Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 9


Kubenea Akana Kumtukana Paul Makonda....Kesi Yaahirishwa Hadi March 10

$
0
0

Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hakutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kama inavyodaiwa.

Kubenea alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa utetezi huku akiongozwa na wakili wake, Peter Kibatala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

“Mimi sijasema hayo maneno kuwa Makonda ni mjinga, mpumbavu, kibaka na cheo chenyewe cha kupewa, bali nilimwambia wewe umeteuliwa na Rais na mimi nimechaguliwa na wananchi,” alidai.

Kubenea aliendelea kudai kuwa Desemba 14, 2015, katika kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd kilichopo Mabibo External kwenye mgomo wa wafanyakazi wa kiwanda hicho, alimwambia Makonda hawezi kufunga mkutano bila ya yeye kuzungumza kwa sababu ni mwakilishi wa wananchi.

Alidai kuwa Makonda alimjibu kila alipokuwa akizungumza kuwa yeye ndiye mtu wa mwisho kwa kuwa ni rais wa Kinondoni. 

“Nilimjibu na mimi ni mbunge, nimeteuliwa na wananchi, lazima aheshimu uwapo wangu pale,” alidai.

Kubenea alidai kutokana na msimamo wa Makonda wa kutotaka kumpa nafasi ya kuzungumza na wafanyakazi, alimwambia hajavamia mkutano huo bali aliitwa. 

“Nikamwambia mimi siyo kibaka bali nimechaguliwa na watu, baada ya kauli hiyo, alimuamuru Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Magomeni, Denis anikamate nikapumzishwe mahabusu,” alidai.

Alidai kuwa mkuu huyo wa wilaya, aliamuru pia kukamatwa kwa raia mmoja wa China anayedaiwa kuwanyanyasa wafanyakazi hao ili achunguzwe.

Kesi hiyo itaendelea Machi 10, mwaka huu. Kubenea anadaiwa kutenda kosa hilo Desemba 14, 2015 katika Kiwanda hicho.

Rais Wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Awasili Tanzania

$
0
0
RAIS wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Truong Tan Sang, amewasili  nchini  jana  saa  mbili  usiku tayari kwa  kuanza ziara ya siku tatu nchini, ambapo pamoja na masuala mengine, atasaini mkataba wa masuala ya Kodi na mwenyeji wake Rais John Magufuli.

Mkataba huo unalenga kuchochea biashara kati ya Vietnam na Tanzania kwa kuwa utatoa fursa kwa wafanyabiashara wa pande zote kutotozwa kodi mara mbili katika biashara na uwekezaji watakaoufanya.

Rais huyo anatarajiwa kupigiwa mizinga 21 leo, ikiwa ni pamoja na kukagua gwaride rasmi, ambapo baadaye atatambulishwa kwa viogozi mbalimbali wa Serikali, kabla ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa Dar es Salaam kuhusu ujio wa Rais huyo wa Vietnam, baada ya viongozi hao kutia saini mkataba huo, mgeni huyo na ujumbe wake atakwenda kwenye ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyopo katika Mtaa wa Lumumba jijini humo kukutana na Mwenyekiti wa chama hicho, ambaye ni Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Rais huyo wa Vietnam ambaye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa Chama cha Kikomunisti cha nchi hiyo chenye uhusiano wa muda mrefu na CCM, atakwenda kwenye Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) Ubungo, Dar es Salaam kutembelea viwanda na kupata taarifa za fursa za uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini.

Aidha, ratiba hiyo imeeleza kuwa atahudhuria mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili, kabla ya kukutana na Spika wa Bunge, Job Ndungai na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein katika wakati tofauti.

Pamoja na ujumbe wake atatembelea hifadhi ya wanyama ya Saadan iliyoko Bagamoyo na kuondona nchini Machi 11 kuelekea Msumbiji kuendelea na ziara yake.

Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe wakishuka kutoka kwenye ndege mara walipowasili katika Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akimkaribisha Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (katikati) mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere akiongozana na mkewe 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Vietinam , Trung Tan Sang, Mkewe Mai Thi Hahn  na  Mkuu, Kassim Majaliwa wakitazama ngoma baada ya Rais huyo   kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salam kwa ziara ya siku tatu nchini, Machi8, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wamiliki wa Magari 213 Matatani..... TRA Yatoa Siku 4 Wajitokeze Kulipa Kodi Haraka

$
0
0

MAGARI 213 yanafuatiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kubainika yameingizwa nchini bila kulipiwa kodi na watu binafsi pamoja na taasisi mbalimbali zikiwemo za dini.

Miongoni mwa magari hayo, yamo yaliyoingizwa kwa misamaha ya Kituo cha Uwekezaji (TIC) ambayo (misamaha) imetajwa kutumika isivyo.

Mamlaka imesema inafuatilia kuhakikisha wahusika sanjari na waliosaidia ukwepaji huo wa kodi, wanachukuliwa hatua.

TRA imetaja majina na taasisi zinazohusika na uingizaji magari hayo, kupitia matangazo kwa vyombo vya habari na imetoa siku nne wajitokeze kulipia ushuru kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.

Ukaguzi uliofanywa na mamlaka, ndiyo umebaini kuwepo kwa magari hayo yaliyoingizwa nchini na kusajiliwa bila kufuata taratibu za forodha hivyo kuyafanya yamilikiwe bila kulipiwa kodi stahili.

Orodha ya magari 213 na namba za usajili, mmiliki na aina ya gari imetolewa katika vyombo vya habari na mamlaka hiyo imewataka wahusika wajitokeze haraka kulipia gharama hizo.

Baadhi ya kampuni, taasisi na watu binafsi, wameingiza magari zaidi ya moja.

Miongoni mwa taasisi zilizotajwa kwenye orodha hiyo zenye magari zaidi ya moja ni JM Hauliers Limited (26), Al-Jabri Co Ltd (16) na Kampuni ya Dhandho Road Hawlage iliyoingiza 18.

Kampuni nyingine na idadi ya magari yaliyoingizwa kwenye mabano ni Bamboo Rock Limited (7) na Dayosisi ya Musoma, ambayo hata hivyo haikufafanuliwa ni ya madhehebu gani ya dini, imeingiza magari manane.

Wengine ni Fai Limited (3), Nam Transport Company (6), Neni Enterprises (2) na Relief Partner International yenye magari matatu.

Kwa upande wa watu binafsi wenye magari zaidi ya moja yaliyoingizwa bila kulipia ushuru ni pamoja na Aloyce Kajijira (6), Mohamed Masoud (5), Mwesige Rwiza (5), Nassor Zakaria (3), Rumishaeli Shoo (3), Ruwaida Ally (4) Simon Mehi (2), Yahya Hilal (5) na Zahor Issa mwenye magari matatu.

Wapewa siku nne
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo aliwataka wamiliki wa magari yaliyoorodheshwa kufika katika ofisi zilizo karibu, wafanyiwe uhakiki walipe ushuru stahiki kabla ya Machi 12 mwaka huu.

Alisema baada ya tarehe hiyo, TRA itachukua hatua ya kufuatilia magari hayo na kuyakamata.

Alisema ufuatiliaji wa magari yaliyoingizwa nchini bila kulipiwa ushuru ni endelevu.

Waliouziwa matatani
Akizungumzia watakaokuwa wameuziwa magari hayo bila kufahamu kama yalitolewa bila kulipiwa kodi stahili, Kayombo alisema pia wanatakiwa kujitokeza.

Alisema walioyanunua magari hayo, ambayo namba zake zimeoneshwa, wanapaswa kujitokeza wapigiwe hesabu, walipe kiasi kinachodaiwa na mamlaka.

Kwa mujibu wa Kayombo, watakapofika katika ofisi za TRA, zitafanyika taratibu kuangali jinsi ya kulipa, kwani yapo magari ambayo hayakulipiwa kabisa au yamelipiwa kidogo kutokana na kufanya udanganyifu katika malipo.

Waliosaidia ukwepaji kodi
Hata hivyo, Kayombo alisema baada ya kulipa gharama hizo, hatua nyingine zitachukuliwa.

Hatua hizo za kisheria, zitahusu waliopitisha magari hayo na waliosaidia katika kufanya udanganyifu wa kulipa kodi stahiki kwa magari hayo.


Ajali Mbaya Iliyohusisha Daladala na Malori Mawili Yaua Watu 4 na Kujeruhi 25 Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Ajali Mbaya imetokea leo asubuhi eneo la Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam ikihusisha malori mawili  na daladala iliyo kuwa ikitokea Gongo la Mboto kuelekea Ubungo

Kwa mujibu wa mganga mkuu Hospitali  ya  Amana, Dr Stanley Binagi, watu wanne wamefariki dunia huku 25  wakijeruhiwa.

Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugongana na Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.


Picha: Raisi Magufuli Amtembelea Maalim Seif katika Hoteli ya Serena kwa ajili ya kumjuilia hali yake.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea na kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Maalim Seif Shariff Hamad, katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam, ambako anapata mapumziko baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Hindu Mandal alikokuwa amelzwa kwa matibabu.

Pamoja na kumpa mkono wa pole, Rais Magufuli amemuombea Maalim Seif Shariff Hamad kupona haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

"Nilishtushwa sana na taarifa za kuugua kwako, lakini sasa nafurahi kukuona ukiwa mwenye afya nzuri ikilinganishwa na taarifa nilizozipata hapo awali, nakupa pole sana" amesema Rais Magufuli wakati akimjulia hali hotelini hapo.

Kwa upande wake Maalim Seif Shariff Hamad amemshukuru Rais Magufuli kwa ukarimu na upendo aliouonesha kwa kumtembelea hotelini hapo, na amewahakikishia watanzania kuwa hali yake sasa inakwenda vizuri na inazidi kuimarika kila kukicha.

"Sasa hivi ninaweza kutembea vizuri, kufanya shughuli zote mwenyewe bila ya msaada wa mtu yeyote yule, na ni matumaini yangu kwamba baada ya muda mfupi, hali yangu itarudi kama kawaida, nije nishirikiane na watanzania wenzangu katika kutekeleza majukumu ya nchi yetu"  Maalim Seif alimweleza Rais Magufuli.
 
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
09 Machi, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumjulia hali  na kusema kuwa hali yake ya kiafya inaimarika siku baada ya siku.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam mara baada ya kumjulia hali jijini Dar es Salaam.

Rais Wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Akaribishwa Ikulu, Jijini Dar Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kushoto) akimkaribisha mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.

Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye koti la drafti) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Kulia niRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa tatu kushoto) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Wa pili kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakipanda jukwaani kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakiwa katika jukwaa kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (mwenye tai nyekundu) akikagua gwaride la heshima katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016.
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akipokea zawadi ya ua toka kwa mtoto mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 akiwa amefuatana na mmewe kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.
  Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe mama Mai Thi Hanh wakiwasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbalikati ya Tanzania na Vietnam.(Picha Zote Na Benedict Liwenga-MAELEZO)

TRA Yakusanya Trilioni 1.04 Mwezi Februari Ambayo ni Sawa na Asilimia 101% Ya Lengo La Ukusanyaji Mapato

$
0
0

Katika Kipindi cha miezi nane  kuanzia  Julai 2015 hadi Februari mwaka huu, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imekusanya jumla ya Sh  Trilioni 8.5  ikilinganishwa na lengo la kukusanya Sh trilioni 8.6 ambayo ni sawa na asilimia 99 ya makusanyo yote.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Alphayo Kidata wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu  mwenendo wa ukusanyaji wa mapato, matumizi ya mashine za EFDs, kusitisha kwa bei elekezi na usajili wa vyombo vya moto.

Amesema lengo la Mamkala hiyo ni kukusanya Trilioni 12.3 hadi ifikapo Juni mwaka huu na kwamba asilimia moja iliyobakia katika kukamilisha asilimia 100 ya ukusanyaji wa mapato kati ya Julai mwaka jana  hadi Juni mwaka huu,  itakamilika ndani ya miezi nne iliyosalia ambayo itaisha Juni mwaka huu.

Amesema pia kwa mwezi Februai pekee, Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya mapato ya kiasi cha Sh Trilioni 1.04 kwa upande wa Tanzania  Bara na Zanziba ambayo kiasi hicho ni sawa na asilimia 101.18 ya lengo la ukusanyaji ambayo ilikuwa ni Sh  Trilioni  1.028 kwa mwezi.

Amesema kuongezeka kwa mapato haya kunatokana na kudhibiti kwa mianya ya ukwepaji wa kodi na kuweka mazingira rafiki kwa mlipa kodi, kurekebishwa kwa misamaha ya kodi ambayo ilikuwa inachangia upotevu wa mapato, kuongezeka kwa watumiaji wa mashine za EFDs pamoja kudhibiti eneo la forodha ambalo lilikuwa linasababisha upotevu wa mapato ya TRA.

Maeneo yaliyochangia kuongezeka kwa mapato hayo:          
“Maeneo ambayo yamechangia kuongezeka wa mapato haya ni kuimarishwa kwa bandari yetu kwa kuziba mianya ya ukwepaji kodi , kurekebishwa kwa misamaha ya kodi ambayo hapo awali ilikuwa inachangia upotevu wa ukusanyaji wa mapato, kuongezeka kwa matumizi ya utumiaji wa mashine za EFDs kwa wafanyabiashara, Mamlaka kuwatengenezea mazingira mazuri kwa walipa kodi, kudhibitiwa kwa eneo la forodha ambapo wajanja wachache walikuwa wanatumia mwanya huu kuikosesha serikali mapato” amesema Kidata.

Kwa mwezi Januari walikusanya Trilioni 1.079:
Katika  kipindi cha Januari pekee, Mmalaka hiyo ilikusanya  kiasi cha  Trilioni 1.079kwa Tanzania bara na visiwani ambapo kiasi hicho ni sawa na asilimia 102 ya lengo la Sh Trilioni 1.059 kwa mwezi.

“Makusanyo  haya ya Januari yametokana na ari  na uthubutu ambao TRA imejiwekea katika kusimamia na kuhakikisha inaendelea kuziba mianya ya ukwepaji kodi na kuweka mazingira rafiki kwa mlipakodi  kwa kulipa kwa wakati na urahisi kwa kutumia mifumo mbalimbali iliyopo”ameongeza.

Faini ya mashine za EFDs kwa Wafanyabaishara:
Kidata amesema katika kipindi cha mwezi Februari pekee, Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya  faini ya Sh 800milioni kwa watu wa jiji la Dar es Salaam ambapo walikiuka na kufanya makosa katika utumiaji wa  mashine za EFDs.

“Kuanzia mwezi Machi mwaka huu kila mtu anayetakiwa kutumia mashine za EFDs atumie  vinginevyo hatua kali za kisheria zitafuatwa”amesema Kidata.

Amesema utaratibu wa matumizi ya EFDs ulifanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza iliwahusisha  wafanyabiashara ambao wamesajiliwa kutoa VAT na awamu ya pili ilihusisha  wafanyabaishara ambao hawakusajiliwa na Vat ambao mauzo yao kwa mwaka ni zaidi ya Sh 14milioni.

Serikali kugawa bure mashine za EFDs:
Kwa upande wake Kamishna wa Kodi za Ndani kutoka TRA, Yusuph Salum alisema  serikali imeagiza Mamlaka ya Mapato nchini kutoa bure mashine za EFDs kwa wafanyabiashara  wadogo ambao uwezo wa kununua mashine hizo unaweza kuathiri mitaji yao ya biashara.

“Kwa sasa tuko katika hatua za mwisho kukamilisha manunuzi wa mashine za uniti 5700 na kwamba wafanyabiashara wakubwa hawatahusika na mgao wa mashine hizi za bure bali wao wataendelea na utaratibu wa zamani wa kujirejeshea gharama za mashine kupitia ritani za mwezi” amesema Salum.

Amesema pamoja na kuwepo kwa sheria inayomtaka mfanyabiashara kununua , kutumia mashine, kutoa risiti na kulipa kodi, TRA imebaini wafanyabiashara waliowengi hawana mashine hizo za kutolea risiti pindi wanapofaya  mauzona hivyo kuikosesha serikali.

Usajili wa magari:
Kidata alisema TRA, imefanya ukaguzi na kubaini kuwepo kwa magari ambayo yaliingizwa nchini na kusajiliwa bila kufuata taratibu za forodha hivyo kuyafanya yamilikiwe bila kulipiwa kodi stahiki na kwamba kuna jumla ya magari 9000 ambayo yanaingia nchini na kutolewa.

“Wamiliki wa magari wote  tayari  tumeshawataarifu  kufika TRA kufanyiwa uhakiki ili kuyalipia kodi stahiki lakini pia kumekuwa na matumizi mabaya ya misamaha iliyotolewa hasa kwa upande wa magari, hivyo utaratibu wa misamaha uliwekwa kwa ajili ya kuwapa nafuu wawekezaji ili wahusika wamekuwa wakiitumia vibaya kwani magari yameingizwa mengi kuliko mahitaji na kupelekea serikali kukosa mapato” amesema

Amesema sheria za kodi zinatoa misamaha mbalimbali kupitia utaratibu wa Kituo cha Uwekezaji cha Taifa(TIC) na mashirika yasiyo ya kiserikali na kwmaba nia na madhumuni ya misamaha hiyo ni kuvutia uwekezaji na kutoa unafuu wa huduma kwa jamii.

Kufutwa kwa bei elekezi:
Katika hatua nyingine,  Mamlaka hiyo imefuta bei elekezi katika  mchakato wa uthaminishaji wa bidhaa bandarini kwa sababu  ni kinyume cha sheria ya Jumuiay ya Afrika Mashariki na kwamba TRA itaendesha shughuli za kiforodha kulingana na sheria husika.

“Tumeona bei elekezi haisaidi kwa sababu uingizaji wa bidhaa unatawaliwa na sheria ya Afrika Mashariki ambapo na sisi Tanzania ni wanachama, hivyo Mamlaka itadhibiti ukaguzi na uthaminishaji halisi ili kila mfanyabaishara alipe ushuru na kodi kulingana na thamani ya bidhaa husika, hata hivyo uthaminishaji mizigo kwa wafanyabiashara umepelekea wengine kulipa kodi kubwa kuliko thamani ya bidhaa husika” amesema.

Mama Janeth Magufuli Akimkaribisha Mke Wa Rais Wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh Ofisini Kwake.

$
0
0
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akifurahia zawadi ya kinyago cha kuchonga alichokabidhiwa na mwenyeji wake mama Janeth Magufuli kama zawadi 9 Machi, 2016 katika ofisi za Mke wa Rais Jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli (kulia) 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akisalimiana na akina mama waliompokea mara alipotembelea katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akimpa zawadi mama Janeth Magufuli ikiwa shukurani yake mara alipotembelea katika ofisi yake 9 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Afanya Mazungumzo Na Rais Tuong Wa Vietnam Leo

$
0
0
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga.
Rais Truong wa Vietnam akimsifia jambo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati akimuaga baada ya mazungumzo yake na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (kulia)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga na kulia ni Dk. Asha-Rose Migiro.
 Mwenyekiti wa CCM Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo hayo .

Maongezi Ya Rais Magufuli na Rais Truong Wa Vietnam Baada Ya Kukutana IKULU Yako Hapa

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Mheshimiwa Truong Tan Sang ambaye amewasili hapa nchini jana jioni tarehe 08 Machi, 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku nne, amepokelewa rasmi na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika lango kuu lililopo Mashariki mwa Ikulu, Rais Truong Tan Sang amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na amepigiwa mizinga 21 iliyokwenda sambamba na nyimbo za mataifa yote mawili.

Pamoja na mapokezi hayo, Marais hao wawili wamefanya mazungumzo ya faragha ambayo yamehudhuriwa pia na makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, na baadaye kufuatiwa na mazungumzo rasmi kati ya Rais Magufuli na ujumbe wake na Rais Truong na Ujumbe wake.

Katika Mazungumzo hayo, Rais Magufuli ameahidi kuuendeleza na kuuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Vietnam ambao ulijengwa na waasisi wa mataifa haya mawili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Ho Chi Minh, hata kabla ya Uhuru, huku akitilia mkazo juu ya ushirikiano katika maendeleo ya kiuchumi.

Rais Magufuli amemweleza Rais Truong Tan Sang kuwa katika miaka mitano ijayo, Tanzania imedhamiria kujikita katika uanzishwaji wa viwanda vingi, na hivyo ametaka mahusiano kati ya Tanzania na Vietnam yajielekeze katika kuendeleza Kilimo na ufugaji na hivyo kuiwezesha nchi kuwa na uhakika wa chakula na pia kupata ziada itakayouzwa nchi.

"Tunatambua jinsi Vietnam ilivyopiga hatua kubwa katika uvuvi, uzalishaji wa kahawa na uzalishaji wa mpunga. Uzalishaji katika maeneo hayo umeiwezesha kuwa nchi inayoongoza duniani, na sisi Tanzania tunataka kujifunza kutoka kwenu" Amesisitiza Rais Magufuli.

Kufuatia hali hiyo, Rais Magufuli amemuomba Rais Truong Tan Sang, kuwa uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizi mbili ujikite katika kuendeleza kilimo hususani kutumia zana bora za kilimo badala ya jembe la mkono, Kilimo cha umwagiliaji badala ya kutegemea mvua, kuzingatia mbinu bora za ugani, kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazao na kupata masoko ya mazao.

Kwa upande wake Rais wa Vietnam Mheshimiwa Truong Tan Sang amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuiongoza awamu ya Tano na amemhakikishia kuwa Vietnam itaendelea kushirikiana na Tanzania, huku ikitambua mchango mkubwa uliotolewa na watu wa Tanzania walioiunga mkono juhudi za kuiunganisha nchi hiyo na kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti mwaka 1968.

Amesema kwa kuzingatia mazingira bora ya Tanzania yenye amani na utulivu, Vietnam imedhamiria kuwa Tanzania iwe kituo chake cha kuzifikia nchi nyingine za Afrika Mashariki na sehemu nyingine za Afrika.

Rais Truong Tan Sang ameomba mahusiano ya Tanzania na Vietnam, sasa yajielekeze katika kuongeza Biashara, huku akieleza kuwa biashara ya Dola za Marekani milioni takribani milioni 300 haitoshi, na hivyo amependekeza wafanyabiashara wa Tanzania kuunganishwa na wenzao wa Vietnam ili mauzo ya bidhaa kutoka pande zote mbili yaongezeke hadi kufikia dola za Marekani bilioni 1 ifikapo mwaka 2020.

Ameongeza kuwa Vietnam ipo tayari kutiliana saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano katika biashara, Viwanda na Kilimo, na ametoa mwaliko kwa wakulima wa Tanzania kwenda kujifunza nchini Vietnam.

Mara baada ya Mazungumzo hayo, Marais wote wawili wamezungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari ambapo wote wawili wamesisitiza kuwa, nchi zao zipo tayari kukuza zaidi mahusiano na ushirikiano kwa faida ya wananchi wake.

Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-09 Machi, 2016.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamis ya March 10

Rais wa Zanzibar Dr. Shein Amtembelea na Kumjulia hali Maalim Seif Jijini Dar es Salaam

$
0
0

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiambatana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala bora Mheshimiwa Dkt. Mwinyihaji Makame, amemtembelea kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Shariff Hamad ambaye yuko hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko baada ya kutolewa hospitali.

Amesema afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku. Dkt. Shein alifika hotelini hapo jana  saa mbili usiku. (Picha na Salmin Said, OMKR)


Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimjulia  hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar  Maalim Seif Shariff Hamad hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimjulia  hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar  Maalim Seif Shariff Hamad hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Picha na OMKR

Viongozi wa Chadema Waanza Kuwasili Jijini Mwanza

$
0
0

Viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema wameanza kuwasili jijini Mwanza ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika vikao vya juu vya chama hicho.

Leo, wajumbe wa Kamati Kuu wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe watawasili jijini Mwanza.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene ilieleza kuwa Kaimu Katibu Mkuu, Salum Mwalim ameshawasili  na Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika na wakurugenzi wengine walitegemewa kuwasili muda wowote kwa ajili ya kikao cha Sekretarieti inayokutana kabla ya kile cha Kamati Kuu inayoketi kwa siku mbili kuanzia leo.

Baada ya kuwasili jijini Mwanza, Mwalimu alikutana na waratibu wa kanda zote za chama hicho ambako alipokea taarifa fupi ya maandalizi ya awali ya vikao vya Sekretarieti, Kamati Kuu na Baraza Kuu ambalo litaketi Machi 12 kisha kufuatiwa na kikao kingine cha Kamati Kuu Machi 13 asubuhi na jioni kutakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya Furahisha.

Machi 14, sekretarieti itakutana tena kuhitimisha vikao hivyo.

James Lembeli Aruka Kihunzi Kingine....Wenje Aandaa Mashahidi 693 Kupinga Ushindi wa Stanslaus Mabula

$
0
0

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje (pichani) anakusudia kuita mahakamani zaidi ya mashahidi 693 kupinga ushindi wa mbunge wa sasa, Stanslaus Mabula (CCM).

Wakili wa Wenje, Deya Outa aliieleza mahakama kuwa mashahidi hao ni pamoja na waliokuwa wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura, wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.

“Tunatarajia kuita mahakamani mashahidi wasiopungua 693 kuthibitisha madai yetu, kulingana na mahitaji ya hoja tunazotaka kuzithibitisha mahakamani,” alidai wakili Outa.

Pande zinazohusika kwenye shauri hilo namba 3 la mwaka 2015, juzi ziliweka wazi hoja wanazokubaliana na zile wanazobishania kabla ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Kakusulo Sambo anayesikiliza shauri hilo kuihairisha hadi Machi 14, mwaka huu, itakapoanza kusikilizwa mfululizo.

Pamoja na Mabula, wadaiwa wengine katika shauri hilo linalovuta umati wa wasikilizaji ni aliyekuwa msimamiza wa uchaguzi Nyamagana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kutokana na wingi wa mashahidi na muda wa mwaka mmoja uliowekwa kisheria wa mashauri ya uchaguzi kusikilizwa na kuamuliwa, wakili Outa alisema iwapo muda huo utaisha kabla hawajamaliza kutoa ushahidi wao, wataiomba mahakama kuwaongezea muda wa ziada.

Lembeli apeta 
Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama mjini kupitia Chadema, James Lembeli ameruka kihunzi kingine baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga inayosikiliza shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo kutupilia mbali pingamizi la mashahidi wa mlalamikaji lililokuwa limewekwa na mawakili wa upande wa mshitakiwa.

Akitoa uamuzi huo jana mjini Kahama, Jaji Moses Mzuna alisema ni kinyume cha sheria na wala siyo haki kuzuia mashahidi wa mlalamikaji kutoa ushahidi wao, hivyo ni vyema wakatoa na haki ikatendeka.

Uamuzi huo ulifuatia mvutano mkali wa kisheria uliotokea Machi 4, mwaka huu, baina ya mawakili wa upande wa utetezi na wakili wa mlalamikaji ambapo Jaji Mzuna aliahirisha shauri hilo, hadi alipolitolea uamuzi jana asubuhi.

Katika mvutano huo, mawakili wa utetezi Anthony Nasimire, Denis Kahangwa na Castuce Ndamugoba walipinga mashahidi wa Lembeli kutoa ushahidi wao kwakuwa walikiuka sheria inayowataka kuwasilisha viapo vyao mahakamani ndani ya saa 48, kabla ya shauri kuanza kusikilizwa.

Pia Jaji Mzuna alisema sheria hiyo ni mpya na kwamba haikujulikana kwake, kwa mawakili wa pande zote, na hata katika rejea za kimahakama nchini ndiyo maana hata mawakili wa utetezi wameiwasilisha wakati ushahidi umekwishaanza kutolewa. 

Alifafanua kwamba sheria ya uchaguzi inaelekeza mlalamikaji kutoa ushahidi usioacha mianya ya mashaka, jambo ambalo pia mahakama iliona si vyema mashahidi walioandaliwa kuzuiliwa kutoa maelezo yao, hali itakayobana uwigo wa upatikanaji wa haki.

Kwa upande mwingine Jaji Mzuna aliikataa hoja ya wakili wa Lembeli, Mpale Mpoki kwamba muda wa kuandaa viapo haukuwepo kwa kuwa ilimchukua muda mwingi kuandaa shauri hilo, ambapo Jaji Mzuna alisema haikubaliki kisheria.

Hata hivyo alisema kuchelewa kwa Mpoki kupeleka viapo vya mashahidi hakuwezi kuwa sababu ya Lembeli kupoteza fursa ya kudai haki yake anayohisi alipokonywa, bali muda zaidi umetolewa wa kuandaa viapo hivyo.

Kufuatia hali hiyo Jaji Mzuna aliahirisha shauri hilo hadi Machi 15 mwaka huu ambapo mahakama itaanza kusikiliza maelezo ya mashahidi wa Lembeli waliokuwa wamesubiri uamuzi dhidi ya mvutano huo wa kisheria uliopinga mbunge huyo wa zamani wa jimbo la kahama asipeleke mashahidi wake mahakamani.


Steven Wasira Awekewa Pingamizi Tena

$
0
0

Wapiga kura wa Bunda Mjini waliowasilisha maombi ya kuruhusiwa kukata rufaa nje ya muda, kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Ester Bulaya dhidi ya Steven Wasira, wamekumbana na kigingi kingine cha pingamizi.

Maombi hayo namba 25 ya mwaka 2016 yaliwasilishwa na wapiga kura Magambo Masato na wenzake watatu, wakiiomba mahakama hiyo iwaruhusu kukata rufaa nje ya muda baada ya kutupiliwa mbali na mahakama kuu.

Pingamizi hilo liliwasilishwa jana na wakili wa wajibu maombi wa pili na wa tatu, Paschal Malulu akiiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo kwa kuwa kiapo kilichoambatanishwa ni batili kwa kuwa aliyeapa ni tofauti na aliyethibitisha.

“Haya makosa yaliyofanyika ni makubwa mno, kiasi cha kutokurekebishika, kwa sababu kiapo kimethibitishwa na wakili Constatine Mutalemwa huku aliyeapa ni wakili James Kahangwa,” alidai Malulu.

Alidai kiapo hicho kimekosa nguvu kisheria kwa mujibu wa sheria Na. 19 (1) (2), ni lazima kiwe na mambo ambayo mtu anaweza kuyathibitisha au kuyasimamia, hivyo hii sheria imekiukwa, kwa lugha nyingine kiapo kimekosa uthibitisho.

Malulu alidai kuwa kuna sheria inayosimamia kiapo wala siyo Katiba kwa ujumla wake, kama alivyoitaja Mutalemwa.

Jaji anayesikiliza shauri hilo, Rose Ebrahim aliahirisha shauri hilo hadi Machi 14, mwaka huu atakapolitolea maamuzi pingamizi hilo.

Waangalizi wa Ndani wa Uchaguzi (Cemot) Wakataa Kushiriki Katika Uangalizi wa Uchaguzi wa Marudio Zanzibar

$
0
0

Muungano wa Waangalizi wa Ndani wa Uchaguzi (Cemot) umesema hautashiriki katika uangalizi wa uchaguzi wa marudio Zanzibar utakaofanyika Machi 20 mwaka huu kutokana na kukabiliwa na ukata.

Cemot ni umoja wa taasisi za waangalizi wa ndani wa uchaguzi inayohusisha Kamati ya Uangalizi wa Uchaguzi (Temco) na Muungano wa taasisi zisizo za kiraia za kusimamia uchaguzi (Tacceo) ambazo zilitumia waangalizi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari Arusha katika warsha ya mrejesho wa taarifa ya waangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu, Mwenyekiti mwenza wa Cemot, Martina Kabisama alisema fedha zote zilitumika katika uchaguzi uliopita.

“Kwenda kuangalia uchaguzi ni jambo linalohitaji rasilimali, hivyo hatutakwenda Zanzibar katika uchaguzi wa marejeo kwa kuwa tulikuwa hatujaandaa andiko la kupata fedha za uchaguzi huo,” alisema.

Kabisama alisema Cemot ilikuwa na waangalizi wa muda mfupi 9,400 na wengine 350 waliotoka Tacceo na Temco.

Mwangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu kwa Tanzania Bara na Visiwani, Dk Alexander Makulilo alisema Cemot ilifanya kazi kubwa katika uangalizi na imeandaliwa taarifa inayoonyesha mahitaji ya maboresho katika chaguzi zijazo.

Dk Makulilo ambaye anaongoza timu ya uandishi wa taarifa ya Cemot, alisema uchaguzi wa Zanzibar uliopita ulikwenda vizuri licha ya kuwapo dosari kidogo sawa na Tanzania Bara.

Alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na mashirika yasiyo ya kiserikali, walifanya kazi ya kutoa elimu ya wapigakura, tofauti na Tanzania Bara.

Pia alisema visiwani humo polisi walitekeleza vizuri wajibu wao tofauti na Tanzania Bara.

Dk Makulilo alisema asilimia 87 ya waangalizi wa Zanzibar walieleza polisi walifanya kazi nzuri kwa asilimia 65 kutokana na kusimamia vema uchaguzi.

Waziri Mkuu Asema Tanzania Imepiga Hatua Kiuchumi

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabadiliko ya kiuchumi yaliyofanyika nchini yameifanya Tanzania ipige hatua kubwa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

“Kumekuwa na mabadiliko chanya kwenye ukuaji halisi wa Pato la Taifa, kushuka kwa mfumuko wa bei, na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni. Pato la Taifa limekua kwa wastani wa asilimia 7 na mfumuko wa bei umeshuka hadi kufikia asilimia 5.3 mnamo Juni 2015 ikilinganishwa na asilimia 16 na asilimia 8 ilivyokuwa mwishoni mwa mwaka 2012 na mwanzoni wa mwaka 2013,” alisema.

Alitoa kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Machi 9, 2016) wakati akihutubia kongamano la biashara baina ya Tanzania na Vietnam lililofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Bw. Troung Tan Sang.

Akizungumza kwa niaba ya Rais, Dk. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema mbali ya mabadiliko ya kiuchumi, Tanzania pia imefanya mabadiliko kwenye sheria, mifumo ya kifedha na sekta za kuhudumia jamii za umma.

“Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita tumefanya mabadiliko ya kisera na kwenye sheria zetu ili kuboresha hali ya uwekezaji, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi,” alisema.

Alitoa mwaliko kwa wafanyabiashara walioambatana na Rais wa nchi hiyo kwa kuwaeleza kwamba faida kubwa ya kuwekeza nchini Tanzania ni uwepo wa soko la uhakika kwa wakazi zaidi ya milioni 300 waishio Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika.

“Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya za Kikanda katika SADC na EAC. Uwepo wake katika taasisi hizi ni fursa tosha. Pia Tanzania ni lango kwa nchi sita ambazo hazipakani na bahari. Inasaidia kufanyika biashara katika nchi za Congo (DRC), Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi na Uganda,” alisema.

Akizungumzia kuhusu fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo, Waziri Mkuu aliwakaribisha wafanyabiashara hao wawekeze kwenye kilimo cha biashara na viwanda vya usindikaji ili waweze kusaidia kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.

“Tuwakaribisha kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani za mazao yanayozalishwa nchini, kujenga viwanda vidogo vya kutengeneza vifungashio kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi. Pia mnaweza kuwekeza kwenye utengenezaji wa zana za kilimo ambazo ni za bei nafuu kwa wananchi wetu,” alisema.

Waziri wa Elimu Profesa Ndalichako Aingilia kati Mgogoro wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph Dar es Salaam

$
0
0

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ameingilia kati mgogoro wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph Dar es Salaam, waliogomea kufanya mitihani na kuwataka warejee madarasani wakati matatizo yao yakishughulikiwa.

Wanafunzi hao walikuwa katika siku ya tatu ya mgomo wao jana ambapo pamoja na mambo mengine walikuwa wakilalamikia mapungufu yaliyopo chuoni hapo, ikiwa ni pamoja na maabara za kufanyia mafunzo kwa vitendo, matatizo ya kiutawala, mitaala ya kufundishia pamoja na ada.

Profesa Ndalichako aliwasili chuoni hapo jana asubuhi na kukagua mazingira ya kufundishia ya chuo hicho kwa kutembelea maabara zote chuoni hapo na kisha kwenda kuzungumza na utawala, Serikali ya wanafunzi na mwisho alihutubia wanafunzi wote.

Ndalichako baada ya kuzungumza na pande zote mbili aliagiza wanafunzi hao warejee madarasani kuendelea na mitihani yao na kuutaka uongozi wa chuo uyafanyie marekebisho mapungufu ya kiutawala yaliyojitokeza.

Aidha ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), chini ya Katibu Mtendaji wake, Profesa Yunus Mgaya kufuatilia na kuchunguza kwa makini madai ya wanafunzi hao juu ya kuwepo kwa wahadhiri wasio na sifa zinazotakiwa.

Rais Wa Zanzibar Afanya Mazungumzo Na Rais Wa Vietnum

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akipofika kwa mazungumzo na ujumbe aliofuatana nao,Picha na Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake (kushoto) wakiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Rais wa Vietnam Truong Tan Sang jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akiwa nchini kwa ziara ya Kikazi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akifuatana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(katikati) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Augustin Mahiga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akiagana na mgeni wake Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(katikati) mawair mbali mbali wa Vietnum walioungana na Rais Truong
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images