Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Zanzibar Yasisitiza Ushirikiano na Japan

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, amesisitiza haja ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Japan.

Alisema hiyo inatokana na taifa hilo kutambua hatua za nchi hiyo za kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Dk Shein alisema hayo jana Ikulu mjini Zanzibar, wakati alipozungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe.

Katika mazungumzo hayo Dk Shein alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania ikiwemo Zanzibar, inajivunia uhusiano na ushirikiano mzuri pamoja na hatua za Japan za kuendelea kuiunga mkono katika kukamilisha miradi kadhaa ya maendeleo hapa nchini.

Alisema Serikali ya Japan pamoja na Shirika lake la Maendeleo la Jica, kwa muda mrefu zimekuwa zikiunga mkono uimarishaji wa miradi ya maendeleo hapa nchini, ambapo kwa upande wa Zanzibar nchi hiyo imesaidia mradi mkubwa wa maji katika Mkoa wa Mjini Magharibi, ambao hivi sasa upo katika awamu ya tatu.

Dk Shein pia alitumia fursa hiyo kumueleza Balozi huyo kuwa ipo haja ya kuitangaza zaidi Tanzania kiutalii kutokana na kuweko vivutio kadhaa kama fukwe nzuri za bahari kwa Zanzibar na hifadhi za Taifa kwa Tanzania Bara.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Japan Mhe. Mathias M. Chikawe alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kuonana na Rais

Ushahidi wa Mwalimu Kupigwa Kofi na Afisa Elimu Watua Kwa Mkuu wa Wilaya

$
0
0
CHAMA cha Walimu (CWT) Rukwa, kimemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mathew Sedoyeka ushahidi wa maandishi unaoelezea kitendo cha Ofisa Elimu, Shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Peter Fusi, kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani.
 
Ushahidi huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Rukwa, Hance Mwasajone.
 
Ushahidi huo wa kimaandishi wa tukio hilo umeandikwa na mwalimu mwenyewe, Jacob Msengezi (25) ambaye alisema alipigwa mbele ya wanafunzi wake akiwa darasani shule ya msingi Kianda kabla ya kuamuru walimu wengine kufanya usafi kwa kuokota mbigili ‘miba’ iliyotapakaa katika eneo la shule hiyo akidai kuwa huo ni uchafu.
 
Sedoyeka aliwaruhusu viongozi hao kumtembelea mwalimu na kusisitiza kuwa anafuatilia kwa karibu mkasa huo ili sheria ichukue mkondo wake .

Ahukumiwa Miaka Mitatu Kwa Kosa la Kumtukana Mtandaoni Mwanamke Aliyedai Anatembea na Mumewe

$
0
0


Mfanyabiashara Naila Aminel (24) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh milioni tano baada ya kukiri kutumia mtandao wa kompyuta kutuma ujumbe wa lugha ya matusi.

Aminel ambaye ni mkazi wa Kariakoo, alihukumiwa kifungo hicho jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Said Mkasiwa.

Awali, akisoma mashitaka, Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 13 mwaka huu, maeneo ya katikati ya jiji, wilayani Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.

Mitanto alidai kuwa mshitakiwa alitumia lugha ya matusi dhidi ya Martha Sebarua kupitia mtandao wa kompyuta kinyume na kifungu namba 23 (1) na (3) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya mwaka 2015.

Hata hivyo, Mitanto aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

Mshitakiwa huyo alidai hakumtukana mlalamikaji isipokuwa alifanya hivyo kwa kuwa alimchukulia mume wake na walipiga picha za utupu na kumtumia kwenye simu yake.

Aliiomba pia mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa ana watoto wadogo ambao wanamtegemea.

Hakimu Mkasiwa alisema kuwa mshitakiwa amekiri kutumia lugha ya matusi hafai katika jamii na kwa sababu kosa lake ni la kwanza, atatakiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh milioni tano.

Wakurugenzi Katavi Kikaangoni ......Mkuu wa Mkoa Awataka Warejeshe Milioni 200 Walizolipa Watumishi Hewa

$
0
0
Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Katavi, wameagizwa kurejesha Sh200 milioni wanazodaiwa kuwalipa watumishi hewa ndani ya siku 21.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali mstaafu, Raphael Muhuga alitoa agizo hilo jana katika kikao baina yake na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na waandishi wa habari.

Alikuwa akitoa taarifa ya kubainika kwa watumishi hewa wapya mkoani humo.

Muhuga alisema kuendelea kubainika kwa watumishi hao hewa, itawabidi wakurugenzi kuhakikisha fedha zote zilizolipwa kwa watu hao zinarejeshwa serikalini kwa muda aliowataka wazirejeshe na wampatie taarifa itakayothibitisha fedha hizo kurejeshwa.

Pia, mkuu huyo wa mkoa aliagiza maofisi wa ofisi ya utumishi wachukuliwe hatua ya kinidhamu kwa kusababisha watumishi hao hewa kulipwa fedha.

“Hili siyo suala la bahati mbaya, bali hawa watu walidhamiria kulipa mishahara hiyo hewa naimani wapo wenye maslahi juu ya jambo hili,” alisema Muhuga.

Aliagiza wakurugenzi wote wa halmashauri, wahakikishe maofisa utumishi wanawafuta watumishi hewa wote kwenye leja zao na wawachukulie hatua wote waliohusika na suala hilo.

Hata hivyo, aliishukuru kamati ya watu wanne iliyoundwa kufanya kazi ya uhakiki wa watumishi mkoani humo.

Aliitaka iharakishe kukamilisha uchunguzi wa watumishi 15 ambao taarifa zao zimebainika kuwa na utata.

Serikali Yabaini tani 4,579.2 za Sukari zilizokuwa zimefichwa

$
0
0

Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) imebaini kuwepo kwa sukari iliyofichwa  tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Sukari Kilombero.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentine Mlolowa Taasisi  hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya swala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa mnamo tarehe 05 Mei, 2016 timu ya uchunguzi ilitembelea maghala yaliyopo Tabata Jijini Dar es salaam na kubaini uwepo wa sukari hiyo.

TAKUKURU tayari imetembelea  Maghala ya mfanyabiasha Haruni Daudi Zacharia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Al-Naeem yaliyoko Mbagala na Tabata ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari hapa nchini na anayetuhumiwa kuficha bidhaa hiyo.

Aidha uchunguzi  uliofanywa na Taasisi hiyo ulibaini kuwepo kwa njama za dhati za kutouza  sukari iliyokutwa katika maghala hayo kulikofanywa na mfanyabiashara huyo kwani hata sehemu ya Maghala ilipo sukari hiyo hapakuwa na dalili za upakiaji wa sukari  hiyo ili iweze kusambazwa.

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa katika eneo la Kitumbini  kumekuwa na wananchi wengi wanaohitaji  bidhaa hiyo na wachache sana waliweza kuuziwa  licha ya ukweli kwamba sukari ilikuwepo.

Katika uchunguzi wake TAKUKURU pia  imebaini kuwepo kwa mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko.

Kuficha bidhaa ni kosa la uhujumu uchumi na ni  kinyume na Aya ya 3 Jedwali la kwanza Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 [Chapisho la Mwaka 2002]. Serikali haitavumilia hujuma za namna hii na itachukua hatua kali dhidi ya mfanyabiashara yeyote ataekwenda kinyume na sheria hii.

TAKUKURU  inatoa wito kwa wafanyabiashara wote wa sukari kuacha vitendo vya kuficha sukari na vyombo vya uchunguzi vinafuatilia kote nchini na yeyote atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na mkondo wa Sheria.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Ahudhuria Mazishi ya Lucy Kibaki nchini Kenya.

$
0
0
Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.
 
Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.

Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.

Rais Magufuli Awatunuku Kamisheni Maafisa Wapya 586 wa JWTZ mkoani Arusha

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi tarehe 07 Mei, 2016 amewatunuku Kamisheni Maafisa wapya 586 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kundi la 58/15 waliomaliza mafunzo yao katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) Mkoani Arusha.

Maafisa hao wapya wa Jeshi walianza kozi yao tarehe 04 Mei, 2015 na wamepewa cheo cha Luteni usu.

Kati ya maafisa wapya waliohitimu kozi yao leo, 80 ni madaktari na 6 ni marubani wa ndege waliopata mafunzo yao katika nchi tatu ambazo ni Tanzania, Uganda na Afrika Kusini.

Kabla ya kutunuku Kamisheni kwa maafisa hao, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekagua gwaride la maafisa hao wapya na pia amepokea heshima ya gwaride lililopita mbele yake kwa mwendo wa pole na haraka, na baadaye kusikiliza ujumbe juu ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano, nidhamu ya kazi na uzalendo kupitia muziki wa bendi na kwaya.

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mara nyingine amelazimika kuzungumza na wananchi wa Arusha Mjini waliokuwa wamezuia msafara wake uliokuwa ukitoka Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kwenda Ikulu ndogo ya Arusha, na kuwahakikishia kuwa serikali yake imeanza kuwashughulikia wafanyabiashara ambao wameficha sukari kwa makusudi na kusababisha upungufu wa bidhaa hiyo.

Rais Magufuli amesema tayari vyombo vya dola vimekamata tani 5,000 za sukari iliyofichwa na mfanyabiashara mmoja huko Tabata Jijini Dar es salaam na pia vimembaini mfanyabiashara mwingine aliyeficha sukari hiyo Jijini Arusha.

"Kweli nitawakomesha hawa, wasije wakanilaumu, haiwezekani ukaficha sukari wakati viwanda vyetu vinatengeneza sukari, kuna mmoja mwingine yupo Arusha hapa, nae ameficha sukari, alienda akanunua kwenye viwanda vya sukari vya hapa akaificha yote, leo ninamshughulikia.

"Kuna mwingine alinunua sukari pale Kilombero zaidi ya tani 3,000 akaficha, na mwingine ameshikwa pale Tabata alikuwa ameficha tani 5,000, na wanasubiri katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili ndugu zetu Waislamu wapate shida, haya ni mashetani makubwa, unawafichia watu chakula ambacho wanatakiwa kula, lakini nataka niwahakikishie ndugu zangu, hili ni tatizo la muda Tanzania, sukari itapatikana kwa wingi, na itanunuliwa na serikali, tumeshaagiza sukari lakini hatutawapa vibali hawa wafanyabiashara ambao wanatunyonya, tutanunua wenyewe na tutauza bei ya chini, hilo ndio lengo la serikali" Amesema Rais Magufuli

Aidha, Rais Magufuli amerejea kauli yake kuwa serikali yake haitawavumilia viongozi na watumishi wa umma ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi, huku akisema ataendelea kutumbua majipu kwa yeyote atakayebainika kuchezea mali za umma ili kulinda maslai ya wengi, hususani watanzania wanyonge.

"Ninafanya kwa niaba yenu, ninafanya kwa niaba yenu, ningekuwa sifanyi kwa niaba yenu, na mimi ningeingia madarakani ningeanza kushirikiana na hao, na wengine walifikiria nitashirikiana nao, wamekwama mimi nitawatumbua kila siku ili Tanzania iwe ya neema iweze kwenda mbele, haiwezekani nchi kama hii tajiri, Tanzanite ipo, dhahabu ipo, wanyama mpaka nyani wameanza kuuzwa, wakimalizika nyani si tutauzwa na sisi ndugu zangu, ni lazima nisimamie hili" amesisitiza Dkt. Magufuli.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha
07 Mei, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha Mei 07,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Afisa Mpya wa cheo cha Luteni Usu, Nasra Rashid ambaye alifanya vizuri zaidi kuliko Maafisa Wanafunzi wanawake katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya wananchi General Davis Mwamunyange mara baada ya kuwasili kwenye chuo cha Mafunzo Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitembea kikakamavu mara baada ya kutoka kukagua gwaride katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Ngarenaro waliomsimamisha wakati akitokea kwenye chuo cha Mafunzo ya Kijenshi cha Monduli mkoani Arusha.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Mei 8


Makamu wa Rais: Upinzani Kuna watu makini Wanaoweza Kuikabili Serikali

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na vitendo vya wabunge wa CCM kurusha vijembe na kuutaka Umoja wa Wanawake (UWT) kuwaandalia mafunzo ili waweze kukabiliana na wapinzani ambao alisema wana watu makini na werevu kuweza kukabiliana na Serikali.

Samia, ambaye pia aliweka bayana kuwa chama hicho tawala kilikumbana na upinzani mkali kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua semina ya wabunge, madiwani na viongozi wa CCM wa Mkoa wa Dodoma na baadaye kwenye kikao cha UWT.

Akiwa katika mkutano wa Baraza la UWT, Samia aliwataka viongozi wa jumuiya hiyo kutoa mafunzo maalumu kwa wabunge wapya ili waweze kupambana na wapinzani.

Alihoji ni mambo gani wanayofundishwa wabunge hao wanawake katika kutimiza wajibu wao ndani ya Bunge.

“Tunawafundisha nini ama (tunawafundisha) wakajibu vijembe tu, au wakaseme nini kama wabunge waliotoka UWT?” alihoji.

Samia amesema hayo wakati maneno ya kashfa na vijembe yakizidi kutamalaki ndani ya Bunge na kusababisha kelele, majibizano na wakati mwingine, wabunge wa upinzani kutolewa nje au kususa.

Juzi, wabunge wanawake wa vyama vinavyounda Ukawa walisimama na kupaza sauti kupinga kitendo cha Mbunge wa CCM, Goodluck Mlinga kudai kuwa wanawake wa upinzani hawawezi kupata nafasi za kisiasa bila ya kuitwa “baby”, neno la Kiingereza linalotumika kumaanisha mpenzi.

Naibu Spika Dk Tulia Ackson aliyekuwa anaongoza kikao hicho, alilazimika kuwaamuru wabunge hao waende nje ya ukumbi baada ya kukaidi amri yake ya kuwataka wakae vitini.

Tukio hilo lilitokea siku moja baada ya mbunge mwingine wa CCM, Augustine Holle kudai kuwa wabunge wawili wa Chadema, Tundu Lissu na John Mnyika wana mafaili kwenye Hospitali ya Mirembe ya mjini Dodoma ambayo inahudumia wagonjwa wa akili na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Kauli yake ilisababisha Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara kunyanyuka kwenye kiti chake na kuanza kumfuata mbunge huyo wa CCM kwa kile kilichoonekana kwenda kupambana naye, lakini hakufanikiwa na kuamriwa aende nje.

Mara kadhaa mbunge mmoja anapokuwa anachangia hoja inayogusa upande mwingine, wabunge huwasha vinasa sauti vyao na kutoa maneno ya kejeli, kashfa na dhihaka yanayosababisha Bunge kujaa kelele za mara kwa mara.

Samia na upinzani 
Akizungumza kwenye kikao na viongozi wa CCM wa mkoa, Samia alisema katika kipindi cha miaka 20 tangu siasa za vyama vingi ziliporejeshwa, vyama vya upinzani vimejijenga na sasa vinaweza kukabiliana na Serikali.

“Bila kusahau kwenye Bunge tuna wenzetu kutoka vyama vya upinzani ambao wamekua vya kutosha, wamepevuka vya kutosha,” alisema Makamu wa Rais.

“Katika miaka 20 ya vyama vingi, upinzani umezalisha watu makini ambao wako tayari kupambana na Serikali. Je, wa kwetu tumewaandaaje katika kupambana nao?”

Kuhusu Uchaguzi Mkuu uliopita, Samia alisema CCM ilipata upinzani mkali kutokana na vyama vya upinzani kuimarika na pia chama hicho tawala kukumbwa na mgawanyiko.

“Kukosa umoja ndani ya chama chetu kulifanya adui akaingia akiwa amejiimarisha na kweli alisumbua sana kwenye uchaguzi na ndiyo maana tunasema maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 yaanzie sasa,” alisema Samia.

Alisema kuna baadhi ya viongozi ndani ya chama ambao hawakuwa waaminifu akieleza kuwa ndiyo waliofanya uchaguzi huo uwe mgumu.

CCM ilipoteza makada wawili waliowahi kushika nafasi ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye waliohamia upinzani na kuwa tegemeo kubwa kwenye kampeni, Lowassa akiwa amepewa nafasi ya kugombea urais na Sumaye akitegemewa kwa hoja zake kwenye mikutano mingi.

Pia, mawaziri, wabunge na madiwani wa CCM walikihama chama hicho na kuimarisha upinzani uliofanya mgombea wa CCM, Dk John Magufuli kushinda kwa asilimia 58.2, ambao ni mdogo kwa chama hicho kulinganisha na chaguzi zilizopita.

Aliwataka viongozi wa chama kuondoa woga na badala yake waisimamie Serikali kwa kuwa ilani inayotekelezwa ni ya CCM na akawataka wafanye kazi hiyo kwa kushirikiana na watu wa chini yao.

Akiwa kwenye mkutano wa jana, Samia alisema UWT haina budi kukaa na wabunge hao na kufanya nao mafunzo maalumu kwa sababu kazi kubwa ya makundi ya wanawake ndani ya mabaraza ya kutunga sheria ni kutetea masilahi yao.

Sophia Simba ataka wakuu wa Wilaya
Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba alimuomba Makamu wa Rais kuwaombea kwa Rais Magufuli kuwapa kipaumbele wanawake wengi katika nafasi za ukuu wa wilaya wakati atakapofanya uteuzi akisema wana uwezo mkubwa wa kutumikia nafasi hiyo.

Alisema UWT itakuwa na shughuli mbalimbali ambazo itafanya kwa muda wa siku tatu mkoani Dodoma, ikiwa ni pamoja na kumpongeza Samia ambaye pia ni mmoja wa wadhamini wa umoja huo, kwa kuchaguliwa kwake kushika nafasi hiyo.

Majipu yatatumbuliwa 
Akizungumzia suala la kutumbua majibu, Makamu wa Rais alisema kazi hiyo itaendelea hadi wahakikishe Taifa linarudi kwenye mstari na akaomba viongozi wote kuwa makini katika sehemu zao za kazi. 

“Hapa napo niseme ukweli kuwa majipu siyo tu yapo huko juu, hata katika ngazi za chini yapo tena kuanzia kwenye chama na Serikali. Anzeni kuyatumbua kwa kuwa mkichelewa mtatumbuliwa ninyi,” alisema.

Aliwataka kujiandaa kwa kuwa “mzee wa kutumbua majipu” yupo karibu kukabidhiwa chama ambacho alisema kina majipu.

Chadema Walaani Wabunge wao wa Kike Kudhalilishwa Bungeni

$
0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Dar es Salaam kimelaani kauli iliyotolewa na Mbunge wa CCM, Goodluck Mlinga kuwa ili wanawake wapate nafasi ndani ya chama hicho lazima waitwe ‘baby’ neno linalomaanisha kutumiwa kimapenzi.

Hivi karibuni akichangia mjadala wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mlinga ambaye ni Mbunge wa Ulanga Mashariki alitoa kauli hiyo iliyoibua mtafaruku bungeni na kusababisha wabunge wanawake wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutoka nje ya ukumbi huo baada ya kunyimwa mwongozo na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Akizungumza jana nje ya eneo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), akiwa na viongozi wenzake walipokwenda kuchangia damu, Katibu wa Chadema Dar es Salaam, Henry Kileo alisema wamesikitishwa na kauli hiyo ya mbunge aliyepewa dhamana na kuaminiwa wananchi.

Alisema ili uwe mbunge wa viti maalumu ndani ya Chadema, kuna hatua nne za kupitia ikiwamo wanawake wenyewe kuchaguana ngazi ya wilaya kupitia Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), hivyo siyo rahisi kuwa na kitu kama hicho cha uhusiano wa kimapenzi.

Kileo alisema:‘‘Lakini cha ajabu nimeshangaa hata wenzetu upande wa pili CCM wamekaa kimya bila kutoa kauli ya kukaripia.’’

Alisema Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, inaungana na wabunge wanawake wa Ukawa kupinga kauli hizo za kihuni.

Kuhusu suala la damu, Kileo aliwataka Watanzania kujenga tabia ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wengine waliolazwa katika hospitali na vituo vya afya nchini.

“Chadema Dar es Salaam, tumeonyesha mfano tunaviomba vyama vingine viige mfano huu ili tuwasaidie watu wenye mahitaji ya damu,” alisema Kileo.

Alisema zaidi ya wanachama 40 wakiwamo viongozi wa Chadema wamechangia damu na kwamba mchakato huo utakuwa wa mara kwa mara.

Mbunge wa VitiMaalumu, Ruth Molel alisema wabunge wa Chadema wanaoteuliwa wana taalumu zao na hawabahatishi kupata nafasi hizo kama Mlinga anavyodhani.

“Nimeumia nilivyosikia kauli hii ikitolewa na kijana yule ambaye ni kama mwanangu, kiukweli hajatutendea haki kina mama.Inaonyesha jinsi gani bado ana fikra za mfumo dume,”alisema Molel.

Ofisa Habari wa MNH, Neema Mwangomo alisema kwa siku hospitali hiyo inahitaji damu kwa wastani uniti 80 hadi 100 lakini zinazopatikana ni 40.

Hata hivyo, Mwangomo aliwashukuru viongozi Chadema kwa moyo wao na kuwataka Watanzania wengine kujitokeza kutoa damu katika hospitali hiyo.

Machinga Marufuku Katikati ya Jiji la Dar es Salaam

$
0
0
Zaidi ya wafanyabiashara wadogo 2,000 waliokuwa wakifanya shughuli zao maeneo yasiyo rasmi katika Manispaa ya Ilala, wametengewa masoko manne kwa ajili ya kufanya biashara.

Masoko hayo ni Kigogo Fresh lililopo eneo la Pugu, Ukonga karibu na gereza, Tabata Muslim na Kivule ambayo wafanyabiashara hao maarufu kama wamachinga wanatakiwa kwenda.

Wafanyabiashara waliolengwa zaidi ni wale ambao wanafanya shughuli zao kwa kupanga barabarani, hususan barabara ya mabasi yaendayo haraka na katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo na Mnazi Mmoja kwenye manispaa hiyo. 

Baadhi ya wafanyabishara hao walionyesha wasiwasi wao juu ya uamuzi huo kuwa masoko hayo siyo rafiki kwao kwa biashara wanazozifanya. 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi alisema jana kuwa, utaratibu wa kuwapangia maeneo wafanyabiashara hao ulichelewa kwa sababu walikuwa katika mchakato wa kuwatambua ili mpango wa kuwapeleka ufanyike kwa ufanisi.

Alisema mazingira ya masoko hayo manne yapo vizuri na yana uwezo wa kumudu wafanyabiashara zaidi ya 2,000 na makadirio ni wafanyabiashara 6,000.

Kwa mujibu wa Mngulumi, kesho, manispaa ikishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama itaanza operesheni ya kuwaondoa kwa nguvu. 

“Hapa ni kama nakazia tu uamuzi huu, ila tulishawatangazia awali. Kwa hiyo sitarajii kuona watu maeneo hayo kesho, operesheni hii itaenda sambamba na kuwaondoa wenye gereji bubu na wanaoosha magari,” alisisitiza.

Mwalimu Adaiwa Kumjaza Mimba Mwanafunzi wake wa Darasa la Tano

$
0
0

Mwalimu wa Shule ya Msingi Tambaruka Kata ya Mkwamba wilayani Nkasi mkoani Rukwa, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumsababishia ujauzito mwanafunzi wake anayesoma darasa la tano katika shule hiyo.

Ofisa wa Elimu ya Msingi Wilaya Nkasi, Missana Kwangulla alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa amekabidhiwa katika kituo cha polisi kwa ajili ya hatua zaidi.

Kwangulla alisema anaandaa taarifa kuipeleka kwa Mkuu wa Wilaya kuhusu tukio hilo kwa kuwa jambo hilo lipo chini yake.

Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkwamba, Juvenally Mmanzi alisema jana kuwa, ofisi yake ilipata malalamiko kutoka kwa mzazi wa mwanafunzi huyo.

Alisema walichukua jukumu la kwenda kumpima mtoto huyo katika Zahanati ya Mkwamba na kugundulika ni mjauzito wa miezi miwili na wiki moja.

“Baada ya kujiridhisha tulianza kumhoji binti huyo na kumtaka amtaje mhusika wa ujauzito huo, alimtaja mwalimu wake na kusema alikuwa katika mahusiano naye ya kimapenzi tangu akiwa darasa la tatu,” alisema Mmanzi.

Mama Salama Amtetea Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

$
0
0

SALMA Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ameonesha kukerwa na wale wanaoshambulia utawala wa mumewe (Rais Kikwete) na kwamba, hakuna sababu ya kufanya hivyo.
 
Mama Salma alisema hayo jana kwenye mkutano wa Umoja wa Wanawake (UWT) unaofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa CCM Makao Makuu.

Alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya kujitokeza hadharani kumkingia kifua mtoto wake Ridhiwani Kikwete kuhusu kuhusika kwake na mkataba wenye utata wa Kampuni ya Lugumi.
 
“Kila mwaka naendelea kuisemea serikali iliyopo madarakani mambo mazuri, acheni hali ya kukaa na kuanza kusema kwamba serikali ile ilikuwa vile na serikali hii iko hivi.
 
“Wala msisema yule alikuwa vile na huyu yuko hivi, kwa kumalizia hayo napenda kusema mume wangu ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa anawasalimia sana,” alisema Mama Salma.
 
Akizungumzia utumbuaji wa majipu alisema, serikali kwa sasa imeanza kutumbua majipu makubwa kuanzia juu lakini zipo taarifa kuwa, yapo majipu mengine ngazi za chini pia ndani ya CCM.
 
Alisema, “kila anayejitambua kuwa ni jipu kabla hajafikiwa ni bora akajitumbua mwenyewe au ajipake spriti ili jipu hilo lipoke mapema kabla halijatumbuliwa.”
 
Hata hivyo alionesha wasiwasi kuwa, kuna uwezekano miradi mingi ya UWT ikachukuliwa kutokana na umoja huo kuwa na mali ambazo zinaonekana kumilikiwa bila kufuata taratibu.
 
Alisema, kwa upande wa ardhi kuna viwanja vingi ambavyo havina hati na vimekaa muda mrefu bila kuendelezwa jambo ambalo kwa sasa mameya wanaweza kuvibadilishia matumizi.

Mamlaka ya Mapato (TRA) Yataifisha na Kugawa Bure Sukari Mifuko 5,319 toka Brazil Yenye thamani ya Sh 373.5 milioni

$
0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Million 373.5  kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.

Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.

Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Million 246.

Mizengo Pinda ( Mtoto wa Mkulima ) Aishi Maisha ya Kikulima

$
0
0
WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, maarufu kama Mtoto wa Mkulima, ameamua kuishi maisha tofauti kabisa na watangulizi wake kwa kukwepa kukaa jijini Dar es Salaam na kwenda kijijini kwake baada ya kustaafu.

Pinda aliwahi kukiri kwamba hana nyumba jijini Dar es Salaam zaidi ya kibanda kidogo kilichoko Pugu, ambacho hakina hadhi ya kuishi mtu.

Mtoto huyo wa mkulima amejichimbia katika kijiji cha Makanyagio, Mpanda mkoani Katavi, akiendesha shughuli za kilimo na ufugaji, tofauti kabisa na watangulizi wake ambao baada ya kustaafu waliendelea kuishi jijini Dar es Salaam.

Tangu awamu ya nne ilipoondoka Ikulu Novemba 5, mwaka jana, Pinda hajawahi kufanya safari yoyote nje  ya nchi na wala kujihusisha na shughuli za kitaifa na kijamii kama walivyokuwa watangulizi wake.

Aidha, Mizengo Pinda amepotea kwenye vyombo vya habari kama watangulizi wake.

Mtoto wa Mkulima ni jina ambalo alijipachika mwenyewe baada ya kuteuliwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2008 kuwa Waziri Mkuu.

Pinda alikuwa Waziri Mkuu kati ya mwaka 2008-2015 akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Edward Lowassa (2006-2008), aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

Wakati Salim Ahmed Salim, baada ya kustaafu, aliendelea kuishi kwenye makazi yake Masaki na Unguja, John Malecela naye aliendelea kuishi Sea View, Upanga.

Fredrick Sumaye baada ya kustaafu nafasi hiyo mwaka 2005 aliendelea kuishi jijini Dar es Salaam maeneo ya Kiluvya, wakati Lowassa bado ana makazi Masaki.

Jaji Joseph Warioba, ambaye naye aliwahi kuwa Waziri Mkuu, aliendelea kuishi nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo mwaka 1990.

Hata Waziri Mkuu mstaafu, hayati Rashid Kawawa aliweka makazi yake ya kudumu eneo la Madale jijini Dar es Salaam na ndiko alikozikwa alipofariki Desemba 2009.

Cleopa Msuya anaendelea kuishi kwenye makazi yake yaliyoko Upanga, jirani na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Pinda alikuwa miongoni mwa wanachama 42 wa CCM waliochukua fomu za kuwania kuteuliwa na chama chao kusimamishwa kuwania urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Lakini bahati haikuwa kwake kwani ni miongoni mwa makada ambao majina yao yalikatwa mapema na Kamati Kuu ya chama hicho, hivyo kutofanikiwa hata kuingia kwenye tano bora.

Wanachama wa chama hicho walioingia kwenye tano bora walikuwa Rais John Magufuli, January Makamba, Benard Membe, Dk. AshaRose Migiro na Amina Salum Ali.

Tangu kukatwa jina lake kwenye hatua za awali, Pinda alionekana kujitenga kabisa na masuala ya siasa na kuamua kuishi maisha tofauti na wenzake baada ya kustaafu.

Januari 14, 2010 Pinda alitangaza mali anazomiliki kuwa ni Sh. milioni 25 kwenye akaunti yake, nyumba tatu za kawaida moja ikiwa jijini Dar es Salaam, Mpanda na Dodoma na gari moja alilolinunua kwa mkopo wa Ubunge.

Waziri Pinda aliamua kufanya hivyo ili kuweka bayana mali zake na kuonyesha mfano kwa viongozi wote nchini kufata nyayo kwa kuwa viongozi walitakiwa kuweka bayana mali zao ili kutekeleza sheria ya maadili ya uongozi.

Pinda alisema haelewi maana ya utajiri na kwamba mali alizotaja zimeshamtosheleza.

"Nina nyumba Dodoma ninayojenga kwa mikopo ya nyumba za serikali," alisema Pinda mwaka huo na kueleza zaidi:

"Nina nyumba Mpanda ambayo imepatikana kwa mpango wa kawaida tu, imetokana na visenti kidogo nikanunua pale ambapo bahati nzuri gharama za ujenzi hazikuwa kubwa sana, nikakikarabati kipo pale kipo Makanyagio pale.

"Haya! Ukitoka pale unataka niseme nini tena. Dar es Salaam sina nyumba ya kusema ya maana sana ukienda shambani Pugu kule kipo kinyumba kidogo hivyo inahitajika kazi ya ziada kuweza kufanya paonekane pa maana.

"Kijijini kwa baba yangu pale Kibaoni sina nyumba; pale mlipoona nimekaa na bibi tunapiga porojo, kile kijumba mimi na wadogo zangu tulimsaidia babu kwa ajili ya kumjengea babu yetu na pale ndipo nilipokuwa nafikia siku zote wakati wa likizo."

Pinda, ambaye alikuwa Mbunge tangu mwaka 2000 mpaka 2015, alisema miaka yote alikuwa akifikia kwenye nyumba hiyo ambayo yeye ana chumba chake kimoja hali kadhalika babu yake.

Alisema baada ya kuwa Waziri Mkuu, alijikuta kwenye wakati mgumu sana kwa kuwa alitaka kuendelea kufikia kwenye nyumba hiyo, lakini watu wa usalama walimkataza.

"Nilipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu nikataka nifikie katika ile nyumba, lakini nikaambiwa hapana, haiwezekani; hapafai; huwezi kufikia pale," alisema.

Alisema hilo ndilo lilikuwa tatizo lake la kwanza kwa hiyo atajaribu kujenga tena kitu ambacho na yeye atapata mahala pa kufikia pamoja na wasaidizi wake kwenye eneo hilo wakati huo.

"Nimegundua tatizo ni hawa wakubwa. Pale kijijini kwetu hakuna nyumba za wageni hatuna chochote mi nilidhani nikienda kule nikiachwa kwa babu na bibi, wao wataenda huko umbali wa kilomita wakatafute pa kupumzika, lakini wakasema no! no! no! haiwezekani, nikawaelewa."

Alisema ukiondoa nyumba hiyo, vitu vya maana zaidi hana labda gari la mkopo akiwa Mbunge.

"Hivi ukiwa na hivi nilivyo navyo unahitaji nini cha zaidi tena?

"Kwa hiyo kipato kidogo unachokipata unaweza kukitumia kwa ajili ya huduma za watoto wako kusoma na kadhalika kwa sababu ni vitu viko nje ya taratibu za serikali.”

Rais Magufuli Atetea Uamuzi wake wa Kutimua Wafanyakazi

$
0
0

Rais John Magufuli ametetea uamuzi wake wa kuwatimua baadhi ya watumishi wa umma wanaokiuka maadili akisema anataka kuirejesha nchi kwenye mstari.

Rais amesema hayo leo alipozungumza na waumini katika misa ya Jumapili katika Kanisa Katoliki parokia ya Tokeo la Bwana Burka jijini Arusha.

Amesema watu katili ni wale ambao walikuwa wanawaibia Watanzania na kuwanyonya wanyonge.

Amesema analazimika kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi si kwamba ni katili, bali lengo ni kuwatumikia Watanzania na kuirejesha nchi kwenye mstari.
 
Rais huyo aliyejibatiza “mtumbua majipu”,  amesema Tanzania ni taifa tajiri, hakuna sababu ya wananchi kulalamika kila kona, kwani kuna ardhi ya kutosha, madini ya kila aina, wanyama wa aina mbalimbali ambao baadhi wameanza hadi kupelekwa nje.
 
"Ninapochukua hatua nataka kuweka Tanzania iliyonyooka, mimi tayari nimesema nimejitoa sadaka kwa watanzania hasa wanyonge," alisema.

Picha Mbalimbali za Rais Magufuli Alivyoshiriki Ibada Ya Jumapili Ya Kupaa Kwa Bwana Katika Parokia Ya Toleo La Bwana Jimbo La Arusha Mjini Mei 08,2016

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Mei, 2016 ameungana na waumini wa Parokia ya Toleo la Bwana iliyopo katika Jimbo Katoliki la Arusha kusali ibada ya Jumapili, ambapo katika salamu zake amewaomba watanzania kuendelea kuiombea nchi yao ili kazi anayoifanya ya kukabiliana na matatizo yanayowakabili watanzania wanyonge ifanyike kwa mafanikio.

Dkt. Magufuli amesema hayo alipokaribishwa na Mwenyekiti wa Parokia hiyo Bw. Philemon Mushi kuwasalimu waumini wa kanisa hilo, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Jumapili ya kupaa kwa Bwana.

"Niko pamoja na nyinyi ndugu zangu watanzania na wana Arusha wote, napenda kuwaahidi tena sitawaangusha, nitasimama mbele kuwatetea masikini, siku zote nitakuwa upande wenu, siku zote nitatembea na nyinyi, nasema kwa dhati kabisa na nataka muamini hilo kwamba sitawaangusha" amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa na waumini walioshiriki ibada hiyo.

Rais Magufuli amewahakikishia watanzania wote kuwa atahakikisha ahadi zote alizoziahidi anazitekeleza na amewaomba watanzania wote kuungana na kushikamana ili kufanikisha juhudi za kuijenga Tanzania bora.

"Ninajua kuongoza ni kazi kubwa, ninajua kuongoza Taifa lililo masikini kama Tanzania inahitaji mkono wa Mungu, kwa hiyo niwaombe sana ndugu zangu Wakristo na watanzania kwa ujumla, muendelee kuliombea Taifa hili, kuniombea mimi, na pia kujiombea sisi wote ili amani tuliyonayo katika nchi yetu iendelee kudumu katika maisha yote.

"lakini siku zote katika matendo yetu kila tunapofanya tumtangulize Mungu kwa sababu Mungu ndio kila kitu, lakini tutambue kwamba siku moja tutakufa, kwa hiyo ni vyema katika matendo yetu tutakapokuwa hapa duniani tujitahidi sana kufanya matendo mazuri kwa ajili ya watu na hasa watu wanyonge, ambao kwa kweli watanzania waliowanyonge wanapata shida sana" Amebainisha Rais Magufuli.

Pia Dkt. Magufuli amewasihi watanzania wote kuachana na ushabiki wa vyama vya siasa na badala yake waungane katika ujenzi wa Taifa na kukabiliana na kero zinazowaumiza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha Mei 8, 2016
Sehemu ya waumini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akiwsalimia  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha  Mei 8, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea zawadi ya Rozari kutoka kwa Padri Kiongozi  Peter Pinto Sio Germin Longio  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha Mei 8, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipokea zawadi ya Biblia Takatifu kutoka kwa Padri Kiongozi Peter Pinto Sio Germin Longio  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha Mei 8, 2016

Spika wa Bunge Afungua Mkutano Wa Chama Cha Wabunge Wanaopambana Na Rushwa

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifungua Semina wa Chama cha Wabunge wanaopambana na Rushwa-Tanzania Mjini Dodoma leo tare 8 Mei, 2016.

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifungua Semina wa Chama cha Wabunge wanaopambana na Rushwa-Tanzania Mjini Dodoma leo tare 8 Mei, 2016
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ( katikati  pamoja na viongozi wengine wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa Semina wa Chama cha Wabunge wanaopambana na Rushwa-Tanzania. Wengine katika ni , Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki  (kushoto) na Cecilia Paresso (Mb) – Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho.
Wakili wa kujitegemea Bw. Said Yakubu akiwasilisha mada wakati wa Semina wa Chama cha Wabunge wanaopambana na Rushwa-Tanzania.

(Picha na Ofisi ya Bunge)

ADC Yawafuta Uanachama Wanachama wake Wanne Akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Said Miraaj kwa Kususia Uchaguzi mkuu wa Marudio wa Zanzibar

$
0
0
Chama cha Alliance for Democratic Change ADC kimewafuta uanachama wanachama wake wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Said Miraaj,Katibu Mkuu Bi.Lydia Bendera,Mkurugenzi wa mipango na uchaguzi Bwana Jumanne Magafu pamoja na Katibu wa Kamati ya ulinzi Bwana Juma Wandwi kwa makosa ya kukiuka katiba ya chama hicho kwa kususia kushiriki uchaguzi mkuu wa marudio wa Zanzibar.
 
Maamuzi hayo yamefikiwa katika mkutano mkuu wa chama hicho ambapo akizungumza baada ya ufunguzi aliyekuwa mlezi wa chama cha ADC ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Zanzibar,Mhe.Hamad Rashid amesema katiba ya chama inasisitiza ushiriki katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi,hivyo kutoshiriki ni kukivunja nguvu chama katika mikakati yake ya kuchukua dola.

Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa -ADC- Msajili Msaidizi wa vyama vya siasa Bwana Sisty Nyahoza amesema kitendo cha chama cha siasa kutoshiriki uchaguzi kinakwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa na malengo ya kuanzishwa chama Chochote cha siasa na kusisitiza ipo haja ya kuangalia mfumo wa usajili wa vyama utakaowezesha kutoa adhabu kwa vikavyoonekana kukataa kushiriki katika chaguzi.

Aidha katika mkutano mkuu huo, wajumbe wamemchagua aliyekuwa mlezi wa ADC ambaye kwa sasa ni Waziri wa Kilimo Zanzibar Mhe.Hamad Rashid kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bwana Doyo Hassan Doyo amechaguliwa kushika wadhifa wa katibu mkuu wa chama.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya May 9

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images