Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Madaktari Wataka Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) Itumbuliwe

$
0
0

Waganga wafawidhi wa Manispaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, wamesema Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) ni “jipu” linalohitaji kutumbuliwa kutokana na kuwa na mfumo usioridhisha wa utoaji huduma za dawa.

Wakizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, madaktari hao walisema MSD inahitaji kufanyiwa marekebisho makubwa ya utendaji kazi wake, kama siyo kutumbuliwa kutokana na kuwafanya wafanye kazi katika mazingira magumu na yasiyo na dawa.

Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Azizi Msuya alisema changamoto iliyopo ni upatikanaji wa dawa na mara nyingi wanachoomba MSD sicho wanachopata na kinawaletea uhasama na chuki kwa wagonjwa.

“Wao wananunua palepale na sisi tungeruhusiwa tungenunua. Maduka kama Salama, kopo moja la dawa aina ya paracetamol ni Sh7,000, lakini tukinunua kwao inakuwa Sh15,000 la sivyo turuhusiwe kununua wenyewe kuliko kusubiri dawa mwezi mzima,” alisema Msuya.

Alisema unaweza kuomba dawa aina nyingi zikiwamo za kuponya maisha haraka kama za kuzuia damu kutoka, kuzuia kifua kubana, ukapata nyingine hizo ukakosa. Hivyo kuna hatari ya kufiwa na mgonjwa mkononi.

Dk Emmanuel Kombe, Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makongo alisema Serikali inapeleka fedha na vituo vina fedha yake, lakini cha kushangaza utata wa kupatikana mahitaji yaliyoagizwa kila siku upo palepale.

“Wauguzi wanatukanwa, wanakuwa maadui wa wananchi kwa sababu hospitali hazina dawa, hakuna mwananchi anayefahamu kama MSD ndiyo hawajaleta,” alisema Kombe.

Dk Sebastian Mapunda Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kigogo alisema hiyo ni changamoto ya muda mrefu na wao kama watendaji wanaoshughulika na wagonjwa inawapa shida.

Alisema wananchi wanapoona dawa katika maduka binafsi halafu hospitali hakuna, wanaona kama kuna mchezo unafanywa, kumbe MSD wapo kati kukwamisha.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi alisema atamwandikia barua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amuombe Rais atumbue jipu la MSD.

Tangu aapishwe kuwa Mkuu wa Wilaya, hiyo ndiyo taasisi ya kwanza kukutana nayo na kusikiliza kero zao.

Alisema ameanza na afya kwa sababu ndiyo sekta yenye changamoto nyingi ikiwamo hiyo ya dawa. Hivyo atalishughulikia suala hilo kwa kila njia ikiwamo kumshirikisha Mkuu wa Mkoa.

“Haiwezekani fedha ipo dawa hakuna na hakuna jibu la msingi, na haiwezekani dawa kusubiri taratibu mwezi mzima, wiki tatu kama hakuna ielezwe hakuna ili ufanyike utaratibu wa kununua zinakopatikana kwa sababu afya za binadamu hazitambui Sheria za Ununuzi,” alisema Hapi.

Ofisa Habari wa (MSD), Eti Kusiluka alipingana na madai hayo akieleza kuwa hakuna utaratibu wa kupokea fedha wanapoagiza dawa zaidi ya kupokea mahitaji ya wateja wao na kuyafanyia kazi.

“Serikali ina mipango ya ununuzi na muombaji hupata mahitaji aliyoomba ndani ya siku 14 na 45 na siyo kweli kuwa fedha zao zinang’ang’aniwa,” alisema Kusiluka.

Polisi Kizimbani kwa Kupokea Mshahara wa Jeshi Hilo Kwa Miezi 7 Bila Kufanya Kazi

$
0
0
Aliyekuwa askari wa Jeshi la Polisi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Kuyani Mkunjera (36), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi, kwa kupokea mshahara wa jeshi hilo huku akiwa ameacha kazi kwa kipindi cha miezi saba.

Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Antony Ngowi alisema mshtakiwa alijinufaisha pasipo kufanyia kazi kitu anachonufaika nacho na alipokea fedha kiasi kinachozidi Sh4.6 milioni ambayo ni kinyume cha kifungu cha 23 (1) (a) cha Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sheria namba 11 ya mwaka 2007. 

Ngowi alisema mshtakiwa kuanzia Oktoba 12, 2015 hadi Aprili 28, mwaka huu alijipatia kiasi hicho cha fedha kwa kujinufaisha pasipo kukifanyia kazi kitu anachonufaika nacho, huku akiwa siyo mfanyakazi wa jeshi hilo na akiwa ameajiriwa na taasisi nyingine.

Mshtakiwa alikana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyomtaka awe na kiasi cha Sh3 milioni za ahadi na wadhamini wawili wenye barua za kuwatambulisha, vitambulisho na picha za paspoti.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 23, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Tanzania Kuzalisha Mega wati 200 za Umeme Kutokana Nishati ya Jotoardhi ifikapo 2025.

$
0
0

Tanzania inatarajia kuanza kuzalisha umeme wa jotoardhi zaidi ya megawati 20 ifikapo mwaka 2018 mradi utakaopunguza gharama za nishati hiyo nchini.

Kiwango cha nishati hiyo kitakachozalishwa kutoka miradi minne inayoendelea kufanyiwa kazi kwa sasa, kinatarajiwa kuongezeka mpaka megawati 200 ifikapo mwaka 2025.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Jotoardhi nchini (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe aliwaeleza wajumbe wa mkutano wa wataalamu wa jotoardhi jana kuwa, mbali na mpango huo wa muda mfupi, wamejiwekea malengo ya kuzalisha zaidi ya megawati 200 ndani ya miaka tisa ijayo.

“Hii ni nishati salama na rafiki wa mazingira,” alieleza bosi huyo wa TGDC ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco).

Mpaka sasa miradi inayoendelea kufanyiwa kazi ikiwa kwenye hatua mbalimbali ni Ngozi na Mbaka iliyopo mkoani Mbeya, Kisaki wa Morogoro, Mlima Meru na Ziwa Natron kwenye Mlima Lengai.

Alisema, TGDC inashirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mazingira (UNEP) kufanya mapitio ya jotoardhi, kuendeleza na kuchakata nishati hiyo kabla haijaanza kutumika.

Akifungua mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Pallangyo alisema Tanzania ina hazina ya takriban megawati 5,000 ya nguvu za kuzalisha nishati hiyo na kwamba ipo karibuni kuanza kuitumia.

Alisema mpango wa Serikali ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na utafikiwa endapo kutakuwa na nishati ya kutosha kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.

Polisi Mwanza Yanasa Mtandao wa Ujambazi

$
0
0
Polisi mkoani Mwanza imebaini mtandao unaohusika na ujambazi wa kuvamia, kupora, kujeruhi na kuua wafanyabiashara wa maduka ya fedha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema tayari wamewatia mbaroni watu watatu wanaodaiwa kuhusika na mtandao huo wakiwa na bunduki aina ya SMG ikiwa na magazine nne na risasi 144.

Pia, watuhumiwa hao walikutwa na kofia moja ya kuficha uso, hijabu mbili, jaketi moja pamoja na mabegi mawili wanayotunzia silaha zilizokuwa zimefichwa kwenye nyumba wanayoishi.

“Polisi bado inaendelea kumsaka kinara wa mtandao huu (jina linahifadhiwa), ambaye alifanikiwa kukwepa mtego wa polisi, tunawaomba raia wema kutoa taarifa zitakazofanikisha kumtia mbaroni,” alisema SACP Msangi.

Alisema bunduki iliyokamatwa inaaminika kutumika katika matukio zaidi ya sita ya uporaji katika maduka ya fedha.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga alisema vyombo vya dola tayari vimebaini mitandao saba ya uhalifu mkoani Mwanza.

Kitwanga ambaye pia ni mbunge wa Misungwi aliwaeleza wapigakura wake kuwa tayari mitandao miwili kati ya hiyo saba ilikuwa imeangamizwa, huku jitihada za kuangamiza iliyosalia zikiendelea.

Rais Magufuli: Huyu Shetani Aliyetulaani Watanzania kwanini Asife? Hivi Hatuhurumii hata Kidogo?

$
0
0
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) limetakiwa kuingia ubia na kampuni za madini nchini ili kutengeneza ajira kwa vijana wa Kitanzania ambao wengi wao wako vijiweni.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Rais John Magufuli wakati akizindua majengo ya mifuko ya pensheni ya NSSF na PPF yaliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 60 yaliyojengwa jijini hapa.

Rais Magufuli alisema wakati umefika kwa NSSF kujikita katika biashara ya kupata faida kwa haraka kama vile ya madini ya tanzanite kwa kuanzisha viwanda vya kukata madini hayo na kusanifu ili vijana wafundishwe na hatimaye kuajiriwa katika viwanda hivyo.

Alisema suala la Tanzania kuwa nchi ya tatu duniani kwa kuuza madini ya tanzanite wakati madini hayo yanapatikana hapa hapa tu na kuziacha nchi za India na Kenya zikiongoza, ni suala la kushangaza sana.

Alisema NSSF sasa inapaswa kujipanga na kuingia katika biashara ya madini hususan tanzanite kwa kuingia ubia na kampuni kama hiyo ya Signature inayomilikiwa na mzawa Sailesh Pandit ili ifanye biashara na wanachama wa mfuko huo wapate faida haraka haraka na kuachana na uwekezaji wa majengo.

"Siku nyingine hakuna ubaya hata NSSF mkawa ndio wawekezaji wakubwa wa Tanzanite mkawa mnanunua Tanzanite kutoka kwa vijana hawa badala ya kuwa inavushwa mpaka Kenya na kwenda Kenya, badala ya Tanzania kuwa ya kwanza kuuza Tanzanite duniani inajitokeza India alafu inafata Kenya

"Unajua saa nyingine watu wanatuona Watanzania sijui tukoje,
huyu shetani aliyetulaani sisi Watanzania kwanini asife? hata hatuhurumii kidogo? basi kama ni kuswali na kusali tusali sana ili tubadilike, tuthamini mali yetu kwa ajili ya vizazi vyetu." Alisema RAais Magufuli

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema kampuni ya madini ya Signature iliyopanga katika jengo la mfuko huo la Mafao House imeajiri vijana zaidi ya 47 wa kuchonga tanzanite na watashirikiana katika kuanza biashara hiyo.

Profesa Kahyarara alisema kauli ya Rais ya shirika hilo kujikitaka katika biashara ya tanzanite kwa kuanzisha viwanda vya kuchonga madini hayo wataifanyia kazi haraka iwezekanavyo bila ya wasiwasi wowote.

Hata hivyo, serikali ilishapiga marufuku usafirishaji wa madini ghafi nje ya nchi na kutaka madini yote kuchongwa nchini na wazawa kuanzisha viwanda vya kuchonga madini hayo.

Bomu la Mkono Laibua Hofu Tanga.....Ni baada ya Mtuhumiwa Kulirusha Baada ya Kukurupushwa na Polisi

$
0
0
Kwa mara nyingine jana wakazi wa Jiji la Tanga walikumbwa na taharuki baada ya kijana mmoja kurusha bomu la mkono chini ya daraja wakati wananchi walipokuwa wakimfukuza baada ya kukurupushwa na polisi.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Leonard Paulo alisema kijana huyo alikurupushwa na askari waliokuwa kwenye msako wa kuwatafuta majambazi waliofanya mauaji Aprili 20, mwaka huu katika duka la Central Bakery.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi saa mbili usiku kwenye Mtaa wa Makora, Tarafa ya Ngamiani.

Awali, Kamanda Paulo alisema kijana huyo anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 25 na 30, alipokurupushwa alianza kutimua mbio. 

“Alipoanza kukimbia ndipo wananchi wakaingilia kati, walimfukuza na kumshambulia kwa mawe huku wakimpiga na kitu chenye ncha kali kisogoni, ndipo wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo akafariki dunia njiani,” alisema Kamanda Paulo.

Mapema kabla hajafariki dunia, kamanda alisema kijana huyo alipokurupushwa alikimbia akiwa ameshikilia bomu mkononi.

Kamanda aliwataka wakazi wa Tanga kuwa watulivu kwa sababu vyombo vya dola viko katika operesheni maalumu ya kuwasaka walioshiriki mauaji ya hivi karibuni katika hilo la mikate.

Walioshuhuda tukio hilo walisema kijana huyo alishambuliwa na wananchi baada ya kukwapua simu ya mwanamke mmoja katika Mtaa wa Makorora.

Walisema alianza kukimbia na alipoona wananchi wanamfukuza aliwatahadharisha kuwa wakimsogelea atarusha bomu alilokuwa amelishika mkononi.

Kufuatia kutishiwa na bomu hilo, wananchi waliokuwa wakimkimbiza walipiga simu Kituo Kikuu cha Polisi cha Chumbageni kwa ajili ya kupatiwa msaada.

“Kwa hili tunawapongeza polisi. Walitumia dakika chache kufika eneo la tukio lakini walipobaini kwamba ni bomu, wakaamua kuwasiliana na maofisa wataalamu wa kutegua mabomu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) ambao waliwasili eneo la tukio,” alisema Rajabu Hamis.

Wakizungumza kuhusu tukio hilo, baadhi ya wakazi wa Tanga waliomba vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha ulinzi kwa sababu wamejawa na hofu, kwa kuwa matukio yanayohatarisha amani yanazidi kutokea.

“Hii ni changamoto kwa vyombo vya ulinzi na usalama, matukio haya yanazidi kuwapa hofu wananchi. Mwezi uliopita yalifanyika mauaji makubwa Central Bakery, leo bomu tena,” alisema Kassim Mbughuni.

Neema ya Gesi Yaja ......Wadau Wakutana Kujadili Namna ya Kuanza Mchakato wa Kuchakata Gesi

$
0
0

UJENZI wa Mradi wa Kusindika Gesi (LNG) mkoani Lindi utakaowezesha nchi kuanza kufanya biashara ya gesi nje ya nchi umeanza baada ya jana wadau sita wa mradi huo kukutana na kupeana elimu kabla ya mchakato mzima kuanza wakati wowote mwaka huu.

Kwa kutumia mradi huo, Tanzania itaanza kufanya biashara ya gesi kwa kuuza nje ya nchi baada ya kubaini kuwa gesi iliyogundulika baharini inayofikia kiasi cha futi za ujazo trilioni 47, ni nyingi na ikivunwa mahitaji ya ndani hayawezi kuimaliza hivyo kulazimika kuiuza nje ya nchi na kuongezea Taifa mapato.

Akizungumza jana katika mkutano wa wawekezaji na serikali kupata elimu ya mradi huo kabla ya kuundwa kwa kamati ya majadiliano ya serikali na kuingia mkataba wa ujenzi, Mkurugenzi wa Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kelvin Komba alisema wamekutanisha wadau kutoka serikalini na wawekezaji.

Komba alisema mkutano huo ni kuanza taratibu za awali kuwekeza na kuuza gesi kwa kutolewa kitaalamu rasilimali hiyo kwenye visima na kufikishwa katika mtambo huo wa LNG ambao utaigeuza kuwa kimiminika ili ifae kuingizwa katika matangi na kusafirishwa kwa meli kwenda katika masoko mbalimbali duniani.

Akifafanua zaidi, alisema mtambo huo utaipooza gesi itakayovunwa mpaka nyuzi joto sifuri na kuipooza zaidi mpaka nyuzi joto hasi 100, ndipo inakuwa kimiminika na kufaa kusafirishwa kwenda maeneo mbalimbali duniani.

Mradi huo mkubwa ambao haujawahi kutokea katika historia wa miradi nchini wenye thamani  inayofikia zaidi ya Dola za Marekani bilioni 60 na kutoa ajira karibu 20,000, utawezesha nchi kukua kiuchumi.

Alisema tayari ardhi imepatikana ya hekta 2,071 kwa ajili ya mradi wa LNG huku hekta nyingine 20,000 zinazozunguka eneo la mradi huo, zikitengwa kwa ajili ya viwanda. 

Alizitaja kampuni sita zinazoshirikiana katika ujenzi wa mtambo huo ni TPDC, BG Group, Ophir Energy, Statoil, Exxon Mobil na Pavilion Energy. Mradi huo thamani yake ni kuanzia Dola za Marekani bilioni 30 mpaka bilioni 60.

Msajili wa Hazina Agoma Shirika la UDA Kuchukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

$
0
0

MSAJILI wa Hazina ametupilia mbali maombi ya Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam ya kutaka kurudishiwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) kwa kusisitiza kuwa Kampuni ya Simon Group ina hisa halali katika shirika hilo.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaac Mwita, alikaririwa na vyombo vya habari jana akimtaka Msajili kukadhibidhi shirika hilo kwa uongozi wa Jiji kwa madai kuwa Simon Group walinununua shirika hilo kinyume cha taratibu.
 
Msajili alisema pia serikali haina mpango wa kuuza hisa zake za asilimia 49 inazomiliki katika shirika hilo.
 
Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam waliomba wapewe hisa hizo za serikali ikiwa hawatarudishiwa hisa za Simon Group.
 
Mkuu wa Kitengo cha Habari wa ofisi ya Msajili wa Hazina, Gerard Chami,  jana alisema kuwa ofisi yake haiwezi kubadilisha mkataba wa umiliki wa Uda.
 
“Msajili anakamata hisa za serikali ambazo ni mali ya Watanzania, hazihusiani kwa namna yoyote na hisa asilimia 51 za Jiji ambazo walishaziuza kwa kampuni ya Simon Group. Tunashangaa wanapotaka tuingilie mambo yao ambayo kimsingi hatuhusiki,” alisema Chami.
 
Chami alieleza kuwa kulikuwa na kesi iliyokuwa mahakamani baina ya Jiji na kampuni ya Simon Group Ltd. Iliamuliwa Simon Group ilipe Sh. bilioni 5.5 ili kununua hisa za Jiji na alifanya hivyo na kwa mazingira hayo, Msajili hadi sasa anamtambua kama mwanahisa mwenza wa Uda.
 
Alifafanua kuwa hakuna namna ambayo Msajili atajihusisha na hisa hizo kwa kuwa siyo wajibu wake bali anachotakiwa ni kumtambua mwanahisa mwenzake ambaye kwa sasa ni kampuni ya Simon Group.
 
“Suala hili linachukuliwa kisiasa zaidi, lakini ukweli unajulikana kwani ni sawa mtu alikuwa na mali yake akaamua kugawa sehemu na kumpa mwingine aliyehitaji kwa wakati huo, lakini kwa sababu zake kile alichogawiwa akaamua kuuza kwa mtu mwingine, ni vigumu kurudi kwa sasa kumweleza aliyegawa awali kugawa tena hisa zake," alifafanua.
 
“Yeyote aliyeuziwa hisa hizo sisi tunamtambua ndiye mwanahisa mwenza, tunachojua kwa sasa kampuni ya Simon Group ndiye mwanahisa mwenza kwa kuwa alishamaliza kulipa kwa kutekeleza amri ya mahakama,” alisema.
 
Alibainisha kuwa hisa asilimia 49 za serikali ina hiari nazo kama ni kuuza kwa faida au kwa ajili ya kupeleka fedha katika eneo jingine lenye maslahi ya jamii na siyo kwa Jiji linavyotaka kumpa mwanahisa mwenza katika shirika hilo.
 
Meya Mwita alisema juzi kuwa Baraza la Madiwani la Jiji la Dar es Salaam liliazimia katika kikao chake kuwa fedha zaidi ya Sh. bilioni 5.5 zilizolipwa kwa Jiji na kampuni ya Simon Group kwa ajili ya kununuliwa hisa zisirudishwe hadi tathmini ya kina itakapofanyika na kujiridhisha kuwa hadaiwi chochote kwa kutumia mali mbalimbali za Uda kwa maslahi yake.
 
Pia waliunda kamati ndogo ya wajumbe watatu ambao ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea na Mwanasheria wa Jiji, Jumanne Mtinangi kwa ajili ya kufuatilia suala hilo.
 
Naye Ofisa Habari wa Simon Group, Deus Buganywa, alisema jana hawajapokea barua yoyote kuhusiana na kutakiwa kurejesha hisa hizo baada ya kuulizwa juu ya sakata hilo la Uda.

Kasi ya Watanzania Kujiunga na Makundi ya Kigaidi ya Al-Shabaab na IS Yaongezeka........Waziri Asimulia Wanavyojiunga, Wapinzani Wahoji Wanajeshi Kupewa Ukuu wa Mikoa

$
0
0
Serikali imesema imeshtushwa na wimbi kubwa la vijana wa Kitanzania wanaojiunga na makundi hatari ya kigaidi ya Al-Shabaab na Islamic State, maarufu kama ISIS.

Kauli hiyo imetolewa bungeni mjini Dodoma jana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake ya Sh trilioni 1.6 kwa mwaka 2016/17.

Dk. Mwinyi alisema pamoja na hali hiyo, Serikali imeendelea kupambana na makundi hayo kwa kila njia ili kuhakikisha nchi inakuwa salama katika maeneo yote, yakiwamo ya mipakani.

Alisema matukio ya kigaidi yameendelea kuwa tishio duniani, hivyo Tanzania inapaswa kuchukua tahadhari ya kila namna.

Dk. Mwinyi alisema kuwapo kwa makundi hayo ya Al-Shabaab, Al-Qaeda, Boko Haram na Islamic State, kunafanya tishio la ugaidi kusambaa duniani kote.

“Taarifa za kuwapo baadhi ya Watanzania wanaojiunga na makundi ya Al-Shabaab na ISIS tunazo, kunahatarisha usalama wa Tanzania, hasa ikizingatiwa kiujumla mwingiliano mkubwa uliopo kati ya wananchi wetu na watu wenye malengo tofauti.

“Hatari iliyopo ni uwezekano wa baadhi ya vijana waliojiunga na makundi ya kigaidi ya kimataifa kurejea nyumbani kwa lengo la kutekeleza vitendo vya kigaidi nchini mwetu.

“Tuna kila sababu ya kujizatiti na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama,” alisema Dk. Mwinyi.

Alisema kipindi kilichopita, kumejitokeza viashiria vyenye mwelekeo wa kigaidi, ikiwemo kuvamiwa baadhi ya vituo vya polisi, kuporwa silaha na baadhi ya askari kuuawa na kundi ambalo nia yake haijafahamika.

“Matukio yenye mwelekeo wa kigaidi, ni kama yaliyotokea katika mapango ya Amboni mkoani Tanga, Kitongoji cha Nyandeo wilayani Kilombero pale Morogoro na kukamatwa mabomu ya kutengenezwa kwa mkono katika maeneo mbalimbali yakiwamo Zanzibar,” alisema.

Alisema pamoja na hali hiyo, kwa upande wa mpaka wa kusini mwa nchi, hali imeendelea kuwa shwari, licha ya uwapo wa utata wa mpaka wa Ziwa Nyasa ambao bado haujapatiwa suluhisho.

Kutokana na hali hiyo, amewataka Watanzania  kuendelea kuchukua tahadhari kwa kutoa taarifa ya matukio yanayotishia kuashiria uvunjifu wa  usalama.

Kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana na ule wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu Zanzibar, alisema umefanyika kwa amani na utulivu, licha ya baadhi ya maadui wa ndani na nje kutabiri mambo mabaya.

“Watanzania tunayo sababu ya kujivunia kuwa uchaguzi mkuu ambao kikalenda ni wa tano tangu kuingia mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, uliendeshwa na kuhitimishwa kwa amani, utulivu na mshikamano mkubwa kinyume na maadui wetu wa ndani na nje ya nchi waliotutabiria mabaya,” alisema.

Dk. Mwinyi alisema kwa kutambua umuhimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa vijana, Serikali itaendelea na azma yake ya kuwajenga vijana uzalendo, ukakamavu, maadili mema, utaifa na kutoa stadi za kazi.

Alisema kutokana na uwezo mdogo wa kifedha, suala hilo sasa litatekelezwa kwa kutoa mafunzo kwa baadhi ya vijana wa kujitolea kwa mujibu wa sheria.

“Katika mwaka 2015/16, vijana 27,463 walipatiwa mafunzo mbalimbali, yakiwamo ya kuwapa ujuzi na stadi kazi ili wajiandalie mazingira mazuri ya kujiajiri.

“Nachukua fursa hii kuwaomba vijana wanaopata mafunzo ya JKT, wazingatie maarifa na ujuzi wanaoupata, hususan wa stadi za kazi ili waweze kujiajiri badala ya imani iliyoanza kujitokeza kwa baadhi ya wahitimu kudai ajira kwa maandamano.

“Katika hatua ya kutekeleza agizo la Serikali linalohusu vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuajiri idadi kubwa ya vijana wanaopatiwa mafunzo ya JKT, hadi kufikia Februari, mwaka huu vijana 5,453 waliajiriwa na vyombo vya ulinzi.

“Kati ya vijana hao, 3,521 waliajiriwa na JWTZ, polisi 1,185, Usalama wa Taifa 106, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) 617. Hata hivyo, idadi ya vijana waliopatiwa ajira imeongezeka. Hadi kufikia Aprili, mwaka huu vijana 7,170 wamejiariwa na vyombo hivyo,” alisema Dk. Mwinyi.

==>Kambi ya upinzani wahoji wanajeshi kupewa ukuu wa mikoa
Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, msemaji wa wizara hiyo, Juma Hamad Omar, alihoji hatua ya Serikali kuwateua maofisa wa vyombo vya ulinzi kushika nafasi za kisiasa kama wakuu wa mikoa na wilaya.

Omar ambaye ni Mbunge wa Ole (CUF), alisema Serikali imekuwa na utamaduni wa kuwateua maofisa wa vyombo vya dola waliopo kazini, na baada ya uteuzi huo hufanya kazi kwa mujibu wa chama tawala.

“Wakuu wa wilaya na mikoa wanafungwa na ibara ya 80 (1) (C) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 inayowataja kuwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM katika wilaya husika. Hali kadhalika wakuu wa mikoa wanafungwa na ibara ya 94 (1) (C) inayowataja kuwa wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM katika mkoa husika.

“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka Serikali itambue ibara 147 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka kwamba; ‘Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara 5 ya Katiba hii’,” alisema Omar.

Akizungumzia utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo, alisema katika bajeti ya mwaka 2015/16 Serikali imeweka rekodi mbaya ya kutoa fedha chini ya kiwango kilichoidhinishwa na Bunge kwa miradi ya maendeleo.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Atoa Ushauri Wa Kupunguza Foleni Dar es Salaam

$
0
0

Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutekeleza mipango iliyowekwa na serikali yake endapo atahitaji kumaliza na msongamano katika jiji hilo.

Kikwete alitoa ushauri huo jana, alipotembelea Daraja la Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam, huku akionyesha kuridhishwa nalo na kumtaka Makonda kuweka historia kama mkuu wa mkoa kijana kumaliza msongamano.
 
Alisema kuna mipango ambayo iliwekwa na serikali ya awamu ya nne katika kumaliza msongamano huo, ikiwamo uboreshaji wa reli ili kubabiliana na tatizo la usafiri, uboreshaji wa stendi za mabasi ya kwenda mikoani za Boko, Pugu na Mbezi Luis, ambavyo alisema ni muda mrefu sasa haoni utekelezaji wake.
 
“Kwa mfano kuna ile stendi ya Boko na mingine ni mipango ambayo iliwekwa lakini naona imekaa muda mrefu hakuna utekelezaji wake. Naona tu unakwenda unarudi, unakwenda unarudi, ” alisema.
 
Kikwete alisema hakuna uchawi utakaosaidia kumaliza msongamano katika jiji la Dar es Salaam pasipo kuboresha huduma za msingi katika makazi yaliyoko pembezoni mwa mji huo pamoja kutumia treni.
 
Alisema jiji la Dar es Salaam linahitaji usafiri ambao utachukua idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja na kutolea mfano baadhi ya maeneo ya Ubungo, Tazara, na Mwembechai kwamba endapo yangewekwa reli na treni ikaanza kutumika, ingepunguza idadi ya magari binafsi barabarani.
 
Alisema pamoja na kuanza kwa mradi wa mabasi ya mwendo kasi, bado kunahitajika usafiri wa treni katika jiji, ambao alisema ukiboreshwa vizuri utawavutia hata wa wa maisha ya kawaida kuutumia na pia na kuacha magari yao nyumbani.
 
“Tatizo kubwa la Dar es Salaam wakazi wengi wanapata huduma katika eneo moja, yapo maeneo ya Mabwe Pande, Kigamboni na mengine ya pembezoni. Yatumieni vizuri, wekeni huduma huko, jengeni maduka, osifi na huduma muhimu huko. Sisemi mhamishie huko ofisi za serikali lakini huduma ziingine muhimu ili yule atakayetaka kuja mjini awe amependa mwenyewe,” alisema.
 
Makonda alisema amapokea ushauri huo na ataufanyia kazi na kuongeza kwamba iko mipango mbalimbali ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kupunguza kero mbalimbali katiika jiji hilo.

Jinsi ya Kuandaa na Kutayarisha Dawa Lishe ya Kunenepesha,Kurutubisha na Kuongeza Mwili

$
0
0

Dawa-lishe  ya  kuongeza, kurutubisha  na  kunenepesha  mwili, ni  dawa  maalumu  kwa  watu  wenye  uzito  wa  chini  (  Under weight ) ambao  wanataka  kuongeza  mwili  na  uzito.


Dawa  hii  huwasaidia  watu  ambao  miili  yao  imedhoofu  kutokana  na  sababu  mbalimbali  kama  vile  kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali.

Na  kwa  wale  watu  wembamba  ambao  wanataka  kuongeza  miili  yao, dawa  hii  huwasaidia  vizuri  sana.

FAHAMU  JINSI NA  NAMNA  YA  KUANDAA NA  KUTAYARISHA   DAWA-LISHE  MAALUMU   YA  KUONGEZA, KURUTUBISHA  NA  KUNENEPESHA  MWILI.

MAHITAJI   YA  DAWA –LISHE

i.           Dawa –lishe vijiko  viwili vikubwa.

ii.         Asali  ya  tende  vijiko  vitano  vikubwa.

iii.       Tangawizi  ya  unga  vijiko  vikubwa  viwili

iv.       Unga  wa ufuta

v.         Maziwa  fresh nusu  lita

vi.       Maji  ya  moto  kiasi  cha  milimita  mia  mbili  na  hamsini  ( 250 mills  )


MATAYARISHO
i. Chukua  vijiko  vinne  vyenye  dawa  lishe  yako  kisha  chemsha  na  nusu  lita  ya  maji  hadi  mchanganyiko  wako  utokote  halafu  ipua, chuja , makapi  weka  pembeni  kisha  hifadhi  juisi  yako.

ii.Tayarisha  uji kwa  kutumia  unga  wa  ufuta  na maziwa  fresh

iii.Chukua  vijiko  viwili  vikubwa  vya tangawizi  ya  unga  kisha  changanya  kwenye  kikombe  cha  maji  ya  moto  chenye  ujazo  wa  milimita  mia  mbili  hamsini  (  250  mills )

MATUMIZI:
i. Tumia  kunywa  nusu  lita  ya  dawa –lishe  yako  kisha

ii.Tumia kula  vijiko  vinne  vikubwa  vya  asali  ya  tende

iii.Kisha tumia  kunywa  vikombe  vinne  vya  uji  wa  ufuta  ulio changanywa  na  maziwa  fresh

iv.Halafu  kunywa  glasi  moja  ya  moto  iliyo  changanywa  na  vijiko  viwili  vikubwa vya tangawizi  ya  unga.

UTAFANYA  HIVYO  MARA  MBILI  KWA  SIKU  KWA  MUDA  WA  SIKU  THELATHINI  MFULULIZO.

Baada  ya  siku  thelathini, utaangalia  na  kujitathmini  kiasi  ulicho  ongezeka. Kama  utataka  kuendelea  kuongezeka  zaidi, utaendelea  kutumia  dozi  hii  hadi hapo utakapo fikia kiwango  utakacho  rizika  nacho.

BEI  YA  DAWA-LISHE : Bei  ya  Dawa-Lishe  ni  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU (TSHS.50,000/=)

JINSI  YA  KUIPATA  DAWA  LISHE:
Dawa  hii  inapatikana  katiuka  duka  la dawa  asilia  la  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAN  katika  eneo  la  TABATA  MAKOKA  karibu  na  SHULE  YA  SEKONDARI  YA  MT. ANNUARITE.

Unaweza  kufika  moja  kwa  moja  katika  ofisi  zetu  AU  unaweza  kuletewa  mahali popote  ulipo  jijini  Dar   Es  salaam.

Kwa  wakaazi  wa  ZANZIBAR  watatumiwa dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti  na  kwa  wateja  wetu  wa  ughaibuni watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

Kwa  mawasiliano  zaidi  wasiliana  nasi  kwa  simu

0766  53  83   84

Vile  vile  tunayo  dawa  ya  asili  iitwayo  JIKO  ambayo  inatibu  na  kuponyesha  kabisa  TATIZO  LA  UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu  kuhusu  SAYANSI  YA  NGUVU  ZA  KIUME  pamoja  na  jinsi  dwa  ya  JIKO  inavyo  fanya  kazi  tafadhali  tembelea:

Jeshi La Wananchi ( JWTZ ) Kuendelea Kupewa Mafunzo Ili Liwe Kisasa Zaidi

$
0
0

Na Tiganya Vincent,  MAELEZO--Dodoma
Wizara ya Ulinzi na Kujeshi la Kujenga Taifa imepanga kuendelea kuliimarisha na kuliongezea uwezo Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania kwa kulipatia vifaa na zana za kisasa pamoja na kutoa mafunzo stahiki ili kuwa tayari kukabiliana na adui wa ndani na nje.

Mpango wa Serikali umetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh.Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati akiwasilisha hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2016/17.

Alisema kuwa sanajari na hili , Wizara itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa Wanajeshi nchini ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa huduma na mahitaji ya msingi kama vile chakula , tiba, sare , usafiri na stahili zao.

Mh. Dkt. Mwinyi aliongeza kuwa Wizara itaimarisha uwezo wa Jeshi katika utafiti na kuendeleza teknolojia kwa madhumuni ya kuisaidia uzalishaji wa bidhaa na huduma kwa matumizi ya kijeshi na kiraia hapa nchini na nje ya nchi.

Aidha , alisema kuwa Wizara kupitia Jeshi la Kujenga la Taifa itaendelea kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzo ya uzalendo , umoja wa Kitaifa , ukakamavuna kuwapatia stadi za kazi ili kuwaandaa katika uzalishaji mali.

Dkt. Mwinyi alisema Wizara kupitia Jeshi litaendelea kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kiulinzi na nchi nyingine duniani kupitia Jumuiya za Kimataifa , Kikanda na ushirikiano na nchi moja moja.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Husein Ali Mwinyi ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla shilingi trilioni 1.7 (1,736,530,413,000.00) kwa ajili ya matumizi ya kawaidia na matumizi ya maendeleo.

Alisema kati ya fedha hizo shilingi trilioni 1.4 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na bilioni 248 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Serikali Kushindanisha Wawekezaji sekta ya Nishati

$
0
0

Na Veronica Simba-Maelezo
Serikali imesema ushindani kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta ya nishati, ndiyo njia bora zaidi itakayowezesha kuwapata wawekezaji wenye vigezo vinavyotakiwa.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyasema hayo jana, Mei 10, alipokutana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO kutoka Japan, Norio Shoji na Ujumbe wake, ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika uzalishaji na usafirishaji wa umeme nchini, kwa kutumia vyanzo mbalimbali ikiwemo gesi asilia na jua.

“Kampuni nyingi zimeonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya nishati. Serikali inao uhitaji mkubwa wa wawekezaji walio makini, hivyo tunahitaji kuwapata wawekezaji wenye vigezo kwa kutumia ushindani unaozingatia uwazi,” alisisitiza Profesa Muhongo.

Aliongeza kuwa, ili kuwarahisishia wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini, Wizara inaandaa taarifa maalum itakayobainisha maeneo yanayohitaji uwekezaji pamoja na vipaumbele vyake.

Alisema, taarifa hiyo itakuwa tayari na kutolewa mwishoni mwa mwezi huu (Mei 31, 2016) na kwamba itasambazwa kwa wadau wote wa ndani na nje ya nchi kupitia njia mbalimbali za mawasiliano, ikiwamo tovuti ya wizara.
 
Profesa Muhongo alieleza kuwa, taarifa hiyo pamoja na mambo mengine, itawapa fursa wawekezaji wenye nia, kuchagua aina ya uwekezaji wanaohitaji kufanya na katika maeneo ambayo wanadhani watakuwa na uwezo wa kumudu ushindani kutoka kwa wawekezaji wenzao kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Akifafanua zaidi, Profesa Muhongo alisema kuwa, zoezi la kuwashindanisha wawekezaji walioonesha nia, litakuwa ni endelevu na litakuwa likifanyika kila baada ya muda fulani, ambao utabainishwa katika taarifa husika inayotarajiwa kutolewa.

Akitoa mfano, alisema kuwa, siyo lazima kumpata mwekezaji katika zoezi la ushindanishaji, hivyo ni muhimu zoezi liwe endelevu ili kuweza kutoa fursa kwa wawekezaji wengi zaidi kushiriki na hivyo kumpata mwekezaji mwenye vigezo vyote ambavyo Serikali inavihitaji.

“Endapo tutaendesha zoezi la ushindanishaji wawekezaji na wote walioshindanishwa wasipotimiza vigezo vinavyotakiwa, hatulazimiki kumchukua yeyote tu. Tutakachofanya ni kutokumchukua yeyote kati yao na hivyo kuendelea na zoezi hilo baada ya muda tutakaoubainisha, hadi pale tutakapowapata wawekezaji wenye vigezo tunavyovitaka.”

Profesa Muhongo alibainisha kuwa, mchanganyiko wa nishati ambao Serikali imekusudia kuutumia kama vyanzo vya kuzalisha umeme nchini kwa sasa ni pamoja na gesi asilia, maji, upepo, jua, makaa ya mawe, mvuke (maji moto) na tungamotaka.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo (Kulia), akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO kutoka Japan, Norio Shoji, baada ya kikao baina ya Wizara ya Nishati wa Nishati na Madini na Kampuni husika, kilichofanyika Mei 10 mwaka huu Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Katikati), akiwa katika kikao na Ujumbe kutoka Kampuni ya KOYO ya Japan katika kikao kilichofanyika Mei 10 mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Tahadhari Kuhusu Makachero FEKI Wa TAKUKURU Wanaojifanya Kufuatilia Sakata la Sukari

$
0
0

Tangu kuanza kwa zoezi la kufuatilia wafanyabiashara wanaoficha sukari kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Dr John Pombe Magufuli, kumekuwa na wimbi la watu wanaojiita “makachero wa TAKUKURU  kutoka Makao Makuu” nao wakifuatilia sakata la sukari mkoani Kilimanjaro.

Matapeli  hao ambao kwa sasa wapo  wilayani  SIHA, wamekuwa wakiwasumbua   wafanya biashara kwa kudai kuwa  wametumwa kuwashughulikia huku wakiomba kupewa  fedha ili wawasafishe. 

Kiasi cha fedha ambacho kimekuwa kikiombwa ni kati ya Shilingi 150,000/= hadi 500,000/= kama “gharama ya kuwasafisha kwa Mheshimiwa Rais”

Naomba  wafanya baiashara  Mkoani Kilimanjaro waelewe kwamba, TAKUKURU inao mfumo wa utendaji kazi ambao unajali misingi ya utawala bora na kamwe haihusiki na utapeli wa aina hii.

TAKUKURU katika utendaji wake wa kazi, haiwatozi wafanya biashara fedha kama adhabu kwa kuhifadhi sukari kinyume na taratibu. TAKUKURU  inafuatilia, kuhoji na kumtaka mfanyabiashara kuonesha namna  anavyomiliki sukari hiyo kwa kutoa vielelezo husika. Mwisho wa zoezi hili, atakayetoa tamko ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Ifahamike kuwa hakuna afisa wa TAKUKURU mpaka sasa aliyetumwa kutoka Makao Makuu kuja mkoani Kilimanjaro kufuatilia zoezi la sukari. Zoezi hili mkoani hapa linaendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama kama timu moja na wala halifanywi na TAKUKURU pekee .

Ifahamike pia kuwa hakuna zoezi linaloihusisha TAKUKURU litakaloendeshwa mkoani bila ofisi ya mkoa kuwa na taarifa. 

Kwa misingi hiyo yeyote anayeendesha zoezi hilo nje ya utaratibu nilioufafanua ni tapeli, taarifa zake zitolewe mapema ili akamatwe na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Maofisa wote kutoka ofisi ya TAKUKURU mkoa wanavyo vitambulisho na kama watatiliwa shaka basi ofisi yangu ijulishwe kupitia simu namba   0784 998 804 au 0786 089 805 muda wowote.                                                                
                             
IMETOLEWA NA                                                                  
ALEX J KUHANDA
MKUU WA TAKUKURU  MKOA WA KILIMANJARO
11/5/2106.

Rais Dk. Magufuli Afanya Uteuzi Wa Wenyeviti Wa Bodi Za TAFORI Na TTB

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Makumbusho ya Taifa, Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Katika uteuzi huo Mhe. Rais amemteua Bi. Anna Abdallah (Mbunge Mstaafu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Makumbusho ya Taifa, Dkt. Felician Kilahama (Mbobezi katika fani ya Misitu) kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Kufuatia uteuzi huo wa Mhe. Rais, Waziri wa Maliasili na Utalii kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Shirika la Makumbusho ya Taifa Sura ya 281 kifungu cha 4(2) kikisomwa pamoja na Jedwali aya ya (1a) amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi hiyo;
  1. Amina Amer Issa, Mkurugenzi wa Makumbusho, Nyaraka na Mambo ya Kale Zanzibar.
  2. Ali S. Mcharazo, Mkurugenzi wa Tanzania Library Services, Dar es Salaam.
  3. Godius Kahyala, Dean, College of Arts and Social Sciences University o,f Dar es Salaam.                                                          
  4. Thomas J. Lyimo, Dean, Faculty of Science University of Dar es Salaam.
  5. Oswald Masebo, Mhadhiri, Mkuu wa Idara ya Historia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  6. Lota Melamari, Consult, Management of Natural Resources and       Environment and Coordinator of Tanga Botanical Gardens, Arusha.
  7. Anna M. Kishe, Mtaalam wa lugha za Kiswahili na Kiingereza na       Mhadhiri katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dar es Salaam.
  8.  Donatius M. Kamamba, Mkurugenzi wa Mambo ya Kale, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Aidha, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Sura ya 277 kifungu cha 6(2) kikisomwa pamoja na Jedwali la 2 (1)(a), Mhe. Waziri amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi hiyo;
  1. Salim Maliondo, Profesa wa Biologia ya Misitu Chuo  Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
  2. Susana Augustino, Mhadhiri Mwandamizi matumizi ya mazao ya misitu, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
  3. Deusdedit Bwoyo, Kaimu Mkuruenzi Msaidizi, Maendeleo ya Misitu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es Salaam.
  4. Dismas L. Mwaseba, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Morogoro.
  5. Charles Maguta Kajege, Business Consulatant (Finance), Dar es Salaam.
  6. Lemayon Melyoki Mkurugenzi, Shule ya Ujasiriamali, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  7. Tuli S. Msuya, Katibu Tawala, Mfuko wa Misitu Tanzania, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dar es Salaam.
  8. Emma Liwenga, Mtafiti Mwandamizi, Taasisi ya Tathmini ya Maliasili (IRA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  9. Lawrence Mbwambo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Morogoro.
Pia, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Sura ya 364 kifungu cha 3(2) kikisomwa pamoja na Jedwali 1(2), Mhe. Waziri amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi hiyo;
  1. Ibrahim Mussa, Mkurugenzi wa Masoko, TANAPA
  2. Balozi Joseph Sokoine Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.
  3. Mark Leveri, Mtaalam wa kutengeneza filamu na matangazo ya video, Ex. Tanzania Film Company.
  4. Richard Rugimbana, Mtendaji Mkuu Tanzania Confederation of Tourism (TCT).
  5. Zabein Muhaji Mhita, Mbunge Mstaafu na Mkurugenzi wa Elimu ya  Msingi Mstaafu.
  6. Agustine Kungu H. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera na Uchumi, Wizara ya Fedha na Mipango.
Uteuzi wa Wenyeviti na Wajumbe hao ni wa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe 24/04/2016 hadi tarehe 23/04/2019.

IMETOLEWA NA:
Angelina E.A. Madete
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

10 Mei, 2016

Rais Magufuli Awasili Nchini Uganda Leo Kuhudhuria Sherehe Za Kuapishwa Rais Museveni

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Mei, 2016 amewasili Jijini Kampala nchini Uganda ambapo kesho anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni.

Rais Magufuli ametua katika uwanja wa ndege wa Entebe majira ya saa tano za asubuhi na kupokelewa na Waziri wa Ujenzi na usafirishaji wa Uganda Mheshimiwa John Byabagambi na kisha kuelekea Ikulu ya Entebe ambako amepokelewa rasmi na mwenyeji wake Mheshimiwa Rais Yoweri Kaguta Museveni.

Akiwa katika Ikulu ya Entebe Rais Magufuli amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na pia amepigiwa mizinga 21.

Aidha, Viongozi hao wamefanya mazungumzo ambapo pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano na uhusiano kati ya nchi hizo mbili, Rais Magufuli amemhakikishia Rais Museveni kuwa Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha ujenzi wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka Hoima katika Ziwa Albert nchini Uganda na kupita kaskazini mwa Tanzania hadi bandari ya Tanga.

Rais Magufuli ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mheshimiwa Suzan Kolimba.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Kampala
11 Mei, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kaongeza siku za bure kupanda Mabasi ya Haraka

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea kituo cha Mabasi yaendayo haraka cha Kamata Kariakoo leo, amesema kuwa kuanzia jumatatu Mei 16, 2016 ndio nauli za mabasi ya mwendo wa haraka zitaanza kutozwa.

Pia amewaasa watumiaji wa barabara hasa watembea kwa miguu, baiskeli na maguta wasitumie barabara hizo ili kuepusha usumbufu kwa madereva wa mabasi ya mwendo wa haraka. 

Amesema ameamua kuongeza muda wa kuanza kutoza nauli hizo kwa watumiaji wa mabasi hayo kwaajili ya kuelimisha wananchi namna ya kukata tiketi na jinsi ya kuzitumia wakati wanapoingia kwenye kituo kwaajili ya kusubiri magari.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya May 12

Watu wa 7 wa Familia Moja Wauawa Kikatili Jijini Mwanza

$
0
0
WATU saba wa familia moja wameuawa kikatili wilayani Sengerema mkoani Mwanza juzi usiku. 

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa huo, John Mongella na Kamanda wa Polisi Mkoa, Ahmed Msangi katika eneo la tukio, alisema watuhumiwa katika tukio hilo hawajajulikana.

Kuni aliwataja waliopoteza maisha katika tukio hilo kuwa ni Augenia Philipo (62), Maria Philipo (56), Yohana Mabula (20), Regina Aloyce (12) na Mkiwa Philipo (13) huku wengine wawili wakitambulika kwa jina moja kila mmoja kuwa ni Donald na Samson.

Aidha, chanzo cha mauaji hayo ya kikatili hakijajulikana, ingawa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Zainab Telack alisema huenda mauaji hayo inawezekana yakawa ni ya kulipiza kisasi. 

Vyanzo vingine vinaarifu kuwa mauaji ya namna hiyo ni ya kawaida katika maeneo hayo, hasa msimu huu ambao kaya nyingi zinakaribia msimu wa mavuno.

“Bado kuna mkanganyiko juu ya chanzo cha mauaji hayo, wapo wanaosema kuwa huenda ni ya kulipiza kisasi lakini pia wengine wanasema yanatokana na msimu wa mavuno, lakini tunaamini uchunguzi wa Polisi ndio utakuja na majibu sahihi na ambao umeshaanza kazi hivi tunavyoongea,” alisema Kuni.

Makontena 115 Ya Sukari Yanaswa Jijini Dar es Salaam....RC Makonda Aviagiza Vyombo vya Dola Vifanye Uchunguzi wa Kina

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kuchunguzwa kwa sukari kontena 115 ambayo ni zaidi ya tani 3,000 iliyokutwa katika bandari kavu ya PMM iliyopo eneo la Vingunguti.

Makonda alitoa agizo hilo jana wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari hiyo na kubaini uwepo wa sukari hiyo ambayo ni mali ya Mohamed Enterprises, ambayo kwa taarifa zake aliambiwa zilikuwa kontena 165.

Alisema anazitaka mamlaka zinazohusika kama Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), pamoja na Shirika la Viwango (TBS) kuichunguza sukari hiyo kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza katika uwepo wa sukari hiyo kama sukari kuagizwa kutoka Dubai lakini imetoka Brazil na imepakiwa Dubai, na upangwaji wa kontena hizo katika bandari hiyo.

“Nashindwa kuelewa kwa nini sukari iagizwe kutoka Dubai lakini itoke Brazil na kufungashwa Dubai inaonesha inaweza kuwa imeshawahi kuisha muda wake hivyo nataka ichunguzwe na tunataka tujue kama Mohamed Enterprises anaficha sukari ili ipelekwe kwa wananchi kwa matumizi,” alisema Makonda.

Mbali na kutoa maagizo hayo, Makonda pia amezuia kutumika kwa sukari mifuko 22,000 iliyokutwa katika ghala la Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) lililopo Barabara ya Nyerere na kutaka wapeleke vielelezo kuhusu sukari hiyo kwa mamlaka zinazohusika kama ya matumizi yoyote.

Alisema sukari hiyo inayodaiwa kuwa ni ya viwandani ni lazima iangaliwe kama kweli ipo kwa ajili ya mahitaji ya viwandani au ilikuwa itumike tofauti na ilivyokusudiwa. 

Kwa upande wake, Meneja Operesheni wa bandari kutoka MeTL, Firoz Ebrahim alisema sukari hiyo imefuata taratibu zote na imefika katika bandari hiyo wiki moja iliyopita.

Katika hatua nyingine, Kampuni ya Al Naeem iliyopewa agizo la saa 36 kuanzia juzi iwe imeshaanza kusambaza sukari kwa bei elekezi iliyokuwa katika bandari ya Dar es Salaam, imeanza kutekeleza agizo hilo jana jioni.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images