Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Halima Mdee Amtaka Rais Magufuli Ataje Posho na Marupurupu Anayolipwa

$
0
0

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee amemuomba Rais John Magufuli kuweka wazi posho na marupurupu anayoyapata ili Watanzania wajue kiasi halisi anachokipata mbali na mshahara wake.

Mdee ambaye ni mbunge wa Kawe, alitoa ombi hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Sokoni, Jimbo la Mtama mkoani Lindi, uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo.

Kauli hiyo ya Mdee imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kutaja mshahara wake kuwa ni Sh9.5 milioni kwa mwezi. 

“Juzi Rais anasema eti mshahara wake Sh9.5 milioni, sasa atutajie posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho anakipata,” alisema Mdee.

Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh3 milioni, lakini kuna posho mbalimbali kutokana na kuhudumia wananchi.

“Sisi wabunge mshahara wetu katika hati ya mshahara unasomeka Sh3 milioni, lakini posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika Sh10 milioni, Rais atuambie na yeye posho zake ni kiasi gani,” alisema Mdee.

Mbunge wa Jimbo la Ndanda katika Wilaya ya Masasi, Cecil Mwambe alidai katika mkutano huo kuwa wananchi wa Mtama wamekosa mwakilishi wa kuwasemea matatizo yao, hasa ya upande wa kilimo cha korosho kutokana na mbunge wao, Nape Nnauye kukosa uwezo wa kusimama bungeni kuisema Serikali.

“Mtama mmekosa mwakilishi, hapa kuna tatizo la korosho na mbunge aliyepo anashindwa kulisemea, hivyo mtabaki hivyo hivyo bila kutatua tatizo lenu kwa kipindi cha miaka mitano,” alidai Mwambe.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 4

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

Maalim Seif leo kutangaza msimamo wa CUF Zanzibar

$
0
0

Wakati joto la kuundwa Baraza la Mawaziri Zanzibar likiwa linaendelea kupanda bila ya Chama cha Wananchi (CUF) kuwamo katika serikali, Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, leo anatarajiwa kutoa mwelekeo wa kisiasa wa chama chake baada ya kususia uchaguzi mkuu wa marudio visiwani humu.

Msimamo huo wa CUF kuhusu mwelekeo wa Chama baada ya kugomea uchaguzi mkuu, unakuja baada ya kukamilika vikao vizito vya chama hicho kikiwamo cha Kamati Tendaji na Baraza Kuu la Uongozi vilivyofanyika Shangani Mjini Zanzibar.

Akizungumza toka mjini Zanzibar jana, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, alisema kuwa tamko la chama hicho litatolewa na Katibu Mkuu wa CUF baada ya kukamilika kwa vikao muhimu vya chama hicho.

Alisema vikao hivyo vimefanyika kwa siku nne vikitanguliwa na vikao vya siku mbili vya Kamati Tendaji vilivyofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Maalim Seif.

“Vikao vimekamilika salama na ajenda kubwa tulikuwa tunajadili hali ya kisiasa ya Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa marudio kinyume cha Katiba na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar,” alisema Shehe.

Hata hivyo, alisema maazimio ya kikao hicho yatatangazwa na Maalim Seif ili wanachama na wananchi kwa jumla, wafahamu msimamo wa chama hicho.

Alisema mwelekeo wa CUF kisiasa utaendelea kubakia kupigania haki ya wananchi iliyoporwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), Jecha Salim Jecha, baada ya kufuta matokeo kinyume cha Katiba na Sheria Oktoba 28, mwaka jana.

Aidha, alisema Kikao cha Baraza Kuu kilikuwa cha kwanza kufanyika tangu kilipopitisha azimio la chama la kususia uchaguzi mkuu wa marudio uliyofanyika Machi, mwaka huu.

Msimamo wa Baraza Kuu la CUF umesababisha chama hicho kupoteza viti vyote vya Uwakilishi katika Majimbo 54 na Wadi 111 za madiwani katika Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na kupoteza nafasi ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Hata hivyo, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alisema kuwa anaamini Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, atatumia hekima na busara kwa kutumia nafasi zake 10 za Kikatiba kuwateua viongozi wa vyama vingine kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa madhumuni ya kuendeleza Serikali Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK).

Hata hivyo, nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar iliyokuwa ikishikiliwa na Maalim Seif, imekwama kufanyika uteuzi wake baada ya vyama vilivyoshiriki uchaguzi wa marudio, kushindwa kufikia masharti ya Katiba ikiwamo kupata asilimia 10 ya matokeo ya kura za Rais au viti vya majimbo katika Baraza.

Azimio la CUF linasubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi wa Zanzibar kama dira ya mwelekeo wa hali ya kisiasa ya Zanzibar baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa marudio wakati Rais Dk. Shein akiendelea kukamilisha kupanga safu za uongozi wa serikali yake.

Uhuru Kenyatta Ashupalia Ujenzi wa Bomba la Mafuta Toka Uganda hadi Tanzania.....Aenda Ufaransa kukutana na viongozi wa Total Ili Kuwaomba Lipite Kenya

$
0
0

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya  aliondoka  nchini mwake jana asubuhi kwenda Ufaransa na Ujerumani kwa ziara ya  kazi ambayo pamoja na mambo mengine itahusisha suala la ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda.

Kenya hivi karibuni  imeingia katika mvutano na Uganda,  ikiitaka jirani yake huyo kurudisha mpango wa kulipitisha bomba hilo la mafuta nchini humo (Kenya) badala ya Tanzania.

Suala hilo ni sehemu ya ajenda ya  biashara, ushirikiano na maendeleo ambayo ni moja ya malengo ya ziara ya Rais Kenyatta.

Kituo cha kwanza cha ziara ya Rais Kenyatta kitakuwa Paris,   Ufaransa, kuanzia leo Aprili 4 hadi 6 kabla ya kuelekea Berlin, Ujerumani atakakokaa hadi Aprili 8, mwaka huu.

Itakuwa ni mara ya kwanza katika  miaka 17 kwa Rais wa Kenya kuitembelea Ujerumani.

Mara ya mwisho, ziara ya aina hiyo ilifanywa na Rais Daniel arap Moi mwaka 1999 huku Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, akiitembelea Kenya mwaka 2011.

Ziara nchini Ufaransa kwa mujibu wa Ikulu ya Kenya, imeandaliwa na wizara ya mambo ya nje kwa mwaliko wa Rais François Hollande.

Ziara ya Ufaransa inatarajia kuipa Kenya fursa ya kuzungumzia suala la ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda, ikilenga kuiomba serikali ya nchi hiyo kutia mkono wake  kufanikisha azma yake ya ujenzi wa bomba hilo. Kenye inahesabu imeporwa na Tanzania mradi huo.

Kampuni ya Total ya Ufaransa ni mwanahisa mkubwa wa uwekezaji wa mafuta  Uganda na inaaminika ndiyo iko nyuma ya uamuzi wa hivi karibuni wa Uganda kuachana na mpango wa ujenzi wa bomba hilo kutoka njia ya Hoima- Lokichar- Lamu  ya  Kenya na badala yake kulijenga hadi katika bandari ya Tanga,   Tanzania.

Tofauti na washirika wengine wa uwekezaji huo kutoka Uingereza na China, Total mara kwa mara imekuwa ikisisitiza ujenzi wa bomba hilo kupitia njia ya Kusini nchini Tanzania kwa kile inachosema unafuu na usalama kulinganisha na Kenya.

Tayari mmoja wa viongozi wake waandamizi amemtembelea Rais John Magufuli Ikulu,  Dar es Salaam na kumhakikishia dhamira ya kampuni hiyo pamoja na kupatikana  kwa fedha za ujenzi huo.

Kampuni hiyo pia imetoa tamko jingine hivi karibuni wakati wa mkutano wa wadau wa nishati Afrika Mashariki uliofanyika Dar es Salaam, ikisema inajua jitihada zinazofanywa na Kenya kutaka bomba hilo lijengwe nchini humo, lakini msimamo wake wa kujengwa Tanzania uko pale pale.

Kwa mujibu wa taarifa za Ikulu, Ufaransa iko katika nafasi ya sita kama mmoja wa wawekezaji wakubwa   Kenya.

Uwekezaji huo unaanzia sekta ya uchukuzi, ufamasia, magari na sekta ya huduma zikiwamo SDV-Transami, AGS, Frasers Schneider, Peugeot, Renault, Michelin na Proparco.

Wawekezaji wengine ni   Total Kenya, Bamburi Cement, Alcatel, na kampuni ya mawasiliano ya Ufaransa Telecom yenye ubia na Telkom Kenya na Orange Mobile.

Kwa mujibu wa mpango wa ziara nzima, Rais Kenyatta akiwa Ujerumani atakuwa na  mkutano na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.

Miongoni mwa masuala ya kujadiliwa nchini humo ni pamoja na biashara, uwekezaji na ushirikiano katika usalama, utamaduni na elimu, utalii, amani katika kanda na migogoro ya Sudan Kusini na Burundi.

Umoja wa Ulaya (EU) Waweka Rehani trilioni 2.182 za Tanzania.......Wabunge wa Uingereza Wataka Serikali Yao Ikate Misaada Tanzania

$
0
0

Siku chache baada ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), kufuta Tanzania kwenye nchi wanachama wake na hivyo kuikosesha serikali msaada wa zaidi ya Sh. trilioni moja kutokana na uchaguzi wa Zanzibar, Umoja wa Ulaya (EU), upo hatarini kutotoa Sh. trilioni 1.56 kwa sababu ya suala hilo huku mmoja wa Waziri wa Uingereza, akiitaka serikali yake isitoe Sh. bilioni 622 za msaada kwa Tanzania.

Kwa mantiki hiyo, Tanzania ipo hatarini kupoteza jumla ya Sh. trilioni 2.182 kutoka EU na Uingereza endapo haitaridhishwa na suala la Zanzibar linavyoendelea.

Tangu Juni, 2014, Tanzania na EU ziliingia makubaliano ya msaada wa Euro milioni 100 (sawa na Sh. bilioni 249), kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kiuchumi na kisiasa.

Kwa mujibu wa ufafanuzi uliotolewa jana  na Mkuu wa Kitengo cha Siasa na Habari, Luana Reale, EU imesikitishwa na namna uchaguzi wa marudio Zanzibar ulivyofanyika Machi 20, mwaka huu, baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.

“Tunarudia wito wetu kwa serikali kuonyesha uongozi na kufanya mazungumzo ya pande zinazovutana katika maoni ya kuhakikisha amani na umoja vinaendelea kuwapo nchini,” alisema.

Alisema Tanzania na EU wako katika makubaliano maalum ya utekelezaji wa miradi kuanzia mwaka 2014 hadi 2020 iliyosainiwa Juni 2014, yenye thamani ya Euro milioni 626 (Sh. trilioni 1.56), ikiwa ni wastani wa Euro milioni 100 (Sh. bilioni 249) kwa mwaka.

Alisema kutoka kwa fedha na utekelezaji wa miradi husika, kunakwenda sambamba na makubalinao maalum ya ushirikiano yaliyojikita katika maendeleo ya kiuchumi na kisiasa.

“Maamuzi juu ya ushirikiano wa maendeleo ikiwa ni pamoja na uamuzi wa mwisho wa kiwango cha fedha yatachukuliwa kwa msingi wa matokeo ya mazungumzo,” alisema.

Hata hivyo, haikueleza moja kwa moja kama wataendelea kuchangia bajeti kuu kama ambavyo wamekuwa wakifanya kila mwaka wa fedha.

Uingereza
Waziri wa zamani wa Ulinzi wanchi hiyo, Dk. Liam Fox, alililiambia Bunge la nchi hiyo liinyime Tanzania Paundi milioni 200 ambazo ilitakiwa kutoa kwa sababu ya sakata la uchaguzi wa Zanzibar.

“Walipa kodi wa nchi za Magharibi wanategemea fedha zao kutumiwa kwa njia za kimaadili..Sasa panapokuwa na ukiukwaji wa wazi wa haki za kisiasa au za binadamu, watategemea majibu kutokana na misaada tunayochangia.

“Ukweli ni kwamba Marekani imechukua hatua imara inatoa ishara nzuri…Tunapaswa kuwa tunafanya mapitio ya mchango wetu katika hali kama hiyo,” alisema.

Uingereza imekuwa ikifikia lengo lake la kutenga asilimia 0.7 ya pato lake kila mwaka, kwa ajili ya msaada kwa nchi za nje kutokea mwaka 2013, baada ya Idara kwa ajili ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), kufikia asilimia 32 kwa mwaka mmoja.

 “Kuna sehemu nyingi duniani ambako tunaweza kuwa tunatumia msaada wetu kikamilifu kupunguza umaskini."

Kwa upande wake, Waziri wa zamani wa Mazingira na Mbunge Mwandamizi kutoka Chama cha Conservative, Owen Paterson, alisema DFID inapaswa kupunguza misaada yake kwa Tanzania, sambamba na uamuzi wa Marekani.

 “Wizara ya Mambo ya Nje inasema uchaguzi si halali na tunaendelea kutumia fedha zetu vilevile, hii haiwezi kuwa sawa,” alisema Paterson.

“Wamarekani wamekiri kuwa njia hii haiwezi kuwa sawa na wamechukua uamuzi na sisi tunapaswa kuchukua uamuzi hapo hapo,” alisema.

Hali Ilivyo
Wiki iliyopita, Wizara ya Fedha na Mipango, ilieleza kuwa wahisani 10 kati ya 14 waliokuwa wanachangia mfuko wa bajeti ya Serikali Kuu wamejitoa na kuweka shakani upatikanaji wa Sh. trilioni 1.37 kwa bajeti ya mwaka huu ambazo zilitarajiwa kutoka kwa wahisani.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Servacius Likwelile, alisema waliobaki ni Benki ya Dunia (WB), Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Dernmark na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB).

Wahisani wengine wa bajeti ya Tanzania ni Uingereza, Canada, Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Norway na Sweden. 
 
Dk. Likwelile alieleza kuwa kujitoa kwa wahisani hao kunatokana na changamoto zilizopo katika nchi zao na kwamba mchango wa wahisani katika bajeti ya mwaka 2014/15, ilikuwa trilioni moja, katika bajeti iliyofuata ilishuka hadi Sh. bilioni 800

Chanzo:Nipashe

Rais Magufuli Aagana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Amolo Odinga

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Amolo Odinga amerejea nchini Kenya baada ya kumaliza mapumziko yake ya siku tatu huko Lubambangwe katika Kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita, alikomtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyepo mapumzikoni.

Akizungumza katika uwanja wa michezo wa shule ya Sekondari ya Chato kabla ya kuruka kwa Helkopta, Mheshimiwa Odinga amemshukuru rafiki yake Rais Magufuli kwa kumpokea na pia amewashukuru wananchi wa Chato kwa ukarimu wao kwa wageni.

Mheshimiwa Odinga pia amesema ana imani kuwa Rais Magufuli ataisaidia Tanzania kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo umasikini unawakabili wananchi wake.

"Lakini mimi najua yeye mwenyewe ana maono, anaona mbele na anajua yale ambayo yanatakiwa yafanyike ili Tanzania iinuke, itoke katika hali ya ufukara na kuwa katika hali ya maendeleo zaidi" Amesema Mheshimiwa Odinga.

Mheshimiwa Raila Amolo Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga waliwasili Chato tarehe 02 April, 2016 kwa mapumziko na kuisalimia familia ya Rais Magufuli ambayo ni familia rafiki.

Katika Hatua nyingine Rais Magufuli ameahidi kutoa madawati na vitabu kwa wanafunzi wa shule tatu za Msingi zilizopo Chato, ambao walijitokeza katika uwanja wa Sekondari wa Chato, wakati Rais Magufuli akimuaga mgeni wake Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga.

Shule hizo ni Chato, Kalema na Kitela.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
04 April, 2016

Mbatia Athibitishwa Na Mahakama Kuwa Mbunge Halali Wa Jimbo La Vunjo Baada ya Mrema Kuifuta Kesi

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mh.James Mbatia pichani kati,amethibitishwa na mahakama kuu kuwa mbunge halali wa  Jimbo hilo baada ya Augustino Lyatonga Mrema  kuifuta kesi hiyo

 Kesi hiyo ya uchaguzi katika jimbo la Vunjo ilifunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo, Augustino Lyatonga Mrema.

Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein Kuhutubia Baraza la Wawakilishi Kesho na Kutoa Mwelekeo wa Serikali Yake

$
0
0

Rais wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ) Dk Ali Mohamed Shein kesho atazindua Baraza la Wawakilishi la tisa huku akitarajia kutoa mwelekeo wa Serikali yake mpya iliyopatikana baada ya Uchaguzi wa Marudio wa Machi 20 uliotawaliwa na mgawanyiko wa kisiasa.

Tofauti na hotuba yake ya ufunguzi ya Novemba 2010, Dk Shein atahutubia baraza hilo likiwa na wabunge wa chama kimoja cha CCM baada ya vyama vya upinzani vilivyotangaza kushiriki uchaguzi wa marudio kushindwa kupata viti vya uwakilishi.

Pia, atahutubia akiwa bado hajamteua Makamu wa Kwanza wa Rais kutokana na matokeo ya uchaguzi huo kutofanikisha kupatikana chama cha upinzani chenye kura zisizopungua asilimia 10 za kufanikisha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Chama kikuu cha upinzani cha CUF na vingine tisa vilisusia kushiriki uchaguzi huo baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kutokana na sababu za uvunjifu wa taratibu na sheria za uchaguzi.

Hata hivyo, majina ya wagombea wa vyama hivyo yalijumuishwa kwenye karatasi za kura na kusababisha kuvuna kura kidogo ambazo hazikitosha kutoa Makamu wa Kwanza wa Rais na Wawakilishi ambao miongoni mwao huteuliwa kuwa mawaziri wa SMZ.

Tayari Dk Shein alishaeleza kiufupi baada ya kuapishwa majuma mawili yaliyopita kuwa Serikali yake itakuwa shirikishi kwa kujumuisha upinzani na haitabagua katika utoaji wa huduma za jamii katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Jambo kubwa ambalo Wazanzibari wengi wanasubiri kulisikia kutoka kwa kiongozi huyo  ni iwapo ataeleza kinagaubaga namna atakavyokabiliana na mtanzuko wa kikatiba wakati wa uundaji wa SUK.

Halmashauri ya Jiji la Tanga Hatarini kuvunjwa kufuatia Vurugu Kutokea Tena Leo Kati ya Madiwani wa CCM na CUF

$
0
0

Halmashauri ya Jiji la Tanga ipo hatarini kuvunjwa kufuatia madiwani wake kushindwa kuelewana katika kikao kilichositishwa leo na Mkurugenzi mtendaji.

Kikao hicho cha baraza la madiwani wa Halmashairi ya Jiji la Tanga kwa mujibu wa barua za mwaliko walizopewa madiwani hao kilikuwa ni cha mwendelezo wa mkutano wa desemba 19 mwaka jana ambacho pia kilivunjika baada ya kutokea vurugu.

Chanzo cha kuvunjika kikao cha leo ni baada ya diwani wa kata ya Tangasisi (CUF) ambaye pia ni Naibu Meya, Mohamed Haniu kuchukua kipaza sauti na kutangaza kwamba kama wanataka kikao hicho kiendelee ni lazima ufanyike uchaguzi wa Meya.

“Kwenye wito wa barua za kikao hiki hakuna ajenda ya uchaguzi kwa hivyo tukubaliane  kwanza kwamba tunaanza na uchaguzi wa Meya ndipo tuendelee kwa sababu hatuna meya hadi sasa”alisema Haniu.

Tangazo hilo lilisababisha madiwani wa kutoka chama cha wananchi (CUF) kushangilia jambo lililomlazimu Meya wa Jiji, Mohamed Mustapha (Selebosi) kutamka kwamba kikao anakiahirisha.

Tamko la Selebosi lilisababisha madiwani wa CUF kushangilia kwa mara ya pili huku wakiimba nyimbo za kukisifu chama hicho.

Baada ya kuahirishwa kwa kikao hicho,Meya wa Jiji hilo, Mohamed Selebosi, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdullah Lutavi, Mbunge wa Jimbo la Tanga, Mussa Mbarouk na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Dk Wedson Sichalwe waliingia katika ofisi ya Mkurugenzi kufanya kikao chao cha ndani.

Akizungumza na waandishi wa habari,Kaimu Mkurugenzi , Sichalwe alisema ajenda ambazo zilikuwa zijadiliwe ni kuunda kamati za kudumu za halmashauri, kupanga ratiba za vikao vya halmashauri, kupokea taarifa ya utendaji wa halmashauri katika kipindi ambacho madiwani hawakuwepo na kupokea taarifa ya Serikali.

“Kama mlivyoshuhudia kikao kimevunjika,inapotokea vurugu kama vile hakuna sababu ya kuendelea na kikao, sheria inamruhusu  Meya kukivunja” alisema Dk Sichalwe na kusisitiza kuwa taarifa zaidi atatoa baadaye.

Diwani wa Kata ya Duga (CUF), Halid Rashid alisema watakuwa tayari kuendelea na kikao iwapo madiwani wa CCM watakubali uchaguzi wa nafasi ya meya ufanyike upya kwa sababu hawamtambui Mohamed Mustafa kama Meya.

“Ni bora Halmashauri ya jiji ivunjwe kama Serikali inalazimisha tumtambue Selebosi kuwa ni Meya, sisi hatutakubali akae mbele kuongoza kikao aje huku ndiyo kikao kiendelee” alisema Halid.

Mohamed Haniu (CUF) alisema anaamini Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela anaweza kumaliza mgogoro wa nafasi ya Meya wa Tanga kwa kutumia busara ya kuamuru uchaguzi wa meya ufanyike upya.

Diwani wa kata ya Chumbageni (CCM) Saida Gaddafi aliwataka madiwani kutoka chama cha CUF kukubali matokeo yaliyomtangaza Selebosi kuwa Meya kwa sababu hata wao walimkubali Mohamed Haniu kuwa Naibu Meya.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga aliwahimiza madiwani wa Jiji kukubaliana ili vikao vya kupitisha miradi ya maendeleo ya wananchi viweze kuendelea.

Dalili za kutokea vurugu katika kikao hicho zilijitokeza mapema kufuatia jeshi la polisi kumshikilia Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Tanga na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Meya wa jiji la Tanga, Rashid Jumbe asubuhi kabla ya kuanza kikao hicho.

Taarifa za kushikiliwa na jeshi la Polisi diwani huyo zilienea na hata kikao kilipoanza hakuwepo ukumbini ambapo madiwani wenzake walisema alikamatwa kwa madai ya kuratibu shughuli za matangazo kuhusiana na kikao hicho kwa kutumia gari lililopita mitaani.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,Leonard Paul alithibitisha kukamatwa kwa diwani Rashid Jumbe na kwamba alikuwa akituhumiwa kutangaza mitaani kwa kutumia gari kuhusu kikao hicho.

CUF Yatangaza Rasmi kutomtambua Rais Dkt. Shein na Serikali yake.....Tamko lao Liko Hapa

$
0
0
MAAZIMIO YA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA CHAMA KATIKA KIKAO CHAKE CHA TAREHE 2 – 3 APRILI, 2016 KILICHOFANYIKA MAZSONS HOTEL, MJINI ZANZIBAR

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi) limefanya kikao chake cha kawaida kwa siku mbili, tarehe 2 hadi 3 Aprili, 2016 mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama, Mheshimiwa Twaha Taslima.

Ajenda kuu ya kikao hicho ilikuwa ni Hali ya Kisiasa Zanzibar na mwelekeo wa CUF baada ya kufanyika kile kilichoitwa uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016.

Baada ya kupokea na kujadili kwa kina ajenda hiyo, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

1. Linawapongeza wananchi wote wa Zanzibar kwa ujasiri, uzalendo na ari kubwa walioionesha kwa kuitikia kwa kiasi kikubwa wito wa chama chao cha CUF wa kuwataka wasishiriki katika uhuni na ubakaji wa demokrasia uliopewa jina la uchaguzi wa marudio wa tarehe 20 Machi, 2016.

Baraza Kuu la Uongozi limefurahishwa kuona zaidi ya asilimia 80 ya wapiga kura wa Zanzibar hawakujitokeza kushiriki katika uchaguzi huo haramu na batili, na hivyo kuudhihirishia ulimwengu kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina ridhaa ya wapiga kura hao.

2. Linawapongeza waliokuwa wagombea wa CUF kwa nafasi zote za Urais, Uwakilishi na Udiwani kwa kuheshimu maamuzi ya Chama na kutoshiriki uchaguzi haramu na batili wa marudio licha ya njama nyingi zilizokuwa zikifanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake, Jecha Salim Jecha, za kulazimisha ushiriki wao. Msimamo wa wagombea hao umewadhihirishia na kuwathibitishia CCM kwamba tofauti na wao, viongozi wa CUF hawajali nafasi na vyeo binafsi bali wanachotaka ni kuleta mabadiliko ya kweli kwa maslahi ya watu wote wa Zanzibar.

3. Linawapongeza kwa namna ya pekee wagombea Urais, Uwakilishi na Udiwani wa vyama vyengine vya upinzani ambavyo ni UMD, JAHAZI ASILIA, CHAUMMA, UPDP, DP, na ACT-WAZALENDO, na vile vinavyoshirikiana kupitia UKAWA ambavyo ni CHADEMA, NCCR na NLD vilivyoungana na wananchi wa Zanzibar kususia uchaguzi haramu na batili wa marudio na kusimamia maamuzi halali ya wapiga kura waliyoyafanya kupitia uchaguzi mkuu halali wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

4. Linazishukuru na kuzipongeza jumuiya na taasisi zote za kitaifa na kimataifa pamoja na nchi rafiki za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zilikataa kuleta waangalizi wa uchaguzi katika uchaguzi huo haramu na batili na hivyo kuungana na Wazanzibari katika kutetea maamuzi yao halali waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu halali uliokuwa huru na wa haki wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

5. Linavishukuru na kuvipongeza vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi pamoja na waandishi wa habari na wapiga picha kwa jinsi vilivyosaidia kuonesha ulimwengu uchaguzi mkuu uliokuwa halali, huru na wa haki wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na pia kwa jinsi vilivyoanika uchafuzi wa tarehe 20 Machi, 2016 hasa kule kuonesha vituo vya kupigia kura vikiwa havina watu na hivyo kuwasaidia Watanzania na ulimwengu kuujua ukweli ambao CCM na Tume yao ya Uchaguzi walikuwa wakijaribu kuuficha.

6. Linalaani tabia na mwenendo wa uongo, uzushi, na uvunjwaji wa Katiba, Sheria na Maadili wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha, dhidi ya matakwa na maamuzi halali ya Wazanzibari waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu huru na wa haki wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kitendo chake cha kuiingiza Zanzibar katika dimbwi la chuki, uhasama, uvunjifu wa haki za binadamu na udhalilishaji wa raia kwa sababu tu ya kukiridhisha chama chake cha CCM ambacho kimekataliwa na Wazanzibari.

Vitendo vya Jecha Salim Jecha vimeishushia hadhi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na kuichafulia jina Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya jumuiya ya kimataifa na kuonekana haiko tofauti na nchi nyengine za Afrika zisizoheshimu matakwa na maamuzi ya wananchi katika uchaguzi.

7. Linalaani hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli kuleta nguvu kubwa ya vikosi vya ulinzi na usalama kuja kubaka demokrasia Zanzibar. 

Baraza Kuu linalaani vikali nguvu kubwa iliyotumiwa na vyombo vya dola dhidi ya raia wasio na hatia kwa lengo na madhumuni ya kuwatisha na kuwazuia wasitumie haki zao za msingi kama ibada kwa kuwalazimisha kutotoka nje ya nyumba zao kuanzia saa 2 usiku wakati muda huo ni muda wa ibada ya sala kwa Waislamu ambao ni asilimia 99 ya wananchi wote wa Zanzibar. 

Baraza Kuu pia linalaani mwenendo wa viongozi wa juu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa kutumika waziwazi kisiasa kwa kuegemea upande wa CCM na kuwakandimiza viongozi na wanachama wa CUF kinyume na maadili ya kazi zao.

8. Linalaani vitendo vya Serikali kuunda makundi ya kiharamia ambayo yamekuwa yakiwahujumu raia wasio na hatia yakitumia silaha za moto na silaha za kienyeji huku yakitumia gari za Idara Maalum za SMZ. 

Baraza Kuu linalaani Jeshi la Polisi ambalo limekuwa likiyalinda makundi haya na kutochukua hatua zozote dhidi yao licha ya wananchi wanaohujumiwa kutoa taarifa kwa jeshi hilo. 

Badala yake, katika matukio mengi Polisi imewageuzia kibao wananchi waliohujumiwa kwa kuwakamata na kuwaweka ndani. 

Baraza Kuu linawataka Wakuu wa Jeshi la Polisi kujirudi, kutekeleza majukumu yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao na na kufuata maadili yao na kuwacha kujifanya ni Idara ya Polisi ya CCM.

9. Haliyatambui matokeo ya uchaguzi huo haramu na batili, na kwa msingi huo halimtambui Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar, haliwatambui waliotangazwa kuwa Wawakilishi na wala haliwatambui waliotangazwa kuwa Madiwani.

Baraza Kuu linaungana na wananchi wa Zanzibar waliokataa kuwapa uhalali watu hao na kwa hivyo halitoitambua Serikali, Manispaa na Halmashauri za Wilaya zitakazoundwa na watu hao. 

CUF haitoshirikiana na Serikali itakayoundwa kwa sababu ni kinyume na Katiba ya Zanzibar, kinyume na Sheria ya Uchaguzi na haikutokana na ridhaa ya watu. 

Kwa vyovyote vile, Serikali itakayoundwa haitakidhi matakwa ya Katiba ya Zanzibar na hivyo CUF haitoshiriki kwenye uvunjaji wa Katiba ambayo inaeleza kwa uwazi kabisa namna ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

10. Linawataka wananchi wote wa Zanzibar kutumia njia za amani, za kikatiba na kisheria ambazo zimewahi kutumika katika nchi nyingine duniani kuwakataa watawala waovu na wasio na ridhaa ya watu waliojiweka madarakani kwa kutumia nguvu na ubakaji wa demokrasia kwa kutoipa ushirikiano Serikali itakayoundwa na watawala hao.

11. Linaendelea kuutambua uchaguzi mkuu uliokuwa halali, huru, wa haki na uliofanyika katika hali ya amani na utulivu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na pia linayatambua matokeo yake ambayo yalionesha wazi kwamba chaguo la Wazanzibari ni CUF na Maalim Seif Sharif Hamad kuiongoza Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. 

Kitendo cha zaidi ya asilimia 80 ya Wazanzibari kususia uchaguzi haramu na batili wa tarehe 20 Machi, 2016 kimezidi kuyapa nguvu maamuzi yao ya tarehe 25 Oktoba, 2015 mbele ya macho ya Watanzania na dunia.

12. Linaendelea kuwataka Wazanzibari kuwa watulivu na kulinda amani iliyopo na linawahakikishia kwamba CUF inaendelea na juhudi zake za kutafuta haki yao na kusimamia maamuzi yao waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015 kwa njia za amani na za kidemokrasia. Njia hizo za amani zimefanikiwa na kuungwa mkono na jumuiya ya kimataifa ambayo imeanza kuchukua hatua dhidi ya ubakwaji wa demokrasia uliofanyika.

13. Linazishukuru na kuzipongeza nchi washirika wa maendeleo kwa kuchukua maamuzi ya kuzifutia misaada Serikali za kidikteta za CCM ambazo zimebaka demokrasia na kukanyaga haki za wananchi wa Zanzibar.

Baraza Kuu linatoa wito kwa nchi hizo washirika wa maendeleo na jumuiya za kimataifa kuchukua hatua zaidi dhidi ya Serikali za CCM na madikteta wake walioshiriki katika ubakaji wa demokrasia Zanzibar zikiwemo hatua makhsusi dhidi ya watu makhsusi waliohusika na ubakaji huo wa demokrasia na uvunjaji wa haki za binadamu katika kipindi hiki.

MWISHO, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawahakikishia wanachama wake wote na Watanzania kwa ujumla kwamba chama chao kiko imara na hakitoyumba wala kuyumbishwa katika kutetea na kupigania haki zao hadi tutakapofanikisha ujenzi wa taifa imara linalosimamia na kuheshimu utawala wa sheria, haki za binadamu, demokrasia na utu wa watu wote.

Baraza Kuu linawataka viongozi wa Chama wa ngazi zote watekeleze majukumu yao ya kichama katika nafasi zao na pia Wabunge na Wawakilishi waliopewa ridhaa na Wazanzibari tarehe 25 Oktoba, 2015 kuwatumikia wananchi wote katika kutatua matatizo yao kadiri hali na uwezo wao unavyoruhusu. 

Mbali na maazimio haya, Maalim Seif Sharif Hamad atazungumza na wananchi katika siku chache zijazo ili kuwaeleza kwa kina mwelekeo wa hali ya kisiasa ya Zanzibar na hatua zinazochukuliwa na CUF kuhakikisha maamuzi halali ya kidemokrasia ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015 yanaheshimiwa.

HAKI SAWA KWA WOTE

Limetolewa na:

BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA
THE CIVIC UNITEDN FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi)

ZANZIBAR
3 APRILI, 2016

Serikali Yatoa Tamko kuhusu Wahisani Kuendelea kuisaidia Tanzania katika Bajeti Kuu ya 2016/2017

$
0
0

Serikali imetoa tamko kuhusu wahisani kuendelea kuisaidia Tanzania katika bajeti Kuu ya 2016/2017.

Tamko hilo limetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa Washirika wa Maendeleo bado wanaendelea kuisadia Serikali katika bajeti yake na kwamba tuhuma za kujitoa kwa makundi 14 ya kuisaidia bajeti ya Tanzania sio za kweli.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa bado makundi hayo yanaendelea kuisaidia bajeti ya Tanzania ambapo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Washirika wa Maendeleo nane waliahidi kuendelea kusaidia Bajeti Kuu wakiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ireland, Sweden, na Benki ya Dunia.

Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 baadhi ya Washirika wa Maendeleo wameshathibitisha kusaidia bajeti kuu ya Serikali, Washirika hao ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Denmark, Umoja wa Ulaya pamoja na  Benki ya Dunia.

Washirika wengine wa Maendeleo wataendelea kuisaidia Serikali kupitia wa Mfuko wa Pamoja wa Maendeleo na Miradi.

Washirika hao ni pamoja na Ubelgiji, Canada, China, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Hispania, India, Italia, Japan, Korea ya Kusini, Norway, Sweden, Uholanzi, Uingereza,  Marekani na Uswisi.

Washirika wengine wa maendeleo ambao wanaisaidia bajeti ya Serikali ni Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mashirika ya Umoja wa Mataifa, BADEA, Mfuko wa OPEC pamoja na Saudia Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia.

Taarifa hiyo ya Dkt. Likwelile imeongeza kuwa, Serikali ya pamoja na washirika wa maendeleo wanaoisaidia Tanzania wako katika mazungumzo juu ya namna ya kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na nchi hizo.

Serikali imewashukuru Washirika wa Maendeleo kwa kuendelea kuisaidia Tanzania katika kupelekea juhudi za kimaendeleo zenye tija kwa wananchi.

Rais Magufuli Afuta Sherehe za Maadhimisho ya Muungano Mwaka Huu....Aagiza Fedha Zilizokuwa Zimetengwa Zitumike Kupanua Barabara ya Mwanza- Airpot

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha Shamrashamra za maadhimisho ya siku ya Muungano kwa mwaka huu, ambayo huadhimishwa kila tarehe 26 ya Mwezi Aprili, na badala yake ameelekeza kuwa siku hiyo itakuwa ya mapumziko kama kawaida, na watanzania waiadhimishe wakiwa majumbani kwao ama katika shughuli zao binafsi.

Kufuatia kuahirishwa kwa shamrashamra hizo, Rais Magufuli ameelekeza kuwa fedha zilizopangwa kutumika kwa ajili ya kugharamia Vinywaji, Vyakula, Gwaride, Halaiki, Burudani mbalimbali na Hafla ya usiku ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 2, zitumike kuanzisha upanuzi wa barabara ya “Mwanza – Airport” katika eneo linaloanzia Ghana Quaters hadi Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Barabara hiyo inafanyiwa upanuzi ili kukabiliana na kero ya msongamano mkubwa wa magari ambao unaathiri shughuli za kila siku za wananchi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
04 April, 2016

TRA Yavuka Lengo la Makusanyo Kwa Asilimia 101

$
0
0

TAARIFA KWA UMMA-MAKUSANYO MWEZI MACHI 2016

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya na kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato mwezi Machi 2016 kwa asilimia 101. Lengo hilo limevukwa baada ya TRA kukusanya shilingi trilioni 1.31 kati ya lengo la shilingi trilioni 1.30.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo kuhusu mwenendo wa makusanyo ya mapato, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata amesema ongezeko la makusanyo linatokana na jitihada zinazofanyawa na TRA katika kuongeza kasi ya usimamizi wa ufuatiliaji na ukadiriaji wa kodi kwa usahihi.
 
“Tumejitahidi kudhibiti biashara za magendo katika maeneo ya Ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi, mipakani na maziwa yote," Alisema Kamishna Mkuu.

Amesema hadi kufikia Machi 2016, tayari TRA imekusanya shilingi Trilioni 9.89 sawa na asilimia 99 ya lengo la makusanyo ya shilingi trilioni 9.99 mwaka wa fedha 2015/2016. 

Bw. Alphayo amewasisitiza wafanyabiashara ambao hawajasajili biashara zao kufanya hivyo mara moja kupitia ofisi za TRA zilizoko katika maeneo ya biashara zao na kwa wale wanaoshiriki vitendo vya uingizaji bidhaa za magendo nchini amemewata kuacha mara moja kwani vinaipotezea serikali mapato.

 “Wakikamatwa katika msako unaoendelea watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutaifisha bidhaa hizo, kutozwa faini pamoja na kifungo”, amesisitiza.

Kwa Wafanyabiashara ambao wanastahili kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) Kamishna Mkuu amewataka kujisajili katika ofisi yoyote ya TRA na wahakikishe wanataarifa muhimu ikiwemo anuani inayotambulika na namba simu zinazofanya kazi. 

“Natoa wito kwa wafanyabiashara wote waliosajiliwa na VAT lakini hawatumii mashine za kielektroniki za kodi (EFDs) watumie mashine hizo kwa mujibu wa sheria. Wakibainika hawazitumii watachukuliwa hatua za kisheria kwani zoezi la ukaguzi wa biashara linaendelea mtaa kwa mtaa katika mikoa yote. 

"Aidha wananchi wanakumbushwa kudai risiti za kodi kwa thamani halisi ya manunuzi kila wanapofanya manunuzi au kupata huduma”, alisema Kamishna Mkuu na kuongeza kuwa wananchi wema na wazalendo wenye taarifa za ukwepaji wa kodi wazifikishe TRA kwa usiri. 

TRA inawaahidi donge nono ikiwa ni pamoja na kutunza siri za taarifa hizo. Vilevile wanapoadaiwa rushwa au kutendewa isivyo wasisite kutoa taarifa mara moja.

Imetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA- Makao makuu

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanziba Chafurahishwa na Taarifa ya Serikali ya China Kwamba Uchaguzi Ulikuwa Huru na Hawatakata Misaada

$
0
0

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimefurahishwa na kimepata matumaini  makubwa kutokana na taarifa ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ambayo imeelezea dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na Tanzania na Zanzibar katika jitihada zake za kuimarisha uchumi na ustawi wa jamii.

Kauli hiyo ya Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa mara nyengine tena inathibitisha imani ya kweli ya nchi hiyo katika kuendeleza ushirikiano wa kindugu baina ya nchi zetu mbili ambao umedumu kwa zaidi ya nusu karne sasa.

CCM inayo kila sababu ya kuthamini  uhusiano wetu na ndugu zetu wa China siyo tu kwa sababu ya misaada ya nchi hiyo ya kiuchumi na kijamii ambayo imekuwa ikitoa msukumo mkubwa katika maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla, lakini pia kutokana na dhamiri ya kweli ya nchi hiyo katika kusaidia maendeleo ya wananchi wetu na taifa wakati wa dhiki na vile vile wakati wa faraja. Huu ndio urafiki wa kweli.

Zanzibar bado inakumbuka ya msaada mkubwa wa nchi hiyo, iliyowahi kutolewa katika kujenga na kuviendeleza viwanda mbali mbali ikiwemo kiwanda cha sukari na manukato cha Mahonda, kiwanda cha ngozi na viatu kilichokuwepo Maruhubi, usambazaji wa mabomba ya maji safi na salama katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba, uimarishaji wa kilimo Upenja, Bambi na maeneo mengine mengi.

Jamhuri ya Watu wa China kwa karibu miaka 50 sasa imekuwa ikituma madaktari wake kuja Zanzibar kusaidia huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi mbali mbali katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja na Abdalla Mzee iliyoko Pemba. Huduma za madaktari hao kwa kushirikiana na madaktari wazalendo zimekuwa zikisaidia kuimarisha afya na kuokoa maisha ya wananchi kadhaa hapa nchini.

Mradi wa ujenzi wa hospitali kubwa ya kisasa ya Abdalla Mzee huko Mkoa wa Kusini Pemba unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China pia unathibitisha dhamira ya nchi hiyo katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuimarisha sekta ya jamii. Ni dhahiri mradi huu baada ya kukamilika utaleta sura mpya kwa Pemba.

Ujenzi wa  Uwanja wa Kisasa wa Michezo  wa Amani pamoja na marekebisho yake yaliyofanywa katika miaka ya hivi karibuni pamoja na maandalizi ya Ujenzi wa kiwanja cha mpira wa miguu cha Mao Tse-tung, kiliopo Mjini Zanzibar ni miongoni mwa misaada ya China.

Vituo vya kurushia matangazo ya Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) vya Radio iliyopo maeneo ya Rahaleo na Dole vimejenga kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. 

Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, kwa muda wote zimekuwa zikifaidika kwa kupatiwa nafasi za masomo kwa vijana wake ya taaluma tofauti nchini China ya muda mfupi na mrefu.

Kutokana na dhamira yake hiyo, Chama cha Mapinduzi siku zote kimekuwa kikijivunia ushirikiano wake na Chama cha Kikomunisti cha China (CCP) na kitaendelea kufanya hivyo daima kwa maslahi ya pande zote mbili, kwa kufahamu kwamba itikadi na msimamo thabiti wa CCP mbele ya mataifa mengine duniani, ndio uliyoifanya China leo kuwa moja kati ya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi duniani.

Uhusiano wetu na China ambao uliasisiwa mara baada ya uhuru wa Tanganyika kwa Tanzania Bara na Mapinduzi ya tarehe 12 Januari 1964 kwa Zanzibar, umejengwa kwa misingi ya haki, usawa, kuheshimiana pamoja na kuzingatia na kujali maslahi ya kila upande.

Aidha, Chama Cha Mapinduzi kinatoa pongezi za dhati kwa nchi mbali mbali duniani zinaoungana na Zanzibar na Tanzania kwa kuendelea kuimarisha umoja na uhusiano mwema kwa maslahi ya wananchi walio wengi wa pande zote mbili za nchi hizo.

………………

VUAI ALI VUAI
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR
APRILI 4, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya April 5

Kamati ya Bunge Yaingilia kati Madaktari kutumbuliwa Majipu

$
0
0

Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imelaani wanasiasa wanaoingilia utendaji katika Sekta ya Afya kwa kutoa adhabu kwa madaktari na wauguzi, bila kushirikisha vyombo vyao.

Wakizungumza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jana, wajumbe hao waliitaka Serikali kuepuka unyanyasaji dhidi ya madaktari na wauguzi ili kurudisha amani iliyokuwapo katika sekta hiyo.

Kamati hiyo ilimbana kwa maswali Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamis Kigwangalla ambaye alijitetea hajahusika kusimamisha madaktari na wauguzi tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Serukamba alipongeza hatua ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuingilia kati suala hilo kwa kutoa tamko la Serikali.

Alisema analaani pia Watanzania wote ambao wanachukua sheria mkononi na kuwaadhibu madaktari, akisema tabia hiyo haifai kuvumiliwa.

“Madaktari na wauguzi wana chombo chao. Kama wamekosea tuwapeleke kwenye vyombo vyao watapewa onyo au kuchukuliwa hatua za kinidhamu, jamani tuache siasa kwenye Sekta ya Afya,” alisema Serukamba.

Alisema watoa huduma ya afya wana umuhimu mkubwa katika jamii, lakini siku za hivi karibuni wameonekana kunyooshewa vidole kwa kila jambo wanalolifanya na kuifanya sekta hiyo yenye watumishi wachache kukosa molari.

Akijibu hoja hiyo, Dk Kigwangalla alisema katika kulinda hadhi ya madaktari suala la wananchi kujichukulia sheria mikononi limeikera sana Wizara ya Afya.

Alisema wananchi wamepewa fursa ya kutoa maoni yao katika kila hospitali na kituo cha huduma za afya, hivyo wanapaswa kutoa malalamiko yao na kama watahitaji usiri wafunge katika bahasha maalumu.

“Nitumie nafasi hii kuwataka wananchi wafuate taratibu kadri zilivyowekwa kwa mujibu wa sheria kufikisha malalamiko yao,” alisema Dk Kigwangalla.

Kamati hiyo ilihoji sababu za jengo la Taasisi ya Mifupa (MOI) kuanza kutumika kabla ya ujenzi kukamilika.

Dk Kigwangalla, baada ya kubanwa na kamati hiyo iliyosema kuna mgogoro kati ya mkandarasi anayejenga na taasisi hiyo, aliuagiza uongozi wa MOI kumpa taarifa sahihi kuhusu mkandarasi huyo.

Tamko la Serikali kuhusu kutatua Kero na Changamoto za Sekta ya Usafirishaji Barabarani Ikiwemo Kuyaondoa Matuta Yote Barabarani

$
0
0

1.0Mnamo tarehe 09/4/2015 ulifanyika mgomo wa madereva nchini uliohusu malalamiko na kero  mbalimbali  za  madereva.    

    Katika kuzipatia ufumbuzi kero hizi,  tarehe 02/5/2015 aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Kayanza Pinda,  aliunda Kamati ya Kudumu ya Kutatua Kero na Changamoto mbalimbali katika Sekta ya Usafirishaji. 
    Kamati hiyo inaundwa na Wajumbe kutoka  Serikalini, Umoja wa  Madereva na  Vyama vya Madereva, Vyama vya Watumiaji wa Huduma za Usafiri, pamoja na Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji. Kutokana na  vikao vilivyofanywa na  Kamati hiyo kero na changamoto mbalimbali zilibainishwa na kufanyiwa kazi. Baadhi zimefanyiwa kazi na kukamilishwa; nyingine zinaendelea kufanyiwa kazi ili kukamilishwa na nyingine zitaendela kufanyiwa kazi kwa kuwa ni masuala endelevu.
2.0      Kwa kipindi chote cha utekelezaji wa hatua za kutatua kero na changamoto hizo, kumekuwa na utoaji wa taarifa mbalimbali miongoni mwa wadau kuhusu utendaji na hatua zinazochukuliwa na Kamati. Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kinyume na mamlaka na taratibu zilizokubaliwa na Kamati na zimekuwa zikipotosha umma juu ya usahihi wa hatua na hali halisi ilivyo. 
   Utaratibu huo umekuwa ukisababisha madhara mbalimbali ikiwemo matishio ya migomo miongoni mwa madereva, taharuki miongoni mwa watumiaji huduma na hasara mbalimbali kwa kutokuwepo kwa uhakika wa huduma kwa siku husika. 
 
3.0      Tarehe 01 Aprili, 2016 Kamati ilifanya kikao kilichowajumuisha Mhe. Jenista Mhagama (MB), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu; Mhe. Harrison Mwakyembe (MB), Waziri wa Katiba na Sheria; Mhe. Mhandisi Edwin A. Ngonyani (MB), Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi; Mhe. Anthony Peter Mavunde (MB), Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana na Ajira; Mwakilishi wa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Mwakilishi wa Waziri, Wizara ya Mambo ya Ndani.
   Katika kikao hicho, iliazimiwa kuwa Kamati, kwa kushirikisha wawakilishi wa pande zote, itoe taarifa kwa umma juu ya hatua zilizochukuliwa na mwelekeo uliopo.
 
4.0       Hivyo, Kamati inapenda kutoa taarifa kwa  wadau wote wa sekta ya usafirishaji  na wananchi kwa ujumla kwamba, kufuatia hoja za vikao mbalimbali vya Kamati  ya Kudumu na Kamati Ndogo  vilivyofanyika kati tarehe 12/5/2015 na 01/04/2016, hatua zifuatazo zimechukuliwa:
4.1       Kuhusu kuendelea kutumia mizani ya Kibaha ili kupunguza muda unaotumiwa na mabasi katika mizani ya Vigwaza; Serikali ilifunga Mzani wa Kibaha kutokana na sababu za msingi. Hatua za kuimarisha huduma na kuondoa tatizo la msongamano kwenye mzani wa Vigwaza zimechukuliwa. Hivyo, hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.2       Kuhusu kushughulikia malalamiko ya wadau juu ya matuta ya barabarani; Serikali imeanza taratibu za kuyaboresha matuta ili yasilete madhara na inaangalia uwezekano wa kuyaondoa matuta yote katika barabara kuu na kuweka alama za vivuko (Zebra) kama inavyoelekezwa na Sheria. Utekelezaji unaendelea na hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.3       Kuhusu kutoa elimu juu ya matumizi ya mizani inayowezesha gari kupimwa katika mwendo; Hoja imezingatiwa; elimu imeshaanza na inaendelea kutolewa kwa njia mbalimbali za mawasiliano kwa umma, ikiwamo mabango yaliyopo eneo la Vigwaza, vipeperushi kwa Madereva, vipindi vya TV na Redio. Hivyo, hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.4       Kuhusu kuanzisha utaratibu wa kupima magari bila gharama katika eneo la bandarini kabla ya safari ili kuwawezesha wasafirishaji kuzingatia Sheria kwa kutozidisha uzito; Fedha kwa ajili ya kazi hii zimetengwa katika Mwaka wa Fedha 2015/16, Usanifu umekamilika na taratibu za kumpata mkandarasi wa ujenzi zinaendelea. Hivyo, hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.5       Kuhusu kutoa taarifa ya maandishi kwa umma kuhusu maamuzi ya kutohitaji vibali kwa ajili ya kuondoa magari mabovu na yaliyopata ajali njiani; Maelekezo yametolewa kwa TANROADS ili vibali visihitajike wakati wa hali ya dharura. Iwapo ajali imetokea au gari limeharibika na kufunga barabara, magari husika yaondolewe na kuyaweka mahali ambapo hayataleta usumbufu kwa watumiaji wengine. Hatua baada ya hapo ni lazima zizingatie taratibu na matakwa ya Sheria. Upatikanaji wa vibali hivyo utarahisishwa zaidi baada ya kuzindua utaratibu wa kupata vibali kwa mtandao (e-permit). Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wameagizwa kuleta taarifa ya utekelezaji katika kikao kijacho.
 
4.6       Kuhusu kufanya ukaguzi wa barabara ili kubaini ubovu na mahitaji ya alama katika maeneo mbalimbali na kuyafanyia kazi; Hoja imezingatiwa na kutekelezwa. Ukaguzi unaendelea kufanyika na alama za barabarani zinawekwa sehemu stahili. Hivyo, kwa kuwa utekelezaji wa hoja hii ni endelevu, Kamati imeagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi iendelee kutoa taarifa katika kila kikao, kuhusu maeneo yaliyokarabatiwa na yaliyobaki.
 
4.7       Kuhusu wadau kutoa taarifa kuhusu maeneo yanayopaswa kuwa na alama za barabarani; Wadau wamewasilisha taarifa kuhusu mahitaji ya alama za barabarani zinazostahili kwenye maeneo ya Mlima Sekenke, Iguguno Shamba na Mkoa wote wa Singida; na pia kona zote za Iyovi mkoani Morogoro.
 
Utafiti umefanywa na Wizara ya Ujenzi na kubaini kwamba, jumla ya alama 156 za barabarani zinahitajika kwa mkoa wa Singida. Kwa awamu ya kwanza jumla ya alama 80 zimewekwa kwenye maeneo husika. Utekelezaji unaendelea na Wizara hiyo imeelekezwa kutoa taarifa ya maendeleo katika vikao vijavyo.
 
4.8       Kuhusu kukamilisha ubadilishaji wa aina ya malighafi (materials) itumikayo katika kutengeneza alama za barabarani ili kuzuia kuibiwa kwa alama hizo kwa ajili ya chuma chakavu; Hatua za kubadilisha mali ghafi na kuweka alama za zege kulingana na mahitaji ya eneo husika unaendelea. Hatua za utekelezaji wa zoezi hili zimeanza na pia ni endelevu.
 
4.9       Kuhusu kufanya marejeo (review) ya Sheria na Kanuni ili malipo katika mizani yafanywe pia kwa fedha za Kitanzania; Kamati imeagiza TANROADS kwamba, kwa kuwa ukarabati wa barabara zinazoharibiwa kwa kuzidisha uzito hufanyika kwa dola, malipo ya faini yaendelee kufanywa kwa dola kama inavyoelekezwa na Sheria au kwa fedha za kitanzania kwa kuzingatia viwango halisi vya ubadilishaji fedha vinavyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania wakati wa malipo hayo. Hivyo, hoja hii ya kutaka kurekebisha Sheria imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.10    Kuhusu wamiliki wa daladala na Jeshi la Polisi kukutane ili kujadili na kukubaliana utaratibu wa utakaotumika katika kufanya ukaguzi wa kawaida wa daladala na kuteua maeneo maalum kwa ajili ya kaguzi hizo; Kikao kati ya Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani na Wamiliki wa Daladala na kuwashirikisha pia madereva, kilifanyika tarehe 05/06/2015. Utaratibu umekubalika na maeneo ya kufanyia kaguzi yamebainishwa. Hoja imefungwa, lakini Jeshi la Polisi limeagizwa kuendelea kushirikisha wadau mara kwa mara na kuwasilisha taarifa katika kikao kijacho juu ya utekelezaji wa zoezi la ukaguzi kama ilivyokubaliwa.
 
4.11    Kuhusu kuimarisha usimamizi wa Sheria na matumizi ya ratiba na batli; Maelekezo yametolewa kwa Wakuu wa Usalama Barabarani wa Mikoa (RTO’s) na usimamizi umeimarishwa. Hatua za utekelezaji zinaendelea na hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.12    Kuhusu kutoa elimu kwa umma kuhusu utoaji wa taarifa za vitendo vya rushwa vinavyohusisha askari wa usalama barabarani; Elimu juu ya kutoa taarifa za rushwa inaendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari kama Redio na Televisheni. Vipeperushi kuhusu rushwa vimeandaliwa na kusambazwa. Uelimishaji umma unaendelea kwa kutumia njia mbalimbali za mawasiliano kwa umma. Hatua za utekelezaji ni endelevu na Jeshi la Polisi limeagizwa kuendelea kushirikisha wadau ili kuweka mikakati ya kupata taarifa za vitendo vya rushwa.
 
4.13    Kuhusu kufuatilia kukamilishwa kwa Kanuni zitakazo wezesha malipo ya faini kufanywa kwa njia ya mtandao; Kanuni zimekamilishwa na Mfumo umeanza kutumika kwa majaribio katika mkoa wa Dar es salaam. Hatua za utekelezaji zitaendelea kwa mikoa yote. Jeshi la Polisi limeagizwa kufanya vikao vya ushirikishaji wadau mara kwa mara. Hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.14Kuhusu kuainisha masuala yatakayozingatiwa katika ziara ya mafunzo kwa wajumbe wa Kamati katika nchi jirani; Rasimu ya masuala ya kuzingatiwa bado inafanyiwa kazi. Kamati imeagiza Sekretarieti ifuatilie maoni kutoka TATOA na kushirikisha Vyama vingine vya wamiliki. Hatua za utekelezaji ni endelevu.
 
4.15    Kuhusu kushirikiana na Halmashauri ili kuteua vituo kwa ajili ya pikipiki hasa katika mkoa wa Kigoma; SUMATRA imeanza utekelezaji kwa kutuma mtaalam mkoani Kigoma kwa ajili ya kusimamia zoezi la kuainisha vituo vya pikipiki na bajaji katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji. Hatua za utekelezaji ni endelevu. Kamati imeagiza utekelezaji uendelee na hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.16    Kuhusu kufuatilia kukamilishwa kwa Kanuni zinazotenganisha makosa ya madereva na wamiliki zilizowasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Ufuatiliaji umefanywa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Rasimu ya Kanuni hizo imeboreshwa na kuwasilishwa tena kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua za mwisho kabla ya kutolewa na kuanza kutumika. Kamati imeagiza Kanuni hizo kukamiliswa haraka, taarifa itolewe na mawasilisho yafanywe katika kikao kijacho. Hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.17    Kuhusu kufanya utafiti wa mahitaji ya huduma za usafirishaji katika njia kuu; Utafiti umefanywa kwa kushirikisha Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) katika njia za Dar-Mbeya, Dar-Mwanza na Dar-Arusha; na taarifa inakamilishwa. Kamati imeagiza SUMATRA kuwasilisha taarifa ya matokeo ya utafiti katika kikao kijacho. Hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.18    Kuhusu kufanya utafiti wa mahitaji ya huduma za usafirishaji katika njia zinazohudumiwa na Daladala katika Jiji la Dar es Salaam; Utafiti utafanywa katika robo ya mwisho wa mwaka wa fedha wa 2015/2016. Hatua za utekelezaji zinaendelea na hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.19    Kuhusu kutoa leseni za usafirishaji kwa maombi mapya kwa ratiba za magari ya kuanzia saa 1.30 asubuhi na kuendelea; Utekelezaji umeanza kwa magari ya abiria yanayoomba leseni kwa mara ya kwanza. Hatua za utekelezaji wa zoezi hili ni endelevu. Kamati imeagiza wadau kuwasilisha hoja mpya katika kikao kijacho, kama zipo, kuhusiana na suala hili. Hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.20    Kuhusu kuwasilisha mapendekezo kwa mwakilishi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji juu ya sekta zinazoweza kuendeshwa na wazawa kwa ufanisi ili kuzingatiwa katika mchakato wa kutengeneza Sera ya usafirishaji kwa ajili ya wawekezaji wa ndani (Local Content Policy); Serikali imeanza kulifanyia kazi suala hili kwa pamoja na sekta nyinginezo chini ya uratibu wa OWM-Uwezeshaji. Hatua za utekelezaji ni endelevu. 
 
4.21    Kuhusu kufuatilia matumizi ya pikipiki, bajaji na magari aina ya Probox (michomoko) katika Mikoa ya Iringa na Kigoma; Ufuatiliaji umefanywa na SUMATRA. Vikao vya mashauriano na wadau vinaendelea. Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi imetoa maelekezo juu ya utatuzi wa suala hili. Kamati imeagiza SUMATRA kutoa taarifa kwa umma juu ya hatua zake na kutoa mrejesho katika kikao kijacho juu ya utekelezaji wa maelekezo ya Wizara. Hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.22    Kuhusu kuanzishwa kwa jukwaa (forum) la wadau wa usafirishaji kwa barabara; SUMATRA inaandaa mpango wa namna ya kuanzisha jukwaa hili katika robo ya mwisho ya mwaka wa fedha 2015/2016. Hatua za utekelezaji zimeanza na zinaendelea.
 
4.23    Kuhusu wadau kushirikishwa katika kuelewa utaratibu wa ukokotoaji nauli kwa mujibu wa Kanuni; Wadau wameshirikishwa katika utafiti wa hali ya mahitaji ya huduma za usafirishaji (occupancy ratio) katika njia kuu za mabasi ya mikoani ambao upo katika hatua za mwisho za kukamilishwa taarifa. Ushirikishwaji zaidi utafanyika kupitia mafunzo ya ukokotoaji yatakayofanyika ndani ya Robo ya Mwisho wa Mwaka wa fedha 2015/2016. Hatua za utekelezaji zitaendelea kwa daladala. 
 
4.24    Kuhusu kuharakisha ununuzi wa mitambo ya TBS ya ukaguzi wa ubora wa matairi na vipuri; Utaratibu wa ununuzi wa mitambo unaendelea na bajeti imetengwa kwa mwaka 2015/2016. Hatua za utekelezaji zimeanza na zinaendelea.
 
4.25    Kuhusu kutoa elimu kwa umma juu ya utambuzi wa bidhaa zisizo na ubora na hatua za kuchukua, hususani kuhusu matairi ya magari na vipuri; TBS imekuwa ikitoa elimu kwa njia mbalimbali za mawasiliano kwa umma. Hatua za utekelezaji zimeanza na zoezi hili ni endelevu. Kamati imeagiza Mkurugenzi wa TBS awasilishe taarifa katika kikao kijacho juu ya hatua na mikakati ya ukaguzi hapa nchini na katika nchi ambazo TBS haina vituo/wakala wake wa ukaguzi na namna ya kuzuia Tanzania kuwa dampo la bidhaa zisizo na viwango.
 
4.26    Kuhusu kushirikisha sekta binafsi ikiwemo TATOA ili kuwekeza katika vifaa vya ukaguzi wa ubora wa matairi na vipuri; Jukumu la ukaguzi wa viwango vya ubora wakati wa uingizaji bidhaa ni la serikali kupitia TBS. Hata hivyo, watumiaji binafsi hawakatazwi kuwekeza katika kufanya uhakiki wa bidhaa zao baada ya uingizaji huo. Hatua za utekelezaji ni endelevu.
 
4.27    Kuhusu agizo la Kamati kuwa tarehe 20 Agosti 2015, Kamati itembelee mizani ya Vigwaza ili kupata hali halisi ya kero zinazolalamikiwa na madereva na kuona namna ya kuzishughulikia; Kamati ilitembelea Mizani ya Vigwaza tarehe 20/08/2015 kama ilivyoagizwa na mapendekezo ya maboresho yalitolewa kupitia vikao vya Kamati. Uboreshaji umefanywa na hali ya huduma za mzani huo inaridhisha. Agizo limetekelezwa na kukamilika; na hivyo hoja inafungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.28    Kuhusu Sekretariati kutuma taarifa za mialiko ya vikao na kusambaza Muhtasari mapema ili wajumbe waweze kujiandaa na vikao vijavyo; Maagizo yamezingatiwa na kutekelezwa, kulingana na hali halisi inayojitokeza. Usimamizi wa suala hili utaimarishwa. Hoja imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
4.29    Kuhusu Mamlaka husika (EWURA na WMA) kuwasilisha Mada kuhusu changamoto na taratibu za upakiaji, usafirishaji na upakuaji wa mafuta; Mada ziliwasilishwa na maelezo ya kitaalam kutolewa na wawakilishi wa EWURA, WMA na kampuni ya PUMA katika kikao cha Kamati cha tarehe 11 Machi, 2016. 
     
     Kamati imeagiza EWURA na WMA zifanye utafiti na kutoa taarifa ndani ya siku 60 kuhusu kasoro (shoti) zinazolalamikiwa na wadau, hususani nchini Zambia. Wizara husika ziwasilishe taarifa katika kikao kijacho.
4.30Kuhusu Serikali kutoa ufafanuzi juu ya matumizi ya Mfumo wa Kukata Nukta katika Leseni za Udereva; Ufafanuzi ni kwamba Mfumo wa ukataji nukta katika leseni za udereva bado haujaanza kutumika. Pindi ukiwa tayari taarifa itatolewa kwa umma. 
     Mfumo huo utatumika kwa kila mtu anayeendesha gari kwa sekta zote, ikijumuisha madereva wa magari binafsi. Hivyo, wadau wameombwa kupata uelewa sahihi kupitia ufafanuzi unaotolewa na Jeshi la Polisi mara kwa mara kupitia vyombo vya habari, badala ya taarifa potofu zinazozagaa mitaani. Hatua za utekelezaji wa hoja hii ni endelevu.
 
4.31    Kuhusu kukamilisha marekebisho na kuwasilisha mkataba wa ajira ya madereva ulioboreshwa katika vikao vya Kamati; Mkataba ulioboreshwa umekamilishwa na kuanza kutumika tarehe 01 Julai, 2015. Wadau walipatiwa nakala ya mikataba na vitambulisho ili waanze kutumia katika sehemu zao za kazi. 
     Ukaguzi ulibaini jumla ya mikataba 11, 133 ilitolewa kwa madereva hadi kufikia Desemba, 2015. Hata hivyo, zoezi la ukaguzi wa mikataba lilisitishwa kwa maombi ya wawakilishi wa wafanyakazi kwamba, lisubiri kukamilika kwa majadiliano na muafaka wa viwango vya posho ili vijumuishwe kwenye mikataba hiyo. 
     Hata hivyo, kwa sasa ukaguzi utaendelea kwa mujibu wa Sheria baada ya wadau kuafikiana hivyo. Utekelezaji wa hoja umekamilishwa na imeondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.31.1  Kuhusu Serikali kutoa tamko la kuweka viwango vya posho kwa madereva; Vikao vya majadiliano ya wadau yamekamilishwa na kuafikiwa kwamba majadiliano juu ya suala la posho kwa madereva yafanywe kwa mujibu wa Sheria.Hivyo, Kamati imeagiza Vyama vya Wafanyakazi vitekeleze wajibu wake kisheria kwa kufanya majadiliano na Vyama vya Waajiri au Mwajiri mmoja mmoja katika maeneo yao ya kazi.
 
Kufanikisha majadiliano hayo, Vyama vya Wafanyakazi ni lazima viandikishe wanachama kwa asilimia zaidi ya hamsini ya wafanyakazi waliopo sehemu ya kazi ili vipate uhalali wa kuwawakilisha katika majadiliano na mwajiri husika. Wafanyakazi nao wajiunge na Vyama kwa mujibu wa Sheria za Kazi na kuzingatia taratibu za kisheria ili waweze kudai haki, kufanya majadiliano na kupata haki ya kushiriki migomo kwa utaratibu halali iwapo hakutakuwa na muafaka.
 
Kwa upande mwingine, Waajiri wameagizwa pia kuzingatia Sheria kwa kuruhusu Vyama vya Wafanyakazi kufanya shughuli zao katika maeneo yao ya kazi na kufanya majadiliano kisheria ili kudumisha mahusiano mema baina yao, kukuza tija na ufanisi.
 
Kamati imeagiza Idara ya Kazi na SUMATRA kuimarisha kaguzi katika kampuni za usafirishaji na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote atakayekiuka taratibu zilizowekwa juu ya masuala haya; ikiwemo kuchukua hatua dhidi ya waajiri wasiolipa mishahara wafanyakazi wao au wanaolipa chini ya kima cha chini cha kisheria, kuwashtaki wanaoghushi mikataba na kufuta leseni kwa wanaokiuka masharti ya leseni hizo. 
 
Kamati imeagiza pia, Vyama vya Wafanyakazi viwasilishe mbele ya Kamati, orodha ya wamiliki na madereva wanaokiuka Sheria ili mamlaka husika ziwachukulie hatua stahiki. Majina hayo yatolewe kwa njia za siri kupitia mawasiliano na Afisa Kazi waliyetambulishwa.
 
Hivyo, hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.32   Kuhusu kuhamasisha madereva kujiunga na Vyama vya Wafanyakazi vilivyopo; Serikali imewezesha kuundwa kwa vyama viwili vya wafanyakazi madereva ambavyo ni Chama cha Wafanyakazi Madereva wa Malori Tanzania (CHAWAMATA) kilichosajiliwa tarehe 28/5/2015 na Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU) kilichosajiliwa tarehe 25/6/2015.  Uwepo wa Vyama hivyo, pamoja na vile vilivyokuwepo awali, vya TAROTWU na COTWU (T), utawawezesha Madereva kushiriki ipasavyo  katika majadiliano ya pamoja na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kwa lengo la kuboresha maslahi na haki za madereva.
 
Vyama hivi sasa vinawajibika kisheria kufuata taratibu za majadiliano sehemu za kazi na kuzingatia matakwa ya Sheria na Katiba zao. Vyama husika vimelekezwa kufika katika maeneo ya kazi na kutangaza sera zao kwa njia mbalimbali ili kuvutia wanachama wapya na kuwa na nguvu za kisheria kuwawakilisha na kutetea maslahi ya madereva.
 
Hivyo, hoja hii imekamilishwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.33      Kuhusu Kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali kuhusu Sheria za Kazi, haki na wajibu wa mfanyakazi na mwajiri; Mafunzo yalitolewa kwa wajumbe wa Kamati, wajumbe wa TATOA na TABOA kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 18 Mei, 2015. Uelimishaji umeendelea kufanywa kwa njia ya vyombo vya habari na ushauri kwa wadau husika kulingana na mahitaji. Utekelezaji ni endelevu na hoja hii inaondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.34      Kuhusu Serikali kutoa Tamko la kuongeza mishahara ya madareva; Baada ya kupata ufafanuzi wa kisheria, wadau waliafikiana kuwa suala la nyongeza ya mshahara liachwe lishughulikiwe na Bodi za Mshahara kwa mujibu wa Sheria. Uundaji wa Bodi za Mshahara za Kitaifa umeanza na upo katika hatua za mwisho. 
     Bodi hizo ndizo zitakazofanya utafiti kwa mujibu wa Sheria na kuboresha Kima cha Chini cha Mshahara, Vigezo, Hali na Masharti ya Ajira kwa wafanyakazi wa Sekta ya Umma na Binafsi. Madereva wanawakilishwa katika Bodi na watapata fursa ya kutoa maoni yao yafanyiwe kazi huko na kukamilishwa mwanzoni mwa mwaka wa fedha 2016/17.
 
Hivyo, hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
4.35      Kuhusu Serikali kufanya marekebisho ya Sheria za Kazi na kuboresha kanuni ili kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa mikataba na maslahi ya madereva; Marekebisho ya Sheria za Kazi, Na. 6 na 7 za mwaka 2004 yalikamilishwa na kupitishwa na Bunge mwezi Julai, 2015. 
      Kanuni za Sheria za Kazi, Na. 6 na 7 za mwaka 2004 nazo zimeboreshwa na zinatarajiwa kukamilishwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kutiwa saini na Waziri mwenye dhamana ya masuala ya kazi na ajira hivi karibuni. Aidha, hatua zinaendelea kufanya marekebisho mapya katika Sheria za Kazi ili kuongeza nguvu za Maafisa Kazi kutoa adhabu za papo kwa papo kwa wakiukaji. 
    Jambo hili litasaidia kutolewa kwa mikataba ya ajira na uzingatiaji Sheria na taratibu za kutoa haki nyingine kwa wafanyakazi wote wakiwemo madereva. Uwezekano unaangaliwa ili adhabu za papo kwa papo ziweze pia kutolewa kwa wafanyakazi watakaobainika kutishia au kuitisha migomo kinyume cha Sheria. 
 
Hivyo, hoja hii imefungwa na kuondolewa mbele ya Kamati kwa sasa.
 
5.0         Hitimisho:
Serikali inatoa wito kwa  wamiliki wa vyombo vya usafirishaji, viongozi wa vyama vya wafanyakazi madereva na madereva wote nchini kuzingatia na kutekeleza makubaliano yaliyokwishafikiwa hadi sasa.

Pamoja na juhudi za Serikali kutatua mgogoro wa ajira ya madereva nchini, kumekuwepo matishio ya mara kwa mara ya kuitishwa migomo kwa madereva. Kamati inawakumbusha Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva na Madereva wote kuzingatia taratibu za kisheria katika kufanya migomo mahali pa kazi, kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Na. 6 ya mwaka 2004. Kufanya migomo kinyume cha utaratibu ni kuvunja Sheria na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wale wote watakaoitisha na kushiriki katika migomo hiyo.
 
Aidha, Serikali itaendelea kutoa elimu na  kufuatilia makubaliano yaliyofikiwa na hatua za kisheria zitaanza kuchulikwa dhidi ya wale watakaokiuka utekelezaji wa makubaliano hayo na matakwa ya Sheria kwa ujumla. Taarifa kwa umma zitaendelea kutolewa juu ya hatua za utekelezaji.
IMETOLEWA NA:
Eric F. Shitindi
     MWENYEKITI WA KAMATI
04/04/2016

Wabunge Washtushwa TCRA kutumia Bilioni 18 kwa Semina na Warsha

$
0
0

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji (PIC) imeshtushwa baada ya kubaini Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitumia Sh18 bilioni mwaka 2013/2014 kwa ajili ya mafunzo, semina na warsha.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Lolesia Bukwimba alisema matumizi ya fedha hizo ni makubwa ikilinganishwa na kazi iliyofanywa na mamlaka hiyo kwa mwaka huo wa fedha.

Alisema wakati mapato ya TCRA kwa mwaka huo yalikuwa Sh79 bilioni, gharama za uendeshaji zilikuwa Sh76 bilioni. 

“Hii ina maana fedha zilizopelekwa Hazina zilikuwa kidogo. Kama mamlaka ingepunguza matumizi, Serikali ingepata mapato ya kutosha,” alisema.

Bukwimba alisema hilo ni tatizo na kamati hiyo itatoa maagizo kwa mamlaka hiyo Jumamosi ijayo itakapoitembelea.

“Kuna mambo mengi ya kitaalamu ambayo tunahitaji kuona shughuli zake zinazofanywa na mamlaka, tutatoa maagizo siku ambayo tutaitembelea,” alisema Bukwimba.

Hata hivyo, mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Profesa Haji Semboja aliitetea mamlaka hiyo akisema kiasi hicho kilichotumika kwa ajili ya semina, mafunzo na warsha kinatokana na unyeti wa taasisi hiyo.

“Taasisi inasimamia kampuni zinazotoa huduma za teknolojia za kisasa ambayo ni ngeni hapa kwetu, hivyo wafanyakazi wetu wanatakiwa kuwa na ufahamu zaidi ya hao watoa huduma,” alisema Profesa Semboji.

Semboja, ambaye ni mchumi, alisema: “Pamoja na mambo mengine, wafanyakazi wetu wanasimamia kampuni za mitandao ya simu, matoleo ya simu yanatoka mara kwa mara, wanatakiwa kufahamu teknolojia wanayoisimamia. Hapa ni lazima waende darasani.”

Alisema wafanyakazi hao wakiachwa bila kupata mafunzo ya mara kwa mara watajikuta baada ya kipindi kifupi wanapitwa na teknolojia zinazozidi kuibuka kila wakati.

Kwa upande wake, Sabrina Sungura ambaye ni mjumbe na mbunge wa Viti Maalumu, aliitaka mamlaka hiyo kufanya marekebisho ya minara ya simu mkoani Kigoma.

“Hii ni hatari kwa usalama,” alisema.

Tanzania Na Burundi Zatakiwa Kulegeza Msimamo Ndani Ya Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC)

$
0
0
Tanzania  na Burundi zimeombwa kulegeza misimamo yao kwa kuondoa gharama za vibali vya kufanya kazi kwa raia wa nchi zinazounda jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kama zilivyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya ambazo nazo ni wanachama wa jumuiya hiyo.

Akizungumza jijini Arusha hivikaribuni Katibu wa Chama cha Waajiri Afrika Mashariki (EAEO), Aggrey Mlinuka alisema kuwa hadi sasa nchi za Tanzania na Burundi ndizo nchi pekee zilizobakia katika kutoza gharama za vibali vya wageni hasa raia wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Mlimuka alisema kuwa mbali na nchi hizo kuondoa utaratibu huo pia amependekeza kwamba utaratibu wa utoaji vibali hivyo usichukua muda mrefu kama ilivyo sasa kwa nchi za Tanzania na Burundi na kushauri muda wa kuchukua vibali hivyo haustahili kuzidi siku 30.

Katibu huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE) alisema kuwa  chama chao kiliwasilisha mapendekezo hayo mbele ya  Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Richard Sezibera ambaye anamaliza muda wake April 20 mwaka huu.

“EAEO na Sezzibera tumefanya kazi kubwa kuhakikisha jumuiya inasonga mbele kwa kasi kubwa mbali na changamoto zilizopo katika nchi moja moja, lakini tuna uhakika tutazitatua kwa manufaa na maslahi ya wana jumuiya wote,” alisema Mlinuka.

Alisema kuwa Katibu Mkuu mpya Liberata Mfumukeko kutoka kutoka Burundi anatakiwa kuendeleza pale ambapo Dk Sezzibera anapoishia ambapo ni kuhakikisha kwamba unakuwepo utatu wa ajira katika jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mbali na hilo pia amemtaka katibu mkuu huyo mpya kuhakikisha protokali ya soko la pamoja kipengele cha pili cha jumuia ya Afrika Mashariki kinatekelezeka ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo vya wananchi kuingiliana kutoka sehemu moja kwenda nyingine kibiashara pamoja na kutafuta ajira ndani ya nchi wanachama.

Awali Mwenyekiti wa chama cha waajiri Kenya(FKE) Jacqueline Mugo alisema kuwa nchi wanachama hazipaswi kuwa na uoga katika yale ambayo yanaonekana kuwa na manufaa na uhai wa Jumuia ya Afrika Mashariki yakiwemo masuala ya ajira na mengineyo.

Mkutano wa siku moja ulikutanisha vyama vyote vya waajiri wa nchi zinazounda jumuia ya Afrika Mashariki vikiwa na malengo ya kuhakikisha wananchi wa jumuiya hiyo wanapata ajira popote pale wanapokwenda ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images