Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

LHRC Yaonya Kuhusu Picha za Uchi na za Kutisha

$
0
0
Kituo  cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeonya vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu kuchapisha picha za utupu ama za kutisha katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam , Mkurungenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dk. Helen Kijo Bisimba alisema kuwa, kumekuwa na matukio kadha yanayofanywa na watu juu ya kurekodi na kupiga picha ambazo sio nzuri kwa mujibu wa sheria.

Alibainisha picha hizo kuwa ni pamoja na matukio ya mauaji, ajali za kutisha na miili ya marehemu zinazochapichwa katika mutandao ya kijamii, blog na hata baadhi ya vyombo vya habari bila kijali kwamba, kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Dk. Kijo alisema kuwa, tarehe 4 Mei mwaka huu katika Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Bagamoyo picha za miili ya marehemu (mama na mtoto) ambayo majina yao yamehifaziwa, zilisambazwa katika mitandao ya kijamii zikionesha majeraha ya kutisha   kutokana na kitendo cha kinyama kilichofanywa.

Katika tukio la pili alibainisha kuwa, ilitokea Mkoa wa Kilimanjaro mwaka huu ambapo picha za maiti ya mtoto aliyeuawa na mama wa kambo zilionesha akiwa ndani ya jeneza.

Katika maeneo ya Kibamba Jijini Dar es Salaam, Januari mwaka huu picha za utupu za mwanamke aliyesemekana kuwa ni msukule aliyekutwa kwenya kisima zilizambazwa katika mitandao ya kijamii.

Alisema kuwa, hayo ni baadhi ya matukio hivyo jamii inapaswa kutambua kuwa vitendo hivyo ni udhalilishaji na kinyume cha sheria.

“Kwani kwa mujibu wa haki ya kikatiba ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kila mtu ana haki ya kikatiba ya kuthamini utu wake kuwa faragha akiwa hai au amefariki,” alisema.

Mapato Hospitalini Yanuka Ufisadi.....Vifaa vya Kielektroniki Vya Kuyakusanya Vyaiduwaza Serikali

$
0
0
Ufungaji  wa vifaa vya kielektroniki katika hospitali za Serikali katika mikoa mbalimbali, umeibua fukuto la ufisadi mkubwa, uliokuwa ukifanywa katika makusanyo ya fedha wanazolipa wagonjwa kwa ajili ya huduma.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, alisema tangu mfumo huo wa kielektroniki uanze kutumika katika hospitali nyingi nchini, mapato yameongezeka.

Jafo alisema mafanikio hayo ya ukusanyaji wa mapato kwa mfumo wa elektroniki, yamesababisha katika sekta ya afya kwa sasa ajenda kuu iwe kuongezea mapato ya hospitali zote nchini, kuendane na utoaji wa huduma bora.

Hospitali ya Rufaa Mbeya 
Akitoa mfano wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Jafo alisema kabla ya kufungwa kwa vifaa hivyo, ilikuwa ikikusanya Sh milioni 70 kwa mwezi, lakini baada ya kufungwa vifaa hivyo, mapato yameongezeka zaidi ya mara saba na kufikia Sh milioni 500 kwa mwezi.

Taarifa zinaonesha pamoja na ongezeko hilo la mapato, bado hospitali hiyo iliendelea kukosa vifaa muhimu vya tiba, ikiwemo mashine ya CT-Scan, kiasi cha kusababisha mwanzoni mwa mwaka huu Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla kuwajia juu watendaji wake.

Dk Kigwangalla alielezea kushangazwa kuona hospitali hiyo ikikusanya Sh milioni 500 kwa mwezi, huku ikidai kukosa CT-Scan na kutoa siku 60 kifaa hicho kifungwe.

Katika maelezo aliyopewa, Dk Kigwangalla alielezwa kuwa ingawa ni kweli hospitali hiyo inakusanya Sh milioni 500 kwa mwezi, lakini mahitaji ya dawa pekee yanachukua zaidi ya Sh milioni 300, kabla ya gharama nyingine ikiwemo za usafiri wa magari.

Alielezwa kuwa hospitali hiyo imejipanga kuchukua mkopo kutoka Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF), kwa kuwa ili kupata mashine hiyo, wanapaswa kuwa na kuanzia Sh milioni 800 mpaka Sh bilioni 1.2.

Sekou Toure 
Mbali na Mbeya, katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure kwa mujibu wa Jafo, kabla ya kufungwa kwa vifaa hivyo, ilikuwa ikikusanya kati ya Sh 150,000 mpaka 200,000 tu kwa siku.

Jafo alisema baada ya kufungwa vifaa hivyo, mapato hayo yaliongezeka mpaka karibu mara 21 na kufikia Sh milioni 3.2 kwa kila siku. 

Hospitali ya Tumbi 
Mbali na Mwanza, Naibu Waziri huyo wa Tamisemi, alisema mkoani Pwani katika Hospitali ya Tumbi, nako kabla kufungwa vifaa hivyo, makusanyo yalikuwa Sh 200,000 kwa siku lakini baada ya kufungwa, mapato yakaongezeka mara 20 na kufikia Sh milioni nne kwa siku.

Kutokana na mafanikio ya hospitali hizo, Jafo aliwataka wabunge wote kufuatilia kwa makini hospitali katika halmashauri zao za wilaya, ili kila moja iweke mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kukusanya mapato katika huduma ya afya.

Aliwataka wabunge hao kuweka kipaumbele katika kuhakikisha hospitali zote katika maeneo yao, zinafungwa mifumo hiyo ya kielektroniki, ili fedha zikusanywe kusaidia katika kuboresha huduma za afya katika maeneo hayo.

“Tusipozingatia haya, hata tukipeleka fedha bado tutakuwa na matatizo, ndio maana ajenda yetu kuu ni kutumia mifumo ya kielektroniki, ili kuongeza mapato katika sekta ya afya,” alisisitiza.

Awali Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi (CCM), alitaka kufahamu kama Serikali haioni umuhimu wa kuiongezea fedha Hospitali ya Mji wa Mafinga, ili ihudumie kwa ufanisi idadi kubwa ya wagonjwa wanaohudhuria hospitali hiyo.

Pia Mbunge huyo alitaka kufahamu kama Serikali iko tayari kuiongezea hospitali hiyo watumishi mara mbili zaidi ya kiwango inachopata, ili iwe na uwezo wa kutosha kukabiliana na mzigo wa kazi.

Akijibu maswali ya mbunge huyo, Jafo alisema Serikali imekuwa ikiipatia Hospitali ya Mji wa Mafinga Sh milioni 90 kwa ajili ya maendeleo na Sh milioni 90 kwa matumizi mengineyo ; na kwamba inaweza kuongezewa fedha hizo kulingana na wigo wa upatikanaji wa fedha.

Kuhusu watumishi, alisema hospitali hiyo ina watumishi 209 na upungufu uliopo ni wa watumishi 95, sawa na asilimia 31.3 na kwa mwaka wa fedha 2016/17 imeidhinishiwa kuajiri watumishi 18.

Serikali Yasitisha Kwa Muda Ajira Zote za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

$
0
0

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesitisha kwa muda ajira zote kwenye vyombo vya ulinzi na usalama vilivyomo ndani ya wizara hiyo, ikiwemo Jeshi la Polisi ili kupitia upya utaratibu wa kutoa ajira na kuondoa uwezekano wa watu wasio na sifa kujipenyeza.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alisema hayo jana bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (Chadema), aliyetaka kufahamu ni kwa nini Serikali inasitisha ajira katika Jeshi la Polisi, wakati bado nchi inakabiliwa na uhaba wa askari ndani ya jeshi hilo wakiwemo askari wa kike.

“Tumesitisha kutoa ajira ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ili kuondoa uwezekano wa watu wasio na sifa kujipenyeza na kupata ajira ndani ya vyombo vilivyo chini ya wizara hiyo,” alisisitiza.

Miongoni mwa vyombo hivyo vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mbali na Jeshi la Polisi ni Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uhamiaji. 

Mbali na Komu, Mbunge mwingine ambaye ni wa Viti Maalumu, Hawa Mwaifunga (Chadema), alitaka kufahamu Serikali inachukua hatua gani kuhakikisha askari wasio na sifa wanachukuliwa hatua, ambapo pia alitaka kufahamu utaratibu wa uhakiki vyeti vya askari wasio na sifa ndani ya Jeshi la Polisi umefikia wapi.

Akizungumzia Jeshi la Polisi, Masauni alisema Jeshi la Polisi limo kwenye utaratibu wa kuwachukulia hatua za kisheria askari wachache, wanaochafua taswira na kazi nzuri inayofanywa na Polisi kwa kukiuka sheria, kanuni na taratibu kwa kujihusisha na vitendo vinavyokinzana na maadili.

Kuhusu uhakiki wa vyeti, waziri huyo alielezea kuwa, uhakiki huo unahusu askari wasio na sifa ndani ya Jeshi la Polisi unaendelea na mpaka sasa, askari 19 wamechukuliwa hatua za kisheria baada ya kugundulika kuwa walipata ajira kwa njia zisizokubalika.

Kuhusu uhaba wa askari wa kike, Waziri huyo alikiri kuwa kuna uhaba wa askari wa kike katika Jeshi la Polisi na kutoa mwito kwa wanawake wahamasike zaidi kujiunga na vyombo vya usalama.

Mwaka jana Idara ya Uhamiaji iliyokuwa chini ya Wizara hiyo, ililazimika kufuta ajira mpya 200 za makonstebo na makoplo, baada ya kubaini upatikanaji wa ajira hizo, ulifanyika kwa upendeleo.

Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 30 Jela Kwa Kumuoa Bunti Yake wa Kumzaa

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, jana ilimhukumu kifungo cha miaka 30, Godfrey Mjelwa (48), baada ya kupatikana na hatia ya kuishi kinyumba na binti yake wa kumzaa.

Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo, Mwajuma Lukindo alisema ushahidi wa pande zote ulithibitisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kuishi chumba kimoja na binti yake, kama mke na mume.

Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, Mjelwa aliamua binti yake mwenye umri wa miaka 15 (jina limehifadhiwa) kuwa mke na kuishi naye katika Mtaa wa Kizota Manispaa ya Dodoma. 

Hakimu Lukindo alisema kosa alilokutwa nalo mtuhumiwa ni ‘maharimu’ (kufanya mapenzi na ndugu za damu), licha ya kuwa mtoto huyo bado alikuwa mdogo, lakini ni mtoto wake wa kumzaa.

Mwendesha mashtaka Janeth Mgome, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa, ili liwe fundisho kwa wengine ambao wana tabia ya aina hiyo. 

Utetezi wa mtuhumiwa huyo uliwavunja mbavu watu waliokuwapo mahakamani hapo, kwani alitaka kupunguziwa adhabu kwa kuwa mtoto wake ana miaka 14 na miezi tisa na siku tisa, siyo miaka 15 kama ilivyodaiwa mahakamani hapo.

Waziri Mkuu: Tanzania Kushirikiana Na Jumuiya Ya Madola

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Jumuiya ya Madola inaweza kuiga mbinu ambazo Tanzania imetumia katika kupambana na rushwa zikiwemo za kujumuisha wadau tofauti kwenye vita hiyo.

Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Bibi Patricia Scotland walipokutana kwenye mkutano wa kimataifa uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

“Tanzania iko tayari kushirikiana na ninyi katika kujenga timu hii na ili uweze kupata picha halisi, nakukaribisha Tanzania uje ujionee hatua ambazo tumechukua hadi kufikia hapa tulipo kwenye vita hii dhidi ya rushwa,” alisema Waziri Mkuu ambaye alihudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Alimweleza Katibu Mkuu huyo kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kupambana na rushwa kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwa wananchi. 

“Wananchi wanafurahia juhudi za Serikali, vyama vya kiraia pia vinaunga mkono jitihada zetu na vyombo vya habari vinashirikiana nasi katika vita hii,” alisema.

Waziri Mkuu alitoa wito huo baada ya kuelezwa na Bibi Scotland kwamba anataka kuanzisha idara malum kwenye Jumuiya hiyo ambayo itasimamia mapambano dhidi ya rushwa na makosa ya jinai.

“Nataka tuwe na idara yenye watu mahiri wa idara za uhasibu, mahakama yenyewe ikiwemo waendesha mashtaka na wanasheria kutoka kwenye nchi kadhaa ili washirikishane uzoefu kutoka kwenye nchi zao. Ninaamini katika nchi 53 ambazo ni wanachama wetu, sitakosa watu wa aina hii,” alisema.

Alisema ameamua kufanya hivyo ili aweze kuendanana na malengo makuu matatu ya jumuiya hiyo ambayo ni kupiga vita rushwa, kuhimiza utawala bora na usimamizi wa demokrasia.

IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU

JUMAMOSI, MEI 14, 2016.

Mapambano Ya Rushwa Yanahitaji Juhudi Za Pamoja- Waziri Mkuu

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mkutano wa kimataifa uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani ni kiashiria tosha kwamba tatizo la rushwa ni kubwa sana na linataka juhudi za pamoja katika kukabiliana nalo. (It’s a serious graft that needs concerted efforts).

Ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Waziri wa Nchi wa Uingereza anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa, Bibi Justine Greening walipokutana kwenye mkutano huo uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

Waziri Mkuu ambaye alihudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, alimweleza Bibi Greening kwamba viongozi wa Serikali wa awamu ya tano wameamua kwa dhati kupambana na kila ovu linalotokana na janga la rushwa na pia wameamua kuwajibika na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.

“Sasa hivi nchi yetu ina utamaduni mpya wa kufanya kazi na tumeamua kufanya kazi kwelikweli na siyo tena kwa mazoea, tumeamua kuweka utamaduni mpya wa kupiga vita rushwa ili kuleta uwajibikaji na uwazi miongozi mwa watu wetu,” alisema.

Alipoulizwa ni kitu kimechangia kufanya Tanzania ing’are kimataifa katika vita hii, Waziri Mkuu alijibu kwamba Tanzania imetumia mambo manne ambayo ni kuzuia rushwa isitolewe ama kupokelewa (prevention), kampeni za kuelimisha jamii, kufanya mapitio ya sheria na kuwepo kwa utashi wa kisiasa.

“Serikali inachukua hatua za kiutawala na kisheria kama vile kuanzisha mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi mwezi Julai mwaka huu,” alisema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, Bibi Greening alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kupambana na rushwa na kwamba ndiyo maana Tanzania ilipewa mwaliko maalum wa kushiriki mkutano huo kwa vile baadhi ya mataifa yanaziona juhudi zinazofanywa na Serikali.

Pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu kwa nia ambayo Serikali ya awamu ya tano imeionyesha katika kuwa na mpango wa kuendeleza viwanda.

Pia alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania kwenye mpango wake ilionao wa kupeleka umeme vijijini (Rural Electrification Programe). 

“Tuko tayari kuwasiidia kutekeleza mpango huu kupitia taasisi ya Energy Africa Initiative ambayo inapata ufadhili kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID),” alisema.

Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya kimataifa, Bibi Sarah Sewall ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika mapambano dhidi ya rushwa na kusisitiza kwamba makampuni mengi ya Marekani yana nia ya kuja kuwekeza Tanzania.

“Ninaamini uwekezahji huu utasaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watu wetu. Tunampongeza Rais Dk. Magufuli kwa juhudi anazofanya na nipende kusisitiza kwamba ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani utaendelezwa katika maeneo yetu ya siku zote,” alisema.

Waziri Mkuu alimshukuru Bibi Sewall na kumsisitiza asiache kusaidia kuwahimiza wamarekani wengi waje kutalii Tanzania na wawekezaji zaidi waje kuwekeza nchini katika nyanja mbalimbali zikiwemo uanzishaji wa viwanda, uongezaji thamani kwenye mazao yanayozalishwa nchini na kuhakiksha kuwa Watanzania wanajifunza teknolojia mpya na za kisasa.

IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU

JUMAMOSI, MEI 14, 2016.

Lady Jaydee Amtaka Gardner Aombe Radhi Ndani ya Siku 7

$
0
0

Msanii wa muziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kupitia mwanasheria wake Aman G. Tenga kutoka Law Associates (Advocate) ameandika barua ya kumtaka mtangazaji maarufu wa Clouds Fm, Gardner G. Habash, kuomba msamaha mbele ya umma kutokana na kauli yake ya uzalilishaji aliyoitoa dhidi yake.

Gardner ambaye alikuwa mume wa muimbaji huyo wa Ndindindi, anatuhumiwa kulifanya kosa hilo mnamo tarehe 6 May 2016, akiwa kama mshereheshaji tamasha la Miss TIA 2016 lililofanyika CDS Park (zamani TCC) ambapo alidaiwa kutamka kwa makusudi maneno ya udhalilishaji na kejeli “Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi” mbele ya umma.

Baada ya wiki moja toka tukio hilo litokea, Lady Jaydee kupitia mwanasheria wake ameandika barua hii.
 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya May 15


Safari Ya Mwisho Ya Mtoto Wa Issa Michuzi Maggid Muhidini Michuzi

$
0
0
Baba wa marehemu (mwenye kofia), Issa Michuzi akipewa pole na baadhi waombolezaji mara baada ya maziko ya mtoto wake Maggid Muhidin Michuzi (18) yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana.

Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Sinde Warioba akimpa pole Issa Michuzi.
Rais Mstaa mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akiagana na Issa Michuzi.
Issa Michuzi (mwenye kofia) akifuatiwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete (kulia kwake) na viongozi wengine wa serikali wakati maziko.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi akiweka udongo
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na baba wa marehemu.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Awakemea Wafanyabiashara wa Sukari Wanaompigia Simu Usiku Kutaka Kumpooza

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amefichua kuwa amekuwa akipigiwa simu na baadhi ya wafanyabiashara vigogo wenye nia ya kutaka kupunguza makali ya operesheni inayofanywa na wilaya yake dhidi ya waficha sukari.

Kwamba simu hizo amekuwa akipigiwa hadi usiku wa manane na huku wengine wakimtumia ujumbe mfupi wa simu wa maandishi (SMS). Amekemea wafanyabiashara hao na kutaka waache mara moja mchezo huo, kwani vyombo vya dola vinaendelea kuwafuatilia.

Hapi alisema hayo jana wakati akizungumzia suala la Uadilifu kwenye Mkutano wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wanaotokana na shirikisho hilo.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya alibainisha kwamba amekuwa hapokei simu hizo na SMS hizo za wafanyabiashara wakubwa kutokana na sababu mbalimbali. 

“Sababu ya kwanza sina sababu ya kuzipokea, lakini pili nahofia nikizipokea nitarekodiwa na wafanyabiashara hao na sauti yangu itasambazwa kwenye mitandao, kuonesha nipo pamoja nao.

“Wakati mwingine mpaka usiku wa manane wanapiga simu na kutuma meseji na wengine wanajitambulisha. Lakini huwa namuonyesha mke wangu na kumwambia sina sababu ya kuzipokea, kwani naweza nikapokea lakini katika mazungumzo yetu nikasema neno ‘sawa’, kisha neno hilo linaweza kusambazwa katika mitandao kuonyesha kwamba nia yetu ni moja ya kuficha sukari”, alisema Hapi.

Alisema hao wafanyabiashara wanaoficha sukari, wanaleta madhara makubwa kwa jamii na uchumi wa nchi, kama vile kuua viwanda vya sukari nchini. 

Alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakiweka ‘oda’ katika viwanda vya sukari kuchukua bidhaa hiyo, lakini hawaendi kuichukua kwa madai ya kwenda kuichukua siku za baadaye, lengo likiwa kuificha. 

Hapi aliwaomba wakazi wa wilaya ya Kinondoni, kuendelea kuisaidia serikali kufichua watu wote walioficha sukari.

Uingereza Kusaidia Usambazaji wa Umeme Vijijini

$
0
0
Miezi  michache baada ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia (MCC) kujitoa kusaidia Tanzania katika usambazaji wa umeme vijijini, Serikali ya Uingereza kupitia taasisi yake ya Energy Africa Initiative, imetangaza utayari wa kutoa msaada huo.

Waziri wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa, Justine Greening, ameeleza utayari huo mwishoni mwa wiki, katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliye nchini humo kumwakilisha Rais John Magufuli, katika mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa duniani. Katika mazungumzo hayo, Greening alimhakikishia Waziri Mkuu Majaliwa, kwamba nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania kwenye mpango wake wa kupeleka umeme vijijini.

“Tuko tayari kuwasaidia kutekeleza mpango huu kupitia taasisi ya Energy Africa Initiative ambayo inapata ufadhili kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID),” alisema. 

Pia Waziri huyo wa Uingereza, alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kupambana na rushwa na kwamba ndiyo maana Tanzania ilipewa mwaliko maalumu wa kushiriki mkutano huo, kwa vile baadhi ya mataifa yanaziona juhudi zinazofanywa na Serikali ya Rais Magufuli.

Aidha, alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu kwa nia ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imeionesha katika kuwa na mpango wa kuendeleza viwanda. 

Nguvu mpya Rea 
Hatua hiyo ya Uingereza, imekuja wiki moja kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini Alhamisi wiki ijayo, ambayo mjadala wake utafanyika kwa siku mbili za Alhamisi na Ijumaa, unatarajiwa kuibua hoja ya kufutwa kwa msaada huo wa MCC wa Dola za Marekani milioni 472, uliokuwa utumike kusambaza umeme vijijini.

Mbali na mjadala huo ambao unatarajiwa kung’ang’aniwa na Kambi ya Upinzani Bungeni, hatua hiyo ya Uingereza itaongeza nguvu katika jitihada za Serikali zilizokwishaanza kwa mafanikio za kuwapatia Watanzania umeme wa uhakika.

Taarifa za Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) zinaonesha kuwa, pamoja na MCC kujitoa Machi mwaka huu katika usambazaji umeme, Serikali katika Bajeti ya 2015/ 2016 inayoisha Juni mwaka huu, ilikuwa imeshatenga Sh bilioni 950 kwa ajili ya mradi wa Rea Awamu ya Pili.

Mradi huo wenye lengo la kufikisha umeme kwa vijiji 2,500 na kuunganishia nishati hiyo wateja 250,000 nchi nzima, unatarajiwa kukamilika Juni 30, mwaka huu na kupisha kuanza kwa Rea Awamu ya Tatu, ambayo itaanza Julai mosi na kumalizika baada ya miaka miwili. 

Jitihada zote hizo, lengo lake ni kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2015-2020, ambayo inataka hadi ifikapo mwaka 2020, wananchi waliounganishwa na umeme wafikie asilimia 60 na kiwango cha uzalishaji kifike megawati 4,915.

Mbali na malengo ya Ilani hiyo, jitihada hizo pia zitachangia katika kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa inayotaka Tanzania iwe nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, ambayo imeweka lengo la usambazaji umeme liwe asilimia 50 mwaka huo mwaka 2025 na asilimia 70 mwaka 2033.

Tayari Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameshaelezea nia ya Serikali kutaka sekta ya nishati itoe mchango mkubwa kufikia uchumi huo wa kati, kwa kuwa rasilimali za kufikia lengo hilo kupitia nishati zipo na kinachotakiwa ni dhamira na kasi ya kutekeleza.

Katika kusisitiza kasi na dhamira hiyo ya Serikali, Waziri huyo amekuwa akielezea mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa dira hiyo, iliyotaka ifikapo mwaka 2015 uunganishaji umeme uwe umefikia asilimia 30. Lakini, kutokana na utekelezaji madhubuti wa dira hiyo, kiwango hicho kilivukwa lengo na kufikia asilimia 40 mwaka 2015.

JPM na Marekani 
Mbali na msaada huo wa Uingereza katika kusambaza umeme vijijini, Serikali ya Marekani pia imeelezea kuvutiwa na utendaji wa Rais Magufuli katika kupambana na rushwa, hatua iliyoanza kuvutia wawekezaji wa nchi hiyo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia Masuala ya Kimataifa, Sarah Sewall, katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu Majaliwa nchini Uingereza katika mkutano huo wa kimataifa, ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua katika mapambano dhidi ya rushwa.

Alisisitiza kuwa kampuni nyingi za Marekani, zimeonesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania. “Ninaamini uwekezaji huu utasaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa watu. Tunampongeza Rais Dk Magufuli kwa juhudi anazofanya na nipende kusisitiza kwamba ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani utaendelezwa katika maeneo yetu ya siku zote,” alisema.

Majaliwa ashukuru 
Akizungumza katika kikao chake na Waziri Sewall, Waziri Mkuu Majaliwa alimsisitiza asiache kusaidia kuwahimiza Wamarekani wengi waje kutalii Tanzania na wawekezaji zaidi waje kuwekeza nchini katika nyanja mbalimbali, ikiwemo uanzishaji wa viwanda, uongezaji thamani kwenye mazao yanayozalishwa nchini.

Alimhakikishia kuwa Watanzania wamekuwa wakijifunza teknolojia mpya na za kisasa.

Kuhusu mafanikio katika mapambano na rushwa, Majaliwa alisema mkutano huo wa kimataifa, uliojadili jinsi ya kupambana na rushwa duniani, ni kiashiria tosha kwamba tatizo la rushwa ni kubwa na linataka juhudi za pamoja katika kukabiliana nalo.

Akizungumza na mawaziri hao, Waziri Mkuu Majaliwa alisema kwamba viongozi wa Serikali wa Awamu ya Tano, wameamua kwa dhati kupambana na kila ovu, linalotokana na janga la rushwa na wameamua kuwajibika na kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea.

“Sasa hivi nchi yetu ina utamaduni mpya wa kufanya kazi na tumeamua kufanya kazi kwelikweli na siyo tena kwa mazoea, tumeamua kuweka utamaduni mpya wa kupiga vita rushwa, ili kuleta uwajibikaji na uwazi miongoni mwa watu wetu,” alisema.

Alipoulizwa nini kimechangia kufanya Tanzania ing’are kimataifa katika vita hiyo, Waziri Mkuu alijibu kwamba Tanzania imetumia mambo manne ambayo ni kuzuia rushwa isitolewe ama kupokelewa, kampeni za kuelimisha jamii, kufanya mapitio ya sheria na kuwepo kwa utashi wa kisiasa.

“Serikali inachukua hatua za kiutawala na kisheria, kama vile kuanzisha Mahakama Maalumu ya Mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai mwaka huu,” alisema Waziri Mkuu.

Bunge Larudisha safari za Ulaya na Marekani

$
0
0
Wakati Serikali ya Awamu ya Tano ikizuia maofisa na watumishi wa umma kwenda nje ya nchi kwa safari ambazo si za lazima ili kubana matumizi, Bunge limesema limetenga fungu kwa ajili ya kuwawezesha wabunge kupata mafunzo ya uendeshaji bora wa Bunge nje ya nchi.

Novemba 7, mwaka jana, ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Tano, John Magufuli alipiga marufuku safari za nje kwa maofisa wa serikali isipokuwa tu itakapokuwa lazima na kwa ruhusa ya Ikulu.

Rais Magufuli alisema shughuli nyingi za nje ya nchi zitafanywa na kusimamiwa na mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi hizo.

Wakati Rais Magufuli akitekeleza sera yake ya 'Hapa Kazi Tu' kwa kubana matumizi kiasi cha kuzuia semina elekezi kwa mawaziri ambayo ingeharimu Sh. bilioni mbili, uongozi wa Bunge jana ulisema umepanga kupeleka wabunge ughaibuni kwa ajili ya mafunzo.

Akifungua semina ya wenyeviti wa kamati za Bunge iliyofanyika mjini hapa jana, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema uongozi wa Bunge hilo utaandaa mafunzo kwa vitendo nje ya nchi kwa ajili ya wabunge.

"Katika siku za usoni, pia tutaandaa mafunzo haya kwa vitendo nje ya nchi. Lipo Bunge moja tu Tanzania; na hivyo mafunzo pekee ya vitendo ni kwa kutembelea mabunge ya wenzetu," alisema Ndugai na kuibuka shangwe za wenyeviti wa kamati za Bunge ukumbini.

Baadhi yao walimuomba arudie kuelezea dhamira hiyo. "Nafurahi kwamba tuna mawasiliano mazuri na mabunge mengi ya nchi zinazoendelea kama vile Uingereza, India na hata Marekani," alisema Ndugai ambaye Bunge lake, kwa vyovyote, limeathiriwa na mkakati wa serikali wa kubana matumizi.

"Lakini pia kwa majirani zetu hapa, yaani Zambia, Kenya, Uganda, Afrika Kusini na kadhalika. Tutatumia ujirani na uhusiano wetu na mabunge hayo ili mfaidike kwa mafunzo."

Baada ya kufungua rasmi mafunzo hayo, Ndugai alisema kuwa wameona kuna ulazima wa kuwa na mafunzo kwa wabunge ndani na nje ya nchi kutokana na wengi wao kuwa wageni wa uendeshaji wa Bunge.

"Kazi ni kubwa sana (kuedesha shughuli za Bunge). Ni kama tunaanza upya kwa sababu wabunge wengi ni wapya," alisema.

"Tumeamua kuwa na mafunzo haya ili kuwa na uelewa wa pamoja na kuwa na uendeshaji bora wa bunge." 

Ndugai alisema kutakuwa na mafunzo ndani na nje ya nchi kwa makundi mbalimbali yakiwamo ya wabunge wote, wanawake, vijana, viongozi wa wabunge na kamati za Bunge.

Aliongeza kuwa tayari kuna fungu ambalo limetengwa kwa ajili ya kugharamia mafunzo hayo, lakini hakuwa tayari kuanika kiasi cha fedha kilichotengwa, hata hivyo.Alipoulizwa kuhusu kukinzana na agizo la Rais Magufuli, Spika huyo alisema:

"Ni kweli kwamba alichosema Mheshimiwa Rais cha kupunguza safari za nje. Sisi (Bunge) pia tumejitahidi sana kupunguza safari za nje, lakini katika mafunzo haya, inafikia wakati mtu lazima aone Bunge jingine linafanya nini.

"Wajue nao wenzao duniani wanafanya nini. Ila wasiwe wengi na haitakuwa mara kwa mara." Ndugai pia alilimwagia sifa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kufadhili mafunzo ya wabunge, ikiwamo semina ya jana, kupitia mradi wa wake wa kusaidia mabunge (LSP).

Alisema mradi huo umekuwa ukisaidia kutoa semina kwa kamati mbalimbali za Bunge ili kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati hizo katika kutekeleza majukumu yao ya kikatiba kwa ufanisi zaidi.

Alisema mradi huo ulioanza rasmi 2011, utamalizika mwezi ujao, lakini mazungumzo yanaendelea ili uendelee hadi 2020 na kwamba wafadhili wameonyesha nia ya kuendelea katika Bunge la 11 kuanzia Julai, mwaka huu hadi Juni, 2020.

Katika semina ya jana ambayo Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alishiriki, kulikuwa na mafunzo ya mchakato wa kutunga sheria na uchambuzi wa miswada, mchakato wa maandalizi ya Bajeti ya Serikali na Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 pamoja na majukumu wenyeviti wa kamati za Bunge na namna ya kuzungumza mbele ya hadhara.

Semina hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Naibu Kamishna wa Bajeti - Mikoa na Halmashauri, Dk. Charles Mwamwaja na mawakili Said Yakubu na Harold Sungusia waliokuwa watoa mada, kulikuwa na mafunzo ya namna ya kutumia vyombo vya habari wakati wa shughuli za kamati na mabadiliko, maboresho na hatma ya Bunge.

Masharti
Mwishoni mwa mwaka jana, Ofisi ya Rais ilisambaza mwongozo kwa taasisi na mashirika ya umma unaoweka masharti ambayo watumishi wa umma wanaotaka kusafiri nje ya nchi watatakiwa kuyatimiza ili wapewe kibali cha kusafiri.

Masharti hayo ni kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi na maombi hayo yawasilishwe kwa Msajili wa Hazina kabla ya kwenda Ikulu ili mwombaji aweze kujenga hoja kwa kuzingatia umuhimu wa safari hiyo na tija itakayopatikana kutokana na safari hiyo.

Masharti hayo yanamtaka Mtendaji Mkuu wa Shirika ama taasisi kama Bunge, apime kama safari hiyo ni muhimu kuombewa kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi kabla ya kuwasilishwa Hazina.

Sharti lingine ni kupima umuhimu wa safari hiyo na kuona isipofanyika itaathiri vipi taifa, na mwombaji aeleze manufaa ya safari hiyo kwa taasisi na taifa kama imewahi kufanyika huko nyuma. 

Ofisi za Umma zilipokea barua kutoka kwa Msajili wa Hazina Novemba 12, mwaka jana zikieleza kuwa Rais Magufuli ametoa zuio la jumla kwa safari za nje ya nchi katika utumishi wote wa umma na mihimili yake.

Barua hiyo ya Hazina ilisema zuio hilo litadumu hadi pale itakavyoelekezwa vinginevyo.

 Akihutubia katika ufunguzi wa Bunge la 11 Novemba 20, mwaka jana, Rais Magufuli alisema safari za nje katika mwaka mmoja na nusu wa mwisho ya awamu ya nne zilitafuna zaidi ya Sh. bilioni 4, kiasi ambacho kingeweza kujenga kilometa 40 za barabara ya lami

Vijana Wanaovaa Suruali Chini ya Kiuno Kuchapwa Viboko 70

$
0
0

Wakazi wa Kata ya Karansi, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wametoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60 hadi 70.
 
Uamuzi huo umefikiwa na wakazi zaidi ya 200 wakisema uvaaji huo ni kinyume na mila na desturi za Kiafrika.
 
Vazi lingine lisilotakiwa kwa wanawake ni kuvaa suruali pamoja na vijana kunyoa ndevu mitindo isiyofaa.
 
Mkutano huo ulioandaliwa na wazee wa kimila jamii ya Meru (Wachili) na Wamasai (Malaigwani), uliwavutia wananchi wengi ambao walihudhuria.
 
Sambamba na uamuzi huo utakaokuwa unafanyika hadharani, pia adhabu hiyo itawahusu wezi wa mali na wanaopenda kucheza pool table wakati wa kazi.
 
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wilbrod Mutafungwa alipinga uamuzi huo akisema kwa maazimio hayo ya kuwaadhibu watuhumiwa kwa kuwachapa viboko ni kujichukulia sheria mkononi na ni kinyume na sheria.


Serikali Yanasa Kilo 34,000,000 za Sukari Mafichoni

$
0
0
Shehena ya sukari ya kilo milioni 34 zilizokuwa zimefichwa kwenye maghala ya wafanyabiashara watatu Kilimanjaro imekamatwa na vyombo vya usalama, na serikali mkoani humo imetangaza kuiuza kwa wananchi kuanzia jana kwa bei elekezi ya Sh. 1,800.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecki Sadiki alithibitisha jana kukamatwa kwa shehena hiyo, baada ya makachero wanaoongoza timu maalumu ya ukaguzi wa maghala ya wafanyabiashara na mawakala wa sukari kubaini kufichwa kwa bidhaa hiyo.

“Tumefanya ukaguzi katika maghala 45 na katika harakati hizo tumenasa kilo milioni 34za sukari iliyokuwa imefichwa," alisema.

"Katika zoezi hilo kuna mfanyabiashara mmoja mkubwa, yeye alikutwa na tani 31.33 lakini alikuwa akiiuza, isipokuwa bado tumewapa kazi Mamlaka ya Mapato (TRA) ichunguze kama imehodhiwa isivyo halali,” alisema Sadiki.

Kiasi cha sukari iliyobakia, alisema Mkuu wa M koa huyo, kilikamatwa kwa wafanyabiashara wengine wawili, ambao walikuwa na tani nne kasoro, Moshi mjini na Marangu.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa mkoa, shehena hiyo ya sukari hadi jana mchana ilikuwa ikishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kiuchunguzi na kwamba ametoa amri igawiwe kwa wananchi kwa bei elekezi iliyotangazwa na serikali.

Kuhusu upungufu wa sukari Kilimanjaro, Sadiki alisema "Sisi kama mkoa tumefanya mawasiliano na mawakala walioko Dar es salaam, ambao sukari yao ilikuwa inashikiliwa na vyombo vya usalama na wametuahidi kuukabili uhaba wa sukari uliopo hapa kwetu.

“Jana (juzi) niliwasiliana na Mmiliki wa Kampuni ya Zakaria Enterprises na amekubali kuwapa bidhaa hiyo mawakala ambao ni wadau wa Kiwanda cha Sukari cha TPC," alisema Sadiki. 

"Kwa hiyo tunakwenda vizuri na tumejipanga kuhakikisha kwamba uhaba huo tunaupatia ufumbuzi wa kudumu.Ila ninawaomba wananchi wangu wawe wavumilivu kwa sasa.

"Mawakala wakubwa wa sukari wa Kilimanjaro na mikoa ya Kanda ya Kaskazini ni mfanyabiashara Vicent Laswai ambaye atapatiwa tani 600 za sukari kutoka Kampuni ya Zakaria, alisema Mkuu wa Mkoa huyo.

Aidha, Laswai atapokea tani 640 toka katika Kampuni ya Mohamed Enterprises, alisema.

Kampuni ya Zakaria pia imekubali kutoa tani 640 kwa Kampuni ya Marenga Investment, alisema Sadiki na kubainisha kuwa Mohamed Enterprises imemuahidi kuziba pengo la upungufu utakaojitokeza.

Tangu Rais Magufuli apige marufuku uingizaji sukari kutoka nje ya nchi Februari 17 mwaka huu, baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakificha bidha hiyo kama njia ya kuihadaa serikali kwamba kuna uhaba mkubwa.

Wakati akipiga marufuku, Magufuli alisema kama kutakuwa na uhitaji wa sukari kuingia nchini, vibali atavitoa yeye si mtu mwingine yeyote ili kuviwezesha viwanda vya ndani viendelee kuzalisha bidhaa hiyo, kuendelea kutoa ajira na kuinua kipato cha wakulima wa miwa.

Alisema inasikitisha kuona sukari ikiingizwa nchini kutoka nje wakati nchi ina viwanda vingi vya bidhaa hiyo na kusababisha Watanzania wengi kupoteza ajira kutokana na sukari wanayozalisha kukosa soko.

"Nakuagiza Waziri Mkuu, kuanzia leo, marufuku mtendaji yeyote wa Serikali kutoa kibali cha kuagiza na kuingiza sukari kutoka nje ya nchi...vibali vyote nitatoa mimi," alisema Rais Magufuli.

"Katika kampeni zangu mwaka 2015, nilisema Serikali yangu itakuwa ya viwanda hivyo lazima tuvithamini viwanda vya ndani na kulinda bidhaa zinazozalishwa."

Gigy Money: Niko Kwenye Uhusiano wa Kimapenzi na Gardner Kwa Miezi 6 Sasa

$
0
0
Muuza sura kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Giggy Money’ amefunguka kuwa mtangazaji maarufu Bongo wa Clouds FM, Gardner G. Habash hachomoki kwake na hadi sasa wako kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda wa miezi sita.

Gigy mefunguka haya baada ya picha zinazomuonesha akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na Gardner kusambaa kwenye mitandao ya kijamii. Giggy alisema mtangazaji huyo amekuwa mtu wa muhimu kwake kwa sasa.

“Kwani kuna tatizo nikiwa na Gardner? Yule ni mtu muelewa na sahihi kwangu, ninafikiri kupitia yeye nitajifunza mambo mengi na kuzidi kufanikiwa kwa sababu yeye ni moja kati ya watu ambao wako kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu,” alisema Giggy Money.

Gardner alipotafutwa ili aweze kueleza kuhusu ishu hii alisema:

“Nipo karibu na Giggy lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi, kwa hiyo kama anasema hivyo si kweli lakini yeye ni shabiki wangu na mimi ni mshabiki wake, ninapenda pia kazi anazozifanya,”

Wanaofanya Biashara ya Ngono Wataka ajira Irasimishwe

$
0
0

Baadhi ya wanawake wanaojiuza katika mitaa ya Majengo B na Fisi, mjini Mpanda mkoani Katavi wameitaka Serikali kuandaa utaratibu wa kuwatambua ili nao waweze kulipa kodi na kuliingizia taifa pato kutokana na shughuli wanayofanya ya kuuza miili yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana usiku, baadhi yawanawake hao walisema wanafanya kazi kama zilivyo kazi nyingine kwani zinawaingizia kipato kizuri kinachowasaidia kutimiza mahitaji yao ya msingi hivyo kazi hiyo inapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa na serikali.

Mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce, alisema ni wazi Serikali ikiandaa utaratibu mzuri wa kuwatambua itawafanya waweze kulipa kodi ambayo italiongezea pato taifa tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa hawalipi kodi kwa kuwa hawatambuliwi.

" Sisi kazi yetu ina kipato kizuri kutokana na makubaliano yanayofanyika kati na wateja wetu lakini Serikali haitaki kututambua hivyo sio rahisi hata kututaka tulipe kodi, nchi nyingine watu kama sisi tumetambuliwa na tunalipa kodi serikalini" alisema Rosemary Kazeze.

Aliongeza kwamba kipindi hiki ambacho Serikali inatafakari au haioni umuhimu wa wao kutolipa kodi, anawashauri kina dada poa wenzake kuacha tabia ya kukwepa kwenda Nyumba za kulala wageni zinazotambuliwa na Serikali kwani kufanya  hivyo kunaikosesha serikali mapato

Alisema kuwa siku za nyuma walikuwa wanafanya biashara hiyo katika madanguro kitendo ambacho polisi walikuwa wakiwasumbua kwa kuwakamata kutokana na misako ya mara kwa mara, lakini hivi sasa hawasumbuliwi kwani wamepanga vyumba katika gesti halali na wanalipia vyumba hivyo na mmiliki analipa kodi kwa msingi huo nao wanachangia pato la taifa.

“ Kaka yangu mwandishi tunashukuru sana hata wewe kutufikia, wanatudharau na kutunyanyasa sisi lakini wateja wetu wakubwa ni hao hao viongozi wa serikali na tasisi nyingine lakini wajue kufanya biashara ya ukahaba sio sababu ya kuto muunga mkono Rais wetu katika suala la mapato ya serikali”…alisema Mayasa Hussein

Serikali Yatangaza Msako wa Waliokula Fedha za Watumishi Hewa

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeamua kupambana na wala rushwa ili kiasi kidogo cha rasilmali kilicholengwa kiweze kuwafikia wananchi.
 
Ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Mei 14, 2016) wakati akizungumza na Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini London, Uingereza.
 
“Jambo tuliloamua kuanza nalo ni kupambana na rushwa. Tumeamua kufanya hivyo ili kurudisha umoja na maelewano miongoni mwa Watanzania, tunataka tuibadili Tanzania ili iwe ni ya Watanzania wote… tumechoka kuambiwa sehemu fulani mradi umekamilika halafu ukienda kuangalia hukuti kitu na fedha ile haipo,” alisema huku akishangiliwa.
 
Akizungumzia zoezi la kusaka watumishi hewa, Waziri Mkuu alisema Serikali itawashughulikia wale wote waliohusika na zoezi hilo. 

“Wafanyakazi hewa wamefikia zaidi ya 10,000 na tumeokoa zaidi ya sh. bilioni 4.5 zilizokuwa zikipotea kila mwezi. Tukikamilisha zoezi la kusaka watumishi hewa, sasa tutataka kujua ni akina nani walikuwa wakipokea fedha hizo. Waliohusika tutashughulika nao,”  alisisitiza.
 
Alisema hivi sasa Serikali inalenga kuwa na watumishi ambao wanafanya kazi kwa uaminifu, uadilifu na uwajibikaji mahali pa kazi. “Hiki ndicho kipaumbele cha Serikali ya awamu ya tano na tena zoezi hili litakuwa endelevu”, alisema Waziri Mkuu.
 
Akizungumzia kuhusu ukuaji wa uchumi, Waziri Mkuu ambaye alikuwa London kuhudhuria mkutano uliojadili mapambano dhidi ya rushwa kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, alisema lengo la Serikali hivi sasa ni kuona kuna ukuaji wa uchumi unaoenda sambamba na huduma zinazotolewa kwa wananchi.
 
Alisema viwanda vingi viliuzwa na watu waliovinunua wakageuza kuwa ni maghala ya kufugia wanyama. Sisi tunataka vifufuliwe ili teknolojia mpya na za kisasa zije Tanzania. Nafasi ya kuwekeza iko kwa Watanzania wote walioko nyumbani na ninyi mlioko nje,” alisema.
 
Alisema ardhi ipo ya kutosha na akawataka wawaalike marafiki zao waje kuwekeza nchini, ili mradi wawe ni watu makini, wenye nia ya dhati ya kuwekeza nchini na wenye mitaji na siyo madalali (middlemen). 

“Tunataka usindikaji wa mazao na bidhaa ufanyike nchini mwetu badala ya kupeleka mazao ghafi nje ya nchi, kwa njia hiyo tutakuwa pia tumezalisha ajira kwa watu wetu,” alisema.
 
“Kuna Watanzania wanaishi Botswana, Ujerumani na Poland wameshaleta wawekezaji nchini. Kwa mfano wa Poland wameleta mradi wa umeme katika vijiji vitani wilayani Ileje. Kwa hiyo ninyi endeleeni kuishi Uingereza lakini mhakikishe kuwa ukaaji wenu hapa, unaleta tija kule nyumbani. Kumbukeni Tanzania na muwe tayari kuihudumia Tanzania,” alisema.
 
“Serikali inaamini itanufaika na uwepo wenu hapa Uingereza. Muweke kipaumbele cha kuwekeza nyumbani na mkishindwa mtutafutie marafiki zenu. Mwenye uwezo andaa andiko la mradi halafu uwasiliane na Balozi ili akusaidie kutafuta wahusika kule nyumbani,” aliwaasa.
 
Akijibu swali kuwa ana maoni gani juu ya Bunge kutorushwa ‘LIVE’, Waziri Mkuu alisema hatua hiyo ilichukuliwa ili kuwawezesha watu kufanya kazi kama ambavyo kaulimbiu ya Mhe. Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu inavyosema.
 
“Bunge la Tanzania lilikuwa ni bunge pekee katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na duniani ambalo lilikuwa likirushwa LIVE kuanzia asubuhi hadi usiku. Ina maana katika kipindi cha Bunge la bajeti, ambalo linaendeshwa kila siku kwa miezi mitatu, Watanzania nao wangekuwa LIVE kwa miezi mitatu,” alisema.
 
“Tulilazimika kujifunza kutoka kwenye mabunge mengine. Hivi hapa Uingereza mnaangalia Bunge live kila siku?” alihoji Waziri Mkuu na kujibiwa kuwa linarushwa LIVE kwa kipindi kisichozidi dakika 15 wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu tu.
 
Akitoa ufafanuzi, aliwaeleza kwamba Bunge la Tanzania linarusha ‘LIVE’ kila siku asubuhi wakati wa maswali ya kawaida na Alhamisi asubuhi wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu lakini mijadala yote hurekodiwa na kuhaririwa na kisha kurushwa kuanzia saa 8-9 mchana na saa 3-4 usiku kwa siku husika.
 
Kwa Watanzania wanaopenda kufanya kazi na wanapenda kufuatilia mambo ya Bungeni, walikuwa hawaoni LIVE coverage kwa sababu walikuwa kazini lakini sasa hivi wanaweza kufuatilia masuala ya bunge kwani muda wa jioni uliopangwa mtu anakuwa ametoka kazini na anaweza kuangalia televisheni akiwa nyumbani baada ya kutoka kazini.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, MEI 15, 2016.

Jaji Mkuu: Sheria Ya Makosa ya Mtandaoni Haina Lengo la Kuwakandamiza Watanzania

$
0
0

JAJI MKUU wa Tanzania, Mohammed Chande Othman amesema sheria ya mitandao ilipitishwa kwa lengo jema la kulinda watumiaji, wanajamii na usalama wa Taifa la Tanzania.
 
Ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Mei 14, 2016) wakati akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini London, Uingereza.
 
Alisema watu watatu kati ya wanne nchini Tanzania wakiwemo watoto, wanamiliki simu za mkononi ambayo ni sawa na watu milioni 35 kati ya milioni 45.
 
Alisema sheria hiyo ilitungwa kwa misingi mitatu moja ikiwa ni kumpa mtumiaji uhuru wa kutoa maoni au taarifa, uhuru ambao alisema unalindwa kikatiba lakini akaonya kuwa kila uhuru unaotolewa pia una mipaka yake kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Alisema sheria hiyo pia inatoa uhuru wa mtu kuwa na faragha (privacy) na msingi wa tatu ni sheria hiyo kuzingatia matumizi ya mitandao ili kulinda usalama wa nchi.
 
“Sheria hii inakupa uhuru wa kutumia mtandao kumlinda mwanajamii wenzako. Hapa Uingereza nimeongea na mwendesha mashtaka mkuu ambaye aliniambia kuwa asilimia 60 ya makosa yanayofanyika chini ya sheria ya makosa ya kujamiiana (S3x.ual Offencea Act) yanatokana na mitandao,” alisema Jaji Mkuu wakati akijibu swali kuhusu sheria ya makosa ya mitandao.
 
Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga alisema kuitishwa kwa mkutano wa kupambana na rushwa nchini Uingereza ni mojawapo ya jitihada za Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuanzisha vuguvugu la uanaharakati wa mapambano dhidi ya rushwa.
 
“Kukosekana kwa utawala bora, changamoto za ugaidi, biashara za dawa za kulevya, biashara ya kusafirisha binadamu na uwepo wa rushwa na ufisadi ni baadhi ya mambo yaliyofanya dunia ibadilike. Haya mambo zamani yalikuwa hayana mahali pa kuzungumzwa, kwa hiyo vikao kama hivi vitasaidia kukabili tatizo hili,” alisema.
 
“Rushwa ni kama pweza mwenye vichwa vingi na mikia mingi. Waziri Mkuu David Cameron ameamua kuanzisha movement hii ili kutafuta njia za kukabili janga hili kubwa,” alisema.
 
"Sote tunatambua kuwa mataifa mengi yangependa kuwemo katika hii movement lakini ni faraja kuona kwamba Tanzania imo miongoni mwa waanzilishi na hii ni kwa sababu ya uongozi na ujasiri wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ambaye kwa kweli ni game changer  (akimaanisha kuwa amebadili mwelekeo wa Taifa hili) kwani ana utashi wa kisiasa na ana ujasiri wa kukemea maovu,” alisema huku akishagiliwa
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola alisema vita ya rushwa nchini Tanzania ni endelevu na inafanyika kuitikia wito alioutoa Rais Magufuli wakati akizindua Bunge la Tanzania Novemba 20, 2015.
 
Alisema wanatumia mbinu mbalimbali kupambana na rushwa lakini kubwa wanayoenda nayo hivi sasa ni kutoa elimu kwa watoto na vijana ili kuwabadilisha tabia na utamaduni uliojikita kwenye jamii.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMAPILI, MEI 15, 2016.

Tanzania Kuwa Nchi kwanza Duniani Kutumia Kitambaa Kilichowekewa viatilifu Kudhibiti Malaria.

$
0
0

Tanzania imekuwa nchi ya kwanza duniani kufanya majaribio ya kupambana na mbu waenezao magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria kwa kutumia kitambaa kilichowekewa viatilifu ili kudhibiti ugonjwa malaria ambao ni tishio kwa afya ya wananchi wengi wanaoishi vijijini.

Hatua hiyo ya utafiti imefikiwa na watafiti wa magonjwa ya binadamu katika cha taifa cha Magojwa ya Binadamu (NIMR) katika kituo cha Amani mkoani Tanga ili kuweza kuwadhibiti mbu waenezao ugonjwa malaria ambao unaathiri watu wa rika zote nchini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William Kisinza alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa Habari wa Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani ambao walitembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa huo.

Katika kufanikisha majaribio hayo, Dkt. Kisinza amesema kituo hicho kinaendelea vizuri na majaribio ambapo wanatarajia mchanganuo wa utafiti huo utafanyika mwishoni mwa mwaka 2016 na taarifa kamili itatolewa rasmi mwaka 2017 ili iweze kutumika nchi nzima na duniani kote.

Dkt. Kisinza amesema kuwa mafanikio ya taasisi yake yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo na taasisi nyingine za kitaaluma ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa taasisi hizo ni Chuo Kikuu cha Afya cha Kilimanjaro (KCMC), Kituo cha Kudhibiti Kuzuia na Magonjwa cha Marekani (CDC), Taasisi ya Tiba, Dawa na usafi wa mazingira ya London nchini Uingereza (LSHTM) na Chuo Kikuu cha Brandeis cha nchini Marekani.

Naye Mtafiti Mkuu anayesimamia zoezi la majaribio hayo ya mradi huo wa vitambaa vyenye viatilifu hivyo vijulikanavyo kama “insecticide treated wall liners”, Dkt. Joseph Mugasa amesema kuwa zoezi hilo linahusisha vijiji 44, kaya zaidi ya 25,000 na idadi ya watu wanaonufaika na majaribio hayo ni zaidi ya 100,000 katika maeneo mbalimbali ndani ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Mbali na kuangalia uwezo wa vitambaa hivyo, mradi huo unaangalia pia uwezo wa vitambaa hivyo katika kukabiliana na upugufu wa damu kwa watoto chini ya miaka 11, uwezo wa vitambaa kupambana na mbu sugu kwenye viatilifu vingine na pia kufanya tathmini ya gharama anazoingia mwananchi katika kugharamikia tiba za malaria.

Kitambaa hicho ambacho huwekwa kwenye kuta za nyumba kwandani hutumika sambamba na chandarua ili kuweza kutoa kinga madhubuti mara mbili kumkinga binadamu dhidi ya mbu waenezao magonjwa.

Mradi huo wa majaribio wa kutokomeza ugonjwa wa malaria umeanza kufanyiwa utafiti nchini miaka mtatu iliyopita kuanzia 2013 na unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) chini ya Mpango wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Malaria (PMI) ambao hadi kukamilika kwake utarajiwa kugharibu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 3.

Kwa upande wake Meneja wa Mawasiliano Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani ambaye pia ni Mkuu wa msafara wa waandishi hao Dena Gudaitis amesema kuwa wamefurahishwa kuona Tanzania ilivyosimama imara kujali afya za wananchi wake hasa watu wa kipato cha chini ambao wengi wao wanaishi vijijini.

Katika kutekeleza wajibu wao wa kiuandishi, waandishi hao kutoka ICFJ wanaongozwa na kaulimbiu ya taasisi hiyo inayosema “Andaa mazingira bora ya mwandishi wa habari wa kimataifa ajaye”.

Waandishi hao wa habari wamefanya ziara ya siku tano nchini kuanzia Mei 8 hadi 13, 2016 katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha na Tanga ambapo wametembelea baadhi ya zahanati katika mikoa hiyo, familia zenye watoto walio chini ya mpango wa majaribio wa kudhibiti malaria, vituo vya utafiti vya Korogwe na Amani pamoja na kiwanda cha kutengenezea vyandarua cha A to Z cha jijini Arusha.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya May 16

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images