Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mkurugenzi asimamishwa kazi Itilima, posho zafutwa

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, John Aloyce amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kushindwa kuisimamia halmashuari hiyo na kusababisha kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara kati ya madiwani na watendaji.

Uamuzi huo umechukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana mjini Langangabilili wilayani humo. 

Mbali na uamuzi huo, amefuta posho zote kwa wakuu wa idara na vitengo katika halmashauri zote zilizoko mkoani hapa wanaoingia katika vikao vya madiwani.

Vikao hivyo ni pamoja na Baraza na kamati za halmashauri kwa madai kuwa hazina tija yoyote, na kuelekeza fedha hizo zilizotengwa zifanye kazi nyingine za maendeleo kama vile utengenezaji wa madawati.

Alisema alipata malalamiko dhidi ya Mkurugenzi huyo kupitia wajumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango wa halmashauri hiyo waliofika ofisini kwake, hivyo kuamua kuitisha kikao hicho cha dharura ili kuyasikiliza.

 Katika kikao hicho madiwani hao walisema serikali ilitoa Sh milioni 450 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika halmashauri hiyo lakini kazi hiyo haikufanyika, wanapohoji na kutoa uamuzi umekuwa haufanyi kazi.

“Wilaya yetu ni mpya na katika kuondoa tatizo la watumishi wa halmashauri hii kuishi mbali na makao makuu ya wilaya tuliamua kuanza ujenzi wa nyumba za watumishi na tukaletewa Sh milioni 450. Lakini kila tunapohoji matumizi ya fedha hizo hatupatiwi majibu na tunapomwagiza Mkurugenzi atuletee hakubaliani na maamuzi yetu,”alisema Kuzenza William (CCM), ambaye ni Diwani wa Kata ya Zagayu.

Walisema kuwa hata mapato ya ndani yanayopatikana hayafahamiki licha ya kuwepo kwa ushuru wa mazao mchanganyiko haulipwi na wafanyabiashara walio wengi, hivyo kusababisha shughuli nyingi za halmashauri kukwama na kuzua migogoro ya mara kati ya madiwani na ofisi ya Mkurugenzi.

“Mapato ya ndani hayafahamiki kabisa kuwa ni kiasi gani cha fedha kimepatikana, maana hatusomewi na inaonekana hata ushuru wa mazao mchanganyiko wafanyabiashara hawalipi hii timu ya mkurugenzi inayosimamia mapato sina imani nayo,” alisema Diwani Kata ya Lugulu, Robert Jongela. 

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Daud Nyalamu alisema madiwani wa halmashauri hiyo wanaonekana hawana uamuzi kwani waliagiza kuwa vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 320 vilivyokopwa na halmashauri hiyo kwa ajili ya ujenzi wa maabara 35 za shule za sekondari vifanye kazi, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika na vingi vimeharibika.

“Tulikopa benki Sh milioni 320 kwa ajili ya ujenzi wa maabara 35 zilizoko katika halmashauri yetu, vifaa vimenunuliwa lakini hadi sasa vimesambazwa maeneo mbalimbali havijafanyiwa kazi. Vimeharibika kwani saruji imeganda na mbao zimepinda na hazifai kwa ujenzi. Hii inatokana na uzembe wa Mkurugenzi wetu na kila kukicha halmashauri inadaiwa hadi madiwani hatulipwi stahili zetu,” alisema.

Akizungumzia tuhuma dhidi yake, Aloyce alisema tangu ateuliwe kuwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo miezi sita iliyopita alikuta Sh milioni 126 zilizokuwa zimebaki katika ujenzi wa nyumba za watumishi.

“Mimi wakati nafika katika halmashauri hii nilikuta kati ya Sh milioni 450 za ujenzi wa nyumba za watumishi zilikuwa zimebaki Sh milioni 126, tulikaa na wakuu wa idara tukaamua tuzikope na kujenga ukumbi ukizingatia ya kuwa tulikuwa tunaelekea uchaguzi mkuu hivyo tungeshindwa mahali pa kukusanyia matokeo ya kura,” alisema.

Alisema licha ya tuhuma mbalimbali dhidi ya halmashauri hiyo, iliundwa tume kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kuzichunguza lakini hadi sasa hawajawaletea majibu, hivyo kuomba iundwe tume huru kutoka nje ya mkoa ili kuweza kuzichunguza tuhuma zilizotajwa na madiwani dhidi yake na ikibainika yuko tayari kuachia ngazi.

Vigogo Wawili Maliasili Waliotoa Vibali vya Kusafirisha Tumbili Watiwa Mbaroni

0
0

Kikosi kazi maalumu cha kuchunguza makosa makubwa ya kihalifu kimewatia mbaroni vigogo wawili wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wakihusishwa na utoaji wa kibali cha kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini Albania.

Maofisa hao ni Mkurugenzi wa Idara ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Dk Charles Mulokozi na ofisa mfawidhi wa kituo cha uwindaji wa kitalii, utalii wa picha na Sites cha jijini Arusha, Nyangabo Musika.

Kikosi hicho kinaundwa na wachunguzi kutoka Polisi, Idara ya Uhamiaji, Usalama wa Taifa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kikosi cha kupambana na ujangili nchini na Takukuru.

Wakati Dk Mulokozi anakamatwa, tayari alikuwa amesimamishwa kazi kwa agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kwa kutoa kibali wakati Serikali ilishazuia.

Vyanzo mbalimbali vimesema jana kuwa Dk Mulokozi alikamatwa mwishoni mwa wiki na jana alisafirishwa chini ya ulinzi kwenda kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).

“Hivi tunavyozungumza, Dk Mulokozi yuko njiani anapelekwa Kia chini ya ulinzi mkali wa polisi.Nyangabo yeye tayari yuko mikononi mwa vyombo vya ulinzi na usalama pale Kia,” kilidokeza chanzo chetu cha uhakika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alipoulizwa jana hakukanusha wala kukiri kuwa na taarifa za kukamatwa vigogo hao, lakini alisema atakuwa na mamlaka ya kuliongelea wakiingia mkoani kwake.

“Bado sijapewa hizo taarifa, lakini hata kama ningezijua nisingeweza kuzungumzia tukio la kukamatwa kwao lililofanyika mkoa mwingine. Nikikabidhiwa ndiyo naweza kusema chochote,” alisema Kamanda huyo. 

Hata hivyo, Waziri Maghembe alithibitisha kukamatwa kwa vigogo hao, akisema katika tukio hilo yeyote aliyetia mkono wake lazima akamatwe na kushitakiwa.

“Ni kweli Dk Mulokozi amekamatwa na siyo yeye tu kuna ofisa mwingine pale ofisi yetu ya Arusha naye tumemkamata. Hatuna mchezo katika suala hili,” alisisitiza.

Profesa Maghembe alitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa raia wa Uholanzi waliokamatwa na polisi hawakuwa na vibali halali vya kufanya biashara ya kusafirisha wanyama hai kwenda nje ya nchi kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Hawa Waholanzi walikuwa na tourist visa (waliingia kama watalii). Halafu Watanzania waelewe mtu hawezi kupata kibali cha kusafirisha mnyama hai kabla ya kumkamata, kuhesabiwa, akakaguliwa na kupata vibali stahiki,” alisisitiza.

Raia hao wa kigeni ambao ni ndugu wa familia moja, Artem Alik Vardanyian (52) ni mkurugenzi wa mgahawa huko Uholanzi na Eduard Alik Vardanyian (44), meneja wa hoteli huko huko Uholanzi.

Hata hivyo, vyanzo vingine vimedai  kuwa pamoja na kuwapo kwa vibali hivyo, lakini hapakuwapo na “release order” inayotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kama sheria inavyoelekeza.

Chanzo hicho kilidai wanyama hao walikuwa wasafirishwe kwa kutumia ndege ya mizigo ya kukodi ambayo ilitokea Afrika Kusini na ilikuwa iwapeleke wanyama hao Albania kupitia Nairobi nchini Kenya na Nigeria.

“Hao marubani wa hiyo ndege waliitwa pale Polisi (Kia), wakaandikisha maelezo yao kuwa walikuja kuchukua wanyama hao na wakaambiwa wao waondoke tu hakuna mnyama anaondoka,” alidokeza ofisa mmoja katika uwanja wa Kia.

Rais Magufuli Akabidhiwa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

0
0

Rais John Magufuli, ambaye amejipa kazi ya “kutumbua majipu”, sasa anaweza kufanya kazi yake vizuri zaidi baada ya kukabidhiwa ripoti tano na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambazo anaweza kuzitumia kama kitendea kazi.

Tangu aingie Ikulu, Rais Magufuli na Serikali yake amekuwa akifanya kazi ya kuibua uozo kwenye taasisi za Serikali, kusimamisha na kutengua uteuzi wa watumishi wa umma wanaojihusisha na ufisadi na wakati fulani amekuwa akiitaja ripoti iliyopita ya CAG kuwa ndiyo iliyoanika uozo anaofanyia kazi.

Jana, “mtumbua majipu” huyo alikabidhiwa ripoti ya kwanza ya CAG tangu aapishwe kuwa Rais Novemba 5 mwaka jana na sasa ana kitendea kazi rasmi cha kufanyia kazi.

CAG Mussa Assad alimkabidhi Rais Magufuli taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ikiwa ni kwa mujibu wa Katiba inayomtaka akabidhi ripoti hizo kwa Rais kabla ya mwisho wa mwezi Machi.

Taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa, kaimu mkurugenzi wa mawasiliano – Ikulu, Rais Magufuli, ambaye aliwaomba wabunge kumpa ushirikiano katika kutekeleza kazi za wananchi wakati akizindua Bunge Novemba 20, atazikabidhi ripoti hizo kwenye chombo hicho ndani ya siku saba za mwanzo za Mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi na Moja utakaofanyika mjini Dodoma kuanzia Aprili 19.

“Rais Magufuli amempongeza CAG na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo na ametoa wito kwa chombo hicho kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi. Ameahidi kuwa serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake,” inasema taarifa hiyo. 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya March 29

Wafuasi Zaidi ya 600 wa UKAWA Wakiongozwa na Freeman Mbowe Wafanya Tukio Kubwa Nyumbani Kwa Lowassa

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe, amewashauri Watanzania wasife moyo kwa matokeo mabaya ya uchaguzi yaliyopinduliwa; na kwamba matokeo hayo yawe chachu ya kufanya  vizuri zaidi katika uchaguzi ujao.

Amesema uchaguzi si tukio, bali mchakato; na kwamba kama kuna watu wamekufa moyo kwa sababu ya kilichofanywa na serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupindua matokeo, hasa ya urais,  watafakari upya na wajipange kwa kazi kubwa inayokuja, kwani mafanikio ya kisiasa hayapimwi kwa tukio moja la uchaguzi na matokeo yake. Alisema matokeo hayo yanapswa kuwatia hasira na kuwahamasisha waendelee kupambana,

Mbowe aliyasema hayo Masaki, nyumbani kwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa Zamani ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Chadema aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwenye hafla ya kumshukuru Mungu iliyoandaliwa na familia hiyo. Ukawa unaundwa na Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

“Hatukushinda serikali kuu kama tulivyokusudia na kupenda iwe kwa sababu ambazo si wakati wake kuzisema sasa, lakini ni vema tukumbuke kwamba mapambano tunayofanya, kama kuna yeyote miongoni mwetu anafanya kwa ajili yake binafsi, ana wajibu wa kujitafakari upya,” amesema Mbowe.

Aliongeza kwamba, kazi ya mapambano wanayofanya viongozi sasa ina manufaa kwa kizazi kijacho, na kama wanaoifanya sasa wakafanikiwa kuonja matunda ya kazi ya mikono yao basi ni jambo la kumshukuru Mungu.

“Kazi anayofanya Lowassa (Baba Kadeti) si lazima aone matunda yake leo, huenda mtoto wake ataonja na asipoonja Kadeti basi wajukuu wataonja matunda hayo na kutambua mchango mzuri wa babu yao kwa kazi kubwa ya maana anayofanya sasa,” amesema.

Aliwahimiza Watanzania zaidi ya 600 waliokuwepo kwenye halfa hiyo kuwa wale walio wafuasi wa vyama vya siasa hata wasio na vyama wana wajibu wa kuendelea kwa nguvu zote na kazi ya kupambana ambayo Lowassa amejiunga nayo, kwani wakati wa uchaguzi watu wengi walipigana kumsaidia sio kwa ajili ya familia yake ila walifanya vile kwa sababu ya nchi hii, huku Lowassa akiwa kiongozi na mpeperusha bendera.

Mbowe alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania waendelee kumwombea neema, ujasiri na afya njema Lowassa kwani taifa bado linamhitaji kuliko pengine anavyohitajika na familia yake.

Aidha, Mbowe alimsifu pia Regina, mke wa Lowassa, kwa ujasiri wake na familia nzima kwa uamuzi mzuri na ujasiri aliochukua katika kuhakikisha Watanzania wanatafuta haki na ujasiri kwa kukata minyororo ya watesi.

“Mama ulikuwa mwoga kwenye kampeni katika hatua za awali, lakini baadaye ulipata ujasiri kama mgombea mwenyewe. Asante sana kwa kuondoa woga; asante kwa kuongoza familia, na sasa tuendelee na mapambano.” alihimiza Mbowe

Kabla ya Mbowe kusimama, neno la kuwashukuru watu waliofika nyumbani lilitolewa na Regina akasema familia, hasa Lowassa mwenyewe, ilikuwa inasubiri kwa hamu siku ya kumshukuru Mungu na Watanzania kwa mazuri mengi aliyowatendea.

Hafla hiyo ya shukrani ilianzia kwa ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front, Dar es Salaam. Lilichagizwa na nyimbo kadhaa za shukrani zilizopendekezwa na Lowassa mwenyewe, na kuimbwa na washiriki wote, wakiwamo wa madhehebu mengine ya dini.

Miongoni mwa washiriki wa hafla hiyo ni baadhi ya wanachama wapya wa  UKAWA waliojiengua CCM mwaka jana, wakiwamo Hamisi Mgeja, Mgana Msindai, Lawrence Masha, John Guninita, na wengine.

Ilihudhuriwa pia na wanasiasa, viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali, vijana na wazee, matajiri na watu wa kawaida kutoka sehemu mbalimbali.

“Tumepata mengi mazuri, tunaweza kusafiri kwenda Monduli na kurudi si sababu tuna magari mazuri kuliko wengine; tunaweza kusafiri kwa ndege na tukarudi salama, lakini hata wakati mwingine unasikia mtu anakupigia simu kukusalimu au kukuandikia ujumbe mzuri wa faraja, haya yote  ni sababu ya Mungu na tukaona leo tufike Kanisani kusema Mungu asante kwa mema yote uliyotujalia,” alisema Regina akiwa amejawa tabasamu muda wote, huku akishangiliwa.

Wajukuu wa Lowassa walijumuika kumwimbia babu yao wimbo kutoka miongoni mwa tenzi za Injili zilizoandaliwa kwa ajili hiyo, huku wakiongozwa na mpiga kinanda.

Baada ya wajukuu, Masha alitumbuiza washiriki kwa wimbo wa Kiingereza “Amazing Grace,” akatuzwa kiasi cha Tsh. 50,000 ambacho, hata hivyo, alikigawa kwa wajukuu wa Lowassa.


Zaidi ya Wafanyakazi 400 wa TTCL Kupoteza Ajira

0
0

Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ipo kwenye maandalizi ya kupunguza wafanyakazi wasiohitajika kwa sasa kutokana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

TTCL inayotoa huduma za simu na pia kutoa mitandao kwa kampuni zilizo na leseni ya huduma hizo, itapunguza wafanyakazi 400 ili kuongeza ufanisi na hivyo kumudu ushindani katika sekta ya mawasiliano dhidi ya kampuni binafsi. 

Mapema mwaka jana, Serikali iliamua kununua asilimia 35 ya hisa za TTCL zinazoshikiliwa na kampuni kubwa ya huduma za simu nchini India, Bharti Airtel na baadaye mwezi Mei, 2015 aliyekuwa Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano, January Makamba aliliambia Bunge kuwa Serikali iko katika maandalizi ya mwisho ya kumiliki hisa zote za kampuni hiyo kubwa kwa huduma za simu za mezani nchini.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya kampuni hiyo kinaeleza kuwa kati ya wafanyakazi 1,500 wa TTCL, zaidi ya 400 watapoteza ajira katika mpango huo wa kudhibiti gharama za uendeshaji.

“TTCL itaomba fedha ili kuwalipa wafanyakazi zaidi ya 400 wanaotakiwa kupunguzwa,” alisema mtoaji habari huyo .

“Kuna wafanyakazi wanaingia asubuhi na kutoka jioni bila kufanya kazi yoyote ile na mwisho wa mwezi anakula mshahara zaidi ya Sh800,000. Kumuachisha kazi inakuwa vigumu sana, lakini kama TTCL itasaidiwa na Serikali kufanikisha hilo, itakuwa imejikwamua kwa kiwango fulani.”

Hata hivyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema maandalizi ya kupunguza wafanyakazi yataanza mwezi Aprili kupitia ukaguzi maalumu wa rasilimali watu.

Alisema hatua ya awali kwa sasa ni kuangalia mpango mkakati wa kampuni hiyo jinsi gani inaweza kujijenga upya kutokana na changamoto ya ushindani wa kibiashara.

“Kwa sasa siwezi kusema ni wafanyakazi wangapi wanatakiwa kupunguzwa kutoka miongoni mwa 1,500 kwa kuwa kila mmoja amekuwa akiwasilisha taarifa yake mwisho wa mwaka na wapo wanaotimiza na wengine wanashindwa kutimiza malengo ya kampuni, mchango wao unakuwa kidogo,” alisema.

Dk Kazaura alisema katika lengo la mpango huo ni kuangalia jinsi gani watalaamu waliopo wanatumika kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Alisema kuna wataalamu waliopo kwa sasa ambao hutumika katika shughuli za uzalishaji, lakini kulingana na mabadiliko ya kazi nyingi kufanywa na teknolojia mpya na nafasi ya kazi nyingi katika taaluma zao zimepungua.

“Pamoja na hivyo lakini itakuwa vigumu kuwafahamu ni wangapi ambao hawazalishi katika kampuni hadi kazi hiyo ya HR auditing (ukaguzi wa rasilimali watu) itakapokamilika. Itakuwa tathmini itakayotoa mwelekeo mpya wa kampuni,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu mpango wa TTCL kuomba msaada serikalini, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema hana taarifa yoyote.

Hata hiyo, alisema TTCL ina mamlaka yake ya kujiamulia kuajiri au kupunguza wafanyakazi bila kuingiliwa na Serikali.

Utafiti: Wanawake Wanne Kati ya 10 Wanaofanya Biashara ya Ngono Wana UKIMWI

0
0

Utafiti uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na upimaji wa virusi vya Ukimwi la MATUMAINI, unaonyesha kuwa kati ya wanawake kumi wanaofanya biashara ya ngono wanaopima wanne kati yao wanakutwa na virusi vya Ukimwi.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bw. Onesmo Mwihava amesema wamekuwa wakifanya zoezi la upimaji katika maeneo ya majumba ya starehe, baa na katika baadhi ya madanguro yasiyo rasmi na kuwa licha ya kuwepo kwa jitihada za serikali katika kutokomeza biashara ya ngono lakini wengi wa wanaojiuza wanakutwa wameathirika ama kuwa na magonjwa ya zinaa.

Aidha, Bw. Mwihava amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakijihadhari na suala la kupata mimba na kuacha kuchukua tahadhari kuwa katika kupata maambukizi pamoja na magonjwa ya zinaa ambapo katika utafiti wao, kati ya watu kumi waliojitokeza kupima kati yao sita huwa na magonjwa ya zinaa.

Ameongeza kuwa mojawapo ya waathirika wakubwa wa ugonjwa wa ukimwi pamoja na magonjwa ya zinaa ni vijana kutokana na kutochukua tahadhari kwa kufanya ngono zembe na kuwa hali hiyo mara nyingi hutokana na kiwango cha fedha alizotoa kwaajili ya huduma hiyo.

Mwihava amezitaka taasisi na serikali kulivalia njuga suala la kutokomeza biashara ya ngono pamoja na kutoa elimu kwa vijana na wanaojihusisha na vitendo hivyo haswa baada ya kukamatwa kwakuwa kwa sasa wanawake hao wengi wameanzisha mbinu mpya kwa kukaa katika baa na majumba ya starehe na kutoka na wateja.

Basi Kutoka Mwanza Laua 6 na Kujeruhi 38

0
0

Watu sita wamekufa na wengine zaidi ya 38 kujeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Rufani Mkoa wa Iringa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Mwanza kwenda Iringa kupinduka mlima Ipogolo Manispaa ya Iringa.

Mganga Mkuu Mkoa wa Iringa, Dk Robert Salim alisema waliokufa ni sita, wawili kati yao walifia hospitalini wakati wakipatiwa matibabu. 

Dk Salim alisema waliokufa ni wanaume wanne na wanawake wawili na kwamba, maiti waliotambuliwa ni wawili, Makka Msigwa na Venant Mhagama.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 3.30 usiku baada ya basi la Lupondije aina ya Scania lililokuwa likitoka Mwanza kwenda Iringa kumshinda dereva na kupinduka.

Alisema majeruhi 38 walifikishwa hospitalini hapo, 11 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 27 wamelazwa kwa matibabu.

Kakamba alisema wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Mmoja wa abiria walionusurika katika ajali hiyo, James John alisema walipofika Iringa, dereva waalikataa kuwashusha abiria waliokuwa wakiishia mjini ili awapeleke waliokuwa wakienda Mbeya kwenye basi jingine eneo la Ipogolo.

John alisema kutokana na uamuzi huo abiria waliotakiwa kushuka Kituo cha Kihesa na Kituo Kikuu cha Mabasi Iringa walipitiliza, lakini hawakufika Ipogolo wakapata ajali eneo la mlimani.

Dereva huyo, Castory Mwalusako (35) alisema basi hilo lilimshinda wakati akishuka mlima kutokana na kupoteza upepo kwenye breki na kulikwepa gari dogo lililokuwa mbele yake na kupoteza mwelekeo kisha kupinduka. 


Serikali ya Tanzania kujenga bomba la mafuta kutoka Tanga hadi Uganda....Wafanyabiashara wa Tanzania Kwenda Uganga Kujionea Fursa

0
0
Serikali za Tanzania na Uganda zinatarajia kuanzisha mradi wa uwekezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta unaolenga kuongeza pato la taifa na uchumi wa nchi hizo.

Mradi huo unatarajia kugharimu kiasi cha Dola za Marekani bilioni nne na utekelezaji wake utaanza mwanzoni mwa mwaka 2017.

Kauli hiyo imetolewa jana  Jumatatu (Machi 28, 2016) Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wake na wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini.

Prof. Ntalikwa alizitaja fursa ambazo zitanufaisha taifa kuwa ni pamoja na kodi zitakazolipwa, kuongezeka kwa wigo wa ajira kupitia miradi huo pamoja na tenda mbalimbali zitakazotolewa wakati na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo.

 “Tanzania ina kila sababu ya kupata mradi huo kwa kuwa ina uzoefu wa kuwa na mabomba kama hayo manne nchini na tunajivunia bandari yetu ya Tanga yenye kina kirefu kuliko bandari zote Afrika Mashariki” alisema Prof. Ntalikwa.

Prof. Ntalikwa alisema kuwa mwitikio wa wafanyabishara wa sekta ya mafuta nchini ni mzuri na kubainisha kuwa wanatarajia kusafiri kuelekea nchini Uganda kujionea fursa mbalimbali zinazopatikana nchini humo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa sekta ya mafuta nchini Dkt. Gideon Kaunda alisema kwa upande wao wataitumia vyema fursa ya uwekezaji katika ujenzi wa mradi huo na kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Imeandaliwa na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Ray C Akana Kurudia Madawa ya Kulevya

0
0

Msanii Ray C amevijia juu vyombo vya habari vinavyoandika taarifa za uongo juu yake, kuwa amerudia kutumia madawa ya kulevya, na kuahidi safari hii atavifikisha mahakamani.

Katika ukurasa wake wa instagrama Ray C ameandika ujumbe mrefu kuhusu vyombo vya habari vinavyomchafua, na kwamba wana mpango wa kukwamisha harakati zake za kupambana na madawa ya kulevya.

“Hujuma hizi najua mnazifanya ili niishie njiani katika harakati za kupambana na dawa za kulevya nchini, Mimi na taasis yangu nitaendelea kusonga mbele na hakika sitakwamishwa na nyumbu kama hawa kwanza mwonekano wa picha uko wazi mimi sina nywele fupi kiasi hicho Ray C wa sasa si yule wa kipindi na enzi hizo now I'm not catalysts of drugs, hata hivyo tayari nimewasiliana na mwanasheria wangu ili niweze kuwawajibisha hawa nyumbu” aliandika Ray C.

Pia Ray c amesema kwa sasa yuko kwenye maandalizi ya mwisho kuandaa nyimbo yake, japokuwa bado yuko kwenye dozi ya methadone, inayotibu uathirika wa madawa ya kulevya.

“Mimi Niko katika maandalizi yangu ya mwisho ya kuaanda nyimbo yangu japo bado niko katika dose ya methadone”, aliandika Ray c.
A photo posted by Ray C (@rayc1982) on

Marekani Yasitisha Msaada wa Mabilioni ya Pesa Kwa Tanzania.

0
0

Shirika la ufadhili la serikali ya Marekani limesitisha msaada wake kwa serikali ya Tanzania likilalamikia matukio kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kutekelezwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao.

Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imesema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni moja za Tanzania.

Kupitia taarifa, bodi hiyo imesema: "Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.”

Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao "haukushirikisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa.”

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ali Mohammed Shein alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani, Chama cha Wananchi (CUF).

MCC imesema kwamba huwa inatilia mkazo sana demokrasia na kujitolea kwa nchi kufanikisha uchaguzi huru na wa haki.

"Uchaguzi uliofanyika Zanzibar na kutekelezwa nwa Sheria ya Uhalifu wa Mitandao vinaenda kinyume na hili,” imesema.

Tanzania ilipokea Dola 698 milioni katika awamu ya kwanza.

Pesa za MCC hutumiwa kufadhili miradi ya maji, barabara na nishati.

Tamko la Wizara ya Afya Kufuatia Wananchi Kuwashambulia Watumishi wa Afya

0
0
Ndugu Wananchi,
Nachukua fursa hii nikiwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya afya nchini, kutoa tamko kuhusiana na matukio ya hivi karibuni yaliyoripotiwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusiana na vitendo vya kusikitisha wanavyofanyiwa watumishi wa sekta ya afya, wakiwemo Madaktari kama vile kushambuliwa kwa maneno na vipigo.
Pasi na shaka, vitendo hivyo vitaathiri upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wanaopewa huduma hizo hususan wa kipato cha chini.

Matukio haya yanajumuisha tukio lililotokea tarehe 27.03.2016 katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula, ambapo Dr Dickson Sahini alishambuliwa na ndugu wa mgonjwa aliyepelekwa hapo kuhudumiwa.

Napenda kutamka kwamba nimesikitishwa sana na tukio hilo, na ninalaani vikali matukio ya watumishi wa afya kushambuliwa kwa maneno au kwa vitendo na wananchi wanaopatiwa huduma.

Jambo hili likiendelea litawavunja moyo watumishi wa afya na hivyo kuathiri upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.

Ningependa kuwafahamisha kwamba kwa ujumla wake sekta ya afya inakabiliwa na changamoto nyingi sana katika maeneo ya miundombinu, dawa na vifaa tiba, watumishi wa kutosha, pamoja na kuwa na watumishi wasiozingatia nidhamu, weledi na maadili katika kutimiza majukumu yao.

Ninatambua kwamba changamoto hizi zipo siku nyingi, na zimekuwa zikitafutiwa majawabu na Serikali za awamu zilizopita ikiwemo ile ya awamu ya nne.

Lakini sote ni mashahidi kwamba Serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dr John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inachukua hatua za makusudi katika kutatua changamoto hizi, likiwemo pia suala zima la utendaji unaozingatia uwajibikaji.

Kwa hiyo ninawasihi sana wanachi wanaopatiwa huduma katika vituo vyetu vya afya kote nchini kuacha mara moja tabia ya kujichukulia sheria mikononi na kufanya vitendo vinavyoweza kuwakwaza watumishi wa afya.

Kwa vile nchi yetu inafuata misingi ya utawala unaozingatia sheria, ni vyema wananchi wakafuata taratibu zilizowekwa wanapohisi kwamba hawakupatiwa huduma za afya wanavyostahili.

Aidha nachukua fursa hii kuvitaka vyombo na mamlaka husika kutosita kuwachukulia hatua wananchi wanaokwenda kinyume na matakwa ya sharia ili kuwahakikishia watoa huduma za afya usalama na amani wakati wa utoaji wa huduma hiyo.

Ninaagiza vile vile kwamba hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini ziweke utaratibu mwepesi wa wananchi kufikisha malalamiko yao pindi wanapoona kwamba hawakupatiwa huduma za afya kwa kiwango stahiki.

Napenda pia kuahidi kwamba tutajitahidi kutatua changamoto za kimfumo zilizopo katika utoaji wa huduma za afya nchini ili kuufanya utoaji wa huduma kuwa bora zaidi.

Ndugu Wananchi,
Ninatambua kwamba sehemu kubwa ya watumishi katika sekta ya afya nchini wanafanya kazi zao kwa ufanisi, upendo, uadilifu na kwa kuzingatia matakwa ya weledi (professionalism) na miiko ya taaluma zao (ethics).

Pia ninatambua kwamba wengi wanafanya kazi katika mazingira magumu na wanatumia muda wa ziada kuendelea kuwahudumia wagonjwa hadi wanapoona wapo salama.

Ninawapongeza kwa dhati watumishi hawa na ninawashukuru na kuwatia moyo waendelee kuwa na tabia hiyo nzuri, kwa maslahi ya Taifa letu.

Hata hivyo ninasikitishwa sana na tabia ya watumishi wa afya wachache ambao wanafanya kazi kinyume na maadili na matakwa ya weledi wa taaluma zao.

Napenda kusisitiza kuwa Wizara yangu haitavumilia matukio ambayo watumishi wa Sekta ya Afya watakwenda kinyume na matakwa ya weledi na maadili ya taaluma zao katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Hivyo hatutasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo ili kudhibiti hali hii.

Nimeshaelekeza vyombo vya kusimamia maadili ya watoa huduma za afya nchini, yaani Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC) kuchukua hatua mara moja, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zao, juu ya watoa huduma wote wanaotuhumiwa kukiuka misingi ya weledi na maadili ya taaluma zao.

Endapo tuhuma zao zitathibitika, hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kufutiwa usajili au leseni zao ikibidi.

Hivyo kwa tamko hili ninawaasa na kuwaagiza watoa huduma wa afya wote nchini kufanya kazi zao kwa bidii, kwa nidhamu na kwa kuzingatia weledi na maadili ya kitaaluma kama inavyoelekezwa.

Ndugu Wananchi,
Napenda pia kukumbusha kwamba kazi hii ya usimamizi wa mahusiano mema kati ya watoa huduma za afya na wananchi, na usimamizi wa weledi na maadili katika vituo vya kazi, itafanikiwa kwa ushirikiano wa pamoja wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Tawala, Wakurugenzi, Kamati za Usimamiaji wa Huduma za Afya za Mikoa na Wilaya, Kamati za Usimamiaji wa Huduma za Afya za Hospitali, na Wananchi wote kwa ujumla katika kuwasimamia, kuwaelekeza na kutambua mapungufu ya kimfumo au yale yanayohusu watumishi wa afya yaliyopo na kuchukua hatua zinazostahili mara moja.

Ni lazima tuzingatie Sheria, Kanuni na Taratibu katika kutimiza jukumu hili.

Wizara ya Afya itaendelea kuvijengea uwezo Mabaraza ya kitaaluma ya wataalamu wa afya ili kutimiza wajibu wao kikamilifu.

Tufanye kazi kwa pamoja ili kutekeleza kauli mbiu ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, inayosema ‘HAPA KAZI TU’.

Asanteni sana.
Imetolewa na:
Mhe. Ummy Mwalimu (Mb)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mtwara – Tanzania
29 Machi 2016

Taarifa ya ACT-Wazalendo:Uamuzi Wa Bodi Ya Wakurugenzi Ya MCC Wa Kusitisha Mahusiano Na Tanzania Yatawaumiza Wananchi Wa Vijijini

0
0

 TAARIFA KWA UMMA
UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI YA MCC WA KUSITISHA MAHUSIANO NA TANZANIA YATAWAUMIZA WANANCHI WA VIJIJINI

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeupokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa wa MCC wa kusisitisha mahusiano na Tanzania.

MCC ni Shirika la misaada la Marekani lilianzishwa na Bunge la Nchi hiyo mwaka 2004 kwa lengo la kusaidia miradi ya maendeleo katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa haraka wa uchumi.

Tangu kuanzishwa kwake, shirika hili limesaidia miradi mingi ya maendeleo nchini ikiwemo ujenzi wa barabarani na usambazaji wa umeme vijijini kwa sasa miradi ya aina hiyo inaendelea sehemu mbali mbali hapa nchini na miongoni mwao ni pamoja na mradi wa REA,miradi ya barabara kama ile ya Tnduma Sumbawanga pamoja na Tanga katika barabara ya Horohoro.

Pamoja na vigezo vingine, kigezo mama kwa nchi kufuzu kupata misaada ya MCC ni kwa nchi husika kuzingatia misingi kidemokrasia ikiwemo kufanya uchaguzi ulio huru na haki.

Jana tarehe 28 Machi 2016 Shirika la MCC lilitangaza kusitisha mahusiano na Tanzania kutokana na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM),kubariki kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 Oktoba 205 na kubariki kurudiwa kwa uchaguzi huo tarehe 20 Machi 2016 katika mazingira ambayo hayakuzingatia misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuvunja matunda ya mwafaka wa kisiasa na kikatiba uliojengwa kwa gharama kubwa visiwani humo.

Chama cha ACT-Wazalendo kinapigania nchi yetu kujitegemea kiuchumi kama msingi wa kujenga utu na uhuru endelevu wa kisiasa na kijamii. Hata hivyo tunatambua kwamba katika kipindi hiki nchi yetu inahitaji mahusiano mema na Jumuiya ya Kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani, likiwemo shirika la MCC, katika kuendeleza miradi ya maendeleo. Shirika la MCC limekuwa mdau mkubwa katika miradi ya barabara na kusambaza umeme vijini.

Uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCC utawaumiza na kukwaza juhudi za wananchi wa vijijini katika kujikwamua na umaskini.

Tunasikitika kwamba ubabe wa Serikali ya CCM na woga wake wa kushindana kidemokrasia umesababisha nchi yetu ikose pesa za MCC ambazo zingesukuma mbele juhudi za kupambana na umaskini.

Tunatoa wito tena kwa Serikali ya chama cha Mapinduzi kuacha ubabe na kufifisha juhudi za miaka ishirini za ujenzi wa demokrasia hapa nchini. Tunatoa wito maalumu kwa wadau wote wa siasa visiwani Zanzibar kurudi mezani na kutatua mgogoro wa kisiasa kwa njia za kistaraabu na katika hali ambayo itarudisha heshima ya nchi yetu katika kukuza demokrasia nchini.

Imetolewa na

Theopister Kumwenda
Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje
29/03/2016

Rais Magufuli Awasili Jijini Mwanza Leo Akielekea Chato.....Sikiliza Audio hii Kujua Alichokifanya Baada ya Kutua Uwanja wa Ndege

0
0

Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametua jijini Mwanza akielekea Chato na kutoa maagizo ya kukamilishwa kwa ukarabati njia ya ndege na kuruhusu barabara iliyokuwa imefungwa na uongozi wa Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kuzuia waendesha bodaboda.

Hapo chini kuna ripoti ya dakika tatu ya mambo yote aliyoyafanya Rais Magufuli baada kutua  Mwanza

Wananchi Wa Chato Wajitokeza Kwa Wingi Kumlaki Rais Dkt John Pombe Magufuli

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wakazi wa wilaya ya Chato Mkoani Geita mapema leo.

Wakazi kutoka vitongoji mbalimbali wilayani Chato mkoa wa Geita,wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ambaye amewasili leo mjini humo alikozaliwa.Rais Dkt Magufuli amewasili wilayani Chato kwa mara ya kwanza tangu awe Rais.


Uchambuzi wa Humphrey Polepole Kuhusu Marekani Kusitisha Msaada wa Mabilioni ya Pesa na Shughuli zake Tanzania

0
0

Nianze na nukuu hizi mbili kuntu za Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere- Mwenyezi Mungu amrehemu.


“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country”. June 1991 in Rio De Janeiro, Brazil

"Demokrasia sio chupa ya Coca-Cola ambayo unaweza kuagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika". Juni 1991 Rio De Janeiro, Brazil (Tafsiri ni yangu)

“No nation has the right to make decisions for another nation; no people for another people”. From ‘A Peaceful New Year’ speech, Tanzania, January 1968

"Hakuna Taifa lina haki ya kufanya maamuzi juu ya Taifa lingine; wala watu juu ya watu wengine ". Hotuba ya Amani ya Mwaka Mpya, Tanzania, Januari 1968 (Tafsiri ni yangu)

Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani. Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano.

Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wa Taifa letu. Hakuna namna nyingine ila kushinda hili kama tulivyoshinda mengine huko nyuma. Kwa wale ambao wameuona umri watakumbuka namna tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi 1964 pale walipotaka kuwa na kauli hasi dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Tulivunja uhusiano na Ujerumani Magharibi baada ya kutaka kuingilia Uhuru wa Mataifa Mawili huru yaliyoamua kuungana na kuunda Nchi Mpya ambayo leo tunajivunia, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

1965 Tulivunja uhusiano na Uingereza kufuatia na kitendo cha wazungu wachache kujitangazia Uhuru (Unilateral Declaration of Independence) kule Rhodesia na uingereza kukaa kimya na kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Tulivunja Uhusiano na Uingereza kuieleza Dunia kwamba Uhuru wa nchi za Afrika ni kipaumbele muhimu kwa Tanzania. Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu. 

Napenda ieleweke kwamba kipindi hiki kilichotokea sio kuvunjika kwa uhusiano wetu na Marekani bali taasisi ya MCC ndio imesitisha msaada wao kwetu, lakini mahusiano yetu na marekani bado yako pale pale, na si Marekani au Tanzania inayoweza kuugharimu uhusiano wetu.

MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje. 

Tanzania ilitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili.

MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani, hapa kuna mtego hapa, hapa ni biashara hapa.

Mchakato wa MCC 2 ulipoanzishwa, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo?

Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.

Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina.

Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda. Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani.

Ndio sababu wengi wenu mtakumbuka hata Rais Obama alitangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power na sio kwamba alipenda kwenda kutembea Ubungo. 

Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO. 

Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. 

Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea, ni sawa na ule mchoro wa Mpanda Punde aliyeshika fimbo yenye majani na akiielekeza mbele ya punda, kwamba punda ataendelea kuyafuata majani akidhani atayafikia kumbe ndio anaupiga mwendo. 

Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.

Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo. 

Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.

Wao nao wanayo hadhira ya wapiga kura wao wanayojaribu kuituliza huko nchini kwao kwa uamuzi huu. Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu. 

Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania zaidi na Tanzania inaihitaji Marekani. Marekani inahitaji MCC 2 zaidi hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2.

Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.

Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa zaidi ya Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.

Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wasimame na kusema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".

Huu ni wakati wa kujifunga mikanda na kulinda heshima yetu kama Taifa letu. Tuna vyanzo vya mapato vingi sana ambavyo hatujaanza kukusanya mapato, tuwe wabunifu na tusibweteke na kutegemea mapato yataongezeka maradufu kwa vyanzo vile vile.

Niseme kwa uchache, sababu walizotoa MCC, na ieleweke aliyetoa tamko ni MCC, heri lingetoka tamko hili Wizara ya Mambo ya Nje au Ikulu ya Marekani, moja ni Zanzibar na pili ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber crimes Act).

Sasa hebu tujadili kidogo, hivi kule Zanzibar tulitaka kitokee nini pale ambapo wanasiasa walikuwa hawataki kujadiliana? 

Tume ile ile ya Uchaguzi ambayo bado ilikuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kuuitisha, kuufuta na kuuitisha tena uchaguzi ikachukua nafasi yake. 

Wanasiasa wasio makini wakaishia kuhamishia malumbano mitandaoni badala ya kuitafuta suluhu ya kisiasa na pale siasa iliposhindikana basi wangeitafuta suluhu katika mahakama za Zanzibar. 

Mezani wakashindwa, mahakamani hawakwenda. Tume ikachukua uongozi, uchaguzi ukaitishwa Wananchi wakapiga kura na sasa huko Zanzibar kuna serikali na baraza la wawakilishi.

Hata mimi sifurahii sana njia waliyoichukua Zanzibar lakini ilibidi siasa za madaraka zisite ili tuanze kufanya siasa za maendeleo. Je wamarekani walitaka muujiza gani utokee huko.?

Kuhusu Sheria ya Mitandao, hata mimi siipendi, si twende mahakamani, bunge litaanza vikao muda si mrefu je wabunge si wapeleke hoja ya kuifanyia marekebisho sheria hii. 

Sasa Marekani (MCC) inapoweka shinikizo kwa suala la Sheria ambayo ni jambo la ndani na linaloweza kujadilika, sijaelewa. 

Mbona sie hatujapiga kelele Yule jamaa yao Trump alipotutusi waafrika na kusema sisi stahili yetu ni kuwekwa tena chini ya ukoloni (hapa nimechomekea tu).

INDHARI

Ni aibu kwa viongozi wa kisiasa kufurahia jambo hili, ni ishara ya ukuwadi wa kisiasa na ambao uko tayari kukumbatia mahusiano yanayotweza Uhuru wetu. It is now high time kufanya siasa safi za maendeleo (politics of development) na sio kujikita katika katika siasa za madaraka (Politics of Power).
*************

Imeandikwa  na: Humphrey Polepole.
Mwandishi, Ndg. Humphrey Polepole amenufaika na uelewa wa watu wenye uzoefu wa mahusiano ya Tanzania na nchi za Nje. Aidha, ni mnufaikaji (alumni) wa programu ya uongozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Taarifa Za Watumishi Hewa Zatua Ofisi Ya Rais-tamisemi.

0
0

Mtakumbuka kwamba leo ni siku ya 15 ya utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa la kuwataka kuwaondoa kwenye malipo watumishi hewa.
 
Natumia fursa hii kutoa taarifa kwa Umma kuwa Agizo hilo limetekelezwa kama Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alivyoagiza. 

Taarifa za watumishi hewa tayari zimewasilishwa kwa maandishi Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuanzia mwishoni mwa wiki.

Kwa sasa taarifa hizo zinafanyiwa kazi na zitakapokuwa tayari kwa matumizi ya Umma zitatolewa kwa Vyombo vya Habari kwa lengo la kuufahamisha Umma.

Hivi sasa taarifa hizi zinakusanywa kwa pamoja ili kupata idadi kamili.
 
Wakati huo huo, napenda kuufahamisha Umma kuwa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) yameanza kufanya mazoezi ya utoaji huduma toka siku ya alhamisi tarehe 24/03/2016.  Tunategemea wiki hii mtoa huduma ataendelea kuongeza idadi ya mabasi ya kufanya mazoezi kabla zoezi hili halijaanza rasmi.
 
Imetolewa:
George B. Simbachawene (Mb)
Waziri wa Nchi
29/03/2016.

Rais Magufuli Aagiza kufunguliwa kwa barabara ya Uwanja wa Ndege Mwanza -Igombe hadi Kayenze

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Dakta John Magufuli, ameagiza kufunguliwa kwa barabara ya Uwanja wa Ndege Mwanza -Igombe hadi Kayenze yenye urefu wa km.7 iliyofungwa kupisha upanuzi wa uwanja huo tangu mwaka 2014 na kusababisha usumbufu kwa wananchi waliokuwa wakiitumia hususan wa wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Rais Dakta Magufuli ametoa kauli hiyo mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mwanza kabla ya kuelekea nyumbani kwake wilayani Chato mkoani Geita kwa mapumziko wakati akizungumza na viongozi wa serikali wa mkoa wa Mwanza, vyama vya siasa, madhehebu ya dini, wananchi na waandishi wa habari waliokuwepo kumpokea uwanjani hapo.

Dakta. Magufuli amemwambia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, kuwa anatumia fursa hii kukuagiza kufunguliwa kwa barabara hiyo ambayo anatambua inapita pembezoni mwa uwanja wa Ndege wa Mwanza lakini serikali itaangalia juu ya kuupanua zaidi kuelekea eneo la mashariki ili kutoa nafasi ya barabara kutumiwa na wananchi wa maeneo haya.

 "Nafahamu suala linalowaumiza wananchi la kufungwa kwa barabara ya Airpot-Igombe  yenye urefu wa km7, sasa naagiza kuanzia sasa  kufunguliwa kwa barabara hiyo ili wananchi watumie kupita ili kuondoa usumbufu wa kuzunguka kule maeneo ya Nyakato hadi maeneo ya TX Kata ya Bugogwa, Kata ya Sangabuye,”alsema.

Dakta magufuli amesema serikali katika bajeti ya mwaka 2016/2017 imepanga kutoa fedha kwa lengo la kuhakikisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza unaoboreshwa kuwa wa kisasa ili kuwezesha ndege kubwa kutua kwa wingi lakini pia kutumiwa kimataifa na nchi za Maziwa Makuu kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015.

Aidha amesisitiza kwa kusema kuwa “kamwe sitaki kusikia tena uwanja huu umefungwa na uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) kuangalia kuupanua zaidi kwenda mashariki ili barabara hii pia waitumie wananchi na tutatoa fedha ili ijengwe kwa kiwango cha lami hata kama ni kwa awamu,”

Baada ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Mwanza, ghafla Rais Dakta Magufuli alitoka nje na kuelekea eneo la mighahawa iliyopo nje ya uwanja wa ndege wa Mwanza na kuingia katika moja ya mghahawa na kusalimiana na wateja na wananchi waliokuwa katika maeneo hayo kisha kuagiza chakula na kula pamoja na kuagiza kupewa vinywaji baridi kwa wananchi waliokuwepo eneo hilo.

Kutokana na tukio hilo baadhi ya wananchi waliokuwepo katika eneo hilola mgahawa ambao alikuwa anapata chakula na baadhi ya viongozi wakiwemo madhehebu ya dini na serikali, wameeleza kufurahishwa kwao na hatua hiyo huku mmiliki wa mgahawa huo  akiahidi kubadilisha jina la mghahwa wake na kuupatia jina la Dk Magufuli Cafe ili kuenzi kufika kwake na kula chakula hapo ukizingatia kuwa ni kiongozi mkubwa wanachi.

Huku viongozi wa madhebu ya dini wakiendelea kumuombea sala na dua ili kuendelea kuwatumikia watanzania bila kuchoka na kuhakikisha amani na umoja wa taifa unaendelea kuwa tunu, lakini pia katika dua na sala zao wamemuhakikishia Rais Dk Magufuli kuendelea kumuombea na kumpatia ushirikiano wao ili aweze kutekeleza majukumu yake akiwa na nguvu na afya njema.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mara baada ya kusalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea alipowasili majira ya saa uwanjani hapo majira ya asubuhi ghafla Rais magufuli alikwenda eneo walipokuwa wamesimama watumishi wa uwanja huo na kuwasalimia kwa kushikana nao mikono.

Nao abiria waliokuwa wakisubiri kusafiri na ndege kuelekea jijini Dar es salaam na Bukoba na kwingineko walifurahi kumuona Rais Dk Magufuli na kuchangamkia kusalimiana nae kwa kushikana naye mikono na kuonyesha furaha kwa kitendo hicho cha kumuona kiongozi wao huku baadhi wakidai ni jambo lisilo la kawaida.

Rais Dk Magufuli aliwapongeza kwa sala na dua viongozi wa madhehebu kwa kuendelea kumuombea ili kuweza kuwatumikia wananchi bila kuwabagua kwa itikadi zao za kisiasa na kusisitiza kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufanya kazi bila kuchoka ili kila mtanzania aweze kunufaika na rasilimali zilizopo nchini kisha kuomba ushirikiano kwa wananchi wote ili kufikia malengo.

Kurugenzi ya Mwasiliano ya Rais, IKULU
Dar es salaam
29 Machi, 2016

Picha 5 za Rais Magufuli Alivyojumujika na Wananchi Kupata chakula Kwenye Mgahawa Uwanja wa Ndege Mwanza

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakijipatia chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi.
  
Pamoja nao mezani hapo ni Meya wa Ilemela Mstahiki Renatus Mulunga, Meya wa jiji la Mwanza Mstahiki James Bwire, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Mhe John Mongella na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Ndg Anthony Diallo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakiondoka baada ya kupata  chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi.

Rais Magufuli Awataka Watanzania Waepuke Misaada ya Masharti Toka kwa Wazungu.....Pia ameahidi Kuwapunguzia Kodi Wafanyakazi Hadi Asilimia 10 au 9

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefika nyumbani kwake katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais, ambapoakizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato, ametoa wito kwa kila mtanzania kuchapa kazi kwa juhudi ili nchi iondokane na utegemezi wa misaada ya wafadhili ambayo huambatana na masharti.

Dkt. Magufuli amesema jukumu kubwa lililo mbele ya watanzania kwa sasa, ni kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake pa kazi.

"Kwa hiyo ni lazima tujisimamie sisi wenyewe, na tukijisimama sisi wenyewe kwa kila mmoja kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi afanye kazi kwelikweli, kama ni mkulima afanye ukulima wake kwelikweli, kama ni mfanyabiashara afanye biashara kwelikweli, kama ni mfugaji afuge kwelikweli, kama ni mvuvi avue kwelikweli, Tanzania hii tutavuka" Amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema serikali yake imeamua kuchukua hatua kudhibiti nidhamu serikalini, kwa kuhakikisha inawachukulia hatua watumishi wa umma wanaolisababishia taifa upotevu mkubwa wa fedha, na ameahidi kuwa hatua hizo maarufu kwa jina la "Kutumbua Majipu" zitaendelea kuchukuliwa hadi tatizo hilo likomeshwe.

Dkt. Magufuli pia amekumbusha viongozi wote wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi, kutekeleza wajibu wao ipasavyo na ameweka bayana kuwa mahali popote ambapo hapatakuwa na ufanisi, kiongozi husika atakuwa amedhihirisha kuwa hatoshi kuendelea na wadhifa aliopewa.

Rais Magufuli amewapongeza walimu kote nchini kwa kufanya kazi nzuri ya kufundisha, licha ya changamoto ya ongezeko kubwa la wanafunzi waliojiunga darasa la kwanza mwaka huu, lakini ametaka Wazazi na kamati za shule kushirikiana na walimu kuwasimamia wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

"Niziombe kamati za shule zote Tanzania nzima, kama haziwezi kusimamia nidhamu ya wanafunzi shuleni, zile kamati za shule zijiuzulu. Lakini pia kama wewe ni Mwalimu Mkuu, shule yako kila siku inatoa divisheni ziro nyingi kila mwaka, sioni sababu ya wewe kuendelea kuwa Mwalimu Mkuu" Alisisitiza Dkt. Magufuli.

Kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa, Rais Magufuli amesema uhakiki mdogo uliofanywa hivi karibuni, umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa wakilipwa shilingi bilioni 1 na milioni 800, na kwamba ni matarajio kuwa uhakiki unaofanywa nchi nzima utaisaidia serikali kubaini wafanyakazi hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi za watanzania.

Ametolea mfano wa mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17, na kueleza kuwa mfanyakazi huyo atafikishwa mahakamani.

Pia Rais Magufuli amesema serikali yake imejiandaa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo, lakini amesema kwa wale wanaolipwa mishahara mikubwa ambayo inafikia hadi shilingi milioni 40, itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha mshahara usiozidi shilingi milioni 15.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images