Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mbunge wa Ulanga, Godluck Mlinga (CCM) Atoa Tuhuma nzito kwa TRA, TCRA, EWURA

$
0
0
Mbunge wa Ulanga, Godluck Mlinga (CCM) ameyatuhumu mashirika ya umma ambayo hayajajiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwa watendaji wake wakuu wamepewa malipo ya asilimia 10 ili mashirika hayo yajiunge na kampuni binafsi za bima.

Ameyataja baadhi ya mashirika hayo ya umma yaliyokaidi kujiunga na NHIF licha ya kulazimishwa kisheria kuwa ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Yapo mashirika ya umma yanakataa kujiunga na NHIF wakati sisi wabunge tumejiunga, wao ni nani? Wakubwa wao wanapata asilimia 10 na wanajiunga na kampuni za bima ya afya binafsi…

“Mimi niliwahi kuwa Compliance Officer wa NHIF nikaenda TRA, nikawaeleza umuhimu wa kujiunga NHIF unachangia pesa kidogo unapata huduma nyingi lakini bosi wao akanijibu pesa si tatizo na afadhali ametumbuliwa huyo bosi wao, yule angekuwa ofisini kwangu asingetoka,” alisema Mlinga na kuongeza:

“Kila sehemu wananitaja Mlinga Mlinga, napata vitisho vingi lakini serikali inanilinda na kama jeshi (JWTZ) limeweza kusambaratisha M23 itashindwa kunilinda mimi…wengine wananiita teja hivi teja anavaa suti iliyonyooka kama mimi, siwezi kukasirika kwa sababu si kweli lakini wangeniita mbilikimo ningekasirika kwa sababu kweli.”

Mbunge huyo alitaka serikali ikomeshe tabia ya wanaume kubaka wazee na kufafanua “najiuliza wanawake wa mikoa yenye ubakaji wa wazee ni wagumu kuelewa hadi wazee wabakwe?”

Naye Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby (CCM) amesema sasa ataanza kuacha kuwashawishi wananchi wake kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kutokana na mfuko huo kutopeleka dawa na chanjo za watoto kwenye vituo vya afya, badala yake inapeleka kondomu na vifaa visivyo muhimu kwa wananchi.

Magari ya Washawasha Yazua Mjadala Bungeni

$
0
0

Magari ya washawasha jana yaliibua mjadala bungeni baada ya mbunge  wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema) kubanwa athibitishe kauli yake aliyoitoa  kuwa serikali ilinunua magari ya Polisi ‘Washawasha” 777 wakati ilitumia 50 pekee wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita.

Mbunge huyo alitakiwa kuthibitisha hilo na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kwa kupeleka uthibitisho au kufuta kauli yake baada ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Massauni kuomba mwongozo kupitia kanuni ya 64(a) na 63(1) akiomba mwongozo wa hatua gani anaweza kuchukuliwa Lyimo.

“Kanuni zipo, zinampa haki kila mbunge na Naibu Waziri ameomba mwongozo kwa kanuni ya 64(a) na 63(1) sasa kwa kuwa Susan hayupo hapa sasa hivi, akirejea jioni mwongozo wangu ni kwamba afute maneno yake au alete uthibitisho,” alisema Mwenyekiti huyo wa Bunge.

Lyimo katika mchango wake kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, alisema serikali imenunua magari ya ‘Washawasha” 777 mwaka jana wakati wa Uchaguzi Mkuu lakini yaliyotumika ni 50 pekee.

Tanzia: Msanii wa Vichekesho Mohammed Abdallah (Kinyambe) Amefariki Dunia

$
0
0
Mwigizaji wa comedy Mohammed Abdallah maarufu "Kinyambe" amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya mkoa wa Mbeya alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Mungu amlaze mahali  mahali pema peponi -Amina

Chadema wabeza utumbuaji majipu wa Magufuli, wadai bora Kikwete

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Vincent Mashinji ameponda mtindo wa utawala wa Rais John Magufuli wa utumbuaji wa majipu akisema umekosa dira na kinachoendelea ni utashi wa kisiasa na kukurupuka.

Kazi kubwa aliyoifanya Rais Magufuli tangu aingie madarakani, katika kipindi cha miezi sita sasa ni kubana matumizi ya fedha za umma kwa kufuta safari za nje za watumishi, kuzuia mikutano kufanyika mahotelini, kuhimiza mamlaka husika kukusanya kodi, kupambana na watumishi hewa, kuwasimamisha au kutengua uteuzi wa watendaji aliodai kuwa ni wazembe na walioshindwa kwenda na kasi yake pamoja na kuwashughulikia wala rushwa na wahujumu uchumi.

Katika namna inayoonekana ni kufuata upepo wa kisiasa, Rais Magufuli huwatumbua baadhi ya watendaji kwenye mikutano ya hadhara.

“Kuna vitu vingi vinafanyika lakini hatujui kipi ni kipi na wapi tunaelekea. Kuna mambo mengi yanafanyika, lakini hakuna hata mtu mmoja katika nchi hii anayejua Taifa hili lina mpango gani na linaelekea wapi,” Mashiji anakaririwa na gazeti la Mwananchi.

Huku akifananisha utawala wa Rais Magufuli na wa mtangulizi wake Jakaya Kikwete, Dk Mashinji alisema walau ahadi ya “Maisha bora kwa kila Mtanzania” ilikuwa inaeleweka hata kama haikutekelezeka.

“Rais Kikwete alitwambia Maisha bora kwa kila Mtanzania na tulijua maisha hayo yanapatikana kwa kupambana wenyewe na tulipambana. Lakini sasa hatujui tunaelekea wapi. Hapa kazi tu! Umemfukuza huyu kazi halafu nini kitaendelea? Keshaondoka kakuacha, unaajiri mwingine? Tunahitaji mtu wa kujibu hayo maswali. Nchi yote sasa inavurugwa. Halmashauri zinavurugwa,” alisema.

Katibu mkuu huyo alisema kwa sasa kila kitu kinavurugwa jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa nchi na kwamba inaonekana wazi nchi inaelekea sehemu ambayo mbele kuna giza.

Akitoa mfano wa mfumo ulivyobadilika alisema hivi sasa wakurugenzi wa halmashauri wametangaziwa kusitisha mawakala wote wanaokusanya ushuru badala yake wakusanye wenyewe.

 “Hivi tujiulize halmashauri ina wafanyakazi wangapi ambao wana uwezo wa kukusanya mapato yake? Huku ni kudanganyana,” alisisitiza Dk Mashinji.

Hata hivyo, Dk Mashinji alisema hawapingi anachokifanya bali tofauti yao na Rais Magufuli ni namna ya kukabiliana na jambo. 

“Sisi tunaamini katika mfumo na siyo mtu. Huwezi leo kuniambia meya anaiba Sh5 bilioni halafu chama kisijue. Kwa nini chama kisimwondolee udhamini kabla?” alihoji.

 “Anachofanya sasa ni kudhibiti na siyo kurekebisha mfumo. Rais Magufuli hana dhamana na Mungu, asipokuwepo sioni wa kuendeleza falsafa zake. Kwa nini kusiwe na mfumo madhubuti ambao upo kisheria na kila mmoja aujue na kuufuata?” alieleza.

Mpinzani wa Museveni , Dr Kiiza Besigye Akamatwa Baada ya Kujiapisha Kuwa Rais

$
0
0
Mpinzani mkuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye ambaye amekuwa akipinga ushindi wa Rais huyo, amekamatwa na polisi wa nchi hiyo baada ya jana kujiapisha kuwa Rais ikiwa ni siku moja tu (leo) kabla ya Museven kuapishwa.

Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa vizuizi  vya polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.

Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''.

Video hiyo ilisambazwa kwa kasi  kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliopita akiwaacha kwa mbali wapinzani wake wakuu, Kizza Besigye na Amama Mbabazi.

Kadhalika, Mahakama Kuu nchini humo ilihalalisha ushindi wa Museveni baada ya kutupilia mbali shauri la pingamizi la ushindi huo lililowasilishwa na Amama Mbabazi.

Rais Magufuli , Samia na Kassim Majaliwa Ziarani nje kwa Mpigo - Mwanasheria mkuu atoa ufafanuzi kuhusu kaimu Rais

$
0
0

Viongozi wakuu wote wa Taifa wako nje ya nchi katika ziara za kiserikali kwenye mataifa tofauti.

Rais John Magufuli aliwasili Uganda jana asubuhi kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Yoweri Museveni zinazofanyika leo na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan alikuwa Kigali, Rwanda kuhudhuria mkutano wa dunia wa uchumi.

Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Mwandishi wa Makamu wa Rais, Penzi Nyamngumi zimesema, Makamu wa Rais aliondoka nchini Jumanne akitokea Dodoma na angerejea kesho baada ya mkutano huo.

Kiongozi anayefuatia kwa wadhifa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisafiri juzi kwenda London, Uingereza kumwakilisha Rais Magufuli katika mkutano wa wakuu wa nchi kujadili mapambano dhidi ya rushwa.

Majaliwa katika ziara hiyo ameongozana na Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya anayepaswa kukaimu urais, alisema Makamu wa Rais amekwisha rejea nchini na yuko Mwanza.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 37 (3), inaeleza kuwa endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na Makamu wa Rais, kama naye hayupo, yatatekelezwa na Waziri Mkuu.

Hata hivyo, Ibara ya 37 (6) (b) inasema Rais hatahesabiwa kwamba hayupo iwapo atakuwa nje ya Jamhuri ya Muungano kwa kipindi cha saa 24.

Mtoto wa marehemu, Chacha Wangwe afikishwa kortini kwa makosa ya kimtandao.

$
0
0


BOB Chacha Wangwe (24), mtoto wa mwanasiasa marehemu Chacha Wangwe, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii.

Akisoma kesi hiyo namba 167, Paul Kagoshi mbele ya Waliarandwe Rema, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo alisema kuwa, Bob Chacha Wangwe amefikishwa mahakamani hapo kwa kutenda kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake Facebook.

Mshitakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo  tarehe 15 Machi na kwamba alichapicha maneno haya; “Tanzania ni ambayo….inajaza chuki wananchi … matokeo ya kubaka Demokrasia Zanzibar ni hatari zaidi ya muungano wenyewe…. Haiwezekani nchi ya Zanzibar kuwa koloni la Tanzania bara kwa sababu za kijinga.”

Mahakama Yaiamuru Kampuni ya Mawasiliano ya TIGO Kuwalipa Wasanii Hamis Mwinjuma 'MwanaFA' na Ambwene Yessaya 'AY' Bilioni 2.18

$
0
0
Mahakama ya hakimu mkazi Ilala imeiamuru kampuni ya mawasiliano Tigo, kuwalipa shilingi bilioni 2.18 marapa Mwinjuma 'MwanaFA' na Ambwene Yessaya 'AY', kwa kosa la kutumia nyimbo yao kama Caller Tune(Mwitikio wa simu) bila ruhusa wala mkataba.

Hukumu ya kesi hiyo iliyodumu kwa miaka 4 ilitolewa na hakimu mkazi wa mahakama hiyo  Juma Hassan. 

Ay na MwanaFA waliomba mahakama iwaamrishe Tigo kulipa fidia ya Billion 4.3 kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na gazeti la The Citize.

==>Taarifa zaidi kuhusu jambo  hili endelea  nayo hapo chini
A court has awarded two Tanzanian musicians Sh2.18 billion in special damages in a landmark ruling that could set a precedent in the application of the copyright law in the country.

The huge award was won by Bongo flava artistes Ambwene Yessaya “AY” and Hamisi Mwinjuma “MwanaFA” who had sued mobile phone company MIC Tanzania (Tigo), for unauthorised use of their music as caller tunes. A caller tune is a tone that is in the form of music that is heard by a person making a call as they wait for the person being called to answer the phone.

Ilala Senior Resident Magistrate Juma Hassan granted the award on April 11 after a four-year court battle between the parties. The award also includes a separate Sh25 million in general damages.

News of the fine against Tigo only came to light this week on Tuesday when the firm went to the High Court to block the execution of the award pending its appeal. History in the copyright field would be made should the High Court uphold the judgement by the Ilala District Court.

MwanaFA said it was time those who had in the past taken the basic copyright laws for granted realised that things have changed.

“This is a key moment in copyright in Tanzania. This is something that has been happening for quite a long time now mainly because of lack of knowledge and maybe because of the costs associated with such cases,” he said.

He added: “Nobody is supposed to use your work without your permission or agreement and if at all he has benefited then he is supposed to share with you according to the price tag you have set for your work.”

The mobile network operator has, however, filed for a stay of execution and has appealed against the judgment and decree for payment at the High Court. The appeal was initially set to be heard on Tuesday but was adjourned to tomorrow. The artistes claim that Tigo sold without permission in the form of caller tunes content that belonged to them without any agreement between the two parties. The two songs at the centre of the controversy are Dakika Moja and Usije Mjini, which were both done in collaboration by AY and MwanaFA.

Although there are no figures that were mentioned by both sides on the precise income derived from the sale of the two songs, the two artistes believe the company generated revenue.

According to the judgment, the artistes did not have any agreement with anyone to distribute the songs, they did not have an agreement with the defendant (Tigo) and neither did they contract a third party to handle this kind of distribution on their behalf.

The court in its decree states that the defendant infringed the rights of the plaintiffs over their registered joint authorship of musical work and in the process infringed the copyright and/or neighbourhood rights to which civil remedies are applicable.

The court, therefore, ordered the company to pay Sh 5 million as general damages and Sh2.16 billion as special damages in addition to the costs of the suit.

The artistes had in their application asked for damages totalling Sh4.3 billion, claiming that the defendant had generated a significant sum of income through the sale of their two songs to its subscribers across the country.

In recent years, mobile phone operators have been at the centre of a controversy over how much they pay artistes for using their content, with some singers claiming they were not benefiting from their work.

Customised mobile phone caller tunes in Tanzania are largely songs by Bongo Flava artistes.

According to the Journal of Intellectual Property Law and Practice, copyright subsisting in caller tunes and ringtones is similar to copyright protection in any other musical recording, comprising an underlying musical work and a sound recording which are protected under the Copyright Act.

This type of copyright protection in Tanzania is similar to those in South Africa, the United Kingdom, the United States and Jordan.

Picha: Diamond na Mafikizolo Wakiwa Ndani ya Ukumbi wa Bunge Leo

$
0
0
Kundi maarufu la muziki kutoka Afrika Kusini Mafikizolo pamoja na staa wa bongofleva Diamond Platnumz leo walipata mwaliko wa kuingia Bungeni Dodoma ambapo mastaa hawa wapo Dodoma kwa ajili ya kupiga burudani  Chuo kikuu cha Dodoma.

Rais Yoweri Museveni Aapishwa Rasmi Kuwa Rais wa Uganda

$
0
0
Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameapishwa Rasmi kuwa Rais wa nchi hiyo katika viwanja vya Kololo nchini humo na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Afrika akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutoka Tanzania.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Amwakilisha Rais Magufuli Kwenye mkutano wa Kupambana na Rushwa, London

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa kuingia kwenye ukumbi wa Lancaster House, London nchini Uingereza kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, Mei 12, 2016. Waziri Mkuu Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa nne kulia) akishiriki katika Mazungumzo Rasmi ya Wakuu wa Nchi katika Mkutano kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kwenye ukumbi Lancster House, London, nchini Uingereza Mei 12, 2016. Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tamko La Wizara Kulaani Mauaji Ya Watu 7 Jijini Mwanza Mwanza

$
0
0
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto imesikitishwa na tukio la mauaji ya watu saba wa familia moja waliokatwakatwa mapanga baada ya kuvamiwa nyumbani, katika kijiji cha Sima wilayani Sengerema, mkoani Mwanza, siku ya Jumatano usiku.

Wizara inalaani vikali mazingira ya mauaji ya watu hao wa familia moja, ambapo wauaji walivamia nyumba ya mama mjane na kumuuwa yeye mwenyewe, na watu wengine sita wakiwemo watoto watatu.  

Wizara inapongeza utayari wa uongozi wa mkoa wa Mwanza na jeshi la Polisi amabo waliweza kufika sehemu ya tukio ili kufuatilia mauaji hayo. Ni imani ya Wizara kuwa Polisi kwa ushirikiano wa wananchi wa wilaya ya Sengerama wataweza kuwasaka watuhumiwa wa mauaji na  kuwachukulia hatua kali.  

Wizara inawasisitiza wananchi kutoa taarifa ambazo zitasaidia kuwamata watuhumiwa ili kuondoa hofu miongoni mwa familia za kijiji cha Sima na wilaya ya Sengerema. Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kutarejesha imani na utulivu miongoni mwa wakazi wa Sengerema na hivyo kuweza kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa taifa.

Wizara inasisitiza kwamba  kila binadamu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa Sheria za nchi. Vitendo vya mauaji ya kikatili vinapotokea katika familia zetu vinasababisha hofu kubwa miongoni mwa wanafamilia. Mauaji hayo yanawakosesha amani wanafamilia na yanadhohofisha ari ya ndugu wa familia kufanya shughuli zao kwa amani.  

Wizara inaomba wanafamilia waliopoteza ndugu zao kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi makubwa, wakati Serikali ikiendelea na jitihada za kuwasaka watuhumiwa wa mauaji hayo.

Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
12/5/2016

Rais Magufuli Afanya Mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni Nchini Uganda

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Mei, 2016 amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni muda mfupi baada ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais huyo iliyofanyika katika uwanja wa Kololo Jijini Kampala.

Katika Mazungumzo hayo Rais Magufuli amempongeza Rais Museveni kwa kuapishwa kuwa Rais wa Uganda kwa kipindi kingine cha miaka 5 na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi Uhusiano, ushirikiano na udugu wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo.

Viongozi hao pia wamezungumzia mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima (Ziwa Albert) nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania ambapo pamoja na kuishukuru Uganda kwa uamuzi wake wa kuamua bomba hilo lipitie Tanzania, Rais Magufuli amemshauri Rais Museveni kufupisha muda wa ujenzi wa mradi huo, kwa kutumia mbinu inayojumuisha usanifu na ujenzi (Design and Construct method) na kutumia wakandarasi wengi watakaogawanywa katika vipande tofauti badala ya kutumia mkandalasi mmoja.

"Nashauri tutumie mbinu ya usanifu na ujenzi pamoja, hii ni njia ya haraka zaidi, na pia tugawe vipande vya ujenzi kwa njia yote ya bomba la mafuta yenye urefu wa kilometa 1,410 tunaweza kuwa na Wakandarasi watano mpaka sita ambao watatumia njia hiyo mpya ya usanifu na ujenzi.

"Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza muda utakaotumika kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta, inaweza hata kuchukua mwaka mmoja tu" Amesema Rais Magufuli.


Rais Magufuli amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo faida za mradi huo wa mafuta zitaanza kupatikana mapema badala ya kusubiri miaka miwili au mitatu ijayo, na kwamba hiyo itakuwa inaendana na kauli mbiu yake ya "Hapa Kazi Tu"Pia Rais Magufuli amemshukuru Rais Museveni kwa uamuzi wa nchi hiyo wa kuipa Tanzania umiliki wa asilimia 8 katika mradi huo wa bomba la mafuta.

Kwa upande wake Rais Museveni amesema amefurahishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo, na pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake kubwa ambazo amezifanya katika mapambano dhidi ya rushwa nchini Tanzania.

"Napenda kasi yako ya uongozi, napenda jinsi unavyopambana na rushwa, kwa sababu rushwa ilikuwa inazaa matatizo mengine kama vile ucheleweshaji wa mizigo bandarini na vikwazo vya mpakani, hivyo nakupongeza sana kwa hilo" Amesema Rais Museveni.

Katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais Museveni iliyofanyika kabla ya mazungumzo hayo, pamoja na Rais Magufuli viongozi wengine kutoka Tanzania waliohudhuria ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa na Mkewe Mama Salma Kikwete na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Suzan Kolimba.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU
Kampala
12 Mei, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 13

Mafikizolo Toka Sauzi Na Diamond Platinum's Wafunika Vibaya Tamasha La Vodacom Chuo Kikuu cha Dodoma

$
0
0
Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul “Diamond Platinum’s” pamoja na kundila muziki la Mafikizolo wakiimba wimbo wao wa Color of Afrika wakati wa Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul “Diamond Platinum’s” akiwaimbia kwa hisia wakati wa mashabiki wake waliofika kwenye Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana.
Nyomi ya  mashabiki wa muziki waliofika kwenye Tamasha la Vodacom Kichuo zaidi lillilofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Msanii wa muziki wa kundi la Mafikizolo kutoka Afrika ya kusini,Theo  Kgosinkwe  akionyesha umahiri wake wa kucheza muziki  katika Tamala la Vodacom kichuo zaidi lililofanyika  chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) jana

Maadhimisho Ya Miaka Sita Ya Chama Cha Watanzania Waliosomea China (CAAT)

$
0
0

Chama cha Watanzania Waliosoma China kwa kiingereza China Alumni Association of Tanzania (CAAT) kinapenda kukukaribisha katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 6 (2010-2016) tokea kilipozaliwa.

Sherehe hiyo itafanyika katika ukumbi wa Cardinal Laurian Rugambwa Social Centre pembezoni mwa kanisa la Mtakatifu  Peter (St Peter), Oysterbay Ijumaa ya tarehe 20-May-2016 kuanzia saa 8 alasiri.

Sherehe hiyo itahudhuriwa na viongozi wakubwa kutoka serikalini na baadhi ya wageni kutoka ubalozi wa China.

Pamoja na burudani mbalimbali, maadhimisho hayo yatakuwa na hotuba kutoka viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wa ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China.

Kwenye sherehe hiyo pia utafanyika uzinduzi wa tovuti (website) ya CAAT. Baada ya chakula cha pamoja cha jioni, vilevile kutakuwa na fursa ya wafanyabiashara, wajasiliamali na wafanyakazi waajiriwa kuonyesha bidhaa au matangazo ya bidhaa au huduma wanazotoa.

Dhima kuu ya tukio hilo ni:
•Utambulisho wa jumuia ya CAAT ambayo inajumuisha wataalam wa taaluma mbalimbali waliohitimu mafunzo yao katika Jamhuri ya Watu wa China
•Kubaini na Kuainisha fursa zinazopatikana Tanzania na China kupitia CAAT
•Maonyesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za biashara za wanajumuia.

Wote mliopata kusoma China mnakaribishwa. Hakutakuwa na kiingilio.

Unaweza kushiriki kwa kuthibitisha uwepo wako kwa kupiga simu kwa Katibu Mtendaji wa CAAT kwa kupitia 0783-992020 au 0715-200090 au emailgsoreku@yahoo.com

Asante
 George Oreku
Katibu Mkuu
Chama cha Watanzania Waliosoma China (China Alumni Association of Tanzania)
05-May-2015

Mbunge Apewa Siku 3 Atoe Ushahidi wa Magari 777 ya Washawasha

$
0
0

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amempa siku tatu Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema) awasilishe mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge, maelezo ya utetezi dhidi ya madai aliyotoa bungeni kuhusu Serikali kununua magari ya washawasha 777.

Ndugai alitoa amri hiyo kutokana na mwongozo ulioombwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni juzi akitaka Lyimo athibitishe au afute kauli yake juu ya madai hayo wakati serikali imenunua magari 32.

“Hata kwa akili ya kawaida haiwezekani Serikali ikaagiza magari yote hayo 777 ya washawasha. Ninachokumbuka mimi Waziri huyu aliwahi kusema hapa bungeni kuwa magari hayo 777 ni idadi ya magari yote ya aina mbalimbali yaliyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya polisi,” alisisitiza Ndugai.

“Sasa nakutaka uniandikie rasmi majibu vizuri kuhusu kauli yako hii, nakupa siku tatu uwe umeniletea na baadaye nitaipeleka taarifa yako kwa Kamati ya Maadili ya Bunge, ili kujadili suala hili kwa mapana,”alisisitiza Ndugai.

Awali mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, Ndugai alimpatia mbunge huyo nafasi ya ama kufuta kauli yake hiyo au aithibitishe kabla ya hatua za kikanuni za Bunge hazijachukuliwa dhidi yake.

Lyimo alikataa kufuta kauli hiyo na kudai kuwa anao uthibitisho juu ya idadi hiyo ya magari aliyoitamka na kusisitiza kuwa amenukuu taarifa za idadi hiyo kupitia taarifa iliyotolewa na mtandao wa Jamii forum pamoja na taarifa za Hansad za Bunge.

“Mheshimiwa Spika mimi ni mtu mzima siwezi kwenda kwa hisia za watu, ni kweli jana niliombewa mwongozo bahati mbaya sikuwepo ndani ya Bunge. Nathibitisha kauli yangu na wala siifuti kwa kuwa nina uhakika na idadi ya magari niliyoisema,” alisisitiza mbunge huyo.

Alisema kwa mujibu wa Kanuni ya 63 (2) ya Bunge, mbunge hatasema uongo endapo chochote atakachokisema ndani ya Bunge atakuwa amekirejea kwenye chombo cha habari au taarifa za Bunge.

Wabunge 53 Chadema na CUF Wajitoa TWPG Baada ya Kutoombwa Radhi na Mbunge wa CCM Aliyedai Wamepata Ubunge Kwa Kufanya Mapenzi

$
0
0

WABUNGE wanawake 53 wa kambi ya upinzani kutoka vyama vya CUF na Chadema wamejitoa kwenye Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG) baada ya kutoombwa radhi na Mbunge la Ulanga, Godluck Mlinga (CCM) aliyesema wabunge hao kutoka Chadema walipata ubunge kwa njia ya mapenzi.

Mlinga alisema wabunge wanawake ndani ya Chadema, walipata nafasi hiyo baada ya kuwa ‘baby’ wa watu. Alitoa kauli hiyo wakati anachangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni Mei 5 mwaka huu.

Sambamba na hilo, alisema wabunge wa ndani ya chama hicho wamo pia wenye uhusiano wa jinsia moja. Hata hivyo hakuwataja kwa majina wabunge hao.

“Kila mwanamke ndani ya chadema kaingia ubunge kwa sifa yake lakini sifa kubwa ni lazima uwe baby (mpenzi) wa mtu. Ndani ya Chadema kuna wapenzi wa jinsia moja,” alisema Mlinga. 

Katika barua yao ya kujitoa jana iliyosainiwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa niaba ya wabunge wenzake wa kambi ya upinzani na nakala kupewa Spika, Job Ndugai, ilieleza kuwa kauli ya Mlinga inadhalilisha wabunge hao, utu na heshima ya mwanamke.

“Licha ya juhudi zilizofanywa na wabunge wa upinzani za kutaka mbunge husika(Mlinga) afute kauli yake , juhudi hizo hazikuzaa matunda kutokana na Naibu Spika(Tulia Ackson) kupuuza miongozo iliyokuwa ikiombwa.

"Na kikubwa alichokifanya baada ya mbunge (Mlinga) kumaliza kutukana ni kuwataka watu wa hansard wafute kwenye kumbukumbu za Bunge, kitu ambacho ni kinyume na matakwa ya Kanuni za Bunge,”alisema Mdee kwenye barua hiyo iliyosainiwa na wabunge wa CUF 10 na wa Chadema 43.

Alisema wabunge wa upinzani walisononeshwa zaidi na wabunge wenzao wanawake wa CCM, wakiongozwa na aliyekuwa Katibu wa TWPG, Angela Kairuki na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge,Vijana, Ulemavu na Ajira, Jenista Mhagama kushangilia udhalilishaji huo.

“Ukimya wenu kwenye matukio haya na ushiriki wenu katika kushangilia wakati wanawake wanadhalilishwa inatufanya tuhoji mantiki ya uwepo wetu katika umoja huu ambao tunaambiwa malengo na dhamira yake ni kutuunganisha wanawake katika kumkomboa, kumpigania na kulinda haki na utu wa mwanamke,” alisema Mdee.

Wabunge hawa wanajitoa licha ya baada ya tukio hilo, umoja huo kupitia kwa Mwenyekiti wake, Margaret Sitta kulaani na kueleza kutokubaliana na tabia ya baadhi ya wabunge ya kutumia lugha za matusi, kejeli ,dharau na udhalilishaji wa wabunge wanawake kutoka Chadema kuwa wamepata nafasi hiyo kwa njia ya kuwa ‘baby’ wa mtu.

CCM Yakanusha Kuhusika na Utapeli

$
0
0
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimelaani vikali tabia ya baadhi ya watu wanaotumia vibaya jina la Chama hicho kuwatapeli wananchi kutoa fedha ili wapatiwe nafasi za ajira katika Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) jambo ambalo sio sahihi.

Kimewataka wafuasi wa Chama hicho na wananchi kwa ujumla kuacha tabia ya kuwaaminisha watu  kwamba CCM inatoa nafasi mbali mbali za ajira kwani kufanya hivyo ni kuwagombanisha viongozi na wananchi wao.

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai alisema Chama hicho hakihusiki na utoaji wa ajira ya aina yoyote, hivyo watu wanasambaza utapeli huo kwa njia ya simu na mitandao ya kijamii lengo lao ni kuchafua taswira njema ya chama hicho.

Akifafanua zaidi Ndugu Vuai amesema suala la ajira katika taasisi za kiserikali na binafsi zinazolewa kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa hasa baada ya kutolewa matangazo maalum kulinga na nafasi za ajira zilizopo na sio kutumia simu za mkononi kuwapigia watu ili waweze kutoa fedha kwa ajili ya kuwapatiwa ajira hizo.

“Nimepigiwa simu nyingi na baadhi ya watu wangu wa karibu wakiniuliza juu ya taarifa za Chama kuuza nafasi za ajira, taarifa ambazo nimezipokea kwa mshangao mkubwa kwani ndani ya chama chetu hakuna utaratibu huo. Nawataka wananchi kuwa macho na makini na matapeli wanaotumia hila tofauti kuwaadaa watu kwa nia ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu” Alisisitiza Vuai.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar, alitoa wito kwa wananchi kuwa makini na matapeli hao na mtu yeyote atakayepigiwa simu na kuambiwa atoe kima chochote cha fedha kwa lengo la kupatiwa ajira na CCM asikubali kufanya hivyo na badala yake atoe taarifa haraka katika vyombo vya dola, ili sheria ichuke mkondo wake.

Aliwasihi wananchi kuendelea kuamini  kwamba CCM ni Chama kilichokomaa kisiasa na uzoefu mkubwa wa kusimamia demokrasia ya kweli, usawa, haki, utawala bora, a hivyo hakiwezi kujihusisha na vitendo viovu kwa jamii.
 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM alisisitiza kuwa suala la ajira za JWTZ, Idara Maalum za SMZ na zile za Taasisi nyengine za seriikali, zote hizo zinatolewa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW).
 
Alisema kuwa haiwezekani hata kidogo Chama hicho (CCM) kitowe ajira na kuongeza kuwa taarifa hizo zinazosambazwa na watu ni za kitapeli na zinalenga kuchafua jina la Naibu Katibu Mkuu huyo pamoja na CCM kwa jumla.
 
Aliwaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo na wawe macho na utapeli wa aina hiyo uliozagaa Zanzibar na maeneo mengine nchini, kwani unafanywa na wapinga maendeleo ya CCM na Taifa kwa jumla.

Sakata la Sukari: Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kutetea Walaji Tanzania (TCSA) Atoa Tahadhari

$
0
0
Wakati Serikali ikiendelea kuwaadhibu wafanyabiashara wakubwa kwa madai ya kuficha sukari katika maghala, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kutetea Walaji Tanzania (TCSA), Benard Kihiyo amesema hatua za kuwasaka ni nzuri lakini itaharibu usambazaji na upatikanaji wa bidhaa hiyo.

Kauli ya Kihiyo imekuja wakati msako dhidi ya wanaoficha sukari ukiwa umepambamoto. Jana, mfanyabiashara wa Arusha, Romanus Macha alisalimisha tani 33 za bidhaa hiyo serikalini.

Akizungumza baada ya kutembelewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Arusha, Macha alisema ameamua kusalimisha sukari hiyo ikiwa ni kufuata agizo la Serikali. Alisema alitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa na wa wilaya kuwa ana sukari.

“Mfuko wa kilo 50 nilinunua kwa Sh90,000, nilitegemea kuuza Sh92,000. Kwa kuwa nimeshaisalimisha nasubiri bei elekezi ya Serikali,” alisema Macha.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Daniel Machunda alisema maofisa wake hawakukuta dosari kwenye sukari hiyo lakini wanasubiri ripoti ya polisi kabla ya kuruhusu iuzwe.

“Pia tunataka kujua kama sukari hii ina ubora kwa matumizi ya binadamu,” alisema Machunda.

Katika msako huo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na polisi jana iliwakamata wafanyabiashara tisa waliokuwa wakiuza sukari kinyume na bei elekezi ya Sh1,800 kwa kilo.

Tani 27 zakamatwa
Jijini Dar es Salaam, mifuko 1,092 sawa na tani 27 za sukari ilikamatwa jana maeneo ya Manzese baada ya msako ulioendeshwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni.

Msako huo ulioongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Salum Hapi ulibaini shehena hiyo katika maghala zaidi ya matatu yasiyo rasmi.

Hapi alisema, baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema, waliendesha operesheni hiyo na kuwabaini walioficha sukari.

“Tumeikuta kwenye viroba vya kilo 25 katika maghala mbalimbali likiwamo la Mtaa wa Mferejeni,’’ alisema.

Wataalamu wakosoa 
Wakati polisi na viongozi wengine wakihaha kuwasaka wafanyabiashara hao, wataalamu wameeleza kuwa janga la sukari linatokana na kukosekana kwa sera ya kumlinda mlaji.

Kihiyo alisema kama sera hiyo ingekuwapo, wafanyabiashara wasingekuwa na nguvu ya kuuza sukari kwa bei wanayotaka au kufanya bidhaa hiyo iwe adimu sokoni.

Hata hivyo, maoni hayo yalitofautiana na ya mtaalamu wa masuala ya viwanda na biashara, Adam Zuku ambaye alisema suala la sukari lina siasa ndani yake.

Zuku ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi wa maendeleo ya viwanda wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), alishangaa kuona sukari iliyokamatwa inaachiwa kwa madai kwamba, wafanyabiashara husika hao walikuwa hawajakamilisha taratibu za kuitoa.

“Mbona wakati tunalalamika hakuna sukari hawakusema kwamba wameagiza sukari wanamalizia taratibu ili isambazwe madukani?” alihoji Zuku.

Alisema jambo hilo linatokana na wafanyabiashara hao kujali masilahi yao binafsi. “Wanalalamika kisiasa tu,” alisema Zuku.

Alisema Serikali isipoendelea kuvalia njuga suala hilo, hata viwanda vya sukari vya ndani vitakufa.

Pia, alisema Serikali inatakiwa kuwa na takwimu halisi ya sukari inayohitajika nchini ili kusiwe na mkanganyiko linapotokea tatizo kama hilo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images