Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

RC Makonda Aitisha Kikao na Walimu ili Kujadili Matatizo Yanayowakabili

$
0
0

Mkuu  wa Mkoa  wa  Dar  es  Salaam  Paulo  Makonda  amemwagiza Ofisa Elimu,Raymond  Mapunda  kuitisha  mkutano  wa  walimu  March 26 mwaka  huu ili  kujadili matarizo  yanayowakabili likiwemo  la  kutopanda  madaraja  kwa  wakati.

Makonda  aliyasema  hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akikabidhi  madawati 500 katika shule  ya  msingi  Kawawa yaliyotolewa  na  kampuni  ya  simu  za  mkononi  ya  Tigo.

Mkuu huyo alieleza kuwa yapo matatizo mengi  yanayowakabili walimu yanayotokana  na  watu  wanaojinufaisha matumbo  yao kwa kuwalipa walimu hewa

Katika hatua nyingine,Makonda aliwataka walimu kutovunjwa moyo kutokana na matatizo yaliyopo katika sekta  ya  Elimu.

Naye mkurugenzi wa kampuni ya Tigo,Diego Gutierrez alisema kuwa mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni ya Tigo kuunga mkono jitihada za serikali katika kuleta  maendeleo ya elimu nchini


RC Kijuu: Watumishi HEWA Anzeni Kujiondoa Kabla Sijawakamua Majipu

$
0
0

Mkuu  mpya  wa  Mkoa  wa  Kagera,Meja  Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amewaagiza  watumishi  wasio  na  sifa za  kuajiriwa kujiondoa  kabla  ya March  31  mwaka  huu.

Kijuu  alitoa  kauli  hiyo  jana  wakati  wa  Makabidhiano  ya  ofisi baina  yake  na  mkuu  wa  mkoa  wa  zamani,John Mongella ambapo alisema  kwamba  Tanzania  inawatumishi  hewa  zaidi  ya 2000, hivyo ana imani  hata  Kagera  wapo.

"Hao watumishi  hewa  endapo  watang'ang'ania kubaki katika vitengo  walivyopo  nitawashughulikia wahusika  wakuu  wa  vitengo  hivyo," alisema

Aidha, aliagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kusimamia uundwaji wa mabaraza  ya  usuluhishi kuanzia ngazi za kata hadi  mkoa  ili  kusimamia  haki  za  wananchi.

Pia  aliwataka  watumishi  wa  serikali  mkoani  humo kufahamu maudhui ya "Hapa Kazi Tu", kwa kufanya kazi kwa kasi,haraka, nguvu, maarifa  na  uadilifu.

Aliwataka  kutosubiri  kusukumwa, lakini wajitambue wao ni akina  nani na  wanapaswa  kufanya  nini  kutokana  na  majukumu  waliyopewa.

Alisema  ili  kufikia  lengo  la  Rais John Magufuli la kuwatumikia wananchi  kwa  uaminifu  ni  lazima  kushikiria  uadilifu  na  kutambua  kwamba watumishi wapo kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii.

Zanzibar Yasema Iko Tayari Kufa Njaa Kuliko Kuwanyenyekea Wazungu Wanaoponda Uchaguzi wa Marudio

$
0
0

Licha ya Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) kueleza kusikitishwa kwao na uchaguzi wa marudio Zanzibar kufanyika bila kuwapo maelewano ya pande zinazokinzana, baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia kushiriki, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema iko tayari kufa njaa kuliko kukubali kuingiliwa uhuru wake.

Juzi, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, alimtangaza Dk. Ali Mohamed Shein, mshindi wa uchaguzi wa marudio uliofanyuika Jumapili iliyopita, kwa kura 299,982 sawa na asilimia 91.4, hatua iliyozifanya balozi mbalimbali nchini kueleza maskitiko yao na kusisitiza kuwa ni lazima mchakato wa uchaguzi uwe jumuishi na unaowakilisha kwa dhati matakwa ya watu.

Tamko la mabalozi hao lilitolewa na wawakilishi wa nchi za Ubelgiji, Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Hispania, Sweden, Switzerland, Uingereza na Marekani.

Wakati kauli ya mabalozi hao ikizua hofu kuwa huenda Zanzibar na  Tanzania kwa ujumla ikakatiwa misaada na mikopo kutoka nje, kwa madai ya kupindishwa kwa demokrasia, SMZ imetoa msimamo kwamba haitazipigia magoti nchi wahisani na kwamba imeanza kujipanga  kujitegemea kwa mapato ya ndani katika bajeti yake.

Msimamo huo wa SMZ, ulitolewa jana kwa nyakati tofauti na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed, na Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Omary Yusuph Mzee,  walipozungumza  kuhusu msimamo wa EU, Marekani na washirika wao kusikitishwa na kurudiwa uchaguzi kabla ya kupatikana muafaka wa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana.

Aboud alisema uchaguzi wa marudio umefanyika Zanzibar ikiwa utekelezaji wa masharti ya katiba na sheria na haikuwa muafaka kwa wahisani kuhoji kufanyika kwake.

“Kitendo wanachokifanya washirika wetu wa maendeleo hakikubaliki katika misingi ya utawala wa sheria. Wanaingilia mambo ya ndani wakati Zanzibar ni nchi huru,”alisema Aboud.

Alisema uchaguzi wa Zanzibar unaendeshwa kwa kufuata masharti ya katiba na sheria ya uchaguzi namba 11 ya mwaka 1984 na si maridhiano ya vyama, kama wanavyotaka wahisani.

Aboud alisema Zanzibar iko tayari kushirikiana na washirika wa maendeleo, lakini lazima misaada izingatie utu na heshima ya nchi kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake.

“Zanzibar ni nchi huru na itaendelea kuwa huru. Tuko tayari kupokea misaada inayozingatia utu na heshima kwa Zanzibar na wananchi wake kinyume cha hivyo tuko tayari kufa njaa,” alisisitiza.

Naye Mzee kwa upande wake, alisema jana ofisini kwake, Vuga, visiwani hapa kuwa hategemei hilo kutokea katika kipindi cha miaka mitano kuanzia sasa.

Alisema lengo la serikali kwa sasa ni kuhakikisha inaondokana na utegemezi wa wafadhili na kwamba imeanza kuweka mikakati maalum,  kuhakikisha inajitosheleza kwenye bajeti yake.

Alisema miongoni mwa mikakati inayotarajiwa kufanywa kutimiza lengo hilo ni kuanza kuiga mfumo anaoutumia Rais John Magufuli wa kufuta safari zisizokuwa za lazima kwa viongozi wa serikali.

Aliongeza kuwa mikakati mingine ni kuhakikisha wagonjwa wanaotakiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, wanapata huduma hiyo nchini kwa kuandaa mipango maalum ya kuleta madaktari.

Mzee ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema Zanzibar inatarajia kutumia mapato yake ya ndani kujitosheleza kwenye bajeti yake.

Alisema Rais Dk. Shein juzi alitoa msimamo wa serikali wa kutaka iwekwe mikakati itakayowezesha Zanzibar kujiendesha kwa bajeti yake bila wafadhili.

Mzee alisema Zanzibar inategemea asilimia 20 ya misaada kwa ajili ya kukamilisha bajeti yake kila mwaka pamoja na mikopo kutoka taasisi za fedha, zikiwamo benki za nje.

Alisema bajeti ya Zanzibar inategemea asilimia 26 hadi28 ya mapato yanayotokana na sekta ya utalii wa ndani na nje na kwamba bado kunahitajika mikakati ili kupanua wigo wa kupata fedha.

Kwa mujibu wa Mzee,  Zanzibar inapokea watalii kati ya 300,000 na  400,000 kwa mwaka na kwamba wanatarajia kuongezeka baada ya kufungua ofisi za kuhamasisha utalii wa nje.

Alisema ofisi maalum za kuhamasisha utalii zimejengwa katika mji wa Mumbai, India na nchini China na kwamba kwa sasa watalii wanatoka moja kwa moja kwao na kufikia Zanzibar.

Kwa upande wa ukuaji wa uchumi wa Zanzibar, Mzee alisema unatarajia kukua kwa asilimia 8 hadi 10 kwa mwaka na kwamba tofauti za kisiasa zilizopo Zanzibar haziwezi kuathiri mipango ya serikali.

Katika hatua nyingine, waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Ali Ameir Mohamed, alisema haikuwa muafaka EU na Marekani kusikitishwa na kufanyika kwa uchaguzi wa marudio.

Alisema ZEC ilikuwa na kila sababu za kuitisha uchaguzi wa marudio ili kukamilisha masharti ya katiba, baada ya uchaguzi wa awali kuvurugika.

Mwanasiasa huyo alisema matatizo ya kisiasa ya Zanzibar yaliachwa na wakoloni wenyewe kutokana na matabaka waliyokuwa wameyajenga kabla ya kufanyika kwa Mapinduzi ya Januari 12, 1964.

Alisema wahisani jukumu lao kubwa ni kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika nchi wanazoziwakilisha na si kuingilia mambo ya ndani.

Credit: Nipashe

CCM na CUF Watwangana Ngumi Pemba Wakati Wakisherehekea Ushindi wa Dr. Shein

$
0
0

Jeshi la Polisi jana walitumia mabomu ya machozi kurejesha hali ya amani baada ya wananchi kuanza kupigana kwa sababu za kisiasa wakati wakisherehekea ushindi wa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, katika kijiji cha Mjini Wingwi Wilaya ya Micheweni, Pemba.

Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Micheweni, Rashid Khalid Salim, alidai vurugu hizo zimesababishwa na wanachama wa CCM kutoka katika kijiji cha Kwale wilayani humo.

Alisema baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa marudio, wanachama wa CCM katika kijiji cha Kwale, walianza kukusanyika na ngoma zao na kuanza safari ya kuingia katika kijiji cha Mjini Wingi, sehemu ambayo ni ngome ya wanachama wa CUF, huku wakisherehekea kwa kurusha 'vijembe' (maneno ya kejeli) na matusi.

“Pamoja na kutakiwa kuacha matusi wakati wakisherehekea ushindi wa Dk. Shein, waliendelea na kusababisha wenzao kupandwa na ghadhabu kuwachemka na kuanza kupigana,” alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema baada ya kutokea vurugu hizo, wanachama wa CCM kutoka kijiji cha Kwale, walilazimika kukimbilia Kituo cha Polisi Micheweni.

Alisema askari walipofika eneo la tukio, walianza kupiga mabomu ya kutoa machozi na kuvunja milango ya nyumba.

Mwenyekiti huyo alisema nyumba 15 zilivunjwa milango wakati wakiwasaka watu waliokuwa wakihusishwa na vurugu hizo ambazo zilianza kufanyika saa 10:00 jioni na kuendelea hadi usiku juzi.

Aidha, alisema kwa mujibu wa mabaki ya milipuko, jumla ya mabomu 27 yanadaiwa kupigwa mbali na nyumba kuvunjwa milango na kusababisha watu zaidi ya 28 kuyakimbia makazi yao katika kijiji hicho.

“Watu wanne wamekamatwa akiwamo mtoto mwenye umri wa miaka 13, lakini wananchi wengi wamekimbia makazi yao na kukimbilia katika kisiwa cha Kojani na Maziwang'ombe,” alisema Rashid.

Hata hivyo, alisema jambo la kushagaza polisi wameamua kuwakamata watu waliofanyiwa fujo badala ya kuwakamata waliokuwa chanzo cha vurugu hizo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kwamba watu watano wanashikiliwa kwa uchunguzi wa kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo, alikanusha kuvunjwa milango 15 pamoja na kutumika mabomu 27 kurejesha hali ya utulivu baada ya wananchi kuanza kupigana.

Waliokamatwa katika mkasa huo ni Kombo Khalfan Faki, Salim Hassan Khamis, Mjawiri Faki, Khatib Dawa Juma na Assaa Bakar Ali, wakazi wa kijiji hicho.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa huo, Omar Khamis Othman, alisema hali katika kijiji hicho imerejea kuwa ya kawaida na kuwataka wananchi kuendelea na sherehe za kumpongeza Dk. Shein bila ya kuvunja sheria.

Alisema wananchi waliokimbia makazi yao na kukimbilia katika kisiwa cha Kojani na Maziwang'ombe, watakuwa ndiyo waliohusika na vurugu na kwamba raia mwema hana sababu ya kukimbia askari.

Maalim Seif: CUF haitashiriki uchaguzi wowote chini ya Tume ya Jecha Salim Jecha

$
0
0

SIKU mbili tangu kufanyika kwa uchaguzi wa marudio Zanzibar, na siku moja kabla ya kuapishwa Dk Ali Mohamed Shein, Maalim Seif Shariff Hamad, Mgombea wa Urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana kupitia Chama cha Wananchi (CUF), amesema CUF haitashiriki uchaguzi wowote chini ya Tume ya Jecha Salim Jecha.

Akizungumza katika Hoteli ya Serena ambapo yupo kwa mapumziko baada ya kulazwa, Maalim Seif amesema kuwa kama yatatokea maridhiano yatakaoongozwa na kusimamiwa na taasisi huru za kidemokrasia, bila vitisho vya majeshi na polisi, kuwa na vyombo huru vya habari na tume huru sio hii iliyopo Zanzibar chini ya Jecha, hapo CUF kitaweza kufikiri kushiriki uchaguzi.

Ameongeza kuwa harakati za kudai haki, zitaendelea kwa njia ya amani ili marekebisho ya tume yafanyike kwani kwa utaratibu uliopo hata mwaka 2020 upinzani ukishinda Tanzania bara, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitang’gang’ania madaraka.

“CUF tunaamini katika amani, tusichafue amani, tusichafue nchi yetu, tuendeleze mapambano kwa kutoitambua serikali iliyojiweka madarakani katika uchaguzi haramu wa Machi 20 mwaka huu, wala hatutaipatia ushirikiano wowote katika mambo yote” alisema na kuongeza :

"Uchaguzi wa 20 Machi, sio halali. Jecha hakuwa na uwezo wa kisheria wala kikatiba kufuta uchaguzi, mgogoro uliopo sasa umesababishwa na Jecha, ukapewa baraka za CCM, sababu CCM hawataki kushindwa, na hawataki wapinzani kuongoza. Kila CCM ikishindwa hutoa visingizio.

“Kabla Kikwete (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) hajaondoka madarakani, aliniambia kuwa Maalim CCM wanakuogopa, wanajua ukishinda utaweza kuvunja Muungano, lakini nilimwambia, CCM ndio wenye jeshi, wenyewe ndio wenye dola mimi nitavunjaje Muungano?

"Hiyo ni hofu na visingizio tu ili waendelee kukwapua madaraka.”Alisema.

Ameweka bayana kuwa kwa sasa CCM imewarejesha wananchi miaka 20 iliyopita, kwani uhasama wa watu kutengana kwenye shughuli za kijamii kwa sababu za tofauti za kisiasa zimeanza kurejea baada ya CCM kulazimisha kukwapua madaraka ya wananchi kwa kufuta uchaguzi wa 25 Oktoba mwaka jana.

Akizungumzia suala la Muungano kama ambavyo amekuwa akihusishwa Maalim seif amesema kuwa sasa Muungano utavunjwa na CCM, sio CUF wala yeye kama wanavyosingizia.

Ameongeza kuwa kwa sababu CCM ya bara ndio inalazimisha kuweka viongozi waliokataliwa na wananchi wa Zanzibar na chama chao kwa kutumia majeshi na polisi wao ndio husababisha wananchi wachukie Muungano.

Aidha kuhusu uchaguzi wa marudio wa Machi 20, Seif amesema kuwa CUF imeshinda, kwani wananchi wa Zanzibar waliitikia wito wa CUF, wakasusa, hawakujitokeza kupiga kura.

“Mimi nilishasema tangu awali, kuwa matokeo yameshajulikana kabla ya uchaguzi, sababu ni ya kupika, namhurumia Dk Shein kwa kujisifu kupata kura ambazo hazipo, mawakala waliweka wao na wasimamizi na kuna taarifa kuwa wapigakura walikuwa wanapewa rundo la kura, wapige na kutumbukiza ili kukidhi matakwa ya CCM.” Amesema Maalim Seif.

Maalim Seif amewatakia utulivu Wazanzibar wote, na kuwaarifu kuwa afya yake ni imara, na atarejea Zanzibar wakati wowote kuungana nao.

Wananchi Mwanza waandamana kupinga kuuzwa kwa Mlima wa Buyombe.

$
0
0
Mamia ya wakazi wa mtaa wa Buyombe Kata ya Kahama jijini Mwanza wakiwa na silaha za jadi,wameandamana kupinga vikali kuuzwa kwa Mlima wao kunakodaiwa kufanywa na baadhi ya watumishi wa idara ya ardhi na mipango miji ya jiji hilo kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo cha elimu ya biashara,kampasi ya Mwanza huku baadhi yao wakionyesha hasira zao baada ya kuanza kung’oa vigingi vyote pamoja na mabango ya Chuo hicho.

Wakazi hao wanasema kuwa hawako tayari kuchangia shilingi elfu hamsini kwa kila kaya kwa ajili ya ujenzi wa shule yao ya msingi kwani zaidi ya shilingi milioni mia sita zilizotokana na mauzo ya mlima huo kwa chuo cha elimu ya biashara kampasi ya Mwanza pamoja na wananchi wengine zinatosha kabisa kugharimia miundombinu ya huduma za kijamii kama vile shule,zahanati,maji ya bomba na Barabara.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Buyombe,Emanuel Zambezi amesema madai ya wakazi hao yana mantiki kubwa.

ACT-Wazalendo Wamtaka Spika wa Bunge Kushughulikia Suala la Rushwa Kwa Wabunge Waliotuhumiwa

$
0
0
CHAMA cha ACT Wazalendo kimepokea kwa masikitiko uamuzi uliofanywa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, kwa kuhamisha kamati, Wenyeviti, Makamu Wenyeviti na Wajumbe wa baadhi ya Kamati za Kudumu za Bunge uliofanywa jana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa ACT Wazalendo, Yeremia Maganja, amesema uamuzi huu wa spika unafuatia kashfa nzito ya viongozi na wajumbe wa kamati mbalimbali za Bunge kupokea rushwa kutoka mashirika tofauti ya umma kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari

Amesema bunge ni mhimili wenye jukumu la kuisimamia serikali , hivyo baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) walimwandikia barua za kujiuzulu Spika wa Bunge, Job Ndugai ili kupisha uchunguzi ufanyike na wataobainika kupokea rushwa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Maganja amesema ACT Wazalendo imempongeza Mbunge wao na Wabunge wengine waliochukua hatua ya kujiuzulu ujumbe kwenye kamati zao ili kupisha uchunguzi.

Aidha amesema kuwa uamuzi huo wa mbunge wao unakwenda sambamba na misingi ya Chama cha ACT Wazalendo ya uadilifu na uwajibikaji.

Amesema mabunge yaliyopita, kamati za Bunge zimekuwa zikituhumiwa mara kadhaa kujihusha na vitendo vya kupokea rushwa kutoka kwa Mashirika ya Umma, Makampuni na watu binafsi.

Maganja amesema rai zimekuwa zikitolewa mara kwa mara huko nyuma ya kuitishwa kwa uchunguzi ili kulinda hadhi na heshima ya Bunge ilipuuzwa na matokeo yake, kashfa hizi zimeliondolea heshima Bunge na Wabunge.

Amesema kwa mujibu wa Ibara ya 63(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bunge ndiyo chombo kikuu chenye madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na kuishauri serikali na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake.

Kinapotuhumiwa kupokea rushwa, kinawezaje chenyewe kuisimamia serikali na kuongoza mapambano dhidi ya rushwa?

Maganja amesema uamuzi wa kuwahamisha Kamati viongozi na wajumbe wa Kamati zilizotuhumiwa kupokea rushwa ni sawa na kuufunika uozo na kuendeleza utamaduni mbovu wa siku nyingi hapa nchini wa kuwahamisha au “kuwapangia kazi nyingine” viongozi na watumishi wa umma wanaotuhumiwa kupokea rushwa au kukosa ufanisi.

Kimsingi Utamaduni huu unafifisha mapambano dhidi ya rushwa na uwajibikaji.

Mwenyekiti huyo amemtaka Spika kuonyesha kwa vitendo jinsi ofisi yake inavyochukizwa na vitendo vya rushwa nchini kwa kuitisha uchunguzi utaovishirikisha vyombo vya dola ili ukweli ujulikane.

Wito wa Kufanya Usafi Kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi

$
0
0
Watanzania Wenzangu mtakumbuka kwamba tulikubaliana tuwe tunafanya usafi wa mazingira yetu nchi nzima kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuitikia wito wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliouanzisha tarehe 09 Desemba 2015.

Nachukua nafasi hii kuwasihi Watanzania wote kushiriki kikamilifu kufanya Usafi wa Mazingira kwenye Makazi yetu, Maeneo yetu ya Biashara, maeneo ya Taasisi za Umma na maeneo yenye mikusanyiko ya watu mbalimbali kama masokoni na minadani.

Mbali ya kwamba kufanya usafi kuna fanya mazingira yetu yapendeze na hivyo kuondoa magonjwa yanayo sababishwa na uchafu lakini pia zoezi la kufanya usafi kwa pamoja lina jenga Umoja na Mshikamano wa kitaifa, linaondoa matabaka ndani ya jamii yetu.

Natoa wito kwa kila Mtanzania Kujitokeza kufanya usafi bila kujali uwezo wa mtu,hadhi yake,cheo chake, au nafasi yake katika jamii. Viongozi wa makundi yote katika jamii tuwe mfano katika jambo hili jema.

Nichukue fursa hii kusisitiza tuendelee kujitokeza kufanya Usafi ili Utamaduni huu ujengeke kwa Kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

Watanzania wote wa Mijini na Vijijini tujenge desturi ya kuweka mazingira yetu katika hali ya usafi wakati wote na katika jambo hili kila mmoja wetu awe mlinzi wa kukemea watu wenye tabia za kutupa taka hovyo ili maeneo yetu yawe katika hali ya usafi na yakuvutia wakati wote.

Usafi kwenye nyumba na mazingira yako,Usafi kwenye sehemu ya Shughuli zako na mazingira yake ndio usafi wa Taifa. Tujitokeze,Tuungane tukafanye Usafi kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi kuanzia saa 12 Asubuhi
Asanteni.

Imetolewa na:
George B. Simbachawene (Mb)
WAZIRI WA NCHI
OFISI YA RAIS - TAMISEMI

Ufafanuzi Wa Mapato Na Matumizi Ya Serikali Kwa Mwezi Machi, 2016

$
0
0


A:  MAPATO
(i) Mapato ya kodi (TRA) shilingi 1,283,274,000,000
(ii)Mapato yasiyo ya kodi shilingi 77,504,000,000
(iii)Mapato yatokanayo na vyanzo vya Halmashauri shilingi 43,490,000,000
 
Jumla shilingi 1,404,268,000,000
 
(iv) Tunatarajia pia kupata mikopo na misaada ya mifuko ya Basket na miradi ya maendeleo kutoka kwa washirika wa maendeleo shilingi 71,200,000,000

B: MATUMIZI
1.  Mishahara
(a) Watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa shilingi 484,057,177,680 ikijumuisha malimbikizo ya shilingi 9,479,389,384 na hasa kwa walimu katika Halmashauri 154

(b) Watumishi wa Taasisi na Wakala za Serikali shilingi 97,985,822,320 ikijumuisha malimbikizo ya shilingi 518,822,320 kwa Taasisi na Wakala 24 na hasa sehemu kubwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 
Jumla ya mishahara ni shilingi 582,043,000,000
 
2.Posho ya chakula kwa ajili ya vyombo vya ulinzi na usalama shilingi 43,556,500,000.
3.Ruzuku ya Vyama vya Siasa shilingi 1,433,583,000
 
4.Posho ya Madaktari wanafunzi 1608 shilingi 1,721,000,000.
5.Wizara ya Afya Ununuzi wa madawa na vifaa tiba shilingi 2,597,961,000
 
6.Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa semista ya tatu shilingi 57,040,000,000
 
7.Kutekeleza mpango wa Elimu bure shilingi 18,777,000,000
8.Mapato ya ndani kwa Halmashauri kwa ajili ya miradi na uendeshaji wa ofisi shilingi 43,490,000,000
 
9.Madeni ya watumishi wasio walimu katika Halmashauri  shilingi 3,618,900,612
 
10.Miradi ya umeme shilingi 73,252,000,000
- Wakala wa Umeme Vijijini shilingi 24,020,000,000
-  Mradi wa Umeme Kinyerezi I shilingi 43,800,000,000

-Mradi wa kufua umeme makambako – Songea shilingi 5,482,000,000

11.Malimbikizo ya madeni ya Makandarasi wa barabara shilingi 166,905,919,730
 
12.Miradi ya Maji shilingi 10,951,000,000
13.Mfuko wa Reli shilingi 2,651,000,000
14.Fidia kwa wananchi kupisha mradi wa Kurasini Trade and Logistic Hub shilingi 3,048,904,930
 
15.Mradi wa Ununuzi wa dawa na vifaa Tiba (ORIO) shilingi 2,106,657,644

16.Mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo shilingi 5,124,997,500

Askari Watatu Wasimamishwa Kazi Kwa Tuhuma za Wizi Uwanja wa Ndege

$
0
0

Serikali imewasimamisha kazi Maafisa 3 wa Jeshi la Kikosi cha Zimamoto kwa tuhuma za kushiriki wizi wa mafuta ya Ndege na mmoja kati yao kuiba mizigo ya wateja kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport.
 
Akizungumza katika Ziara ya kushitukiza aliyoifanya katika Viwanja vya Ndege vya Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mh.Mhandisi Hamad Masauni amewataja walio simamishwa kazi ni Khalfani Kisana na Mussa Mandauli ambao walikamatwa na madumu 10 ya mafuta ya Ndege wakiwa na gari la Serikali lenye usajiri STJ 2948 huku askari mwingine aliyejulikana kwa jina la Abas Mwanza akishutumiwa kwa kosa la kushirikiana na mfanyakazi wa Swissport |Lucas Maganda kwa kosa la kuiba mzigo wa abiria.

Akiwa katika kiwanja hicho Mh.Masauni amekagua utendaji kazi katika idara ya Uhamiaji,Polisi na Jeshi la Zimamoto na kuagiza viongozi wa idara hizo zilizopo chini ya Wizara yake kufanya kazi kwa uaminifu na yeyote atakayekiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Picha 10 za Maandalizi ya Kumwapisha Rais mteule wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein katika uwanja wa Aman Kesho Alhamisi March 24

$
0
0
Maandalizi ya kumwapisha Rais Mteule wa Zanzibar hapo kesho  katika uwanja wa Aman Zanzibar yamekamilika. Mpekuzi Blog itakujuza kila kitu. Endelea kuwa nasi

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya March 24

Waziri Mkuu Majaliwa Akutana Na Wawekezaji Wa Sukari Kutoka India

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na ujumbe wa Wawekezaji kutoka India wanaokusudia kuwekeza katika kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari hapa nchini, Ofisini kwake jijini Dar es salaam machi 23, 2016. 

Kushoto kwake ni Waziri wa Kilimo, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Waziri Nape Atuma Salam Za Rambirambi Kufuatia Kifo Cha Aliekuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe, Marehemu Sara Dumba

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa  wanahabari wote kufuatia kifo cha ghafla cha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe na  Mtangazaji Mwandamizi wa zamani wa Redio Tanzania (RTD), Dar es salaam  Marehemu Sara Dumba.

“Pokeeni salamu za rambirambi zangu za dhati kwa kuondokewa na  Mwanahabari  mahiri Bi. Sara Dumba aliyekuwa mfano wa kuigwa” amesema Mhe. Nape.

“Mbali na utangazaji wake mahiri, Bi. Sara Dumba alikuwa mzalendo wa kweli aliyetumikia tasnia hii ya Habari na Serikali kwa uadilifu na upendo wa kweli, tutamkumbuka na tutaukosa mchango wake. Ni wajibu wetu kumuombea mapumziko mema kwa mwenyezi Mungu na kumshukuru kwa mchango wake alioutoa kwa moyo wa dhati”.

“Hakika Sara tutamkumbuka, nawapa pole wananchi wote wa wilaya ya Njombe kwa kuondokewa na kiongozi wao mpendwa  mwenzao”,ameongeza Waziri Nape.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante  Ole Gabriel  naye ametuma salamu hizo “Salaam ziwafikie familia, ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu ambao unawagusa sana, naelewa machungu waliyonayo na huzuni, hata hivyo kwa pamoja ni wakati wa kuzidi kumuombea Marehemu katika safari yake ya mwisho”,amesema Profesa Elisante na kuwatakia moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Baadhi ya wafanyakazi wenzake waliowahi kufanya kazi  pamoja naye ambao ni Aloisia Maneno amesema Bi. Sara alikuwa mwalimu wake katika masuala ya utangazaji kwa kuwa ndiye aliyemfundisha jinsi ya kuandaa kipindi cha watoto  cha Cheichei  Shangazi.

Abdul Ngarawa  amesema kuwa Bi. Sara alikuwa mchapakazi hodari, mtu mwenye kipaji cha utangazaji, mcheshi, mtu mwenye ushirikiano na wafanyakazi wenzake na jasiri asiyeogopa kusema ukweli hata kwa wakuu wake wa kazi pale ambapo kazi hazikufanyika vizuri.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Hajjat Halima Kihemba akizungumzia uhusiano wake na marehemu amesema kwamba yeye alianza kazi RTD  mwaka  1971 ambapo Bi. Sara alimkuta tayari akiwa kazini kati ya mwaka 1974, hivyo walifanya naye kazi pamoja kwenye Idhaa ya Kiingereza ya (External Services) marehemu akiwa  msaidizi wake.

   “Alikuwa ni mtu  mwenye mchango mkubwa na yuko tayari kufanya kazi wakati wote  unapomwihitaji usiku na mchana, mshauri hususan kwa watoto wa kike kuacha kujidharau na kuona kwamba hawezi kufanya kazi ya taaluma ya habari na mtu aliyependa maendeleo.

Kwa  upande wake, Bakari Msulwa ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Kati Dodoma - TBC akimzungumzia  Bi.Sara Dumba amesema kuwa alihamishiwa mkoani Morogoro  mwaka 1990 akiwa mwakilishi wa RTD  na baade Mkuu wa Kanda ya Kati Dodoma  hadi alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi mwaka 2006 .Ameongeza kwamba ni mama aliyekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wanawake, aliandaa vipindi mbalimbali vya biashara na alikuwa yuko tayari kuambiwa ukweli.

“ Kwa kweli Bi. Sara alijenga historia nzuri katika tasnia  ya masuala ya habari na utumishi wa umma akiwa katika ngazi ya ukuu wa wilaya, hivi karibuni nilionana naye mkoani Tabora miezi miwili iliyopita alikuwa na mtazamo wa kuwaunganisha  wafanyakazi wa RTD  ili waweze kuwa na umoja utakaoweza kutupatia nafasi ya kusaidiana kwenye masuala mbalimbali,” Amesema  Msulwa.

 Msulwa amebainisha kuwa Bi. Sara alisema hayo baada ya  kubaini kwamba  hakuna historia ya wafanyakzi wa RTD. Hivyo ameacha changamoto  kwa hao  kuacha historia zao  ili  ziweze kuwa na manufaa kwa watu wengine.

Bi. Sara amefariki   dunia tarehe 21 Machi,  mwaka 2016 Wilayani Njombe,  baada  kuugua ghafla.  Alizaliwa Oktoba 19, 1956. Bi. Sara alianza kazi katika Radio ya Taifa, Radio Tanzania Dar-es-Salaam (RTD) na baadaye Shirika la Utangazaji Taifa (TUT) sasa TBC.

Marehemu  Sara Dumba kabla ya kuteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya mwaka 2006 alivuma katika kipindi cha Majira(yaani habari za hapo kwa hapo) na vipindi vingine vingi.

 Kwa mujibu wa taarifa za Katibu Tawala wa  Mkoa wa Njombe Jackson  Saikadau  amesema mwili wa marehemu  unatarajiwa kuagwa kesho Machi 24, mwaka huu  jijini Dares Salaam na kuzikwa nyumbani kwake eneo la  Mbutu  Mwembe Mdogo, Kigamboni.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amina.

IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
23, MACHI, 2016.

TRL Kusafirisha Saruji Ya Tanga Kwa Njia Ya Reli

$
0
0
Kiwanda cha Saruji Tanga (Simba Cement), kimeingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania (TRL), kusafirisha shehena ya saruji kwa njia ya reli kutoka mkoani Tanga kwenda mikoa ya Mwanza na Kigoma.

Chini ya Makubaliano hayo zaidi ya tani laki nne na nusu zitasafirishwa kwa mwaka na hivyo kupunguza gharama ya bei ya Saruji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Magharibi kutokana na usafirishaji wa reli kuwa wa bei nafuu.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema katika mkataba huo TRL litapata zaidi ya shilingi Bilioni 40 na hivyo kufufua huduma ya usafirishaji wa mizigo katika reli ya kati na kuongeza mapato kwa nchi.

Prof. Mbarawa amewataka wafanyabiashara nchini kuanza kutumia reli kusafirisha bidhaa zao, kwani usafiri huo ni salama na nafuu na unachukua shehena kubwa kwa wakati mmoja.

“Asilimia 95 ya mizigo hapa nchini inasafirishwa kwa barabara hivyo mkakati wa Serikali wa kufufua viwanda utafanikiwa kwa haraka endapo wasafirishaji watatumia njia ya reli “, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, amefafanua kuwa usafirishaji wa reli ukiimarika utapunguza ajali za barabarani zinazosababishwa na malori na kupunguza kasi ya uharibifu wa barabara unaotokea sasa kutokana na maroli kuzidisha uzito.

Prof. Mbarawa amewataka watumishi wa TRL na wananchi kulinda miundombinu ya reli na kutumia fursa ya usafiri huo kujiongezea mapato.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela amesema usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli utatoa fursa za ajira na kuwezesha bandari ya Tanga kupata shehena kubwa ya mizigo na hivyo kurudisha hadhi ya Mkoa wa Tanga.

“Tanga tuna reli, barabara na bandari hivyo tukio la kuanza kusafirisha mizigo kwa njia ya reli itaongeza shehena kubwa katika bandari ,itatengeneza ajira kwa wakazi wa Tanga na kukuza uchumi wa mkoa”, amesema Bw. Shigela.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRL) Bw. Masanja Kadogosa amesema kusainiwa kwa mkataba huo kutawezesha TRL kusafirisha tani elfu thelathini na tano za Saruji kati ya tani laki moja na elfu tano zinazozalishwa na kiwanda hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji Tanga Bw. Reinhart Swart, amesema usafirishaji wa Saruji kwa njia ya reli utaongeza kasi ya usafirishaji wa saruji na kuwezesha kuwafikia watumiaji kwa bei nafuu.

Kiwanda cha Saruji Tanga kinakuwa kiwanda cha kwanza kuingia mkataba na TRL kusafirisha shehena ya mizigo tangu Serikali kuanza mikakati yake ya kufufua reli na kupunguza usafirishaji wa shehena kubwa kwa njia ya barabara na hivyo kuzuia uharibifu wa barabara na kupunguza ajali.

Bunge Latoa Ufafanuzi Kuhusu Madiliko Yaliyofanywa Na Spika Kwa Baadhi Ya Wajumbe Wa Kamati Za Bunge

$
0
0

Kufuatia Mabadiliko ya Wajumbe kwenye Kamati za Kudumu za Bunge yaliyofanywa na Mhe. Job Ndugai (Mb) Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana tarehe 22 Machi, 2016; baadhi ya Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii imenukuliwa ikihusisha mabadiliko hayo kuwa yamefanywa kutokana na tuhuma za rushwa kwa baadhi ya Kamati za Bunge kufuatia ripoti ya chombo kimoja cha Habari. 

Ofisi ya Bunge inapenda kutoa ufafanuzi kuwa madai hayo hayana ukweli wowote, bali mabadiliko yaliyofanywa na Mhe. Spika ni ya kawaida na wala hayakuanisha dosari zozote katika Utendaji wa kamati za Kudumu za Bunge. 

Msingi wa Mabadiliko ya Wajumbe kwenye kamati, umelenga kuzingatia mahitaji mapya na changamoto zilizojitokeza baada ya kuunda Kamati hizo mwezi Januari 2016 ambapo alikuwa ameanza kufanyia kazi mabadiliko hayo tangu mapema mwezi huu. 

Waheshimiwa Wabunge wanaosakamwa kwa uvunjifu wa Maadili kupitia Mitandao ya kijamii na Magazeti, ni budi wakatendewa haki kwa sababu Mhe. Spika anazingatia sana Utawala wa Sheria na kama kuna Mbunge yoyote anaetuhumiwa kwa makosa ya Jinai, Mamlaka za kiuchunguzi zinawajibu wa kutekeleza majukumu yao na pale inapobidi, Bunge lenyewe kupitia kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inaweza kufanya uchunguzi kwa Mamlaka ya Spika. 

Aidha, ifahamike vyema kuwa, kwa mujibu wa Kanuni ya 116 (3) Mamlaka ya kufanya mabadiliko kwenye Kamati za Kudumu za Bunge ni ya Spika na anaweza kufanya hivyo wakati wowote kama alivyofanya mapema mwezi huu ambapo alizingatia maombi ya baadhi ya Wajumbe 15 kuhamia Kamati nyingine kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiafya kwa baadhi ya Wajumbe na pia kuboresha Utendaji wa Kamati hizo kama ilivyojitokeza jana kwa wajumbe 27 kuhamishiwa kamati zingine pia. 

Mhe. Spika anawasihi Wajumbe wote kuendelea kutekeleza majukumu yao kama kawaida katika kamati zao. 

Imetolewa na: 
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
23 Machi, 2016

Kiti cha UPDP chayeyuka Zanzibar....ZEC Yasema Yalifanyika Makosa ya Kiufundi Wakati wa Kujaza Karatasi ya Matokeo

$
0
0

Ofisa mdhamini wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Ali Mohammed Dadi amesema mshindi wa uwakilishi katika Jimbo la Ziwani ni Suleiman Ali wa CCM na si Asaa Hamad wa UPDP aliyetangazwa awali.

Dadi kutoka ofisi ndogo ya Pemba alisema jana kuwa msimamizi wa uchaguzi katika Wilaya ya Chakechake, Othman Hamisi alikosea wakati wa kujaza karatasi ya matokeo ya mshindi wa jimbo hilo.

“Nimezungumza naye na amesema kwamba alitoa ufafanuzi kuwa walifanya makosa katika kuandika matokeo, hivyo aliyeshinda ni mgombea wa CCM,” alisema.

Katika karatasi hiyo ya matokeo iliyokuwa imebandikwa ukutani, Asaa Ali Hamad alionekana kuwa amepata kura 221 dhidi ya 121 za mgombea wa CCM, lakini kwa ufafanuzi huo wa ZEC hakuna chama cha upinzani kilichoshinda nafasi ya uwakilishi au udiwani.

Kwa matokeo hayo, CCM imeshinda majimbo yote ya uwakilishi Unguja na Pemba na hivyo kuzidisha utata kwa Rais mteule, Dk Ali Mohamed Shein anayeapishwa leo, kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa mujibu wa ibara ya 9 (3) ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010.

Awali, kulikuwa na uwezekano wa UPDP kutoa mteule wa nafasi ya makamu wa kwanza wa Rais kwa kuwa kilitangazwa kimakosa kupata kiti cha uwakilishi baada ya CCM lakini baada ya ufafanuzi huo wa ZEC matumaini hayo yameyeyuka. 
 
Kuyeyuka kwa ndoto hiyo ya UPDP kunamaanisha kwamba hakuna chama kilichoshika nafasi ya pili kwa kupata kura asilimia 10 au zaidi, ambacho kwa mujibu wa Katiba hiyo kingekuwa na nafasi ya moja kwa moja kutoa makamu wa kwanza wa rais na baadaye mawaziri wa upinzani kuunda SUK. 
 
Tangu Dk Shein atangazwe kushinda urais katika uchaguzi wa marudio baada ya matokeo ya ule wa awali kufutwa, mjadala mkubwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umekuwa ni jinsi gani atateua Serikali yake kukidhi matakwa ya Katiba ya kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ili kuendeleza maridhiano ya kisiasa yaliyofikiwa baina ya CCM na CUF kabla ya uchaguzi wa 2010.

Wakati Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akisema Rais Shein atatumia busara zake kumpata makamu wa kwanza wa rais, baadhi ya wanasheria wamesema hawaoni ufumbuzi wa moja kwa moja kutokana na upungufu huo wa kikatiba.

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, Rais atateua makamu wa kwanza wa Rais kutoka chama kilichoshika nafasi ya pili na mgombea wake wa urais kupata asilimia 10 ya kura za urais, au nafasi ya makamu wa kwanza itaenda kwa chama chochote cha upinzani kilichoshika nafaso pili kwa wingi wa viti vya majimbo katika Baraza la Wawakilishi.

Uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji La Dar es Salaam Kufanyika Mapema Baada ya Sikukuu ya Pasaka

$
0
0

Baada ya kumpata Meya wa Jiji la Dar es Salaam, mchakato wa kumchagua naibu meya umeanza.

Juzi, Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), Isaya Mwita alichaguliwa kuwa umeya akimshinda mpinzani wake Yusuph Yenga (CCM) kwa kura 84 dhidi ya 67.

Akizungumza jana, Meya Mwita alisema tarehe rasmi ya uchaguzi wa kumpata naibu meya haijafahamika na kwamba leo atashauriana na uongozi wa jiji na kwamba mara tu baada ya Sikukuu ya Pasaka ataitisha kikao cha baraza.

Mchakato wa kumpata naibu meya ni tofauti kwani idadi ya wajumbe watakaopiga ni ndogo ikilinganishwa na ile ya juzi ambayo madiwani wote na wabunge wote wa Mkoa wa Dar es Salaam walipigakura.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe alisema jana kuwa wajumbe watakaomchagua naibu meya hawatazidi 25 kutokana na kanuni zilizopo .

Alisema naibu meya atapatikana katika kikao cha kwanza cha Baraza kitakachoongozwa na meya.

Alisema wajumbe watakaoshiriki kikao hicho ni wabunge wa majimbo, kila manispaa; Ilala, Temeke na Kinondoni itatoa wajumbe watatu watakaoteuliwa na mameya wao na Meya wa Jiji atateua watatu.

Wabunge Waanza Kuhojiwa TAKUKURU Kwa Tuhuma za Rushwa....Zitto Kabwe Apongeza

$
0
0

Siku mbili baada ya baadhi ya wabunge kudaiwa kuhusika katika vitendo vya rushwa, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola amesema taasisi yake inawahoji wote waliotajwa kuhusika na tuhuma hizo.

Hatua hiyo imekuja kutokana na tuhuma za rushwa dhidi ya wabunge wa baadhi ya kamati za Bunge na kusababisha baadhi yao kuomba kujiuzulu ujumbe wakishinikiza uchunguzi ufanyike ili waliohusika wawekwe hadharani na kuchukuliwa hatua.

Mkuu huyo wa zamani wa Intelijensia ya jinai katika Jeshi la Polisi alisema:“Sisi tunachunguza tuhuma zote zinazohusiana na rushwa, kwa maana hiyo tunawachunguza wabunge wote waliotajwa.”

Alisema uchunguzi huo unakwenda zaidi hadi kuyagusa mashirika ya umma kwa kuwa lengo ni kushughulikia kashfa ambayo inaweza kuharibu heshima ya Bunge.

Mashirika ya umma yaliyoguswa katika tuhuma hizo ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).

Alipoulizwa uchunguzi huo utakamilika lini, alisema hawezi kubashiri kwa kuwa hilo ni suala la utendaji ambalo linafuata sheria na taratibu.

Wabunge wafunguka
Wakati Takukuru ikichukua hatua hiyo, wabunge watano waliokumbwa na mabadiliko ya kuhamishwa kamati yaliyosababisha baadhi yao kupoteza nyadhifa zao huku yakielezwa kuwa ni ya kawaida, wamefunguka kuhusu uamuzi huo huku baadhi yao wakiushangaa.

Waliopoteza nafasi zao kutokana na mabadiliko hayo ni Richard Ndassa, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Mitaji (PIC), Mary Mwanjelwa (Ardhi, Maliasili na Mazingira), Martha Mlata (Nishati na Madini).

Waliovuliwa umakamu mwenyekiti ni Dk Raphael Chegeni (Huduma za Maendeleo ya Jamii) na Kangi Lugola (Hesabu za Serikali za Mitaa).

Mwanjelwa alisema inasikitisha na kushangaza kusikia tuhuma zikitolewa kwenye vyombo vya habari na baadaye kuona mabadiliko ya kamati hizo yakifanyika.

Alisema kwa sasa bado anatafakari:“Lakini kwa kuwa Spika ndiyo amepewa mamlaka kwa mujibu wa kanuni za Bunge basi huwezi kupinga,” alisema.

Mlata alisema kwa sasa hawezi kuzungumza kauli yoyote kabla ya kuonana na Spika.

Ndasa alisema Serikali ina mkono mrefu wa kufuatilia na kuchunguza tuhuma hizo ili kujiridhisha huku akisema mabadiliko yaliyofanyika ni kawaida na yapo ndani ya mamlaka ya Bunge na hawezi kuhusisha mabadiliko hayo na tuhuma za rushwa.

Chegeni alikubaliana na mabadiliko hayo huku akibainisha kuwapo kwa kundi la watu wanaojaribu kuchafua taswira ya kamati yake.

“Mabadiliko ni kawaida tu, anaweza kukupeleka kamati fulani na kukurudisha kamati yako ya zamani na wala siwezi kuhusisha na tuhuma za rushwa, lakini kama kuna rushwa kweli lazima iwe na upande wa mpokeaji na mtoaji, mashirika nayo yachunguzwe na Takukuru kama sehemu ya kuanzia,” alisema.

Zitto Kabwe apongeza
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Zitto Kabwe amepongeza hatua ya TAKUKURU kuanza uchunguzi mara moja ili kurejesha heshima ya bunge.

Ni hatua muhimu kwamba TAKUKURU imeanza uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa kwa Wabunge. Ni hatua kubwa itakayopelekea...
Posted by Zitto Kabwe on Wednesday, March 23, 2016

Hukumu ya Kutoa Lugha Chafu Inayomkabili Mbunge Saed Kubenea Itatolewa April 13

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda inayomkabili Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, Aprili 13, mwaka huu.

Hukumu hiyo itatolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya upande wa mashtaka unaowakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa na upande wa utetezi ukiongozwa na Peter Kibatara kuwasilisha hoja zao za mwisho.

Uamuzi huo ulitolewa jana na mahakama hiyo baada ya Kubenea na mashahidi wake watatu, akiwamo mwandishi wa New Habari 2006, Shabani Matutu na Josephat Isango wa Mwanahalisi kutoa ushahidi wao.

Akitoa ushahidi wake, Matutu alidai kuwa Desemba 14, 2016 katika Kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd kilichopo Mabibo External kwenye mgomo wa wafanyakazi, hakusikia Kubenea akimuambia Makonda kuwa ni mjinga, mpumbavu, kibaka na cheo chenyewe kapewa.

Alidai alimsikia mbunge huyo akimuuliza Makonda “kwa nini unafunga mkutano bila ya kunipa nafasi ya kuongea wakati mgogoro nimeuanza mimi kuutatua, mimi siyo kibaka nimekuja baada ya kuitwa na wananchi walionichagua kwa kura 87,000”.

Kubenea anadaiwa kumtolea lugha chafu Makonda alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images