Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tanzania Yapata Dili mpya Uganda La Kujenga Bomba Jingine la Gesi

$
0
0
Baada ya Tanzania na Uganda kukubaliana mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta utekelezwe kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, matumaini mengine mapya yameonekana kutokana na Uganda kuweka wazi azma yake ya kujenga bomba jingine la gesi katika njia hiyohiyo kwa ajili ya biashara na Tanzania. 

Licha ya kutofafanua kwa kina juu ya mpango huo, Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Serikali ya Uganda na Tanzania bado ziko kwenye majadiliano ya kuanzisha mradi mwingine wa bomba hilo la gesi. 

“Ni mpango mpya bado tunajadiliana, kuna uwezekano mkubwa wa kujenga bomba hilo lakini utekelezaji wake utaanza baada ya mradi huo wa bomba la mafuta wa sasa kukamilika,” alisema. 

Waziri Muloni aliyekuwa ameongozana na mwenyeji wake Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alitoa kauli hiyo katika mkutano wa kwanza wa jopo la watalaamu wa sekta mbalimbali waliokutana kwa mara ya kwanza kuandaa mpango wa utekelezaji wa mradi huo. 

Mkutano huo unafanyika ikiwa ni siku sita tangu azungumze na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini akitokea Kampala ambako Rais wa Uganda, Yoweri Museveni alitangaza kuwa bomba hilo la mafuta ghafi kutoka Hoima, Ziwa Albert litapita katika ardhi ya Tanzania kwenda Bandari ya Tanga. 

Waziri Muhongo alisema mbali na bomba hilo, nchi nyingine za Afrika Mashariki pia zimekubali kununua gesi ya Tanzania.

Kuhusu mradi wa bomba, Profesa Muhongo alisema nchi hizo zimekubaliana kukamilisha Kazi hiyo kabla ya makubaliano ya awali ya 2020. 

Makubaliano mengine ya nchi hizo ni kuchangia ujenzi wa mtambo wa kuchakata mafuta ghafi utakaojengwa Uganda ambao alisema utasaidia kuweka akiba ya mafuta kwa ajili ya biashara kwa nchi wanachama. 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akielezea uzoefu wa Tanzania kwenye ujenzi wa miradi  ya mabomba ya gesi na mafuta katika mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini   Uganda, Mhandisi  Irene  Muloni na kulia ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo  ya Madini Nchini  Uganda, Dk. Fred Kaliisa (kushoto) akifafanua  jambo katika kikao hicho. Kulia ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini   Uganda, Mhandisi Irene Muloni.
Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha akifafanua jambo katika mkutano huo.

DPP Amng’ang’ania Zombe na Wenzake Wanne, Awachomoa Watano Baada ya Kubaini Ushahidi Alionao Hauwagusi

$
0
0
Mahakama ya Rufani jana ilianza kusikiliza rufaa dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na askari wenzake wanane kuhusu kesi ya mauaji waliyoshinda.

Katika kesi hiyo namba 358 ya mwaka 2013, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) anapinga Zombe na wenzake kuachiwa huru na Mahakama Kuu katika kesi ya mauaji ya watu wanne iliyokuwa ikiwakabili.

Zombe na maofisa wenzake walifunguliwa mashtaka katika Mahakama Kuu wakidaiwa kuwaua watu wanne wakiwamo wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro, Januari 14, 2006.

Mauaji hayo yalifanyika katika msitu wa Mabwepande, Dar es Salaam na waliouawa walikuwa Mathias Lunkombe, Sabinus Chigumbi maarufu kwa jina la Jongo pamoja na ndugu yake Ephrahim Chigumbi na dereva teksi, Juma Ndugu wa Manzese.

Mahakama Kuu katika hukumu yake ya Agosti 17, 2009 iliwaachia huru washtakiwa wote baada ya kuwaona hawana hatia.

DPP hakuridhika na hukumu hiyo na mwaka huohuo, alikata rufaa Mahakama ya Rufani akidai jaji aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo alikosea kuwaachia huru washtakiwa hao, na kwamba kulikuwa na ushahidi wa dhahiri na wa kimazingira wa kutosha kuwatia hatiani washtakiwa wote.

Rufaa hiyo pia ilitupiliwa ambali na Mahakama Mei 8, 2013 kutokana na dosari za kisheria zilizobainika kwenye rufaa hiyo.

Baadaye DPP alipeleka maombi Mahakama Kuu aruhusiwe kukata tena rufaa hiyo nje ya muda, ombi ambalo lilikubaliwa.

Hata hivyo, katika shauri hili jipya DPP amewaondoa wajibu rufani watano baada ya kubaini kuwa ushahidi alionao hauwagusi katika rufaa hiyo. 

Waliosalia pamoja na Zombe ni Christopher Bageni, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari lakini walioondolewa ni Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Abineth Salo na Festus Gwabisabi.

Katika rufaa hiyo iliyosikilizwa jana na majaji Bernard Luanda, Sauda Mjasiri na Semistocles Kaijage, DPP anapinga hukumu iliyowaachia huru.

Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, Wakili wa Serikali, Timon Vitalis aliieleza Mahakama kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani wajibu rufani hao kwani unadhihirisha walikuwa na nia moja ya kutenda kosa pamoja na mtenda kosa halisi (Koplo Saad Alawi aliyetoroka).

Alisema kuwa kitendo cha wajibu rufani hao ambao ni maofisa wa polisi wenye wajibu na uwezo wa kuzuia uhalifu kuwapo eneo la tukio la mauaji wakashuhudia na kushindwa kuzuia ni dhahiri kuwa walikuwa na nia moja na mtenda kosa.

Kuhusu Zombe, Vitalis alisema kitendo cha kuwaelekeza watuhumiwa namna ya kueleza (walipoitwa kuhojiwa kwenye Tume ya Rais) na kutangaza kuwa watu waliouawa waliuawa kwenye mapambano na polisi ni dhahiri alikuwa akimsaidia mtenda kosa kusema uongo ili kumlinda.

Wakijibu hoja hizo kwa nyakati tofauti, mawakili wa utetezi walisema hakuna ushahidi wa dhahiri wa kuwatia hatiani wajibu rufani hao na kwamba Mahakama Kuu ilitathmini vema na kujiridhisha kuwa hawana hatia.

Hivyo waliiomba Mahakama hiyo iwaone kuwa hawana hatia kwa mashtaka yanayowakabili, huku Wakili Dennis Msafiri akisisitiza kuwa Jamhuri inapaswa kutumia nguvu nyingi kumtafuta muuaji halisi kama walivyoelekezwa na Mahakama Kuu na si kutumia muda mwingi kuendelea kuwang’ang’ania wajibu rufaa.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Luanda aliahirisha shauri hilo akisema kuwa wanakwenda kutafakari hoja za pande zote na kwamba wanahitaji muda kuandika uamuzi ambao watautoa pale utakapokuwa tayari.

Wafanyabiashara Walioficha Sukari Waanza Kukamatwa

$
0
0
Kauli  ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuwa baadhi ya wafanyabiashara wameficha sukari ili kutengeneza uhaba sokoni utakaopandisha bei ya bidhaa hiyo, imedhihirika baada ya baadhi ya wafanyabiashara hao kuanza kukamatwa wakiwa na vidhibiti.

Kutokana na hali hiyo iliyosababisha bei ya bidhaa hiyo kuanza kupanda, Waziri Mkuu Majaliwa, alitangaza uamuzi wa Serikali kuagiza sukari yake nje itakayouzwa kwa bei elekezi kwa wananchi ya Sh 1,800 kwa kilo, ili kuzuia ongezeko hilo haramu la bei.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Wilaya ya Singida, Saidi Amanzi alitangaza polisi kuwashikilia wafanyabiashara wawili wa mjini hapa kwa tuhuma za kukutwa na zaidi ya mifuko 655 ya sukari, sawa na tani 24.3, ikiwa imekifichwa kwenye stoo zao.

Kwa mujibu wa Amanzi, wafanyabiashara hao walikamatwa kwenye msako ulioendeshwa na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa Singida pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Amanzi alisema kuwa msako huo uliendeshwa baada ya kupata taarifa za siri kuwa kuna baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wameficha sukari, ili waje kuiuza kwa bei ya juu kwa wateja wao kwa kisingizio kuwa kuna uhaba mkubwa wa bidhaa hiyo.

“Katika msako huo, tumemnasa Mohamed Alute Ally (44), mfanyabiashara wa eneo la Unyankindi aliyekutwa na mifuko 335 ya kilo 25 kila mmoja na Yusufu Suleiman (39), mfanyabiashara wa eneo la Minga katika manispaa ya Singida aliyepatikana na mifuko 320 ya kilo 50,” alisema.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa mwito kwa wafanyabiashara wote kuacha kuficha bidhaa zote muhimu, ikiwemo sukari na mchele, bali waiuze kwa bei halali kwa wateja wao. 

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Joseph Mchina, amesema msako mkali unaohusisha kikosi kazi maalumu pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama utaendelea kwa nguvu zote na kusisitiza kuwa kuhodhi bidhaa kwa sababu yoyote ile ni kosa la uhujumu uchumi.

Mmoja wa Wakala wa Kiwanda cha Sukari cha TPC Moshi Mjini, Salim Nagji, amesema mfuko mmoja wa sukari huuzwa Sh 92,650 lakini tangu sukari iadimike mfuko unauzwa kati ya Sh 115,000 na Sh 120,000 huku kilo moja ikiuzwa kati ya Sh 2,400 na Sh 2,800 kwa kilo kinyume na bei elekezi ya Sh 1,800.

Serikali Yaupokea Ushauri wa Zitto Kabwe....Yaahidi Kuufanyia Kazi

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imepokea ushauri uliotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo) wa kuishitaki Benki ya Standard (ICBC) ya Uingereza, kuhusu ufisadi uliofanyika katika mkopo wa Dola za Marekani milioni 600 (Sh trilioni 1.2) ambazo Serikali ilikopa kwa kutumia hati fungani.

Ushauri mwingine uliotolewa na Zitto ambao Waziri Mkuu amesema Serikali itaufanyia kazi ni kuhusu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuwafikisha mahakamani wahusika wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, ili sheria ichukue mkondo wake.

Zitto alitoa ushauri huo bungeni mjini Dodoma juzi, wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, iliyowasilishwa na Waziri Angela Kairuki.

Hotuba ya bajeti ya ofisi hiyo inajadiliwa na wabunge pamoja na ile ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), iliyowasilishwa na Waziri wake, George Simbachawene.

Akizungumza na wanahabari jana, Waziri Mkuu alisema, hoja ya Zitto ina mashiko na akiwa msimamizi wa shughuli za Serikali bungeni, atahakikisha ushauri huo unafanyiwa kazi. 

“Sisi kama Serikali tutaifanyia kazi na pale tutakapoona tumefikia katika hatua ya kutoa taarifa kwa umma kuhusu utekelezaji wa ushauri huo, tutafanya hivyo,” alisema.

Benki ya Standard 
Kuhusu Benki ya Standard ya Uingereza, Zitto alisema mkopo huo wenye riba yenye kuweza kupanda na kushuka, umeanza kulipwa Machi mwaka huu na utalipwa mpaka mwaka 2020 kwa mikupuo tisa inayolingana.

Alisema, ifikapo mwaka 2020, Tanzania itakuwa imelipa deni hilo pamoja na riba ambayo ni Dola za Marekani milioni 897 sawa na Sh trilioni 2, huku akidai kuwa mkopo huo umegubikwa na ufisadi na wapo baadhi ya Watanzania wamefikishwa mahakamani kuhusu sehemu ya mkopo huo.

Alisema Takukuru katika kesi hiyo, inasaidiwa na wataalamu kutoka Uingereza katika kesi inayohusu Benki ya Uingereza, huku kukiwa na Watanzania walioandika ‘petition’ kutaka Benki ya Standard kuchunguzwa wakitaka ukweli wote kujulikana.

Escrow 
Kuhusu IPTL Tegeta Escrow, Zitto alisema mwaka 2014, Takukuru iliijulisha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kwamba ilikuwa inachunguza na kumaliza uchunguzi kuhusu miamala ya kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow Benki Kuu ya Tanzania kwenda Benki ya Stanbc Tanzania.

Alisema katika taarifa zote ambazo Takukuru inatoa kuhusu kesi za ufisadi, hakuna mahali inapozungumzia maendeleo ya suala hilo.

TCRA Yatoa Onyo Kwa Wafanyabiashara Wanaobadili IMEI za Simu FEKI ili Kuwahadaa Wananchi

$
0
0

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kiama kwa wafanyabiashara wa vifaa vya mawasiliano, kuacha kuwahadaa wananchi kwa kutoa punguzo ili kuwashawishi kununua simu bandia na kutishia kuwafunga miaka 10 jela, faini ya Sh30 milioni au vyote kwa pamoja watakaobainika.

Hatua hiyo imekuja wakati mamlaka hiyo ikiwa katika hatua ya kutekeleza mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi, huku ikitarajia kuzima simu feki ifikapo Juni 16.

Akizungumza na vyombo vya habari jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA, Mhandisi James Kiraba alisema kuna wafanyabiashara wajanja wanaobadilisha namba za utambulisho za vifaa vya elektroniki (IMEI) ili kuwahadaa wateja kuwa simu zao siyo feki.

Kwa ujanja huo, namba ya utambulisho inakuwa inatumika na simu zaidi ya moja na kutambulika na mfumo licha ya kuwa ni feki.

Pamoja na kuonekana ni halisi kwa kipindi wanachozinunua, alisema simu hizo zinazobadilishwa IMEI nazo zitazimwa Juni 16 kwa kuwa ni feki.

“Mamlaka inawakumbusha wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi kuwa ni kosa kubadilisha namba tambulishi za vifaa vya simu za mikononi (mobile devices), kwani adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka 10 au faini isiyopungua Sh30 milioni au vyote kwa pamoja,”alisema.

Alisema kumekuwa na udanganyifu kwa baadhi ya wauzaji wa simu kwa kutoa punguzo kwa wananchi ili kuwashawishi kuzinunua simu bandia kwa bei nafuu.

Kiraba alisema wananchi wanapaswa kuwa makini na hilo, huku wakihakikisha kuwa simu zao zimehakikiwa ili kuzuia usumbufu wa aina yoyote, utakaoweza kujitokeza wakati kipindi cha mpito kitakapomalizika.

Alisema idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango (bandia) zimeendelea kupungua kutoka asilimia 30 Desemba mwaka jana hadi kufikia asilimia 13 Machi.

Alisema uchambuzi wa Februari ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia tatu, vilevile idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 18 huku simu halisi zilikuwa sawa na asilimia 79.

“Uchambuzi wa Machi unaonyesha idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia nne, huku idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 13, uchambuzi huu unahusisha makampuni yote ya simu nchini,” alisema.

Shirika La Umeme Tanzania Tanesco Lazindua ”Tanesco Huduma";

$
0
0
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), limezindua huduma mpya inayotoa nafasi kwa wateja kutoa na kupata taarifa kupitia mfumo wa mawasiliano uliounganishwa kwenye simu za kiganjani unaoanza kwa majaribio katika mkoa wa kihuduma wa Kinondoni Kaskazini.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema jana jijini Dar es salaam kuwa, mfumo huo ambao uko kwenye programu maalumu, utasaidia kuboresha utendaji kazi wa shirika.

“Mfumo huu utaongeza kasi ya uwajibikaji wa watendaji kuwahudumia wananchi, lakini kwa sasa tumeuanza kwa majaribio katika mkoa wetu wa Kinondoni Kaskazini, wateja wetu watatoa taarifa za matukio yanayowakabili hata wale wanaoomba rushwa, watujulishe tupate ushahidi tuchukue hatua,” alisema Mramba.

Alisema mfumo huo umeundwa kutokana na ushirikiano kati ya Tanesco na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (Costech) na alisema itawapunguzia usumbufu wateja wa kupiga simu kwenye vituo vya huduma wanapokuwa na malalamiko binafsi au ya maeneo wanayoishi.

“Naamini majaribio haya yatakuwa na mafanikio, yatawawezesha wateja wa Tanesco wote nchini kuunganishwa kupata huduma hiyo,” alisema Mramba.

Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Hassan Mshinda alisema hatua hiyo imewapa moyo wa kuendelea kujituma zaidi kwa kuwa vijana wao wamepata nafasi ya kuonyesha kiwango cha ubunifu kwenye masuala ya teknolojia kulingana na dunia inavyokwenda.

Meneja Mwandamizi wa Mauzo na Masoko wa Tanesco Kinondoni, Nicholaus Kamoleka alisema mfumo huo unaitwa ‘Tanesco  Huduma’ wateja wataipata kwa kuiomba kupitia soko la programu la Google liitwilo ‘Play Store’.   
Wataalamu wa Mtandao wa COSTECH
Viongozi wa Tanesco na Tume ya sayansi na Teknolojia COSTECH wakifurahia jambo.

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC ) Lakanusha Kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic

$
0
0

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, linapenda kutoa taarifa sahihi juu ya taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na vyombo mbalimbali vya habari, pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu TPDC kufungua Akaunti za ESCROW katika Benki ya Stanbic.

Ni vyema ikaeleweka kwamba, Akaunti ya  ESCROW  ni Akaunti  maalumu inayoweza kufunguliwa  baina ya  Kampuni, Taasisi,  au Mashirika mbalimbali ya binafsi na yale ya umma kwa matumizi maalumu. 

Lengo la Akaunti ya ESCROW ni kuhifadhi fedha au kupitisha malipo kwa ajili ya shughuli maalum ikiwemo miradi au kazi yoyote maalumu na malipo haya hufanyika baada ya pande mbili kuridhia.

TPDC ilifungua Akaunti tatu za Esrow baada ya Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT)  kutoa idhini kufunguliwa kwa akaunti kwenye Benki ya Stanbic, ikiwa ni moja ya masharti yaliyowekwa na mkopeshaji ili  kutoa mkopo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ya gesi asilia, kutoka Benki ya Exim ya China. 

Mkopeshaji alipendekeza Akaunti hizo zifunguliwe kwenye benki ya Stanbic na ambapo taratibu za manunuzi zilizingatiwa, ikiwemo ushindanishaji wa watoa huduma.

 Akaunti hizo tatu zilizofunguliwa ni pamoja na:
1. Akaunti ya Mapato ya Gesi
Lengo la akaunti hii ni hifadhi mapato yote yatakayo tokana na mauzo ya gesi kwa njia ya bomba jipya.

2.  Akaunti ya Uendeshaji
Akaunti hii ina jukumu la kuhifadhi fedha zinazohitajika kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa mradi wa miundombinu hiyo mipya ya gesi asilia.

3.  Akaunti ya Kulipia Deni
Akaunti hii imefunguliwa kwa ajili ya kulipa madeni yatokanayo na mkopo.

Akaunti hizi zinadhibitiwa na masharti yaliyowekwa kwenye makubaliano (Mkataba) ya Menejimenti ya Akaunti hizo yaliyosainiwa kati ya Benki ya Stanbic (kama Benki ), TPDC (kama mtumiaji wa mwisho), Benki ya Exim ya China (kama Wakopeshaji) na Wizara ya Fedha (kama mdeni kwa niaba ya Serikali ya Tanzania).

TPDC inapenda kuufahamisha umma kwamba, baada ya taratibu zote hizo kufuatwa, si sahihi kuuhusisha mchakato huu na tuhuma zozote na ukiukwaji wa sheria za nchi. 

Aidha, ifahamike kwamba Akaunti ya ESCROW ni akaunti ya kawaida kabisa katika utekelezaji wa miradi kama huu wa gesi asilia.

TPDC Kwa Maendeleo ya Taifa!
Imetolewa na:
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji- TPDC
S.L.P 2774
Dar Es Salaam

Mapendekezo Ya Sheria Ya Wazee Kuwasilishwa Bungeni

$
0
0
NAIBU WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali imekamilisha mapendekezo ya uundwaji wa Sheria ya Wazee ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa Bunge wa Septemba.

Dk. Kigwangalla aliyasema hayo jana (Ijumaa, Aprili 29, 2016) wakati akitoa ufafanuzi kwa Viongozi wa Mtandao wa Wazee waliomtembelea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ofisini kwake mjini Dodoma.

Dk. Kigwangalla alisema kuwepo kwa Sheria ya Wazee kutawezesha mambo mbalimbali yanayohusu wazee kutekelezwa kwa mujibu wa sheria hiyo likiwemo suala la pensheni.

“Mimi pamoja na Waziri wangu, Ummy Mwalimu baada ya kupewa jukumu la kuongoza wizara tuliunda kikundi cha wazee kwa ajili ya kuamua mambo makubwa mawili ambayo tutayatekeleza likiwemo la pensheni kwa wazee wote,” alisema.

Naibu Waziri huyo alisema suala jingine ambalo wamepanga kulitekeleza ni utoaji wa huduma ya bure kwa wazee, ambapo watawapatia bima ya afya ili wasiendelee kusumbuka.

Kwa upande wake Waziri Mkuu aliwahakikishia wazee hao kwamba Serikali inawatambua na ndiyo sababu ya waliamua wawe na sehemu ya kufikishia malalamiko yao ambayo ni Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto .

Kuhusu ombi la wazee hao kwa Rais Dk. John Magufuli la kuwa na uwakilishi Bungeni kwa kupitia nafasi zake 10 za uteuzi, Waziri Mkuu alisema amelipokea na atalifikisha kwa Mhe. Rais.

Pia amewataka wapanue taasisi yao na kuimarisha mtandao uweze kujulikana na wazee wengi zaidi, wawe na viongozi kuanzia ngazi za vijiji ambapo Serikali ipo tayari kushirikiana nao kwa karibu.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na utoaji wa huduma za afya kwa wazee katika hospitali mbalimbali alizotembelea na kukuta yameanzishwa madirisha maalumu ya kuhudumia.

Akizungumzia kuhusu suala la wazee kupewa elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI aliwataka waandaaji wa matamasha na semina za mafunzo hayo kujumuisha watu wote wakiwemo wazee.

Naye Mwenyekiti wa mtandao huo , Bw. Sebastian Bulegi alisema lengo la kumtembelea Waziri Mkuu ni kumuomba awafikishie shukurani zao kwa Rais Dk Magufuli kwa kuwapatia wizara maalumu inayoshughulikia masuala yao.

“Vile vile shukurani hizi tufikishie kwa mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli kwa kufanya wazee kuwa agenda yake ya kwanza na tayari ameshatembelea makazi ya Nunge Kigamboni (Dar es Salaam) na Bukumbi (Mwanza),”alisema.

Mwenyekiti huyo ambaye aliambatana na wajumbe wanane wa mtandao huo unaoundwa na Asasi 26 za wazee katika ngazi za wilaya na mkoa kutoka mikoa ya Kigoma, Tanga, Arusha, Mwanza, Lindi na Dodoma, aliiomba Serikali isimamie kutokomeza mauaji ya wazee.

Ombi jingine alilolitoa kwa Serikali ni utekelezwaji wa Sera ya Wazee ya mwaka 2003, Sera ya Matibabu bure kwa wazee, mafunzo ya kupambana na UKIMWI pamoja na uwakilishi katika ngazi za kutoa maamuzi.

Pia wazee hao wamemhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamekubali ombi linalotolewa na viongozi wakuu wa nchi la kuwataka wawaombee ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo, baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980, DODOMA.
JUMAMOSI, APRILI 30, 2016.

Abiria Wanusurika Kufa Katika Ajali ya Ndege Mjini Bukoba Leo

$
0
0
Watu kadhaa wamenusurika  kufa baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Auric Air waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Uwanja wa Ndege wa Manispaa ya Bukoba ilipokuwa ikitua na rubani kupoteza uelekeo  kama inavyo onekana pichani.

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Jijini Mwanza ,tukio limetokea majira ya saa nne asuhuhi ya leo Jumamosi April 30,2016.

Aliyejifanya Ofisa usalama wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Atupwa jela Miaka 12

$
0
0

Mahakama ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, imemhukumu kwenda jela miaka 12, Qasama Machibya aliyejifanya ofisa usalama wa Taifa kwenye ziara ya Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete mwaka 2013.

Kabla ya hukumu, mshtakiwa alijitetea mahakamani hapo kuwa kitambulisho alichokutwa nacho siyo chake na anashangaa kuona kuna picha yake na jina lake.

Alidai kuwa hizo ni mbinu za polisi kumminya, hivyo aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu na kwamba ana ugonjwa wa Ukimwi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Gabriel Kurwijila alisema utetezi wa mshtakiwa hauifanyi mahakama kutomtia hatiani kwa kuwa hana cheti cha ugonjwa.

Alisema kutokana na mahakama kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka uliowasilishwa inamtia hatiani kwa makosa matatu.

Kurwijila alisema kosa la kwanza ni kughushi nyaraka ya Serikali hivyo, atakwenda jela miaka mitano na kosa la pili la kujifanya ofisa usalama wa Taifa kifungo chake ni miaka miwili.

Alisema katika kosa la tatu la kuudanganya umma kwa kutoa nyaraka iliyoghushiwa hivyo, atatumikia adhabu gerezani miaka mitano.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elias Mgobela alisema mshtakiwa alikamatwa wakati Kikwete alipokuwa akitarajia kuhutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara.

Makonda Asema hataki kuwaona wasanii nyumbani kwake.......Ni Baada ya Kumtosa kwenye uzinduzi wa kampeni ya usafi

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema hataki kuwaona nyumbani kwake wasanii ambao wamekacha kuhudhuria kampeni yake ya usafi ambayo imezinduliwa Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Paul Makonda ameonesha kusikitishwa na idadi ndogo ya wasanii waliojitokeza kuunga mkogo kampeni hiyo.

“Lakini nashukuru wasanii wote ambao wamejumuika nasi, na kwa kweli hiki ni kipimo cha kuwatambua marafiki zangu wa kweli ni wapi. Na mimi niwaambie tu, sitaki kuona msanii yoyote nyumbani kwangu ambaye hawezi kuniunga mkono kwenye mambo yangu ya maendeleo,” alisema Makonda.

“Sitaki hiyo tabia, nimemuona Steve Nyerere hapa amekuja akiwa amechelewa hilo ni onyo, ukirudia tena nakushughulikia. Huwezi kuwa rafiki yangu alafu kwenye mambo kama haya huhangaiki, wengine wanataka waombwe, eti mbona hujanipigia simu kuniomba nipost, we nani?. Swala la usafi siyo la serikali ni swala la kila mtu,” aliongeza Makonda.

Wasanii ambao walihudhuria uzinduzi huo ni, Mchizi Mox, Yamoto Band, Diamond na team ya Wasafi, Mwasiti, Queen Darleen, Salam TMK pamoja na Steve Nyerere wa bongo movies.

Katika hatua nyingine Makonda amevitaka vyombo vya usafiri jijini Dar es salaam kuwa na vifaa vya kuwekea uchafu.

Pia wamewataka wafanyabiashara siku ya jumamosi, kufungua maduka yao saa 3 asubuhi ili muda wa asubuhi wautumie kwa ajili ya kufanya usafi.

CCM Yawataka Wafanyabiashara Kupuuza kauli za Wanasiasa kuwa Rais Magufuli Analengo la Kuwakomoa.

$
0
0

Chama cha Mapinduzi kimewataka watanzania kupuuza kauli za baadhi ya wanasiasa zinazodai kuwa rais Magufuli analengo la kuwakomoa wafanyabiashara na kinazieleza kauli hizo kuwa ni za uchochezi kwakuwa serikali ya awamu ya tano haina tatizo na wafanyabiashara na watumishi waadilifu bali wanaolihujumu taifa kwa manufaaa binafsi.
 
Kauli hiyo ya chama imetolewa na msemaji mkuu wa CCM Christopher Ole Sendeka wilayani Simanjiro alipokuwa akizungumza na wananchi wanachama wafuasi wa CCM na viongozi wa mila katika kata ya Shambarai.

Kwa upande katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Shabani Mdoe amewataka wananchi kuwa makini na viongozi wasio waadilifu huku mkuu wa wilaya ya Simaniro Mahamoud Kambona akiwata viongozi wa mila kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo.

Katika mkutano huo viongozi wa mila kutoka jamii ya wafugaji pia walipata nafasi ya kupaza sauti na kutaka serikali na jamii iheshimu maamuzi wanayoyatoa kama viongozi katika jamii.

Watu 4 na wengine 29 Wajeruhiwa Baada ya Basi la HBS Walilokuwa Wakisafiria Kupinduka Jijini Mbeya

$
0
0
Watu wanne wamekufa papo  hapo na wengine 29 kujeruhiwa baada ya basi la HBS linalodaiwa kuwa ni mali ya kampuni ya Sabena walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Mbeya kwenda Tabora kuacha njia na kupinduka katika eneo la maji mazuri, barabara kuu ya Mbeya – Chunya wilayani Mbeya.
 
Basi hilo likiwa limebeba abiria wengi kuliko uwezo wake, lilianza safari yake ya kuelekea Tabora likitokea jijini Mbeya, lakini inadaiwa kuwa likiwa kwenye mtelemko na kona kali za mlima Mbeya likafeli breki na ndipo dereva wake akaamua kuruka na kuliacha likijiendesha lenyewe hali ambayo ilisababisha lipoteze mwelekeo na kuanguka mtaroni.

Muuguzi wa zamu katika hospitali ya rufaa ya kanda ya nyanda za juu kusini, Jesca Kahangwa amethibitisha kupokea miili ya watu wanne na majeruhi 29 wa ajali hiyo, huku akidai kuwa hali za majeruhi wengi bado ni mbaya.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewahi katika eneo la ajali na baada ya kupata maelezo ya chanzo cha ajali hiyo, akaliagiza jeshi la polisi kuwatafuta na kuwakamata haraka dereva, kondakta na mmiliki wa gari hilo kwa kosa la kuendesha gari bovu barabarani.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya Tarehe Moja Mwezi wa 5

Tume ya Pamoja Kufuatilia Ziara ya Rais Magufuli Nchini Rwanda

$
0
0

Kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda kilichofanyika kuanzia tarehe 29 – 30 Aprili, 2016, kimekamilika Mjini Gisenyi, Rwanda, ambapo wataalam wa sekta mbalimbali wameazimia kuharakisha maeneo ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. 
 
Kikao hicho cha 14 cha ushirikiano kimefanyika kufuatia maagizo ya Marais wa Tanzania na Rwanda wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli nchini Rwanda mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu. 
 
Wakati wa ziara hiyo, wakuu hao walikubaliana kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na kuibua maeneo mapya yanayolenga kuinua shughuli za kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.
 
Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha wataalamu kiongozi wa ujumbe wa Tanzania Balozi Ramadhan M. Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania aliwakumbusha wajumbe wa pande zote mbili kuendesha mazungumzo na mjadala kwa kuzingatia maagizo ya viongozi hao na vilevile kuchangamkia fursa za ushirikiano wa shughuli za kiuchumi za wananchi wa pande zote mbili baada ya mindombinu ya kikanda kuimarika. 
 
Kwa upande wake, Balozi Jeanine Kambanda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda na mwenyeji wa kikao hicho, alihimiza wajumbe kujiwekea malengo yanayotekelezeka na tarehe za ukomo kwenye maeneo yote watakayokubaliana ili kusukuma utekelezaji na kupata matokeo ya haraka. 
 
Pamoja na mambo mengine, pande zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta muhimu kama vile miundombinu ya ushoroba wa kati (central corridor), kuharakisha ujenzi wa reli ya kati katika kiwango cha kimataifa (standard gauge), kukuza ushirikiano katika sekta ya anga hususan baina ya mashirika ya ndege ya Rwandair na ATCL, kuimarisha ushirikiano katika sekta za sayansi na teknolojia, afya, kilimo na ufugaji, utalii, elimu, mawasiliano n.k.
 
Mkutano huo pia umekubaliana kuanzisha Kamati ya Pamoja ya Utekelezaji (Joint Implementation Committee) kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu maeneo yote ya ushirikiano yaliyokubaliwa katika Kikao hicho cha 14. Kamati hiyo itakayoongozwa na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizo mbili, itakutana kila robo mwaka.
 
Aidha, Serikali ya Rwanda imeonesha utayari wake wa kuleta nchini Maafisa na Watumishi wa Serikali kwa lengo la kupata uzoefu na mafunzo katika vyuo vya kitaalamu nchini kama vile Chuo cha Diplomasia  (CFR), Chuo cha Taifa cha Utalii na Wanyamapori  (Mweka) na Chuo cha Usafirishaji (NIT).
 
Kwa upande wa Tanzania, Serikali imedhamiria kuwakutanisha wataalamu wa mitaala ya elimu kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Rwanda kwenye upande wa kuandaa mitaala ya elimu ya tehama kwenye shule za awali, msingi na sekondari.
 
Mkutano ujao wa kumi na tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda utafanyika mwaka 2018, nchini Tanzania.
 
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Gisenyi, Rwanda
30 Aprili, 2016

Serikali Yaokoa Sh. Bilioni 15.4 za Mishahara HEWA Machi hadi Aprili 24

$
0
0

Serikali imetangaza kuokoa kiasi cha Sh15.4 bilioni katika kipindi cha kuanzia Machi hadi Aprili 24 ambacho kingelipwa kwa watumishi hewa 8,236 ambao wamebainika hadi sasa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Angela Kairuki aliliambia Bunge jana kuwa kazi ya kuwasaka watumishi hewa bado inaendelea nchini kote.

Alisema watumishi hao wamebainika katika maeneo mbalimbali na kati yao 1,614 ni wa Serikali Kuu na 6,624 wa Serikali za Mitaa.

Waziri alisema kuwapo kwa watumishi hewa kumewafukuzisha kazi maofisa 56 na taratibu za kuwafungulia kesi mahakamani zinaendelea ikiwamo kutakiwa kulipa hasara yote ambayo waliisababisha.

Alisema mapambano dhidi ya watumishi hewa ni endelevu ili kukomesha tabia hiyo inayolitia hasara taifa.

“Mheshimiwa Rais alitangaza siku za hivi karibu na mtaona nami natangaza leo idadi ikiwa juu kuliko aliyotangaza Rais na vyombo vingine vitaendelea kutangaza maana tuko kwenye kazi kila siku,alisema Kairuki.

Alitaja changamoto kubwa katika wizara yake ni kuwa ni tofauti ya mishahara kwa wafanyakazi ambayo inaonekana ni kubwa kati ya mtu wa chini na wa juu yake, jambo alilosema Rais ameamua kulisimamia ili kulipunguza.

“Tofauti ya mishahara ni kubwa, kuna baadhi ya maeneo mtu anatakiwa kupokea mshahara wa miezi 50 au 30 ili aweze kumfikia mwenzake mwenye mshahara mmoja tu,” alisema Kairuki.

Kuhusu suala la ajira, alisema katika mwaka wa fedha wa 2016/17, Serikali imepanga kuajiri watumishi 71,496 kuanzia mwezi huu na akawataka waajiri kuacha kuwahamisha watumishi endapo hakuna fedha za kuwalipa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akutana Na Viongozi Wa Mtandao Wa Vyama Vya Wazee Tanzania

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake  bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania Ofisini kwake  bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na viongozi wa Mtandao wa Vyama vya Wazee Tanzania baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake jijini bungeni mjini Dodoma  Aprili 29, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Wziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Hamis Kigwangalla .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Serikali kutumia shilingi bilioni 59.5 kuwezesha vijiji nchi nzima

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Philip Mpango, amesema kuwa serikali imepanga kutumia shilingi 59.5bn kwaajili ya kuviwezesha vijiji nchi nzima katika kipindi cha mwaka fedha 2016/2017

Dokta Mpango, aliwaambia wabunge mjini Dodoma, jana tarehe 30, Machi, 2016, kwamba fedha hizo ni kwajili ya kukiwezesha kila kijiji shilingi 50m kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali.

Alisema kuwa fedha hizo zimewekwa kwenye mfuko wa Hazina, ili kuwawezesha wadau na taasisi zitakazo husika  kupanga utaratibu mzuri wa matumizi ya fedha hizo.

“Fedha hizi zitaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu” aliongeza Waziri Mpango

Akizungumza kuhusu mikopo ya wanawake na vijana, Dokta Mpango, alisema kuwa serikali, kupitia Ofisi hiyo ya Waziri  Mkuu, imepanga kutumia shilingi 1bn kuendeleza ujuzi kwa vijana wasio na ajira na shilingi 1.955bn kuwainua wanawake kiuchumi

Alifafanua kuwa halmashauri za wilaya, miji na majiji zitaendelea na utaratibu wao wa kutenga asilimia 5 ya mapato yao ya ndani kutoa mikopo kwa vijana na asilimia nyingine 5 kwaajili ya kuwawezesha wanawake katika maeneo yao.

Serikali Yaendelea Kuhakiki Madeni ya Walimu

$
0
0

WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe. Dakta Philip Mpango, ameliambia Bunge mjini DODOMA, jana tarehe 30, Aprili, 2016, kwamba serikali inaendelea kuhakiki madeni ya walimu yaliyowasilishwa kwaajili ya malipo baada ya kubaini kuwepo kwa udanganyifu kwenye baadhi ya madai hayo

Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016, serikali ilipokea madai yenye jumla ya shilingi Bilioni 29 na Milioni 800 na imelipa  20.125bn, huku madai mengine yakizuiwa baada ya kubainika hayakuwa halali.

Alitolea mfano wa mtumishi mmoja aliyewasilisha madai ya shilingi 600m badala ya shilingi laki 6, huku madai mengine yaliyolipwa miaka ya nyuma yakiwasilishwa kama madeni mapya

Dakta Mpango alisema kuwa serikali inathamini mchango wa walimu katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini na kwamba itaendelea kulipa madai yao na watumishi wengine wa umma baada ya kuyachambua, kuyahakiki na kujiridhisha kuwa ni halali.

Auawa na Mdogo wake Baada ya Kumfumania Akifanya Mapenzi na Mkewe

$
0
0

Mkazi wa Mahembo Manyanda Manyilizu (40) ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mdogo wake baada ya kumfumania akiwa na mkewe.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Dismas Kisusi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Mawemilu.

“Manyilizu alimkuta mdogo wake akifanya mapenzi na mkewe, alivyomuhoji, mdogo wake alichukua kitu akampiga nacho kichwani hivyo alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu katika zahanati ya Kijiji cha Mawemilu,” alisema Kisusi.

Alidai mtuhumiwa na mwanamke walikimbia baada ya kufanya tukio hilo.

Katika tukio jingine, watu wawili wameuawa kwa kupigwa mawe na marungu kisha miili yao kuchomwa moto na wananchi.

Kisusi alisema tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Shimba wilayani Kahama.

Kisusi alisema watu hao walituhumiwa kuwa ni majambazi baada ya kumvamia Mchongaraji Ndalawa (65), akiwa amelala nyumbani kwake wakimtaka awape fedha.

“Alivyosema hana walimkata kwa panga kichwani, ndipo wananchi walijichukulia sheria mkononi kwa kuwaua,” alisema.

Majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama na hali yake inaendelea vizuri.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images