Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Kuendelea Kuwachukulia Hatua Waliobadili Matumizi ya Ardhi Ya Makazi kuwa ya Biashara

$
0
0

Serikali imesema kuwa itawachukulia hatua za kisheria wananchi waliobadili matumizi ya Ardhi ya makazi kuwa maeneo ya biashara kinyume cha sheria na kuifanya Serikali kukosa mapato  stahiki ya kodi ya Ardhi.

Hayo yamebainishwa  leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Kodi toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Bi.Rehema  Kilonzi wakati  akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu  mapato yaliyokusanywa kutokana na kodi ya pango la ardhi kwa mwaka  fedha 2015/2016.

Amesema kuwa  baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali nchini wameyageuza maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya makazi ya watu kuwa maeneo ya nyumba za kulala wageni,hosteli, maeneo ya biashara jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 chini ya fungu la 33.

“Rai yetu kwa wananchi waliopata fursa ya kumiliki maeneo yaliyopangwa na kumilikishwa kisheria,tunawaomba walipe kodi ya Pango la ardhi kwa wakati kuepuka usumbufu wa kufikishwa Mahakamani .”alisisitiza  Kilonzi.

Amesema katika kipindi cha mwaka wa 2015/2016 Serikali imefanikiwa kukusanya kiasi cha Bilioni 60 kutokana na kodi ya Pango la Ardhi ambazo ni sawa na asilimia 85 ya lengo lililowekwa la kukusanya shilingi bilioni 70.

Amesema  mkakati wa wizara  hiyo ni kuhakikisha kuwa inafikia lengo la kukusanya Kodi  hiyo na kuongeza kuwa hiyo imesambaza maafisa wake katika Ofisi zote za Kanda ili kuhakikisha kuwa Halmashauri na Manispaa zinasambaza hati za madai ya Kodi ya pango la Ardhi na kuwafikia wadaiwa wote kwa wakati muafaka.

Amesema wizara hiyo inaendelea na mkakati wa kufungua mashauri ili kupata kibali cha mahakama cha kukamata mali za wadaiwa sugu na  kuwapokonya hati milki katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumzia hatua hiyo amesema kuwa katika  jiji la Dar es salaam mashauri yataanza kusikilizwa katika Baraza ya Nyumba na Ardhi La Wilaya ya Kinondoni kuanzia mwezi Mei 2016,  kisha zoezi hilo litaendelea kwa Mikoa na Wilaya zote Jijini hilo.

Akitoa ufafanuzi kuhusu Kodi ya Ardhi inayotozwa na wizara hiyo amesema kuwa  inatozwa kwa kuzingatia Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 chini ya fungu la 33.

Amesema kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu ( kuanzia Februari 2016) Wizara imewafikia  wamiliki wa Ardhi 679 katika Maeneo ya Sinza na Kijitonyama Jijini Dar es salaam na kufanya uthamini wa maendelezo kwa kwa wale waliokiuka masharti ya matumizi yaliyopangwa ambapo ilibainika kuwa kuna ukiukwaji wa masharti ya Uendelezaji kwa kubadili matumizi yaliyoainishwa katika milki zao.

Aidha, amesema kutokana na uthamini uliofanyika mwezi Februari Serikali inatarajia kukusanya jumla ya milioni mia nane kama faini kutokana na ubadilishaji wa matumizi ya maeneo usiozingatia Sheria za Ardhi katika maeneo ya Sinza na Kijitonyama.

Mchango wa Ndg. Zitto Kabwe Bungeni 28 Aprili 2016.......Kazirudisha Upya hizi Tuhuma mbili za Rushwa

$
0
0
Mheshimiwa Spika, Tangu tuanze Mkutano huu wa Bajeti mwaka 2016 kumekuwa na malalamiko kutoka kwa Wabunge na hasa wabunge wa kambi ya Upinzani Bungeni kuhusu ukiukwaji wa Sheria mbalimbali za nchi katika masuala ya Bajeti. 

Jana jioni Mwenyekiti wa Bunge Mheshimiwa Andrew Chenge alitoa Changamoto kuwa Wabunge tuseme ni sharia gani zimekiukwa katika mchakato mzima wa Bajeti ya Nchi hivi sasa. Kwa maoni yangu, kuna ukiukwaji kadhaa wa sharia ya Bajeti, sharia namba 11 ya mwaka 2015 katika mchakato wa Bajeti ya Mwaka huu. Nitaeleza kwa ufupi.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 8 cha sheria ya Bajeti kinaeleza namna ambavyo mfumo wa Bajeti ya Serikali unapaswa kuwa. 

Vifungu cha 8(1)(b) na 9(1)(a) na 19(1) vinaeleza namna mchakato wa Bajeti unavyopaswa kuwa. Vifungu hivi vinataka “Planning and Budget Guidelines” zipitishwe na Bunge katika mkutano wake wa Mwezi Februari kila mwaka. Sheria inataka “budget ceilings” ziidhinishwe na Kamati ya Bajeti na baadaye Bunge linapokaa kama Kamati ya Mipango.

Mheshimiwa Spika, Bunge lilikaa kama Kamati ya Mipango na kupitisha Mpango wa Bajeti uliokuwa na Bajeti ya Tshs 23.7 trilioni kama ulivyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango. Hata hivyo Bajeti inayojadiliwa sasa ni Tshs 29.5 trilioni tofauti kabisa na sio tu viwango vilivyopitishwa na Bunge mwezi Februari bali pia hata vipaumbele vyake ni tofauti. 

Hili ni suala la Utawala bora (governance issue) kwani taratibu za utungaji wa Bajeti zimeainishwa na sheria na kama sheria hazifuatwi ni vigumu sana hata Bajeti yenyewe kutekelezwa.

Ili kurekebisha hali hii ni lazima Bunge likae tena kama kamati ya Mipango na kupitisha upya viwango vya juu vya bajeti kabla ya mjadala wa Bajeti kuendelea au angalau kabla ya kupitisha Bajeti Kuu mwezi wa Juni 2016.

Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais Ikulu inapasa kuzingatia sana sheria na taratibu tulizojiwekea kwani madhara ya kutofuata sheria ni makubwa mno.

 Kwa mfano hivi sasa Bajeti za Taasisi hazimo kwenye vitabu vya Bajeti ya Serikali kinyume na Sheria ya Bajeti ambapo hivi sasa Bajeti za Taasisi zote za Umma zinakuwa ni sehemu ya Bajeti ya Serikali na Wabunge wanapaswa kuwa na nyaraka za bajeti hizo. 

Ofisi ya TR kwa mujibu wa kifungu cha 17(a) cha Sheria ya Bajeti ilipaswa kuunganisha Bajeti za Mashirika yote ya Umma na kutoa kitabu chake kwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, Serikali inapaswa kutoa maelezo ya kina kwa Wabunge kuhusu masuala haya ili kuzuia ukiukwaji wa Sheria tulizojitungia wenyewe.

TAKUKURU na kesi za Ufisadi Mkubwa Nchini

1. Ufisadi wa HatiFungani ya Tshs 1.2 trilioni Standard Bank ya Uingereza

Mheshimiwa Spika, Tarehe 8 Machi mwaka 2013 Serikali ya Tanzania ilikopa fedha $600 milioni ( 1.2 trilioni) kutoka nje kwa msaada wa Benki ya Standard ya Uingereza ambayo sasa inaitwa Standard Bank ICIC Plc. Mkopo huo wenye riba yenye kuweza kupanda (floating rate) umeanza kulipwa mwezi Machi mwaka huu ( kama Serikali imeanza kutekeleza mkataba). 

Mkopo huu utalipwa mpaka mwaka 2020 kwa mikupuo 9 inayolingana. Ifikapo mwaka 2020, Tanzania italipa deni pamoja na riba jumla ya $897 milioni ( takribani tshs 2 trilioni ).

Mkopo huu umegubikwa na ufisadi na kwa kuwa baadhi ya Watanzania wamefikishwa mahakamani kuhusiana na sehemu ya mkopo huu, sitapenda kueleza upande wa waliopo mahakamani.

Kesi iliyopo mahakamani inahusu $6 milioni ambazo inasemekana ( kwa mujibu wa nyaraka za mahakama) kuwa zilitumika kuhonga maafisa wa Serikali ili Benki hiyo ya Uingereza iweze kupata biashara iliyopata. 

Jambo la kushangaza ni kwamba wanaosemekana kula rushwa hiyo hawapo mahakamani mpaka sasa. Vile vile waliotoa rushwa hiyo hawapo mahakamani mpaka sasa. Waliopo mahakamani ni wanaosemekena kutumika kupeleka rushwa. 

Mjumbe kashtakiwa, lakini aliyemtuma hajashtakiwa na aliyepelekewa kilichotumwa hajashtakiwa. Hapa kuna tatizo la msingi ambalo tukilitatua Serikali yetu itaepuka masuala kama haya siku za usoni.

Mheshimiwa Spika, Hapa mbele yangu nina barua ambayo kundi la Watanzania zaidi ya 2000 kutoka kona zote za dunia wamesaini kutaka Benki ya Standard ya Uingereza ichunguzwe kwenye suala hili la HatiFungani. 

TAKUKURU walitumia taarifa ya Taasisi ya Uingereza ya SFO katika kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya Watanzania wanaotajwa katika sakata hili. 

SFO haikufanya uchunguzi dhidi ya Benki ya Uingereza ya Standard Bank. Hatujui ni kwa maslahi mapana ya Uingereza au ni kwa kupitiwa. Sisi Tanzania tumejikuta tunafuata matakwa ya Uingereza katika jambo hili, kiasi cha hata kutumia ushauri wa kitaalamu wa Waingereza katika jambo hili. 

Leo hii TAKUKURU inasaidiwa katika kesi hii na wataalamu kutoka Uingereza katika kesi inayohusu Benki ya Uingereza! Watanzania walioandika petition kutaka Benki ya Standard kuchunguzwa wanataka ukweli wote kujulikana – Standard Bank walihusika kwa kiwango gani katika kutoa rushwa ili kupata biashara? TAKUKURU wanapaswa kufanyia kazi jambo hili kwa kuwafungulia mashtaka Standard Bank, mashtaka ya kutoa rushwa ili kupata biashara nchini. 

Hata hivyo TAKUKURU inaogopa wazungu, inaogopa kuwaudhi watu wanaowapa ushauri wa kitaalamu kuhusu kesi za rushwa!

Mheshimiwa Spika, maslahi ya Tanzania hapa ni makubwa mno. Iwapo tutafanikiwa kuonyesha kuwa Benki ya Standard ilihonga kupata biashara nchini kwetu Tanzania itafaidika kwa namna mbili. 

Moja, itakuwa ni fundisho kubwa kwa makampuni ya kimataifa kwamba Afrika sio mahala pa kuhonga na kupata kazi na kutoadhibiwa. Mbili, Tanzania haitalipa mkopo huu na riba zake. 

Tutakuwa tumeokoa zaidi ya tshs 2 trilioni katika Deni la Taifa na kuelekeza fedha tulizokuwa tulipe riba kwenda kwenye kuhudumia wananchi wetu kwenye Afya na Elimu. 

TAKUKURU waongozwe na maslahi mapana kwa Taifa badala ya kutafuta sifa ndogo ndogo za ‘wangapi wamefikishwa mahakamani’. Ni lazima taasisi zetu sasa zianze kutazama mambo kwa picha kubwa.

Mheshimiwa Spika, hii sio mara ya kwanza SFO kufanya ilichofanya dhidi ya Tanzania. Mnakumbuka kesi ya rada na Shirika la BAE la Uingereza. Safari hii Tanzania isikubali kubeba tu makubaliano ambayo SFO inafanya na makampuni ya kimataifa.

 Ni lazima tufanye uchunguzi wetu na tufungue kesi dhidi ya makampuni haya. Haiwezekani wawe ni Watanzania tu wanaoshtakiwa kwa rushwa na kuwaacha wanaotoa rushwa hizo wakiendelea na biashara zao kama kawaida.

Mheshimiwa Spika, Taarifa zilizopo sasa kwenye vyombo vya habari ni kwamba Benki hii kupitia tawi lake la Tanzania ( Stanbic Bank ) siku ambayo walipata ‘deal’ la Bond ndio siku hiyo hiyo walipewa kazi na Serikali ya kufungua akaunti ya Escrow kuhusu fedha za Bomba la Gesi kutoka Mtwara. 

Kimsingi biashara hii ya Escrow akaunti katika Benki hii ni kubwa zaidi kutoka ile ya mkopo kwani ni biashara ya kutunza fedha za Bomba kwa miaka 20! Benki hii ilipata biashara kubwa kama hii bila ya kuwepo kwa zabuni yeyote ile na kuleta ushindani. 

Lakini pia kama kulikuwa na umuhimu wa kufungua akaunti hii ni kwanini Shirika la TPDC halikufungua akaunti hii katika Benki Kuu ya Tanzania? Haya ndio mambo TAKUKURU wanapaswa kuchunguza katika kulinda maslahi ya nchi yetu dhidi ya makampuni makubwa kutoka nje.

Mheshimiwa Spika, Vile vile kuna taarifa kwamba hata fedha ambazo zilipatikana kutokana na mkopo huu hazikufika kule kunakotakiwa. 

Nimewasilisha maswali Wizara ya Fedha kutaka kujua miradi ambayo fedha hizi zilikwenda. Hata hivyo kutokana na orodha ya miradi niliyonayo na kutokana na habari za hivi karibuni za Serikali kudaiwa na wakandarasi, mradi wa Kinyerezi na hata mradi wa Kiwira, ni dhahiri kuwa sehemu ya fedha zilizopatikana katika mkopo huu hazikupelekwa huko. Uchunguzi wa kina unatakiwa kwenye eneo hili ili kupata ukweli na kuzuia mambo kama haya kutokea siku za usoni.

Mheshimiwa Spika, nitatumia kanuni ya 120(2) kutaka Bunge tako tukufu kuunda Kamati Teule kuichunguza Benki ya Standard ICBC ya Uingereza na kampuni yake dada ya Stanbic Tanzania kuhusiana na Mkopo wa Hatifungani $600m, matumizi ya mkopo huo na ufunguzi wa Akaunti ya Escrow ya Bomba la Gesi la Mtwara – Dar es Salaam. 

Kwa sasa ninawasilisha mezani nyaraka zote nilizonazo kuhusiana na Mkopo huu kwa ajili ya Bunge kupitia kabla ya kuwasilisha Hoja ya Kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuichunguza Standard Bank ICBC na Stanbic Tanzania

2. Uchunguzi wa IPTL Tegeta Escrow Account

Mheshimiwa Spika, Mwaka 2014 TAKUKURU waliijulisha Kamati ya Bunge ya PAC kwamba ilikuwa inachunguza na kumaliza uchunguzi kuhusu miamala ya kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow Benki Kuu ya Tanzania kwenda Benki ya Stanbc Tanzania.

Katika taarifa zote ambazo TAKUKURU inatoa kuhusu kesi za ufisadi, hakuna hata siku moja wanasema kuhusu uchunguzi huu na lini wahusika waliochota fedha za umma watafikishwa mahakamani. Naomba tupate kauli ya Serikali kuhusu jambo hili kwani ni moja ya JIPU kubwa ambalo tunadhani Serikali inalikimbia. 

Serikali inaogopa nini? Serikali inamwogopa nani? Kwanini kesi ya ufisadi wa IPTL unakaliwa kimya? Kwa maslahi ya nani?

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha
Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kigoma Mjini

Rais Magufuli Awasili Mkoani Dodoma Kwa Usafiri wa Gari

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma wakati akitokea mjini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukielekea Dodoma kutokea mjini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Picha 9 za Jeshi letu la JWTZ Likiwa Katika Uwanja wa Mapambano Huko Congo DRC

$
0
0
Hapa  kuna Picha Kadhaa za Wanajeshi wetu wa JWTZ  Wakiwa  katika  uwanja wa Mapambano katika Misitu ya Ben Congo DRC.

Juzi kati, jeshi letu limetunukiwa  medani na MONUSCO Kwa umahili wake

==>Habari hii,picha pamoja na video ni kwa hisani ya  mwandishi na correspondent wa ITV anayeripoti toka Congo ndg. Eshongulu Eshongulu Eshongulu

Hapa chini kuna video wakitunukiwa Medani na MONUCSO 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 29

Huduma Ya Treni Ya Abiria Kutoka Dar Kwenda Bara Kuanza Tena Jumapili Mei Mosi, 2016

$
0
0
Treni ya kwanza ya abiria ya Deluxe  kutoka Dar es Salaam kwenda bara itaondoka saa 2 asubuhi siku Jumapili Mei Mosi, 2016 kuelekea Kigoma.

Kuanza kwa safari hiyo kunatokana na kutengemaa kwa eneo korofi baina ya  stesheni za  Kilosa mkoani  Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Wakuu wa Idara za uendeshaji wa kampuni ya Reli Tanzania (TRL) iliyotolewa  Aprili  26, 2016 baada ya ukaguzi wa kina wa  eneo la Gulwe, imesema  sasa eneo hilo  linapitika  na kwamba tuta limeiamarika na kuwezesha treni zote za abiria na mizigo kupita kwa usalama kabisa.

Mara ya mwisho huduma za treni za abiria ya kawaida zilihamishiwa Dodoma mnamo Aprili 07, 2016.

Ratiba za safari treni ya kawaida kutoka Dar es salaam kuelekea Mwanza na Kigoma  ni kila siku ya Jumanne na Ijumaa saa 11 jioni ambayo imepangwa kuanza Jumanne Mei 3, 2016.Wakati treni ya  Deluxe inaondoka Dar es salaam kila Jumapili saa 2.00 asubuhi.

Na kutoka Mwanza na Kigoma treni ya kawaida inatoka huko kila siku ya Alhamisi na Jumapili saa 11.00 jioni kwa Kigoma na saa 12 jioni kwa Mwanza. Treni ya DELUXE  nayo inatoka  Kigoma au Mwanza kila siku ya Jumanne saa 2.00 asubuhi.

Wasafiri wote wanaombwa kufanya mipango  ya safari (booking) katika stesheni zetu husika na sio vinginevyo.

Aidha taarifa za uhakika kuhusiana na taratibu  za safari zetu za treni za abiria  na  mizigo  zinapatikana  katika vituo vyetu vyote vya TRL.

Uongozi wa kampuni  ya TRL  unawaomba radhi  wateja wake na wananchi kwa ujumla kwa usumbufu wowote uliojitokeza katika kipindi chote  hicho ambacho huduma zetu zilipokuwa zinaanzia na kuishia Dodoma badala ya Dar es salaam kama ilivyo kawaida.

Aidha Kampuni inashukuru jitihada za  Serikali pamoja na taasisi zake kadhaa   kufanikisha kurejesha hali ya miundombinu  ya reli  katika hali yake ya kawaida.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Aprili 28, 2016
DAR ES SALAAM

DC Wa Kinondoni Ally Hapi Aanza Mapambano Dhidi Ya Watumishi Hewa, Abaini 89 Waliolipwa Zadi Ya Sh Bilioni 1.331

$
0
0

Mkuu  wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema idadi ya watumishi hewa katika wilaya hiyo, imeongezeka hadi kufikia 89 wakiwa wamesababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni moja.

Aidha, Hapi amebaini uwepo wa watumishi vivuli 81 katika kada ya ualimu na hivyo kutoa siku saba kwa maofisa utumishi wa wilaya hiyo, kuhakiki watumishi vivuli ili kubaini idadi yao na hasara waliyosababisha.

Hapi aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, na kueleza kuwa awali wakati akiingia katika ofisi yake wiki iliyopita alikuta kuna watumishi hewa 34 waliokuwa wamesababisha hasara ya Sh milioni 512.

Alisema baada ya kufanya uhakiki zaidi walibainika watumishi hewa wengine 55 walioisababishia serikali hasara ya Sh milioni 619 na hivyo kufanya jumla ya hasara kuwa Sh 1,131,754,081.

“Bado uhakiki wa kina unaendelea ili kuhakikisha tunamaliza hili tatizo la watumishi hewa katika wilaya ya Kinondoni, awali walikuwa 34 lakini sasa wameongezeka 55 na kufikia 89,” alisema Hapi.

Akifafanua kuhusu watumishi vivuli, Hapi alisema watumishi hao ni wale ambao walihamishwa bila kufuata taratibu na hivyo kuendelea kupokea mshahara wa kazi yake ya awali badala ya kazi yake mpya.

Alisema walibaini kuwepo kwa walimu katika idara ya elimu ya msingi 42 ambao baada ya kufuatilia hawakuonekana katika shule yoyote ya wilaya hiyo.

“Kwa hiyo hili nalo ni tatizo kuna walimu wengine wanapokea mshahara mkubwa, lakini mtu alishahamishwa lakini anaendelea kupokea mshahara wa zamani ambao haufanyii kazi,” alisema.

Katika hatua nyingine, Hapi aliwataka wafanyabiashara ndogo ndogo walioko katika maeneo yasiyoruhusiwa kuondoka katika maeneo yasiyoruhusiwa baada ya siku saba alizotoa kukamilika.

Alisema agizo hilo alilitoa ikiwa ni sehemu ya kuweka Manispaa ya Kinondoni katika hali ya usafi ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya Rais John Magufuli ya usafi wa kudumu.

Spika Apangua tena Kamati za Bunge, Wabunge Wapinga

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko mengine ya kamati za Bunge kwa kuwaongeza wabunge wapya na kuwahamisha wengine kwenda kwenye kamati nyingine, jambo ambalo limepingwa na baadhi ya wabunge wakidai linapunguza ufanisi.

Juzi, Spika Ndugai (pichani) aliwaongeza wabunge wanne wapya walioapishwa bungeni Aprili 19, kwenye kamati za Miundombinu; Ardhi, Maliasili na Utalii; Kilimo, Mifugo na Maji; na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Hayo ni mabadiliko ya pili tangu Bunge la 11 lianze rasmi vikao vyake katikati ya Novemba mwaka jana, ikiwa ni kipindi kifupi cha mabadiliko ikilinganishwa na Bunge la Tisa na 10.

Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Bunge, mabadiliko hayo yamefanyika kwa mujibu wa kanuni ya 116 (3) na (5) ya Kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2016, ili kuhakikisha kila mbunge anakuwa mjumbe wa kamati mojawapo ya Bunge. 

“Aidha, mabadiliko haya ni kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kadri itakavyowezekana, Muundo wa Kamati za Kudumu za Bunge unazingatia aina za wabunge kwa jinsia, pande za Muungano na Vyama vya Siasa vyenye uwakilishi bungeni, ujuzi maalumu, idadi ya wajumbe kwa kila kamati na matakwa ya wabunge wenyewe,” inasema taarifa hiyo.

Baadhi ya wabunge jana walipinga mabadiliko ya mara kwa mara ya wajumbe wa kamati, wakieleza kuwa hayaleti tija na uamuzi huo haufanywi kwa umakini.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo), alisema mabadiliko hayo yanaonyesha namna ambavyo Spika Ndugai “anavyokosa umakini katika uundaji wa kamati hizo”.

“Spika hakuwa makini wakati anaziunda kamati hizo na sina jingine zaidi ya kusema, maana hilo liko wazi,” alisema Zitto.

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Mariam Msabaha alisema uundaji wa kamati kila mara, unatokana na kiongozi huyo kutokuwa na umakini na mara nyingi anafanya kazi kwa shinikizo la vikao vya chama.

Msabaha alisema utaratibu wa kuvunja kamati na kuziunda unatokana na vikao vya wabunge wa CCM, ambavyo humshauri Spika juu ya nini kifanyike ili waweze kuubana upinzani, ushauri ambao anadai wakati mwingine unakosa tija.

Mbunge wa Sengerema William Ngeleja (CCM) alisema mabadiliko yanayofanywa hayana madhara yoyote, kwa kuwa ni jambo la kawaida kufanya maboresho na kuwataka wabunge kujifunza kupitia mchezo wa mpira ambao kila mtu anakuwa na namba yake, lakini uwanjani anacheza namba zote.

“Waangalie mfano wa Profesa Makame Mbarawa ambaye alipewa Wizara ya Maji, lakini akaondolewa baada ya wiki tatu na kupelekwa kusimamia barabara ambako ameonyesha uwezo mkubwa, iweje kwa wabunge?” alihoji Ngeleja.

Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola alisema mabadiliko yanayofanywa hayawezi kuleta tija katika bunge hilo, kwani watu wanashindwa kujipanga vyema kwa kuwa hawajui kesho itakuwaje.

Lugola alihoji juu ya mafunzo waliyopata kila kamati, lakini wanabadilishwa bila utaratibu huku akisema hata kamati ya uongozi inaathirika zaidi, kwani wanapobadilishwa na kuondolewa wenyeviti lazima kamati ya uongozi ibadilike.

Spika Ndugai hakupatikana jana kueleza kwa kina mabadiliko hayo. Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alisema siyo msemaji na Ndugai na ndiye angepaswa kuulizwa jambo hilo.

Katika taarifa hiyo ya Bunge, Spika Ndugai aliwataka wajumbe wa kamati sita ambazo hazina viongozi kuwachagua mapema iwezekanavyo kama kanuni za Bunge zinavyohitaji.

Kamati hizo ni Hesabu za Serikali (PAC) Mwenyekiti; Kamati ya Nishati na Madini, (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti); Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti); Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti); Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (Mwenyekiti) na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Makamu Mwenyekiti.

CHADEMA Yatangaza Kutoshiriki Kura ya Maoni ya Katiba Mpya

$
0
0

DK. Vincent Mashinji Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema), amesema kuwa Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ndiyo msingi imara pekee unaoweza kuweka mifumo na taasisi kwa ajili ya maendeleo ya kweli yatakayogusa maslahi ya Watanzania wote badala ya nchi kuongozwa na kauli za viongozi.

Kutokana na umuhimu huo wa kuzingatia maoni ya wananchi yanayobeba matakwa yao katika mchakato wa Katiba Mpya, amesema kuwa Chadema hakitashiriki kura ya maoni ya Katiba Mpya Inayopendekezwa ambayo ilipitishwa na Bunge Maalum la Katiba baada ya kubadili na kuondoa mapendekezo yaliyotolewa na wananchi kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya.

Badala yake, Chadema kitaendelea kuweka agenda ya kupigania Katiba Mpya na bora katika vipaumbele vyake, kwa sababu itatibu vidonda na kumaliza makovu yaliyoko katika jamii kutokana na matatizo mbalimbali kama vile ukosefu wa haki, migogoro ya ardhi, wananchi kukosa huduma za msingi za kijamii zikiwemo elimu, maji na afya.

Dkt. Mashinji aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipoukaribisha ujumbe wa Chama cha Centre Party cha Norway uliofika ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutia saini makubaliano ya ushirikiano kati ya vyama hivyo kwenye Mradi wa Elimu ya Demokrasia awamu ya pili unaofanyika Wilaya ya Mtwara Vijijini.

Dkt. Mashinji pia amekishukuru chama hicho kwa kusaidia kutoa elimu ya uraia kwa Watanzania hususani maeneo ya vijijini katika mradi ambao unahusisha vyama vyote vya siasa vyenye uwakilishi ndani ya Bunge, huku akisisitiza kuwa Chadema kiko tayari kwa ushirikiano unaozingatia maslahi na matakwa ya wananchi hasa katika kukuza uelewa wa kudai haki, demokrasia na uongozi bora ndani ya nchi.

“Suala la Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi kama ilivyowasilishwa kwenye rasimu ya pili na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ni agenda muhimu kwa Watanzania wapenda nchi yao na sisi ni kipaumbele kwa mwaka huu na kuendelea hadi hapo nchi yetu itakapopata Katiba Mpya ya Wananchi.

“Jana na leo tumewasikia baadhi ya viongozi wa serikali wakisema kuwa wanajiandaa kuitisha kura ya maoni…hatutashiriki kura ya maoni ya Katiba Mpya Inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba. Tunajua Watanzania wengi wanataka Katiba Mpya iliyotokana na maoni yao, si ile iliyochakachuliwa bungeni.

“Katiba Mpya iliweka masuala kuhusu haki za wananchi, kuimarisha misingi na kuweka mifumo ya demokrasia na uongozi bora, walau kwa kuanzia. Hatuwezi kusema sasa tutatumia mikakati gani kuwahamasisha Watanzania kuidai Katiba Mpya…tutajua namna ya kuvuka tukishafika mtoni,” Alisema

Aidha, Katibu Mkuu Dkt. Mashinji alisisitiza kuwa suala la nchi kuwa na misingi na mifumo imara ya demokrasia na uongozi bora ni muhimu kwa Tanzania, katika wakati ambapo nchi inaelekea kwenye uchumi mkubwa wa nishati ya gesi na mafuta, akisema vinginevyo ni hatari iwapo taifa lenye utajiri mkubwa wa rasilimali, litaendelea kuwa na wananchi waliokata tamaa kutokana na mfumo mbovu uliopo.

Kwa upande wake ujumbe huo uliokuwa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Centre Party, Knut Olsen, ulisema kuwa chama hicho kinashukuru kwa mradi huo kuingia katika hatua ya pili kuanzia mwaka 2016-2019 huku hatua ya kwanza ikiwa na mafanikio makubwa katika jamii ya wananchi wa maeneo ya pembezoni.

“Kama unavyojua, mradi huu kupitia TCD unahusisha vyama vyote vyenye uwakilishi ndani ya bunge, na lengo letu ni kuwajengea uwezo viongozi wa vyama hasa wanawake na vijana katika ngazi ya jamii kwenye vitongoji, vijiji, kata na bunge ili waweze kushiriki mchakato wa maamuzi. Tunatarajia kuendelea kupata ushirikiano katika hatua ya pili,” alisema Inger Bigum, ambaye ni Meneja wa Mradi hapa nchini.

Wengine waliokuwa katika ujumbe huo wa Centre Party ni pamoja na Vijana Sara Hamre Katibu Mkuu wa, Katibu Mkuu wa Wanawake, Eline Stokstad-Oslan na Kristin Madsen Katibu Mkuu wa Wazee.

Mradi huo wa Elimu ya Demokrasia katika Wilaya ya Mtwara Vijijini unaohusisha vyama vyenye uwakilishi bungeni kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) chini ya ufadhili wa chama hicho, katika awamu ya kwanza ulihusisha kata za Msangamkuu, Nanyamba, Ziwani na Mbembaleo na katika sasa awamu ya pili utakuwa katika kata za Mkunwa, Tangazo, Mayanga na Madimbwa.

Trump Achekwa Baada Ya Kushindwa Kulitamka Jina la Nchi yetu Tanzania

$
0
0

Mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani ambaye amekuwa akiongoza kwenye kinyang’anyiro hicho, Donald Trump amejikuta akikosolewa vikali kuhusu upeo wake juu ya sera za nje pale aliposhindwa kulitamka bayana jina la Tanzania.

Drump ambaye Jumanne aliyopita alivuna ushindi wa kishindo kwenye majimbo yote manne yaliyopiga kura za mchujo alijikuta akitumbukia kwenye kadhia hiyo wakati akielezea vipaumbele vya Marekani kuelekea mataifa ya kigeni.

Alikuwa akigusia juu ya mashambulizi ya mabomu yaliyotokea katika ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na Kenya na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali huku watu kadhaa wakipoteza maisha.

Akiwa katika hali ya kujiamini, Trump alisema kuwa iwapo ataingia madarakani moja ya vipaumbele vyake ni kuendelea kutetea masilahi ya Marekani na kudhihirisha hilo aliamua kutolea mfano mashambulizi hayo ya kigaidi.

Lakini wakati akilitaja jina la Tanzania, mfanyabiashara huyo alijikuta akigusa hisia za wengi pale alipolitaja jina hilo kinyume na inavyotamkwa.“ Ona mashambulizi yaliyotokea katika miaka ya 1990 katika ubalozi wetu nchini Tan-ZAY-nee-uh”.

Matamshi hayo yalizusha mjadala mkubwa huku baadhi ya wakosoaji wake wakiingia kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kumuelezea kama ni mtu asiyekuwa na upeo mkubwa kuhusu siasa za kimataifa.

Baadae kambi ya kampeni ya Trump ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikisema kuwa kuteleza kwa mgombea wao katika matamshi ya jina halisi la Tanzania hakumaanishi kuwa uwezo wake kuhusu masuala ya usalama,diplomasia ya kimataifa na biashara ya kimataifa ni wa kutiliwa mashaka.

Serikali Yashauriwa Kuwa na Hisa Kwenye Kampuni za Madini ili Kujua Mapato halisi Yanayoingizwa na Wawekezaji wa Kigen

$
0
0
Serikali imeshauriwa kuwa na sehemu ya umiliki katika kampuni zinazochimba madini na gesi ili kujua mapato halisi yanayoingizwa na wawekezaji wa kigeni. 

Aidha, imeshauriwa kuzilazimisha kampuni hizo kurejesha nchini asilimia 60 ya mauzo yake, ili kuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, pamoja na kuimarisha Shilingi ya Tanzania.

Ushauri huo ulitolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyestaafu, Ludovick Utouh pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji wa Uwazi katika mapato ya Madini, Gesi na Mafuta (EITI), Jaji mstaafu Mark Bomani, wakati wa uzinduzi wa ripoti za kamati za mwaka 2013 na 2014 uliofanyika jana Dar es Salaam.

Akizindua ripoti hizo, Utouh alisema, Tanzania haijafaidika na rasilimali za madini, jambo lililosababishwa na kujiondoa kufanya biashara, hivyo kuzipa mwanya kampuni za kigeni kuendesha biashara bila uwazi kuhusu mapato zinazoyapata kutokana na mauzo ya madini.

“ Serikali iliangalie jambo hili na kulirekebisha, Serikali ya Botswana ina hisa kwenye migodi hiyo, hivyo wanakuwa na mwakilishi kwenye bodi jambo ambalo linakuwa rahisi kufuatilia mapato yanayopatikana, lakini sisi hapa tulijiondoa kwa madai kuwa Serikali haifanyi tena biashara,” alisema Utouh.

Alisema, Serikali ikifanya hivyo itaweza kupata mapato mengi zaidi kuliko ilivyo sasa, ambapo imejiondoa kabisa katika umiliki wa migodi ilhali rasilimali hizo ni za Watanzania.

 “Wawekezaji wanakuja na fedha na utaalamu, lakini sisi cha kwetu ni rasilimali, ni lazima tugawane nao na tuwe na mwakilishi kwenye bodi, badala ya kusubiri mrabaha unaotokana na faida anayopata mwekezaji. Huu utaratibu wa kuwaachia kila kitu sio mzuri,” alisema Utouh.

Naye Jaji Bomani alisema, Serikali inatakiwa kuzilazimisha kampuni zinazochimba madini nchini kurejesha asilimia 60 ya mauzo yake ili kuimarisha akiba ya fedha za kigeni. Alisema, kwa kufanya hivyo, Shilingi ya Tanzania itaimarika.

Alisema, hatua hiyo ikichukuliwa, sekta ya madini itakuwa imetoa mchango wake kwa pato la Serikali, licha ya kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo. 

Alitaja moja ya changamoto hizo kuwa ni kupanua wigo wa wachimba madini kama vile wachimbaji wa kati na ambao pato lao linazidi Sh milioni 200, kwa mwaka ambao, alisema wanastahili kutoa mchango kwa pato la Serikali.

Alisema mpaka sasa ni kampuni kubwa tu zinahusika, lakini akasema umefika wakati wachimbaji wa kati nao waingizwe kwenye utaratibu huo. 

Alipendekeza kuwa umefika wakati sekta ya madini ipanuliwe hadi kwenye uchimbaji wa makaa kuiwezesha nchi kufaidika zaidi na shughuli za rasilimali hiyo, ambayo inaweza kuwa na manufaa makubwa kwa nchi.

EITI ni shirika la kimataifa ambalo liliundwa mwaka 2002 na nchi mbalimbali zenye sekta ya madini. Linafanya ufuatiliaji juu ya sekta ya madini na gesi na kuona kama kuna uwazi katika biashara yake.

Tanzania ilijiunga na shirika hilo mwaka 2009. Kazi kubwa ya kamati iliyoundwa kushughulikia shughuli hizo hapa nchini ilikuwa ni kukusanya taarifa juu ya malipo ambayo kampuni za madini zilikuwa zinalipa serikali ya Tanzania na kuzilinganisha na mapato ambayo yalikuwa yamepokelewa serikalini na kutoa taarifa kila mwaka.

Rufaa Kupinga Kuachiwa Huru Abdallah Zombe na Wenzake kusikilizwa Leo

$
0
0
Abdallah Zombe (kushoto) akiwa na wakili wake, Richard Rweyongeza katika Mahakama ya Rufaa, Dar es Salaam
****
Mahakama ya Rufaa leo inatarajiwa kusikiliza rufaa ya kupinga kuachiwa huru kwa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na askari wenzake wanane waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji.

Rufaa hiyo inatarajiwa kusikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Bernard Luanda, wengine ni Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles Kaijage. 

Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), alikata rufaa mwaka 2013, akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliyowaachia huru Zombe na wenzake, baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi ya mauaji ya watu wanne iliyokuwa inawakabili.

Katika rufaa hiyo, DPP anadai kuwa Jaji Salum Massati alikosea kuwaachia huru washitakiwa hao kwa sababu kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani wote. 

Mbali na Zombe, wajibu rufaa wengine ni ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, Konstebo Jane Andrew, Konstebo Emanuel Mabula, Konstebo Michael Shonza, Koplo Abeneth Salo, Koplo Rajabu Bakari na Koplo Festus Gwabisabi.

Katika kesi ya msingi inadaiwa Januari 14, 2006, katika msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis, Dar es Salaam Zombe na wenzake waliwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Morogoro, Mathias Lunkombe, Sabinus Chigumbi na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, pamoja na dereva teksi Juma Ndugu.

Baada ya kusikiliza kesi hiyo, Agosti 17, 2009, Jaji Massati aliwaachia huru washitakiwa kwa kuwa upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao bila kuacha shaka na Mahakama ikiwaona hawana hatia kwa makosa yaliyokuwa yanawakabili.

Oktoba 6, 2009, DPP alikata rufaa Mahakama ya Rufani, akipinga hukumu hiyo kwa madai kuwa Jaji Massati alikosea kuwaachia huru washtakiwa hao, pia kulikuwa na ushahidi wa dhahiri na wa kimazingira unaotosha kuwatia hatiani washtakiwa wote.

Hata hivyo Mei 8, 2013 Mahakama ya Rufaa ilitupilia mbali rufaa hiyo kutokana na dosari za kisheria zilizobainika kwenye rufaa, lakini DPP alipeleka maombi Mahakama Kuu ili aruhusiwe kukata tena rufaa nje ya muda. 

Mahamaka Kuu ilikubali maombi yake, akakata tena rufaa inayotarajiwa kusikilizwa leo.

Naibu Spika Achafua Hali ya Hewa Bungeni Baada ya Kumwita Mbunge BWEGE

$
0
0

Naibu Spika Tulia Ackson, ambaye katika vikao vya Bunge anatakiwa kusimamia mijadala kwenye chombo hicho cha kutunga sheria, jana alizua kizaazaa baada ya kumuelezea mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Selemani Said Bungara kuwa ni bwege, akimtaka aache kuonyesha hali hiyo.

Kwa mujibu wa toleo la pili la Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Oxford) la mwaka 2004, neno bwege linamaanisha “mtu mjinga, mpumbavu, bozi, fala gulagula”.

Kitendo cha kutumia neno bwege kumuelezea mbunge huyo kilisababisha wapinzani wacharuke, na kuibua bungeni kesi ya mtu aliyefunguliwa mashtaka mkoani Arusha kwa kosa la kumuelezea Rais John Magufuli kuwa ni bwege.

Bila ya kuruhusiwa, mmoja alifungua kipaza sauti na kusema: “Hatimaye msamiati wa bwege watua bungeni sasa kutumika rasmi. Futa lugha ya kuudhi; bwege bwege.”

Hata hivyo, wabunge hao wa upinzani hawakushinikiza Dk Tulia kufuta kauliz yake, lakini baadaye wakiwa nje ya ukumbi waliponda kitendo hicho cha kiongozi huyo wa Bunge ambaye aligombea uspika kwa tiketi ya CCM kabla ya kujitoa na muda mfupi baadaye kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa mbunge na hivyo kupata sifa ya kugombea nafasi hiyo ya naibu spika.

Dk Ackson aliamsha tafrani hiyo saa 5:48 asubuhi baada ya Bungara, ambaye ni maarufu kwa jina la Bwege, kusimama bila kufuata kanuni za Bunge, kupinga maelezo ya Waziri wa Habari, Nape Nnauye juu ya uamuzi wa Serikali kusitisha shughuli za Bunge kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni nchini.

“Na wewe Mheshimiwa Bwege, hebu kaa chini. Usionyeshe ubwege wako hapa,” alisema Dk Ackson kumzuia mbunge huyo asiendelee kuzungumza wakati mjadala ukianza kuwa mkali.

Mjadala huo uliendelea bila ya wapinzani kuhamaki, lakini baada ya Nape kutoa taarifa akieleza kuwa uamuzi wa kuanzisha studio za Bunge ulifanywa na Bunge la Kumi ambalo yeye hakuwamo, ndipo wapinzani walipokumbusha kauli hiyo ya naibu spika.

“Bunge linaonyeshwa asubuhi na kurudiwa kuonyeshwa usiku na kuna wanahabari hapa Dodoma wana kamera zao na wanaripoti bunge hili. Tusitumie bunge hili kupotosha,” alisema Nape kabla ya mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kuingilia kati.

Msigwa: Hii ni taarifa au hotuba? 
Spika: Msigwa jifunze kusikiliza kwanza, unaipokea taarifa yake ama vipi?

Msigwa: Taarifa yake naikataa kwa sababu anasema uongo. Leo na wewe umemuita mtu bwege. Kuna mtu kule Arusha alimuita Rais Magufuli bwege na akapelekwa mahakamani. Na wewe tutakupeleka mahakamani.

Mkazi huyo wa Arusha, Isaack Habakuk Emily alipandishwa kizimbani takribani wiki mbili zilizopita akikabiliwa na shtaka la kumuita Rais kuwa ni bwege.

Msigwa alisema Bunge “nalo ni jipu” kwa kuwa haliwezi kuishauri Serikali kutokana na kufanya maamuzi bila ya kushirikisha makamishna wake, akitoa mfano wa chombo hicho kurejesha Sh6 bilioni serikalini ambazo zilibanwa kwenye matumizi yaliyoelezewa kuwa hayakuwa muhimu.

Baada ya Msigwa kumaliza kuchangia, alifuatia mbunge wa viti maalumu (Chadema), Tunza Malapo ambaye aliungana kauli na Msigwa na kumponda Nape na uamuzi wa Serikali.

Wakati Malapo akiendelea kuchangia, alisimama Khatibu kutoa taarifa.

“Kwa taarifa yako wewe Malapo aliyelishauri Bunge kutorushwa live ni Nape vuvuzela,” alisema.

“Kwani kuanzisha studio za Bunge maana yake ni Bunge kutorushwa moja kwa moja?”

Wakizungumzia tukio hilo la asubuhi, mbunge wa Kalenga (CCM), Godfrey Mgimwa alisema Dk Tulia alighafilika wakati akitoa kauli hiyo baada ya kurushiwa maneno mara kwa mara na wabunge wa upinzani, tena bila kufuata kanuni na taratibu za kibunge.

“Kwanza mtu mwenyewe (Bungara) huwa anapenda kuitwa bwege sasa kama ukiamua kumuita bwege utakuwa umekosea?” alihoji.

Alisema mara nyingi huibuka mvutano bungeni kwa sababu baadhi ya wabunge hawataki kuzingatia kanuni za chombo hicho cha kutun ga sheria.

Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Antony Komu alisema: “Kauli iliyotolewa na Naibu Spika inaonyesha wazi kuwa ni kiongozi anayekiuka misingi, taratibu na kanuni za Bunge. Tazama anatukana watu tu bila kujali jambo lolote, hii si sawa kabisa.”

Alisema Bunge linapaswa kuongozwa kwa haki na si kama ilivyo sasa ambayo inawafanya wabunge wa CCM waonekane kuwa na haki zaidi ya upinzani.

“Mfano (mbunge wa Tarime Vijijini-Chadema, John) Heche aliomba mwongozo akanyimwa ila Dk Kigwangalla akapewa,” alisema.

Kwa takribani wiki moja Bunge lilikuwa limepoa kutokana na wabunge wa vyama vya upinzani kususia kuchangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, lakini jana walishiriki kwenye mjadala wa wizara ya Ofisi ya Rais na kurejesha uhai kwenye chombo hicho.

Katika hoja zao jana, wabunge hao walijikita zaidi kuponda Serikali ya Awamu ya Tano kuwa inakiuka kanuni za utawala bora na kupinga uamuzi wake wa kusitisha matangazo ya Bunge, jambo lililomlazimu Nape kusimama mara kwa mara kutetea uamuzi wa Serikali, huku Dk Ackson akitoa ufafanuzi wa kanuni za Bunge.

Mara zote ambazo Nape na Dk Ackson walikuwa wakitoa ufafanuzi wao, walizomewa na wabunge hao wa upinzani huku mbunge wa Konde (CUF), Khatibu Said Haji akimfananisha Nape na “vuvuzela” kwa maelezo kuwa ndiye aliyeishauri Serikali kusitisha matangazo hayo. 

Akichangia mjadala huo, Mchungaji Msigwa alisema utawala bora na unaozingatia sheria hauanzi na bajeti, bali huanza na utawala bora.

“Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, dhana nzima ya utawala bora haionekani. Utawala bora ni kuongoza nchi kwa ufanisi, tija na kwa uwazi, uadilifu, uwajibikaji na ushirikishwaji wa watu kwa kufuata utawala wa sheria,” alisema.

Alisema ni ajabu Ofisi ya Rais-Utawara Bora kuomba bajeti ya Sh800 bilioni wakati nchi haina utawala bora. Alirejea kauli ya kiongozi wa upinzani bungeni, Freeman Mbowe kuwa Serikali inaongozwa bila ya maamuzi yake kuwekwa kwenye Gazeti la Serikali.

“Walikuwa wanafanya kazi kama sisi tu mawaziri vivuli wa upinzani.Wanatoa maagizo wakati hawapo kisheria. Huu si utawala bora,” alisema Mchungaji Msigwa.

Alisema licha ya jambo hilo kubainika wazi Bunge lilikaa kimya huku akidai kuwa hata baadhi ya mawaziri walikuwa wanajua jambo hilo, na kwamba wanapokuwa nao katika mgahawa wa Bunge, wamekuwa wakiponda na kuukosoa utendaji kazi wa Serikali ya Rais Magufuli.

“Mawaziri mnakuwa kama vinyonga. Kwenye chai mnasema ukweli, mkija bungeni mnakaa kimya.Huwa tunawarekodi na mkibisha tutataja mmoja mmoja humu ndani,“ alisema Msigwa huku akimtaja Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla kuwa ni mmoja wa mawaziri hao baada ya waziri huyo kusimama kuomba mwongozo, kupinga kauli ya mbunge huyo.

Dk Kigwangalla alitumia kanuni 68 (7) na 63 (1) kuomba mwongozo, akimtaka Mchungaji Msigwa athibitishe kauli yake kwa kuwataja kwa majina mawaziri wanaopingana na uongozi wa Serikali.

Dk Ackson naye alitoa ufafanuzi akinukuu kifungu cha 63 (1) (2), kinachomtaka mbunge kuthibitisha jambo analolisema hapohapo ama apewe muda na kwamba atatoa maelezo ya kuwataka Dk Kigwangalla na Mchungaji Msigwa kuwasilisha ushahidi wao.

Msigwa: Mbona Kigwangalla unajihisi mwenye hatia? 
Dk Ackson: Msigwa unaongea na kiti usibishane na mbunge.

Msigwa: Mheshimiwa Spika wakati wa kuchangia tunakuwa na taarifa sio mwongozo ila nashangaa huyu (Dk Kigwangalla) kaomba mwongozo kapewa. Ila tunaendelea tu ila kiti bado kinayumba.

Dk Ackson: Mbunge anaweza kukosea na wengi tu hukosea. Ametaja kanuni zinazohusu utaratibu naomba tusiendelee kujibizana.

Akiendelea na mjadala huo Mchungaji Msigwa alisema Bunge la Tisa na la Kumi yaliendeshwa kwa uwazi mkubwa tofauti na Bunge la Kumi na Moja, kwamba hata utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne ulikuwa haubani demokrasia na kuzuia matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja.

“Bunge ni mkutano wa wazi wa wananchi wote, lakini Serikali hii inaanza kuminya na kuweka siri. Huu si mkutano wa unyago, tunaongelea matumizi ya fedha za Watanzania,” alisema.

“Serikali inayokandamiza uwazi ni Serikali iliyojaa uoga na inayoficha madudu. Mnasimama na kusema mnakusanya fedha za kuvunja rekodi sasa mnaficha nini kuwaonyesha Watanzania hiki mnachokifanya?”

Huku akiipongeza Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Mchungaji Msigwa alisema pamoja na udhaifu wake, ilikuwa haizuii watu kuzungumza na kusema ukweli.

“Nyinyi mmekuja na ‘hapa kazi tu’, lakini hamtaki kukosolewa. Wakati tunamkosoa Kikwete wabunge wa CCM mlikaa kimya na kutuzomea, leo mnaufyata na inaonekana hata Dk Magufuli akidondosha kijiko, mtasimama na kupiga makofi kwa sababu ya uoga wenu,” alisema Mchungaji Msigwa na kuwataka wabunge kuhoji mambo kwa maslahi ya wananchi. 

Mfanyabiashara Auawa gesti Kwa Kuchomwa Kisu

$
0
0

Mfanyabiashara wa mazao, Eliusta Peter(40),   amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni akiwa katika  nyumba ya kulala wageni wilayani Kilombero.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema tukio hilo lilitokea   Aprili 22  baada ya  wahudumu wa nyumba  ya wageni ya  Sayari kubaini   maiti katika chumba namba mbili.

Inadawa Aprili 20 mwanamke huyo  akiwa na kijana mmoja ambaye  jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi, walifika kwenye nyumba hiyo na kuchukua chumba kimoja wakisema  wao ni wafanyabiashara wa mazao.
 
“Mwili wa marehemu uligundulika ukiwa kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Sayari chumba namba mbili   saa 11 jioni na ulipochunguzwa ikagundulika kuwa kifo kilisababishwa maumivu ya jereha,”alisema Matei.

Mwanamke huyo  alikuwa na jeraha   kushoto mwa bega lake lililotokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali

Matei  alisema kwa taarifa walizozipata  bila shaka kijana aliyekuwa naye  anahusika na mauaji hayo.

Wakati huo huo, jeshi la polisi wilayani Kilosa limemkamata Rogasian Jeremia kwa tuhuma za kumshambulia mkewe,   Faustina Sizayi(25) kwa kumkatataka kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mtuhumiwa alikamatwa akiwa anajihusisha na kazi ya ulinzi wa maduka baada ya polisi kumsaka kwa muda mrefu na ndipo Aprili  24  alikamatwa  baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

UVCCM Wamtaka Fredrick Sumaye Amwache Rais Magufuli Afanye Kazi Yake

$
0
0
Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umesema Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe na uwezo wa kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali na masuala ya utawala.

Sumaye ametakiwa amuache Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Magufuli ili atimize majukumu yake kwa sababu alipewa dhamana ya kuwa Waziri mkuu lakini hakufikia hata theluthi ya utendaji unaofanyika sasa.

Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa ccm wa kata mbili za kwandele na mbichi jimbo la Rombo mkoani kilimanjaro.

Shaka alisema anachokifanya Sumaye na baadhi ya wanasiasa muflis wanaojaribu kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni kutaka nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani wananchi wameyasahau.

Alisema kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika utendaji na usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais hakuna atakayempita Sumaye.

Aidha Kaimu huyo alimuonya Sumaye kuacha kumfuatafuata Dk Magufuli katika mikakati yake ya kutumikia nchi na juhudi anazozichukua dhidi ya mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma nchini.

Alisema wakati Rais Magufuli akiwa katika dhamira njema na nia ya wazi kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na heshima  kina sumaye na wenzake wafumbe midomo yao na waache mara moja kumbughudhi Rais kwa ajili ya kusaka umaarufu wa kisiasa.

Pia shaka aliwataka wananchi wa jimbo la Rombo kujitayarisha ili kumpiga chini mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chadema Joseph Selasini kwa sabahu ni dhaifu na hatoshi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.

"Siku zake za kuitwa mbunge wa Rombo sasa zinahesabika, Selasimi hajui anachokifanya wala hajali shida na matatizo yaliopo katika jimbo lake,lazima adui huyo apigiwe mwaka 2020 "alisisitiza shaka

Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Juma Raib Juma aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini kuacha mara moja tabia ya kushiriki na kuchagua vyama na wagombea wa nafasi mbali mbali kwa ukabila, ujimbo au nasaba.

Raibu alisema ikiwa wananchi wa kaskazini sasa wanaishi katika Mikao yote ya Tanania, si jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni wabaguzi kwa misingi ya asili au ujamaa.

"Tunachotaka kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya Kaskazini ni kumuasi baba wa Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere, hakutuacha tukiwa tumegawanyika , tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa ukabila au udini, chadema acheni kwasabahu hilo ni balaa au janga katika jamii "alisema Raib.

Jumla ya wanachama wapya 103  walijiunga na chama cha mapinduzi pia shaka alipata nafasi ya kuangalia mechi ya soka kati ya timu za kata za makiidi na mahare wilaya ya Rombo.

Bosi wa Zamani wa TRA na Wenzake Wawili Warudishwa Tena Rumande Hadi Tarehe 3 Mwezi Ujao

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imesita kutoa uamuzi wa kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni kwa madai, jalada lake limeitishwa Mahakama Kuu.

Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.

Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu amesema kuwa, hana mamlaka ya kutolea uamuzi wa kesi hiyo kutokana na jarada lake kuitishwa Mahakama Kuu leo asubuhi.

Kutokana na hali hiyo Hakimu Mchaura amesema kwamba, kesi itatajwa tena tarehe 12 Mei mwaka huu na watuhumiwa watarudishwa rumande.

Muda mfupi baada ya hakimu Mchaura kusema  hivyo, Kitilya na wenzake  walirudishwa tena mbele ya Hakimu  huyo  baada ya hakimu kupata amri kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akimtaka kesi hiyo itajwe Mei 3, mwaka huu badala ya tarehe 12 Mei mwaka huu aliyoipanga awali.

Hakimu Mchauru amesema, sababu za kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi itatajwa tena tarehe 3 Mei mwaka huu na yale yaliyozungumzwa asubuhi yatabaki kama ilivyo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya April 30

sponsored post: Fahamu Kuhusu Misukule Wa Maofisini Na Jinsi Ya Kujikinga Usifanywe Msukule Wa Ofisini

$
0
0

Na. Dokta  Mungwa  Kabili...0744  000 473

SWALI : Mtaalamu, kwa  heshima  na  taadhima  ninaomba  unisaidie  suala  langu. Mimi ni  mwanamke  mkaazi  wa  manispaa  ya  Nyamagana, jijini  Mwanza,  umri  wangu ni  miaka  37, mume  wangu ana  miaka  45 sasa.  Tangu  tumefunga  ndoa, huu  ni  mwaka  wa  kumi na  tano.  Mimi   nina jishughulisha  na  biashara  ya  ufundi cherehani. Mume  wangu amesoma hadi  Chuo  Kikuu, amesomea  mambo ya  kompyuta.
 
Tangu mwaka  2000  mume wangu  amekuwa  akifanya  kazi  kwenye  Internet  Café ya  Muhindi . Hela  anayo  lipwa kidogo sana, na  kutokana  na  uchapaji  kazi  wake, kampuni  nyingi zimekuwa  zikimfuata  zikitaka  kumuajiri tena  kwa  kulipa  hela  nyingi  zaidi  ya zile  anazo lipwa  kwa  huyo tajiri muhindi.
Unyayo

Lakini  cha  kushangaza mume  wangu  amekuwa  akiwakatalia. Maisha  tunayo  ishi hayaridhishi hata kidogo, tunazidiwa  mpaka  na  vijana  wadogo  walio anza  maisha  juzi tu. Nikimwambia  mume  wangu, atafute  sehemu  yenye  maslahi, anakataa. Nikiwambia  tutunze  hela, afungue  nay eye  internet  café yake, anakataa  pia, yeye  amekazana  na  kumtumikia  huyo  muhindi.

Siku moja  nikiwa  naongea  na  shoga  yangu  mmoja, akaniambia  inawezekana  mume  wangu  atakuwa  amefanywa  msukule  wa  ofisini  na  huyo  bosi  wake  muhindi.  Eti  mtaalamu, hivi  ni  kweli, jambo  hilo  linawezekana kwamba  kweli  mume  wangu  amefanywa  msukule  wa  kazi  na  bosi  wake ?  kama  ni  kweli ninamtoaje  kwenye  huo  utumwa ?

DR. MUNGWA  KABILI  ANAJIBU.
Pole  sana  dada  angu  kwa  madhila  yaliyo mkuta  mume  wako.   Ni kweli  kabisa, wapo misukule  wa  ofisini.  Uchawi  huu, hufanywa  na  wamiliki  wa  kampuni  na  biashara  mbalimbali. Walengwa  wakuu  wa  uchawi  huu  ni  kwanza wafanyakazi  wachapakazi   walio  na  weledi  wa  kazi  husika, na  pili wafanyakazi  ambao  nyota  zao  zinaendana  na  biashara  husika.

Wapo  misukule  wa  aina  mbili. Misukule  wanao  onekana  kwa  macho  ya  nyama, na  misukule wasio  onekana.
 
Misukule wasio  onekana  ni watu  wanao  dhaniwa  kufa, lakini  kiukweli  wanakuwa  hawajafa, isipokuwa  wanakuwa  wamechukuliwa  kichawi.
 
Ilihali  misukule  wanao  onekana, ni  watu  wanaoishi  kama  watu  wengine, lakini  nyota  zao zinakuwa  zimechukuliwa  na  wachawi  kwa matumizi  yao  binafsi (wachawi ) na  pia  nafsi.

KUFAHAMU  KWA  UNDANI  KUHUSU  MISUKULE  WASIO  ONEKANA, TAFADHALI TEMBELEA :

Misukule wa  maofisini  wapo  katika  kundi  la  misukule  wanao  onekana .  Watu  hawa hupumbazwa kufungwa  kichawi  na  kufanywa  watumishi  wa  walio  wapumbaza, kwa  kadri  walivyo  nuiziwa.  Wapo  walio nuiziwa  kuwatumikia  mabosi  wao kwa  miaka kumi, wengine  ishirini, wengine  thelathini  na w engine  katika  maisha  yao  yote.
 
Msukule  huyu  anaweza  kuwa  bar maid, meneja  wa  bar, House  Girl, House  Boy, Mkata  majani, mkurugenzi  wa  kampuni kubwa, Mwalimu, daktari,mwanasheria, fundi wa  magari, Mtayarishaji  wa  muziki, muuza  mayai, au  Ice  Cream  nakadhalika.

JINSI  MISUKULE  WA MAOFISINI  WANAVYO  TENGENEZWA.
Ili kumtengeneza mtu na  kumfanya  awe msukule  wa  ofisi mambo  yafuatayo  hufanyika.
 
Kwanza  zinachukuliwa  nyayo  zake, kisha  zinafungwa  kwenye  kitambaa  cheusi  pamoja  mchanganyiko wa  miti  ya  kichawi ya  aina  arobaini  na  dua  maalumu  ya  kumfunga  muhusika.

Pili  linachimbwa  shimo lenye  urefu  wa  futi  saba, ndani ya  shimo hilo inafanyika  kafara  ya PUNDA  MWENYE  ALAMA  YA  MSALABA  MGONGONI  na  kondoo  mwenye  rangi  nyeusi  bila  doa  lolote, halafu nyayo  za  mtu   huyo  zilizo  fungwa  kwenye  kitambaa  cheusi zikiwa pamoja  na  miti  arobaini  ya  kichawi na  dua  yake, vinatupiwa  kwenye  shimo  hilo  huku  maneno  Fulani  ya  kichawi  yakitamkwa.

Baada  ya  hapo  litachukuliwa jiwe  lenye uzito  unao endana  na  idadi  ya  miaka  ambayo  mchawi  anataka  kumtumikisha  muhusika.

Kama  anamtaka  kwa  mwaka mmoja, basi  jiwe  huwa  na  uzito  wa  kilo  moja, kama  ni  miaka  kumi  basi  jiwe  huwa  na  uzito  wa  kilo  kumi, kama  ni  miaka  thelathini, basi  mawe  yawe  na  uzito  wa  kilo  thelathini, na  kama  anataka  kumtumikisha  maisha  basi  ataweka mawe  yenye  uzito wa  kilo  hamsini hadi  miaka. Mawe  hayo  hukandamiza hicho  kitambaa.

Baada  ya  hapo shimo  hilo  litafukiwa  kwa  udongo  wa makaburini. Mambo  haya  yakisha fanyika, utachukuliwa  mchanga wa  kwenye  kivuli cha muhusika, utachanganywa  na  dawa nyingine  za  kichawi  ambazo idadi  yake  ni  tisa, vitu vitafungwa  kwenye  kitambaa  cheusi, na  kuhifadhiwa  kwenye  kibuyu  au  chungu cheusi  chenye  dawa  za  kichawi  kwa  siku  saba, baada  ya  hapo  atachukuliwa  kuku  mweusi  ambaye  ataunguzwa  kwenye  chungu  cheusi  akiwa  mzima  hadi  awe majivu.

Majivu  hayo, yatagawanywa mara  mbili, kisha  fungu la kwanza  atalishwa  PUNDA  MWENYE  ALAMA  YA  MSALABA  MGONGONI  na  kisha  atazikwa  akiwa mzima  mzima, na  fungu  la  pili  atalishwa  kondoo  mweusi   na  kuzikwa  akiwa  mzima  mzima.

Baada  ya  hapo  litafanyika  tambiko  jingine  la kafara  ya  PUNDA  MWENYE  ALAMA  YA  MSALABA  MGONGONI  na  kondoo mweusi.

Kabla  ya  kuchinjwa  kondoo  pamoja  na  punda  hao  watalishwa  dawa  fulani  za  kichawi, na  baada  ya  kuchinjwa nyama  ya  punda  na  kondoo  watakao  tolewa  kafara, itatumika  kumlisha  mtu  au  watu  walio  kusudiwa. Mara  nyingi  huwa  kwenye sherehe, hafla, au  anaweza  kukuita  nyumbani  kwake, kisha  nyama  husika  ikawa  kitoweo chako.
 
MTU  AKIFANYIWA  ULOZI  HUU, HUWA  MTUMISHI  MTIIFU   KATIKA  MAISHA  YAKE  YOTE.  AINA  HII  YA  ULOZI  HUTUMIKA  PIA  KATIKA  MAPENZI.

Jinsi  Ya  Kujikinga  Na  Ulozi  Huu:
Ili  kujikinga  na  ulozi  huu, mhusika  afanyiwe  tambiko  maalumu  la  kumkinga  dhidi  ya  uchawi  na  ulozi  wa  aina  yote  ile. Na  kama  tayari  mtu ameshafanyiwa  ulozi  huu, basi  lifanyike  tambiko  maalumu  la  kurudisha  nyota  yake  na  kumfungua  kutoka  kwenye  kifungo  hicho.
 
Katika  tambiko  hilo, ni lazima  sehemu  iliyo  tumika  kuzika  unyayo wa  muhusika, igunduliwe na  kisha  tambiko  maalumu  likafanyike  katika  eneo  hilo.

KWA   MAKALA  KUHUSU  ULIMWENGU  USIO ONEKANA, TEMBELEA  KILA  SIKU:

Rais Magufuli Afungua Rasmi Kikao Kazi Cha Makamanda Wa Polisi....Akerwa na Mikataba Mibovu Inayolidhalilisha Jeshi la Polisi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka Jeshi la Polisi nchini na Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujirekebisha kwa kutekeleza wajibu wao huku wakitanguliza maslahi ya taifa.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo jana tarehe 29 Aprili, 2016 wakati akifungua kikao cha kazi cha Makamanda wa polisi wa mikoa, Mawakili wafawidhi wa serikali  wa Mikoa na Wakuu wa upelelezi wa Mikoa na Vikosi, kinachofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Dodoma uliopo katika eneo la Tambukareli Mjini Dodoma.
 
Awali kabla ya kutoa hotuba yake Rais Magufuli aliwapa nafasi Makamanda na Mawakili Wafawidhi hao kutoa maoni yao juu ya changamoto zinazowakabili katika kutekeleza wajibu wa kufanya upepelezi na kuendesha mashitaka, hususani kujua sababu za kuchelewesha kesi za makosa ya jinai, ambapo wamedai ufinyu wa bajeti ndio sababu kubwa ya kucheleweshwa kwa kesi za hizo.
 
Kufuatia kutajwa kwa changamoto hiyo Rais Magufuli ameahidi kuhakikisha anawatafutia fedha kwa ajili ya kukabiliana nazo, lakini ametaka fedha zitakazotafutwa zitumike vizuri kwa kuwa taarifa zinaonesha Jeshi la Polisi limekuwa likihusishwa na matumizi mabaya ya fedha hali inayoongeza ukubwa wa matatizo yanayokwamisha utendaji wake wa kazi.
 
Ametolea mfano wa taarifa za matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kununulia vifaa na sare za askari, ama mikataba yenye mashaka inayotiwa saini kati ya Polisi na wawekezaji kuwa ni baadhi ya mambo yanayoongeza hali ngumu ya utendaji kazi kwa jeshi hilo.
 
"Oysterbay pale ni eneo ambalo ni very prime, kila mmoja anajua, mmeingia kwenye mikataba mnayoijua nyinyi, akapewa mtu anawajengea pale, sifahamu kama majengo hayo yanafaa. Palikuwa na ubaya gani eneo la Oysterbay likawa na hati, mkaitumia hiyo hati kwenda kukopa benki na kujenga nyumba hata za ghorofa 20 pale, mkaweka investment  na Polisi wenu wakakaa pale. Nimesema lazima nizungumze kwa uwazi, nisiposema kwa uwazi nitajisikia vibaya nikimaliza mkutano huu, nataka muelewe na muelewe ukweli direction  ninayoitaka mimi" Amesema Rais Magufuli
 
Aidha, Rais Magufuli ameitaka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka kujipanga kufanya kazi kwa ufanisi na ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya serikali kushindwa katika kesi nyingi mahakamani licha ya kuwa na wanasheria mahiri.
 
"Niwaombe mawakili na polisi wanaohusika na upelelezi mtangulize maslai ya nchi mbele, kwa sababu kumekuwa na usemi kwa baadhi ya wapelelezi na mawakili wachache, nasema wachache, panapokuwa na kesi inayohusiana na pesa pesa, wana misemo yao wanasema dili limepatikana, na saa nyingine kesi inapopelekwa mahakamani wana-collude Mawakili wa serikali na mawakili wanaomtetea  mhalifu, na wanapo-collude siku zote serikali inashindwa. Unapoona hali hiyo ya kila siku serikali inashindwa, halafu siku hiyo unataka serikali ikuwezeshe, kwa vyovyote serikali inapata kigugumizi" amesisitiza Rais Magufuli.
 
Dkt. Magufuli pia amelitaka Jeshi la Polisi kujiepusha na kashfa ambazo zimekuwa zikisemwa dhidi yake, ikiwemo maafisa wa Polisi kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kuazimisha silaha kwa wahalifu wa ujambazi.
 
Hata hivyo Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Polisi na ofisi ya Mkurugenzi wa  Mashitaka kwa kazi kubwa wanayoifanya na ametaka apelekewe mpango wa mahitaji yao ili atafute namna ya kuimarisha vyombo hivyo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
29 Aprili, 2016 

MSD Yaigeuzia Kibao Muhimbili Kuhusu Kuhusu Utata wa Dawa Uliobuliwa na CAG

$
0
0
Sakata la upotevu wa vifaatiba na dawa kutoka Bohari ya Dawa (MSD) kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kipindi cha miaka minne limeingia katika sura mpya baada ya MSD kuigeuzia kibao hospitali hiyo, huku ikitoa ushahidi wa ankara 23 zilizotumika kupelekea vifaa hivyo kwa kipindi cha miaka minne. 

Ripoti iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Juma Assad inaonyesha ukaguzi ulifanyika Muhimbili, huku rekodi zikionyesha kwamba hospitali hiyo ilikuwa ikiagiza mzigo kutoka MSD, lakini hazionyeshi kupokea vifaa hivyo tangu mwaka 2012/14.

Kwa kutumia vielelezo vya nyaraka hizo mbele ya vyombo vya habari jana, MSD ilitoa ufafanuzi kuwa haihusiki katika upotevu huo kwani iliwasilisha MNH vifaatiba na dawa zenye thamani ya Sh2.6 bilioni na kupokewa stoo kwa nyakati tofauti kwa kipindi cha miaka minne. 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Lauren Bwanakunu alisema hati za CAG, zinaonyesha kuwa MSD haina tatizo lolote. 

“Ankara hizo siyo kwamba dawa hazikufika hospitalini hapo, bali hazikuonekana kwenye vitabu vya kupokelea mali vya Hospitali ya Taifa Muhimbili,” alisema. 

Alisema baada ya kupitia nyaraka zake, MSD imefanikiwa kupata uthibitisho wa hati za kupelekea mali za dawa na vifaatiba vyote vilivyopelekwa Muhimbili, ambavyo ni pamoja na dawa za figo na moyo. 

Bwanakunu alisema pamoja na juhudi hizo, Bohari ya Dawa imewasiliana na Muhimbili ili kuainisha taarifa za kwenye ankara na shehena ya dawa na vifaatiba vilivyopelekwa hospitalini hapo, kwani utaratibu wa kupeleka na kukabidhi dawa hospitalini unamlazimu mpokeaji kusaini ankara inayoonyesha mzigo uliopelekwa kwa mteja (delivery notes) ambazo zote zipo Bohari ya Dawa. 

“Vitabu vyetu kutoka kwa CAG vipo na tumepata hati safi, tumethibitisha kwamba mzigo wote wa ankara 23 ulipelekwa Muhimbili kwa kipindi cha miaka minne,” alisema.

 Alisema MSD ilikuwa ikiwasilisha dawa tangu mwaka 2012 kwa mujibu wa maombi kutoka MNH, hivyo hospitali hiyo inapaswa kujibu kwa kuwa imekuwa ikipokea dawa hizo kwa kipindi tofauti. 

“Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh2.03 bilioni vilikuwa vikiagizwa kwa tarehe tofauti kwa miaka mitatu lakini havikuwahi kuingizwa katika rekodi. 

"Kulingana na utaratibu wa usambazaji wa MSD, mteja hukiri kupokea mzigo kupitia Ankara ya mauzo (Sales Invoice), jukumu la kuandika hati ya mapokeo (GRN) ni la mteja husika ambaye ni Muhimbili,” alisema Bwanakunu huku akionyesha nakala hizo. 

Ankara zilizotolewa jana na MSD zinaonyesha kuwa ilikuwa ikihudumia hospitali hiyo tangu Mei 14, 2012 hadi Desemba 4, 2014, lakini katika ankara hiyo, Muhimbili haikuonyesha kuwahi kupokea vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh2,028,625,100. 

 Alichosema CAG 
Katika ukurasa wa 37, taarifa ya CAG, inaeleza kuwa ukaguzi huo ulibaini kuwa dawa na vifaatiba vyenye thamani ya Sh2.03 bilioni havijafika Muhimbili tangu Mei 2012 licha ya kuonekana kwenye ankara 23 za MSD. 

Nakala hiyo ilieleza kuwa kwa hali ya kawaida, haikutarajiwa bidhaa hizo kuchukua zaidi ya wiki moja kufikishwa sehemu husika ukizingatia ofisi za MSD na MNH zote zipo Dar es Salaam. 

“Hali hii inaashiria uwezekano wa upotevu wa dawa na vifaatiba pasipo uongozi kuwa na taarifa. Menejimenti inashauriwa kuchunguza jambo hili ili kubaini kama kweli bidhaa hizo bado zipo safarini,” inasema taarifa ya CAG. 

Msimamo wa Muhimbili
Akijibu hoja hiyo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha alisema MNH inazo hati za kupokelea ‘Develivery note’ za mizigo iliyopokea bila ankara, kinachohitajika ni MSD kuoanisha ankara walizozitaja na hati walizozifikisha hospitalini hapo. 

Aligaesha alisema namba za ankara zilipatikana kwenye maelezo ya MSD yaliyowasilishwa MNH ikionyesha matumizi ya hospitali kwenye akaunti iliyopo MSD kutokana na fedha ambazo Serikali inapeleka huko. 

“Ili kukamilisha utaratibu wa kupeleka mzigo mahali, mzigo huo unapaswa uambatane na nyaraka kama mkataba kati ya mnunuaji na muuzaji, ankara na hati ya kupokelea. Endapo mzigo ulioletwa ni wa msaada, mkataba hauhitajiki, kwenye msaada ni lazima hati ya kupokelea iwepo na nakala inayoonyesha thamani ya mzigo,” alisema. 

Alisema kwa muda mrefu imekuwa ni kawaida MSD kupeleka baadhi ya mizigo Muhimbili au wazabuni walioagizwa na MSD ikiwa haina viambatanisho hivyo muhimu, kwani mpaka sasa Muhimbili ina orodha ya mali ambazo zilipelekwa kwa kutumia hati ya kupokelea katika kipindi husika.

 “Hata hivyo, tulifuatilia ankara za mizigo iliyokwishapokewa kutoka MSD ili tuweze kupewa ankara husika kwa mizigo tuliyopokea bila kiambatanisho hicho, lakini kwa bahati mbaya ankara zilizodurufiwa kutoka kwenye mfumo wa MSD hazionyeshi namba ya hati (customer reference) na hazijasainiwa na wao wala sisi,” alisema Aligaesha. 
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Victoria Elangwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Sako Mwakalobo.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa MSD (kushoto), kuzungumza na wanahabari.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Terry Edward.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images