Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya March 15


Ester Bulaya Apeta Tena Mahakamani....Pingamizi La Stephen Wassira Latupiliwa Mbali

$
0
0
Mahakamaa Kuu Kanda ya Mwanza, imetupilia mbali maombi ya baadhi ya wapigakura wa Jimbo la Bunda Mjini ya kuruhusiwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Makahama Kuu wa kufuta shauri lao la kupinga matokeo ya uchaguzi.

Maombi hayo yaliwasilishwa na Magambo Masato na wenzake wanne wanaompigania Stephen Wassira, wakiiomba mahakama hiyo kuwaruhusu kukata rufaa Mahakama ya Rufani baada ya kutoridhiswa na uamuzi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana yaliyompa ushindi Ester Bulaya (Chadema), dhidi ya Stephen Wasira (CCM).

Jaji anayesikiliza shauri hilo namba 25 la mwaka 2016, Rose Ebrahim alisema jana kuwa anakubaliana na pingamizi lililowekwa na wajibu maombi kuwa hayana mashiko kisheria.

Pingamizi hilo lilowasilishwa na Wakili Mfawidhi wa Serikali, Paschael Marungu alidai aliyesaini hati ya maombi siyo aliyethibitisha kwani hilo ni kosa la kisheria.

Wakili Marungu alidai hati hiyo ilisaniwa na Wakili Denis Kahangwa na kuthibitishwa na Wakili Constantine Mutalemwa kwamba hilo ni kosa kisheria, hivyo kuiomba mahakama kutupilia mbali.

Akitoa uamuzi juu ya pingamizi hilo, Jaji Ebrahim alisema anakubaliana na pingamizi hilo kwani, makosa yaliyofanywa hayarekebishiki.

“Haya maombi nayatupilia mbali hayana miguu ya kusimamia, ni kosa kubwa hati kusainiwa na mtu mwingine halafu ikathibitishwa na mwingine, hakuna namna ya kurekebisha, lazima sheria ifuatwe na taratibu zake,” alisema.

Awali, Magambo na wenzake walifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga ushindi wa Bulaya, lakini ilitupiliwa mbali kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya sheria.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana, Bulaya alipata kura 29,973 na Wasira wa CCM aliambulia 19,123 ikiwapo tofauti ya kura 10,000.

Hata hivyo, Wasira alilalamikia matokeo hayo akidai uchaguzi ulitawaliwa na udanganyifu.

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :

CUF Watoa Sababu za Maalim Seif Sharif Hamad Kuishi Serena Hoteli Pamoja na Gharama Iliyotumika Hadi sasa

$
0
0

SIRI imefichuka kuhusu hatua ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar (SUK), Maalim Seif Sharif Hamad, kuishi hotelini jijini Dar es Salaam.

Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), amekuwa akiishi katika Hoteli ya Serena jijini Dar tangu aliporuhusiwa kutoka Hospitali ya Hindu Mandal Machi 8, mwaka huu alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa ofisa wa ngazi za juu wa CUF, alishangazwa na hatua ya baadhi ya watu kuhoji kiongozi huyo kuendelea kuishi hotelini hapo.

Alisema hatua ya kiongozi huyo kuishi hotelini ni matokeo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kushindwa kutekeleza ahadi ya kumpa nyumba pindi anapokuwa Dar es Salaam katika shughuli zake.

Alisema kutokana na hali hiyo imekuwa ni utaratibu kwa kiongozi huyo kufikia katika hoteli hiyo na gharama za kuishi hotelini hapo hulipwa na SMZ kwa mujibu wa sheria.

“Tangu mwaka 2010 Maalim aliahidiwa atapewa nyumba na Serikali ya SMZ lakini hilo halijafanyika, hiyo nyumba hajapewa hadi leo ndiyo maana mara zote akija Dar hufikia hotelini.

“SMZ ndiyo wenye jukumu la kulipa na si vinginevyo, kwani hata kama kama kuna viongozi wa SMZ wamepewa nyumba kwa muda wote, lakini Maalim Seif hajapewa, sasa kama unataka kujua kwa undani unaweza kuwauliza viongozi wa Serikali wao ndiyo wenye majibu zaidi,” alisema ofisa huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe

Gharama zilizotumika kwa siku 7
Kwa mujibu wa chumba anachoishi kiongozi huyo chenye hadhi ya rais ambacho hutozwa kwa Dola za Marekani 2,801.50, ambapo dola moja ni sawa na Sh 2,180. Hivyo kwa siku saba hadi kufikia leo Serikali imemlipia Maalim Seif,  Sh milioni 42.946.

Kauli ya CUF
Alipotafutwa Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Hamad Masoud Hamad, alisema hatua ya Maalim Seif kuishi hotelini inatokana na maagizo ya daktari wake ambaye amemtaka apumzike kwa sasa.

Alisema kutokana na hali hiyo baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali alipokuwa akipatiwa matibabu alikwenda katika Hoteli ya Serena anapofikia kila mara anapokuwa jijini Dar es Salaam.

Alipoulizwa ni nani anayelipa gharama za kuishi hotelini hapo, Hamad alisema wanaoweza kuzungumzia suala hilo ni viongozi wa SMZ.

“Magufuli (Rais), alipokwenda kumwona alimuuliza ni nani anayemlipia gharama za hoteli na Maalim alisema wazi ni SMZ, lakini ninachotaka kuwaambia Maalim Seif hana nyumba Dar es Salaam.

“… kama wapo viongozi waliopewa nyumba wa SMZ ni hao lakini si Maalim Seif, tangu mwaka 2010 hana nyumba na hufikia hotelini, hana nyumba ya Serikali wala yake binafsi,” alisema Hamad.

SMZ wazungumza
Alipotafutwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, alisema Maalim Seif anastahiki zake kama kiongozi wa SMZ ikiwemo kupatiwa haki ya matibabu pamoja na mahala pa kuishi.

“SMZ ni wajibu wake kuwahudumia viongozi na wananchi wake kwa ujumla, Maalim Seif bado ni Makamu wa Kwanza wa Rais hivyo ana wajibu wa kuhudumiwa.

“Na katika hili anahudumiwa na SMZ ikiwemo kulipiwa hoteli pindi awapo nje ya Zanzibar na si hilo tu pia tunahusika kumpa stahiki zake zote ikiwemo matibabu.

“Kwa kawaida pindi kiongozi yoyote wa kitaifa anapokuwa Dar es Salaam na kama hana nyumba SMZ hulipa malazi ya kiongozi wake na Maalim bado ni kiongozi na hata kama akiondoka kwenye uongozi bado anazo stahiki zake ikiwemo kuhudumiwa kama kiongozi mstaafu,” alisema Waziri Aboud.

Alisema pamoja na hali hiyo kwa sasa Serikali ya Muungano ndiyo inayolipa gharama za Maalim Seif kuishi hotelini kwa agizo la Rais Dk. John Magufuli.

Alisema ahadi ya Rais Magufuli ya kusaidia kulipia hoteli anayoishi Maalim Seif inaonesha ni namna gani Serikali zote mbili ya Muungano na ile ya Zanzibar zinavyoshirikiana kwa dhati.

“Kwa ubinadamu wake Rais Magufuli tunamshukuru sana kwani inaonesha namna gani kiongozi huyo wa Jamhuri ya Muungano alivyo na mapenzi mema  na Zanzibar pamoja na viongozi wake.

“… ila pamoja na yote SMZ bado ina wajibu wa kutekeleza wajibu wake wa kuwatunza viongozi wake wote wakiwemo waliokuwa ndani ya Serikali pamoja na wale waliostaafu,” alisema Aboud.

Katibu Mkuu Mpya wa Chadema Asema Yeye Ndiye Aliyebuni Kaulimbiu Ya "Mabadiliko - Lowassa"

$
0
0

Wakati wengi wakizidi kuhoji uwezo wa Katibu Mkuu mpya wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, kutokana na kutokuwa na jina kubwa katika uwanja wa siasa, mbali na elimu aliyonayo, kipaji chake na uwezo binafsi, vimezidi kufichuka.

Mwishoni mwa wiki, Chadema ilimteua Dk. Mashinji kuwa Katibu Mkuu mpya kushika nafasi ya Dk. Wilbroad Slaa aliyejiuzulu nafasi hiyo Julai 30, mwaka jana kwa kile akichodai kuwa ni utaratibu kutofuatwa wa kumkaribisha Edward Lowassa, aliyehamia katika chama hicho kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kisha kuteuliwa kuwa mgombea urais kupitia chama hicho akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Hata hivyo, wakati wengi wakihoji uwezo wake, imefahamika kuwa Dk. Mashinji kwa kushirikiana na kamati yake, ndiyo waliobuni kaulimbiu (slogan), ya `Lowassa Mabadiliko, Mabadiliko Lowassa,' ambayo ilitumika katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana na kuwa kivutio kikubwa.

Akihutubia mamia ya wananchi wa Jiji la Mwanza katika viwanja vya Furahisha, Katibu Mkuu huyo, alisema: "Katika mkakati wetu kama kamati ya wataalam, tulileta kauli ya Mabadiliko Lowassa, Lowassa Mabadiliko, wameiiga, lakini hawawezi kuwa kama sisi, tunamaanisha mabadiliko tunayoyazungumzia na tutayatekeleza kimkakati na kimfumo zaidi."

Kauli hiyo ambayo hadi sasa inatumika kwenye vikao vya ndani, nje na mikutano ya hadhara vya Chadema, alishirikiana na Kamati ya Wataalam ya Ukawa ambayo imekuwa ikibuni na kushauri mambo mbalimbali ya uendeshaji wa umoja huo.

Katika umoja huo unaohusisha vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD, kamati ya wataalam iliongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu na Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania, Dk. Rodrick Kabangila na Makamu akiwa Dk. Mashinji na Katibu alitoka CUF.

Dk. Kabangila, alisema alikutana na Dk. Mashinji Chuo Kikuu cha Makerere, nchini Uganda, akiwa mwaka wa tatu naye wa pili, wakishirikiana kwenye uongozi wa Umoja wa Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma chuoni humo.

Baada ya kurudi nchini walikutana tena Muhimbili na kuendelea kushirikiana ikiwamo kuandika majarida mbalimbali ambayo walimpelekea Mbowe kwa ajili ya utekelezaji.

Anasema mwaka 2011, baada ya kujiondoa katika Chama cha Madaktari nchini, baada ya kuona mgongano mkubwa na kutoeleweka katika wanayoyapigania, aliingia kwenye siasa na kwa pamoja waliwekwa kwenye Kamati ya Afya ya Chadema, yeye akiwa mwenyekiti na Mashinji akiwa makamu mwenyekiti.

Alisema baada ya kufanya vizuri kwenye kamati hiyo, walipewa Kamati ya Maandalizi ya Ilani ya Chadema, nako alikuwa mwenyekiti na mwenzake makamu.

Amponda Dr. Kigwangalla
Dk. Kabangila, alimshangaa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Hamis Kingwangala, ambaye amendika kwenye ukurasa wake wa Facebook akimponda Dk. Mashinji, na kwamba wakati wa mgomo wa mwaka 2005 alikuwa ni mwanafunzi aliye katika mafunzo ya vitendo (internship) na kwamba mgomo huo uligawanyika katika maeneo matatu ya wanafunzi wanaofaya mafunzo kwa vitendo, daraja la kati na wakongwe, na kwamba Dk. Mashinji alikuwa katika daraja la juu na alisimamia masuala ya ngazi hiyo.

Alisema katika mgomo wa mwaka 2011, walikuwa na Dk. Kigwangalla, yeye (Kabangila) akiwa ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Madaktari Tanzania na Makamu wa Rais, na walishirikiana wote na Dk. Mashinji kwa kuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa na misimamo thabiti, mtendaji makini na mfuatiliaji wa mambo.

"Namshangaa sana Dk. Kingwangalla, sijui ni siasa inamlevya au baada ya kuwa waziri anasahau kabisa jinsi walivyopambana kuboresha sekta ya afya na maslahi ya madaktari nchini, unapokuwa mtaalam unapaswa kupinga kitaalam na siyo kusema mambo kirahisi rahisi na pasipokuwa na taarifa kamili, kwa sasa inaonekana amesahau kabisa udugu wa kitaaluma tuliofundishwa na tunapaswa kuuhubiri. Ukweli anaujua ila anajilazimisha kutoujua," alisema.

Amuua Mwanafunzi Mwenzake kwa Kumkata na Wembe

$
0
0

Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Mtwara Ufundi mkoani Mtwara, Tawfiq Hamisi (17), amefariki dunia baada ya kukatwa na kiwembe katika mkono wake wa kulia na mwanafunzi mwenzake Issac Yohana (16).

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe, amesema kabla ya kifo hicho kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mtuhumiwa ambaye ni Isaac anayedaiwa kuficha kiatu cha mwenzie ambapo baada ya mzozano akaamua kumkata na kiwembe mwenzie chini ya bega lake la kulia.

Ameongeza kuwa marehemu ni mwenyeji wa mkoa wa Tanga huku mtuhumiwa ni mwenyeji wa wiayani Newala mkoani Mtwara, na kwamba taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka kwao zinafanywa na uongozi wa shule, huku mtuhumiwa akishikiliwa na jeshi la polisi kwa upelelezi zaidi.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Ligula, Dkt. Mdoe Mhuza, amethibitisha kupokelewa kwa mwili wa marehemu majira ya saa 11 alfajiri na kudai kuwa bado uchunguzi zaidi unaendelea kwa ajili ya kuweza kubaini chanzo cha kifo chake.

Profesa Baregu: Utawala wa Rais Magufuli Ni Wa Kijeshi

$
0
0
SIKU moja baada ya Rais Dk. John Magufuli kuteua wakuu wa mikoa wapya, mtaalamu wa sayansi ya siasa, Profesa Mwesiga Baregu, ameibuka na kusema kuwa kuwapo kwa wanajeshi wengi wastaafu katika uteuzi huo inadhihirisha wazi kuna dalili za utawala wa kijeshi nchini.
 
Profesa Baregu amesema kuwa  wanajeshi huwa hawana hulka ya kidemokrasia.

“Kitu kimoja kinachojitokeza kwenye uteuzi huu ni kuwepo kwa wanajeshi wastaafu, na mimi ninavyoelewa wanajeshi huwa hawana hulka za kidemokrasia. Hii inaonyesha wazi kwamba utawala huu ni wa kijeshi,” alisema.

Profesa Baregu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema haileti picha nzuri kuwapo kwa wanajeshi wengi katika utawala kwa sababu tawala za mikoa na wilaya ni saula la kiraia na demokrasia zaidi.

Alisema rasimu ya katiba ambayo yeye alikuwa mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ilipendekeza kupitia upya tawala za mikoa na kupunguza idadi yake.

“Kutokana na hilo, mamlaka ya wananchi inamezwa kwa sababu wakuu wa mikoa na wilaya ni wengi na kunakuwepo na mgongano mkubwa,” alisema.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ali, alisema uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya ni wa rais na wanaoteuliwa ni watu mchanganyiko.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (Ruco), Profesa Gaudence Mpangala, alisema kila anapoingia kiongozi mpya anaunda timu ambayo anaona ataendana nayo.

Waziri Mkuu Amwagiza CAG Aende Bukoba Haraka Kumaliza Mgogoro wa Viwanja

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aende Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kufanya upya tathmini na kukagua ugawaji wa viwanja 843 kwenye manispaa hiyo.

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa agizo hilo jana (Jumatatu, Machi 14, 2016) wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mayunga mjini Bukoba.

Alifikia hatua hiyo baada ya wananchi kubeba bango lenye ujumbe kuelezea kutopewa viwanja hivyo vilivyopimwa na Manispaa ya Bukoba. 

Viwanja hivyo vilipimwa na kugawiwa kwa wananchi ambao baadhi yao baada ya kulipa fedha, hawajapewa viwanja hivyo ikiwa ni takriban miaka zaidi ya 10.

Akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Kagera, Waziri Mkuu alilazimika kumpandisha jukwaani Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Bw. Wallace Karia ili atoe maelezo ya nini kimekwamisha wananchi kupewa viwanja hivyo.

Katika maelezo yake, Bw. Karia alisema mwaka 2003, vilitengwa viwanja 843, kati ya hivyo 352 vilikuwa eneo la Kyabitembe, 137 Ihungo na Rwome na vingine 132.

Bw. Karia ambaye hana muda mrefu tangu ahamishiwe katika manispaa hiyo, alisema kumbukumbu za ofisi zinaonesha kuwa viwanja 182 ndio wahusika hawajapewa, na viwanja vingine 85 vilikuwa havijapimwa eneo la Kilimahewa na Kashai, huku kukiwa na vingine 5,000 vya mradi.

Aliongeza kuwa walitarajiwa kuwalipa wananchi hao katika mwaka wa fedha 2016/17; kauli ambayo ilisababisha kelele kutoka kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Waziri Mkuu.

Kutokana na hilo, Waziri Mkuu aliingilia kati na kumueleza Mkurugenzi huyo kuwa kelele hizo zinaashiria kuwa watu hao hawajaridhishwa na majibu yake.

Alisema anafahamu kuwa mkurugenzi huyo na meya ni wapya, lakini akawaagiza ndani ya mwezi mmoja, kufanya mapitio ya viwanja hivyo 843, na hasa watu 182 ambao hawajapatiwa viwanja wahakikishe wanawapatia kwa sababu viwanja vipo.

“Rais mstaafu alikuja hapa na kupewa kilio cha kupunjwa fedha. Najua wakati huo mtasema ninyi hamkuwepo. Wewe (MD) na Meya wako mkae na kupitia mikataba na mafaili. Nyie na mkoa mkae pamoja na kujua vile viwanja vilivyochukuliwa na JWTZ. Nitamleta CAG hapa, ndani ya mwezi mmoja afanye mapitio ya viwanja tu,” alieleza Waziri Mkuu na kushangiliwa na maelfu ya wananchi.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu pia aliwahakikishia wakazi wa Manispaa ya Bukoba kuwa watalipwa fidia zao baada ya kukubali kupisha ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh. bilioni 31.

Waziri Mkuu aliendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa kutembelea wilaya za Misenyi na Karagwe na leo atakuwa wilayani Ngara.

VIDEO: Rais Magufuli awapa Siku 15 Wakuuu Wa Mikoa Kuondoa Majina ya Wafanyakazi Hewa Wanaolipwa Mishahara....Tazama Video hii

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema jumla ya wafanyakazi 202 katika halmashauri 14 katika mikoa ya Singida na Dodoma waligundulika kuwa hewa na kulipwa mishahara kila mwezi.

Rais ameyasema hayo alipokuwa akiwakumbusha wakuu wa kikoa wapya ambao amewaapisha leo Ikulu jijini Dar es salaam.

''Kwa mikoa miwili tuu wafanyakazi hao 202 wanalipwa mishahara hewa na kwenye data ilionyesha wengine wamefariki, wamestaafu, wamefukuzwa , wengine likizo bila malipo wote hao kumbe wanalipwa malipo ya serikali fedha ambazo zingetumika kutatua matatizo ya wananchi''.Amesema Rais Magufuli

Kwa msingi huo kwa halmashauri 180 nchini ina maana kwa mahesabu ya haraka haraka kuna wafanyakazi 2000 na zaidi wanalipwa mishahara hewa.

Hivyo Rais Dkt Magufuli ametoa agizo kwa wakurugenzi wa taasisi za serikali kuanzia leo ndani ya siku 15 kuhakikisha wanapitia majina ya waajiriwa wote wa serikali na kuondoa majina ya ambao wanalipwa bila kufanya kazi.

==>Tazama Video hii Kumsikiliza Rais Magufuli Akiongea

Picha : Rais Magufuli Awaapisha Wakuu Wapya Wa Mikoa Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi,Zelote Steven Zelote kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga  kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga kuwa mkuu wa mkoa wa Geita,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Emmanuel Edward Maganga kuwa mkuu wa mkoa wa Kigoma,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Paul Christian Makonda kuwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Mh.Anne Kilango Malecela kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Rais Magufuli Ataka Vijana Waache Kucheza Pool table na Badala Yake Wafanye Kazi.....Asiyetaka ALAZIMISHWE na Ikibidi Apelekwe Kambini Akafanye Kazi

$
0
0

Rais John Magufuli leo amewaapisha wakuu wa mikoa wapya aliowateua hivi karibuni na katika hotuba yake amewataka wakuu wa mikoa hao wapya kuhakikisha vijana wanafanya kazi na kuacha uzembe.
 
Rais Magufuli amewataka wakuu wa mikoa hao kuhakikisha hakuna vijana ambao watakuwa wanakwenda kucheza pool table asubuhi na badala yake vijana hao wanatakiwa kufanya kazi kweli kweli hata kwa kulazimishwa.

"Nimeamua kuwateua wakuu wa mikoa nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika mikoa yenu.

"Napenda niwape pole kwa sababu mtakwenda kufanya kazi kweli kweli kutatua kero za wananchi wetu.

"Lakini pia niwaombe wakuu wa mikoa mkasimamie watu wafanye kazi hasa vijana.

"Haiwezekani vijana leo hii unawakuta saa mbili asubuhi wanacheza Pool table wakati wakina mama wanalima shambani, kama hawataki kufanya kazi kwa kupenda walazimishwe kufanya kazi. Atakayekataa mpelekeni  kambini akafanye kazi" amesema Rais Magufuli

Rais Magufuli ameongelea pia suala la wafanyakazi hewa kwenye Halmashauri zote nchini ambapo  amewapa siku 15 wakuu wapya wa mikoa kuhakikisha hakuna wafanyakazi hewa katika Halmashauri zote nchini.

"Niwape grace time ndani ya siku 15 wakurugenzi wawe wamejumlisha na wamewatoa wafanyakazi hewa katika payroll

"Mshahara wa mwezi tukigundua mkurugenzi amelipa mshahara hewa ajue hana kazi na tunampeleka mahakamani

"Singida na Dodoma ina wafanyakazi hewa 202 wanalipwa mishahara hewa na kwenye data ilionyesha wengine wamefariki, wamestaafu, wamefukuzwa , wengine likizo bila malipo wote hao kumbe wanalipwa malipo ya serikali fedha ambazo zingetumika kutatua matatizo ya wananchi" 

"Nimeamua kuwateua nyinyi kama wakuu wa mikoa nikiamini mtaniwakilisha vizuri popote.


"Tusiogope kuchukua maamuzi, nafuu uchukue maamuzi hata kama ni mabaya yatarekebika huko mbele."Amesema Rais Magufuli

==>Kwa habari zaidi tazama video hii umsikilize 

VIDEO: Rais Magufuli Awataka Wakuu wa Mikoa Kuwaweka Ndani Hata Masaa 48 Viongozi Wanaonyanyasa Wananchi

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Magufuli akihutubia Wakuu wa Mikoa wapya 26 na Watumishi wengine wa Serikali walioapishwa leo amesema; "Nimewateua ninyi (Wakuu wa Mikoa) muende mkawatumikie Wananchi na sio kwenda kufanya siasa. 

"Ilinichukua muda sana kuteua kwa sababu nilitaka kujihakikishia kuwa ninateua watu makini.

"Mkienda Mikoani nataka  mkatatue kero za Elimu, Ajira, Ujambazi na nyingine kwa kushirikiana na viongozi wengine na Mumtangulize Mungu naye atawasaidia.

"Kuna viongozi huko wananyanyasa wananchi, unakuta katibu tarafa, mtendaji wa kata ananyanyasa  tu  wananchi  bila  sababu.

"Ninyi  mna mamlaka  ya  kumuweka  mtu  ndani  hata  masaa 48. Kawawekeni wengi ili kusudi wajue kwamba wananchi wanatakiwa kuheshimiwa." Amesema Rais


==> Tazaidi, tazama  video  hii  kumsikiliza  Rais akiongea

Vurugu Zanzibar: Bomu Larushwa na Kulipua nyumba ya Kamishna wa Polisi Hamdani Omar Makame

$
0
0
Hamdani Omar Makame, Kamishna wa Polisi Viswani Zanzibar
 

Habari kutoka visiwani Zanzibar zinaeleza kwamba, nyumba kadhaa ikiwemo  ya Hamdani Omar Makame ambaye  ni Kamishna wa Polisi Viswani Zanzibar  zimelipuliwa kwa mabomu.

Habari hizo zinaeleza kwamba, Jeshi la Polisi linaendesha kamata kamata ya watu waliohusika kwenye tukio hilo  ambapo  mpaka  sasa  watu 31 wametiwa  mbaroni.

Tukio hilo limezidisha hali ya wasiwasi visiwani humo ambapo ni siku 5  tu  zimesalia  kabla  ya  uchaguzi  wa  marudio  kufanyika

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Asema Serikali Itaendelea Kudhibiti Uingizaji wa Sukari Kutoka Nje Ya Nchi

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kudhibiti uagizaji wa sukari kutoka nje ili kulinda soko la ndani.

Ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Machi 14, 2016) wakati akizungumza na uongozi wa kiwanda cha sukari cha Kagera pamoja na uongozi wa mkoa wa Kagera alipotembelea kiwanda hicho ambapo alisema wamezuia sukari kutoka nje ili kuhakikisha sukari inaisha katika maghala yao.

Akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Kagera, Waziri Mkuu ameviagiza viwanda kuzalisha sukari nchini vizalishe sukari ya kutosha ili kukidhi mahitaji ya soko.

Alisema mahitaji halisi ya sukari hapa nchini ni tani 420,000 huku uwezo wa viwanda vya ndani ni kuzalisha tani 300,000 hivyo alitoa wito kwa viwanda hivyo kuongeza uzalishaji.

“Tunahitaji viwanda vya ndani vizalishe sukari ya kutosha na mahitaji yawe yamefikiwa kama tulivyokubaliana, lengo ni kuzuia uagizaji wa sukari kutoka nje ambao ukiendelea utavivuruga viwanda vya ndani,” alisema.

Pia alivitaka viwanda hivyo viwe vimefikia malengo ya kuzalisha sukari ya kutosha katika kipindi cha kuanzia miaka mitatu hadi minne kama walivyokubaliana katika kikao cha wadau wa sukari nchini kilichofanyika hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika mashamba ya miwa, ununuzi wa mitambo pamoja na kuajiri idadi kubwa ya watumishi ambao ni Watanzania.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Ash Rana alisema kwa sasa wanazalisha tani 60,000 za sukari na kwamba wana lengo la kuzalisha tani 120,000 katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Alisema uzalishaji wa sukari kiwandani hapo umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo mwaka wa fedha wa 2011/2012 walizalisha tani 35,362 na mwaka 2015/2016 wamezalisha tani 60,000.

Ofisa huyo aliiomba Serikali ipunguze riba ya mikopo ya kwenye uwekezaji wa sekta ya kilimo ambapo kwa sasa wanatozwa asilimia 20 kiwango ambacho alisema ni kikubwa sana.

Alisema wana mipango ya kukiboresha na kukipanua zaidi kiwanda hicho na hivi sasa wako katika hatua za mwisho za kupata mkopo wa Dola za Marekani milioni 68 ambao kati ya hizo, dola milioni 10 zitapelewa katika uboreshaji wa umwagiliaji na zilizobaki katika kuimarisha miundombinu ya kiwanda hicho.

IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MACHI 15, 2016.

Ikulu Yakanusha Taarifa Ya Marais Wastaafu Kupunguziwa Ulinzi

$
0
0
Gazeti la JAMBOLEO, toleo namba 2381 la tarehe 15 Machi, 2016 limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho "Magufuli awapunguzia ulinzi marais wastaafu".

Taarifa yake kamili ipo katika ukurasa wa nne, na inaeleza kuwa Mheshimiwa Rais John Magufuli amewapunguzia ulinzi Marais wastaafu na imewataja marais hao kuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.

Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa taarifa hizo sio za kweli na inalitaka gazeti hilo kukanusha habari hiyo mara moja, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha, Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa utaratibu wa ulinzi wa Marais wastaafu haujabadilishwa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-15 Machi, 2016

Kamishna Wa Jeshi La Polisi Zanzibar Azungumza Na Wandishi Wa Habari Juu Ya Milipuko Ya Mabomu Inayotokea Unguja Na Pemba

$
0
0
Na Mwashungi Tahir na miza Kona – Maelezo Zanzibar    
Nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame imeripuliwa  na kitu kinachosadikiwa kuwa  ni bomu na watu wasiojulikana  majira ya saa 5.00 usiku huko Kijichi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Kilimani, Kamishna Hamdani amesema tukio hilo limeathiri sehemu ya paa la nyumba na dari na  kujeruhi baadhi ya watu  waliokuwa wamelala  na kusababisha hasara kubwa.

Amesema tukio hilo linafanana na  lile lililotokea tarehe 03 mwezi huu katika Maskani ya CCM Kisonge Unguja hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu wanaofanya  uhalifu huo.

Akizungumzia  matukio  mengine ya uhalifu na kuchoma moto nyumba, maskani na kituo cha Afya huko Pemba, alisema  Jeshi la Polisi limeanza msako mkali na kuwatia mbaroni watu 31 ambao wanaendelea kuhojiwa na watakaohusika watafikishwa  katika vyombo vya sheria.

Kamishna Hamdani amewatoa hofu  wananchi kuhusu usalama wao na mali zao kuelekea uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 20 mwezi huu na kuwepo kwa ongezeko la askari katika maeneo  mengi ya mijini na vijijini  ni  moja ya juhudi za kuimarisha  ulinzi  na kuhakikisha  uchaguzi huo utakuwa salama na amani.

Ametahadharisha kuwa mtu yoyote atakayejihusisha kuanzisha vurugu au kufanya kitendo chenye ishara ya  uvunjifu wa amani atapambambana na vyombo vya sheria.

Kamishna Hamdani ametoa wito kwa wananchi waliojiandikisha kupiga kura kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili waweze kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba bila ya woga  kwani jeshi hilo limejipanga  kuimarisha ulinzi  sehemu  zote.

Waziri Mkuu Ampa RAS Kagera Siku 5 Ampeleke Taarifa Za Matumizi Ya Milioni 120 Za Hospitali Ya Mkoa

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera na kumpa siku tano Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Adam Swai amletee taarifa juu matumizi ya sh. Milioni 80 ambazo ni fedha za UKIMWI.

Pia amemtaka ifikapo Machi 20, nwaka huu awasilishe taarifa nyingine ya matumizi ya sh. Milioni 40 za ukarabati wa jengo la wagonjwa maalum  (Grade A)

Ametoa agizo hilo leo asubuhi (Jumanne,  Machi 15, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo baada ya kutembelea maeneo kadhaa yakiwemo wodi ya watoto, wodi ya wazazi, chumba cha wagonjwa mahututi (ICU ) na chumba cha kuhifadhia maiti.

"Kulikuwa na frsha za ukimwi sh. Milioni 80 ambapo kila mtumishi alipaswa kupata sh. 200,000/- lakini ninyi mmewapa sh. 80,000 /-. RAS fedha hizi zimeenda wapi?  Nataka uniletee taarifa ofisini kwangu Dar es Salaam ifikapo tarehe 20 mwezi huu," alisema huku akishangiliwa.

"Kwa mujibu wa taarifa ya CAG pale grade A kuna mgogoro wa sh. milioni 40. Wewe taarifa unayo lakini hujaifanyia kazi yoyote.  Nataka tarehe 20 nayo hii pia niipate na nione umetoa mapendekezo gani."

Kuhusu tatizo la madaktari katika hospitali hiyo, Waziri Mkuu alisema atawasiliana na Waziri wa Afya ili madaktari watano ambao wanasubiri ajira rasmi lakini wameanza kazi kwa mkataba hospitali hapo wapewe ajira rasmi. Pia alisema amebaini upungufu wa madaktari bingwa uliopo katika hospitali hiyo.

Pia aliahidi kufuatilia maombi yao ya gari la wagonjwa hasa ikizingatiwa kuwa anayo maombi kama hayo kutoka hospitali za Mawenzi (Kilimanjaro), na Ligula (Mtwara).
 
Katika hatua nyingine,  Waziri Mkuu aliwapongeza watumishi wa hospitali hiyo kwa huduma zao nzuri wanazotoa kwa wagonjwa.  "Nineridhishwa na kauli walizotoa wagonjwa juu yenu. Tofauti na hospitali nyingine nilizopita, wao wamesema hawajatozwa fedha ili wapatiwe dawa. Nimefarijika sana."

"Endeleeni kuwa na huruma kwa wagonjwa. Endeleeni kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa. Hawa wagonjwa hawakuogopa kuelezea hisia zao. Wamesema kwa uwazi kabisa kwamba mnawajali," alisema.

Mapema,  akisoma taarifa mbele ya Waziri Mkuu,  Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk.  Thomas Rutachunzibwa alisema hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari bingwa pamoja na madaktari wa kawaida.

"Tunao madaktari 10 lakini wanaohitajika ni 30. Tunao madaktari wasaidizi wanane lakini wanaohitajika ni 23 na madaktari bingwa waliopo ni watatu tu lakini wanaohitajika ni 24. Tunaomba tupatiwe watumishi hawa ili tuweze kutoa huduma kulingana na matarajio ya wananchi wetu," alisema.

Akifafanua kuhusu mahitaji ya hospitali hiyo, Dk. Rutachunzibwa alisema wanahitaji sh. bilioni 1.8 kwa mwaka bila ya kuweka mishahara ili waweze kufanya kazi yao kwa umakini. 

"Tunahitaji sh. milioni 802 kwa ajili ya matumizi ya kawaida lakini tunachopokea hivi sasa ni sh. milioni 299 ambayo ni sawa na asilimia 30 ya mahitaji yetu."

"Bajeti ya dawa tuliyotenga ni sh. milioni 960 lakini tunapokea sh. milioni 143 ambazo kiuhalisia zinatosha kwa matumizi ya miezi miwili tu. Tumelazimika kufanya marekebisho ya bei za dawa kwa ridhaa ya Bodi ya hospitali ili tuweze kumudu kutoa huduma kwa wananchi," alisema.

Alisema ili kubana mianya ya upotevu wa mapato, wanahitaji kuwa na kompyuta 15 lakini hadi sasa wamefanikiwa kununua kompyuta mbili tu ambazo ziko Grade A na idara ya wagonjwa wa nje (OPD) ili kuimarisha utaratibu wa ukusanyaji mapato.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, MACHI 15, 2016.

Taarifa Nzima ya ChannelTEN Jumanne hii ya March 15, 2016

$
0
0

Taarifa  Nzima  ya ChannelTEN   Jumanne  hii  ya   March 15, 2016




Waziri Mkuu Amwagiza Waziri wa Kilimo Kufuatilia Vitalu Misenyi

$
0
0

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bw. Mwigulu Nchemba afanye mapitio ya vitalu vyote vilivyoko katika ranchi ya Kitengule wilayani Karagwe na kujua nani anamiliki kitalu kipi na kama hajaendeleza kwa mujibu wa makubaliano ni vema akanyang’anywa.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo juzi jioni (Jumatatu, Machi 14, 2016) alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Kihanga wilayani Karagwe ambapo aliitaka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ifanye mapitio katika vitalu vyote na kuangalia wamiliki ni akina nani na kukagua vibali vyao.

Pia aliagiza wavamizi wote kuondoka katika pori la akiba la Kimisi lililoko wilayani Karagwe ambao wanatoka nchi jirani na kuwataka warudi makwao na wakaanze upya kutuma maombi ya kuja kuishi nchini.

“Lazima tulinde nchi hii kwa pamoja. Pamoja na kuwa tunatambua ujirani uliopo na uanachama wa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki bado kuna taratibu na kanuni ambazo ni lazima zifuatwe. Tunao utaratibu wa kutoa kibali cha muda usiozidi miezi sita… hawezi mtu kuja akaamua kukaa tu bila kibali na wala Mtanzania huwezi kwenda nchi jirani ukaamua kukaa tu bila kufuata taratibu,” alisisitiza.

Akizungumzia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji iliyokithiri mkoani Kagera, Waziri Mkuu alisema inasababishwa na viongozi na wananchi kuruhusu watu wa mataifa mengine kuingia nchini bila ya kufuata utaratibu, ambapo aliwataka wabadilike na waache tabia hiyo.

“WanaKaragwe mmeamua kuruhusu watu wa mataifa mengine waje kufaidi rasilmali zetu. Hapa kuna Warundi na Wanyarwanda. Je wamefikaje kama siyo ninyi kuwaruhusu?" alihoji.

“Lazima tushirikiane kulinda mipaka, nimeangalia mpaka wa nchi yetu kule Misenyi naona mambo ni hovyo hovyo tu. Vitalu vingi vinamilikiwa na wageni, kuanzia namba 1,5,7,9,10,11 na 12 na wengine hawajaendeleza kabisa. Kwa mfano kitalu namba tano kinatumiwa kulima bangi, Wizara mnasubiri nini kuwanyang’anya na kukirudisha kwa Watanzania?”

“Wizara mfanye mapitio katika vitalu vyote vilivyo pembezoni mwa vijiji. Angalieni nani anamiliki, amepewa kwa kazi ipi na kama kama hajafanya kitu chochote  basi ni vema wakabidhiwe Watanzania wenye mifugo ili wavitumie kunenepesha mifugo yao,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.

Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu alisema kuna kitalu kimoja kina hekta 36,000 na ilikubalika kuwa kitajengwa kiwanda cha kusindika nyama nyama ya ng’ombe lakini hata hivyo hakijafanyika kitu. “Wizara mkafanye mapitio mumpunguzie eneo huyo mmiliki ili wafugaji wa Karagwe wafuge na kunenepesha ng’ombe wao na kisha kuuza katika kiwanda hicho.

Waziri Mwigulu ambaye ameambatana Waziri Mkuu katika ziara hii ya siku tatu, ameenda Karagwe leo hii kutekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu wakati Waziri Mkuu akielekea wilaya ya Ngara

IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, MACHI 15, 2016.

Serikali Yatangaza Rasmi Kugundulika kwa Futi za Ujazo wa Gesi Tirioni 2.17 katika Bonde la Ruvu

$
0
0

Serikali imetangaza rasmi kugundulika kwa futi za ujazo wa Gesi Tirioni 2.17 katika Bonde la Ruvu mkoani Pwani,  katika eneo lijulikanalo kama Mamba Kofi One ikiwa ni moja ugunduzi ulifanywa na Kampuni ya Dodsal ikishirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Akitoa tamko hilo mbele ya vyombo vya habari ofisini kwake Dar es Salaam jana asubuhi, Waziri wa  Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa hadi kufikia Machi mwaka huu jumla ya gesi yote iliyogunduliwa nchini ni trioni 57.23.

"TPDC imerekebisha muundo wake tunataka iwe inajishughulisha  na utafutaji wa gesi ya mafuta hivyo kufuatana na sheria ya petroli ya mwaka jana kazi zote zitasimamiwa na TPDC na haitaendelea kusimamia makampuni mengine badala yake tuameazisha wakala wakusimamia kazi ," alisema Muhongo.

Akitolea ufafanuzi kuhusiana  na kugundulika kwa gesi hiyo asilia iliyopo nchi kavu imefikia futi za ujazo tirioni 10.17, na baharini katika kina kirefu cha futi za ujazo ni 47.08.

Waziri Muhongo alisema ufumbuzi huo umefanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kushirikiana na Kampuni ya Haydrocarbons and Power Limited (DODSAL) hivyo wakiendelea na utafiti wataweza kuvuka hata futi 10 kama walivyo dai.

Alisema kuwa takribani futi za ujazo  elfu moja zina uwezo wakuzalisha jumla ya megawati za umeme zipatazo 5000 wakati huo bado wanaendelea na  utafiti wa gesi katika maeneo ya kusini mwa Tanzania ambapo kumegundulika kuwa na gesi nyingi .

"Nilazima taifa letu liwe na umeme mwingi, na umeme wa kutosha kwani tukifanya hivyo tunaweza kufikia kwenye bigawati kama nchi za kusini walivyoweza kupata umeme mwingi," alisema Muhongo.

Akijibu maswali kuhusiana  na kunufaika kwa wananchi na gesi hiyo alisema tayari wameaza kunufaika kwani kabla ya awamu ya tano ya Rais Dk. Jonh Magufuli,  jumla ya megawati 700 hadi 800 ndizo zilikuwa zikitumika katika matumizi ya umeme ambapo katika kipindi cha  awamu ya tano jumla megawati 1000 zinaendelea kutumika.

"Ifahamike kuwa faida ya gesi kwa wananchi ni ya siku nyingi kwani viwanda takribani 37 vimekuwa vikitumika kwa matumizi ya gesi kikiwemo kiwanda cha Saruji " alisema.

Awali kabla ya uzinduzi huo Meneja Utafiti wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Gesi (TPDC), Venosa Ngowi alisema wanatarajia kumpatia ripoti ya mapendekezo ya juu ya gharama za uuzaji wa gesi nchini ifikapo Aprili,20 mwaka huu.

Ngowi alisema zoezi linalofanyika ni mazungumzo ya wawekezaji na watalamu wa nchi husika kuweza kufanya uhakiki wa gharama wa bei za gesi nchini.

Alisema moja ya changamoto wanazokutanazo ni kuwepo kwa gharama nyingi  zinazo muhusu mwekezaji.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images