Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wanafunzi wahaha Baada ya Serikali Kukifunga Chuo cha Mbeya Polytechnic Kwa Tuhuma za Kudahili Wanafunzi Wasio na Vigezo

$
0
0
Ellertoni Mwamasika (Mkurugenzi wa Chuo cha PolyTechnic)

Baraza la Udhibiti wa Vyuo vya Ufundi nchini Tanzania NACTE imekifungia chuo cha Biashara, Mifugo na Kilimo cha Mbeya Polytechnic kwa kushindwa kukidhi vigezo ikiwa ni pamoja na kudahili wanafunzi wasio na sifa.

Akisoma uamuzi huo kwa niaba ya NACTE, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla amesema kuwa taarifa kutoka NACTE zinaonesha kuwa chuo hichi kina mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya mifugo ambayo hayajathibitishwa na vyombo husika vya serikali.
 
Pia amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikidahili wanafunzi wasiokuwa na vigezo, akitolea mfano wanafunzi wanaosoma kozi ya mifugo ambapo kati ya wanafunzi 359 ni wanafunzi 89 pekee ndiyo wanaotambulika kuwa na vigezo husika.

Wakizungumza kwa uchungu baadhi ya wanafunzi wamelalamikia chuo hicho kwa kuwasababishia upotevu wa muda na gharama, ambapo baadhi yao walikuwa tayari wamehitimu na walikwenda chuoni hapo kufuatilia vyeti.

“Mimi nimetoka mbali, nimekuja kufuatilia cheti changu, sasa nina miezi miwili hapa, kila siku nazungushwa nazungushwa, kumbe walijua wanakuja kufungiwa, kwahiyo cheti changu sipati, na muda nimepoteza, nimekaa hapa miaka mitatu halafu leo naambiwa miaka yangu mitatu haina maana tena, sikubali sikubali..” amesema mwanafunzi Catherene Buda
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo hicho Ellertoni Mwamasika, ameomba radhi na kusema kazi ya kuendesha chuo ni ngumu “Chuo kinawaomba radhi wote, ila mjue kuwa kazi hii ya kuendesha chuo ni ngumu”

Hata hivyo serikali imesema wanafunzi wenye sifa watahamishiwa katika vyuo vingine huku ikimuagiza mmiliki wa chuo hicho kuwalipa wanafunzi gharama zao zote kabla hawajatoka chuoni hapo.

Ole Medeye Atimka Chadema Na Kuhamia UDP Leo .....Kilichomfanya Ahame ni Wabunge wa Upinzani Kutomheshimu Naibu Spika

$
0
0
Kada wa Chadema na mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye ametangaza leo rasmi kuhamia chama cha UDP.

Ole Medeye amezungumza hayo mbele ya mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho,Mwananyamala jijini Dar.

Medeye amezungumza kwa kujipambanua kuwa yeye anasimamia haki na demokrasia, na kwamba amekerwa sana na tabia ya vyama vya Upinzani kutomheshimu Naibu Spika,Dkt. Tulia Ackson Mwansasu,pichani kati ni Mwenyekiti wa chama cha UDP,Mh.John Cheyo akishuhudia tukio hilo.

Ole Madeye ambaye amehamia chama hicho ikiwa ni baada ya miezi tisa tangu alivyojiunga na Chadema akitokea CCM Agosti 2015,  amekabidhiwa kadi ya UDP na Mwenyekiti wa chama hicho, John Cheyo akiwa na wafuasi wengine tisa wapya kutoka Chadema akiwamo mke wake, Anatonia Lekule.
 
Amesema alipitia katiba za vyama vyote hajaona katiba inayosimamia misingi ya kidemokrasia ya kweli na kwamba UDP ndiyo chama pekee Tanzania chenye katiba inayotetea demokrasia.

Watanzania Watakiwa Kushirikiana Kupiga Vita Matukio Ya Mauaji

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania, viongozi wa dini zote kushirikiana kwa pamoja kupiga vita matukio maovu ya mauaji yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema anatarajia hali ya amani, usalama na utulivu inaendelea kuwepo nchini, hivyo wananchi hawana budi kushirikiana na kushikamana na Serikali katika kuhakikisha matendo maovu hayatokei katika maeneo yao.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Jumamosi, Juni 11, 2016) wakati  alipowasili mkoani Geita kwa ajili ya kuhudhuria ibada ya kuwekwa wakfu Padre Flavian Kassala kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Geita.

“Mfano tukio la Mwanza watu wanavaa kanzu na wanaingia msikitini na kukuta wenzao wanafanya ibada kisha wakawachinja, hii haiwezekani kwa binadamu wa kawaida hivyo tushirikiane katika kupiga vita matendo haya,” alisisitiza.

Hivi karibuni jumla ya watu 15 waliuawa kwa kukatwakatwa na mapanga katika mikoa ya Mwanza,Tanga, Dar es Salaam  na Mara.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga amesema vitendo vya watu kuuawa kwa kukatwa mapanga vimepungua baada ya kuanzisha kampeni maalumu ya kukemea mauaji hayo.

Alisema katika kampeni hiyo wameamua kuwatumia walimu, viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wauguzi ambao wamekuwa wakiwaelimisha wananchi kuachana na imani potofu za kishirikina na badala yake wajikite katika masuala ya maendeleo.

Taarifa ya ACT-Wazalendo baada ya polisi kuzuia kongamano la kuchambua Bajeti

$
0
0
Baada ya Jeshi la polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, Chama Cha ACT- Wazalendo kilipanga kufanya kongamao Jumapili ya June 12 2016 kwa lengo la kujadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017.

Taarifa iliyotolewa na chama cha ACT-Wazalendo kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho Anne Mghwira imesema kwamba kongamano hilo lililenga kumpa fursa ya pekee kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe kusema yale ambayo angeyasema bungeni baada yeye na wabunge wenzake sita wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bajeti bungeni.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika hali isiyo ya kawaida walipewa taarifa na mwenye ukumbi (LAPF Millenium Tower) kwamba polisi walikuwa wametanda katika eneo la ukumbi tangu saa kumi na mbili asubuhi na ilipofika saa nne kamili asubuhi mwenye ukumbi aliwataarifu rasmi kuwa amepewa taarifa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni kwamba chama chao hakina kibali cha kufanya kongamano hilo na hivyo asiwafungulie ukumbi huo.

Hivyo kupitia taarifa hiyo chama ACT-Wazalendo kimesema kimesikitishwa sana na hatua hiyo ya polisi na wanaitafsri kuwa ni mwendelezo wa hatua za uhakika katika kufifisha demokrasia katika nchi.

Majaliwa ahudhuria sherehe za kumsimika askofu Geita

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Askofu wa Jimbo la Geita , Mhashamu Flavian Kassala  katika Ibada ya kusimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki la Geita Juni 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Maliwa akiwapungia waumini wa Kanisa katoliki  jimbo la Geita baada ya kuhudhuria sherehe za kumsimika Askofu wa jimbo hilo, Flavian Kassala  zilizofanyika mjini Geita Juni 12, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Taarifa ya ACT- Wazalendo Kuhusu Kupotea Kwa Zitto Kabwe Tangu Jana Jioni

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA
Tunaujulisha UMMA kwamba Kiongozi wa Chama chetu cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe amekuwa anatafutwa na Polisi tangu jana usiku.

Mpaka sasa hatujui Kiongozi wetu yupo wapi na yupo kwenye Hali gani. Askari kanzu wanalinda nyumbani kwake na kwa watu wake wa karibu. 

Sisi kama chama tunaliambia jeshi la Polisi kuwa lolote litakalotokea kwa Kiongozi wetu wao watajibu kwa umma.
 
Msafiri Mtemelwa,
Kaimu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya June 13

Waziri Mkuu Awataka Viongozi Wa Dini Kushirikiana Na Serikali Kupambana Na Rushwa, Ufisadi

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili zikiwemo za rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Amesema siku zote kumekuwa na ushirikiano mzuri kati ya Serikali na Asasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya Dini katika kuwapatia huduma za kijamii kama vile, afya, elimu, maji, utunzaji wa mazingira na nyingi nyingine.

Waziri Mkuu Majaliwa aliyasema hayo jana mchana (Jumapili, Juni 12, 2016) wakati alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli katika Ibada ya kuwekwa wakfu  na kusimikwa kuwa Mhashamu  Askofu Flavian Kassala kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Geita.

“Serikali inatambua jitihada kubwa zilizowekwa na Kanisa Katoliki katika Jimbo hili la Geita na Tanzania kwa ujumla hivyo wito wangu kwa Baba Askofu na Waumini wa Kanisa kwa ujumla wenu ni kuwaomba muendelee na kazi hii nzuri ya kutoa huduma muhimu kwa jamii,” alisema.

Alisema maendeleo ya nchi yanawategemea wote hivyo ushirikiano  kati ya Kanisa na Serikali utawezesha maendeleo ya Taifa kupatikana kwa kasi zaidi na kunufaisha wananchi wote.

Waziri Mkuu alisema jukumu la Serikali ni kuweka mazingira wezeshi ambayo yatasaidia Mtanzania kujikomboa na umaskini na kwamba kazi kubwa ya viongozi wa dini kuunganisha jamii na wala siyo kuwatenganisha.

Hata hivyo Waziri Mkuu alisema kinachotakiwa kufanywa na wote ni kumwuomba Mwenyezi Mungu awawezesha kuwaelewa viongozi walioko madarakani na kutii maelekezo yanayotolewa kwani hata vitabu vya dini vinaelekeza kutii mamlaka.

Alisema iwapo waumini watatii na kuzingatia mafundisho ya kiroho yanayotolewa na viongozi wao wa dini ni dhahiri kwamba yatajenga imani miongoni mwao na upendo utatawala katika jamii nzima.

Waziri Mkuu alisema Serikali itaendelea kushirikiana na Madhehebu yote katika kuwahudumia Watanzania wote bila ubaguzi, hivyo aliwasihi waendelee kuwekeza katika huduma za jamii ikiwemo Shule, Vyuo, Zahanati kwa kuwa wana jukumu la kushirikiana kwa pamoja kujenga taifa.

Wakati huo huo Waziri Mkuu aliwaomba wote kwa pamoja waunge mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli katika kupambana na uzembe, ubadhirifu na wote wanao kiuka maadili ya utendaji wa kazi.

Kwa upande wake Askofu Renatus Nkwande wa Jimbo la Bunda ambaye alikuwa msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki Geita amewaomba waumini kumpa ushirikiano Askofu mpya wa jimbo hilo.
 
 IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, JUNI 12, 2016.

Utendaji wa Mkuu wa Wilaya Wakwaza Madiwani Morogoro

$
0
0

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamesa hawajaridhishwa na utendaji kazi wa Mkuu wa Wilaya hiyo, John Henjewele kushughulikia migogoro ya ardhi inayoendelea wilayani humo.

Waliyasema hayo katika mkutano na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi mwishoni mwa wiki iliyopita juu ya utatuzi wa migogoro ya ardhi wilayani humo.

Diwani wa Mbigiri, Juma Rajab alisema amejaribu  kufika ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya kuhoji uhalali wa mashamba kuendelea kushikiliwa na wawekezaji hewa ambao hawayaendelezi, lakini hapati ushirikiano.

Diwani wa Kata ya Makole, Anfas Kaunda alimueleza Lukuvi kuwa kuna shamba namba 35 lililopo Kijiji cha Mambeya ambalo lilifutiwa hati na kurejeshwa serikalini tangu 1984, lakini hadi leo halijakabidhiwa kwa kijiji.

Akizungumza  baada ya mkutano, Henjewele alisema diwani huyo ana mgogoro na wananchi wake ambao amewakodisha mashamba ya Serikali kwa gharama kubwa.

Pemba Walalamikia Kupigwa Mabomu ya Machozi Zaidi ya 100.........Ni katika vijiji Ambavyo watu Wasiofahamika waliharibu na kufyeka mazao

$
0
0

Wakazi wa Pemba wamelalamikia Jeshi la Polisi kuvamia maeneo yao na kupiga mabomu ya machozi na kufanya doria usiku wa kuamikia juzi katika mitaa na vijiji mbalimbali kisiwani humo na kuzua hofu miongoni mwao.

Maeneo yaliyokabiliwa na hali hiyo ni pamoja na Mahuduthi, Kengeja, Mgagadu na Kiwani, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba ambako polisi wanadaiwa kupiga mabomu ya machozi zaidi ya 100 na kutumia risasi za mpira kuwatawanya watu.

“Ilikuwa saa 1.30 usiku (wa kuamkia Jumamosi), gari za polisi zilifika kiamboni (kijijini) kwetu zikipiga misere kwa kasi, sote tukawa na hofu, watu walikimbia na kwenda kujificha, wengine waliumia na baadaye wakapiga mabomu mfululizo, sijui waliondoka saa ngapi maana tulijifungia ndani,” alisimulia Zuberi Said (34), mkazi wa Kiwani.

Baadhi ya wakazi wa vijiji hivyo walidai huenda hatua hiyo ya polisi ilitokana na matukio ya kuhujumu mali za viongozi wa Shehia yanayoendelea.

Inadaiwa kuwa watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Ijumaa waliteketeza miti na mashamba yanayomilikiwa na Sabiha Mohamed Ali na Abdalla Makame Hamad, ambao ni mashekha wa Shehia za Kendwa na Kiwani wilayani humo.

Ilidaiwa watu hao pia waliteketeza migomba na mikarafuu mali ya viongozi hao na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Hemed Suleiman Abdallah aliyefika kujionea uharibifu huo alisema: “Sijui sababu ni nini, ila huenda ni kutokana na siasa chafu zinazoendelea hapa.”

Alilitaka Jeshi la Polisi na askari alioongozana nao katika ziara hiyo kufanya uchunguzi haraka ili kuwabaini na kuwakamata watu waliohusika na vitendo hivyo. “Wala msisubiri baada ya miezi 20 ndipo mkaanza kuchukua hatua,” alisema.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mkoani Pemba, Mohamed Salim aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya Abdalla, alikiri kuwapo kwa hujuma na kuwatuma askari katika vijiji hivyo kufanya doria.

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

CCK Yamkingia Kifua Naibu Spika Dk Tulia Ackson

$
0
0
CHAMA Cha Kijamii (CCK) kimelaani mpango unaofanywa na wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wa kutaka kumng’oa Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson na kimewataka kufuata kanuni za uendeshaji wa Bunge.

Hayo yamo kwenye taarifa ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCK, Constantine Akitanda aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana, iliyotokana na tathmini ya Bunge tangu kurejeshwa Mfumo wa vyama vingi vya siasa, chanzo na kupevuka kwa ususaji wa shughuli za Bunge.

Kuhusu mpango wa kutaka kumng’oa Dk Tulia, Mwenyekiti huyo wa CCK alisema; “Hivi sasa kuna propaganda inayoenezwa ya kutaka kumng’oa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa madai ametumwa na Rais kuminya uhuru na demokrasia ndani ya Bunge.

“Hii si mara ya kwanza kwa kambi ya rasmi ya upinzani kulalamikia kiti cha Spika. Pia si mara ya kwanza kwa kambi hiyo kususa na kutoka nje ya bunge, pia si mara ya kwanza wabunge wa upinzani kukorofishana na kiti cha spika na kususa,” alisema.

Akitanda alisema tatizo la kambi hiyo ni pale spika anaposimamia kanuni huku wao wakikataa kwa makusudi, kufuata taratibu na kanuni za uendeshaji wa shughuli za Bunge, jambo alilosema haliwezi kufumbiwa macho.

“Kanuni zipo wazi kama hujaridhika na maamuzi ya kiti cha Spika unaruhusiwa kukata rufaa na hoja ikajadiliwa, sasa wabunge wetu wa Kambi Rasmi ya Upinzani sijui ni kwa nini hawataki kufuata utaratibu huu, ambao ni wa kikanuni.Wao wanataka kumng’oa Naibu Spika tu basi, kanuni je?” 

Alisema dalili za kukataliwa kwa Naibu Spika na wabunge hao zilionekana tangu mwanzo kwani walimkataa hata kabla ya kuanza kazi kwa madai kuwa ametumwa na Ikulu, na hata siku ya kujieleza akiomba kura alikuwa anazomewa na wabunge wa kambi hiyo.

“Kimsingi tangu mwanzo wabunge wetu wa upinzani hawakumtaka Dk Tulia kutokana na umahiri wake wa kuzijua na kuzisimamia kanuni kwa ustadi mkubwa.”  

Akitanda alisema tangu Bunge la vyama vingi lianze mwaka 1995, wabunge wa upinzani kutokana na uchache wao wamekuwa wanalalamikia kiti cha Spika na kutofautiana na Spika au kudai wanaburuzwa na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema katika kipindi cha mwaka 2010 hadi sasa ambapo Chadema kwa mara ya pili imetoa kiongozi wa upinzani bungeni, nchi imeshuhudia wabunge wa upinzani wakitumia muda mwingi kulalamikia kiti cha Spika.

“Kwa kipindi cha 2010 hadi 2015, Spika wa Bunge alikuwa Anne Makinda na Naibu Spika Job Ndugai. Wapinzani walimlalamikia sana spika wakimtuhumu kuwa anailinda serikali na kuwa kiti cha Spika kimemshinda."

Alisema picha ambayo Watanzania wanaipata kutoka kwa Kambi Rasmi ya Upinzani yenye nia ya kumng’oa Dk Tulia kwa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye, ni mwendelezo wa wazi wa udhalilishaji wa wanawake kuwa hawana uwezo wa kuongoza.

Lipumba kueleza hatima yake ndani ya CUF leo

$
0
0

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, leo anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari   kueleza hatima yake ndani ya chama hicho.

Habari zinasema amechukua hatua hiyo baada ya kuibuika   wimbi la wana CUF kumtaka arudi katika nafasi yake ya uenyekiti huku chama hicho kikitangaza kufanyika kwa mkutano mkuu  Agosti 21, mwaka huu.

Wakati hayo yakiendelea taarifa za ndani zinaeleza kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita Profesa Lipumba, aliondoa barua yake ya kujiuzulu uenyekiti na  alikutana na Katibu Mkuu wa CUF na kujadili kwa kina suala hilo.

Chanzo chatu cha uhakika ndani ya CUF kilisema  baada ya mazungumzo ya kina, Maalim Seif  alimthibitishia Profesa Lipumba, kupokewa kwa barua yake huku akimuomba asubiri ushauri wa wanasheria kuhusu hatima yake ya kurejea ofisini.

“Kesho (leo) Profesa atazungumza na wana habari asubuhi na kikubwa ataeleza kwa kina hatima yake ndani ya CUF.

“Kikubwa tunategemea atafungua ukurasa mpya na kutangaza kukijenga chama chetu,” alisema mtoa habari wetu ambaye yupo karibu na Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba   alijiuzulu nafasi hiyo Agosti 5, mwaka jana kwa kile alichodai kutoridhishwa na hali ya mambo ikiwamo umoja ndani ya Ukawa na kupokewa kwa aliyekuwa mgombea urais aliyekuwa anaungwa mkono na vyama Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na vuguvugu la wana CUF kuendesha makongamano nchi nzima kutaka     Profesa Lipumba arudi kwenye madaraka kwa madai kwamba   chama hicho kimekosa mtu imara upande wa Bara.

Licha ya hali hiyo wanachama hao walikuwa wakitaka  uitishwe Mkutano Mkuu Maalumu ambao unatakiwa kujadili hoja ya kujiuzulu kwa Profesa Lipumba, kwa mujibu wa Katiba ya CUF.

Godbless Lema Amnyooshea Kidole Mwigulu Nchemba

$
0
0

WAKATI  Rais Dk. John Magufuli akitarajiwa kumwapisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, Ikulu, Dar es Salaam leo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amemnyooshea kidole waziri huyo.

Kupitia taarifa yake   kwa vyombo vya habari jana, Lema ambaye ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, alisema  wizara hiyo ni nyeti na muhimu kwa usalama wa taifa  hivyo Mwigulu anapaswa kuwa makini, mwangalifu na mwenye utulivu.

“Ni heshima kubwa uliyopewa na Rais, unapaswa kuwa makini, mwangalifu na mwenye utulivu. Natarajia   jambo la kwanza utakalofanya ni kutambua kuwa  na wingi wa silaha za kisasa kwa askari wetu si suluhisho la ulinzi na amani katika taifa letu, bali haki na matumaini ya wananchi ndiyo msingi madhubuti wa amani na utulivu wa nchi.

“Polisi wetu na askari magereza wanaishi maisha magumu, mishahara haitoshi  wanahitaji uelewa wako juu ya maisha yao na kazi zao.

“Umeteuliwa wakati  Serikali kupitia jeshi la polisi inatumia nguvu zote kukandamiza na kuangamiza demokrasia.

“Vyama vya siasa vimezuiwa kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima kwa sababu ambazo hazina msingi wowote kinyume cha sheria na Katiba ya nchi, huku pia uhuru wa maoni, habari na taarifa ukiwa shakani,” alisema.

Alisema taifa linatarajia Waziri Mwigulu atakuwa  mshauri mzuri wa Rais  Magufuli kuhusu masuala hayo pamoja na wajibu wa polisi katika demokrasia kwa sababu  kuitia  shaka demokrasia ni kuharibu ustawi wa jamii nchini.

Alimshauri  Mwigulu  kutafuta waraka wa hotuba ya kambi ya upinzani kwa wizara hiyo iliyozuiliwa kusomwa bungeni kwa sababu ina mambo mengi ambayo yanaweza kumsaidia.

“Kuna mambo mengi tulilieleza katika hotuba  yetu… ni vema ukaitafuta hotuba hiyo na ukatazama kwa makini mambo ambayo yalizuiwa kusomwa na uone namna utakavyowajibika juu ya mambo hayo.

“Hapo ndipo unapaswa kuanzia. Na wananchi wanasubiri kukupima katika hilo.

“Hata hivyo, ninakutakia kila la heri katika wajibu wako huu mpya, ninafahamu changamoto  za wizara hii hasa wakati huu ambao mauaji ya binadamu  na ugaidi ni tishio duniani na Afrika Mashariki,” alisema.

Pamoja na kumwapisha Waziri Mwigulu leo, Rais Magufuli pia anatarajiwa kumwapisha Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu ndiye alikuwa Wazira wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Freeman Mbowe na Viongozi Wengine wa Chadema Wakamatwa.....Alipo Zitto Kabwe Bado ni Utata

$
0
0
Wakati Polisi ikimshikilia kwa saa mbili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe mkoani Mwanza, jeshi hilo limefuta kongamano la kujadili Bajeti ya Serikali lililoandaliwa na ACT Wazalendo jijini Dar es Salaam huku kiongozi wake, Zitto Kabwe akisakwa.

Jeshi hilo lilizuia mkutano wa hadhara wa Chadema uliokuwa ufanyike wiki iliyopita mjini Kahama ambako lilitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama na wafuasi wa chama hicho, katika kile kilichoelezwa kulikuwa na dalili za uvunjifu wa amani.

Jeshi hilo pia lilizuia msafara wa viongozi wa chama hicho kuingia katika ofisi zake za Shinyanga walipokuwa wakielekea Mwanza.

Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene ilieleza kuwa mbali na Mbowe, jeshi hilo pia lilikuwa linawashikilia Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi na Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita.

Wengine ni Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka na viongozi wengine na wanachama wa chama hicho waliokuwa wanashikiliwa katika kituo cha Polisi Nyakato, jijini Mwanza.

Makene alisema tangu asubuhi ya jana, Mbowe na viongozi wenzake walikuwa wakizunguka katika maeneo kadhaa ya jijini Mwanza kuwasalimia wananchi katika ‘vijiwe’ mbalimbali kabla hawajakamatwa.

Alisema, “Hadi sasa (saa 11 jioni) hakuna maelezo ya kushikiliwa kwao.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alithibitisha kukamatwa kwa viongozi hao na kubainisha kuwa waliachiwa bila kufunguliwa kesi yoyote.

“Walikutwa Igoma Sokoni wakizungumza na wananchi. Mikutano ya namna hii imezuiwa. Wamefungua kesi mahakamani, hivyo hakuna haja ya kufanya tofauti mpaka itakapohukumiwa,” alisema Msangi.

Alifafanua kuwa jeshi hilo halina uhasama wowote na Chadema au chama kingine chochote na "hatuwezi kukiingilia kinapofanya mikutano yake ya ndani au hotelini. Kilichozuiwa ni mikutano ya hadhara.”

Wakati Msangi akisema hayo, kongamano la ACT Wazalendo ambalo lilitakiwa lifanyike jana kuanzia saa 7:00 mchana kwenye Ukumbi wa Jengo la LAPF; Millennium Towers, Kijitonyama lilizuiwa na polisi.

Tangu mapema asubuhi, askari polisi walitanda katika eneo la ukumbi huo kuzuia kongomano hilo.

Ukumbini hapo, waandaaji walisema hakuna anayeruhusiwa kuingia kwani wamepewa maelezo ya kuufunga baada ya tukio lililoandaliwa kuahirishwa.

Zaidi ya viti 210 vilikuwa vimepangwa kwa ajili ya kongamano hilo na mmoja wa viongozi wa ukumbi huo alionekana akiondoa mabango yaliyokuwa yanautambulisha mkutano huo wa ACT.

Viongozi watatu wa ukumbi huo walikataa kueleza kinagaubaga juu ya sakata hilo, lakini taarifa za jumla zilisema mkutano umezuiwa.

Mmoja wa watumishi wa ukumbi huo, alisema: “Tuliandaa kila kitu, ila shughuli imeahirishwa. Ukumbi unatakiwa kufungwa. Hautatumika kwa leo.”

Ilipofika saa 5:00 asubuhi, Msemaji wa ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis alisema chama kinafanya mkutano wa dharura kwenye ofisi zake za makao makuu na baadaye kingezungumza na waandishi wa habari.

Saa 8:00 mchana, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Anna Mghwira akiwa na viongozi wenzake, isipokuwa Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe alikuwa mbele ya kamera za wanahabari akifafanua kilichotokea kwa wanachama, wafuasi wa chama hicho na Watanzania kwa ujumla.

Alisema ilipotimu saa 4:00 asubuhi walipewa taarifa na mwenye ukumbi kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni limemjulisha kuwa chama hicho hakina kibali cha kuendesha kongamano hilo na kwamba kisiruhusiwe kufanya hivyo.

“Huku ni kufifisha demokrasia. Wapigania haki za kiraia wasimame imara na vyama vya upinzani katika kuilinda,” alisema Mghwira.

Wakati kongamano hilo likizuiwa, kuna taarifa za kukanganya juu ya alipo Zitto baada ya kudaiwa alikuwa anasakwa na polisi tangu juzi.

Taarifa hizo zinakuja siku chache baada ya kiongozi huyo kuitwa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam na kuhojiwa juu ya kauli alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara zinazokosoa utendaji wa Serikali na kupinga matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar.

Baadaye jioni, Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Msafiri Mtemelwa alitoa taarifa kuwa Zitto ametoweka na hajulikani alipo. Hiyo ilikuwa ni baada ya askari kanzu kumtafuta kwa muda kwa saa kadhaa.

“Zitto amekuwa akitafutwa kwa muda mrefu. Askari wanalinda nyumbani kwake tangu jana (juzi) usiku. Hivi sasa ametoweka, hatujui alipo. Lolote litakalompata, Jeshi la Polisi litajibu,” alisema Mtemelwa.

Awali, Mghwira alipoulizwa imekuwaje kuhusu Zitto alijibu kuwa mkutano ulikuwa wa dharura ndiyo maana viongozi wote hawakuwapo.

Audio: Gwajima afyatuka tena, amshauri Magufuli aihame CCM....Adai amenasa njama Mbaya

$
0
0

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye anafahamika kwa kutoa kauli ‘tata’, amefyatuka tena akimshauri Rais John Magufuli kuihama CCM endapo kile alichokiita ‘njama alizozibaini’ ndani ya chama hicho zitaletwa mezani.

Gwajima ambaye amekiri kuwa katika kampeni alikuwa hamkubali Dk. Magufuli kutokana na kutokuwa na imani na CCM, amesema amemkubali  sana baada ya kuanza kazi ya urais kutokana na hatua ambazo amekuwa akizichukua ndani ya muda mfupi.

Akizungumza katika ibada ya Jumapili kanisani kwake, Gwajima ameeleza kuwa amebaini njama za baadhi ya wanachama wa CCM ambao ‘dili’ zao mbalimbali ikiwa ni pamoja na ‘flow meter’ ya mafuta yaingiayo nchini na makontena yaliyokamatwa yalikuwa yanawahusu, wameanza kampeni ya chinichini nchi nzima kutaka Rais Magufuli asipewe uenyekiti wa chama hicho.

Amesema kuwa watu hao wanazunguka nchi nzima kuwashawishi wanachama wa CCM kuridhia hoja ya kutenga uenyekiti wa chama na urais, ili kumnyima nafasi hiyo Rais Magufuli ambaye utendaji wake umewabana bila kujali ni wa chama chake.

Hivyo, amemshauri Rais Magufuli kuwa endapo itatokea hilo, akihame chama hicho na kuendelea na kazi yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mengine, msikilize mwenyewe hapo chini:

Zitto Kabwe Aibuka Baada ya Kupotea kwa Siku Mbili.....Kasemaje??? BOFYA Hapa

$
0
0
Baada ya taarifa za kutoweka, Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka leo na kusema yuko salama wa afya huku akilaani mbinu za Jeshi la Polisi kutaka kumkamata kwa siri bila kufuata utaratibu unaotakiwa.

Tangu Jumamosi usiku, vyombo mbalimbali vya habari viliripoti Zitto kutofahamika alikokuwa baada ya simu zake zote kutopatikana huku viongozi wa chama hicho wakihofia kukamatwa na polisi baada ya kubaini njia za uviziaji wa kumkamata nyumbani
kwake.

"Ilikuwa Jumamosi , walikuja nyumbani kwangu wakiwa na magari matatu ila hawakufanikiwa, siwezi kukamatwa kwa `terms' zao ila nitakuwa tayari kukamatwa kwa `terms' zetu na wala siyo kuviziana, kama nina makosa kwa nini wanivizie,"amesema Zitto Kabwe na kuongeza;

''Watu wetu wa Usalama wa Chama walihakikisha kwamba sitakamatwa ili niweze leo kupata fursa kuzungumza na watanzania kupitia nyie wana habari
 

''Hatufahamu Watawala wanaogopa nini mpaka kuzuia mikutano ya wanasiasa
 

''Nasikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Mbowe wa Chadema Huko Mwanza kisa eti kawasalimia wananchi, huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa kidemokrasia
 

''Tunalaani tabia za Kidikteta za Rais Magufuli .Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonyesha Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari, Tumkatalie
 

''Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza alifanya Rwanda, tumegundua kuwa alikwenda kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na Kuongoza Kidikteta
 

''Hauwezi kupambana na Ufisadi kama haumpi nguvu ya Kiutendaji wa CAG. Kwa hali Hii anayokwenda Magufuliajiandae kuwa rais wa term moja kwa sababu watanzania hawataweza kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa .
 

''CCM wamdhibiti Magufuli, na wasipomdhibiti sisi na Watanzania Tutamdhibiti
 

''Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga, akimfunga Zitto watazaliwa wakina Zitto wengine, na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama kidete mpaka nchi irudi kwenye misingi''
 

''IGP ameagizwa na Magufuli anikamate, lakini hawezi kunikamata bila kufuata utaratibu, hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi hatukamatwi kwa kuviziwa viziwa, tumewaonyesha kwamba Polisi wanaweza kutukamata kwa kufuata terms zetu na sio zao
 

''Karibuni kesho saa tisa kwenye Kongamano letu, Hatuwezi kuacha kufanya siasa, lazima tuendelee kufanya siasa, mmehudhuria mikutano yetu hamjaona hata sisimizi amekanyagwa
 

''Wanasema Bajeti imeongezeka kwa 32% ukweli ni kwamba Bajeti imeshuka kwa maana Dola imeporomoka''

Mwigulu Nchemba Aapishwa Rasmi Kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.......Atoa ONYO Kali kwa Wauza Dawa za Kulevya

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo badala yake watafute shughuli halali za kujiingizia kipato.

Waziri Nchemba ametoa agizo hilo mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyemteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mh.Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Aidha Waziri Nchemba alisema kuwa atahakikisha anasimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kwa kuziba mianya inayohatarisha amani na utulivu katika nchi.

Naye Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa atahakikisha anashirikiana na wataalum wa sekta tatu zilizo katika Wizara yake ili kufanya mapinduzi katika maeneo hayo yaliyoajiri zaidi ya asiimia 80 ya Watanzania.

Pia Waziri Dkt. Tizeba alisema kuwa Wizara itahakikisha inashugahulikia changamoto zinazozokabili vyama vya ushirika ambavyo vimekuwa havifanyi vizuri katika miaka ya hivi karibuni.

Mawaziri walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi anayejaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya Rais kutengua uteuzi wa Mh. Charles Kitwanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba wakipongezana mara baada ya kuapishwa Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba (kulia) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kuwaapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mwigulu Nchemba Apokelewa Makao Makuu Ya Wizara Ya Mambo Ya Ndani.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, muda mfupi baada ya Rais Dkt. John Magufuli kumwapisha Waziri Mwigulu Nchemba kuongoza wizara hiyo leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba(Kushoto), akikaribishwa Makao Makao ya Wizara hiyo na Katibu Mkuu Meja Jenerali Projest Rwegasira.Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamad Masauni na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Yahya Simba.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Mawasiliano, Jane Massawe, mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiweka saini mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi baada ya kuapishwa kwake. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Yahya Simba.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Makamu wa Rais akagua mradi wa mabasi ya mwendo kasi na kugawa futari kwa wenye mahitaji maalum

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es salaam ambayo kwa kiasi kikubwa yamerahisisha usafiri na kutaka wananchi kuyatunza mabasi hayo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteremka kwenye basi la mwendo kasi baada ya kupanda na kujionea ubora na uzuri wa mabasi hayo ambayo yamerahisisha usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.( Picna na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalumu wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiongoza dua hiyo Mussa Salum .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Futari Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Baraza la Waislam mkoa wa Dar es Salaam Bibi Pili Abdala Mwale wakati wa shughuli hiyo maalum ya kukabidhi furati na chakula kwa watu wenye mahitaji maalum, Jangwani jijini Dar es salaam.( Picna na OMR)
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images