Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatau Ya March 13


JWTZ Wamuokoa Daktari Aliyesusiwa Maiti na Wananchi Wakimtuhumu Kusababisha Kifo cha Mgonjwa Wao

$
0
0

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kambi ya Ikola wamelazimika kulinda nyumba ya mganga wa Zahanati ya Kapalamsenga iliyopo Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi baada ya wanakijiji kupanga kutelekeza mwili wa mgonjwa wanayedai daktari huyo amesababisha kifo chake kwa kukataa kumtibu.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 10.00 alfajiri baada ya wanakijiji kupata taarifa kuwa mgonjwa wao huyo, Bibiana Karangi (49) ambaye mganga huyo alidaiwa kukataa kumtibu, amefariki.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, Hamad Mapengo alisema siku ya tukio saa saba usiku, mgonjwa huyo alifikishwa katika zahanati ya kijiji hicho na walipomuamsha mganga huyo nyumbani kwake umbali mita 20, alikataa akiwataka wampeleke Kituo cha Afya Karema.

Inadaiwa kuwa mgonjwa huyo alipofikishwa Kituo cha Afya Karema aligundulika kuwa na upungufu wa damu, hivyo alitakiwa apelekwe Hospitali ya Wilaya ya Mpanda, lakini wakati akiwa bado kituoni hapo alifariki dunia.

Baada ya mgonjwa huyo kufariki, wanakijiji hao walipata taarifa ndipo waliamua kukusanyika kwa lengo la kwenda Karema kuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka nyumbani kwa mganga wa zahanati hiyo ili wamsusie afanye maziko mwenyewe wakidai ndiye aliyesababisha kifo hicho kwa kutompatia huduma mapema.

Kutokana na mpango huo, viongozi wa kata hiyo walipata taarifa hizo na kuomba msaada kwa wanajeshi wa Ikola ambao walifika na kuizingira nyumba ya mganga huyo, hivyo kuwalazimu wananchi hao kuanza kutawanyika.

Mwenyekiti huyo alisema kutokana na mazingira hayo ilimlazimu yeye na kaimu mganga mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Dk Naibu Mkongwa kwenda kumuondoa mganga huyo na kumpeleka mjini Mpanda kwa kuhofia usalama wake na familia yake.

Baada ya kuondolewa kijijini hapo ndipo askari wa JWTZ walipoondoka nyumbani kwa mganga huyo.

Ofisa Tarafa wa Karema, Zawadi Mirambo alifika kijijini hapo na kufanya kikao na wananchi, lakini maoni ya wanakijiji hao yalitofautiana na wauguzi ambao walidai mgonjwa huyo alikuwa na maradhi, hivyo ushauri wa kwenda kituo cha jirani ulikuwa sahihi.

Hata hivyo, wanakijiji hao walidai imekuwa ni kawaida kwa mganga huyo kukataa kutoa huduma kwa wagonjwa usiku hata kwa wajawazito.

TAKUKURU Yaanza Kuchunguza Jinsi Waziri Lukuvi alivyokataa Rushwa ya Bilioni 5

$
0
0

Takukuru imeanza kuchunguza taarifa kwamba Waziri wa Ardhi, William Lukuvi alikataa kupokea rushwa ya Sh5 bilioni iliyotaka kutolewa na wafanyabiashara wawili wakubwa ili kuwapitishia mradi wa Sh84 bilioni.

Katika mahojiano  na gazeti  la Mwananchi  hivi  karibuni, Waziri Lukuvi alisema kwamba lengo la wafanyabiashara hao ilikuwa ni kufanikisha mpango wao wa kuiuzia Serikali ardhi kwa bei kubwa kwenye eneo linalotakiwa kujengwa mji wa kisasa wa Kigamboni.

Licha ya kukataa kutaja majina ya wafanyabiashara hao, Lukuvi alisema mtandao huo wa wafanyabiashara ni hatari na unaweza kusababisha mtu ashindwe kufanya kazi ya wananchi iwapo ataendekeza rushwa.

Jana, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Valentino Mlowola alisema kutokana na taarifa ya kiongozi huyo, ofisi yake iliamua kuchukua chanzo hicho na kuanza kazi ya uchunguzi.

Hata hivyo, Mlowola hakutaka kuweka wazi kazi ya uchunguzi huo imeanza lini wala ilipofikia. 

 “Kueleza tumeanza lini hilo ni suala la kiufundi, tumeshaanza kushughulikia,” alisema Mlowola ambaye Rais John Magufuli amemuidhinisha rasmi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo baada ya kukaimu kwa miezi kadhaa.

Katika ufafanuzi wake, kamishna huyo wa zamani na mkurugenzi wa Intelijensia ya Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi, alisema taasisi hiyo kwa sasa imekuwa ikichukua tuhuma yoyote ya rushwa kutoka chanzo chochote baada ya kuripotiwa.

Katika mahojiano hayo, Waziri Lukuvi alisema wafanyabiashara hao waliwaeleza marafiki zake wa karibu kuwa wangempa rushwa.

Mji huo mpya wa Kigamboni unajumuisha kata za Kigamboni, Tungi, Vijibweni, Mjimwema, Kibada, Somangila na eneo lote hilo lina ukubwa wa takribani ekari 6,000.

Awali mradi huo ulitarajiwa kugharimu Sh13 trilioni ambazo zingetolewa na Serikali, lakini ikaamua kushirikisha sekta binafsi ili kuujenga na Serikali ishughulikie uwezeshaji wa awali.

Lukuvi ambaye alihamishiwa Wizara ya Ardhi mapema mwaka jana na kubakizwa katika wizara hiyo na Rais Magufuli, alisema amegundua kuna mtandao mkubwa wa rushwa unaoanzia ngazi ya halmashauri mpaka wizarani ambao unahusisha maofisa wa Serikali na viongozi wa wizara.

“Kama ukiwa na tamaa huwezi fanya kazi uliyotumwa. Kuna wakati walikuja ni wafanyabiashara wawili wakubwa na kutaka wanipe Sh5 bilioni ili nikubali kupitisha mradi wao wa mabilioni ya shilingi na walitangaza kwa marafiki zangu kuwa wangenipa fedha, lakini hapa hawawezi,” alisema Lukuvi.

Aliongeza: “Wakati naingia tu wizara hii nilikuta harakati za kukamilisha mradi wa Kigamboni ukiwa katika hatua za mwisho na kila kitu kilikuwa kimekamilika. Lakini nilipopitia vizuri nilikataa kuwalipa wafanyabiashara hao. Cha ajabu hazikupita siku mbili walipata taarifa wakaja mbio kutaka kuniona.”

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, wafanyabiashara hao walitaka walipwe Sh141 milioni kwa kila ekari wakati wao walinunua ardhi kutoka kwa wananchi kwa Sh5 milioni kwa ekari, jambo ambalo alisema lilishapitishwa awali.

“Niligundua pale kuna udanganyifu na wizi mkubwa. Haiwezekani mwekezaji anunue kutoka kwa wananchi ekari moja kwa Sh5 milioni, kisha Serikali tumlipe Sh141 milioni kwa ekari kwa kuvuka pantoni tu. Ni wizi mkubwa.

"Kama kweli Serikali ina fedha hizo kwa nini tusimlipe mwananchi moja kwa moja?” alihoji.

Waziri Lukuvi alisema endapo njama hizo zingefanikiwa, Serikali ingetumia zaidi ya Sh84 bilioni kuwalipa wawekezaji hao hewa kwa kuwa mmoja anamiliki takribani ekari 200 na mwingine 400.

“Niliwaambia Serikali haiwezi kuwalipa fedha hizo na badala yake waende kuiendeleza ardhi wenyewe kulingana na mradi unavyotaka. Walitaka kutajirika kwa ujanja ujanja,” alisema Lukuvi na kuongeza:

“Eti walidai wamekopa fedha benki kwa ajili ya mradi huo. Haiingii akilini mtu utumie Sh5 milioni, halafu uje uvune mabilioni ya fedha kwa kuvuka pantoni tu.”

Picha 12 za Mkutano wa Hadhara wa Kumtambulisha Katibu mkuu CHADEMA Dr Vicent Mashinji -Furahisha Mwanza

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vicent Mashinji, jana alitambulishwa rrasmi kwa wakazi wa Mwanza kwenye uwanja wa furahisha.

Viongozi mbalimbali wa kitaifa wa Chadema pamoja na baadhi ya Wabunge kutoka Chadema walikuwepo kuushuhudia utambulisho huo wa Katibu Mkuu wao kwa wananchi.

Tangaza Biashara Yako Au Bidhaa Yako Kwenye Mtandao huu Kwa BEI NZURI Kabisa

$
0
0

Tunakaribisha  matangazo  ya  aina  zote.Bei  zetu  ni  nzuri  sana  na  kamwe  hutajuta  kutangaza  biashara  yako  kupitia  mtandao  huu....

Kwa Siku tunafunga na Pageviews zaidi  ya  laki tano kama graph  inavyoonyesha  hapo  chini
Kama  una  tangazo, basi  wasiliana  nasi  kwa  kutuandika  email  ambapo  tutakutumia  bei  ya  matangazo.

Email  yetu:  mpekuziblog@gmail.com

Kauli Ya Abbas Kandoro Baada Ya Rais Magufuli Kutomchagua Kuwa Mkuu wa Mkoa

$
0
0
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe  Magufuli  alitoa orodha ya wakuu wapya wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.

Katika orodha hiyo Rais Magufuli , amewaacha wakuu kadhaa akiwamo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro.

Kipindi cha Sun Rise cha Radio Times Fm, kimefanya mahojiano na Kandoro asubuhi ya leo, ambapo amekiri kuachwa kwake na kuongeza kuwa tayari amefikia kikomo cha uongozi kwa maana umri wake haumruhusu kuendelea kutumikia nyadhifa hiyo.

“Unajua kuna watu wakituona wanajua kwamba bado tupo kwenye ujana, Ndugu mtangazaji mimi nina miaka 66 sasa hivi, tayari umri umenitupa mkono katika nafasi hii.

“Haijanishtua kwa sababu wakati tunapewa hii mikataba tuliambiwa kabisa ukomo wa mkuu wa Wilaya ni miaka 60 na Ukuu wa Mkoa ni miaka 66, hivyo nmetimiza umri wangu kisheria na napenda nimshukuru Mh Rais kwa hili” Alisema Abbas Kandoro.

Mpaka kustaafu kwake, Kandoro amehodhi nafasi ya ukuu wa Mikoa katika zaidi ya Mikoa Sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Singida na Mbeya.

Zitto Kabwe Ataka Benk Ya Standard Ichunguzwe Upya Kwa Rushwa......Anakuomba Mtanzaia Uweke saini yako Kwenye Petition Hii ili Uchunguzi Ufanyike

$
0
0

Mbunge  wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amesema Benki ya Standard inapaswa kuchunguzwa kwa rushwa kuhusu suala la hati fungani ya Dola za Marekani milioni 600.

Amesema kwa sasa deni la Taifa limepanda na kufikia dola bilioni 15  sawa na Sh trilioni 30, ambapo kutokana na ukubwa wa deni hilo, Tanzania hulipa huduma ya deni la Taifa takribani Sh trilioni 2.2 kila mwaka.

Alisema licha ya hali hiyo bajeti ya kuhudumia deni la Taifa ni kubwa zaidi kuliko bajeti ya wizara yoyote nchini.

Alisema kutokana na suala hilo katika madeni hayo yapo ambayo yamepatikana kwa rushwa na mengine yamechukuliwa kwa matumizi ya anasa.

“Kitaalamu madeni haya yanaitwa ‘Odious debts’. Moja ya Deni la hovyo ni la dola za Marekani milioni 600 ambalo Tanzania ilikopa kutoka Benki ya Standard ya Uingereza kupitia hati fungani.

“Taasisi ya SFO ya Uingereza inayoshughulika na rushwa kubwa imeonyesha kuwa mkopo huu ulipatikana kwa rushwa. Taasisi ya Corruption Watch ya Uingereza imeonyesha kuwa Tanzania imepata hasara ya takribani dola milioni 80 sawa na bilioni 160 kwa kuchukua mkopo huu.

“… hata hivyo uchunguzi wa SFO haukuhusisha maofisa wa juu wa Standard Benki makao makuu na hivyo kufunika kombe mwanaharamu apite.

“Iwapo uchunguzi ungegundua kuwa Standard Benki walihusika moja kwa moja na hongo hii, Tanzania ingefutiwa deni lote na kuokoa fedha nyingi sana ambazo zingewekezwa kwenye sekta za elimu, afya na maji,” alisema Zitto.

Mbunge huyo wa Kigoma Mjini, alisema wanaitaka Benki ya Standard ya Uingereza ichunguzwe upya na SFO kuhusu tuhuma za rushwa ili kupata biashara Tanzania ya hati fungani pamoja na kujua ukweli wa kile alichodai ufisadi huo.

Kutokana na hali hiyo alisema wameandaa maombi kwa kuitaka FSO ya Uingereza ifungue upya uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya kuwa mabosi wa Benki ya Standard ya Uingereza walihusika na mipango ya kutoa hongo ili kupata biashara Tanzania.

Alisema ikibainika mabosi hao walishiriki maana yake Tanzania itafutiwa deni lote kwa sababu benki hiyo itawajibika kurudisha fedha za watu kwani Hati fungani itaonekana ni batili.

Zitto  alisema hivi sasa Tanzania inaanza kulipa deni hilo kuanzia Aprili, mwaka huu na kama wasipozuia tunazuia kwa maombi haya kwa FSO.

Alisema iwapo deni hilo litalipwa juhudi za Rais Dk. John Magufuli, kupata mapato zitaathiriwa na sekta nyeti kama elimu, afya na maji zitakosa bajeti ya kutosha.

Alisema kutokana na hali hiyo aliwaomba Watanzania kote duniani kuitaka SFO ifungue uchunguzi kwa kuzingatia ushahidi mpya dhidi ya Benki ya Standard ambayo sasa inaitwa ICBC plc

Standard Bank wachunguzwe Kwa rushwa Hati Fungani ya USD 600m Kwa Tanzania Deni la Taifa la Tanzania sasa ni USD 15...
Posted by Zitto Kabwe on Saturday, March 12, 2016

==>Petition hii imeletwa kwenu na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi ughaibuni. 
 
Bofya hapo chini kuweka saini yako ili  kuwashawishi SFO wafanye uchunguzi upya. Tetea Tanzania yako. Uzalendo wako ndio uhai wa Tanzania yako. 

<<<BOFYA  HAPA>> 

Bofya  hapo  juu  kuweka saini yako

Kigwangalla Awapa Pole CHADEMA Kwa Kumchagua Dr. Machinji Kuwa Katibu Mkuu Wao

$
0
0

Zikiwa zimepita siku mbili toka kupatikana kwa Katibu Mkuu mpya wa CHADEMA Dk Vincent Mashinji,  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla  ameibuka na kuwapa pole CHADEMA kama walimchagua Katibu Mkuu wao kwa kuangalia historia yake.
 
Kupitia Account yake ya Facebook Dk Hamisi Kigwangalla anakiri wazi kuwa Dkt. Mashinji ni msomi mzuri na mwanasiasa mzuri ingawa anadai hana uhakika kama alimaliza masomo ya ubingwa.
 
"Ndg., Dkt. Mashinji is a friend, brother and colleague. Hakuwahi kutuokoa mimi na Dkt. Ulimboka, na hakuwahi kuongoza mgomo, sema alishiriki mgomo ulioongozwa na mimi na Dkt. Ulimboka. 

"Kiukweli, ni mwanasiasa mzuri, msemaji, msomi mzuri (tumesoma naye MBA chuo kimoja), sina hakika kama alimaliza masomo ya Ubingwa maana alinyanyaswa na Supervisor wake, akasusa akaamua kujiiunga masomo ya MBA na sina hakika sana kuhusu 'msimamo usiotetereka'. 

"Maana baada ya vitisho vya 2005, aliyumba sana na tulimtenga na ku-aVoiD kumualika vikao vya CC ya mgomo. Hivyo, kama kigeZo kilikuwa ni hii historia, pole kwa CHADEMA." Ameandika Dk Kigwangalla


Ndg., Dkt. Mashinji is a friend, brother and colleague. Hakuwahi kutuokoa mimi na Dkt. Ulimboka, na hakuwahi kuongoza...
Posted by Hamisi Kigwangalla on Sunday, March 13, 2016

Anna kilango Malechela: Rais Magufuli Anaujua Utendaji Wangu ndio Maana Amenipa Nafasi ya Ukuu wa Mkoa.

$
0
0

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Same Mashariki ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa mteule wa Shinyanga, Anna Kilango Malechela, amesema jitihada zake na utendaji katika kuihudumia jamii ndio sababu kuu iliyomfanya Rais Magufuli  kumpa nafasi ya kuuongoza mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza kupitia Kipindi cha Sun Rise cha Times Fm, Malechela amedai hata ‘anguko’ lake katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, aliangushwa na watu wenye sababu binafsi na si kukataliwa na Wananchi.

“Mungu ni mwema, sikuwa na hili wala lile, nimekaa Bungeni miaka 15 na Mh Rais akiwa kama Mbunge, kwahiyo alikuwa anaona utendaji wangu, kupambana na kero za wananchi na jinsi nilivyo na jitihada.

“Unajua wanaosema tunabebwa tulianguka kwenye uchaguzi, watazame kwa  upana zaidi, wengine tuliangushwa, naahidi kutumia kauli mbiu ya kazi tu kuitumikia Shinyanga” Alisema Mama Anna Kilango.

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Lampongeza Rais Magufuli Kwa Kutumia Lugha Ya Kiswahili Kwenye Mikutano ya Kitaifa na Kimataifa

$
0
0
Na Lorietha Laurence- MAELEZO
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa uzalendo wake wa kuitumia lugha ya Kiswahili katika mikutano mikubwa na hafla mbalimbali za kitaifa na kimataifa.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi BAKITA, Prof. Martha Qorro ameeleza msimamo huo wa Rais Dkt.Magufuli  umewasidia Watanzania kupata taarifa moja kwa moja kutoka tukio husika.

“Uamuzi na msimamo wa Rais Magufuli wa kutumia lugha ya Kiswahili katika mikutano mikubwa ikiwemo  mkutano mkuu wa 17 wa viongozi wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umepokelewa kwa furaha kubwa na wananchi na wadau wengi wa Kiswahili ndani na nje ya Tanzania” alisema Prof.Martha.

Aliongeza kuwa kupitia msimamo huo wa Mhe. Rais Magufuli,   Baraza linaamini kwamba hatua hiyo itasaidia kukuza lugha ya Kiswahili na kutoa fursa ya ajira kwa Watanzania kupitia tafsiri na ukalimani na hivyo kuwapelekea maendeleo wananchi wote wa Afrika Mashariki.

Naye Katibu Mtendaji wa BAKITA Dkt. Seleman Sewangi ametoa wito kwa viongozi wengine wa ngazi mbalimbali za Kitaifa kufuata nyao za Mhe.Rais Magufuli kwa kuipa kipaumbele lugha ya Kiswahili ili kufikisha ujumbe kwa Watanzania walio wengi.

“Natoa wito kwa viongozi wetu wa ngazi mbalimbali za kitaifa kuitumia lugha ya Kiswahili katika mikutano mikubwa na hafla mbalimbali za kitaifa na kuachana na dhana ya kutumia lugha ya kigeni yenye lengo la kuwafurahisha wageni wachache” alisema Dkt. Sewangi.

Aidha, aliongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya kiswahili inatumiwa vizuri, Baraza hilo linaendelea kutekeleza mkakati wa kukamilisha kanuni zitakazopelekwa bungeni ili kumuwezesha Waziri mwenye dhamana kuwa na mamlaka ya kusimamia sheria ya lugha ya Kiswahili ya mwaka 1961 iliyorekebishwa mwaka 1985 ili kuipa nguvu ya kumshitaki mtu yeyote kwa matumizi mabaya ya lugha hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi,Taasisi ya Taaluma za Kiswahili chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Ernesta Mosha ameziomba ofisi za Serikali hususani mahakama kutumia lugha ya Kiswahili kwa kuwa ni lugha inayoeleweka na Watanzania wengi ikizingatiwa kuwa sio wote wanajua kutumia lugha ya kiingereza.

Kampuni ya Total Yamhakikishia Rais Magufuli Ujenzi wa Bomba la Mafuta Kutoka Uganda Hadi Tanzania Haraka Iwezekanvyo

$
0
0
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo  amemuhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha Mafuta kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga hapa Tanzania haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.

Bw. Javier Rielo ametoa ahadi hiyo leo tarehe 14 Machi, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam.

Mradi huo utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.

Katika Mazungumzo hayo Bw. Javier amemueleza Rais Magufuli kuwa Kampuni yake inatarajia kutumia dola za kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa.

Pamoja na kuukaribisha uwekezaji huo mkubwa kwa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka kampuni hiyo kuharakisha mchakato wa kuanza kwa mradi, na ameshauri muda wa miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi huo upunguzwe, ili manufaa yake yaanze kupatikana mapema.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, amesema Wizara yake ipo tayari kuhakikisha mradi huo unafanikiwa, na itatoa ushirikiano wa kutosha kuharakisha utekelezaji wake.

Prof. Mhongo amebainisha kuwa licha ya kwamba hali ya kijiografia, hali ya hewa na bandari ya Tanga vinatoa mazingira bora ya kufanikiwa kwa mradi huo, Tanzania pia inatarajia kunufaika na bomba hilo, kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta zinazoendelea katika ziwa Tanganyika na katikati mwa Tanzania, ambazo zikikamilika kwa mafanikio inatarajiwa bomba hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
14 Machi, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa wajumbe walioambatana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,   Javier Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,   Javier Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam

CUF Watoa Tamko Zito Kuhusiana na Hali ya Kisiasa Zanzibar

$
0
0
Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa tareh 25 Oktoba 2015, usalama wa raia wa Zanzibar na mali zao umekuwa katika hali tete. 


Hali hii inatokana na kushuhudiwa kushamiri kwa matukio ya kuogopesha wananchi na kufurutu ada ukiukwaji wa HAKI ZA BINAADAMU miongoni mwa wananchi kunakofanywa na vyombo vilivyopewa dhamana ya kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi yetu raia wake na mali zao.

Katika siku za hivi kadribuni, hususan baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Sali Jecha, kutangaza kinyume na katiba ya nchi, kufuta uchaguzi wa 25 Oktoba 2015 na matokeo yake, Zanzibar imeshuhudia uingizwaji na uingiaji mkubwa wa askari, vifaa na zana nzito za kivita katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Sambamba na hayo kumekuwepo kwa askari wengi wa JWTZ wanaorandaranda mitaani wakiwa na silaha nzito za kivita na operasheni isiyo rasmi ya kuwakamata na kuwabambikizia kesi wananchi wasio na hatia na hatimaye kuwaweka katika vituo mbali mbali vya polisi na kuwanyima dhamana hata kwa makosa ambayo kisheria yanapaswa kudhaminiwa.

Katika mwezi wa February 2016 huko kengeja wafuasi wa CUF walikamatwa na polisi na kuwekwa ndani kwa tuhuma ya kuchoma tawi la CCM la eneo hilo. Polisi walichukuwa hatua hiyo mara tu tukio hilo liliporipotiwa kwao. Aidha katika mwezi huu wa Machi baadhi ya matawi ya CUF na Baraza za CUF zilichomwa moto na kuteketea tikitiki.

Taarifa ya uhalifu huu zlipripotiwa katika vituo vya polisi na RB kuandikwa, hata hivyo hadi hii leo hakuna yoyote aliyekamatwa kwa tuhuma ya uhalifu huo. Matukio ya uchomwaji moto na uharibifu wa mali za CUF umetokea mahala mwingi Unguja na Pemba kama vile Kisauni ambapo ofisi mpya ya CUF jimbo la Dimani zilizogharimu zaidi ya sh 90m zilichomwa moto tarehe 24/03/2015 na kuteketea. Kwa makusudi kabisa, hata baada ya polisi kupata taarifa hiyo na kulikagua eneo husika hakuna yeyote aliyetuhumiwa na kukamatwa.

Mtakumbuka kwamba tabia hii ya wananchi ambao kwa asilimia kubwa huwa ni CCM au vyombo vya serikali vilikuwa vikihujumu kwa makusudi mali ya CUF na hata mali ya serikali kama vile shule, zahanati, visima vya maji nk. Tukio la Shengajuu la 1996 ambapo watu waliofanya tukio la kcuhoma moto shule, kutia kinyesi visima walikamatwa wakiwa na petrol, bunduki, mapanga, madoo ya kinyesi vyote vikiwa usoni ya gari la idara ya usalama wa Taifa lenye namba za usajili ZNZ 1296).

Baada ya tukio hilo la kufedhehesha serikali na mapambamo yaliyofuata baina ya wafuasi wa CUF na wahalifu (usalama wa Taifa), serikali iliwaadhibu kwa kuwapiga, kuwaibia mali zao, kuwafanyia vitendo vya kinyama na kuwaweka ndani kwa zaidi ya miezi 9 wananchi wasio na hatia. Hivyo haya yanayoendelea hivi sasa huko Pemba si mambo mageni hasa katika kipindi hiki ambapo SMZ imechukia sana kwanini CUF wamegomea kushiriki uchaguzi batili wa madrudio wa 20/03/2016.

Sisi CUF tunaamini pasipo na shaka yeyote kwamba matukio ya kuchomwa moto kwa masikani na matawi ya CCM huko Pemba ama baadhi ya nyumba za watu binafsi na mali za serikali ni mwendelezo tu wa siasa chafu za chuki zinazoendelezwa na serikali dhidi ya wananchi wasio na hatia. CUF imesikitishwa sana na vitendo hivi vya kihuni na visivyoonyesha siasa za kistaarabu na inalaani vikali na kwa nguvu zote uhalifu huu ambao unarejesha nyuma ‘spirit’ ya kushindana bila kupigana.

Kwa upande mwengine, CUF imepokea taarifa kwamba zaidi ya wananchi 30 wengi wakiwa wafuasi, viongozi na wanachama wa CUF wamekamatwa na polisi na wameshikiliwa katika vituo mbali mbali vya polisi huko pemba. Utendaji huu wa Jeshi la polisi umeipelekea Zanzibar kugawika vipande vipande na kuwa chanzo cha siasa za chuki, uhasama na kusababisha nchi yetu kushindwa kutekeleza shughuli zake za kimaendeleo.

Kwa mfano amri ya Mkuu wa Mkoa kaskazini Pemba kupiga marufuku watu wasitembee baada ya saa mbili za usiku na kwamba atakayevunja amri hiyo atakamatwa na kushtakiwa kwa kosa la uzembe na uzururaji ni hatua nyengine ya SMZ ya kuwahalalilisha na kuwaweka wananchi wa mkoa wa Kaskazini Pemba katika hali ngumu ya maisha. Amri hii inazuwia hata sala za Isha na Alfajiri jambo ambalo waumini wa Kiislamu hawatakubaliana nalo.

CUF inamtaka Mkuu wa Mkoa uliotajwa hapo juu awache ukereketwa na aendeshe mkoa kwa hekima, busara, na weledi. Kuongoza watu kwa amri za kidikteta kumepitwa na wakati. Asome alama za nyakati, aache kutoa amri zinazopingana na hata haki za binaadamu.

Chama Cha Wananchi CUF kinaamini kuwa kutokea kwa matukio haya ni mwendelezo wa njama za CCM zinazoratibiwa na kutekelezwa kimkakati kwa malengo mahususi ya kuamsha hamasa na kupandisha joto la jazba miongoni mwa wananchi ili kuhalalisha mpango maalum na kutoa fursa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kutumika kutisha, kukamata, kupiga na kufungulia mashtaka wananchi wasio na hatia.

Kutokana na unyeti wake matukio ya uvunjifu wa amani na hatua za ukiukwaji wa HAKI ZA BINAADAMU, hayapaswi kupuuzwa kwani yanaweza kupelekea kufanikiwa kwa dhamira mbaya waliyonayo baadhi ya watu katika nchi yetu wasioitakia mema Zanzibar na kwa hivyo kuathiri umoja wa kimataifa uliopo uliopatikana kwa gharama kubwa ya jasho la viongozi wazalendo, Mheshimiwa Rais mstaafu wa Zanzibar Dr. Amani Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na uhai wa wananchi wanyonge. Kwa hivyo sisi katika CUF:

• Tunavinasihi vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi yetu kukataa katakata kuingia katika mtego wa mipango miovu ya wanasiasa waliofilisika wenye lengo la kuleta taharuki miongoni mwa wananchi na kuamsha hamasa na kupandisha jazba na ghamidha zitakazopelekea kuchafuka kwa hali ya amani ya nchi yetu. CUF inatoa wito kwa kwa vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama hapa nchini kusimamia amani na utulivu pasi na kuegemea upande wowote wa kisiasa.

Ni muhimu vyombo hivyo vikajipambanua na kujijengea heshima na kulinda imani ya wananchi waliyonayo kwao. Kinyume na haya, vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hasa jeshi la polisi na jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ, ambalo katika siku za hivi karibuni limeonekana kutumika vibaya, kufahamu kuwa mustakbali wa utu wa raia, mali zao na amani ya nchi yetu imo mikononi mwao na watakuwa wa mwanzo kuwajibika endapo jahazi la amani yetu litakwenda mrama.

• Tunaziomba Taasisi za kiraia za ndani kuacha woga na badala yake kupaza sauti zao masikioni mwa viongozi madhalimu kukemea unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za binadamu. Aidha, CUF inaziomba jumuiya za kimataifa kuendelea kuitazama Zanzibar kwa umakini wa hali ya juu kufuatilia mwenendo na matukio na kuweka kumbukumbu kwa hatua za baadae kwa kila anaeonekana kushtadi kuonea wananchi wanyonge kutokana na nafasi yake katika utumishi wa umma.

• Tunatoa wito kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, John Magufuli, kuchukua dhamana ya uongozi kukataa kuhadaiwa na wasaidizi wake na kukomesha matumizi mabaya ya vyombo vya ulinzi na usalama vilivyo chini ya amri yake na kudhibiti uhuni wa kisiasa wa baadhi ya watendaji wa vikosi vya Idara Maalum ya Zanzibar kama Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania. Kwa la zanzibar, Rais Magufuli hana pa kupenyea na kwamba atawajibika kutokana na mfumo wa Katiba, sheria na utaratibu wa kuongoza nchi tuliojiwekea.

• Tunatambua usumbufu, idhilali na mateso makubwa yanayowapata wananchi wa visiwa vyote vya zanzibar kufuatla maamuzi yao ya tarehe 25 Oktoba 2015 ya kuikataa CCM na kuamua kufanya mabadiliko katika uongfozi wa nchi. CUF inawaomba wananchi wote kuendelea na kujipamba na mavazi ya subira na kuamini kuwa hizi ni hatua za mwisho za CCM kuelekea kufutika katika nyoyo za wazanzibari na kwamba wananchi wote wausiane katika kuvumilia na kukataa kuchokozeka kwa lengo la kutunza amani ya nchi yetu na kufikia malengo yetu ya muda mrefu ya kukamata hatamu za dola ya zanzibar bila kuathiri wanachi wetu.

• CUF inawahakikishia wananchi wote kuwa haitarudi nyuma katika mapambano ya kudai haki ya wananchi na kwamba maamuzi yao ya tarehe 25 Oktoba 2015 yatazingatiwa, kuheshimiwa na hatimaye haki kutamalaki katika visiwa vya zanzibar. Ni wajibu kwa wazanzibari wote kutambua kuwa giza nene hufuatiwa na miale ya nuru inayotoa faraja kwa kila mwanandamu.
……………………………….
HAMAD MASOUD HAMAD
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA
MAWASILIANO KWA UMMA

Picha: Wafuasi wa CHADEMA Wafurika Mahakamani Kufuatilia Kesi ya Ezekiel Wenje ...Polisi Walazimika kutumia nguvu ya ziada kuimarisha ulinzi

$
0
0
Mamia ya wafuasi wa CHADEMA  wakiongozwa  na  Mwenyekiti  wao Freeman Mbowe leo  wamefurika mahakama  kuu  jijini  Mwanza katika kesi ya  mbunge wa zamani wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA)  anayepinga  matokeo  ya  Stanslaus Mabula (CCM). 

Polisi  wametumia  nguvu  ya  ziada  kuhakikisha  ulinzi  unaimarika  mahakamani  hapo
Ezekia Wenje akiwa  Mahakamani
Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula akiwa mahakamani
Ezekiel Wenje akisubiri kutoa ushahidi
Freeman Mbowe na  Ezekiel Wenje wakiwa mahakamani

Afisa Mifugo Anusurika Kutumbuliwa Jipu Na Waziri Mkuu

$
0
0

AFISA MIFUGO wa kata ya Kakunyu, wilayani Misenyi mkoani Kagera, Bw.Eric Kagoro amenusurika kutumbuliwa jipu kwenye mkutano wa hadhara kuhusiana na sakata la kuruhusu ng’ombe 291 waje kulishwa kwenye ranchi ya mifugo ya Misenyi.
 
Tukio hilo limetokea leo mchana (Jumatatu, Machi 14, 2016) wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mamia ya wananchi waishio jirani na ranchi hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye makao makuu ya ranchi hiyo.
 
Waziri Mkuu alimuibua Bw. Kagoro katikati ya mkutano kwa kumtaja jina na tuhuma zinazomhusu kuhusu mifugo iliyokamatwa. “Afisa Mifugo wa kata yupo hapa?." Aliuliza  Waziri Mkuu.  "Wewe ndiyo Eric?” Alipojibu ndiyo akaulizwa tena:”Nimekujuaje?”
 
“Nimeambiwa wale ng’ombe waliokamatwa ni wa rafiki yako na wewe ndiye ulitoa kibali waje kulishwa kwenye ranchi hii. Siyo kazi yako kuruhusu mifugo ya nje ije kulishwa hapa kwenye ranchi. Kuanzia sasa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingiza mifugo kwenye ranchi ili ipate malisho “
 
“Leo Nimekusamehe .Kazi yako ni kuhakikisha mifugo ya kwenye kata hii iko salama. Kazi yako ni kuwasaidia wafugaji wa kata hii wafuge vizuri na uhakikishe mifugo yao inakuwa na tija.” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
 
Kwa upande mwingine,  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaasa watendaji wa kata na vijiji kutotumia nafasi zao kuleta migogoro baina ya watu wa nje na wananchi wanaowaongoza. “Mwenyekiti wa kijiji huna ruhusa ya kugawa kitalu cha ranchi au kuruhusu mtu yeyote akalime ndani ya ranchi”, alisema.
 
Aliwataka pia maafisa uhamiaji wawe makini na vyeti vya kuandikisha uraia wanavyovitoa kwa wananchi wanaoishi mipakani kwani imekuwa ni mianya ya kuleta migogoro ya ardhi. “Watu wa uhamiaji kuweni makini na CN mnazotoa (CN=Certificate of Naturalisation). Wote wanaoomba CN wanataka blocks tu”
 
Alitoa agizo kuwa watafutwe watu wote walioingia nchini kwa mgongo wa CN, wakamatwe na kurejeshwa makwao. “Kuna watu wamekuja hapa nchini wakaomba CN lakini wakikaa wanaleta wenzao waje kununua ardhi kwa kutumia mgongo wa CN  zao.”
 
Alisema kuna watu wametoka wilaya ya Karagwe ambako pia kuna tatizo kama la Misenyi na kuwataka wahusika wajiandae kuchujwa na kuchukuliwa ardhi zao kama watakuwa hawajaziendeleza ili wapewe Watanzania wenye uhitaji wa kulima na kufuga.

Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 14, 2016

$
0
0
Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 14, 2016







Kesi ya IPTL Dhidi ya Zitto Kabwe kusuluhishwa Machi 23 Kwa Siri

$
0
0

Mahakama Kuu inatarajia kusuluhisha kesi iliyofunguliwa na Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) dhidi ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe na wenzake Machi 23, mwaka huu.

Kesi hiyo namba 175 ya mwaka 2014 ilipangiwa kuanza kufanyiwa usuluhishi jana mbele ya Jaji Salvatory Bongole, lakini ilishindikana kutokana na upande wa walalamikaji ambao ni IPTL kushindwa kufika mahakamani.

Hata hivyo, Kaimu Msajili wa Mahakama hiyo Kitengo cha Usuluhishi, Beda Nyaki alisema kesi hiyo itasikilizwa kwa siri baina ya pande hizo.

“Kesi hii haiwezi kuripotiwa kwenye vyombo vya habari kwa sababu ipo katika hatua za kwanza za usuluhishi, hivyo kitu kitakachoongolewa baina ya walalamikaji na walalamikiwa kitakuwa ni siri yao,” alieleza Nyaki.

Alisema kusikilizwa kwa faragha kwa kesi hiyo ni hatua ya kupunguza gharama na muda.

Katika kesi hiyo, Kampuni za IPTL, Pan Africa Power Solutions (T) Limited na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hizo, Harbinder Sing Seth walifungua madai ya Sh500 bilioni dhidi ya Zitto, Mhariri wa gazeti la Raia Mwema, Kampuni ya Raia Mwema na Kampuni ya Flint Graphics ikiwa fidia kwa kuwakashfu kuhusiana na sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow.

Mawakili wanaomtetea Zitto ni Wakili Ntemi Masanja na Ivone Sianga ambao walidai kuwa walalamikaji walishindwa kufika mahakamani hapo na kusababisha kuahirishwa kwa kesi.

Ilidaiwa kuwa walalamikaji hao walichukua hatua ya kufungua kesi hiyo kufuatia makala aliyoyaandika Zitto katika gazeti la Raia Mwema la Agosti 13, 2014 katika ukurasa wa saba na wa 14, ikiwa na kichwa cha habari “Fedha za IPTL ni mali ya umma.’’

Walalamikaji hao walidai kuwa makala hiyo ni ya upotoshaji na ilikuwa na lengo la kuwachafua mbele ya jamii.

Shule Ya Sekondari IYUNGA Ya Jijini Mbeya Yafungwa

$
0
0

Uongozi mkoani Mbeya umeifunga Shule ya Sekondari Iyunga baada ya mabweni matatu kuungua moto na wanafunzi kulala nje kutokana na kuyaogopa mabweni yaliyobaki.

Kwa kawaida likizo fupi ilitakiwa kuwa kipindi cha pasaka, lakini shule hiyo ilifungwa Machi 11 hadi 25 na kwamba itaendelea kufungwa hadi Aprili Mosi.

Mkuu wa shule hiyo, Edward Mwantimwa alitoa maelezo hayo kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jaffo aliyefika shuleni hapo juzi kujionea uharibifu uliotokana na moto uliounguza mabweni matatu kwa nyakati mbili tofauti.

Mwantimwa alisema mara ya kwanza mabweni ya Nyerere na Mkwawa yaliungua Februari 29 na Machi 7 la Shaban Robert, jambo ambalo lilisababisha hofu kwa walimu na wanafunzi na kuanza kuyasusa mabweni mengine.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyirembe Munasa akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa alimueleza naibu waziri hatua zilizochukuliwa ikiwamo wadau kutoa misaada na kwamba, pia walikuwa wanaandaa harambee ambayo wangependa ifanyike Dar es Saalaam.

Jaffo alilitaja tukio hilo kuwa ni janga na kuahidi kuwashirikisha wabunge wote kuchangia kurudisha hadhi ya shule hiyo.

“Kuungua kwa shule hii kumeonyesha mengi yakiwamo ya uchakavu wa miundombinu,” alisema.

Alimtaka Nyirembe kusimamia ukarabati wa shule hiyo na uwe umekamilika ifikapo  Aprili Mosi.

Walimu Wanaotuhumiwa Kufanya Mapenzi na Wanafunzi Jijini Mwanza Waundiwa Kamati Maalum

$
0
0

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Mwanza kimeunda kamati kuchunguza tuhuma dhidi ya baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari Mihama wilayani Ilemala kujamiiana na wanafunzi wao.

Mwenyekiti wa CWT mkoani hapa, Sibora Kisheri alisema wameunda kamati hiyo baada walimu wanane, akiwamo mkuu, Joseph Marifedha kusimamishwa kazi kwa amri ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo, Magessa Mulongo kwa tuhuma hizo.

“Haiingii akili kuona walimu wote wakawa na sifa ya makosa yanayofanana, hivi hakuwapo hata mmoja aliyeshtukia mchezo huo na kuwashauri wezake,” alisema Kisheri.

Alisema uchunguzi huo unalenga kubaini kiini cha tuhuma hizo na kuishauri Serikali na vyombo husika hatua stahiki za kuchukua kuhakikisha kila upande unatendewa haki.

Aliwaasa walimu kufuata sheria, kanuni na misingi ya kazi kwa kutimiza wajibu na kuepuka mambo yanayokinzana na taaluma hiyo.

Hivi karibuni Mulongo aliwasimamisha walimu hao baada ya kupata taarifa kuwa walikuwa wakijihusisha na vitendo hivyo.

Vigogo wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (Rahco) Wafikishwa Mahakamani

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (Rahco), Benhadard Tito na wenzake wawili wamepadishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka manne.

Vigogo wawili wa Rahco na mfanyabiashara wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka, kula njama na kusababisha hasara ya dola za Marekani 527,540.

Mbali na Tito, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria wa Rahco, Emmanuel Massawe na mfanyabiashara ambaye pia ni mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.

Washtakiwa hao watatu walisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, huku upande wa mashtaka ukiwa na Maghela Ndimbo, Janeth Machulya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis.

Mawakili hao, wakiongozwa na Vitalis walidai kuwa washtakiwa wote watatu katika nyakati tofauti kati ya Septemba Mosi, 2014 na Septemba 30, 2015 katika Mkoa wa Dar es Salaam walikula njama ya kutenda makosa hayo chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.

Katika kesi hiyo, ilidaiwa kuwa Februari 27, 2015, Tito katika ofisi za Rahco zilizoko wilayani Ilala, alitumia madaraka yake vibaya kwa kuipitisha kampuni hiyo ya Rothschild kama mshauri wa mradi wa uimarishaji wa Reli ya Kati bila idhini ya Bodi ya zabuni ya Rahco, hivyo kwenda kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma.

Tito na Massawe wanadaiwa kuwa Machi 12, 2014 katika ofisi hizo za Rahco walitumia madaraka yao vibaya kwa kutia saini barua rasmi ya kuichagua kampuni hiyo, kama mshauri katika mchakato wa uimarishaji wa njia ya Reli ya Kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge).

Kati ya Machi 12 na Mei 20, 2015 katika ofisi za Rahco, Tito na Massawe wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kushindwa kuwasilisha mkataba wa huduma ya ushauri, baina ya kampuni hizo mbili kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Pia wanadaiwa kuwa kati ya Mei 20 na Juni 20, 2015 katika ofisi hizo washtakiwa hao, walishindwa kuwasilisha nakala ya mkataba kati ya kampuni hizo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mbali na mashtaka hayo, washtakiwa hao kwa pamoja kwa nyakati tofauti kati ya Machi Mosi na Septemba 30, 2015 walitoa huduma ya ushauri kwa kampuni hiyo, bila kufuata taratibu za ununuzi na malipo na walisababisha hasara ya dola za Marekani 527,540 ambazo zililipwa kama gharama za malipo ya awali.

Agosti 18, 2015, Tito akitekeleza majukumu yake, alitumia vibaya mamlaka kwa kuipatia kampuni ya China Railway Construction Corporation kazi ya ujenzi wa reli kwa kilomita mbili za kiwango cha kisasa kutoka Soga, iliyogharimu dola Marekani 2, 312,229.39 bila ya kuwa na idhini ya bodi ya zabuni ya Rahco.

Washtakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu. Uamuzi wa dhamana utatolewa Ijumaa.

Makahaba 287 Pamoja na Wateja Wao Watiwa Mbaroni Jijini Dar es Salaam

$
0
0

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata jumla ya watu 287 ambao ni dada poa pamoja na kaka poa katika operation maalum iliyofanyika maneo mbalimbali ya Jiji hilo.

Operation hiyo ilitangazwa na kamishna wa kanda maalum mnamo Tarehe 7 mwezi wa 3 na kuazimia kuwakamata madada poa na makaka poa pamoja na wateja wao ambao watakutwa wakiwanunua.

Katika mkoa wa kipolisi wa ilala operation hii imefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa 51 kutoka katika maeneo mbalimbali yakiwemo msimbazi,Buguruni,na stakishari,pia imewakamata jumla ya makaka poa 12 ambapo 11 wanatokea Buguruni na mmoja kutoka msimbazi.

Mkoa wa kipolisi wa temeke umefanikiwa kuwakamata jumla ya madada poa 22,ambapo changombe walipatikana 12,na mbagala walipatikana madada poa 10.
 
Aidha katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni operation hiyo imefanikiwa kuwakamata madada poa 76 kutoka maeneo ya osyterbay madada poa 49,magomeni 23,na kawe madada poa 4,pamoja na makaka poa 4.

Akizungumza na wanahabari jana makao makuu ya polisi kanda maalum ya Dar es salaam ,Kamishna wa kanda hiyo CP Simon Sirro aliwataka watu wenye tabia kama hizo kuacha mara moja kwani ni kinyume na mila na desturi za mtanzania ambapo amewataka kutafuta biashara nyingine halali za kufanya.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images