Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 18


Symbion Tanzania, Tanesco Zabaruzwa Kortini Zikidaiwa Bilioni 560

$
0
0

Kampuni kutoka Falme za Kiarabu, Rental Solutions and Services LLC imeiburuza mahakamani kampuni ya kufua umeme ya Symbion Tanzania Limited, ikidai kulipwa Dola za Marekani 228,070,655.67 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 560 kama fidia na malipo ya ukodishaji wa mitambo ya kuzalishia umeme nchini.

Kesi hiyo Namba 234 ya mwaka 2016 imefunguliwa katika Mahakama Kuu Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mdaiwa wa pili katika shauri hilo ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambalo limeunganishwa katika kesi hiyo kama mdau mkuu kwenye sakata hilo ambapo maamuzi yatakayotolewa na mahakama yanaweza kuiathiri.

Katika hati ya madai, Kampuni ya Rental Solutions and Services inadai Symbion Dola za Marekani 28,070,655.67 kama malimbikizo ya gharama za ukodishwaji wa mitambo, ambayo hadi sasa Symbion imeshindwa kulipa na pia katika shauri hilo Symbion itatakiwa kulipa Dola za Marekani milioni 200 ambazo ni fidia kwa kampuni hiyo kula hasara kutokana na Symbion kuvunja masharti ya mkataba na kuchelewesha au kushindwa kufanya malipo hayo.

Kwa mujibu wa hati hiyo ya madai, fedha hizo zinatokana na kazi zilizofanywa na kampuni hiyo ya Uarabuni ya kusambaza, kusimika na kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme ambayo ilikodishwa na Symbion kwa matumizi ya miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme kwa ajili ya Tanesco ili usambazwe kwenye Gridi ya Taifa kama ilivyokubaliwa kwenye mikataba.

Rental Solutions and Services pia katika kesi hiyo, inaiomba Mahakama kutamka kuwa kushindwa kwa Symbion kulipa gharama hizo za ukodishaji kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba na pande zote mbili kumesababisha uvunjifu wa mkataba na hivyo sio halali na haistahili kuendelea.

Inadaiwa kuwa kati ya Septemba 2011 hadi Juni 2013, Rental Solutions and Services iliingia mikataba mbalimbali na Symbion ambapo pale ilipohitajika mikataba hiyo iliongezewa muda ili kukidhi mahitaji kwa mujibu wa mikataba hiyo kwa lengo la kusambaza na kusimika mitambo ya umeme ili kusambazwa kwenye Gridi ya Taifa.

Septemba 21, 2011 kampuni hiyo ya Uarabuni iliingia mkataba na Symbion kwa ajili ya kusambaza na kusimika mitambo ya umeme katika Kituo cha Zuzu cha Tanesco chenye nguvu ya kilovolti 33 kilichoko Dodoma yenye uwezo wa kuzalisha megawati 50.

Katika mitambo hiyo, pande husika zilikubaliana malipo ya Dola za Marekani 1,374,500 kwa mwezi kwa kipindi ambacho kingeishia miezi sita. Inadaiwa kuwa kwa kipindi hicho, Symbion ingepaswa kulipa jumla ya Dola za Marekani 8,247,000.

Hati ya mdai inaonesha kuwa mkataba kama huo uliingiwa na pande zote mbili Februari 12, 2012, kuhusu mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 55 kwa kipindi cha miezi 12 kwa gharama ya Dola za Marekani 1,666,000 kwa mwezi.

Mitambo hiyo ipo katika vituo vya Arusha na Dodoma. Kwa mujibu wa hati ya madai, kulikuwepo na ongezeko wa muda wa matumizi wa mitambo hiyo katika vituo vya Dodoma na Arusha ambapo Rental Solutions and Services ilitimiza matakwa yake kama ilivyo kwenye mikataba na iliwasilisha hati za malipo kwa Symbion ili kukamilisha malipo ya kukodi kitambo hiyo kama inavyotakiwa.

Pamoja na Rental Solutions and Services kutimiza masharti ya mikataba hiyo, kati ya Dola za Marekani 77,667,666.28, Symbion imelipa dola 49,597,010.61 tu. Hivyo, Rental Solutions and Services inadai kuwa hadi sasa, bila uhalali wowote, Symbion imeshindwa kutimiza masharti ya mkataba kwa kutolipa kiasi cha dola 28,070,655.67.

Samia: Utumbuaji Majipu Serikalini Haumuonei Mtu

$
0
0

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema serikali haina nia ya kumwonea mtu, inapochukua hatua ya kutumbua majipu kwa watumishi wa umma.

Samia aliyasema hayo juzi baada ya kupokea taarifa ya Mkoa wa Morogoro, iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa huo, Dk Steven Kebwe akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani humo.

Alisema lengo la kutumbua majipu ni kurekebisha na kurejesha nidhamu, uadilifu na uwajibikaji serikalini, kama ilivyoangizwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili Watanzania wote wafaidike na matunda ya nchi yao.

“Mtasikia katika serikali tunarekebisha, majipu yanatumbuliwa... kwa kweli hatuna nia ya kumwonea mtu, tunarekebisha kama ilivyoagizwa katika Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi ili Watanzania wote wafaidi matunda ya nchi yao,” alisema Samia.

Alisema katika marekebisho hayo, serikali imechukua hatua ya kukata mishahara ya walio juu na kunyanyua ya walio chini waje juu kidogo na kwamba jitihada zote hizo ni katika kufanya mambo yaende vizuri nchini.

“Tunapozungumzia amani na utulivu ni pamoja na kuhakikisha kwamba walio chini wapo vizuri, wasipokuwa vizuri hakuna amani na utulivu, kazi itawapata watu wa kamati ya ulinzi na usalama, kuwatuliza kila siku na hawatatulizika kwa sababu wana shida,” alisema Makamu wa Rais na kuongeza: “Lakini tukiwatuliza kwenye mambo yao wana maji, wana umeme, wana chakula, mtoto anaenda shule vizuri, anapata afya, akienda zahanati dawa zipo, watatulia tu.”

Alisema kwa hivi sasa kuna tatizo la watumishi hewa na wengine wamediriki kumdanganya mkuu wao wa kazi na hayo ndiyo mambo ambayo hayaleti picha nzuri katika serikali.

Aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya nchini kuunga mkono jitihada hizo za serikali ili kurejesha nidhamu na uwajibaikaji kwa watumishi wote. Wakati huo huo, Makamu wa Rais ametembelea kiwanda cha kutengeneza nguo cha Mazava, ambapo aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuzingatia masharti ya ajira na wafanyakazi kuchapa kazi kwa bidii ili Taifa lipate kodi na wao wapate mapato.

Akizungumza na wafanyakazi, Samia aliuhakikishia uongozi wa kiwanda hicho kuwa serikali itazifanyia kazi changamoto za eneo na ukosefu wa ujuzi kwa kuwapeleka vijana wengi kwenye vyuo vya elimu ya ufundi stadi (VETA) kujifunza ushonaji.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo kwenye viwanda na kusisitiza kwamba kupitia mpango wa EPZ, viwanda vingine vinatarajiwa kujengwa mkoani humo, jambo ambalo litaongeza ajira kwa vijana.

Kiwanda hicho ambacho kilianza uzalishaji mwaka 2010 kina wafanyakazi zaidi ya 2,000 na kwamba asilimia 100 ya nguo zinazozalishwa kiwandani hapo, zinauzwa nje ya nchi, ambapo soko kuu liko Marekani.

Gwajima: Mafisadi Wanataka Kumkwamisha Rais Magufuli

$
0
0

Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema mafisadi walioinyonya nchi katika Serikali ya awamu ya nne, ndiyo wanaoona utawala wa Rais John Magufuli haufai. 

Akizungumza masuala ya kitaifa kwa kifupi, huku akitoa mafundisho kwa waumini wake jana katika ibada kanisani kwake, Gwajima alimtaka Dk Magufuli aendelee kushikilia uzi huo huo bila kuulegeza. 

Gwajima ambaye mwaka jana, wakati wa vuguvugu za kampeni ya Uchaguzi Mkuu, aliwahi kusema wasiopenda kuona yeye akimsaidia aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa basi wachukue ndimu wale, jana alisema mafisadi ni wachache na Magufuli anafanya kazi ili kuhakikisha Watanzania wengi wananufaika na uongozi wake. 

Mara kadhaa, Askofu Gwajima alikaririwa akisema kuwa atamsaidia kiongozi yeyote mwenye lengo la kuleta mabadiliko ya taifa, bila kujali anatoka chama gani.

 Katika mikutano yake, Gwajima alikuwa akiwataka waumini wake kuchagua kiongozi wanayedhani atawaletea mabadiliko, na alikaririwa na vyombo vya habari akiingia katika malumbano makali na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilibrod Slaa ambaye mbele ya waumini wake alimwita kuwa ni rafiki yake. 

Jana akimzungumzia zaidi Dk Magufuli, Askofu Gwajima alisema, “wasikukatishe tamaa endelea hivyo hivyo kuna wanyonyaji walipenyeza mirija yao katika Serikali iliyopita wakati wao umefika, wanatapatapa.” 

Askofu Gwajima alisema yeye ataendelea kupambana na ufisadi kumsaidia Dk Magufuli kwa kutumia jina la Yesu Kristo na si vyombo vya dola.

Alisema mkono wake ni mgumu kama wa chuma na kwamba kwa kulitumia jina hilo, hawezi kushindwa kuwashughulikia watu wa aina hiyo. 

“Nitatumia jukwaa hili hili la Yesu Kristo kuwasambaratisha wasioitakia mema Serikali ya Magufuli, kwani zama zao zimekwisha,” alisema. 

Askofu huyo alisema kuna taasisi zilifikia hatua ya kutengeneza magonjwa na hizo hizo zinatoa misaada ya dawa kwa Tanzania. 

“Yaani makampuni yanatengeneza magonjwa halafu hao hao wanatoa misaada ya dawa hizo kwa Tanzania, unajiuliza ilikuwa serikali ya namna gani,” alisema. 

Alisema taasisi hizo ziko tayari kuua Watanzania ili kujipatia fedha chafu ambazo maisha ya ndugu zetu yanapotea. 

“Kuna watu wananiuliza Gwajima Ufufuo na Uzima ni kanisa, dhehebu au wanaharakati unasema kila kasoro iliyo mbele yako, nikawajibu ni majeshi ya Yesu Kristo,” alisema. 

Aliyataka madhehebu mengine ya dini kukemea maovu ili kuleta maisha bora ya waumini wao. 

Gwajima aliwataka waumini hao, kutumia jina la Yesu Kristo kila wanafanya ibada kwani maombi yao yatajibiwa kwa kutaja jina hilo.

Vigogo Jiji la Dar es Salaam Wakalia Kuti Kavu....Makonda Afichua Siri Mikataba Tata, Ataka Mamlaka za Uteuzi Ziwaondoe

$
0
0

Kamati maalumu ya uchunguzi iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda imefichua madudu na harufu ya ufisadi katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya mji.

Kutokana na madudu hayo, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha wazi kuwa hataki kufanya kazi tena na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe na Kaimu wake, Sarah Yohana na kuwasilisha majina yao kwa mamlaka husika ya nidhamu kwa hatua zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, alisema hivi karibuni aliunda kamati hiyo maalumu kufuatilia maeneo hayo muhimu kutokana na malalamiko ya muda mrefu, ambayo ofisi yake ilikuwa ikipokea kutoka kwa wananchi.

Alisema kwa mujibu wa uchunguzi, kamati hiyo ilibaini kuwa katika stendi ya mabasi ya Ubungo, kumekuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma, ikiwemo kutokuwasilishwa kwa mapato halisi yanayotokana na makusanyo ya kila siku serikalini.

“Kamati ile imebaini kuwa pale ubungo kunatumika sheria ndogo mbili za ukusanyaji mapato moja ya mwaka 2004 na nyingine mwaka 2009 kwa lengo la kunufaisha wachache,” alisema Makonda.

Alifafanua kuwa Sheria Ndogo ya Mwaka 2004 ya ukusanyaji mapato ndani ya kituo hicho, inaonesha kuwa kila basi linatakiwa kutozwa Sh 4,000, hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 42 kutokana na mabasi 350 yanayoegeshwa kituoni hapo.

Hata hivyo, alisema kutokana na mabadiliko ya tozo, sheria hiyo ilibadilishwa mwaka 2009 na kila basi likawa linatozwa Sh 8,000 na hivyo makusanyo ya mwezi yakapanda na kufikia Sh milioni 82 kwa mwezi.

“Lakini cha kushangaza tumebaini kuwa bado kampuni inayokusanya mapato katika kituo cha Ubungo, inawasilisha mapato hayo kwa kutumia sheria ya mwaka 2004 yaani Sh milioni 42 badala ya Sh milioni 82 kwa mwezi…” 

“…Mbaya zaidi kamati ile katika ukaguzi wake, ilikuta kampuni ya ukusanyaji mapato hayo stendi ya Ubungo inayo Sheria ya Mwaka 2009 lakini katika nyaraka za Halmashauri ya Jiji zinaonesha sheria inayotumika ni ya mwaka 2004,” alisisitiza Makonda.

Alisema katika uchunguzi ilibainika kuwa kampuni iliyo chini ya Halmashauri ya Jiji inayokusanya mapato hayo stendi ya Ubungo, ilisaini mkataba wa ukusanyaji mapato hayo kwa mara ya kwanza Januari 31, 2004 na baadaye ikasaini tena mkataba Januari 30, mwaka jana.

Kwa mujibu wa Makonda, kwa hali ilivyo tangu Sheria Ndogo ya Mwaka 2009 ipitishwe, haijawahi kutumika na hivyo kulisababishia hasara jiji hilo ya Sh bilioni tatu kutokana na mapato katika stendi hiyo kuendelea kuwasilishwa kwa kutumia sheria ya mwaka 2004.

“Ukipiga hesabu za harakaharaka utagundua kuwa kila mwezi Sh milioni 42 zimekuwa zikipotelea kwenye mikono ya wachache, kwa maana hiyo kuanzia mwaka 2009 Sh bilioni tatu zimepotea na kila mwaka tumekuwa tukipoteza Sh milioni 500, huu ni ufisadi wa aina yake kwa kweli,” alisema.

Alisema wakati fedha hizo zikipotea kwenye mikono ya wachache, kamati hiyo pia ilibaini kuwa hali ni mbaya katika kituo hicho cha Ubungo kwani pamoja na ukosefu wa vyoo na maegesho bora kwa mabasi, lakini pia vibanda vya biashara vilivyomo ndani ya stendi hiyo, vimekuwa vikitumika kukandamiza maskini na kunufaisha wachache.

“Kwa mujibu wa taratibu, kila kibanda mle ndani ya stendi kinatakiwa kukodishwa kwa Sh 200,000 kwa mwezi, lakini tumebaini kuwa wapo watu wachache wamevihodhi na kuvikodisha kwa zaidi ya Sh milioni 1.5,” alisema.

Kuhusu mkataba wa maegesho katikati ya jiji kupitia Kampuni ya National Parking System (NPS), alisema kamati hiyo pia imebaini kuwa Halmashauri ya Jiji imeiongezea mkataba wa miezi 10 kampuni hiyo kinyume cha taratibu wakati mkataba wake ulikuwa umeshamalizika.

Alisema mara baada ya mkataba huo kumalizika Agosti mwaka jana Mkurugenzi wa Jiji, Kabwe aliiandikia barua kampuni hiyo na kuiongezea muda wa miezi sita kwa madai kuwa mchakato wa kutafuta mzabuni mpya pamoja na kwamba umeanza, haujakamilika.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi Yohana naye aliandika miezi kadhaa baadaye barua na kuiongezea tena kampuni hiyo muda wa miezi minne iendelee kukusanya kodi ya maegesho kwa kuwa bado mchakato wa kutafuta mzabuni mpya haujakamilika.

“Barua zote mbili zina saini ya viongozi hawa wawili, hatua hizi ni kinyume kabisa na maadili ya viongozi pamoja na Katiba ya nchi. Haiwezekani mchakato wa kumtafuta zabuni uchukue zaidi ya miezi sita,” alieleza Makonda.

Pamoja na hayo, Makonda pia alisema kamati hiyo katika uchunguzi wake dhidi ya Kampuni ya Tambaza inayosimamia makosa ya pikipiki na maegesho ya magari katika sehemu zisizotakiwa, imekuwa ikitoza fedha nyingi za faini kinyume cha mkataba.

“Mkataba wao unaonesha wazi kuwa wanatakiwa wakikamata pikipiki yenye makosa watoze faini ya Sh 20,000 lakini imebainika wao wanatoza zaidi ya Sh 80,000. Licha hivyo pia mkataba unawataka wazingatie dharura na kutotumia lugha chafu lakini yote haya hawayazingatii,” alisema.

Alisema tangu Rais John Magufuli aingie madarakani amekuwa mstari wa mbele kupiga vita ubadhirifu wa fedha za umma, rushwa na ufisadi hivyo akiwa kama Msaidizi wa Rais anaunga mkono juhudi hizo ndio maana hawezi kunyamazia madudu yeoyote yanayohusu ufisadi.

“Nimewasiliana na mamlaka husika ya nidhamu ili ichukue hatua stahiki dhidi ya viongozi hawa wawili Kabwe na Yohana na nimeiambia mamlaka hii kwa uwazi kabisa siwahitaji kuendelea nao hapa Dar es Salaam,” alisisitiza.

Aidha, alisema tayari amewasiliana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu mikataba hiyo yote mitatu ambayo imeahidi kuanza kuifanyia kazi leo.

Alisema ameamua kuchukua hatua hiyo ya kuwashughulikia wakurugenzi hao kwa kuwa wao ndio tatizo kwani mikataba hiyo hata ikivunjwa kwa sasa itakuwa ni kazi bure kama viongozi hao wataendelea kuwepo.

Hii ni mara ya pili kwa Stendi ya Ubungo kuingia katika kashfa ya ubadhirifu wa fedha, ambapo mwaka 2011, Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda aliagiza ufanyike uchunguzi, uliobaini kuwepo kwa madudu, hali iliyosababisha mzabuni aliyekuwepo kuondolewa.

Kampuni binafsi zaongoza kuajiri wahamiaji haramu

$
0
0

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga, Anamaria Yondani ameeleza kuwa kipindi cha miezi mitatu wamekamata wahamiaji haramu 283, huku kampuni binafsi zikiongoza kwa kuajiri watu hao kinyume cha utaratibu.

Pia alifafanua kuwa wahamiaji hao 111 walikuwa sio rasmi, 45 walifikishwa mahakamani, saba walifungwa, 103 walifukuzwa nchini, 172 waliachiwa huru na waliomaliza kifungo ni wanne.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mwishoni mwa wiki, Yondani alisema kukamatwa kwa wahamiaji hao kumetokana na kufanya msako mbalimbali na kutoa elimu ya dhana ya uhamiaji shirikishi katika makundi mbalimbali ya kijamii.

Alisema wamewakamata wahamiaji haramu hao 283 wengine wakiwa wameajiriwa kwenye baadhi ya kampuni binafsi kinyume cha sheria na taratibu za nchi, wakiwa wanatoka katika mataifa tofauti tofauti.

“Kipindi cha miezi mitatu tumefanikiwa kukamata wahamiaji haramu 283 huku kampuni binafsi zikiongoza kuwapatia ajira kinyume na taratibu, mimi nilikuwa nawaomba wamiliki wa kampuni hata wanapokuwa na vibali vya kisheria wahamiaji hao basi wawaingize katika ajira kwa kufuata utaratibu na sheria za nchi,” alisema.

Alisema wengi wa hao wana vibali vya kuishi, lakini anaingizwa kwenye ajira kinyume cha taratibu na ndio wengi wao wamekamatwa kwa makosa hayo.

 Wahamiaji hao wanatoka nchi za Kenya, Jamhuri ya Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Rwanda, Somalia, Ethiopia na China.

Miswada Tata Kutua Bungeni .....Serikali Kubanwa kwa Maswali 553 Huku 88 Yakiwa ya Papo Kwa Papo

$
0
0

Serikali inatarajiwa kuwasilisha miswada mbalimbali ya sheria katika Mkutano wa Bunge la Bajeti utakaloanza kesho mjini Dodoma ili ijadiliwe na kupitishwa na wabunge. 

Miswada mingi ya sheria imekuwa ikilalamikiwa na wadau, hata Rais John Magufuli wakati akizindua Bunge la 11 mwaka jana, alilalamikia Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011.

Alisema kuwa sheria hiyo inatoa mianya kwa watumishi kuiba fedha za umma. 

Katika mkutano huo, Bunge linatarajia kujadili na kupitisha miswada miwili ambayo ni wa Sheria ya Matumizi wa mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2016.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya jana alisema Serikali itawasilisha pia bungeni miswada mingine ya sheria ijadiliwe na kupitishwa baada ya kupitisha bajeti kukamilika.

Hata hivyo, alisema Bunge bado halijapokea miswada itakayowasilishwa na Serikali zaidi ya hiyo miwili, lakini kuanzia Juni 24 hadi 30 zimetengwa kwa ajili ya kujadili miswada mingineyo.

Mwandumbya alisema pamoja na shughuli hizo, jumla ya maswali 465 yataulizwa na kujibiwa na Serikali bungeni na kila Alhamisi yataulizwa Maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu na anatarajia kujibu jumla ya maswali 88.

“Baada ya wabunge kujadili miswada itakayowasilishwa na Serikali, hoja ya kuahirisha Bunge itatolewa Julai Mosi. Hapo Bunge litakuwa limemaliza kazi yake ya kujadili bajeti za wizara zote katika mkutano huu,” alisema Mwandumbya.

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) Yalalaimika Kukandamizwa na Serikali

$
0
0

Mtandao wa Madeni na Maendeleo Tanzania (TCDD) umeitaka Serikali kutafakari upya Sheria ya Asasi za Kiraia ili kuyaondolea mzigo wa uendeshaji Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) badala ya kuyafungia kutokana na sababu mbalimbali. 

Hivi karibuni Serikali kupitia kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, ilifuta usajili wa NGO’s 110 kwa kuendesha shughuli zao kinyume cha Sheria ya NGOs Na 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005. 

Kwa mujibu wa msajili huyo, mashirika hayo ni yale ambayo hayajawasilisha taarifa za mwaka kwa kipindi cha miaka miwili bila kutoa sababu za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCDD, Hebron Mwakagenda alisema kuna haja kwa Serikali kuangalia mashirika hayo kabla ya kukimbilia kuyafungia. 

Aliiomba Serikali ifute ada ya mwaka na ilipwe wakati wa kusajili tu na aliikosoa pia sheria hiyo akisema inayalazimisha mashirika hayo kupeleka taarifa zao Dar es Salaam kutoka kila kona ya nchi badala ya kupeleka kwenye ngazi za wilaya.

“Maofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri za wilaya ambao pia ni wasajili wasaidizi na waratibu wa shughuli hizi wapewe mamlaka ya kupokea taarifa za utendaji kila mwaka kwa niaba ya msajili ili kuepusha usumbufu wa kusafiri hadi Dar es Salaam.” Alisema Hebron Mwakagenda

Edmund Simon wa asasi ya Umoja wa Wawezeshaji kutoka Kigoma iliyo chini ya mtandao huo, alisema Serikali inapaswa kuzisaidia NGOs na asasi badala ya kuzikandamiza. 


Mkuu wa Wilaya Amzuia Waziri Nchemba Kwenda Kijijini Kusikiliza Kero za Wananchi

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, juzi alimzuia Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba kwenda kijiji cha Mikomario wilayani Bunda kutatua mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji kwa madai ya wasiwasi wa usalama kuwa mdogo. 

Baada ya jitihada zake za kumzuia kugonga mwamba, Nyamubi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Bunda aliamua kujitenga na ziara hiyo kwani licha ya kufika eneo la mkutano, hakujihusisha na lolote kwa kuamua kukaa pembeni. 

“Mheshimiwa waziri nakushauri usiende Kijiji cha Mikomario kwa muda huu ambao unakaribia usiku kwa sababu usalama utakuwa ni mdogo kutokana na ukorofi wa wananchi wa eneo lile,” alishauri Nyamubi wakati akizungumza na Nchemba ofisini kwake.

Hata hivyo, waziri Nchemba alisisitiza kuwa lazima aende kuzungumza na wananchi hata kama atalazimika kuhutubia kwa kutumia taa za gari kwa sababu aliwaahidi kuwa angefika na kuzungumza nao na walikuwa wakimsubiri tangu mchana.

 “Mheshimiwa kaimu mkuu wa mkoa, bado sijashawishika kutotimiza ahadi ya kwenda kuzungumza na wananchi wale, wamenisubiri tangu asubuhi na nimepata taarifa wako uwanjani hadi jioni hii wakinusubiri. Kutokwenda ni kutowatendea haki,” alisisitiza Nchemba.

Baada ya msimamo huo, ndipo Nyamubi alipotangaza kujitoa kwa lolote ambalo lingetokea, licha ya kuwamo kwenye msafara wa viongozi uliofika kijijini hapo saa 12.40 jioni, hakukaa meza kuu wala kujishughulisha na lolote hadi mkutano ulipomalizika kwa amani saa 1.10 usiku.

Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho ambacho kimekuwa na mgogoro wa ardhi kwa miaka 30 sasa bila ufumbuzi, Waziri Nchemba aliahidi kuutafutia ufumbuzi, lakini akawasihi kuwa na subira kwa sababu lazima awasiliane na wizara nyingine zinazoguswa nao.

“Suala hili ni la kisheria, hivyo linatakiwa kutatuliwa kisheria badala ya mapigano, nipeni fursa ili wizara yangu iwasiliane na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Tamisemi ili kwa pamoja tuutafutia ufumbuzi.

“Wenye mamlaka ya kupanga na hata kubadili matumizi ya ardhi ya kijiji ni ninyi wananchi kupitia mikutano na Serikali yenu ya kijiji, viongozi na wataalamu kazi yetu ni kutoa ushauri kuhakikisha uamuzi wenu unakuwa halali,” alisema. 

Wakiwa na mabango yenye ujumbe, wakazi hao walimpongeza waziri kwa kutimiza ahadi ya kuzungumza nao ili kutafutia ufumbuzi mgogoro huo unaohusu hekta 2, 500 zinazodaiwa kutolewa kwa mwekezaji bila ridhaa ya Serikali ya Kijiji. 

Ratiba ya Mkutano wa Bunge la Bajeti 2016/17 Linaloanza Kesho Tarehe 19 Hadi Mwezi wa 7 Tarehe 1

$
0
0
Mkutano wa Tatu (3) wa Bunge la Kumi na Moja (11) unatarajia kuanza mjini Dodoma kesho tarehe 19 Aprili 2016. Mkutano huu ni mahususi kwa ajili ya kujadili na kupitisha Bajeti ya Serikali.

Wabunge wote wametakiwa kuwasili mjini Dodoma siku ya Jumapili tarehe 17 Aprili 2016

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Lipumba Azidi Kuitesa CUF

$
0
0

Wanachama  wa Chama cha Wananchi (CUF), wameanza kushikana uchawi, huku viongozi wakitakiwa kutoa maelezo ya kwanini wameshindwa kujadili hatua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

Pamoja na hali hiyo, wanachama hao wamemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kutambua kuwa ana wajibu wa kuwasiliana na Profesa Lipumba ili arejee katika nafasi yake ya zamani kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam jana, wakati wa  kongamano lililoandaliwa na Kata ya Makurumla Manispaa ya Kinondoni, ambapo mmoja wa wana CUF Mohamed Mgomvi, alisema anashangazwa na hatua ya kikao cha Baraza Kuu kushindwa kujadili barua ya kujiuzulu Profesa Lipumba.

Alisema CUF kwa upande wa Bara, imebaki haina mtu madhubuti ambaye anaweza kukiendesha kama alivyokuwa kiongozi huyo.

“Ninashangaa hapa mzee Wandwi (Mustafa), kama Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama unashindwa kusema ukweli. Leo hii (jana) CUF imebaki yatima tangu alipoondoka Profesa Lipumba halafu mnasema tupo naye pamoja.

“Haiingii akilini hata kidogo, ni unafiki umetawala kwa baadhi ya viongozi ambao kila kukicha wanakutana na Lipumba wanamuonyesha wanamhitaji, akitoka mnamsema vibaya.

“…napenda kukuambia leo CUF hakuna mwenye uwezo wa kuvaa viatu vya Profesa Lipumba tunamhitaji kiongozi wetu, tumechoka kuburuzwa na unafiki unaoendelea ndani ya chama,” alisema Mgomvi.

Naye Mangaa Dachi, alisema  kwa mujibu wa katiba ya CUF barua ya kujiuzulu Profesa Lipumba inatakiwa iwasilishwe katika kikao cha mkutano mkuu uliomchagua kuliko ilivyo sasa.

“Hivi mnajua kama chama tunavunja Katiba? Kama ndivyo hivyo bado suala la Profesa Lipumba linatakiwa kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu, nasi tunamtaka Lipumba arudi katika nafasi yake,” alisema Dachi.

Pamoja na hali hiyo wanachama hao walilalamikia mfumo wa upatikaji wa wabunge wa viti maalumu ndani ya chama hicho kuwa umekuwa ukihusishwa na tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wakurugenzi.

“Hatuwezi kuvumilia hali hii hata mfumo wa upatikaji wa wabunge wa viti maalumu hivi sasa watu wanafanya wanavyojisikia, leo kuondoka kwa Lipumba wapo baadhi ya wakurugenzi wanatajwa kuchukua fedha kutoka kwa baadhi ya wabunge waliopo sasa ili wawape ubunge,” alisema.

Akifungua kongamano hilo, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CUF, Mustafa Wandwi, alisema pamoja na yanayoendelea bado wako pamoja na Profesa Lipumba kwa kila jambo linaloendelea ndani ya chama hicho.

Alisema kutokana na hoja ya washiriki wa kongamano hilo, bado kuna kila sababu ya kutafakari kwa kina suala la Profesa Lipumba lakini hata katika kikao cha Baraza Kuu la Uongozi kilichofanyika hivi karibuni visiwani Zanzibar, suala hilo lilijadili kwa kina.

Rais Magufuli Amteua Mathias Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan.

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe kuwa Balozi wa Tanzania  nchini Japan.
 
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 18 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi   John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Chikawe umeanza tarehe 13 Aprili, 2016.
 
Kabla ya kupangiwa kituo hicho cha kazi, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe aliteuliwa kuwa Balozi mnamo tarehe 15 Februari, 2016.
 
Mheshimiwa Chikawe aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nachingwea kati ya Mwaka 2005 na 2015, na kwa vipindi tofauti katika Serikali ya awamu ya nne alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili, 2016

Makamu Wa Rais Mhe. Samia Azindua Mbio Za Mwenge Wa Uhuru Mkoani Morogoro Leo

$
0
0
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro leo.

Katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais alimnukuu Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere akisema kuwa nia ya Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo ni kumulika mipaka ya nchi yetu dhidi ya maadui, kuleta matumaini pale ambapo hakuna matumaini, kuondoa chuki pale ambapo kuna chuki na kuleta heshima pale ambapo kuna dharau.

Alisema nia hiyo ya kuwepo kwa Mwenge wa Uhuru kama alivyomnukuu Baba wa Taifa, inaendana na dhana ya kutumbua majipu katika Serikali ya awamu ya tano. Alisema utumbuaji majipu unalenga kuleta matumaini kwa wananchi ambao wamekata tamaa na kuleta heshima kwa wananchi waliodharauliwa.

“Kaulimbiu ya mbio ya za mwenge mwaka huu ni hii: Vijana ni nguvu kazi ya taifa, washirikishwe na wawezeshwe,”alisema Makamu wa Rais na kuongeza kuwa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa hawajatumika ipasavyo kutokana na sababu mbalimbali.

Alizitaja baadhi ya sababu au changamoto zinazowakabili vijana nchini kuwa ni ukosefu wa ajira, uwezo mdogo wa kuajiri kwenye soko la ajira, ukosefu wa mitaji rafiki kwa vijana, maeneo ya kufanyia kazi pamoja na mitazamo hasi kwa baadhi ya vijana kwa kuchagua kazi.

Makamu wa Rais pia amewataadharisha vijana kutokana na ongezeko kubwa la maambukizi ya ukimwi na matumizi ya madawa ya kulevya. 

Amesema vijana wenye umri kati ya miaka 16-24 ndiyo wanaongoza kwa kuathiriwa na maambukizi ya ukimwi.

 Amesema athari za ukimwi na madawa ya kulevya kwa vijana ni kubwa lakini pia zinaongeza mzigo kwa jamii na serikali katika kuwatibu, kuwahudumia na kuongezeka kwa vifo.

Kwa upande wake, Waziri Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, amemtambulisha George Jackson Kijimba kuwa ndiye kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu akisaidiana na wakimbiza mwenge  wengine watano.

 Alisema sherehe za kuhitimisha mbio hizo za mwenge wa uhuru zitafanyika mkoani Simiyu tarehe 14 Oktoba mwaka huu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Taifa kwenye Sherehe za uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa zilizofanyika leo april 18, 2016 katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

Serikali Yakanusha Kuhusu Swala La Leseni Ya Madini Kutolewa Katika Hifadhi Ya Mwiba

$
0
0

Gazeti la Raia Tanzania Toleo Na.0615 la Tarehe 15 Aprili, 2016 liliandika taarifa  yenye kichwa cha habari “Mbunge apewa mgodi hifadhini” huku likieleza kuwa Mbunge wa Meatu, Salum Khamis Salum (CCM), ametumia ushawishi alionao kisiasa kufanikisha upatikanaji wa leseni ya kuchimba shaba katika eneo la Gururum lililomo ndani ya Hifadhi ya Mwiba, Meatu mkoani Simiyu.

Gazeti hilo lilieleza kuwa leseni hiyo ilitolewa na Ofisa Madini Kanda ya Ziwa, Mhandisi Juma Sementa, yenye uhai wa miaka Saba na kwamba upatikanaji wa leseni hiyo haujawaridhisha wadau kadhaa wa ardhi na mazingira kwani mbali na sheria ya kuzuia uchimbaji madini ndani ya maeneo ya hifadhi nchini, wadau wengine hawakuhusishwa katika upatikanaji wake.

Wizara inapenda kutoa taarifa kuwa, wilayani Meatu kuna hifadhi ya Maswa (Maswa Game Reserve) na Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori katika eneo la Makao (JUHIWAPOMA) ambapo Jumuiya hiyo ilipitisha Mpango wa Kanda za Matumizi ya Rasilimali kwa mwaka 2015-2017 na kutenga eneo la Gururum lenye ukubwa wa kilomita 16.5 sawa na asilimia 2 ya eneo lote, kama kanda ya uchimbaji madini baada ya madini ya shaba kugundulika katika eneo hilo.

Katika eneo hilo la Gururum mpaka sasa jumla ya viwanja 82 vya uchimbaji mdogo wa madini (PML) vimetolewa ambapo kwa sasa hakuna shughuli zozote za uchimbaji zinazoendelea hadi tathmini ya uharibifu wa mazingira (EIA) itakapokamilika ambayo ipo katika hatua ya uwasilishwaji.

Hivyo tunautaarifu Umma kuwa mpaka sasa hakuna mgodi katika hifadhi ya Mwiba na kwamba leseni za uchimbaji mdogo wa madini zimetolewa katika eneo lililorusiwa tu kwa ridhaa ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori katika eneo la Makao (JUHIWAPOMA).

Tunawaasa waandishi wa habari kuhakiki taarifa wanazotoa katika vyombo vya habari kwa kuwasiliana na wahusika wanaotajwa katika habari husika ili kuepuka kutoa taarifa potofu kwa Umma.

IMETOLEWA NA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
18 APRILI, 2016

Tanzia: Aliyekuwa Mkurugenzi wa BoT Amatus Liyumba afariki dunia

$
0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania ( BOT), Amatus Liyumba amefariki dunia, msiba uko nyumbani kwake maeneo ya Triple Seven, Mikocheni jijini Dar.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peoni

Rais Magufuli Atinga Benki ya CRDB Tawi la Holland Jijini Dar es Salaam Leo

$
0
0


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezua taharuki mjini leo baada ya kufika katika Tawi la CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari binafsi lenye namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya adamu na hawa wala bendera.

Tukio hilo lililochukuwa takribani dakika 25, limetokea majira ya saa nne asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam katika tawi la benki hiyo ambalo liko katika makutano ya Barabara ya Ohio na Samora bila kutarajiwa.

Mara baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo makutano ya barabara hizo yalifungwa huku ndipo rais aliposhuka kwenye gari  na kuingia ndani ya benki hiyo.

Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyo  wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao walikwisha ingia.

Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa staili ile kwani baadhi ya wananchi walidai kuwa hawajaona tukio kama lile kwa marais wote waliopita.

James Charles, ambaye ni dereva wa Texi, alisema baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimalishwa walishtuka huku wasijue ni nini kinaendelea, hadi pale walipomuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.

“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja hata hivyo hatujui kama hiyo ilikuwa inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu haiwezekani aende akachukue fedha kwa utaratibu ule ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,” alisema Charles.

Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu, alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.

“Mimi wakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma kwa ujumla kila mmoja wetu alishtuka lakini hatukujua kilichomleta,”alisema.

Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari huku akiwapungia mkono wananchi.


Taarifa ya Wizara: Mabadiliko ya muda wa matumizi ya daraja la Kigamboni kesho

$
0
0
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya ufunguzi wa Daraja la Kigamboni kesho, Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016.

Kutokana na ufunguzi huo, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataarifu watumiaji barabara na Wananchi wote wanaotumia daraja hilo kuwa huduma ya magari kutumia daraja hilo itafungwa kwa muda kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana ili kuwezesha kufanyika kwa sherehe hiyo ya ufunguzi wa daraja. Aidha, huduma katika Daraja la Kigamboni itarejea kama kawaida kuanzia saa 8:00.

Daraja la Kigamboni lililoanza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5.

Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
18 Aprili, 2016.

Rais Magufuli ateua Mkuu Mpya wa Wilaya ya Kinondoni kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Paul Makonda

Ufafanuzi wa SSRA kuhusu hali na mwenendo wa NSSF Kifedha

$
0
0

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zisizo rasmi kuhusu hali na mwenendo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikieleza kwamba mali za Mfuko huo zimetumiwa vibaya na hivyo kuathiri mafao kwa wanachama.

Taarifa hizi zimesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wanachama wa NSSF na wadau wa Sekta ya Hifadhi ya jamii kwa ujumla kwa kuhofia usalama wa wa fedha na mafao yao.

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kuwaondoa hofu wanachama wote wa Mfuko wa NSSF na Wananchi kwa ujumla na kuwahakikishi kwamba Mfuko wa NSSF upo katika hali nzuri kifedha na unaendelea kulipa mafao ya wanachama kama kawaida.

Kama mnavyofahamu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko alikwishateuliwa na anaendelea na majukumu ya kusimamia shughuli zote za Mfuko.

Vilevile, taratibu za kupata Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko huo zipo katika hatua za mwisho.

Aidha, SSRA kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania kwa mamlaka waliyopewa chini ya Kifungu cha 6(2) (c) cha Sheria Na.8 ya mwaka 2008 ikisomwa pamoja na kifungu cha 40 na cha 48 wanaendelea kufanya kaguzi za Mifuko yote ukiwemo Mfuko wa NSSF kwa lengo la kuhakikisha kwamba muda wote Mifuko yote inakuwa katika hali nzuri kwa maslahi ya wanachama na taifa kwa ujumla.

Mwisho, Mamlaka inapenda kuwaondoa wasiwasi wanachama walioathirika na taarifa hizi pamoja na wanachama wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuwahakikishia kwamba fedha na mafao yao yapo salama na Mamlaka inazifanyia kazi kero zao kwa bidii kubwa.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images