Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Maalim Seif Awahutubia Wamarekani Kuhusu Sakata Zima la Zanzibar

$
0
0
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema vitendo vya unyanyasaji wapinzani vinavyoendelea nchini ni maradhi yanayokikumba chama tawala. 

Maalim Seif aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano uliondaliwa na Kituo cha Elimu cha Kimkakati cha Kimataifa cha Marekani (CSIS) juzi, uliofanyika Washington DC nchini Marekani. 

Akizungumzia kukandamizwa kwa wapinzani nchini, Maalim Seif alitoa mfano wa yeye kuhojiwa na polisi 11 kwa saa tatu na kijana aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitatu au kulipa faini ya Sh7 milioni kwa kumkosoa Rais John Magufuli kwenye ukurasa wa facebook. 

Kadhalika alitoa mfano wa viongozi wa Chadema kuhojiwa polisi na baadhi kuwekwa rumande kwa saa kadhaa huku kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo naye akihojiwa kwa kufanya mkutano. 

“Tunashuhudia mmomonyoko wa hali ya juu wa demokrasia sasa hivi… na hali hii itazidi miezi michache ijayo,” alisema. 

Alisema wapinzani wanakandamizwa zaidi upande wa Zanzibar, na kusema kuwa CUF inataka ufafanuzi wa Muungano na wala si kuufuta. 

Kiongozi huyo wa CUF alimlaumu Rais John Magufuli na kusema licha ya kuwa nchi za nje zinamuona anafanya vyema katika kupambana na rushwa, lakini Wazanzibari hawana furaha na uongozi wake. 

“Kuna mitazamo tofauti hasa kwa walio nje ya Tanzania kwamba anapambana na rushwa, lakini kama kiongozi wa nchi, ameshindwa kufanya majukumu yake kuhusu Zanzibar,” alisema 

Alisema mara zote Rais Magufuli anapoulizwa kuhusu suala la Zanzibar, husema hawezi kuchukua hatua.

“Wazanzibari wanachokitaka ni kuona Rais Magufuli anawajibika kama kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Maalim Seif ambaye katika mkutano huo, aliambatana na mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa Ladhu na katibu wake, Issa Kheri Hussein. 

Pamoja na mambo mengine, Maalim Seif alisema chama chake kipo tayari kufanya uchaguzi mwingine, endapo utasimamiwa na taasisi za kimataifa zisizofungamana na upande wowote. 

Alisema wakati wakisubiri hilo, wafuasi wa chama hicho wanaendelea kufanya mgomo baridi usio na nia ya vurugu ili kuonyesha kuwa mambo hayawezi kwenda kama kawaida. 

Akijibu swali la mmoja wa waliohudhuria mkutano huo kuhusu kutuhumiwa kuuvunja Muungano endapo atakuwa Rais wa Zanzibar, Maalim alisema chama tawala kimekuwa kikivibatiza vyama vya upinzani majina ya uongo ili kuvibomoa.

 “Kuna wakati walikiita CUF kuwa ni chama cha Kiislamu, lakini hilo si kweli, tumenyang’anywa ushindi zaidi ya mara tano na wala hatujaleta fujo,” alisema. 

Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast, Maalim alielezea jinsi uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana ulivyofutwa na kusema kuwa CUF imekuwa ikinyang’anywa ushindi tangu mfumo wa uchaguzi wa vyama vingi uanze mwaka 1995. 

“Tumefanya chaguzi tano, 1995, 2000, 2005, 2010 na 2015 katika chaguzi zote hizi, watu wa Zanzibar waliichagua CUF kuongoza Serikali. Lakini CUF imenyimwa kushika madaraka,” alisema Maalim na kuongeza:

 “Kuna harufu ya hatari, kwa miaka yote hiyo tumejitahidi kuwatuliza wafuasi wetu, tumeangalia namna ya kuzungumza na wenzetu ili waheshimu maamuzi ya watu, lakini hawasikii.” 

Alisema uchaguzi wa mwaka jana ulifanyika kwa uhuru na haki na matokeo yalionyesha kuwa CUF kimeshinda, lakini polisi waliizingira Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na baadaye Mwenyekiti wa tume hiyo, Jecha Salim Jecha akayafuta matokeo hayo. 

Alisema hata Umoja wa Ulaya (EU) walitoa ripoti yao wiki mbili zilizopita, iliyoonyesha kuwa ZEC haikuwa na mamlaka ya kufuta matokeo hayo. 

“Nilijaribu kuwasiliana na Dk Ali Mohamed Shein , lakini hakutaka kupokea simu yangu, lakini baadaye nilimuandikia barua nikitaka mazungumzo naye, alikubali kwa masharti kuwa wawepo watu wengine.”alisema na kuongeza: “Tukakubaliana tufanye mazungumzo, lakini wawepo viongozi wakubwa, wakati tukiendelea na mazungumzo, Jecha alitangaza kuwa uchaguzi utarudiwa Machi 20.” 

Maalim Seif alitaja athari za kufutwa kwa uchaguzi huo kuwa ni pamoja na kuvunja maridhiano ya kisiasa ya Zanzibar na Maamuzi ya Wazanzibari wengi walioamua nchi yao iongozwe kwa Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Alitaja athari nyingine kuwa ni kuwarudisha nyuma watu wa visiwa vya Unguja na Pemba, kuibuka kwa siasa za chuki, migogoro na kubaguana. 

“Hayo ni pamoja na kudhoofika kwa sekta za uchumi, biashara, ukosefu wa ajira na maendeleo kwa jumla, na siyo kwa Zanzibar pekee bali kwa Jamhuri yote ya Muungano wa Tanzania, hasa iwapo Mataifa yataitenga na kulinyima Taifa misaada, hali ambayo haiwezi kuepukika”. alisema 

Akieleza msimamo wa waandaaji wa mkutano huo, uliojumuisha marais mbalimbali wastaafu wa Marekani na Ulaya, Mkurugenzi Mkuu wa NDI, Peter Craig aliwataka viongozi wa kisiasa wa nchi nyingine za Afrika kuiga mwenendo wa Maalim Seif. 

“Tunaomba watu wengine wenye migogoro ya aina hii waige mfano huu wa Seif Sharif Hamad na sisi tutakuwa pamoja nao mpaka haki itendeke na ipatikane na tukianzia na Zanzibar,” alisema

Lowassa Amwandikia Waraka Mzito Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu

$
0
0

WAZIRI Mkuu wa zamani na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema kwa mwamvuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, amemwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi   (IGP), Ernest Mangu.

Katika barua hiyo, Lowassa  amehoji hatua ya Jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano na maandamano kwa vyama vya siasa vya upinzani nchini.

Katika barua yake hiyo ya jana, Lowassa  alisema amelazimika kuchukua hatua hiyo kwa vile  wakati agizo hilo la  kupiga marufuku   mikutano inatolewa, alikuwa nje ya nchi ingawa alifikisha ujumbe na Watanzania wenye nia njema wa ndani na nje kuhusu hatua hiyo ya polisi.

“Kwanza niwie radhi kwamba nimelazimika kwa nafasi yako na yangu, kukiuka taratibu za itifaki hata nikalazimika kuandika waraka huu kwako.

“Ninafanya hivyo si kwa sababu yoyote, bali kwa sababu tu jambo au mambo yaliyonisukuma kukufikishia ujumbe huu yana uzito mkubwa na kimsingi yanaweza kuathiri mustakabali mwema wa taifa.

“IGP, siyo desturi yangu kuandika waraka wa namna hii mtandaoni au kupitia vyombo vya habari, ingawa safari hii nimelazimika kufanya hivyo   kuweka rekodi sahihi,   na kukosoa sababu ulizotoa kuwa nyuma ya agizo lako hilo,” alisema Lowassa.

Alisema wakati akiwa anatafakari kwa mshangao agizo hilo na baada ya kurejea nchini, alipigwa na butwaa zaidi baada ya kusikia Jeshi la Polisi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, limewazuia viongozi wao taifa wa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara.

“Agizo hilo lilifuatiwa na tukio la kukamatwa, kushikiliwa na kuhojiwa kwa viongozi hao, akiwamo Mwenyekiti wetu, Freeman Mbowe huko Mwanza hivi majuzi.

“Katika matukio hayo yote, polisi mnadai kuwa na taarifa za intelijensia ambazo zinaonyesha kuwapo  uwezekano wa kutokea  vurugu kwenye mikutano hiyo ya hadhara ya vyama vya siasa,” alisema.

Lowassa  alisema madai hayo ya polisi hata IGP Mangu, aliwahi  kuyatoa awali kutokana na sababu wanazozijua wao wenyewe kama njia ya kuminya haki za msingi za katiba za vyama vya siasa kujumuika na kutimiza majukumu yao ya siasa.

“Si hivyo tu, uzoefu wa historia unakinzana na kwenda kinyume kabisa na madai hayo, kwa sababu  yako matukio mengi ambayo yamethibitisha kwamba mijumuiko ya wanasiasa wa vyama vya upinzani, yakiwamo maandamano na hata mikutano, imekuwa ikifanyika kwa amani.

“Iko mifano mingi inayoonyesha kwamba  tumefanya shughuli mbalimbali za siasa kwa maana ya maandamano na mikutano yahadhara kwa amani na pasipo kuwapo hata   ulinzi wa polisi.

“…Mifano ya namna hiyo ndiyo inayosababisha baadhi yetu si tu tupingane na maagizo yanayotoa mwelekeo wa kukandamizwa   uhuru wa  katiba wa vyama vya siasa vya upinzani kujumuika, bali kwenda mbali zaidi na kutilia shaka hata maagizo hayo na kuyaona kuwa na misukumo iliyojificha nyuma ya kichaka cha ‘sababu za intelejensia,” alisema.

Alisema anaandika barua hiyo aliyoiita waraka kwa mkuu huyo wa polisi kwa dhati   kwamba,  kilichotokea Kenya hivi karibuni ambako mahakama ilitupilia mbali maagizo ya namna hiyo ya polisi kujaribu kuzuia haki ya katiba ya vyama vya upinzani kuandamana ndicho kinachoelekea kutokea hapa nchini.

Lusinde: Wabunge wa Chadema wameniomba nimwambie Mbowe asiwaburuze, ni dikteka

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), jana alitema cheche Bungeni akimnyooshea kidole kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema.

Lusinde alisema kuwa amepokea malalamiko kutoka kwa wabunge wa Chadema, wakitaka amfikishie taarifa Mwenyekiti wao huyo kwani hawawezi kumwambia. 

Alisema wabunge hao wamemwambia kuwa wao hawapendi kususia vikao lakini wamekuwa wakilazimishwa na Mbowe.

“Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya viongozi madikteta ndani ya nchi hii ni Mbowe [Freeman], anawatoa wabunge kwa nguvu. Wabunge [wa Chadema]wako hapo kwenye chai wamenituma mimi nije niwasemee humu ndani,” alisema Lusinde.

“Wameniomba, wamesema… ‘Lusinde kuna mambo sisi hatuwezi kumwambia Mbowe nenda ukamwambie’. Tunatumia fursa hii kumwambia Mbowe warudishe wabunge ndani ya Bunge, usiwanyanyase. Anawapigia simu wakae kwenye chai badala ya kuingia Bungeni, tabia gani hiyo,” alisisitiza.
 
Hata hivyo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi alikanusha taarifa hizo na kueleza kuwa wabunge hao wanaamini kuwa hivi sasa wanaweza kuwawakilisha wananchi hata wakiwa nje ya Bunge na kwamba hivi sasa wanaendelea kufanya vikao vyao wakiijadili bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2016/17.

Sugu alisema kuwa wanaendelea kujadili Bajeti hiyo katika ukumbi wa zamani wa Pius Msekwa katika eneo hilo la Bunge na kwamba wanajadili pia njia bora zaidi ya kuwafikishia wananchi.

Akitolea ufafanuzi maelezo ya Lusinde, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Ackson Tulia alieleza kuwa wabunge wote wa upinzani wanaotoka Bungeni wakati vikao vya Bunge vikiendelea wanatoka kwa utashi wao na hawalazimishwi kufanya hivyo.

Trump Asisitiza Waislamu Wasiingie Marekani

$
0
0
MGOMBEA wa kiti cha urais wa kupitia chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amesisitiza kuwa, mauaji ya watu 50 yaliyotokea kwenye Klabu ya wapenzi wa jinsia moja, yamethibitisha msimamo wake wa kutaka waislamu wapigwe marufuku kuingia humo.

Katika hotuba yake kwenye jimbo la New Hampshire, Trump amesema mfumo wa Idara ya uhamiaji nchini Marekani, umeruhusu familia ya Omar Marteen, aliyetekeleza mauaji hayo kuingia nchini Marekani.

Alidai kuwa, bado mfumo huo umeendelea kuruhusu wauaji wengine kuingia nchini humo bila vikwazo.

Alisema, sababu moja wapo inayochochea muuaji kuwepo nchini Marekani, ni familia ya Marteen kuingia nchini humo.

Aliongeza kuwa, mfumo wa idara ya uhamiaji isiyotekeleza wajibu wake, bado hairuhusu kujua ni nani anayepaswa kuingia Marekani ili raia wa nchi hiyo walindwe.

Kwa upande wa Mgombea urais kupitia Democratic, Hillary Clinton, akitoa risala za pole kwa waathiriwa wa mkasa huo, alisema Trump ni kama mtoto anayesema ovyo kwa namna anavyougeuza mkasa huo wa kitaifa kujipongeza binafsi.

Akizungumza jimboni Ohio, Hillary, amekosoa mpango wa mpinzani wake ambaye ni Trump, kuwazuia waislamu kuingia Marekani

“Hatua hiyo ya uchochezi ya vitisho kuzuia familia na marafi ki wa kiislamu kuingia marekani, pia mamilioni ya wafanyabiashara na watalii waislamu kuingia nchini, inaumiza sehemu kubwa ya waislamu wanaopenda uhuru na kuchukia ugaidi,” alisisitiza.

Naye Rais wa Marekani, Barack Obama alisema, hakuna ushahidi kuwa aliyetekeleza mashambulizi hayo alikuwa sehemu ya mpango mkubwa wa mashambulizi.

Obama alieleza kwamba, shambulio hilo lilisukumwa na msimamo binafsi wa mshambuliaji huyo na hakuna ushahidi kuwa, Marteen alipata maelekezo kutoka nje ya nchi kutekeleza mauaji.

Lakini, Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la FBI,James Comey, alisema kuna ishara kuwa Marteen alishawishika kupitia mitandao ya intaneti ila bado haijajulikana kama kijana huyo alikuwa anaunga mkono kundi gani la kigaidi.

Comey alisema, muuaji huyo alieleza kuunga mkono kundi la wanamgambo wa Dola ya Kiislamu (IS) pamoja na kundi hasimu na IS la Al Nusra kutoka nchini Syria.

Katika hatua nyingine,Silaha mbili zilizotumiwa na Marteen zimebainika kununuliwa kwenye kituo cha kuuza silaha.

Mmiliki wa duka hilo Edward Henson, alisema Marteen alipitia taratibu zote zinazopaswa kufuatwa wakati wa kununua silaha hizo.

Naye mke wa zamani wa Marteen, Sitora Yusufi y, amemwelezea mumewe kama mtu aliyekuwa na tabia za ugomvi ya kutaka kupiga watu lakini hakuwa na itikadi kali za kidini.

Tukio hilo lililohusisha mauaji ya watu 50 na kujeruhi wengine zaidi ya 53 yalitekea kwenye klabu ya starehe ya mashoga iliyopo Frolida Jumapili ya wiki iliyopita.

Marteen,alivamia kwenye klabu hiyo kisha kuwafyatulia risasi mfululizo watu waliokuwepo ndani. 

Wakati akitekeleza mauaji hayo, Marteen aliwateka nyara watu wengine zaidi ya 30 ambao waliokolewa na polisi. 

Mtuhumiwa huyo ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi, ilielezwa alishawahi kuhojiwa na maofisa usalama mwaka 2013 na 2014 akihusishwa na makundi ya kigaidi.

Taarifa Ya Utekelezaji Wa Maagizo Ya Serikali Kuhusu Ukomo Wa Matumizi Ya Simu Bandia Nchini Ifikapo 16 Juni 2016

$
0
0
1.0   UTANGULIZI

1.1.Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni taasisi ya Serikali yenye dhamana ya kusimamia shughuli za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta hapa nchini. Kuwepo kwa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010 na Kanuni za EPOCA (CEIR) za mwaka 2011 zimewezesha kutekelezwa kwa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi.


1.2.Mfumo huu wa kielektroniki ulizinduliwa rasmi tarehe 17 Desemba 2015 na unahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi  (IMEI) kwa lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vinavyoibiwa, kuharibika, kupotea au ambavyo havikidhi viwango (bandia) vya matumizi katika soko la mawasiliano. Namba tambulishi za vifaa vyote vya mawasiliano vya mkononi ambavyo vimeibiwa, vimeharibika, kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaruhusiwa kuunganishwa kwenye mitandao ya watoa huduma ifikapo kesho tarehe 16 Juni 2016.

1.3.Kipindi cha mpito cha kuelimisha umma pamoja na zoezi la wateja kuhakiki simu walizo nazo au wakati wanataka kununua simu mpya lilianza mwezi Desemba 2015 wakati mfumo ulipozinduliwa na litamalizika kesho tarehe 16 Juni 2016. Hata hivyo, elimu kwa umma kuhusu simu bandia imekuwa ikitolewa nchini tangu mwezi Novemba 2011 baada ya Kanuni za CEIR kutoka, kufuatia kupitishwa na Bunge Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta tarehe 20 Juni 2010 ikielekeza kuwekwa kwa mfumo wa namba za utambulisho wa vifaa vya Mawasiliano vya kiganjani.

2.0    KAZI ZILIZOFANYIKA TANGU KUZINDULIWA KWA MFUMO

2.1 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imeendelea kusimamia kwa karibu makampuni ya simu hapa nchini katika uendeshaji wa kila siku wa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi. Hii imesaidia pamoja na mambo mengine kupata taarifa za namba tambulishi (IMEI) na kuzifanyia uchambuzi wa kina ili kupata mwelekeo halisi kabla ya kipindi cha mpito kuisha hapo tarehe 16 Juni, 2016.


2.2 Mamlaka ya Mawasiliano iliendelea pia na kampeni za kutoa elimu kwa umma kuhusu jinsi ya kuhakiki namba tambulishi (IMEI) za vifaa vya mkononi (mobile devices). Katika kampeni hizo wananchi walipata uelewa wa kutambua uhalisia wa simu zao ikiwa ni pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua simu mpya. Makampuni yote ya simu hapa nchini kwa nyakati tofauti wameshiriki pia katika kuelimisha umma, ikiwa ni pamoja na kuwapelekea ujumbe mahususi moja kwa moja kwa watumiaji wote wa simu za mkononi. Hali kadhalika Shirika la Viwango Tanzania na Tume ya Ushindani nchini, wameshiriki moja kwa moja katika kutoa elimu kwa umma sambamba na Mamlaka ya Mawasiliano.


2.3     Kipindi cha kuanzia Desemba 2015 mpaka mwezi Mei 2016 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa elimu kwa umma katika mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mbeya, Rukwa, Ruvuma, Iringa, Dodoma, Singida, Tabora, Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara na Kagera. Pia elimu kwa umma ilitolewa Zanzibar. Mamlaka imefanya pia elimu kwa umma katika miji ya, Morogoro, Pwani, Lindi na Mtwara wiki iliyopita pamoja na wiki hii. Aidha kesho ambayo ndio siku ya ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini, kutakua na mkutano wa wafanya biashara wa simu wa mkoa wa Dar es Salaam. Mkutano huo utawahusisha pia mafundi wa simu, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa. Pamoja na mikutano ya hadhara na mikutano ya barabarani (road shows), elimu imetolewa kwa wauzaji wa simu, Mafundi wa Simu na Maafisa Biashara pamoja na Kamati za Ulinzi na Usalama za maeneo husika.


3.0     UCHAMBUZI WA NAMBA TAMBULISHI (IMEI)


Wakati mfumo warajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi unazinduliwa mwezi Desemba 2015, idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango (bandia) zilikuwa sawa na 4% na zile ambazo zilikuwa zimenakiliwa (duplicates) zilikuwa ni sawa na 30%. Hii ikiwa na maana 66% ni sio simu bandia. Uchambuzi huu haukuhusisha taarifa za makampuni ya Viettel na Smile.




Kielelezo 1: Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI) za Disemba, 2015


Uchambuzi wa mwezi Februari 2016 ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na 3%, vilevile idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na 18%. Simu halisi zilikuwa sawa na 79%.


Kielelezo 2. Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI) February 2016


Uchambuzi wa mwezi Machi 2016 ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na 4%, na idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na 13%. 83% zikiwa simu halisi. Uchambuzi huu unahusisha taarifa za makampuni yote ya simu nchini.




Kielelezo 3: Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI) za Machi, 2016


Uchambuzi wa mwezi Aprili 2016 unaonyesha hakuna mabadiliko yoyote ya idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango (invalid) hivyo kubakia 4%, na idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa ziliongezeka kutoka 13% na kufikia 14%. Vilevile idadi ya namba tambulishi za simu halisia ilipungua kutoka 83% mpaka 82% kama ilivyoonyeshwa katika kielelezo kifuatacho.




Kielelezo 4: Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI) za Aprili, 2016


Matokeo ya uchambuzi wa mwezi Aprili, 2016 umeonyesha namba tambulishi ambazo zilikua zimenakiliwa kuongezeka na kuleta taswira kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa wauzaji wa simu wasio waaminifu kupunguza bei za simu zao zenye namba tambulishi zilizonakiliwa na kuwafanya watumiaji wa simu katika maeneo husika ambayo elimu kwa umma ilikua bado haijawafikia kushawishika kununua simu hizo.Matokeo haya yalitoa msukumo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na wadau wote kuongeza nguvu zaidi kuelimisha wananchi katika maeneo yaliyobakia kuhusu umuhimu wa kuhakiki simu zao ikiwa ni pamoja na kuelewa zaidi utaratibu wa kufuata wakati mtu atakapo hitaji kununua simu mpya.


Kielelezo 5: Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI) za Mei, 2016


Uchambuzi wa mwezi Mei, 2016 ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na 3%, na idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na 2% ambapo 95% zikiwa simu halisi. Uchambuzi huu unahusisha taarifa za makampuni yote ya simu nchini.


Matokeo haya mazuri yanaonyesha matokeo ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Makampuni ya simu hapa nchini pamoja na wadau wengine katika kuelimisha umma juu ya kuhakiki uhalisia wa simu walizo nazo ikiwa ni pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua simu mpya.


Kielelezo 6: Uchambuzi wa takwimu za namba tambulishi (IMEI) za Juni, 2016


Uchambuzi uliofanywa tarehe 14 Juni 2016 unaonyesha mabadiliko chanya ya idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango (invalid) kupungua kutoka 3% hadi kufikia 2.96%, na idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zikipungua kutoka 2% hadi kufikia 0.09%. Vilevile idadi ya namba tambulishi za simu halisia zimeongezeka kutoka 85% mpaka 96.95% kama ilivyoonyeshwa katika kielelezo 6 hapo juu.


Matokea haya yanaonyesha mwitikio mzuri wa wananchi juu ya uelewa wao katika suala zima la uzimaji wa simu ambazo hazikidhi viwango. Matokeo hayo yanatoa picha nzuri hasa tunapoelekea kuhitimisha zoezi la uzimaji wa simu bandia kesho tarehe 16 Juni 2016.


4.0     CHANGAMOTO

Pamoja na jitihada mbalimbali zilizofanywa na Mamlaka pamoja na wadau wengine bado kuna changamoto ambazo zinahitajika kutatuliwa. Changamoto hizo ni pamoja na:


(i)  Uaminifu mdogo kwa baadhi waauzaji wa simu kwa kutoa punguzo kwa wananchi ili kuwashawishi kuzinunua simu bandia kwa bei nafuu;


(ii)Gharama zinazohitajika katika kuwafikia wananchi na kuelimisha ili waweze kuelewa zaidi juu ya mpango mzima wa kuhakiki simu zao; na


(iii)Uelewa mdogo wa baadhi ya wananchi katika kuitikia wito wa kuhakiki simu zao katika kipindi cha mpito.


5.0     HITIMISHO


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inaendelea kumbusha watanzania wote kuwa ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa simu yake ni halisi na sio bandia kwani kuanzia kesho, hakuna simu bandia itakayoweza kufanya kazi nchini. Vilevile Mamlaka inawakumbusha wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi kutambua kuwa ni kosa kubadilisha namba tambulishi za vifaa vya simu za mkononi (mobile devices) kwani adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka kumi (10) au faini isiyopungua TZS millioni 30 au vyote kwa pamoja.


Mamlaka inatoa wito kwa wale wote wote wanaofanya biashara za kuingingiza simu hapa nchini kutoka nje wahakikishe kuwa simu wanazoleta zinakidhi viwango, zimehakikiwa kwa mujibu wa Shirika la Viwango Tanzania. Aidha Mamlaka inawakumbusha kwa mara nyingine kuwa wanapaswa kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano kwa mujibu wa Sheria. Hii pia ni kwa mafundi wote wa simu nchini, wanatakiwa kuanza mchakato wa kupata leseni ya kutengeneza simu, ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuwaorodhesha wanaoleta simu zao kutengenezwa ili kuepuka kuwa sehemu ya mtandao wa wizi wa simu.


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inayapongeza makampuni ya simu kwa ushirikiano mzuri wanaondelea kuuonesha katika kutekeleza agizo hili la Serikali kupitia Mamlaka. Hali kadhalika, jitihada zao za kushiriki elimu kwa umma kwa wateja wao pamoja na kuwapatia simu wateja waliokuwa wanatumia simu bandia, kumepelekea agizo hili kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu. Mafanikio ya jambo hili, kwa kiasi kikubwa yametokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali wa Mawasiliano, wakiwemo jeshi la Polisi, Tume ya Ushindani pamoja na Shirika la Viwango Tanzania.


Mhandisi James Kilaba

KAIMU MKURUGENZI MKUU

15 Juni, 2016


Maelezo ya ziada kwa Wahariri


FAIDA ZA MFUMO WA RAJISI YA NAMBA TAMBULISHI


Mfumo huu wa rajisi una faida zifuatazo:

  1. Kuthibiti wizi wa simu. Iwapo mtu atapoteza au ameibiwa simu ya kiganjani na akatoa taarifa kwa mtoa huduma, simu hiyo itafungiwa isiweze kutumika kwenye mtandao mwingine wowote wa simu za kiganjani. Mteja anaponunua simu ni lazima adai risiti halali na halisi  na pia garantiii ya miezi 12. Mteja anatakiwa aihifadhi risiti hiyo angalau kwa miezi mitatu. Baada ya hapo, iwapo simu imekuwa inatumika, taarifa za matumizi zinaweza kutumika kama uthibitisho mbadala wa milki ya simu husika.
  1. Kuhimiza utii wa sheria: Kifungu cha 128 cha EPOCA kinamtaka mtumiaji wa simu kutoa taarifa ya kupotea au kuibiwa kwa simu au laini ya simu. Kifungu cha 134 kinayataka makampuni ya simu kutokutoa huduma kwa simu ambayo imefungiwa kama ilivyoelezwa hapo juu. Mara tu mteja anapopoteza simu yake ya kiganjani anatakiwa kutoa taarifa kwa kituo cha Polisi  cha karibu ambapo atapewa namba ya kumbukumbu ya taarifa ya tukio, maarufu kama RB. Anatakiwa aende kwa mtoa huduma kutoa taarifa ya tukio akiwa na hiyo RB na uthibitisho wa umilki wa simu iliyopotea (risiti aliyopewa wakati wa kununua iwapo itakuwepo).
Mtoa huduma kwanza atahakiki umilki wa simu iliyopotea au kuibiwa na atampatia mteja namba ya kumbukumbu kwamba simu hiyo imefungiwa isutumike kwenye mitandao ya simu na hatimaye ataifungia simu hiyo ndani ya saa 24.


  1. Kujenga misingi ya matumizi ya simu halisi, zisizo bandia. Mtumiaji ataweza kutambua iwapo simu aliyo nayo inakidhi viwango, ni halisi na sio bandia.

Kamati ya Bajeti Kufanya Mkutano wa Wadau wote wa masuala ya kodi

$
0
0

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa mujibu wa Kanuni ya 118 ya Kanuni za Kudumu za Bunge,  Toleo la mwaka 2016, Nyongeza ya Nane, Sehemu ya Tatu  Kifungu cha 9, imepewa jukumu la kusikiliza maoni na mapendekezo ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha kila mwaka.

Katika kutekeleza jukumu hilo, Kamati ya Bajeti imepanga kufanya Mkutano wa Wadau wote wa masuala ya kodi (Public Hearing) kwa ajili ya kusikiliza maoni yao na mapendekezo kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2016.

Mkutano huo umepangwa kufanyika siku ya Alhamisi Tarehe 16 Juni 2016 kuanzia Saa Tano asubuhi katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Mkoani Dodoma.
 
Kwa kuzingatia umuhimu wa Muswada huo, Kamati inawaalika wadau wote kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.

 Maoni ya wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa njia ya Posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo:

Katibu wa Bunge, 
Ofisi ya Bunge, 
S.L.P 941,
 DODOMA 
Barua pepe: cna@bunge.go.tz 
 
Imetolewa na,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano. Ofisi

Basi la Kampuni ya Tahmeed Lateketea Kwa Moto

$
0
0

Basi la Abiria la Kampuni ya TAHMEED linalofanya safari zake kati ya Tanga- Dar es Salaam, limeteketea kwa moto katika barabara ya Chalinze- Segera.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na ajali hiyo lakini mizigo ya abiri ndiyo imeteteketea ndani ya basi hilo.

Ajali imetokea wakati basi hilo likiwa limesimama baada ya Abiria mmoja kuomba Msaada akajisaidie (kuchimba dawa) na ndipo abiria waliokuwamo ndani ya gari alianza kusikia harufu ya moshi wa tairi linaloungua na ndipo wakatoka nje ya gari na muda mfupi gari lote likashika moto.

Benki Pitieni Upya Riba Zenu – Majaliwa

$
0
0

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezitaka benki nchini zipitie upya riba zake ili Watanzania waweze kukopa na kurejesha kwa urahisi.

Amesema riba kubwa zinazotozwa na baadhi ya benki, huduma zisizokidhi mahitaji na uelewa mdogo wa masuala ya kifedha ni miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo wananchi wanapotaka huduma za kifedha.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Juni 15, 2016) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Jumuiya ya Benki za Wananchi (COBAT) mjini Dodoma.

Mkutano huo ulijumuisha wajumbe kutoka mikoa 10 ya Kigoma, Lindi, Simiyu, Manyara, Katavi, Mbeya, Mwanza, Morogoro, Singida na Dodoma kati ya mikoa 18 ya Tanzania Bara ambayo bado haina Benki za Wananchi ila ipo katika hatua za kuanzisha.

Amesema changamoto nyingine ni kutokuwepo kwa taarifa mbalimbali za sheria na taratibu ambazo zinakwamisha ufanisi wa kiutendaji kwa baadhi ya taasisi hasa zile zinazolenga kuwahudumia watu wa kipato cha chini.

“Tunahitaji kutafuta njia bora ya kutatua changamoto hizi, na Benki za Wananchi ni kiungo muhimu katika kushughulikia changamoto zinazokabili utoaji wa huduma za kifedha,” amesema.

Waziri Mkuu amesema ni muhimu kuanzisha Benki za Wananchi katika kila Mkoa ili kuweza kusambaza huduma hizo karibu zaidi na walengwa, hali ambayo itasaidia kupunguza umasikini kupitia ukuaji wa shughuli za kiuchumi.

Amesema Serikali itaangalia uwezekano wa kuiwezesha mikoa ambayo itaonyesha ari zaidi ya kuanzisha benki zao na akatoa wito waandae mikakati ya kuhamasisha wananchi ili wakusanye mitaji ya kutosha.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa COBAT, Bibi Elizabeth Makwabe amesema Jumuiya yao ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa na wanachama saba na sasa hivi wamefikia 10 huku wananchi wanaowahudumiwa na benki hizo ni zaidi ya milioni mbili.

Amesema Jumuiya za Benki ya Wananchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo mfumo hafifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) pamoja na ufinyu wa mitaji.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,   
DODOMA.

JUMATANO, JUNI 15, 2016.

Simu Feki Kuzimwa Kesho Rasmi - TCRA

$
0
0
SIMU ziliingizwa nchini zikiwa hazina kiwango kuzimwa rasmi kesho, katika kuhakikisha kila mtu anatumia simu kiwango kwa usalama  na ulinzi wa nchi.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Mhandisi James Kilaba amesema kuwa katika uzimaji wa simu wameshatoa elimu juu ya simu hizo.

Kilaba amesema kuwa simu ambazo watu walibadilisha (Flash) nazo zitazimwa kutokana na kufanya hivyo ni kosa la kisheria na mtu anayefanya hivyo kifungo chake ni miaka 10.

Amesema hakuna kitu chochote kinachofanya simu zisiweze kuzimwa hivyo watu wajiandae kwa zoezi hilo na simu zitakazozimwa wametakiwa kuzihifadhi katika mazingira salama.

Aidha amesema wametoa elimu ya kutosha, hivyo kesho kutakuwa na mkutano wa wadau mbalimbali wa makampuni ya simu, na wamiliki wa maduka ya simu pamoja na mafundi katika kubadilishana mawazo wakati wa kuzima simu feki.

‘’Simu feki kesho zitazimwa, hatutakuwa na mabadiliko ya kuongeza muda au vinginevyo kutokana na elimu iliyotolewa juu ya simu ya  feki ambazo baada ya soko kushindikana mjini walipeleka vijijini’’amesema Kilaba  .

Watendaji Wabadhirifu Wa Bodi Ya Mikopo Kukiona –profesa Ndalichako.

$
0
0
WAZIRI wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa  Joyce Ndalichako ametangaza kiama kwa watendaji wote wa  Bodi ya Mikopo waliofanya ubadhirifu wa fedha za wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa kuwapa watu wasiohusika.

Joyce ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo. 

Amesema kuwa bodi ya mikopo baada ya kufanya ukaguzi maalum katika hoja 17 ni hoja moja imepata majibu na kuzaliwa dosari zingine ambazo ni kutokuwa na mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu kwa watu ambao wanarejesha mikopo.

Amesema kuwa kutokana na matatizo ya bodi ya mikopo ameigiza bodi kuhakikisha wanachukua hatua kwa watendaji wote waliosimamishwa ikiwemo kuwafikisha vyombo vya dola.

Joyce amesema kuwa katika dosari nyingine wanafunzi zaidi ya 2,000 wamepewa mikopo katika vyuo viwili lakini wanafunzi hao hawapo katika vyuo vilivyotajwa.

Amesema kuwa kuna wanafunzi wanalipwa sehemu mbili  ya mikopo ya bodi kwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa wakati mmoja huku kuna wanafunzi hawapati  mikopo kabisa na ni watoto wa masikini.

Aidha amesema bodi hiyo inatakiwa kufanyia kazi dosari zote pamoja na hatua ambazo wamezichukua kwa baadhi ya watendaji ambao wamefuja fedha za walipa kodi.

Joyce amesema kuwa matatizo mengine ni Baraza la Usajili wa vyuo vya  Elimu na ufundi (NACTE) kufanya  kazi ambazo wao wenyewe hawana uwezo nazo ikiwemo kukagua baadhi ya vyuo ambavyo vingine vinatoa digrii ya pili.

Amesema yote wanaangalia kwa kupitia sheria na kuona jinsi ya kuboresha utendaji kazi kwa NACTE

Rais Magufuli awataka watanzania kuungana na Waislamu walio katika mfungo kuliombea taifa

Shamba La Waziri Wa Serikali yhaMapinduzi Zanzibar Lavamiwa Na Kukatwakatwa Na Watu Wasiojulikana

$
0
0

SHAMBA la mikarafuu , minazi pamoja na mihogo la Waziri asiye na wizara maalumu Zanzibar Said Soud Said limevamiwa na kuhujumiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia june 14 mwaka huu .
 
Katika hujuma hizo zilizotokea katika shamba lililoko Mgelema Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake , jumla ya mikarafuu 29 , minazi 16 pamoja na mashina 250 ya muhogo yamengo’lewa na baadhi ya mengine kufyekwa na kitu chenye ncha kali .
 
Katika tukio hilo mikarafuu michanga  15 imeng’olewa na kutupwa ndani ya shamba , na mengine  14 iliyokuwa tayari kuzaa imekatwa na kuachwa ndani ya shamba .
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi , Said Soud Said alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinafanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini waliohusika na vitendo  hivyo vya kuhujumu mazao makuu ya uchumi wa nchi .
 
Aidha alieleza kwamba , baadhi ya wananchi wanalichukulia suala la siasa kama ni chuki au fitina , na kuwashangaa wanaoendesha humuma hizo kwani haziwezi kusaidia kutatua changamoto za kisiasa .
 
“Ni jambo la akushangaza kuona mikarafuu , minazi pamoja na mihogo inafanyiwa hujuma namna hii , ni vyema vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili wausika wapatikane na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria ”alisisitiza.
 
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla akizungumza katika eneo la tukio alisema Serikali imejapanga vyema kukabiliana na vitendo vya hujuma na kuwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya ulinzi kufanikisha kukamatwa kwa wahusika wa vitendo hivyo .
 
Alisema kwamba Serikali inategemea zao la Karafuu pamoja na minazi kwa ajili ya kukuza uchumi wake , na kwamba kitendo cha kukatwa kwa mikarafuu sio tu kwamba kinarudisha nyumba maendeleo ya mwananchi bali pia na Taifa kwa ujumla .
 
“Matendo haya kwa kweli sio kama yanaathari kwa mwenye shamba pekee , bali hta uchumi wa Nchi unaathirika kwani Serikali inategemea sana zao la karafuu kupata fedha za kigeni ”alieleza .
 
Kwa upande wake kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan ameahidi kwamba askari wataendesha doria na msako wa kuwasaka wahusika ili waweze kufikishwa kwenye mahakamani .
 
Alisema kwamba katika msako huo , watawatumia askari Shehia , Polisi jamii pamoja na wananchi wa kawaida na kuongeza kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua hata kama watakuwa nje ya Mkoa huo .
 
Kwa hili hatutakuwa na huruma na mtu , tutafanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za jeshi ,pia tutawatumia askari shehia , polisi jamii pamoja na raia wema abao wamekuwa wakitupa taarifa ”alisisitiza .
 
Hivyo Kamanda shekhan amewataka wananchi kutotumia fursa hiyo kutoa taarifa ambazo sio sahihi na ambazo zinawahusu wananchi wenye chuki binafsi. Na kwamba jeshi la polisi litazifanyia uchunguzi taarifa hizo kabla ya kuzichukulia hatua .
 
Matendo ya hujuma kwa baadhi ya mali za wananchi yanaendelea kutokea katika mikoa ya Pemba baada ya kumalizika uchaguzi Mkuu wa marejeo uliofanyika machi 20 mwaka 2016 yakihusishwa na itikadi za kisiasa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 16

Taarifa ya CUF: Kauli ya Maalim Seif kuhusu maombi ya Prof. Lipumba kurejea uongozini

Serikali Kutunga Sheria Kupiga Marufuku Wasichana Wa Kazi Chini Ya Miaka 18

$
0
0
SERIKALI imekusudia kutunga sheria ya kupiga marufuku ajira za wasichana wa kazi wenye umri chini ya miaka 18 kabla ya mwisho wa mwaka 2016.
 
Hatua hiyo inaelezwa inakusudia kuinua hadhi ya kazi na ajira  za wasichana wa kazi nchini, kwani muda wa kurasimisha ajira hizo umefikia wakati wake.
 
Hayo yamebainishwa jana mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumzia na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika inayoadhimishwa tarehe 16 Juni kila mwaka.
 
Alisema hatua inachuliiwa na Serikali kutokana na wasichana wengi wa ndani  kutumikishwa kazi hiyo katika umri mdogo na kulipwa ujira mdogo.
 
“Tumepanga kutunga kanuni na sheria ya kupiga marufuku ajira za wasichana wa kazi wenye umri chini ya miaka 18, na ndio maana tunawachukua katika umri mdogo sana na kuwalipa ujira mdogo, hivyo ukimchukua binti wa miaka 18 utaweza kuinua hadhi ya kazi ya kazi yenyewe” alisema Waziri Ummy.
 
Akizungumzia kuhusu maadhimisho hayo, Waziri Ummy aliitaka jamii kukataa kurubuniwa kwa pesa na katika kuwafichua watu wanaofanya vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo kulawiti na kuwabaka na badala yake watoe taarifa katika vyombo vya dola ili adhabu kali zichuliwe dhidi yao.
 
Aidha Waziri Ummy aliwata wazazi nchini kujenga tabia ya kukagua maumbile ya watoto wao hususani watoto wa kike ikiwemo kuwaogesha angalau mara moja kwa mwezi, kwani kwa kufanya hivyo kutamwezesha mzazi kufahamu afya ya kimwili ya motto wake.
 
Kwa mujibu wa Waziri huyo alisema vitendo vya ulawiti havifanywi kwa watoto wa kike pekee bali na watoto wa kiume pia wamekuwa wahanga wa vitendo hivyo, ambapo ameitaka jamii kutowaamini ndugu au jamaa zao kulala kitanda chumba kimoja na watoto wao.
 
“Kwa mujibu wa taarifa za jeshi la Polisi, vitendo hivi vimekuwa vikifanyika zaidi majumbani kwa asilimia 49,  asilimia 23 wakati wa kurudi na kwenda shule na asilimia 15 wakiwa shuleni, hivyo kwa takwimu hizi unaweza kuona ukubwa wa tatizo ulivyo” alisema Waziri Ummy.

Shirikisho La Wanafuzi Vyuo Vya Elimu Ya Juu Tanzania Lalaani Kauli Za Gwajima Juu Ya Viongozi Wa CCM

$
0
0
Siku chache baada ya Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kuwashutumu viongozi wa CCM kwamba wanamipango ya kutomkadhi chama Rais Dk. John Magufuli, Shirikiho la Wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), limemshukia na kulaani vikali kauli hiyo kwamba ni yauchochezi.

Akizungumza jana latika Ofisi za Shirikisho hilo, jijini Dar es Salaam, Katibu wa TAHLISO Siraji Madebe, amesema, Gwajima kama kiongozi wa dini ajitokeze hadharani kutaja viongozi anaodai walimpigia simu kuelezea mkakati huo wa kutomkabidhi Chama Dk. Magufuli.

SOMA TAARIFA KAMILI KAMA ILIYOTOLEWA NA TAHLISO
Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania limeshitushwa na taarifa za uchochezi zilizotolewa na kiongozi wa dini wa kanisa la Ufufuo na Uzima hivi karibuni likituhumu viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuwa na mipango ya kutokumkabidhi Chama Raisi  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mh. John Joseph Pombe Magufuli.

Sisi kama Vyuo Vikuu tunalaani vikali sana kauli yenye dalili za uchochezi zinazotaka kupandikiza chuki miongoni mwa viongozi wetu wa Serikali  na Chama kwa ujumla.

Lakini kama kiongozi wa dini mwenye hofu ya Mungu tunamtaka ajitokeze kuwataja hadharani wale waliompigia simu kumuomba awasaidie bila kuwasahau na wale wanaozunguka mikoani kwa ajili ya kuhamasisha zoezi hilo kama alivyoeleza.

Ndugu waandishi wa habari, pamoja na mambo mengine kwa faida ya watanzania kiongozi huyu angetaka ufafanuzi juu ya jambo hili angewasiliana na katibu wetu wa Chama cha Mapinduzi Comrade Abdulrahman Kinana au Naibu Katibu Mkuu wetu wa Chama Cha Mapinduzi Comrade Rajab Luhavi badala ya kwenda kuaminisha waumini na watanzania jambo lisilokuwa na uhakika.

Lakini ndugu zangu katika maelezo yake alidhihirisha wazi kwamba hakiungi mkono Chama Cha Mapinduzi na pia hakumuunga mkono mhe. Rais katika kipindi cha kampeni, hivyo asichukue nafasi hiyo ya kutaka kugombanisha na kukisambaratisha Chama Chetu.

Tunatoa rai kwa viongozi na Taasisi za kidini zote nchini kutojihusisha na masuala ya kisiasa na badala yake kutekeleza majukumu yaliyokusudiwa kwa uwepo wao. 

Kuhusisha siasa na dini ni kuchochea uhasama na kupandikiza mbegu za chuki, vurugu, uchochezi na kuhatarisha uvunjifu wa amani baina ya wananchi, viongozi na Taifa kwa ujumla. 

Hivyo hatuko tayari kuwavumilia watu wote wenye nia ya kutuvurugia amani tuliyo nayo na kutuingiza kwenye migongano ya kidini.

Tanzania ni moja na watanzania ni wamoja bila kujali tofauti za kisiasa, kidini na kikabila.

Mwisho tunapenda kuiomba serikali kupitia vyombo vya dola kushughulikia kwa kina jambo hili na kulichukulia hatua ili kukomesha vitendo vya uchochezi baina ya watanzania na baina ya viongozi.

Rais Magufuli Amteua Dk Rubaratuka Kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

$
0
0

Rais John Magufuli amemteua Prof. Ignas Aloys Rubaratuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia Mwezi Aprili mwaka huu.

Taarifa hiyo ilitolewa na Dk. Leonard Chamuriho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano jana  jijini Dar es Salaam.

“Kwa mujibu wa sheria Na. 17 ya mwaka 2004 ya Mamlaka ya Usimamizi wa bandari nchini rais Magufuli amemteua Pr. Rubaratuka ambaye alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TPA,” alisema Chamuriho.

Alisema kuwa Makame Mbarawa, Waziri wa Uchukuzi ameteuwa watu wanane kuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika kipindi cha miaka mitatu.

“Aidha, Waziri mwenye dhamana ya sekta ya uchukuzi kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa kifungu Na. 6(2) cha sheria Na. 17 ya TPA ameteua watu nane kuwa wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya TPA,” amesema.

Alitaja wajumbe hao na vitengo vyao wakiwemo Jaffeer Mchano kuwa Mkurugenzi wa Mipango na Huduma wa Tanzania Investment Bank, Deusdedit Conatus Kakoko kuwa Meneja Miradi Tanroads.

Wengine ni Malata Pascal, Mkurugenzi Msaidizi, Division of Litigation and Abritration na Masanja Kungu Kadogosa kuwa kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).

Polisi Dar es Salaam Wamng’ang’ania Zitto Kabwe

$
0
0
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imesema inaendelea na upelelezi kuhusu tuhuma zinazomkabili Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Kabwe Zitto ambaye ni Mbunge Kigoma Mjini na watakapokamilisha atafikishwa Mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema, sababu za kumhoji Zitto ni kutokana na kauli za uchochezi alizozitoa katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Zakhem, Mbagala.

Alisema, tayari Zitto ameshahojiwa katika kituo hicho mara mbili, lakini bado jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili kujiridhisha dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Sirro alisema jeshi hilo haliwezi kuruhusu siasa ambazo zinavunja amani, hivyo ameendelea kuwataka wanasiasa kufuata taratibu na endapo wamekataza kufanya mikutano basi watii.

“Kama hakuna amani hakuna siasa hatuwezi na hatutakubali kuruhusu amani tuliyonayo itoweke sababu ya wanasiasa lazima kutii ili kulinda amani yetu,” alisema Sirro.

Hivi karibuni Zitto alijisalimisha Kituo cha Polisi na kuhojiwa kwa zaidi ya saa tatu baada ya kuandikiwa barua ya kuitwa kituoni na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Camilius Wambura.

Hatua ya Zitto kuhojiwa ilitokana na maudhui ya hotuba yake aliyoitoa Juni 5, mwaka huu kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Zakhem, Mbagala wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kutoka katika mahojiano hayo, Zitto alisema haoni kama hotuba aliyoitoa ina tatizo lolote, kwani hotuba hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kisiasa.

Simu FEKI Kuzimwa Leo.....Mafundi Wapewa ONYO Kali

$
0
0
IKIWA leo saa sita usiku Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatarajia kuzima simu feki za mkononi, mafundi wa simu nchini wanatakiwa kuanza mchakato wa kupata leseni ya kutengeneza simu kutoka mamlaka hiyo.

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa uamuzi wa kuzima simu feki.

Alisema mafundi wa simu, wanatakiwa kuomba leseni ya kutengeneza simu na kuweka utaratibu wa kuwaorodhesha wanaoleta simu zao kutengenezwa ili kuepuka kuwa sehemu ya mtandao wa wizi wa simu.

Akizungumzia simu feki, Kilaba alisema idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango, zimebaki kuwa ni asilimia 2.96 huku namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zimefika 0.09.

Kilaba alisema idadi ya namba tambulishi, ambazo hazina kiwango zimepungua kutoka asilimia 3 kwa mwezi Mei hadi kufikia asilimia 2.96 huku namba tambulishi zilizonakiliwa zimepungua kutoka asilimia 2 hadi 0.09.

Alisema idadi ya namba tambulishi za simu halisi, imeongezeka kutoka asilimia 85 mwezi Mei mwaka huu hadi kufikia asilimia 96.95 ilipofika juzi.

Wakati TCRA inazindua mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi Desemba mwaka 2015, idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango (bandia) zilikuwa sawa na asilimia 4 na zile ambazo zilikuwa zimenakiliwa zilikuwa ni sawa na asilimia 30.

“Pamoja na kuwapo idadi ndogo ya watu ambao wanatumia simu feki, msimamo wetu bado uko palepale ifikapo kesho (leo) saa sita usiku, maana suala la usalama halitegemei idadi ndogo ya simu hizo,” alisema.

Aliwakumbusha Watanzania wote kuwa ni jukumu la kila mmoja, kuhakikisha kuwa simu yake ni halisi na sio bandia, kwani kuanzia leo, hakuna simu bandia itakayoweza kufanya kazi nchini.

“Nawakumbusha wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi kutambua kuwa ni kosa kubadilisha namba tambulishi za vifaa vya simu za mkononi, kwani adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka kumi (10) au faini isiyopungua Sh millioni 30 au vyote kwa pamoja."

Kilaba aliwataka wanaofanya biashara za kuingiza simu hapa nchini kutoka nje, wahakikishe kuwa simu wanazoleta zinakidhi viwango, zimehakikiwa kwa mujibu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kuwa na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano kwa mujibu wa Sheria.

Watuhumiwa wa Ubakaji na Waliosambaza Picha za Uchi za Msichana Morogoro Waendelea Kusota Rumande

$
0
0

Waendesha mashtaka wa serikali Morogoro wamepewa miezi miwili kuwasilisha cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili kuachia ama kuendelea kushikilia dhamana ya washtakiwa wanne wa kesi ya usambazaji wa picha chafu za ngono.

Washtakiwa hao ni wale waliopiga picha chafu za ngono dhidi ya mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Dakawa, Mvomero.

Mbele ya waendesha mashtaka wa serikali Gloria Rwakibalila, Edgar Bantulaki na Calistus Kapinga ilidaiwa mahakamani hapo na Ivan Msacky, Hakimu wa Mahakama hiyo kuwa, suala la dhamana chini ya Katiba ni haki ya kila mshtakiwa lakini akaonesha kushangazwa na upande wa mashtaka kutoeleza kwa uwazi sababu za kuendelea kuizuia dhamana hiyo.

Hakimu Msacky amewataka waendesha mashtaka hao kuhakikisha wanawasilisha mahakamani cheti kinachozuia dhamana kwa washtakiwa hao na sababu zake ili kesi hiyo iweze kuanza kusikilizwa.

Kesi hiyo ya jinai namba 54 ya mwaka 2016 inawakabili washtakiwa sita ambao ni Idd Adam Mabela, Zuberi Thabit, Rajab Salehe, Ramadhani Ally, Muksin Ng’ahy na John Peter ambao wanakabiliwa na shtaka la kusambaza picha chafu za ngono za msichana mwenye umri wa miaka 21 wilayani Mvomero mkoani humo. Washtakiwa wanaotaka dhamana ni mshtakiwa namba tatu hadi sita.

Hata hivyo, Hakimu Msacky jana aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe 29 Juni mwaka huu ambapo kesi hiyo itaendelea kujadili suala la dhamana kwa washtakiwa hao.

Katika kesi hiyo iliyosikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 18 Mei mshtakiwa namba 1 na 2 wanatuhumiwa kumbaka na kumuingilia kinyume na maumbile msichana huyo Aprili 27, saa 1 usiku katika nyumba ya kulala wageni ya TITII iliyopo katika Tarafa ya Dakawa, Mvomero.

Katika kesi ya kwanza ya kubaka na kulawiti inayowakabili washtakiwa Mabela na Thabiti, wakazi wa jijini Mbeya ilishindwa kusikilizwa jana  kutokana na wakili wa washtakiwa Mohamed Mkali kutokuwepo mahakamani.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images