Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Picha: Ester Bulaya Awasili Jijini Mwanza Baada Ya Kuhojiwa Kwa Masaa Matatu na Kisha Kuachiwa Huru

0
0
Mbunge  wa  Bunda  mjini.Ester Bulaya   amewasili  jijini  mwanza  usiku  huu  baada  ya  kuhojiwa  kwa  masaa  matatu  jijini  Dar  na  kikao  cha  kamati  ya  haki, kinga  na  madaraka ya  bunge.


Bulaya  alikamatwa  usiku  wa  manane  wa  kumkia  leo  kwa  amri  ya  spika  wa  bunge  ambapo  alisafirishwa  hadi  jijini  Dar es Salaam   kwa  ndege  kujibu  tuhuma zinazomkabili.

Akiongea  na  waandishi  wa  habari  baada  ya  kurejea  jijini  Mwanza usiku huu, Bulaya  amesema  anashangazwa  na  kitendo  cha  serikali  kutumia  pesa  na  nguvu  nyingi  kumkamata  wakati  pesa  hizo  zingeweza  kutumika  kuboresha  maisha  ya  askari  polisi 


Breaking News: Dr Vicent Mashinji Atangazwa Rasmi Kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Kuchukua Mikoba ya Dr Slaa

0
0
Dr. Vicent Machinji ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kupitishwa na Baraza Kuu la Chadema, katika kikao chake kilichokaa jijini Mwanza.

Katika Kikao hicho cha Baraza Kuu kilichodumu hadi saa  nne usiku, Freeman Mbowe alitangaza jina la Dk. Machinji na kuungwa mkono na wajumbe wa baraza hilo, hivyo anajaza nafasi iliyoachwa na Dk. Willibrod Slaa, aliyejienguwa ukatibu mkuu wa chama hicho.

Jina la Dk. Machinji halikuwa miongoni mwa wanachama wa Chadema ambao walikuwa wanatarajiwa kumrithi Dk. Slaa kwani waliokuwa wanatabiriwa kukatia kiti hicho ni Salum Ally Mwalimu, Frederick Sumaye, Benson Kigaila, John Mnyika, Dk. Marcus Albanie na Prof. Mwesiga Baregu.

Nafasi ya Katibu wa Chadema ilikuwa wazi tangu Dk. Slaa alipoondoka Chadema muda mfupi baada ya chama hicho kumpitisha Edward Lowassa aliyetokea CCM kuwa mgombea urais wa chama hicho na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya March 13

Wafanyakazi Waliofukuzwa NIDA Wagoma Kupokea Barua Za Kuachishwa Kazi

0
0

Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) waliofutiwa mikataba ya kazi, wamegoma kupokea barua za kuachishwa kazi wakidai kwamba hawajui kilichoandikwa kuhusu hatima ya madai yao.

Wafanyakazi hao walikutana jana Dar es Salaam na kiongozi wao, Seif Kibangu alisema wamekubaliana kutochukua barua hizo hadi pale watakapopata ushauri kutoka kwa wanasheria.

“Licha ya mishahara ya miezi mitatu tuna madai yetu mengine ikiwamo makato ya mafao yetu yaliyotakiwa kupelekwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, pia tumekuwa tukikatwa bima ya afya asilimia tatu ya mishahara yetu hatujui hatma yake. 

"Sasa leo wanataka tuchukue barua hizo tena kwa kusaini kabla ya kujua kilichoandikwa hapana tuendelee kuvumilia haki yetu tutaipata,” alisema Kibangu.

Aliwakosoa waliochukua barua hizo akisema waliajiriwa kwa makundi, ingawa pia wapo waliopewa kazi hiyo kwa vimemo.

“Hili ni jasho letu, hatuibi cha mtu kwa hiyo tunastahili kupata haki zetu zote, mishahara tunayodai kwa miezi mitatu, acha hayo madai mengine... Tunadaiwa huko tunapoishi kwa kweli tunaomba wahusika waingilie kati jambo hili linatuumiza na kuyumbisha maisha yetu,” alisema.

 Akizungumza kwa niaba ya madereva wenzake, George Mmari alidai kuna gharama nyingi walizoingia ambazo Nida inapaswa kuzilipa ikiwamo malipo ya kuegesha na kuosha magari waliyokuwa wakiendesha.

Akizungumzia madai hayo, Ofisa Habari Mwandamizi wa Nida, Rose Mdami alieleza kushangazwa na hatua ya wafanyakazi hao kugoma kuchukua barua zao badala ya kuzipokea ili wajue kilichoandikwa ili kama wana madai waandike barua na kuyaorodhesha.

Nyumba za Wananchi , Kituo cha Afya na Ofisi za CCM Zachomwa Moto Pemba

0
0

Zikiwa zimebakia siku saba kufanyika marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, kumejitokeza viasharia vya uvunjifu wa amani kwa kuharibiwa majengo ya Serikali na nyumba za watu binafsi.

Usiku wa kuamkia jana, Kituo cha Afya cha Kiuyu Minungwini, Maskani ya CCM Junguni pamoja na nyumba za wananchi katika maeneo ya Kangagani, Makangale, Msuka, Tumbe na Shumba, zimeteketezwa kwa moto na watu wasiofahamika.

Akizungumza kwa nyakati tofauti alipotembelea waathirika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud mohamed alilaani kitendo hicho.

Alisema kinachoonekana, hujuma hizo zinapangwa na watu wasioitakia mema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa lengo la kutaka kuwajengea hofu wananchi, nchi inapoelekea kwenye uchaguzi wa marudio, Machi 20.

Hata hivyo, aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, itachukua hatua za haraka ili kuwabaini wote waliohusika na hujuma hiyo.

“Hivi ni vitendo vya makusudi, haiwezekani matukio hayo yote yatokee siku moja katika maeneo tofauti na kwa wakati mmoja, tutahakikisha wahusika tunawasaka na kuwafikisha mahakamani,” alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza doria ili kuhakikisha amani na utulivu unadumishwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir Ali aliahidi kuwasaka na kuwachukulia hatua watakaobainika kuhusika kwa matukio hayo.

Alitoa rai kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa za watu wanaowatilia shaka katika maeneo yao.

“Tusiwaonee haya hawa watu, wanachangia kurudisha nyuma maendeleo yenu, mkiwaficha mtakuwa mnajiumiza wenyewe,” alisema kamanda huyo.

Mwenyekiti wa CHADEMA Ahukumiwa Kifungo cha Miezi 6 Kwa Kosa la Kumsaidia Ndugu Yake Kujitetea Mahakamani

0
0

Mwenyekiti wa Chadema, Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Jacob Munyaga (60), amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miezi sita gerezani kwa kosa la kumsaidia ndugu yake maelekezo ya namna ya kujitetea mahakamani.

Ilidaiwa kuwa kiongozi huyo alimsaidia mtuhumiwa Charles Mloba namna ya kujieleza mahakamani dhidi ya shauri la kujeruhi linalomkabili, kinyume cha sheria inayotoa fursa hiyo kwa mawakili pekee.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya hiyo, Francis Kishenyi akitumia kifungu cha 114(1) (A) cha Sheria ya Makosa ya Jinai namba 16 ya mwaka 2002 inayotoa adhabu kwa yeyote anayefanya kazi ya uwakili au usaidizi wa kisheria bila kuwa na sifa.

“Kwa mujibu wa kifungu hicho, adhabu kwa mshtakiwa inaweza kuwa kulipa faini ya Sh500 au kifungo cha miezi sita jela.

"Mahakama hii imeamua utumikie kifungo cha miezi sita jela kwa sababu umebainika kufanya vitendo hivi mara kwa mara,”
alisema hakimu huyo.

Alisema mshtakiwa huyo ana haki ya kukata rufaa kupinga adhabu hiyo ndani ya siku 30 kuanzia jana.

Awali, akijitetea kabla ya hukumu, Munyaga alidai alimsaidia mshtakiwa ambaye ni ndugu yake baada ya kumuomba amwelekeze namna ya kujitetea mahakamani dhidi ya mashtaka yanayomkabili.

Mshtakiwa Charles Mloba na mwenzake Mafuru Iloze, wote wakazi wa Kisiwa cha Ilugwa wilayani Ukerewe wanakabiliwa na kesi ya kujeruhi kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Jinai iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002

Mbunge wa CCM Faustine Ndugalile Awakosoa Mawaziri wa Rais Magufuli

0
0

Mbunge  wa Kigamboni, Dar es Salaam ,Faustine Ndugalile (CCM) amekosoa utendaji wa mawaziri wa serikali ya Rais Magufuli  akisema wanatishia wafanyakazi badala ya kuwaelekeza katika utendaji wao.

Katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wa twitter kwa lugha ya kiingereza, Ndugalile ameandika: "Ministers should encourage or provide practical solutions to problems instead of barking orders and terrorizing civil servants."

 Kwa lugha ya kiswahili, mbunge huyo alimaanisha:" Mawaziri wanatakiwa kuwatia moyo au kutoa suluhisho kwa matatizo badala ya kufoka na kuwatisha watumishi wa umma."

Alipoulizwa kuhusu ujumbe huo,Ndugalile alikiri kuwa ni wake na kusisitiza kuwa ni wajibu wake kama mbunge kuisimamia serikali.

"Mimi ni mbunge, kazi  ya  mbunge ni kuisimamia serikali.Ikifanya vizuri tutaisifia, ikikosea tutaikosoa.

"Nimesema baadhi  ya  mawaziri- sio wote wanawatisha wafanyakazi. Kazi ya kiongozi ni kuonyesha uongozi na si kuwa bosi.

"Inaonyesha kuna baadhi ya  mawaziri wamekuwa kila kitu ;wao ndo mawaziri,ndo wakurugenzi, ndo wakuu wa idara..." alisema

Ndugalile anakuwa mbunge wa kwanza wa CCM kukosoa kasi ya mawaziri wa Rais Magufuli, huku mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe akimkosoa Rais Magufuli kwa kuwasimamisha baadhi ya watendaji wa serikali bila kufuata taratibu za utumishi wa umma na sheria za kazi.

Akifafanua zaidi, Ndugalile alisema baadhi ya mawaziri wamekuwa wakitoa amri zisizotekelezeka na zinazotofautiana  na  ilani ya uchaguzi ya CCM  ya mwaka 2015.

"Kuna baadhi ya mawaziri wanatoa amri zisizotekelezeka.Kwa mfano, mtu anatoa amri itekelezwe ndani ya siku 3, itawezekanaje? umewapa rasilimali za kutekeleza?" alihoji Ndugalile.

Hata hivyo, Ndugalile alisema anaunga mkono hatua za kudumisha nidhamu kwa watumishi wa umma zinazofanywa na mawaziri.


Katibu Mtendaji NACTE Ajiuzulu....Ni Kutokana na Tuhuma za Kughushi Vyeti

0
0
==>Aliyekuwa Katibu Mtendaji wa NACTE Dokta Primus D Nkwera (kulia) akifafanua jambo
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la  Elimu ya Vyuo vya Ufundi( NACTE),Dr. Primus Nkwera amejiuzulu nafasi yake.

Uamuzi wa kujiuzulu  kwa  Dr. Nkwera ulitangazwa katika ofisi  kuu  za Baraza  hilo  zilizopo  Mikocheni  Dar es Salaam juzi na Mwenyekiti  wa  Bodi,Mhandisi Steven Mlote na kusababisha  baadhi  ya  wafanyakazi  kuangua  kilio.

Akizungumza katika kikao cha dharura cha wafanyakazi wote wa baraza hilo,Mlote alisema Dr. Nkwera amejiuzulu  ili  kulinda  hadhi  ya Nacte kutokana  na  habari iliyoandikwa na Gazeti la Dira ikimtuhumu mambo mbalimbali.

Gazeti  hilo la Dira la Jumatatu tarehe 07/03/2016 toleo no.405 lilimtuhumu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dr.Primus Nkwera  kughushi vyeti vya shahada ya uzamivu  baada ya kusomeshwa na serikali Afrika Kusini na kufeli.

Mlote alisema kwa mujibu wa Dr. Nkwera, nafasi hiyo haipaswi kushikwa na mtu mwenye tuhuma  ya  aina  yoyote, na ametafakari na kuona ajiweke kando na uongozi wa Nacte ili uchunguzi ufanyike akiwa pembeni.

"Tumetumia muda mwingi kutafakari hoja  ya  Dr. Nkwera na hatimaye tumekubali kujiuzulu kwake kwa shingo upande," alisema Mlote na kuongeza:

"Kazi kubwa iliyofanywa na Dr. Nkwera akiwa kiongozi wa Nacte inafahamika na kila mmoja, vilio na machozi ya wafanyakazi wenzake yanadhihirisha kuwa kujiuzulu kwake kunaacha simanzi kubwa.

"Najua mmepata mshtuko mkubwa, lakini Dr Nkwera hajafa, yuko hai na huyu bado ni mtumishi wa serikali. Alichofanya ni kuamua kuachana na ukatibu utendaji.

"Tutaendelea kumtumia itakapobidi kwa ushauri.Wakati mwingine lazima mkubaliane  na  hali  hii, lakini pia  endeleen kuchapakazi kwa ufanisi kama  kawaida kana kwamba bado mko na Dr. Nkwera."

Kutokana  na  kujiuzulu  kwake, Mlote alisema bodi imemteua Mkurugenzi wa Mitaala wa Nacte, Dr Adolf Rutayunga kukaimu nafasi hiyo  wakati taratibu nyingine zikiendelea.

Akizungumza na wafanyakazi hao, Dr. Rutayunga alisema viatu alivyoviacha Dr. Nkwera ni vikubwa kwake, lakini  akaahidi kuendeleza yote  aliyoyaacha.


Mkuu wa Mkoa Wa Dar es Salaam Ampa ONYO Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amemtaka Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob, kuacha malumbano ya kisiasa na badala yake ajikite kufanya kazi.

Onyo hilo Sadiki limekuja baada ya Meya Jacob kukaririwa akisema manispaa hiyo ina uwezo wa kukabiliana na uamuzi wa serikali wa kutoa elimu ya bure bila kuhitaji fedha zinazotolewa na utawala wa Rais John Magufuli.

Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni inaongozwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao ni mwamvuli unaojumuisha wabunge na madiwani kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF).

Sadiki alisema hahitaji malumbano na kiongozi huyo ambayo hayana tija.

"Mimi sipendi malumbano yasiyo na tija baina ya viongozi," alisema Mkuu wa Mkoa na kuongeza; "unapokataa msaada kama huo wa kupunguza mapungufu katika sekta ya elimu, wanaoathirika ni watu waliowachagua."

Serikali imepanga kutumia Sh. Bilioni 137 kugharamia elimu bure katika miezi sita ya kwanza ya Rais wa tano, Magufuli.

Kiasi cha Sh. bilioni 18.77 kilitumwa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari za halmashauri zote hapa nchini na vyombo vya usimamizi wa mitihani kwa kila mwezi wa Januari na Februari, kwa ajili ya wanafunzi kusoma bure.

Pesa zilizogawanywa kwenye akaunti za shule za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote ni Sh. bilioni 15.7 kila mwezi na Sh. bilioni 3 kila mwezi kwenye akaunti vyombo vya usimamizi wa mitihani katika Halmashauri zote hapa nchini.

Mkuu wa Mkoa alisema fedha hizo zitapelekwa katika Manispaa zote na ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kutumia fedha hizo katika matumizi yaliyokusudiwa na si vinginevyo.

Sadiki alisema kwa sababu Rais Magufuli ni kiongozi wa wote, ana haki ya kutoa kwa wote bila kuzuia wala mipango yake kukataliwa.

"Yule ni mkuu wa nchi, hata kama wanakusanya fedha za kutosha, zipo taratibu za matumizi ya fedha hizo," alisema Sadiki.

Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mipango wakati akitoa taarifa ya kuanza kwa utumaji wa fedha za elimu bure Januari 6, mwaka huu, walimu wakuu wa shule zote za Msingi na Sekondari katika halmashauri zote hapa nchini wanatakiwa kuweka wazi matumizi ya fedha hizo katika mbao za matangazo kwa kila shule, ili kila mzazi aweze kujua kiasi gani kimetumika.

Sadiki alikuwa akizungumza wakati akipokea msaada wa ahadi ya ujenzi wa madarasa 12 katika mkoa wa Dar es Salaam kutoka kwa Wamiliki wa Malori Tanzaznia(Tatoa), yenye thamani ya Sh. milioni 300.

Mkoa wa Dar es Salaam, alisema Sadiki, una upungufu wa vyumba vya madarasa 7,223, lakini pia uhitaji wa madawati 66,000.

"Yapo maeneo mengi ya kujenga shule, nawaomba wadau wetu muendelee kuhamasisha kupata shule nzima kwani shule nzima inahitaji madarasa kuanzia 22," alisema.

Waziri Mkuu Awasili Kagera Kwa Ziara ya Siku 3....Asema Serikali ina Mpango wa Kununua Meli Mpya na Ndege Mbili

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeanza kukusanya fedha kwa ajili ya kununua meli mpya kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye Ziwa Victoria.

“Rais John Pombe Magufuli kasema ununuzi wa meli mpya uko pale pale. Tutanunua meli ya kusafirisha abiria katika Ziwa Victoria kama ambavyo aliahidi wakati wa kampeni,” alisema huku akishangiliwa.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Machi 13, 2016) wakati akitoa maelekezo baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Kagera ambako amewasili leo kwa ziara ya siku tatu kwa ajili ya kukagua masuala ya wakimbizi pamoja na mwenendo wa ranchi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na jinsi zinavyotumika.

Mbali ya ununuzi wa meli hiyo, Waziri Mkuu alisema Serikali pia imejipanga kununua ndege mbili ili kuimarisha usafiri wa anga hapa nchini. 

“Tuna dhamira ya kununua ndege walau mbili kwa ajili ya shirika letu la ndege la ATC. Tumelazimika kuwaomba Watanzania wenzetu warudi nyumbani ili kusaidia kuendesha shirika letu,” alisema.

Waziri Mkuu alisema suala hilo limeshafika mbali na utekelezaji wake hautachukua muda mrefu kuanzia sasa.

Alitumia fursa hiyo kuwaarifu wana Kagera kwamba hivi karibuni Serikali itaanza mradi wa kujenga bomba la kusafirisha mafuta ambalo litapita kwenye mkoa huo na hivyo ktoa ajira kwa wakazi wake. 

“Bomba litaanzia Tanga, kupitia Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Simiyu, Geita, Kagera hadi Uganda. Na humu njiani litakuwa na vituo vya kusukumia mafuta, kwa hiyo tuna uhakika wa kupata ajira kwa ajili ya watu wetu,” alisema.

Rais Magufuli awathibitisha watendaji wakuu wa TRA na TAKUKURU

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za serikali.

Waliothibitishwa ni Bw. Alphayo Kidata, aliyekuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambaye anakuwa Kamishna Mkuu wa TRA, na Bw. Valentino Mlowola aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambaye anakuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TAKUKURU).

Watendaji hawa wamethibitishwa kuanzia leo tarehe 13 Machi, 2016

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
13 Machi, 2016

Breaking News: Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 26....Kati Yao 13 ni Wapya, 7 Wamebakizwa na 5 Wamehamishwa

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.

Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
 
Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
  1. Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
  2. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga - Mkuu wa Mkoa wa Geita.
  3. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu - Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
  4. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga - Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
  5. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga - Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
  6. Mh. Godfrey Zambi - Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
  7. Dkt. Steven Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  8. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
  9. Mh. Anna Malecela Kilango - Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
  10. Mhandisi Methew Mtigumwe - Mkuu wa Mkoa wa Singida.
  11. Mh. Antony Mataka - Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
  12. Mh. Aggrey Mwanri - Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
  13. Mh. Martine Shigela - Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
  14. Mh. Jordan Mungire Rugimbana - Mkuu wa Mkoa Dodoma.
  15. Mh. Said Meck Sadick - Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
  16. Mh. Magesa Mulongo - Mkuu wa Mkoa Mara.
  17. Mh. Amos Gabriel Makalla - Mkuu wa Mkoa Mbeya.
  18. Mh. John Vianey Mongella - Mkuu wa Mkoa Mwanza.
  19. Mh. Daudi Felix Ntibenda - Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
  20. Mh. Amina Juma Masenza - Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
  21. Mh. Joel Nkaya Bendera - Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
  22. Mh. Halima Omary Dendegu - Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
  23. Dkt. Rehema Nchimbi - Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
  24. Mhandisi Evarist Ndikilo - Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
  25. Mh. Said Thabit Mwambungu - Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
  26. Luteni Mstaafu Chiku Galawa - Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).
Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
13 Machi, 2016

Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 13, 2016

0
0
Taarifa ya habari ChannelTEN, Machi 13, 2016




Waajiri na Wadaiwa wa Mikopo ya Elimu ya Juu Wapewa siku 60.....HESLB yatoa namba za Mawasiliano

0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inatoa siku 60 kuanzia tarehe 14 Machi, 2016 kwa wanufaika wote wa mikopo wanaodaiwa na HESLB kujitokeza na kuanza kulipa madeni yao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha, katika muda huu wa siku 60 waajiri pia wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao wa kisheria wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao waliohitimu katika vyuo vya elimu ya juu ndani na nje ya nchi. Taarifa zinazopaswa kuwasilishwa zijumuishe majina kamili ya waajiriwa, vyuo na mwaka waliohitimu.

Itakumbukwa kuwa Sheria iliyoanzisha HESLB (Sura 178) (kama ilivyorekebishwa) inatoa wajibu kwa mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu na pia wajibu kwa mwajiri.

Wajibu wa Mwajiri
Hivyo basi, taarifa hii inalenga kuwakumbusha waajiri ambao bado hawatimizi wajibu wao kisheria (kifungu cha 20) wa kuwasilisha majina ya waajiriwa wao wote ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu kwa HESLB ndani ya siku 28 tangu waajiriwe. 

Adhabu ya kutotekeleza wajibu huu kwa mwajiri ni faini ya shilingi milioni saba (Tshs milioni 7) au kifungo au vyote kwa pamoja.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, baada ya HESLB kupokea orodha kutoka kwa mwajiri, itafanya uchambuzi ili kubaini wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu na kumwelekeza mwajiri kuingiza makato ya marejesho kwenye mshahara wa mnufaika na kuwasilisha makato hayo kwa HESLB. 

Adhabu ya kutowasilisha makato kwa HESLB ni faini ya asilimia 10 ya makato yote ambayo hayajawasilishwa na faini hii inapaswa kulipwa na mwajiri.

Wajibu wa mnufaika wa mkopo na wazazi, walezi, wadhamini
Aidha, pamoja na wajibu wa mwajiri kama ulivyofafanuliwa hapo juu, wanufaika wote wa mikopo ya elimu ya juu tangu mwaka 1994, wana wajibu wa kisheria (Kifungu cha 19 cha sheria ya HESLB), pamoja na mambo mengine, kuitaarifu HESLB kwa maandishi mahali alipo na kuandaa utaratibu wa kulipa deni lake la mkopo wa elimu ya juu.

Iwapo mnufaika wa mkopo atashindwa kutoa taarifa hizo, adhabu yake ni kushitakiwa mahakamani.
 
Aidha, HESLB inapenda kuwakumbusha wazazi, walezi na wadhamini wa wanafunzi walionufaika na mikopo kuwa wana wajibu wa kisheria (chini ya kifungu cha 22 cha sheria ya HESLB) wa kuhakikisha kuwa taarifa muhimu za mnufaika waliyemdhamini zinaifikia HESLB.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, taarifa hizo ni pamoja na mahali alipo mnufaika, majina aliyotumia wakati akipata mkopo, mwajiri wake na kuhakikisha mnufaika aliyemdhamini anarejesha mkopo wake kwa HESLB.

Iwapo mwajiri, mnufaika au mdau yeyote ana swali, awasiliane na HESLB kwa simu zifuatazo: 0754 373481; 0763 459 165 au 022 2772432/33.

Lengo la HESLB ni kuhahakisha madeni yote yanakusanywa ili kuongeza uwezo wa kukopesha watanzania wengi zaidi. Ili kutekeleza hili, wanufaika, waajiri na wadau wengine wote wanapaswa kutimiza wajibu wao wa kisheria ili HESLB itekeleze majukumu yake kama ilivyokusudiwa wakati ilipoanzishwa mwaka 2004.

HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

Mwisho
Imetolewa na:
Bw. Jerry Sabi,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji – HESLB
Dar es Salaam – Jumapili, Machi 13, 2016

Viongozi wa dini wahimizana kujitenga na siasa Zanzibar

0
0

VIONGOZI wa dini wa Tanzania Bara na Visiwani wamekutana visiwani Zanzibar na kuja na tamko juu ya hali ya amani visiwani humo ambalo pamoja na masuala mengine, wamehimizana kujitenga na siasa za vyama.

Aidha, viongozi hao kutoka madhehebu ya Kikristo, Kiislamu na Jumuiya ya Hindu wametaka wananchi watakaoshiriki kupiga kura katika uchaguzi wa marudio wahakikishiwe amani inatawala na wale ambao hawatashiriki, wasibughudhiwe na pia wahakikishiwe amani.

Pia wametaka vyama vya siasa vinavyotoa kauli na taarifa zisizo sahihi na hivyo kuleta uchochezi viache mwenendo huo ili kudumisha amani kwani kila mmoja ana wajibu wa kuitetea tunu hii ya taifa.

 Kikao cha viongozi hao kilifanyika juzi visiwani hapa chini ya Baraza la Viongozi wa Dini mbalimbali kwa Ujenzi wa Amani Tanzania (IRCPT).

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na baraza hilo, imetaja baadhi ya viongozi wa dini walioshiriki kuwa ni Askofu wa Kanisa la Anglikana, Jimbo la Dar es Salaam, Valentino Mokiwa, Askofu wa Jimbo Katoliki la Zanzibar, Augustino Shao na Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum.

Wengine ni Askofu Dickson Kaganda; Shehe Norman Jongo ambaye ni mfanyakazi, Ofisi ya Mufti, Zanzibar; Shehe wa Tumbatu, Abdul Yusuf Mzee, Ismail Asahil na Godda Muyya ambaye ni Mwenyekiti wa Inter religious Peace Council, Tanzania 

Wakizungumzia hali halisi ya Zanzibar na nini kifanyike kudumisha amani, viongozi hao walisema viongozi wa dini wajitenge na siasa za vyama kwani wao wanapaswa kuwa nguzo za jamii zenye imani na asili tofauti, wasuluhishi na watetezi wa amani nchini.

Walisema wana mashaka kwamba kuna mgawanyiko miongoni mwa jamii unaosababishwa na tofauti mbalimbali zikiwemo za kisiasa. 

Baada ya majadiliano ya kina, mambo mengine waliyoazimia ni kwamba, kwa kutambua kuwa Zanzibar ni moja na watu wake ni wamoja, amani ni tunu adhimu kwa Watanzania wote.

Waliwapongeza Wazanzibari kwa kuwa wavumilivu na kulinda amani katika kipindi cha kuanzia uchaguzi uliofutwa hadio sasa. Walitaka pia vyombo vya usalama wawabaini na kuwachukulia hatua vikundi vya uvunjifu wa amani ili wananchi waishi kwa amani.

Walivitaka vyombo husika kutumia nguvu inayostahili badala ya kuogopesha umma. Viongozi hao wa dini wameitaka Tume ya Uchaguzi kuwa waadilifu kusimamia haki, sheria, kanuni na uwazi kudumisha amani katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Vile vile wamevitaka vyombo vya habari kusaidia kuhakikisha nchi inapita kwenye uchaguzi kwa usalama na amani kwa kutoa taarifa sahihi, kuzingatia maadili na kufuata taratibu na sheria zilizopo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ataka usafirishaji Haramu wa Madini Udhibitiwe

0
0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera kudhibiti usafirishaji haramu wa madini ya bati, akieleza kuwa yuko mwanamke ambaye si rais wa Tanzania anayesafirisha kinyume cha utaratibu.

Alitaka kujua hatua zilizochukuliwa kudhibiti hali hiyo na kumhoji Mkuu wa Wilaya, Benedict Lenga endapo anafahamu watu wanaosindikiza wezi hao wa madini.

“Madini ni tija, lazima tujue yanasafirishwa kwa kigezo kipi.Tunajua wakati mwingine tunasindikiza watu wanaoiba madini yetu,” alisema Majaliwa na kuhoji endapo Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) ndiye anayesindikiza. Hata hivyo, alijibiwa kuwa hahusiki.

Aidha, alimtaka Lenga na watu wake waimarishe ulinzi ili biashara hiyo ya madini idhibitiwe. Majaliwa alikuwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya mkoa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa, John Mongella, alipowasili hapa jana kuanza ziara ya siku nne.

Huduma ya usafiri wa Reli ya Kati Yaanza Rasmi

0
0

Huduma  ya usafiri  wa reli ya Kati iliyokuwa imesimama kwa takribani miezi miwili sasa imerejea kufuatia  kukamilika kwa ukarabati wa reli  hiyo katika eneo la kidete wilayani kilosa, mkoani Morogoro.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa  amesema  hayo baada ya kukagua na kuridhika na ukarabati uliofanywa katika maeneo ya Magulu, Munisagara, Mzaganza na kidete Wilayani Kilosa.

“Hakikisheni mnailinda reli hii kwa manufaa yenu na ya Taifa, leo hii reli iko  vizuri na treni ya kwanza kutoka Dar Es Salam  kwenda bara itapita na kumaliza changamoto ya usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi wanaotumiia reli hii”.Amesema Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo ya Kilosa, Magulu, Munisagara, Mzaganza, Kidete, Godegodena Gulwe ambao maeneo yao yanakabiliwa na mafuriko ya mto Mkondoa kuacha Kilimo cha kuelekeza Maji kwenye reli bali washirikiane na Serikali kudhibiti maji hayo kwenda kwenye  hifadhi ya reli.

Amesema Shirika la Reli Tanzania ( TRL) linaendelea kuhakikisha  kuwa treni  inayopita  kwenye reli ya Kati  inapata mzigo mwingi wa kusafirisha kutoka bandarini za Tanga na Dar Es Salaam kuelekea mikoa ya Mwanza, Kigoma na Mpanda, hivyo wafanyabiashara watumie fursa hiyo ili kupunguza mzigo unaosafirishwa kwa Nadia ya barabara.

Waziri Profesa Mbarawa ameteembelea bwawa la Kidete linaloelezwa kuwa chanzo cha mafuriko pindi linapojaa wakati wa mvua za Vuli  na Masika katika mikoa ya Dodoma na Iringa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa John Henjewele amemhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa ofisi yake itafuatilia kwa karibu malalamiko ya wananchi wanaoishi karibu na reli  ya Kati ili kuyapatia ufumbuzi na kuwataka wananchi hao kuitumia fursa ya kuwa karibu na reli kunufaika kiuchumi.

Takribani Shilingi millions 926 zimetumika katika ukarabati wa reli hiyo kufuatia uharibifu uliotokea mwezi  Januari na kukata Mawasiliano ya reli Kati ya mikoa ya  Dodoma na Morogoro na kusababisha Safari za treni kutoka bara kuishia Dodoma.

Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,, Uchukuzi na Mawasiliano Serikalini.

Waziri Mkuu Aishukia Idara Ya Uhamiaji Kwa Kuruhusu Uingizaji Holela wa Wageni

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Hamad Masauni aimarishe udhibiti katika idara ya uhamiaji kwa kuwasimamia kwa karibu Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Kagera pamoja na maafisa uhamiaji wa wilaya za mipakani.

Ametoa agizo hilo jana mchana (Jumapili, Machi 13, 2016) wakati akitoa maelekezo baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Kagera ambako amewasili leo kwa ziara ya siku tatu kwa ajili ya kukagua masuala ya wakimbizi pamoja na mwenendo wa ranchi zilizo chini ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na jinsi zinavyotumika.

“Idara ya Uhamiaji umakini wenu katika mkoa huu bado ni mdogo. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani eneo hili ni lazima liimarishwe. RIO na DIO wa wilaya zote lazima mbadilike. Mmejisahau na mmesahau wajibu wenu wa kuilinda nchi. Ni lazima mbadilike mara moja,” alisema.

“Mmesahau kuwa watu wetu wanapaswa kulindwa na kuishi kwa usalama, badala yake kila mara tunasikia watu wakiuawa. Wizara ya Mambo ya Ndani kitengo cha Uhamiaji tutakiangalia mara mbili mbili ili kudhibiti hali hii,” alisema.

Alisema wilaya za Misenyi, Kyerwa na Ngara zimekithiri kwa udhaifu mkubwa wa kuleta raia kutoka nje na kuwaruhusu wafanye kazi za Watanzania na kuitaja wilaya ya Birahamulo kwamba yenyewe ina tatizo kama hilo lakini ni kwa kiwango kidogo.

“Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa nataka mhakikishe kuwa mkoa wa Kagera siyo eneo la kuingilia wavamizi. Kama ni watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tunao utaratibu wa jumuiya hii ya kutoa vibali kwa watu wake, nao ni lazima ufuatwe,” alisisitiza.

Waziri Mkuu alisema anazo taarifa kuwa mifugo ya kutoka nchi jirani inaingizwa hapa nchini na kunenepeshwa katika ranchi za taifa na kisha inarudishwa kwao kuuzwa. 

“Hivi ni kwa nini nyama ya ng’ombe wa Tanzania haina ubora wa kuuza kwenye masoko ya nje halafu sisi tunaruhusu watu wa nje waje wafaidike na rasilmali zetu?” alihoji.

“Ng’ombe anayeswagwa kutoka Kagera hadi Kilosa atakuwa na nyama nzuri huyo? Ng’ombe anayeswagwa na kuchapwa fimbo kutoka Itilima hadi Rufiji; je ngozi yake itakuwa nzuri hadi ipate thamani ya kuuzwa nje ya nchi?” alihoji na kuibua minong’ono miongozi mwa viongozi wa mkoa huo waliokuwa wakimsikiliza.

“Inasikitisha kuona mkoa huu una ranchi za kutosha lakini hazitumiki kwa manufaa ya wananchi wa mkoa huu. Mkuu wa Mkoa tumekupa dhamana ya kuongoza mkoa huu. Ukiona mmojawapo wa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambao hawatimizi wajibu, waripoti kwa mamlaka za juu ili hatua za kinidhamu zichukukuliwe mara moja,” alisema.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuhimiza makusanyo ya kodi kwenye ngazi ya Halmashauri ili kukuza pato la Taifa. 

“Ninawasihi Halmashauri mhakikishe mnakusanya mapato katika vyanzo mlivyovianisha na pia muwe waaminifu katika matumizi ya fedha hizo,” alisisitiza.

Mapema, akisoma taarifa ya mkoa huo mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Bw. John Mongella alisema mkoa huo una eneo la hekta 176,000 ambazo ni za ranchi tu; maeneo ambayo alisema ni nyeti kiuchumi na kiusalama kwa sababu yamekaa mipakani.

Alitaja tatizo la wakimbizi kutoka nchi jirani kama changamoto nyingine kubwa ambayo inaikabili mkoa huo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, MACHI 13, 2016.

AJALI: Basi la Leina Tours lapata ajali Kimara Bucha

0
0
Basi la Leina Tours lililokuwa likitokea Kahama kuja Dar es Salaam, limeacha njia na kutumbukia katika mtaro eneo la Kimara Bucha  usiku  wa kuamkia leo

Idadi ya waliofariki haijafahamika  ila waliojeruhiwa ni zaidi ya 30 na walikimbizwa  Haospitali  ya  Mwananyamala na Muhimbili.

Serikali Yatenga Bilioni 811 Zitakazotumika Kutekeleza Ahadi ya Rais Magufuli Ya Kukipatia Kila Kijiji Milioni 50

0
0

Serikali  imetenga jumla ya Sh bilioni 811 zitakazotumika kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kukipatia kila kijiji Sh milioni 50 kwa ajili ya shughuli za maendeleo. 

Imeelezwa kwamba serikali imeshaanza kushirikisha wadau mbalimbali kupata maoni ya jinsi ya kuendesha mpango huo kwa ufanisi na tija.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) alisema serikali itaanza kutoa fedha hizo kuanzia mwaka wa fedha ujao.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki baada ya mkutano wa wadau waliokuwa wanajadili rasimu ya mpango huo wa utoaji fedha kwa ajili ya maendeleo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa halmashauri za wilaya, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), mabenki, mifuko ya hifadhi ya jamii na vikundi mbalimbali. 

“Kwa kuanzia, fedha hizo zitatolewa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka mitano,” alisema.

Alisema fedha hizo zitatolewa kupitia benki kabla ya kutolewa kwa vikundi mbalimbali kama Vicoba, Saccos na vikundi vingine kulingana na taratibu zitakazowekwa.

Alisema mpango utaanza na mikoa 10 iliyo nyuma katika kutumia huduma za kifedha kwa kuzingatia taarifa ya utafiti ya Finscope ya mwaka 2013.

Mikoa hiyo ni Singida, Lindi, Mtwara, Mbeya, Shinyanga, Geita, Kagera, Dodoma, Rukwa na Ruvuma. 

Akifungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uhusiano ya Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama, alisema mkutano huo ulilenga kupata maoni ya wataalamu ya namna bora ya kuutekeleza.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri, Kaimu Mkurugenzi, Maendeleo ya Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Victor Mwainyekule alisema mawazo yaliyopatikana yatazingatiwa kuboresha mpango huo unaolenga kupambana na umaskini.

Mkuu wa Uendeshaji, Benki ya Wanawake (TwB), Zablon Yebete alisema mpango huo ni uwekezaji mkubwa kwa Watanzania unaopaswa kuungwa mkono na vyombo vya fedha na wadau wengine nchini.

“Tunatakiwa kuunga mkono mpango huu unaohusisha vyombo vya fedha katika utekelezaji wake kwa faida ya taifa,” alisema. 

Kwa mujibu wa mpango huo, walengwa watapatiwa mafunzo ya ujasiriamali kabla ya kupatiwa fedha hizo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images