Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wachungaji Wawili wa KKKT Wafikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Mauaji.......Mmoja wa Moravian Mbaroni kwa Kukutwa na Meno 11 ya Tembo Kanisani

0
0
Wakati mchungaji wa Kanisa la Moravian akikamatwa na meno ya tembo 11 ndani ya kanisa, huko Moshi wachungaji wawili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.

Tukio la wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro linawahusisha wachungaji wawili wa KKKT, Rodrick Mlay (52) na Godbess Mamkwe (38) pamoja na wananchi watatu ambao jana walipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini humo kwa madai ya kuua kwa kukusudia.

Wakati wachungaji hao wawili wakipanda kizimbani, Polisi mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wanawashikilia watu wawili akiwamo mchungaji wa Kanisa la Moravian kwa tuhuma ya kunaswa wakiwa na meno ya tembo 11 wakiwa wameyahifadhi ndani ya kanisa.

Akizungumzia meno hayo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi katika Kanisa la Moravian lililopo Kijiji cha Usevya, Wilaya ya Mlele.

Nyanda alisema mchungaji huyo akiwa na mwenzake ambao wote majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za upelelezi, walikamatwa kufuatia taarifa zilizolifikia jeshi hilo na askari wa hifadhi kuwa, watu hao wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na wamekuwa wakiyahifadhi ndani ya kanisa.

Baada ya taarifa hizo, polisi na askari hao walifanya uchunguzi kuhusiana na taarifa hizo kwa kufika katika kanisa hilo na kufanya upekuzi uliofanikisha kukamatwa kwa meno hayo yakiwa yamehifadhiwa kwenye tenga la kubebea mizigo.

Kaimu kamanda huyo alisema katika matukio mengine mawili tofauti yaliyotokea Mei 8, saa mbili usiku kwenye maeneo ya Mgolokani, Kata ya Sitarike wilayani humo, polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi hiyo walimkamata mtu mmoja akiwa na jino moja la tembo.

Nyanda alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya askari kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake na kukamata jino hilo na lingine la simba.

Alisema wote waliokamatwa kwenye matukio hayo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Katika tukio la wachungaji waliofikishwa mahakamani mjini Moshi, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Julieth Mawole alisema wakiwa na wananchi watatu aliowataja kwa majina ya Fadhili Mkenda (36), Jackson Ruben (45) na Mathayo Moses (27), Mei 4 katika eneo la Kilema Pofo wanadaiwa kumuua kwa makusudi Frank Peter (19).

Hakimu Mawole aliwataka watuhumiwa hao kutojibu lolote na kesi dhidi yao itasikilizwa Mei 23 katika Mahakama Kuu Kanda ya Moshi na wote walipelekwa rumande kwa sababu shtaka waliloshtakiwa nalo halina dhamana kisheria.

Katika hatua nyingine, raia wa Marekani, Mbaraka Mtambo (50) amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na maganda mawili ya kobe bahari aliyokuwa ameyafichwa kwenye begi la nguo.

Kamanda wa Polisi wa JNIA, Martin Otieno alisema raia huyo mwenye asili ya Tanzania, alikamatwa juzi saa 3.45 usiku akijiandaa kwa ajili ya safari ya kwenda Marekani na ndege ya Shirika la KLM kupitia Uholanzi.

Vita Ya Sukari Yazidi Kupamba Moto.....Kilo 622,000 Zakamatwa Morogoro, RC Dodoma Aagiza Tani 154 Ziuzwe Kwa Wananchi

0
0
Suala la uhaba bandia wa sukari limeendelea kuitikisa nchi, lakini vyombo vya ulinzi na usalama vikifanya kazi nzuri baada ya kuwatia nguvuni wafanyabiashara wengine, waliohodhi bidhaa hiyo kinyume cha sheria huku ikiwamo kukamata kilo 622,000 za mfanyabiashara Haruni Zakaria mkoani Morogoro.

Mwishoni mwa wiki, mfanyabiashara huyo anayemiliki Kampuni ya Al Naeem, alikutwa akiwa ‘ameficha’ tani 4,579.2 za bidhaa hiyo katika maghala yake yaliyoko Tabata, Dar es Salaam. 

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), wachunguzi wa taasisi hiyo na wa Jeshi la Polisi, walifanya ukachero wao katika maghala ya kampuni hiyo yaliyopo Mbagala na Tabata, Mei 5, mwaka huu.

Lakini siku chache baada ya kunasa sukari hiyo, kikosi kazi cha Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoa wa Morogoro kilichoundwa na Mkuu wa Mkoa huo, Dk Kebwe Steven Kebwe kufuatilia wafanyabiashara walioficha sukari, kimebaini kiasi cha kilo 622,000 za sukari zilizofichwa katika maghala mbalimbali yaliyomo mkoani humo. 

Dk Kebwe amemwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei kuweka ulinzi kwenye maghala hayo yaliyokutwa yameficha sukari hiyo na kuhakikisha inauzwa kwa bei elekezi, iliyowekwa na serikali kwa wananchi.

Pia alimwagiza kuwafikisha wafanyabiashara walioficha sukari hiyo mahakamani mara moja na kumsaka mfanyabiashara Sadick Yassin ambaye alifunga duka lake wakati wa ukaguzi na kutokomea kusipojulikana.

Mali ya Zakaria wa Dar
Akizungumza jana, Dk Kebwe alisema sukari hiyo imebainika kuwa ni mali ya mfanyabiashara mmiliki wa Kampuni ya Al Naeem Enterprises na kuhifadhiwa katika maghala mbalimbali ya Kiwanda cha Sukari Kilombero (K1) tani 429, Kiwanda cha Sukari Kilombero (K2) tani 135 na katika Manispaa ya Morogoro tani 58.4, jumla kuwa ni tani 622.4

“Nimeunda kikosi kazi cha kufuatilia wafanyabiashara walioficha sukari katika maghala yao katika ukaguzi wa awali, jumla ya tani 622.4 za sukari zimebainika kwenye maghala mbalimbali na sukari yote iliyobainika ni mali ya Al-Naeem Enterprises na tayari maghala hayo yenye sukari yapo chini ya ulinzi wa vyombo vya dola,” alisema.

Licha ya kumwagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa kuweka ulinzi katika maghala hayo na kusimamia sukari hiyo inauzwa kwa bei elekezi ya serikali, pia alimwagiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakiki iwapo sukari hiyo imelipiwa kodi ya serikali.

Dk Kebwe pia aliwataka wananchi katika maeneo mbalimbali mkoani humo, kutoa taarifa za wafanyabiashara au watu walioficha sukari ili hatua zichukuliwe mara moja dhidi yao. 

Kabla ya kuweka msimamo wa Serikali ya Mkoa dhidi ya wafanyabiashara dhalimu, Dk Kebwe na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa walifanya ziara ya kushtukiza ya kuhakiki upya maghala ya wafanyabiashara wa maduka ya jumla katika Manispaa ya Morogoro.

Katika ghala la Kampuni ya Sukari Kilombero lililipo mjini Morogoro lilikuwa na tani 58.4 za sukari ambayo ni mali ya Al Naeem Enterprises.

Msimamizi wa ghala hilo, Robert Charles alimfahamisha Mkuu wa Mkoa na timu yake kuwa sukari hiyo ipo kwa muda wa mwezi mmoja sasa baada ya kununuliwa na mfanyabiashara huyo kutoka kiwandani Kilombero.

Alisema sukari tani 58.4 iliyokutwa ndani ya ghala hilo ni mali ya mfanyabiashara Zakaria aliyeinunua kutoka kiwandani Kilombero na kuihifadhi hapo akisubiri kusafirishwa na kuwauzia wanunuzi wa jumla. 

Baadhi ya wauzaji wa maduka ya jumla waliokaguliwa na timu ya Mkuu wa Mkoa, Thabit Islam na Hassan Binzoo walisema hali ya upatikanaji wa sukari katika kipindi hiki ni mgumu kutokana na kuadimika ghafla.

Dar yanaswa nyingine
Katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, zimekamatwa tani 2,700 za sukari zikiwa zimefichwa katika ghala moja eneo la Mbagala. 

Akitoa taarifa hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana, Paul Makonda, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Photidas Kagimbo alisema sukari hiyo imekamatwa baada ya Rais kutoa agizo la kuwabaini wale wote walioficha sukari na kusababisha wananchi kuteseka kupata bidhaa hiyo.

Kagimbo alisema licha ya kukamatwa kwa sukari hiyo Manispaa hiyo bado inaendelea na msako ili kuwabaini na wafanyabiashara wengine waliohodhi bidhaa hiyo.

Msako mkali Kahama
Wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Polisi imefanya upekuzi katika baadhi ya maghala ya kuhifadhia sukari na kuwabaini baadhi ya wafanyabiashara wanne wanaojihusisha na kazi hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Michael Nyange alisema wamefanya ukaguzi katika maghala ya wafanyabiashara wakubwa wa sukari, ambayo ni ya wafanyabiashara John Hango (walikuta mifuko miwili ya kilo 50), Nyorobi Kisabu (hakuna kilichokutwa), Mshaka Kaziro (hakuna kilichopatikana) na Alex Magina (mifuko 40, yenye kilo 50 kila mfuko). Alisema kazi hiyo itakuwa endelevu.

RC Dodoma aagiza iuzwe
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ameagiza tani 154 kuuzwa kwa wananchi kwa bei elekezi, huku akiwataka wafanyabiashara ambao bado wameficha sukari kuitoa mara moja kabla rungu halijawashukia.

Takukuru kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani hapa walikamata na kuzifungia tani 154 za sukari katika ghala la mfanyabiashara Haidary Gulamali na sasa Rugimbana ametoa agizo la kufunguliwa kwa ghala hilo ili litoe huduma kwa wananchi.

Mkuu wa Mkoa akiwa amefuatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa alisema wameamua kufungua ghala na kuanza kutoa huduma kwa wananchi ambao wanauhitaji mkubwa kwa sasa wa sukari.

Mbunge Apinga Wakunga Wanaume Kuruhusiwa Kuwahudumia Wanawake Wakati wa Kujifungua

0
0

Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Riziki Mngwali amepinga mpango wa Serikali kuajiri wakunga wanaume katika baadhi ya zahanati kuhudumia wajawazito wakati wa kujifungua kuwa ni udhalilishaji dhidi ya wanawake.

Mbunge huyo ameitaka Serikali kuzingatia mila za Kiafrika, akisema imezoeleka kuwa huduma ya ukunga kwa wajawazito wakati wa kujifungua hutolewa na wataalamu wanawake.

“Serikali haioni kuwa kwa kuweka wakunga wanaume katika baadhi ya zahanati zake nchini ni kuwadhalilisha wajawazito wanaojifungua?”alihoji Mngwali.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jaffo alisema wakunga wanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga inayowataka kutoa huduma ya kumsimamia mjamzito wakati wa uchungu, kujifungua na baada ya kujifungua bila kujali jinsia.

Alisema pamoja na sheria hiyo, kumekuwa na changamoto zinazotokana na mila na desturi za jamii ambazo husababisha baadhi ya wahitaji wa huduma hiyo kutokubali kuhudumiwa na wakunga wanaume.

“Kutokana na hali hii, Serikali itaendelea kuajiri wataalamu wengi ili pale penye changamoto paweze kupatiwa ufumbuzi bila kukwaza jamii husika,” alisema Jaffo.

Naibu waziri alisema hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa mbunge huyo kuuliza swali hilo bungeni, lakini tayari amewasiliana na uongozi wa Mkoa wa Pwani ambao umeeleza kuanza kulifanyia kazi jambo hilo na kwa baadhi ya maeneo wameshaanza kupeleka wakunga wanawake.

Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Waendelea Kupungua.

0
0
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Aprili 2016 na kusema kuwa umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.4 iliyokuwepo mwezi Machi, 2016.
 
Hii inamaanisha kuwa  kasi ya upandaji wa bei ya  bidhaa na huduma kwa mwezi Aprili 2016 imepungua kidogo ikilinganishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma  iliyokuwepo mwezi Machi mwaka huu.
 
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo ametoa taarifa hiyo jana jijini Dar es salaam na kueleza kuwa kupungua kwa mfumuko huo kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali nchini.
 
Alisema Takwimu zilizokusanywa katika mikoa yote ya Tanzania Bara kwenye bidhaa zinazotumika kupima mfumuko wa bei kwa mwezi Aprili 2016 zimeainisha kuwa bidhaa zisizo za vyakula katika soko zikiwemo Gesi , dizeli na mafuta ya taa zimechangia kupungua kwa mfumuko huo.
 
Alisema kuwa pamoja na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa hizo kwa mwezi Aprili 2016, baadhi ya bidhaa za vyakula ikiwemo mchele, unga wa Mahindi na mkaa ilionyesha kuongezeka katika kipindi hicho.
 
Akizungumzia Kuhusu Fahirisi za Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania kwa mwezi Machi na Aprili Bw. Kwesigabo alisema kuwa zimeongezeka hadi kufikia 102.46 kutoka 101:93 za mwezi Aprili.
 
Alisema kuwa tofauti na mwezi Machi bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi kwa mwezi Aprili ni unga wa muhogo, dagaa, choroko, maziwa ya ungana na matunda aina ya machungwa.
 
Aidha,bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na mvinyo, bia kuni na mazulia.
 
Kwa upande wa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Aprili, 2016 umefikia shilingi 97 na senti 60 ikilinganishwa na uwezo wa shilingi 98 na senti 11  wa mwezi Machi 2016.
 
“Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Aprili 2016 umepungua, hii ina maana kuwa sasa mtu anahitaji kuongeza  ya shilingi 2.40 ili aweze kununua bidhaa na huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua mwezi Machi ” Alisema Kwesigabo.
 
Kwa upande wa mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki mwezi Machi, 2016, Kwesigabo alisema una mwelekeo unaofanana; Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 5.27 kutoka 6.45 huku Uganda ukifikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 6.2 zIlizokuwepo mwezi Machi 2016.
Mtaalam wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Prof. Haji Semboja akifafanua kwa waandishi wa Habari kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Aagwa Na Mabalozi Wapya Chikawe Na Kisamba

0
0
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Balozi Mathias Chikawe, alipofika kumuaga katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, jana, Mei 9, 2016.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiagana na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Japani, Balozi Mathis Chikawe, baada ya mazungumzo yao
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba akisaini kitabu cha wageni, alipofika kumuaga Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Balozi Mathew Kisamba alipofika kumsalimia katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, jana, Mei 9, 2016.

(Picha na Bashir Nkoromo)

Ijue Sayansi Ya Kusimama Kwa Uume

0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani.

Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ?

Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu

HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME
Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo :

Hatua  ya  kwanza, ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari.

Na  hatua  ya  pili  ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa STRONGER  AND  LONGER  ERECTION

JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA.

1. HATUA   YA  KWANZA:

DAMU  KUTIRIRIKA  KWA  KASI KUINGIA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME  NA  KUUFANYA  UUME  KUSIMAMA  NA  KUWA  MGUMU.

Unapopata  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  fahamu iliyopo  kwenye  ubongo,  hupeleka  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo, ambayo  nayo  hupeleka  taarifa  hadi  kwenye  mishipa  ya  uume. Taarifa  inapofika  kwenye  mishipa  ya  uume  huifanya  mishipa hiyo  ku-relax  na  hatimaye   kufanya  mishipa  ya  ateri  kufunguka  na  kutanuka. Mishipa  ya  ateri  inapo  tanuka  na  kufunguka, huruhusu  damu  kuingia  kwa  kasi  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  huume  kusimama.

Ni  muhimu  kujua  kuwa, mishipa  ya  uume  inapo relax  hupelekea  kuisukuma na  hatimaye  kuiziba  mishipa  ya  vena  iliyo  karibu  na  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuiondolea  uwezo  wa  kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  sehemu  nyingine  za  mwili.

N.B: Kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyingine  za  mwili.  Au  kwa  lugha  nyingine  unaweza  kusema, kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  kwenye  mishipa  ya  uume.
 
2. HATUA  YA  PILI  :
DAMU  KUENDELEA  KUHIFADHIWA  KATIKA  UUME  WAKATI  UUME  UKIWA  UMESIMAMA  NA  HIVYO  KUUFANYA  UUME  UENDELEE  KUDUMU  KATIKA TENDO LA NDOA   KWA  MUDA  MREFU.

Uume  ulio  simama, ili  uendelee  kusimama, ni  lazima  mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo   wa  kunyonya  damu  kutoka  katika  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyinginezo  za  mwili. .

Mishipa  ya  Vena  ndio  inayo  husika  na  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume na  kupeleka  sehemu  nyingine  za  mwili.  Ili  uume  uendelee  kusimama  lazima  mishipa  hii  ya  vena  iwe imezibwa. Ili  iweze  kuzibwa   ni  lazima  misuli  laini  ya  kwenye  uume  iwe - ime  relax na  hivyo  kuifanya  mishipa  ya  vena  kushindwa  ku  nyonya damu  kutoka  kwenye  uume.

Endapo  mishipa  ya  vena  itazibuka , basi  itanyonya  na  kutoa  damu yote  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume uliosimama  na  kuipeleka  sehemu  nyinginezo  za  mwili  na  hatimaye  uume  huo ulio simama  na  utasinyaa  mara  moja.

JINSI  UUME  UNAVYO  SIMAMA  NA  KUSISIMKA.
Tumeisha  zifahamu  hatua  mbili  muhimu  katika  kusimama  kwa  uume

Jinsi  Uume  unavyo  simama: Katika  uume  kuna chemba  yenye  mishipa  laini  sana, ambayo  ndio  huufanya  uume  kusimama.

Mishipa  hii  ipo kama  sponji  hivyo  huweza  kunyauka  na  kutanuka.

Damu  inapoingia  ndani  ya  mishipa  hii  huufanya  uume  kusimama  na  kuwa  mgumu  kama  msumari.

Damu  inapoendelea  kuhifadhiwa  ndani  ya  mishipa  hii  wakati  wa  tendo  la  ndoa, huufanya  uume  uendelee  kusimama.

Mwanaume  unapo  patwa  na  wazo la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  fahamu  iliyo  kwenye  ubongo  hupeleka  ishara  kwenye  uti  wa mgongo, ambao  nao  hufikisha   taarifa  kwenye  mishipa  ya  uume.

Taarifa  ikisha  fika  kwenye  mishipa  ya  uume, huifanya  mishipa  ya  uume  ku-relax  na  mishipa  ya  uume  inapo  relax, hufanya  mambo  makuu  mawili;

i. Kwanza  hufanya  mishipa  ya  ateri  kufunguka na  hivyo  damu  kutiririka  kwa  kasi  sana  kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume

( Mishipa  ya  ateri  ndio  inayo  tumika  kama  njia  ya  kuingiza  damu  kwenye  uume. Bila  mishipa  ya  ateri  imara  na  yenye  afya, damu  haiwezi kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume, na  damu  isipoweza kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume, basi  uume  hauwezi  kusimama )

ii.Pili huibana  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuizuia    kunyonya  damu  kutoka  kwenye  uume  na  kuipeleka  kwenye  sehemu nyingine  za  mwili. Matokeo  yake  kuufanya  uume  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Kumbuka ,kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  neva  iliyo  karibu  na  mishipa ya  uume, ni kunyonya  damu kutoka  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  kwenye  sehemu  nyingine  za  mwili. Kwa  lugha  nyingine, kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  kwenye  mishipa  ya  uume ulio simama.

Kadri  damu  inavyo  zidi  kuingia  ndani  ya mishipa  ya  uume, ndivyo  uume  unavyo  zidi  kuwa  mgumu  na  kukakamaa.

Na  kadri  damu  inavyo  hifadhiwa  ndani  ya  mishipa  ya  uume, ndivyo  uume  unavyo endelea  kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa kwa  muda mrefu.

Baada  ya  kumaliza  kufanya  tendo  la  ndoa,mishipa  ya  uume inarudi  katika  hali  yake  ya  kawaida (inanyauka ), ikisha  nyauka, mishipa  ya  ateri  inanyauka  pia, vena  zinafunguka  na  kunyonya  damu  katika  mishipa  ya  uume  na  kuirejesha  katika  sehemu nyinginezo  za  mwili  na  hatimaye  uume  kurudi  katika  hali  ya  kawaida  ( Flaccid ).

Hali  hii  itaendelea  kujirudia  kwa  kadri  utakavyo  kuwa  ukiendelea kufanya  tendo  la  ndoa.

Mambo  Muhimu  Katika  Kuufanya Uume  Usimame na  Kuendelea  kudumu  katika  kusimama  kwa  muda  mrefu wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Ili  uume  uweze  kusimama  imara  kama  msumari na  uendelee  kusimama  imara  na  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo la  ndoa, ni  lazima  mambo  yafuatayo yawepo.

1. Mishipa ya   uume iliyo  imara  na  yenye  afya  njema.

2. Mfumo   mzuri  wa damu  katika   mwili  mzima.

3.Mtiririko  imara  wa  damu kuingia  na  kutoka  ndani  ya  mishipa  ya  uume.

4. Ushirikiano  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  ya  kwenye  ubongo  (nerves), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  mishipa  ya  kwenye  uume.

Ili  mwanaume  aweze  kuwa  imara  katika  tendo  la  ndoa, ni  lazima  mambo  manne  niliyo yataja  hapo  juu  yawe  sawa  sawa  bila  hitilafu  yoyote. Kinyume  chake, mwanaume  hawezi  kuwa  na  nguvu  za  kiume.

MAMBO   YANAYO SABABISHA   UKOSEFU/UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Tumeshajua   nguvu za  kiume  ni  nini, jinsi  uume  unavyo  simama, hatua  za  kusimama  kwa  uume, pamoja  na  mambo  yanayo  fanya  uume  uweze  kusimama  na  kuwa  na  uwezo  wa  kuendelea  kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Ni  vyema  tukajua  mambo  yanayo  sababisha  kushindwa  kusimama  kwa  uume, mambo  yanayo  sababisha  uume  ushindwe kuendelea  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa   pamoja  na  mambo  yanayo  fanya  mtu  ashindwe  kurudia  tendo  la  ndoa.

Yafuatayo  ni  mambo  yanayo  sababisha  ukosefu wa  nguvu  za  kiume.

1. MAGONJWA  YANAYO  SHAMBULIA  MFUMO  WA  DAMU  PAMOJA  NA  MISHIPA  YA  DAMU.

Damu  ndio  nishati  inayo wezesha  kusimama  kwa  uume  na kuufanya  kuwa  mgumu na  imara  kama  msumari.

Damu  ndio  nishati  inayo weza   kuufanya  uume uendelee kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Damu  ndio  nishati  inayo  upa  uume  uimara  na  uwezo  wa  kurudia  tendo  la  ndoa  zaidi  ya  mara  moja.

Hivyo  basi  ili  uume  uweze  kuwa  imara na  wenye  nguvu, pamoja  na  kuwa  na  uwezo  wa  kumudu  na  kustahimili   tendo  la  ndoa  wakati  wowote , basi  ni  lazima   mwanaume  awe  na mfumo  imara  wa  damu  utakao  ruhusu  kutiririka  kwa  damu  kwenda  katika  sehemu mbalimbali  za  mwili  ikiwamo  uume.

Ili  mfumo  uweze  kuwa  imara  ni  lazima  mhusika  awe  na  damu  ya  kutosha, na  pili  awe  na  mishipa  ya  damu  yenye  afya.

Katika  mwili  wa  mwanadamu,kuna  mishipa  inayo  tumika  kusafirisha  damu  kutoka  katika  sehemu moja  ya  mwili kwenda  katika  sehemu  nyingine  ya  mwili  ikiwemo  uume. Mishipa  hiyo  ni  kama  vile  vena (veins), atery ( ateri) na  capillary  ( kapilari )

Mishipa  hii  ya  damu  inapaswa  kuwa  imara  na  yenye  afya  njema  wakati  wote.   Mishipa  hii  ikipatwa  na  hitilifu, basi  itazuia  kusafirishwa  kwa  damu  katika  sehemu  mbalimbali za  mwili  wa  mwanadamu  na  hatimaye  kufanya  suala  la  kuwa  na  nguvu  za  kiume  kwa  mhusika  kuwa  ugumu  kwa  sababu   ya  kushindwa  kupeleka  damu  kwenye  mishipa  ya  uume.

Magonjwa  kwenye  mishipa  ya  damu  huzuia   kutirika  kwa  damu kwenye  ogani  muhimu   kama  vile  moyo, ubongo na  figo.

VIASHIRIA  VYA  MAGONJWA  KWENYE  MISHIPA  YA  DAMU.
Utajuaje  kwamba  una  magonjwa  kwenye  mishipa  yako  ya  damu ?

Ukiwa  una  matatizo  yafuatayo ya  kiafya, ni  ishara  kwamba, una  magonjwa  kwenye  mishipa  yako  ya  damu:

1.  Kolestrol ( Ama  lehemu  kwenye  damu )
Kolestrol  nyingi  kwenye  damu, huzuia  kutiririka  kwa  damu. Kolestrol  ikizidi  kwenye  damu,  hupelekea  kuziba   mishipa  ya  ateri  ambayo  kazi  yake  ni  kupeleka  damu  kwenye  uume. Matokeo  yake  ni  mhusika  kutokuwa  na  uwezo  wa  kusimamisha  uume  wake barabara  kwa  sababu uume  hauwezi  kusimama  bila  damu  kuingia  ndani  ya  mishipa  ya  uume. 
 
 Hivyo  basi pamoja  na  dawa  ya  nguvu  za  kiume, yakupasa  kutibu  kolestrol. Unaweza  kuondoa  kolestrol  kwenye  damu  kwa  kutumia  dawa  mbali  za  asili  kama  vile mdalasini,uwatu, habbat sodah  etc.  Jinsi  ya  kujitibu  kolestrol  kwa  kutumia dawa asilia  tafadhali  tembelea


2.      Shinikizo  Kubwa  la  Damu
Shinikizo  Kuu la  Damu husababisha  mishipa  ya  ateri  ambayo  hutiririsha  damu  iingiayo  kwenye  uume  kuziba  na  kushindwa kutanuka  kwa  kiwango  inachotakiwa  kutanuka.

Pia  huifanya  mishipa  laini  katika  uume   kushindwa  ku-relax  na  hivyo  kushindwa  kuizuia  mishipa  ya  vena  ya  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  kwenye  maeneo  mengineyo  ya  mwilini.

Matokeo  yake  kunakuwa hakuna  kiasi  cha  kutosha  cha  damu  iingiayo  kwenye  uume  na  hivyo  kufanya  uume  ushindwe  kusimama.

Vile  vile  hata  kiasi  kidogo  cha  damu  kinacho  ingia  kwenye  uume, kinashindwa  kuendelea  kuhifadhiwa  ndani  ya  uume  wakati uume  ukiwa  umesimama, na  matokeo yake  ni  uume  kusinyaa  ndani  ya  kipindi kifupi  sana  tangu  usimame.

Pamoja  na kutumia  dawa  ya  nguvu  za  kiume, unapaswa   pia  kutumia  dawa  asilia  kujitibu  tatizo  la  shinikizo  kuu  la  damu.

Kufahamu  jinsi  ya  kujitibu  tatizo  la shinikizo  la  damu  kwa  njia  ya  asilia, tembelea :


3.  Ugonjwa  wa  kisukari :
 Ugonjwa  wa  kisukari  ni  miongoni  mwa  vyanzo  vikuu  vya  tatizo  la  ukosefu wa  nguvu  za  kiume.  Kusimama  kwa  uume  kunategemeana  na  kutiririka  kwa  damu  mwilini. Kisukari  huathiri  mishipa  ya  damu pamoja  na  usambazaji  wa  damu  kwenye  ogani  muhimu  mwilini  kama  vile  moyo, ubongo, figo  na  uume.

Kiukweli, mwanaume  mwenye  kisukari  yupo  katika  risk  kubwa  ya  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume,m tena  katika  kiwango  kikubwa  sana.

Unashauriwa pamoja  na kutumia  dawa  ya  nguvu  za  kiume, tumia  pamoja  na  dawa  mbalimbali  za  asili  kwa  ajili  ya  kubalance  sukari  yako mwilini. 
 
Zipo  dawa  mbalimbali  za  asili  zinazo  saidia  kubalance  kiwango  cha  sukari  mwilini. Dwa  hizo  ni  pamoja na mdalasini, unga  wa  uwatu, mbegu  za  uwatu, manjano, majani  ya  manjano,mbegu  za  katani, nakadhalika. Namna  ya  kutumia  dawa  hizo  kujitibu  tatizo  la  sukari, tafadhali  tembelea :http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/jitibu-kisukari-presha-shinikizo-la.html

4. Magonjwa  ya  figo
Tatizo  la  ugonjwa  wa  figo  huathiri  vitu vingi  ambavyo  ni  muhimu  sana  katika  kuufanya  uume  uweze  kusimama  na  kuendelea  kudumu  katika  kusimama.

Tatizo  la  figo, huathiri  homoni, huathiri kutiririka   kwa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume. Huathiri  mfumo  wa mishipa  ya  neva  pamoja  na  nishati  ya  mwili mzima.

Pamoja  na  dawa  ya  kutibu  tatizo  la  nguvu za  kiume, unapaswa  pia, kutibu  tatizo  la  figo. Kufahamu  jinsi  ya  kujitibu  magonjwa mbalimbali  ya  figo  kwa  kutumia  dawa mbalimbali  asilia, tembelea :http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/jitibu-kisukari-presha-shinikizo-la.html

5.        Ugonjwa  wa  moyo
Moyo  ndio  supplier  mkubwa  wa  damu  katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili.  Ugonjwa  wa  moyo  hupunguza  uwezo  wa  moyo  kusambaza  damu  kwenye  mishipa  mbalimbali  ya  damu  na  hivyo  kuathiri  utendaji  kazi  wa  mishipa ya  damu  kama  vile  ateri  na  vena. Matokeo  yake  ni  mishipa  hiyo  kushindwa  kupeleka  damu  ya  kutosha  katika  uume  pamoja  na  kushindwa  kuifanya  mishipa  ya  uume  kurelax na  matokeo  yake,. Ukosefu  wa nguvu  za  kiume. Hivyo  basi, pamoja  na  dawa  ya  nguvu  za  kiume, unapaswa  pia   kutibu  tatizo  la  moyo. Kufahamu  jinsi  unavyo  weza  kutibu ugonjwa  wa  moyo  kwa  dawa  asilia, tembelea :


6.  Kupwaya  kwa  mishipa  ya  vena.
Kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  kwenye  uume   kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika sehemu  nyingine  za  mwili.  Mishipa  ya  vena iliyopo  karibu  na  uume  kazi  yake  kubwa  ni kuhakikisha  hakuna  damu  yoyote  kwenye mishipa  ya  uume. ( KUMBUKA  KUWA  DAMU NDIO  HUFANYA  UUMU  USIMAME, HIVYO CHOCHOTE  KILE  KITAKACHO  FANYA  DAMU ISIKAE  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME , KITAFANYA  UUME  USINYAE  )

Ili  uume  uendelee  kusimama  ni  lazima, mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo  wa kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya uume  kupeleka  nje  ya  mishipa  ya  uume.

Na  ili  mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo  wa   kunyonya  damu  kutoka  kwenye   mishipa ya  uume  ulio  simama  na  kuipeleka  kwenye sehemu  nyingine  za  mwili,  ni  lazima mishipa  ya  uume  iwe  imara  na  thabiti  isiyo na  hitilafu  yoyote  ile.

Mishipa  ya  vena  ikipwaya, mwanaume hutokuwa  na  uwezo  wa  kusimamisha  uume wako, na  ikitokea  umefanikiwa kuusimamisha  basi  utasimama  ukiwa legelege  sana  na  utasinyaa  ndani  ya  muda mfupi  sana, kwa  sababu  damu  iliyo  ingia ndani  ya  uume  wako  na  kuufanya  usimame, itanyonywa  ndani  ya  muda  mfupi  sana  na kutolewa  nje  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo kuufanya  uume  wako  usimame.

 Tatizo  la  kupwaya  kwa  mishipa  ya  vena linasababishwa  na  kupiga  punyeto  kwa muda  mrefu  pamoja  na  ugonjwa  wa kisukari.

KUPIGA  PUNYETO  KWA  MUDA  MREFU: Kupiga  punyeto  kwa  muda  mrefu  ni  moja kati  ya  vyanzo  vikuu  vya  tatizo  la  la ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  Asilimia kubwa  ya  vijana  wenye  tatizo  la  ukosefu wa  nguvu  za  kiume, linasababishwa  na upigaji  wa  punyeto  kwa  muda  mrefu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Unapopiga  punyeto  unakuwa  unaiminya mishipa  ya  uume   ambayo  ndio  inaufanya uume  usimame.

Matokeo  yake  unaifanya  mishipa  hiyo  ilegee na  kutokuwa  na  uwezo  wa  kusimama  tena.

Mishipa  ya  uume  iliyo  legea  kutokana  na upigaji  punyeto, huleta  madhara  yafuatayo  :

i.           Huondoa  uwezo  wa  mishipa  ya  uume kurelax.

( Unapopata  wazo  la  kufanya  tendo  la ndoa, mishipa  ya  uume  ina relax  , mishipa  iki  relax  husababisha  mishipa ya  ateri  kupanuka  na  kuruhusu  damu kingie  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na hatimaye  kuufanya  uume  usimame  na kuwa  mgumu)
 
ii.Mishipa   ya  kiume  ikishindwa  ku relax husababisha  mishipa  ya  ateri  kuziba

iii. Mishipa  ya  ateri  ikiziba, damu  haiwezi kutiririka  kuingia  kwenye  mishipa  ya uume, na  hata  ikitokea  damu  imeingia ndani  ya  mishipa  ya  uume  basi huingia  kiasi  kidogo sana   tena  kwa presha  ndogo  sana  hivyo  basi  hata kama  uume  utasimama   basi utasimama  ukiwa  legelege  sana

iv. Mishipa  ya  uume  ikishindwa  kurelax basi  haitakuwa  na  uwezo  wa  kuipush na  kuiziba  mishipa  ya  vena  ambayo ndio  hunyonya  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  ulio  simama. 
 
Matokeo  yake  basi, damu  kidogo  iliyo ingia  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na kuufanya  uume  kusimama, hunyonywa na  kutolewa  nje  ya  mishipa  ya  uume ndani  ya  sekunde  chache  sana  na hivyo  kuufanya  uume usinyae  ndani ya  muda  mfupi  sana.

v. Mishipa  ya  uume  kulegea

vi. Uume  kurudi ndani  na  kusinyaa  na kuwa  kama  uume  wa  mtoto

6. Tatizo  la  unene  kupita  kiasi : Tatizo  la unene  na  uzito  kupita  kiasi  ni  miongoni mwa  mambo  yanayo  sababisha  upungufu wa  nguvu  za  kiume. Unene  kupita  kiasi humuweka  mtu  katika  hatari  ya  kupatwa na  magonjwa  kama  vile  kisukari, presha, moyo  na  shinikizo  kuu  la  damu. 
 
Na magonjwa  ya  kisukari, moyo,presha  na shinikizo  la  damu  husababisha  upungufu na ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, na  hivyo kumuweka  muhusika  katika  hatari  kuu  ya kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa nguvu  za  kiume.

Hivyo  basi  kwa  wewe  mwenye  tatizo  la unene  na  uzito  kupita  kiasi , pamoja  na kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume,  ni  vyema ukafanya  na  mpango  wa  kupunguza  unene na  uzito  wako.

JINSI  YA  KUPUNGUZA  UZITO  NA  UNENE KWA  KUTUMIA  TIBA  ASILIA, TAFADHALI TEMBELEA:


7.   Matatizo  Katika  mfumo  wa  Ubongo

Uume  hauwezi  kusimama   bila  ya  kuwa  na ushirikiano  na  ubongo.  Ili mtu  uume  uweze kusimama, mtu  lazima  apate  wazo  la kufanya  tendo  la  ndoa  (UBONGO  UNA HUSIKA  HAPO ), akishapata  wazo, ubungo hupeleka  ishara  kwenye  mishipa  ya  fahamu iliyopo  katika  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo hupeleka  taarifa  kwenye  mishipa  ya  uume then  uume  usimama.   
 
Hivyo  basi  ili  mtu  aweze  kuwa  na uwezo  wa kusimamisha  uume  wake  ni lazima  kuwa  na  mawasiliano  mazuri  na  imara  kati  ya mishipa  ya  fahamu ( ubongo ), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo   na  mishipa  ya  kwenye    uume.  Bila ushirikiano  kati  ya  vitu  hivyo  vitatu, uume hauwezi  kusimama.

Magonjwa  yanayoweza  kuathiri  ushirikiano  kati  ya  mishipa  ya  ubongo  na  mishipa  ya  uume, yanaweza  kusababisha  kushindwa  kusimama  kwa  uume.

Magonjwa  hayo  ni  pamoja  na  kiharusi,kupoteza  kumbukumbu  (  Alzheimer ), multiple  sclerosis pamoja  na  ugonjwa  wa  Parkinson.

Ni  vyema  mgonjwa  akatibiwa  kwanza magonjwa  hayo  kabla  ya  kuanza  kutumia dawa  ya  nguvu  za  kiume.  Kufahamu  jinsi ya  kujitibu  magonjwa  tajwa  hapo  juu  kwa njia  asilia,tafadhali  tembelea

Mambo   mengine  yanayo  sababisha  ukosefu na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni pamoja  na  maumivu & majeraha  kwenye  uti wa  mgongo,  chango  la  kiume , ngiri  na matatizo  katika  homoni.

 VIASHRIA  VYA  MTU  MWENYE  TATIZO  LA UKOSEFU/UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA KIUME.

Mtu  mwenye  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za kiume  huwa  na  dalili  zifuatazo ;

1. Kushindwa  kabisa  kusimamisha  uume wake

2. Uume  kusimama  ukiwa  legelege

3. Kuwahi  kumaliza  tendo  la  ndoa

4. Mwanaume  kutokuwa  na uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  katika  baadhi ya  staili  ( Mara  nyingi   mwanaume huyu huwa  na  uwezo  wa  kufanya tendo  la  ndoa    staili  moja  tu ).  Hapa mwanaume  anakuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  staili  ya   “ missionary” pekee.  Ikibadilishwa   staili, mwanaume  anakuwa hana  tena  uwezo wa  kusimamisha  uume  wake  japo katika  hali  ya  u lege  lege

5. Uume  kutokuwa  na  uwezo  wa kusimama  wenyewe   bila kushikwashikwa  ama  kutomaswa kwa muda  mrefu.

6. Uume  kusinyaa  ukiwa  ndani  ya mwanamke.

7. Uume  kusinyaa, pindi  inapotokea activity  yoyote  ya  kiungo  ama  ogani nyingine  ya  mwanaume  wakati  wa tendo  la  ndoa. Kwa  mfano, wakati  wa tendo  la  ndoa, ikitokea  mwanaume amekohoa  au  kupiga  chafya, uume  nao unasinyaa.

8. Uume  kusinyaa  mara  tu  baada  ya kutolewa  ndani  ya  uke ( Kwa  mfano kama  unafanya  tendo  la  ndoa, halafu uume  ukatoka  nje, kitendo  cha kuushika  kuurudisha ndani, tayari  una sinyaa )

9. Kutokuwa  na  uwezo  wa  kurudia  tendo la  ndoa.

10.  Kupatwa  na  maumivu  wakati  wa tendo  la  ndoa.

VIASHIRIA  VYA  MWANAUME  ASIYE  NA TATIZO  LA UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA KIUME.

Mwanaume  asiye  na  tatizo  la  ukosefu  wa nguvu  za  kiume, huonyesha  ishara  zifuatazo ;

i.Uume  husimama  ukiwa  imara  kama msumari.

ii.Hukaa  kifuani  kwa  muda  mrefu  ( Wastani  ni  kati  ya  dakika  20  hadi  45 )

iii.Huweza  kurudia  tendo  la  ndoa  zaidi ya  mara  tatu  bila  misuli  ya  uume kuchoka.

iv.Huweza  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa staili  yoyote  ile

v.Uume  husimama  wenyewe  bila kushikwa  shikwa  wala  kuwa stimulated  kwa  namna  yoyote  ile

vi.Kwa  ufupi  anakuwa  na  uwezo  wa kufanya na  kukamilisha  tendo  la  ndoa kwa  uukamilifu  mkubwa.

TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  LA UKOSEFU/UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA KIUME.

Dawa  asilia  ya  JIKO   ni  dawa  asilia  inayo tibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.

                              MFUMO   WA  DAWA
Dozi  ya  dawa  ya  JIKO ni  mkusanyiko  wa dawa  nne  asilia  zenye  uwezo  mkubwa  sana katika kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Dawa  hizi  zipo  katika  mfumo  wa  MIZIZI  na UNGA  UNGA.

JINSI   DOZI  YA  DAWA  YA  JIKO  INAVYO FANYA  KAZI.
Dozi  ya  dawa  ya  JIKO  inafanya  kazi zifuatazo  katika  mwili  wa  mwanadamu.

KAZI  INAYO  FANYWA  NA  DAWA  YA  JIKO .
Dawa  ya  JIKO  inasadia  katika  mambo makuu yafuatayo:
1.  Inasaidia   kuimarisha  mishipa  ya  uume  ulio legea  na  hivyo  kuufanya  uume  uwe  na uwezo  wa  kusimama  barabara  kama msumari  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

2. Inasaidia  kusafisha  mishipa  ya  kwenye uume  na  hivyo  kusaidia  katika  kuongeza kasi  ya  msukumo  wa  damu  kwenye mishipa  ya  kwenye  uume.

3. Huongeza  damu  mwilini

4. Husaidia  kuongeza  msukumo (pressure)  wa damu  kwenye  mishipa  ya  uume  na  hivyo kuufanya  uume  kuwa  na  nguvu  za  ajabu.

5. Huipa  misuli  ya  uume  uwezo  wa  kuziba  wa kuizuia  mishipa  ya  vena   kunyonya  damu kwenye  mishipa  ya  uume  wakati  wa  tendo la  ndoa  na  matokeo  yake  kukupa  uwezo wa  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  muda  mrefu

               ( Kuzuia  hali  ya  kufika  kileleni haraka  )

6. Husaidia  kurelax  mind  na  hivyo  kumfanya mtu  awe  na  uwezo  wa  kuconcentrate  wakati wa  tendo la  ndoa   bila  kuathiriwa  na msongo  wa  mawazo

7.  Hurejesha, kuimarisha  na  kuboresha ushirikiano  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  ya  kwenye  ubongo  (nerves), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  mishipa  ya  kwenye  uume
8. Humfanya  mwanaume  awe  na  uwezo  wa kurudia  tendo  la  ndoa  mara  nyingi  zaidi bila  kuchoka.
9. Husaidia  kuongeza  hamu  ya  tendo  la  ndoa.10. Husaidia  kuurudisha  nje  uume  ulio ingia ndani.
11. Husaidia  kutibu  side effects  za  punyeto na  matumizi  ya  muda  mrefu  ya dawa  kali za  (za  kizungu ) za  kuongeza  nguvu  za kiume.

12. Husaidia  kutibu  chango  la  kiume.

13.Dawa  hii  huwasaidia  hata  wanawake wanao sumbuliwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa hamu ya  tendo  la  ndoa.

BEI  YA  DAWA:  Dozi  ya  dawa  ya  JIKO inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI ELFU  THEMANINI  TU  (Tshs.80,000/=)

MAHALI  TUNAPOPATIKANA :
Dozi  ya  dawa  ya  JIKO, inatolewa  na  duka  la dawa  asilia  la  NEEMA 

HERBALIST  &   NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC. Tunapatikana jijini  DAR ES  SALAAM, katika  eneo  la UBUNGO     karibu  na  SHULE  YA MSINGI  UNGUNGO  NATIONAL  HOUSING  NYUMA  YA  JENGO  LA  UBUNGO  PLAZA.

Kwa  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu, tunatoa huduma  ya kuwapelekea  dawa  mahali  walipo ( DELIVERY )

Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  DAR  ES  SALAAM, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  mabasi, wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa kwa   njia  ya  boti  na  kwa  wateja  waliopo Ulaya, America  na  Arabuni, watatumiwa dawa  kwa  njia  ya  DHL  au POSTA.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA

0766  53  83  84.
Na  kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, endelea  kutembelea:

UDA Yazikwa Rasmi.....Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Yavunja Mkataba

0
0

Hatimaye  uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, umevunja mkataba wa uwekezaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam(UDA) na Kampuni ya Simon Group Limited inayomilikiwa na mfanyabiashara, Robert Kisena.

Mkataba huo ambao umekuwa ukipigiwa kelele ndani na nje ya Serikali, umetajwa kutokufuata taratibu za kisheria na kukiuka Sheria ya Manunuzi (PPRA).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita alisema uamuzi huo umefikiwa, baada ya kufanyika kikao halali cha Baraza la Madiwani.

Aidha baraza hilo la madiwani pia limeamua kwamba, asilimia 51 ya hisa zilizokuwa zinamilikiwa na kampuni hiyo zirudishwe chini ya uongozi wa jiji hilo.

Mwita alisema madiwani walipitia upya mkataba wa uwekezaji kati ya kampuni hiyo na Halmashauri ya Jiji, ambapo walibaini udhaifu katika maeneo mbalimbali wakati wa makabidhiano.

Meya huyo anayetokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutoshirikishwa wakati wa makabidhiano.

“Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imevunja mkataba wa makubaliano ya kuuza Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa mfanyabiashara Robert Kisena, baada ya kubaini kuwapo udhaifu wakati wa kuuza shirika hili,” alisema.

Mwita alisema halmashauri ya jiji kipindi hicho, haikufuata utaratibu wa utangazaji wa zabuni wakati wa kuuza shirika hilo, hali iliyoonyesha wazi  viongozi waliokuwa madarakani wakati huo, walikuwa na maslahi binafsi katika kukabidhi shirika hilo mikononi mwa kampuni hiyo.

Alisema hadi sasa shirika hilo bado limesajiliwa kwa jina la Halmashauri ya Jiji kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), hali inayowapa nguvu ya kuvunja mkataba huo kwa sababu mmiliki wake kisheria bado ni jiji.

“Tuliambiwa Simon Group, alikuwa anakwenda benki kuchukua mikopo kwa hati ya Shirika la UDA, tumefuatilia benki mbalimbali tumebaini hakuna hata hati moja ya shirika iliyowasilishwa kwenye benki  kama dhamana ya mikopo,”alisema.

Alisema shirika hilo hadi sasa lina Sh bilioni 5.9 ambazo zililipwa na Simon Group kama malipo halali ya kuuziana shirika, jambo ambalo haliko sawa.

“Hatuwezi kuona mikataba ya kifisadi inaendelea kuimaliza Serikali, lazima tuchukue hatua ambazo ni pamoja na kuangalia taratibu za kisheria ili kuivunja,’ alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, baraza hilo limeunda timu ya watu watatu wakiongozwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ili kuangalia athari ambazo zinaweza kujitokeza wakati wa kuvunjwa kwa mkataba huo.

Akizungumzia hatua hiyo, Ofisa Habari wa Kampuni ya Simon Group, Deus Bugaywa alisema hadi sasa halmashauri ya jiji haijatoa taarifa yoyote ya kuonesha kama mkataba huo umevunjwa, licha ya magari ya UDA kuanza kazi leo.

“Hatujapewa taarifa yoyote ambayo inasema mkataba kati ya UDA na Halmashauri ya Jiji umevunjwa, tunaamini bado ni wana hisa halali tutafanya kazi kwa ubia kama ulivyo mkataba wetu,”alisema Bugaywa.

Alisema kampuni hiyo, ilifuata taratibu zote za kisheria wakati wa kuingia makubaliano, wala hakukuwa na ukiukwaji wa kisheria.

Alisema kama watakabidhiwa barua ya kuvunjika kwa mkataba huo, wataangalia taratibu za kisheria ili waweze kudai haki yao.

UKAWA Wadai Rais Magufuli Ndo Chanzo cha Sukari Kuadimika Nchini

0
0

Kambi  Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema tatizo la sukari nchini limetokana na uamuzi usio sahihi wa Rais Dk. John Magufuli, kwa kupiga marufuku uingizwaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi bila kufanya tathmini.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Waziri Kivuli wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Anthony Komu, alisema agizo hilo lilitolewa kwa kukurupuka na ndilo lililosababisha sukari kuadimika.

Komu ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Vijijini, alisema kama malengo ni kulinda viwanda vya ndani, basi lisifanyike kwa sukari pekee kwa sababu viwanda vipo vingi na bado bidhaa zinaingia kutoka nje nchi.

Alisema kuna harufu ya upendeleo kutokana na Rais kuwa swahiba wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye ni mmiliki wa mashamba ya Mtibwa, hivyo amefanya hivyo kwa kupewa ushauri mbaya huku nchi ikiingia kwenye upungufu mkubwa wa sukari.

Alihoji kwa nini apige marufuku kwenye sukari tu wakati kuna viwanda vya nondo, saruji na vinginevyo na vinaleta bidhaa kutoka nje.

Alisema kilichofanywa na Rais ni kukurupuka na ni kuvunja sheria.

Komu alisema kitendo cha Rais kutoa amri ya walioficha sukari wany’ang’anywe, ni kupora haki za watu na kuua mitaji yao kibiashara.

“Hakuna sheria ambayo inaruhusu kwenda kukagua maghala ya wafanyabiashara na kugawa bidhaa bure, hii hali hata wawekezaji wataogopa kuja kuwekeza nchini kwa sababu wataona mazingira ya hapa nchini ni hatarishi," alisema Komu.

Alisema serikali iandae njia mbadala ya kuwafidia watu walionyang’anywa maana wengine wamekopa kwenye taasisi za kifedha.

“Agizo la Rais lina walakini, kwani ni nani katika biashara za watu...tunakokwenda ni kubaya kwani upungufu wa sukari ulijulikana tangu Februari, lakini akapiga marufuku sukari kutoka nje,” alisema Komu.

Alisema katika tafiti mbalimbali ikiwamo ripoti iliyotolewa na Shirika la BBC, mahitaji ya sukari nchini kwa mwaka ni tani 590,000, lakini uwezo uliopo ni tani 300,000, hivyo serikali ilikuwa ni busara iruhusu kuingizwa kwa sukari kwa sababu viwanda vya ndani vimekosa uwezo.

Alisema Rais anatakiwa kukemewa na kuambiwa kwamba anakwenda kinyume na kwamba wao kambi ya upinzani hawatetei wanaoficha sukari, lakini serikali itafute namna ya kukabili hali hiyo.

Naye Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, alisema taifa lina viwanda vinne vikubwa vya sukari, lakini bado havina uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha.

Alisema serikali imefanya sukari ionekane kama dawa za kulevya kutokana na kuadimika huko.

Alisema sukari hadi iletwe nchini, ni takriban wiki tano na wanaoingia kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani watahitaji sukari kushinda vitu vingine.

“Sisi hatutetei walioficha, lakini wamenunua ili kuuza kwa taratibu kulingana na bei ya soko wasibughudhiwe maana kuna hatari ya benki kushindwa kurejeshewa fedha zilizokopwa,” alisema Kubenea.

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari Ajisalimisha Polisi, Ahojiwa Kwa Masaa 6

0
0

Polisi wilayani Arumeru jana iliwashikiliwa kwa muda mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na madiwani 35 wa Chadema kwa tuhuma za kuvamia eneo na kuharibu mali.
 
Viongozi hao, wiki iliyopita walivunja uzio wa mabati uliojengwa jirani na halmashauri na mfanyabiashara Itandumi Makere, wakimtuhumu kupata eneo hilo la Serikali kinyume cha sheria.
 
Nassari na madiwani hao, walishikiliwa kwa muda baada ya kujisalimisha katika Kituo cha Polisi Usa River. Viongozi hao, baada ya kufika polisi saa tatu asubuhi walihojiwa kwa zaidi ya saa sita kwa tuhuma hizo.
 
Nassari alisema kitendo hicho cha kufikishwa polisi na kuhojiwa hakiwatishi kwani wanachokifanya ni kutetea ardhi ya Wameru.
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Meru, Wille Njau alisema wamedhalilishwa na hatua hiyo kwani walikuwa wanatekeleza uamuzi ya Baraza la Madiwani.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alikiri kuhojiwa kwa mbunge na madiwani hao na kusema wanafanya uchunguzi na jalada litawasilishwa kwa mwanasheria mkuu wa Serikali.

Majaliwa Akutana Na Wawekezaji Wa Umeme Wa Gesi Toka Japan

0
0
Shirika la Koyo la kutoka Japan limepania kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na umeme jua ili kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi waishio vijijini.

Hayo yamesemwa jana jioni (Jumatatu, Mei 9, 2016) na Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa shirika la Koyo, Bw. Norio Shoji wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam.

“Tumepanga kuwekeza kwenye maeneo matano ambayo mojawapo ni kujenga mtambo wa kuchakata gesi kwa kutumia gesi asilia inayozalishwa hapa nchini. Mtambo huu utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 1,000 za umeme,” alisema.

“Pia tunao mpango wa kujenga mitambo ya umemejua inayoweza kujiunganisha kwenye gridi (on-grid/off grid solar power plants) kwa ajili ya maeneo vijijini  na yale yasiyofikika kwa urahisi zaidi ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa usambazaji umeme kwenye gridi ya Taifa ili Tanzania iweze kuzalisha zaidi nishati hiyo na kuiuza nchi jirani,” aliongeza.

Bw. Shoji alimweleza Waziri Mkuu kwamba wana nia ya kuwekeza pia katika sekta nyingine kama kilimo, sayansi ya tiba (medical science), usafishaji na uyeyushaji madini (refinery-smelting), uzalishaji wa bidhaa za viwandani na teknohama.

Akifafanua zaidi Bw. Shoji alisema shirika lake kwa kushirikiana na makampuni mengine makubwa ya Japan pamoja na Serikali ya nchi hiyo wamedhamiria kuwekeza kwenye miundombinu hiyo kwa sababu wanataka Tanzania iwe ni kitovu (hub) cha uzalishaji na iweze kulisha nchi jirani katika SADC na EAC.

Akitolea mfano, Bw. Shoji alisema mbali na miradi mingine wanayotaka kuwekeza, gharama za kuweka mtambo wa kuzalisha megawati 1,000 za umeme hazitapungua kiasi cha dola za marekani bilioni moja (sawa na sh. trilioni 2.2).

Waziri Mkuu alimshukuru Bw. Shoji kwa nia yake aliyoionyesha na akamtaka achague eneo mahsusi kwa sababu Tanzania inahitaji umeme wa kutosha katika kutekeleza azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.

“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ili kuongeza ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake. Tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye nishati ya umeme katika mikoa ya Kusini, ya Kaskazini, ya Magharibi na hata mikoa ya kati,” alisema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, Bw. Suleiman M. Nassor alisema shirika la Koyo litafanya uwekezaji huo kwa kushirikiana na kampuni ya SSF Limited ambayo inajihusisha na masuala ya nishati.

“Tunashirikiana na shirika la Koyo pamoja na Serikali ya Japan ili kuleta unafuu wa maisha kwa Watanzania wenzetu,” alisema Bw. Nassor.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Kampuni ya Japan ya KOYO na   kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited ambazo kwa pamoja  zimekusudia  kushirikiana ili kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam May 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  KOYO ya Japan, Bw.  Norio Shoji  baada ya kukutana na Mtendaji huyo na ujumbe wake ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. Kampuni hiyo ikishirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited inakusudia kuwekeza  kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kumwakilisha Rais Magufuli London.

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni (Jumanne, Mei 10, 2016) kwenda London, Uingereza kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi unaojadili suala la kupambana na rushwa (Anti-Corruption Summit 2016) utakaofanyika Mei  12, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana, Waziri Mkuu amesema anaenda kumwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli kwa sababu siku hiyo hiyo, atalazimika kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Museveni.

“Mheshimiwa Dk. Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na siku hiyo hiyo, mmoja wa marais wa nchi wanachama anaapishwa. Kwa hiyo amelazimika kwenda kuhudhuria sherehe hizo,” alifafanua Waziri Mkuu.

Akizungumzia kuhusu mada ya mkutano huo, Waziri Mkuu amesema Tanzania inafanya vema katika mapambano dhidi ya rushwa na kwamba baadhi ya nchi zimeanza kuvutiwa na juhudi ambazo Serikali imekuwa ikichukua.

“Waziri Mkuu wa Uingereza ameandaa mkutano huu na alimwalika Mheshimiwa Rais Magufuli ili ahudhurie akiwa ni miongoni wa wakuu wa nchi 60 watakaohudhuria mkutano huo. Tanzania ni miongini mwa nchi mbili kutoka bara la Afrika ambazo zimealikwa kushiriki. Nchi nyingine ya kutoka Afrika ni Nigeria,”alisema.

Waziri Mkuu atafuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola, wataalamu wa sekta ya rushwa na wanasheria

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU-2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MEI 10, 2016.

Waziri Mkuu: Serikali Itaagiza Tani 70,000 Za Sukari

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaagiza kutoka nje ya nchi tani 70,000 za sukari ambapo kati ya hizo, tani 11,957 zimeshawasili nchini na zitaanza kusambazwa kesho (Jumatano).

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 10, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Akitoa ufafanuzi wa sukari ambayo imekwishawasili nchini, Waziri Mkuu alisema tani 2,000 zitapelekwa mikoa ya Kaskazini, tani 3,000 (mikoa ya Kanda ya Ziwa), tani 2,000 (mikoa ya Kusini), tani 2,000 (Nyanda za Juu Kusini) na tani 2,000 (mikoa ya Kanda ya Kati).

“Tani nyingine 24,000 za sukari zitawasili Ijumaa hii na hadi zitoke bandarini itakuwa kama Jumapili kwa hiyo zinaweza kusambazwa kuanzia Jumatatu. Tani nyingine 20,000 zitawasili baadaye, ama mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi Juni,” alisema Waziri Mkuu.

Amesema anawataka Watanzania wasihofu kuhusu uhaba wa sukari uliojitokeza hivi karibuni kwani umesababishwa na watu wachache. 

“Mheshimiwa Rais ameagiza watu waliohodhi bidhaa hii wakamatwe na sukari isambazwe. Lakini pia tunaagiza kwa muda mfupi kwa sababu viwanda vyetu vinatarajia kuanza uzalishaji ifikapo Julai,” alisema.

Amewataka wasambazaji wa sukari waziuze kwa wafanyabishara wadogo ili wao wawawuzie wananchi kwa bei elekezi ya sh. 1,800. 

Pia amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi la ukaguzi ili kubaini zaidi wale waliohodhi bidhaa hiyo.

Akifafanua kuhusu mkakati wa Serikali kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, Waziri Mkuu amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha tatizo la uhaba wa sukari nchini linakwisha ifikapo 2019. 

“Wananchi wasiogope, Serikali imechukua hatua kwa udhibiti mzuri ili tusije kuporomosha soko letu la ndani,” alisema.

“Tunao mkakati wa kuboresha viwanda vya ndani, wenye viwanda wenyewe au kwa ubia na wawekezaji kutoka nje, wanaweza kufungua mashamba kwenye maeneo matatu tuliyotenga kwa ajili hiyo,” alisema.

“Serikali imetenga maeneo matatu yanayofaa kwa kilimo cha miwa huko Bagamoyo, Ngerengere na Kigoma. Huko wanaweza kulima na kujenga viwanda vya sukari na uzalishaji ukawa unapanda mwaka kwa mwaka hadi tutakapoweza kuimaliza hii gap iliyopo,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
S . L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MEI 10, 2016.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Akagua Daraja la Nyerere Leo

0
0


Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipewa maelezo ya awali na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipokagua daraja hilo leo Mei 10, 2016. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akionyeshwa barabara zinazopishana ya juu na ya chini, alipokagua daraja ya Nyerere, Dar es Salaam, leo Mei 10, 2016.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiuliza jambo, alipokagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo Mei 10, 2016. Kushoto ni Mama Salma Kikwete.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembea kwenye daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo Mei 10, 2016, walipokagua daraja hilo.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama moja ya ofisi zitakazotumiwa na magari kulipia ushuru wa kutumia daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo leo Mei 10, 2016. (Picha na Bashir Nkoromo).

Chadema Kuijadili Serikali ya Rais Magufuli

0
0

Kamati Kuu ya Chadema itakutana mjini Dodoma katika kikao chake cha kikatiba kuanzia Mei 11 Jumatano na Alhamisi kitakachojadili mwenendo wa Serikali ya CCM chini ya Rais John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene imesema kikao hicho, pamoja na mambo mengine, kitajadili taarifa ya hali ya siasa nchini.

Pia kikao hicho kitajadili na kupitisha mpango kazi wa chama kwa mwaka huu unatokana na Mpango Mkakati wa Chama wa miaka 5 kabla ya Sekretarieti kuanza utekelezaji.

Mpango huo utahusisha shughuli mbalimbali za chama ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa chama nchi nzima na kuendelea kuwatumikia wananchi.

Mbunge Adai Kuna Wabunge Wanavuta Bangi na Madawa ya Kulevya Bungeni

0
0

Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Msabaha (Chadema) ametoa tuhuma nzito kuwa ndani ya Bunge kuna wabunge vijana wanaovuta bangi na kutumia dawa za kulevya.

Mbunge huyo amemuomba Rais John Magufuli kuagiza wabunge wa aina hiyo ambao hata hivyo hakuwataja wapelekwe Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili kufundishwa nidhamu.

Msabaha ametoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Ulinzi na JKT iliyowasilishwa na Waziri mwenye dhamana na Wizara hiyo, Dk Hussein Mwinyi.

“Wabunge nao waende JKT kwa sababu hili Bunge wameingia vijana wengine ambao ni mateja wa unga na wengine wanavuta bangi. Wengine wanawavua mama zao nguo,” amesema Msabaha.

“Wengine mama zao wameshakufa wanakuja humu wanawatukana mpaka wazazi wao. Kwa hiyo niombe Rais Magufuli vijana wote wabunge ambao hawana nidhamu waende JKT,” alisisitiza.

Mbunge huyo amesema wabunge wa aina hiyo hawana viwango vya kuzungumza ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria hivyo ni vyema waende JKT ili wakirudi wawe wamejua namna ya kuchangia.

Ingawa hakumtaja Mbunge yeyote, lakini mchango  ulioibua mtafaruku bungeni ni wa Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyedai wabunge wa viti maalumu Chadema huitwa Baby ili kupewa nafasi hiyo.

Tafsiri ya kauli hiyo ni kuwa wabunge wa viti maalum Chadema lazima wafanye mapenzi au kuwa na mahusiano na viongozi wa juu wenye mamlaka ndani ya chama hicho ndipo wateuliwe kuwa wabunge.

Idadi ya Simu Bandia Yapungua nchini.....TCRA Yatoa Onyo Kwa Wanao Flash Simu

0
0

Serikali imewataka wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi (mobile devices) kuacha mara moja tabia ya kubadilisha namba tambulishi (‘kuflash’) za vifaa hivyo kwani  watakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 10 au faini isiyopungua Sh. milioni 30 au vyote viwili.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

“Namba tambulishi  (IMEI) za vifaa vyote vya mawasiliano ya mkononi ambavyo vimeibiwa,vimeharibika,kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaruhusiwa kuunganishwa kwenye mitandao ya watoa huduma ifikapo tarehe 16 June 2016, "alisema Mungy.

Akizungumzia kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya simu zote zisizokidhi viwango, Mungy alibainisha kuwa idadi ya  simu hizo imeshuka kutokana na elimu ambayo wameitoa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Alisema  lengo la elimu hiyo kwa umma ni kujenga uwezo kwa wananchi kutambua simu zisizokidhi vigezo kabla ya kufika ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini.

Mungy alifafanua kuwa uchambuzi wa IMEI unaonyesha kuwa hadi Februari,2016  idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia tatu ambapo namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 18 na simu halisi zilikuwa sawa na asilimia 79.

“Kwa mwezi Machi 2016 ulionyesha kuwa Idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango ni asilimia nne, na idadi ya zile zilizonakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 13 ambapo uchambuzi huu umehusisha taarifa za kampuni zote za simu nchini,’’. alifafanua Mungy.

Aliongeza kuwa matokeo hayo mazuri ni matunda ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya mamlaka hiyo, Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Tume ya Ushindani (FCC),kampuni za simu, pamoja na wadau wengine katika kuelimisha umma juu ya uhakiki wa simu walizonazo ikiwa ni pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua simu ikiwemo kuzihakiki ubora wake.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Mawasiliano  wa Mamlaka hiyo, Injinia Gabriel Mruma amesema kuwa ni vyema Watanzania wakajenga utamaduni wa kununua simu  zenye ubora kuepuka usumbufu wakati Tanzania inapoelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia.

TCRA ina dhamana ya kusimamia shughuli za mawasiliano ya Kielektroniki na Posta hapa nchini.

Kuwepo kwa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2011 kumewezesha kutekelezwa kwa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi.

Mfumo huu wa kielektroniki ulizinduliwa tarehe 17, Desemba 2015 na unahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi kwa lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vilivyoibiwa,kuharibika au kupotea,bandia vya mawasiliano katika soko.

Hizi ndizo tozo za kutumia Daraja la Nyerere

0
0
Serikali imetangaza rasmi kuanza kwa tozo kwa vyombo vya usafiri vitakavyopita katika daraja la Nyerere kuanzia Jumamosi tarehe 14 ,mwezi huu.

Akizungumzia na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kuwa kuanzia  siku   hiyo , vyombo  vyote vya usafiri vitatakiwa kulipia ushuru wa kupita katika daraja la Nyerere.

“Tumeanza kutoza tozo hii mara baada ya kufunguliwa kwa daraja hili na kuanza kutumika kwa kupita bila kulipa kwa vyombo vya usafiri  tangu Aprili 19 mwaka huu na sasa tunaanza rasmi kutoza tozo kwa ajili ya kukusanya gharama za usimamizi, utunzaji na uendeshaji wa daraja hili.” alisema Mhandisi Nyamhanga.

Mhandisi  Nyamhanga amefafanua kwamba watembea kwa miguu watapita bure katika daraja hilo huku wenye baiskeli wakilipia Sh. 300, pikipiki Sh. 600, waendesha maguta ,bajaji na magari ya kawaida(Saloon Cars) watatakiwa kulipia Sh.1500.

Mabasi yanayobeba  abiria 15 yatalipia  Sh. 3,000, yale ya abiria zaidi ya 15  Sh. 5,000  na yale yanayobeba  abiria zaidi  ya 29 yatalipia Sh. 7,000.

Aidha magari yenye tani zaidi ya mbili mpaka saba yatalipia Sh. 7,000, tani 7 hadi 15 watalipa Sh.10,000, tani 15 mpaka 20 watalipa Sh.15,000  na yale yenye  tani 20 mpaka 30 yatalipia Sh. 20,000.

Mhandisi Nyamhanga ameongeza kuwa magari yenye namba za Jeshi la Wananchi(JWTZ), Jeshi la Polisi(PT), Jeshi la Magereza(MT), gari za wagonjwa, magari ya zimamoto na magari yenye vibali maalum yataruhusiwa kupita bure.

Serikali Yakata Rufaa Kwa Mara Pili Kupinga Bosi wa Zamani wa TRA na Wenzake Kufutiwa Shitaka la Kutakatisha Pesa

0
0

Upande wa Jamhuri umekata rufaa kwa mara ya pili katika kesi inayowakabili Harry Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomoni katika Mahakama ya Rufaa baada ya rufaa hiyo kukataliwa katika Mahakama Kuu.

Kitilya, alikuwa Kameshina Mkuu wa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Sinare, Mkuu wa Idara ya ushirikiano na Uwekazaji Katika Benki ya Stanbic na Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic

Rufaa hiyo imekatwa na Buswalo Mganga, Mwendesha mashitaka wa Serikali (DPP) katika kesi hiyo baada ya kutoridhika na uamuzi wa Mahakama Kuu ulifanywa wiki iliyopita na Moses Mzuna, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Mganga alitangaza kukata rufaa mara baada kushindwa pingamizi lao la kupinga kufutwa kwa shitaka la nane la utakatishaji fedha lililofutwa na Emilis Mchauru Hakimu Mkazi Kisutu.

Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kutenda makosa saba baada ya kufutwa kosa la nane na kwamba bado watuhumiwa hao wapo lumande.

Jalada la kesi hiyo lipo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwamba kesi hiyo ilipangwa kutajwa tena tarehe 18 Mei mwaka huu.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya May 11

Mwanafunzi Askari Chuo cha Anga cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ajiua Kwa Kujipiga Risasi

0
0

Mwanafunzi wa Chuo cha Anga (Skua) cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopo Kange jijini Tanga, Philip Fred (28) amejiua kwa kujipiga risasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kwamba tukio hilo ni la jana saa 1.15 usiku katika chuo hicho kilichopo kata ya Maweni nje kidogo ya jiji.

Alisema askari mwenye cheo cha Koplo mwenye namba MT 81627 alijiua wakati akiwa katika eneo la lindo chuoni hapo.

“Kimsingi chanzo cha kifo cha askari jeshi huyo bado hakijajulikana na imefahamika kwamba alikuwa ni mwanafunzi wa ‘Level one’ chuoni hapo na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa Bombo”, alisema Kamanda.

Katika tukio jingine Kamanda alisema askari wanamshikilia mkazi wa mtaa wa Mgwisha, kata ya Pongwe jijini Tanga, Masudi Hamis (22) kwa tuhuma za kukutwa na sare moja ya askari wa JWTZ.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images