Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Chadema Waungana na CUF Kutomtambua Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.

$
0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza rasmi kutoitambua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), inayoongozwa na Dk Ali Mohamed Shein. 

Mbali na kutoitambua Serikali hiyo, chama hicho kimesema leo kitatoa mkakati mzito wa namna ya kushughulikia suala la matangazo ya Bunge la Kumi na Moja kutoonyeshwa moja kwa moja (live) na televisheni.

Msimamo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari jana mjini Dodoma katika kikao cha pamoja kati ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji, manaibu wake wawili, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar). 

Pia walitoa taarifa juu ya mambo yanayojadiliwa katika kikao cha siku mbili cha Kamati Kuu (CC) kinachofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe. 

Akizungumzia hali ya kisiasa Zanzibar, Mwalimu alisema chama hicho hakitampa ushirikiano Dk Shein. 

“Kikao maalumu cha Kamati Kuu ya Chadema kilichoketi Jumatatu, tumefikia msimamo wa kutoitambua Serikali ya SMZ. Msimamo wa Maalim Seif Shariff Hamad ndiyo msimamo wetu,” alisema. 

Maalim Seif aliwania urais Zanzibar kupitia CUF katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kabla ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta matokeo yake na kutangaza uchaguzi wa marudio ambao mgombea huyo na chama chake walisusia. 

“Hatutatoa ushirikiano kwa SMZ na katika kikao cha leo (jana) cha CC tutawasilisha azimio hilo.Hali ya kisiasa Zanzibar ni mbaya mbaya sana. Wazanzibari wanaelekea kununa,” alisema Mwalimu. 

Mwalimu alisema hawatafanya maandamano Zanzibar lakini hali itakuwa mbaya zaidi kwani Wazanzibari wengi wanaelekea kununa na kwamba hilo litasababisha hali mbaya zaidi.

“Hali ya Zanzibar si nzuri kama CCM wanavyoeleza.  Watu hawazikani, hawatembeleani tumerudi kulekule kama mwaka 1995 kabla ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema. 

Mashinji alisema kikao hicho cha kamati kuu kitapokea taarifa kutoka kwa wabunge wa Chadema, kuhusu Bunge kutoonyeshwa ‘live’ na athari zake kwa wananchi. 

“Uhuru wa wananchi kupata habari litajadiliwa kwa kina. Sasa hivi Bunge letu liko gizani tunapata habari za kupapasa tu. Tutatoka na mkakati kabambe wa kushughulikia suala hili,” alisema.

Akizungumza hatua hiyo iliyochukuliwa na Bunge, Mnyika alisema kinachoonekana sasa ni kama chombo hicho kimetekwa na Serikali na hilo litatolewa tamko zito rasmi leo na Mbowe mwenyewe.

“Kuna mambo makubwa tuki- yawekea mkakati huwa Serikali inasalimu amri. Tunataka kutoka kwenye huu mkwamo ili Bunge lionyeshwe live,”alisema. 

Januari 27, Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alitangaza Serikali kusitisha matangazo hayo ya moja kwa moja kama njia ya kubana matumizi. 

Waziri huyo aliliambia Bunge matangazo hayo yatarushwa vipande muhimu vya mijadala usiku katika kipindi maalumu cha Leo katika Bunge ambacho kitarushwa saa nne za usiku uamuzi ambao ulipingwa vikali ndani na nje ya Bunge. 

Leo, Nape atawasilisha bajeti ya wizara yake bungeni ambako mjadala mzito unaotarajiwa kulitikisa Bunge ni suala hilo la kutoonyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni. 

Wadau wa habari wamepiga kambi mjini hapa kujaribu kuishawishi Serikali na Bunge kubadili msimamo huo

Spika Job Ndgai Awagomea Wabunge Waliotaka Utaratibu wa Kusaini Mara Mbili Kwa Vidole Ufutwe

$
0
0
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amejibu mwongozo ulioibuliwa na wabunge bungeni wa kutaka utaratibu wa kusaini kwa kutumia kidole mara mbili kwa siku uondolewe, kwa kusisitiza kuwa utaratibu huo hautabadilishwa.

Majibu ya mwongozo huo aliyatoa bungeni Dodoma jana wakati akijibu mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago (Chadema), aliyemtaka Spika autolee majibu mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Konde Khatib Said Haji hivi karibuni wa kutaka utaratibu huo ufutwe.

“Mheshimiwa Spika inaonesha kuna dalili ya Bunge lako kutojibu miongozo inayoulizwa hapa bungeni. Hivi karibuni tuliuliza juu ya namna ya kusaini kwa kutumia madole sijui kidole lakini mpaka leo hatujapatiwa majibu,” alisema.

Akijibu mwongozo huo, Ndugai alijibu kwa kifupi kuwa utaratibu wa kusaini wabunge ni mara mbili kwa siku na wanatakiwa wakandamize kidole chao hadi taa ya kijani iwake ndipo watakuwa wamesajiliwa rasmi.

“Nataka nitoe ufafanuzi, nasikia kuna malalamiko juu ya utaratibu wa kusaini, maagizo ni hivi, unaposaini pale kandamiza kidole chako hadi taa ya kijani iwake, utakuwa tayari umesajiliwa si kugusa tu. Ule mfumo unaitwa press and hold,” alisema Spika na kufunga mjadala wa suala hilo.

Hivi karibuni, Mbunge Haji, aliomba mwongozo na kuitaka ofisi ya Bunge iwaondolee mara moja utaratibu wa kusaini kwa kutumia vidole mara mbili kwa siku kwa kuwa wao si wanafunzi.

Katika mwongozo wake, alisema kitendo cha kutakiwa kusaini mara mbili kwa siku ni kero kwa wabunge na uonevu kwa kuwa hata Bunge hilo limekuwa likitumia muda wa mapumziko wa wabunge kwa kazi za Bunge.

“...tatizo langu ni kitendo cha wabunge kutakiwa kusaini mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, wakati mwingine tunatoka hapa saa saba, wabunge tunashughulikia mambo mpaka saa 12, mbunge anatumia muda wake wa mapumziko na ule wa kuhudhuria kikao cha jioni,” alisema.

Alisema inasikitisha kuona mbunge anatolewa kwenye kazi za kujenga taifa ili aje tu asaini kwa kidole tena mara ya pili. 

Alisema jambo hilo linawatatiza wabunge kwa kuwa wanajiona kama wanachukuliwa kama wanafunzi kwa kufuatiliwa kwani hata kwenye benki wafanyakazi hawasaini na kufuatiliwa kama ilivyo kwa wabunge hao.

Alifafanua kuwa kabla ya kuomba mwongozo huo, alifanya utafiti kwenye benki mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao nao wana utaratibu kama huo wa Bunge lakini hakuna mahali wanapotakiwa kusaini kwa vidole mara mbili.

Kwa upande wake, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson wakati akijibu mwongozo huo alisema kutokana na namna wabunge hao walivyopokea suala hilo, pamoja na kwamba kikanuni jambo hilo halikutakiwa kuombewa mwongozo bado litaangaliwa. 

“Hata hivyo nifafanue kuwa kusaini mara mbili lengo lake si kuwafanya wabunge wanafunzi, ila lengo ni kutaka kujua nani wapo humu ndani (bungeni),” alisema Dk Ackson.

Gari lagonga mwendesha baiskeli na kusababisha kifo Jijini Mwanza

$
0
0

Mnamo tarehe 11.05.2016 majira ya 13:30hrs mchana katika barabara ya Mwanza – Simiyu eneo la Igoma Kata ya Nyakato Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza, gari namba T. 488 CDZ aina ya Scania Tractor likiendeshwa na dereva aitwaye Enock Mshihiri miaka 24, msukuma mkazi wa Igoma lilimgonga mwendesha baiskeli aitwaye Sanyiwa Nengo miaka 60, msukuma mkazi wa Busekwa na kusababisha kifo chake papo hapo. 

Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa Scania kushindwa kulimudu gari alipokua barabarani. Mtuhumiwa wa ajali hiyo amekamatwa, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayo mkabili. Mwili wa marehemu upo hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi AHMED Z. MSANGI anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa nipamoja na kufuata na kuheshimu sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. 

Lakini pia anatoa wito kwa watumiaji wengine wa barabara wakiwemo watembea kwa miguu nao wachukue tahadhari pindi wanapokua barabarani.

Imetolewa na:
SACP. AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linafanya uchunguzi juu ya mauaji ya watu 7 yaliotokea Wilayani Sengerema.

$
0
0

Kwamba tarehe 11.05.2016 siku ya jumatano majira ya saa 03:45hrs usiku katika Kijiji na Kata ya Sima Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, watu wawili wasiofahamika majina wakiwa na mapanga walivunja mlango na kuingia kwenye nyumba ya Mama Eugenia Philipo miaka 60, akiwa amelala na familia yake na  kuwakata mapanga sehemu mbalimbali za miili yao hadi kufariki papo hapo, Mama mwenye Kaya Bi Eugeni, Mdogo wake, Watoto, pamoja na watu wengine wawili waliokua wakifanya kazi hapo nyumbani kwao wakitokea Ngara Mkoani Kagera.

Waliouawa 1. Eugenia Philipo miaka 60 Mama mwenye Kaya, 2. Maria Philipo miaka 50, mdogo wa Mama Mwenye Kaya 3.Mabula Makeleja miaka 20 mwanafunzi wa kidato cha nne, 4. Mkiwa Philipo mika 12, mwanafunzi shule ya msingi 5. Leonard Aloyce miaka 13 mwanafunzi shule ya msingi sima wote wa familia moja na 6. Donald miaka 40, pamoja na 7. Samson miaka 23 wakazi wa Ngara waliokuwa wakifanyakazi hapo nyumbani kwa Bi Eugeni.

Aidha katika utekelezaji wa mauaji hayo watu hao walianza kuingia kwenye nyumba walipokuwa wamelala watoto wa familia hiyo pamoja na wafanyakazi, na baada ya kuwakata mapanga hadi kuwaua waliingia kwenye nyumba ya jirani alipokuwa amelala Mama mwenye Kaya na mdogo wake Bi Maria na kuwaua vivyo hivyo, kisha wakaondoka eneo la tukio na kwenda kusiko julikana. Huku watoto wengine wanne wakinusurika kwenye mauaji hayo baada ya kujificha chini ya uvungu wa kitanda.

Jeshi la Polisi linawashikilia watu nane kwa mahojiano dhidi ya mauaji hayo na msako mkali wa kuwasaka wahusika wengine waliohusika kwa namna yeyote katika mauaji hayo bado unaendelea. 

Chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana, uchunguzi bado unaendelea. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawaomba wananchi wenye mapenzi mema na nchi yao watusaidie kutupa taarifa za wahusika wa  mauaji hayo ili tuweze kuwakamata.

Imetolewa na:

SACP: AHMED MSANGI                         
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

Rais Magufuli Ataka Walioua Watu 7 wa Familia Moja Kwa Mapanga Wakamatwe Haraka

$
0
0

Rais  Dk. John Magufuli amesema amesikitishwa na mauaji ya kinyama ya watu saba wa familia moja waliokatwa mapanga katika Kijiji cha Sima wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Kutokana na hali hiyo, Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuwasaka kwa nguvu zote, watu waliohusika na mauaji hayo na kuhakikisha wanatiwa mbaroni ndani ya kipindi kifupi.

Akitoa salamu za pole nyumbani kwa wafiwa jana, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, alisema Rais Magufuli ameguswa na tukio hilo na kusema umefika wakati wa wananchi kumwabudu Mungu ili maovu kama hayo yasitokee.

“Wakati nakuja huku, Rais Magufuli amenituma nimfikishie salamu zake za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki mliofiwa.

“Ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinawasaka na kuwatia mbaroni watu waliohusika na tukio la kinyama ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria,” alisema.

Alisema Rais Magufuli ametaka wahusika wote wakamatwe ndani ya kipindi kifupi, kwa sababu mauaji ya aina hiyo hayakubaliki hata kidogo.

Samia alisema Rais Magufuli amewataka wananchi kumcha Mungu kwa kuwa wakishika imani na kumwabudu maovu yatapungua.

Alisema jamii ya wacha Mungu haina maovu mengi kama hayo.

Kuwasili kwa Samia katika msiba huo, kuliamsha vilio vingi kutoka kwa wananchi waliokuwapo.

Samia alitembelea sehemu ambayo ujenzi wa makaburi matano ulikuwa unaendelea kwa gharama za Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.

Miili ya watu hao watano inatarajia kuzikwa leo kijijini Sima.

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Akutana Na Viongozi Mbalimbali London Uingereza

$
0
0
Waziri Mkuu wa Norway, Bibi Erna Solberg amesema nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania katika suala la kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike.

Bibi Solberg ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Mei 12, 2016) alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ya ana kwa ana kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani.

Akizungumza na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Lancaster House, jijini London, Uingereza, Bibi Solberg alisema: “Malengo yetu kwa Tanzania ni kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike,” na kuongeza kuwa mbali ya kuwa ni mdau wa maendeleo kwa miaka mingi, asilimia kubwa ya fedha za bajeti zinazotolewa na nchi hiyo kwa ajili ya misaada ya maendeleo zinaelekezwa Tanzania.

“Sasa hivi kuna Serikali mpya iliyoingia madarakani. Tengenezeni ajenda zenu na mzilete ili tuone ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia,” alisema.

Akizungumzia kuhusu mkutano wa kupambana na rushwa, Bibi Solberg alisema ameufurahia mkutano huo sababu umetoa fursa kwa watu kulizungumzia kwa uwazi tatizo la rushwa. 


“Watu waliouwa hawalizungumzii suala hilo, hivi sasa wameanza kulijadili na kupanga mbinu ya kukabiliana na janga hilo kubwa,” alisema.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Majaliwa aliishukuru Serikali ya Norway kwa misaada ambayo imekuwa ikiipatia Tanzania kwa kipindi kirefu.

Waziri Mkuu Majaliwa alimhakikishia Waziri Mkuu wa Norway kwamba fedha zote za misaada zinazotolewa kwa Serikali ya Tanzania ziko salama na zitatumika kwa uwazi na kwa malengo yaliyopangwa.

“Malengo ya Serikali ya sasa ni kuleta maendeleo ya kiuchumi lakini pia nchini mwetu kuna amani na usalama kwa sababu kama hakuna amani ina maana hakuna usalama,” alisema Waziri Mkuu.

Alimhakikishia Bibi Solberg kuwa Tanzania ni salama na wala hawana haja ya kutilia shaka juu ya uwepo wa amani. 


Pia alimtaka awahimize wawekezaji kutoka kwao waje kuwekeza kwenye uchakataji wa gesi ya kimiminika (LNG) kwa sababu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Katika mkutano huu, Waziri Mkuu amefuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola, wataalamu wa sekta ya rushwa na wanasheria.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na  Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna Solberg katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.  Kulia ni  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna  Solberg (kulia) katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.  Wanne kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman  na watatu kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya  Ulaya na Amerika katika `Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa wa Uingereza   (Minister of State for International  Development) , Justine Greening  katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa Lancaster House, London Uingereza, May 12, 2016.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Ataka Haki Itendeke Wakati wa Kutumbua Majipu

$
0
0

Wakati viongozi wakiendeleza kasi ya Rais John Magufuli ya utumbuaji wa majipu, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wanaoiga kasi hiyo kutenda haki, ikiwamo kufuata taratibu na sheria.

Akizungumza kwenye maadhimisho Siku ya Wauguzi Duniani mkoani Geita jana, Samia aliwataka viongozi na wanasiasa kufuata taratibu za kazi, ikiwamo kutoa nafasi ya kujitetea kwa watumishi wanaotuhumiwa.

Alitoa kauli hiyo, baada ya wauguzi kulalamika kwenye hotuba yao kwamba kuna viongozi waliwatumbua wauguzi bila kuwatendea haki.

“Hata hivyo, nakiomba Chama cha Wauguzi Tanzania (Tanna), kuweka utaratibu wa kufuatilia maadili ya wauguzi na kuwachukulia hatua za kisheria, wale wote ambao wanakwenda kinyume na kiapo chao cha kazi,” alisema.

Rais wa Tanna, Magesa Paul alimuomba Makamu wa Rais kutembelea maeneo yao ya kazi, ili ajionee hali halisi ya wauguzi wanavyofanyakazi katika mazingira magumu, ikiwamo kukosa vitendea kazi na nyumba za kuishi.

Jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda aliwataka wauguzi kuhakikisha wanatii maadili ya kazi, bila hofu ya kupigiwa simu na baadhi ya viongozi wa Serikali waliozoea kutaka upendeleo wa huduma, kinyume na maadili yao.

“Tunaomba wauguzi mkitendee haki kiapo chenu cha kazi, na mtumie siku hii muhimu kuutathmini utendaji wenu wa kazi katika kuwasaidia wananchi,” alisema.

Alisema Serikali inatambua changamoto za wauguzi, hivyo wasitumie matatizo yao katika kuwanyanyasa wagonjwa, bali wawasaidie na kuwaonyesha upendo.

Akisoma risala kwa niaba ya wauguzi wenzake, muuguzi wa Hospitali ya Temeke, John Mgonja alilaani tabia ya baadhi ya viongozi wa Serikali kutumia madaraka kuvuruga utaratibu wa muda wa kuwaona wagonjwa.

“Bila kujali muda uliowekwa wa kuwaona wagonjwa, baadhi ya viongozi hutaka kuingia kuwaona wagonjwa wao kutokana na madaraka waliyo nayo, bila kujali kuwa kufanya hivyo kunachelewesha huduma,” alisema.

Mganga Mkuu wa Mkoa, Musa Wambura aliwaomba wauguzi kuhakikisha wanafanya kazi kwa umakini na weledi, ili kuepusha lawama kwa wananchi.

Frederick Sumaye ( Waziri Mkuu Mstaafu ) Ateuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Ya CHADEMA

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu,Fredrick Sumaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mwenyekiti wa Chadema – Taifa Freeman Mbowe,amekiambia Kikao cha Kamati Kuu jana kuwa, anampendekeza Sumaye kuwa mjumbe wa CC kwa lengo la kuimarisha chama hicho.

Amesema, dhamira ya Chadema ni kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi ujao, kwa kutumia kila mwanachama kufanya kazi ya uenezi.

Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Sumaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Naye Sumaye amemshukuru Mbowe kwa kumteuwa kushika nafasi hiyo na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu zake zote.

Rais Magufuli Aondoka Kampala Kurejea Nchini Tanzania.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kikundi cha ngoma za asili cha Entebe nchini Uganda wakati akiondoka kurejea nchini.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita mbele ya gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili ya kumuaga katika uwanja wa ndege wa Entebe wakati akiondoka kurejea nyumbani Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi na baadhi ya  viongozi mbalimbali wakati alipowasili kwenye hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa Viongozi wakuu wanchi mbalimbali siku walipowasili Kampala nchini Uganda.
Waandishi mbalimbali wa Habari kutoa nchi tofauti wakiwa na shauku ya kupata picha ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumalizika kwa sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni zilizofanyika kwenyeuwanja wa Uhuru wa  Kololo, Kampala nchini Uganda. Katika Picha hiyo Rais Dkt. Magufuli alikuwa akizungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Picha na IKULU.

TiGo Yakata Rufaa Kupinga Kuwalipa AY na MwanaFA Shilingi Bilioni 2.18

$
0
0

Kampuni ya simu ya MIC Tanzania (Tigo) imekata rufaa kupinga hukumu iliyoamuru iwalipe Sh2 bilioni wanamuziki wawili, Ambwene Yesaya na Hamisi Mwinjuma kutokana na kutumia bila ya ridhaa yao, nyimbo za wasanii hao nyota nchini.

Yesaya, ambaye ni maarufu kwa jina la kisanii la AY na Mwinjuma anayejulikana kwa jina la MwanaFA, walifungua kesi hiyo ya madai kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala kupinga kitendo cha kampuni hiyo ya huduma za simu kutumia nyimbo zao kwenye miito ya simu bila ya ridhaa yao.

Nyimbo mbili zilizotumika kwenye miito hiyo ya simu ni “Dakika Moja” na “Usije Mjini” ambazo nyota hao wameshirikiana.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Juma Hassan alitoa hukumu ya kesi hiyo Aprili 11, akiwapa ushindi wasanii hao maarufu katika muziki wa vijana uliopachikwa jina la Bongo Fleva.

Katika hukumu hiyo, Mahakama iliiamuru Tigo kulipa Sh5 milioni kama faini ya uharibifu na kulipa Sh2.16 bilioni kama faini ya jumla.

Iwapo wasanii hao watashinda rufani hiyo, watakuwa wameandika historia katika matumizi ya Sheria ya Haki Miliki na watakuwa wasanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kufungua kesi na kushinda.

Katika rufaa hiyo, Tigo kupitia kampuni ya Law Associates imeainisha sababu saba za rufani, ikidai hakimu wa Mahakama ya Ilala alikosea kisheria kuwapa ushindi wasanii hao kwa kuwa hawakuthibitisha madai yao wala hasara waliyopata.

Kampuni hiyo pia inadai kuwa mbali na kutoeleza hasara waliyoipata kutokana na kazi zao kutumika kwenye miito ya simu, walitakiwa kueleza faida ambayo wangepata kama kazi zao zisingetumika kwenye miito hiyo.

Sababu nyingine ya Tigo kukata rufaa hiyo ni wasanii hao hawakuwa wamesajili kazi zao Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota).

Tigo inadai kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi ya msingi, wadai walisema wamesajili kazi hizo, lakini waliwasilisha barua ya Baraza la Sanaa (Basata) ya kutambua kupokea kazi zao na si cheti cha usajili cha Cosota.

Kwa mujibu wa Tigo, wanamuziki hao walipaswa kuwasilisha mahakamani cheti cha usajili wa Cosota ambako kuna utaratibu wa kujisajili ikiwa ni pamoja na kujaza fomu maalumu baada ya kulipia malipo ya usajili ya kila mwaka.

Kampuni hiyo inasisitiza kuwa wasanii hao hawakuwa na haki ya kudai fidia hiyo wakati hawajasajili kazi hizo Cosota na hivyo kuiomba Mahakama Kuu itengue hukumu iliyowapa ushindi.

Akizungumzia hukumu iliyowapa ushindi, MwanaFA alisema huu ni wakati wa mabadiliko.

“Wale waliokuwa wanachukulia Sheria ya Hakimiliki kama mzaha, watambue kwamba zama zimebadilika,” alisema nyota huyo wa muziki wa rap ambaye aliingia kwenye muziki akijitambulisha kama Mwanafalsafa kabla ya kufupisha jina lake na kuwa MwanaFA.

“Hakuna anayetilia maanani kutumia kazi za wasanii bila ridhaa yao huku akinufaika na wasanii kubaki wanalialia. Huu ni wakati wa kutambua kuwa inawezekana kupata haki yako iwapo utasimama kidete kuitetea kwa sababu sheria zipo.”

Akisisitiza, AY ambaye pia ni nyota katika muziki wa rap aliyeimba R&B akishirikiana na Diamond katika siku za karibuni, alisema huo ni mwanzo wa wasanii kufunguka masikio na kutambua haki zao.

Alisema wasanii wamekuwa wakilalamika juu ya haki za kazi zao, lakini hawachukui hatua.

“Wakati ni sasa, muziki ni kazi kama kazi nyingine na ni ajira pia, hivyo unastahili kuheshimiwa,” alisema AY

Serikali yapata bilioni 1.71 kutokana na maonesho ya vito Jijini Arusha.

$
0
0
Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa madini Tanzania (TAMIDA) iliendesha Maonesho ya tano ya Kimataifa ya Madini ya Vito yaliyofanyika Jijini Arusha katika Hoteli ya Mount Meru kuanzia tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016. 

Maonesho haya  hufanyika kila mwaka Jijini Arusha  na hukutanisha washiriki mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wachimbaji, Wafanyabiashara wa madini ya vito wa ndani na  nje, wanunuzi wa madini wa ndani na nje, na wataalam mbalimbali wenye uzoefu wa shughuli za madini  ya vito.  

Maonesho hayo yalihudhuriwa na washiriki 813 kutoka katika nchi 26 duniani ambazo ni Tanzania  Marekani, Sri Lanka, India, Kenya, China, Ujerumani, Namibia, Australia, Austria, Israel, Italia, Uingereza, Hong Kong, Switzerland, Zambia, Madagascar, Afrika Kusini, Msumbiji, Urusi, Cameruni, Canada, Malawi, Sudani, Malta, na Thailand). 

Aidha, wanunuzi (buyers) wa madini walikuwa 353, Walioshiriki kuonesha madini kwenye mabanda (Exhibitors) 300, na wageni mbalimbali 160.

Lengo kubwa la Maonesho haya ni kama ifuatavyo: kufanya Arusha kuwa kitovu cha madini ya vito katika Afrika ili hatimaye iwe ni kitovu cha biashara ya madini hayo; fursa ya masoko kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa mdini ya vito nchini; na kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini ya vito hapa nchini.

Katika maonesho hayo, madini yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 4.5, sawa na Shilingi Bilioni 9.9 yaliuzwa.

Serikali ilipata jumla ya Shilingi bilioni 1.71, ambapo Shilingi bilioni 1.3 zilitokana na mnada wa madini yaliyokamatwa na kutaifishwa na Serikali, Shilingi milioni 388 zilitokana na mrabaha uliolipwa kutokana na madini yaliyonunuliwa, na Shilingi milioni 26 zilitokana na vibali vya kusafirisha madini nje ya nchi.

Manufaa mengine yaliyopatikana wakati wa maonesho ni pamoja na wageni kuingiza fedha za kigeni hapa nchini ambazo hutumika kwa ajili ya malazi, usafiri, chakula na kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii hapa nchini.

Ili kuweka utaratibu utakaodhibiti shughuli za madini ya vito  hususani tanzanite, Serikali inakusudia kuanzisha minada ya ndani mbali na mnada unaofanyika wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Vito Jijini Arusha. Minada hiyo itatoa fursa kwa wafanyabishara wa ndani kununua madini kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani madini hayo na kutengeneza vidani mbalimbali. 

Ili kuimarisha shughuli za uongezaji thamani madini ya vito nchini, Serikali inakusudia kuimarisha Kituo cha Jimolojia kilichoko Arusha (Tanzania Gemmological Centre -TGC) ili kufundisha na kuzalisha vijana wa Kitanzania wa kutosha wenye ujuzi wa kusanifu na kung’arisha madini ya vito. Tayari vijana 29 wameshapata mafunzo ya miezi 6 ya ukataji wa madini ya vito kutoka kwenye kituo hicho tangu 2014. Wanafunzi wengine 18 wanaendelea na mafunzo ya miezi 6 yaliyoanza mwezi Machi, 2016.

Aidha, upo mpango wa kuanzisha EPZ eneo la Merelani ambapo ni karibu na machimbo ya tanzanite kwa lengo la kupata eneo maalum ambapo shughuli za biashara ya madini na uongezaji thamani madini ya tanzanite zitafanyika kwa uhuru na wazi. Pamoja na juhudi zote hizo, Serikali itaendelea kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa madini mbalimbali nje ya nchi ikiwemo Tanzanite kwenye viwanja vya ndege na kwenye migodi ambapo madini yanazalishwa.  

Wito wa Serikali ni kuwataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuzingatia sheria zilizopo wakati wa kufanya shughuli zao.

Imetolewa na;
KAIMU KAMISHNA WA MADINI
MHANDISI ALLY SAMAJE

Serikali Yatoa Bilioni 2.3 Kuwalipa Wafanyakazi Wa NIDA

$
0
0

SERIKALI imeipatia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shilingi Billioni 2.3 (Bilioni mbili na milioni mia tatu) kwa ajili ya kuwalipa waliokuwa watumishi wa muda wa mamlaka hiyo, wapatao 597, waliosimamishwa kazi hivi karibuni.

Malipo hayo yanahusisha mishahara yao ya miezi minne, ukiwemo mshahara wa mwezi mmoja wa notisi ya kusimamishwa kazi, pamoja na malimbikizo ya madeni yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Kabla ya NIDA kuwalipa watumishi hao fedha hizo, Wizara ya Fedha na Mipango iliamua kufanya uhakiki ili kujiridhisha kama madai hayo yalikuwa sahihi.

Uhakiki huo ulihusisha mahojiano ya ana kwa ana na watumishi hao pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali zikiwemo majalada, mikataba ya ajira, madaftari ya mahudhurio, taarifa za kazi za kila siku na namba zao za akaunti za benki zilizokuwa zikitumika kulipa mishahara.

Katika uhakiki huo imebainika kuwa kulikuwa na kasoro ama changamoto kadhaa zikiwemo za kimikataba kati ya NIDA na watumishi hao.

Wakati wa zoezi hilo, jumla ya watumishi 597 walipaswa kuhakikiwa lakini  majina ya watumishi yaliyowasilishwa kuhakikiwa ana kwa ana kutoka NIDA, Tanzania bara yalikuwa 565.

Hata hivyo, watumishi 516 pekee ndio waliojitokeza katika zoezi hilo na wengine 49 hawakujitokeza.

Watumishi wa muda 32 kutoka NIDA Tanzania Zanzibar, wanaofanya jumla ya watumishi wa Mamlaka hiyo waliosimamishwa  kazi kufikia 597, walihakikiwa kwa kupitia majalada yao yaliyoko ofisi za NIDA Makao Makuu, na kubaini mikataba yao haikuwa na kasoro.

Kwa mantiki hiyo watumishi 427 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ndio waliokidhi vigezo vya kulipwa stahili zao za kuachishwa kazi.

Aidha, watumishi wengine 121, walibainika kuwa na kasoro mbalimbali ambazo zinapaswa kurekebishwa na Menejimenti ya NIDA kabla ya kufanya malipo hayo.

Baadhi ya kasoro zilizobainika katika uhakiki huo ni pamoja na kukosekana kwa mikataba na majalada yao katika Ofisi ya mwajiri, kukosekana majina yao kwenye daftari la mahudhurio kazini, kuwa na utata kwenye mikataba (kutofautiana tarehe na sahihi za wahusika), kufanana kwa namba za majarada, na kukosekana kwa barua za kusitishwa kazi.

Wizara ya Fedha na Mipango imemaliza kazi yake ya uhakiki na kwamba jukumu la kuwalipa watumishi wa NIDA wanaostahili limeachwa mikononi mwa menejimenti ya NIDA.

Imetolewa na:
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

13 Mei, 2016

Tanzania Yatakiwa Kushiriki Mkutano Wa Uwekezaji Norway

$
0
0

WAZIRI MKUU wa Norway, Bibi Erna Solberg amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ahakikishe Tanzania inatuma wawakilishi wa Serikali kwenye mkutano wa uwekezaji unaopanga kujadili fursa za uwekezaji barani Afrika utakaofanyika jijini Oslo, Norway, Oktoba mwaka huu.

Bibi Solberg ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Mei 12, 2016) alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ya ana kwa ana kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani.

Akizungumzia kuhusu mkutano huo, Waziri Mkuu wa Norway alisema mkutano huo umeandaliwa na taasisi binafsi ya Norway Africa Business Association (NABA) na kwamba anazo taarifa kuwa utalenga kujadili fursa za uwekezaji barani lakini focus ikiwa ni Tanzania.

“Ni vema Tanzania ikatuma wawakilishi kwenye mkutano ili waje kuelezea fursa zilizoko nyumbani. Serikali ilete watu wa kuja kuelezea hali halisi ikoje nchini Tanzania,” alisema.

Alisema ili fursa za uwekeaji ziweze kutumika ipasavyo, ni vema Tanzania ikawa na mfumo wa kimahakama unatoa haki bila upendeleo (a fair judicial system) kwani utasaidia kujenga hali ya kujiamini kwa wafanyabiasha wanaokuja kuwekeza Tanzania.

“Mfumo huu utaleta hamasa kwa wawekezaji, kwani watajua kwamba mitaji yao iko salama na inalindwa kisheria, hivyo hawatakuwa na hofu,” alisema.

“Hata hivyo, napenda kusisitiza kuwa makampuni yanayotoka nje na kuja kuwekeza Tanzania hayana budi kuheshimu sheria za nchi yenu pamoja na za huku wanakotoka,” alisisitiza.

Akijibu hoja hiyo, Waziri Mkuu alisema usawa wa kisheria upo nchini kwa sababu Tanzania imesaini mikataba ya kimataifa ya MIGA na ICSID (International Centre for Settlement of Investment Disputes) ambayo inahusika na usuluhishi wa migogoro ya kibiashara.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa alimweleza Bibi Solberg kuwa Tanzania inahitaji kujifunza kutoka Norway katika suala la uanzishwaji wa mfuko wa ili mapato yatokanayo na rasilmali za nchi yatunzwe kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Naye akaipongeza Serikali ya awamu kwa kuanzisha wazo la kutaka kuanzisha mfuko huo hata kabla ya kuanza kuuza rasilmali hizo. Pia alimtihibitishia Waziri Mkuu kuwa wao wako tayari kubadilishana uzoefu na Tanzania katika suala hilo.

IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, MEI 13, 2016.

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Kwa Vyombo vya Habari

$
0
0

Mwanamke mmoja amejeruhiwa kwa kukatwa na panga kwenye bega la mkono wa kulia wilayani sengerema.

Watu wanne wanaozaniwa kuwa ni wezi walivamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa mbao silvia oscar na kujeruhi watu wawili huko igombe wilayani ilemela.

Katika tukio la kwanza.
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la juliana mashiko miaka 41 mkulima na mkazi wa kijiji cha kizugwangoma alijeruhiwa kwa kukatwa na panga kwenye bega la mkono wa kulia na mathias saliana miaka 19 hali iliyopelekea kurupushani na yowe akiomba msaada kutoka kwa majirani ili waweze kumsaidia. 


Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 13.05.2016 majira ya 02:30hrs katika kijiji na kata ya kizugwangoma wilaya ya sengerema mkoa wa mwanza.

Inadaiwa kuwa mathias saliana alikwenda nyumbani kwa bi juliana akiwa na panga akidai apewe fedha kwa lazima huku mwanamke huyo akigoma nakuamua kumkata panga bi juliana kwenye bega la mkono wa kulia ndipo mwanamke huyo alianza kupiga yowe akiomba msaada kutoka kwa majirani, ndipo majirani walifika na kumsaidia mama huyo.

Aidha baada ya kumsaidia bi juliana, wananchi hao walimkamata kijana huyo na kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake kisha wakamfikisha kwenye kituo cha polisi akiwa na hali mbaya kiafya na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya misheni ya wilaya ya sengerema akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake katika kupambana na uhalifu katika mkoa wetu wa mwanza. 


Lakini pia akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi bali watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi pindi wanapomkamata mhalifu ili aweze kufikishwa polisi na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria ili iwe mfano kwa watu wengine.

Katika tukio la pili.
Watu wanne wanaozaniwa kuwa ni wezi walivamia nyumbani kwa mfanya biashara wa mbao wa kigote – igombe anayejulikana kwa jina la bi Silvia Oscar miaka 30 na kumjeruhi kwa kumkata na kitu chenye ncha kali kwenye kiganja cha mkono wa kushoto, akafanikiwa kujiokoa kwa kukimbia na kuwaacha watu hao ndani ya nyumba. 


Ndipo walipokutana na baba mzazi wa Silvia anaeishinae hapo nyumbani kwake aitwaye Oscar Mkaima miaka 57 ambaye walimjeruhi kidogo kwa kumkata na kitu chenye ncha kali kichwani. 

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 12.05.2016 majira ya saa 20:40hrs usiku katika mtaa wa kitoge- Igombe kata ya Bugogwa wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Inadaiwa kuwa wahalifu hao waliingia ndani ya nyumba hiyo na kuwakuta wenye kaya wakiwa wanakula chakula, hawakuchukua kitu chochote. 


Majeruhi wametibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani, watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano dhidi ya tukio hilo.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi amesema jeshi la polisi linafanya msako mkali wa kuwatafuta watu waliohusika kwa namna moja au nyingine kwenye tukio hilo na kuhakikisha wanakamatwa, pia ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za wahalifu au uhalifu mapema ili wahalifu wawezwe kukamatwa na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi zinavyo elekeza.

Imesainiwa na. 

Sacp: Ahmed Msangi

Kamanda wa Polisi (m) Mwanza

Tanzania Yang’ara Mkutano Wa Kupambana Na Rushwa London

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema viongozi wakuu wa nchini na washiriki wa mkutano wa kimataifa wa kupambana na rushwa wamevutiwa na jitihada ambazo Tanzania imezichukua kukabiliana na janga hilo.

Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Mei 13, 2016) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wake kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

Waziri Mkuu alisema katika kikao cha kwanza kilichohudhuriwa na wakuu wa nchi na viongozi wa kitaifa wapatao 20, alipata fursa ya kuelezea jinsi Tanzania ilivyoweza kupambana na rushwa kwa kuzingatia vigezo vikuu vinne.

Waziri Mkuu alivitaja vigezo hivyo kuwa ni kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazohusu masuala ya rushwa; uanzishwaji wa mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai, mwaka huu; mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya wananchi na utaratibu wa kubaini wala rushwa kwa kushirikisha jamii ikiwemo kutunza siri za watoa taarifa.

“Ziko sheria ambazo zinafanyiwa kazi hivi sasa ambazo ni lazima zipitishwe na Baraza la Mawaziri kabla mahakama hii haijaanzishwa, zikishapitishwa na Baraza ndipo zitaanza kutumika,” alisema.

Akifafanua kuhusu mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya maendeleo, Waziri Mkuu alisema kwamba katika bajeti ya mwaka huu, Serikali imeweza kuongeza kiasi cha fedha zilizotengwa kwa shughuli za maendeleo kutoka asilimia 27 hadi kufikia asilimia 40.

“Kuongezeka kwa kiwango hiki ni ishara tosha  kuwa tumelenga kutoa huduma kwa Watanzania na muhimu katika rushwa ni udhibiti wa fedha hizo na kuhakikisha zinakwenda kwenye miradi; matuizi mazuri ya fedha za Serikali, matumizi mazuri ya fedha zinazochangiwa na wahisani ili ziweze kutekeleza miradi iliyokusudiwa,” alisema.

“Tumekubaliana na uwepo wa uwazi na kushirikishana taarifa hasa katika kupeana taarifa za makampuni yanayoanzishwa na kusajiliwa katika nchi zinazoendelea kama njia ya kudhibiti tabia ya nchi ndogo kama Ireland na Panama kupokea na kuficha fedha zinazotoka kwenye nchi zinazoendelea” alisema.

Alisema kila nchi imesisitizwa kutumia raia na kuwalinda watoa siri, kutumia mifumo ya kiintelijensia, kutumia wanasheria na kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya watu wanaokamatwa kwa masuala ya rushwa.

Waziri Mkuu alisema alipata fursa ya kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. David Cameron ambaye mbali na kupongeza juhudi za Serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kupambana na rushwa pia aliahidi kutoa mwaliko ili Tanzania iweze kushiriki kwenye mkutano mwingine wa masuala ya rushwa utakaofanyika Japan, Julai mwaka huu.

“Anataka Tanzania iende kwenye mkutano huo ili ikaelezee mafanikio iliyoyapata katika kukabili suala hili, ili pia nchi nyingine ziweze kuiga utaratibu ambao Serikali imeutumia hadi tukafanikiwa katika mapambano dhidi ya rushwa,” alisema Waziri Mkuu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ofisi yake haijahusika na kuandaa mkutano wa wanadiaspora waishio Uingereza kama ambavyo imedaiwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna watu maalum wamechaguliwa kushiriki mkutano huo.

Amesema mkutano huo umepangwa kufanyika kesho (Jumamosi, Mei 14, 2016) na uko wazi kwa Watanzania wote kushiriki ili waje kusikiliza nchi yao imefanya nini na kama kuna masuala yanahitaji ufafanuzi, watapatiwa fursa hiyo.

“Kulikuwa na hofu ya watu wanaotoka mbali kutoweza kushiriki sababu ya gharama, lakini nasema yeyote mwenye uwezo wa kuja aje ndiyo maana tumeuweka muda wa asubuhi ili watu waweze kushiriki na kuwahi kurudi makwao,” alisema.

IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU

IJUMAA, MEI 13, 2016.

Rais Magufuli Afanya ziara ya Kushtukiza Uwanja wa Ndege Dar es salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja dhidi ya dosari za ukaguzi zilizopo katika kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (Terminal One) Dar es salaam.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 13 Mei, 2016 alipofanya ziara ya kushtukiza katika uwanja huo na kubaini kuwa mashine za ukaguzi za sehemu ya kuwasili abiria na mizigo hazifanyi kazi kwa muda mrefu.

Maafisa wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere waliokuwa wakitoa maelezo juu ya hali ya kitengo cha ukaguzi wa mizigo na abiria katika uwanja huo, walikuwa wakitoa taarifa zinazotofautiana kuhusu utendaji kazi wa mashine za ukaguzi, hali iliyosababisha Dkt. Magufuli aamue kuiagiza wizara husika kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuchukua hatua mara moja.

“Unajua mimi sipendi kudanganywa, ni vizuri uzungumze ukweli tu, kwa nini nimeanzia hapa huwezi ukajiuliza? eeeh sasa sipendi kudanganywa, ukinidanganya nitachukia sasa hivi, wewe umenidanganya kwamba hiyo ndio mbovu na hii ndio nzima, nikawaambia muiwashe hiyo nzima, akaja huyu mwenzako amezungumza ukweli kabisa, akasema hii ni mbovu kwa miezi miwili." Dkt. Magufuli aliwahoji Maafisa wa uwanja wa ndege

“Kwa hiyo mizigo inayoingia humu huwa hamuikagui kwa namna yoyote ile, kwa hiyo mtu nikiamua kuja na madawa yangu ya kulevya, nikaja na dhahabu zangu, na almasi zangu na meno ya tembo kwa kutumia hizi ndege ndogondogo napita tu” Rais Magufuli aliendelea kuwabana maafisa hao wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara hii ya kushtukiza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Jijini Kampala nchini Uganda ambako jana alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

Habari Zilizopo Katika Magazeto ya Leo Jumamosi ya May 14

Nape Nnauye Asulubiwa Bungeni ......Wabunge Wamwita ni Waziri Mzigo ( Lumbesa)

$
0
0
Wabunge wamemcharukia Waziri wa Habari, Nape Nnauye kwamba aliwahi kuwaita mawaziri wa Serikali iliyopita mizigo, lakini yeye amezuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, ili wananchi washindwe kumpima kama ni mzigo au lumbesa. 

Hayo yalijitokeza jana wakati wabunge walipochangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari kwa mwaka 2016/2017, iliyowasilishwa bungeni na Waziri Nape. 

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) alieleza kushangazwa na hatua ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhimiza wananchi kudai risiti wanaponunua bidhaa, lakini haitaki wananchi waone inavyopanga matumizi yake. 

Alisema Nape akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, aliwaita baadhi ya mawaziri ni mizigo, lakini amepewa wizara hiyo amezuia mijadala ya wazi ambayo ingesaidia wananchi kumpima.

“Nilipoona amepewa wizara ya habari nikajua ataruhusu mijadala ya wazi ili tumuone yeye kuwa hatakuwa mzigo, lakini yeye akawa lumbesa. Hilo amelizuia kwa hiyo tunashindwa kumpima,” alisema. 

Alisema waziri huyo hawezi kukwepa lawama ya hicho kinachoendelea cha kuzuia matangazo ya Bunge, kwa vile wanaopiga picha na kuhariri taarifa zinazorushwa ni watumishi wa TBC. 

Udhibiti wa Bunge 
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (Act-Wazalendo), alisema kuwa wabunge wote waliopinga Bunge kutoonyeshwa ‘live’ na kusababisha mtafaruku bungeni, wameitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge. 

“Wabunge hapa tulisimama tukapinga na wapo waliounga mkono, lakini kiti chako kimetuita wabunge wote tuliopinga kauli ya Serikali kwenye kamati ya maadili. Jana mimi nimepata barua,” alisema Zitto. 

“Kwamba mnatubana kusema. Mnazuia Bunge lisionekane. Hata kutoa maoni ndani ya Bunge tunakwenda kuhojiwa? TBC ni chombo cha umma, siyo chombo cha Serikali, inaendeshwa kwa kodi za wananchi,” alisisitiza. 

Baada ya mchango huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alisema si kweli wabunge hao wanahojiwa kutokana na michango yao, bali wanahojiwa kutokana na mambo waliyoyafanya kwa kutotii maagizo ya kiti wakati wa mjadala wa ‘Bunge Live’. 

Kwa upande wake, Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), aliunga mkono hoja ya Zitto ya kuifanya TBC iendeshwe kama inavyoendeshwa BBC kwa kupewa  leseni maalumu. 

Pia, aliitaka Serikali kupeleka muswada bungeni utakaowabana wamiliki wa vyombo vya habari kuwa na mikataba na waandishi wanaowaandikia, pia, akadai baadhi ya vyombo haviwalipi waandishi wake. 

Hata hivyo Mbunge wa Viti Maalumu, Agness Marwa (CCM) alitetea uamuzi wa Serikali kuondoa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, akisema wabunge wanaodai hilo ni wale waliokuwa wakiuza sura. 

Katika hatua nyingine, Waitara alisema kitendo cha Nape kuwaalika wabunge kwenye muziki, baada ya bajeti yake kupita ilikuwa ni kuwahonga. 

Juzi jioni wakati akitoa matangazo kabla ya kuahirisha Bunge, Naibu Spika alisema baada ya kupitisha bajeti ya Wizara ya Habari, wanamuziki Diamond Plutnum na King Kiki watatumbuiza katika viwanja vya Bunge. 

“Mnaposema mnabana matumizi hao wanamuziki wameletwa kwa gharama za nani,” alihoji mbunge huyo.

 “Wabunge wote ambao wataenda katika hiyo miziki ili kuunga mkono habari ya Nape mtakuwa mmekula rushwa,” alisisitiza Waitara, kauli ambayo ilimfanya Naibu Spika, Dk Tulia kufafanua, akisema suala hilo lilitangazwa bungeni kama mengine, lisiingizwe kosa la jina la rushwa. 

Upinzani na udikteta 
Msemaji mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Joseph Mbilinyi, alisema kitendo cha Serikali kuminya uhuru wa habari ni kuelekea kwenye udikteta.

 “Kana kwamba haitoshi, Serikali sasa imezuia Televisheni ya Umma, inayoendeshwa na kodi ya wananchi (TBC1) kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mijadala inayofanyika bungeni. Dalili hizi siyo njema kwa ukuaji wa demokrasia na uhuru wa habari hapa nchini na zinatoa taswira ya utawala wa ki-dikteta,” alisisitiza. 

“Tunaitaka Serikali kuliomba radhi Bunge hili, kwa kosa la kuminya uhuru wa habari kinyume na Katiba na kuviacha vyombo vya habari hususan vya umma kufanya kazi zao za kuhabarisha umma kwa uhuru,” alisema.

Lipumba Amvaa Rais Magufuli.....Asema Vitisho Vitaangamiza Uchumi wa Taifa, Ampigia Hesabu za Kiuchumi Duniani Kuhusu Sukari

$
0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameeleza kuchoshwa na utendaji wa Rais John Magufuli katika kukabiliana na changamoto za kiuchumi.

Prof. Lipumba alitoa kauli hiyo jana  mbele ya waandishi wa habari  katika Ofisi Kuu ya CUF iliyopo Buguruni, Dar es Salaam.

Katika kukabiliana na changamoto za nchi hususani sekta ya uchumi, Prof. Lipumba amemshauri Rais Magufuli kutafuta ushauri sambamba na taratibu za kujenga uchumi wa soko shirikishi kutoka kwa Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu.

Alisema, uzoefu wa Rais Mkapa wa kujenga utawala wa serikali unaweza kumsaidia kufanya uamuzi sahihi utakayosaidia wananchi badala ya kukagandamiza.

Mchumi huyo alieleza kuwa, vitisho na ubabe wa Rais Magufuli vinaweza kuwaogopesha watendaji wake wakiwemo mawaziri na hivyo kushindwa kumueleza hali halisi na kwamba, kitendo hicho kinaweza kuathiri maendeleo ya nchi.

“Kuna dalili kwa baadhi ya watendaji wa serikali hasa mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya za kushindwa kutoa fikra zao zenye lengo la kuimarisha uchumi wa nchi au kueleza hali halisi iliyopo kwa kuhofia vitisho vya rais ili wasitumbuliwe,” amesema.

Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo wakati nchi ikiwa kwenye sintofahamu ya upatikanaji wa sukari ambapo kwa mujibu wake (Lipumba), uhaba huo umesababishwa na agizo la rais la kuzuia uingizwaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.

“Agizo alilolitoa Rais Magufuli Februari 28, 2016 wakati akiwashukuru waandishi wa habari, wasanii na makundi yaliyoshiriki kwenye kampeni zake za uchaguzi 2015 ndilo lililosababisha haya,” alisema na kuongeza;

“Kauli ya serikali ya kuzuia utolewaji wa vibali vya uingizwa wa sukari kutoka nje ndiyo iliyosababisha upungufu wa sukari, asiuaminishe umma kuwa sababu ni wafanyabiashara kuficha sukari.

“Kwa mwenendo huu nchi haitaendelea kutokana na kwamba badala ya vyombo vya dola kushughulikia masuala ya msingi ili kuleta tija katika maendeleo ya Taifa, vinahaha kutafuta sukari zilizofichwa.”

Alitoa mfano wa kitendo cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) cha kutafuta wafanyabiashara wanaoficha sukari badala ya kushughulika na masuala nyeti ya ubadhilifu wa mali za umaa kama Tegeta Escrow.

“Wafanyabiashara wanaopata kibali na wanaopitisha sukari kwa magendo wanapata faida kubwa kwa sababu bei ya sukari katika soko la dunia mwezi Agosti 2015 ilikuwa Dola za Marekani 250 kwa tani moja,” amesema.

Alifafanua kuwa, kama dola moja ni sawa na Sh. 2000 tani moja ya sukari iliuzwa Sh. 500,000 sawa na Sh. 500 kwa kilo moja na kwamba, ukiongeza na gharama za usafiri kila kilo moja ya sukari itafika kwa Sh. 600.

“Wafanyabiashara wakubwa na wa kati wanaoingiza sukari nchini hupata faida kubwa ukilinganisha na viwanda vya ndani kutokana na kwamba, uzalishaji sukari viwandani unagharimu mtaji mkubwa na kupelekea bei kuwa kubwa na kusababisha kupoteza soko,” alisema.

Alishauri kuwa, kama serikali ina lengo la kulinda viwanda vya ndani ihakikishe inaanda mfumo wa mnada wa ugawaji wa leseni ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara na viwanda kupata leseni za kuingiza sukari inayotoka nje ili viwanda vipate masilahi pamoja na wafanyabiashara.

“Ingawa utolewaji wa vibali utaathiri viwanda vya ndani kutokana na kushindwa kushindana na wafanyabiashara, ni vema serikali ikatoa vibali kwa watu wote,” alisema.

Kama serikali inataka kujenga uchumi wa viwanda haina budi kutoa motisha kwa wawekezaji ili wavutiwe kuwekeza katika sekta zote nchini.

“Rais anahitaji aelewe uchumi wa soko shirikishi, awape nafasi wahusika, asifanye maamuzi kwenye mikutano ya siasa au hadhara,” alisema.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images