Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Asamehe Wafungwa 3,551

$
0
0

Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,551, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projest Rwegasira ilisema wafungwa 580 wataachiwa huru, huku wengine 2,971 watapunguziwa moja ya sita ya vifungo vyao.

Alisema rais ametoa msamaha huo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aliwataja watakaonufaika na msamaha huo kuwa ni wafungwa wenye ugonjwa wa ukimwi, kifua kikuu na saratani ambao wapo kwenye hatua za mwisho. Wengine ni wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea, wajawazito na wale waliongia na watoto gerezani.

Wafungwa wengine watakaonufaika na msamaha huo ni wenye ulemavu wa akili ambao wamethibishwa na jopo la waganga kuwa wana tatizo hilo.

Katibu mkuu wa wizara hiyo alisema msamaha huo hautawagusa wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa au kifungo cha maisha jela.

Pia, wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya, upokeaji na utoaji rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, unyang’anyi kwa kutumia silaha na kubaka ni miongoni mwa waliokosa msamaha huo.

Wengine ambao hawataguswa na msamaha huo ni wale wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kupatikana na  silaha, wizi wa magari na pikipiki, kuwapa mimba wanafunzi na ubadhirifu wa fedha za Serikali.

Wafungwa wengine watakaoendelea kubaki magerezani ni wale waliohukumiwa kutokana na usafirishaji wa nyara za Serikali na ujangili, utekaji wa watoto, biashara ya binadamu, kukutwa na viungo vya binadamu na waliojaribu kutoroka wakiwa chini ya ulinzi.

Katika maadhimisho ya Uhuru yaliyofanyika Desemba 9, 2015, Rais Magufuli aliwasamehe wafungwa 2,336, kati ya hao 117 waliachiwa huru huku 2,219 wakipunguziwa moja ya sita ya vifungo vyao.

Kwa idadi hiyo mpaka sasa wafungwa 5,887 wamenufaika na msamaha wa Rais Magufuli tangu aingie madarakani baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015.

Mwenyekiti Aweka Majina HEWA Mradi wa Kuokoa kaya Masikini (TASAF )

$
0
0

Wananchi wamemkataa mwenyekiti wa kitongoji cha Mwanogi kijiji cha Bulima, Kata ya Nyashimo wilayani Busega katika Mkoa wa Simiyu, wakimtuhumu kuweka majina hewa katika mradi wa kuokoa kaya masikini unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).

Mwenyekiti huyo wa kitongoji, Ester Ng’ombe anatuhumiwa pia kufanya kazi kwa ubaguzi wa vyama vya siasa.

Akizungumza katika kikao, mwenyekiti wa kamati ya mipango na fedha ya kijiji cha Bulima, Zablon Ntinika alisema wamefikia uamuzi wa kumsimamisha kazi mwenyekiti huyo baada ya uchunguzi walioufanya kubaini majina matano ambayo ni hewa yakipatiwa fedha.

Alisema wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mwenendo wa mwenyekiti huyo katika utendaji wake wa kazi katika kitongoji hicho lakini wamebaini mengi. 

Mwenyekiti huyo anayetuhumiwa, alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema kuwa yeye hayatambui bali ni siasa za chuki dhidi yake.

Ng’ombe alisema chanzo si majina feki bali ni siasa zinazochochewa na wanasiasa wa kata hiyo ambao wanataka kuichafua sifa yake ili aweze kuondolewa na wananchi waliomchagua.

Mwanafunzi Amkaanga kortini polisi anayedaiwa kumbaka katika kibanda cha ulinzi cha benki.

$
0
0

Mwanafunzi wa kidato cha tatu, juzi alimkaanga askari polisi anayedaiwa kumbaka kwa kuieleza Mahakama jinsi alivyotendewa kitendo hicho katika kibanda cha ulinzi cha benki.

Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Misungwi, Ruth Mkisi, shahidi huyo alidai siku ya tukio askari huyo, Raphael Sixstus (30), alimuita alipokuwa akipita karibu na Benki ya CRDB Tawi la Misungwi, alipoitikia wito ghafla alivutiwa ndani ya kibanda hicho na kumbaka.

“Wakati akinitendea kitendo hicho, alikuwa akinitishia kisu huku akiniambia nikipiga kelele ataniua, niliogopa nikaa kimya ingawa niliumia na kutokwa damu nyingi sana,”alidai shahidi huyo.

Akiongozwa na Mwendasha Mashtaka wa Polisi, Doreth Mgenyi, mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16 alidai kabla ya kumbaka, mshtakiwa huyo alimvua nguo zote za ndani.

Awali, Mwendesha mashtaka alipokuwa akimsomea makosa mshtakiwa huyo alidai kuwa Novemba 20, mwaka jana, akiwa eneo la lindo katika Benki ya CRBD Tawi la Misungwi, alimbaka mwanafunzi huyo saa 1.00 usiku wakati akitoka mashine kusaga unga katika maeneo ya Bomani.

Hakimu Mkisi aliahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kusikilizwa kwa upande wa mashtaka kuita mashahidi wengine. Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana.

Tahadhari ya Mvua kubwa na Upepo mkali f kuanzia tarehe 26-04-2016 Hadi 29-04- 2016

$
0
0

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetahadharisha uwepo wa mvua kubwa na upepo mkali unaozidi kasi ya kilomita 40 kwa saa iliyotarajiwa kuanza jana hadi keshokutwa.

Sambamba na upepo huo, taarifa hiyo ya TMA imesema mvua za zaidi ya milimita 50 zinatarajiwa kunyesha huku bahari ikitarajiwa kuwa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0 

Taarifa hiyo imeelezwa kuwa hali hiyo imesababishwa na mgandamizo mdogo wa hewa katika Pwani ya Tanzania unaotakana na kimbunga cha Fantala.

Maeneo yaliyotajwa na TMA kwamba yataathiriwa na hali hiyo ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Mtwara, Unguja na Pemba na kwamba mvua hizo pia zinatarajiwa kusambaa hadi katika maeneo ya mikoa ya Kilimanjaro na Mashariki mwa Manyara.

Ofisa Habari wa TMA, Monica Mutoni aliwataka wakazi wa maeneo hayo na watumiaji wa bahari kuchukua hatua stahiki ili kuepuka uwezekano wa kupata madhara yanayoweza kujitokeza.

“Mvua hizi ni kama zile zilizonyesha wiki iliyopita. Wajibu wetu ni kutoa taarifa pale tunapoona kiwango cha juu cha mvua na upepo ili watu wachukue tahadhari. Kwa watumiaji wa bahari umakini uzidi kuongezeka kwani mawimbi yatakuwa makubwa na upepo wa bahari utakuwa kilomita 30 kwa saa,” alisema Mutoni. 

Ripoti ya CAG Yawaweka Kikaangoni Vigogo wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD)

$
0
0


Ripoti iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Musa Juma Assad imezichanganya Hospitali ya Taifa Muhimbili na Bohari ya Dawa (MSD), huku Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akihitaji maelezo ya kina kuhusu mkanganyiko huo. 
 
Ummy ameitaka MSD kuandika maelezo ya kina kwa maandishi, kuhusu vifaa vya Sh2 bilioni ambavyo viko njiani kwenda Muhimbili kwa miaka minne sasa, kabla wizara yake haijatoa tamko rasmi. 
 
Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu  jana alisema bohari haina mzigo wowote ulio njiani kuelekea Muhimbili bali imekuwa ikisambaza dawa zake nchi nzima. 
 
Bwanakunu alisema tatizo lililojitokeza ni mfumo wa kompyuta ambao unaonyesha mzigo upo njiani, hivyo muamala katika kompyuta unavyoshindwa kukamilika, mzigo lazima uonekane upo njiani. 
 
“Mwaka 2012 tulibadilisha mfumo wa kompyuta kutoka wa awali mpaka tunaotumia sasa, hivyo kuna miamala ilihitaji kubadilishwa, mwaka huu tulifanya zoezi la kukamilisha baadhi na si kwa Muhimbili pekee kwa mfano kuna mzigo unatoka MSD Ubungo kwenda Mulebaukifika kule mtu anashindwa kuingiza kwenye mfumo kwamba umepokelewa,” alisema Bwanakunu. 
 
Alifafanua kwamba majibu ya MSD kwa CAG yalieleza kuwa walitengeneza timu ya uchunguzi na baadhi ya watu walichukuliwa hatua, “nimeshachukua hatua za haraka baada ya kupata hiyo ripoti, tangu mwanzoni mwa mwaka huu wale ambao hawakujaza hiyo miamala tulishawachukulia hatua, hakuna mali iliyopotea MSD.” 

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba kuna ripoti ya Muhimbili ambayo inaonyesha katika vitabu kwamba kuna mzigo ambao Muhimbili iliununua kutoka MSD, lakini haujafika, lakini Bwanakunu alipoulizwa alisema hakuna vitabu vinavyoonyesha kuwa Muhimbili inadai vifaa tiba na dawa MSD. 
 
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru alisema kwa taarifa alizonazo mpaka sasa CAG alifanya ukaguzi katika vitabu vya MSD na si wao na alipouliza vifaa viko wapi alijibiwa kuwa vinakwenda MNH. 
 
Alisema kuwa Watanzania wawe na subira na kwamba watapewa majibu kesho (leo), baada ya Muhimbili kupekua kwa kina vitabu vya mwaka 2012, ili kujiridhisha iwapo vifaa vilipokelewa au havikuwahi kununuliwa Muhimbili. 
 
“Hiyo ripoti tumeiona leo Jumanne. Hayo mambo yametokea mwaka 2012 huwezi kuwa na jibu la kila kitu, kesho tunataka tukapitie hiyo ripoti kwa sababu ni ukaguzi wa MSD, tukaangalie vitabu hivyo vifaa vilifika?” Alisema Museru. 
 
Naye Waziri Ummy Mwalimu alisema katika ripoti hiyo kuna hoja mbili ambazo ni MSD na TFDA, huku akifafanua kwamba amezungumza na Mkurugenzi wa MSD lakini hajaridhika na majibu na kumtaka aandike maelezo ya kina. 
 
“Nimetaka maelezo ya maandishi kutoka kwa MSD na TFDA kuhusu ripoti ya CAG tumekubaliana na Katibu Mkuu walete maandishi ndiyo tutatoa msimamo rasmi wa wizara, kwa upande wa MSD ndiyo maana tuliweka pembeni wale wakurugenzi wanne sababu ya changamoto hii ambayo CAG amekutana nayo,” alisema Ummy.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 27

Mwanza Yaokoa zaidi ya Bilioni kwa kubana matumizi

$
0
0

Halmashauri ya Jiji la Mwanza, imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 1 baada ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima tangu mwezi Januari mwaka huu na kuzielekeza fedha hizo kwenye utengenezaji madawati 6,840.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Adam Ngowi, amesema uamuzi wa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ulifikiwa ili kutekeleza agizo la rais Dkt. John Magufuli linalotaka ifikapo Juni 30 mwaka huu tatizo la madawati liwe limemalizika.

Ngowi amesema wanafanya utengenezaji wa madawati hayo ili kupunguza pengo la madawati 11,400 ambalo linasababisha wanafunzi zaidi ya elfu thelathini kujifunza wakiwa wamekaa chini katika halmashauri hiyo.

Aidha, amesema kuwa katika utatuzi wa changamoto hiyo wanakumbwa na changamoto ya upatikanaji wa vifaa ikiwemo mbao hali ambayo inafanya utengenezaji wa madawati hayo kwenda taratibu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Nyamagana, Baraka Konisaga ametembelea kuona hali halisi ya utengenezaji wa madawati hayo na kusema kuwa kutokana na changamto hiyo wanaweza kufanikiwa kutatua tatizo hilo lakini sio kwa muda ambao wamepangiwa.

Konisaga amewataka wakazi wa wilaya ya Nyamagana kila mmoja wao kwa nafasi yake achangie jitihada hizo za kukamilisha madawati ili kuendana na muda uliopangwa na rais kukamilisha zoezi hilo.

Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako atoa Onyo kwa Wasimamizi wa Elimu

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewatahadharisha kuwawajibisha maafisa elimu wa shule za msingi watakaoshindwa kusimamia elimu na kusababisha wanafunzi wamalize shule za msingi bila kujua kusoma na kuandika.

Prof. Ndalichako amesema hayo Mjini Iringa katika mafunzo ya wakaguzi na wadhibiti wa ubora wa elimu mashuleni kutoka wilaya 31 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Prof. Ndalichako amesema kuwa ni aibu kwa wanafunzi waliosoma miaka saba darasani hawajui kusoma na kuandika wakati Wakaguzi na Wasimamizi wa Elimu wapo katika maeneo husika na kuwataka wajitathimini kama wanatekeleza wajibu wao ipasavyo.

Waziri huyo pia amewataka wadhibiti hao wa elimu kufanya ukaguzi wa vitabu na vifaa vya kufundishia vikiwa na ubora unaokubalika huku akiahidi kuzingatia mahitaji ya walemavu katika shule za serikali.

Kwa upande wao walimu pamoja na wadhibiti hao wa elimu wameiomba serikali kushughulikia madai yao na kuboresha mazingira ya kufanyika kazi ikiwemo pamoja na fungu la kutosha na kuendeshea ukaguzi wa elimu.
Mkuu wa wilaya bwana Richard Kasesela akitoa salamu alisema " ni wakati muafaka kubadili KKK iliyopo iliyo zoeleka sasa yaani KULA, KULALA na KUCHEZA kuiirejesha kwenye maana halisi ya KUSOMA, KUANDIKA na KUHESABU.
Mkuu wa mkoa Bi.Amina Masenza akimkaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Ndalichako,Bi Masenza alimuomba waziri wa Elimu kuhakikisha Wahakiki ubora wanapewa kipaumbele katika kukuza elimu Tanzania.
Baadhi ya waliohudhuria mafunzo kwa wakaguzi wa uhakiki ubora wa elimu Tanzania yaliyofanyika katika chuo cha walimu Kleruu leo. Mafunzo hayo yajumuisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Katavi, Sumbawanga, Songwe na Mbeya.

Mbunge: Pinda alitaka kuchomokea dirishani Baada ya Kutoswa na CCM

$
0
0

Mbunge wa Ulanga, Gudluck Mlinga (CCM), amesema Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, alitaka kuchomokea dirishani baada ya kutoswa katika uteuzi wa urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Mlinga ambaye pia ni mtoto wa marehemu, Selina Kombani, alitoa kauli hiyo juzi jioni, wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Alisema baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia upinzani na wenzake, Pinda naye alitaka kuwafuata, lakini akashtuka na kubaki CCM.

“Yule mwingine alituzingua tukampiga chini akaenda upinzani, Pinda naye mwaka jana alitetereka, tukamtosa akataka kuchomokea dirishani… akashtukia akabaki, kwahiyo CCM hatufanyi mambo kwa kuambiwa kama wanavyofanya upinzani,” alisema.

Kauli ya Mlinga ilionekana kumkera Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy (CCM) ambaye aliomba kutoa taarifa: “Mheshimiwa mwenyekiti nampa taarifa mzungumzaji, amemvunjia heshima Pinda kwa kusema alitokea dirishani, afute kauli yake mara moja au athibitishe ni lini Pinda alitokea dirishani… mtoto huna adabu, huna nidhamu,” alisema Keissy huku akishangiliwa na wabunge wa upinzani.

Baada ya taarifa ya Keissy, mwenyekiti akamtaka Mlinda kuendelea kuchangia na kujikita kwenye hoja.

“Pamoja na umbile langu ndogo, leo nipo hapa kuwapa semina wabunge wa upinzani. Huyo mwenyekiti wenu namfahamu kwa sababu nimeoa huko, kwahiyo aibu yake aibu yangu, na hata ile hotuba yake aliandikiwa hapo mlangoni… mimi ningekuwepo asingetoa.

“Wabunge wa upinzani waelewe nimewaambia  natoa somo kwao na naomba nitoe mfano mwingine. Haya mambo ya mnakaa hapa eti mwenyekiti kasema, kila kitu mwenyekiti… mimi namfahamu huyo mwenyekiti wenu kwa sababu nimeoa huko, tangu nampata binti yao yeye ni mwenyekiti, nimeoa yeye ni mwenyekiti hadi nimezaa mtoto wa pili bado yeye ni mwenyekiti.

“Juzi nilisikitika sana kuna mmoja alikuwa anahoji mshahara wa Rais, yeye anachangia chama Sh milioni tatu kila mwezi… sasa hizo fedha zinakwenda wapi?” alihoji Mlinga ambaye alitumia muda wake wote kuvishambulia vyama vya upinzani, huku akizomewa na wabunge wa upinzani wakimwambia “teja huyooo”.

Rais Magufuli Awaapisha Makatibu Tawala Wapya Wa Mikoa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na kuwapangia vituo vyao vya kazi.

Makatibu Tawala hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na kisha wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Makatibu Tawala walioapishwa ni;
  1.     Arusha -         Richard Kwitega
  2.     Geita -             Selestine Muhochi Gesimba
  3.     Kagera -          Armatus C. Msole
  4.     Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour
  5.     Pwani -           Zuberi Mhina Samataba
  6.     Shinyanga -    Albert Gabriel Msovela
  7.     Singida -         Dr. Angelina Mageni Lutambi
  8.     Simiyu -          Jumanne Abdallah Sagini
  9.     Tabora -         Dkt. Thea Medard Ntara
  10.     Tanga -           Eng. Zena Said
Makatibu Tawala wengine wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale waliohamishwa vituo vya kazi na wale waliobaki katika vituo vya kazi walivyokuwep,o ambao tayari walishakula kiapo cha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaa
27 Aprili, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha ndugu Albert Gabriel Msovela kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Ikulu jijini Dar es salaam April 27,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha ndugu Amantius Casmiri Msole kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Ikulu jijini Dar es salaam April 27,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha ndugu Angelina Mgeni Lutambi kuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Ikulu jijini Dar es salaam April 27,2016

Waziri Mkuu Amjibu Freeman Mbowe

$
0
0
Waziri Mkuu kassim Majaliwa, amemjibu kiongozi wa upinzani Bungeni Freeman Mbowe, aliyehoji siku za hivi karibuni kitendo cha Serikali kutotoa hati maalumu ya mwongozo (Instrument) inayoitambulisha serikali iliyopo madarakani kwa mujibu wa sheria.

“Instrument ipo, na tayari imeshasainiwa na rais kwa mujibu wa sheria, kwa sasa mchakato wa kuitangaza kwenye magazeti ya Serikali inaendelea” amesema Waziri Mkuui Majaliwa

Amesema viongozi wote wa serikali wapo kwa mujibu wa sheria na kanuni za serikali.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema haya wakati alipokuwa akihitimisha hotuba yake ya kulitaka bunge likubali kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi yake kwa mwaka wa fefdha 2016/17

Mahakama ya Kisutu Yafuta shtaka la Kutakatisha fedha dhidi ya Aliyekuwa bosi wa TRA, Harry Kitilya na wenzake Wawili

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, leo imefuta shtaka la utakatishaji fedha (money laundering) lililokuwa likimkabili Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya sambamba na waliokuwa wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Sioi Sumari na Shose Sinare.

Awali watatu hao walikuwa wamenyimwa dhamana. Kutokana na uamuzi huo, mawakili wao sasa wanaweza kuwaombea dhamana.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), iliwafikisha mahakamani watatu hao April 1, kwa kisa la:- Kula njama na kujipatia kwa udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na. 12 ya Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.

Watuhumiwa hao walidaiwa kufanikiwa kujipatia fedha kwa njia ya kughushi dola milioni 6, kama malipo ya kufanikisha serikali ya Tanzania kupata mkopo wa dola milioni 550 kutoka Benki ya Stanbic ya Jijini London mkopo ambao ulipitia benki ya Stanbic tawi la Tanzania.

Serikali yakiri upungufu wa sukari, yaagiza nje ya nchi

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza maofisa biashara wa wilaya, mikoa na Taifa kukagua maghala yote ya wafanyabiashara walioficha sukari na kuwachukulia hatua.

Waziri Majaliwa alisema hayo leo asubuhi wakati akihitimisha mjadala wa hotuba ya mapato na matumizi ya ofisi yake na kuliomba Bunge likubali kupitisha.

Waziri Mkuu alisema ni kweli kwamba kuna upungufu wa sukari nchini, ingawa pia upo udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara.

Alisema takwimu kutoka kwa wataalamu zinaeleza kwamba mpaka sasa kuna tani 37,000 za sukari katika maghala nchini, lakini imekuwa haionekani kwa sababu wafanyabiashara wakubwa wameificha ili waiuze kwa bei kubwa.

“Ninawaagiza maafisa wa biashara kushughulikia suala hili, na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuwa wamekwenda kinyume na taratibu  tulizojiwekea,”  alisema Majaliwa.

Kamishna Mkuu wa Zamani wa TRA na Wenzake Wawili Wanyimwa Dhamana

$
0
0

Baada  ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kuondoa shitaka la utakatishaji fedha katika kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni, upande wa mashitaka umekata rufaa ya kupinga mwelekeo wa kuondolewa kwa shitaka hilo, anaandika Faki Sosi.

Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.

Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu amesema kuwa, shitaka la nane linalowakabili watuhumiwa hao lina upungufu kisheria hivyo mahakama italifuta shitaka hilo.
 
Jopo la mawakili wa upande wa utetezi linaongozwa na Dk. Lingo Tenga liliomba mahakama kuwapa wateja wao dhamana yenye masharti nafuu.

Baada ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi  kusimamisha kusikiliza kesi hiyo kwa dakika 30, aliporejea tu, Oswadi Tibabyekonya, Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali alileta notisi ya rufaa kutoka Mahakama Kuu iliyokuwa ikipinga mwelekeo wa kufutwa kwa shitaka la utakatishaji fedha.

Hakimu Mchaura baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, alihailisha shauri hilo na kwamba, uamuzi atautoa tarehe 29 Aprili mwaka huu. Watuhumiwa wote wamekosa dhamana wamerudishwa rumande.

Serikali Yazuia Uingizaji Holela Wa Mchele.

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vya dola viimarishe ulinzi kwenye mipaka ya nchi na hasa katika mwambao wa Bahari ya Hindi ili kuzuia uingizwaji holela wa mchele wa magendo kutoka nje ya nchi.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatano, Aprili 27, 2016) wakati akijibu hoja za wabunge na kuhitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma.

“Napenda kuviagiza vyombo vya dola viendelee kuimarisha ulinzi wa mipaka yetu hasa katika mwambao wa Bahari ya Hindi ili kuzuia uingizwaji holela wa mchele wa magendo kutoka nje ya nchi. Endapo patatokea upungufu wa mchele nchini, Serikali itaangalia uwezekano wa kuruhusu kuagiza mchele kutoka nje,” amesema.

Waziri Mkuu amesema katika kipindi cha miaka sita iliyopita, kumekuwa na ongezeko la asilimia 14 katika uzalishaji wa mpunga hapa nchini na hivyo kufanya kiwango cha uzalishaji kiwe ni kikubwa kuliko mahitaji.

“Takwimu za uzalishaji mpunga zinaonesha kuwepo ongezeko katika kipindi cha miaka sita iliyopita ambacho kiliongezeka kutoka tani 1,699,825 mwaka 2009/2010 hadi kufikia tani 1,936,909 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 14. Katika kipindi chote hicho, kiwango cha uzalishaji wa mpunga kimekuwa kikubwa kuliko mahitaji,” amesema.

“Kutokana na mwenendo huo mzuri wa uzalishaji wa mpunga hapa nchini, Serikali ilisitisha kutoa vibali vya kuagiza mchele kutoka nje ya nchi tangu Machi, 2013. Hatua hii itasaidia wakulima wetu kupata soko la uhakika na bei nzuri, jambo ambalo linawaongezea kipato na pia kuwahamasisha kuongeza uzalishaji zaidi,” amesema.

Akizungumzia kuhusu deni la sh. bilioni 134 ambalo Serikali inadaiwa na Bohari ya Dawa nchini (MSD), Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kulishughulikia deni hilo kwa kumwelekeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ahakiki deni hilo. “Mpaka sasa CAG amehakiki madai ya jumla ya shilingi bilioni 67 na kazi ya uhakiki inaendelea.”

Akifafanua kuhusu vigezo vilivyutumika kugawanya majimbo mapya ya uchaguzi, Waziri Mkuu alisema mwaka 2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea maombi 77 ya kuanzishwa majimbo mapya, ambapo Halmashauri 37 ziliwasilisha maombi ya kugawa majimbo ya uchaguzi na maombi 40 yalitoka katika majimbo yaliyokuwepo yakiomba kugawanywa. Kati ya maombi yaliyowasilishwa, maombi 35 tu ndiyo yalikidhi vigezo na yalistahili kugawanywa.

“Kutokana na ongezeko la Halmashauri mpya ambazo kisheria ni majimbo ya uchaguzi, ongezeko la idadi ya wabunge wanawake wa viti maalum na uwezo wa ukumbi wa Bunge; Tume iliamua kutumia vigezo vitatu tu ili kupata idadi ya majimbo yanayoweza kugawanywa. Vigezo hivyo ni: Wastani wa idadi ya watu (Population Quota), mipaka ya kiutawala na uwezo wa ukumbi wa Bunge,” alisema.

Waziri Mkuu alisema chini ya mchakato huo, Tume ilianzisha majimbo mapya 25  ambapo majimbo 19 yalitokana na ongezeko la Halmashauri mpya; na majimbo sita yalitokana na kigezo cha wastani wa idadi ya watu.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alibainisha kwamba kwa sasa Serikali haina mpango wa kuongeza maeneo mapya ya utawala zikiwemo wilaya na mikoa mipya kwa sababu bado inaendelea kujengea uwezo wa rasilmali watu na vitendea kazi katika maeneo mapya ya utawala yaliyopo hivi sasa.
Bunge limepitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2016/2017.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980, DODOMA.
JUMATANO, APRILI 27, 2016.

Mjane Wa Baba Wa Taifa, Mama Maria Nyerere Atembelea Daraja La Nyerere Kigamboni Leo

$
0
0
Mke wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Maria Nyerere ametembelea Daraja la Nyerere linalounganisha eneo la Kigambaoni na Kurasini Jijini Dar es salaam na kuipongeza serikali na wananchi wote wa Tanzania kwa kufanikisha ujenzi wa Daraja hilo kubwa na la kisasa kwa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.

Mama Maria Nyerere aliyeongozana na Mwanae Mheshimiwa Makongolo Nyerere amesema kukamilika kwa daraja hilo ambalo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 254.12 kumekamilisha mpango wa miaka mingi ulioanzishwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa na nia ya kujenga daraja katika eneo hilo la mkondo wa bahari lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti haikuwezekana.

Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuamua Daraja hilo liitwe Daraja la Nyerere kwa heshimu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na amebainisha kuwa uamuzi huo utaviwezesha vizazi vijavyo kutambua juhudi zilizofanywa na mmewe katika ujenzi wa nchi.

"Mimi ninamshukuru sana Rais kwa maana ilikuwa lipewe jina lake, lakini yeye Mungu akamjaalia akasema kwamba hapana tukumbuke tulikotoka, kwa hiyo najisikia vizuri sana, na familia nayo inajisikia vizuri sana, lakini zaidi na watanzania wanajisikia vizuri sana, kwa maana watakuwa wanaulizana Nyerere alikuwa ni nani?" Amesisitiza Mama Maria Nyerere.

Daraja la Nyerere lenye urefu wa meta 680, upana wa meta 3.2, njia sita za magari na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 2.5, lilifunguliwa na Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 19 Aprili, 2016 na linakuwa kiunganishi muhimu kati ya Kigamboni na katikati ya Jiji la Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
27 Aprili, 2016

Waziri Mkuu Majaliwa atembelewa na Waziri Viwanda wa Singapore Bungeni Mjini Dodoma.

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amewakaribisha wafanya biashara kutoka nchini Singapore kuja kuwekeza nchini Tanzania kutokana na fursa zilizopo nchini katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo mjini Dododma alipokuwa akiongea na Ujumbe wa Singapore ulioongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Biashara na Viwanda Mhe. Kol Poh Koon aliyeambatana na wafanyabiashara mashuhuri kujifunza na kujionea fursa zilizopo nchini katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa anaamini kampuni za Singapore zitakazowekeza nchini zitakuwa na tija katika sekta ya mafuta na gesi asilia, kilimo, Uchukuzi pamoja na Viwanda katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

Kuhusu kuimarika kwa ushirikiano kati Tanzania na Singapore, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali iko mstari wa mbele katika kuhakikisha inawajengea uwezo watumishi wake katika kada za uhandisi, sheria na wachumi ambao watakuwa msaada mkubwa katika sekta ya mafuta na gesi inayokua nchini ambapo Singapore wamepiga hatua kubwa katika sekta hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Biashara na Viwanda kutoka nchini Singapore Mhe. Dkt. Kol Poh Koon ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kushirikiana na nchi yake huku akionesha kuridhishwa kwake na uhusianao mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Waziri huyo wa Biashara na Viwanda kutoka nchini Singapore amesema kuwa nchi yake itatoa ushirikiano mkubwa kwa Tanzania katika kuhakikisha inawajengea uwezo watendaji wakuu wa Serikali ili Tanzania iweze kufikia malengo waliojiwekea katika kuwahudumia wananchi wake.

Aidha,   awali akiongea na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Medalled Karemaligo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage, Mhe. Dkt. Kol amesema kuwa nchi yake itatumia rasilimali walizonazo ikiwemo rasilimali watu kuwafundisha wataalamu kutoka Tanzania ili waje kuwafundisha wataalamu wengine hapa nchini kwa manufaa ya nchi hizo mbili.

Kuhusu Bandari ya Dar es salaam, Mhe. Dkt. Kol amesema kuwa bandari hiyo ni nzuri ikilinganishwa na bandari nyingine zilizopo katika ukanda wa Bahari ya Hindi kwa kuwa ipo karibu zaidi na Singapore hali ambayo itarahisisha biashara baina ya nchi hizo mbili.

Katika kuonesha nchi yake inavyojali ushirikiano na Tanzania, Mhe. Dkt. Kol amemkaribisha Waziri wa Nishati na Madini kwenda kushiriki wiki ya nishati nchini Singapore ambayo huadhimishwa Oktoba kila mwaka.

Ujumbe huo kutoka nchini Singapore upo nchini kwa muda wa siku tano kuanzia Aprili 26 hadi 30, 2016 ambapo wanatembelea maeneo mbalimbali ya ikwemo Dar es salaam, Dodoma na mkoa wa Morogoro ambapo watazindua mradi wa ushirikiano utakaojulikana kama “Star City”.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Biashara na Viwanda wa  Singapore, Dkt. Koh Poh Koon na ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa  Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (kulia kwake) na ujumbe wake, Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 27, 2016. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akiongea na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Singapore, Dkt. Koh Poh Koon (katikati) leo mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Balozi wa Singapore nchini Tanzania.

Makamu Wa Rais Mhe. Samia Akutana Na Uongozi Wa Baraza La Tawla Na Uongozi Wa Skaut Leo

$
0
0
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kazi kubwa ya Chama Cha Skauti wa Kike nchini hivi sasa ni kuhakikisha kinarejesha heshima ya mwanamke katika jamii.

Samia ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na baadhi ya wanachama wa chama hicho waliofika ofisi kwake Ikulu kwa ajili ya kuelezea shughuli zao katika kusaidia watoto wa kike waweze kujitambua na hatimaye kulitumikia Taifa.

Alisema pamoja na chama hicho kinafundisha kujenga ujasiri na kuwa huru kwa mtoto wa kike lakini kuna haja ya kukumbushana umuhimu wa kuzingatia mila na desturi nzuri zilizopo katika matendo yao ili kurejesha heshima ya mwanamke.

"Sasa hivi utakuta binti kavaa kipanti kinambana hasa, anazunguka barabarani huku na kule, mwenyewe anajiona yuko sawa...hicho ni kinyume kabisa na maadili yetu, mila na desturi zetu za kiafrika tumeziacha kabisa." alisema Makamu wa Rais.

Aidha alisema katika enzi hizi za utandawazi kumekuwa na urushwaji wa mambo yasiyo na maadili katika mitandao jambo ambalo mtoto wa kike anaweza kuutumia uhuru huo kwa kufanya mambo kinyume na mila na desturi.

Alisema pamoja na kwamba Tanzania inapingwa na mataifa makubwa kwa kupitisha sheria ya makosa ya mtandao lakini bado chama hicho kina kazi kubwa ya kusaidia jitihada za serikali katika kulea watoto wa kike kimaadili.

"Nyinyi Girl Guide mna hiyo kazi ya kusaidia kuwalea watoto wa kike waliojengeka vizuri kimaadili na wanazingatia mila na desturi," alidokeza Samia

Makamu wa Rais alikitaka chama hicho pia kuandaa miradi kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa vyoo bora mashuleni kulingana na mahitaji ya watoto wa kike na hivyo kuwawezesha kuhudhuria masomo siku zote bila kukosa kama ilivyo kwa wavulana.

Mwenyekiti wa chama hicho, Matilda Balawa alimshukuru Makamu wa Rais kwa kukubali kuwa mwanachama na kupongeza utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa SKAUT Nchini.Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa SKAUT Nchini.
Makamu wa Rais Mhe. Samia akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Baraza la TAWLA

Makala Awavalia Njuga Watumishi HEWA Jijini Mbeya

$
0
0

Timu ya watu 16 imeundwa ili kuhakiki upya watumishi hewa katika halmashauri zote mkoani Mbeya, lengo likiwa ni kujiridhisha.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema kwenye uzinduzi wa mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma kutokana na kuwapo kwa tatizo la watumishi hewa.
 
“Rais alituagiza kuhakiki watumishi wote na ikafanyika hivyo, lakini kutokana na kuwapo kwa udanganyifu nimeunda timu ambayo imeanza kazi jana (juzi) kuhakiki upya watumishi ili kujiridhisha na kupata ukweli wa watumishi wetu,” amesema.
 
Makalla amesema timu hiyo imegawanyika katika makundi mawili na kwamba, wajumbe wanatoka idara mbalimbali za Serikali wakiwamo wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Polisi Temeke Wakamata 'Panya Road' 18

$
0
0

Jeshi la Polisi linawashikilia vijana zaidi ya 18 wenye umri kati ya miaka 14 na 20 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo ya Wilaya ya Temeke.

Kamanda  wa polisi wa Temeke, Gilles Muroto amesema leo kuwa vijana hao, wanaohusishwa na kundi la Panya Road linalofanya unyang'anyi maeneo ya jiji la Dar es Salaam, walikamatwa jana nyakati tofauti baada ya polisi kuendesha msako wa  kuzuia na kupambana na wahalifu.

Alisema vijana hao wanatoka maeneo ya Buza Kanisani, Chanika, Yombo Kirakala, Buza Changulu, Yombo Makangawe na moja anayeishi maeneo ya Mwananyamala lakini alikamatwa Temeke.

"Kama Kamanda Simon  Sirro alivyosema kuwa ni lazima wahalifu wadhibitiwe katika mko huu. Temeke hatuwez kumwangusha, tunatekeleza agizo lake," alisema Kamanda Muroto.

Alisema vijana hao wanajihusisha na vitendo vya uporaji wa mali mbalimbali kuanzia mitaani, pia kujeruhi watu hali inayosababisha wakazi wa eneo husika kuishi kwa hofu.

Alisema upelelezi ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Wakati huohuo, Kamanda Muroto amesema polisi inashikilia  mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa Buza baada ya kumkuta na puli 120 za dawa za kulevya aina ya bangi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images