Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Aongoza Kikao Cha Baraza La Mawaziri

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto) akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichofanyika leo katika ukumbi wa Tamisemi Mjini Dodoma,(wa pili kushoto) ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]

Mamlaka ya Bandari-TPA Yataja Sababu Iliyosababisha Mizigo Bandarini Dar es Salaam Kupungua

$
0
0
Siku moja baada ya serikali  kuziagiza mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi wa kina ili kubaini sababu za kupungua kwa shehena ya kontena zinazoingia nchini kupitia Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi jirani, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Injinia Alois Matei, leo amejitokeza mbele ya waandishi wa habari  ili kutaja chanzo cha mizigo kupungua bandarini.

Agizo la kuzitaka mamlaka ya Bandari-TPA, na Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kufanya uchambuzi  huo lilitolewa juzi Bungeni   April 30 na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dr. Philip Mpango .

Dr  Mpango alisema katika kipindi cha mwezi Oktoba mwaka jana na Machi mwaka huu kontena zilizopelekwa nchini Congo zilishuka kutoka 5,529 hadi 4,092, wakati yale yaliyokuwa yakipelekwa nchini Malawi yalishuka kutoka kontena 337 hadi 265, huku yale ya Zambia yakishuka kutoka 6,859 hadi kufikia 4,448, hivyo akaziagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA na Mamlaka ya Mapato-TRA, zichambue mwenendo huo ili kubaini chanzo cha kupungua.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Injinia Alois Matei amesema sababu kubwa  ya kupungua kwa makontena hayo imesababishwa  na kuyumba kwa  uchumi wa dunia  hasa China na kwingineko ambako mizigo inayopitia bandari ya Dar es Saam hutoka.

“Biashara za bandari dunia nzima zimeshuka.Kipindi hiki kuna mtikisiko kidogo kutokana na uchumi wa dunia kuyumba hasa China na kwingineko.

"Juzi tuliongea na wenzetu wa Singapore ambao walikuja hapa nchini, nchi yao ni moja ya nchi inayofanya biashara ya bandari kwa kiasi kikubwa. Wao pia walisema wamekumbana na tatizo hilo la kushuka kwa mizigo katika kipindi cha hii miezi mitatu." Amesema Matei

Katika hatua nyingine, Injinia  Matei  amesema serikali imepanga kutumia dola milioni 690 kuimarisha miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam ili kuongeza uwezo wa kupokea mizigo hadi kufikia tani milioni 38 ifikapo 2030 kutoka tani milioni 16 za mwaka 2014/15.

Akifafanua kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Matei amesema mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana na Benki ya Dunia,Trade Mark East Africa na DFID  na unatarajia kuanza   kabla ya mwisho wa mwaka 2016.

“Serikali,Benki ya Dunia,Trade Mark East Africa na DFID zimetiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa utekelezaji wa mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam” alisisitiza Matei.

Akizungumazia maeneo yatakayohusika katika maboresho hayo Injinia Matei amesema kuwa yatahusisha uboreshaji na uongezaji wa kina kufikia mita 14 katika gati namba 1 hadi 7 ili kuwezesha meli kubwa zaidi kutia nanga.

Maeneo mengine ni ujenzi wa gati mpya ya kushushia magari katika eneo la Gerezani Creek, uchimbaji ili kuongeza kina cha lango la kuingilia meli hadi kufikia mita 14 pamoja na sehemu ya kugeuzia meli.

Eneo jingine  ni uhamishaji wa gati la mafuta la Koj pamoja na bomba la mafuta katika eneo la ujenzi, uboreshaji wa mtandao wa reli ndani ya bandari na ujenzi wa sehemu ya kupakilia na kushushia mizigo.
Mhandisi Mkuu  wa TPA Bi Mary Mhayaya akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa Flow meter mpya ya Kigamboni ambao umeshakamilika na hivyo kuwezesha mafuta yote yanayoingia  nchini kupitia Bandari ya Dar es Salaam kupimwa na kujulikana kiasi halisi kilichoingizwa hapa nchini ili kuiwezesha Serikali kupata mapato stahiki ikiwemo kodi

Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein Aapishwa Rasmi Kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei, 2016 ameapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake ndani ya Baraza hilo.

Rais Shein ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, tukio ambalo limeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Viongozi wengine walioshuhudia tukio hilo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo mchana ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Mawaziri, uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI Mjini Dodoma.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
02 Mei, 2016

Mahakama ya Kisutu Yatoa Hati ya Kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob

$
0
0


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar imetoa hati ya kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob (Pichani)kutokana na kutofika mahakamani.

Meya huyo anakabiliwa na shitaka la kumshambulia  mwandishi wa Habari wa gazeti la Uhuru, Christopher Lissa na kumsababishia maumivu makali.

Kesi hiyo jana ililetwa mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa ajili ya usikilizwaji ambapo upande wa mashitaka ulikuwa na shahidi mmoja.

Wakili wa serikali Onolina Mushi alidai kwamba,kesi hiyo ililetwa kusikilizwa lakini mshitakiwa pamoja na wakili wake hawajafika mahakamani.

Kutokana na hali hiyo,aliiomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo pamoja na kupanga tarehe nyingine ya kuendelea kusikiliza shauri hilo.

Hakimu alikubali maombi hayo ikiwemo ya kutolewa hati ya kukamatwa kwa Meya huyo.Kesi hiyo iliahirishwa hadi Mei 23 mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji.

Katika kesi hiyo,Boniface anadaiwa kutenda kosa hilo  Septemba 11, mwaka jana, maeneo ya Kinondoni, Dar es Salaam, kipindi hicho akiwa na cheo cha Udiwani kata ya Ubungo.
Ilidaiwa kwamba,mshitakiwa huyo alimpiga Lissa kwa mateke na ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makali.

Shitaka la pili ilidaiwa kwamba ,mshitakiwa huyo katika tarehe hiyo kwa makusudi na kinyume cha sheria aliharibu kamera aina ya Nicon yenye thamani ya sh. milioni nane mali ya Kampuni ya Uhuru Publication Limited.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya May 3

Makonda Awasainisha Mikataba ya Kutafuta Watumishi HEWA Wakuu wote wa Idara Jiji la Dar es Salaam

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dares Salaam, Paul Makonda amewasainisha mkataba wakuu wote wa idara kusimamia na kuhakikisha hakuna mtumishi hewa atakayebainika kwenye idara zao.

Katika utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilotoa Machi 15 mwaka huu kwa wakuu wa mikoa kufuatilia na kubaini watumishi hewa, Mkoa wa Dar es Salaam umebainika kuwa na watumishi hewa 209 walioisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni mbili.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Makonda alisema hayupo tayari kuendelea kuona watumishi hewa wanaendelea kuwapo.

Alisema ni jukumu la kila mkuu wa idara kuhakikisha anasimamia eneo lake. Makonda alisema mkataba utaanza kazi rasmi baada ya siku saba.

Alisema baada ya hapo, atakayebainika kuwa na mtumishi hewa, atawajibika katika kulipa gharama zote za hasara alizoingiza kwa malipo yatakayofanyika.

“Nataka ndani ya siku saba hizi mpitie upya, mhakiki watumishi wenu baada ya hapo sitataka kusikia sababu yoyote lazima tufanye kazi kila mmoja kwa nafasi yake na msisubiri kila kitu msimamiwe,” alisema Makonda.

Pia aliwataka wakuu hao kuhakikisha kila mwisho wa wiki wanampelekea taarifa ya kila idara jinsi watakavyofanya kazi.
Wakuu wa Idara mbalimbali  wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wakisaini mkataba wa kutafuta watumishi hewa katika manispaa zao jijini Dar es Salaam, na atakaye shindwa kuwafichua baadae wakija kujulikana atawajibishwa yeye.
Wakuu wa Idara mbalimbali  wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wakiapa kiapo cha mkataba wa kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jijini la Dar es Salaam jana walipo apishwa na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo 'Ageuka Mbogo' Baada ya Kukabidhi Zawadi HEWA Mei Mosi

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo ameagiza ifikapo leo, wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo, wawe wamewapa zawadi zao watumishi bora wa mwaka huu baada ya kubaini walitoa zawadi hewa kwenye sherehe za Mei Mosi.

Ameagiza pia Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Pwani pamoja na mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha, nao kutoa zawadi ya fedha kwa wafanyakazi waliofanya vizuri kwenye vitengo vyao, badala ya kuwapa vyeti pekee.

Akizungumza juzi kwenye sherehe za Mei Mosi zilizofanyika kimkoa wilayani Mkuranga, Ndikilo alitoa siku tatu zinazoisha leo, taasisi hizo ziwe zimetekeleza agizo hilo. Alisema walichofanya ni masihara na yeye hayuko tayari kufanyiwa mzaha katika suala hilo, lililoandaliwa kwa muda mrefu.

“Katika risala ya Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Pwani walilalamika kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya waajiri kuwakopa zawadi za fedha watumishi wanaofanya vizuri kama motisha,” alisema.

Aliendelea,“Lakini kwa hali hii siwezi kukubaliana nalo, nawapa siku tatu muwe mmewalipa watumishi hao vinginevyo atakayeshindwa aje ofisini kwangu akutane na adhabu niliyoiandaa.”

Alisema hawezi kuvumilia watu wazembe wanaofanya dharau kwenye mambo mazito na kwamba atachukua hatua kali kwa halmashauri ambazo zitashindwa kutoa zawadi hizo kwani zingine zimetoa kwa nini wengine washindwe.

“Mimi siyo mtani wenu, wala si saizi yenu, haiwezekani mniite nije kutoa zawadi hewa, ndo maana hatua zikichukuliwa za kinidhamu mnasema mnaonewa, ikifika Jumatano muwe mmeshawapa zawadi zao wahusika, huu ni mzaha umepitiliza kiwango anayedhani tunatania aendelee aone,” alisema Ndikilo.

Licha ya ofisi ya Katibu Tawala pamoja na Shirika la Elimu Kibaha, taasisi nyingine zilizotakiwa kutekeleza agizo ni Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Halmashauri ya Mji Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji .

“Hatutaniani hapa,huu ni mzaha uliopitiliza kiwango,.ujumbe umefika.Namna hii mnakatisha tamaa watumishi kwa kudai kuwa mchakato bado ni jambo ambalo halijanifurahisha na nisingependa hali hii ijitokeze tena,” alisema Ndikilo.

Awali, akisoma risala ya Tucta, Amini Msambwa alisema kuwa wafanyakazi wana haki ya kutimiziwa haki zao za msingi na siyo lazima zipatikane kwa shinikizo la maandamano, migomo na hata kufungia nje waajiri.

Msambwa alisema kuwa moja ya changamoto ni baadhi ya wawekezaji wa nje na wa ndani, kuwanyima fursa wafanyakazi kujiunga na vyama vyao sehemu za kazi, ambayo ni haki yao ya kisheria na kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu ya Dhana ya Mabadiliko ilenge kuinua hali za wafanyakazi.

Aliyejifungua Watoto 3 Anaomba Asaidiwe kwani naye ni Mgonjwa wa Pumu

$
0
0
MKAZI wa Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Julietha Sokoine (24) amejifungua watoto wa watatu na ameiomba serikali, taasisi,mashirika na watu binafsi kumpatia msaada wa kifedha utakaomsaidia kuwatunza watoto hao.

Pia alisema msaada huo pia utamuwezesha kupata tiba ya ugonjwa wa pumu ambao umemsababisha kuvimba mwili wote.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, Sokoine ameiomba jamii kumsaidia kutokana na kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu ambao pia umesababisha kuwa na hali ngumu ya kimaisha ambayo inamfanya kushindwa kuwatunza vizuri watoto wake.

Alisema watoto hao, Daniel Sokoine,David Sokoine na Davis Sokoine walizaliwa kwa pamoja Machi 22, mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa Dodoma huku kati ya wawili wa wakiwa na uzito kilo mbili na nusu na wa mwisho kilo mbili.

“Hali yangu siyo mzuri kutokana na mimi mwenyewe kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu,ambapo wakati mwingine nalazimika kuwanywesha maziwa ya ngombe watoto hao pindi ninapozidiwa na ugonjwa huo”alisema .

Kwa upande wake baba wa watoto hao Sokoine Chipanta alisema pamoja na juhudi za kilimo hata hivyo mazao  yake yalinyauka na jua.

Alisema kutokana na hali hiyo analazimika kutafuta vibarua ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya kununua chakula pamoja na matunzo ya watoto hao.

Alisema kwa wale wote watakaoguswa na kuamua kumpa msaada wawasiliane naye kwa namba ya simu +255 652 744 510.

Mkuu Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Afungwa Mwaka Mmoja kwa Kosa la Kuajiri Watumishi Wenye Elimu ya Darasa 7

$
0
0

MKUU wa Chuo cha Uhasibu (IAA) Njiro mkoani Arusha, Profesa Johannes Monyo amehukumiwa kifungo cha nje kwa sharti la kutofanya kosa lolote ndani ya mwaka mmoja.

Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa iliyopita na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Devotha Msofe baada ya kujiridhisha kuwa Profesa Monyo alifanya makosa ya kuajiri watumishi wanane wenye elimu ya darasa la saba bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma.

Hakimu Msofe alisema Profesa Monyo akiwa Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Njiro, aliwaingiza watumishi wanane kwenye ajira ya kudumu bila ya kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu Mkuu Utumishi.

Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani kwa mashahidi 10 pamoja na vielelezo vinane vilivyotolewa mahakamani hapo na upande wa mshtakiwa kuwa na mashahidi wawili, mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka kuwa Profesa Monyo alifanya kosa hilo la kuajiri wafanyakazi hao wanane bila kufuata taratibu za kisheria.

“Mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa ulifanya kosa hili la kuajiri wafanyakazi wanane bila kufuata misingi na kanuni za utumishi wa umma hivyo mahakama hii inakutia hatiani kwa kukupa kifungo cha nje kwa sharti la kuutofanya kosa lolote katika kipindi cha mwaka mmoja,” alisema Hakimu Msofe.

Awali, Mwanasheria kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Adam Kilongozi alidai kuwa Juni, 2010 Profesa Monyo anatuhumiwa kuwapa ajira watumishi wanane ambao ni Pamela Maboko, Samson Mbarya, Mawazo Ndaro, Juma Nyarutu, Lilian Ngowi, Godfrey Mollel, Musa Maiki na Salim Shabani.

Kosa jingine ni Profesa Monyo kwa kutumia mamlaka yake vibaya, kuwaingiza watumishi hao wanane katika ajira, ilhali akijua elimu zao ni darasa la saba. Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo kutolewa, Profesa Monyo ameonesha kusudio la kukata rufaa kupitia kwa wakili wake, Severine Lawena.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa, mwandishi  alimhoji Mwanasheria wa Takukuru, Kilongozi, kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma au Kanuni zake inasemaje juu ya mtumishi anapohukumiwa akiwa bado yupo kazini, ambapo alisema kama mtuhumiwa amehukumiwa na akaonesha nia ya kukata rufaa, basi hukumu hiyo inaweza kufanya kazi au kutofanya kazi hadi hapo rufaa itakaposikilizwa.

Alisisitiza kuwa Takukuru wameshatuma nakala hiyo ya hukumu Tume ya Utumishi wa Umma, mwajiri wa Profesa Monyo, ili mamlaka husika zilifanyie kazi suala hilo lakini pia ni lazima mwajiri wake naye ajiridhishe na hukumu hiyo.

Mlinzi wa Wizara ya Ujenzi atupwa jela miaka mitatu Kwa Kosa la Kushindwa Kuzuia Wizi wa Kiti na Kompyuta

$
0
0

Mkazi wa Temeke Ramadhani Kusena (48) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kushindwa kuzuia wizi usitokee katika Wizara ya Ujenzi, wakati akiwa mlinzi wa eneo hilo. 

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Catherine Kioja alisema jana kuwa mahakama imemtia hatiani mshtakiwa huyo baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wanne. 

Mbali na kifungo hicho, mahakama pia imemuamuru mshtakiwa huyo kulipa fidia ya Sh500,000 kwa kushindwa kuzuia wizi wa kiti na kompyuta katika chumba namba 303 kilichopo katika ofisi za wizara hiyo. 

Hakimu Kioja alisema mshtakiwa huyo anaweza kukata rufaa kama ataona hajatendewa haki na mahakama hiyo katika hukumu hiyo. 

Awali, kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Grace Mwanga uliomba mahakama kutoa adhabu kulingana na shtaka hilo. Hata hivyo, Mahakama ilimpa nafasi mshtakiwa ajitete kwanini asipewe adhabu. 

Akijitetea, mshtakiwa huyo aliomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa anategemewa na familia. Wakili Mwanga alisema mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 7, 2014 katika ofisi za wizara hiyo Mtaa wa Samora Dar es Salaam. 

Wafanyakazi wa Kiwanda cha Urafiki na Kampuni ya Vinywaji ya Pepsi (SBC) Wagoma.......Mabomu Yatumika Kuwatuliza, Polisi Apigwa Jiwe Kichwani

$
0
0

Miezi michache baada ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kukwaruzana na Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea chanzo kikiwa ni mgogoro wa Kiwanda cha Urafiki na kupelekana mahakamani, jana mabomu yalirindima kiwandani hapo wakati wafanyakazi wakiendeleza madai ya malimbikizo ya mishahara. 

Awali, viongozi hao walifikishana mahakamani baada ya Kubenea kudaiwa kumtukana Makonda ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wakitatua moja ya migomo ya wafanyakazi hao. 

Kubenea alihukumiwa kifungo cha miezi mitatu nje na kutotakiwa kutoa lugha ya matusi kama alivyofanya kwa mkuu huyo, lakini madai ya wafanyakazi wa Urafiki bado hayajapata suluhu. 

Katika vurugu hizo zilizoanza jana asubuhi askari mmoja alipigwa jiwe kichwani huku wafanyakazi watatu wakizirai. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alisema vurugu hizo zilianza baada ya wafanyakazi hao kutoelewana. 

“Waliokuwa tayari kuendelea na kazi walizuiwa na wenzao,” alisema Fuime. 

Akizungumzia kuhusu askari kupigwa jiwe baada ya kuwasili eneo la tukio huku wafanyakazi watatu wakizirai alisema: “Wamepelekwa hospitali na tunawashikilia watu wanne.”

Mgomo huo ulianza mwishoni mwa mwaka jana wakati wafanyakazi hao wakidai stahiki ya mishahara na posho za usafiri, chakula na pango la nyumba. 

Hukumu ya madai iliyotolewa Februari mwaka jana na Mahakama ya Kazi (CMA) iliagiza wafanyakazi hao zaidi ya 800 walipwe Sh4.5 bilioni kuanzia Aprili 30. 

Jana wakati wakifuatilia utekelezaji wa hukumu hiyo, vurugu zilitokea huku magari zaidi ya 10 yaliyosheheni askari yakiwasili eneo la kiwanda hicho na kufanikiwa kutuliza vurugu hizo. 

Meneja Rasilimali Watu wa kiwanda hicho, Dickson Machilika alisema uongozi upo tayari kuwalipa stahiki zao, lakini umepanga kulipa kwa awamu. 

Alisema uzalishaji wa kiwanda umeshuka na hata wafanyakazi wanaingia mara moja tofauti na awali kulipokuwa na awamu tatu. 

Wakati huohuo, Wafanyakazi wa Kampuni ya Vinywaji ya Pepsi (SBC) jana waligoma wakishinikiza uongozi wao kuwapa mikataba ya kuongezewa mishahara. 

Katika mgomo huo, polisi walilazimika kufyatua mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyakazi hao ambao walikuwa mbele ya lango la kampuni hiyo wakiimba. 

Wafanyakazi hao waliilaumu kampuni hiyo kwa kumpa wakala jukumu la kuajiri na kulipa mishahara yao jambo linalosababisha ucheleweshwaji wa malipo. 

“Wakala hatumtaki na kwa nini kampuni kubwa kama hii badala ya kuajiri watu, wanawapa mawakala na kusababisha sisi kutolipwa haki zetu,” alisema Dunia Shabani.

Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Irenus Mushongi alisema anashangaa kitendo hicho kwani walifanya mazungumzo na wafanyakazi hao na walikuwa katika hatua za kutafuta ufumbuzi.

 “Mipangilio ipo tena kwa mujibu wa sheria nashangaa kabla ya makubaliano wamelianzisha,” alisema. 

Ofisa Kazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi na Ajira, Omari Sama alisema madai hayo yalifikishwa wizarani na kujadiliana na pande zote na kutoa muda kwa mwajiri kutekeleza madai yao ndani ya siku 30.

Kanisa Katoliki Lachomwa Moto Karagwe

$
0
0
Picha si ya tukio halisi

Watu wasiofahamika wamechoma moto Kanisa Katoliki Kigango cha Nyarwele, Parokia ya Kimiza, Jimbo la Kayanga wilayani Karagwe, Mkoa wa Kagera.

Katika tukio hilo la jana usiku, mali zote zilizokuwamo ndani ambazo thamani yake haijajulikana ziliteketea.

Shuhuda wa tukio hilo, Paulina Nkuba (67) alisema alifika eneo la tukio asubuhi baada ya kupewa taarifa na mjukuu wake anayesoma Shule ya Msingi Kimiza.

Alisema baada ya kufika katika eneo la tukio alipiga yowe kuomba msaada na alipoona watu hawatokei, alitoa taarifa kwa uongozi wa kitongoji ndipo waliwajulisha wananchi na kuanza kukusanyika. 

Paroko wa Parokia ya Kimiza, Padre Fortunatus Bijura alisema kitendo hicho ni cha kuhuzunisha na kusisitiza hawataacha kusali kwa kuwa hata chini ya mti watafanya ibada.

Askofu wa jimbo hilo, Almachius Vicent Rweyongeza aliwataka waumini wasilipize kisasi hata kama wakimjua aliyechoma kanisa hilo.

Mwenyekiti wa kamati ya kanisa hilo, Sabas Kafuba alivitaja baadhi ya vitu vilivyoteketea kuwa ni jengo, nyaraka, meza, viti, kinanda na jenereta.

Akizungumza na wananchi, ofisa upelelezi wa Wilaya ya Karagwe aliyejitambulisha kwa jina la Masoud aliwataka kuunda vikundi vya ulinzi na kutoa taarifa za kukomesha uhalifu huo.

Hatua Mbili Muhimu Katika Kusimama Kwa Uume na Tiba ya Ukosefu wa Nguvu za Kiume

$
0
0
Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani.

Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ?
Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu. Dalili  kuu  za  ukosefu  & upungufu  wa  nguvu  za  kiume  ni  kufika  kileleni  haraka  na kushindwa  kurudia  tendo  zaidi ya  mara moja.

HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME
Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo :

Hatua  ya  kwanza, ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari.

Na  hatua  ya  pili  ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION

JINSI   HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA.

1. HATUA   YA  KWANZA:

DAMU  KUTIRIRIKA  KWA  KASI KUINGIA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME  NA  KUUFANYA  UUME  KUSIMAMA  NA  KUWA  MGUMU.

Unapopata  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  fahamu iliyopo  kwenye  ubongo,  hupeleka  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo, ambayo  nayo  hupeleka  taarifa  hadi  kwenye  mishipa  ya  uume. Taarifa  inapofika  kwenye  mishipa  ya  uume  huifanya  mishipa hiyo  ku-relax  na  hatimaye   kufanya  mishipa  ya  ateri  kufunguka  na  kutanuka. Mishipa  ya  ateri  inapo  tanuka  na  kufunguka, huruhusu  damu  kuingia  kwa  kasi  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  huume  kusimama.

Ni  muhimu  kujua  kuwa, mishipa  ya  uume  inapo relax  hupelekea  kuisukuma na  hatimaye  kuiziba  mishipa  ya  vena  iliyo  karibu  na  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuiondolea  uwezo  wa  kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  sehemu  nyingine  za  mwili.

N.B: Kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kunyonya  damu  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyingine  za  mwili.  Au  kwa  lugha  nyingine  unaweza  kusema, kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  kwenye  mishipa  ya  uume.

2. HATUA   YA  PILI :

DAMU  KUENDELEA  KUHIFADHIWA  KATIKA  UUME  WAKATI  UUME  UKIWA  UMESIMAMA  NA  HIVYO  KUUFANYA  UUME  UENDELEE  KUDUMU  KATIKA  TENDO LA NDOA   KWA  MUDA  MREFU.

Uume  ulio  simama, ili  uendelee  kusimama, ni  lazima  mishipa  ya  vena  isiwe  na  uwezo   wa  kunyonya  damu  kutoka  katika  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyinginezo  za  mwili. .

Mishipa  ya  Vena  ndio  inayo  husika  na  kunyonya  damu  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume na  kupeleka  sehemu  nyingine  za  mwili.  Ili  uume  uendelee  kusimama  lazima  mishipa  hii  ya  vena  iwe imezibwa. Ili  iweze  kuzibwa   ni  lazima  misuli  laini  ya  kwenye  uume  iwe - ime  relax na  hivyo  kuifanya  mishipa  ya  vena  kushindwa  ku  nyonya  damu  kutoka  kwenye  uume.

Endapo  mishipa  ya  vena  itazibuka , basi  itanyonya  na  kutoa  damu yote  kutoka  kwenye  mishipa  ya  uume uliosimama  na  kuipeleka  sehemu  nyinginezo  za  mwili  na  hatimaye  uume  huo ulio simama  na  utasinyaa  mara  moja.

TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  LA  UKOSEFU NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME

Ili  kufahamu  kuhusu  tiba  asilia  ya  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  vyema  kwanza  ukajua  chanzo   pamoja  na  dalili  za ukosefu  wa  nguvu  za  kiume na jinsi  ambavyo  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  hutokea.

Kufahamu  kuhusu chanzo  cha tatizo  la ukosefu  &   upungufu  wa  nguvu  za  kiume,  pamoja  na dalili  za  ukosefu  &  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  na  jinsi  tatizo  la ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  linavyo  tokea, tafadhali  tembelea :


Tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume  hutibiwa  na  kuponyeshwa  kabisa  kwa  kutumia  dawa  asilia iitwayo  JIKO.    JIKO  hutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.

JINSI   DAWA ASILIA   YA   JIKO  INAVYO  FANYA  KAZI
Dawa  ya JIKO   hutibu  na  kurekebisha  hitilafu  zote zilizopo  katika  mfumo  wa  nguvu  za  kiume . Kufahamu  zaidi  kuhusu  jinsi dawa  ya  JIKO  inavyo  tibu  tatizo  la  ukosefu   na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, tafadhali  tembelea :


BEI  YA  DAWA:  Dozi  ya  dawa  ya  JIKO  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU  (Tshs.80,000/=)

MAHALI   TUNAPOPATIKANA :
Dozi  ya  dawa  ya  JIKO, inatolewa  na  duka  la  dawa  asilia  la  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC. Tunapatikana  jijini  DAR ES  SALAAM, katika  eneo  la  UBUNGO  nyuma  ya jengo  la  UBUNGO  PLAZA  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu, tunatoa  huduma  ya kuwapelekea  dawa  mahali  walipo  ( DELIVERY )

Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  DAR  ES  SALAAM, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  mabasi, wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa   njia  ya  boti  na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  DHL  au POSTA.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA :0766  53  83  84.

Na  kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, endelea  kutembelea:

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Awaasa Wanafunzi Kuhusu Ajira

$
0
0

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, amewasaa wanafunzi kuchagua kozi zitakazowapatia ajira wanapo hitimu masomo yao.

Akizungumza katika mahafali ya 10 ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Baobab, wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani juzi, Kikwete alisema wimbi kubwa la vijana wasio na ajira limechangiwa na uchaguzi mbaya wa kozi ambazo haziendani na soko la ajira la sasa.
 
“Nawasaa kuwa makini katika kuchagua kozi zinazoendana na soko la jira ndani na nje ya nchi ili muweze kuajiriwa na kujiajiri pindi mnapohitimu,” alisema.
 
Alisema zipo fursa mbalimbali ikiwamo za kibiashara katika soko la Afrika Mashariki, Afrika na Dunia, ambazo kama wahitimu watasoma kozi zinazoendana na fursa zilizopo watajikomboa na changamoto ya ukosefu wa ajira.
 
“Nimetembea nchi nyingi duniani na kuona fursa mbalimbali, ni vyema basi vijana wakawa wanafanya maamuzi sahihi ili waweze kutumia fursa hizo.” 
 
“Vijana wengi wamekuwa wakichagua michepuo ya kozi ambazo haziendani na mahitaji ya soko la ajira na kuwafanya kushindwa kupata nafasi katika soko la ajira,” aliongeza kusema.
 
Aidha, Kikwete alizitaka shule na vyuo nchini kufundisha lugha kubwa duniani kama Kichina na Kifaransa ili kuwaongezea uwezo wahitimu kufanya kazi katika maeneo mbalimbali dunia.
 
Aidha, alizishauri shule kutoa mafunzo ya ujasiriliamali ili kupanua fikra za vijana na waweze kujitengenezea ajira wanapohitimu.
 
Naye Mkurugenzi wa Shule ya Baobab alisema shule hiyo imefanikiwa kutoa wahitimu 774 kwa kipindi cha miaka 10, ambao asilimia 95 walipata ufaulu wa kujiunga na vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Alitaja idadi ya wahitimu wa mwaka huu kuwa ni 244, wasichana 176 na wavulana 68.

Umoja wa Ulaya Wapongeza Hatua Zinazochukuliwa na Rais Magufuli

$
0
0

Umoja wa Mataifa ya Ulaya umepongeza hatua zinazochukuliwa na rais Dkt. John Magufuli,katika kudhibiti vitendo vya rushwa nchini na kuahidi kutoa misaada zaidi ili kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi.

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Mwanza na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguezi,pamoja na Mkuu wa idara ya siasa na mawasiliano wa umoja wa ulaya walipomtembelea Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.

Pamoja na mambo mengine Umoja huo wa Ulaya umetembelea mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji ambapo umeiomba serikali ya Tanzania kuondoa urasimu katika upatikanaji wa vibali vya uwekezaji.

Licha ya Kupongeza hatua hizo za rais John Magufuli katika kupambana na rushwa Ujumbe huo wa Umoja wa ulaya umetaka serikali iweze kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza katika kuchangamkia fursa za miradi inayofadhiliwa na Umoja huo lakini pia ni njia moja wapo ya kudumisha mahusiano ya Kimataifa.

Ujumbe huo umetembelea baadhi ya miradi wanayoifadhili mkoani humo ikiwemo mradi wa maji safi na usafi wa mazingira Jijini Mwanza pamoja na mradi wa kuongeza thamani ya ngozi katika chuo cha Teknolojia DIT tawi la Mwanza.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Atoa ONYO Kali kwa Wanaume Wanaowapa Mimba Wanafunzi

$
0
0

Serikali imewaagiza Maafisa maendeleo ya Jamii na maafisa ustawi wa Jamii wa wilaya,kata na mikoa nchini kuwafatilia wanaume wanaowapa ujauzito watoto wa shule na kuwafikisha Mahakamani.

Akizungumza leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, amesema serikali haitamvumilia mwanaume yoyote anaempa mwanafunzi ujauzito.

Mhe. Ummy amesema kuwa serikali ya awamu ya tano itawachukulia hatua wanaume wote na hakutakuwa na huruma juu ya hilo huku akisisitiza wanawake ambao si wanafunzi ni wengi mitaani.

Hapo awali Akijibu Swali la Mbunge wa Ileje, Mhe. Janeth Mbene, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo amesema kuwa tatizo la watoto kupewa ujauzito nchini linatokana na vishawishi wanavyokutana wakiwa njiani wakati wanakwenda mashuleni.

Rais Magufuli Ashiriki Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Mkoani Dodoma

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa.


Mwenyekit wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kushoto ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.

PICHA NA IKULU

Kesi Kitilya na Wenzake Yaahirishwa tena mpaka Mei 18

$
0
0

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam inatarajia kuanza kusikiliza rufaa ya kupinga kufutwa shtaka la nane katika kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wawili, mei 5, mwaka huu.
 
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache baada ya mahakama hiyo kuitisha jalada halisi la kesi hiyo la kujipatia dola milioni 6 za marekani, aprili 29.

Mbali na Kitilya, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa mrembo wa  Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na mwanasheria wa benki ya Stanbic, Sioi Solomon.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro aliieleza mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, mbele ya hakimu Mkuu Mkazi  Mh. Emmillius Mchauru, kwamba shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, hakimu Mchauru alisema alitarajia kutoa mwenendo wa kesi hiyo, lakini amepokea taarifa kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kwamba washtakiwa wanatakiwa kufika mahakamani huko.

Hakimu Mchauru alisema kutokana na taarifa hiyo aliyopokea kutoka kwa viongozi wake wa juu, washtakiwa na mawakili wao hawana budi kufika mahakama kuu ili kujua nini kitajiri.

Mawakili wanaowatetea washtakiwa hao ni Dk.Lingo Tenga, Majura Magafu na Alex Mgongolwa.

Hakimu Mchauru aliahirisha kesi hiyo hadi mei 18, ambapo alisema washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu kama taratibu za kisheria zinavyosema, licha ya kuitwa mahakama kuu.

Hata hivyo, baada ya kufika mahakama kuu, Jaji Mfawidhi Moses Mzuna alisema suala ambalo lipo mbele yake linahusu taarifa ya pendekezo la kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufutwa shtaka la nane la utakatishaji fedha lililowasilishwa na mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

Shtaka hilo la utakatishaji fedha inadaiwa watuhumiwa wote kwa pamoja  kati ya march 2013 na septemba 2015 Jijini Dar es Salaam walitakatisha fedha dola za kimarekani milioni sita kwa kuzihamisha kutoka katika akaunti ya kampuni ya Egma  zilizokuwa zimefunguliwa benki ya Stanbic tawi la Tanzania kwa namba mbalimbali.

Jaji Mzuna alisema kutokana na uwepo wa taarifa hiyo mezani kwake, pande zote mbili zinapaswa kufika siku ya alhamis mei 5, mwaka huu kwa ajili ya kuanza usikilizwaji wa rufani.

Pia alisema licha ya kupanga tarehe hiyo kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, endapo kama upande wa Jamhuri haujawasilisha hati ya rufani katika muda uliotolewa, basi itatolewa taarifa ya mwenendo wa kesi hiyo.

Baada ya kutoa maelezo hayo, wakili Magafu aliieleza mahakama kwamba wanakubaliana na hatua hiyo, licha ya kuwa upande wa Jamhuri haukufika mahakamani hapo.

Uamuzi wa kufutwa kwa shtaka la nane la utakatishaji fedha, ulitolewa na hakimu Mchauru baada ya kukubaliana na hoja za mawakili wa utetezi  kwamba halijakidhi vigezo vya kisheria.

Hata hivyo, uamuzi huo ulipingwa baada ya Jamhuri kupitia wakili mkuu wa serikali, Oswald Tibabyekomya kudai kuwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP) amewasilisha hati ya kusudio la mapendekezo ya kukata rufaa

Sumaye Ampiga Kijembe Rais Magufuli

$
0
0

FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu ameeleza kushangazwa na Serikali ya Rais John Magufuli kupenda kusifiwa zaidi na kuchukia kukosolewa

Sumaye bila kumtaja jina Rais Magufuli ameleza kushangazwa na hatua ya serikali kuminya uhuru wa habari na kwamba, kufanya hivyo kunalenga kuficha madudu yanayofanywa na watendaji wake.

“Wapowatawala ambao hawapendi kusemwa lakini wanapenda sana kusifiwa. Kiongozi mwenye tabia ya udikteta hataki kusikia kingine zaidi ya sifa zake tu.

“Huyo ni mtu hatari na katika nchi ya namna hiyo hakuna uhuru wa habari wala uhuru wa kutoa maoni kwa woga wa kupotezwa kusikojulikana,” amesema Sumaye.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habri za Siasa (TAPOREA), Sumaye amesema, serikali inakiuka Katiba ya nchi.

Amesema, serikali yoyote inayopambana na vyombo vya habari na kuminya uhuru wa kufanya kazi zao huwa ina tatizo kwa upande wa wanaotawala.

Akitolea mfano wa hatua ya serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya bunge Sumaye amesema, kwa kufanya hivyo serikali imevunja Katiba.

“Unapoondoa matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya Bunge, kwanza ni kuvunja katiba. Ibara ya 18 (d) ya Katiba inasema, kila mtu ana haki ya kupewa taarifa wakati wote.

“Kwa kuzuia Bunge kuoneshwa ‘live’ (moja kwa moja) wewe serikali unataka kutoa taarifa ya Bunge kwa wakati unaoutaka na kwa taarifa unayoitaka wewe,” ameeleza Sumaye.

Kuhusu sababu iliyotolewa kwamba, matangazo hayo yanatumia gharama ya Sh. 4 bilioni amesema haina mashiko.

Sumaye amesema, hata kama matangazo hayo yatarushwa na ofisi za bunge bado, gharama zitaongezeka zaidi kwa sababu Bunge litahitaji kununua mitambo pamoja na kuajiri wafanyakazi wake.

Sumaye amesema, serikali yenye demokrasia ya kweli lazima ikubali wananchi wake kutoa maoni.

“Serikali yoyote yenye utawala bora, ingependa mambo yake inayoyafanya kwa ajili ya wananchi wake mambo hayo yajulikane kwa wananchi hao.

“Ukiona serikali inaficha mambo yake lazima kuna mambo wanayoyafanya ambayo hayafai na wasingependa jamii ijue,” amesema Sumaye.

George Maziku, Mkurugenzi Mtendaji wa TAPOREA amezungumzia ripoti ya hali ya uhuru wa waandishi wa habari na uhuru wa vyombo vya habari kimataifa, iliyotolewa na Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka lenye Makao Makuu yake nchini Ufaransa haipendezi.

Amesema, ripoti hiyo inaonesha kuwa, katika miaka 10 iliyopita zaidi ya waandishi wa habari 800 kutoka mataifa mabalimbali duniani wameuawa wakiwa wanatekeleza kazi zao.

“Kitisho kingine kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini ni utamaduni mpya ulioasisiwa na kuimarishwa na watawala wa sasa na kuvishinikiza vyombo vya habari kutomkosoa Rais John Magufuli na serikali yake.

“Matokeo yake, vyombo vingi vya habari nchini vimelazimika kuandika habari za kumfurahisha Rais Magufuli,” amesema Maziku.

Polisi wawili watuhumiwa kuomba rushwa milioni 7.2/

$
0
0

POLISI mkoani Rukwa inawashikilia askari wake wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Nkasi, wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh milioni 7.2 wamsaidie mtuhumiwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Rukwa, Leonce Rwegasira alitaja askari hao kuwa ni Konstebo Filbert Ruhemeja na Konstebo Bahati Sengerema, ambao walikuwa wakifanya kazi katika Kituo cha Polisi mjini Namanyere wilayani Nkasi.

Alisema polisi inawafanyia uchunguzi wa kina askari wake wawili, wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kuomba rushwa ya Sh milioni 7.2 na iwapo watabainika halitasita kuwatimua na kuwafikisha mahakamani.

Rwegasira alisema hayo jana ofisini kwake wakati anazungumza na mwandishi wetu alipotaka kujua ni hatua gani zilizochukuliwa dhidi ya polisi hao kutokana na kuwepo kwa tuhuma hizo za kuomba na kupokea rushwa.

Alisema askari hao wawili wa polisi, wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya fedha kutoka kwa mtu mmoja  ili wamsaidie katika shitaka linalomkabili.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images