwa jina la Mohamed Abdallah akiwa na bastora aina ya nolinko, risasi 19 na bomu la kutupa kwa mkono.

“Baada ya kufanya mauaji Tanga na kikundi chake walikimbilia hapa Dar es Salaam, naye akachomoka na kuanza kupambana na polisi, na askari wetu waliweza kumjeruhi vibaya sana naye wakati akipelekwa hospitali alifariki dunia."

Kamanda Siro amesema mtu huyo ni kiongozi mkubwa aliyebaki katika kundi la majambazi mkoani Tanga na amehusika katika mauaji ya watu wanane pamoja na  ujambazi uliofanyika katika kituo cha mafuta mjini humo.

“Wananchi na hasa raia wema waendelee kutupa taarifa kwa watu wanaowatilia mashaka,” amesema.

Wananchi Watinga Mahakamani Kufungua Kesi ya Kupinga Agizo la Serikali Kuzuia Matangazo ya Moja kwa Moja ya Bunge

$
0
0
HATUA ya serikali kuzuia kurusha moja kwa moja mjadala wa vikao vya Bunge kama ilivyokuwa awali, bado inaumiza wananchi.
 
Safari hii wananchi wametinga mahakamani na kwamba leo wamefika katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kufungua kesi ya kuitaka mahakama hiyo kutengua agizo la serikali la kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Januari mwaka huu, Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Michezo na Sanaa alilieleza Bunge hatua ya kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya chombo hicho kama ilivyokuwa awali.

Miongoni mwa sababu alizotoa ni kwamba, serikali imekuwa ikibeba mzigo mkubwa wa gharama katika kuendesha matangazo hayo pia watumishi wa umma kutumia muda mwingi kuangalia Bunge badala ya kufanya kazi.

Hatua ya serikali kuzuia kurusha matangazo hayo ya moja kwa moja imeibua mjadala mkubwa kitaifa ambapo kada mbalimbali nchini zimekuwa zikipinga hatua hiyo.

Katika kesi iliyofunguliwa leo, ina walalamikaji 10 ambao ni Azizi Himbuka, Perfect Mwasililwa, Rose Moshi, Penina Nkiya, Andrew Mandari, Hilda Sigara, Juma Uloleulole, Kubra Manzi, Ray Kimbito na Ben-Rabiu Saanane.

Kesi hiyo imesikilizwa na Profesa Ferdinand Wambari, Jaji Kiongozi katika mahakama hiyo, na jaji mwengine katika kesi hiyo Sakieti  Kihiyo, hata hivyo hakuwepo mahakamani leo.

Washtakiwa kwenye kesi hiyo ni Nape pamoja na George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambapo Abubakari Mrisho, ndio wakili wa upande wa walalamikiwa.

Kwa upande wa walalamikaji unasimamiwa na Peter Kibatala na Omari Msemo ambao ni mawakili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Kesi ya msingi iliyofunguliwa ni kuitaka mahakama kutengua uamuzi uliotolewa na Nape ambaye aliwasilisha kauli ya serikali bungeni.

Walalamikaji wanaitaka mahakama itangaze kuwa, Raia wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wana haki ya kikatiba ya kujua majadiliano yanayoendelea bungeni kwa mujibu wa ibara ya 18(B), (d) na 29 (1).

Pili walalamikaji wamedai kuwa, serikali imekiuka haki ya kikatiba kwa kuzuia bila kuwa na sababu za msingi haki ya wananchi kusikia majadiliano ya Bunge kwa kuzuia kurusha matangazo ya moja kwa moja.

Tatu, walalamikaji wameitaka mahakama kuilekeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurejesha haki ya kikatiba ya wananchi kwa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Nne, walalamikaji wamedai kuwa, matokeo ya kuzuia matangazo hayo ni kunyimwa kwa haki za Watanzania kutokana na kushindwa kuwasimamia pia kuwafuatilia wabunge na mwenendo wao bungeni.

Tano, walalamikaji hao wamedai kuwa, sababu za kuzuia matangazo hayo hazijitoshelezi hivyo Watanzania na walalamikaji wanayo haki ya kupata taarifa ya vikao vya Bunge  kwa maslahi ya taifa.

Hata hivyo upande wa utetezi ulidai kuwa, walichelewa kupata taarifa ya mashtaka hayo hivyo hawakupata muda wa kutosha wa kuaandaa majibu. Kutokana na hivyo, mahakama iliuambia upande wa walalamikiwa kwamba, watajibu mashtaka hayo 15 Julai siku ambayo kesi hiyo itatajwa.

Serikali: “Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria ya Tanzania”

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Amon Mpanju amesema kuwa mapenzi ya jinsia moja hayakubaliki na Serikali ilishaweka msimamo wake katika hilo.

Akizungumza mapema leo katika mkutano wa wadau wa haki za binadamu uliofanyika katika hoteli ya Blue Pearl wa kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu (Universal Periodic Review), Mhe. Mpanju ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo alisema  mapendekezo yaliyowasilishwa Mwezi Mei mwaka huu katika mkutano wa Baraza la haki za binadamu uliofanyika Geneva, serikali ilikubali mapendekezo Mia thelathini (130) na mengine 72 iliyakataa.

“Sehemu ya mapendekezo hayo serikali iliyakataa kwa sababu kuna mengine yapo kinyume na katiba, sheria, mila na desturi zetu, kwani katika mapendekezo hayo yapo yanayotaka mapenzi ya jinsia moja jambo ambalo haliwezi kukubalika”, Mhe. Mpanju alisema

“Hivyo wakati mkijadili namna ya kupanga mikakati ya utekelezaji ili serikali ione umuhimu wa kukubali sehemu ya mapendekezo hayo naomba msijielekeze kwenye yale yaliyo kinyume na imani”, Mhe. Mpanju alisisitiza 

Aidha, Mhe. Naibu Katibu huyo alisema serikali imefungua milango kwa kushirikiano na tume, wadau wa haki za binadamu wapeleke serikalini  sababu zenye mantiki ili kuona ni mambo gani  ambayo serikali inaweza  kuyashugulikia na kuyatekeleza.

Akizungumza katika Mkutano huo, Bwana Onesmo Olengurumwa kutoka taasisi ya watetezi wa haki za binadamu (THRDC) alisema kuwa wadau wamekutana katika mkutano huo   kujadili ni kwa namna gani wataishawishi serikali ili iweze kuyakubali mapendekezo yaliyobakia na kuyaweka katika utekelezaji.

Akifungua mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Iddi Mapuri alisema kuwa mkutano huo umelenga katika kuweka mikakati ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo hayo na alipongeza mchango mkubwa unaotolewa na wadau wa haki za binadamu katika kuhakikisha masuala ya haki za binadamu yanapata msukumo mkubwa hapa nchini.


Bwana Onesmo Olengurumwa (aliyevaa koti la Drafti) kutoka taasisi ya watetezi wa haki za binadamu (THRDC) akijadiliana jambo na Mkurugenzi  wa Idara ya huduma za sheria wa Tume ya Haki za Binadamu, Bwana Nabor Assey( aliyevaa shati la bluu). Nyuma yao ni Bwana Laurent Burilo burilo, Mratibu wa Mpango kazi wa Haki za Binadamu(katikati) na Bwana Deugratius Bwire kutoka (THRDC


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Amon Mpanju (aliyevaa miwani) akiteta jambo na Bwana Onesmo Olengurumwa (aliyevaa koti la Drafti) kutoka taasisi ya watetezi wa haki za binadamu (THRDC) katika mkutano huo wa  kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu na kuweka mikakati ya kuishawishi serikali kukubali mapendekezo mengine ambayo iliyakataa.

Sehemu ya wadau wa haki za binadamu wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo wa kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya June 28

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images