Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Atishia Kuwatumbua JIPU Mawaziri Wawili......Wenzao Wabaki Vinywa Wazi Kikaoni

$
0
0
Operesheni ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri wawili ambao  pia walikuwa  manaibu  mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Taarifa kutoka katika chanzo cha kuaminiwa zimeeleza kuwa Rais Magufuli alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Mawaziri hao na kuwafokea mbele ya mawaziri wenzao  kwa kuwataja majina katika kikao maalum cha mawaziri kilichofanyika hivi karibuni.

"Ni mazingira ambayo mawaziri hawakuyazoea kwamba Rais anawaambia moja kwa moja kwa majina, anafoka akisema anaweza kuwafukuza wakati wowote.....

"Mawaziri wamezoea mara kwa mara wanapofanya kosa au uzembe wanaonywa kwa staili tofauti, ni kama ya kistaarabu hivi. Sasa huyu bwana mkubwa hana mchezo, aliwataja kabisa, tena mbele ya wenzao ambao walibaki vinywa wazi.

“Wewe (anataja jina la Waziri) na mwenzako (anamtaja jina pia) nitawatumbua,” Chanzo cha gazeti la Rais Mwema kinamkariri Rais Magufuli.

Mawaziri hao ambao ni wabunge wa kuchaguliwa majimboni kwa upande wa Tanzania Bara, wanaongoza wizara nyeti ambazo zinasimamia sekta mtambuka, wizara ambazo zinagusa sehemu ya ahadi za mabadiliko alizonadi Magufuli wakati akigombea urais katika kampeni za mwaka jana.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli aliwaonya pia mawaziri wengine ambao alionesha kutoridhishwa na utendaji wao kwakuwa hawaendani na kasi yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Magufuli alitaka atoe mfano kwa mawaziri wengine kwamba wao si watu maalum sana. Kama wanavyotumbuliwa watu wengine na wao pia wanaweza kutumbuliwa,” kiliongeza chanzo hicho

Rais Magufuli aliunda Baraza lake la Mawaziri mwishoni mwa mwaka jana na kuwashauri wasifanye sherehe ya kuteuliwa kwakuwa wakifanya vibaya hatawaonea haya atawaondoa mara moja bila kujali majina yao.

Utendaji wa Rais Magufuli umeendelea kusifiwa kila kona hususan katika kuwawajibisha viongozi wa ngazi zote na kuonesha nia ya dhati ya kuwahudumia watanzania huku akipambana na uzembe na ufisadi.

TRA Yabakiza Tshs. Trilioni 2.363 Kufikia Lengo Lao

$
0
0
Na Ally Daud- Maelezo.
Mamlaka  ya mapato Tanzania (TRA) imebakiza Tsh. Trilioni 2.363 ili kufikia lengo  waliojiwekea la kukusanya mapato ya trilioni 12.363 katika  mwaka wa fedha 2015/16, ambapo hadi sasa imekusanya kiasi cha Tsh. Trilioni 10.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi  wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa ya ajira za taasisi hiyo  Kamishina Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata alisema taasisi yake imefanikiwa kukusanya kiasi cha  sh trilioni 10 katika muda waliojiwekea na kuahidi kumalizia kiasi cha shilingi trilioni 2.363 kabla ya mwaka mpya wa fedha wa Serikali unaoanza mwezi Julai mwaka huu.

“Tumejiwekea malengo ya kukusanya kiasi cha fedha cha shilingi trilioni 12.363 kwa mwaka huu wa fedha na tumefanikiwa kukusanya shilingi trilioni 10 mpaka mda huu ila tunaendelea na kutimiza lengo letu hadi kufikia July mwaka huu na tutajipanga upya mwaka ujao wa fedha kufikia malengo mapema” alisema Bw. Kidata.

Aidha Bw. Kidata amesema kuwa kwa mpango huo wa mafunzo ulioanzishwa kwa  kushirikiana na Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA) ni mafunzo ya mwaka mmoja yanayoendana na usaili mpya kwa wahitimu ili  kufanya Mamlaka hiyo kuwa na wafanyakazi waadilifu na wachapa kazi ili kupaisha uchumi nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo cha cha Usimamizi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo alisema kuwa wameamua kuanzisha mpango huo kwa kushirikiana na Mamlaka ya mapato  ili kufundisha wafanyakazi wa TRA maadili na nyenzo za utendaji kazini  pamoja na kuendesha mafunzo ya dini ili kuwafanya wafanyakazi wawe wacha mungu katika kazi zao.

Aidha Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TRA Bw. Victor Kimaro aliwataka wafanyakazi wote wanatakiwa wafanye kazi kwa maadili hususani upande wa ukusanyaji kodi na Chuo hicho kimewafundisha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa ushindani katika maeneo ya kazi ili kuliletea taifa maendeleo yaliyokusudiwa.
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (katikati) akionesha kitabu cha mtaala mpya wa mafunzo kwa wafanyakazi (TRA) watakaopata fursa za kusoma katika Chuo cha Usimamizi wa Kodi (ITA), kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof. Isaya Jairo na kushoto na kushoto ni Kaimu Mkurugugenzi Rasilimali Watu na Utawala Bw. Victor Kimaro.
Baadhi ya washiriki  waliohudhuria katika uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango wa mafunzo ya kuhitimu kwa wafanyakazi waliopo kwenye fursa za ajira Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliofanyikia jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Rasmi  Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata

Waliombaka na Kumlawiti Binti wa Miaka 21 Morogoro Wapandishwa Kizimbani

$
0
0
WATU sita wanaodaiwa kumbaka na kumlawiti msichana kisha kumrekodi na kusambaza video hiyo, leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.

Miongoni mwa watuhumiwa hao ni pamoja na Iddi Adamu Mabena (32) Mkazi wa Njombe na Zuberi Thabiti (30) Mkazi wa Mbalali, Mbeya ambapo kesi hiyo inasimamiwa na waendesha mashtaka watatu wa serikali- Grolia Rwakibalila, Edgar Bantulaki na Kalistus Kapinga.

Akisoma maelezo ya kosa katika shtaka la kwanza la kubaka na kulawiti, Wakili Rwakibalila aliwataja wahusika kuwa ni pamoja na Iddi Adamuna Zuberi Thabiti.

Mwendesha mashataka huyo amedai kuwa, washtakiwa hao kwa pamoja huku wakijua kufanya hivyo ni kosa, walimbaka na kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka 21 na kumsababishia maumivu makali.

Wakili huyo alidai kuwa, washtakiwa hao walimbaka na kumuingilia kinyume na maumbile msichana huyo tarehe 27 Aprili, saa 1 usiku katika  nyumba  ya  kulala  wageni ya Titii iliyopo  katika Tarafa  ya  Dakawa  Wilaya  ya  Mvomero.

Hata hivyo, mawakili wote wa serikali walipinga dhamana ya washtakiwa hao kwa madai kuwa, kesi hiyo imegusa hisia za watu wengi hivyo kwa usalama wao pia kuhofia kuharibu ushahidi ni bora waendelee kushikiliwa.

Mbele ya Marry Moyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi washtakiwa hao walikana kuhusika na mashtaka hayo ambapo wamerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana. Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Juni Mosi mwaka huu na kwamba, upelelezi haujakamilika.

Katika shtaka la pili washtakiwa hao wakiwa na wenzao wanne walipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo wakikabiliwa na shtaka la kusambaza picha chafu za ngono katika mtandao wa kijamii wa whatsapp.
 

Edgar Bantulaki, mwendesha mashataka amedai kuwa, washtakiwa hao wamefanya kosa hilo chini ya kifungu cha sheria namba14 (1) (b) na 2 (b) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.

Bantulaki amewataja washtakiwa wengine kuwa ni pamoja na mshtakiwa namba 1 na 2 na Rajabu Salehe, (30), Ramadhani Ally (26), Muhsin Ng’ahy (36), John Peter (24) wote wakiwa ni wakazi wa Wami, Dakawa wilayani Mvomero.
 

Mwendesha mashtaka huyo amedai kuwa, washtakiwa wote kwa pamoja walianza kusambaza picha hizo kati tarehe 28 hadi 30 Aprili mwaka huu wilayani Mvomero na mkoa mzima wa Morogoro kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp.
 

Hata hivyo Ignas Kunge, wakili wa mshtakiwa wa nne (Ally) aliiomba mahakama kumpa dhamana mshtakiwa wake jambo lililopingwa na mawakili wa serikali kwasababu suala hilo limegusa jamii zaidi pia kwasababu za kutoingilia na kuharibu upelelezi wa kesi hiyo.
 

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Ivan Msaki, washtakiwa hao walikana kuhusika na shtaka hilo ambapo wamerejeshwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Juni Mosi mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa kwa kujadiliwa suala la dhamana iliyopingwa kwa kiapo na mawakili wa serikali.

Urlich Matei, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro amesema, washtakiwa hao wamepandishwa kizimbani kati ya 11 waliokuwa wakituhumiwa kuhusika na tuhuma hizo kufuatia upelelezi kutokamilika dhidi yao.

Kamanda Matei amesema, katika hatua za awali upelelezi kipolisi ulikamilika kwa watuhumiwa sita wa mwanzo ambao ndio wamefikishwa mahakamani.

Aidha amesema kuwa, vitendo vilivyofanywa na watuhumiwa ni vibaya na ambavyo kamwe haviwezi kuvumiiwa na jamii katika nchi.
 

Hivyo ametoa rai kwa wananchi kuacha kufanya uhalifu kwa kutumia mitandao kwani sheria yake iliyopitishwa na bunge hivi karibuni haitamwacha mtu akiwa salama.
 

Hata hivyo kamanda huyo ameomba polisi wapewe kifaa kama cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili waweze kufanya kazi zao kwa uhuru na kukamilisha mwenendo wa kesi mapema.

Amesema, kwa sasa uhalifu kwa njia ya mitandao unakuwa kwa kasi duniani kote na kwamba, mtu anaweza kutenda makosa mengi yanayosumbua jamii ikiwemo wizi mkubwa na mdogo wa fedha kwenye benki, makosa ya udhalilishaji, lugha za matusi na mengine mengi.


Amesema kuwa, kupatikana na kifaa hicho kutasaidia ushahidi kuwa madhubuti na sio rahisi kumwondoa mtu katika hatia.


Pia amewataka wananchi wote hususan vijana kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yao badala ya kutumia muda mwingi katika mitandao
  ya kijamii
Safari ya kuelekea kizimbani ikiwa imeiva.

Zuberi Thabit mtuhumiwa wa ubakaji.
Idd Adamu mtuhumiwa wa kurekodi video za ubakaji.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali awataka Mawakili wa Serikali kutoa ushauri wa Mikataba kwa makini.

$
0
0

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju amewataka Mawakili wa Serikali kuwa makini na kutoa ushauri kwa uadilifu na uweledi wa hali ya juu pindi wanapotoa ushauri wa kisheria kuhusu mikataba mbalimbali.

Mhe. Masaju ameitoa kauli hiyo alipokuwa akiongea  na Mawakili  wa Serikali wakati wa ufunguzi wa mafunzo yanayohusu uhakiki wa mikataba ya ununuzi wa umma leo Mjini Dodoma.

Alisema ni vyema wakatekeleza jukumu hilo kwa makini kwani ushauri unaotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia mawakili hao ndio msimamo wa Serikali.

“Ninapenda kuwakumbusha kwamba ninyi ni watumishi wa umma na mnaongozwa na Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 pamoja na kanuni zake za mwaka 2003” alisema Mhe. Masaju na kuongeza kuwa:

“Kama walivyo watumishi wengine wa umma na kwa msingi huu, ninyi ni sehemu ya Serikali na nafasi yenu katika Serikali ni kubwa”.

Pia aliwataka wanasheria wa Serikali kujengewa uwezo kuhusu uhakiki wa mikataba na iwapo watashindwa kutekeleza wajibu huo ipasavyo watawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua stahiki za kinidhamu.

Alisema kuwa kutokana na kuongezeka kwa thamani ya mikataba inayohakikiwa na wanasheria wa taasisi  ya manunuzi ni wazi kwamba kuna umuhimu wa Maafisa Sheria kupatiwa mafunzo hayo.
 
“Wanasheria wa Serikali wanaohakiki mikataba hii wanawajibika kuzingatia sheria zinazohusiana na mikataba husika pamoja na maadili ya Wanasheria wa Serikali katika Utumishi wa Umma kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 27 cha Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya mwaka 2005”,alisema Mhe. Masaju.
 
Mhe. Masaju alishauri utaratibu wa mikataba yote kuhakikiwa Dar es Salaam ubadilike kwani unasababisha ongezeko la gharama kwa taasisi za Serikali na kuchelewesha miradi.

Alifafanua kuwa Divisheni ya Mikataba iko Makao Makuu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pekee hivyo, mikataba yote ya mikoani ni lazima ipelekwe Dar es Salaam kwa ajili ya kuhakikiwa.

“Hii inasababisha wadau hasa wa kwenye Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa, Jiji na wengine walioko mikoani kusafiri na kupeleka mikataba Dar es Salaam kwa ajili ya uhakiki” alisema Mhe. Masaju.

Hivyo alisema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeona umuhimu wa kuwajengea uwezo Mawakili wa Serikali wa Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilizoko Mikoani ili hatimaye baadhi ya Mikataba kutoka kwa wadau walioko wilayani na mikoani iwe inapelekwa katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali zilizoko mikoani.

katibu Mkuu Ujenzi Afanya ziara ya Kushtukiza katika Mitambo ya Kupimia Mafuta.....Ataka Taarifa Ndani Ya Siku Mbili Uharibifu Wa Flow Meter Na Camera Bandarini

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi Dkt. Leornad Chamuriho ameupa siku mbili uongozi wa Bandari unaosimamia Mita ya Kupimia mafuta nchini (Flow Meter) iliyoko Kigamboni jijini Dar es salaam kuhakikisha kuwa unatoa taarifa ndani ya siku mbili kuhusu hitilafu iliyojitokeza kwenye mfumo wa kufungua valvu za mita hiyo upande wa umeme.

Aidha, ameuagiza uongozi huo kutoa taarifa kuhusu hitilafu ya kamera 2 za usalama zilizoungua na kushindwa kufanya kazi kwa takribani mwezi mzima.

Katibu Mkuu huyo ametoa maagizo hayo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika mita hiyo eneo la mji Mwema Kigamboni leo jijini Dar es salaam na kubaini upungufu wa utendaji wa baadhi ya maeneo.

Maeneo hayo ni pamoja na  kamera za kufuatilia mwenendo wa usalama wa mita hiyo, valvu zilizoshindwa kufanya  kazi upande wa mfumo wa umeme hivyo kubakiwa na njia ya analoji kutokana na hali ya mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha jijini Dar es salaam.

“Ifikapo Jumatatu nipatiwe taarifa kuhusu matengenezo ya vifaa hivi, hatua zilizochukuliwa na mnieleze lini ukarabati wake utakamilika pia ujenzi wa paa kuzuia athari ya mvua kwenye mita hii” amesema Dkt. Chamuriho.

Ameongeza kuwa dhumuni la Serikali ni kuhakikisha vifaa hivyo vinafanya kazi katika viwango vinavyostahili ili kulinda mapato yanayotokana na mafuta yanayoingia nchini ili Serikali ipate kodi halali na hivyo kuongeza mapato ya nchi na kuondoa malalamiko kwa wateja.

Kwa upande wake Meneja Mradi wa Ujenzi wa Mita hiyo  kutoka Mamlaka ya  Bandari nchini Mhandisi Mary Mhayaya ameeleza kuwa uharibifu wa vifaa hivyo umesababishwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na tayari vifaa hivyo vimeanza  kukabarati.

" Kisichofanya kazi ni mfumo wa kufungua mafuta upande wa umeme kwenye baadhi ya valve, upande wa analoji unafanya kazi vizuri na kazi ya upakuaji mafuta kupitia mfumo wa analojia inaendelea kama kawaida" Amesisitiza.

Amesema kuwa tayari wamemweleza mkandarasi aliyefunga vifaa hivyo kuvifanyia marekebisho haraka iwezekanavyo.

Naye Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Hebel Mhanga amesema kuwa ofisi yake inajukumu la kuhakikisha inatoa huduma sahihi kwa wateja wanaotumia mitambo hiyo iliyopo bandarini  hapo na Serikali inapata mapato kulingana na huduma iliyotolewa.

Mita ya Kupimia Mafuta yalnayoingia nchini iko katika hatua ya majaribio kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo tayari meli tatu zimefanyiwa majaribio ya upakuaji wa mafuta huku moja ikiwa imefanyiwa vipimo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya May 19

Zitto Kabwe, Halima Mdee na John Heche Wawekwa Kitimoto.....Wahojiwa Kwa Dadkia 90 Kwa Kufanya Fujo Bungeni

$
0
0
MBUNGE wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo) na wenzake wawili, jana wamehojiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika kwa kufanya fujo bungeni kuhusu suala la Bunge kutorushwa ‘live’.

Mbali na Zitto, wengine waliohojiwa ni pamoja na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema). Wabunge hao walihojiwa kwa tuhuma za kufanya fujo bungeni wakati ilipotolewa hoja ya Bunge kutorushwa moja kwa moja ‘live’, akiwa pamoja na wabunge wawili; Mdee na Heche.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya kamati hiyo, kimesema Zitto alihojiwa na kamati hiyo kwa muda wa zaidi ya saa moja kwa makosa mbalimbali, ikiwamo kufanya fujo bungeni Januari 27, mwaka huu.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Zitto alifanya fujo hizo baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, kuahirisha kujadili hoja ya serikali iliyowasilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kuhusu Bunge kutorushwa ‘live’.

Hatua hiyo inatokana na hoja iliyowasilishwa na Zitto aliyetaka kuahirishwa kujadili hotuba ya Rais kutokana na kauli ya Waziri Nape ya kutorushwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Zitto, alihojiwa na kamati hiyo ya Mkuchika kwa kilichoelezwa alisimama na kuomba mwongozo kuhusu jambo ambalo limekwishatolewa uamuzi kinyume na Kanuni ya 72 (1) na 68 (10 ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016.

Mbali na hilo pia anadaiwa kusimama na kuzungumza bila utaratibu kinyume na Kanuni ya 60 (2) na 12 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, jambo ambalo lilileta fujo na kuvunja shughuli za Bunge.

Katika barua za mwito zilizosainiwa na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, Mei 12, mwaka huu, inaelezwa kwamba pamoja na mambo mengine na Mwenyekiti wa Bunge kumsihi mbunge huyo bado aliendelea kuzungumza na kusimama ikiwa ni kuonesha dharau kwa mamlaka ya Spika na shughuli za Bunge kinyume na kifungu namba 24 (d) na (e) cha Sheria ya Kinga na Haki za Bunge.

Barua hiyo ilieleza kuwa kutokana na vitendo hivyo vinavyokiuka Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, Sura namba 296 na Kanuni za Bunge, wabunge hao walionywa kuwa endapo wasingefika mbele ya kamati hiyo jana hatua za kisheria zingechukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa kifungu cha 15 na 31 (1)(a) na sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge.

Magari Ya Washawasha Kugeuzwa ya Zimamoto

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Yusufu Hamad Masauni, amesema Serikali iko katika mchakato wa kuangalia uwezekano wa kubadili matumizi magari ya polisi ya kuzuia ghasia kwa kurusha maji ya kuwasha maarufu washawasha yaweze kutumika kuzima moto.

Kauli hiyo ilitokana na swali la nyongeza la Mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga aliyeuliza ni kwanini Serikali inanunua magari ya washawasha yasiyo na tija ambayo hutumika nyakati za uchaguzi tu badala ya kununua magari ya zimamoto.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Masauni alisema magari ya washawasha bado yana tija kwani Serikali inafanya taratibu ili magari hayo yatumike kuzima moto kwenye majanga na isiwe kwa washawasha pekee na kuwataka wabunge hasa wa upinzani kuondoa fikra za kuyapinga magari ya washawasha kwani sasa itakuwa ni neema kwao badala ya kutumika kwa kudhibiti vurugu pekee. 

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana Serikali ilinunua magari ya washawasha 777 kwa bei ya kati ya Sh150 milioni na Sh400 milioni, hata hivyo taarifa zingine zilisema magari yaliyotumika wakati wa uchaguzi ni 50.

Awali Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema), aliuliza swali la msingi kwamba ni lini Serikali itapeleka huduma ya zimamoto katika mpaka wa Tunduma ili kuokoa mali za wafanyabiashara wanaosubiri kuvuka pindi ajali ya moto inapotokea.

Naibu Waziri Masauni alisema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika halmashauri ya Mji wa Tunduma lina kituo katika eneo la mtaa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Momba katika Mkoa wa Songwe, kinachohudumia wilaya yote ukiwamo mpaka huo.

Alisema kwa sasa kituo hicho kina gari moja ambalo nalo liko kwenye matengenezo mjini Mbeya likiendelea kufanya matengenezo huku askari wakiendelea kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na majanga ya moto.

Masauni alisema ni azma ya Serikali kupeleka huduma ya zimamoto katika maeneo ya nchi ikiwamo Tunduma, mpango huo unategemea upatikanaji wa fedha kwa Serikali.

Kuhusu ujenzi wa kituo cha Polisi cha Mbozi, alimuomba mbunge wa eneo husika avute subira ili waweze kuona namna bora ya kufanya kwani bajeti ya Serikali ni ndogo na vituo vinavyotakiwa kujengwa ni vingi.

Mbunge wa CCM Anusurika Kupigwa na Wabunge wa UKAWA

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Jackline Msongozi juzi jioni alinusurika kipigo kutoka kwa wabunge wanawake wa UKAWA baada ya kuwaeleza kuwa upande huo una wabunge wawili tu wenye michango ya maana ambao ni Upendo Peneza (Viti Maalumu Chadema) na Magdalena Sakaya (Kaliua - CUF).

Akichangia mjadala wa bajeti kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Msongozi aliishambulia kambi ya upinzani akieleza kuwa kuna mlevi mmoja amechangia upande wa upinzani kuhusu uuzwaji wa nyumba za Serikali wakati waliohusika na uuzwaji huo wamehamia upinzani ambao ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Msongozi alisema hakuna mke mwenza anayeweza kumsifia mwenzake, hivyo upinzani hauwezi kuisifia CCM kutokana na kazi wanayoifanya.

Baada ya kusema maneno hayo na wabunge wengine kuchangia, Bunge lilipoahirishwa wabunge wanawake wa upinzani wakiongozwa na Sabrina Sungura na Ester Matiko walimfuata Msongozi wakitaka kumshambulia, lakini aliondoka moja kwa moja pasipo kusimama popote.

Sungura alipoulizwa alisema kuwa mbunge huyo angesimama wangemshughulikia.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Yapandisha Mshahara Kima cha chini Hadi 300,000/ Kutoka 150,000 Ya Hapo Awali

$
0
0

Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imetangaza bajeti ya Serikali hiyo ya Sh bilioni 841.5 kwa mwaka wa fedha 2016/2017; na kupandisha mshahara kwa kima cha chini kutoka Sh 150,000 hadi Sh 300,000.

Hatua hiyo imelenga kuongeza ufanisi na kupambana na ugumu wa maisha kwa wafanyakazi wake, kubana matumizi ya ndani na kuifanya nchi kuwa ya viwanda. 

Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk Khalid Salum Mohamed ndiye aliwasilisha bajeti hiyo katika Baraza la Wawakilishi mjini Zanzibar.

Alisema vipaumbele katika bajeti hiyo ni katika kuimarisha sekta ya elimu, afya na miundombinu ya bandari na uwanja wa ndege. 

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakadiria kutumia Sh bilioni 841.5 kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Kati ya fedha hizo, Sh bilioni 445.6 kwa kazi za kawaida na Sh bilioni 395.9 kwa kazi za maendeleo.

Alisema katika mwaka wa fedha 2016-2017 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ipo katika mchakato wa kukamilisha na kuanza kwa miradi miwili mikubwa ya miundombinu, ambayo ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume katika jengo la abiria.

Aidha alisema ujenzi wa bandari ya kisasa ya Mpigaduri, utasaidia kuongeza mapato na ajira kwa wananchi wa Zanzibar mara utakapomalizika. 

Dk Salum alisema bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 inakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwamo kupungua kwa fedha kutoka kwa washiriki wa maendeleo; na ndiyo maana bajeti hiyo itajikita zaidi katika kuweka kipaumbele cha makusanyo ya kodi ya ndani.

“Tumeweka kipaumbele zaidi katika makusanyo ya kodi kupitia vyanzo vyake, ambapo taasisi za ukusanyaji kodi Mamlaka ya Mapato (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) tumezipa majukumu makubwa zaidi katika makusanyo ya kodi,” alisema Dk Salum.

Alifahamisha kwamba TRA inatarajiwa kukusanya Sh bilioni 188.8, wakati ZRB itakusanya Sh bilioni 237.4. Waziri huyo alisema muelekeo wa uchumi wa Zanzibar ni kufikia uchumi wa kati na usipungue asilimia nane kwa mwaka na kuifanya nchi kuwa ya viwanda.

Alisema SMZ imelenga Zanzibar kuwa nchi ya viwanda katika sekta ya kilimo na uvuvi na kuimarisha sekta ya utalii.

 Aidha, alisema serikali imesikia kilio cha kupungiza kodi ya mishahara ya wafanyakazi zaidi kipato cha chini, ambapo sasa kitapunguzwa kutoka asilimia 13 hadi 9. 

Salum alitangaza kwamba katika bajeti ya fedha kwa mwaka 2016-2017, hakutakuwa na ongezeko la kodi kwa lengo la kupunguza mzigo kwa wananchi.

Edward Lowassa na Fredrick Sumaye Watajwa Katika Sakata la Uuzwaji wa Nyumba za Serikali.......Mbowe Atoa Ufafanuzi

$
0
0
Uuzwaji wa nyumba za serikali umegeuka mwiba huku wabunge wakiendelea kuhoji hatua zilizochukuliwa kutokana na kadhia hiyo

Hatua hiyo iliyotekelezwa mwaka 2002  hadi 2004 ilizusha malalamiko mengi tangu wakati huo na sasa imeibuka tena bungeni

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano jana, mbunge wa Nachingwea, Hassani Masala (CCM) alihoji mfumo uliotumika kuuza nyumba za serikali

Alisema haungi mkono kwa vile umesababisha viongozi wapya wa serikali wanaoteuliwa kujikuta wakiishi katika nyumba za wageni.

Mjadala huo uliibuliwa juzi na msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni kupitia kwa waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless Lema kabla ya Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu kumtaka kuondoa baadhi ya maneno katika hotuba yake likiweo suala la uuzwaji wa nyumba za serikali.

 Ritha Kabati Amvaa Lowassa
Akichangia mjadala huo jana, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ritha Kabati alimtaja aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kuwa alinunua nyumba ya serikali iliyouzwa mwaka 2002 yenye jengo namba 68.

Alisema hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilisema nyumba za serikali 7,921 ziliuzwa tangu mwaka 2002 hadi 2004 na kutaka serikali ya awamu ya tano kurejesha nyumba hizo kutokana na walionunua kukiuka mikataba na malengo ya mauzo.

“Naomba niwaambie usiangalie boriti lililo katika jicho la mwenzako wakati kwako lipo, kwani hata mgombea wao wa urais Edward Lowassa alihusika kwa kununua nyumba ya plot namba 68 na Fredrick Sumaye alikuwa Waziri Mkuu na kuhusika kuuza nyumba hizo,” alisema Kabati.

Baada ya kueleza hayo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliomba kumpa taarifa mbunge huyo kuwa taarifa hiyo ni kwa maslahi ya taifa, hata kama mhusika atakuwa katokea kambi ya upinzani sheria itachukua hatua.

"Kambi ya upinzani tunapoibua jambo huwa linakuwa kwa maslahi ya Taifa, hivyo ni vyema wabunge wote mtambue kuwa kosa likifanywa na kiongozi  ni lazima hatua zichukuliwe bila kujali ni wa Chadema, CUF au CCM.

"Tunapokuwa tunatoa uamuzi kama kambi ina maana sheria ifuate mkondo wake." Alisema Mbowe huku akishangiliwa na wabunge wa UKAWA

Awali katika michango mbalimbali ya wabunge wa upinzani wamekuwa wakilalamikia kuuzwa nyumba hizo za serikali na kudai kuwa watumishi wapya wengi walioajiriwa, wamekuwa wakikosa maeneo ya kuishi.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) akichangia mjadala huo alilalamikia kuuzwa kwa nyumba hizo pamoja na nyingine za Tazara zipatazo 500 na kuamua kumpatia Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ripoti aliyodai inaonesha nyumba hizo zilivyouzwa.

Sakata la Lugumi: CHADEMA Yajipanga Kumng'oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema uzito wa Rais John Magufuli kumwajibisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kutokana na kutajwa kuhusika na Kampuni ya Lugumi inayodaiwa kulitapeli Jeshi la Polisi, utasababisha waanze harakati za kumng’oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Rais John Magufuli hana budi kuchukua hatua haraka kumwajibisha Waziri Kitwanga kama alivyofanya kwa watumishi wengine wa umma katika operesheni ya kutumbua majipu.

Waziri Kitwanga anadaiwa kuwa na hisa kwenye Kampuni ya Infosys Ips Tanzania Limited ambayo ilipewa zabuni ya kutoa huduma za kitaalamu na Kampuni ya Kimarekani ya Biometrica kuhusu uwekaji wa mashine za kielektroniki za kuchukua alama za vidole kwenye vituo 108 vya polisi. 

Mkataba wa kuweka mashine hizo uliingiwa kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises ambayo ililipwa Sh34 bilioni kati ya Sh37 bilioni za mkataba, wakati kazi ya kufunga mashine hizo ilifanyika kwenye vituo 14 tu hadi wakati Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipofanya ukaguzi.

Hata hivyo, kampuni hiyo inadai kuwa Kitwanga, ambaye ni mmoja wa waasisi wa Infosys, alijiondoa kwenye uendeshaji tangu mwaka 2010, wakati mkataba huo ulisainiwa mwaka 2011.

Chadema bado inaona kuwa Rais Magufuli anatakiwa kumwajibisha waziri huyo wa Mambo ya Ndani.

“Kama Rais akishindwa kuchukua hatua katika hili, Serikali itang’oka madarakani. Sisi Chadema tutaiondoa. Haiwezekani wakati Lugumi inachunguzwa mhusika mkuu (Kitwanga) aendelee kuwa waziri, tena wa wizara inayohusika na mkataba wa Lugumi,” alisema Mwalimu.

Mwalimu alisema, Rais anapaswa kujitokeza hadharani na kueleza uhusiano wake na Kitwanga na awaeleze Watanzania kuwa kutokana na uswahiba wao ndiyo sababu ya kutomchukulia hatua.

“Mbona anawatumbua marafiki wa wenzake? Kwa nini marafiki zake anashindwa kuwatumbua? Ukiwa kiongozi mwenye kubagua katika uamuzi ni hatari kwa uchumi wa Taifa, ni sawa na baba anayewabagua watoto wake matokeo yake ni kuzalisha chuki tu.”

Licha ya Mwalimu kutotaka kuweka wazi mpango huo, kwa mujibu wa Ibara ya 53 A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo.

 Kwa mujibu wa Ibara hiyo, hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu inapaswa kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote.

Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni 372, kati yao wabunge wa upinzani ni 118.

“Hilo tutalifanya iwapo tu Rais atashindwa kumwajibisha Kitwanga. Ila huyu waziri naye anapaswa ajipime mwenyewe ili kumlinda bosi wake (Waziri Mkuu). Afanye kama Edward (Lowassa-waziri mkuu mstaafu) aliamua kujiuzulu wadhifa wake ili kumlinda Jakaya (Kikwete-Rais wa Awamu ya Nne) kwa kosa ambalo yeye hakulifanya,” alidai Mwalimu.

Mwalimu alidai kwamba Serikali imezuia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge kuhofia uchafu wa viongozi, likiwamo sakata la Lugumi.

“Ndiyo maana tunasema CCM ni ileile maana wametumbua majipu, sasa imebaki mitoki. Ni kama imewashinda maana ipo sehemu mbaya,” alisema.

Licha ya mkakati huo wa Chadema, Aprili 19 mwaka huu, Kitwanga alisema kuwa hahusiki katika sakata hilo na juzi alijibu hoja ya Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) lililomtaka ajiuzulu, akisema hawezi kuwajibu watoto ili kuonyesha tofauti yake na wao.

Katika maelezo yake, Mwalimu aliorodhesha utumbuaji ambao Rais Magufuli ameufanya tangu aingie madarakani, ukiwamo wa watendaji waliofanya vurugu tu katika vikao kwa kusisitiza kuwa ni ajabu kuona mpaka sasa hajamchukulia hatua yoyote Kitwanga wakati ukweli uko wazi kuwa anahusika na sakata la Lugumi. 

Baada ya ripoti ya CAG kuibua udhaifu huo kwenye mkataba, Kamati ya Hesabu za Serikali ya Bunge iliunda kamati ndogo kufuatilia tuhuma hizo baada ya kutoridhishwa na maelezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kuhusu mkataba huo.

Kampuni ya Infosys ni wakala wa kampuni maarufu duniani ya kutengeneza kompyuta ya Dell, ikijihusisha na usambazaji wa vifaa hivyo, matengeneza na utoaji huduma za kitaalamu.

Kaimu katibu mkuu huyo wa Chadema alisema, chama hicho pia kinajipanga kuanza ziara yake nchi nzima na ajenda kuu itakuwa kuanika mambo yote mabaya yanayofanywa na Serikali.

Ali Kiba Asaini Mkataba na Kampuni kubwa ya Muziki duniani ya Sony jijini Johannesburg, Afrika Kusini

$
0
0
Mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba leo amesaini mkataba na  Sony Music , kampuni kubwa ya muziki inayofanya kazi na mastaa wa dunia kama Beyonce, John Legend na Chris Brown.

Moja ya kazi za mkataba huo ni kumtengeneza Alikiba kweye kiwango cha juu zaidi kimuziki, kibiashara na kugharamia video zake na anaporekodi audio zake, kila anapotoa muziki mpya unaachiwa kwa nguvu ya usimamizi wa Sony Music kwenye masoko makubwa ya muziki kama Marekani, Ulaya na Africa.

Mkataba  huo aliosaini Ali kiba unafanana  na ule aliosaini mwimbaji staa wa Nigeria Davido ambapo unavipengele vya kusababisha kolabo kwa urahisi zaidi na mastaa wakubwa wakiwemo wa Marekani.

Rais Magufuli Akutana Na Mabalozi Mbalimbali Pamoja Na Katibu Mtendaji Wa SADC Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke wakati wa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke akimkabidhi Kitabu kinachohusu masuala mbalimbali ya Ujerumani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Ikulu Balozi wa Uturuki hapa nchini Yasemin Aralp aliyefika kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Denmark hapa nchini Eina Hebogrd Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Denmark hapa nchini Eina Hebogrd mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax Ikulu jijini Dar es Salaam. Dkt. Stergomena alifika Ikulu kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax pamoja na Maafisa wengine kutoka Ikulu na  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Ndugu Egon Kochanke pamoja na ujumbe wake. Wengine katika picha ni Maafisa mbalimbali kutoka Ikulu.

Picha na IKULU

Basi la Mwendo Kasi Lagonga na Kuua Mtoto Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Basi la mwendo kasi ( DART)  limemgonga na kumuua mtoto huku mama yake akinusurika baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kushindwa kulipita basi hilo

Ajali hiyo imetoke leo katik eneo la Shekilango jijini Dar es Sallam.
Pikipiki iliyohusika kwenye ajali hiyo

Atiwa Mbaroni Kwa Kumbaka Mtoto wa Miaka 7

$
0
0

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia mkazi wa eneo la Bombambili, Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kukutwa akimbaka mtoto wa miaka saba anayesoma darasa la pili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuber Mwombeji alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Mei 18 mwaka huu saa 11 jioni nyumbani kwao na mtoto huyo.

Alifafanua kuwa siku ya tukio mkazi huyo alikwenda sehemu hiyo kuangalia runinga sebuleni na baada ya muda mfupi binti huyo alirejea nyumbani akitokea shule.

“Msichana huyo alikuja sebuleni kuangalia runinga wakati huo wafanyakazi wa ndani wa nyumba hiyo walikuwa nje na ndipo kijana alipopata mwanya wa kufanya ukatili huo,” alisema kamanda.

Alisema baada ya muda mfupi kupita, mfanyakazi wa kike aliingia sebuleni ghafla na kumkuta akimbaka mtoto huyo.

Alifunga mlango, kisha aliwaita majirani na viongozi wa Serikali wa mtaa huo.

Kamanda alisema wananchi walimkamata mtuhumiwa na kumpeleka polisi. Pia, mtoto huyo alichunguzwa na madaktari walithibitisha kuwa aliingiliwa kimwili na kuharibiwa sehemu zake za siri.

Uhakiki watumishi HEWA Manispaa Moshi waanza upya

$
0
0

Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Jeshi Lupembe, ameanza upya uhakiki wa watumishi wote walio chini ya halmashauri hiyo wapatao 2,427.

Uhakiki huo ambao tayari umefanyika kwenye kata 12 kati ya 21 za manispaa hiyo, umetokana na kubaini uwepo wa watumishi hewa 19 katika uhakiki wa awali ulioagizwa na Rais John Magufuli na kuwezesha kuokoa Sh milioni 33.5.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa watumishi hewa 19 waliobainika awali, tayari wahusika wameandikiwa barua za kurejesha fedha zote kabla ya Mei 30, mwaka huu na baadhi yao wameanza kulipa.

Lupembe alisema ameona ni jambo la busara kufanya uhakiki wa watumishi wote walio chini ya halmashauri hiyo, kwa lengo la kujiridhisha kama watumishi wote wana nyaraka sahihi za ajira, ikiwa ni pamoja na kubaini ambao walipaswa kupandishwa vyeo lakini bado. 

Alisema hadi kufikia Mei 16 tayari watumishi 907 walikuwa wamehakikiwa na matarajio ni kuhakiki watumishi wote 2,427.

Daktari Kortini Akituhumiwa Kusababisha kifo cha Mtoto

$
0
0

Daktari Msaidizi wa Zahanati ya Rwamchanga, Miriam Martine amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kujibu mashtaka ya kusababisha kifo cha mtoto mchanga na kushindwa kumzalisha mama yake.

Akimsomea mashtaka juzi mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Emmanuel Ngaile, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Paschael Nkenyenge alidai kuwa Mei 15, katika zahanati hiyo, mshtakiwa huyo alishindwa kumzalisha mama huyo, Mugesi Juma kwa uzembe na kusababisha mtoto huyo ambaye ni pacha kufa.

Mshtakiwa huyo alikana shtaka na kupatiwa dhamana ya Sh5 milioni za maneno baada ya wadhamini wawili kukidhi masharti yaliyowekwa na mahakama hiyo, ikiwamo mmoja kuwa mtumishi wa umma. Kesi hiyo namba 85/2016, iliahirishwa hadi Mei 27, itakapotajwa tena.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Naomi Nnko alimsimamisha kazi daktari huyo siku moja baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Wakati huohuo; Mwalimu wa kujitolea wa Shule ya Sekondari Nagusi wilayani Serengeti, Fikiri Bunduki Mochemba (22) mkazi wa Kijiji cha Singisi amefikishwa mahakamani hapo kujibu shtaka la kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili (17) shuleni hapo.

Mshtakiwa alikana shtaka na kurudishwa rumande hadi Juni mosi.

Waziri Mkuu: Wanafunzi Wote Nchini Watakalia Madawati

$
0
0

Serikali imewahakikishia Watanzania kuwa inaendelea kuweka utaratibu kuongeza madawati na miundombinu ya vyumba vya madarasa nchini, kuhakikisha wanafunzi wote wanaokaa chini na kurundikana madarasani, wanapata madawati na vyumba vya kutosha.

Lakini, imesema hawawazuii wadau mbalimbali ikiwamo watanzania, kuchangia katika kuongeza miundombinu hiyo huku wabunge wakipongezwa kwa kuunga mkono serikali kwa kuchangia madawati.

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa alisema hayo bungeni jana wakati akijibu maswali ya papo na hapo na kueleza kuwa ni jukumu la serikali kumaliza mirundikano hiyo na watafanyia kazi.

Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Mahawe (CCM) aliyetaka kujua baadhi ya wananchi wanaodaiwa kulipa kodi mara mbili na kutofaidika na sera ya elimu bure.

Akijibu swali hilo, Majaliwa alisema suala la elimu bure limekuwa likichanganywa na wakati mwingine kupotoshwa.

Alisema elimu bure ni mkakati unaolenga katika elimu ya msingi na sekondari kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wazazi kwa kupunguza michango iliyokuwa inawakwaza .

Alisema wameanza na maeneo ambayo wameondoa ada kwa sekondari Sh 20,000 hadi 70,000, ulinzi, maji umeme na mitihani kwa kutenga fungu kuipa shule kulipia ili wazazi wasipate mzigo wa michango na wanaendelea kuangalia maeneo mengine wanayochangia ili kuwapunguzia mzigo.

Bomba la Mafuta Kutoka Uganda Kuongeza Ajira

$
0
0
Serikali  imetaja manufaa ya mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania kuwa miongoni ni kuongezeka kwa uwekezaji wa fedha za kigeni na fursa za ajira.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliliambia Bunge jana kuwa Aprili mwaka huu, Tanzania ilisaini Makubaliano ya Awali (MoU) na Serikali ya Uganda kwa ajili ya ujenzi wa bomba hilo kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Alisema bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,443 ambazo kati ya hizo, kilometa 1,115 zitakuwa upande wa Tanzania.

“Bomba hilo litakuwa na uwezo wa kusafirisha mapipa 200,000 ya mafuta ghafi kwa siku,” alisema Profesa Muhongo akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2016/17 yanayofikia Sh 1,122,583,517,000.

Aliyataja manufaa ya bomba hilo kwa Tanzania kuwa ni kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato kupitia Bandari ya Tanga, tozo ya kupitisha mafuta ghafi kwenye bomba na ajira za kudumu kwa Watanzania 1,000 na 10,000 za muda.

Alisema majadiliano ya utekelezaji wa mradi huo kati ya Serikali za Tanzania, Uganda, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) pamoja na kampuni za Total (Ufaransa), CNOOC (China) na Tullow (Uingereza) yameanza.

Alisema katika kuimarisha ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Serikali ya Uganda imealika nchi za Burundi, Kenya, Rwanda na Tanzania kushiriki katika uwekezaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi nchini Uganda.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images