Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Naibu Spika Azima Mjadala Bungeni wa Kupanda Kwa Sukari

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amezima hoja ya Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) aliyeomba suala la kupanda bei ya sukari lijadiliwe bungeni.

Wakati hayo yakitokea wananchi wa Mkoa wa Mbeya wameviomba vyombo vya dola kupekua malori yanayotokea Malawi, kwa madai yanabeba sukari ya magendo na kuingiza nchini.

Akitumia kifungu cha Kanuni za Bunge cha 47(1, 2, 3), mbunge huyo alisema bungeni mjini hapa jana, kuwa suala hilo ni muhimu kwa Watanzania hivyo ni vyema likajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Alisema tangu itangazwe utaratibu wa kusitisha sukari kuingizwa nchini kutoka nje, bidhaa hiyo imekuwa adimu na bei yake imekuwa inapanda kila siku na kusababisha maisha ya wananchi kuzidi kuwa magumu.

Hata hivyo, kabla hajamalizia kuzungumza, Dk Ackson alimkatiza Bashe, akisema suala hilo lilishafanyiwa kazi Alhamisi wiki iliyopita, wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

“Mtakumbuka Waziri Mkuu Alhamisi ya wiki iliyopita, alitoa maelezo na akatoa maelekezo kuwa sukari itaruhusiwa kuingizwa nchini kwa kiasi ambacho alitaja,”alisema.

Alisema pamoja na udharura wake kwasababu ilishatolewa maelekezo, wabunge wasubiri yale maagizo ya Waziri Mkuu kuuliza kama sukari imeingia ama haijaingia na kama hajaingia lini inaingia.

Wiki iliyopita, Waziri Mkuu akijibu hoja iliyoibuliwa bungeni hapo inayohusu pia bei ya sukari, Waziri Mkuu alisema serikali imeruhusu kiasi kidogo cha sukari kuingizwa nchini ili kupunguza tatizo la upungufu wa bidhaa hiyo.

Kwa mujibu wa Majaliwa, Tanzania ina uwezo wa kuzalisha tani 300,000 za sukari kwa mwaka wakati nchi inahitaji tani 420,000 hivyo kuwepo na upungufu wa tani 120,000.

Aidha, mapema mwezi uliopita, serikali ilitangaza kuwa bei elekezi ya sukari itakuwa Sh 1,800 kwa kilo, lakini hali katika maeneo mbalimbali nchini ni tofauti, kwani bidhaa hiyo muhimu inauzwa kwa bei ya juu.

Katika maeneo mbalimbali ukiwamo Mkoa wa Dar es Salaam, sukari inauzwa kuanzia Sh 2,200 hadi Sh 2,500 kwa kilo.

Baadhi ya wafanyabiashara nchini wameamua kufanya njama za kuficha bidhaa hiyo ili kuonekana kuwa kuna uhaba ili waruhusiwe kuagiza kutoka nje, jambo ambalo limekwishakataliwa na Rais John Magufuli.

Wiki iliyopita, mkoani Singida, wananchi walisaidia kukamatwa kwa mifuko 655 ya sukari sawa na tani 24.3, na kutiwa nguvuni wafanyabiashara wawili pia wakihusishwa na bidhaa hiyo ambayo ilifichwa stoo.

Waliokamatwa ni Mohamed Alute Ally (44) mfanyabiashara wa Unyankindi aliyekutwa na mifuko 335 ya kilo 25 kila mmoja na Yusufu Suleiman (39) mfanyabiashara wa Minga aliyepatikana na mifuko 320 ya kilo 50.

Taarifa ya kukamatwa kwa sukari hiyo na wafanyabiashara hao ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Saidi Amanzi.

Taarifa zilieleza kuwa mfuko mmoja wa sukari ambao huuzwa kwa Sh 92,650 sasa unauzwa kati ya Sh 115,000 na Sh 120,000 huku kilo moja ikiuzwa kati ya Sh 2,400 na 2,800 kwa kilo kinyume cha bei elekezi ya Sh 1,800.

Kutoka Mbeya, wananchi jijini hapa wamevitaka vyombo vya dola kuyapekua malori yanayotokea nchi jirani ya Malawi, kwa kile walichodai yanabeba sukari ya magendo na kuingiza nchini.

Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao, walisema hivi karibuni kuna malori manane ya kampuni moja  yalibeba shehena ya sukari yakitokea Malawi na yaliegesha kwenye moja ya kituo cha mafuta cha Uyole kwa lengo la kutafuta wateja.

Mkazi mwingine wa Mtaa wa Soweto, Hamphrey Lyoto alisema suala la uingizwaji wa sukari, linafanywa mchana ambapo malori yanapeleka sukari kwenye nyumba ya mfanyabiashara mmoja eneo hilo aliyejiwekea kiwanda cha kuweka sukari kwenye mifuko ya kilo moja moja na nusu kilo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula alipoulizwa juu la suala hilo, alisema hafahamu lolote kwa kuwa ameanza kazi hivi karibuni, lakini aliahidi kulifutalia.


Majibu ya Snura baada ya Chura wake Kupigwa Nyundo na Serikali

$
0
0

Baada ya wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kuufungia wimbo wa Snura, Chura jana, muimbaji huyo anaonesha kutoshtushwa na hatua hiyo hasa kutokana na support anaiyopata kutoka kwa mashabiki wake.

Kwa ufupi haoneshi stress, walau kwa kile alichokiandika kwenye Instagram.“Ingekua ndio hela leo ningekua bilionea lo!!! Nawapenda sana kwakweli na nawatakia usiku mwema,” aliandika Snura kwenye Instagram.

Aliongeza hashtag: #utaipenda2_ndimuimekolea_malimao_kama__210_habarizetuwanazo_ilazaohatuna.”

Pamoja na wimbo huo kufungiwa kuchezwa kwenye redio na TV, Snura aliagizwa kuhakikisha amefuta video zake zote mtandaoni.

Wabunge Wagomea Utaratibu wa Kujisajili Mara Mbili....Wadai wao ni Watu wazima na Sio Wanafunzi

$
0
0

Wabunge wameitaka Ofisi ya Bunge iwaondolee mara moja utaratibu wa kusaini kwa kutumia vidole mara mbili kwa siku kwa kuwa wao si wanafunzi.

Hoja hiyo iliwasilishwa kwa njia ya mwongozo na kuungwa mkono na wabunge wote isipokuwa mawaziri na Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) mjini Dodoma jana.

Katika Mwongozo wake, mbunge huyo alisema kitendo cha kutakiwa kusaini mara mbili kwa siku ni kero kwa wabunge na uonevu kwa kuwa hata Bunge limekuwa likitumia muda wa mapumziko wa wabunge kwa kazi za Bunge.

“Mheshimiwa Naibu Spika wewe mwenyewe muda mfupi umetangaza matangazo mbalimbali yanayotaka baadhi ya wajumbe wa kamati wakutane baada ya saa saba mchana, tunafanya kazi nje ya mapumziko yetu, haya haina tatizo... “...tatizo langu ni kitendo cha wabunge kutakiwa kusaini mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, wakati mwingine tunatoka hapa saa saba, wabunge tunashughulikia mambo mpaka saa 12, mbunge anatumia muda wake wa mapumziko na ule wa kuhudhuria kikao cha jioni,” alisema Haji.

Alisema inasikitisha kuona mbunge anatolewa kwenye kazi za kujenga taifa ili aje tu asaini kwa kidole tena mara ya pili.

Alisema jambo hilo linawatatiza wabunge kwa kuwa wanajiona kama wanachukuliwa kama wanafunzi kwa kufuatiliwa kwani hata kwenye benki wafanyakazi hawasaini na kufuatiliwa kama ilivyo kwa wabunge hao.

Alifafanua kuwa kabla ya kuomba Mwongozo huo, alifanya utafiti kwenye benki mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambao nao wana utaratibu kama huo wa Bunge lakini hakuna mahali wanapotakiwa kusaini kwa vidole mara mbili.

“Kutokana na uzito wa jambo hili naomba kutoa hoja wabunge mniunge mkono mpango huu ukome,” alisema na wabunge takribani wote walisimama ishara ya kumuunga mkono na kumpigia makofi na vigelegele.

Kwa upande wake, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alisema kutokana na namna wabunge hao walivyopokea suala hilo, pamoja na kwamba kikanuni jambo hilo halikutakiwa kuombewa mwongozo bado litaangaliwa.

“Hata hivyo, nifafanue kuwa kusaini mara mbili lengo lake si kuwafanya wabunge wanafunzi, ila lengo ni kutaka kujua nani wapo humu ndani (bungeni),” alisema Dk Ackson.

Hukumu ya Kesi Kafulila Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Itatolewa Mei 17

$
0
0

Mahakama  Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo, David Kafulila inatarajia kutoa hukumu Mei 17, mwaka huu.

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora anayesikiliza kesi hiyo mjini Kigoma, Ferdinand Wambali alisema baada ya pande zote kuwasilisha ushahidi na maelezo yao mahakamani hapo amepanga kutoa hukumu tarehe hiyo.

Kutolewa kwa tarehe hiyo ya hukumu kunatokana na kufungwa kwa utoaji ushahidi wa maelezo ya kesi hiyo ambayo aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, aliwa mshitakiwa wa tatu katika kesi hiyo.

Baada ya kukamilika kwa ushahidi wa pande zote, Jaji Wambali ameomba kupatiwa muda wa kutosha kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo ili atoe hukumu ya haki.

Katika kesi hiyo Namba Mbili ya mwaka 2015, David Kafulila aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo anaitaka mahakama itengue matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa CCM, Hasna Mwilima na badala yake mahakama imtangaze yeye (Kafulila) kama mshindi halali wa uchaguzi katika jimbo hilo.

Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Mwilima, Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyeiwakilisha Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Katika kesi hiyo, Wakili Kenedy Mfungamtama anamsimamia Mwilima wakati David Kafulila akisimamiwa na Wakili Profesa Abdallah Safari na Daniel Rumenyela.

Ijue Sayansi Ya Kusimama Kwa Uume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani.

Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ?

Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu

HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME
Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo :

Hatua  ya  kwanza, ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari.

Na  hatua  ya  pili  ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa STRONGER  AND  LONGER  ERECTION

JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA.

1. HATUA   YA  KWANZA:

DAMU  KUTIRIRIKA  KWA  KASI KUINGIA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME  NA  KUUFANYA  UUME  KUSIMAMA  NA  KUWA  MGUMU.

Unapopata  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  fahamu iliyopo  kwenye  ubongo,  hupeleka  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo, ambayo  nayo  hupeleka  taarifa  hadi  kwenye  mishipa  ya  uume. Taarifa  inapofika  kwenye  mishipa  ya  uume  huifanya  mishipa hiyo  ku-relax  na  hatimaye   kufanya  mishipa  ya  ateri  kufunguka  na  kutanuka. Mishipa  ya  ateri  inapo  tanuka  na  kufunguka, huruhusu  damu  kuingia  kwa  kasi  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  huume  kusimama.

Ni  muhimu  kujua  kuwa, mishipa  ya  uume  inapo relax  hupelekea  kuisukuma na  hatimaye  kuiziba  mishipa  ya  vena  iliyo  karibu  na  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuiondolea  uwezo  wa  kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  sehemu  nyingine  za  mwili.

N.B: Kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyingine  za  mwili.  Au  kwa  lugha  nyingine  unaweza  kusema, kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  kwenye  mishipa  ya  uume.
 
2. HATUA  YA  PILI  :
DAMU  KUENDELEA  KUHIFADHIWA  KATIKA  UUME  WAKATI  UUME  UKIWA  UMESIMAMA  NA  HIVYO  KUUFANYA  UUME  UENDELEE  KUDUMU  KATIKA TENDO LA NDOA   KWA  MUDA  MREFU.

Uume  ulio  simama, ili  uendelee  kusimama, ni  lazima  mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo   wa  kunyonya  damu  kutoka  katika  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyinginezo  za  mwili. .

Mishipa  ya  Vena  ndio  inayo  husika  na  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume na  kupeleka  sehemu  nyingine  za  mwili.  Ili  uume  uendelee  kusimama  lazima  mishipa  hii  ya  vena  iwe imezibwa. Ili  iweze  kuzibwa   ni  lazima  misuli  laini  ya  kwenye  uume  iwe - ime  relax na  hivyo  kuifanya  mishipa  ya  vena  kushindwa  ku  nyonya damu  kutoka  kwenye  uume.

Endapo  mishipa  ya  vena  itazibuka , basi  itanyonya  na  kutoa  damu yote  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume uliosimama  na  kuipeleka  sehemu  nyinginezo  za  mwili  na  hatimaye  uume  huo ulio simama  na  utasinyaa  mara  moja.

JINSI  UUME  UNAVYO  SIMAMA  NA  KUSISIMKA.
Tumeisha  zifahamu  hatua  mbili  muhimu  katika  kusimama  kwa  uume

Jinsi  Uume  unavyo  simama: Katika  uume  kuna chemba  yenye  mishipa  laini  sana, ambayo  ndio  huufanya  uume  kusimama.

Mishipa  hii  ipo kama  sponji  hivyo  huweza  kunyauka  na  kutanuka.

Damu  inapoingia  ndani  ya  mishipa  hii  huufanya  uume  kusimama  na  kuwa  mgumu  kama  msumari.

Damu  inapoendelea  kuhifadhiwa  ndani  ya  mishipa  hii  wakati  wa  tendo  la  ndoa, huufanya  uume  uendelee  kusimama.

Mwanaume  unapo  patwa  na  wazo la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  fahamu  iliyo  kwenye  ubongo  hupeleka  ishara  kwenye  uti  wa mgongo, ambao  nao  hufikisha   taarifa  kwenye  mishipa  ya  uume.

Taarifa  ikisha  fika  kwenye  mishipa  ya  uume, huifanya  mishipa  ya  uume  ku-relax  na  mishipa  ya  uume  inapo  relax, hufanya  mambo  makuu  mawili;

i. Kwanza  hufanya  mishipa  ya  ateri  kufunguka na  hivyo  damu  kutiririka  kwa  kasi  sana  kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume

( Mishipa  ya  ateri  ndio  inayo  tumika  kama  njia  ya  kuingiza  damu  kwenye  uume. Bila  mishipa  ya  ateri  imara  na  yenye  afya, damu  haiwezi kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume, na  damu  isipoweza kuingia  kwenye  mishipa  ya  uume, basi  uume  hauwezi  kusimama )

ii.Pili huibana  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuizuia    kunyonya  damu  kutoka  kwenye  uume  na  kuipeleka  kwenye  sehemu nyingine  za  mwili. Matokeo  yake  kuufanya  uume  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Kumbuka ,kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  neva  iliyo  karibu  na  mishipa ya  uume, ni kunyonya  damu kutoka  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  kwenye  sehemu  nyingine  za  mwili. Kwa  lugha  nyingine, kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  kwenye  mishipa  ya  uume ulio simama.

Kadri  damu  inavyo  zidi  kuingia  ndani  ya mishipa  ya  uume, ndivyo  uume  unavyo  zidi  kuwa  mgumu  na  kukakamaa.

Na  kadri  damu  inavyo  hifadhiwa  ndani  ya  mishipa  ya  uume, ndivyo  uume  unavyo endelea  kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa kwa  muda mrefu.

Baada  ya  kumaliza  kufanya  tendo  la  ndoa,mishipa  ya  uume inarudi  katika  hali  yake  ya  kawaida (inanyauka ), ikisha  nyauka, mishipa  ya  ateri  inanyauka  pia, vena  zinafunguka  na  kunyonya  damu  katika  mishipa  ya  uume  na  kuirejesha  katika  sehemu nyinginezo  za  mwili  na  hatimaye  uume  kurudi  katika  hali  ya  kawaida  ( Flaccid ).

Hali  hii  itaendelea  kujirudia  kwa  kadri  utakavyo  kuwa  ukiendelea kufanya  tendo  la  ndoa.

Mambo  Muhimu  Katika  Kuufanya Uume  Usimame na  Kuendelea  kudumu  katika  kusimama  kwa  muda  mrefu wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Ili  uume  uweze  kusimama  imara  kama  msumari na  uendelee  kusimama  imara  na  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo la  ndoa, ni  lazima  mambo  yafuatayo yawepo.

1. Mishipa ya   uume iliyo  imara  na  yenye  afya  njema.

2. Mfumo   mzuri  wa damu  katika   mwili  mzima.

3.Mtiririko  imara  wa  damu kuingia  na  kutoka  ndani  ya  mishipa  ya  uume.

4. Ushirikiano  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  ya  kwenye  ubongo  (nerves), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  mishipa  ya  kwenye  uume.

Ili  mwanaume  aweze  kuwa  imara  katika  tendo  la  ndoa, ni  lazima  mambo  manne  niliyo yataja  hapo  juu  yawe  sawa  sawa  bila  hitilafu  yoyote. Kinyume  chake, mwanaume  hawezi  kuwa  na  nguvu  za  kiume.

MAMBO   YANAYO SABABISHA   UKOSEFU/UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Tumeshajua   nguvu za  kiume  ni  nini, jinsi  uume  unavyo  simama, hatua  za  kusimama  kwa  uume, pamoja  na  mambo  yanayo  fanya  uume  uweze  kusimama  na  kuwa  na  uwezo  wa  kuendelea  kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Ni  vyema  tukajua  mambo  yanayo  sababisha  kushindwa  kusimama  kwa  uume, mambo  yanayo  sababisha  uume  ushindwe kuendelea  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa   pamoja  na  mambo  yanayo  fanya  mtu  ashindwe  kurudia  tendo  la  ndoa.

Yafuatayo  ni  mambo  yanayo  sababisha  ukosefu wa  nguvu  za  kiume.

1. MAGONJWA  YANAYO  SHAMBULIA  MFUMO  WA  DAMU  PAMOJA  NA  MISHIPA  YA  DAMU.

Damu  ndio  nishati  inayo wezesha  kusimama  kwa  uume  na kuufanya  kuwa  mgumu na  imara  kama  msumari.

Damu  ndio  nishati  inayo weza   kuufanya  uume uendelee kusimama  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

Damu  ndio  nishati  inayo  upa  uume  uimara  na  uwezo  wa  kurudia  tendo  la  ndoa  zaidi  ya  mara  moja.

Hivyo  basi  ili  uume  uweze  kuwa  imara na  wenye  nguvu, pamoja  na  kuwa  na  uwezo  wa  kumudu  na  kustahimili   tendo  la  ndoa  wakati  wowote , basi  ni  lazima   mwanaume  awe  na mfumo  imara  wa  damu  utakao  ruhusu  kutiririka  kwa  damu  kwenda  katika  sehemu mbalimbali  za  mwili  ikiwamo  uume.

Ili  mfumo  uweze  kuwa  imara  ni  lazima  mhusika  awe  na  damu  ya  kutosha, na  pili  awe  na  mishipa  ya  damu  yenye  afya.

Katika  mwili  wa  mwanadamu,kuna  mishipa  inayo  tumika  kusafirisha  damu  kutoka  katika  sehemu moja  ya  mwili kwenda  katika  sehemu  nyingine  ya  mwili  ikiwemo  uume. Mishipa  hiyo  ni  kama  vile  vena (veins), atery ( ateri) na  capillary  ( kapilari )

Mishipa  hii  ya  damu  inapaswa  kuwa  imara  na  yenye  afya  njema  wakati  wote.   Mishipa  hii  ikipatwa  na  hitilifu, basi  itazuia  kusafirishwa  kwa  damu  katika  sehemu  mbalimbali za  mwili  wa  mwanadamu  na  hatimaye  kufanya  suala  la  kuwa  na  nguvu  za  kiume  kwa  mhusika  kuwa  ugumu  kwa  sababu   ya  kushindwa  kupeleka  damu  kwenye  mishipa  ya  uume.

Magonjwa  kwenye  mishipa  ya  damu  huzuia   kutirika  kwa  damu kwenye  ogani  muhimu   kama  vile  moyo, ubongo na  figo.

VIASHIRIA  VYA  MAGONJWA  KWENYE  MISHIPA  YA  DAMU.
Utajuaje  kwamba  una  magonjwa  kwenye  mishipa  yako  ya  damu ?

Ukiwa  una  matatizo  yafuatayo ya  kiafya, ni  ishara  kwamba, una  magonjwa  kwenye  mishipa  yako  ya  damu:

1.  Kolestrol ( Ama  lehemu  kwenye  damu )
Kolestrol  nyingi  kwenye  damu, huzuia  kutiririka  kwa  damu. Kolestrol  ikizidi  kwenye  damu,  hupelekea  kuziba   mishipa  ya  ateri  ambayo  kazi  yake  ni  kupeleka  damu  kwenye  uume. Matokeo  yake  ni  mhusika  kutokuwa  na  uwezo  wa  kusimamisha  uume  wake barabara  kwa  sababu uume  hauwezi  kusimama  bila  damu  kuingia  ndani  ya  mishipa  ya  uume. 
 
 Hivyo  basi pamoja  na  dawa  ya  nguvu  za  kiume, yakupasa  kutibu  kolestrol. Unaweza  kuondoa  kolestrol  kwenye  damu  kwa  kutumia  dawa  mbali  za  asili  kama  vile mdalasini,uwatu, habbat sodah  etc.  Jinsi  ya  kujitibu  kolestrol  kwa  kutumia dawa asilia  tafadhali  tembelea


2.      Shinikizo  Kubwa  la  Damu
Shinikizo  Kuu la  Damu husababisha  mishipa  ya  ateri  ambayo  hutiririsha  damu  iingiayo  kwenye  uume  kuziba  na  kushindwa kutanuka  kwa  kiwango  inachotakiwa  kutanuka.

Pia  huifanya  mishipa  laini  katika  uume   kushindwa  ku-relax  na  hivyo  kushindwa  kuizuia  mishipa  ya  vena  ya  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  kwenye  maeneo  mengineyo  ya  mwilini.

Matokeo  yake  kunakuwa hakuna  kiasi  cha  kutosha  cha  damu  iingiayo  kwenye  uume  na  hivyo  kufanya  uume  ushindwe  kusimama.

Vile  vile  hata  kiasi  kidogo  cha  damu  kinacho  ingia  kwenye  uume, kinashindwa  kuendelea  kuhifadhiwa  ndani  ya  uume  wakati uume  ukiwa  umesimama, na  matokeo yake  ni  uume  kusinyaa  ndani  ya  kipindi kifupi  sana  tangu  usimame.

Pamoja  na kutumia  dawa  ya  nguvu  za  kiume, unapaswa   pia  kutumia  dawa  asilia  kujitibu  tatizo  la  shinikizo  kuu  la  damu.

Kufahamu  jinsi  ya  kujitibu  tatizo  la shinikizo  la  damu  kwa  njia  ya  asilia, tembelea :


3.  Ugonjwa  wa  kisukari :
 Ugonjwa  wa  kisukari  ni  miongoni  mwa  vyanzo  vikuu  vya  tatizo  la  ukosefu wa  nguvu  za  kiume.  Kusimama  kwa  uume  kunategemeana  na  kutiririka  kwa  damu  mwilini. Kisukari  huathiri  mishipa  ya  damu pamoja  na  usambazaji  wa  damu  kwenye  ogani  muhimu  mwilini  kama  vile  moyo, ubongo, figo  na  uume.

Kiukweli, mwanaume  mwenye  kisukari  yupo  katika  risk  kubwa  ya  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume,m tena  katika  kiwango  kikubwa  sana.

Unashauriwa pamoja  na kutumia  dawa  ya  nguvu  za  kiume, tumia  pamoja  na  dawa  mbalimbali  za  asili  kwa  ajili  ya  kubalance  sukari  yako mwilini. 
 
Zipo  dawa  mbalimbali  za  asili  zinazo  saidia  kubalance  kiwango  cha  sukari  mwilini. Dwa  hizo  ni  pamoja na mdalasini, unga  wa  uwatu, mbegu  za  uwatu, manjano, majani  ya  manjano,mbegu  za  katani, nakadhalika. Namna  ya  kutumia  dawa  hizo  kujitibu  tatizo  la  sukari, tafadhali  tembelea :http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/jitibu-kisukari-presha-shinikizo-la.html

4. Magonjwa  ya  figo
Tatizo  la  ugonjwa  wa  figo  huathiri  vitu vingi  ambavyo  ni  muhimu  sana  katika  kuufanya  uume  uweze  kusimama  na  kuendelea  kudumu  katika  kusimama.

Tatizo  la  figo, huathiri  homoni, huathiri kutiririka   kwa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume. Huathiri  mfumo  wa mishipa  ya  neva  pamoja  na  nishati  ya  mwili mzima.

Pamoja  na  dawa  ya  kutibu  tatizo  la  nguvu za  kiume, unapaswa  pia, kutibu  tatizo  la  figo. Kufahamu  jinsi  ya  kujitibu  magonjwa mbalimbali  ya  figo  kwa  kutumia  dawa mbalimbali  asilia, tembelea :http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/jitibu-kisukari-presha-shinikizo-la.html

5.        Ugonjwa  wa  moyo
Moyo  ndio  supplier  mkubwa  wa  damu  katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili.  Ugonjwa  wa  moyo  hupunguza  uwezo  wa  moyo  kusambaza  damu  kwenye  mishipa  mbalimbali  ya  damu  na  hivyo  kuathiri  utendaji  kazi  wa  mishipa ya  damu  kama  vile  ateri  na  vena. Matokeo  yake  ni  mishipa  hiyo  kushindwa  kupeleka  damu  ya  kutosha  katika  uume  pamoja  na  kushindwa  kuifanya  mishipa  ya  uume  kurelax na  matokeo  yake,. Ukosefu  wa nguvu  za  kiume. Hivyo  basi, pamoja  na  dawa  ya  nguvu  za  kiume, unapaswa  pia   kutibu  tatizo  la  moyo. Kufahamu  jinsi  unavyo  weza  kutibu ugonjwa  wa  moyo  kwa  dawa  asilia, tembelea :


6.  Kupwaya  kwa  mishipa  ya  vena.
Kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  kwenye  uume   kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika sehemu  nyingine  za  mwili.  Mishipa  ya  vena iliyopo  karibu  na  uume  kazi  yake  kubwa  ni kuhakikisha  hakuna  damu  yoyote  kwenye mishipa  ya  uume. ( KUMBUKA  KUWA  DAMU NDIO  HUFANYA  UUMU  USIMAME, HIVYO CHOCHOTE  KILE  KITAKACHO  FANYA  DAMU ISIKAE  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME , KITAFANYA  UUME  USINYAE  )

Ili  uume  uendelee  kusimama  ni  lazima, mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo  wa kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya uume  kupeleka  nje  ya  mishipa  ya  uume.

Na  ili  mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo  wa   kunyonya  damu  kutoka  kwenye   mishipa ya  uume  ulio  simama  na  kuipeleka  kwenye sehemu  nyingine  za  mwili,  ni  lazima mishipa  ya  uume  iwe  imara  na  thabiti  isiyo na  hitilafu  yoyote  ile.

Mishipa  ya  vena  ikipwaya, mwanaume hutokuwa  na  uwezo  wa  kusimamisha  uume wako, na  ikitokea  umefanikiwa kuusimamisha  basi  utasimama  ukiwa legelege  sana  na  utasinyaa  ndani  ya  muda mfupi  sana, kwa  sababu  damu  iliyo  ingia ndani  ya  uume  wako  na  kuufanya  usimame, itanyonywa  ndani  ya  muda  mfupi  sana  na kutolewa  nje  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo kuufanya  uume  wako  usimame.

 Tatizo  la  kupwaya  kwa  mishipa  ya  vena linasababishwa  na  kupiga  punyeto  kwa muda  mrefu  pamoja  na  ugonjwa  wa kisukari.

KUPIGA  PUNYETO  KWA  MUDA  MREFU: Kupiga  punyeto  kwa  muda  mrefu  ni  moja kati  ya  vyanzo  vikuu  vya  tatizo  la  la ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  Asilimia kubwa  ya  vijana  wenye  tatizo  la  ukosefu wa  nguvu  za  kiume, linasababishwa  na upigaji  wa  punyeto  kwa  muda  mrefu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Unapopiga  punyeto  unakuwa  unaiminya mishipa  ya  uume   ambayo  ndio  inaufanya uume  usimame.

Matokeo  yake  unaifanya  mishipa  hiyo  ilegee na  kutokuwa  na  uwezo  wa  kusimama  tena.

Mishipa  ya  uume  iliyo  legea  kutokana  na upigaji  punyeto, huleta  madhara  yafuatayo  :

i.           Huondoa  uwezo  wa  mishipa  ya  uume kurelax.

( Unapopata  wazo  la  kufanya  tendo  la ndoa, mishipa  ya  uume  ina relax  , mishipa  iki  relax  husababisha  mishipa ya  ateri  kupanuka  na  kuruhusu  damu kingie  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na hatimaye  kuufanya  uume  usimame  na kuwa  mgumu)
 
ii.Mishipa   ya  kiume  ikishindwa  ku relax husababisha  mishipa  ya  ateri  kuziba

iii. Mishipa  ya  ateri  ikiziba, damu  haiwezi kutiririka  kuingia  kwenye  mishipa  ya uume, na  hata  ikitokea  damu  imeingia ndani  ya  mishipa  ya  uume  basi huingia  kiasi  kidogo sana   tena  kwa presha  ndogo  sana  hivyo  basi  hata kama  uume  utasimama   basi utasimama  ukiwa  legelege  sana

iv. Mishipa  ya  uume  ikishindwa  kurelax basi  haitakuwa  na  uwezo  wa  kuipush na  kuiziba  mishipa  ya  vena  ambayo ndio  hunyonya  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  ulio  simama. 
 
Matokeo  yake  basi, damu  kidogo  iliyo ingia  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na kuufanya  uume  kusimama, hunyonywa na  kutolewa  nje  ya  mishipa  ya  uume ndani  ya  sekunde  chache  sana  na hivyo  kuufanya  uume usinyae  ndani ya  muda  mfupi  sana.

v. Mishipa  ya  uume  kulegea

vi. Uume  kurudi ndani  na  kusinyaa  na kuwa  kama  uume  wa  mtoto

6. Tatizo  la  unene  kupita  kiasi : Tatizo  la unene  na  uzito  kupita  kiasi  ni  miongoni mwa  mambo  yanayo  sababisha  upungufu wa  nguvu  za  kiume. Unene  kupita  kiasi humuweka  mtu  katika  hatari  ya  kupatwa na  magonjwa  kama  vile  kisukari, presha, moyo  na  shinikizo  kuu  la  damu. 
 
Na magonjwa  ya  kisukari, moyo,presha  na shinikizo  la  damu  husababisha  upungufu na ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, na  hivyo kumuweka  muhusika  katika  hatari  kuu  ya kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa nguvu  za  kiume.

Hivyo  basi  kwa  wewe  mwenye  tatizo  la unene  na  uzito  kupita  kiasi , pamoja  na kutumia  tiba  ya  nguvu  za  kiume,  ni  vyema ukafanya  na  mpango  wa  kupunguza  unene na  uzito  wako.

JINSI  YA  KUPUNGUZA  UZITO  NA  UNENE KWA  KUTUMIA  TIBA  ASILIA, TAFADHALI TEMBELEA:


7.   Matatizo  Katika  mfumo  wa  Ubongo

Uume  hauwezi  kusimama   bila  ya  kuwa  na ushirikiano  na  ubongo.  Ili mtu  uume  uweze kusimama, mtu  lazima  apate  wazo  la kufanya  tendo  la  ndoa  (UBONGO  UNA HUSIKA  HAPO ), akishapata  wazo, ubungo hupeleka  ishara  kwenye  mishipa  ya  fahamu iliyopo  katika  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo hupeleka  taarifa  kwenye  mishipa  ya  uume then  uume  usimama.   
 
Hivyo  basi  ili  mtu  aweze  kuwa  na uwezo  wa kusimamisha  uume  wake  ni lazima  kuwa  na  mawasiliano  mazuri  na  imara  kati  ya mishipa  ya  fahamu ( ubongo ), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo   na  mishipa  ya  kwenye    uume.  Bila ushirikiano  kati  ya  vitu  hivyo  vitatu, uume hauwezi  kusimama.

Magonjwa  yanayoweza  kuathiri  ushirikiano  kati  ya  mishipa  ya  ubongo  na  mishipa  ya  uume, yanaweza  kusababisha  kushindwa  kusimama  kwa  uume.

Magonjwa  hayo  ni  pamoja  na  kiharusi,kupoteza  kumbukumbu  (  Alzheimer ), multiple  sclerosis pamoja  na  ugonjwa  wa  Parkinson.

Ni  vyema  mgonjwa  akatibiwa  kwanza magonjwa  hayo  kabla  ya  kuanza  kutumia dawa  ya  nguvu  za  kiume.  Kufahamu  jinsi ya  kujitibu  magonjwa  tajwa  hapo  juu  kwa njia  asilia,tafadhali  tembelea

Mambo   mengine  yanayo  sababisha  ukosefu na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni pamoja  na  maumivu & majeraha  kwenye  uti wa  mgongo,  chango  la  kiume , ngiri  na matatizo  katika  homoni.

 VIASHRIA  VYA  MTU  MWENYE  TATIZO  LA UKOSEFU/UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA KIUME.

Mtu  mwenye  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za kiume  huwa  na  dalili  zifuatazo ;

1. Kushindwa  kabisa  kusimamisha  uume wake

2. Uume  kusimama  ukiwa  legelege

3. Kuwahi  kumaliza  tendo  la  ndoa

4. Mwanaume  kutokuwa  na uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  katika  baadhi ya  staili  ( Mara  nyingi   mwanaume huyu huwa  na  uwezo  wa  kufanya tendo  la  ndoa    staili  moja  tu ).  Hapa mwanaume  anakuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  staili  ya   “ missionary” pekee.  Ikibadilishwa   staili, mwanaume  anakuwa hana  tena  uwezo wa  kusimamisha  uume  wake  japo katika  hali  ya  u lege  lege

5. Uume  kutokuwa  na  uwezo  wa kusimama  wenyewe   bila kushikwashikwa  ama  kutomaswa kwa muda  mrefu.

6. Uume  kusinyaa  ukiwa  ndani  ya mwanamke.

7. Uume  kusinyaa, pindi  inapotokea activity  yoyote  ya  kiungo  ama  ogani nyingine  ya  mwanaume  wakati  wa tendo  la  ndoa. Kwa  mfano, wakati  wa tendo  la  ndoa, ikitokea  mwanaume amekohoa  au  kupiga  chafya, uume  nao unasinyaa.

8. Uume  kusinyaa  mara  tu  baada  ya kutolewa  ndani  ya  uke ( Kwa  mfano kama  unafanya  tendo  la  ndoa, halafu uume  ukatoka  nje, kitendo  cha kuushika  kuurudisha ndani, tayari  una sinyaa )

9. Kutokuwa  na  uwezo  wa  kurudia  tendo la  ndoa.

10.  Kupatwa  na  maumivu  wakati  wa tendo  la  ndoa.

VIASHIRIA  VYA  MWANAUME  ASIYE  NA TATIZO  LA UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA KIUME.

Mwanaume  asiye  na  tatizo  la  ukosefu  wa nguvu  za  kiume, huonyesha  ishara  zifuatazo ;

i.Uume  husimama  ukiwa  imara  kama msumari.

ii.Hukaa  kifuani  kwa  muda  mrefu  ( Wastani  ni  kati  ya  dakika  20  hadi  45 )

iii.Huweza  kurudia  tendo  la  ndoa  zaidi ya  mara  tatu  bila  misuli  ya  uume kuchoka.

iv.Huweza  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa staili  yoyote  ile

v.Uume  husimama  wenyewe  bila kushikwa  shikwa  wala  kuwa stimulated  kwa  namna  yoyote  ile

vi.Kwa  ufupi  anakuwa  na  uwezo  wa kufanya na  kukamilisha  tendo  la  ndoa kwa  uukamilifu  mkubwa.

TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  LA UKOSEFU/UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA KIUME.

Dawa  asilia  ya  JIKO   ni  dawa  asilia  inayo tibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.

                              MFUMO   WA  DAWA
Dozi  ya  dawa  ya  JIKO ni  mkusanyiko  wa dawa  nne  asilia  zenye  uwezo  mkubwa  sana katika kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

Dawa  hizi  zipo  katika  mfumo  wa  MIZIZI  na UNGA  UNGA.

JINSI   DOZI  YA  DAWA  YA  JIKO  INAVYO FANYA  KAZI.
Dozi  ya  dawa  ya  JIKO  inafanya  kazi zifuatazo  katika  mwili  wa  mwanadamu.

KAZI  INAYO  FANYWA  NA  DAWA  YA  JIKO .
Dawa  ya  JIKO  inasadia  katika  mambo makuu yafuatayo:
1.  Inasaidia   kuimarisha  mishipa  ya  uume  ulio legea  na  hivyo  kuufanya  uume  uwe  na uwezo  wa  kusimama  barabara  kama msumari  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

2. Inasaidia  kusafisha  mishipa  ya  kwenye uume  na  hivyo  kusaidia  katika  kuongeza kasi  ya  msukumo  wa  damu  kwenye mishipa  ya  kwenye  uume.

3. Huongeza  damu  mwilini

4. Husaidia  kuongeza  msukumo (pressure)  wa damu  kwenye  mishipa  ya  uume  na  hivyo kuufanya  uume  kuwa  na  nguvu  za  ajabu.

5. Huipa  misuli  ya  uume  uwezo  wa  kuziba  wa kuizuia  mishipa  ya  vena   kunyonya  damu kwenye  mishipa  ya  uume  wakati  wa  tendo la  ndoa  na  matokeo  yake  kukupa  uwezo wa  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  muda  mrefu

               ( Kuzuia  hali  ya  kufika  kileleni haraka  )

6. Husaidia  kurelax  mind  na  hivyo  kumfanya mtu  awe  na  uwezo  wa  kuconcentrate  wakati wa  tendo la  ndoa   bila  kuathiriwa  na msongo  wa  mawazo

7.  Hurejesha, kuimarisha  na  kuboresha ushirikiano  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  ya  kwenye  ubongo  (nerves), mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  mishipa  ya  kwenye  uume
8. Humfanya  mwanaume  awe  na  uwezo  wa kurudia  tendo  la  ndoa  mara  nyingi  zaidi bila  kuchoka.
9. Husaidia  kuongeza  hamu  ya  tendo  la  ndoa.10. Husaidia  kuurudisha  nje  uume  ulio ingia ndani.
11. Husaidia  kutibu  side effects  za  punyeto na  matumizi  ya  muda  mrefu  ya dawa  kali za  (za  kizungu ) za  kuongeza  nguvu  za kiume.

12. Husaidia  kutibu  chango  la  kiume.

13.Dawa  hii  huwasaidia  hata  wanawake wanao sumbuliwa  na  tatizo  la  ukosefu  wa hamu ya  tendo  la  ndoa.

BEI  YA  DAWA:  Dozi  ya  dawa  ya  JIKO inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI ELFU  THEMANINI  TU  (Tshs.80,000/=)

MAHALI  TUNAPOPATIKANA :
Dozi  ya  dawa  ya  JIKO, inatolewa  na  duka  la dawa  asilia  la  NEEMA 

HERBALIST  &   NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC. Tunapatikana jijini  DAR ES  SALAAM, katika  eneo  la UBUNGO     karibu  na  SHULE  YA MSINGI  UNGUNGO  NATIONAL  HOUSING  NYUMA  YA  JENGO  LA  UBUNGO  PLAZA.

Kwa  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu, tunatoa huduma  ya kuwapelekea  dawa  mahali  walipo ( DELIVERY )

Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  DAR  ES  SALAAM, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  mabasi, wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa kwa   njia  ya  boti  na  kwa  wateja  waliopo Ulaya, America  na  Arabuni, watatumiwa dawa  kwa  njia  ya  DHL  au POSTA.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA

0766  53  83  84.
Na  kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, endelea  kutembelea:

Snura Akubali Yaishe....Awaomba Radhi Watanzania Kwa Video ya Chura

$
0
0

Mwimbaji wa muziki wa Mduara nchini Snura Mushi ameomba radhi kwa umma wa Watanzania kwa kosa la kutengeneza, kuzindua na kuweka mitandaoni video ya udhalilishaji wa mwanamke na isiyozingatia maadili ya Kitanzania ya muziki unaoitwa "Chura".

Akizungumza na vyombo vya habari leo Snura amesema wakati wa utayarishaji wa video hiyo mvua ilinyesha hivyo madansa walilowana.

"Baada ya kuona wamelowa ilibidi tusitishe kupeleka katika televisheni na kuiacha you tube, Snura hajafungiwa bali video yangu ilisitishwa na mimi nilizuiwa kujihusisha na sanaa mpaka nijisajili," amesema Snura.

Meneja wa mwanamuziki huyo Hemedi Kavu amesema tayari walishakwenda Basata tangu jana kuomba usajili, leo wamepatiwa cheti cha usajili.

"Tumeshajisajili Basata, pia tayari tumeshaitoa video hiyo kwenye mtandao wa YouTube, tumeshalitekeleza na akaunti ya wimbo huo imeshafutwa na tunatarajia kuifanya video hiyo upya," amesema Hemedi Kavu.

Kikwete 'Agoma' Kumkabidhi Rais Magufuli Chama......Mwinyi,Mkapa,Malecela Kukutana kwa Dharura Kumjadili

$
0
0
Hali si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na mchakato unaoendelea wa kumkabidhi Rais Dk. John Magufuli uenyekiti wa chama hicho, kukumbwa na sintofahamu.

Taarifa kutoka ndani kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC), kilichofanyika juzi Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma, zimethibitisha kutokea mgawanyiko wa vigogo ndani ya chama hicho.

Hali hiyo imekuja baada ya kutokea kwa mvutano juu ya tarehe rasmi ya kufanyika kwa mkutano mkuu maalumu uliopangwa Juni mwaka huu, ambao pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete atakabidhi kijiti kwa Rais Magufuli.

Chanzo cha kuaminika ndani ya kikao hicho kilidokeza  kuwa, kabla kilifanyika kikao kidogo kilichokuwa na wajumbe wanne ambao pamoja na mambo mengine walijadili ajenda muhimu  ikiwamo ya kupanga tarehe kwa ajili ya mkutano huo.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kikao hicho kidogo kilishirikisha viongozi wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete, Rais Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Habari hizo zinaeleza kuwa, katika kikao hicho kidogo viongozi hao walikubaliana wakatangaze tarehe rasmi, na Rais Magufuli alikubali kukabidhiwa uenyekiti wa chama kama ulivyo utaratibu wa CCM  lakini baada ya kikao cha Kamati Kuu kuanza, Kikwete alikataa kuruhusu hoja hiyo ijadiliwe, hatua iliyozua mfarakano.

“Baada ya kumalizika kwa kikao kile viongozi hao wanne waliingia ndani ya kikao cha CC ambacho kilikuwa na ajenda kadhaa ikiwemo ya mkutano mkuu maalumu ambapo mwenyekiti alirusha na kutaka hoja ya tarehe isijadiliwe,” kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, ilipofika ajenda ya tatu ambayo iliwasilishwa na Katibu Mkuu, Kinana kuhusu kutangazwa kwa tarehe ya mkutano mkuu maalumu,  Kikwete aligoma isijadiliwe na badala yake aliahirisha kikao na kutoka nje.

Chanzo hicho kilisema, uamuzi wa Mwenyekiti Kikwete wa kuahirisha kikao ulijikita katika suala la gharama za mkutano ambazo zinakadiriwa kuwa ni zaidi ya Sh bilioni mbili, hivyo aliwataka wajumbe waahirishe kikao ili kutoa fursa ya kutafuta fedha.

Taarifa hizo zilieleza kuwa, kutokana na hali hiyo yaliibuka makundi mawili, moja linalomuunga mkono Kikwete na jingine linalopingana na hoja hiyo, likidai kuwa fedha si tatizo kwa chama hicho kwa kwani kina miradi, ruzuku na marafiki wengi.

“Wanaompinga mwenyekiti walishangazwa na hoja hiyo wakisema kuwa, suala la fedha ni la watendaji wa chama na si la mwenyekiti, kitendo ambacho wamekitafsiri kwamba mwenyekiti hana dhamira ya dhati ya kukabidhi chama kwa sasa,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliendelea kutoa taarifa kuwa, baada ya Kikwete kugoma kujadili tarehe alisimama mjumbe Jenista Mhagama, ambaye alipinga uamuzi huo, huku akisema suala hilo ni lazima lijadiliwe kwa kina na tarehe ya mkutano mkuu itangazwe.

“Kauli ya mwenyekiti inaonekana iliwaudhi baadhi ya wajumbe, lakini Jenista alizungumza vizuri sana na kumhoji mwenyekiti inakuaje hataki kusema lini utafanyika mkutano mkuu maalumu ili akabidhi chama.

“Maana suala la makabidhiano ni la utamaduni wa ndani ya CCM, Jenista alisema aliyekaa muda mrefu alikuwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere pekee lakini na yeye alikabidhi kwa mzee Mwinyi (Ali Hassan) na pia ilipofika wakati kama huu mzee Mwinyi naye alikabidhi kwa mzee Mkapa.

“Si hilo tu hata mzee Mkapa naye alikabidhi chama kwake (Jakaya Kikwete), sasa inakuwaje yeye leo hataki kufuata utaratibu huo ambao ni wa kawaida ndani ya chama?,” kilihoji chanzo hicho.

Chanzo kingine cha habari kilisema kuwa baada ya mwenyekiti huyo wa CCM taifa kuahirisha kikao hicho juzi, aliondoka na kurejea jijini Dar es Salaam kwa gari tofauti na ratiba iliyokuwa imepangwa.

“Ratiba ya chama ilikuwa baada ya kikao cha jana (juzi) mwenyekiti angelala Dodoma na badala yake alipoahirisha kikao kwa utata alipanda kwenye gari na kuondoa hali ya kuwa alitakiwa kurejea Dar leo (jana).

“Baada ya kikao hicho alitoka mzee Kinana akiwa amekasirika sana, tena huku akiwa amekunja sura, unajua siku zote mzee Kinana anaamini kwamba kile kilichokuwa kinapiganiwa na chama hivi sasa ndicho kinachotekelezwa na Rais Magufuli tena kwa vitendo tofauti na huko nyuma,” kilisema chanzo chetu.

Baraza la Wazee kukutana
Taarifa nyingine zinaarifu   kwamba, kutokana na hali hiyo Baraza la Wazee la CCM linaloundwa na viongozi wastaafu, linatarajiwa kukutana kati ya leo na kesho kwa lengo la kujadili hali hiyo ili kuondoa mtanziko huo uliojitokeza.

“Ninachotaka kukuambia katika kipindi cha siku mbili baraza la ushauri la wazee litakutana na kujadili hali hii na baada ya hapo watakwenda kwa mwenyekiti kumshauri juu ya uamuzi wake na autafakari kwa kina.

“Tunajua tunakwenda vizuri katika hili na hakuna kitakachoharibika na wazee wetu watamshauri vema mwenyekiti ili kupata mwafaka wa kudumu na mkutano mkuu utafanyika mwezi uliopangwa,” chanzo hicho kilisema.

Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM, linaongozwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (Mwenyekiti), Pius Msekwa (Katibu) na wajumbe ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu (Bara), John Malecela.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akutana Na Alex Msama Mkurugenzi Wa Msama Promotion

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma May 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa  Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma May 5, 2016. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mbunge wa Urambo, Magreth Sitta (katikati) kwenye viwanja vya  Bunge mjini Dodoma May 5, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Tundu Lissu Amshauri Rais Magufuli Atumbue Washauri wake

$
0
0

RAIS John Magufuli ametakiwa kutumbua majipu ya wanasheria walioshindwa kumshauri kufuata sheria ya kukasimisha mamlaka ya kiuwaziri kwa mawaziri walioteuliwa miezi sita iliyopita.
 
Tundu Lissu amesema hayo Dodoma wakati akitoa maoni kuhusu Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya wizara ya Sheria na Katiba kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, Bungeni mjini Dodoma.

“Kwa kuangalia mifano ya matangazo mbalimbali ambayo yametolewa na watangulizi wa Rais Magufuli tangu sheria ya utekelezwaji wa majukumu ya kiuwaziri ilipotungwa mwaka 1980, hata mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa kwanza angeweza kumtengenezea draft ya Tangazo la aina hiyo,” amesema Lissu.

Ameongeza “iweje watu wenye Shahada za uzamivu na uzamili katika sheria washindwe kufanya hivyo kwa karibu ya nusu mwaka tangu wateuliwe? Kama ni majipu ya kutumbuliwa na Magufuli, basi wasomi hawa wa sheria ni majipu na wanastahili kutumbuliwa.”

“Kwa sababu Rais Magufuli sio mwanasheria, amemteua Mwansheria Mkuu wa Serikali ambaye kwa mujibu wa ibara ya 59(3) ya katiba ndiye mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya kisheria,” amesema Lissu.

Kwa sababu hiyo, Rais Magufuli amemteua Dk. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Katiba na Sheria ili awe mshauri wake mkuu katika utekelezaji wa madaraka yake katika masuala ya kikatiba na kisheria kwa mujibu wa ibara 54(3).

“Kwa bahati nzuri Rais amewateua Dk Harrison Mwayembe, Dk Sifuni Mchome, na Amon Mpanju kuwa viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria ambao wote wasomi wabobezi wa sheria,” amesema.

Amehoji kuwa “Kambi ya Upinzani ianataka kupata majibu sahihi ni kwa nini wanasheria wabobezi wote hawa wameshindwa kumshauri Rais Magufuli kutoa tangazo la kukasimisha majukumu ya kiuwaziri kwa mawaziri mbalimbali aliowateua miezi sita iliyopita?”

Amesema kila mtu anafahamu kwamba Rais sio mwanasheria lakini kutokuwa mwanasheria haimaanishi kuwa juu ya sheria bali anapaswa kufuata sheria za nchi.

Lissu amesema, maana na athari ya kisheria ya kutokuwepo kwa tangazo la ukasimishaji wa majukumu ya kiuwaziri ni kubwa kutokana na kwamba mawaziri walioteuliwa wamefanya mambo makubwa mengi ambayo yalikuwa kinyume cha sheria.

Mmiliki wa Timu ya TP Mazembe Atangaza Kuwania Urais Jamhuri ya Demokrasia ya Congo

$
0
0

MOISE Katumbi Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga, Mkurugenzi wa klabu ya TP Mazembe na mfanyabiashara marufu nchini Kongo ametangaza kugombe urais wa Novemba mwaka huu.

Muungano wa vyama kadha vya upinzani umemuidhinisha Katumbi kuwa mgombea huku muungano huo ukiwa umegubikwa na hofu ya huenda Rais Joseph Kabila akaendelea kushikiri madaraka kinyume na katiba hiyo.

Katumbi amekuwa Gavana wa jimbo la Katanga tangu 2007 chini ya chama cha People’s Party for Reconstruction and Democracy(PPRD) na baadae akajiuzulu nafasi hiyo septemba 2015 ambapo mwaka huu 2016 amekuwa akitoa kauli zinazo mtaka Kabila kuheshimu katiba ya taifa hilo inayo mtaka kustaafu mwishoni mwa mwaka huu.

Licha ya Katumbi kumsaidia Kabila katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011 kwasasa anaonekana kuwa mbali na kiongozi huyo tangu kujiuzulu kwake 2015.

Hata hivyo mfanyabiashara huyo amekuwa na umaarufu mkubwa kutokana na kumiliki klabu ya TP Mazembe tangu 1997.

Uchaguzi huo unaonekana kuwa na mchuano mkali kwa kuwa Katumbi ana nguvu kubwa ya kiushindani kuanzia katika jimbo la katanga na katika ngazi ya taifa licha ya kukabiliwa na tuhuma za ubadhilifu wakati wauongozi wake.

Wachunguzi wa habari za siasa wamesema nchi hiyo inanyemelewa na machafuko iwapo Rais Kabila atataka kuendelea kuongoza taifa hilo kwa nguvu kama ilivyo fanyika Burundi na Rais Nkurunzinza.

Rais Magufuli Amuapisha Dkt. Asha-rose Migiro Kuwa Balozi Wa Tanzania Nchini Uingereza Katika Ikulu Ndogo Ya Chamwino

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Hafla ya kuapishwa kwa Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro imefanyika leo tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kallaghe ambaye amerudishwa nyumbani.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Dkt. Migiro ameahidi utumishi uliotukuka na kwamba atahakikisha uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Uingereza unaimarishwa zaidi, hususani katika kuvutia uwekezaji, biashara na utalii baina ya nchi hizi mbili.

Dkt. Migiro pia ametoa wito kwa watanzania waliopo hapa nchini na waishio Uingereza kuitumia ofisi hiyo ya ubalozi ipasavyo, ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali hasa za kiuchumi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
05 Mei, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.

Kambi Rasmi ya Upinzani Yapinga Tabia Ya Kutumbua Majipu Inayofanywa na Serikali ya Rais Magufuli

$
0
0
KAMBI Rasmi ya Upinzani imepinga tabia ya ‘kutumbua majipu’ inayofanywa na serikali ya Dk John Magufuli hivyo imewataka watumishi na watendaji wa umma waliosimamishwa au kufukuzwa kazi na mawaziri, kufungua mashauri Mahakama Kuu ya Tanzania ili kupinga kufukuzwa kwao na baadhi ya mawaziri.

Hayo yamesemwa leo katika hotuba ya maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.

Kwa mujibu wa hotuba hiyo, Lissu amesema kuwa baadhi ya mawaziri waliosimamisha na au kufukuza kazi watumishi wa umma kwa jina maarufu kutumbua majipu, walifanya maamuzi hayo kinyume cha sheria.

Ameongeza kuwa Mawaziri hao hawakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kwa sababu hawajakasimishwa mamlaka ya utekekelezaji wa majukumu yao kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 5(1) cha utekelezaji wa majukumu ya kiuwaziri.

Kutokana na hali hiyo kambi ya upinzani imesema watumishi wote ambao wametumbuliwa wana haki na uwezo wa kwenda mahakamani na kuomba mahakama kutengua utumbuaji wa majipu uliofanywa na mawaziri wasiokuwa na mamlaka hayo kinyume cha sheria.

“Kambi rasmi ya upinzani inaamini kuwa kwenda kwa watumishi hao mahakamani hakutawasaidia pekee kupata haki zao, bali pia kutakomez a vitendo vya kuendesha nchi kienyeji na bila kufuata sheria vinavyoelekea kushamiri chini ya utawala wa Rais John Pombe Magufuli,” amesema Lissu.

Mume Amuuwa Mke Wake Pamoja Na Mtoto Kwa Kuwachinja Na Kisu Wilayani Bagamoyo Mkoa Wa Pwani

$
0
0
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Frowin Peter Mbwale (26) mkazi wa Kawe Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuua kwa kuwachinja mkewe Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emanuel Frowin (3) kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Bonaventura Mushongi alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:30 jioni eneo la Zinga kata ya Dunda Tarafa ya Mwambao wilayani Bagamoyo.

Mushongi alisema kuwa katika hali isiyo kuwa ya kawaida juzi siku ya tukio mtuhumiwa akiwa na mwenzake alijulikana kwa jina la Rajabu Juma (20) Mkazi wa Makongo Jijini Dar es Salaam waliwaua watu hao kwenye vichaka vilivyopo kwenye eneo hilo la Kaole.

“Muda huo mtuhumiwa akiwa na mwenzake alimhadaa mke wake kuwa waende kwenye nyumba yao ambayo inaendelea kujengwa kwa lengo la kuitazama ambapo mke wake alikubali na kumbeba na mtoto wao na kwenda huko ambako aliwachinja shingoni,” alisema Kamanda Mushongi.

Alisema kuwa mtuhumiwa kumbe lengo lake halikuwa kuangalia ujenzi wa nyumba yao huko Kaole kumbe alikuwa na lengo lingine la kufanya unyama huo ambao aliutekeleza akiwa na rafiki yake huyo ambaye walishirikiana kumchinja mke na mtoto wake.
“Chanzo cha mauaji hayo ni mtuhumiwa huyo alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa ana uhusiano na mwanaume mwingine aitwaye Hamza mkazi wa Kawe Jijini Dar es Salaam na kusababisha mauaji hayo ya kusikitisha ambayo yamewaumiza watu wengi,” alisema Mushongi.

Alibainisha kuwa miili ya marehemu hao ilikutwa ikiwa imechinjwa na watu hao umbali wa mita 100 kutoka barabara ya magari itokayo Kaole kwenda eneo la Mbegani.

Aidha alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa majira ya saa 3:30 usiku baada ya wananchi Zinga kuwatilia mashaka walipokuwa wakijaribu kutaka kutoroka na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika, miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kusubiri ndugu kwa ajili ya mazishi.

Hatma ya Bosi wa Zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya na wenzake Kujulikana Kesho Mahakama Kuu

$
0
0
Rufani ya aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la Tanzania ambaye pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare imesikilizwa leo Mahakama kuu.

Upande wa utetezi umedai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu haikumaliza kusikiliza kesi hiyo lakini upande wa serikali umesema haki wanayo kwa sababu shitaka la nane limeshamalizika.

Mahakama Kuu imeeleza kuwa kesho ndio itatoa uamuzi wa Rufani hiyo kama isikilizwe mahakamani hapo au la. 

CCM Yakanusha Mwenyekiti wake Jakaya Kikwete 'Kugoma' Kukabidhi Uenyekiti kwa Rais Magufuli

$
0
0

Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinatoa taarifa potofu kuhusu mchakato wa  Mwenyekiti wa sasa wa CCM Dkt. Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti cha uongozi wa CCM kwa Rais John Pombe Magufuli kama ilivyo mila na desturi ya Chama Cha Mapinduzi. Yamekuwepo madai eti Mwenyekiti amekataa au anachelewesha kukabidhi kijiti.

Habari hiyo sio kweli kabisa na ni kinyume chake, kwani Dkt. Kikwete amekuwa akisisitiza kukabidhi madaraka mapema iwezekanavyo. 

Kwa ajili hiyo kwenye kikao cha Mei 3, 2016 alikataa kusiongezwe agenda nyingine ambazo zitalazimisha Mkutano Mkuu Maalum kuchelewa kufanyika kwa sababu ya kukamilisha maandalizi ya agenda hizo. Alisisitiza agenda iwe moja tu.

Dhamira ya kufanyika Mkutano Mkuu maalum mwezi Juni, 2016 iko pale pale. Kilichoelezwa kwenye kikao ni kutaka kukamilisha utaratibu wa kupata fedha za kugharamia mkutano huo. Taratibu zikikamilika tarehe itapangwa. Mipango ya kutafuta pesa inaendelea na ikikamilika tarehe itatangazwa.

Tunawataka wana-CCM wasihamanike wala kubabaishwa na taarifa za upotoshaji zinazofanywa na watu wenye nia mbaya na CCM. Hawa ni wale wale ambao wamekuwa wakiiombea mabaya CCM bila ya mafanikio.

Pia tunapenda kukanusha madai ati kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwatahadharisha Wajumbe wa Kamati Kuu kuhusu ukimya wa Ndugu Edward Lowassa. Hakuna wakati wowote kauli kama hiyo aliitoa. Ni uzushi mtupu. Jina la Ndugu Lowassa halikutajwa kabisa.

Aidha, tunapenda kukanusha madai ya kufanyika mkutano baina ya Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu wa CCM kuhusu uchaguzi wa Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM. 

Hapajawahi kufanyika mkutano wa aina hiyo siku yoyote na mahali popote. Hivyo madai ya kuwepo kwa tofauti baina ya Viongozi wakuu kuhusu nani achaguliwe kuwa Katibu wa Wabunge wa CCM hayana msingi wowote.

Kamati Kuu iliteua Wabunge wanne kugombea na kuwaachia Wabunge wa CCM kuamua. Kuhusisha Viongozi na hasa kuzua kuwepo kutokuelewana ni jambo la kusikitisha. Ni taarifa ya uongo yenye nia ovu kwa CCM na Viongozi wake.

Tunapenda kuwatahadharisha waandishi wa habari kuandika habari za ukweli. Waache kuzua mambo yenye kupandikiza chuki na mgawanyiko usiostahili kuwepo ndani ya CCM na kuyaeneza kwa watu. Waheshimu maadili ya kazi zao.

Napenda kuwahakikishia na kusisitiza kuwa hakuna mgogoro wa kukabidhi kijiti cha uenyekiti katika CCM na wala hautakuwepo.

Imetolewa na;
 
Ndugu Christopher Ole Sendeka  
MSEMAJI WA CCM                 
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
05/05/2016

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Awataka Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Wafuate Taratibu Na Sheria Zilizopo Vyuoni

$
0
0
SERIKALI imekanusha madai ya kutoa maelekezo kwa Uongozi wa vyuo vya elimu ya juu ya kuwanyanyasa wanafunzi wa vyuo hivyo wanaojihusisha na masuala ya siasa na badala yake imewataka wafuate kanuni na taratibu zilizowekwa sehemu husika.

Hata hivyo imesema itaendelea kuwahudumia Watanzania wote ikiwemo kutoa elimu kuanzia ngazi awali hadi elimu ya juu bila kujali ya itikadi za dini wala vyama vyao vya siasa.

Waziri Mkuu,Kassm Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Mei 5, 2016) wakati akijibu swali la papo kwa papo la Mheshimiwa Ester Matiko (Viti maalum Chadema) aliyetaka kujua kama Serikali imetoa maelekezo kwa uongozi wa vyuo vikuu kunyanyasa wanafunzi wanaojihusisha na masuala ya siasa.

“Nakanusha si kweli kwamba kuna maelekezo kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu na pia hakuna unyanyasaji wowote wa vyuo na Watanzania wote wanao uhuru wa kujiunga na vyama vyote wanavyovitaka, lakini kila eneo limeweka utaratibu wake hivyo wafuate taratibu na sheria  katika sehemu husika,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeondoa tozo ya asilimia 15 ya eneo la manunuzi ya vifungashio katika zao la korosho ili kumfanya mkulima kupata tija zaidi.

Akijibu swali la papo kwa papo la Mheshimiwa Katani Katani (Tandahimba-CUF) aliyetaka kujua ni lini tozo hiyo itaondolewa, Waziri Mkuu Majaliwa amesema tayari tozo hiyo imeshaondolewa na gharama hizo kwa sasa zipo katika mfuko wa wakfu ulioundwa na wadau wa zao hilo na unachangiwa na asilimia 65 ya tozo za korosho zinazouzwa nje.

Amesema mfuko huo wa wakfu unatakiwa kusimamia upatikanaji wa masoko ya zao la korosho, kununua pembejeo, kusimamia uboreshaji na upanuzi wa mashamba na kugharamia tatifi mbalimbali kwa ajili ya kupata ubora wa zao hilo.

Akijibu kuhusu suala la madai ya wakulima ambao korosho zao zimepotea ghallani, amesema mfumo wa uuzwaji wa zao hilo wa stakabadhi ghalani ni wa kiushirika na unasimamiwa na Mrajisi ni vema wakulima wakadai haki yao katika mikutano ya ushirika wao na kama hawaridhiki na majibu waende mahakamani ili kupata haki yao.

Amesema kwa sasa Serikali itahamishia nguvu zake katika kusimamia mazao mengine ya pamba, tumbaku na kahawa kama walivyofanya kwenye zao la korosho ili wakulima wa mazao hayo nao wapate tija.

Akijibu swali la Mheshimiwa Joseph Kekunda (Sikonge-CCM) aliyetaka kujua Serikali inampango gani wa kutatua migogoro ya wakulima na wakulima ,Waziri Mkuu amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha inakomesha migogoro hiyo ambazo ni pamoja na kupima maeneo na kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi.

Pia kuweka mipaka katika maeneo mapya na kutumia ranchi zilizopo kwa ajili ya wafugaji wakubwa na kwamba itatenga maeneo ya kilimo na kuyabainisha kwa wananchi ili kuepuka muingiliano uliopo hivi sasa

Mwanasheria Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni ‘Atumbuliwa’ kwa Kusababisha Hasara ya Mabilioni ya shilingi

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mheshimiwa Boniface Jacob ametangaza kumsimamsha kazi mwanasheria mkuu wa manispaa hiyo, Burton Mahenge na Mthamini wa Manispaa Einhard Chidaga.

Uamuzi huo umechukuliwa kwa kauli moja na madiwani wa manispaa hiyo kufuatia kikao chao mwishoni mwa mwezi uliopita.

Mheshimiwa Jacob amewaeleza waandishi wa habari kuwa wawili hao wameisababishia hasara kubwa, kupoteza mali, na kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.

Makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo ni:

1. Miradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa.
Manispaa ilipaswa kupata shilingi Milioni 900 kwa mwaka kwa uwekezaji huo. Lakini kutokana na mgogoro wa kimkataba Mapato hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi Bilioni 4.5 mpaka sasa.

2. Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za Magomeni Kota.
Manispaa  iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota, hivyo kuwaondoa wapangaji hao na kubomoa Nyumba hizo longer, wapangaji walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika Nyumba na kutoa madai ya kujengewa nyumba ama kulipwa fedha za fidia kutokana na Usimamizi hafifu wa shauri hili Mahakama liamuru Manispaa kukaa na kumalizana na wapangaji nje ya mahakama.

Halmashauri ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji kiasi cha shilingi 1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya mwaka na kumpatia kila mpangaji kiwanja. Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi 3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo kwa mchanganuo wa shilingi 695,520,000/= pango la mwaka na 2,576,000,000/= fidia ya viwanja 644.

3.Uwekezaji eneo la Coco Beach Oysterbay
Manispaa iliingia mkataba na Q - Consult Limited, Kampuni hiyo ilishindwa kutekelezwa mradi kwa wakati na Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-Consult Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo. 

Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini haikuwa na hatua zozote zilizochukuliwa na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa na Serikali Mwanasheria Mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa Mwanasheria alikuwa hajakata rufaa.

4.Mradi wa Ujenzi wa maduka Makumbusho (Eastern Capital Ltd)

Mkataba juu ya uendeshaji wa stendi haina manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1% ya makusanyo kwa mwaka sawa na Shilingi Milioni 4 tu kwa mwaka, wakati kabla ya uwekezaji, local standy Halmashauri ilikuwa ikipata Milioni 12 kwa mwezi.

5. Kubomolewa kwa ofisi ya Kata ya Msasani.
Mwananchi ajulikanaye kwa jina la Chacha aliingilia eneo la ofisi ya kata ya Msasani na baadae kuishtaki Manispaa. Usimamizi dhaifu wa shauri hilo kuisababishia mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna ufuatiliaji unaendeleaje. 

Hata hivyo kwa makusudi Bw. Chacha aliamua kuuza Kiwanda hili kwa Lake Oil CO. Limited wakati shauri halijaisha.

Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa shauri hilo, yangu upande wa pili ulikataa Jaji, tuna zaidi ya mwaka hatujapangiwa Jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.

6.Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment) Hill Road Oysterbay.
Mradi inafanyika kwa ubia na mwekezaji Texas Enterprise Company Ltd, mkataba uliingiwa mwaka 2009, na mradi umesimama kwa muda mrefu sasa.

Pamefanyika mabadiliko katika mkataba na mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa sababu ya kuchelewa kwa mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna makubaliano wa Financial proposal na Investment capital.

7. Ujenzi wa Nyumba za makazi (Apartment s) Kiwanda no. 314 Toure Drive.
Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited mkataba uliingiwa 2009.

Mabadiliko yamefanyika katika Mkataba bila idhini ya Halmashauri na kuisababishia mradi kuchelewa kukamilika, Manispaa inakosa manufaa ya mali yake kwa kuchelewa kukamilika mradi.

Halmashauri bado inaendelea kufuatilia miradi mwingine ambayo umeingia na haina manufaa kwa Halmashauri.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya May 6

Baba Aua Mtoto wa Kambo chumbani.......Yadaiwa ni Baada ya kumtuma mkewe Dukani kununua Dawa

$
0
0

Watu wawili wamekufa katika matukio mawili tofauti, akiwamo mtoto Mariam Haule (2) kwa kunyongwa na baba yake wa kambo baada ya kumtuma mama yake dukani kisha kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alisema jana kuwa, tukio hilo lilitokea Mei 2.

Issa alisema kuwa mtuhumiwa huyo mkazi wa Kijiji cha Usimba, Wilaya ya Kaliua mkoani humo kabla ya kufanya mauaji hayo, alimtuma mkewe, Kalunde Malugu kwenda dukani kununua dawa .

Alisema baada ya mkewe kwenda dukani, alipata mwanya wa kufanya mauaji hayo kisha kutokomea kusikojulikana.

“Tunawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano ili tuweze kumkamata mtuhumiwa afikishwe kwenye mkondo wa sheria,” alisema Issa.

Kamanda huyo alisema jeshi hilo litahakikisha mtuhumiwa huyo anakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

Mama wa mtoto huyo alisema alitumwa na mumewe dukani kununua dawa, lakini aliporudi alikuta mlango umefungwa na alipoingia ndani alibaini mtoto wake ameuawa.

Alisema hafahamu sababu za mauaji hayo na wala hakukuwa na malalamiko au madai yoyote kutoka kwa mumewe kuhusiana na mtoto huyo.

Katika tukio la pili; Mkazi wa Kijiji cha Rwamkoma wilayani Butiama, Magesa Machera (46) amekutwa ameuawa kwa kunyongwa baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi alisema tukio hilo lilitokea Mei 3, mwaka huu saa tisa usiku.

Alisema inadaiwa kuwa siku ya tukio hilo, mpenzi wake, Remmy Samwel (35) alitoka nje kwenda kujisaidia, lakini aliporudi alimkuta Machera akiwa chini amekufa.

Ng’anzi alisema mpenzi wake huyo ambaye ni mgeni katika kijiji hicho huwa na mazoea ya kwenda kumsalimia mara kwa mara na walikuwa wakinywa pombe za kienyeji. “Uchunguzi wa mauaji hayo unaendelea na polisi inamshikilia mpenzi wake,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Singida Asimamishwa Kazi Baada ya Kutoa Taarifa za Uongo Kuhusu Watumishi HEWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Mathew Mtigumwe.
***
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Singida, Simion Mumbee amesimamishwa kazi baada ya kudaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu watumishi hewa.

Katika taarifa hiyo, Mumbee anadai watumishi hewa 19 waliogundulika kwenye halmashauri hiyo hawajaisababishia hasara Serikali jambo linalodaiwa kuwa si kweli.

Akizungumza jana kwenye ufunguzi wa kikao cha maendeleo mkoani humo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe alisema anamsimamisha kazi mkurugenzi huyo ili kupisha uchunguzi.

“Nilipotuma tume kufuatilia suala la watumishi hewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida, ilibaini wapo na wameisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh125 milioni,” alisema Mtigumwe.

Alisema taarifa ya Mumbee ililenga kuidanganya Serikali. Mtigumwe alimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa, Dk Angela Lutambi kumuandikia barua ya kumsimamisha kazi mara moja.

Mtigumwe alisema hana nafasi ya kufanya kazi na watumishi wa aina ya Mumbee.

Wakati huo huo; Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amemsimamisha kazi Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Philbert Mtweve kwa tuhuma za kuwalipa mishahara watumishi hewa wanane na kuisababishia Serikali hasara ya Sh27 milioni.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images