Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Oparesheni ya Kuwaondoa Ombaomba Jijini Dar es Salaam Yagonga Mwamba..... Polisi Wapanga Mikakati Mipya

$
0
0
OPERESHENI ya kuondoa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam imegonga mwamba kutokana na kukinzana na baadhi ya mamlaka katika kuwaondoa watu hao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam leo , Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP),Simon Sirro amesema kuwa operesheni ya kuondoa omba omba imeshindikana kutokana na baadhi ya mamlaka kushindwa kuhusishwa.

Amesema kuwa wanaendelea kujipanga kwa kuhusisha mamlaka zote ili kuweza kutekeleza operesheni hiyo kwa ufanisi.

Amesema kuwa kuna omba omba wengine wameweza kuondoka baada ya tangazo kutolewa hivyo waliobaki waondoke kwa savabu operesheni itakayoanza haitaangalia uso wa mtu.

Jeshi Polisi limeweza kukusanya zaidi ya sh. Milioni 911 ambazo zimekusanywa kutokana na makosa mbalimbali ya magari  pamoja na pikipiki katika jiji la Dar es Salaam.

Kamanda Sirro amesema kuwa hawajisifii kukusanya fedha hizo, nia yao ni kuona watu hawafanyi makosa ya usalama barabarani.

Wakati huohuo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata jambazi sugu, Shaban Ramadhan (35) ambaye alikuwa anamiliki bunduki mbili za kivita SMG na risasi nane.

Kamishina Sirro amesema kuwa walipata taarifa kutoka kwa watu juu ya mtu huyo kumiliki silaha ambapo alikutwa na silaha moja huku moja ikiwa kwa rafiki yake wa kike, Fatuma Salehe (20).

Aidha jeshi la polisi limeonya wananchi kununua gari katika sehemu zinazotambulika  kutokana na kuibuka uhalifu wa watu kuuza gari zisizo kuwa zao.

Aliyemtukana Rais Magufuli kwenye Facebook Apata dhamana

$
0
0

Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imempa dhamana Mtuhumiwa Isaac Abakuki anayetuhumiwa kumtukana Rais John Magufuli kupitia kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Hakimu mfawidhi Agustino Rwezire amesema Mahakama baada ya kupitia  hoja mbili zilizotolewa  na upande wa mashtaka na mshtakiwa, imeridhia kutoa dhamana kama haki ya msingi ya mshtakiwa kutokana na kosa alilotenda ambapo dhamana hiyo ni ya Wadhamini wawili waliotakiwa kuwa na jumla ya shilingi milioni tano.

Kwenye siku ya kwanza kufikishwa Mahakamani Polisi walisema Tarehe 17 March 2016 Isaac Abakuki akiwa nyumbani kwake Olasiti Arusha alipokea ujumbe kwenye account yake ya Facebook ukisema ‘mnamlinganishaje Magufuli na Nyerere’ ukiwa ni Ujumbe wa mjadala ulioanzishwa kwenye mtandao wa kijamii kufuatia hatua ya Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds 360 CloudsTV na kuwapongeza Watangazaji wa kipindi hicho.

Baada ya kusoma huo ujumbe Mtuhumiwa aliandika comment kujibu alichokisoma na kuandika ;Hizi ni siasa za maigizo halafu mnamfananisha huyu bwege na Nyerere wapi  buana“….. comment ya mtuhumiwa iliwaudhi na kuwakwaza watu wengi walioona Facebook na wakaamua kufikisha malalamiko yao kwa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA.
TCRA kwa kushirikiana na Polisi baada ya kufanya uchunguzi wa kina walifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa 22 March 2016 kwenye hoteli ya Annex Arusha na alipandishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza April 15 2016, kesi yake itaendelea tena May 17 2016.

Breaking News:Hamphrey Polepole Ateuliwa Kuwa Mkuu wa Wilaya ta Musoma

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Hamphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara.

Bw. Hamphrey Polepole anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Musoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Uteuzi wa Bw. Hamphrey Polepole umeanza leo tarehe 18 Aprili, 2016

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili, 2016

Mkuu Wa Mkoa Wa Mwanza Aagiza Aliyedhulumiwa Kiwanja Arejeshewe

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ameuagiza uongozi wa Jiji la Mwanza kuhakikisha linakabidhi kiwanja namba 28-A kilichopo katika eneo la Bugando ifikapo Aprili 25, 2016 kwa mmiliki halali wa kiwanja hicho bwana Justine Eminoga ambacho amekuwa akikidai kutoka kwa mfanyabiashara wa Jijini humo kwa zaidi ya miaka sita sasa.

Mongella amefikia hatua hiyo mara baada yakupokea malalamiko kutoka kwa bwana Justine ambaye alifika katika Jiji la Mwanza kwa ajili kufatilia suala lake ambalo limedumu kwa zaidi ya miaka sita sasa. Akitoa malalamiko yake mbele ya mkuu huyo wa mkoa, bwana Justine alidai kuzulumiwa kiwanja hicho na mfanyabiashara aliye mtaja kwa jina Shanif Mansour ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwimba.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametoa siku saba kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kuhakiki  watumishi, ili kubaini endapo kuna watumishi hewa waliosalia katika zoezi la awali, zoezi la sasa ambalo linasimamiwa na Ofisi ya katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kwa kamati maalumu zilizo undwa na mkuu wa Mkoa huo,

Akiwa katika ziara hiyo mkuu huyo wa mkoa aliagiza kukamatwa kwa Afisa Utumishi msaidizi wa jiji la Mwanza Henry Sedetale, ambaye alisaidia watumishi hewa watano kuchukua mikopo ya zaidi ya Mil.90 kutoka katika benki tofauti tofauti, hata hivyo taarifa kutoka  Taasisi yakupambana na kuzuia rushwa mkoani Mwanza  iliyotolewa wakati wa kikao hicho na mkuu wa Takukuru mkoani humo, ilisema mtuhumiwa huyo tayari alikuwa ametiwa nguvuni na taasisi hiyo kwa mahojiano zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza yupo katika ziara kujitambulisha katika mkoa huo na hii ikiwa ni Wilaya yake ya tatu mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi na Magu hapo awali.

Imetolewa na
Atley J. Kuni
AFISA HABARI NA MAHUSIANO –RS MWANZA. 18 Aprili, 2016

Waziri Mkuu Awasili Dodoma Tayari Kwa Kikao cha Bunge la Bajeti Kinachoanza Kesho

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana  (kulia) , Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (Wapili kushoto) na Mbunge wa  Nachingwea, Hassan Masala baada ya kuwasili kwenye uwanja w ndege wa Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Arili 19, 2016.. Watatu kulia  Mbunge wa Bunge  la Afrika ya Mashariki Adam Kimbisa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana  (kulia) , Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (Wapili kushoto) na Mbunge wa  Nachingwea, Hassan Masala baada ya kuwasili kwenye uwanja w ndege wa Dodoma kuhudhuria kikao cha Bunge kinachotarajiw kuanza Aprili 19, 2016.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 18, 2016

$
0
0

Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 18, 2016 





Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya April 19

Mkuu wa Idara ya Utumishi Jijini Mwanza Kikaangoni Kwa Mikopo ya Watumishi Hewa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amemueleza Mkuu wa Idara ya Utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Sigrifid Kaunala kuwa ni miongoni mwa watumishi watakaochunguzwa kutokana na kugundulika kuwepo kwa baadhi ya watumishi hewa waliopata mamilioni ya fedha kama mikopo kutoka taasisi za fedha.

Mongella alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Jiji hilo ambao pamoja na mambo mengine alitumia nafasi hiyo kuzungumzia suala la watumishi hewa.

Alisema baada ya uchunguzi wa uhakiki wa awamu ya pili wa watumishi hewa uliofanywa na Serikali mkoani humo umebaini kuwepo kwa watumishi watano (majina yao yanahifadhiwa) waliojipatia mikopo ya mamilioni ya fedha kutoka taasisi za fedha hali inayoonesha baadhi ya mikopo hiyo isingetolewa bila ya kibali cha waajiri wao.

“Mkuu wa utumishi nasikia hata wewe unahusika kwenye sakata hili la watumishi hewa, haiwezekani mambo haya yatokee na wewe usijue na wewe ni miongoni mwa watu tunaowachunguza,” alisema Mongella.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa ya kuhakiki watumishi hewa, Waryoba Sanya alisema kazi ya kuhakiki watumishi walioko kazini lilianza jana kwa kuanza na uhakiki wa watumishi wote wa Ofisi Kuu ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza walioko kazini na kuwa lilikuwa linaendelea vizuri.

Rais Magufuli Kumwapisha Balozi Mteule Mheshimiwa Mathias Chikawe Leo asubuhi

$
0
0

Itakumbukwa kuwa leo ( jana ) asubuhi tarehe 18 Aprili, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

Tunapenda kuwataarifu kuwa Balozi Mteule Mathias Meinrad Chikawe ataapishwa kesho (Leo) tarehe 19 Aprili, 2016 saa 3:00 Asubuhi, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

18 Aprili, 2016

NEEC Yaja na Ajira Yangu Kuwainua vijana Kiuchumi

$
0
0

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wameanzisha mpango wa Ajira Yangu wenye lengo la kuwainua vijana kiuchumi vijana.

Akizungumza jana, Katibu wa Baraza hilo, Beng’i Issa alisema mpango huo unafanyika kwa mfumo wa shindano kwa kuwashindanisha vijana nchi nzima kuanzia miaka 18 hadi 35.

“Mpango huu umebuniwa kwa ajili ya vijana kupata ujuzi wa kuanzisha na kuendeleza biashara na kuwawezesha mitaji, ili waweze kuanza au kuboresha biashara zao, na kutengeneza nafasi za ajira kwao wenyewe na kwa vijana wengine pia,” alisema Issa .

Issa alisema Ajira Yangu Business Plan Competition itahusisha vijana wanaotaka kuanza biashara au wanaotaka kupanua na kuboresha biashara zao bila kujali kiwango cha elimu.

Alisema vijana hao wanatakiwa kuja na mipango rasmi ya biashara kwa ajili ya mashindano katika sekta za kilimo na kilimo usindikaji, ikiwa ni pamoja na viwanda, vyombo vya habari, masoko na mawasiliano, michezo, vifaa, sanaa na utamaduni, utalii na burudani.

Alisema mipango hiyo pia ilenge katika mazingira na utunzaji wa mazingira, ikiwa ni pamoja na biashara ya kijamii, biashara inayohusu habari na mawasiliano, teknolojia, ikiwa ni pamoja na usindikaji biashara.

Alisema awamu ya kwanza ya mpango huo itawahusu vijana kujaza fomu ya ushiriki zilizo kwenye tovuti za ILO na NEEC ambapo mwisho wa maombi utakuwa Mei 9 mwaka huu kuanzia jana.

Issa alisema awamu ya pili itahusisha mafunzo ya siku moja ya kina ya mipango ya biashara ambayo itawakutanisha vijana 25 watakaochaguliwa na baadaye vijana hao watawasilisha mipango yao kwa majaji na wawekezaji na hapo vijana 10 watapewa mitaji yenye jumla ya dola za Marekani 75,000 (zaidi ya Sh milioni 150) .

Mratibu Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO), Dk Annamaria Kiaga, alitaka vijana wengi kujitokeza kwani shirika lake lina mipango ya baadaye ya kuinua vijana.
Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) jijini Daar es Salaam jana  kuhusiana na Progrmu ya umoja wa mataifa kuhusu Ajira kwa vijana. Kushoto ni Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga.

RC Paulo Makonda Aibua Madudu Zaidi Jengo la Machinga Comlpex

$
0
0

Mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kufanyika kwa uchunguzi jengo la Machinga Complex kubaini uhalali wa mkataba uliowezesha ujenzi wa jengo hilo, ikiwa ni pamoja na gharama halisi za ujenzi.

Alisema hayo kutokana na jengo hilo kuwa na deni la zaidi ya Sh bilioni 36, kiasi ambacho ni mara tatu ya thamani halisi ya jengo hilo na kuleta shaka ya ufisadi ndani yake. Jengo hilo lina thamani ya Sh bilioni 12.

Alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itaanza kufanya uchambuzi wa mkataba ili kupata uhalali wa gharama na kujua kiwango kinachostahili kulipwa na wafanyabiashara hao.

“Katika miradi mingi duniani huu ni wa aina yake, mradi ambao kabla haujaanza unaweka jiwe la msingi unaanza kudaiwa benki, mpaka unakuja kumaliza deni lako ni kubwa linakaribia robo mbili au tatu ya mkopo wenyewe, kabla hata hujaanza kupangisha hata mtu. 

“Kwa takwimu zinaonesha tumekopeshwa na jengo limejengwa Sh bilioni 12.7, lakini mpaka dakika hii mnadaiwa Sh bilioni 36 na nyinyi ndio mnatakiwa kuzilipa, sasa kwa maelezo hayo ndio mnapata picha kwa nini tumeamua kujipa muda,” alisema Makonda.

Alisema katika maelezo ya awali yanaonesha kuwa jengo hilo lina mkanganyiko mkubwa na inawezekana kuwa ni miongoni mwa miradi iliyofanyiwa ufisadi mkubwa.

Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene aliifuta bodi inayosimamia jengo hilo na kumsimamisha kazi meneja anayesimamia jengo hilo na kumtaka kwenda katika ofisi za jiji kwa ajili ya kumpangia kazi nyingine.

Katika hatua nyingine, Simbachawene alilikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza wafanyabiashara bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa wafanyabiashara hao.

Majeruhi wa Bodaboda Waielemea Taasisi ya Mifupa (MOI)

$
0
0

Ajali nyingi za bodaboda na mabasi ya abiria zimetajwa kuwa sababu kubwa za Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuelemewa wagonjwa wengi wanaofikishwa kwa ajili ya upasuaji wa dharura. 
 
Hali hiyo imesababisha changamoto kubwa kwa Wizara ya Afya kwani madaktari waliopo katika taasisi hiyo ni wachache na wanazidiwa na majukumu. 
 
Kutokana na changamoto hiyo, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema atahakikisha anashirikiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kutatua tatizo la kukithiri kwa ajali za bodaboda ili kupunguza mzigo mzito unaoikabili MOI kwa sasa. 
 
Hii itakuwa mara ya pili kuweka mkakati wa kuona uwezekanao bodaboda kutumika bila ya kusababisha maafa.

Mwaka 2014 Jeshi la Polisi kwa ushirikiano na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dares Salaam na Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu (Sumatra) Kanda ya Mashariki walizuia bodaboda na bajaji kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam. Hata hivyo, kampeni hiyo haikufanikiwa. 
 
Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa kozi ya wiki moja ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu inayofanyika hapa nchini kwa ushirikiano baina ya MOI na Taasisi ya Mifupa ya Chuo Kikuu cha Weil Cornel kutoka New York, Marekani, Ummy alisema asilimia 75 ya wagonjwa wanaofikishwa MOI ni kutokana na ajali za bodaboda na mabasi ya abiria. 
 
“Tumeelezwa kwamba kati ya wagonjwa 50 wanaofikishwa MOI, asilimia 75 ni wa ajali za bodaboda na mabasi ya abiria.
Hii ni changamoto kwetu. MOI walikuwa wanapokea wagonjwa 20 kwa siku, lakini kwa sasa wanapokea wagonjwa 50,” alisema Ummy. 
 
“Kwa hiyo, hii inaleta uzito na mzigo mkubwa kwa sekta ya afya katika kutoa huduma za afya ikiwamo upasuaji huu. 
 
Nitaongea na Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ana dhamana ya kuhakikisha hii biashara ya bodaboda inaendeshwa bila kuleta madhara makubwa kwa jamii.” 

Kuhusu madaktari, Ummy alisema taasisi hiyo inakabiliwa na uchache wa madaktari bingwa wa upasuaji wa ubonMOI go na mishipa ya fahamu, kwani mpaka sasa kuna madaktari wanane pekee nchi nzima; mmoja yupo Hospitali ya Bugando na saba wako MOI. 
 
“Kubwa tunalojifunza hawa ambao ni wachache wataweza kujengewa uwezo ili kuweza kujua changamoto na mahitaji ya sasa katika kufanya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu, na serikali tumeahidi tutaongeza wataalamu katika fani hiyo na kununua vifaa vya kisasa vya CT Scan na MRI ili kuwaongezea ufanisi,” alisema Ummy. 
 
Pia, alisema ametoa maelekezo kwa taasisi ya MOI kuhakikisha inasomesha wataalamu wengi zaidi. 

“Nipo tayari hata kutoa maelekezo kwamba katika zile nafasi ambazo wizara inasomesha madaktari kwenda nje ya nchi, basi tuongeze wale ambao wanasomea kozi hii na watakapokuja kuanza kazi mshahara wao utakuwa mkubwa wasianze na mshahara mdogo.” 

Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dk Othman Kiloloma alisema tayari wameshaanza kuyafanyia kazi maagizo ya Waziri kwa kupanga ratiba za kwenda kufanya upasuaji mikoani kwa wenye uhitaji. 
 
“Aprili 25 timu ya madaktari 10 itaondoka kwenda mikoa mitano, itaanza na Mwanza siku nne, Shinyanga tatu, Singida nne, Dodoma nne, Morogoro siku tatu na baada ya wiki mbili tutaondoka tena kwenda mikoa mingine kuanzia Bukoba mpaka Mbeya. Tutatoa taarifa kadri tunavyoendelea,” alisema Dk Kiloloma.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Asema Serikali Itaendelea Kuwatumbua Majipu Wala Rushwa Bila Kujali Hadhi Zao

$
0
0

Serikali  ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli, itaendelea kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi kwa nguvu zote bila kutetereka.

Lengo la hatua hiyo ni kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali na kuboresha uwajibikaji na maadili katika usimamizi wa rasilimali za umma na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alisema hayo katika hotuba yake kwa Taifa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Hivyo aliwaomba Watanzania wote kuunga mkono kwa vitendo juhudi na maelekezo ya Dk Magufuli za hatua anazozichukua dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi nchini. 

Kutokana na hatua hizo, Makamu wa Rais alisema hadi sasa jumla ya kesi 596 za rushwa zinaendelea mahakamani na jumla ya Sh 6,543,342,793 tayari zimeokolewa.

“Naomba nitumie fursa hii kuwakumbusha Watanzania wenzangu kujiepusha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa,” alisema Samia na aliwataka watumishi wa umma, watumishi katika sekta binafsi, wajasiriamali na kila mmoja kujiepusha na vitendo vya rushwa na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba, sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizowekwa.

“Kama nilivyokwishasema mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu zinaendelea kuhimiza mapambano dhidi ya Rushwa chini ya kaulimbiu “Timiza Wajibu wako, kata Mnyororo wa Rushwa,” aliongeza Makamu wa Rais.

Samia alisema suala la rushwa limeongelewa mara nyingi na athari zake zinajulikana ikiwa ni pamoja na ubadhirifu wa mali za umma, mikataba isiyofaa kwa taifa na udanganyifu na kupokea fedha ili kukiuka sheria kwa manufaa binafsi huchangia kwa kiwango kikibwa kuwanyima wananchi hazi zao na kudhoofisha ustawi wa taifa letu.

Mbali na hatua hiyo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuendelea na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, pia alisisitiza kwa mara nyingine kwa kusema kuwa Serikali haina nia ya kumwonea mtu inapochukua hatua ya kutumbua majipu kwa watumishi wa umma.

Akishangiliwa na wananchi wakati akiwahutubia kwenye sherehe hizo, Makamu wa Rais alisema lengo la Serikali la kutumbua majipu ni kurekebisha na kurejesha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji serikalini kama ilivyoagizwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili Watanzania wote wafaidike na matunda ya nchi yao.

“Mnasikia katika Serikali ya Awamu ya Tano tunarekebishana, majipu yanatumbuliwa ...kwa kweli hatuna nia ya kumwonea mtu, tunarekebishana na hilo ndilo lililomo katika agizo ya Ilani yetu ya CCM ili kuwanufaisha Watanzania wote wafaidi matunda katika nchi yao,” alisema Makamu wa Rais.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Yamuonya Uhuru Kenyatta

$
0
0

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetishia kuichukulia Kenya hatua kali isiposalimisha kwa mahakama hiyo washukiwa watatu wanaokabiliwa na mashtaka ya kutatiza mashahidi.

Msemaji wa ICC Fadi el Abdallah alisema mahakama hiyo itairipoti Kenya kwa Baraza la Mataifa Wanachama wa Mkataba wa Roma (ASP)  kama itaendelea  kushikilia msimamo wa kutowawasilisha Wakenya hao watatu mbele ya mahakama hiyo mjini Hague, Uholanzi.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Bi Fatou Bensouda, amepata kibali cha kuwakamata aliyekuwa mwanahabari Walter Osapiri Barasa, wakili Paul Gicheru na Philip Bett kwa madai ya kutatiza mashahidi katika kesi dhidi ya Naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua arap Sang.

Agizo la kukamatwa kwa Bw Barasa lilitolewa Oktoba 2013 ilhali lile la kukamatwa kwa Philip Bett na Paul Gicheru lilitolewa Septemba 2015 kwa madai kuwa walihonga mashahidi.

Kesi dhidi ya Bw Ruto na Sang ilitupiliwa mbali mapema mwezi huu kwa misingi kuwa ilikosa ushahidi wa kutosha kutokana na mashahidi kutatizwa.

Akihutubia hafla ya maombi mjini Nakuru mnamo Jumamosi, Rais Kenyatta alitangaza kuwa hakuna Mkenya mwingine atakayefikishwa katika mahakama ya ICC kujibu mashtaka.

Alisema kusitishwa kwa kesi hizo ndio mwisho wa ushirikiano baina ya Kenya na mahakama hiyo ya kimataifa.

“Ukurasa huo tayari tumefunga na hatutakubali Mkenya kurudi katika mahakama ya ICC. Tuna mahakama zetu za kutatua matatizo yetu,” akasema rais katika uwanja wa michezo wa Afraha.

“Kenya ikipuuza agizo la kuwasilisha washukiwa hao, majaji watawasilisha ripoti yao mbele ya Baraza la Mataifa Wanachama wa Mkataba wa Roma ambalo litachukua hatua zinazostahili,” akasema Bw Fadi.

Kifungu cha 87(7) cha Mkataba wa Roma kinasema: “Nchi mwanachama ikikataa kushirikiana na ICC na kutatiza utendakazi wake, mahakama inaweza kuwasilisha malalamishi kwa baraza la ASP.”

Wiki iliyopita, Bi Bensouda alisema kusambaratika kwa kesi dhidi ya Bw Ruto na Bw Sang kulichangiwa kwa kiwango kikubwa na kutatizwa kwa mashahidi na akataka washukiwa hao watatu wapelekwe ICC.

Alisema mashahidi 17 ambao walikuwa wameandaliwa na upande wa mashtaka walijiondoa baada ya kutishwa na kutengwa.

Hapo jana, Fadi alisema ICC inajua kuhusu tangazo la Rais Kenyatta wa Kenya kutosalimisha washukiwa hao na kuwa inafuatilia hatua hiyo kwa karibu.

“ICC haijapokea pingamizi zozote rasmi kutoka Kenya kuhusu mashtaka ya Wakenya watatu wanaoshukiwa kutatiza mashahidi wa kesi za ghasia  baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2007,” alisema Bw Fadi.

Sera Ya Rais Magufuli ya Kubana Matumizi Yawaliza Wafanyabiashara Dodoma

$
0
0

Sera ya Rais John Magufuli ya kubana matumizi serikalini imekuwa majanga kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma, huku wizara nazo zikionja cha moto. 

Katika kipindi hiki cha kuanza kwa mkutano wa Bunge la Bajeti, wafanyabiashara mkoani hapa wamelalamikia biashara kudorora tofauti na kipindi kilichopita. 

Biashara kubwa zinazofanywa wakati wa vikao vya Bunge ni vyumba vya kulala wageni, usafiri wa teksi, kumbi za mikutano na vyakula. 

Mkutano wa bajeti uliopita, vyumba vya kulala wageni katika mji wa Dodoma vilikuwa vimejaa hata kabla ya kuanza mkutano wa Bunge, lakini hali hiyo imekuwa tofauti baada ya jana karibu nyumba zote za kulala wageni kuwa na nafasi nyingi huku nyingine zikiwa hazina wageni kabisa.

Mkutano huo unaoanza leo kupitisha bajeti za wizara na Serikali Kuu, huwa na mjadala mkali na maofisa wa wizara kutoka vitengo mbalimbali husafiri kutoka Dar es Salaam na sehemu nyingine nchini kwa ajili ya kusaidia utoaji wa majibu na hoja zinazotoka kwa wabunge. 

Kutokana na hali hiyo hoteli, nyumba za kulala wageni hutegemewa kuwa zimeshachukuliwa hadi siku chache kabla ya kuanza kwa mkutano rasmi na mji wa Dodoma huanza kushamiri kibiashara, lakini kutokana na sera ya ubanaji matumizi wa Serikali ya Dk Magufuli, mji huo umepooza kama hauna wageni. 

Hata baadhi ya mawaziri wameeleza kuwa hawatachukua maofisa wengi kutoka wizara wanazozisimamia kwa ajili ya kushughulikia makadirio ya matumizi ya wizara zao, watakapowasilisha ndani ya Bunge, kama ilivyokuwa katika Serikali zilizopita. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba alisema wizara yake imepunguza kwa zaidi ya nusu ya maofisa wanaokwenda kuhudhuria vikao hivyo Dodoma. 

“Katika Bunge hili si zaidi ya maofisa 10 watakaohudhuria ambao ni waziri, katibu mkuu na naibu wake, wakurugenzi mazingira, muungano sera na mipango, mhasibu mkuu pamoja na mkurugenzi wa Baraza la Mazingira Tanzania (NEMC),” alisema. 
       

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema ingawa wizara yake haijafika muda wa kupanga juu ya maofisa wangapi wanaostahili kuhudhuria vikao hivyo, lakini ni lazima wahakikishe wanapunguza idadi hiyo. 

“Lazima tuangalie umuhimu wa mtu kulingana na sekta yetu ya elimu hatutaweza kuja na watu kama ilivyozoeleka huko nyuma,” alisisitiza Profesa Ndalichako ambaye awali alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (Necta). 

Katika kuonyesha hatua za ubanaji matumizi zimeanza kuuma katika mji wa Dodoma, mmoja wa wahudumu katika nyumba ya kulala wageni iliyopo eneo la Majengo Mapya ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema: “Mwaka huu hakuna biashara kabisa, hata waliopata watu ni wale ambao wamekuja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Mei Mosi zinazofanyika kitaifa hapa Dodoma.” 

Alisema wageni wa vikao vya Bunge la Bajeti huomba nafasi siku tatu kabla ya kuanza kwa vikao, lakini mwaka huu hadi kufikia jana mchana hakuna watu walioonyesha kutaka nafasi katika nyumba hiyo. 

Wafanyabiashara wa saluni ambao nao wanategemea vikao vya Bunge kuongeza mapato yao, walisema hali ya kibiashara ni mbaya na kwamba ina tofauti kubwa na vikao vingine vilivyopita.

Hata bei ya vyakula katika masoko mbalimbali haijapanda kama ilivyokuwa wakati wa vikao vilivyopita, hali iliyokuwa inayowalazimu wakazi wa mji huo kufanya manunuzi wiki moja kabla ya vikao vya Bunge kuanza.

Pia, kwa upande wa wingi wa watu na magari kwenye mji huo hali imekuwa tofauti na vikao vilivyopita vya bajeti, ambavyo kulikuwa na idadi kubwa ya watu siku mbili kabla ya kuanza vikao. 

Kama ilivyo kawaida ya maandalizi ya Bunge, barabara za maeneo mbalimbali mjini hapa zimeanza kufanyiwa ukarabati kwa kuwekewa viraka kwenye maeneo yenye mashimo na usafi kwa kuondoa mchanga barabarani. 

Wabunge Wabanwa, Sasa Kusajiliwa Kwa Kuchukuliwa Alama za Vidole 10.........Wapiga Picha za Tv na Redio Marufuku Bungeni

$
0
0

Bunge  linaanza rasmi usajili wa wabunge na watumishi wa Bunge hilo pamoja na wageni mbalimbali, wanaoingia bungeni kwa kutumia mfumo wa kisasa wa kuchukua alama za vidole.

Sambamba na mfumo huo, Bunge pia limetoa taarifa rasmi ya kudhibiti urushaji wa matangazo ya Bunge ambayo sasa vyombo vya habari vya kielektroniki havitaruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi wa bunge na kamera kwa lengo la kurekodi yanayoendelea.

Na badala yake, jukumu la kurusha matangazo ya vikao vya Bunge litafanywa na Bunge lenyewe kupitia Feed Maalum ili kurahisisha kila kituo cha redio na televisheni kupata matangazo hayo kwa sehemu walipo bila kufunga mitambo yao bungeni.

Hayo yalibainishwa jana na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah wakati akitoa taarifa kwa Naibu Spika wa Bunge hilo, Dk Tulia Ackson alipofanya ukaguzi wa ukarabati uliofanywa ndani ya Ukumbi wa Bunge linaloanza vikao vyake vya Bajeti katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11 mjini hapa.

Dk Kashilillah alisema kuanzia jana wabunge wataanza usajili kwa njia ya kuchukuliwa alama za vidole badala ya utaratibu wa zamani wa kujisajili kwa kutumia makaratasi. 

Alisema usajili huo utachukua alama za vidole vyote 10 na lengo la kutumia mfumo huo ni kuboresha kanzi data ya Bunge na kwamba usaili huo utapunguza pia matumizi ya makaratasi ambayo yana gharama.

“Tumeanza usajili huo leo (jana) kwa wabunge waliofika, ila tutaendelea kusajili nadhani ndani ya wiki tutakuwa tumekamilisha kazi hiyo, na tumejipanga kuifanikisha kwa haraka,” alisema Dk Kashilillah.

Akizungumzia usajili huo, Dk Kashilillah alisema utasaidia kufahamu idadi ya wabunge waliohudhuria vikao vya bunge na hivyo itakuwa rahisi kwenye kazi ya upigaji kura wakati wa kupitisha hoja mbalimbali.

Alisema Bunge limeboreshwa na kuwa la kisasa zaidi ambapo kila meza ya mbunge ndani ya ukumbi huo, itakuwa na ‘tablet’ itakayomuwezesha kufuatilia majadiliano ya bunge hata ya siku zilizopita na pia wabunge wataweza kuona ratiba ya shughuli mbalimbali za Bunge.

Akizungumzia elimu kwa wabunge hao juu ya matumizi ya mfumo huo, Dk Kashilillah alisema wameandaa utaratibu wa kuwaelimisha wabunge hao juu ya matumizi ya mfumo huo, ili iwe rahisi kwao kuutumia.

Naye Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Bunge, Didas Wambura alisema wamejipanga vizuri kuhakikisha matangazo ya bunge yanapatikana kwenye vituo vya televisheni kama ilivyopangwa.

Wambura alisema kuanzia sasa Bunge litarusha matangazo ya Bunge lenyewe kupitia feed maalumu ili kurahisisha kila kituo cha televisheni na redio kupata matangazo hayo kwa sehemu walipo, bila kufunga mitambo yao bungeni.

“Tutarusha matangazo ya Bunge wenyewe tutatumia Feed Maalumu itakayorushwa na satelaiti ya INTELSAT 17,” alisema Wambura.

Kutokana na hatua hiyo, vituo vya televisheni na redio nchini havitaruhusiwa kuingiza kamera zao ndani ya Ukumbi wa Bunge kurekodi vikao hivyo na badala yake wanapaswa kutumia Masafa ya Matangazo ya Bunge.

Katika mabadiliko hayo, pia idadi ya viti vipya 94 vimefungwa ndani ya Ukumbi wa Bunge hilo na hivyo kufanya idadi ya vitu vyote vya ukumbi kuwa 404.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya alisema watakaa na wadau wote wa habari ili kuona ni namna gani wataweza kupata matangazo hayo.

“Haturuhusu wapiga picha za televisheni na redio kuingia na kamera ndani ya Ukumbi wa Bunge kurekodi, kazi hiyo itafanywa na Bunge, ila waandishi wa habari wa magazeti na wapigapicha za mnato wataendelea kuingia,” alisisitiza Mwandumbya.

Picha 6 za Muonekano wa Daraja la Kisasa la Kigamboni Litakalozinduliwa Leo na Rais Magufuli

$
0
0
Daraja la kisasa la Kigamboni linalounganisha eneo la Kigambonina upande wa Kurasini likikatisha bahari ya Hindi. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kulizindua rasmi daraja hilo  leo Jumanne Aprili 19, 2016.
Akina mama na watoto wao wakilishangaa daraja hilo la kisasa
Barabara inayoelekea kwenye daraja hilo

Jinsi Kitambi Kinavyopatikana na Jinsi Kinavyoondolewa na Dawa ya Mkataa Kitambi

$
0
0

Kitambi  ni  ile  hali  ya  tumbo  kuwa kubwa  na  kuchomoza  kwa  mbele  na  wakati mwingine  kufikia  hatua  ya  kunin’ginia.
JINSI  KITAMBI  KINAVYO  PATIKANA
Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati  ya bilioni 50  hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili wa binadamu.

 Kwa wanawake  seli hizo  zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye  nyonga, kiunoni na kwenye makalio.

Kwa upande  wa  wanaume seli  hizo zinapatikana  sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia.

Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:

i.Njia  ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi

ii.Na  njia  ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

SABABU ZA KUPATA KITAMBI
Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika  mwili  wa  mwanadamu, hali  inayo  sababishwa  na  mtu  kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.

VYAKULA  VINAVYO  CHANGIA KULETA  KITAMBI

Vyakula vinavyochangia  kuleta  kitambi ni  pamoja  na :
i.Vyakula  vyenye  mafuta  mengi  kama  vile  nyama nyekundu  (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama  ya  kuku  wa  kizungu  ( iwe  ya  kuchemsha, kukaanga  ama  kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi ya kukaanga kwa  mafuta  (chips) pamoja  na  pizza.

ii.Vyakula vyenye wanga mwingi kama  vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate  mweupe.

iii. Vyakula  na  vinywaji  vyenye  sukari  nyingi  iliyo  ongezwa( added  sugar ), kama  vile  soda  na  keki.

iv. Vyakula  vilivyo  tengenezwa  kwa  ngano  na  sukari kama  vile  keki, skonzi, chapatti, maandazi, mkate  mweupe  nakadhalika

v. Pamoja  na  vinywaji  vilivyo  tengenezwa  kwa  kutumia  ngano  kama  vile  bia  za  aina  mbalimbali  na  kadhalika.

Vyakula  vilivyo  tajwa  hapo  juu, vikitumiwa  bila  kuzingatia  kanuni  za  mlo  kamili, huchangia  kuleta  tatizo  la  kitambi.

vi. Sababu nyingine ni  kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na  viungo(  physical  exercises  )  kwa  muda  mrefu.

JINSI YA KUJUA KAMA UNA KITAMBI
Kitambi kinaweza kuonekana kirahisi kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya vipimo vya kiuno(waist) na nyonga (hips).

Mzingo wa kiuno ukiwa >102 cm au 40  kwa wanaume na >88 cm au 35  kwa wanawake, na uwiano wa kiuno na hips(Waist-Hip Ratio) ikiwa >0.9 kwa wanaume na >0.85 kwa wanawake.

BMI ya 30 au zaidi inaashiria 'Obese' uzito kuzidi kiasi. Kuwa na mzingo uliozidi kawaida ni kiashiria hatari cha matatizo ya kimetaboliki, kuliko hata cha BMI.

Kipimo kingine cha kitambi ambacho kimeonyesha uwezo zaidi kuliko BMI katika kutabiri uwezekano mkubwa wa magonjwa ya moyo ni Index Of Central Obesity(Waist-To-Height Ratio-WHtR) ambapo uwiano ukiwa sawa na 0.5 au zaidi, hii ikimaanisha mzingo wa kiuno angalau ni nusu ya kimo cha mtu.

Kipimo kingine ni Body Volume Index, kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.

MAMBO  YANAYO  MUWEKA  MTU  KATIKA  HATARI  YA  KUPATWA  NA  KITAMBI
Tumekwisha  ona  hapo  juu jinsi  kitambi  kinavyo  patikana  na  vyakula  pamoja  na  sababu  nyinginezo  zinazo  sababisha  kutokea  kwa  kitambi, sasa  tutazame  mambo  yatakayo  kufanya  uwe  katika  hatari  ya  kupatwa  na  kitambi.

Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za kitaalamu, mambo  yafuatayo  huwaweka  watu  katika  hatari  kubwa   ya  kupatwa  na  kitambi :

1. Ulaji  mbovu  wa  chakula; Ulaji  mbovu  wa  chakula  ni  ulaji  usio  zingatia  kanuni  za  mlo  kamili. Hapa  mtu  hufululiza  kutumia  chakula  cha  aina  fulani  pekee  bila  kuzingatia  aina  nyinginezo  za  chakula.  Mfano; mtu  anaweza  kuwa  anakula  mlo  ufuatao :

Asubuhi :  Mchemsho  ama    supu  ya  ng’ombe , chapatti  tatu  na  soda  moja.  Mchana :   Ugali  nyama  choma anashushia  kwa  maji  na  soda.

Jioni :  Mchemsho  wa  kuku  na  bia  mbili  nakuendelea.

Usiku  :  Chips  mayai  au  chips  kuku  au  chips  mishikaki  na  bia.

Mtu  huyu  akiendelea  na  utaratibu  huu  kwa  muda  mrefu, ni  lazima  atapatwa  na  kitambi.

2. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  mafuta  mengi

3. Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye wanga  mwingi  

4.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vyenye  sukari  iliyo  ongezwa ( added  sugar  ).

5.Ulaji  mfululizo  wa  vyakula  vya  ngano.

6.Ulaji  mfululizo  wa   vinywaji  vyenye ngano  na  sukari.

7.Kutofanya  mazoezi  ya  mwili  na viungo  ( physical  exercises  ).

Mhusika  anapokuwa  katika  makundi  yote  yali yotajwa  hapo  juu, hali  huwa  mbaya  zaidi. 

NJIA ZA KUONDOA KITAMBI
Kuwa  na  kitambi  ni  lugha  ya  mwili  ( body-language )  inayo  leta  ujumbe  kwako  kwamba  “ Mwili    wako  haupo  salama  tena “

Kama  una  kitambi   maana  yake  una  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini, mwili  wako  unatumika  kuhifadhi  mafuta  usiyo  yahitaji.

Hali  hii  kitabibu  imaanisha  kwamba, ogani  nyinginezo  zilizomo  ndani  ya  mwili  wako  zinao gelea  kwenye  mafuta( fats  )  yasihotika  yaliyomo ndani  ya  mwili  wako,  jambo  linalo  kuweka  katika  hatari  kubwa  sana  ya  kushambuliwa  na  magonjwa  hatari  kama  vile  shinikizo  kubwa  la  damu, kiharusi  na kisukari  na  kwa kutaja  machache.

Hivyo  basi  ili  kuondokana  na  hatari  hiyo, yakupasa   kupambana  kuondoa  hayo  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini  mwako.

NJIA  ZA  KUONDOA  KITAMBI.
Unaweza  kuondokana  na  kitambi  kwa  kufanya  diet  pamoja  na  mazoezi ya  mwili  na  viungo.

Vilevile  unaweza  kuondoa  kitambi  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  dawa  asilia  ya  kuondoa  kitambi  na  kuondoa  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

DAWA   ASILIA  YA  KUONDOA  KIAMBI  NA  MAFUTA  MWILINI.
Hii  ni  njia  ya  uhakika  kabisa  ya  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

 Unaweza  kuondoa  tatizo  la  kitambi  pamoja  na  kupunguza  mafuta  mwilini  kwa  kutumia  DAWA  ASILIA   IITWAYO YA  MKATAA  KITAMBI.

 Dawa   hii  ni  ya asili  kabisa
“  Pure  Herbal “, ambayo  haijachanganywa  na  kemikali  yoyote, haina  side  effect kwa  mtumiaji  na  inaondoa  kabisa  tatizo  la  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

JINSI  DAWA  YA  MKATAA  KITAMBI  INAVYO  FANYA  KAZI.
1.Huyeyusha  mafuta  yasiyo  hitajika  mwilini.

2.Husaidia  kupunguza  hamu  ya  chakula.

3.Inazuia  kutengenezwa  kwa  seli  za  mafuta  ( fat cells  ) katika  mwili  wa  mwanadamu. Unapokula  chakula  chenye  mafuta  mengi, dawa  hii asilia  hupambana  kuyafanya  mafuta  hayo  yasitengeneze  seli  za  mafuta  mwilini  mwako. Hali  hii  huuepusha  mwili  wako  kuhifadhi  mafuta   yasiyo  hitajika  mwilini.

4. Husaidia  kupunguza  uzito wa mwili  kwa  haraka  sana  endapo  itatumika  pamoja  na  diet  ya  kabechi.

UFANISI  WA  DAWA.
Ufanisi  wa  dawa  hii  ni  wa  asilimia  mia  moja. Dozi  ya  dawa  hii  hutumika  kwa  muda  wa  siki  ishirini  na  moja.

MATOKEO  YA  DAWA:
Dawa  hii  huondoa  kabisa  kitambi  ndani  ya  siku  kumi  na  nne.

BEI  YA  DAWA :
Dawa  hii  inaoatikana  kwa  kiasi  cha  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU  (Tshs. 50,000/=)

MAHALI  TUNAPO  PATIKANA.
Tunapatikana  jijini  DAR  ES  SALAAM, katika  eneo  la  UBUNGO  karibu  na  SHULE  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

KWA  WATEJA  WASIO  WEZA  KUFIKA  OFISINI  KWETU.
Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu  Tabata, tunao  utaratibu  wa  kuwafikishia  dawa  mahali  popote  walipo  ndani  ya  jiji  la  Dar  Es  salaam.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  DAR  ES  SALAAM.
Kwa  wateja  waliopo  nje  ya  Dar  Es  salaam, tunawatumia  dawa  kwa  njia  ya  MABASI.

Kwa  wateja  wa  ZANZIBAR  tunawatumia  dawa  kwa njia  ya  boti.

KWA  WATEJA  WA  NJE  YA  NCHI:
Kwa  wateja  wa  nje  ya  nchi, tunatumia  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA : 0766  53 83 84

TUTEMBELEE:

Rais Magufuli Amuapisha Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe Mathias Chikawe Ikulu Jijini Dar es Salaam

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi wa Tanzania nchini Japani asubuhi hii  Mhe.Mathias Chikawe Ikulu jijini Dar es Salaam.

==>Tazama video hii kuona akila kiapo

Breaking News: Rais Magufuli Amsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe

$
0
0

Rais Magufuli amemsimamisha kazi mchana huu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Wilson Kabwe kutokana na ufisadi wa kutisha katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya mji  na  kuisababishia  serikali  hasara  ya  sh. bilioni 3.

Rais Magufuli amechukua uamuzi huo mchana huu wakati wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Paul Makonda alitoa Hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam  ikiwemo  ripoti ya tume aliyounda  kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo.

Akieleza zaidi, Makonda  amesema, Kamati aliyounda  ilibaini kuwa pale ubungo kunatumika sheria ndogo mbili za ukusanyaji mapato moja ya mwaka 2004 na nyingine ya mwaka 2009  ambazo zote zilisainiwa na Wilson Kabwe.

Amesema  kuwa Sheria  ya Mwaka 2004 ya ukusanyaji mapato, inaonesha kuwa kila basi  linaloingia Ubungo linatakiwa kutozwa Sh 4,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 42 kutokana na mabasi 350 yanayoegeshwa kituoni hapo   na   Sheria  ya Mwaka 2009 ya ukusanyaji mapato, inaonesha kuwa kila basi  linaloingia Ubungo linatakiwa kutozwa Sh 8,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 82  kwa mwezi

Makonda amesema kwamba, Kabwe alisaini mikataba miwili, wa 2004 na wa mwaka 2009  ambapo ule wa mwaka 2004  ulipelekwa jiji  na  ule wa 2009 ukapelekwa kwa mzabuni, hivyo jiji wanajua kuwa kila basi linatozwa sh. 4000 kwa  siku wakati mzabuni  anatozwa  8000 kwa siku

Makonda pia ameongeza kuwa Mkurugenzi huyo vilevile amekiuka sheria ya kutoa zabuni baada ya anayefanya kazi ya kutoza kodi za 'packing' katika jiji la Dar es salaam kumaliza muda wake lakini Mkurugenzi alimuongezea muda wa miezi minne kwa barua na baadaye miezi 6 kwa kisingizio kwamba mchakato unaendelea wa kumpata mtu mwingingine bila ya kutangaza dhabuni jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Kutokana  na  maelezo hayo, Mheshimiwa Rais ametangaza kumsimamisha kazi bwana Kabwe ambaye  ni  Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam  na ameagiza vyombo vya dola vianze uchunguzi mara moja ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa

“Kama vyombo hivyo vitamsafisha mimi sitakuwa na neno,” alisema Rais Magufuli huku akisisitiza kuwa ni muda wa watu waliowafanya wananchi kulia kwa muda mrefu, na wao waanze kulia ili wananchi wacheke. 
Wilson Kabwe

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images