Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Naibu Waziri Anthony Mavunde Apewa Maji Machafu na Wapiga Kura Wake Ili na Yeye Ayanywe

$
0
0

Wakazi wa Kijiji cha Nala na vitongoji vyake juzi walimpelekea maji machafu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde wakimtaka ayanywe kwa kuwa ndiyo wanayotumia.

Mavunde alikutana na mkasa huo muda mfupi alipoingia kwenye kijiji hicho umbali wa kilomita tisa nyakati za jioni, ambako wakazi wa eneo hilo walikuwa wakimsubiri tangu asubuhi. 

Mama mmoja aliyekuwa eneo hilo, alifika na chupa ya maji akimtaka Naibu Waziri ayaonje mbele yao, kwani nao ni binadamu kama yeye na wanayatumia, lakini Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Paul Luhamo alimzuia kuyanywa.

Pamoja na taarifa ya kijiji iliyotolewa na Ofisa Mtendaji wa Kata, Mathias Ndologa, wakazi hao walilipuka na kupiga kelele wakiipinga taarifa hiyo kwamba iligusa kwa juu matatizo yao, lakini ikaacha jambo kubwa la maji.

Kwenye risala yake, Ndologa alikuwa ameelezea suala la maji, umeme, miundombinu na upungufu wa madawati, lakini kelele zilizidi kutoka kwa wananchi wakisema jambo la msingi kwao ni moja tu, yaani maji.

Muda mfupi kelele zilianza watu wakitaka kuuliza mambo waliyoyaita ni ya msingi, ndipo Mavunde akaamuru wapewe nafasi ya kuuliza kwanza kabla hajasimama kuwasalimia.

Mmoja wa wauliza maswali alikuwa Daudi Lusinde, ambaye alieleza namna wakazi wa kijiji hicho wanavyopata adha kubwa katika kutafuta maji ambayo aliyaita ni kama dhahabu kwao.

Lusinde alisema wamepata tabu hiyo kwa muda mrefu na bado hawajaona mwanga wa matumaini zaidi ya kuendelea kuumia huku ndoo ya maji ikifikia bei ya Sh500.

“Bei ya sukari inapanda kila kukicha, lakini siyo shida hapa tatizo ni maji, mheshimiwa sisi tunanunua maji kwa gharama kubwa na ukishindwa kiasi hicho unalazimika kuchangia maji na mifugo sijui kama tutapona,” alisema Lusinde na kusababisha mkutano kulipuka kwa shangwe.

Uongozi wa kijiji na chama wilaya ulizuia kelele za vijana waliomtaka mbunge huyo aende hadi maeneo wanayochota maji akajionee, ikiwamo uchafu wa maji pamoja na umbali wake.

Akijibu hoja hizo, Mavunde alieleza kusononeshwa na kuahidi kuanzia leo ataanza kutekeleza ahadi yake hiyo kabla ya kufanya jambo lolote.

“Kwa kweli maji ni moja ya ahadi nilizoahidi kwenu, kesho ni Jumapili siyo siku ya kazi, lakini kuanzia keshokutwa (Jumatatu) nitaleta hapa wataalamu kuanza kuchimba kisima kwa gharama zangu,” alisema Mavunde.

Huku akiwa amesimama na maji aliyopewa, alisema yuko tayari kuacha shughuli za Bunge akashirikiane nao kuhangaikia maji, hadi pale watakapoyapata na kuanza kujenga matangi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Naibu Waziri alisema katika kipindi cha kampeni alifika eneo hilo na kuahidi kuwapatia maji, lakini muda ulikuwa bado. Hata hivyo, Serikali ya awamu ya tano ina miezi sita madarakani.

“Hiyo ilikuwa ni sehemu ya ahadi yangu kwenye kampeni, kwa hiyo matatizo ya maji hapa nayajua na kweli ni makubwa, ndiyo maana nimeamua kuvuruga kila ratiba ili niokoe watu hawa kweli wako kwenye mateso,” alisema.

Mhandisi wa Maji Manispaa ya Dodoma, Simon Sasala alisema kijiji hicho kina wakazi 7,600 ambao wanahitaji lita 230,000 za maji kwa siku, lakini kuna kisima kinachotoa lita 89,000 na wakati mwingine hakifanyi kazi. 

Sasala alisema maji hayo hayatoshelezi kwani yapo kwa asilimia 39, hali ambayo inawapa shida hasa kina mama kutokana na wengi wao kulazimika kufuata maji ya kutumia umbali mrefu.

Aswekwa Mahabusu Kwa Kusema Uongo Mbele ya Mkuu wa Mkoa

$
0
0
Mkazi wa Kijiji cha Natambiso, Kata ya Natta wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, Christopher Nyamasagi ameswekwa mahabusu kwa tuhuma za kutoa taarifa ya uongo kuwa mjumbe mmoja mwanamke aliombwa rushwa ya ngono ili wapate mikopo ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Alitoa madai hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Msingi Natta Mbisso mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo.

Kabla ya kukamatwa, Nyamasagi aliyekuwa na bahasha ya kero mkononi, alidai kuwa walichanga fedha ili waanzishe Saccos ya kukopeshwa fedha na NSSF Mkoa wa Mara.

“Mkuu wa Mkoa tulikamilisha vigezo vya usajili, baada ya kuchangia zaidi ya Sh11 milioni, wakatoa elimu namna ya uendeshaji na baadaye tukafungua akaunti mwaka 2014, tukaanza kufuatilia mikopo, tulisumbuliwa sana na kufikia hatua ya kutuambia kama tunataka mkopo, mjumbe mmoja mwanamke atoe rushwa ya ngono ili tupatiwe,” alidai Nyamasagi.

Wakati mkuu huyo wa mkoa akishangazwa na madai hayo, alisimama mwanamke mmoja wa kijiji hicho na kukanusha huku akitaka Nyamasagi awaombe radhi wanawake kwa taarifa yake ya uongo inayolenga kuwadhalilisha.

Ndipo Mulongo alimuagiza kamanda wa polisi wilayani hapo amkamate Nyamasagi na kumuweka mahabusu kwa tuhuma za kudanganya. Alisema kikao hicho kililenga kujadili kero na siyo kudhalilishana.

Polisi Waua Majambazi Wawili Mkoani Mwanza...... Walikuwa Wakitaka kuiba Nyumbani kwa Mfanyabiashara wa Madini

$
0
0

Watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mkoani Mwanza baada ya kurushiana risasi na askari wakati wakiwa kwenye harakati za za kuvamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa madini, Baraka Said.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Augustino Senga alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita saa 5:30 usiku katika Mtaa wa Kigala Kata ya Buswelu Wilaya ya Ilemela. Alisema katika tukio hilo polisi walikamata silaha moja na risasi 21.

Senga alisema majambazi hao waliokuwa wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 na 45 hawajafahamika majina wala makazi yao.

“Baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuwapo kwa majambazi yanayokusudia kuvamia kwa mfanyabiashara huyo, tuliweka mtego eneo la tukio ndipo majambazi hayo yalikuja yakiwa kwenye gari jeusi majira ya saa tano usiku,” alisema Senga.

Katika tukio jingine, Wakazi wa stendi mpya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Daudi Joseph (32) na Magashi Mzee wameuawa kwa kupigwa mawe na fimbo na wananchi baada ya kudaiwa kuwatapeli wafanyabiashara wa ng’ombe.

Tukio hilo lilitokea Mei 5, saa saba mchana katika mnada wa mifugo uliopo Kijiji cha Maligisu wilayani Kwimba Mkoa wa Mwanza.

Senga alisema walichukua fedha kwa wafanyabiashara hao wa mifugo wakidai kuwauzia ng’ombe, lakini badala yake walitokomea pasipo kufanya hivyo.

Wakati huohuo, watu wanne wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamevamia duka na kupora fedha ambazo haijajulikana kiasi chake.

Senga alisema tukio hilo lilitokea katika Kata ya Kishiri, wilayani Nyamagana.

Alisema watu hao walivamia duka hilo linalomilikiwa na Phares Grabriel (56).

Senga alisema pia walivamia duka la jirani la Revocatus Phares(28) na kuiba kompyuta mpakato, simu moja na kutokomea na pikipiki.

Vigogo Chadema Kyela Wavuliwa Uongozi kwa Usaliti

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, Saadati Mwambungu pamoja na wajumbe 19 wa kamati ya utendaji wa wilaya hiyo, wamevuliwa uongozi baada ya kutuhumiwa kukihujumu chama.

Hatua hiyo ilifikiwa juzi jioni na uongozi wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, chini ya mwenyekiti wake, Dk Stephen Kimondo na Mratibu wa Kanda, Frank Mwaisumbe na kuweka wilaya hiyo chini ya uangalizi wa uongozi wa Mkoa wa Mbeya ndani ya siku 30 wakati wakiendelea na uchunguzi.

Mratibu wa Chadema katika Kanda hiyo, Frank Mwaisumbe alisema jana kuwa baada ya kufanyia kazi tuhuma 17 zilizowasilishwa kwao na wanachama wa chama hicho wilaya, walibaini kuwa tuhuma saba kati yake zina ukweli dhidi ya viongozi hao hivyo wakafikia uamuzi wa kuwasimamisha na kuwataka kurudisha mali zote za chama hicho ndani ya siku 30.

“Ni kweli jana (juzi) tulifika Kyela na katika kikao chetu na kamati ya utendaji ya wilaya tulipowahoji ilionekana tuhuma saba zina ukweli na baadhi ya watuhumiwa walikiri. Miongoni mwa tuhuma hizo ni matumizi mabaya ya fedha na mali za chama, kutoshiriki vyema Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana hadi tukapoteza jimbo, hususani siku ya kuhesabu kura za jumla viongozi walikimbia.

“Siku ile ya uchaguzi wa mwaka jana kuna vijana wetu walikamatwa wakituhumiwa kuvunja ofisi pale halmashauri ya Kyela na wakahukumiwa, lakini hakuna kiongozi yeyote ngazi ya wilaya aliyethubutu hata kwenda kuwaona pale gerezani hadi walipojinasua wenyewe,” alisema Mwaisumbe.

Alisema kutokana na mkutano wao wa juzi wajumbe wake kutotimia ili kufikia uamuzi halali wa kuwachukulia hatua zaidi, uongozi wa Kanda uliamua kuwasimamisha na chama kuwa chini ya mkoa, huku ukifanyika utaratibu wa kuitisha mkutano mkuu ambao utawajadili kwa kina na kuona kama watafukuzwa moja kwa moja au la.

Mwambungu alipoulizwa juu ya kutimuliwa kwao, alikiri huku akisisitiza kwamba tuhuma zilizotolewa hazina ukweli wowote kikatiba, na badala yake zimetengenezwa na ‘genge’ la watu wachache kwa uchu wa madaraka, lakini hana kinyongo kusimamishwa uongozi kwa kuwa ipo kikatiba ndani ya Chadema.

Alisema; “Kwanza ni heshima kwa kuwa jambo hili lipo kikatiba. Lakini katika mkutano wa juzi akidi ya wajumbe haikutimia kwani Chadema Wilaya ya Kyela ina wajumbe 349 wa mkutano mkuu, lakini kwa juzi wajumbe waliohudhuria walikuwa 120 tu.

“Ndiyo maana uongozi wa Kanda ulitoa siku 30 za kufanyika mkutano mkuu utakaowajumuisha wajumbe wote 349 na ndipo itakapofahamika… kama ni kufukuzwa au kuendelea na uongozi,” alisema.

Mwambungu alisema kati ya wajumbe 19 wa kamati ya utendaji ya wilaya, wajumbe saba waliamua kujiuzulu uongozi na baadaye wakaungana na wengine ambao waliunda tuhuma hizo kwa lengo na kuuangusha uongozi ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mwaka 2020.

Spika wa Bunge Job Ndugai Awaonya Wabunge Kuhusu Kujihusisha na Rushwa.......Awataka Wajiandae Kuupokea Muswada Unaozuia Wafanyabiashara Kuwa Wanasiasa

$
0
0

Spika wa Bunge, Job Ndugai, ametaja sababu zinazochochea wabunge kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa, ni presha kutoka kwa wananchi inayotokana na kutakiwa kuchangia masuala mbalimbali katika majimbo yao.

Spika huyo pia amewatangazia rasmi wabunge kuwa Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inatarajia kuwasilisha bungeni muswada wa sheria utakaotenganisha uongozi na biashara.

Aliyasema hayo wakati akizungumza katika uzinduzi wa Chama cha Wabunge wanaopambana na Rushwa (APNAC), mjini Dodoma. Aliwataka wabunge hao kujiepusha na vitendo vya rushwa licha ya kuwa na maslahi madogo.

Pia aliwataka wajiandae na sheria hiyo kutokana na ukweli kuwa katika bunge hilo wabunge wengi pia ni wafanyabiashara. 

Presha za rushwa 
Alitaja sababu za wabunge wa Tanzania kujiingiza kwenye rushwa ni presha za wananchi wao kuwataka wachangie kila inapotokea msiba, sherehe, madawati, madarasa, barabara hadi ada.

Alisema kutokana na kipato kidogo cha fedha, wabunge wengi hutafuta mbinu mbadala za kupata fedha kumudu gharama hizo. Mishahara ya wabunge na marupurupu yake kwa mwezi yanakadiriwa kufikia zaidi ya Sh milioni 11 kwa mwezi.

Sababu nyingine ni mikopo yenye riba kubwa ambayo wabunge wengi wameichukua ikiwa ni pamoja na maslahi madogo wanayopata wabunge hao. 

“Kutokana na hali hii wakati mwingine humfanya kiongozi ahangaike kutafuta fedha na ndipo wengine hujiingiza katika vitendo hivi vya rushwa.

"Nawatahadharisha ninyi kama wabunge mnao wajibu wa kudhibiti rushwa na kuwa mfano katika jamii,” alisema. 

Spika alilia maslahi
 Alisema katika eneo la maslahi, ofisi ya Bunge inatambua kuwa bado maslahi wanayopata wabunge hao ikilinganishwa na kazi wanayofanya ni madogo hivyo, wanaendelea kuangalia namna ya kuyaboresha.

Ndugai alisema wabunge wa Tanzania wana wajibu na jukumu kubwa la kudhibiti rushwa kwa kutunga sheria zinazopaswa kutumika katika kuunga mkono au kuleta miswada itakayosaidia kutokomeza rushwa. Alisema pia moja ya kazi ya wabunge ni kushauri na kusimamia Serikali.

Alisema ni vyema pale ambapo kuna viashiria vya rushwa wakatoa ushauri huo bila kukubali kushawishiwa kwa rushwa.  

“Vilevile katika kupitisha bajeti za serikali, hapana budi kuhakikisha vyombo vinavyohusika na mapambano dhidi ya rushwa vimetengewa fedha za kutosha,” alisema.

Aliwaasa wabunge kujiepusha na vishawishi vya rushwa kwa kuwa nafasi waliyonayo ni nyeti. Alisema pia kutokana na mwenendo wa umakini wa Serikali ya Awamu ya Tano, inawezekana wakawepo watu wanaoona umakini huo kama maslahi yao na kutumia njia pekee ya kuwarubuni wabunge.

“Nawaasa msishawishike,” alisisitiza. Alisema kwa mujibu wa Jumuiya ya Vyama vya Wabunge Wanaopambana na Rushwa Afrika (GOPAC), takribani dola za Marekani bilioni 50 hutoroshwa Afrika kutokana na rushwa. “Hizi ni fedha nyingi sana za walalahoi zinazotumika kwa maslahi ya wachache,” alisema.

Pia amehamasisha wabunge hao kujiepusha na vitendo vya rushwa kwa kile alichosema, katika awamu hii ya serikali ya awamu ya tano, yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo lazima aingie matatani. 

Sheria ya maadili 
“Muda si mrefu nitawaalika waje watoe semina kwenu kuhusu undani wa sheria hiyo ili wote muielewe vyema.

"Nawashauri muisome vizuri sheria hii ikija kwa sababu wengi wetu pamoja na ubunge tunafanya biashara ili tujiendeshe vizuri,” alisisitiza Ndugai. 

Alisema sheria hiyo ikipitishwa, haitakuwa ya kwanza Tanzania kuitekeleza kwani nchi nyingi duniani zimekuwa na mfumo unaotenganisha viongozi wake na biashara.

“Wenzetu ni kawaida ukiingia kwenye siasa unakabidhi biashara yako mpaka pale utakapomaliza uongozi wako ndio unaruhusiwa kuendelea, naomba mjiandae kuipokea sheria hii, ni sheria nzuri na ina malengo mazuri,” alisema. 

Akizungumzia rushwa, alisema kila bunge lina sababu zake za wabunge kujiingiza katika vitendo vya rushwa .


APNAC yapongeza kupunguza rushwa 
Akiwasilisha mada ya kuhusu tathmini ya shughuli za APNAC katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Mhadhiri wa Siasa katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Davis Mwamfupe, alisema chama hicho kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kueneza uelewa wa tatizo la rushwa hususan kwa wabunge.

Hata hivyo, alisema changamoto kubwa iliyopo katika kutatua tatizo la rushwa, ni kutokana na mara zote rushwa kufanyika kwa siri na hufanywa na watu wenye nafasi kubwa katika jamii wakiwemo wanasiasa na wachumi hivyo kuwa vigumu kuwakamata.

Aliwataka wabunge hao kutotumia nafasi zao ndani ya Bunge na kukemea rushwa kwa mdomo pekee bali waoneshe dhahiri kuichukia na kupambana nayo kwa vitendo. 

Mbunge wa Nkasi, Ally Keissy, wakati akichangia mada hiyo ya rushwa, alisema tatizo la rushwa litamalizika endapo Mahakama na vyombo vya dola vitachunguzwa kutokana na ukweli kuwa kesi nyingi za rushwa zimefunguliwa, lakini hazishindi.

UKAWA Waigomea Serikali Kuhamishwa Machinga Katikati ya Jiji la Dar es Salaam

$
0
0
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi
 
Sakata la kuhamishwa kwa wafanyabiashara wadogo katikati ya Jiji la Dar es Salaam limeingia mdudu baada ya madiwani wa Ukawa kugomea uamuzi uliotolewa na uongozi wa jiji hilo.

Uamuzi huo uliotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi, unadaiwa kutowashirikisha wadau hao na wafanyabiashara wenyewe.

Mwenyekiti wa madiwani wa Ukawa, Manase Mjema amesema Mngurumi ametoa umuzi huo bila pia kumshirikisha hata Meya wa Ilala, Charles Kuyeko.

Wamesema masoko ya Kivule, Tabata Muslim, Ukonga na Kigogo Fresh ambayo mkurugenzi huyo amesema yametengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao, hayajaboreshewa miundombinu yake ikiwamo ujenzi wa vyoo na mabomba ya maji.

Wamemtaka kusitisha mchakato huo mpaka watakapo jadiliana tena

“Ieleweke kwamba hatupingi hatua hii, lakini Mngurumi alipaswa kutushirikisha madiwani ili tutoe mawazo ambayo yangesaidia kuboresha mpango wake huu,” alisema Mjema.

Alisema Mngurumi angetumia busara ya kushirikiana na baraza la madiwani na angewapa muda wafanyabiashara hao kujiandaa, tofauti na muda wa siku mbili aliowapa kuondoka kwenye maeneo hayo.

“Tulitegemea mkurugenzi angekaa na madiwani na wafanyabiashara meza moja ili kutoa uamuzi ambao ungekuwa na tija kwa pande zote, badala ya kukurupuka kama alivyofanya,” alisema Mjema ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kimanga (Chadema).

Kwa upande wake, Kuyeko alidai kupewa maagizo na Mngurumi jana kuitisha mkutano na wanahabari ili kukazia agizo hilo.

Hata hivyo, meya huyo alishindwa kufanya hivyo kwa madai ya kutoshirikishwa.

“Nilisita kuunga mkono uamuzi wake kwa sababu baraza langu la madiwani halijui kinachoendelea zaidi ya kusikia katika vyombo vya habari,” alidai Kuyeko.

Diwani wa Kata ya Tabata (Chadema), Patrick Asenga ambaye eneo lake limetengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao, alisema hawezi kuwapokea kwa sababu eneo hilo lina mgogoro na halmashauri.

Mjumbe wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wadogo, Idd Omary alisema wamekubaliana kutohamia katika masoko waliyopangiwa kwa sababu hawakushirikishwa katika mchakato wote na Mkurugenzi huyo.

“Mngurumi alimtuma mwakilishi katika kikao cha jana (juzi), kilichotukutanisha na uongozi wa Manispaa ya Ilala. Tulimuuliza masoko waliyotupangia yana miundombinu mizuri, tukajibiwa ndiyo, lakini siyo kweli, hayana vyoo wala maji,” alidai Omary.

Akizungumzia madai ya madiwani hao, Mngurumi alisema anashangazwa na kauli zao kwani kuna mambo walikubaliana na Meya Kuyeko ambayo hakuyataja na badala yake alisema atawasiliana naye kwa mara nyingine kwa mazungumzo zaidi.

Mbunge Alaani Matusi na Udhalilishaji Bungeni

$
0
0

MBUNGE wa Siha (Chadema), Godwin Mollel, amelaani lugha chafu zinazotumika bungeni ambazo zinawazalilisha wanawake na kwamba kitendo hicho kinashusha hadhi ya Bunge.

Alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizindua kitabu cha siri za utumishi madhabahuni kilichotungwa na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mikaeli Memiri.
 
Aliwataka wanafunzi kuwa na nidhamu ili watakapobahatika kuwa wabunge wazingatie maadili na kuwatumikia wananchi.
 
Alisema kukosekana kwa maadili kwa baadhi ya wabunge kumesababisha kuwapo lugha za uzalilishaji dhidi ya wanawake, jambo ambalo linatakiwa kukemewa.
 
Alisema kuna mila ambazo zinamkandamiza mwanamke katika kupata uongozi kwa kudhani kuwa nafasi hiyo inatolewa kwa njia ya ngono, jambo ambalo sio la kweli.
 
Kuhusu kitabu alichozindua, Mollel alisema mwandishi ameonyesha udhubutu, hivyo kuna haja ya serikali kuwasaidia vijana kama hao ili waweze kukua kiuchumi pamoja na kufahamika.
 
Alisema mara nyingi watungaji wa vitabu hawathaminiki huku baadhi ya watu wakitumia mawazo yao kujinufaisha huku wahusika wakiendelea kubakia maskini.
 
Aliahidi kumsaidia mwanafunzi huyo ambaye ametumia muda mwingi kutunga kitabu hicho ambacho kitasaidia kuielimisha jamii.
 
Naye Memiri alisema lengo la kutunga kitabu hicho ni kutaka kubadilisha fikra za jamii pamoja na kufikia malengo yake ya kuwasaidia wanaoishi katika mazingira magumu.
 
Alisema amepitia shida nyingi katika maisha yake lakini licha ya changamoto alizokuwa nazo ikiwamo kusomesha watoto wawili, alitumia mkopo wake aliopatiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kutunga kitabu hicho.
 
Alisema anakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo kukosekana kwa ofisini, vitendea kazi kama mashine za kuchapishia vitabu na hivyo kufanya shughuli zake katika mazingira magumu.
 
Kwa upande wake, Mwalimu wa Shule ya Mtakatifu Peter Clavery, Oswald Nyinge, alisema mara nyingi serikali inawathamini watungaji wa vitabu ambao ni maprofesa wakati ni sehemu yao ya kazi na kuwapuuza waandishi wachanga hali inayowakatisha tama, hivyo kuna haja ya serikali kuwatambua pamoja na kuwaongezea uwezo.

Waziri Nchemba Awapasha Wafugaji na Wakulima

$
0
0
WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, amewataka wakulima na wafugaji kuacha kutumia uhai wa mtu kama fidia ya mifugo au mashamba yaliyoharibiwa kwa kuuana katika mapigano ya wenyewe kwa mwenyewe.

Nchemba alisema hayo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa baraza jipya la wakulima, wafugaji pamoja na wavuvi, mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
 
Alisema vitendo vya mauaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na jamii za wafugaji na wakulima kuuana havistahili kuendelea kuwapo katika jamii iliyostaarabika.
 
Mwigulu alisema hakuna mifugo wala mashamba yenye thamani zaidi ya maisha ya binadamu, hivyo jamii hizo mbili zinatakiwa kutafuta namna sahihi ya kutatua migogoro baina yao na siyo kuendeleza mapigano na kupoteza maisha ya binadamu wenzao.
 
“Ni aibu sana mtu kuua kwa ajili ya shamba au mifugo kwakuwa hakuna kitu kinachoweza kulinganishwa na maisha ya mtu, hivyo basi fidia za mifugo au shamba zifanyike kwa vitu na siyo maisha ya mtu.”alisema.
 
Mwigulu alisema kuwepo kwa baraza hilo ni matarajio ya serikali kuwa mapigano yaliyokuwa yakisabababisha vifo vya watu wengi yatakomeshwa kwa njia ya marishiano na siyo mapigano.
 
“Niwapongeze sana kwa kuunda chombo hiki kikubwa na cha kitaifa, ni matarajio yangu kuwa kila eneo kuanzia ngazi ya chini litaunda chombo kama hiki kwa ajili ya kutatua kero zenu bila kutoa damu ya mtu,” alisema.
 
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Adam Ole Mwarabu, alisema lengo la kuunda chombo hicho ni pamoja na kulinda haki za makundi hayo.
 
Alisema kuwapo kwa baraza hilo kutasaidia kuondoa uonevu wa kunyang’anywa mifugo, ardhi, nyavu, mazao na kulipishwa faini kubwa bila ya kufuata sheria kwa wahusika.

Rais Magufuli Awagomea Wabunge Nyongeza Ya Mikopo Ya Magari

$
0
0

Katika kile kinachoonekana amedhamiria kuendelea kubana matumizi ya serikali, Rais John Magufuli amekataa ombi la kuongeza fedha za ununuzi wa magari kwa wabunge pamoja na fedha za mfuko wa bunge.

Baada ya kuchaguliwa, wabunge walipatiwa milioni 90  za mkopo kwa ajili ya ununuzi wa magari, lakini baadhi yao walieleza kutoridhishwa na kiasi hicho, wakidai hakitoshelezi na kutaka kiongezwe hadi sh. milioni 120.

Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa wabunge waliwasilisha ombi kwa Rais Magufuli kuongezwa fedha lakini ombi hilo limekataliwa.

Chanzo cha kuamini kimedokeza kuwa mmoja wa wabunge wa CCM alimkumbushia Rais Magufuli ombi hilo wakati wa kikao cha chakula cha jioni, kilichofanyika wiki iliyopita mjini Dodoma.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli alikataa kuwaongezea wabunge fungu hilo kwa madai kuwa serikali yake haina fedha.

Kilieleza pia kuwa Rais Magufuli alikataa kuongeza fungu la mfuko wa jimbo kwa kuwa serikali haina fedha huku akiwataka wabunge kufanya kazi kwa bidii.

"Rais alisema kwa sasa hali si nzuri, amekumbana na changamoto mbalimbali na kutuahidi kulichukua ombi letu, endapo hali itatengemaa atatuangalia kwa sababu hata yeye analitambua hilo kwa sababu alikuwa mbunge."Kilisema chanzo hicho

Waziri Ataka Wakurugenzi NHC Washindanishwe

$
0
0

NAIBU  Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi, Angeline Mabula, ametaka wakurugenzi  wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika mikoa yote washindanishwe   kujua utendaji kazi wao.

Waziri Mabula, alitoa kauli hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki  wakati akifungua  kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi  wa shirika hilo kilichokuwa kikijadili mipango na makisio  ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/17 kabla ya kuwasilishwa bungeni.

Alisema  hatua hiyo itasaidia kutambua wakurugenzi ambao wanasubiri kubebwa na wenzao kwa kushindwa kufanya kazi kwa weledi.

Alisema ujenzi na ununuzi wa nyumba unahitaji fedha nyingi, wananchi hununua nyumba kupitia mikopo kutoka benki.

"Serikali inatambua umuhimu wa taasisi za fedha  katika kusaidia ukuaji  wa sekta ya nyumba jambo ambalo hufanywa duniani kote, "alisema.

Alisema Serikali inatambua bado kuna changamoto  ya riba kubwa ya mikopo  ya nyumba  inayotozwa  na benki ambayo sasa ni kati ya asilimia 18 hadi 25.

Alisema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwamo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuona namna bora ya kuwezesha benki kupunguza riba katika mikopo ya nyumba.

“Serikali itahakikisha benki zote  zinashiriki  kukopesha wananchi   waweze kununua nyumba, kufanya hivi kutachochea ukuaji wa uchumi na wananchi watatumia nyumba zao kupata mikopo ya benki kwa ajili ya kuanzisha miradi yao ya maendeleo."

Mkurugenzi Mkuu  NHC, Nehemia Mchechu, alisema   moja ya majukumu  ya baraza  hilo ni kujadili mipango  na makisio ya mapato  na matumizi ya wizara  kabla ya kuwasilishwa bungeni.

“Serikali imeweka msisitizo  zaidi katika ukusanyaji wa mapato, kupitia kikao hiki tutapata  maoni  na mikakati  ya kuboresha  ukusanyaji wa kodi za ardhi,” alisema.

Lowassa: Bado Nipo Nanyi Kuwaletea Maendeleo

$
0
0

Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa amewahakikishia wananchi wa Monduli kuwa bado yupo nao katika kuwaletea maendeleo.

Lowassa ambaye alikuwa mbunge wa Jimbo la Monduli karibu miongo miwili enzi akiwa mwanachama wa CCM, alisema juzi kuwa bado atashirikiana na wananchi wa jimbo hilo.

Lowassa alihamia Chadema na kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25  mwaka jana.

Akizungumza katika mahafali ya shule ya sekondari ya  Irkisongo iliyopo wilayani humo juzi, Lowassa alielezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika wilayani humo kwa kushirikiana na wananchi.

Alitaja baadhi ya miradi hiyo kama maji ya kutosha mpaka miaka 20 ijayo na hospitali kubwa ya kisasa ambayo itawafanya wananchi wengi kupata huduma za afya bila  kulazimika kwenda mjini Arusha.

Mafanikio mengine ni pamoja na kukubaliana kuhifadhi shule za sekondari za wasichana zilizopo Monduli ambazo ni  Masai, Enyorata,Irkisongo na Kipok.

"Bado nitaendelea kuyahifadhi mambo ya Monduli, ntashirikiana na mbunge si kumwangusha bali kuhakikisha maendeleo ya Monduli yanabaki palepale." Alisema

Aliwataka wazazi kuhakikisha wanaendelea kuwasomesha watoto wao licha ya kuwapo kwa shida kubwa ya ajira

Alisema wanafunzi hao na wengine wanamaliza  masomo yao wakati mgumu,dunia ikiwa imebadilika.

"Wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne, cha sita na vyuo vikuu hawakutani na ajira, Ajira imekuwa tatizo kubwa."Alisema

Alisema pamoja na ukubwa wa tatizo hilo, silaha pekee wanayoweza kuwapatia watoto wao ni elimu.

"Hizi fedha, nyumba na magari yataisha na kupotea,lakini elimu itabaki vichwani."Alisema

Bush Asema Hatampigia Kura Donald Trump

$
0
0

Aliyekuwa mgombea wa urais wa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Jeb Bush amesema hatampigia kura Donald Trump katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika nchini humo Novemba mwaka huu.

Bush alisema kuwa Trump hana tabia wala mienendo ya kuwa Rais wa Marekani.

‘‘Marais wa Marekani wanasifa zao na wanakubalika kwa watu, lakini huyu jamaa hana sifa hata moja ndiyo maana kila siku namkana na kusema hafai kabisa kuwa rais wa nchi hii, ’’alisema Bush

Jeb ni mojawapo wa wanachama mashuhuri wa Republican kutanganza hadharani kuwa hatampigia kura Trump kwa sababu ya kampeni yake ya kiburi ambayo imegawanya Chama cha Republican.

Juzi Spika wa Bunge, Paul Ryan alisema hatamuunga mkono mfanyabiashara huyo tajiri ingawa atakutana naye wiki ijayo.

Hata hivyo, Trump aliungwa mkono na mgombea urais wa zamani wa nchi hiyo, Bob Dole aliyeshindwa katika uchaguzi na Bill Clinton wa Chama cha Democratic mwaka 1996.

Wiki iliyopita Seneta wa Texas, Ted Cruz alijitoa katika kinyang’anyiro cha kuwania uteuzi wa kugombea urais kwa Republican baada ya kushindwa katika uchaguzi wa awali dhidi ya mpinzani wake huyo.

Cruz aliwaambia wafuasi wake katika mji wa Indianapolis kwamba: “ Njia hii kuelekea ushindi imefungwa” na kusema kuwa wapiga kura wamechagua njia nyingine.

Alitoa shukrani kwa wafuasi wake wote. Trump alipata ushindi mkubwa Indiana huku Cruz akishika nafasi ya pili na gavana wa Ohio John Kasich akiwa katika nafasi ya tatu.

Trump alisema huo ni ushindi mkubwa kwake na kumpongeza Cruz akimuita yeye na wagombea wengine 15 waliokuwa wanagombea uteuzi wa Republican kuwa ni werevu na wenye nguvu.Alitoa wito wa kuwa na umoja ndani ya chama hicho.

Kwa upande wa Democratic seneta wa Vermond, Bernie Sanders ameshinda katika jimbo la Indiana dhidi ya Hillary Clinton

Wagombea hao wawili walibadilishana ushindi kabla ya Sanders kuibuka mshindi kwa asilimia saba ya kura. Hata baada ya ushindi huo wa Sanders katika jimbo la Indiana, Hillary anaongoza katika idadi ya wajumbe ikionyesha kwa mahesabu ni vigumu kwa Sanders kuteuliwa kuwa mgombea wa Democratic

Sitta Alaani Wabunge wa Kike wa Chadema Kudhalilishwa Bungeni

$
0
0


Mbunge wa Urambo Mashariki, Magreth Sitta amekemea lugha za udhalilishaji zinazotolewa dhidi ya wabunge wa kike ikiwa ni pamoja na sakata la lugha ya maudhi dhidi ya wabunge wa viti maalum wa Chadema wiki iliyopita.

Akitoa hoja binafsi bungeni mjini Dodoma, Mama Sitta ambaye ni Mwenyekiti wa wabunge wanawake, amesema kuwa vitendo havikubaliki na ni kinyume cha katiba na kanuni za Bunge.

Alisema kuwa vitendo hivyo licha ya kuwa vinawadhalilisha wabunge wanawake, vinashusha heshima ya chombo hicho cha kutunga sheria. Aliongeza kuwa ingawa Naibu Spika aliagiza lugha zote za udhalilishaji dhidi ya wabunge wanawake kuondolewa kwenye kumbukumbu ya Bunge, vitendo hivyo havikubaliki na havipaswi kujirudia.

Wiki iliyopita, wabunge wanawake wa Chadema walitoka nje ya Bunge kupinga kauli aliyoitoa Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kuwa wabunge wa viti maalum wa chama hicho hupata nafasi hiyo kwa kuitwa ‘baby’ (kuwa na uhusiano wa kimapenzi) na viongozi wa ngazi za juu wa chama.

Rais Magufuli Afungua Jengo la Kitega Uchumi la Mfuko wa Pensheni PPF Jijini Arusha

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akikata utepe kuzindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016. Wa pili (kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama, (kushoto) ni Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro (wa kwanza kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Ramadhan Kijjah, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduai wa Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.

Jengo hilo lililozinduliwa leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia wakazi wa arusha na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati alipozindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2016.

Sehemu ya wadau kutoka NSSF waliohudhuria uzinduzi huo wa wenzao wa PPF.

Kigwangalla Amtaka Gardner Aombe Radhi kwa Kumdhalilisha Lady Jaydee

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla, amemtaka mtangazaji wa Clouds FM, Gardner G Habash kumuomba radhi aliyekuwa mke wake, Lady Jaydee kwa ‘kile alichokiita’ kama udhalilishaji kwake na kwa wanawake wote.

Wikiendi iliyoisha imesambaa video mtandaoni ikimuonesha mtangazaji huyo akiongea kwenye tamasha alilokuwa mshereheshaji: "My name is Captain Gardner G Habash all the way from Clouds FM, Jahazi hatari sana. Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi.”

Video hiyo imesababisha hasira kubwa kwa mashabiki wa Jaydee na watu wengi kwa ujumla.

“Ndg. Gardner amefanya udhalilishaji mkubwa si tu Kwa @JideJaydee bali ametukana wanawake wote. Mimi #BaloziWaWanawake namtaka aombe radhi,” ameandika mheshimiwa Kigwangalla kwenye Twitter.

“Natoa rai kwa uongozi wa @cloudsfm kumtaka Ndg. Gardner afute kauli yake na aombe radhi kwa @JideJaydee na kwa umma ili kulinda heshima yao,” ameongeza.

“Jamani, sijui ugomvi wao wala sina interest ya kujua, sema alichokisema G na nikasikia ni katika tusiyosemaga hadharani kwa heshima ya mama,” amefafanua.

“Sina maana wamchukulie hatua. Watambue tu kosa lake na wamtake kwa heshima kwa mama aombe radhi. Mimi ni mtumishi namba 2 kwenye Wizara inayosimamia ‘mambo ya wanawake’! I know what I am talking about hapa.”

==>Video Hii Hapa

SUMATRA Yatangaza Nauli Za Usafiri Wa Mabasi Yaendayo Haraka.

$
0
0
Hatimaye  Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetangaza nauli zitakazo tumika kwa mabasi yaendayo kasi kuwa ni 400, 650 na 800 kwa safari za Mbezi mwisho hadi Kivukoni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Giliard Ngewe amesema nauli kutoka Mbezi mwisho hadi Kimara Sh400, na nauli ya Sh650 itatumika maeneo ya  Kimara  kwenda  Kivukoni, Kimara –Kariakoo, Kimara – Morocco, Kariakoo - Kivukoni.

Amesema nauli ya Sh800 ni Mbezi Mwisho-Kimara –Kivukoni, kivukoni-Kimara- Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho-Kimara- Kariakoo, Kariakoo-Kimara-Mbezi Mwisho, Mbezi Mwisho Kimara- Morocco,na Morocco- Kimara-Mbezi Mwisho.

“Chombo chochote cha usafiri hakitaruhusiwa kutumia barabara za mwendo kasi kuanzia kesho, watakao kiuka agizo watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni za biashara zao” amesema.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu nauli zitakazotumika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka unaotarajiwa kuanza rasmi Mei 10, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi kutoka SUMATRA Bw. Nahson Sigala.
Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Nahson Sigala akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu viwango vipya vya nauli baada ya SUMATRA kufanya tathmini ya viwango vya nauli iliyopendekezwa awali na Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT na kubaini kuwa gharama zilizopendekezwa ni kubwa mno. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe (Kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu DART Bw. Ronald Lwakatare wakimkabidhi leseni ya usafirishaji Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Katikati)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya UDA-RT Bw. David Mgwassa (Kushoto) akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) Bw. Giliard Ngewe baada ya kupokea leseni ya usafirishaji kutoka SUMATRA.

PICHA NA FATMA SALUM

Rais Magufuli Ayaagiza Mashirika ya Hifadhi ya Jamii Kuwekeza kwenye Viwanda badala ya Majengo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameyaagiza mashirika yote ya Hifadhi ya jamii kutoendelea kuwekeza katika miradi ya majengo na badala yake yajielekeze katika ujenzi wa viwanda na miradi mingine inayozalisha ajira na kuchangia zaidi katika pato Ia taifa.

Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo leo Jumatatu tarehe 09 Mei, 2016 alipofungua majengo mawill ya vitega uchumi ya Mfuko wa Pensheni (PPF) na Shirika Ia Hifadhi ya Jamii(NSSF) yaliyopo Jijini Arusha.

Pamoja na kuyapongeza mashirika hayo kwa kujenga majengo ya kisasa jijini Arusha na maeneo mengine hapa nchini, Dkt. Magufuli amekosoa uwekezaji mkubwa unaofanywa na mashirika hayo kwa kujenga majengo ya gharama kubwa ambayo licha ya kuwa wananchi wa kawaida hawawezi kumudu gharama za kupanga kwa ajlli ya kuendesha shughull zao, hayana manufaa ya kutosha ikilinganishwa na endapo mashirika hayo yangewekeza katika miradi inayozalisha ajira nyingi, faida ya haraka na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika palo Ia taifa.

"Hii mifuko ya hifadhi ya jamii kuanzia leo muache kuwekeza katika majengo, wekezeni kwenye viwanda, leo mngekuwa na viwanda vya sukari hawa watu wasingetuchezea kuficha sukari, na inawezekana hata kama ingepungua tungewambia nyinyi agizeni sukari.

"Mchango wa mifuko ya hifadhi za jamii katika nchi yetu, ambayo iko saba, imekuwa ikichangia pato la taifa kwa asilimia 12, lakini hifadhi ya jamii sehemu nyingine duniani, imekuwa ikichangia palo la taifa kwa asilimia 40, kwa hiyo kuna mahali tumekosea, na ndio maana mlipokuwa mkizungumza hapa sijui mlijua nitakayowaambia, ninawapongeza mliwekeza katika majengo, jengo Ia PPF na jengo IB NSSF ukipiga hesabu za kawaida haya majengo yamegharimu zaidi ya shilingi bllioni 60, lakini tujiulize hawa wananchl waliosimama hapa watayatumiaje haya majengo" Amesema Dk. Magufuli huku akishangiliwa na wananchi wa Arusha waliojtokeza kushuhudia ufunguzi huo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya May 10

Songas Yazima Mitambo Yao kwa Kuidai Tanesco Sh Blioni 194

$
0
0
Kampuni ya kufua umeme kwa njia ya gesi asilia, Songas Limited imezima mitambo yake, baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kushindwa kulipa deni la Dola 90 milioni za Marekani sawa na Sh193.5 bilioni, jambo linalotishia ukosefu wa nishati hiyo muhimu nchini.

Hata hivyo, Tanesco imepinga uamuzi huo na kueleza kuwa ni vitisho kwa wananchi na inakiuka vifungu namba 4.4 , 4.6 na 17 vya mkataba ulioingiwa na Songas. 

Mkurugenzi Mkuu wa Songas, Nigel Whittaker alisema jana kuwa wameamua kuchukua hatua ya kuzima mitambo hiyo baada ya kuzidiwa na gharama za uendeshaji kutokana na deni hilo.

“Mtambo huo uliopo Ubungo unazalisha Megawati 189, tumefikia hatua ya kuzima kidogo kidogo kuanzia Aprili 29 mwaka huu kutokana na deni hilo, Tanesco imekuwa ikisuasua katika kulipa,” alisema Whittaker.

Alisisitiza kuwa mradi huo wa Songas, ulioanzishwa tangu mwaka 2004 , ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania na umekuwa ukizalisha umeme kwa kutumia gesi asilia kutoka Songosongo na kuuingiza katika gridi ya taifa.

Whittaker alieleza kuwa kiasi cha umeme wanaozalisha ni takriban asilimia 20 ya nishati inayozalishwa nchini.

“Ilikuwa tuifunge mitambo hii tangu mwaka jana, lakini Serikali ilituomba tuendelee wakati ikisimamia hatua ya kulipwa, tunaendelea lakini hatimaye tumekwama kwa kuwa kuna mahitaji ya msingi ambayo yanategemea fedha ikiwamo matengenezo ya mitambo hiyo,”alisema.

Alisema pia wamejikuta katika hali ngumu kwa kudaiwa na taasisi kadhaa za Serikali ikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), na Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC), hivyo wanaendelea kujadiliana na Tanesco na Serikali ili kuangalia jinsi ya kushughulikia jambo hilo kwa kutambua umuhimu wa mradi huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba, alisema Songas wamevunja makubaliano ya mkataba hususan kifungu cha 4.4 ambacho kinaitaka Songas kutoa siku 90 ya kuwa na majadiliano.

Aliwatoa wananchi hofu kwa nchi haitaingia gizani kwa kuwa licha ya Songas kutangaza kuzima kabisa mitambo yote Mei 11.

"Tayari walikwisha kuwa wameanza kuizima na haututokea mgawo. Ingawa ni kweli wanatudai, lakini siwezi kusema kiasi gani nami nitakuwa nimekiuka huo mkataba, kwa hili walilofanya tutachukua hatua hatukubaliani nao,” alisema.

Songas ambao taarifa ya hivi karibuni ya Serikali inaonyesha kuwa wanauzia umeme Tanesco kwa senti za 2.4 za Marekani kwa uniti, wanalipwa capacity charge ya Dola za Marekani 5.2 milioni kwa mwezi ambazo ni sawa na wastani wa Sh11.4 bilioni.

Kulingana na hesabu hizo, kila mwaka kampuni hiyo inalipwa Sh136.9 bilioni tangu 2001 walivyoingia mkataba na Tanesco.

Mahitaji makubwa ya umeme Tanzania mara ya mwisho yalirekodiwa kuwa megawati 898.5.

Makonda Awasimamisha Kazi Vigogo wawili wa Manispaa Kwa Tuhuma za Kushindwa kutoa Maelezo kuhusu Watumishi Hewa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewasimamisha kazi wakuu wawili wa idara katika manispaa mbili kwa tuhuma za kushindwa kutoa maelezo kuhusu watumishi hewa katika idara zao, huku wakiendelea kuidhinisha mishahara yao kwa miaka mingi.

Makonda aliwataja watumishi hao waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkuu wa Idara ya Utumishi wa Manispaa ya Ilala, Francis Kilawe na Mkuu wa Idara ya Afya Temeke, Syrivia Mamkwe na kuagiza uchunguzi dhidi ya tuhuma zao ufanyike haraka.

Kiongozi huyo alichukua uamuzi huo baada ya hivi karibuni kuwaapisha wakuu wa idara kutoka manispaa tatu ili kusema ukweli na kuwapa wiki moja kuhakiki watumishi hewa katika maeneo yao ya kazi.

Makonda alisema hadi kufikia jana, jumla ya watumishi hewa 39 waligundulika na kufikisha 248 kutoka 209 wa takwimu za awali. 

Kati yao, 26 wanatoka Ilala, wawili (Kinondoni) na 11 (Temeke) na kulisababishia jiji hilo kupata hasara ya zaidi Sh3 bilioni.

“Kilawe ameshindwa kujieleza kuhusu watumishi hewa 11 ambao hajui wako wapi, lakini wanapokea mishahara tangu mwaka 2010.Huku yeye akisaini mishahara yao,” alisema Makonda.

Makonda ambaye pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aliongeza kuwa Mamkwe alishindwa kujieleza walipo watumishi hewa wawili ambao bado wanaendelea kupata mishahara huku akiwa kiongozi wa idara husika.

Kutokana na hali hiyo, Makonda amewaongezea wiki mbili maofisa wanaochunguza suala hilo ili kuwabaini zaidi watumishi hewa kwa madai kuwa bado wanaonekana katika mfumo wa kupokea malipo kutoka Hazina kwenda katika manispaa. 

“Huu ndiyo mkutano wangu wa mwisho kwenu.Wiki hizi mbili zikiisha tutaanza uchunguzi dhidi yenu na tukibaini watumishi hewa katika idara yako utawajibishwa ,” alisema Makonda ambaye pia ni Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa UVCCM.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images