Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

VIDEO: Msanii Ray C Apewa Msaada na Jeshi la Polisi ya Baada Kuzidisha Madawa ya Kulevya

0
0

Msanii wa muziki Rehema Chalamila a.k.a Ray C usiku wa jana alikamatwa na jeshi la polisi maeneo ya Kinondoni Manyanya almaarufu ‘Kinondoni kwa Mpemba’ jijini Dar es salaam baada ya  kuzidisha madawa ya kulevya na kuanza kupiga makelele barabarani akidai anataka kutekwa huku akitishia kuvua nguo.

Habari zinadai kuwa mama yake mzazi amekuwa akikesha kumtafuta mrembo huyo kutokana na kuzama kwenye vijiwe vya mateja wa madawa hayo na kushindwa kuonekana nyumbani.

Sambamba na hilo siku za hivi karibuni mwanamuziki Jay Dee, alionekana kuwa naye karibu na kudai kuwa Ray C, anahitaji marafiki wazuri na watu wavumilivu kuweza kumsaidia kwani kumlaumu pekee hakuwezi kumjenga bali ni kuzidi kumharibu kisaikolojia.

Mmoja wa wasanii wa Bongo Movie, Esha Buheti, kupitia mtandao wa kijamii ameweza kueleza jinsi gani alivyoguswa baada ya kumuoa Ray C akiwa chini ya ulinzi wa polisi akiwa hajitambui na kuongea maneno yasiyoeleweka na kudai kuwa awali alijua mrembo huyo anasingiziwa tuu.

Ameandika “Nashindwa hata niongee nini jamani, Ray C leo Kinondoni umenitoa machozi, jamani tufanye kitu tumsaidie Ray C, I mean it jamani siku zote nlikuwa najua anaonewa ila nilichokishuhudia leo nimeumia kutoka moyoni amedhalilika mwanamke mwenzetu, jamani tufanyeje?”

Akaendelea “Nilikua na Kabula, Kinondono kwa wapemba tumefuata chips mara tukasikia mtu anasema me Ray C nataka kuvua nguo, nikajua utani kushuka ni Ray C anasema nishikeni kuna watu wanataka kuniteka, alikuwa na nguvu sana watu kumshika akaanza kuongea vitu havieleweki, akaanza kutafuta kisu ajichome, watu walimzuia sana walishindwa akaanza kugaragara kwenye matope akipiga kelele,”

“Kiukweli nilijikuta nalia mara ikaja gari ya polisi ikambeba ila kwa tabu sana alikua akipiga kelele jamani nisaidieni msiniache kiukweli mpaka Ray C anaondoka na ile gari ya polisi sikujua anapelekwa wapi alikuwa kama mtu alopata kichaa, YARRAB TUNAMSAIDIAJE RAYC?”

Baada ya ujumbe huo, aliamua kupost video tena na kuandika:
"Ray C hastahili haya jamani kweli Leo hii anafikia hatua hii? Najua hajitambui ila tumfikirie mwanamke mwenzetu ambae ni mamaake, anajiskiaje? Rayc nn kimekupata ? Hiii video inasambaa kila sehem kweli huyu ndo RAYC AMBAE NI NEMBO YA TAIFA? Plz tumsaidie manake tusimhukumu? MBONA sisi kila siku mungu tunamkosea na hesabu makosa yetu? 

"We need to do something jamani @tzshaderoom @mangekimambi_ @divathebawse @babutale @ @mwanafa @linexsundaymjeda @paulmakonda naomba tumstiri huyu mtu plz plz @lisa_fickenscher ( tunafanyaje kumsaidia jamani tusichoke me natamani aende rehab mwaka mzima) 

"Leo rayc umedhalilika najua haikua akili yako mama DAAAAH hata sijui amepelekwa wapi maskini 😢😢 atakua amelala wapi? Vipi kuhusu kesho Yake? Mamaake anajiskiaje? 

"Inaumaa jamani tusikubali kumpoteza huyu dada nawaombaa 🙏🙏🙏 tusaidiane  @rayc1982 my love kama hauko sawa jamani ongea na watz wapo tayari kujitolea kwa hali na mali my love"


PPFT : Gwajima Afutiwe usajili kwa kutoa kauli za uchochezi.

0
0

Ushirika wa wachungaji wa Kanisa la Kipentekoste Tanzania (PPFT)umeiomba serikali ifute usajili wa Kanisa la Ufufuo wa uzima la Askofu Josephat Gwajima kwa kukiuka maadili ya kanisa kwa kutoa kauli za uchochezi na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.
 
Mwenyekiti wa ushirika wa wachungaji hao Askofu Pius Ikongo mwenye makao yake katika Halmashauri ya wilaya ya Mwanga amesema,kauli hizo zinaweza kubadili fikra za wananchi na kuzaa chuki dhidi ya serikali yao na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

Askofu Ikongo ametoa tamko hilo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kueleza kuwa kitendo kilichofanywa na Askofu Gwajima kinapaswa kulaaniwa na wapenda amani wote waliopo ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti huyo wa ppft amesema, kosa kubwa ambalo limewaumiza wachungaji wa Kipentekoste ni kitendo cha Askofu Gwajima kutumia Kanisa kama jukwaa la kisiasa kwa kuleta uchonganishi kati ya serikali ya awamu ya nne na iliyopo madarakani.

Mgeja Ataka Rais Mstaafu Benjamin Mkapa Naye Ashitakiwe

0
0
MKURUGENZI wa Taasisi ya Tanzania na Maendeleo, Khamis Mgeja, amesema Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, anapaswa kuwa mtuhumiwa wa kwanza kupandishwa kizimbani katika mahakama ya mafisadi inayotarajiwa kuanzishwa Julai mwaka huu.

Amesema kiongozi huyo ndiye alihusika na kuisababishia hasara Serikali ikiwamo kuota   mizizi ya ufisadi serikalini.

Mgeja  amesema  pia kuwa Rais Dk. John Magufuli, anapaswa kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya au kufanya marekebisho ya haraka katika baadhi ya sheria zinazowalinda viongozi kama njia ya kuondoa mfumo unaokumbatia wahalifu.

Hayo aliyasema   Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema  Rais  Magufuli akiamua kutenda haki katika kuwawajibisha mafisadi na wahujumu uchumi  anapaswa kuanza na Rais Mkapa.

“Juzi,  Mkapa tumemsikia kwenye mdahalo anaomba radhi, angekuwa muungwana  angeenda mahakamani kwa makosa aliyowatendea watanzania, tunamuomba rais Magufuli  aanze kumshughulikia Mkapa  kupitia mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi   aimbie dunia makosa aliyoyafanya.

“Mkapa ni jipu ila limekaa pabaya ikiwezekana rais asaidiwe,” alisema Mgeja.

Mgeja   alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Shinyanga kabla ya kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka  2015.

Alisema Rais mstaafu Mkapa ndiyo chanzo cha nchi kuwa maskini kwa kuwa  aliuza rasilimali kwa bei ya kutupwa   na kuruhusu ubinafsishwaji  holela nchini.

“Utetezi anaoendelea kuutoa kwa wananchi majukwaani baada ya kutoka madarakani  haujitoshelezi kwa kuwa  makosa aliyoyafanya ni mazito, angekuwa muungwana angeenda mahakamani kutuomba radhi,” alisema Mgeja.

Alisema  taasisi hiyo haimani kama Mkapa alifanya mambo hayo kwa bahati mbaya  kwa kuwa alikuwa akitoa uamuzi kupitia Ikulu ambayo ni taasisi yenye wataalamu ambao wangeweza kumshauri vizuri au hata kumzuia.

“NBC kaiuza kwa Sh bilioni 16 wakati ilikuwa na mali ya zaidi ya Sh bilioni 100 …  wakati anatoa uamuzi  huo alikuwa mzima au alikuwa amejitwanga (kulewa) kwa sababu ni mwanachama mzuri wa hiyo kitu,” alisema Mgeja.

Akizungumzia uamuzi wa aliyekuwa mmoja wa wanachama wa Chadema, Goodluck ole Medeye kuhamia UDP,  alisema   mpaka sasa anaona Chadema ndiyo chama pekee cha upinzani ambacho kina nguvu  ya kuondoa CCM katika dola.

CUF Yamtega Lipumba .......Yamtaka Achukue Upya Fomu za Kugombea Uenyekiti wa CUF

0
0

CHAMA cha wananchi CUF kimesema mkutano mkuu wa taifa ambao unategemewa kumpata Mwenyekiti wa chama hicho, upo pale pale, na kuweka msimamo kuhusu Ibrahimu Lipuma kuwa kama anataka kurejea katika nafasi yake achukue fomu.

Tamko hilo ni kufuatia sintofahamu kwa wanachama wa chama hicho kuwa huenda mkutano mkuu usiwepo kutokana na ujio wa ghafla wa Prof. Ibrahim Lipumba aliyekua Mwenyekiti wa chama ambaye alijihudhuru cheo hicho.

Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho amesema tayari fomu za ugombea zimeshapelekwa katika ofisi ya wilaya tayari kwa kujazwa.

“kuanzia 1 Julai washiriki katika ngazi ya Mbali mbali ikiwemo Mwenyekiti wa chama pamoja na Makamu mwenyekiti wachama hicho na wataanza kuchukua fomu hadi Julai 20,” amesema.

Amesema, 21 Agosti baada ya zoezi la ujazaji fomu kukamilika, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho Kitaifa watakaa kuchagua viongozi hao katika ukumbi wa Land Mark Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Lipumba alijihudhuru katika kipindi cha uchaguzi Mkuu 25 Oktoba kutokana na sababu aliyoitoa kuwa ni uwepo wa aliyekua Mgombea urais, Edward Lowassa kuwa alihamia kwenye chama kwa kutofuata utaratibu.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema kutokana na katiba ya chama, Lipumba hatakiwi kurudi katika nafasi hiyo kwa kutengua kujiuzulu kwake isipokuwa kama anahitaji nafasi hiyo achukue fomu upya kugombea nafasi hiyo katika Mkutano Mkuu wa Taifa

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamisi ya June 18

Simu FEKI 600,000 Zazimwa.....TCRA Yaendelea Kusaka Zingine

0
0

Uzimaji wa Imei bandia ulifanyika usiku wa kuamkia jana kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika simu zaidi ya 600,000 zenye Imei batili. 

Kwa mujibu wa TCRA, Imei ni namba ya kimataifa ya utambuzi wa vifaa vya kielektroniki, ikiwamo simu. Ina tarakimu 15 ambazo ni za kipekee kwa kifaa husika na zinatambulika kimataifa. Namba hizo hutumika kudhibiti bidhaa bandia au simu kutumiwa na mtu mwingine. 

Jana, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alisema takwimu hizo ni zile ambazo zimetokana na kazi ya kukata mawasiliano katika simu bandia iliyofanyika kuanzia saa sita usiku mpaka saa kumi alfajiri ya jana. 

Alisisitiza kuwa mtambo huo unaendelea na kazi kuhakikisha kuwa hata simu ambazo hazipo au hazikuwa hewani zitakapowashwa hazitafanya kazi. 

“Kazi ya kuzima simu hizo ilianza usiku wa kumkia jana saa sita usiku na kila kampuni ya mtandao wa simu ilipaswa kuzima simu za wateja wake ambazo ni feki na kazi ya mtambo ni kuhakikisha simu iliyozimwa inapowekewa kadi ya mtandao mwingine haifanyi kazi na kuhakikisha simu zote feki zitakazoingia nchini hazifanyi kazi,” alisema Mungy. 

Hata hivyo, kuna baadhi ya wamiliki wa simu ambao walitilia shaka ufanisi wa mtambo huo kwa madai kuwa tayari walishathibitishiwa na TCRA kwamba simu zao ni feki, lakini bado zinafanya kazi. 

“Simu yangu mimi niliangalia nikaambiwa ni feki na niibadilishe kabla ya tarehe 16 Juni, lakini jana wamezizima feki ya kwangu bado inafanya kazi kama kawaida napiga na kupokea simu kama zamani,” alisema Nael Joseph. 

Kuhusu suala hilo, Mungy alisema: “Hoja hizo zimejitokeza kwa wingi na wengine walifikia hatua ya kuushutumu mtambo wetu kuwa ni feki na kuwa umeshindwa kuzima simu feki ukazima orijino, lakini ukweli ni kwamba mtambo ule hauzimi kama taa au kama ule uliozima matumizi ya analojia bali unazima taratibu

"Niweke sawa kwamba mtambo huu hauonei mtu na unazima simu zote zilizo feki.” 

Mungy aliongeza kuwa wengi wamekuwa hawaelewi mantiki ya ujumbe wa uthibitisho.Alisema ujumbe unamtaka mmliki wa simu kuoanisha jina linalotajwa kama ndilo jina halisi la simu yake. “Kama jina linalotajwa na Imei linaoana na lililoandikwa kwenye simu yako, basi sio feki, lakini majina yakiwa hayafanani ndipo simu inakuwa feki,” alifafanua. 

Vodacom wazungumza 
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom, Rosalynn Mworia alisema walipewa jukumu la kuzima simu feki za wateja wao na TCRA.

“Jana saa sita usiku tulitekeleza agizo kama lilivyotolewa na TCRA na inavyoonekana wengi wao walikuwa wamejipanga kwani simu nyingi zimezimwa, lakini baadhi wamerejea hewani japokuwa wapo ambao mpaka sasa hawajarudi,” alisema Mworia . 

Gwajima Atoweka.......Polisi Waendelea Kumsaka Usiku na Mchana

0
0
Baada ya kuweka kambi kwa zaidi ya saa saba nyumbani kwa Askofu Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Jeshi la Polisi limesema bado linamsaka kiongozi huyo wa kiroho usiku na mchana.

Juzi askari wa jeshi hilo, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam walishinda mbele ya geti la nyumba ya askofu huyo kwa zaidi ya muda huo bila kufunguliwa na kuondoka bila kumkamata, hiyo ikiwa ni mara ya pili kwa chombo hicho cha dola kufanya hivyo katika kipindi cha miezi 16.

Baada ya kushindwa kumtia nguvuni mapema mwaka jana, Askofu Gwajima alijisalimisha kituoni siku iliyofuata.

Lakini jana, Gwajima hakufanya hivyo,  na haijulikani alipo. Kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema wanaendelea kumtafuta askofu huyo na kuwataka wenye taarifa za mahali aliko, waisaidie polisi.

Akieleza sababu za kwenda nyumbani kwake bila ya kumtaarifu askofu huyo, Kamanda Sirro alisema hawalazimiki.

“Si lazima apelekewe taarifa, askari walikwenda kwa nia njema ya kuonana naye ndiyo maana hawakutoa taarifa,” alisema Sirro na kuongeza: “Kama amejificha, tukimbaini alipo tutamkamata na atambue bado tunamtafuta.”

Askofu Gwajima anatafutwa na polisi katika kipindi ambacho mkanda unaodhaniwa una sauti yake, umezagaa kwenye mitandao ya jamii.

Sauti kwenye mkanda huo inasema Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika wakati wa utawala wake ambayo rais wa sasa, John Magufuli anayashughulikia.

Pia, sauti hiyo inadai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM wametuma watu mikoani kupiga kampeni ya kutaka Magufuli asipewe uongozi wa chama hicho kwa sasa kama ilivyo utaratibu wa chama hicho.

Wakizungumza  kwa sharti la kutotajwa majina yao kwa kile walichodai si wasemaji wa familia wala kanisa, watu wa karibu na askofu huyo walisema wanashangaa kuona polisi wanamtafuta bila kufuata taratibu kama kumuandikia barua.

Mmoja wa watu hao alisema hadi sasa wanashindwa kufahamu kama waliokuja kwa askofu ni askari kama inavyoelezwa au majambazi kwa sababu hawakuwa na sare wala vitambulisho.

Alisema sababu anayotafutiwa Gwajima ni kukinanga chama, wanaomtafuta ni wana usalama ambao hawatakiwi kuwa na chama kitu ambacho kinatia shaka.

Makachero Watumwa Mwanza na Arusha Kuchunguza Mauaji ya dada wa bilionea Msuya

0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam limetuma timu ya maofisa wake kwenda mikoa ya Arusha na Mwanza kufanya upelelezi wa mauaji ya dada wa bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya. 

Hadi sasa jeshi hilo limewakamata watu wanne kwa tuhuma za mauaji hayo, akiwamo mumewe Aneth, mfanyakazi wao wa ndani na hawara wa mfanyakazi huyo.

Kamanda Sirro hakumtaja mtuhumiwa wa nne aliyekamatwa kwa tuhuma za mauaji hayo yaliyogusa hisia za watu. 

Aneth aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojuliana Mei 26 mwaka huu, nyumbani kwake Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambao inadaiwa hawakuchukua kitu chochote ndani na kutoweka. 

Sirro alisema alituma maofisa hao kwenda Mwanza na Arusha kufanya upelelezi wa mauaji ya Aneth ili kubaini chanzo chake.

Hata hivyo, hakutaka kufafanua zaidi sababu za kutuma timu hiyo kwenye mikoa hiyo wakati mauaji hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam. 

“Jeshi la polisi bado tunafuatilia, kwa sasa tumeshatuma maofisa wetu wameenda katika mkoa wa Mwanza na Arusha ili kufanya upelelezi zaidi,”alisema Sirro.

Alisema jeshi hilo linaendelea kuwahoji watuhumiwa wanaowashikilia ili kubaini chanzo cha mauaji hayo, hivyo upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Bilionea Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 12 na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kandokando ya barabara eneo la Mojohoroni wilayani Hai Mkoa wa Kilimanjaro.

Februari 10, mawakili wanaosimamia kesi ya bilionea huyo, Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emmanuel Safari na John Lundu, waliiambia mahakama kuwa Serikali inakusudia kuita mashahidi 50 kuthibitisha mashtaka na kuwasilisha vielelezo 40, ikiwamo bunduki iliyotumika katika mauaji hayo.

Mawakili hao walidai mipango ya kumuua bilionea Msuya ilianza Julai 26, mwaka 2013 jijini Arusha, ikiwahusisha washtakiwa hao baada ya kuahidiwa wangelipwa Sh5 milioni kila mmoja.

Simbachawene Amtwisha Mzigo Paul Makonda

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene amekuwa kiongozi wa pili kumhoji Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu mradi wa mabasi wa Udart. Jana Simbachawene alipotembelea mradi huo alimtaka Makonda kuweka askari wa kutosha watakaodhibiti uvunjwaji wa sheria katika mradi huo.

Huyo ni kiongozi wa pili kumhoji Makonda kuhusu mradi wa Udart, baada ya hivi karibuni Rais John Magufuli kumtaka asimamie kwa kutoa adhabu kali kwa wale watakovunja sheria kwenye mradi huo.

Katika ziara yake jana, Simbachawene alipanda gari nambari T121DGW kutoka Kimara mpaka Kiarikoo Gerezani na alipofika alipokelewa na Mkuu wa Mkoa, wakuu walaya na viongozi wengine.

Hata hivyo, aliwataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa mpya kwa kujenga vituo vya maegesho ya magari karibu na stendi za mabasi ya haraka ili watu wanaotaka kwenda mjini wawe wanaegesha magari yao na kupanda mabasi hayo, ambako mbali na kuwahi kazini wataokoa gharama za mafuta.

Katika hatua nyingine; Simbachawene amepiga marufuku ombaomba na wafanyabiashara maeneo ya mjini na kumtaka Makonda kutekeleza maagizo hayo kwa kuweka askari wa kuwaondoa.

Alisema watu wanaowapa ombaomba pesa siyo kwamba wana mipango mizuri na Serikali kwa kuwa watoto wanaotumika kuomba walitakiwa wawe shule.

Makonda alisema kuwa utekelezaji wa maagizo hayo umeanza mara moja, kwani yaliyotolewa yapo kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, Makonda alisema kuwa ana mpango wa kuongeza muda wa kufanya biashara katika maduka makubwa na katika soko la Karikaoo kuwa mpaka saa nne za usiku.

Makonda Kupiga Marufuku Uvutaji Sigara Hadharani

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema waendesha bodaboda na abiria wasiovaa helmet watakamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua.

Makonda aliyemwakilisha Makamu wa Rais kwenye futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa wateja na wadau wake juzi, alisema abiria na wapanda vyombo hivyo wanatakiwa kuvaa helmet.

Alisema kupanda pikipiki bila usalama ni kwamba abiria anadhamiria kujiua, kwa sababu akipata ajali ni rahisi kupoteza maisha kwa kupiga kichwa chini.

“Nimeshawasiliana na kamati yangu ya usalama barabarani mkoa, hili nitalisimamia kikamilifu lazima wote wawe na helmet na wakikamatwa wote watashtakiwa,” alisema.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kupanda bodaboda bila kuvaa kofia hiyo, ni sawa na mtu anayechukua vidonge na kunywa na pombe kali, ambayo matokeo yake ni kifo.

Makonda alisema kazi hiyo ataifanya kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani ili apate thawabu ikiwamo kuruhusu maduka makubwa kufanya kazi hadi usiku wa manane.

Alisema hiyo itasaidia wanaofanya kazi wakirudi nyumbani wanafuturu baadaye wanaswali Tarawehe, hivyo wanaweza kwenda kufanya manunuzi usiku.

Alisema kitakachofanyika ni kuimarisha usalama wa raia kupitia kamati yake ya ulinzi na usalama ya mkoa. 

Pia, alisema atatangaza kupiga marufuku uvutaji sigara hadharani zaidi kwenye mikusanyiko na kupambana na vijana na watu wanaojihusisha na uvutaji wa shisha (bangi).

“Mtu asiyevuta sigara, anakerwa sana na moshi ndiye anayeathirika zaidi, nitatangaza rasmi hivi karibuni marufuku ya kuvuta sigara, sasa watu watafute kwa kuvutia… nitatangaza na hatua za kuchukua,” alisema. 

Makonda alitumia nafasi hiyo kuwataka NMB kuchangia madawati, kwa shule za msingi na sekondari katika mkoa wake.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker alisema utamaduni wa kufuturu pamoja hasa katika Afrika unadumisha amani, umoja na upendo miongoni mwa Waislamu na watu wengine, hivyo wao wanauendeleza.

Hatma ya Kesi ya Chadema Dhidi ya Polisi Kuzuia Mikutano ya Kisiasa Kujulikana Jumatatu June 21

0
0
Hatima ya shauri lililofunguliwa na Chadema dhidi ya Polisi kupinga amri ya kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa itajulikana Juni 21, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza itakapotoa uamuzi kuhusu pingamizi lililowasilishwa na upande wa utetezi kuomba litupiliwe mbali.

Jaji Mohamed Gwae anayesikiliza shauri hilo, alifikia uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote za utetezi na mleta maombi.

Awali, Mawakili wa utetezi, Robert Kidando na Obadia Kajungu waliomba Mahakama kutupilia mbali maombi ya Chadema kuruhusiwa kufungua kesi yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kwa madai kuwa hayajakidhi mahitaji ya kisheria.

Akifafanua, Wakili Kidando alidai mleta maombi hajataja baadhi ya vifungu muhimu ikiwamo kifungu cha 5(1)(2), vinavyoipa Mahakama mamlaka ya kisheria kusikiliza na kuamua maombi hayo.

Madai hayo yalipingwa na mawakili wa Chadema; Gasper Mwanaliela na John Mallya waliodai hoja za wajibu maombi hazina uhalali kisheria kwa sababu hati ya maombi yaliyopo mbele ya Mahakama yamekidhi mahitaji ya kisheria.

Wakili Mallya alidai kisheria, hati ya maombi inapaswa kuwa na vitu vitatu muhimu; hati ya kiapo, maelezo ya mleta maombi na ombi la shauri kusikilizwa kama inavyoelekezwa na kifungu cha 5(3).

Wakili Mallya aliomba Mahakama kutupilia mbali pingamizi la upande wa utetezi na kumpa nafuu mleta maombi, kesi yake kusikilizwa na kuamuliwa.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Gwae aliahirisha shauri hilo hadi Juni 21, Mahakama itakapotoa uamuzi huku akiuagiza upande wa utetezi kuwasilisha hati kinzani kujibu hoja za mleta maombi.

Katika maombi ya msingi, Chadema inaomba Mahakama kutamka kuwa amri ya polisi na utekelezaji wake ni batili, kwa sababu ni kinyume cha katiba na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.

Madini ya Helium Yagundulika Nchini

0
0

TANZANA kwa sasa inajikita zaidi katika utafiti wa madini yanayohitajika zaidi duniani yakiwemo yanayotumika kutengeneza vifaa vya simu na betri za magari, Bunge linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma limeambiwa.

Aidha katika juhudi hizo, madini aina ya helium (he) yanayotumika kwa ajili ya mitambo ya Apollo na pia kutumika kwenye vifaa vya matibabu kama MRI na NMR yamegundulika kuwepo nchini Tanzania.

Akijibu maswali ya wabunge jana, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema kwamba baadhi ya madini kama chuma na shaba, uhitajikaji wake duniani umepungua sana kwa sasa.

Katika maswali yao, Mbunge wa Igunga (CCM), Dalaly Kafumu alitaka kuthibitishiwa kuhusu uwepo wa taarifa kwamba utafiti wa madini nchini mwetu umepungua sana.

Akijibu swali hilo, Profesa Muhongo alitoa ufafanuzi kwamba madini yamekuwa yakitafutwa kwa vipindi na yanapokuwa mengi, uhitajikaji wake hupungua sambamba na utafiti.

Alifafanua kwamba katika miaka hii uhitaji wa baadhi ya madini kama shaba na chuma umepungua sana.

“Ndio maana utaona hata uchumi wa Zambia umeyumba kwa sababu China ambayo ndio mnunuzi mkubwa wa shaba kutoka nchini humo imepunguza mahitaji ya madini hayo,” alisema Muhongo.

Alisema madini yanayotengeza vifaa vya simu (rare earth mineral) na yale yanayotengeza betri (graphite) yataendelea kutafutwa kila mara kutokana na uhitajikaji wake na ndio maana akasema Tanzania nayo inajikita zaidi katika kusaka madini hayo.

Alifafanua kwamba madini hayo yanayotengeneza betri za magari yataendelea kuhitajika sana kwa sababu ulimwengu wa sasa unajikita zaidi katika kutengeneza magari yanayotumia umeme kwa wingi.

Kuhusu madini ya helium ambayo huwa katika mfumo wa gesi inayopatikana katika kina kifupi, Waziri Muhongo alifafanua kwamba utafiti ulifanywa na vyuo vikuu vya Oxford na Durham ulithibitisha kwamba kuna madini hayo nchini.

Alifafanua kwamba kiwango kilichogunduliwa cha madini hayo katika Ziwa Rukwa ni mita za ujazo bilioni 52.2 na kwamba utafiti zaidi unaendelea. Kwa sasa nchi inayozalisha kwa wingi madini hayo ni Marekani ambako hata hivyo, Profesa Muhongo, alisema yamekuwa yakipungua siku hata siku.

RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) -Sehemu ya Kwanza

0
0

MTUNZI:ENEA FAIDY
Ilikuwa ni majira ya saa moja jioni ambapo mkuu wa while ya Mabango alikuwa ofisini kwake akiwa amechanganyikiwa sana kwani hali ya shule hiyo ilizidi kutisha sana hasa baada ya kutokea kwa vifo vya wanafunzi kumi na tano mfululizo ndani ya wiki moja tu. Tena vifo vya ghafla tu.

Mkuu wa shule mama Dayana Mbeshi alikuwa kwenye wakati mgumu sana kubaini chanzo cha tatizo lakini bado hakupata majibu.Mara ghafla mlango wa ofisi ukagongwa, akaingia mwalimu wa malezi wa shule hiyo akiwa na USO wa huzuni sana hali iliyomshtua sana mkuu wa shule

"vipi kulikoni?"
"hali mbaya mkuu.. wanafunzi wawili wamefariki tena bwenini" mwalimu wa malezi alizungumza kwa huzuni iliyochanganyika na hofu.

"what? mmh! sio bure.. kuna kitu hapa..!" alisikika mwalimu Mbeshi huku akiinamisha kichwa chake chini na kukiegemeza kwenye kiganja chake

Aliyemtukana Rais Magufuli Akabidhiwa Mchango wa Sh. Mulioni 4.5

0
0

Wanaharakati na wadau wa mitandao ya kijamii nchini wamemkabidhi Sh4.5 milioni aliyekutwa na hatia ya kumtukana Rais John Magufuli ili akalipe faini aliyotakiwa atoe na mahakamani kuepuka kifungo cha miaka mitatu.

Mshtakiwa huyo, Isaack Habakuki alikutwa na hatia baada ya kukiri kosa la kumtukana Rais kupitia ukurasa wake wa facebook.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imemtaka kutoa Sh 7 milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
 
Mratibu aliyekuwa anakusanya michango hiyo kwa Kanda ya Kaskazini,  Diwani wa Levolosi,  Ephata Nanyaro amesema jana kuwa  wamefanikiwa kupata michango hiyo kupitia makundi ya mitandao ya kijamii waliyoyaanzisha.

"Lengo ni kumsaidia mwenzetu kwa kuwa kupitia sheria hii ya mitandao tunaamini hakuna aliyesalama na sheria hii itawagusa wote, " amesema Nanyaro.

Naye,  Habakuki amewashukuru Watanzania waliojitolea kumchangia akisema kupitia adhabu hiyo atakuwa wa kwanza kufundisha jamii kuhusu sheria za mitandaoni

Mke Wa Rais Mama Janeth Magufuli Akabidhi Vyakula Vya Futari Kwa Vituo Vinne Vya Kulea Watoto Yatima Jijini Dar Es Salaam

0
0
MKE wa Rais Mama Janeth Magufuli amekabidhi chakula kwa ajili ya futari wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa vituo vinne vya kulea watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu Jijini Dar es salaam.

Vyakula hivyo vimekabidhiwa leo tarehe 18 Juni, 2016 katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu Jijini Dar es salaam vimejumuisha Mchele kilogramu 500, Sukari kilogram 500 na Tende kilogramu 28.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vyakula hivyo, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli aliyeongozana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewatakia heri Waislamu wote katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwasihi waendelee kuliombea Taifa amani na utulivu.

“Tunawatakia mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, katika kipindi hiki tunawaomba mzidi kuiombea nchi yetu amani, viongozi wetu wa nchi na watanzania wote kwa ujumla, nchi ikiwa na amani ndio mambo mengi mazuri yanaweza kufanyika”

Kwa niaba ya vituo vilivyopatiwa vyakula hivyo, Mwenyekiti wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo amemshukuru Mke wa Rais kwa kutoa vyakula hivyo na ameeleza kuwa kitendo hicho kinaonesha mshikamano na ushirikiano walionao watanzania wote bila kujali tofauti ya dini, kabila wala maeneo wanayotoka.

“Kwa hiyo ndugu zangu mna imani ya kikristo lakini mnatambua waislamu ni ndugu zenu, wote tunajenga nyumba moja, mshikamano ndio tunu tuliyoachiwa na Baba yetu wa Taifa, leo mmeguswa kuona wenzenu tunafanya ibada na nyinyi mmeingia kwenye ibada, sasa ibada ya kutoa ni ibada kubwa sana, sio nchi nyingi katika Afrika zinafanya kitendo hiki, watu hawaelewi, ni nchi chache sana ambazo imani moja inaunga mkono imani nyingine, lakini sisi waislamu tunalitambua hili hata toka kipindi ambacho mtume wetu SWA anapigana kusimika dini hii kwa waumini alipata nusura kwa wakristo”

Vituo vilivyokabidhiwa vyakula hivyo ni Charambe Islamic Center, Tasofe Lqadiria, Nur Twarigatu Lqadiria na Zawiyatul Lqadiria.

Breaking News: Jeshi la Polisi Lawatawanya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Dodoma Ambao ni Wafuasi wa Chadema Kwa Kufanya Mahafali Bila Kibali

0
0
Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma  limewasambaratisha wanafunzi  wa vyuo vikuu  wanachama wa Chadema ( Chadema Students Organization -CHASO )waliokuwa wakishiriki hafla ya mahafali katika  Ukumbi wa African Dreams  ulipo Area D mjini Dodoma.
 
Katika hafla hiyo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambapo baadhi ya wanafunzi wamekamatwa baada ya kuwambiwa watawanyike na kurudi majumbani kwao. 

Polisi wamesema mikusanyiko  yote ya kisiasa ilishapigwa marufuku, hivyo hata mahafali hiyo ilikuwa batili

Rais Magufuli Kukabidhiwa Uenyekiti wa CCM July 23 Mwaka Huu

Ray C apelekwa sober house Bagamoyo, uongozi wa sober wazungumzia

0
0

Muimbaji mkongwe wa muziki nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’ Ijumaa hii amepelekwa Life and Hope & Rehabilitation Centre (Sober House) iliyopo Bagamoyo kwa ajili ya kusaidiwa kuanacha na matumizi ya Madawa ya kulevya, uongozi wa sober hiyo umethibitisha.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja toka aonekane katika video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha jinsi anavyosaidiwa na jeshi la polisi baada ya kudaiwa kutaka kijichoma kisu.

Mmoja kati ya wasimamizi wa kituo cha Life and Hope & Rehabilitation Centre (Sober House) ambacho pia kilimsaidia Chidi Benz kuachana na matuzi ya Madawa ya kulevya, Karim Banji, amesema kuwa ni siku moja toka Ray C apelekwe katika kituo hicho.

“Kweli jana tumempokea Ray C, na kusema kweli kwa sasa siwezi zungumzia maendeleo yake kwa sababu ni siku ya kwanza, lakini leo mchana amekula vizuri na nimemuacha amepumzika,” alisema Karim.

Pia alisema bado hajajua Ray C atakaa kwa muda gani ndani ya sober house.

“Kusema kweli mgonjwa akiletwa hapa, atapimwa afya na baada ya hapo anawekwa katika chumba maalum kwa siku tatu ili aweze kukabiliana na hali ngumu, na baada ya hapo ataendelea na matibabu ya kawaida, kwa hiyo kikubwa ni kuombea tu,” alisema Karim.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Awakemea Wanafunzi wa Kike Wanaofanya Biashara ya Kuuza Miili Yao

0
0

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amekemea tabia chafu zinazofanywa na baadhi ya wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu nchini wanaodiriki kushiriki kujiuza miili yao katika mahoteli makubwa na majumba ya starehe na kuwataka kuacha tabia hiyo.

Makamu wa Rais alisema hayo katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo hicho Kikuu ya kuadhimisha siku ya wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe pamoja na Uzinduzi wa Kampeni za uchangiaji wa Ujenzi wa Bweni la wanachuo wa kike.

Alisema baadhi ya wanafunzi hao walidiriki kujiuza miili yao kwa ajili ya tamaa ya kupata vitu vya anasa zikiwemo simu zenye gharama kubwa, mavazi na vitu vingine jambo ambalo linafedhehesha jamii, wazazi na walezi wao.

Makamu wa Rais alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wa kike wanaosoma katika vyuo vikuu nchini kujikita katika elimu ili waweze kufanikiwa kwenye maisha yao ya baadaye.

“Vyuo vimeharibika kwa tamaa, sisi tulisoma hapa Mzumbe na tuliweza kuishi, lakini wanafunzi wa sasa mnaingiwa na tamaa ya mashindano ya mavazi utadhani mnagombea Umiss,” alisema Suluhu.

Aliongeza kuwa,“nimeambiwa hapa Morogoro wapo baadhi ya wanachuo wa kike wanakwenda kujiuza miili katika hoteli moja kubwa na kwenye majumba ya starehe kwa tamaa tu, mnataka kuwa na simu ya laki saba na mavazi ya gharama kubwa itawezekana wapi, mnatukwaza wazazi wenu.”

Aliwaonya wanavyuo wenye tabia hiyo ya kuuza milii yao kuacha mara moja, huku akisisitiza kuwa dunia ipo tu hivyo wasifukuzane nayo kwani mambo hayo watayakuta baada ya kumaliza masomo yao.

Makamu wa Rais alitoa mfano kwa kuwaambia wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe, “ukitaka kushika nafasi kubwa kama hii ‘yangu’ ni lazima ufuatiliwe historia yako tangu chini ukiwa shule ya msingi sasa kwa hali hiyo watoto wetu mtakosa fursa za kuwa viongozi wa juu.”

Alisema mtoto wa kike anakuwa na safari ndefu zaidi yenye misukosuko mingi kuliko mtoto wa kiume anapokuwa akitafuta elimu.

Samia alisema katika hatua ya elimu ya juu hasa kwa wanawake imegubikwa na changamoto ambazo kama wanajamii wa Tanzania tunapaswa kuungana na serikali kuziondoa ili kumuwezesha mtoto wa kike kufika mbali kielimu.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa mabweni, ufinyu wa fedha za kukidhi mahitaji na mtazamo hasi wa walimu na wanafunzi wa kiume dhidi ya wanafunzi wa kike wanapokuwa vyuoni.

Katika hatua nyingine, alisema Serikali imeanza kutoa elimu bure kwa wanafunzi wote kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne na kwamba hatua hiyo imeongeza idadi ya wanafunzi wakiwemo wa kike.

Aliyelawiti Watoto Wawili Akijifanya Polisi Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 60 Jela

0
0
MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara imemhukumu, Ally Mpemba au Ustadhi (32), Mkazi wa Mtaa wa Bunda Stoo mjini Bunda kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya kubaka watoto wawili kwa zamu akijifanya polisi.

Adhabu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Bunda, Said Kasonso, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo pasipo kuacha shaka yoyote.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Hamuza Mdogwa, kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Januari 17 mwaka huu, majira ya saa 8:30 mchana, katika kijiji cha Kitaramanka wilayani hapa.

Alisema kuwa mshtakiwa huyo aliwakuta watoto hao wakiwa katika eneo hilo na akawatisha kuwakamata akidai kuwa yeye ni askari Polisi na kwamba wamefanya kosa hivyo atawachukua maelezo yao na baadaye awapeleke kituoni.

Aliongeza kuwa mshtakiwa huyo alitoa Sh 200 na kumpatia mtoto mmoja aende akanunue daftari la kuandikia maelezo yao, na baada ya mtoto huyo kwenda ndipo alipombaka aliyebaki na kisha kumwambia adhabu yake imekwisha sasa aende nyumbani.

Alisema kuwa baada ya yule aliyetumwa daftari kurudi, Mpemba alimbaka pia na kumuamuru arudi nyumbani adhabu yake imekwisha na kwamba watoto hao baada ya kufanyiwa unyama huo walikwenda kutoa taarifa nyumbani kwa wazazi wao.

Aidha alisema kuwa Ofisa Mtendaji wa kata hiyo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho walimkamata mshtakiwa huyo na kumfikisha Polisi.

Kabla ya adhabu kutolewa mshtakiwa huyo alipewa fursa ya kujitetea na akaiomba Mahakama hiyo impunguzie adhabu.

Hata hivyo mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo kwa sababu makosa aliyofanya ni ya kinyama na ya udhalilishaji mkubwa kwa watoto hao wenye umri wa miaka 16 kila mmoja.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Kasonso, alisema kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na kwamba kwa kosa la kwanza la kubaka mtoto wa kwanza ataenda jela miaka miaka 30 na la pili pia atatumikia kifungo cha miaka 30 jela na adhabu zote zinakwenda kwa pamoja hivyo atatumikia kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye nia na tabia kama hiyo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images