Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mfungo wa Ramadhani Wapangua Ratiba ya Bunge

$
0
0

Bunge limetengua kanuni zake na kubadilisha muda wa kumaliza shughuli zake kwa lengo la kuruhusu wabunge Waislamu kutimiza wajibu wao wa kiimani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Utenguzi wa kanuni hizo ulipitishwa jana baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Jenister Mhagama kuomba Kanuni ya 28(4), ambayo kwa ujumla wake inaelekeza kwamba Bunge litaendelea kukaa hadi saa 2:00 usiku.

Mhagama aliomba kanuni hiyo itenguliwe na badala yake, kuanzia siku ya kwanza ya Ramadhani, Bunge lirejee saa 10:00 alasiri kama ilivyo sasa na kuahirishwa saa 12:00 jioni. Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wote waliokuwamo ndani.

Majambazi Yaliyotoroka Mapangoni Jijini Mwanza Yazua Hofu......Baadhi ya Wananchi Waanza Kuyahama Makazi Yao

$
0
0

Siku moja baada ya kutokea mapambano ya zaidi ya saa 16 baina ya Jeshi la Polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kwenye mapango ya mlima ya Utemini, wananchi wa eneo hilo wameingiwa na hofu ya usalama wao baada ya baadhi yao kuona wahalifu wakitoroka wakati wa tukio hilo.

Wananchi hao wana hofu kuwa majambazi waliotoroka wanaweza kurejea na kuwadhuru na tayari baadhi wameanza kuhama makazi yao.

Hofu ya wananchi hao imekuja baada ya polisi kupambana na watu hao usiku wa kuamkia juzi, wakitumia silaha kali zilizo sababisha kizaazaa kwa wakazi wa Utemini, kutokana na milio ya risasi na mabomu.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Utemini Ibanda, kata ya Mkolani, Jukael Kiula jana  alisema baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na mapango hayo wameanza kuhama makazi yao wakihofia kurejea kwa majambazi hao.

“Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya majirani, walikuwa wakiwaona watu wakipanda na kushuka kutoka kwenye milima yenye mapango waliyojificha watu hao. Lakini hawakuwatilia shaka wakidhani ni watu wanaopasua mawe, hadi siku polisi walipopambana na majambazi hayo,” alisema Kiula.

Mwenyekiti huyo aliiomba Serikali kuimarisha ulinzi na doria kwenye mtaa huo ili kuwahakikishia usalama wananchi.

“Hata ikibidi, askari wa Jeshi la Wananchi waweke kambi ya muda kwenye eneo hilo kudhibiti vitendo vyovyote vya uvamizi,”alisema.

Akizungumza na wakazi wa Utemini jana, mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga aliwahakikishia kuwa Serikali itaimarisha ulinzi kudhibiti uwezekano wa wahalifu kuendelea kutumia mapango hayo kujificha.

Konisaga ambaye alitembelea eneo la tukio jana, aliwaomba wakazi kutoa taarifa za maficho ya wahalifu pale wanapohisi kuna nyendo zinazotilia shaka.

Kamanda wa polisi wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema kiama cha wahalifu kimefika na kwamba tayari vyombo vya dola vimebaini mitandao ya uhalifu na wahusika na itawasaka usiku na mchana.

“Hatutakuwa na msalie mtume katika mapambano dhidi ya ujambazi Mwanza. Wote wanaojihusha na ujambazi watambue kuwa yatawakuta yaliyowakuta wenzao waliojaribu kupambana na polisi,” alionya Kamanda Msangi.

Mkuu wa Mkoa, John Mongella alisema mkakati wa kuifanya Mwanzaa iwe salama umeanza na hakuna mhalifu atakayeingia Mwanza na kutoka salama.

Kipindupindu Chatafuna Milioni 900

$
0
0

Serikali imetoa Sh900 milioni kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu nchini. Fedha hizo zilitolewa katika kipindi cha Novemba mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema watu 21,634 waliugua ugonjwa huo na wengine 338 kufariki dunia tangu ulipolipuka Agosti 15 mwaka jana.

Kuongezeka kwa kasi ya kusambaa ugonjwa huo nchini na ongezeko la wagonjwa na vifo kulimfanya Rais John Magufuli kufuta sherehe za Uhuru (9 Desemba) na kuwataka wananchi wote akiwamo yeye kushiriki usafi wa maeneo yao ya kuishi kuepuka ugonjwa wa kipindupindu.

Alisema kuenea kwa ugonjwa huo nchini ni aibu kwa kuwa unatokana na uchafu ambao unaweza kusafishwa bila gharama yoyote.

Waziri Ummy alizungumzia mgawanyo wa fedha hizo kuwa Sh520 milioni ziligawanywa kwenye mikoa iliyoathirika na ugonjwa huo, Sh251.1 milioni zilitumiwa kununulia dawa na vitenganishi.

Alisema Sh328.8 milioni zilitumika kwa kamati za afya kitaifa na pia kutekeleza shughuli mbalimbali za uelimishaji jamii, mafunzo ya wataalamu wa afya na kuwapeleka katika mikoa ili kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo.

Waziri huyo alisema takwimu za mwezi uliopita zinaonyesha kuwa idadi ya wagonjwa imepungua, sambamba na idadi ya mikoa na wilaya. 

“Ifahamike kuwa maji na mazingira yetu bado yanaweza kutunza vimelea hawa wa kipindupindu na jitihada tulizojiwekea, nasisitiza ziwe endelevu kwa mikoa yote,” alisema Waziri Ummy.

TRA Yakusanya Trilioni 1.032 Mwezi wa Tano

$
0
0

Ikiwa imewekewa lengo la kukusanya Sh12.054 kwa kipindi cha Julai 2015 hadi Mei 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kufikia malengo kwa kukusanya Sh1.032 trilioni kwa kipindi cha mwezi uliopita, ikiwa ni sawa na asilimia 100.7 ya lengo lililowekwa.

Makusanyo hayo yanaifanya Serikali ya Awamu ya Tano iliyoingia madarakani Novemba 5, 2015 kukusanya zaidi ya Sh6.567 trilioni katika kipindi cha miezi mitano. Takwimu zinaonyesha kwamba kuanzia mwezi Desemba, TRA haijakusanya mapato chini ya Sh1 trilioni.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi, jana, Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata alisema lengo lao kwa mwezi uliopita lilikuwa ni kukusanya Sh1.025 trilioni na kwamba, kuanzia Julai 2015 hadi Mei 2016 wamekusanya Sh11.956 trilioni.

“TRA imejiwekea mikakati thabiti ya kuongeza mapato kwa kipindi cha mwezi mmoja uliobaki ili kuweza kufikia au kuvuka lengo kwa mwaka huu wa fedha na kwa sehemu kubwa tumeendelea kupambana na magendo, hususan katika mipaka,” alisema Kidata.

Lowassa Awatakiwa Waislam Mfungo Mwema wa Mwezi wa Ramadhani

$
0
0

Waziri Mkuu wa Mstaafu ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa Tiketi ya Chadema ameibuka na kuwatakia mfungo mwema waislam wote nchini.

Kupitia ukurasa wake wa facebook. Lowassa ameandika;
"Waumini wa kiislam Tanzania wanaungana na wenzao kote duniani katika kutimiza moja ya nguzo tano Za uislam kufunga Ramadhan. 

"Mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ni kipindi muhimu sana kwa waislam kuwa karibu na mola wao.
 
"Kwa niaba ya Mke wangu Regina na Mimi binafsi, nachukua nafasi hii kuwatakia waislam wote nchini,kila la kheri na baraka tele kwenye mwezi huu.
 
"Hata hivyo nasononeshwa na hali ya maisha ya watanzania nchini hivi sasa inavyozidi kuwa ngumu.Bei Za bidhaa mbalimbali zimezidi kupanda na zaidi kuadimika kwa sukari ambayo ni bidhaa muhimu sana hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
 
"Nawaomba wafanyabiashara kupunguza bei ya bidhaa hususan zile muhimu katika mwezi huu, ili ndugu zetu waislam watimize Ibada yao vizuri.
 
"Aidha kwa waislam nawaomba tutumie mwezi huu kuliombea taifa letu amani,upendo na mshikamano.Lakini zaidi kuomba haki na hamu ya watanzania kuona mabadiliko ya kisiasa yanafanyika kwa amani na wale wenye ulevi wa kuminya haki hiyo, hawapati tena nafasi kutekeleza uovu wao na zaidi Kuwaombea viongozi wetu wawe na hofu ya Mungu.
 
"Mbarikiwe sana na nawatakia kila la Kheri."

CCM Yatangaza Kuzunguka Nchi Nzima Kuwakabili CHADEMA Waliojipanga 'Kumharibia' Rais Magufuli kwa Wananchi

$
0
0

Siku chache baada ya Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kufanya mikutano nchi nzima kwa lengo la kuishtaki kwa wananchi Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, CCM wamejibu mapigo  kwa kuapa kuwafuata kila kona watakayopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka alisema kuwa chama hicho hakiwezi kuvumilia kuona Chadema wanazunguka kuharibu taswira ya Rais Magufuli na Serikali yake ambayo alieleza kuwa imefanya kazi kubwa kuwatumikia wananchi katika kipindi kifupi.

Alisema kuwa wamepata taarifa zisizo na shaka kuwa Kamati Kuu ya Chadema iliyokutana Mei 16 mwaka huu ilibaini kuwa kwa muda mfupi, Magufuli ametekeleza ajenda zote ilizokuwa ikinadi wakati wa Uchaaguzi Mkuu.

Ole Sendeka alisema kuwa utendaji wa Rais Magufuli unatuma ujumbe wa dhahiri kuwa Chadema watashindwa tena katika uchaguzi wa mwaka 2020. 

Aliongeza kuwa malalamiko ya udikteta wanayoyasambaza yanaonesha kuwa hawana mjadala wowote wa kumkosoa Rais Magufuli.

“Tunawaonya viongozi wa Chadema. Wanapaswa kutumia majukwaa hayo kunadi sera za Chadema. Nataka kuwahakikishia kuwa, kama Chadema wataenda sehemu fulani Jumatatu, sisi tutakuwa pale Jumanne kusafisha hali ya hewa kwa kuwaeleza ukweli wananchi,” alisema Ole Sendeka.

Chadema wamepanga kufanya mikutano nchi nzima kwa kile walichoeleza kuwa ni kuishtaki Serikali kwa wananchi kuhusu mwenendo wa Serikali ikiwa ni pamoja na kubanwa kwa Demokrasia na Bunge kwa ujumla na utumbuaji majipu usiofuata sheria na taratibu.

Jeshi la Polisi Lapiga Marufuku Maandamano na Mikutano ya vyama vya Siasa

$
0
0


Ndugu zangu waandishi wa habari,
Katika siku za hivi karibuni, Jeshi la Polisi nchini, limepokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya mikutano na maandamano . hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake vya mbalimbali vya habari limebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder).

Aidha vyama vingine vya siasa vimeonyesha dhamira ya kupinga kile ambacho kitasemwa na wapinzani wao.

Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya kisiasa.

Kwa hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia tarehe 07/06/2016 hadi hapo hali ya usalama itakapotengemaa.

Jeshi la Polisi linawataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi.

Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili.

Aidha Jeshi la Polisi linawataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii.

Asanteni sana kwa kunisikiliza .

Imetolewa na:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi.

Rais Magufuli amteua Jaji Ferdinand Wambali kuwa Jaji Kiongozi

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Juni, 2016 amemteua Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi.

Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Shaaban Ally Lila aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mkoani Tanga.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

07 Juni, 2016


Bodi ya Mikopo Yakanusha Taarifa Zilizosambazwa Mitandaoni Kuhusu Maombi Ya Mikopo 2016/2017

$
0
0


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).

Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Baada ya kukamilika kwa taratibu hizo, mwongozo wa utoaji mikopo utatolewa rasmi na kutangazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na tovuti ya Bodi ya Mikopo www.heslb.go.tz

IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016

Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz)

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Azindua Mpango wa Maendeleo wa Taifa

$
0
0
UCHUMI wa Tanzania unazidi kukua kwa kiwango cha asilimia 7 kwa mwaka kutokana na juhudi za makusudi zilizofanywa na Serikali ikiwemo kuimarisha miundombinu, ukuzaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano na uchimbaji wa madini.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati alipokuwa akizindua Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/2017- 2020/2021.

Majaliwa alisema Mpango huo unalenga kuboresha maisha ya Watanzania kijamii na kiuchumi ili kuwaondolea umaskini kwa kuweza mkazo katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na viwanda.

“Umaskini umepungua kwa asilimia 6.2 na bado tunaendelea kufanya juhudi kubwa ili kupunguza umaskini,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa na kuongeza kuwa watanzania 10.78 milioni bado ni maskini.

Kwa mujibu wa Majaliwa alisema kuwa ukuaji wa uchumi inabidi uwe shirikishi kwa kila mwananchi kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali.

Akizungumzia suala la uwekezaji katika viwanda, Majaliwa alisema Watanzania wanapaswa kuwezeshwa katika kupata mitaji ya kuwekeza na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na kufikia uchumi wa kati.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na  Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema wakati umefika wa kuhakikisha ukuaji wa uchumi unatiliwa mkazo na serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji hasa katika viwanda na madini.

“Tumeamua kuboresha miundombinu ikiwemo ya ujenzi wa reli, kuboresha bandari zetu na kufufua Shirika la Ndege (ATCL) na kutekeleza miradi mikubwa ya uchimbaji wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na Liganga ambavyo vitaongeza pato la mtanzania kutoka dola za Kimarekani 1006 hadi 1500 ifikapo 2020,” amesema Dkt. Mpango.

Mpango huu wa Maendeleo ambao umezinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu una Kauli Mbiu isemayo “Kujenga Uchumi wa Viwanda ili kuchochea Mageuzi ya Uchumi na Maendeleo ya Watu”.

Rais Magufuli Apokea Shilingi Bilioni 12 Ya Tume Ya Uchaguzi Zilizokuwa Zimebaki Baada ya Uchaguzi Mkuu

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekabidhi shilingi Bilioni 12 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, zilizobaki baada ya uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amekabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha kwa Rais Magufuli leo tarehe 07 Juni, 2016 Ikulu Jijini    Dar es Salaam na kueleza kuwa bakaa ya fedha hizo haikuathiri kwa namna yoyote uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

"Mheshimiwa Rais fedha ambazo tunakukabidhi, tulijibanabana sana, japo muda wenyewe ulikuwa mfupi lakini tulijibanabana sana bila kuathiri utendaji wa shughuli za uchaguzi, isije ikawa inatoa sura kwamba iliathiri, haikuathiri, na katika hali hiyo kama ambavyo wengi ni mashahidi, hatujisifii, lakini uchaguzi ulienda vizuri" Amesema Jaji Mstaafu Lubuva.

Akizungumza baada ya kupokea mfano wa hundi hiyo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuokoa fedha hizo na kuzirejesha serikalini ili zipangiwe majukumu mengine na ametaka taasisi nyingine za serikali ziige mfano huo wa uzalendo na kutanguliza maslahi ya taifa.

"Kitendo hiki ambacho mmekionesha leo, kinaonesha ni kwa namna gani Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya uongozi wako Mheshimiwa Mwenyekiti ilivyo na watu makini na waadilifu sana, kwa sababu hizi fedha ambazo kwa lugha uliyotumia ni bakaa, kutokana na zile ambazo mlipewa zaidi ya Shilingi Bilioni 270, mkatumia shilingi Bilioni 261.6, mkabakiza shilingi Bilioni 12, mngeweza kuamua kusema hamkubakiza na hakuna mtu yeyote ambaye angewauliza, na saa nyingine pengine hakuna mtu yeyote ambaye angejua, mngeweza pia kusema kiasi mlichotupa hakijatosha, tunaomba mtuongezee ama mngetengeneza maneno mazuri mazuri ya matumizi, bado nina uhakika serikalini wasingejua" Amesema Rais Magufuli.

Pamoja na kukabidhi hundi ya bakaa ya shilingi Bilioni 12, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amemuomba Rais Magufuli aisaidie tume hiyo kupata jengo lake la ofisi kwa kuwa hivi sasa tume inatumia majengo ya kupanga ambayo yanaigharimu tume hiyo takribani shilingi Bilioni 1 na Milioni 400 kila mwaka kwa kulipia kodi ya pango, usafiri na gharama nyingine za uendeshaji.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amelikubali ombi hilo na kuamua kuwa fedha ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeziokoa (Shilingi Bilioni 12) kutoka kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana zitumike kujenga ofisi ya tume, na amependekeza ofisi hiyo ijengwe mkoani Dodoma.

"Na mimi ningefurahi zaidi kama hilo jengo lingejengwa Dodoma, kwa sababu Dodoma ndio makao makuu ya nchi hii, na hasa kwa sababu Dodoma ni katikati ya Tanzania" Amesisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amelikubali pendekezo la tume hiyo la kuanzishwa kwa mfuko wa tume ya uchaguzi ambao utakuwa unakusanya fedha kila mwaka kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaofuata, badala ya kuendelea na utaratibu wa sasa wa kusubiri mwaka wa uchaguzi ndipo zitengwe fedha zote za kugharamia uchaguzi huo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam

07 Juni, 2016

Polisi Watumia Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Wafuasi wa CHADEMA

$
0
0
Polisi mkoani Kahama wametumia mabomu ya machozi kutawanya makundi ya wananchi wanaokutwa wamekusanyika katika maeneo mbalimbali.

Mabomu hayo yameendelea kurindima katika viwanja vya CDT ili kuwatawanya wananchi hao waliokusanyika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara wa Chadema.

Mkutano huo ulipangwa kufanyika leo kuanzia saa 9.00 alasiri kabla ya polisi kuupiga marufuku na jeshi hilo kuzuia mikutano mingine kama hiyo nchini.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni la leo na Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo, Nsato Mssanzya amepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadharahadi hali ya usalama itakapotengemaa.

Amesema Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yoyote au chama chochote kitakachokaidi agizo hilo.

Jinamizi la Lowassa latimua wanaCCM 62 Songea

$
0
0

Wakati CCM Ruvuma ikiwatimua wanachama 62 kwa usaliti ikiwamo kumuunga mkono Edward Lowassa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, wabunge wa chama hicho wameteua wenzao 15 kufanya tathmini ya uchaguzi huo ikiwamo mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho.

Katika tukio la kwanza, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kupokea maoni kutoka kwa wanachama kupitia vikao kuanzia kata hadi mkoa, na kubaini kuwapo waliokiingiza chama kwenye matatizo makubwa kutokana na usaliti.

Alisema, hadi sasa viongozi tisa wametimuliwa wakiwamo wanachama 53 wa kawaida, baadhi wamepewa onyo kali, wengine walipewa ushauri.

Mwisho alisema mchakato wa kuwawajibisha wengine unaendelea ngazi za juu, kutokana na CCM mkoa kutokuwa na maamuzi nao.

Wabunge wachunguza
Katika hatua nyingine, chama hicho kimeunda kamati maalumu ya wabunge 15 kwenda kutathmini uchaguzi huo badala ya kutegemea ripoti zinazotolewa na makatibu wa wilaya na mikoa pekee. 

Hatua hiyo ilifikiwa juzi mjini Dodoma baada ya wabunge wa chama hicho kukutana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na kukubaliana kuchukua hatua.

Katibu wa wabunge wa CCM, Jason Rweikiza alisema kamati ya wabunge hao itawahoji wabunge wote wa CCM 267 kwa kuwa wao ndiyo wahusika wakuu, kuangalia changamoto walizokutana nazo.

Wajumbe hao 15 ni Joseph Mhagama, Dk Faustine Ndugulile, Joseph Kakunda, Profesa Anna Tibaijuka, Mboni Mhita, Peter Serukamba, Innocent Bashugwa, George Mkuchika, Munira Mustapha, Jasmini Tiisekwa na Abdallah Ulega.

Kamati hiyo itaangalia mfumo wa kura za maoni kwa wagombea ubunge, ili kuondoa watu wasiokitumikia chama ambao wamekuwa wakitumia fedha zao kupitia kwenye kura za maoni.

Bunge Lakanusha Uvumi Ulioenea Kuhusu Afya ya Spika wa Bunge Job Ndugai

$
0
0
Ofisi ya Bunge imesema Spika wa Bunge, Job Ndugai anatarajiwa kurejea nchini muda wowote akitokea India alipokuwa akifanya uchunguzi wa afya yake.

Taarifa hiyo ya Bunge imekuja siku moja baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza kuwa kiongozi huyo yuko katika hali mbaya, jambo ambalo limeelezwa siyo kweli. Takribani wiki ya tatu sasa, Ndugai hajaonekana bungeni.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya Bunge, Owen Mwandumbya alisema jana kuwa kiongozi huyo amekwenda India kwa uchunguzi.

Alisema Spika aliporejea kutoka India Desemba mwaka jana, alitakiwa kurudi tena baada ya muda kwa ajili ya uchunguzi.

“Atarudi muda wowote kuanzia hivi sasa kwani yuko nchini India,” alisema Mwandumbya.

Alifafanua kuwa hali ya spika iko vizuri na hivi sasa anafanya mambo ya kawaida ili aweze kurejea nchini.

Mwaka jana baada ya Ndugai kuwasili kutoa India, alisema afya yake iko imara na anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na madaktari.

Kikwete Ataka Vijana Duniani Wathaminiwe na Kuwezeshwa

$
0
0
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amesema,     ingawa   idadi kubwa ya vijana wasiokuwa na  uhakika wa maisha yao wala kazi zenye tija na staha wapo katika nchi zinazoendelea, dunia katika ujumla wake inapashwa  kuonyesha  utashi wa kisiasa na udhubutu   wa kuwekeza    kupitia vijana.

Amesema,  mazingira   ya mamilioni ya vijana  kukaa bila shughuli ya aina yote kunatoa mwanya kwa vijana hao   kurubuniwa   na kutumiwa na watu wasiokuwa  na nia  njema na hivyo kutishia  hali ya Amani,  usalama na ustawi wa mwanadamu na hatimaye kushindwa kufikia au kupata faida za kidemografia na maendeleo endelevu.

Mhe. Kikwete ameyasema   hayo  ( jumanne) hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, wakati alipotoa mhadhara   wa  13 wa kumbukumbu ya Rafael M. Salas. Mhadhara huu  ambao  mada yake  ilikuwa ni “ kuwekeza kwa vijana ili kupata faida ya kidemografia na maendeleo endelevu” uliandaliwa na  Shirika  la    Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya Watu( UNFPA) ikiwa ni sehemu ya   mikutano ya mwaka ya  Bodi  za Mashirika na Mifuko  iliyopo chini ya Umoja wa Mataifa.

Miongoni wa  viongozi  waliohudhuria na  kushiriki mhadhara  ni  pamoja na  Naibu  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Bw. Jan Eliasson, na  Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA  Dr. Babatunde Osotimehin ,  Bi. Carmelita R. Salas ambaye ni Mjane wa  Bw.  Rafael Salas aliyekuwa  Mkurugenzi  Mtendaji wa  kwanza wa  UNFPA, Mabalozi na wataalamu mbalimbali.

“Tafiti na taarifa mbalimbali zikiwamo za Umoja wa Mataifa, zinaonyesha wazi  ongezeko la  idadi kubwa ya vijana  wanaokadiriwa kufikia 1.8 bilioni  idadi ambayo ni hazina na raslimali kubwa, lakini  pamoja na uwingi wao, wengi bado wanaishi katika hali ya umaskini uliokidhiri,  na ukosefu wa fursa mbalimbali ambazo zingewazesha  kuishi  maisha yenye staha”. akasema Kikwete.

Na kuongeza kuwa, kati ya vijana hao 1.8 bilioni, 74 milioni hawana  ajira  akiwaelezea kama vijana wanaosubiri treni  kando ya reli, treni ambayo haiji.  Mazingira haya  yanadhihirisha upotevu wa  raslimali kubwa ambayo imewekezwa kwa vijana hao na  ambao wamepoteza matumaini.

Akafafanua zaidi kwa kutoa takwimu mbalimbali zinazoonyesha tofauti  ya  faidia za kidemografia  kati ya mabara ya Ulaya, Asia, Amerika ya Latini na Afrika ikiwa ni pamoja na utofauti wa matumizi ya raslimali watu kwa nchi zile ambazo zimethubutu kuwekeza kwa vijana.

Rais Mstaafu Kikwete katika  mhadhara wake huo  na ambao ulipokelewa vema sana na wajumbe waliohudhuria, pia ametoa  vielelezo vya kitakwimu vinavyoainisha  namna  gan  bara la  Afrika  lilivyo nyuma  karibu katika ikielemewa  kila eneo kuanzia  upatikanaji na   utoaji wa huduma za uzazi salama,  idadi ya wakunga wenye elimu ya kutosha, upatikanaji wa huduma za afya,  elimu,  maendeleo ya kijamii na yenye tija na stahiki na  kiwango  cha matumizi ya njia za kisasa  za uzazi wa mpango.

“Vijana  wakiwezeshwa, wakiaminiwa,  wakipewa fursa na wakithubutishwa wanauwezo mkubwa sana wa kuleta mabadiliko. Tunatakiwa  kuwaamini, tunatakiwa kuwashirikisha na kusizisikia sauti zao” amesema.
 
Na kuongeza kuwa , mipango  na sera zinazoandaliwa kwaajili yao vijana  ni vema  zikawa  shirikishi na kuzingatia  mawazo, maoni na matakwa ya vijana.

“Haya  na mengi mengi yakitekelezwa kwa kuzingatia mazingira  ya kila nchi na vipaumbele vyake,  tunaweza kugema nguvu kazi hii kubwa kujiletea maendeleo endelevu pasipo kumwacha yeyote nyuma” akasisitiza  Rais Mstaafu.
 
Katika  hotuba  yake hiyo iliyosheni takwimu na utafifi wa kisayasi, siyo tu  kwamba imeainisha hali halisi ya  mazingira waliyomo vijana bali pia imechochea  majadiliano na takafuri  ya kina.

Baadhi ya mambo  ambayo ameyatilia mkazo ni pamoja na  umuhimu wa  jamiii kuzingatia uzazi salama na wa mpango na kuwa na idadi ndogo  ya  watoto na ambayo wazazi wataweza kuimudu na elimu  itakayokidhi mahitaji ya  soko la ajira  lishe bora na  uchumi imara na endelevu.

Akimkaribisha Rais Mstaafu kuzungumza,  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Elliason pamoja na  mambo mengine  alimwelezea  Mhe. Kikwete  kuwa ni kiongozi  mpenda amani na  aliyemstari wa mbele katika kusimamia  afya ya mama na mtoto.


Serikali kuunda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Yamungu kayandabila amesema kuwa serikali iko mbioni kuunda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga.

Dkt Kayandabila ameyasema hayo jana  jijini Dare s Salaam alipokuwa akizungumza katika kipindi cha asubuhi cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds Fm.

“Sisi kama serikali tumesikia kilio cha wapangaji na tuko mbioni kumaliza tatizo hili kwa kuunda chombo kitakachodhibiti upandaji wa kodi hizi za nyumba kiholela,tumeshapokea kesi nyingi sana kutoka kwa wananchi na hivyo tumejipanga kulitatua kabisa tatizo hili”Alisema Dkt Yamungu.

Aidha katibu mkuu huyo amewaasa wapangaji wa nyumba za kupanga kuhakikisha wanakuwa na mikataba ya kisheria yenye makubaliano ya pande zote mbili kupunguza migongano isiyokuwa ya kilazima na kushauri kama watashindwa kumudu gharama za mwanasheria wanaweza kuwatumia wenyeviti wa serikali za mitaa kama mashaidi katika kusaini mikataba yao.

Awali ya yote Dkt Yamungu alizungumzia kukamilika kwa Sera ya nyumba ambayo iko mbioni kukamilika ikizungumzia masuala haya yote na kwa kiasi kikubwa sera hii itapunguza migogoro mingi ya masuala ya nyumba kwa ujumla.

Mwaka huu mwezi wa nne Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi aliweka wazi Bungeni nia ya serikali kutungwa kwa sheria itakayounda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga.

Zitto Kabwe Aitwa Polisi Kwa Mahojiano

$
0
0

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe jana tarehe 7/6/2016  aliitwa Polisi  na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam  ACP Camilius Wambura.

Kwa mujibu wa Katibu Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho  Ado Shaibu, amesema ACP Wambura amemuita Zitto Kabwe kuhojiwa ikiwa ni siku moja imepita tangu azindue operesheni Linda Demokrasia ambayo inatarajiwa kuzunguka nchi nzima kupinga ukandamizwaji wa Demokrasia nchini

Amesema licha ya Zitto kuitwa na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam  Wambura aliomba Zitto  asiende jana kwa kuwa ni karibu na masaa ya kufuturu na  kumtaka  aende leo  saa tatu asubuhi.

Kwa upande mwingine  Shaibu amesema  Chama cha ACT-Wazalendo kitawasiliana na wanasheria wao ili kupata tafsiri ya kimahakama ya uhalali wa jeshi la polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ambayo inatambuliwa na kulindwa na katiba.

Kesi ya Aliyemtukana Rais Magufuli facebook Kuanza Kusikilizwa Mfululizo Kuanzia Leo

$
0
0

Kesi inayomkabili Isaac Abakuk ambaye anatuhumiwa kumtukana Rais John Magufuli kwenye ukurasa wake wa facebook jana June 07 2016 ilishindwa kuendelea kutokana na upande wa Jamhuri kutokamilisha ushahidi na kuiomba Mahakama kuahirisha shauri hilo hadi  leo June 08 2016.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Augustine Rwezire wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha alikubali ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo ambapo inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo. Mshtakiwa anaendelea kuwa nje kwa dhamana kusubiri kesi yake itakapotajwa.

AUDIO: Mwembe Ambao usiku Hubadilika kuwa Mwalimu Nyerere na Mama Nyerere Wavuta Mamia ya Watu Kuushuhudia Tanga

$
0
0

Mti wa  ajabu aina ya Muembe umewavuta mamia ya wakazi wa Tengamano Jijini Tanga kuushuhudia ambapo inadaiwa kuwa mwembe huo ikifika majira ya jioni hubadilika na kuwa  na taswira ya mwalimu Nyerere kwa upande mmoja na Mama Nyerere kwa upande wa pili

Tukio hilo limesemekana lilianza kujitokeza June 6 2016.  "Ni kama muujiza fulani sio kwamba jambo hili liliwahi kujitokeza,  hapa nilipo ndio naona hali halisi ya huu mwembe, ni kama mtu alijaribu kuuchonga"- Anasimulia shuhuda wa Tukio hilo  Awadhi Ally

Bonyeza play hapa chini kusikiliza

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya June 8

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images