Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu: Sukari Haitakuwa Tatizo Ramadhani

$
0
0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema sukari haitakuwa tatizo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na wakuu wa mikoa wamepewa maelekezo kilo moja isizidi Sh 2,300. 

Alisema hayo jana wakati wa mahojiano na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano uliofanyika Chuo cha Mipango mjini hapa.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema hadi Mei 13, mwaka huu walikuwa wamepokea tani nyingine 35,000 za sukari na haitakuwa tatizo kwa kuwa tayari jitihada kuwa serikali imefanya katika kushughulikia suala hilo.

Pia alisema sukari nyingine tani 11,000 imeshatoka na inasambazwa na nyingine tani 20,000 iko tayari Tanzania na tani nyingine 35,000 zinakuja kabla ya Juni 30, mwaka huu.

Alisema sukari wameigawa kwa kanda kutokana na kanda kutofautiana kulingana na wingi wa watu kwa mujibu wa mgawo wa Bodi ya Sukari Tanzania wamepeleka maeneo yote.

“Niwasihi Waislamu wenzangu ambao wamefunga Ramadhani kwamba suala la sukari halitakuwa tatizo,” alisema. 

“Mwito wangu kwa wafanyabiashara kuwa waaminifu na kutambua sukari ni mahitaji ya Watanzania wote.”

Alisema suala la bei wameangalia kule juu wanaponunua Brazil, Uarabuni na Malawi wameshaweka viwango vya bei ambavyo wakuu wa mikoa wataangalia sukari haitazidi Sh 2,300 kwa kilo ili Watanzania wote wamudu kununua.

Alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuacha kuficha sukari kwani hayo ni mahitaji ya wananchi wote na hawana sababu ya kufanya hivyo. 

Katika miezi ya karibuni, sukari ambayo ni moja ya bidhaa muhimu nchini, imepanda bei hadi kuuzwa kati ya Sh 2,500 hadi 3,000 kwa kilo kutoka Sh takriban 1,800, hali iliyosababisha serikali kuingilia kati kuwataka wafanyabiashara kuuza kilo moja kwa Sh 1,800 na kuagiza sukari kutoka nje ili kukabili upungufu uliopo.

Bajeti ya Magufuli 2016/17 Hadharani Leo....Macho na Masikio Yote Yaelekezwa Dodoma

$
0
0


TANZANIA kama zilivyo nchi nyingine za Afrika Mashariki, leo inawasilisha bungeni mjini Dodoma Bajeti ya Serikali ili Bunge liijadili na kuipitisha, ianze kutekelezwa katika mwaka mpya wa fedha 2016/17 unaoanza Julai mosi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango anatarajiwa kuiwasilisha bajeti hiyo inayoelezwa kuwa na Sh trilioni saba zaidi ya ile iliyopitishwa na Bunge hilo mwaka jana, ambayo utekelezaji wake unaishia Juni 30, 2016.

Hii ni bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, ambaye ameeleza kuwa anataka kujenga Tanzania ya viwanda, ambayo nia ni kuifanya iwe na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Tofauti na bajeti ya mwaka jana ya jumla ya Sh trilioni 22.495 zilizotengwa kutoka katika vyanzo vya ndani na nje, bajeti nzima ya mwaka huu kwa mujibu wa mapendekezo ya ukomo wa bajeti hiyo yaliyowasilishwa kwenye mkutano wa wabunge wote Dar es Salaam, Aprili 6, mwaka huu ni Sh trilioni 29.539.

Bajeti hiyo inayosubiriwa kwa hamu na Watanzania, inatajwa kutokana na vyanzo mbalimbali vya ndani na nje ambavyo kutokana na mapendekezo hayo ya awali, serikali imepanga kutumia Sh trilioni 17.719 kwa matumizi ya kawaida na Sh trilioni 11.82 kwa matumizi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 40 ya mapato ya ndani.

Mapato ya kodi na yasiyo ya kodi yaliainishwa katika mapendekezo hayo ya bajeti kuwa ni Sh trilioni 2.693 wakati mapato kutoka Halmashauri yakiwa ni Sh bilioni 665.4. 

Bajeti hiyo ya mwaka mpya wa fedha inategemewa kujumuisha fungu kutoka kwa washirika wa maendeleo ambalo ni asilimia 12 tu ya bajeti yote sawa na Sh trilioni 3.600.

Miongoni mwa vipaumbele vinavyotajwa kuzingatiwa katika bajeti hiyo ambavyo Dk Mipango aliwahi kuviainisha ni pamoja na utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka huo mpya wa fedha kwa kipindi cha miaka mitano.

Vipaumbele vingine ni viwanda vya kukuza uchumi pamoja na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda, kufungamanisha maendeleo ya uchumi na rasilimali watu na kuweka mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara. Lengo la serikali ni kuhakikisha uchumi unakua kwa asilimia mbili zaidi kufikia asilimia 7.2 badala ya asilimia saba iliyopo.

Inategemewa pia kuwa mkazo zaidi kwenye bajeti hiyo utawekwa katika kukamilisha miradi ya maendeleo inayoendelea, miradi mipya, kulipa madeni yaliyohakikiwa na utekelezaji wa maeneo yote ya vipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa mwaka wa fedha unaoisha.

Mchango wa washirika wa maendeleo katika bajeti hiyo unahusisha misaada na mikopo, inayojumuisha maendeleo, mifuko ya pamoja ya kisekta na kibajeti. 

Katika bajeti inayosomwa leo, serikali imependekeza mikopo ya Sh trilioni 5.374 kutoka katika soko la ndani kwa ajili ya kulipia hatifungani zilizoiva pamoja na mipya kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ya pamoja na kulipa malimbikizo ya madai yaliyohakikiwa.

Aidha, katika mapendekezo yake ya ukomo wa bajeti hiyo, Dk Mpango alisema serikali inatarajia kukopa Sh trilioni 2.11 kutoka kwenye soko la nje kwa masharti ya kibiashara.

Matarajio ya ongezeko la makusanyo ya kodi ni kufikia asilimia 12.6 huku makusanyo ya ndani na Halmashauri yakitegemewa kufikia asilimia 14.8. 

Tangu Aprili 22, mwaka huu, wizara mbalimbali ziliwasilisha makadirio ya mapato na matumizi yake kwa mwaka wa fedha 2016/17 zikianzia na Ofisi ya Waziri Mkuu na kumaliziwa na Wizara ya Fedha na Mipango iliyowasilisha makadirio yake Juni mosi, mwaka huu.

Kwa siku sita kuanzia Juni 2, mwaka huu, serikali kwa kushirikiana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ilikuwa inafanya majumuisho kwa kuzingatia hoja zenye maslahi kwa Taifa zilizojitokeza wakati wa kujadili Bajeti za Wizara.

Zipo changamoto mbalimbali zilizoelezwa na wabunge katika mijadala hiyo ya Bajeti za Wizara ambazo inatarajiwa kuwa serikali itakuwa imezichukua na inaweza kuzifanyia marekebisho kupitia Bajeti Kuu leo.

Bajeti ya leo ambayo itasomwa saa 10 kamili jioni na kuoneshwa moja kwa moja katika televisheni nchini, itatanguliwa na Taarifa ya Hali ya Uchumi itakayosomwa na Dk Mpango leo asubuhi.

Kesho wabunge watapata fursa ya kusoma na kutafakari hotuba hizo mbili kabla ya Ijumaa kuanza mjadala wake ambao utadumu kwa siku saba hadi Juni 20, mwaka huu ambayo utahitimishwa kwa uamuzi wa kura.

Wapinzani Walegeza......Waahidi Kuwasilisha Vipande Muhimu vya Hotuba Kivuli ya Bajeti

$
0
0

Wakati hatua ya upinzani kumsusia Naibu Spika, Dk Tulia Ackson ikiingia siku ya nane, Kambi ya upinzani imesema leo itawasilisha vipande muhimu vya hotuba kivuli ya bajeti ambavyo ni vya msingi.

Naibu msemaji wa kambi hiyo kwa Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde alisema kutokana na umuhimu wa vipande hivyo ambavyo hakuvitaja, atavisoma kwa ufupi na kuviwasilisha, kisha kuondoka.

Wabunge wa upinzani walianza kususia vikao anavyoongoza Dk Tulia Jumanne ya wiki iliyopita, kufuatia kitendo cha kiongozi huyo kuzuia hoja ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kuhusu kutimuliwa kwa wanafunzi 7,802 wa chuo kikuu cha Dodoma (Udom).

Jumatatu ya wiki iliyopita Dk Tulia alizuia hoja ya Nassari akieleza kuwa kutokana na anavyoona sakata hilo la wanafunzi wa Udom halikuwa la muhimu kusimamisha shughuli za Bunge kwa wakati huo kwa kuwa Serikali tayari ilishatoa majibu.

Kitendo hicho kilisababisha wabunge wa upinzani kupinga uamuzi huo jambo lililosababisha Dk Tulia kuahirisha shughuli za Bunge kabla ya muda huku Nassari akitolewa bungeni na askari wa Bunge.

Baada ya hatua hiyo, wabunge wa upinzani walitoka bungeni na kukutana katika ukumbi wa Msekwa na baadaye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema wameazimia kususia vikao vyote vitakavyoongozwa na Dk Tulia, kwa kuwa hawako tayari kuona demokrasia inaminywa.

Kutokana na hali hiyo Jumanne ya wiki iliyopita wabunge hao waliingia bungeni kama kawaida na Dk Tulia alipomaliza tu kusoma dua ya kuliombea Bunge, walitoka nje hadi kipindi hicho kilipomalizika na Dk Tulia kumwachia mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kuongoza ndipo wote waliporudi.

Mbali na hatua hiyo, Mbunge wa Simanjiro, James Millya kwa niaba ya wabunge wenzake aliwasilisha hoja kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, akieleza nia ya kumng’oa Naibu Spika madarakani.

Hoja hiyo imekubaliwa na Spika Ndugai ambaye juzi katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi ya Bunge ilieleza kuwa anakusudia kuiwasilisha kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iweze kufanyiwa kazi.

Hata hivyo, wabunge wa CCM juzi walikutana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kukubaliana kuwapuuza wapinzani, wakisema Naibu Spika aendelee kuongoza Bunge kwa kuwa hajavunja kanuni yoyote.

Katibu wa wabunge wa CCM, Jason Rweikiza, alisema, “Kinachofanywa na wabunge wa upinzani kutoka nje ni uhuni na wananchi waliowachagua wajue wabunge wao ni wahuni.”

Alisema mbuge mwenye malalamiko dhidi ya mbunge mwenzie au Spika au naibu anajua cha kufanya.

Aliyemtukana Rais Magufuli , Isaac Emily Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 3 Jela au Kulipa Faini Ya Sh. Milioni 7

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Wa Arusha,imemhukumu  Isack Habakuki(40) mkazi Wa Olasiti, kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya shilingi milioni 7 kwa kosa la kumtukana Rais Magufuli kupitia mtandao wa facebook.

Mshtakiwa amekiri kutenda kosa hilo na amekubali kulipa faini ambapo mahakama imeamuru alipe fedha hizo kwa awamu mbili.Katika awamu ya kwanza atalipa July 8 2016 sh mil 3.5 na August 8 2016 atalipa kiasi kilichobaki cha sh mil 3.5.

Isack anayeishi Kata ya Olasite, anadaiwa kutoa lugha ya matusi na dhihaka kwa Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na alikamatwa Machi 23, mwaka huu mjini Arusha na kupelekwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kisha alirejeshwa tena Arusha Aprili 14, mwaka huu kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile,  Wakili wa Serikali, Gaudensia Massanja, alidai kuwa Isack alikuwa akikabiliwa na kosa moja ambapo kwa kufahamu na kwa makusudi mtuhumiwa huyo alitumia mtandao wa Facebook kwa nia ya kumtukana Magufuli.

Alidai kwamba mtuhumiwa katika ukurasa wake wa Facebook alichangia maneno yanayosema: “Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi buana.”

Wanahisa Wa Nmb Wapitisha Gawio La Shilingi Bilioni 52

$
0
0

BENKI ya NMB kwa mwaka jana imepata faida ya Sh. Bil. 150.2 kiwango ambacho ni kikubwa kuliko benki yoyote hapa nchini, faida hiyo ni zaidi ya asilimia 33 ya faida yam waka 2015 kwa benki zote.

Hayo yameelewa na Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker katika Mkutano Mkuu wa 16 wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika jumamosi jijini Dar es Salaam, huku benki hiyo ikiainisha mafanikio makubwa kwa mwaka 2015 na maono ya mafanikio zaidi kwa mwaka 2016 matumaini ambayo wanahisa waliyapokea kwa mikono miwili.

Katika mkutano huo, wanahisa walipitisha gawio la shilingi Bilioni 52 ambapo kila hisa itapata gawio la shilingi 104. Kwa maana hiyo, serikali itapata gawio la shilingi Bilioni 16.5 kama gawio la hisa zake 31.8 wanazomiliki kwenye benki ya NMB.

 Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas alisema "Tuna furaha kwamba benki imeendelea kuimarika kifedha katika kasi ile ile iliyopita, na nguvu ya ukuaji imezidi kuwa juu na kuongezeka kwa asilimia 18, hivyo kutanua thamani ya jumla ya taasisi hii, ikiwa ni pamoja na tahamni ya hisa zenu,"

 Alifafanua ya kwamba, NMB imeendelea pia kutanua soko na pato katika mikopo na amana, na kwamba pato litokanalo na riba lilikua kwa asilimia 5 kutoka Sh. Bil. 417 mwaka 2014, hadi kufikia Sh. Bil. 438 kwa mwaka uliopita wa 2015.

"Licha ya faida ya jumla kuu kushuka kulinganisha na mwaka jana, lakini gawio la Wanahisa litabaki kama lilivyokuwa, ambako kila hisa moja itakuwa na thamani ya shilingi 104, uamuzi ambao ulifurahiwa na kupongezwa na wanahisa walioshiriki mkutano huo," alisema.

Alivitaja baadhi ya vikwazo vya maendeleo ya benki hiyo mwaka jana kuwa ni pamoja na mzunguko finyu wa pesa kutokana na harakati za Uchaguzi Mkuu, kushuka mara kwa mara kwa thamani ya shilingi katika soko la kubadilishia fedha.

Barnabas aliongeza kuwa, moja ya masuala muhimu ambayo NMB ilijikita kuyafanyia kazi mwaka jana ni pamoja na kumalizia uboreshaji matawi 98 waliyoachiwa na NBC ambayo yalikuwa katika hali mbaya na kuhamisha Makao Makuu ya Benki hiyo.

Aliongeza kuwa, katika kipindi cha miaka 10 sasa, NMB imejipambanua kama kinara miongoni mwa taasisi za kifedha, na kwamba moja ya ubinafsishaji ulioipa Serikali faida ni pamoja na wa benki hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ineke Bussemaker akizungumza na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa 16 wa mwaka wa benki hiyo uliofanyika, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika mkutano huo, wanahisa walibariki gawio la shilingi bilioni 52 lililotokana na faida ya shilingi Bilioni 150.2 ya faida baada ya kodi iliyoipata benki ya NMB ambapo Kila hisa itapata gawio la shilingi 104 kiwango ambacho ni cha juu kuliko benki yoyote nchini.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB Ineke Bussemaker,azkingumza na Mwenyekiti wa Bodi, Profesa Joseph Semboja wakati wa Mkutano wa 16 wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni kwa wiki.Katika mkutano huo, wanahisa walipitisha gawio la shilingi Bilioni 52 baada ya kupata faida baada ya kodi ya shilingi Bilioni 150.2 kwa mwaka 2015. Kwa gawio Hilo, Kila hisa itapata gawio la shilingi 104 kiwango ambacho ni cha huu kuliko benki yoyote nchini
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ineke Bussemarker kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa 16 wa benki hiyo. kushoto ni Ofisa Mkuu wa Fedha wa NMB(chief finance officer), Waziri Barnabas. Mkurugenzi wa NMB alikuwa akitangaza maazimio ya wanahisa ambao walipitisha gawio la jumla la shilingi Bilioni 52 lililotokana na faida ya shilingi Bilioni 150.2 na hivyo Kila hisa ikipata gawio la shilingi 104 kiwango ambacho ni cha juu kabisa kuliko benki nyingine yoyote.

Mwisho

Leo ndio siku ya mwisho ya kununua Hati Fungani ya NMB. Tembelea tawi lolote la NMB au piga simu 0800 11 22 33


Hotuba Ya Waziri Wa Fedha Na Mipango, Mheshimiwa Dkt. Philip I. Mpango (Mb), Akiwasilisha Bungeni Mapendekezo Ya Serikali Kuhusu Makadirio Ya Mapato Na Matumizi Ya Fedha Kwa Mwaka 2016/2017

$
0
0

 UTANGULIZI
1.      Mheshpika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17. 

Pamoja na hotuba hii, ninawasilisha vitabu vinne vinavyoelezekina makadirio ya Bajeti. Kitabu cha Kwanza ni Makadirio ya Mapato; Kitabu cha Pili ni Makadirio ya Matumizi ya Kawaida kwa Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za Serikali; Kitabu cha Tatu ni Makadirio ya Matumizi ya Kawaida kwa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na Kitabu cha Nne ni Makadirio ya Matumizi ya Maendeleo kwa Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Taasisi na Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2016 pamoja na Muswada wa Sheria ya kuidhinisha matumizi ya Serikali wa mwaka 2016 ambayo ni sehemu ya Bajeti hii.

2.Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu kwa baraka na amani anayoendelea kuijalia nchi yetu na pia kwa kuniruhusu kusimama hapa mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/17. Aidha, kwa namna ya pekee nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais na mwanamama wa kwanza kushika nafasi hiyo katika historia ya nchi yetu. 
 Nampongeza pia Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Vilevile, nampongeza Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa kwa kuchaguliwa na wananchi wa jimbo la Ruangwa kuwa Mbunge wao na kuteuliwa na Mhe. Rais na kuthibitishwa na Bunge kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Napenda pia kukupongeza wewe Mheshimiwa Spika pamoja na Naibu Spika kwa kuchaguliwa kuongoza Bunge letu Tukufu.  Kadhalika, natumia fursa hii kumpongeza Mhe. Mohamed Othman Chande, Jaji Mkuu wa Tanzania, kwa kuongoza mhimili wa Mahakama kwa weledi mkubwa.

3.Mheshimiwa Spika, niruhusu pia niwashukuru sana waheshimiwa wenza wa viongozi wetu wa kitaifa: Mama Janet Magufuli, Bwana Ameir Hafidh Ameir (mume wa Mhe. Makamu wa Rais), Mama Mwanamwema Shein, Mama Mary Majaliwa, Mama Fatuma Ramadhani Mganga (mke wa Mhe. Spika), Bwana James Andilile (mume wa Mhe. Naibu Spika) na Mama Saada El-Maamry Othman (mke wa Mhe. Jaji Mkuu) kwa kuwasaidia na kuwatunza viongozi wetu vizuri.  Asante kwenu wote na Mungu awabariki.

4.Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine natoa shukrani za pekee kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniteua kuwa Mbunge na Waziri wa Fedha na Mipango. Ninatambua kwamba wananchi wa Tanzania wananidai! Tarehe 29 Februari, 1968 Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwasilisha hati ya madai kama ifuatavyo, nanukuu: “Tunadai nini basi kwa wale wenzetu waliojaliwa kupata elimu? Tunadai huduma kwa wananchi na huduma ambayo ukubwa wake utalingana na kiasi cha elimu waliyoipata” mwisho wa kunukuu. 

Hivyo, napenda kumuahidi tena Mhe. Rais na Watanzania kwamba nitaibeba dhamana hii kwa bidii na uadilifu ili kulipa deni langu kwa nchi yangu. Vilevile, nawapongeza waheshimiwa Wabunge wote kwa kuchaguliwa kwenu na kuwa sehemu ya Bunge hili.  Napenda pia kuwapongeza Waheshimiwa Mawaziri wenzangu na Naibu Mawaziri kwa dhamana kubwa tuliyopewa na Mheshimiwa Rais kuwatumikia Watanzania. 
 
Nampongeza pia Dkt. Thomas Kashililah, Katibu wa Bunge na Bw. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa Mahakama kwa kuratibu vyema shughuli za Bunge na Mahakama kwa mtiririko huo. Napenda pia kumpongeza Prof. Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa kazi nzuri anayoifanya ya kukagua na kutoa taarifa za matumizi ya fedha za umma kwa wakati.

5.Mheshimiwa Spika, ninaishukuru sana Kamati ya Bunge ya Bajeti chini ya uenyekiti wake Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara vijijini na Makamu Mwenyekiti Mhe. Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo, kwa kuchambua kwa kina bajeti za Mafungu yote na kutoa mapendekezo na ushauri. 
 Aidha, napenda kuwashukuru wenyeviti wa kamati za kisekta kwa ushauri na mapendekezo waliyotoa wakati wakichambua rasimu ya Bajeti hii. Ninamshukuru pia Mhe. George Mcheche Masaju (Mb), Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kutayarisha kwa wakati Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Matumizi wa mwaka 2016 ambayo ni sehemu ya Bajeti hii.

6.Mheshimiwa Spika,napenda kumpongezaMhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji, Mbunge wa Jimbo la Kondoa kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na pia ninamshukuru kwa ushirikiano anaonipatia katika utekelezaji wa majukumu yangu. 
Aidha, napenda kumshukuru Dkt. Servacius B. Likwelile, Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango kwa uratibu na usimamizi mzuri wa maandalizi ya Bajeti hii. Kadhalika, nawashukuru Naibu Makatibu Wakuu; Gavana wa Benki Kuu; Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania; Msajili wa Hazina; Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu; Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara; Wakuu wa idara, vitengo na Watumishi wote wa Wizara na taasisi zake kwa kazi kubwa waliyoifanya kukamilisha Bajeti hii.

7.Mheshimiwa Spika,Bajeti hii imezingatia mawazo na mapendekezo ya wadau mbali mbali wakiwemo wenye viwanda, wafanyabiashara na wengine wengi. Nawashukuru wote kwa mawazo na ushauri wao. Kipekee niwashukuru wajumbe wa kamati ya wataalamu na ushauri wa masuala ya kodi (Task Force) na kamati ya kitaifa ya ushauri wa kodi (Think Tank) kwa ushauri wao mzuri walionipa.
 

Aliyoyazungumza Zitto Kabwe baada ya kuhojiwa na polisi Kwa Masaa Matatu Leo

$
0
0


ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo ameonya utawala wa Rais John Magufuli kuacha tabia ya kutaka kuziba midomo wapinzani.

Amesema, Serikali ya Rais Magufuli haipo tayari kukosolewa na wapinzani na kwamba, inatengeneza mazingira ya kuwanyamazisha sambamba na kuminya demokrasia.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema hayo leo baada ya kutoka kuhojiwa na Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke na Naibu Kamanda wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa saa tatu.

“Mambo kama haya yalikuwa yanaanza kusahaulika katika mfumo wetu wa kisiasa nchi, lakini nyie ni mashahidi mnaona jinsi demokrasia inavyominywa na kuingia kwenye mashaka makubwa. Ni muhimu wananchi wakasimama kidete ili kuitetea demokrasia,” amesema Zitto na kuongeza;

“Wanatia woga wa watu kuzungumza mawazo yao ya kisiasa jambo ambalo si haki kwa kuwa ni sehemu ya wajibu wetu wa kisiasa. Hofu inayojengwa na serikali juu ya wanasiasa wa vyama vya upinzani haina maana.

“Kama leo polisi wametumia zaidi ya masaa matatu, hayo masaa waliyoyapoteza wangefanya kazi ya kupambana na majambazi, wahalifu na madawa ya kulevya badala ya kupoteza nusu siku kwa kutuhoji maswali,” amesema Zitto.

Anasema kuwa, ratiba ya kuzunguka mikoani itasitishwa kutokana na tamko lililotolewa jana na jeshi hilo.

Jeshi hilo limelizuia mikutano ya kisiasa hadi litakapotoa taarifa na kwamba, wanasheria wa ACT-Wazalendo  wataenda mahakamani ili kupata tafsiri sahihi.

“Lakini kama mnavyofahamu, jana limetolewa tamko la kuzuia mikutano yote hadi tamko lingine litakapotoka, hivyo basi tulikuwa tunashauriana na wanasheria ili wapate tafsiri ya kisheria kutoka mahakama kutokana na kwamba siyo sahihi polisi kuzuia mikutano.

“Lazima tuende mahakamani sababu bila ya kupata tafsiri ya mahakama, hatuwezi kufanya mikutano na hatutaki nchi iingie kwenye fujo,” amesema.

Steven Mwakibolwa, Mwanasheria wa ACT amesema kuwa, Zitto alihojiwa juu ya hotuba aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jumapili wiki iliyopita na kwamba, yuko nje kwa dhamana isiyo na malipo.

“Tusubiri Jumatano wiki ijayo ili tujue kama atapelekwa mahakamani au upelelezi utajiridhisha kuwa hana makosa.

“Aliulizwa maswali mengi ambayo yalihusiana na hotu yake aliyotoa, amelezea kwa kina alichokisema maswali yote alijibu.”

Mwakibolwa amesema kuwa, kwa sasa si vema kueleza maswali aliyoulizwa kwa kuwa si muda na wakati sahihi wa kuliongelea suala hilo sababu liko chini ya upelelezi.

 ==> Msikilize hapo chini akiongea

Serikali kununua ndege tatu na meli moja kuboresha usafiri.

$
0
0

Serikali imejipanga kununua ndege tatu na meli moja kwa ajili ya kuboresha usafiri wa anga na majini katika maziwa makuu kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.

 Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Philip Mpango wakati akiwasilisha taarifa ya Hali ya Uchumi 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/17.

 “Serikali itanunua meli moja mpya ya usafirishaji wa abiria na mizigo katika Ziwa Victoria na ukarabati wa meli za MV Victoria, MV Butiama na MV Liemba na kuimarisha Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikijumuisha ununuzi wa ndege 3 mpya” alisema Waziri Mpango.

 Alisema miongoni mwa ndege hizo kuwa ni Bombardier CS300 yenye uwezo wa kubeba abiria 100 – 150 na ndege mbili Bombardier Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 67- 88 kila moja.

 Aidha, Waziri Mpango alisema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kujenga na kuboresha miundombinu wezeshi, kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara, kuhamasisha ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma.
 
Kwa mujibu wa Mpangpo Ili kuhakikisha utekelezaji huo unafanikiwa Serikali imeweka jitihada mahususi za kuongeza kasi ya kulipa fidia katika Maeneo Maalum ya Uwekezaji (EPZs na SEZs); Benki ya Rasilimali kuongeza utoaji wa mikopo katika sekta mbali mbali kutoka shilingi  bilioni 538.7 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 726.9 kwa mwaka 2016.

Aliongeza kuwa jitihada nyingine ni pamoja na kuitangaza Benki ya Maendeleo ya Kilimo na huduma zake ili wananchi waweze kutumia fursa za mikopo zinazopatikana katika benki hiyo na kuwezesha Kituo cha Uwekezaji Tanzania kuwa na ardhi yenye hatimiliki kwa ajili ya kuikodisha kwa wawekezaji wa nje.

Kwa mujibu wa Waziri Mpango miradi mingi mikubwa itatekelezwa kwa ubia. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Biashara na Huduma Kurasini, miradi ya Chuma-Liganga na makaa ya mawe – Mchuchuma na Mradi wa barabara wa Dar es Salaam – Chalinze- Morogoro Express Way.

 Waziri Mpango alisema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi ambayo ilishaanzishwa ikiwa ni pamoja na nishati ukiwemo mradi wa Liquified Natural Gas, kilimo cha mazao, mifugo, uvuvi, misitu, maji na miundombinu ya reli na barabara.

Naibu Spika awavuruga wabunge wa Ukawa, Aagiza wasilipwe Posho wakisusa

$
0
0

Hatimaye Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson ametoa maamuzi kuhusu hoja ya wabunge kulipwa posho au kutolipwa wanapoingia Bungeni na baadae kutoka nje kwa shughuli zisizo za Kibunge.

Akisoma muongozo wake muda mfupi kabla ya kuahirisha kikao cha Bunge jioni hii baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango kusoma Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17, Dk. Tulia alisema kuwa wabunge wanaofanya vitendo hivyo hawatalipwa posho.

Alitoa uamuzi huo baada ya kurejea kanuni za Bunge akitumia kanuni ya tano fasili ya kwanza ya toleo la mwaka 2006 na maamuzi yaliyowahi kufanywa na Spika waliotangulia katika hali kama hiyo.

“Hivyo basi, kwakuwa jambo hili halikubaliki, na kwakuwa miongozo kadhaa imeshatolewa kuwasihi waheshimiwa Wabunge wasitoke nje ya ukumbi wa Bunge kwa shughuli zisizo rasmi. 

"Naagiza kwamba wabunge wote wanaojisajili kisha kutoka ukumbini kwa kususia vikao vya Bunge, hawatastahili kulipwa Posho kwa siku zote ambao wamekuwa wakijisajili kuingia ukumbini na kisha kutoka ukumbini,” alisema Naibu Spika.

Wabunge wa Upinzani wamekuwa wakitoka nje ya Bunge muda mfupi baada ya kuingia Bungeni katika vikao vyote vinavyoongozwa na Naibu Spika kwa madai kuwa hawana imani naye kwakuwa amekuwa akiongoza Bunge kwa ubabe na kuwapendelea wabunge wa CCM.

Watumishi NIDA Kuanza Kulipwa

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 9

Viongozi CHADEMA Akiwemo Freeman Mbowe wazuiwa kuingia ofisini Shinyanga

$
0
0
Viongozi na makada wa Chadema waliokuwa wakisafiri kutoka Kahama kuelekea jijini Mwanza jana wamejikuta wakishindwa kuingia kwenye ofisi za chama hicho mjini Shinyanga kutia saini kitabu cha wageni baada ya Jeshi la Polisi kuzuia shughuli yoyote ya chama hicho mjini humo.

Waliokumbwa na adha hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Vicent Mashinji na wabunge Godbless Lema, Ester Bulaya, John Heche, Halima Mdee na viongozi kadhaa wa kitaifa wa Chadema.

Magari manne ya polisi yaliyosheheni askari waliobeba silaha na mabomu ya kutoa machozi yaliupokea msafara wa Chadema uliokuwa ukielekea Mwanza, mara tu ulipoingia mjini Shinyanga na kuusindikiza hadi nje ya mji kuhakikisha hausimami ndani ya mji huo.

Kodi ya Kusajili Gari Kwa Kuandika Jina Lako Yaongezeka Kutoka Milioni 5 Hadi 10

$
0
0

Serikali imebainisha kuwa kodi ya usajili wa namba binafsi kwenye magari unategemea kupanda kutoka shilingi 5,000,000 mpaka shilingi 10,000,000 kila baada ya  miaka mitatu.

Hayo yamesemwa jana Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2016/17.

“Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Magari inayohusu kodi ya Usajili na Uhamisho wa Umiliki wa magari na kufanya ada ya usajili wa namba binafsi kupanda kutoka 5,000,000 hadi shilingi 10,000,000 kila baada ya miaka mitatu,” alisema Dkt. Mpango

Akitoa sababu ya kupandisha kodi hiyo, Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo imepanda ili kuhuisha viwango vinavyopendekezwa kulingana na thamani halisi ya fedha nchini.

Aidha, Dkt Mpango alitaja kodi nyingine zinazopanda katika sheria ya magari ni pamoja na usajili wa magari kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi 250,000 na pikipiki kutoka shilingi 45,000 hadi shilingi 95,000.

Katika hatua hiyo, Dkt. Mpango amesisitiza kuwa ongezeko hilo la kodi katika Sheria hiyo inayohusisha magari na pikipiki utaongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 26,915.9.

Bajeti ya Kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17 yenye jumla ya Shilingi Trilioni 29.5 imewasilishwa Juni 8, 2016 inategemewa kujadiliwa kwa muda wa siku saba na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Juni 10, hadi 20, 2016 ambapo mjadala utahitimishwa kwa kura ya wazi itakayopigwa na Wabunge.
.

Wasiotumia EFDs Marufuku Kufanya Biashara na Serikali

$
0
0

KUANZIA Julai mosi mwaka huu, serikali imepiga marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki - EFDs.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema hayo jana bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma jana. 

Aidha, Dk Mpango aliwapongeza wafanyabiashara walioitikia matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ambayo inamtaka kila mfanyabiashara isipokuwa wale ambao wametangazwa rasmi na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato kutotumia mashine za EFD kutoa risiti kila anapouza bidhaa au huduma.

Alisema ili kuwa na usimamizi mzuri wa fedha za serikali na kuhakikisha kwamba zinatumika kama ilivyokusudiwa, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Fedha za Umma na kanuni zake, alitangaza kuwa malipo yote lazima yaambatanishwe na ankara za madai au stakabadhi (tax invoice) zilizotolewa na mashine za EFD.

“Kwa sababu hiyo kuanzia tarehe 1 Julai 2016, ni marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki - EFDs.

Mwanza, Kagera, Kigoma Zaongoza kwa Umasikini wa Kipato

$
0
0

PAMOJA na maendeleo yaliyotokana na kukua kwa pato la wastani la Mtanzania na kupungua kwa umasikini wa mahitaji ya msingi, serikali imeainisha mikoa mitano iliyokithiri kwa umasikini wa kipato.

Akiwasilisha bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi ya 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016/17, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema mkoa unaoongoza ni Kigoma ambao wakazi wake asilimia 48.9, wanakabiliwa na umasikini uliokithiri wa kipato.

Mikoa mingine yenye umasikini wa kipato kiwango chake katika mabano ni Geita (asilimia 43), Kagera (asilimia 39), Singida (asilimia 38.2) na Mwanza (asilimia 35.3). 

Katika wilaya zilizokithiri kwa umasikini wa kipato, ni Kakonko mkoani Kigoma na Biharamulo mkoani Kagera, ambapo Dk Mpango alisema katika wilaya hizo, takribani asilimia 60 ya watu wake, wako chini ya mstari wa umasikini wa mahitaji ya msingi.

Tathmini ya hali ya umasikini kimaendeleo iliyoainisha umasikini huo, imetumia takwimu za Sensa ya Watu ya mwaka 2012 na Utafiti wa Hali ya Kipato na Matumizi katika Kaya wa 2012, ulionesha pia ahueni ya umasikini katika mikoa mitano.

Dk Mpango alitaja mikoa hiyo yenye ahueni na idadi ya watu wanaokabiliwa na umasikini wa kipato katika mabano kuwa ni Dar es Salaam (asilimia 5.2), Kilimanjaro (asilimia 14.3), Arusha (asilimia 14.7), Pwani (asilimia 14.7) na Manyara (asilimia 18.3). 

Pamoja na tathmini ya kimkoa na kiwilaya lakini katika nchi nzima, alisema kati ya mwaka 2010 na 2015, Pato la Mtanzania liliongezeka kutoka Sh 770,464.3 kwa mwaka mpaka Sh milioni 1.9 mwaka 2015 sawa na mara 2.5.

Aidha kupungua kwa umasikini nako kulikuwa kasi katika kiwango cha asilimia 6.2 ndani ya miaka mitano tu kati ya mwaka 2007 na 2012, ikilinganishwa na kupungua kwa umasikini kwa asilimia 4.6 tu katika miaka 15 kulikotokea mwaka 1992 mpaka 2007.

Kuhusu ajira, Dk Mpango alisema Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014 ulionesha kuwa nguvukazi ya Taifa ilikuwa watu 25,750,116 sawa na asilimia 57 ya watu wote wa Tanzania Bara.

Kati ya nguvu kazi hiyo, wanawake wametajwa kuwa 13,390,678 sawa na asilimia 52 na wanaume ni 12, 359, 438 sawa na asilimia 48. 

Pamoja na nguvukazi kuwa watu milioni 25.8, utafiti huo kwa mujibu wa Dk Mpango, ulionesha kuwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi walikuwa watu milioni 22.3 tu na sababu za watu kushindwa kufanya kazi zilikuwa ni ulemavu na ugonjwa wa muda mrefu.

Aidha, kati ya nguvu kazi ya taifa; watu milioni 25.8, utafiti huo umeonesha kuwa asilimia 77.8 ndio walikuwa katika ajira, wengi wakiwa wa vijijini sawa na asilimia 82.2 ikilinganishwa na mijini ambapo Dar es Salaam waliokuwa wakifanya kazi ni asilimia 59.8 tu.

Mafanikio ya kupungua kwa umasikini, yameonekana pia katika kuongezeka kwa umri wa kuishi wa Mtanzania kutoka miaka 51 ilivyokuwa mwaka 2001 mpaka miaka 61 kwa takwimu za mwaka 2012.

Vifo vya watoto wachanga chini ya mwaka mmoja, pia vimepungua kufikia 43 kwa kila watoto hai 1,000 mwaka 2015 kutoka vifo vya watoto 51 kwa kila watoto hai 1,000 mwaka 2010.

Kuhusu watoto wa chini ya miaka mitano, pia vifo vyao vimepungua kutoka vifo vya watoto 81 kwa kila watoto hai 1,000 mwaka 2010 mpaka vifo vya watoto 67 kwa kila watoto hai 1,000 mwaka 2015.

Mafanikio hayo ya kupungua kwa vifo na kuongezeka kwa umri wa kuishi wa Mtanzania, katika upande mwingine yameleta changamoto kutokana na kuongezeka kwa wasichana waliopata ujauzito utotoni.

Kwa mujibu wa Dk Mpango, idadi ya wasichana wanaopata mimba katika umri wa miaka 15 hadi 19 imeongezeka na kufikia asilimia 27 mwaka 2015, kutoka asilimia 23 mwaka 2010.

Dk Mpango alisema hali hiyo si dalili nzuri kwani kunaashiria kuongezeka kwa utegemezi na kudumaza jitihada za kuondoa umasikini katika jamii na kuwataka wabunge kushirikiana na Serikali kuhimiza watoto wa kike, kuongeza bidii katika masomo ili kwa pamoja kupatikane manufaa kutokana na mapambano ya umasikini.

Rais Magufuli Mgeni Rasmi siku ya Kimataifa ya Albino

$
0
0
Na: Lilian Lundo- MAELEZO
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa  kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama cha Watu Wenye Ualbino Nchini  (Tanzania Albinism Society) Nemes Temba ameeleza kuwa kupitia maadhimisho hayo jamii itapata fursa ya kupewa elimu muhimu kuhusu ualbino ili kuondoka na dhana potofu hususani ushirikina.

“Maadhimisho haya ambayo yataanza Juni 11 hadi Juni 13, 2016 yatasindikizwa na mambo mbalimbali ikiwemo  huduma za afya hususani uchunguzi na matibabu ya saratani ya ngozi pamoja na nasaha za viongozi na mabalozi, utambulisho wa Miss Albino Tanzania na uzinduzi wa kamusi ya ulemavu,” alisema Temba.

Temba aliendelea kuainisha kwamba  siku hiyo itawapa fursa watoto wenye ualbino waishio kwenye vituo mbalimbali nchini kutembelea mji wa Bagamoyo kujionea mambo mbalimbali chini ya ufadhili wa shirika la UNICEF.

Aidha Mwenyekiti huyo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapa vipaumbele watu wenye ulemavu akiwemo Dkt. Abdallah Possi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu hii inadhihirisha kuwa ulemavu si hoja bali utendaji kazi ndio kitu umuhimu.

Makamu Wa Rais Mhe. Samia Akutana Na Hashim Thabeet Mchezaji Wa NBA Leo

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mchezaji wa kikapu wa kulipwa nchini Marekani, Mtanzania Hashim Thabeet, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa  kuanzisha na kukuza michezo pamoja na vituo vya Michezo hapa Nchini.

Mchezaji wa kikapu wa kulipwa nchini Marekani, Mtanzania Hashim Thabeet akisaini moja ya mpira mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, akipokea Zawadi ya Mpira kutoka kwa Mchezaji wa Mpira wa kulipwa wa Kikapu nchini Marekani Hashim Thabeet, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa  kuanzisha na kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mchezaji wa Mpira wa kulipwa wa Kikapu nchini Marekani Hashim Thabeet, wakati alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo Juni 09,2016 kwa ajili ya kumuelezea kuhusu lengo na mpango wake wa  kuanzisha na kukuza vituo vya Michezo hapa Nchini. (PIcha na OMR)

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza

$
0
0
Tarehe 08.06.2016 majira ya saa 08:00hrs hadi saa 15:00hrs katika kisiwa cha Maisome kambi ya uvuvi migongo kata ya Maisome tarafa Kahunda  wilaya Sengerema  mkoa wa Mwanza, katika tukio la kwanza askari wakiwa doria  katika kisiwa tajwa hapo juu wakiambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Sengerema walifanikiwa kukamata nyavu (kokolo) haramu za kuvulia samaki 17 na timba 81 ambayo ni mitego ya kienyeji ya kutegea samaki, vilivyotelekezwa na wavuvi wasiojulikana  baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa askari wanaofanya doria na misako katika maeneo yao.


Jeshi la polisi linaendelea na misako pamoja na doria katika kisiwa hicho kwa kuhakikisha watuhumiwa waliotelekeza nyavu hizo haramu wanakamatwa na wengine wanaoshirikiana nao pia wanasakwa ili kukomesha uvuvi haramu katika kisiwa hicho, hii ni baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema kwamba katika kisiwa tajwa hapo juu kuna wavuvi ambao hutumia zana haramu katika shughuli zao za uvuvi za kila siku kitendo ambacho ni kinyume na sheria na taratibu za nchi.

Aidha tukio lingine sawa na tarehe na majiara tajwa  hapo juu kwenye kisiwa cha Kasarazi kata ya Bulyaheke tarafa ya Buchosa wilaya ya Sengerema, askari wakiwa doria walifanikiwa kukamata nyavu haramu za kuvulia samaki 9 na timba 04 zilizotelekezwa na wavuvi wasiojulikana  baada ya kupokea taarifa ya uwepo wa askari wanaofanya doria katika kisiwa hicho. Jeshi la polisi bado linaendelea na upelelezi pamoja na msako wa kuwasaka wavuvi wanaojihusisha na uvuvi haramu ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Baada ya zana hizo haramu kukamatwa ziliteketezwa kwa moto mbele ya uongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya na serikali ya vijiji hivyo na wananchi wakishuhudia, huku msako na doria katika visiwa hivyo na visiwa vingine vya jirani bado unaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi akiwataka waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwani limedhamiria kukomesha uhalifu katika mkoa wa Mwanza na kusimamia sheria na taratibu za nchi.

Katika tukio la pili
Mnamo tarehe 08.06.Majira ya saa 13:06 katika kijiji cha Sima kata ya Sima wilaya ya Sengerma mkoa wa Mwanza, askari wakiwa doria walifanikiwa kumkamata Sophia Sato miaka 54 mkazi wa kijiji cha Sima akiwa na pombe aina ya gongo lita 64 zikiwa ndani ya nyumba yake kitendo ambacho ni kinyume na sheria na taratibu za nchi.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa anafanya biashara hiyo ya kuwauzia wananchi wa kijiji hicho pombe hiyo haramu na kuifanya kazi hiyo kama  chanzo chake cha mapato kitendo ambacho ni uvunjwaji wa sheria, ndipo jeshi la polisi lilipokea taarifa kutoka kwa raia wema na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Aidha katika tukio lingine sawa na tarehe tajwa hapo juu majira ya saa 13:50 katika kijiji hicho cha Sima kilichopo wilaya ya Sengerema, askari waliokuwa doria walifanikiwa kukamata mitambo miwili ya kutengeneza pombe  haramu ya gongo na mapipa mawili yaliyotelekezwa na Elizabeth Martine aliyetoroka baada ya kupewa taarifa za uwepo wa askari wanaofanya doria.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa tajwa hapo juu amekuwa akijihusisha  na utengenezaji wa pombe hiyo haramu kwa muda sasa, na amekuwa akiwauzia wakazi wa kijiji hicho. Jeshi la polisi linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa pamoja na kuwasaka wahusika wengine anaoshirikiana nao katika biashara hiyo haramu ya pombe ya gongo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi akiwaomba waendelee kushirikiana na jeshi la polisi ili tujenge sote kwa pamoja Mwanza salama zaidi na kuweza kukomesha uhalifu katika mkoa wetu.

Imesainiwa na:
Sacp: Ahmed Msangi
Kamanda wa polisi (m) mwanza

Mahakama ya Rufani Yatengua Hukumu ya Mahakama Kuuu Dhidi ya Bosi wa Zamani wa TRA na Wenzake......Yaamuru Jalada Lirudi Mahakama Kuu Kwa Ajili ya Kusikilizwa

$
0
0

Mahakama ya Rufani Tanzania, imeamuru jalada la kesi inayomkabili Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kurudishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa rufani ya Jamhuri.

Pia, imeagiza jalada hilo lipangiwe kusikilizwa kwa jaji mwingine dhidi ya rufaa ya kupinga kuondolewa shtaka la utakatishaji fedha katika kesi ya kujipatia Dola za Marekani milioni 6.
 
Hukumu hiyo ilisomwa jana na Msajili wa Mahakakama ya Rufani, Zahra Maruma baada ya kusikilizwa na jopo la majaji watatu, likiongozwa na Mwenyekiti Salum Masati akisaidiana na Kipenka Musa na Augustine Mwarija.
 
Msajili Maruma alisema mahakama hiyo imeona kwamba Jaji Mfawidhi Moses Mzuna alikosea kukubali pingamizi la utetezi na kutupilia mbali kusikiliza rufani ya kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wa kuliondoa shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya Kitilya na wenzake.

“Mahakama hii imebatilisha uamuzi uliotolewa na Jaji Mzuna na kwamba imeamuru jalada lirudishwe Mahakama Kuu kwa ajili ya kupangiwa jaji mwingine wa kusikiliza rufani ya upande wa Jamhuri kuhusu kuondolewa kwa shtaka hilo” alisema Msajili na kuongeza.

“Kwa kuondolewa shtaka hilo Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) hakuwa na namna ya kurudi Mahakama ya Kisutu kuomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka kwa sababu kila shtaka linajitegemea na kwamba shtaka la kutakatisha fedha lilishaondolewa na kumalizika katika hati hiyo ya mashtaka dhidi ya washtakiwa” alisema Msajili Maruma wakati akisoma hukumu hiyo.

Akifafanua zaidi alisema Mahakama ya Rufani imebatilisha uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu na kuamuru kusikilizwa rufani ya DPP kama ilivokuwa imekatwa.

Mapema Mei 31, mwaka huu upande wa Jamhuri ukiongozwa na DPP, Biswalo Mganga, Naibu DPP, Osward Tibabyekomya, Mawakili wa Serikali Waandamizi, Shadrack Kimaro na Awamu Mbagwa uliomba mahakama hiyo kuangalia uhalali wa kuondolewa shtaka la kutakatisha fedha pamoja na uamuzi wa Jaji Mzuna kutupilia mbali rufani yao.

“Watukufu Majaji ni rai yetu upande wa Jamhuri, tunaomba  mahakama hii iangalie upya na kuiamuru Mahakama Kuu kusikiliza rufaa ya kuliondoa shtaka la kutakatisha fedha …”alidai DPP Mganga.
 
Akiwasilisha hoja za rufaa hiyo mahakamani hapo, Tibabyekomya alidai kuwa malalamiko yao ni kwamba Jaji Mfawidhi, Mosses Mzuna alikosea kukataa kusikiliza rufaa ya kuondolewa kwa shtaka hilo na mahakama ya chini.

Alidai kuwa kinachashtakiwa katika shtaka ni kosa ambalo limekamilika na kwamba linasisimama kwa kujitegemea.

“Watukufu majaji kitendo cha kufuta kabisa shtaka la nane la kutakatisha fedha dhidi ya washtakiwa kulihitimisha shtaka hilo kama lilivyokua limeshtakiwa  kwa kuwa lilikuwa linajitegema”alidai na kuongeza kuwa.

“Jaji Mzuna alikataa kwamba mahakama yake haina uwezo wa kuruhusu kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka na kwamba uamuzi huo ulionyesha haiwezekani kufanyika mabadiliko amri ambayo inahitimisha shtaka la nane” alidai msaidizi huyo wa DPP.
 
Mawakili wa utetezi wakijibu hoja za Jamhuri kwa nyakati tofauti; Wakili Majura Magafu alidai kuwa rufaa hiyo haina mashiko ya kisheria na kwamba ilifunguliwa mapema kinyume cha sheria mahakama hiyo itupilie mbali.

“Hakimu Mchauru hakukosea kama inavyodaiwa na Jamhuri kwa sababu alitoa nafasi kwamba wakati utakapofika kisheria wataruhusiwa kufanya mabadiliko… “alidai Magafu.
 
Dk. Ringo Tenga alidai kuwa baada ya kuondolewa shtaka hilo, upande wa Jamhuri haukuwasilisha maombi ya kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka.

Alex Mgongolwa alidai kuwa hoja zao za utetezi kwamba rufaa hiyo haina sababu za kutosholeza kisheria imefunguliwa kinyume cha sheria mahakama ifutilie mbali.

Mbali na Kitilya, washtakiwa wengine ni, aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na mwanasheria wa benki ya Stanbic Tanzania, Sioi Solomon.

Mchanganuo Mzima wa Bajeti ya Serikali 2016/ 2017 Iliyosomwa Jana Bungeni..... BOFYA HAPA Kujua nini Kimepanda na Nini Hakijapanda

$
0
0
SERIKALI imewasilisha Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 ya Sh trilioni 29.53, ambayo nguvu kubwa imewekwa katika kukusanya mapato kwa kulinda viwanda vya ndani na kubana matumizi ya serikali ili kuelekeza sehemu kubwa ya matumizi katika maeneo ya vipaumbele.

Katika bajeti hiyo, bidhaa za lazima zinazogusa maisha ya wananchi ikiwemo mafuta ya petroli na dizeli pamoja na ushuru wa barabara na maji ya kunywa, havijaguswa huku bidhaa za starehe kama bia, sigara, soda, juisi na nyingine kama nguo za mitumba, huduma za kupanga nyumba na uhamishaji fedha kwa simu, vikipandishwa kodi, huku kiinua mgongo cha wabunge, kufutiwa msamaha wa kodi.

Aidha, makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi, ikiwemo mapato ya taasisi za udhibiti kama Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Mafuta (EWURA), Shirika la Viwango (TBS), Jeshi la Polisi (Trafiki) na mamlaka nyingine za udhibiti, sasa yatapelekwa moja kwa moja katika Mfuko Mkuu wa Serikali ambapo mahitaji yao ya fedha yatatolewa na Wizara ya Fedha na Mipango, badala ya kujigawia kutokana na bakaa ya mapato waliyokusanya.

Aidha, maduka ya kutoa huduma katika majeshi, yamefutiwa kodi rasmi na badala yake, Serikali inajipanga kuongeza posho kwa askari, ili iwasaidie kukidhi mahitaji yao, huku taasisi za umma na ofisi zote za Serikali, zikipigwa marufuku kufanya biashara na mzabuni asiyetumia mashine za kodi za kielektroniki (EFD’s).

Kodi juu 
Katika bidhaa zilizoongezewa ushuru na kodi ni pamoja na vinywaji baridi, kutoka Sh 55 kwa lita mpaka Sh 58, huku ushuru wa forodha katika maji ya matunda (juisi) yanayotumia matunda yanayozalishwa hapa nchini, ukipanda kidogo kutoka Sh 10 mpaka 11 kwa lita. Juisi zinazotokana na matunda ambayo hayazalishwi hapa nchini, ushuru wake pia umepanda kutoka Sh 200 kwa lita hadi Sh 210 kwa lita.

Bia, vilevi, mvinyo 
Kwa upande wa bia, serikali imependekeza bia inayotokana na nafaka ya hapa nchini, ambayo haijaoteshwa kama kibuku, ushuru upande kutoka Sh 409 kwa lita mpaka 430.

Bia zingine, ushuru wake pia umepanda ambao sasa utatoka Sh 694 mpaka 729 kwa lita, huku bia zisizo na kilevi, ikiwa ni pamoja na vinywaji vya kuongeza nguvu, ushuru ukipanda kutoka Sh 508 kwa lita mpaka Sh 534.

Kwa upande wa mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu zilizolimwa nchini kwa kiwango cha asilimia 75, ushuru wake umepanda kutoka Sh 192 kwa lita mpaka Sh 202. 

Ushuru wa mvinyo unaotengenezwa na zabibu zilizolimwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25 kutoka Sh 2,130 kwa lita mpaka Sh 2,237. Vinywaji vikali, havikuachwa nyuma maana ushuru umepanda kutoka Sh 3,157 mpaka Sh 3,315.

Sigara 
Sigara zisizo na kichungi zinazotengenezwa kwa tumbaku ya hapa nchini kwa kiwango angalau asilimia 75 kutoka Sh 11,289 hadi Sh 11, 854 kwa kila sigara 1,000. 

Kwa upande wa sigara zenye kichungi zinazotengenezwa kwa tumbaku ya nchini kwa angalau asilimia 75, ushuru juu kutoka Sh 26,689 hadi Sh 28, 024 kwa kila sigara 1,000. 

Sigara zenye sifa tofauti na hizo, ambazo hazina vigezo hivyo vya tumbaku ya ndani, ushuru wake umepanda kutoka Sh 48,285 hadi Sh 50,700 kwa kila sigara 1,000.

Katika tumbaku ambayo iko tayari kutengenezwa kuwa sigara, ushuru wake umeongezeka kutoka Sh 24,388 hadi Sh 25,608 kwa kilo huku ushuru wa sigara aina ya Sigar ukibaki kuwa asilimia 30. 

Vilainishi, gesi asilia, simu juu 
Katika mafuta ya kulainisha mitambo, ushuru umepanda kutoka Sh 665.50 kwa lita hadi Sh 699 kwa lita, huku ushuru wa grisi za kulainisha mitambo, ukipanda kutoka senti 75 kwa kilo, hadi senti 79 kwa kilo.

Gesi asilia pia ushuru umepanda kutoka senti 43 kwa futi za ujazo mpaka senti 45 kwa futi za ujazo. 

Kuhusu viwango vya ushuru wa kuhamisha fedha kwa kutumia simu, serikali imependekeza kutoza ushuru wa asilimia 10, kwenye ada zinazotozwa na watoa huduma wa simu, katika kutuma na kupokea fedha, badala ya ushuru huo kutozwa tu katika kutoa fedha.

Kwa mujibu wa Dk Mpango, kwa utaratibu wa sasa, baadhi ya kampuni zinazotoa huduma zimetumia mwanya wa kuhamisha sehemu kubwa ya ada hizo kwenye kupokea fedha na hivyo kuwa nje ya wigo wa kodi. 

Ulaji wa wabunge, hisa
Kwa upande wa kiinua mgongo cha wabunge wakati wa kustaafu, sasa kitatozwa kodi kila mwisho wa muhula wa miaka mitano ili kujenga misingi ya usawa na haki katika utozaji wa kodi kwa kila mtu anayestahili kulipa.

Aidha, mapato yote yatokanayo na hisa katika kampuni mbalimbali sasa yatatozwa kodi, baada ya kufutwa kwa msamaha kwa waliokuwa wakimiliki hisa chini ya asilimia 25.

Kodi ya mishahara 
Katika kodi inayokatwa katika mishahara (P.A.Y.E), imepunguzwa kutoka asilimia 11 mpaka tisa kwa wafanyakazi wanaopata mshahara wa kuanzia Sh 170,000 lakini hauzidi 360,000. Kwa wanaopata zaidi ya 360,000 lakini haizidi 540,000, watakatwa Sh 17,100 pamoja na asilimia 20 ya kiasi kinachozidi Sh 360,000.

Kabla ya hapo walikuwa wakikatwa Sh 20,900 na asilimia 20 ya kiasi kinachozidi Sh 360,000. 

Wanaopata zaidi ya Sh 540,000 lakini haizidi Sh 720,000, watakatwa Sh 53,100 pamoja na asilimia 25 ya kiasi kinachozidi 540,000. 

Kabla ya hapo, walikuwa wakikatwa Sh 56,900 na hiyo asilimia 25 ya kiasi kilichozidi 540,000. Kwa wanaopata zaidi ya Sh 720,000 wao watakatwa Sh 98,100 pamoja na asilimia 30 ya kiasi kinachozidi Sh 720,000.

Kabla ya hapo, walikuwa wakikatwa Sh 101,900 pamoja na asilimia 30 ya kiasi kilichozidi Sh 720,000. 

Kodi za nyumba 
Serikali pia imependekeza malipo ya kupanga nyumba, nayo yatozwe kodi ambayo haikuweka kiwango, ila imependekeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato, apewe mamlaka ya kukadiria kiwango cha chini na cha juu cha mapato yapatikanayo na pango ili yatozwe kodi.

Kodi za nyumba, usajili magari, pikipiki 
Mbali na mapato ya kodi za nyumba, Serikali imependekeza kupandisha ushuru wa kusajili magari na pikipiki kutoka Sh 150,000 hadi Sh 250,000 kwa kila gari na kutoka Sh 45,000 hadi Sh 95,000 kwa kila pikipiki. 

Kwa watumiaji wa namba binafsi za magari, ada sasa itapanda kutoka Sh milioni 5 kila baada ya miaka mitatu mpaka Sh milioni 10.

Kodi ya majengo 
Aidha, kodi za majengo sasa hazitakusanywa na halmashauri, badala yake TRA ndiyo inayopewa mamlaka hayo ya kukadiria, kukusanya, kuhifadhi na kuiwakilisha katika halmashauri husika. 

Mbali na TRA kupewa mamlaka ya kukusanya kodi ya majengo, serikali pia imependekeza kupunguza misamaha ya kodi za majengo ili majengo mengi zaidi yaingizwe katika orodha ya kulipa kodi.

Ulindaji wa Viwanda 
Saruji aina ya (HS Code 2523.29.00) zinazotoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ushuru wake wa forodha umepandishwa kutoka asilimia 25 mpaka asilimia 35 ili kulinda saruji inayozalishwa nchini dhidi ya ushindani wa bei ya saruji kutoka nje ya nchi.

Kwa bidhaa za chuma ikiwemo mabati kutoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, nazo ushuru umetoka asilimia 0 mpaka 10, ili kulinda uzalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini, huku bidhaa za nondo kutoka nje nazo zikipandishwa kodi kutoka asilimia 10 mpaka 25, kwa nia ya kulinda viwanda vya ndani.

Nyavu za kuvua samaki kutoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ushuru wake umepanda kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 huku vichujia vya vilainishi na petroli kutoka nje ya nchi vikiongezwa ushuru kufikia asilimia 25 kutoka asilimia 10, ili kulinda bidhaa za ndani.

Sukari, ngano, mitumba, mafuta ya kula 
Katika sukari, serikali imekusudia kupunguza msamaha wa kodi na hivyo waagizaji wa bidhaa za sukari kutoka nje watalazimika kuanza kulipa ushuru wa asilimia 15 kutoka asilimia 10, huku ikitarajiwa kuongezeka zaidi na kuwa asilimia 20 mwaka 2017/18 na asilimia 25 mwaka 2018.19, ili kulinda viwanda vya ndani.

Kwa upande wa ngano kutoka nje, ushuru umepunguzwa kutoka asilimia 35 mpaka 10, kwa kuwa nchi za Afrika Mashariki hazina uwezo wa kuzalisha kulingana na mahitaji. 

Kwa upande wa nguo na viatu vya mitumba Serikali imepandisha ushuru kutoka dola za Marekani 0.2 mpaka dola za Marekani 0.4 kwa kilo, kwa nia ya kudhibiti nguo hizo lakini pia imetangaza kujiandaa kuzuia uingizaji wake.

Kwa upande wa mafuta ya kula kutoka nje nayo ushuru umepanda kutoka asilimia 0 mpaka 10 kwa mafuta ghafi ya kula, ili kuimarisha kilimo cha mbegu za mafuta na viwanda vya ndani. 

Tozo za pamba, kahawa, korosho 
Miongoni mwa tozo zilizofutwa kuondoa kero kwa wananchi ni mchango kwa kila kiwanda cha kuchambua pamba wa Sh 450,000 na ada ya vikao vya halmashauri wakati wa kujadili wafanyabiashara wa pamba ya Sh 250,000.

Kwa upande wa kahawa, Serikali imefuta ada ya leseni ya kusindika kahawa ya dola za Marekani 250, huku ushuru wa kusafirisha korosho wa Sh 50 kwa kilo, ukifutwa. 

Tozo zingine zilizofutwa katika korosho ni ushuru wa chama kikuu cha ushirika Sh 20 kwa kilo, gharama za mtunza ghala Sh 10 kwa kilo, kikosi kazi cha kufuatilia masuala mbalimbali Sh 10 na makato ya unyaufu.

Pia Serikali imepanga kuendelea kufuta tozo nyingine zinazokatwa na halmashauri, wakala na mashirika katika mazao ya wakulima, baada ya kufanya tathmini za kina.

Maduka kambi za jeshi 
Serikali imependekeza kufuta msamaha wa kodi uliokuwa ukitolewa katika maduka na migahawa maalumu kwa ajili ya askari wa majeshi, kutokana na msamaha huo kutumiwa vibaya na kupoteza mapato ya serikali na badala yake, askari watapata posho mpya juu ya posho ambazo wamekuwa wakipewa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images