Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wakuu Wa Mikoa Wawasilisha Ripoti Za Watumishi Hewa ........Mwanza Yaongoza Kuwa na Watumishi Hewa Wengi Ikifuatiwa na Arusha

$
0
0
Hatimaye  wakuu wa Mikoa yote nchini wametii agizo la Rais John Magufuli lilokuwa linawataka wasilishe ripoti ya idadi ya watumishi hewa kwenye mikoa husika.

Wakuu hao wa mikoa wapya wamewasilisha ripoti za watumishi hao jana Jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Georgy Simbachawene ili kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watumishi waliohusika katika kashfa hizo.

Katika ripoti hizo zilizowasilishwa, Mkoa wa  Mwanza unaongoza kuwa na watumishi hewa 334 ukifuatiwa na mkoa wa Arusha  270.

Mkoa wa Dar Es Salaam.
Akiwasilisha ripoti ya watumishi hewa,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema katika mkoa wake baada ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na kamati mbali mbali wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 73 ambao watumishi hao hewa wamepelekea serikali kupotea pesa zaidi ya Milioni 316 kwa mwaka mmoja.

“Katika mkoa huu tumepata watumioshi hewa 73, ila wengi watahoji mkoa huu mkubwa kwa nini unakuwa na watumishi hewa wachache, nataka kukwambia Waziri, bado tunaendelea na uchunguzi wa kina,” alisema Makonda .

Mkoa wa Arusha.
Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda alisema mkoa huo umegundurika kuwepo na watumishi hewa 270 ambao wamekuwa wakiisababishia hasara serikali ya Bilioni 1.8 kwa kipindi cha Mwaka mmoja,

Mkoa wa Dodoma.
Pia Mkuu wa Dodoma Jordan Rugimbana alisema katika mkoa wake wamegundua kwenye mkoa huo una watumishi hewa 101 ambao amedai wameisabishia hasara serikali milioni 287.3 kwa kipindi cha miezi sita.

Mkoa wa Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema katika mkoa wake wamegundua kuwa kuna watumishi hewa 15 ambapo amemweleza Waziri Simbachawene kuwa licha ya hao,  kuna watumishi 145 ambao hajaonana nao huku akidai kuwa akimaliza kuonana nao huenda idadi ya watumishi hewa ikaongezeka.

Mkoa wa Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenelal Mstaafu Salum Kijuu alisema mkoa wake wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 14 ambao wamesababisha upotevu wa pesa za serikali Milioni 49.1

Mkoa wa Katavi.
Pia Mkuu wa mkoa huu, Jeneral Raphael Muhuga alisema mkuo huo umegundulika kuwepo kwa watumishi hewa 21 ambao wameitia hasara serikali Milioni 20.7.

Mkoa wa Kigoma.
Mkuu wa Mkuo huyo, Bregedia Jenaral Mstaafu Emmanuel Maganga alisema katika mkuo huo wamebaini kuwepo watumishi hewa 171 ambao wameitia hasara serikali milioni 114.6.

Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa huo,Merck Sadick alisema wamebaini mkoa wake una watumishi hewa 111 ambao wameisababishia serikali hasara ya milini 281.4.

Mkoa wa Lindi
Kwa Upande wa Mkuu wa mkoa huo,Godfrey Zambi alisema mkoa wake unawatumishi hewa 57 ambao wameitia hasara serikali milini 36.2.

Mkoa wa Manyara.
Kwa Upande wake mkuu wa mkoa huo,Joel Bendera, alisema mkoa huo umekuwa na watumishi hewa 42 ambao wameitia hasara serikali Milioni milioni 313.9.

Mkoa wa Mara.
Kuhusu Mkuoa wa Mara,Mkuu wa mkoa huo,Magesa Mulongo alisema katika mkoa wake wamebaini kuna watumishi hewa 94 ambao wameitia hasara serikali milioni 121.

Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya,Mkuu wa Mkuo huo,Amos Makalla alisema katika mkoa wake kumekuwa na watumishi hewa 98 ambao pia wameitia hasara serikali Milioni 459 .6.

Mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa mkoa huo,Dkt Steven Kebwe,ambapo alisema mkoa wake umegundulika kuwepo na watumishi hewa 122 ambao wameitia hasara serikali milioni 450.7.

Mkoa wa Mtwara.
Mkuu wa mkoa huo, Halima Dendegu amesema mkoa wake umebainikika kuwepo kwa watumishi hewa 17, huku watumishi wengine 285 uchunguzi ukiendelea, ambapo watumishi hao 17 wameitia hasara serikali milioni 216.5.

Mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa John Mongella alisema mkoa wake umengundulika kuwa na watumishi hewa 334.

Mkoa wa Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Dkt Rehema Nchimbi alisema mkoa wake umekuwa na watumiwa na hewa 34 ambao amedai wamekuwa wakiitia hasara serikali Milioni 20.1.

Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Mkoa huyo,Mhandisi Evarist Ndikilo alisema Mkoa wake umekuwa na watumishi hewa 150 huku akishindwa kusema hasara ya fedha za serikali kwa madai kuwa uchunguzi unaendelea.

Mkua wa Rukwa.
Mkuu wa mkoa huo,Kamishna Mstaafu Zerote Steven alisema mkoa wake umekuwa na watumishi hewa, 18 na wametia hasara serikali milioni 55.6.

Mkuo wa Ruvuma,
Mkuu wa Mkoa huo,Thabiti Mwambungu alisema mkoa huo umekuwa na watumishi hewa 35 ambao wameitia hasara serikali milioni 58.4.

Mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa huo,Antony Mataka alisema mkoa huo umegundulika  kuwa na watumishi hewa 62  ambao wameitia hasara serikali ya Milioni 320.9.

Mkoa wa Singida,
Mkuu wa mkoa wa huo,Mhandisi Methew Mtigumwe alisema kuwa wafanyakazi hewa katika mkoa wake  ni 231 na kueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini zaidi.

Mkoa wa Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alianisha kuwa katika mkoa wake watumishi hewa ni 48 ambapo wanaitia hasara Serikali Milioni 118.7.

Mkoa wa Tanga.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela alisema kuwa watumishi hewa katika mkoa wake ni 104ambapo alisema kuwa tathimini ya kuhakiki bado inaendelea.

Hata hivyo katika mkoa wa Shinyanga hali ilikuwa tofauti na mikoa mingine ambapo hadi sasa hakuna watumishi hewa kutokana na mikakati iliyowekwa  kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 na mkuu wa mkoa aliyepita.

Pia, Mkoa wa Songwe hauna  watumishi hewa kunatokana na kwamba mkoa huo ni mpya  na mkuu wake wa mkoa ameapishwa wiki moja iliyopita. 


Rais Magufuli Azungumzia Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi

$
0
0

Rais John Magufuli amewatoa hofu wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhusu uteuzi wao kwa kuwataka kuchapa kazi kwa bidii ili wawe na nafasi nzuri ya kuteuliwa badala ya kufanya kazi kwa wasiwasi jambo ambalo matokeo yake yatakuwa kuondolewa.

Dk Magufuli alitoa kauli hiyo juzi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Chato mara baada ya kutua kwa helikopta akitokea Mwanza kuelekea nyumbani kwake Kijiji cha Rubambangwe kwa mapumziko.

Akiwahutubia mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika uwanjani hapo, Dk Magufuli alisema anatambua kuwa bado hajachagua wakuu wa wilaya na wakurugenzi hali ambayo imewafanya baadhi yao kuwa na wasiwasi na kushindwa kutekeleza majukumu inavyotakiwa.

“Kama wewe ni mchapakazi mkuu wa wilaya, mkurugenzi una wasiwasi gani? Tena unapokuwa na wasiwasi ndivyo uwezekano wa kung’olewa unakuwa mkubwa,” alisema Dk Magufuli huku akishangiliwa na kuongeza:

“Lazima niwaambie waheshimiwa wakuu wa wilaya, ukiwa na wasiwasi hutafanya kazi na sisi tunakuona tu unafanya kazi kwa wasiwasi utaondoka tu kwani wasiwasi ni dalili nzuri ya kukufanya uondoke.”

Aliwatoa hofu akisema hata watakaoondolewa kwenye nafasi hizo watapangiwa kazi nyingine lakini akawaambia kwamba hata kama wataondolewa wasihofu kwani haitakuwa mbaya kwa kuwa hawakuzaliwa na ukurugenzi au ukuu wa wilaya.

Alisema Watanzania wanatakiwa kumwamini na kurudia kauli yake kwamba hatawaangusha akiahidi kuondoa kero ambazo zimegeuka mzigo kwa wananchi.

“Wako wengine walianza kulalamika natumbua mno majipu, siyo kutumbua tu ikiwezekana kuna mengine nitayakata kabisa na mguu wake, Tanzania lazima iwe yenye neema, haiwezekani kuwa na wafanyakazi 5,000 wanaolipwa mishahara mikubwa halafu Watanzania milioni 50 wanalia… nitakwenda kujibu nini kwa Mungu,” alisema.

Alisema ataendelea kuwatumbua (kuwawajibisha viongozi wazembe) hata kama wanafika 50,000 ilimradi Watanzania milioni 50 wapate neema ya kufaidika na rasilimali yao.

Alisema watu katika nchi hii wanaishi bila raha na kuwaahidi kuwa itapatikana kwa kila mmoja kufanya kazi kwa bidii hasa vijana na kuacha tabia ya kucheza pool huku mama zao wakienda shambani kulima na kusubiri kula tu.

Binti Ajinyonga huko Longido ...Aacha majina ya watu anaowadai na Kuagiza Walipe Kabla Maiti Yake Haijasafirishwa

$
0
0

Binti mmoja anayejulikana kwa jina la Jesca ambaye ni mfanyakazi wa Longido Mountain Lodge amekutwa amejinyonga katika hotel ya Longido Mountain Lodge na kuacha ujumbe kuwa kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote 

Amesema amejinyonga kwa ridhaa yake mwenyewe.Katika ujumbe huo, ametaja majina ya watu anaowadai na kuagiza  walipe madeni yake kabla ya mwili wake kusafirishwa kwao pamoja na namba za Mama yake mzazi.
Mimi Jesca Reinald Elisante Leo tarehe 29 , 03 , 2016 nimeamua kujinyonga kwa ridhaa yangu mwenyewe hakuna mtu yeyote anayehusika na kifo changu na hizi ni namba ya Mama  yangu,0672740439.

Ninao wadai
Mama Diana  33,000/=
John Memory card 4 GB
Boss Mshahara 60,000/=

wanao nidai
Zai 20,000/=alipwe na ninao wadai wahakikishe wanalipa kabla sijarudishwa kwetu.

NB:HAKUNA ANAYEHUSIKA NA KIFO CHANGU.
Ndugu zangu nawapenda sana
vitu vyangu vyote vipelekwe kwetu
Jau Kwenye Kuni.

Askari Polisi Anatafutwa Na Jeshi La Polisi Baada Ya Kugundulika Alijipatia Ajira Kwa Vyeti Vya Kugushi.

$
0
0

Zoezi la kuhakiki watumishi hewa lililoamriwa na Rais John Magufuli limemkumba Askari Polisi aliyeajiriwa mwaka 2003 baada ya kubainika kuwa ametumia vyeti vya kugushi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amemtaja Askari huyo kuwa ni Emanuel Nikolas Nyangoli mwenye namba F5425 Pc ambaye baada ya kutuhumiwa kuwa na vyeti vya kughushi aliamua kutoroka na hajulikani aliko.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amesema Askari Emanuel Nyangol amefanya kazi ndani ya jeshi la Polisi kwa muda wa miaka 13 bila kujulikana kuwa ana vyeti vya kugushi,

Vielelezo vya kuonyesha jeshi la polisi lina taarifa kuwa uajiriwa wa askari huyo ni wakutatanisha ndio ulio mfanya atoroke baada ya kujua jeshi la polisi lina  taka kumfungulia mashitaka

Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma linawaomba wanchi ambao watakuwa na tarifa za Emanuel Nyangoli watoe tarifa kwa kituo chochote cha polisi au apige kwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Nomber 0715 009 956.

Breaking News: Wabunge Watatu Wafikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Rushwa

$
0
0
Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa
**
Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wamefikishwa mahakama ya Kisutu leo kwa tuhuma za rushwa.

Wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge wanatuhumiwa kushawishi na kupokea rushwa  ya shilingi Milioni 30 toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo

Mwendesha Mashitaka wa Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mahela Ndimbo mbele Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,  Thomas Simba amesema tukio hilo lilitokea  Machi 15 mwaka huu  majira saa 2  had saa 4 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Ndimbo alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao wakiwa wajumbe Kamati Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) waliomba  rushwa ya sh.milioni 30 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Gairo, Mbwana  Magota.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,Thomas Simba aliutaka upande wa mashitaka upeleke ushaidi  wa watuhumiwa wa rushwa .

Washitakiwa waliposomewa shitaka la kuomba rushwa wote walikana na dhamana yao kuwa wazi kwa masharti ya kila mmoja kwa na mdhamini wa mmoja wa sh.milioni tano pamoja na hati ya kusafiria ambapo wote walikidhi masharti ya dhamana hiyo.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba ameairisha kesi hiyo mpaka Aprili 14 mwaka huu itakapotajwa tena .


TRA Yakamata Magari Matano ya TFF Kutokana na Malimbikizo ya Kodi ya Bilioni 1.118

$
0
0

Mamlaka ya mapato nchini (TRA) imeibukia tena Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lakini safari hii haijapiga kufuli account za TFF badala yake imeondoka na magari matano yanayomilikiwa na shirikisho hilo kutokana na kulidai kiasi kikubwa cha kodi.

TRA imeamua kuchukua magari hayo ikitaka TFF kulipa deni la malimbikizo ya kodi mbalimbali wanayodaiwa ili warejeshewe magari yao.

Richard Kayombo ni afisa wa TRA amethibitisha kuyakamata magari hayo yanayomilikiwa na TFF lakini amefafanua sababu zilizopelekea kufanya hivyo.

“Ni kweli tumekamata magari matano ya TFF na hayo magari yamekamatwa kama sehemu ya mwendelezo wa kuweza kupata mapato yanayotokana na deni la kodi ambalo TFF hawajalipa.

“Mpaka sasa tunawadai billion 1.118 ambayo ni kodi mchanganyiko kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Ikumbukwe hapo nyuma tulikamata account zao kwasababu deni lilikuwa ni billion 1.6 na tukaweza kupunguza sehemu ya deni lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari matano.”

Hii ni mara ya pili kwa TFF kupigiwa hodi na TRA ikilalamikiwa kulimbikiza madeni ya kodi, mara ya kwanza TRA ilizifunga account zote za TFF lakini safari hii wameamua kuyashikilia magari yao.

Kwa mujibu wa Kayombo, magari hayo yapo kwenye yard ya YONO likiwemo basi ambalo hutumiwa kuisafirisha timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Nchi 10 kati ya 14 za Umoja wa Ulaya Zatangaza kusitisha Ufadhili wao Kwa Bajeti ya Serikali ya Tanzania Kisa Uchaguzi wa Zanzibar

$
0
0

Nchi 10 kati ya 14  za umoja wa Ulaya zimetangaza kusitisha ufadhili wao kwa bajeti ya serikali ya Tanzania.

Hii inafuatia uamuzi wa shirika la utoaji misaada la serikali ya marekani (MCC) kuondoa msaada wa dola 472 ( Trilioni 1 )  wa kufadhili miradi ya maendeleo wakidai kuwa uchaguzi wa Marudio zanzibar haukuwa huru na wa haki.

Karibu theluthi moja ya bajeti ya Tanzania ilitegemea msaada toka mataifa ya nje katika bajeti ya mwaka 2015/2016. 

Chanzo: BBC

CCM Yatoa Tamko Baada ya Wabunge Wake Kufikishwa Mahakamani Leo Kwa Tuhuma za Rushwa

$
0
0

Kwa kipindi cha hivi karibunin kumekuwepo na tuhuma za baadhi ya wabunge kujihusisha na masuala ya rushwa.

Tuhuma hizo zimekuwa zikifanyiwa kazi na vyombo vya dola na kwamba tayari baadhi ya wabunge wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kinasikitishwa sana na tuhuma hizo, hasa pale zinapowahusisha wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi  na kinaunga mkono jitihada za vyombo vya dola katika kutafuta ukweli wa tuhuma hizo.

Lazima ifahamike kuwa vitendo vya rushwa havina itikadi,dini, wala kabila na kwamba havikubaliki kwa namna yoyote kwani vina madhara makubwa kwa taifa.

CCM inavishauri vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua stahiki wabunge wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Chama cha mapinduzi kwa upande wake hakitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wabunge wake watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.
 

Taarifa Rasmi ya TAKUKURU Kuhusu Kuwafikisha Wabunge Watatu Mahakamani Kwa Rushwa

$
0
0

WABUNGE WATATU WAJUMBE WA KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA RUSHWA
--
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 31/3/2016 imewafikisha Mahakamani wabunge watatu ambao ni wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa kosa la kushawishi na kuomba rushwa ya Shilingi Milioni thelathini (30,000,000/-) kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 (i)(a). 

Wabunge hao ni Mheshimiwa Suleiman Ahmed Saddiq Mbunge wa Mvomero;Mheshimiwa Victor Mwambalaswa Mbunge wa Lupa na Mheshimiwa Kangi Lugola Mbunge wa Mwibara.

Wabunge hao wamesomewa shitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mfawidhi, Mh.Thomas Simba. 

Akisoma mashtaka hayo wakili wa TAKUKURU, Maghera Ndimbo akishirikiana na Emmanuel Jacob alisema kuwa mnamo Machi 3, 2016 majira ya saa 2 - 4 usiku, katika Hotel ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar es Salaam washtakiwa wote watatu waliomba rushwa ya shilingi Mil.30 kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo kwa lengo la kumsaidia ili Taarifa ya Halmashauri hiyo ambayo ilikuwa kwa wakati huo ijadiliwe  tahere 16/3/2016 ipitishwe bila marekebisho.

Uchunguzi wa shauri hili bado unaendelea na washtakiwa wote watatu mahakama imewaachia kwa dhamana ya kila mtuhumiwa kuwa na mdhamini mmoja na kulipa  shilingi milioni 5. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 14/4/ 2016 itakapotajwa tena.
 
TAKUKURU inawajulisha wananchi wote kwamba hakuna mtu ambaye yupo juu ya Sheria.  Rushwa haivumiliki!

IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU
31 MACHI, 2016

James Lembeli (Chadema ) Aangukia Pua Kesi ya Kupinga Ushindi wa Mbunge wa CCM Kahama

$
0
0

Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo imetupilia mbali maombi ya James Lembeli wa CHADEMA ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini wa Oktoba 25 2015, kwa madai kwamba taratibu zilikiukwa.

Akisoma hukumu iliyochukua saa tatu Jaji wa Mahakama hiyo Moses Mzuna amesema ushahidi uliotolewa na upande wa Lembeli haukuwa na nguvu za kutosha kuishawishi mahakama hiyo kutengua matokeo ya uchaguzi kwani sehemu kubwa ni wa maneno.

Jaji Mzuna amesema kitendo cha Lembeli kulalamikia vitendo vya rushwa vidavyodaiwa kufanywa na mgombe wa kiti hicho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumanne Kishimba kushindwa kuvitolea taarifa kwenye vyombo vya dola kimedhoofisha ushahidi na kuuwekea mashaka. 

Kwa upande wa mashahidi waliounga mkono kuwepo kwa vitendo vya rushwa Jaji Mzuna amesema wameshindwa kujenga hoja kwa mlolongo unaofanana kiasi kwamba wameonekana kana kwamba walikuwa na ushahidi wa kutengenezwa.

Akitoa hukumu hiyo, Jaji Mzuba amefafanua kuwa madai ya unyanyasaji wa wafuasi wake waliokamatwa na polisi katika hoteli ya Golden Rock na wengine katika kata ya Ngogwa yamekosa nguvu kufuatia kukosekana kwa kielelezo cha maandishi kinachoonesha kwamba walikuwa mawakala wake.

Mzuna amesisitiza, sababu ya Lembeli kushindwa kupeleka malalamiko kwenye kamati ya maadili ya uchaguzi iliyowekwa kisheria kwamba hakuwa na muda wa kutosha haikubaliki kwa kuwa mpiga kura yeyote anayemuunga mkono angeweza kulalamika.

Kufuatia uamuzi huo wa mahakama kutupilia mbali maombi ya kutengua matokeo hayo Lembeli amesema anaiheshimu mahakama, na kwamba atashauriana na wakili wake kuona kama haki haikutendeka ili kukata rufaa.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini aliyekuwa mlalamikiwa namba moja katika shauri hilo Kishimba alipohojiwa amesema Jaji ametenda haki kama walivyotenda haki wananchi wa Kahama kwa kumpa kura za ushindi katika uchaguzi wa oktoba 25,2015.

Shauri hilo lilikuwa limevuta hisia za wananchi wa Kahama na kuhudhuria kwa wingi leo kwenye hukumu yake huku makundi ya kisiasa yaani wana-CCM na wana-CHADEMA yakijionesha wazi kwa kushangilia bila dalili zozote za uvunjifu wa amani.

Taarifa Ya Habari za Channel TEN Alhamisi ya Leo March 31 “Full Video”

$
0
0

Taarifa Ya Habari za Channel TEN   Alhamisi  ya  Leo  March 31   “Full Video”



Jeshi la Polisi Tarime/Rorya Laanza Msako wa Wanaume Wanne Waliombaka Binti Mmoja kwa Zamu na Kumharibu Vibaya

$
0
0

JESHI la Polisi katika Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya mkoani Mara, linawasaka watuhumiwa watano wanaotajwa kuhusika kubaka wasichana wawili katika eneo hilo.

Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Andrew Satta alisema, watu hao wanatuhumiwa kuwabaka wasichana hao katika matukio mawili tofauti yaliyotendwa kwa nyakati tofauti Machi 26, mwaka huu katika wilaya za Rorya na Tarime.

Satta alisema kuwa, katika tukio la kwanza mwanafunzi wa shule ya msingi Kibasisi iliyopo kwenye kijiji cha Kangariani wilayani Tarime (Jina limehifadhiwa), alibakwa na watu wawili wakati akirejea nyumbani kutoka shuleni siku hiyo ya Machi 26.

Kamanda Satta alisema kuwa, mwanafunzi huyo alikutana njiani na watu wawili waliokuwa wamejifunga vitambaa vyeusi usoni, ambao walimkamata kwa nguvu, kumburuza vichakani na kumbaka kwa zamu. Alieleza zaidi kuwa, baada ya kumbaka, watu hao walimdhibiti asipige kelele kwa kumfunga kitambaa mdomoni.

“Walipomaliza kumbaka walitokomea kwenye vichaka na kutorokea mahali pasipojulikana, lakini Polisi inawasaka,” alisema na kuongeza kuwa, tukio hilo liliripotiwa Polisi na mwanafunzi huyo.

Katika tukio la pili, Kamanda Satta alisema kuwa, siku hiyo usiku kwenye kijiji cha Ruhu kwenye mwalo wa wavuvi wilayani Rorya, msichana mwenye umri wa miaka 21 (Jina limehifadhiwa), alidanganywa na vijana wanne kuwa aliitwa na rafiki yake wa kiume, jambo lililomfanya awaombe wamsindikize alipo na walitii.

Kamanda Satta alisema kuwa, bila kujua nia ya vijana hao kumdanganya hivyo, binti huyo ambaye hata hivyo anawatambua na kufahamu majina yao, alikubali na kuondoka nao. 

Alisema kuwa baada ya kufika kwenye eneo la mwalo wa wavuvi, karibu na vichaka, huku kukiwa na giza nene, waliamua kumkamata kwa nguvu na kumfunga mdomo kwa kitambaa asiweze kupiga kelele.

“Walipofanikiwa kudhibiti asipige kelele vijana hao wanne walimbaka kwa zamu na kumwacha akiwa hoi vichakani, ndipo binti huyo alipoamua kujikongoja hadi kwenye eneo alipopata msaada wa wasamaria waliomsindikiza kutoa taarifa kwenye kituo cha Polisi na kwenda hospitali kwa matibabu”, alisema.

Watu hao waliotajwa na binti huyo kuwa ndio waliombaka ni pamoja na Ophia Robert ambaye amekamatwa, Nchama Bureki, Robert Shija na mwingine aliyetajwa kwa jina moja, Mashije. 

Aliwaonya wanaoendeleza ubakaji katika kanda hiyo kuacha kwa sababu msako unaofanywa ni endelevu na jeshi hilo halitasita kuwachukulia hatua za kisheria.

Wabunge Wataka Wanaoharibu Miundombinu ya DART wachukuliwe hatua Kali

$
0
0

KAMATI ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imeiagiza serikali kuwachukulia hatua kali wale wote waliovamia miundombinu ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) na kuigeuza kuwa masoko ya bidhaa zao.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza amesema hali hiyo haivumiliki na inapaswa kukomeshwa mara moja.

Kamati hiyo ilikutana kwa mara ya pili na uongozi wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jana jijini Dar es Salaam.

“Tumejionea katika ziara yetu tuliyoifanya katika miundombinu ya mradi kuwa baadhi ya wafanyabiashara wadogo wameivamia miundombinu na kuigeuza kuwa masoko,” alisema.

Rweikiza ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Vijijini alisema jambo hilo haliwezi kufumbiwa macho kwani mradi huo umegharimu fedha nyingi na zitalipwa na kodi ya Watanzania.

Alisema pia baadhi ya madereva wa magari na pikipiki maarufu kama bodaboda wameharibu baadhi ya miundombinu na kwamba wanatakiwa kudhibitiwa.

Aliitaka serikali kuweka ulinzi na wote wanaobainika wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Aliutaka uongozi wa DART kuipatia majibu kamati yake kulingana na maswali waliyouliza ifikapo Aprili 4 mwaka huu.

Kamati ilitaka kujua miongoni mwa mambo mengine suala la nauli za mabasi, tarehe ya kuanza kwa mradi, na mkataba kati ya DART na mtoa huduma wa mpito wa mradi.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa DART, Ronald Lwakatare alisema wakala umejipanga kutoa majibu kwa kamati ya Bunge kwa wakati ili kuiwezesha kuzifahamu kazi za wakala na changamoto zilizopo.

 “Tunazo changamoto nyingi zikiwemo za ofisi, uchache wa wafanyakazi, ufinyu wa bajeti na uharibifu wa miundombinu,” alisema.

Alisema kamati hiyo, serikali na wakala zinatakiwa kuwa karibu ili awamu ya kwanza ya mradi iweze kukamilika na kuanza na awamu nyingine.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo aliwataka wananchi kuendelea kuwa na subira na kuahidi kuwa mradi huo utaanza hivi karibuni na kutoa huduma nzuri ya usafiri.

“Kuna mambo yanakamilishwa ndani ya serikali na wadau wake yakiwemo kufunga mfumo wa utozaji nauli kwa njia ya kadi na mengine,” alisema waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe. 

Alisema nauli zitakazotozwa katika mradi huo zitakuwa rafiki kwa wananchi hivyo wasiwe na wasiwasi.

Mwakyembe Apokea Marekebisho ya Sheria Manunuzi

$
0
0

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe amepokea taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka Tume ya kurekebisha Sheria.

Akipokea taarifa hiyo jana Jijini Dar es salaam Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe alisema taarifa hiyo ya utafiti itasaidia kurekebisha sheria ya manunuzi ambayo inalenga kukuza uchumi wa nchi.

“Mimi na wataalamu wangu tumeipokea taarifa hii, tutaiangalia na kuhakikisha tunaifikisha Wizara ya Fedha na Mipango na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuendelea na utaratibu unaofuata ili mchakato wa marekebisho uweze kufanyika kwa haraka”alisema Dkt Mwakyembe.

Akifafanua juu ya sheria ya manunuzi ya Umma, Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi  amesema kuwa Tume imefanya utafiti wa sheria hiyo kwa kushirikisha wadau mbalimbali.

Tumepata maoni mengi na ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi na wasimamizi wa manunuzi ya Serikali kwa namna wanavyoiona sheria ya manunuzi ya Umma,na sisi tumeyachambua maoni hayo kwa kutumia vigezo vya sheria”alisema  Jaji Mujulizi.

Aidha,Tume imetoa maoni kwa Serikali kusimamia sheria ili iweze kuendana na ukuaji wa uchumi nchini kwa kurekebisha baadhi ya sheria ili kuepuka muingiliano uliopo kati ya sheria ya manunuzi na sheria nyingine.

Marekebisho ya sheria hii ni moja ya agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli  lililotolewa Novemba 2015 alipokua akizindua Bunge la 11.
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi (Kushoto) akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma, katikati ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe na kulia ni katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome.

Zitto Kabwe Kutumia Ripoti ya CAG Kuwaumbua Watumishi HEWA Wizara ya Ujenzi

$
0
0

Mbunge wa Kigoma mjini kupitia ACT wazalendo Zitto Kabwe, ameitaka serikali kuwabainisha wafanyakazi hewa kwenye wizara, baada ya agizo la Rais la kuhakiki watumishi hewa kwenye halmashauri kutekelezwa.

Zitto Kabwe ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake facebook, na kuonesha kushangazwa kwa wizara kutoweka wazi wafanyakazi hewa waliomo humo, huku akijitolea kubainisha wale wa kwenye wizara ya ujenzi.

“Watumishi hewa kwenye wizara mbona hatusikii? Wakuu wa mikoa wameagizwa kutambua watumishi hewa. Mawaziri hawakuagizwa. Ok ngoja nijitolee kutambua watumishi hewa wizara ya ujenzi kupitia ripoti za CAG 2010/2011 mpaka 2014/2015”, aliandika Zitto Kabwe.

Hivi karibuni mikoa yote nchini imetekeleza agizo la kuhakiki wafanyakazi hewa walioko kwenye halmashauri zao, huku mkoa wa Mwanza ukiongoza kwa kuwa na wafanyakazi hewa 334

Watumishi hewa kwenye Wizara mbona hatusikii? Wakuu wa mikoa wameagizwa kutambua watumishi hewa. Mawaziri hawakuagizwa....
Posted by Zitto Kabwe on Thursday, March 31, 2016

Profesa Muhongo Asema Kitendo Cha Marekani Kusitisha Misaada ya MCC Hakitaathiri Miradi ya REA ya usambazaji wa Umeme vijijini

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo amesema kuwa kwa   Tanzania  kutopatiwa  fedha na Marekani  kupitia Mfuko wa  Maendeleo  ya Changamoto za Milenia (MCC) ambazo ni Dola za Marekani  milioni 472 kwa ajili ya miradi ya  barabara,  maji na umeme hazitaathiri  miradi ya usambazaji umeme  vijijini inayofadhiliwa na  Wakala wa Nishati  Vijijini (REA).

Aliyasema hayo  jijini Dar es salaam wakati  akifanya majumuisho  ya vikao vyake na wakandarasi wanaosambaza umeme  vijijini  ambavyo vilianza tarehe  29 Machi, 2016 na kuhudhuriwa na watendaji wa Wizara, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na REA.

Profesa Muhongo alisema kuwa fedha hizo zilikuwa haziendi moja kwa moja katika mfuko wa REA wala serikali kuu kama inavyodaiwa na watu wengi.

“Zile fedha za MCC tulikuwa tunakaa na MCC, tunasema bwana katusaidie kusambaza umeme mfano Shinyanga, kwa hiyo anachukua zile fedha zake anaenda na wakandarasi wake moja kwa moja Shinyanga, huku miradi ya REA ikiendela kama ilivyopangwa, ” alisema Profesa Muhongo.

Alisema kuwa miradi ya MCC ilikuwa ikisaidia juhudi za serikali katika kusambaza umeme   vijijini na mijini lakini fedha hizo zilikuwa hazipelekwi  REA.

Alisisitiza kuwa kabla ya MCC kuanza kutoa fedha za kuendeleza miradi ya umeme, serikali  tayari ilikwishaanza kusambaza  nishati hiyo kwa wananchi na kwamba   kuna wadau mbalimbali wanaochangia  miradi hiyo na hata kama wasipochangia, jukumu la serikali  la  kuwasambazia wananchi wake  umeme linabaki kuwa pale pale.

“Isichukuliwe kwamba fulani asipochangia, sasa taifa zima miradi yake imekufa, hivyo dhana ya kusema kwamba fedha hizo zilikuwa zinapelekwa REA ni upotoshwaji wa hali ya juu, kwamba REA itaathirika kwa kukosa hizo  fedha si kweli,” alisema Profesa Muhongo.

Akielezea utekelezaji wa miradi ya REA awamu ya pili, Profesa Muhongo alisema awali jumla ya shilingi bilioni 881 zilitengwa lakini zikaongezeka shilingi bilioni 60 ambapo  hadi kukamilika kwa awamu hiyo ya pili   jumla ya vijiji 2500 vinatarajiwa kupata umeme, huku wateja wa awali 250, 000   kuunganishwa na huduma hiyo hadi kufikia mwezi Juni, mwaka huu ambao ni ukomo wa utekelezaji wa awamu hiyo.

Kuhusu tathmini ya wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini, Profesa Muhongo alisema kuwa wakandarasi wengi wametekeleza miradi hiyo kwa  asilimia kati ya 75 na  85, huku wengine wakivuka wastani wa REA  ambao ni asilimia 87.

Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo alitoa miezi miwili kwa wakandarasi ambao hawajakamilisha  miradi na kusisitiza miradi yote kukamilishwa mwezi Mei au  Juni 15, mwaka huu  kabla ya kuanza kwa awamu ya tatu inayotarajiwa kuanza ifikapo Julai mosi mwaka huu.

Aliongeza kuwa katika  utekelezaji wa miradi ya umeme  vijijini, serikali imebaini kuwa  wapo wakandarasi wanaotumia  vifaa hafifu kama  transfoma na nguzo na kusisitiza  ukaguzi kufanyika na kampuni itakayobainika kutumia vifaa hafifu itafutwa mara moja kabla  ya awamu  ya tatu.

Ili kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi, Profesa Muhongo aliitaka  TANESCO kwa kushirikiana na Wizara  kuhamasisha wananchi hasa waishio  vijijini  kujiunga na huduma ya umeme,  na  TANESCO kusogeza  huduma  karibu na wananchi ili kuepusha wananchi  kusafiri umbali mrefu  kufuata huduma ya kuunganishiwa umeme au changamoto nyingine zinazotokana na nishati hiyo.

Akizungumzia kuhusu malipo ya wakandarasi hao, Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imeendelea kulipa wakandarasi wote kwa wakati kulingana kazi  zinazofanyika.

Wakati huo huo Profesa Muhongo alisema kuwa mitambo ya kuzalisha umeme  kwa kutumia gesi asilia ya Kinyerezi I  kwa sasa inazalisha Megawati 150 na kuongeza kuwa malipo kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya Kinyerezi II inayojengwa na kampuni ya Sumitomo kutoka nchini Japan yameshakamilika

Mwenyekiti wa Kitongoji Auawa Baada ya Kufumaniwa Akifanya Mapenzi na Mke wa Mtu Vichakani

$
0
0

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bweya katika Kijiji cha Bweya mkoani Geita, Augustine Katemi (42) ameuawa baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu vichakani.

Mwenyekiti huyo alifariki dunia papohapo baada ya kudaiwa kushambuliwa kwa sime na mume wa mwanamke huyo, mkazi wa Kijiji cha Luchili, Wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza.

Tukio hilo lilitokea saa nne usiku Machi 28 baada ya marehemu kudaiwa kukutwa akifanya tendo la ndoa na Chausiku Isangula (32).

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Latson Mpojoli alisema  hana za taarifa za tukio hilo na kuahidi kufuatilia.

Ilielezwa kuwa Katemi aliuawa baada ya kushambuliwa kwa sime na kufa papohapo na baada ya tukio hilo, mtuhumiwa anadaiwa kumshambulia mkewe kwa kutumia sime hiyohiyo na kumsababishia majeraha makubwa sehemu mbalimbali za mwili na amelazwa kwenye Kituo cha Afya cha Nzera.

Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Bweya, Samson Walwa alisema baada ya kutokea tukio hilo wananchi waliendesha msako na kumtia mbaroni mtuhumiwa wakati akijaribu kutoroka kuelekea Sengerema.

Walwa alisema mtuhumiwa alikamatwa nyumbani kwa Edward Iswalala alipokuwa amefikia kwa siri kutoka Luchili ili kufuatilia mwenendo wa mkewe ambaye anadaiwa kuwa awali alimuaga kuwa anakwenda kumsalimia baba yake mzazi anayetibiwa kwa mganga wa kienyeji.

“Inavyosemekana alikuwa akifuatilia mienendo ya mke wake… sisi tulipomkamata tumemkabidhi Kituo cha Polisi cha Nzera pamoja na nguo za marehemu (mwenyekiti) na zile za mkewe kwani alipofanya mauaji hayo alizichukua nguzo zao hadi tulipomkata nazo,” alisema Walwa.

Mmoja wa wananchi walioshuhudia tukio hilo, Jumanne Tole alisema, Chausiku alimuaga mumewe kuwa alikuwa anakwenda kijiji cha Kalebezo kumsalimia baba yake mzazi kwa waganga wa tiba asilia alikokuwa anatibiwa lakini baada ya kufika na kumsalimia, alikwenda kwa kaka yake aitwaye Ndagabwene Isangula huko Bweya alikofikwa na mkasa huo.

Alisema kuna madai kuwa mtuhumiwa alifika kijijini hapo kwa siri akiwa amevaa nguo na kofia zilizochakaa ili asifahamike wakati akifuatilia nyendo za marehemu na mkewe na akafanikiwa ikidaiwa kwamba alikuwa na watu ambao walikuwa wakimpatia taarifa hizo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo April 1, 2016

Mkazi wa Mwananyamala Apandishwa Mahakamani Kwa Kutishia Kumuua Rais Magufuli Kwa Kujitoa Mhanga

$
0
0

Kondakta wa daladala, Hamim Seif (42) mkazi wa Mwananyamala Ujiji, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kutishia kumuua Rais John Magufuli kwa maneno.

Seif alipandishwa kizimbani mahakamani hapo jana mchana na kusomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kenneth Sekwao.

Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo na Hakimu Mkazi, Hellen Liwa alisema kuwa dhamana ya mshtakiwa huyo iko wazi na alitakiwa kuwa na wadhamini wawili, kutoka taasisi ya Serikali inayotambulika, ambaye atasaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni.

Licha ya dhamana yake hiyo kuwa wazi, mshtakiwa huyo alishindwa kukamilisha masharti hayo kwani baada ya kusomewa mashtaka alipoulizwa kama alikuwa na wadhamini alishindwa kuwapata.

Akimsomea shtaka linalomkabili, Wakili Sekwao alisema kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya Soweto, Makumbusho wilayani Kinondoni kinyume cha kifungu cha 89 (2) (a) na kifungu cha 35 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu.

Wakili Sekwao alisema akiwa katika baa hiyo, mshtakiwa alitishia kumuua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli kwa maneno kwa njia ya kujitoa mhanga.

Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli, mimi nimo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza,” alisema Wakili Sekwao akimnukuu mshtakiwa huyo.

Hata hivyo, Wakili Sekwao alisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na akaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kesi hiyo kutajwa.

China Yasema Uchaguzi wa Zanzibar Ulikuwa Huru na Wa Haki.....Yaahidi Kuendelea Kutoa Misaada na Kushirikiana na Tanzania

$
0
0
Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing amefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ofisini kwa Waziri huyo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Balozi wa China amesema kuwa Serikali ya China inaamini kwamba uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika mwishoni wa wiki iliyopita ulikuwa huru na haki. 

Balozi Youqing amesema kuwa Makamu wa Rais wa China ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kwake na kwa watu wa Zanzibar kwa kuendesha uchaguzi huo katika misingi ya haki na uhuru. 

“Alikuwepo shuhuda wetu katika kushuhudia uchaguzi huo na alituambia kuwa ulikuwa wa haki na uhuru,” alisema Balozi huyo.

Katika mazungumzo hayo Balozi Youqing alisema Serikali ya China itaendelea kutoa misaada na kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwani huo ni wajibu wa mataifa makubwa kwa nchi zinazoendelea. 

Alimhakikishia Mheshimiwa Makamba kwamba China ina mipango mingi ya ushirikiano na Tanzania, ikiwemo kwenye sekta ya umeme na itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania, ikiwemo kupitia makampuni ya China, ili kuhakikisha malengo ya Tanzania kwenye sekta ya umeme yanatimia.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Makamba alimshukuru Balozi Youqing pamoja na Serikali ya China kwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

 “Ujumbe na salamu ulizotoa leo umetupa faraja Watanzania. Urafiki baina ya nchi zetu, na baina ya vyama vyetu vya CCM na CCP, ni wa muda mrefu, ni wa majira yote, na umejengwa kwenye misingi ya kuheshimiana na hauna budi kuendelezwa”, alisema Mheshimiwa Makamba.

Pia Waziri Makamba na Balozi Youqing walikubaliana kutembelea Pemba na Unguja kwa pamoja mwezi Aprili ili kukagua na kutengeneza miradi ya maendeleo kati ya China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Vilevile, walikubaliana kuhusu kutengeneza mradi mkubwa wa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na China kwenye teknolojia zitakazosaidia kupunguza matumizi ya mkaa, hivyo kuhifadhi mazingira.

Waziri Makamba pia amemueleza Balozi Youqing kuhusu hitaji na umuhimu wa ushirikiano katika kuiwezesha Tanzania kumiliki teknolojia ya uzalishaji wa nishati kwa kutumia taka ngumu zinazozagaa katika miji ya Tanzania ambapo Balozi Youqing aliahidi kulifuatilia suala hilo.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
OFISI YA MAKAMU WA RAIS.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images