Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Video: Makonda Atangaza VITA na Wafanyakazi Hewa jijini Dar es Salaam

$
0
0

Muu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kazi ya kutafuta watumishi hewa katika manispaa za jiji la Dar es Salaam bado linaendelea baada kubaini njia chafu wanazotumia watumishi hewa hao.

Akizungumza leo na waandishi habari ,Makonda amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ni kioo kwa nchi hivyo jitihada zinaendelea ya kutafuta na kazi hiyo itafanywa sekta kwa sekta.

Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya katika jiji la Dar es Salaam hakuna kufanya kazi yeyote mpaka wamelize kutafuta watumishi hewa kwa kutumia malipo ya watumishi kutoka taasisi za fedha(Pay Row).

Makonda amesema idadi ya watumishi hewa 71 aliowasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –Tamisemi, Georgre Simbachawene  ni ndogo katika  jiji la Dar es Salaam hivyo kazi lazima iwe endelevu.

Amesema kuwa watumishi Hewa hawawezi wakawa wanalipwa mshahara huku wanaofanya kazi kwa moyo mmoja wanajisikia  vibaya hivyo ni lazima watafutwe na wachukuliwe hatua na vyombo vya dola.

Mkuu Mkoa amesema kuwa kati ya watumishi hewa 71 ni watumishi 34 hewa wamefunguliwa mashitaka katika mahakama mbalimbali kutokana kuchukua fedha wasioifanyia kazi.

==> Zaidi, Tazama video hii kumsikiliza Paul Makonda akiongea

Kampuni ya Lugumi Yajitokeza na Kusema Mkurugenzi wake Hajatoroka nchi.....Bofya Hapa Kuisoma Taarifa Yao

$
0
0

Lugumi  Enterprises ni kampuni iliyoandikishwa na kufanya kazi hapa Tanzania na imekuwa ikifanya kazi mbalimbali ikiwemo ununuzi na ufungaji mashine za utambuzi wa alama za vidole yaani Automated FingerPrint Information System (AFIS)

Hivi karibuni kumekuwa na habari zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kwa namna ambayo inapotosha ukweli kuhusu kampuni yetu iliyotekeleza mradi huu muhimu kwa nchi yetu na, mradi wa AFIS. 

Aidha taarifa hizo katika mitandao na magazeti mbalimbali imekuwa ikitoa habari zisizo na ukweli wowote kuhusu mtendaji mkuu Bwana Said H. Lugumi.

Ukweli ni kwamba mnamo mwaka 2011 Jeshi la Polisi liliingia mkataba na kampuni ya Lugumi Enterprises Limited wa kufunga mitambo ya utambuzi kwa kutumia alama za vidole (AFIS) katika vituo vya Polisi kwa mujibu wa matakwa ya Jeshi. Vituo vilikuwa nchi nzima Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za kampuni yetu, ukweli ni kwamba mkataba huu umetekelezwa nasi kwa kushirikiana na wabia wetu katika kuhakikisha mkataba huo unatekelezwa ipasavyo.

Kwa mujibu wa mkataba, kama kuna mgogoro katika utekelezaji,upande usioridhika na utekelezaji wake, utatangaza mgogoro kwa mwanasheria mkuu.

Si jeshi la polisi kwa upande mmoja wala sisi kwa upande mwingine aliyetangaza mgogoro wowote dhidi ya mwingine,kwa mujibu ya matakwa ya mkataba.
  
Kwa mantiki hiyo basi, mambo yaliyo mengi yalitajwa katika vyombo vya habari si ya kweli na ni upotoshaji mkubwa na ni muhimu kuyapuuza, na kuendelea na shughuli za kawaida za ujenzi wa taifa. 

Ni katika muktadha huo huo tunapenda kuujulisha umma kwamba tuhuma nyingi za uzushi zimetungwa kumwelekea Mtendaji Mkuu Bwana Said H. Lugumi ikiwemo kuzushiwa kutoroka na kukamatwa nje ya nchi na kadhalika.

Taarifa hizo ni uzushi mtupu, ni za kupuuza, Mkurugenzi wetu yuko nchini na anaendelea na shughuli zake za kawaida.

Imetulazimu kuandika na kueleza haya maana tumeona  vyombo vya habari vimezidi kuandika na kupotosha umma kuhusu jambo hili.

Mwili Uliozama na Gari Baharini Jijini Dar es Salaam Wapatikana

$
0
0
Mnamo majira ya saa 10 alfajiri, gari aina ya Hiace  iliteleza toka kwenye kivuko na kutumbukia katika bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam.

Gari hiyo ilikuwa na abiria wawili. Mpaka majira ya asubuhi, jeshi la zimamoto na uokoaji lilifanikiwa kuupata mwili mmoja na likaendelea kuutafuta mwili wa pili. 
 
Mchana  huu  umepatikana mwili wa pili  wa Nice Karagwe  huku zoezi la kuitoa gari likiendelea

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Atumbua Watumishi Watano Ilemela Kwa Tuhuma za ubadhirifu wa Fedha za Umma

$
0
0

Mkuu wa wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amewasimamisha kazi maofisa watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka.

Akiwa katika ziara ya siku moja ya kujitambulisha wilayani Ilemela leo, Mongella ameagiza kushushwa cheo kwa ofisa wa ardhi wa wilaya hiyo, Anicet Rweyemamu kwa tuhuma za kushindwa kusimamia watumishi walio chini yake wanaotuhumiwa kupokea Sh12 milioni kutoka kwa mwananchi mmoja aliyekuwa akitaka ardhi, lakini hajapewa hati hadi sasa.

Wengine walioangukiwa na rungu la mkuu huyo ni Debora Tongora ambaye pamoja na Alex Chigulu wanatuhumiwa kupokea fedha hizo kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kuwapatia viwanja.

Wakati Tongola tayari amefunguliwa mashtaka dhidi ya tuhuma hizo, Chigulu amehamishiwa mkoani Singida lakini Mongella ameagiza arejeshwe Mwanza ili afikishwe mahakamani.

“RPC wasiliana na mwenzako wa Singida ili huyo mtumishi atiwe mbaroni muda huu na kesho arejeshwe Mwanza kukabiliana na mashtaka dhidi yake. Hatuwezi kuwavumilia watumishi wanaoharibu sehemu moja halafu wanakimbia uhamisho kwenye maeneo mengine,” amesema Mongella

Ofisa uvuvi wa Kituo cha Kirumba, Ivon Maha ameshushwa cheo huku Peter Revelian akiondolewa kutoka nafasi ya mweka hazina.

Watumishi hao wa Idara ya Uvuvi wameondolewa madarakani baada ya kutuhumiwa kuhusika na upotevu wa zaidi Sh40 milioni zilizotokana na kodi na ushuru.

Awali, Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Manju Msambya alimweleza Mongella kuwa wilaya hiyo tayari imetengeza madawati 7, 200 kati ya 29, 000 yanayohitajika.

“Wilaya yetu inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu katika shule za umma na tayari tumewasilisha maombi ya walimu wapya,” amesema Msambya

Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulungi alimuahidi mkuu huyo wa mkoa kuwa baraza lake litaongeza juhudi katika usimamizi wa utendaji kwa watumishi wa halmashauri hiyo.

Waziri Mkuu Aongoza Wakazi Wa Dodoma Mazishi Ya Askofu Isuja wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya waumini na wakazi wa mkoa wa Dodoma katika mazishi ya Mhashamu Askofu Mstaafu, Mathias Isuja wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

Amesema kifo hicho ni pigo kwa watu wote na si kwa kanisa pekee kwa sababu walimtegemea kulisaidia Taifa kiroho na kimaendeleo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 20, 2016) wakati akizungumza na waumini na wakazi wa mkoa huo na mikoa jirani kwenye ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiaskofu la Mtume Paulo wa Msalaba mjini Dodoma.

Askofu Isuja ambaye alizaliwa Agosti 14, 1929 alikuwa Askofu wa kwanza mzalendo katika Jimbo la Kanisa Katoliki la Dodoma. Alistaafu kazi ya uaskofu mwaka 2004 kwa mujibu wa sheria ya kanisa. Alifariki Aprili 13, mwaka huu.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kumuenzi Askofu Isuja kwa kazi nzuri aliyoifanya wakati wa uhai wake na kuyaendeleza yote aliyoyaanzisha kwenye maeneo aliyowahi kuyatumikia.

“Tumepoteza mtu makini, sisi ni mashahidi wa mchango mkubwa wa marehemu siyo tu katika kutoa huduma za kiroho, bali pia huduma za kijamii zilizolenga kuleta maendeleo kwa wananchi katika jimbo hili la Dodoma na katika taifa kwa ujumla,” amesema.

Mapema, akitoa mahubiri wakati wa ibada hiyo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Judathadeus Ruwa’ichi alisema waumini wa kanisa hilo wa mkoa wa Dodoma na Tanzania nzima wanapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha marefu aliyomjalia Askofu Isuja.

“Tunapaswa kumshukuru kwa maisha marefu ambayo Mungu alimzawadia baba yetu Isuja. Katika Zaburi ya 90 tunasoma kuwa mwanadamu ana miaka ya matazamio ambayo ni 70, lakini yeye alipewa miaka ya matazamio 70 na akazawadiwa nyongeza ya miaka 10 na kisha miaka mingine sita na nusu,” alisema.

Alisema zawadi nyigine ambayo Mungu aliwapatia waumini hao ni ya imani ambayo Baba Askofu Isuja aliipokea, aliifundisha na aliishi na akawataka waendelee kumshukuru Mungu kwa hilo.

“Miaka 56 ya utumishi wake kama padre na askofu ni zawadi kwa Dodoma na Tanzania na siyo kwake yeye binafsi,” alisema.

Ibada hiyo ya mazishi ilihudhuriwa na Maaskofu Wakuu na Maaskofu wa kawaida 28 kutoka majimbo ya Dodoma, Mwanza, Mbeya, Njombe, Mpanda, Iringa, Songea, Tabora, Morogoro na Mahenge. 

Mengine ni Musoma, Rulenge, Mbinga, Moshi, Same, Kahama, Sumbawanga, Shinyanga, Mtwara na Lindi. Majimbo mengine ni Bukoba, Tanga, Singida, Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha, Kondoa na Kayanga.
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980.
DODOMA.

JUMATANO, APRILI 20, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mathias Isuja  katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa  Kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba,  Aprili  20, 2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Askofu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mathias Isuja katika mazishi yaliyofanyika kwenye Kanisa   Kuu la Mtakatifu Paul wa Msalaba Aprili 20, 2016.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 21

Naibu Meya wa Jiji La Dar es Salaam Kupatikana Leo

$
0
0
Meya wa jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita
 
Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, anatarajiwa kupatikana leo katika kikao cha kwanza cha Baraza la Jiji kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee.

Uchaguzi wa naibu meya unafanyika baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata meya wa jiji hilo uliohitimishwa Machi 22, mwaka huu kufuatia kutawaliwa na ‘figisufigisu’ kati ya CCM na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) zilizosababisha uaharishwe mara tatu.

Katika kinya’nga’nyiro hicho, Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), Isaya Mwita aliibuka kidedea kwa kupata kura 84 dhidi ya Diwani wa Kata ya Mburahati (CCM), Yusuph Yenga aliyepata kura 67.

Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita jana alisema  kuwa, maandalizi ya kikao hicho kitakachokuwa na ajenda ya uchaguzi wa kumpata naibu meya yamekamilika.

Wagombea nafasi hiyo ni Kafana Mussa wa (CUF) na Mariam Lulida wa CCM.

Tofauti na uchaguzi wa meya, uchaguzi wa leo hautarajiwi kuwa na mvutano mkubwa baina ya Ukawa na CCM kwa kuwa haujumuishi madiwani wote wa jiji hilo, isipokuwa kitakuwa na wajumbe 18.

Kati ya wajumbe hao, kila manispaa itatoa wajumbe wanne wakiwamo mameya, wakati wabunge watano wa majimbo wataruhusiwa kuingia kwenye baraza hilo litakalokuwa chini ya uongozi wa meya huyo mpya. 

TAKUKURU Yalikana Tamko la Wakili wake Kwamba Mahakama ya Kisutu Imejaa Rushwa......Yasema Hayo Yalikuwa ni Maoni yake Binafsi

$
0
0

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na matamshi yaliyotolewa na Leonard Swai, Wakili wa TAKUKURU aliyenukuliwa kwenye vyombo vya Habari tarehe 15/4/2016 kuhusiana na hali ya Rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 

Wakili huyo alinukuliwa akisema kuwa“Kuna Rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu” baada ya kutolewa hukumu ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Bw. William Mhando ambaye alionekana hana hatia.
 
Wakili Leonard Swai si msemaji Rasmi wa Taasisi hivyo matamshi aliyoyatoa si msimamo wa TAKUKURU kuhusu Mahakama. Tunaiomba Idara ya Mahakama na jamii kwa ujumla itambue kuwa matamshi hayo aliyoyatoa ni maoni yake binafsi.
 
TAKUKURU ina jukumu la kisheria la Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Mahakama ni muhimili wa Serikali unaotoa haki. Tunaamini kila Taasisi itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata miongozo ya Sheria zilizopo.
 
TAKUKURU inaheshimu uhuru na mamlaka ya Mahakama na itaendelea kufanya hivyo katika utekelezaji wa majukumu yake.

IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO,
TAKUKURU MAKAO MAKUU
20 April, 2016

Rais Magufuli Amteua Mhandisi Paskasi Muragili Kuwa Mkurugenzi Mkuu CDA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhandisi Paskasi Muragili kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA).

Taarifa iliyotolewa jana  tarehe 20 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Paskasi Muragili umeanzia tarehe 17 Februari, 2016.

Kabla ya Uteuzi huo Mhandisi Paskasi Muragili alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA), nafasi aliyoichukua kuanzia mwaka 2012.

Bungeni: Mbunge Apendekeza Serikali Ipange Bei Elekezi ya Maziwa

$
0
0

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Gibson Ole Maiseyeki (Chadema) amesema bei ya maziwa nchini ni ndogo kuliko ya maji, hivyo kuitaka Serikali kupanga bei elekezi ya bidhaa hiyo ili kuleta tija kwa wafugaji.

Maiseyeki alisema Tanzania ni nchi ambayo wafugaji huuza maziwa kwa bei ndogo, kuliko nchi nyingine duniani.

 “Ni lini Serikali itakuja na bei elekezi ya maziwa, ili kuipa tija sekta ya wafugaji nchini?” alihoji Maiseyeki.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha alisema bei ya bidhaa mbalimbali zinatokana na nguvu ya soko.

Katika swali la msingi, Maiseyeki alitaka kufahamu jitihada za makusudi za Serikali kuwatafutia wafugaji mbegu bora za mifugo, huku akiwasambazia kwa bei nafuu ili kuondokana na aina ya mifugo ambayo haina tija. 

Ole Nasha alisema Serikali inajitahidi kuhakikisha wafugaji wanapata mbegu bora za mifugo kwa kutumia njia mbalimbali, ikiwamo uhawilishaji.

Bungeni: Serikali yaanza Kuzipanga Shule Katika Makundi ili Kuweka Viwango vya Ada Elekezi

$
0
0

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, imeanza zoezi la kupanga shule katika makundi ili kuweka viwango vya ada kwa kuzingatia ubora wa huduma na kwamba haitaathiri ubora wa elimu.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya, aliyasema hayo wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema). 

Mdee alitaka kufahamu iwapo Serikali imebaini kiwango cha gharama kwa kila mwanafunzi kwa shule za bweni na kutwa, iwapo hakitasababisha kuporomoka kwa ubora wa elimu.

Manyanya alisema wizara hiyo imefanya utafiti kuhusu gharama za kila mwanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari. 

“Baada ya utafiti, wizara yangu ilifanya mazungumzo na baadhi ya taasisi zinazosimamia elimu kwa shule zisizokuwa za Serikali na kukubaliana jinsi ya kufikia viwango vya ada elekezi,” alisema.

Alisema wizara inatarajia ubora wa ada elekezi hautaathiri elimu kwa shule binafsi, kwa sababu itapangwa kulingana na ubora wa miundombinu ya shule.

Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema) alitaka kufahamu jinsi Serikali inavyotaka kupanga bei elekezi wakati imeifanya elimu kuwa biashara.

Manyanya alisema siyo mara ya kwanza kwa Serikali kupanga bei elekezi kwa faida ya wananchi na kwamba, imefanyika kwa upande wa huduma ya maji hivyo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (Ewura) wamefanya.

Bungeni: Tani Milioni 2 za Muhogo wa Tanzania Kuuzwa nchini China kwa Dola

$
0
0

Serikali imepata soko nchini China, kupeleka tani milioni 2 za mihogo zenye thamani ya Dola 300 milioni za Marekani.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana  na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masalla (CCM). 

Masalla alitaka kufahamu jitihada za Serikali katika kuwatafutia wakulima nchini masoko ya mazao yao.

Akijibu swali hilo, Mwijage alisema mbunge huyo amewahisha masuala ya bajeti ijayo na kwamba, Serikali tayari imepata soko la mihogo nchini China.

Awali, Mbunge wa Viti Maalumu, Hamida Mohamed Abdallah (CCM) alitaka kujua Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya Mwaka 1996-2020, jinsi inayolenga kuvifanya viwanda vya usindikaji mazao kuongeza thamani na kukuza uchumi.  

Bungeni: Watuhumiwa 135 Wakamatwa kwa Makosa ya Mauaji ya Vikongwe Nchini

$
0
0

Watuhumiwa 135 wamekamatwa kwa makosa ya mauaji ya vikongwe nchini, kati ya Julai mwaka jana na Machi mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Faida Mohamed Bakari (CCM).

Faida alitaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na Serikali kukomesha mauaji hayo na msaada wanaotoa kwa wanawake wanaotumia kuni kupikia, ambayo ni moja ya chanzo kinachosababisha macho kuwa mekundu na hivyo wauaji kuwaua.

“Watu wamekuwa wakiuawa kwa kufukiwa wakiwa hai kwa sababu ya macho mekundu, yanayotokana na moshi wa kuni au kupika kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe,” alisema.

Masauni alisema licha ya watuhumiwa hao kukamatwa, kuna kesi 222 zinazoendelea mahakamani.

“Serikali inafanya jitihada mbalimbali ikiwamo kuhamasisha utengenezaji majiko sanifu, kupeleka gesi na umeme vijijini,”alisema. 

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu, Tauhida Cassian Galloss (CCM), alitaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kunusuru vikongwe.

Masauni alisema Polisi imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na mauaji hayo, ikiwamo kufanya operesheni na misako ya mara kwa mara kuwabaini waganga wa jadi wanaojihusisha na upigaji ramli chonganishi na wasiofuata taratibu za sheria. Pia, alitaka jamii kutoa ushirikiano.

Bungeni: Mbunge aibana serikali Kuhusu fedha za Maendeleo

$
0
0

Mbunge wa Kavuu, Dk Prudenciana Kikwembe (CCM) ameitaka Serikali kueleza ni lini itatoa fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwa wakati.

Dk Kikwembe akiuliza swali la nyongeza bungeni, alisema mara nyingi fedha za maendeleo zimekuwa zikipelekwa katika maeneo husika kwa kuchelewa na hivyo kuchelewesha miradi mingi.

“Ni lini fedha za utekelezaji wa shughuli za maendeleo zitatolewa kwa wakati na fedha zinapochelewa na kutolewa mwishoni mwa mwaka wa fedha, fedha hizo huwa zinaenda wapi?”Alihoji Dk Kikwembe.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alikiri kuwa miradi mingi ya maendeleo imekuwa ikisuasua kutokana na ukosefu wa fedha.

Hata hivyo alisema, kutokana na jitihada zilizopo za kukusanya mapato ya Serikali, tayari baadhi ya miradi iliyokwama imeshaanza kutekelezwa na anaamini miradi yote iliyokuwa imekwama itatekelezwa kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha.

Awali, katika swali la msingi Mbunge huyo alitaka kujua ni lini kata ya Mamba, Majimoto, Chamaledi na Mwampuli zitapatiwa maji safi na salama .

Akijibu swali hilo Jaffo alisema ili kutatua changamoto ya maji katika kata ya Mamba, Serikali imetenga Sh milioni 24 katika bajeti ya mwaka 2015/2016 kwa ajili ya kuchimba kisima kirefu katika kijiji cha Ntaswa ambacho hakina maji kati ya vijiji vilivyopo.

Alisema vijiji ambavyo havijapata huduma ya maji katika kata ya Majimoto ni Kuchimba na Ikulwe ambavyo alisema vimetengewa Sh milioni 48.4 katika bajeti ya mwaka 2015/2016 kwa ajili ya kuchimba visima virefu kila kijiji.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla Aonja Moto wa UKAWA.....Madiwani 34 Wakiongozwa na Meya wao Wasusia Kikao chake cha Kujitambulisha

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amekumbana na joto la Mbeya baada ya meya wa jiji hilo, Mchungaji David Mwashilindi na madiwani wake 34 kususia kikao chake cha kujitambulisha kwa wananchi, baada ya kudaiwa kwenda kukagua Soko la Mwanjelwa bila kumpa taarifa yoyote meya wa jiji hilo.

Meya alifikia uamuzi huo ndani ya ukumbi wa Mkapa muda mfupi kabla ya Makalla kuanza kuzungumza na watumishi wa jiji, wananchi, wazee maarufu, viongozi wa dini na machifu ambapo Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyirembe Sabi alimkaribisha Meya Mwashilindi kuzungumza chochote kwa niaba ya madiwani wake.

Hata hivyo, Meya Mwashilindi alipochukua kipaza sauti alisema: “Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, nakumbuka kwa mara ya kwanza kukutana na wewe tulizungumza kwamba tufanye kazi, siasa zimekwisha. Lakini masikitiko yangu ni kwamba leo hii umekwenda Soko la Mwanjelwa bila ya mimi mwenye jiji kupewa taarifa yoyote wala madiwani wangu. Sasa hiki kikao hakinihusu hivyo muendelee na kikao chenu.”

Baada ya kusema maneno hayo alikabidhi kipaza sauti kwa mkuu wa wilaya, kisha akachukua nyaraka zake akainuka pamoja na madiwani wote kupitia Chadema na kutoka ukumbini huku wakisikika wakisema,‘hizi ni siasa ambazo tulizikataa, lakini wanatulazimisha kuendesha siasa. Hatuwezi kupuuzwa kwa kiasi hiki.”

Mkuu wa Wilaya, Mnasa alisema anaamini taratibu na ratiba yote ilipangwa vizuri hivyo hawaoni sababu ya madai ya madiwani hao kwamba hawakushirikishwa kwenye ziara hiyo, wao kama wawakilishi wa Rais hawaangalii siasa, bali wanaangalia uchapakazi na siyo masuala ya siasa.

Akizungumzia kitendo cha meya na madiwani wake kususia kikao hicho, Makalla alisema ‘Nashangazwa na uamuzi wa madiwani hawa kwa kitendo hiki, kwani siku ile nilipotembelea Shule ya Sekondari Iyunga, nilisema kwamba Aprili 20 ambayo ndiyo leo (jana) nitakuwa na ziara ya jiji na kabla ya kikao nitataka kutembelea Soko la Mwanjelwa,” alisema Makalla.

Alisema suala la meya na madiwani wake kutoshirikishwa kwenye ziara ya kwenda Soko la Mwanjelwa halimhusu, kwani mwenye wajibu wa kupeana taarifa ni kwenye ngazi ya halmashauri ya jiji, lakini siyo yeye (Makalla).

“Jamani mimi sijaja kufanya siasa nimekuja kufanya kazi ya wananchi na nilishatahadharisha jambo hili, sasa kwa kitendo hiki ndiyo siasa na wananilazimisha kufanya siasa, lakini wao ndiyo watahukumiwa na wananchi. Na ninasema kama Mola ataendelea kunilinda kubaki katika mkoa mwaka 2020 nitakwenda kuwaambia hiki kinachofanyika sasa na wawakilishi wao,” alisema Makalla.

Awali Makalla akiwa katika Soko la Mwanjelwa alinusa harufu ya ufisadi kwenye soko hilo na kuagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoa huo, kufanya uchunguzi ndani ya wiki nne wa uhalali wa fedha kiasi cha Sh22.9 bilioni iliyotumika katika ujenzi huo ukiwa ni mkopo kutoka Benki ya CRDB.

Makalla alitoa agizo hilo jana mchana baada ya kutembelea soko hilo na kuzungumza na wafanyabiashara wa jijini hapa, ambao walimueleza wanashindwa kumudu gharama ya upangaji ya vyumba vya biashara ambayo inaanzia kiasi cha Sh500,000 kwa chumba kimoja kwa mwezi, ndiyo maana hawataki kuingia ndani ya soko hilo.

Mwenyekiti wa soko hilo, Peter Chacha alimueleza Makalla kwamba wasipokuwa makini soko hilo litabaki gofu, kwani wafanyabiashara hawataki kuingia kwa kuogopa gharama kubwa ya vyumba hivyo, alimuomba afanye awezalo kukaa chini na uongozi wa benki ambao unadai fedha zao kwa jiji na kuona namna ya kupunguziwa gharama hiyo.

“Ni kweli wenzetu jiji, wametingwa na deni la mkopo kutoka Benki ya CRDB, ndiyo maana wamekuja kutubana sisi wafanyabiashara kwa kutupangia chumba kuanzia Sh500, 000 hadi Sh 800,000, kitu ambacho hatuwezi kumudu hata kidogo,”alisema Chacha 

Baada ya kusikiliza kilio cha wafanyabiashara hao, Makalla alisema kiasi cha Sh22.9 bilioni iliyotumika kwenye ujenzi wa soko hilo haiendani na thamani yake, hivyo vyombo vya dola vikiongozwa na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mbeya, wanafanya uchunguzi wa kina na kuwanasaka wale wote waliohusika kwenye mchakato mzima wa ujenzi wa soko hilo.

“Nataka kupata taarifa ya mchanganuo mzima wa namna ya fedha ilivyokopwa, ilivyotumika na mkataba wake ulivyokuwa ndani ya wiki nne, taarifa hii niipokee na wale watakaobainisha kufuja fedha watapelekwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.

"Kwenye hili, kuna watu waliotufikisha hapa, Sh22.9 bilioni iliyotumika kwenye ujenzi huu haiendani na ujenzi wa soko hili, kuanzia muda uliotumika na gharama ya kodi ya upangishaji wa vyumba siyo rafiki ni kubwa mno, hivyo jiji na CRDB mkae muone namna ya kupunguza gharama hiyo, kwani hali ilivyo sasa lile soko litabaki gofu."

Bungeni: Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa Wawasilishwa Bungeni......Trilioni 107 Zahitajika Kutekeza Mpango Huo

$
0
0

Shilingi trilioni 107 zinahitajika kugharamia utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2016/21, ambao utategemea sana makusanyo ya kodi na ukijikita katika kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya viwanda.

Akiwasilisha bungeni jana Mpango huo wa Pili wa Maendeleo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango alisema katika fedha hizo, Sh trilioni 59 zitatolewa na serikali, huku kiasi kilichobaki cha Sh trilioni 48 zitachangiwa na sekta binafsi pamoja na mikopo na misaada kutoka nje.

Akitoa mchanganuo wa ugharamiaji mpango huo, Dk Mpango alisema kila mwaka serikali itatoa Sh trilioni 11.8 na kwamba katika kipindi cha miaka mitano ya mpango huo, serikali itakuwa imetoa jumla ya Sh trilioni 59.

Alisema eneo la pili la gharama za mpango huo, litabebwa na sekta binafsi, mkopo na misaada kutoka nje na kuwa serikali inaweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi kuwekeza katika miradi ya maendeleo.

Alisema katika mpango huo, kuna ongezeko kubwa la fedha za kugharamia mpango huo, ukilinganisha na ule wa kwanza na sababu ya ongezeko hilo ni ukubwa wa miradi tarajiwa sambamba na nia ya kuchochea upatikanaji wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji wa biashara na uwekezaji.

Alisema nchi ikiwekeza kwenye ujenzi wa viwanda, huvutia misaada kutoka nje na hiyo imetokana na uzoefu wa nchi nyingine zilizoweka mikakati kwenye uwekezaji wa viwanda. 

“Mantiki yetu ni kwamba nchi haina budi kuwa na mkakati mahususi wa kukusanya fedha kuwezesha utekelezaji wa mpango huu kwa ufanisi,” alisema Dk Mpango.

Kwa upande wa serikali, Dk Mpango alisema fedha za kugharamia mpango huo, watazipata kwenye makusanyo ya kodi na yale yasiyo ya kodi, ambapo serikali imeainisha miradi mikubwa ya kielelezo kama ile ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga.

Aidha, eneo jingine ni ujenzi wa Reli ya Kati na kuboresha miundombinu mingine, zikiwemo barabara na usafiri wa anga. 

Hata hivyo, Dk Mpango alisema katika eneo la kufungamanisha maendeleo ya uchumi na maendeleo ya watu, bado kiwango cha umaskini nchini ni kikubwa.

Alisema hivi sasa nchini kuna watu maskini zaidi ya milioni 10, idadi ambayo ni kubwa kuliko baadhi ya nchi Afrika na kusema Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2016/17 hadi 2021, umelenga kupunguza kiwango hicho.

Dk Mpango alisema hatua hiyo inatokana na ule mpango wa kwanza 2011/16 kufikia ukomo wake ifikapo Juni mwaka huu huku kukiwa bado na changamoto nyingi. 

Alisema pamoja na mpango unaoisha muda wake kutekelezwa kwa kiasi, lakini bado zipo changamoto kubwa zinazopaswa kupewa kipaumbele katika mpango huo mpya ili kuhakikisha jitihada zinawekwa katika kuleta maendeleo ili kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

“Tanzania ina watu maskini zaidi ya milioni 10, idadi hii ni kubwa kuliko baadhi ya nchi barani Afrika na idadi hii haishiriki kikamilifu katika uzalishaji, kaya nyingi zimebeba mzigo mkubwa wa wategemezi kufuatia kasi kubwa ya kuzaliana na athari za magonjwa yakiwemo Ukimwi,” alieleza Dk Mpango.

Aidha, aliongeza changamoto nyingine inayoongeza kasi ya umaskini wa watu ni ukosefu wa ajira na kwamba kati ya vijana 800,000 wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka baada ya kumaliza masomo, ni 200,000 ndio wanaobahatika kupata ajira katika sekta rasmi.

Hivyo mpango huo wa maendeleo kwa mwaka 2016/17 umelenga kuongeza kasi ya ukuaji uchumi kwa kuhakikisha unaongezeka kutoka asilimia 7.0 ya mwaka 2015 hadi kufika asilimia 10 ifikapo mwaka 2020.

Aidha, mpango huo umelenga kuongeza pato la wastani kwa kila mwananchi kutoka Dola 1,006 kwa mwaka 2015 hadi kufikia Dola 1,500 ifikapo mwaka 2020 na pia kuhakikisha mauzo ya nje ya bidhaa za viwandani yanaongezeka kutoka asilimia 24 mwaka juzi hadi kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2020.

Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa mwaka 2016/17, umeweka vipaumbele vikuu vinne vilivyolenga ukuzaji viwanda kwa lengo la kuifanya nchi itimize malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Vipaumbele hivyo ni;
  1. Kuwa na viwanda vya kukuza uchumi
  2. Kufungamanisha maendeleo ya uchumi na rasilimali watu, 
  3. Kuweka mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji na 
  4. Kipaumbele cha nne ni kusimamia utekelezaji wa mpango huo.
Katika vipaumbele hivyo, sekta zote zitaangaliwa na kuwekewa mikakati ya kuziboresha ikiwemo viwanda, kilimo, afya, elimu, miundombinu, rasilimali watu kwa kuhakikisha nchi inafikia malengo yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati.

Katika utekelezaji huo, viwanda vilivyokufa na vile visivyoendeshwa kwa tija vitafufuliwa na vingine kuanzishwa ili visaidie kuongeza uzalishaji wa mazao yenye thamani na kukuza kipato cha watanzania na taifa kwa ujumla.

Aidha, Dk Mpango amewaasa Watanzania kuacha na kuukana utamaduni wa kuishi maisha ya kipato wasichoweza kukimudu na badala yake wafanye mageuzi ya mfumo wa maisha kwa kujizatiti kuzalisha mali huku serikali ikiweka nguvu kwenye ukusanyaji mapato ya kodi na yale yasiyo ya kodi.

Akihitimisha hotuba yake hiyo bungeni, alisema hakuna budi kwa Watanzania kubadilika na kubadilisha mfumo wa maisha.

 “Desemba 9, mwaka huu tutaadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa nchi yetu, maana yake ni kuwa kiumri nchi yetu si changa tena, ina umri wa mtu mzima anayepaswa kuwa na familia na uwezo wa kujitegemea kimaisha, hatupaswi kuwa wategemezi, sharti tujijenge,” alisema Dk Mpango.

Alisema katika hilo hakuna njia ya mkato na kwamba nchi inapaswa kujizatiti kukusanya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi kutoka vyanzo vyetu vya ndani kwa nguvu zote na kuacha matumizi ya starehe.

Dk Mpango alisema matumizi ya starehe katika maisha ya sasa na ya uchumi wa nchi hayapaswi kuendekezwa na Watanzania, ikiwa wanataka kuondokana na umaskini na utegemezi wa kibajeti.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuondokana na umaskini na kuwasaidia wananchi kuzalisha mali hivyo vita vya mageuzi ya mfumo wa maisha ni lazima ufanywe kuanzia ngazi ya familia ili kuishi maisha ya kipato wanachoweza kukimudu na sio kuisha maisha ya ufisadi.

“Ndio sababu Rais Dk John Magufuli amekuja na kauli ya kutumbua majipu inayoendelea na dhana nzuri ya kukubali tiba kwa kuwa wapo wengi miongoni mwetu watajitahidi kukataa kupokea maumivu haya, japo hii ndiyo njia pekee ya kupona,” alisema Dk Mpango.

Akizungumzia ukuaji wa uchumi kwa kuwekeza kwenye viwanda, alisema hiyo ndiyo njia ya uhakika kufikia maendeleo endelevu inayotumiwa na nchi nyingi duniani na Tanzania imeamua kujipanga upya kiuchumi kufikia huko.

“Ni dhahiri katika njia hii kutakuwa na vikwazo pamoja na ushindani katika masoko ya mitaji ya bidhaa, ila ili tuvuke tunahitaji dhamira ya dhati kuibadilisha nchi yetu kuwa sehemu bora zaidi ya kuishi kwa wananchi wote,” alisema Dk Mpango.

Lugumi Aakaangwa Bungeni.....PAC Yaunda Kamati Ndogo Yenye Nguvu Zaidi, Ripoti Kutinga Bungeni Kama ya Escrow

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly
 
Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) haijaridhishwa na majibu yaliyotolewa na maofisa wa juu wa Jeshi la Polisi kuhusu Mkataba wa Lugumi Enterprises, na hivyo kamati hiyo imeamua kuunda kamati ndogo leo itakayochunguza kwa undani sakata hilo  ambapo ripoti  ya  uchunguzi huo itawasilishwa bungeni kama ilivyokuwa sakata la Escrow.

Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata  kutoka chanzo cha kuaminika, PAC haikuridhishwa na majibu ya hoja nyingi zilizotolewa na watendaji wakuu akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu mkataba wa Lugumi baada ya kukutana nao jana mjini Dodoma.

“PAC imelazimika kuunda kamati ndogo kesho (leo), itakayokuwa na nguvu kuhoji mambo yote ukiwemo mkataba huo kwa sababu majibu yaliyotolewa hayakuridhisha,” kilieleza chanzo hicho.

Kiliongeza kuwa baadhi ya mambo yanayokanganya PAC ni kufahamu nani mkweli kati ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kupitia taarifa ya ukaguzi na maelezo ya Jeshi la Polisi kuhusu gharama za mkataba.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, taarifa ya CAG inaonesha kuwa mkataba huo ni wa Sh bilioni 37.742 wakati maelezo yaliyotolewa na viongozi wa Jeshi hilo walipohojiwa na PAC hiyo jana, walisema ni Sh bilioni 37.163.

Hivyo kuwepo kwa tofauti ya zaidi ya Sh milioni 578.972. Aidha, utata mwingine ni jeshi hilo kukosa maelezo ya kwa nini katika kutafuta mzabuni kwenye mradi huo, walitumia mfumo wa mzabuni mmoja badala ya wengi.

Chanzo chetu kilisema katika mahojiano na viongozi hao wa polisi, walishindwa kutoa maelezo yanayojitosheleza kwa nini kitengo cha manunuzi cha jeshi hilo walitumia mfumo huo.

Hivyo kutokana na utata huo, Kamati hiyo imeamua kukutana na Spika leo ili kumtaarifu hatua waliyofikia ya kuunda Kamati Ndogo.

Juzi, taarifa ya Utekelezaji wa Mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises ulioshinda zabuni mwaka 2011 ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi vya wilaya nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37, ulitua ndani ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na kuanza kujadiliwa.

Akizungumza  juzi bungeni, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilaly alisema taarifa ya utekelezaji wa mkataba huo ilifikishwa bungeni Jumatatu na juzi asubuhi wamepewa na wakaanza kuujadili.

Awali, Aprili 5, mwaka huu mjini Dar es Salaam, Kamati hiyo ilitoa siku saba kuanzia siku hiyo kwa Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi iliyopewa zabuni ya kufunga mashine 108 katika vituo tajwa nchini ila hadi sasa ni vituo 14 tu ndivyo vilivyofungwa mashine hizo.

Hatua hiyo ilikuja baada ya kamati hiyo kukutana na Jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu za jeshi hilo za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kubainika kuwa na ukiukwaji wa utekelezaji wa mkataba huo.

Ukiukwaji wa utekelezaji wa mkataba huo mwingine ni pamoja na kampuni hiyo kulipwa asilimia 99 ya fedha zote za mkataba huo wenye thamani ya Sh bilioni 37, huku kazi iliyofanywa ni chini ya robo.

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

TUCTA Yapinga Mpango wa Rais Magufuli Kukata Mishahara ya Watumishi wa Umma Kutoka Milioni 40 hadi 15 Kwa Mwezi

$
0
0

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta) limepinga mpango wa Rais John Magufuli wa kukata malipo ya mishahara ya watumishi wa umma kutoka Sh40 milioni kwa mwezi hadi Sh15 milioni.

Akizungumza na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Kanda ya Ziwa jijini Mwanza jana, Naibu Katibu Mkuu wa Tucta, Hezron Kaaya alisema uamuzi huo ni kinyume na sheria na utaligharimu Taifa iwapo wahusika wataamua kwenda mahakamani kupinga mishahara yao kupunguzwa. 

“Watendaji hawa hawakujipangia mishahara wao wenyewe, bali malipo haya yalipangwa na bodi za mashirika na taasisi husika ambazo kisheria zimepewa mamlaka hayo. Malipo haya hayawezi kupunguzwa kwa kauli za kisiasa bila kuzingatia mahitaji ya kisheria,” alisema.

“Iwapo Serikali itatekeleza lengo hili bila kuwapo mjadala mpana na makubaliano ya kisheria kati ya wahusika, basi ijiandae kulipa mamilioni ya fedha kama fidia iwapo watakaokatwa mishahara yao watakwenda mahakamani.”

Akiwa mjini Chato wakati wa mapumziko ya wiki moja, Rais Magufuli alitangaza kupunguza mishahara ya juu kutoka Sh40 milioni hadi Sh15 milioni kwa mwezi, akisema wapo watumishi wa umma wanalipwa masilahi manono na kuishi kama wako peponi, huku wanaolipwa Sh300,000 wakiishi kama wako jehanamu.

Kaaya aliishauri Serikali kuendelea kuwalipa mishahara hiyo minono wahusika hadi mwisho wa mikataba yao, ndipo lengo la kuipunguza litekelezwe ama kwa kuwapa wahusika mikataba mipya au kuajiri watu wengine.

“Serikali inaweza kuwa na nia njema kupunguza tofauti kubwa ya mishahara kati ya kada ya juu na chini, lakini utekelezaji wake lazima usubiri muda mwafaka mikataba ya sasa itakapomalizika,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine; Tucta imepinga hatua zinazochukuliwa na baadhi ya mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya ya kutangaza kuwasimamisha kazi watumishi wa umma ambao hawapo chini ya mamlaka zao kinidhamu.

Tangazo la Nafasi ya Kazi.....Anahitajika Administrative Officer

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images