Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu: Tatizo la ajira kwa vijana lapungua.

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana nchini kimepungua kwa asilimia 2.5 na kwamba Serikali itaendeleza juhudi za kuvutia uwekezaji ili kupunguza zaidi kiwango hicho.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Aprili 22, 2016) wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma.

“Utafiti wa hali ya ajira nchini wa mwaka 2014 umeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006 hadi asilimia 10.3 mwaka 2014. Aidha, ukosefu wa ajira  kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014,” amesema.

Waziri Mkuu amesema moja ya changamoto zinazosababisha ukosefu wa ajira ni vijana kutojengewa maarifa na ujuzi wa kuajiriwa na kuajirika. Hivyo, Serikali itaendelea kutekeleza Programu ya Miaka Mitano ya Kukuza Ujuzi Nchini (2015/2016 – 2019/2020).

“Programu hiyo inalenga kuongeza idadi ya watu wenye kiwango cha juu cha ujuzi kutoka asilimia tatu ya sasa hadi asilimia 12 inayotakiwa kuendesha uchumi wa viwanda. Vilevile, kupunguza idadi ya watu wenye kiwango cha ujuzi wa chini kutoka asilimia 75 ya sasa hadi asilimia 54,” amesema.

Amewaagiza watendaji wakuu wa wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, taasisi za umma, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha kuwa ukuzaji wa ajira  unakuwa ni agenda ya msingi ya kudumu katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumzia kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu hususan watu wenye ualbino, Waziri Mkuu amesema Serikali inafanya jitihada kubwa kukomesha vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwakamata wote wanaojihusisha na vitendo hivyo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

“Ukatili huo umesababisha watu wenye ualbino kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu. Hali hiyo haikubaliki na haivumiliki katika jamii ya Watanzania. Napenda kusisitiza watu wenye ulemavu wana haki ya kuthaminiwa utu wao na kulindwa dhidi ya ukatili na aina yoyote ya ubaguzi,” amesema.

Waziri Mkuu amesema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaviboresha Vyuo vya Ufundi na Marekebisho (Vocational and Rehabilitation Training Centres) vya watu wenye ulemavu nchini ili kutoa ujuzi unaoendana na mahitaji yao katika soko la ajira ikiwa ni pamoja na kuandaa walimu wa elimu maalum na kutoa vifaa saidizi kwa walimu na wanafunzi wenye ulemavu mashuleni.

Akitoa maelezo kuhusu juhudi za Serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi, Waziri Mkuu amesema Serikali imesaidia uanzishwaji wa taasisi mwavuli ya kusimamia VICOBA inayoitwa VICOBA FETA ambayo imeanza kuonyesha matunda mazuri.

“Takwimu zilizotolewa mwezi Februari 2016 na taasisi hiyo zinaonesha kuwa kuna vikundi 100,000 vya VICOBA vyenye wanachama milioni 2.2 na mtaji wa shilingi trilioni 1.2. Ni jambo la kujivunia kwamba asilimia 79 ya wanachama wa VICOBA ni wanawake,” amesema.

Amezitaka Halmashauri zote nchini ziweke orodha sahihi ya vyama vya ushirika wa kuweka na kukopa vilivyosajiliwa kwa kila kijiji na kuchukua hatua za kuwezesha uanzishaji na usajili wa SACCOs zinazokidhi vigezo kulingana na shughuli za uzalishaji katika Halmashauri husika.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, APRILI 22, 2016.

--
Irene K. Bwire

Sad News: Mwanamuziki Nguli wa Congo Papa Wemba Afariki Dunia

$
0
0

Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani.

Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi

Papa Wemba  alipoanguka na kupoteza fahamu katikai ya onesho

Taarifa ya Utekelezaji Ya Kamati Ndogo ya PAC Kuhusu Mkataba wa Lugumi

Tamko La Jukwaa La Wahariri Juu Ya Matangazo Ya Bunge

$
0
0
Bodi ya Jukwa la Wahariri Tanzania (TEF) iliyokaa Ijumaa Aprili 22, 2016 jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine ilijadili hali ya mwenendo wa tasnia ya habari nchini hasa juu ya haki ya wananchi kupata habari.

Katika kujadili hali hiyo, TEF imeguswa kwa namba ya kipekee kabisa na mwenendo mzima wa urushaji wa bahari za Bunge kwa njia ya redio na luninga, hususan katika mkutano wa tatu wa Bunge la 11 unaoendelea mjini Dodoma kwa sasa.

Itakumbukwa kwamba Muhimili wa Bunge kupitia Kitengo chake cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Aprili 15 2016 ulitoa taarifa kwa umma ikieleza utaratibu mpya ambao sasa umeanza kutumika katika kurusha matangazo ya redio na luninga kutoka Bungeni.

Katika taarifa hiyo, Ofisi ya Bunge ilisema kuwa imeamua kuboresha mfumo wa urushaji wa Matangazo ya Bunge kwa Bunge lenyewe kurusha Matangazo ya Vikao vyake pamoja na Vipindi mbalimbali vyenye Maudhui kuhusu Shughuli za Bunge ambazo hazijapata fursa ya kufahamika vyema kwa umma kuanzia katika Mkutano wa Bunge la Bajeti unaoendelea sasa.

Ofisi hiyo ilisema kuwa mfumo huo mpya ni Utamaduni wa kawaida kwa kila Bunge hususani Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola kuwa na Studio zake kwa lengo la kurusha Matangazo ili yawafikie wadau kwa lengo la kurusha kupitia vituo vyao. Kwa maana hiyo, Bunge lilisisitiza kuwa chini ya utaratibu huo mpya, jukumu la kurusha Matangzo ya Vikao vya Bunge litafanywa na Bunge lenyewe kupitia FEED MAALUM ili kurahisisha kila Kituo cha Radio na Televisheni kupata Matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga Mitambo yao Bungeni Dodoma.

Katika kutekeleza uamuzi huo na mfumo huo mpya, kila kituo cha Televisheni na Redio sasa watatumia Masafa ya Matangazo ya Bunge (Frequencies) bure kupitia FEED MAALUM itakayorushwa na Satellite ya INTELSAT 17 ambayo iko nyuzi 66 Mashariki kwa masafa maalum ambayo pia yaliwekwa wazi.

Kwa mantiki hiyo, Bunge sasa limezuia vituo vyote vya televisheni nchini kupeleka kamera zake ndani ya Bunge kwa kuwa habari hizo zitapatikana kwenye feed maalum ambayo ni ya Bunge ambayo inasimamiwa na waandishi wa Bunge ambao pia ndio wanaamua nini kionyeshwe kwa utashi wao.

Baada ya kutafakari hatua hizi mpya za Bunge na baada ya kufuatilia kile kinachorushwa, mambo kadhaa yamethibitika:-

Mosi, habari kutoka ndani ya Bunge sasa zinachujwa mno kupitia mfumo huu mpya wa feed maalum;

Pili, ubora za picha zinazorushwa kupitia feed hii nao ni wa kiwango cha chini pia;

Tatu, kwa mantiki ya kawaida kabisa, hatua hizi zote zimepunguza na kukwaza haki ya wanahabari kufanya kazi yao kwa uhuru, lakini pia inawanyima wananchi haki ya kupata kwa uhakika na bila kuchujwa kile kinachofanywa na wawakilishi wao.

Kwa kuzingatia haya yote, TEF inasema bayana kwamba:

 Hatua hizi mpya za kuzuia kamera za televisheni kuingia Bungeni ni hatua za dhahiri kabisa za kukwaza uhuru wa habari nchini na kukuza censorship nchini. Hali hii haisaidii siyo Bunge tu, bali hata wabunge, wananchi na taifa kwa ujumla katika kupiga hatua za kweli katika kujenga demokrasia na kulinda haki za kupata habari na uhuru wa kujieleza nchini;
 
    TEF imeanza kuingiwa na hofu kwamba sababu za awali zilizokuwa zimetolewa za kuzuia utangazaji wa moja kwa moja wa Bunge kupitia TBC kwa sababu ya gharama, huenda hazikuwa za dhati. Hali hii imejionyesha hasa baada ya vituo binafsi vya televisheni kujitokeza na kuendelea kuonyesha vikao vya bunge moja moja, lakini navyo sasa vimenyimwa fursa hiyo kwa utaratibu huu mpya wa feed maalum.

    Ni dhahiri sasa, ushiriki wa wananchi katika kufuatilia mwenendo wa Bunge na wabunge wao umekwazwa sana kwa hatua hizi mpya na kwa maana hiyo, kupunguza ushiriki wa wananchi katika mfumo wa utawala wa nchi yao.

Kwa kuzingatia haya yote, TEF inatoa rai kwa uongozi wa Bunge kufikiria upya hatua hizi za kuzidi kufunika shughuli za Bunge kwenye blangeti zito la usiri na censorship, hivyo uruhusu kituo chochote cha televisheni chenye nia, uwezo na utayari wa kurusha matangazo ya Bunge moja moja bila kulazimika kujiunga na feed maalum iliyoanzishwa.

Tunaamini kwamba kama hali hii ya kutumia feed maalum itaachwa iendelee hakika Tanzania kama taifa tunapiga hatua nyuma kwa yale mazuri machache tuliyokuwa tumeyafikia, mojawapo, uhuru wa Bunge kuendesha mambo yake kwa uhuru na uwazi mkubwa hivyo kuwa mfano mojawapo wa taasisi za umma zinazojiendesha kwa uwazi.

Imetolewa leo, Jumapili Aprili 24 2016 jijijni Dar es Salaam na Jukwaa la Wahariri Tanzania.

Theophil Makunga                 Neville Meena

Mwenyekiti                             Katibu

Bomba la Mafuta Kutoka Uganda kuingiza Bilioni 4.8 Kila Siku

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga ukikamilika utaliingizia Taifa Sh4.8 bilioni kila siku.

Amesema fedha hizo zitatokana na usafirishaji wa mapipa 200,000 kila siku yatakayotozwa dola 12.2 (zaidi ya Sh24,000) kila moja. 

Profesa Muhongo alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini akitokea Kampala ambako Rais wa Uganda, Yoweri Museveni juzi alitangaza kuwa bomba hilo la mafuta ghafi kutoka Hoima, Ziwa Albert litapita katika ardhi ya Tanzania kwenda Bandari ya Tanga.

Alisema katika kujipanga kwa ajili ya mradi huo, tayari Serikali imetoa kibali kwa wanafunzi 22 ambao wamepelekwa nje ya nchi kusomea masuala ya mafuta na gesi katika ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu. 

“Bomba litakamilika Juni 2020 na itakuwa ni zawadi kwa Rais John Magufuli kabla hajarudisha fomu ya kuomba tena kugombea awamu ya pili ya urais.Lakini tutajitahidi likamilike kabla ya muda huo,” alisema Profesa Muhongo.

Alisema utakapokamilika, yatahitajika magari 100,000 ya kutolea mizigo katika Bandari ya Tanga.

Juzi, taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa ilieleza kuwa Serikali ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wa kutumia Bandari ya Tanga.

Rais Museveni alitangaza uamuzi huo wakati wa mkutano wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika jijini Kampala juzi na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga na Profesa Muhongo. 

TAKUKURU Yaanza Kuchunguza Mabilioni ya Kikwete

$
0
0

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza kuchunguza fedha za uwezeshaji maarufu kama ‘Mabilioni ya JK’ ambazo hazikurejeshwa na wakopaji nchi nzima. 

Msemaji wa Takukuru, Tunu Mleli alisema jana kuwa taasisi hiyo imechukua jukumu hilo kwa sababu moja ya majukumu yake ni kuchunguza masuala ya rushwa na kutoa rai kwa mtu mwenye ushahidi au taarifa kuhusu suala hilo kuzitoa kwa taasisi hiyo.

“Takukuru ipo wazi kuzipokea taarifa hizo ili zitusaidie kwenye uchunguzi,” alisema Tunu.

Kati ya Sh50 bilioni zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, ni Sh43 bilioni tu zilizorejeshwa, huku Sh7 bilioni zikidaiwa kutafunwa. 

Fedha hizo zilitolewa na Kikwete kwa ajili ya kuwawezesha kimitaji, wajasiriamali nchi nzima, mikopo ambayo ilipitia benki za CRDB, NMB, Community Bank na Benki ya Posta Tanzania. 

Fedha hizo kutoka Mfuko wa Rais, zilikuwa zikikopeshwa kwa riba ya asilimia 10, ambapo asilimia mbili ilikuwa inaingia serikalini na nane ilikuwa inabaki kwenye benki hizo. 

Hata hivyo, baadhi ya vyama vya Akiba vya Kuweka na Kukopa (Saccos), vilivyopewa fedha hizo, vilitoa mikopo hiyo kiholela, huku baadhi ya viongozi wakidaiwa kutengeneza majina feki na kukopeshana fedha hizo. 

Imedaiwa kuwa Saccos nyingi ambazo zilifuja fedha hizo katika mikoa mbalimbali, viongozi wake wengi walikuwa pia ni viongozi wa kisiasa na wengine wakiwa na nyadhifa serikalini. 

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, baadhi ya waliokopeshwa fedha hizo na Saccos mbalimbali, hawakuwa wanachama, bali walichomekwa baada ya kuonekana kuna fursa ya ‘kupiga dili’.

Chanzo kutoka Takukuru, kimedokeza  kuwa makamanda wa taasisi hiyo katika mikoa mbalimbali, wamepewa maelekezo ya kuchunguza mahali yalipo mabilioni hayo na nani waliyafuja.

 “Ni kweli tumepewa maelekezo ya kuchunguza fedha hizo. Unajua hizi ni fedha za umma haziwezi kutafunwa tu hivihivi na Serikali ikakaa kimya,” alidokeza mmoja wa maofisa wa Takukuru. 

Machi mwaka jana, aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Christopher Chiza aliagiza kufanyika kwa ukaguzi wa kina wa fedha hizo.

Alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake katika Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (Neec), ambako aliagiza watakaobanika kuhusika na ubadhirifu wa fedha hizo wachukuliwe hatua za kisheria.

“Lazima tuangalie mabilioni ya JK yalipotelea wapi, yalivyofujwa na wahusika wapo wapi ili sheria ichukue mkondo wake. Nimeambiwa kuna zilizobaki tujue ziko wapi,” alikaririwa Chiza akisema. 

Lakini Desemba 24, 2013, mtangulizi wa Chiza, Mary Nagu alikaririwa akisema Sh43 bilioni kati ya Sh50 bilioni za mabilioni ya JK zilizokopeshwa kwa wajasiriamali 74,701 zilikuwa zimerejeshwa. 

Nagu alitoa takwimu hizo alipokuwa akizungumzia mafanikio ya Serikali ya Rais Kikwete katika, utaratibu uliofanywa pia na wizara nyingine. 

Suala la mabilioni hayo ya JK limekuwa likiibuka mara kwa mara bungeni na katika mitandao mbalimbali ya kijamii huku wananchi wakitaka zirejeshwe.

Nape Ataja Majipu Manne Katika Sanaa Nchini,aahidi Kuyatumbua

$
0
0

Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na michezo nchini,Nape Nnauye ametaja mambo manne ambayo ni vikwazo ndani ya sekta ya sanaa ya filamu nchini na kuyaita kwamba ni majipu huku akisisistiza kwamba serikali itakwenda kutunga sera ya sekta hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17.

Nape,aliyataja mambo hayo na kuyafananisha na majipu kuwa ni uporaji wa kazi za wasanii nchini,ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za wasanii nchini,usimamizi mbovu wa bodi ya filamu nchini sanjari na tatizo la mfumo mbovu wa usambazaji wa kazi za wasanii nchini.

Akizindua tamasha la filamu la Tanzanite International Film
Festival(TIFF) jijini Arusha juzi ambao ulihudhuriwa na wasanii maarufu wa filamu nchini waziri huyo alisema kwamba jipu la kwanza ambalo atakwenda kulitumbua ni uporaji wa kazi za wasanii nchini.
 
“Jipu la kwanza tutalitumbua kwenye bajeti yetu ya mwaka 2016/17 ni uporaji wa kazi za wasanii nchini wengi wananyonywa jasho lao”alisema
Nape

Hatahivyo,alisema kwamba jipu la pili ni ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za wasanii za filamu nchini na kudai kwamba chini ya uongozi wake atahakikisha anaimarisha miundombinu bora kwa lengo la kuwasaidia wasanii hao pamoja na kulinda haki zao.

Alisema ya kwamba mfumo wa kazi za usambazaji wa kazi za wasanii nchini pamoja na hakimiliki ni wa kinyonyaji huku akitolea mfano wa kazi za msanii maarufu wa sanaa hiyo nchini marehemu Stephen Kanumba na kusema kwamba familia yake hainufaiki na matunda ya kazi zake hadi sasa kutokana na mfumo mbovu wa usimamizi wa kazi za wasanii nchini.

Alitaja takwimu kwamba mwaka 2011/12 jumla ya filamu 218
zilitengenezwa nchini na mwaka 2014/15 kazi hizo ziliongezeka hadi kufikia 14,00 huku akidai hilo linadhihirisha kwamba sekta hiyo inakua kwa kasi nchini na kuongeza ajira 
 
Hatahivyo,Rais wa shirikisho la wasanii wa filamu nchini(TAFF),Simon Mwakifamba aliwataka wasanii wa filamu nchini kujiandaa kisaikolojia kukabiliana na soko la ushindani wa filamu duniani kwa kuwa wabunifu.

“Serikali tunaiomba iandae sera itakayoandaa mazingira mazuri kwa wasanii nchini kuhusu usalama wa kazi zao”alisema Mwakifamba

Naye, muaandaji wa tamasha hilo,Said Sassi alisema kwamba tatizo la uharamia wa kazi za wasanii nchini limetanda na kuwaomba wafanyabiashara na makampuni kujitokeza kudhamini vipindi mbalimbali vya luninga kwa lengo la kuinua sekta hiyo.

Mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya vito ya Tanzanite One Mining Ltd ambao ni miongoni mwa wafadhili wa tamasha hilo,Feisal Shabhai alisema lengo la kampuni yao kujitosa kufadhili tamasha hilo ni kutoa mchango wao katika kusaidia jamii kupitia faida wanayoipata ili kuinua sekta ya ajira nchini.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 25


CAG Kuanika Mafisadi Bungeni Leo Wakati Akiwasilisha Ripoti Yake

$
0
0

Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) leo anawasilisha bungeni ripoti ya mwisho ya ukaguzi wa hesabu za serikali ya mwaka 2014/15.

Ingawa haijajulikana rasmi nini kilichomo ndani yake, baadhi ya watu waliohojiwa wanatarajia CAG kubaini mchwa wanaotafuna fedha za umma na namna ya kukabiliana nao.

Aidha wengine wanatarajia taarifa ya hali bora zaidi ya usimamizi wa fedha za umma kuliko kipindi cha nyuma. 

Ripoti hiyo awali ilikuwa imepangwa kuwasilishwa bungeni mwishoni mwa wiki (Aprili 22) kabla ya kuahirishwa hadi leo.

“Ni kweli CAG atawasilisha ripoti kesho (leo) bungeni, ”Naibu Katibu wa Bunge na Utawala, Joel Joel alithibitisha juu ya kuwasilishwa kwa ripoti hiyo leo. 

Miongoni mwa wabunge waliozungumza na mwandishi wa habari hizi, wamesema wanatarajia CAG kuonesha mambo mazuri kwa maana ya taasisi zilizofanya vizuri katika usimamizi wa fedha za umma lakini pia mambo mabaya.

“Lazima ripoti itaibua madudu maana walizoea (watendaji serikali) kana kwamba hapakuwapo na serikali,” alisema Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy na kusisitiza kuwa pamoja na wabunge wenzake, watamsaidia Rais John Magufuli kupambana na ubadhirifu serikalini.

Keisy alisema akiwa mbunge, anaamini pamoja na wenzake, wanachosubiri ni kuona ripoti hiyo na kuhakikisha wanaohusika na kuchezea fedha za serikali, kabla ya kufikishwa mahakamani, wanarudisha fedha hizo. 

“Atakachosema CAG sisi tutakuwa tayari kusimama kusaidia Rais aendelee kupambana na ubadhirifu,” alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mbinga Vijijini, Martin Msuha, alisema ripoti hiyo ni muhimu katika usimamizi wa serikali na inategemewa kuwa na mambo mazuri na mabaya kwa maana ya majipu ambayo yatapaswa kutumbuliwa.

Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza alisema matarajio waliyo nayo ni kwamba ubadhirifu na wizi utakaoibuliwa na ripoti hiyo utashughulikiwa mara moja.

 “Kama kuna ubadhirifu, mishahara hewa na wizi vyote vishughulikiwe...kama kuna ubadhirifu na wizi wowote, mwizi mahali pake ni jela,” alisema Rweikiza akishutumu uwapo wafanyakazi hewa katika halmashauri yake.

Mwenyekiti wa Halmashauri mbaroni kwa kuhifadhi wahamiaji haramu nyumbani

$
0
0

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Simon Kagoli amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuhifadhi wahamiaji haramu nyumbani kwake na kuwatumikisha mashambani.

Kagoli ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kageji, anakabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kuishi na watu ambao sio raia, kuwasaidia raia wa kigeni kutenda kosa na kuajiri na kuwatumikisha wageni shambani mwake. 

Kesi hiyo namba 114/2016 iko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Kibondo, Robert Male.

Mwendesha Mashitaka wa Uhamiaji, Richard Mwangole alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa makusudi huku akijua kuwa kuhifadhi wahamiaji haramu ni kosa kubwa. 

Anatuhumiwa kuwafanyisha kazi wahamiaji hao na kuwalipa ujira wa Sh 110,000 kila mmoja. Male alikana makosa na yuko nje kwa dhamana.

Alidhaminiwa na wadhamini wawili, kila mtu kwa dhamana ya Sh milioni moja.

Viongozi wa Chama cha UDP Watimkia CCK

$
0
0
Viongozi wa Chama cha UDP wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Kijamii (CCK), kwa madai kinaongozwa kibabe, hakuna mikutano wala vikao vinavyofanyika ili kukijenga.

Viongozi hao ni aliyekuwa mkurugenzi wa uchaguzi wa UDP na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya na Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam na mjumbe wa kamati kuu, Joachim Mwakitiga.

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa kadi za chama chao kipya jana, viongozi hao walisema UDP imegeuzwa mali ya mtu mmoja ambaye huamua mustakabali wa chama kwa matakwa yake. 
 
Mwakitiga alisema uhai wa chama ni mikutano ambayo inawapa fursa viongozi kujadili na kupanga mikakati ya kukijenga.

Alisema jambo la kushangaza kwenye chama hicho mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, John Cheyo haitishi mikutano wala vikao vya ndani. 

Makunganya alidai kwa miaka mitano chama hicho hakijaitisha mikutano wala vikao vya kamati kuu na halmashauri kuu ya chama.

Alisema chama ni taasisi na taasisi ni watu, hivyo, viongozi waanzilishi wanatakiwa kufahamu kwamba chama siyo mali yao bali ni ya wanachama wote. 

Makunganya alisema amejiondoa katika chama hicho ili kutafuta demokrasia ya kweli sehemu nyingine.

Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi alisema wameanza operesheni ya kukijenga chama chao na viongozi wataanza kuzunguka nchi nzima kufungua matawi na kuchagua viongozi. 
Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma (kulia), akizungumza wakati wa kuwapokea viongozi hao. Kushoto Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara aliye hamia CCK.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam, Joachim Mwakitiga aliyejiunga na chama hicho na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya aliyehamia chama hicho.

Nafasi za Kazi Tumaini University

Nafasi za Kazi Iringa Urban Water Supply ( IRUWASA )

Serikali Yaunda Kamati Ya Kuanzisha Tume Ya TEHAMA

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, ameunda Kamati ya mpito ya kusimamia uanzishwaji wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  (TEHAMA) ambapo ameipa miezi sita kufanya kazi kuanzia mwezi Aprili, 2016 ya kuhakikisha kuwa Tume ya TEHAMA inaanza kazi rasmi.

Katika kuhakikisha kuwa Tume ya TEHAMA inaanza kazi mara moja, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano, Prof. Faustin Kamuzora, amewakabidhi wajumbe wa Kamati hiyo Amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na.532 iliyotolewa kupitia gazeti la Serikali Na. 47 la tarehe 20 Novemba, mwaka 2015 iliyoanzisha Tume na Hadidu za Rejea zinazoainisha majukumu yao.

Majukumu hayo ni pamoja na kusimamia uanzishwaji wa Tume, kuandaa sheria ya kuanzisha Tume, na kutengeneza Mpango Mkakati wa Tume. 

Prof. Kamuzora amewataka wajumbe wa Tume hiyo  kuepuka kuweka mitazamo au maslahi binafsi ya wao wenyewe au ya taasisi zao katika kipindi cha kuanzisha Tume, bali waishauri Serikali namna nzuri ya kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaanza kazi ya kusimamia na kuratibu masuala ya TEHAMA nchini.

Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao na Katibu wa Kamati ya Kuanzisha Tume ya TEHAMA nchini ni kama ifuatavyo:
  1. James Kilaba (Mwenyekiti), Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,
  2. Samson Mwela (Katibu), Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
  3. Idris Rai (Mjumbe), Makamu Mkuu wa Chuo, SUZA,
  4. Joan Mbuya (Mjumbe), Mkurugenzi wa Sera na Mipango-Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali,
  5. George Mulamula (Mjumbe), Mkurugenzi Mtendaji-DTBi,
  6. Juma Rajabu, (Mjumbe), Mkurugenzi Mtendaji-Maxcom Africa,
  7. Maharage Chande, (Mjumbe), Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Ofisi ya Rais-President’s Delivery Bureau, na
  8. Nicolaus Mhonyiwa (Mjumbe), Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA-Ofisi ya Msajili wa HAZINA.
Aidha, Tume ya TEHAMA inatarajiwa kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na yafuatayo: Kushiriki katika kushauri juu ya uwekezaji wa TEHAMA nchini kwa ubia na sekta binafsi; kuwatambua, kujenga uwezo na kuwaendeleza wataalam wa TEHAMA; kushauri na kushiriki pamoja na wadau katika tafiti za TEHAMA, uwekaji viwango na ubunifu katika sekta ya TEHAMA; na kushiriki katika kusimamia miundombinu na programu za kitaifa za TEHAMA.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano, Dkt. Eng. Maria Sasabo, alisisitiza kuwa Kamati ina kazi kubwa ya kuona namna bora zaidi ya kuhakikisha kuwa Tume itatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na masuala ya uwekezaji; na kusimamia vema  viwango vya wataalamu wa Sekta. Naye Mwenyekiti, Inj. James Kilaba, kwa niaba ya Kamati alishukuru kwa kuaminiwa na Serikali na pia aliahidi kuwa watatekeleza majukumu yao kikamilifu. Pia alimalizia kwa kusema, “hatutawaangusha”.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikali

Nafasi Mbalimbali za Kazi Toka Benki ya NMB....Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 4 Mwezi wa 5

$
0
0

Jedwali  hapo chini linaonyesha nafasi mbalimbali toka Benki ya  NMB.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na nafasi hizo <<  BOFYA  HAPA> ili  uipakue PDF  yenye maelezo  ya  kina
 

Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako atolea ufafanuzi sera ya Elimu Bure

$
0
0

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewataka walimu na maafisa elimu kusimamia vyema majukumu yao na kuhakikisha utoaji elimu bora kwa wanafunzi ili kupata wataalamu watakaolisaidia taifa.

Waziri Ndalichako, ameyasema hayo Jijini Arusha, alipokutana na wakuu wa shule,maafisa elimu na watendaji wakuu wa idara za elimu ambapo amesisitiza nidhamu ili kusaidia matokea mazuri na ya haraka ya kuboresha elimu nchini.

Waziri Ndalichako, amesema kuwa wataalamu mbalimbali ambao wanahitajia katika idara mbalimbali katika kukuza maendeleo wote wanahitaji zaidi mchango wa sekta ya elimu katika kuwapata wataalamu hao.

Aidha katika ziara aliyoifanya katika mkoa huo wa Arusha, Waziri Ndalichako, ametoa ufafanuzi zaidi wa sera ya elimu bure ambapo amesema kuwa wazazi bado wanajukumu la kushirikiana na serikali katika kuwasadia watoto kupata elimu bora.

Prof. Ndalichako amesema serikali haijawazuia wananchi wanaotaka kuchangia sekta ya elimu kutokana na changamoto zilizopo lakini haiko tayari kuona mwanafunzi anarudishwa nyumbani kwa sababu ya michango ya aina hiyo.

Afisa Uchaguzi Halmashauri Ya Serengeti Ahukumiwa Miaka Saba Jela.

$
0
0

AFISA uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Bw.  Julius Bujabhi Makwasa amehukumiwa kifungo cha Miaka 7 jela baada ya kupatikana na hatia ya Makosa 34 yakiwepo ya Rushwa.

Mnamo mwaka 2013 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mara ilimfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Afisa uchaguzi wa Halmashauri hiyo Bwana Julius Bujabhi Makwasa na wenzake wawili wakishitakiwa kwa makosa thelathini na manne yakiwemo ya matumizi mabaya ya fedha za umma, kuisababishia hasara Halmashauri ya Serengeti, kusaidia kutenda kosa, kughushi na kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri wao.

Washitakiwa wengine katika shauri hilo la uhujumu Uchumi E.C.C 130/2013 lililokuwa likisikilizwa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mheshimiwa Ismail Emanuel Ngaile,  walikuwa  Bi Scola Daudi Mosi ambaye ni mtunza kumbukumbu wa Halmashauri hiyo na Bwana Dickson Julius Makwasa ambaye ni mtoto wa mshitakiwa wa kwanza.

Ilidaiwa na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Wakili Martin Makani mbele ya mheshimiwa Ngaile kwamba mshitakiwa wa kwanza Julius Makwasa  ambaye majukumu yake yalikuwa pamoja na kuviteketeza vifaa vya uchaguzi muda wa uchaguzi unapopita na mshitakiwa wa pili Scola Mossy ambaye  majukumu yake ni pamoja kusimamia kumbukumbu zinazoingia na zinazotoka nje ya Halmashauri hiyo,  kwa nafasi zao hizo,  walikuwa na jukumu la kuharibu nyaraka za uchaguzi mkuu wa Octoba 2010 kama ilivyokuwa imeelekezwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Katika kutekeleza jukumu hilo ilielezwa kwamba, waliandaa majina ya vibarua na kuingiza majina hewa ishirini na tano (25) kuonyesha kwamba majina hayo hewa pia yalishiriki  kuchimba mashimo, kusomba nyaraka hizo za uchaguzi na kuzipeleka kwenye mashimo kisha kuziteketeza kwa moto hivyo kustahili malipo.

Katika udanganyifu huo ilielezwa kwamba, mshitakiwa wa kwanza na wa pili waliweza kuandaa nyaraka za kuipotosha Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kuwawezesha kujipatia jumla ya shilingi million tatu laki nane na elfu hamsini (Tsh 3,850,000/=) kwa kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri .

Aidha katika mashitaka hayo, mshitakiwa wa tatu Dickson Makwasa ambaye ni mtoto wa mshitakiwa wa kwanza yeye alishitakiwa kwa kosa moja la kusaidia kutenda kosa kwa maelekezo ya baba yake Julius Bujabhi Makwasa, ambapo ilielezwa na upande wa mashitaka kuwa alielekezwa na baba yake kutafuta na alitafuta wanafunzi wenzake na kuwapeleka ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa mtunza fedha na huko walitakiwa kutia sahihi mbele ya majina hewa yaliyokuwa yameorodheshwa  kisha kulipwa fedha zilizoainishwa kwa kila jina kama kwamba ni wao walifanya kazi ya kuteketeza vifaa hivyo vya uchaguzi.

Hata hivyo baada ya kupokea fedha hizo wanafunzi hao walitakiwa wazikabidhi kwa mshitakiwa wa tatu na wakazikabidhi, ambaye naye alimkabidhi mshitakiwa wa kwanza ambaye ni baba yake.

Baada ya mahakama kupitia ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka na ule wa utetezi iliridhika kwamba mshitakiwa wa kwanza alitenda makosa yote (33) aliyoshitakiwa nayo na hivyo kuhukumiwa kifungo, kulipa faini ya shillingi millioni tano (Tsh.5,000,000/=) au kifungo jela miaka saba na kurejesha fedha jumla ya shilingi million tatu, laki nane na hamsini elfu ( 3,850,000/=) hasara aliyoisababishia Serikali, alishindwa kulipa fedha hizo na kupelekwa jela kuanza kutumikia kifungo.

Mshitakiwa wa pili alionekana hana hatia hivyo mahakama ilimuachia huru, kwa upande wa mshitakiwa wa tatu ambaye kosa lake lilikuwa kusaidia kutenda kosa kwa maelekezo ya baba yake alipatikana na hatia ya kosa hilo na alihukumiwa kulipa faini ya shilingi million moja (TSH.1000,000/=) au kwenda jela miaka mitatu, aliweza kulipa fedha hizo na akaepuka kifungo.

TAKUKURU Mkoa wa Mara inatoa mwito kwa wazazi hasa walio kwenye utumishi wa umma kuacha tabia ya kuwashirikisha watoto katika kufanikisha vitendo vya uvunjaji wa sheria, kwa kuwa kuendelea kufanya hivyo kutapelekea kujenga jamii ya kihalifu kutokana na vijana kuiga tabia za kihalifu zinazoonyeshwa kwao na wazazi.
 
IMETOLEWA NA
HOLLE J. MAKUNGU 
MKUU WA TAKUKURU(M)MARA
25 APRILL 2016.

CAG Akabidhi Ripoti ya Ukaguzi ya Mwaka wa fedha Unaoishia Juni 30, 2015.

$
0
0

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad amekabidhi ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 bungeni leo mjini Dodoma ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.

Katika ripoti yake, CAG ametoa mapendekezo kadhaa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuboresha matumizi ya fedha za Serikali kwa malengo yanayokusudiwa.

Miongoni mwa maeneo ambayo CAG ametoa mapendeklezo ni Ofisi ya Masjili wa Vyama vya Siasa nchini ifuatilie suala la uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa wakati kulingana na matakwa ya sheria.

Hatua hiyo ya CAG inafuatia ukaguzi uliofanywa kwenye vyama vya siasa nchini vyenye usajili wa kudumu ambavyo jumla yao ni vyama 22.

Prof. Assad alisema kuwa kati ya vyama hivyo vyenye usajili wa kudumu, ni chama kimoja ndicho kilichowasilisha hesabu zake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni 2015 ambacho ni Chama cha Wananchi (CUF).

Vyama vingine 21 havikuwasilisha vitabu vya hesabu kwa ajili ya ukaguzi kinyume cha kifungu Na. 14 cha Sheria ya vyama vya siasa Na. 5 ya mwaka 1992.

Trafiki afariki Dunia Kwa Kugongwa na Gari Wakati akiongoza magari

$
0
0

Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Pwani kituo cha Kibaha, EX.F 8471 PC Joseph Mchiwa  amefariki baada ya kugongwa na gari usiku wa kuamkia jana eneo la kwa Mbonde mjini Kibaha wakati akishughulikia tukio la ajali ya basi mali ya kampuni ya Champion ililokuwa limeacha njia na kuingia kwenye mtaro uliopo eneo hilo.

Ajali hiyo ya basi ilisababisha msongamano mkubwa wa magari katika barabara kuu ya Dar es Salaam- Morogoro kwa zaidi ya saa  mbili na hivyo ilimlazimu askari  huyo pia kuyaongoza magari yaliyokuwa yamekwama  kutokana na kuwepo foleni katika eneo hilo.

Kamanda wa Polisi Pwani, Boniveture Mushongi alisema askari huyo ambaye ni Trafiki wa Mailimoja na mkazi wa Kimara alikua zamu usiku huo na kama kawaida ilipotokea ajali ya basi la kampuni ya Champion alifika eneo la ajali kuishughulikia na wakati akitekeleza kazi hiyo ndipo saa 3:30 usiku alipogongwa na gari ingine iliyokuwa katika mwendo kasi na kufariki papo hapo.

Matukio Ya Ubakaji Yaongezeka Nchini Na Kufikia 1765.

$
0
0

Matukio ya ubakaji hasa kwa watoto wadogo yamekuwa yakiongezeka kwa kiwango kikubwa, ongezeko hili limebainika kutokana na ufuatiliaji tulioufanya kupitia matukio yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi ambapo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2016 kumeripotiwa matukio 1765 ukilinganisha na matukio 1585 katika kipindi kama hicho mwaka 2015 ikiwa ni ongezeko la matukio 180.

Katika matukio ya Januari hadi machi 2016, jumla ya watuhumiwa 823 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani ingawa bado kumekuwa na tabia ya wazazi na walezi kuficha watuhumiwa wa ubakaji na  kumaliza kesi hizo kirafiki au kifamilia jambo ambalo ni kinyume cha sheria bila kuzingatia madhara aliyoyapata mtoto.

Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linakemea vikali wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo viovu vya ubakaji na wazazi ama walezi wanaofumbia macho vitendo hivyo na kuingia makubalino na watuhumiwa kwa kupeana fedha kama fidia ili wamalize kesi kiundugu au kifamilia.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa  Wazazi, walezi, Viongozi wa dini, Asasi za kiraia, walimu na Wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano katika kushughulikia vitendo hivyo ikiwemo kuwafichua wazazi au walezi wanaofanya makubaliano ya kumaliza kesi za ubakaji kirafiki au kifamilia ili kukomesha vitendo hivyo.

 Imetolewa na:
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Makao Makuu ya Polisi.   
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images