Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Jinsi Dawa Asilia Ya Mvunge Inavyo Tumika Katika Kunenepesha Na Kuongeza Ukubwa Wa Mwili.

$
0
0
Mti  wa  mvunge  ni  mti  ulio  thibitishwa  kisayansi, kuwa  na  uwezo   mkubwa  wa  kusaidia  kunenepesha  na  kuongeza  ukubwa  wa  mwili.  http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1675676/-/11rp5fp/-/index.html

Mti  wa mvunge  ni  mti  wenye faida  na  matumizi  mengi.  Karibu  kila  sehemu  ya  mti  huu  ina  faida  mwanadamu. 

Tunda  la  mvunge  husaidia  kunenepesha  mwili kuongeza ukubwa  wa  mwili.

Pia  husaidia  kunenepesha  pamoja  na  kuongeza  nguvu  ya  mwili  kwa  watu  walio  dhoofika  kutokana na  sababu  mbalimbali  kama  vile  kuugua  maradhi  tofauti  tofauti pamoja  na  msongo  wa  mawazo.

JINSI  YA  KUTUMIA  MTI  WA  MVUNGE  KATIKA  KUNENEPESHA   MWILI.
Ili uweze  kunenepesha  mwili  wako  kwa  kutumia  tiba  ya  mti  wa  mvunge, unatakiwa  kufanya  kama  ifuatavyo :

1.   MAHITAJI :
i.     Unga  wa   mti  wa  mvunge  vijiko  vidogo  vitatu.
ii.     Maji  lita  moja.

2.   MATAYARISHO
Chukua  vijiko  vidogo  vitatu  vya  unga  wa  mti  wa  mvunge, kisha  changanya  kwenye  maji  lita  moja  halafu  chemsha  hadi   dawa  yako  itokote  na  kubadilisha  rangi ya  maji  kuwa  ya  damu ya  mzee,.   Kisha  ipua, chuja,weka  makapi  pembeni, ubaki  na  juisi  yako.

MATUMIZI  :
Tumia  kunywa  vikombe  viwili  asubuhi, na  vikombe  viwili  jioni. Utafanya  hivyo  kwa  muda  wa  siku  thelathini.  UTAPATA  MATOKEO  MAZURI  SANA. MWILI  WAKO  UTAONGEZEKA, KUNENEPA  NA  KUNAWIRI.

LISHE   YA   KUTUMIA   PAMOJA  NA  TIBA  YA  MVUNGE.
 Pamoja  na   tiba  ya  mvunge, unashauriwa  kutumia   “ mboga  ya  ufuta “  walau  mara   mbili  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini .   Unaweza  kula  eidha  kwa  ugali, au  wali, au mkate, chapatti, vitumbua  maandazi  nakadhalika.  Kama  utakuwa  na  nafasi  ya  kutumia  mboga  ya  ufuta   katika  milo  yako  mitatu, itakuwa  ni  jambo  zuri  zaidi.

JINSI   YA   KUTAYARISHA  MBOGA  YA  UFUTA.

MAHITAJI :
 i.     Ufuta   vijiko  vikubwa   vinne
ii.     Nyanya   nne
iii.    Kitunguu  maji  kimoja
iv.    Mafuta  ya  kupikia.

MATAYARISHO
Unga ufuta  wako  kwa  mafuta, nyanya  na  vitunguu  kisha  uupike  hadi  uive.

MATUMIZI
Tumia  ufuta  wako  kama  mboga, kwa  kulia  na  ugali, wali,chapatti, maandazi  nakadhalika.

Fanya  hivyo  mara  mbili  kwa  siku  kwa  siku  thelathini.
JINSI  YA  KUPATA  DAWA  YA  MVUNGE :
 Kwa  mahitaji  yako  ya  dawa  ya  MVUNGE   pamoja  na  UFUTA  fika  katika  ofisi  za  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC, duka  la  kuuza  dawa  mbalimbali  za  asili  lililopo  jijini  Dar  Es  Salaam, katika  eneo  la  UBUNGO  jirani  na  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING, nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa  wateja  wa  jijini  Dar  Es  Salaan, wasio   na  nafasi  ya  kufika  ofisini  Ubungo, watapelekewa  dawa  mahali  walipo, kwa  wateja  waliopo   mikoani  na  nchi  jirani, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabasi, kwa  wateja  waliopo   Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  Boti, kwa  DIASPORA, watatumiwa  dawa  kwa   njia  ya  POSTA  au  DHL.

KWA  MAWASILIANO   YA  SIMU, PIGA  SIMU NAMBA  0766  53  83  84.

Na  Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu,  tembelea  kila  siku :


Wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam Wagoma

$
0
0
Wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam mpaka sasa wamegoma wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha kwa ajili ya kujikimu.
 
Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi, Shamila Mshengema amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizo kuwa zikitolewa na bodi juu ya lini fedha hizo zitatolewa.
 
Kwa kawaida pesa ya chakula huingiziwa kila baada ya siku 60 na mpaka sasa yapata wiki mbili pesa hiyo haijaingizwa
 
Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Rais Magufuli Kuzulu chuo hicho kwa ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba.

Kauli ya Serikali kuhusu wanafunzi 7802 wa UDOM waliorudishwa nyumbani

Wabunge wa Upinzani wametoka nje ya bunge kuonyesha kutokuwa na imani na Naibu Spika Tulia Ackson

$
0
0
Wabunge wa vyama vya upinzani leo wametoka nje kwa mara nyingine kupinga Naibu Spika Dk. Tulia Ackson kuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.

Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge asubuhi wabunge hao wametoka nje na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.

Hata hivyo Dk. Tulia ameanza kupaniwa na wapinzani tangu jana. Ni kwa madai kuwa wapinzani hawamwamini tena.

Wameeleza kuwa, namna anavyoliongoza Bunge, kauli zake na kuyumba kwake katika kusimamia haki kwa wabunge wa Ukawa na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumechochea kuonekana kuwa, nafasi aliyonayo haimstahili.

Kutokana na hali hiyo, Freeman Mbowe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana aliahidi kuanzisha mgomo dhidi ya Dk. Tulia.

Mbowe aliwaambia hayo wabunge wenzake mjini Dodoma kwenye kikao cha dharura alichoitisha na kushirikisha waandishi wa habari.

Alisema, Dk. Tulia ndio tatizo kuu la Bunge la Kumi na Moja na kwamba, kiongozi huyo wa Bunge kila anapokuwa kwenye kiti na kuongoza Bunge, mtafaruku hutokea.

“Nitapendekeza kuwa kila kikao cha Bunge kinachoongozwa na Tulia Ackson, sote tutoke nje ili kuonesha kwamba hatuna imani naye katika kuendesha shuguli za bunge,” Mbowe alisema jana.

Utekelezwaji wa kauli ya Mbowe umeanza leo ambapo sasa Dk. Tulia amebaki na wabunge wa CCM pekee.

Mabadiliko Ya Tarehe Ya Kuripoti Katika Makambi Ya Jkt Kwa Vijana Wa Form Six Waliochaguliwa Kujiunga Na Mafunzo Ya JKT

$
0
0

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linautangazia umma mabadiliko ya tarehe ya kuripoti makambini vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2016 na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2016.

Taarifa ya awali kwa vyombo vya habari nchini ilianisha tarehe ya kuripoti kuwa ni tarehe 01 June hadi tarehe 05 Juni 2016. 

Tarehe hiyo imeafanyiwa mabadiliko badala yake vijana hao wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 07 June hadi tarehe 10 June 2016 bila kukosa.

Atakayesikia tangazo hili amtaarifu na mwezie.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 31 Mei 2016

Nyongeza Ya Majina ya Vijana Waliomaliza Kidato cha 6 Wanaotakiwa Kujiunga na JKT Kabla ya Tarehe 10 Mwezi wa 6

$
0
0

Vijana wafuatao wameongezwa kuhudhuria mafunzo ya jkt katika makambi mbalimbali kama inavyoonekana hapo chini.

Pia baadhi ya vijana wamehamishwa makambi kutokana na sababu mbalimbali.Waripoti kwenye makambi kama inavyoonekana  hapa chini kabla ya tarehe 10 juni 2016.

S/NO    JINA                                                        KIKOSI
1     ABDILLAH RAMADHANI HAJI         MGAMBO JKT
2     ABDUL M. MTEKETA         MGAMBO JKT

3     ABDULAZIZ SALUM AHMAD         MARAMBA JKT

4     AGNES PETER MAGANGA         RUVU JKT

5     AGNESS EMMANUEL KITANDU         RUVU JKT

6     AGNESS PETER MAGANGA         MARAMBA JKT

7     AJUAE DAVIS AMINIELI         KANEMBWA JKT

8     ALEX MLOSO         MARAMBA JKT

9     ALFRED AIDAN MBANO         RUVU JKT

10     ALLY KAFERA ALLY         KANEMBWA JKT

11     ALVIN ISMAEL MAKUNDI         RUVU JKT

12     AMBWENE FRANK MWAKANEMA         MARAMBA JKT

13     AMOS ASEGE         RUVU JKT

14     AMOS KINGU         MARAMBA JKT

15     ANNA JORAM TIMBA         RUVU JKT

16     ANNA M. JANUARY         MSANGE JKT

17     ANTIA PANCRAS KAKWERA         RUVU JKT

18     AVITUS MUSHABI         RUVU JKT

19     BEATRICE BONFACE         MARAMBA JKT

20     BEAUTNESS JOHN NJAU         RUVU JKT

21     BENJAMIN STEPHEN NYANDA         RUVU JKT

22     BERNADINAH T. MAYOMBYA         RUVU JKT

23     BIBIANA CLETUS NJOKHA         RUVU JKT

24     BONIFACE DEOGRATIUS         RUVU JKT

25     BONIFACE JOHN         RUVU JKT

26     BRENDA JOHN BABU         MARAMBA JKT

27     BUNURI JUMA         RUVU JKT

28     CALISTER MKOLO         RUVU JKT

29     CAROLINE HENRY KABOGO         MARAMBA JKT

30     CAROLINE SOSTHENES MAHERI         RUVU JKT

31     CECILIA MPEMBA         RUVU JKT

32     CLEMENCE GWINO         RUVU JKT

33     COSTANTINE PETER         RUVU JKT

34     DANIEL BENEDICT MASHIKU         MAKUTOPORA JKT

35     DAVID L. MARIBA         RUVU JKT

36     DAVID R. MKUMBO         RUVU JKT

37     DENIS G SADALA         MARAMBA JKT

38     DEOUS SILIVESTA LUBINGA         RUVU JKT

39     DIALO MNYUKI         MAFINGA JKT

40     DICKSON JOCTAN MATOGO         MARAMBA JKT

41     DONAT ERENEST MAJALA         MAKUTOPORA JKT

42     DONATH ERNEST MAJALA         MAKUTOPORA JKT

43     DORCUS DEOGRATIUS         RUVU JKT

44     EDDAH SAUL ASWILE         RUVU JKT

45     EDWARD MMBARA MKIZU         MARAMBA JKT

46     ELAIN DIDAS MUTABINGWA         RUVU JKT

47     ELIAN E. NGONDO         RUVU JKT

48     ELINAZI YOAZ MSUYA         RUVU JKT

49     ELIZABETH DANIEL KIYABO         MGAMBO JKT

50     ELIZABETH MWAKITEGA         RUVU JKT

51     ELVIS MAHENGE SIMON         RUVU JKT

52     EMMA A. KILONZO         RUVU JKT

53     EMMANUEL PHILIPO         MGAMBO JKT

54     EVELYNE SCARION         RUVU JKT

55     EZEKIEL KWAKA MSESE         RUVU JKT

56     FABE MAGNUS NGONYANI         MAKUTOPORA JKT

57     FANUEL VICTOR KISIRI         RUVU JKT

58     FELICIAN PASCHAL ULAYA         RUVU JKT

59     FESTO MWAKAYO         RUVU JKT

60     FRANCES MASHAKA LUJAJI         RUVU JKT

61     FRODIANUS FIDERI         RUVU JKT

62     GABRIEL PATRICK LWESYA         MLALE JKT

63     GAUDENSIA MOHAMED MWALUNGWE         MAKUTOPORA JKT

64     GEORGE STANSLAUS SHAYO         RUVU JKT

65     GEORGIA ISHENGOMA         RUVU JKT

66     GERVAS PASCHAL KIHANGA         RUVU JKT

67     GETRUDE J. MASIMBANI         RUVU JKT

68     GIFTI A. LUGOME         MARAMBA JKT

69     GLORIA ALBERT MARINGO         RUVU JKT

70     GODFREY CHRISTIAN ROEBERT         RUVU JKT

71     GOODLUCK JOHN WILLSON         MGAMBO JKT

72     GREEN EUSTAD         RUVU JKT

73     GROLIA GODWIN KAHWA         MAFINGA JKT

74     HAJI SHEMHILU         RUVU JKT

75     HAPPINESS MGURU         RUVU JKT

76     HARRISON DAVID MRANGO         RUVU JKT

77     HASSAN RAJABU NJAU         RUVU JKT

78     HAWA ISSA MDENG'O         MARAMBA JKT

79     HAWA ISSA MDENG'O         MARAMBA JKT

80     HERI MOHAMED MKUMBEGE         RUVU JKT

81     HERIETH MAHENGE         RUVU JKT

82     HINDU HAMIS MRISHO         RUVU JKT

83     IBRAHIM ABDALLAH         RUVU JKT

84     IELEEN DIDAS MUTABINGWA         RUVU JKT

85     IMELDA IGNAS MBUNDA         MAKUTOPORA JKT

86     INZARI CHARLES LUGUTU         BULOMBORA JKT

87     IRENE KYENKUNGU         RUVU JKT

88     JACKLINE ADAM LEYNA         MGAMBO JKT

89     JACKLINE HERBET STEWARTH         MARAMBA JKT

90     JACKSON LUPAKISYO MWAIPUNGU         RUVU JKT

91     JAFARI S. JAFARI         RUVU JKT

92     JANE MGINJA MTIMBA         RUVU JKT

93     JANETH FORTUNATUS WAMBURA         RUVU JKT

94     JANETH V. KILONZO         RUVU JKT

95     JAPHET MASOTA         MARAMBA JKT

96     JASMIN MARTIN         RUVU JKT

97     JASMIN MARTIN SHAYO         MARAMBA JKT

98     JASMINE RASULI         RUVU JKT

99     JASON STEVEN         RUVU JKT

100     JIDIRU IZADINI KALOKOLA         RUVU JKT

101     JOHANITHA JOHN         MAFINGA JKT

102     JOHNSON JONATHAN JOHN         RUVU JKT
103     JORAM MBOMA JONATHAN         RUVU JKT
104     JOSEPH E. JOHNSON         MARAMBA JKT
105     JOSEPH REGNALD TUNGALAZA         RUVU JKT
106     JOSEPH TARIMO         RUVU JKT
107     JOSEPHINE BONIFACE MHANDO         RUVU JKT
108     JUENI MALIJANI         RUVU JKT
109     JUSTINE REGNALD MAKENE         RUVU JKT
110     KELVIN GEDION LEMNGE         MARAMBA JKT
111     KHADIJA E. KALONGA         RUVU JKT
112     KIBIBI HASAN JAMBIA         MARAMBA JKT
113     LAULENCIA ENGITRAUDA         842KJ
114     LEAH THOMAS MTWEVE         RUVU JKT
115     LILAN HENRY CASTORY         MAKUTOPORA JKT
116     LILIAN KANG'WA MASANJA         RUVU JKT
117     LUCIA JORAM TIMBA         RUVU JKT
118     LUGENDO LUCAS CHAPUGA         RUVU JKT
119     MARIAM M. JUMA         RUVU JKT
120     MARIAM WAMBURA         MSANGE JKT
121     MARIAMU S LIPENDE         MAKUTOPORA JKT
122     MARKO MICHAEL KASONI         RUVU JKT
123     MARTIN EWALD MALYAWERE         RUVU JKT
124     MARTINA GEORGE MWAILUSI         RUVU JKT
125     MARY ANTHONY MASSAWE         RUVU JKT
126     MARY I MREMA         MAKUTOPORA JKT
127     MASTERBETTER JOHN         RUVU JKT
128     MATHIAS BAHATI ORESTI         MAKUTOPORA JKT
129     MESHACK MARTIN LYIMU         MARAMBA JKT
130     MESHACK MARTIN LYIMU         RUVU JKT
131     MICHAEL DEOGRATIUS NJAU         MGAMBO JKT
132     MIRIAM M. JUMA         RUVU JKT
133     MUSSA KALUME AGUSTINE         RWAMKOMA JKT
134     MUSSA S. MAIGE         RUVU JKT
135     MWAMINI KADUMA         RUVU JKT
136     NAISHOOKI WILBERT OLE-MBILE         RUVU JKT
137     NAOMI ENMANUEL LEKASHINGO         MARAMBA JKT
138     NASRA NURDIN YUSSUPH         RUVU JKT
139     NEEMA JAMES MANYAMA         RUVU JKT
140     NEEMA MAIKO MASAGASI         RUVU JKT
141     NEEMA MSUYA         RUVU JKT
142     NESTARY AGATHON NDUNGURU         MAFINGA JKT
143     NESTARY AGATON NDUNGURU         MAFINGA JKT
144     NICODEMO JACOB         RUVU JKT
145     NOEL JAMES MWAKISOMBE         RUVU JKT
146     NORBERT NOEL         KANEMBWA JKT
147     NUSRAT ZAKARIA         RUVU JKT
148     OCTAVIAN BUBERWA         RUVU JKT
149     OMARI DIWANI OMARI         RUVU JKT
150     OMARY MAKOTA ALLY         KANEMBWA JKT
151     PAUL KATUNZI         MSANGE JKT
152     PRISCILA WENDE MGANA         MAKUTOPORA JKT
153     PROJESTUS H.CHAMAHANGA         RUVU JKT
154     RACHEL DAVID ISSAME         RUVU JKT
155     RACHEL DAVID ISSAME         RUVU JKT
156     RACHEL RAYMOS FOYA         RUVU JKT
157     RAHEL FESTUS ISOKOZA         RUVU JKT
158     RAMADHANI ALLY NJERA         RUVU JKT

159     RAMADHANI MBWAMBO         MARAMBA JKT

160     RAMADHANI RAJABU RAMADHANI         RUVU JKT

161     RAMADHANI RAJABU RAMADHANI         RUVU JKT

162     RECHO DANIEL MWALIMU         MAKUTOPORA JKT

163     REHEMA DEUS RUBALE         RUVU JKT

164     REHEMA SHAWARI IKAJI         MARAMBA JKT
165     REMIDIUS REYMOND MUTA         RUVU JKT

166     RETISIA SAANANE         RUVU JKT

167     RIDHIWANI SHABANI MAKUMBI         MGAMBO JKT

168     RISHAD KIHOMO MLELWA         RUVU JKT

169     ROGERS JOHN EZEKIEL         RUVU JKT

170     ROMAN CASTORY         RUVU JKT

171     ROSEMARY T. MASIAGA         MSANGE JKT

172     SADICK HASHIM MWAISAKA         RUVU JKT

173     SAIMON P. SOZIGWA         MARAMBA JKT

174     SALA A. MWAKAJWANGA         RUVU JKT

175     SALEHE MACHIBYA JONIOR         MGAMBO JKT

176     SALMIN AMRI         MARAMBA JKT

177     SALOME AMOS         RUVU JKT

178     SALOME SHITUNGURU         RUVU JKT

179     SHUKRANI MWAIPWISI         MAFINGA JKT

180     SIMON P. SOZIGWA         RUVU JKT

181     SOLINA SABAS         RUVU JKT

182     SOPHIA DEUS RUBALE         RUVU JKT

183     SOPHIA S. MATHIAS         MARAMBA JKT
184     STEPHEN F. NDALUSE         RUVU JKT

185     STIVEN NDALUSO         RUVU JKT

186     SUSAN PATRICK MNASIZU         RUVU JKT

187     SWEED IDD         RUVU JKT

188     TATU HAMAD HATIBU         RUVU JKT

189     TATU JUMA MYOVELA         MARAMBA JKT

190     TOMESTECLES H.CHAMAHANGA         RUVU JKT

191     TUMAINI JOHN MAKUNENGE         BULOMBORA JKT

192     TUMPALE JAPHET         RUVU JKT

193     VAILET GEORGE SIMBA         RUVU JKT

194     VALERIAN VEREMUND CHARLE         MAFINGA JKT

195     VERONICA CASMIR NDAMBARIKA         MAKUTOPORA JKT

196     VERUS THOBIAS KASONSO         RUVU JKT

197     VERUS TOBIAS KASONSO         RUVU JKT

198     VICTOR DAUDI ANYASIME         RUVU JKT

199     VICTOR L. AMBELE         RUVU JKT

200     VICTORY HENRY         RUVU JKT
201     WALTER FRUGENCE SAMKY         RUVU JKT

202     WILLIAM OSIAS MWANYIKA         RUVU JKT

203     WILLIAM PATRICK ASSEY         MGAMBO JKT

204     YASSER HAMAD MALESA         MARAMBA JKT

205     ZAMDA MWALIMU         MAKUTOPORA JKT

Rais Magufuli Ashiriki Katika Hafla Ya Utoaji Wa Tuzo Za Rais Kwa Wazalishaji Bora Wa Viwanda Kwa Mwaka 2015.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda  PMAYA The President’s Manufacure of the Year  pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya June 1


Taarifa toka Ikulu kuhusu uteuzi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO

$
0
0

TAARIFA KWA UMMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Dkt. Alex L. Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.), amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO kuanzia tarehe 31/5/2016 hadi tarehe 30/5/2019;
1.   Dkt. Samwel Nyantahe
2.   Dkt. Lugano Wilson
3.   Bw. David Elias Alal
4.   Mhandisi Stephen Peter Mabada
5.   Mhandisi Leonard R. Masanja

Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb) amekamilisha uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kuanzia tarehe 30/5/2016 hadi 29/5/2019 wajumbe  hao ni :

    Bw. Abdalah H. Musa
    Dkt. Coretha Komba
    Bw. Felix M. Maagi
    Dkt. Lightness Mnzava
    Bw. John B. Seka

Uzinduzi wa Bodi hizo utafanyika Makao Makuu ya Mashiriki hayo Siku ya Alhamisi tarehe 2 Juni, 2016, saa 4:00 asubuhi kwa Bodi ya STAMICO na saa 8:00 mchana kwa Bodi ya TANESCO.

Imetolewa na;
KATIBU MKUU
31 MEI, 2016

Rais Magufuli Awatangazia Vita Wafanyabiashara ‘Wajanja’

$
0
0
Rais John Magufuli amesema Serikali yake itaendelea kupambana na wanaoingiza bidhaa zilizochini ya kiwango na wale wanaokwepa kodi.

Amesema kwa kufanya hivyo, wanachangia kuviua viwanda vya ndani ya nchi.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana kwenye hafla ya utaoji wa Tuzo ya Rais ya wazalishaji bora wa viwandani kwa mwaka 2015 zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zimeandaliwa na Shirika la Wenye Viwanda Nchini (CTI).

Rais amesema pia hatawavumilia watendaji wote watakao wakwamisha wafanyabiashara wenye nia ya kuanzisha viwanda nchini kwa sababu zisizo za msingi na kuwaahidi kuwasaidia waweze kufanikisha ndoto zao.

Pia, amesema ni vizuri wafanyabiashara wote nchini wakatumia fursa zipatikanazo katika awamu hii ya uongozi wake, ili wasije kuzijutia baadaye.

“Nasema kwa dhati kutoka moyoni, you have my support, mkishindwa katika kipindi cha awamu ya tano basi hamtaweza tena,” alisema.

Rais Magufuli alisema nchi inapokuwa na viwanda vingi vitatoa ajira kwa Watanzania, vitaongeza mapato kwa Serikali na kuingiza fedha za kigeni kwa kuuza bidhaa nje ya nchi.

“Nina dhamira ya dhati ndani ya moyo wangu kuwasaidia wenye nia ya kuanzisha ya viwanda, siwachukii matajiri nawapenda matajiri,” alisema.

Rais Magufuli aliwapa moyo wafanyabiashara wenye viwanda kuanzisha vingine ili Serikali iweze kunufaika zaidi.

Alisema Tanzania ina rasilimali nyingi kama maliasili na madini na akawahakikishia wawekezaji kuwa lipo soko kubwa la bidhaa watakazozitengeza lenye watu milioni 160 katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Magufuli alisema sekta ya viwanda ni muhimili mkubwa wa uchumi katika nchi huku akitolea mfano wa nchi za China, India, Korea Kusini, Malaysia, Thailand na Vietnam  ambazo zimekuwa kwa kasi kwa sababu ya uwepo wa viwanda.

Alisema viwanda vinapoanzishwa nchini badala ya kuuza mali ghafi kwa bei ndogo zitatengenezwa bidhaa ambazo zitauzwa nje ya nchi na kutoa ajira kwa Watanzania.

“Badala ya kuuza ngozi tutengeneze viatu hapa hapa nchini au badala ya kuuza ng’ombe Comoro tumepeke nyama iliyosindikwa,” alisema.

Alisema nchi kama ya Sudan Kusini ina mahitaji makubwa ya unga wa mahindi.

“Lakini wanaofaidika na soko hilo ni Wakenya ambao wanakuja nchini wananunua mahindi, wanasaga na kuyapeleka huko,hivi wafanyabiashara tunashindwa hata kuanzisha viwanda vya kusaga mahindi,” alisema

Alisema Mkoa wa Arusha una ng’ombe wa  maziwa lakini yananunuliwa na Wakenya ambao wanayasindika kwenye viwanda vyao na kuja kuyauza hapa nchini.

Hata hivyo, alisema Serikali inaangalia uwezekano wa kuanzisha benki ya maendeleo ya viwanda kwa lengo la kutoa mikopo yenye masharti nafuu na riba ndogo.

Kuhusu kuondoa kwa changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo ya viwanda nchini, Magufuli alisema Serikali imeshatenga Sh1trilioni katika mwaka wa fedha ujao kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

Pia, Serikali imeunda kamati maalumu itakayoangalia mazingira ya ufanyaji biashara nchini ikiwamo kodi na tozo mbalimbali.

“Nchi yetu inakuwa na kodi za ajabu ajabu, mfano zao la kahawa kulikua na zaidi ya kodi 30. Haya ndiyo tunayoyaangalia,” alisema.

 Kuhusu upatikanaji wa mitaji na riba kubwa zinazotozwa na benki, alisema katika kukabiliana na matatizo hayo Serikali inajiandaa kuanzisha benki ya viwanda itakayowasaidia wenye wawekezaji.

Kwa upande wake  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema Serikali imejikita katika kuhamasisha ujenzi wa viwanda vingi zaidi nchini.

“Tumeandaa mkakati wa pamba hadi inakuwa nguo, alizeti hadi mafuta na tunaendelea kufufua viwanda vilivyokufa,” alisema.

Akizungumzia changamoto zinazowakabiri wenye viwanda nchini, mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), Samuel Nyantahe alisema uchakavu wa miundombinu ya umeme na miundombinu ya barabara imekuwa ikiongeza gharama za uzalishaji.

Pia, alilalamikia uwapo wa utitiri wa kodi, mamlaka za usimamiaji biashara na uwapo wa bidhaa bandia zinazotishia bidhaa za ndani.

Serikali Yaitaka RITA Kutoa Elimu Kwa Wananchi Kuhusu Umuhimu Kuandika Wosia Wa Mirathi

$
0
0

SERIKALI imeitaka wakala wa usajili,Ufilisi na Udhamini, RITA, kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuelewa umuhimu wa kuandika wosia na mirathi ,ili kuondoa migogoro kwa familia wakati wa kugawa mirathi ya marehemu.

Rai hiyo imetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu, alipokuwa akifungua kampeni ya siku nne ya kisheria inayotolewa bure na RITA, kuhusu kuandika mirathi na wosia na kuwaelekeza eneo salama la kuhifadhi wosia ukisha andikwa na mhusika   ili kuondoa migogoro mingi kwa familia pindi mhusika anapofariki dunia.

Mkuu huyo wa wilaya, alisema,wananchi wengi hawana elimu juu ya wosia na mirathi hivyo RITA, ambayo ni wakala wa  serikali ina jukumu kubwa la kuhakikisha elimu inawafikia wengi na hivyo kuwezesha wajane na watoto ambao ndio waathirika  kupata mirathi .

Alisema wosia unasaidia kutatua migogoro ambayo ingelijitokeza wakati wa kugawa mirathi ya marehemu na mtu kuandika wosia sio uchuro bali ni kuweka utaratibu wa mali za muhusika zitakavyogawiwa pindi akisha fariki dunia.

Aliikumbusha jamii kuwa msimamizi wa mirathi sio mrithi wa mali ya marehemu bali jukumuake ni kukusanya mali yote na madeni yote ya marehemu na kusimamia ugawaji na ulipaji wake na kamwe msimamizi yeyote asijihusishe na urithi .

Jamii nyingi zimekuwa zikiingia kwenye migogoro ya kugawana mirathi kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha ya kuandika wosia  kabla ya kifo na matokeo yake wanaoathirika ni wajane na watoto ambao hukosa haki yao .

Awali mratibu wa kampeni hiyo,msajili na wosia kutoka makao makuu ya RITA, Augostino Mbuya, alisema migogoro mingi imekuwa ikijitokeza kwenye familia wakati wa kugawa mirathi kutokana na kutokuwepo kwa wosia ambao ni mwongozo wa jinsi ya kuigawa mali ya marehemu kwa wahusika na matokeo yake watoto na wajane hukosa haki yao ya kurithi.

Alisema kutokana na hali hiyo RITA, ipo tayari kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma hiyo ya kuandika wosia kutokana na wananchi wengi kutokuwa na elimu na kufahamu wapi watapata huduma hiyo ya kuandika wosia na ugawaji wa  mirathi za marehemu

Mbuya,alisema mkakati uliopo ni kusogeza huduma ya kuandika wosia na mirathi ngazi za mikoa na wilaya pamoja na kuhakikisha wanakuwepo wanasheria wa kutosha lengo ni kuiwezesha jamii kuondokana na migogoro ambayo inaweza kuepukwa wakati wa kugawa mali za marehemu.

Alisema tangia kuanzishwa kwa huduma hiyo ya Rita, imeweza kusajili wosia zaidi ya 300 na 30 kati yake zimeshachukuliwakwa  utekelezaji .

Akisoma taarifa ya kazi za Rita, msajili wa mirathi na wosia, kutoka makao makuu ya Rita, Joseph Mwakatobe amesema mahakama kuu imeiteua RITA, kusimamia utatuzi wa migogoro  ya urithi na uandishi wa wosia lngo ni kuondoa migogoro inayojitokeza pindi mtu anaofariki dunia.

Alisema Rita, itaendesha kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi kuhusu kuandika mirathi na wosia katika mkoa wote wa Arusha,ili kuwezesha wajane na watoto wanapata haki yao ya kurithi mali za marehemu .

Aliongeza kuwa kuandka wosia ni swala lahiari ya mtu,na Rita, imekuwa ikikumbana na changamoto mbaimbali zkiwemo za kutokuwepo na wosia wakati wa mirathi .

Aliongeza kuwa mirathi inatolewa kulingana na sheria za dini ya kiislamu, mila na sheria ya India ya mwaka 1865 ambayo inahusisha makundi yote ambayo hayapo kwenye makundi ya kidini na mila.

Waziri Mkuu: Wataalamu Wa Malikale na uhifadhi wa urithi Kuweni Wabunifu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa mambo ya malikale na uhifadhi wa urithi asilia (natural heritage) watafute mbinu zitakazoimarisha utunzaji wa rasilmali hizo bila kuathiri mifumo ya uchumi ya nchi zinazoendelea.

Ametoa wito huo jana (Jumanne, Mei 31, 2016), wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa siku nne unaojadili Uhifadhi wa Urithi wa Dunia wa Afrika kama Nyenzo ya kuleta Maendeleo Endelevu ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha.

Waziri Mkuu alisema kuna baadhi ya nchi ambazo ni maskini sana lakini zimebarikiwa kuwa na rasilmali kama madini na gesi asilia lakini kwa sababu rasilmali hizo ziko karibu sana na vivutio vya urithi asilia wa dunia, watu wa nchi hizo wanazuiwa kuchuma rasilmali zao ili wasiharibu vivutio hivyo.

“Tunatambua umuhimu wa kutunza rasilmali na vivutio vya urithi asilia. Hivi ni kwa nini zisitafutwe teknolojia zinazofaa ambazo zitaruhusu uvunaji wa gesi asilia na madini bila kuathiri uhifadhi wa vivutio vya urithi asilia wa dunia (world heritage sites)?”, alihoji Waziri Mkuu.

“Serikali za nchi za Kiafrika zinahitaji suluhisho kama hili wakati zikiendelea kutafuta njia sahihi za kuwianisha uhifadhi wa vivutio vya urithi wa dunia na changamoto ya kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake,” amesema.

“Sisi viongozi ambao wengi wetu ni wanasiasa, hatukatai ushauri wa wataalamu lakini tunawasihi baadhi yenu ambao mnashiriki mkutano huu muhimu, mtafute njia mbadala za kufumbua tatizo hili badala ya kuendelea kutegemea njia za kizamani za kukabiliana na changamoto kama hizi ili sote tuweze kunufaika na rasilmali zilizopo ikiwa ni pamoja na kutunza vivutio vya urithi asilia wa dunia,” aliongeza.

Alisema kama rasilmali hizo zitachambuliwa vizuri na kwa njia sahihi bila kuathiri vivutio vya urithi wa dunia, ni dhahiri kuwa zitaingiza mapato ambayo kiuchumi yatasaidia kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi ambao pia watasaidia kwenye uhifadhi wa vivutio hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilmali nyingi zikiwemo za ardhini (madini), misitu, wanyama na maeneo ya kihistoria na kusisitiza kuwa Watanzania wana jukumu la kuzilinda ili zilete tija kwa wananchi wote.

“Tukizitunza rasilmali zetu zitasaidia kupata mapato kutokana na utalii Serikali itapeleka sehemu ya mapato haya katika miradi mbalimbali na hivyo kuchangia kwenye pato la Taifa,” amesema.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na UNESCO hasa katika masuala yanayohusu uhifadhi wa vivutio vya dunia kutokana na umuhimu wake kwenye maendeleo endelevu.

Alisema wizara yake imelenga kusimamia, kuendeleza na kuimarisha utunzaji wa maliasili na uhifadhi wa vivutio asilia na vya kiutamaduni (natural and cultural heritage) kwa kushirikiana na wadau wengine hapa nchini.

Naye Mkurugenzi wa Uhifadhi Malikale wa UNESCO, Dk. Mechtild Rossler aliwataka washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali duniani wawe tayari kupitia upya shughuli zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia wajibu wa nchi za Kiafrika katika kuandaa mwelekeo wa miaka ijayo.

Alisema katika miaka 40 ya utendaji wa UNESCO, idadi ya vivutio vya urithi wa dunia imeongezeka na kufikia 89 ambapo kati ya hivyo viko baadhi vinakavyobiliwa na changamoto ya kufutika kutokana na athari za kigaidi, matukio ya kivita na kazi za kibinadamu.

“Vivutio 16 kati ya 48 viko katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara na hivi vinakabiliwa na tishio la kupotea kutokana na vita, harakati za kigaidi na shughuli za kiuchumi za kibinadamu zikiwemo uchimbaji wa madini na gesi asilia,” alisema.

Aliwataka washiriki wa mkutano huo wakumbuke kuwa vivutio vya urithi wa dunia ni vielelezo vya jamii na pia huchangia uchumi kwa kutoa ajira kwenye jamii husika.

Mkutano huo unaohudhuriwa na washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani, unajumuisha washiriki kutoka nchi 36 zikiwemo nchi 12 ambazo ni za nje ya bara la Afrika.

Waziri Mkuu amerejea mjini Dodoma  jana mchana kuendelea na vikao vya Bunge.

Magufuli: Serikali Itakomesha Watumishi na Wanafunzi Hewa

$
0
0

RAIS John Magufuli (pichani) amesema Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kumaliza makosa yote yaliyojitokeza huko nyuma ikiwemo tatizo la watumishi na wanafunzi hewa lililoibuka hivi karibuni.

Amewataka Watanzania kuacha kuingiza siasa kwenye makosa yanapojitokeza, hasa yale yanayogusa sehemu nyeti kama elimu, kwani yakiachwa kuna uwezekano wa kutengeneza taifa la watu wa ajabu.

Alisema tangu aingie madarakani amekumbana na changamoto mbalimbali, ikiwemo matatizo ya rushwa, ukwepaji kodi, watumishi hewa na sasa amekumbana na tatizo la wanafunzi hewa.

“Nchi yetu ina changamoto na mambo mengi sana hata mimi nimekumbana na changamoto naziona mwenyewe, nikigeuka hivi watumishi hewa ambao hadi sasa wamefikia 10,500, nikigeuka hivi kuna wanafunzi hewa,” alisisitiza.

Alisema ni Tanzania pekee ambayo mtu anaweza kupata daraja la nne kidato cha nne katika elimu ya sekondari, halafu akapata fursa ya kujiunga na chuo kikuu na kupatiwa mkopo wa serikali, wakati mhitimu aliyefaulu kidato cha sita akikosa fursa hiyo.

Alisema endapo kulifanyika makosa lazima yarekebishwe, kwani inafahamika fika mtu akimaliza kidato cha nne akifeli ataanzia ngazi ya Astashahada, Stashahada ndio apate nafasi ya kujiunga chuo kikuu.

“Sasa hapa kwetu ni tofauti ukifeli kidato cha nne unajiunga chuo kikuu,” alihoji na kuwataka watu waache siasa kwenye makosa kwani mambo kama hayo yakiachwa kuna hatari ya nchi kutengeneza taifa la ajabu.

Hivi karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako aliivunja Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na kuwasimamisha kazi viongozi wanne waandamizi kwa tuhuma za kudahili wanafunzi wasio na sifa.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya TCU, Awadh Mawenya naye alisimamishwa kazi kwa kosa la kushindwa kuwachukulia hatua watumishi waliodahili wanafunzi hao wasio na sifa. 

Profesa Ndalichako alichukua hatua hizo baada ya TCU kudahili wanafunzi 489 waliopata daraja la 4.32 katika mitihani yao ya kidato cha nne lakini walijiunga na chuo kikuu na kupatiwa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 784.

Waziri Mkuu: Serikali Itahakikisha Inaendelea Kulinda Rasilimali Za Nchi Ikiwemo Urithi Wa Dunia

$
0
0
SERIKALI ya awamu ya tano  imesema kuwa itaendeleza jitihada za kutunza na kulinda urithi wa dunia ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi maeneo ya uhifadhi ili watanzania wote waweze kunufaikana rasilimali za nchi .

Hayo yalisemwa na  waziri mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akifungua mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa Afrika kama nyenzo ya maendeleo endelevu unaoendelea jijini Arusha

Majaliwa alisema kuwa rasilimali zilizopo ni za watanzania na ili kuhakikisha kuwa wananufaika nazo serikali itahakikisha  inatunza na kulinda uhifadhi ili yawe endelevu na  kusaidia vizazi vijavyo.

Alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi tajiri yenye urithi na hivyo ili kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika haswa waishio maeneo ya uhifadhi serikali itatoa elimu ya kutosha ili waepuke kuchangia uharibifu wa mazingira unaotokea kwenye hifadhi za taifa .
 
“Rasilimali hizi ni zetu na hivyo hata wanaoishi maeneo ya hifadhi watusaidie kwa wale wanaoingilia na kuharibu  kwani hata hizo mali asili zinatusaidia sote na ndiyo sababu  tumewekea mikakati ya kutunza maeneo hayo ili yawe endelevu"alisema

Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi alisema kuwa madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto na mambo ambayo yanatishia  na kuathiri uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia katika afrika .

Aidha mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kupitia upya shughuli zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.

Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kushawishi wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku inayotokea kwenye maeneo ya urithi wa dunia  kutokana na makundi ya kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.

Aliongeza kuwa pia  mkutano huo umejikita kwenye sera ya UNESCO  ya mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa uridhi wa dunia.

Mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia utakuwa na manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa bali pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya wageni watakao huthudhuria  mkutano huu pamoja na kuanzisha mitandao wa kitaaluma na kujenga mitaji wa kijamii” alisema Malinzi

Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro

Wahadhiri UDOM Wataja Kiini cha Mgomo Kilichosababisha Wanafunzi 7802 Warudishwe Nyumbani

$
0
0
JUMUIYA ya Wanataaluma ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA) imesema kilichotokea si walimu kugoma kufundisha programu ya Stashahada Maalumu ya Elimu, Sayansi, Hisabati na Tehama, bali tatizo ni kutoelewana na Menejimenti ya chuo kutokana na mazingira mabovu ya uendeshaji wa programu hiyo chuoni hapo.

Aidha, imelaani kitendo cha wanafunzi 7,802 wa Programu Maalumu ya Ualimu wa Msingi na Sekondari, waliorudishwa nyumbani bila kupewa muda wa kutosha kujiandaa kwa kuzingatia umri wao na mazingira waliyokuwa wanaishi, hali inayofanya wazagae mitaani huku wakiwa hawana pa kwenda.

Hayo yako kwenye tamko lililotolewa jana na Katibu wa jumuiya hiyo, Lameck Thomas, ambalo lilieleza kuwa lawama zimekuwa zikitupwa kwa walimu kutokana na taarifa hizo kutolewa na upande mmoja, ambao ni Menejimenti ya chuo kwenda serikalini bila kuwepo na taarifa yoyote kutoka kwa walimu kupitia jumuiya yao.

Thomas alisema si kweli kama walimu waligoma kufundisha lakini tatizo kubwa ni kutoelewana kati ya walimu na Menejimenti ya chuo kutokana na mazingira mabovu ya uendeshaji wa programu hiyo chuoni hapo.

"Hatuzungumzii fedha zaidi tunazungumzia suala la kuboresha elimu ili taifa lipate walimu wa baadaye katika kufundisha Sayansi, Hisabati na Tehama, vifaa vya kufundishia navyo ni changamoto kubwa,” alisema.

Katibu huyo alisema kama Jumuiya ya Wanataaluma wanapata hisia kwamba Wizara ya Elimu, imeamua kwa makusudi kushirikiana na uongozi wa chuo kupotosha uhalisia wa jambo hilo kwani hakuna hata wakati moja ambao wamefanya mawasiliano na walimu wenyewe kupata ukweli kutoka upande wao.

“Alichosema waziri bungeni juzi ni taarifa ya upande mmoja ambayo haitatupeleka kwenye utatuzi wa kudumu wa suala hili kutokana na ukweli kwamba walimu nao wana mengi ya kuzungumza,” alisema katibu huyo.

Alisema serikali imejenga desturi ya kuonana na menejimenti za vyuo pindi yanapotokea matatizo bila kupata taarifa kutoka vyanzo vingine hali ambayo imekuwa inasababisha vyanzo sahihi vya matatizo kutojulikana kwa uwazi.

Alisema changamoto za ufundishaji kutokana na uhaba na walimu kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo. Akitoa mfano alisema kwa sasa Chuo cha Sayansi Asilia na Hesabu, kina upungufu wa walimu 128 waliokuwa wanahitajika kufundisha programu hiyo kwa ufanisi; na kwa muhula uliopita walimu 72 tu ndio walibeba mzigo wa upungufu huo na muhula huu hali ilikuwa inaelekea kuwa mbaya zaidi.

“Wingi wa wanafunzi na uhaba huu wa walimu ulisababisha upangaji wa ratiba na kufundisha kutokana na ukweli kwamba kozi ziligawanywa katika mikondo mingi ambayo walimu walilazimishwa kuifundisha huku wakiwa na majukumu ya kufundisha kozi za shahada na majukumu mengine,” alifafanua.

Alisema chuo kimekuwa na desturi ya kupokea wanafunzi wengi bila kuzingatia idadi ya walimu waliopo na miundombinu ya kufundishia na kujifunzia na hiyo si mara ya kwanza kwa chuo kufanya hivyo, kwani mwaka 2008 walileta wanafunzi wengi ambao matokeo yake walimu kufundisha masomo mengi kuliko uwezo wao wa kazi.

Alisema taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma ilipotoshwa, kwani haijaeleza ukweli wa madai uliowasilishwa na chuo husika. 

Alisema katika Chuo cha Sayansi Asilia na Hesabu taarifa inasema yaliyowasilishwa ni madai ya Sh milioni 367.8 na kupungua mpaka Sh milioni 90 wakati uhalisia ni kwamba madai hayo hata yangebanwa namna gani yasingepungua mpaka chini ya Sh milioni 223.7.

Alisema mfano mwingine ni Chuo cha Elimu Masafa na Sayansi za Kompyuta ambao taarifa inasema waliwasilisha madai yanayozidi Sh milioni 100 wakati taarifa ya chuo inasema ni madai ya Sh milioni 53.7 tu.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Edson Baradyana alisikitishwa na yaliyotokea na kuitaka serikali kufanya jitihada za makusudi ili kumaliza mgogoro huo na hilo litawezekana kama walimu, wanafunzi na Menejimenti kukaa pamoja.

Baradyana alisema wanafunzi hawakutendewa haki kwani ilitolewa notisi ya ghafla ya kuondoka chuoni huku wengine wakiwa hawana nauli na hawakujua pa kwenda hali inayofanya waendelee kuzurura mitaani.

Alisema wanaamini kama Menejimenti ya chuo ingeonesha ushirikiano wa karibu kwa walimu wanaofundisha programu hiyo na kushirikiana, hayo yasingetokea au yasingekuwa makubwa kiasi hicho.

“Lazima kuangaliwa na kutatuliwa kwa changamoto nyingine zilizoibuliwa na wanataaluma na wanafunzi katika uendeshaji wa programu hiyo badala ya kujikita kwenye suala la malipo tu, serikali iwe na utaratibu wa kuwasiliana na walimu na wanafunzi mara kunapotokea matatizo vyuoni ili kupata taarifa toshelezi kutoka pande zote,” alisema Mwenyekiti wa Udomasa.

Aidha, wakati wa kurejeshwa nyumbani kwa wanafunzi hao wa Udom kukibebwa kisiasa na vyama vya upinzani, taarifa ya serikali imeeleza kuwa wahadhiri waliogoma, walitaka kulipwa posho ya zaidi ya Sh milioni 900.

Akitoa taarifa ya pili bungeni juzi usiku, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako  alisema wanafunzi hao si sehemu ya kazi zilizoko katika mikataba ya ajira ya wahadhiri hao, ila ni sehemu ya kazi ya ziada.

Kwa kuwa kazi hiyo ni ya ziada, Profesa Ndalichako alisema walikubaliana walipwe posho ya kazi ya nyongeza ambayo uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma ulikuwa tayari kutoa zaidi ya Sh milioni 200.

Kwa mujibu wa Profesa Ndalichako, wahadhiri hao walisisitiza kuwa wanataka posho hiyo iwe zaidi ya Sh milioni 900, jambo lililokataliwa na Mkaguzi wa Ndani wa Mahesabu wa Udom aliyesema kuwa kiwango hicho ni kikubwa kuliko uhalisia wa kazi yenyewe.

Kutokana na kutokubaliana kati ya wahadhiri hao na uongozi wa Udom, wahadhiri hao ndio wakaitisha mgomo wa kufundisha wanafunzi hao huku wakiendelea na kazi za kufundisha walio katika programu za shahada ya kwanza na kuendelea.

Profesa Ndalichako alisema kwa uamuzi huo wa wahadhiri, serikali isingeweza kuwachukulia hatua kwa kuwa wamegomea kazi ya ziada na si kazi waliyoajiriwa na kuingia mkataba na chuo.

Kwa hali hiyo, Profesa Ndalichako alisema serikali ililazimika kuingilia kati ambapo Mei 10, mwaka huu Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya alikwenda chuoni hapo kutafuta suluhu.

Mbali na Naibu Waziri, alisema hata makatibu wakuu wa wizara hiyo nao walikwenda kuzungumza na wahadhiri hao bila mafanikio, huku wanafunzi hao wakikaa chuoni bila kuingia darasani kwa wiki ya tatu.

Profesa Ndalichako alisema mbali na madai ya wahadhiri hao, pia wakati wa kutafuta suluhu ya jambo hilo, walitazama suala la tija kwa wanafunzi hao wa diploma maalumu ambao ni zaidi ya 7,800 na pia kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza ambao pia wanapaswa kufundishwa na wahadhiri hao.

Kutokana na kukosa masomo kwa wiki tatu mfululizo na kuwepo kwa uwezekano wa kukosekana tija katika ufundishaji, Profesa Ndalichako alisema ndio uamuzi wa kuwarudisha nyumbani wanafunzi hao ukafanyika ili serikali iangalie upya utaratibu wenye tija zaidi wa kuwaendeleza wanafunzi hao.

Aidha, Profesa Ndalichako alisema wakati wanafunzi hao wakitakiwa kurudi nyumbani, walizingatia hali yao ya kipato, kwa kuwa tayari walikuwa wameshapewa fedha za kujikimu za siku 60 tangu Aprili 21, mwaka huu. 

Profesa Ndalichako aliwataka wanafunzi hao kuvuta subira wakati serikali inatafuta namna bora ya kuwapatia elimu hiyo kwa kuzingatia tija kwao.

Shein: Hakuna Mtu Wala Nchi Yakuweza Kuniondoa Madarakani

$
0
0
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema hakuna nchi au jumuiya za kimataifa zitakazomwondoa madarakani yeye kwa sababu amechaguliwa kihalali na wananchi kwa kura nyingi kwa mujibu wa Katiba.

Dk Shein alisema hayo wakati akizungumza na wanachama na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika matawi ya Wesha Tibirinzi, Pembeni Shengejuu na Maziwa Ng’ombe, Micheweni katika ziara ya kuwafariji kutokana na matukio ya hujuma zilizofanywa na wapinzani huko Pemba.

Aliwataka wafuasi wa CCM na wanachama wake waliopo Pemba, wasibabaishwe na kauli zinazotolewa na viongozi wa vyama vya siasa wanaopita na kudai kwamba uchaguzi mwingine unakuja.

“Mimi ndiye Rais halali wa Zanzibar nimechaguliwa katika uchaguzi ulioitishwa na Tume ya Uchaguzi... wananchi msisikilize uvumi na kauli za wapinzani zenye lengo la kuwababaisha na kuwayumbisha katika shughuli zenu za maendeleo,” alieleza Dk Shein.

Dk Shein alisema amesikitishwa na kauli za uchochezi zinazotolewa na viongozi wa vyama vya siasa zenye malengo ya kuishawishi jamii kutengana na kugombana na kususiana hata katika shughuli za jamii ikiwemo misiba.

Alisema kiongozi anayefanya vitendo vyenye lengo la kuwagawa wananchi kwa malengo ya kisiasa  huyo ameishiwa na hana nafasi katika jamii. 

“Huyo kiongozi anayewashawishi wananchi kususia shughuli za jamii na maendeleo basi huyo ameishiwa kisiasa na hana nafasi katika jamii ya wananchi na ninyi mpuuzeni.Alikuwa na nafasi ya kushiriki katika uchaguzi lakini alisusa,” alieleza.

Alisema viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) wameishiwa hoja kwa sasa na hawana la kufanya baada ya kugomea kushiriki katika uchaguzi halali wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu ambao umetoa nafasi kwa CCM kushinda katika uchaguzi wa kishindo.

Mapema Dk Shein ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM aliwataka wanachama wa chama hicho kutembea kifua mbele na kuachana na unyonge kwa sababu chama chao ndiyo kilichoshika dola na kuunda serikali.

Akizungumzia yanayotokea Pemba, Dk Shein alisema, “Nimesikitishwa na taarifa za matukio mbalimbali yanayofanyika huku Pemba ikiwemo watu kususiwa maiti, kushushwa katika gari za abiria baada ya kuwa na itikadi tofauti......haya matukio hayakubaliki na yanakwenda kinyume cha maamrisho ya dini zote.”

Aliwataka viongozi waliopewa majukumu kwa mujibu wa Katiba kufanya kazi zao na kupambana na vitendo vya ubaguzi ikiwemo vya kuonewa kiholela wananchi.

Mbowe: Tupo Tayari Kutimuliwa Wote Bungeni

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson sasa amesababisha makubwa zaidi; wabunge kutoka vyama vya upinzani wako radhi kutimuliwa wote iwapo kiongozi huyo ataongoza vikao vyote vilivyosalia na wao kuendelea na msimamo wao wa kumsusia. 

Jana, Dk Ackson aliingia kuongoza kipindi cha maswali na majibu na wabunge wote wa vyama vya upinzani wakatoka ndani ya ukumbi na alipomuachia mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kuendelea na shughuli zilizosalia, walirejea ukumbini. 

“Kama Naibu Spika atakuwepo kwenye kile kiti, hatatuona bungeni, hata kama ni leo, ni kesho hata Bunge lote. Tuko tayari kuchukua gharama hiyo,” alisema kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe akiwa nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kuongoza wabunge wenzake kutoka ukumbini wakati wa kipindi cha maswali na majibu. 

Kauli hiyo ya Mbowe imekuja siku moja baada ya Dk Ackson kukataa Bunge kujadili sakata la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) waliotimuliwa kwa maelezo kuwa hawafundishwi kwa muda mrefu kutokana na walimu wao kugoma wakidai malimbikizo yao. 

Kitendo cha Dk Ackson kukataa hoja hiyo ijadiliwe, kilisababisha vurugu bungeni kiasi cha kuita askari kuingia kuwatoa wabunge waliokuwa wakipiga kelele na baadaye kuwaamuru waliokataa kukaa waondoke ukumbini. 

Wakiwa nje, walifikia uamuzi wa kususia vikao vyote vitakavyoongozwa na Naibu Spika na wakaanza kutekeleza uamuzi huo jana asubuhi. 

Kauli ya Mbowe pia imekuja siku moja baada ya Kamati ya Maadili, Kinga na Haki za Bunge kuwasimamisha wabunge saba kutoka vyama vya upinzani kuhudhuria vikao vya kuanzia mkutano huu hadi ujao kwa maelezo kuwa walifanya fujo wakati wakipinga hoja ya Serikali ya kusimamisha matangazo ya moja kwa moja ya baadhi ya shughuli za Bunge. 

Jana, Mbowe alisema wako tayari kutimuliwa wote kama uamuzi huo utawapendeza viongozi wa Bunge kwa kuwa siasa inaweza kufanywa ndani na nje ya Bunge. 

Mbowe alisema kuwa hali ilishafika hatua nzuri ya kujenga demokrasia nchini na kwamba pamoja na matatizo yaliyokuwepo, hali ilikuwa ikienda vizuri. 

“Lakini tangu kuingia kwa Serikali ya Awamu ya Tano mnaweza kuona Bunge limegeuka kituko. Bunge limegeuka mahali pa kukomoana. Bunge limekuwa mahali pa kutishana,” alisema Mbowe. 

“Naibu Spika anaamua kusitisha mjadala wa maana ili apate muda wa kuwadhibiti na kuwafukuza wabunge bungeni na anaona sifa. 

Tunaacha kujadili hoja ya msingi kama mambo ya Udom. Watoto wadogo wanalala nje haoni ni muhimu, anaona muhimu ni kuwafukuza wabunge wa upinzani.” 

Mbowe, ambaye pia ni mbunge wa Hai, alisema hawezi kukaa, kumsikiliza na kumheshimu Dk Ackson, bali wapinzani wataheshimu anayewaheshimu bila kujali anatoka chama gani na hawatamuheshimu asiyewaheshimu bila kujali cheo chake. 

“Sasa leo (jana) tumekataa kushiriki kipindi cha maswali na majibu kwa sababu yeye (Dk Ackson) anasimamia kipindi hicho na akitoka tutarudi bungeni. 

Akija mwenyekiti, akija Spika mwenyewe tutarudi bungeni. Lakini kama Naibu Spika atakuwepo kwenye kile kiti hatatuona bungeni, hata kama ni leo, ni kesho hata Bunge lote. Tuko tayari kuchukua gharama hiyo,” alisema Mbowe.

Dk Ackson alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia Septemba mwaka 2015 hadi Novemba 2015 alipochukua fomu za kugombea uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya CCM. 

Siku moja kabla ya CCM kuchagua mgombea wake, Dk Ackson alijitoa, hatua iliyoonekana ni kumpisha kada mwenye uzoefu zaidi, Job Ndugai. 

Wakati CCM wakisubiri uchaguzi wa mgombea wao, Rais John Magufuli alimteua Dk Ackson kuwa mbunge na baadaye akachukua fomu za kuwania unaibu spika, akiwa mgombea pekee wa chama hicho. 

Tangu aanze kuongoza Bunge, Dk Ackson amekuwa akikwaruzana na wabunge wa upinzani, ambao walishawahi kuhusisha kuteuliwa kwake na Rais kuwa mbunge ili apate mwanya wa kugombea unaibu spika, na mpango wa Serikali kutaka kulidhibiti Bunge. 

Akizungumzia mkakati wao jana, Mbowe alisema kwa kuwa siasa haifanywi bungeni tu, watakwenda kwa wananchi kuwashitaki viongozi wa Bunge. 

Alisema watafanya hivyo kwa kuwa kitendo cha kuwafungia wabunge wa upinzani kuwatetea wananchi ndani ya Bunge, kinaweza kufanywa pia nje ya chombo hicho. 

“Tutawaamsha wananchi nje ya Bunge kwa kuwa ni fursa hivyo tunakutana na wabunge wote waliotimuliwa na tutaungana wote bila kujali chama cha siasa kwa kuwa tumekubaliana kusimamia ajenda ya nchi na si ya chama chochote,” alisema Mbowe. 

LHRC yataka wabunge warudishwe 
Wakati wabunge saba wakianza kutumikia adhabu ya kufungiwa kuhudhuria vikao, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelitaka Bunge kuwarejesha ili kuendelea na majukumu yao. 

Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho, Dk Helen KijoBisimba alisema hoja ya kuwafukuza wabunge hao kwa sababu ya kudai haki ya kurushwa bunge ‘live’ ni kuwapokonya haki Watanzania waliowachagua kwenda kuwawakilisha bungeni. 

“Wabunge hao wamechaguliwa na wananchi na wanatetea bunge hilo kurushwa ‘live’ kwa maslahi ya wananchi waliowatuma, halafu kiti cha Spika kinaamua kuwafukuza bungeni. 

"Endapo ningepewa nafasi ya kuwashauri wapiga kura, ningewaambia kwenda kushiriki vikao vya Bunge wenyewe kwa sababu wabunge wao wameondolewa bungeni, hata mimi mbunge wangu wa Kawe ameondolewa,”alisema.

Mauaji ya Kutisha: Watu 8 Wakamatwa Kwa Mwenyekiti wa Kitongoji na Kuchinjwa Kinyama

$
0
0
MAUAJI ya Watanzania kwa njia ya kuchinjwa yanaendelea kushika kasi baada ya usiku wa kuamkia jana wakazi wanane wa kitongoji cha Kibatini, kata ya Mzizima jijini Tanga kukusanywa kwa mwenyekiti wa kitongoji na kisha kuuawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana.

Watu hao ambao inadaiwa kuwa ni majambazi walivamia usiku wa kuamkia jana kwa kuvunja milango ya nyumba tatu ambazo wakazi hao walikuwa wamelala na kuwachinja kisha kuiba biskuti, mchele na sukari na kutokomea navyo kusikojulikana.

Wauaji hao inadaiwa wana uhusiano na wahalifu ambao wamekuwa wakijificha ndani ya mapango ya Majimoto na kujihusisha na matukio kadhaa ya uvamizi ili kupora vyakula na kusababisha mauaji ya wakazi wa Jiji la Tanga, ikiwamo katika duka kuu la Central Bakery mwishoni mwa Aprili mwaka huu.

Mmoja wa shuhuda wa mauaji hayo, Kea Leonard (70) ambaye pia ni mkazi wa Kibatini, katika mahojiano jana alisema wanaamini kwamba chanzo cha mauaji ya wenzao ni kulipiza kisasi.

“Wiki iliyopita majira ya saa tano asubuhi hapa tulikamata vijana saba kati ya wanane wenye umri wa kama miaka 13 ambao walikuwa wakiranda randa hapa kitongojini ili kutafuta namna ya kuvuka mto kwenda ng’ambo ya pili na ndipo mmoja wao alipotutoroka,” alieleza Leonard na kuongeza:

“Watoto hao tulipowaweka chini ya ulinzi na kuwahoji tukaanza kuwatilia shaka hivyo mwenyekiti aliamua kuripoti Polisi na ndipo hao wakawachukua kwa ajili ya mahojiano na hatukufuatilia tena kujua kwamba waliachiwa au la kwa sababu hao watoto sio wenyeji wala wakazi wa eneo hili.”

Aliongeza kwamba wakati wahalifu hao wanavamia nyumba ya mjumbe wa serikali ya kitongoji kabla ya kumtoa nje walisikia mmoja wa watu hao akimhoji kuhusu mahali walipopelekwa watoto saba.

Diwani wa Kata ya Mzizima, Fredrick Charles alizungumza na waandishi wa habari na kuthibitisha kwamba kati ya watu waliokufa mmoja ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mleni uliopo kwenye kata hiyo.

“Hali ya usalama hapa kwetu Mzizima si shwari kwa sababu wananchi wangu wa Kibatini wamevamiwa na kuchinjwa usiku wa kuamkia jana majira ya saa sita usiku,” alisema Chiluba. 

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mleni kilichopo kitongoji hicho, Shabani Amani alisema wamepatwa na hofu kubwa kuhusu matukio hayo.

“Tunadhani kuna mapungufu katika suala la ulinzi hapa kwa sababu baada ya kutokea matukio kadhaa eneo letu hasa baada ya kudaiwa kwamba mapango waliyojificha wahalifu yako hapa jirani na kwetu kikosikazi cha mchanganyiko wa askari polisi na wa JWTZ wanafanya doria kwa saa 24 lakini tunashangaa kwa nini matukio yanaendelea,” alisema Amani.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul alithibitisha mauaji hayo. “Mei 30, mwaka huu majambazi waliokuwa na visu na mapanga walivamia kaya tatu na kuua wananchi majira ya saa saba usiku,” alisema Kamanda Paul.

Aliwataja waliouawa ni Issa Hussein (50) ambaye ni mmiliki wa kaya hiyo pamoja na kuibwa biskuti, mchele na sukari katika duka dogo. Wa kaya nyingine ni Mkola Hussein (40) na Hamis Issa (20), Hamis Issa (20) na aliyemtaja kwa jina la Mikidadi (70).

Kamanda aliwataja marehemu wengine ni Mahamud (35) ambaye ni mkwe wa Mikidadi, Issa Ramadhani (25), Kadir (25) na Salum ambao ni wachunga ng’ombe kijijini humo. 

Hata hivyo, mashuhuda wa tukio hilo akiwemo mke wa marehemu Mkola aitwaye Aisha Saidi, alisema walipofika nyumbani hapo waligonga mlango na kumtoa nje Mkola na kuondoka naye.

“Nimeachwa mjane na watoto sita... Baada ya hao watu kuingia walimkamata Mkola na kumdai aeleze kwamba watoto wao saba wamepelekwa wapi na alipojibu sijui wakamtoa nje na kumkusanya pamoja na wanakijiji hao wengine na kuwachinja eti tu kwa sababu hawakutaja mahali walipopelekwa watoto,” alisema Aisha.

Katika hatua nyingine, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa kupokea taarifa za vitendo vya mauaji ya kikatili vinavyoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali nchini.

“Wimbi hili la matukio ya vitendo vya mauaji na ukatili uliojitokeza kwa kufuatana mwezi Mei 2016 yanavunja haki ya kuishi ambayo ndio msingi wa haki zote za binadamu kwa ujumla wake.

"Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vikali mauaji haya yote na matendo yote ya kikatili dhidi ya mwanadamu yanapotokea popote nchini,” ilieleza taarifa ya Mwenyekiti wa Tume, Bahame Nyanduga.

Tume iliishauri serikali kupitia Jeshi la Polisi ichukue hatua mahsusi kuhakikisha ulinzi wa wananchi dhidi ya mauaji na vitendo hivi, kwani jukumu la kwanza la kuhakikisha usalama wa wananchi ni jukumu la serikali. 

Jeshi la Polisi lihakikishe watu wote waliohusika kutekeleza mauaji haya wanakamatwa ili sheria ichukue mkondo wake, ilieleza.

Mama Magufuli awasili mikoa ya kusini kwa ziara ya kikazi.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akimkaribisha Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani huko kwa ajili ya Ziara ya kikazi katika mikoa ya kusini.

Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi na Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na kinamama waliojitokea kumpokea alipowasili Mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi akimshukuru Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli kwa kuamua kufanya ziara ya kikazi mkoani humo.
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akiongea kwa niaba ya kina mama waliojitokeza kumpokea Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli ambapo alimuahidi kuendelea kumuunga mkono kwenye shughuli zake na kumtaka kwenda mkoni humo mara kwa mara kwa ajili ya ziara za kikazi.Katikati mwenye pochi ya bluu ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya Ungo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli alipofika mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya kikazi. Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa

Serikali Yatoa Ufafanuzi Uboreshaji wa Maslahi ya Polisi na Nafasi za JKT

$
0
0
Serikali imesema kuwa itaendelea kuboresha maslahi ya askari wa Jeshi la Polisi na kuwajengea nyumba za kisasa za kuishi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina wakati akijibu maswali ya wabunge kuhusu mkakati wa Serikali wa kuboresha maslahi ya Askari wa Jeshi hilo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Bungeni mjini Dodoma leo
 
Amesema kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 itatekeleza Mpango kabambe wa ujenzi wa nyumba za Polisi 4136 ambao utakwenda sambamba na ujenzi wa vituo vya Polisi.

Amesema Serikali imechukua hatua za haraka kulishughulikia suala la ukosefu wa nyumba za askari hao katika maeneo mbalimbali nchini ili kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yenye ukosefu wa nyumba hizo.

Amelieleza Bunge kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa maslahi ya Askari Polisi yanaimarishwa ikiwemo malipo ya Posho ya pango kwa askari wasio na nyumba ambayo ni asilimia 15 ya mishahara yao ili waweze kulipia gharama hizo.

Ameongeza kuwa  askari wenye utalaam maalum wakiwemo madereva na madaktari wamekuwa wakilipwa posho ya asilimia 15 ya mishahara yao na kuongeza kuwa askari wanaoajiriwa katika ajira mpya kama madaktari wamekuwa wakilipwa mishahara sawa na madaktari wengine bila kujali vyeo vyao.

“Serikali tumefanya jitihada kubwa sana kuboresha maslahi ya askari wetu, kama Serikali tumetoa posho za nyumba, posho za utalaam maalum kwa askari wote ambayo ni asilimia 15 ya mshahara wa kila Polisi hii yote ni kuwafanya askari wetu waweze kumudu gharama za maisha” Amesisitiza Mhe. Mpina.
 
Ameeleza kuwa kwa askari wanaofanya kazi katika mazingira magumu wakiwemo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wamekuwa wakipewa posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu (Hardship allowance) kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kila mwezi.
 
Mhe. Mpina amebainisha kuwa askari wote wanaohitimu mafunzo yao wamekuwa wakikatiwa Bima ya Afya kwa asilimia 100 na Serikali pamoja na udhamini wa mikopo mbalimbali katika taasisi za kifedha ili waweze kupewa mikopo na taasisi hizo.
 
Aidha, amesisitiza kuwa serikali imewapandishia kiwango cha Posho ya katikati ya mwezi (Ration Allowance) kutoka shilingi 180,000 za awali hadi 300,000 ambazo wanalipwa kwa sasa nchi nzima.
 
Katika hatua nyingine Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imetoa ufafanuzi kuhusu vijana wa kidato cha nne kutochukuliwa kujiunga na  Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi  amesema kuwa hatua ya kuwachukua vijana wote wanaomaliza kidato cha nne kwa sasa haiwezekani kutokana na uwezo mdogo wa kifedha wa Serikali.
 
Amesema kuwa uwezo wa JKT kuchukua vijana wa kujitolea kwa sasa ni 5000 hadi 7000 kwa mwaka kulingana na bajeti inayotolewa na kuongeza kuwa mpango wa Serikali ni kuendelea kutenga fedha na kujenga kambi zaidi za mafunzo ili kuwawezesha vijana wengi kujiunga  na mafunzo hayo kulingana na upatikanaji wa fedha.
 
Kwa upande wa wahitimu wa kidato cha sita wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa Sheria Mhe. Mwinyi amesema Serikali imewachukua vijana 14,000 na inaendelea kujenga uwezo wa ndani wa kuchukua vijana wengi zaidi.
 
Amesema Serikali inakusudia kujenga majengo ndani ya makambi ili kuwezesha vijana wote wanaohitimu kidato cha sita kupitia JKT kabla ya kujiunga na vyuo mbalimbali hapa nchini.
 
Aidha, Amefafanua kuwa kwa wale wanaojiunga na JKT kwa kujitolea ambao idadi yao inafikia 5000 sio wote wanaopata nafasi ya kuajiriwa katika vyombo vya Ulinzi na Usalama na kuongeza kuwa ni asilimia 71 ndio hupata ajira kwenye vyombo hivyo huku waliobaki wakilazimika kurudi nyumbani.
 
Amebainisha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaangalia utaratibu wa kuwawezesha vijana hao ili wanaporudi uraiani waweze kupatiwa mitaji ya kuwawezesha kujiajiri wenyewe.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images