Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

SSRA Yatetea Uraia Wa Dr Wangwe Ambaye Aliteuliwa Kukaimu NSSF na Kisha 'Kutumbuliwa' ndani ya Masaa Matano

$
0
0

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imetetea uraia wa Dk Carina Wangwe ikisema ni Mtanzania kwa kuandikishwa tangu mwaka 1999.

Dk Wangwe aliteuliwa juzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama kuwa kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kudumu katika nafasi hiyo kwa saa tano kabla ya uteuzi huo kutenguliwa kwa maelezo kuwa taratibu hazikuwa zimekamilika.

Kutenguliwa huko kulielezwa na baadhi ya watu kuwa ilikuwa ni kwa sababu mkuu huyo wa Tehama SSRA ni raia wa Uganda, madai ambayo yalikanushwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue,.

Taarifa ya ufafanuzi iliyotolewa jana usiku na Kitengo cha Mawasiliano cha SSRA, ilisema Dk Wangwe aliandikishwa kuwa raia baada ya kukidhi vigezo vya kuasiliwa (naturalisation) kwa mujibu wa kifungu cha 11 cha Sheria ya Uraia Na. 6 ya mwaka 1995.

Sambamba na hilo, taarifa hiyo ilisema Dk Wangwe aliukana uraia wa Uganda ikiwa ni pamoja na kurudisha pasipoti ya nchi hiyo aliyokuwa akiimiliki.

“Hivyo amekuwa raia wa Tanzania kwa kipindi cha miaka 17 na anamiliki cheti cha uraia Na. 58391 kilichotolewa na mamlaka husika tarehe 23 Aprili, 1999,” inasomeka taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inasema Dk Wangwe ni mtumishi halali wa SSRA kuanzia mwaka 2011 hadi sasa baada ya kukidhi vigezo vya uraia na utaalamu.

“Ana uzoefu wa miaka 21 akiitumikia Tanzania katika nyadhifa tofauti ikijumuisha Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi (miaka mitatu), Mfuko wa Pensheni wa PPF (miaka 9) na SSRA,” inasema taarifa hiyo.

Chadema Yaunda Chombo Kipya Cha Kulisimamia Jiji la Dar es Salaam

$
0
0

Katika kile kinachoonekana kutaka kuliongoza Jiji la Dar es Salaam kwa mafanikio ya kupigiwa mfano, Chadema imeunda chombo kipya cha uongozi katika jiji hilo na kukiita ‘Uongozi wa Dar es Salaam Kuu’.

Pia, imemteua Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara kuwa mwenyekiti wa chombo hicho.

Chama hicho kikuu cha upinzani nchini kimeunda chombo hicho, huku kikieleza kuwa na uhakika wa kushinda uchaguzi wa meya wa jiji hilo kwa ushirikiano na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutokana na kuwa na idadi kubwa ya madiwani ikilinganishwa na CCM.

Uchaguzi huo umeahirishwa mara tatu na ya mwisho kwa kutumia zuio ‘batili’ la Mahakama na kuzua mtafaruku kati ya wabunge na wadiwani wa chama hicho dhidi ya polisi, jambo lililosababisha wabunge wawili, Halima Mdee na Waitara pamoja na madiwani watatu kufikishwa mahakamani wakidaiwa kumshambulia Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya kikao cha Kamati Kuu jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema katiba ya chama hicho iliubadilisha Mkoa wa Dar es Salaam kuwa mamlaka ya kichama ya kimkoa na hivyo wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke zimepewa jina la mkoa badala ya wilaya.

“Baada ya kuona sintofahamu ya uchaguzi wa meya na namna ambavyo Serikali inavifanyia vyama vinavyounda Ukawa kuhusu suala hilo, chama kiliunda uongozi wa kimkoa, kimeamua kujipanga upya katika Jiji la Dar es Salaam,” alisema Mbowe.

Alisema wameunda chombo hicho kwa mujibu wa Ibara ya 6.1.3 ya katiba ya chama hicho ili kurejesha demokrasia iliyopotea katika Jiji la Dar es Salaam.

 Ibara hiyo inasema; Kwa kuzingatia ibara ya 6.1.2, ngazi ya juu ya chama itateua kamati ya muda itakayokuwa na wajibu wa kuratibu shughuli za chama na kuwaunganisha wanachama katika eneo lisilo na uongozi wa kikatiba mpaka watakapofikia uwezo wa kuwa na uongozi wa kikatiba.

Alisema kifungu hicho kinaongezewa nguvu na kifungu cha katiba cha 7.5.1 kinachoeleza jinsi ngazi za uongozi zinavyoundwa katika kila eneo la mkoa wa kiutawala wa Serikali Kuu, “Katika ngazi hii patakuwa na mikoa ya chama ambayo imetimiza masharti yaliyobainishwa na katiba na sehemu (c) inasema wilaya za Dar es Salaam zitakuwa na hadhi sawa ya kimkoa ya chama.”

Mbowe alisema mikoa hiyo ya kichama ya Kinondoni, Ilala na Temeke, itakuwa na chombo kitakachoiunganisha ambacho ni uongozi wa Dar es Salaam Kuu. 

“Uongozi huo umeteuliwa makusudi ili kuongeza nguvu, usimamizi na uratibu wa operesheni za chama katika jiji hili,” alisema. 

 Alisema chombo hicho kitakuwa na wajumbe wasiozidi 25 na uongozi wa chama hicho katika mikoa ya Kinondoni, Temeke na Ilala utabaki vilevile.

Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema kamati inayounda chombo hicho itawahusisha wabunge wote wa kuchaguliwa na wa viti maalumu wa Chadema mkoani humo na mameya wa Ilala na Kinondoni.

Wabunge hao ni Mdee, John Mnyika (Kibamba), Waitara, Saed Kubenea (Ubungo), Susan Lyimo, Anatropia Theonist na Lucy Mollel.

Wengine ni mgombea wa Chadema katika nafasi ya umeya wa Jiji, Yesaya Mwita, Meya wa Ilala, Charles Kuyeko na Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob pamoja na baadhi ya madiwani na viongozi wengine wa chama hicho jijini Dar es Salaam akiwamo Henry Kilewo ambaye ni Katibu wa Chadema Mkoa.

“Mwenyekiti wa kamati hii atakuwa Waitara na Makamu wake ni Bernard Mwakyembe ambaye ni diwani kutoka Wilaya ya Temeke. Katibu atakuwa Kilewo na Mweka Hazina ni Lyimo,”alisema Mbowe.

Dc -Paul Makonda Azindua Vitambulisho Vya Walimu Kupanda Daladala Bure Jijini Dar Es Salaam

$
0
0

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezindua vitambulisho vitakavyotumiwa na walimu kupanda daladala bure wakati wakitoka nyumbani kwenda kazini.

Katika hatua nyingine Makonda ameziomba sekta mbalimbali nchini kushiriki katika kutoa mawazo yao ya maendeleo ili taifa lisonge mbele badala ya kuwa watazamaji.

Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam jana mbele ya wazazi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Turiani wakati akizindua vitambulisho hivyo vitakavyotumiwa na walimu wa wilaya yake kupanda daladala bure kufuatia mpango aliouanzisha wiki iliyopita wa kuwasaidia  walimu hao.

"Nawaomba watanzania na sekta mbalimbali kuwa na mawazo ya maendeleo ambayo yatawekwa mezani na kuyafanyia kazi jambo litakalo msaidia Rais wetu Dk.John Magufuli katika kuliinua taifa kiuchumi badala ya kumuachia kila kitu akifanye yeye" alisema Makonda.

Makonda alitoa mwito kwa makondakta wa daladala kutoa ushirikiano kwa walimu hao kesho wakati watakapoanza kupanda magari yao huku wakijua walimu ndio waliowafundisha na kufikia hatua hiyo ya kazi walizonazo.

Ofisa Elimu wa Sekondari wa Wilaya hiyo, Rogers Shemwelekwa aliwaomba wananchi hao na walimu kuendelea kuunga mkono jitihada za Makonda za kuwaletea maendeleo na kumuombea kwa mungu badala ya kumbeza kwani kazi hizo anazozifanya ni kwa ajili ya wananchi.

Waziri Mkuu Atuma Mawaziri Watatu Kutatua Migogoro Ya Ardhi Simiyu

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atawatuma mawaziri watatu waje mkoa wa Simiyu ili wakae na uongozi wa kila wilaya pamoja na wananchi ili kubaini tatizo la mipaka baina ya wilaya hizo na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana(Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa vijiji vya Mwakaluba na Mwandoya akiwa kwenye siku ya tano ya ziara yake mkoani Simiyu.

“Tangu niingie hapa mkoani malalamiko ya mipaka nimeyapokea kila mahali nilikopita. Nimeamua kuwatuma mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi; Waziri wa Maliasili ua Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bw. George Simbachawene waje mkoa huu kutatua matatizo yenu,” alisema.

“…Nitawatuma waje na wapite kila wilaya, wakae na kuzungumza na wakulima na wafugaji ili kubaini ni chanzo cha tatizo la migogoro hii kwenye mipaka ya vijiji na hifadhi ya Serengeti. Pia Waziri wa TAMISEMI itabidi atoe ufafanuzi kuhusu agizo lao la kutofanya shughuli yoyote mita 60 kutoka kwenye mto Simiyu ili wananchi waelewe,” alisema.

Mapema, Mbunge wa Kisesa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi (OMR – Mazingira) alimweleza waziri Mkuu mbele ya wananchi hao kwamba limetolewa zuio linalowakata wakazi wa mkoa huo wasifanye shughuli zozote umbali wa mita 60 kutoka kwenye kingo za mto huo.

“Limebandikwa tangazo linalokataza wananchi waishio kando ya mto Simiyu wasifanye chochote kuanzia Julai 30, 2016. Wananchi hawajashirikishwa wala kuelezwa chochote zaidi ya kuona bango la matangazo tu. Watu wananakatazwa wasichote maji wala kunywesha mifugo wakati hakuna mabwawa, itawezekanaje? Tunaomba kauli yako kuhusu jambo hili,” alisema.

Ili kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi hapa nchini, Waziri Mkuu alisema Serikali ina mpango wa kuunda mabaraza ya ardhi 100 kwa nchi nzima ambayo yatakuwa na jukumu la kutatua migogoro ya ardhi kwa wakati.

Akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Bw. Erasto Sima alisema wilaya hiyo iliyoanzishwa Julai mosi, 1987 ina ukubwa wa kilometa za mraba 8,835 ambapo asilimia 49 (sawa na kilometa za mraba 4,329) ya eneo lote la wilaya hiyo ni hifadhi za wanyamapori.

Alilitaja eneo hilo kuwa ni pori la akiba la Maswa, sehemu ya hifadhi ya Serengeti, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na pori la hifadhi ya usimamizi wa wanyama (WMA) la Makao na kwamba asilimia 51 iliyobakia indiyo inayotumiwa kwa makazi ya watu, kilimo na malisho ya mifugo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya March 6

Mbowe Afunguka Sakata la Umeya Dar

$
0
0
Freeman  Mbowe, mwenyekiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) amesema kuwa, umoja huo kamwe hautaomba Umeya wa Jiji la Dar es Salaam bali watadai.

Amesema, Jeshi la Polisi linafanya hujuma kwa kuzuia mikutano pamoja na kukamata wabunge pia madiwani wa Ukawa na kwamba, hiyo ni mikakati ya kukisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda uchaguzi wa umeya Dar es Salaam.

Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema-Taifa amesema umoja huo haupo tayari kushiriki uchaguzi wa Meya kwa kushtukiza akidai kuwepo kwa mkakati huo.

Amesema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho na kwamba, mara zote wamekuwa wakitaarifiwa kwa kushitukiza ili wasipate muda wa kujiandaa.

“Sasa tumechoka kuwabembeleza, mara zote huwa tunafanya kwa kuheshimu maamuzi yao hata kama wanavunja katiba,” alisema Mbowe na kuongeza;

“Jana ( juzi) wabunge na madiwani wetu walienda kwa Mkurugenzi wa Jiji kwa lengo la kutaka kujua tarehe ya uchaguzi, lakini hatukupata, kwa kuwa tumeshaomba hawataki sasa tutakachoamua tusilaumiane. Tumechoka kudai haki kwa kubembeleza na sasa hatutaomba tena.”

“Tunakosa imani na viongozi wa kiserikali na Jeshi la Polisi kwa ujumla juu ya utendaji wake na kutokana na yanayoendelea yakiwemo ya viongozi wetu wa chama kukamatwa tunapata wasiwasi inawezekana polisi ni vibaraka wa (CCM),”amesema Mbowe.

Akieleza baadhi ya maazimio ya Kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichokaliwa tarehe 1 Machi mwaka huu alisema, kilitafakari utendaji wa Rais John Magufuli na kubaini kuwa, serikali yake inavunja misingi ya utawala bora ikiwemo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kusimamia majukumu yake.

Alisema chama kinaandaa mkutano mkubwa utakaofanyikia Mwanza ambao utashirikisha viongozi wa nchi nzima pamoja na wabunge kwaajili ya kujadili hali ya chama na jinsi ya kujipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2020.Mkutano unatarajiwa kuanza tarehe 13 Machi mwaka huu.

Ikulu Yavunja Ukimya Sakata la Umeya Dar

$
0
0
Ikulu imevunja ukimya kuhusu ile sinema ya kuahirishwa mfululizo kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam kwa kusema haitaona tatizo lolote iwapo Halmashauri hiyo itaongozwa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Uchaguzi huo utakapofanyika na vyama hivyo kushinda na kuongoza Jiji, Ikulu imesema, hakutaathiri hata kidogo shughuli zake za kila siku hivyo haina mkono wake kwenye sarakasi za uchaguzi huo.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, alipoulizwa  ni kwanini Ikulu isiingilie kati na kuamuru kufanyika kwa uchaguzi huo ambao umeshapigwa danadana muda mrefu.

“Hilo la hisia kwamba Ikulu ina mkono wake kwa kuhofia Ikulu kuwa chini ya Ukawa si kweli hata kidogo,” alisema Balozi Sefue.

 "Sisi tuogope nini wakati wao hawataathiri shughuli zetu za kila siku? Nakuhakikishia hatuoni tatizo lolote."

Kumekuwa na tetesi kwamba serikali inahofia upinzani kuchukua Jiji, kwani Ikulu ni kama itakuwa ndani ya eneo linalotawaliwa na wapinzani hali itakayoleta mgongano wa kiutendaji na kimaslahi.

Balozi Sefue alisema Jiji kuongozwa na Ukawa hakuwezi kuwanyima usingizi hata kidogo kwasababu iko miji mingi mikuu duniani ambayo inaongozwa na vyama vya upinzani na shughuli za Ikulu kwenye miji hiyo zinaendelea kama kawaida.

“Sisi hatuhofii na wala hatuoni sababu ya kuingilia uchaguzi huo ati kwa kuhofia Ukawa kuongoza Jiji, mbona miji mbalimbali duniani inaongozwa na vyama vya upinzani na mambo yanakwenda kama kawaida?" Alihoji.

"Sisi hatutakuwa wa kwanza duniani na wala hakuna kitakachobadilika.”

Kuhusu zoezi hilo kutawaliwa na ubabaishaji, Balozi Sefue alisema kwa sasa Ikulu haiwezi kuingilia kati na kulazimisha siku ya uchaguzi huo kwasababu wahusika wapo na hawajasema kama wameshindwa.

“Waziri anayehusika na Tamisemi yupo na hasema kwamba ameshindwa. Sasa kwanini sisi tuingilie suala lao?

"Mimi naamini hawajashindwa na wakishindwa wenyewe wanajua waende wapi kwa ajili ya ufumbuzi.

Mvutano wa Umeya wa Jiji umetokana na vyama vinavyounda Ukawa kuvuna madiwani wengi kuliko CCM katika jiji la Dar es Salaam hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kutwaa Halmashauri ya Jiji, ikiwa uchaguzi huo utafanyika kwa uhuru na haki.

Jiji lina madiwani 76 wa CCM wakati Ukawa ina 87.
Tayari Halmashauri mbili kati ya tatu za Dar es Salaam zinaongozwa na Ukawa: Ilala na Kinondoni wakati CCM ikiongoza Temeke pekee.

Hata idadi ya wabunge kwa Dar es Salaam, Ukawa imeizidi kwa mbali CCM ambayo imepata wabunge wanne tu ambao ni Faustine Ndungulile wa Kigamboni, Issa Mangungu (Mbagala), Bona Kaluwa (Segerea) na Mussa Azan Zungu (Ilala).

Katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana Ukawa ilichukua majimbo ya Kawe linaongozwa na Halima Mdee (Chadema), Ukonga la Mwita Waitara (Chadema), Ubungo la Saed Kubenea (Chadema), Kibamba la John Mnyika (Chadema) na Kinondoni la Maulid Mtulia (CUF).

Katika kuonyesha kuwa sakata hilo bado ni moto, madiwani na wabunge wanaotoka Ukawa, juzi walivamia ofisi za Jiji wakishinikiza waambiwe tarehe ya uchaguzi huo.

Wanachama hao wa Ukawa walikaa kwa saa nzima kwenye ofisi hizo bila kupata jibu kutoka kwa wahusika na walisikika wakilaumu uongozi wa Jiji kuwa umepanga kuwahujumu.

Ingawa Ikulu ilisema kuwa haiwezi kuingilia suala hilo kwa kuwa Waziri husika hajashindwa, kuna dalili kwamba waziri mwenye dhamana amenawa mikono na hajui namna ya kutatua tatizo hio

Jiji liko chini ya Tamisemi ambayo iko Ofisi ya Rais hivyo kumekuwa na hofu kwamba iwapo Ukawa watachukua kiti cha Meya, kutakuwa na mgongano mkubwa wa sera na utekekelezaji wa ilani ya upinzani na ya Ukawa.

Vyama vya Ukawa vilishatoa angalizo hivi karibuni kwamba serikali inajaribu kutengeneza mgogoro ili kumpa nafasi Rais John Magufuli kuvunja Halmashauri ya Jiji na kuunda tume ya jiji.

Sheria ya Tamisemi ya mwaka 1982 inampa mamlaka Rais kuvunja Halmashauri ya Jiji/Mji/Manispaa na kisha kuteua tume.

Mwaka 1996, Fredrick Sumaye, akiwa Waziri Mkuu, aliivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuunda tume iliyoongozwa na Charles Keenja.

Wiki iliyopita ziliibuka vurugu za kurushiana makonde kati ya wafuasi wa Ukawa na Polisi kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi huo kutokana na madai ya kuwepo zuio la muda Mahakama lilowekwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambalo baadaye ilibainika kwamba lilikuwa feki.

Kabla ya wiki iliyopita, uchaguzi wa Meya wa Jiji ulishaahirishwa mara moja kwa sababu za kiujanja ujanja kutokana na pingamizi la CCM.

Video: Rais Magufuli Akimtangaza Katibu Mkuu Kiongozi Mpya Baada ya 'Kumtumbua' Ombeni Sefue

$
0
0
Video ya Rais Magufuli  akimtangaza John Kijazi Kuwa Katibu mkuu Kiongozi kuchukua nafasi ya Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Awawasimamisha Kazi Madaktari Wawili na Wauguzi Watano kwa Kusababisha kifo cha mjamzito na Watoto wake Mapacha

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo amewasimamisha kazi madaktari wawili na wauguzi watano wa Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure kutokana na uzembe unaodaiwa kusababisha kifo cha mama mzazi Pendo Masanja na watoto wake mapacha.
 
Tukio hilo linakuja ikiwa ni siku chache baada ya mapacha wengine kupoteza maisha wakati wa kuzaliwa katika hospitali ya wilaya ya nyamagana iliyopo Butimba jijini Mwanza kwa kile kinachoelezwa kuwa ni uzembe wa wauguzi pamoja na madaktari wa hospitali hiyo kushindwa kumhudumia kwa wakati mama mjamzito Suzan John machi 3 mwaka huu.
 
Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza pia amewasimamisha kazi wauguzi wengine wawili wa hospitali ya Butimba ambao ni Nathan Bagaya na Edina Mwesiga,Daktari mmoja wa Hospitali hiyo Furaha Kingunge na dereva wa gari la kubeba wagonjwa ( AMBULANCE) Ghalib Hamad, huku akitangaza kuunda tume ya watu wanne ikiongozwa na mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dk. Onesmo Rwakyendera kwa ajili ya kuanza uchunguzi dhidi ya watumishi hao.
 
Tume iliyoundwa na mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza kuchunguza uzembe wa madaktari pamoja na watumishi wa hospitali hizo mbili za butimba na Sekou Toure, huenda ikaja na majawabu sahihi na ufumbuzi wa changamoto zinazopelekea kutokea kwa vifo vya watoto wachanga na akinamama wajawazito wakati wa kujifungua.

Serikali Yaanzisha Mfumo Mpya Wa Malipo Ya Mishahara Kwa Watumishi Wa Umma

$
0
0

SERIKALI imeanzisha mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao unalenga kuondoa tatizo la madai ya malimbikizo ya stahili zao.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa sekta mbalimbali  katika wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu.
 
Waziri Mkuu alisema mfumo huo ujulikanao kama LAWSON, unatumika kwenye ajira za watumishi wote nchini, wa Serikali Kuu na wale wa Serikali za Mitaa  
 
Waziri Mkuu alisema mfumo huo unasaidia kutunza, kutuma na kuhuisha  taarifa za watumishi kwa wakati na kwa ufanisi tangu mtu anapoajiriwa hadi inapofikia wakati wa kupandishwa madaraja na hadi anapostaafu.

Kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo, maafisa utumishi walipaswa kukusanya taarifa za watumishi wote walioajiriwa na kuzipeleka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili zikathibitishwe kabla ya kuzipeleka HAZINA kwa maandalizi ya mishahara. 
 
Akitolea mfano wa kada ya ualimu, Waziri Mkuu alisema ajira za walimu zilikuwa zinaanzia Idara ya Utumishi wa Walimu  (TSD)  lakini anapaswa aende kuripoti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri  (DED) ambaye ni mwajiri wake chini ya TAMISEMI.

 "Hii ilileta ugumu wa malipo ya kupanda madaraja, uhamisho ama likizo kwa sababu mwajiri anakuwa hajatenga hizo fedha."
 
"Sasa hivi tuna Tume ya Utumishi wa Walimu  (TSC) ambayo iko chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. Kwa hiyo ni rahisi wao kukaa pamoja na kuamua tuwapandishe daraja walimu 10 na wote hao wakalipwa bila bila kuchelewa," alisema.
 
Alisema mfumo huo umeanza kutumika tangu mwaka 2012 na ulianza kwa ajira mpya za walimu na hadi sasa umethibitisha kuwa inawezekana kumlipa mtumishi mshahara wake hata kama ameajiriwa ndani ya mwezi huohuo.
 
"Kama mtumishi anaripoti kwenye kituo kipya hata iwe wilaya ya wapi ili mradi amefika na barua zake zote na ziko sahihi mtu huyu ataingiziwa taarifa zake na wakati huohuo taarifa zitaonekana Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na pia zitapokelewa kwa maafisa wanaoshughikia mishahara kule HAZINA."
 
Alisema changamoto pekee waliyokutana nayo wakati mfumo huo umeanza ilikuwa ni kutoingizwa taarifa za wale ambao wameripoti baada ya tarehe 10 ya mwezi husika. 

"Hii ni kwa sababu matayarisho ya mishahara yanakuwa yameshaanza. Kwa hiyo wengi walishauriwa kuripoti kati ya tarehe 25 hadi tarehe 9 ya mwezi uliofuata na wote hawa hawakupata matatizo ya kucheleweshewa mshahara," alisema.
 
Akifafanua kuhusu upandishaji madaraja ya watumishi, Waziri Mkuu alisema  Serikali imeondoa utaratibu wa mtumishi kulazimika kuandika barua ya kukiri kupandishwa daraja/cheo ndipo aanze kupata stahili zake mpya. 

"Hii imeondoa ucheleweshaji wa kufanyika marekebisho ya mshahara  na pili imeondoa tofauti za mishahara kwa watumishi wenye ngazi moja (sifa sawa za kitaaluma, tarehe moja ya kuajiriwa) ambao walikuwa wakilipwa tofauti kwa sababu mmoja aliwahi kuandika barua ya kukiri na mwingine alichelewa kuandika barua hiyo hiyo " alisema

AKATISHA ZIARA KUTOKANA NA MSIBA
Wakati huohuo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amelazimika kukatisha ziara ya mkoa wa Simiyu ambayo ilikuwa imalizike kesho kutokana na msiba wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambayo alipangiwa kuitembelea leo.
 
Mkurugenzi huyo Bw. Traceas Kagenzi alifariki dunia usiku wa kuamkia jana kutokana na shinikizo la damu. Atasafirishwa kwenda Muleba  kwa mazishi.

Akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada ya kumuombea marehemu Kagenzi iliyofanyika nyumbani kwake Maswa mjini, Waziri Mkuu alisema ameshtushwa na msiba huo uliotokea ghafla na kwamba Taifa limempoteza mtumishi mahiri ambaye bado Taifa lilikuwa likimtegemea.

"Nimeshtushwa sana na taarifa za msiba huu. Nimeambiwa hadi juzi usiku alikuwa akishirikiana na Mkuu wa Wilaya hii kuandika taarifa ya ziara ya wilaya hii. Kwa niaba ya Serikali, ninawapa pole sana wafiwa na Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi," alisema.

"Nimelazimika kukatisha ziara ya mkoa huu kwa sababu huyu ni mtumishi mwenzetu" alisema Waziri Mkuu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, MACHI 6, 2016.

Breaking News : Rais Magufuli Ampiga Chini Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.....John Kijazi Kateuliwa Kuchukua Nafasi Yake

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. 

Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi  wa Mawasiliano,
 IKULU-Dar es Salaam
06March,201
Katibu Mkuu Kiongozi Mpya, Balozi John William Kijazi

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya March 7

Ziara ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Yawapa Kiwewe Wakuu wa Wilaya Kagera

$
0
0

Kasi ya kutumbua majipu imeonekana kuwatia kiwewe wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Kagera kwa kufanya kazi na mikutano ili kuhakikisha hakuna makosa yatakayoonekana wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ya kukagua miradi ya maendeleo inayoanza kesho kutwa.

Kwa wiki moja sasa, wakuu hao wanafanya mikutano ya kila siku na kukagua miradi hiyo ili kuhakikisha hakuna makosa yanayoweza kusababisha kutumbuliwa majipu.

Mkuu wa Wilaya ya Missenye, Festo Kiswaga alisema mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa wamechukua tahadhari kwa kuhakikisha kila eneo liko salama.

“Tunafanya maandalizi kila sehemu na idara maana ni vigumu kutabiri Waziri Mkuu atatembelea wapi,” alisema Kiswaga.

Alisema ratiba ya maeneo atakayotembelea Waziri Mkuu imebadilika mara tatu tangu walipotaarifiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Jackson Msome alisema wanalazimika kuzingatia kanuni ya mchezo wa soka kwa kuelekeza maandalizi kila idara kuanzia sehemu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

“Ni lazima kujiandaa kila idara kufanikisha ziara ya Waziri Mkuu kwa sababu hatuwezi kujiamini na ratiba bila kuchukua tahadhari ya ziara za kushtukiza eneo lolote,” alisema Msome.

Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Darry Rwegasira alisema licha ya ratiba kuonyesha kuwa Waziri Mkuu atatembelea na kuzindua jengo la upasuaji katika kituo cha Afya cha Nyakanazi, wamefanya maandalizi katika eneo lote ili kuepuka kushtukizwa iwapo ratiba itabadilika ghafla.

Mfanyabiashara mjini Bukoba, Dennis Gregory alisema wanakusudia kuwasilisha kwa Waziri Mkuu changamoto ya bei ndogo ya kahawa inayouzwa nchini ikilinganishwa na Uganda.

Mwanafunzi Atoroka Bwenini Usiku, Abakwa na Kisha Kunyongwa

$
0
0

Mwanafunzi  wa bweni wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya kata ya Mnero, tarafa ya Ruponda, wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, Agnes Jeremiah (18) ameuwawa kwa kunyongwa na watu wasiofahamika usiku kisha mwili wake kutupwa kichakani.

Habari za uhakika kutoka wilayani humo na ambazo zimethibitishwa na Jeshi la Polisi zinaeleza mwanafunzi huyo alinyongwa Februari 27, mwaka huu saa 4:30 usiku.

Mashuhuda wamesema kuwa Agnes alikuwa na tabia kutoroka bwenini nyakati za usiku na kwenda nje ya shule.

“Taarifa ambazo tunazisikia huyu marehemu alikuwa akitoroka bwenini usiku na kwenda anakokufahamu mwenyewe kabla ya kurejea alfajiri,” alisema mmoja wa watoa  ambaye hakupenda jina lake litajwe

Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Renatha Mzinga amekiri kutokea kifo cha mwanafunzi huyo, na kueleza uchunguzi walioufanya umebaini alikuwa ni tabia ya kutoroka bwenini nyakati za usiku na kwenda kwa mpenzi wake wa kiume.

“Ni kweli taarifa ya kifo cha huyo mwanafunzi Agnes Jeremiah ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mandawa, akiwa bwenini huko Mnero Sekondari alitoroka usiku kwenda kwa mwanaume,” alisema Mzinga.

Mzinga alisema uchunguzi unaonyesha mwanafunzi huyo alipofika eneo la kichaka kilichopo karibu na kanisa la Roma, alibakwa na wanaume kisha kunyongwa shingo na mwili wake kutelekezwa papo hapo.

Akasema katika kufuatilia tukio hilo, wanamshikilia mkazi wa kijiji cha Mnero Ngongo, Abdallah Ismaili (19) ambaye ni dereva wa bodaboda kwa mahojiano zaidi.

”Inasemekana huyu dereva wa bodaboda ndiye aliyekuwa akienda Shuleni hapo kumchukuwa na kumpeleka kwa mwanaume wake ambaye kwa sasa ametoweka kijijini hapo,” alisema Mzinga.

Hata hivyo, kamanda huyo wa Polisi Lindi hakuwa tayari kutaja jina la mwanaume anayedaiwa kuwa na mahusiano na mwanafunzi huyo, kwa maelezo kwamba anaweza kuvuruga upelelezi.

“Tunaendelea kumsaka huyu mwanaume wake aliyekuwa akipelekwa mwanafunzi huyu, hivyo iwapo tutamtaja jina tunaweza kuharibu upelelezi wetu.”

Siku 67 za Ombeni Sefue Ikulu Kabla ya Kutumbuliwa JIPU Jana

$
0
0
JANA ilikuwa siku ambayo Rais John Magufuli alitoa uamuzi mzito wa kubadilisha nafasi za uongozi wa ngazi ya juu zaidi kwa viongozi ambao amefanya nao kazi baada ya kumuondoa Balozi Ombeni Sefue aliyekuwa katibu Mkuu Kiongozi, akiwa mstari wa mbele kutangaza wanaotumbuliwa majipu.
 
Balozi Ombeni Sefue alikuwa kivutio cha  wengi  kwenye vyombo vyahabari kutokana na kutoa taarifa za kutenguliwa uteuzi kwa watumishi waandamizi wa umma, lakini jana hali ilikuwa tofauti baada ya kibao kugeuka.

Ombeni Sefue aliibukia kuwa kipenzi cha vyombo vya habari katika muda mfupi aliofanya kazi na Rais Magufuli, huku mitaani akivuta wengi karibu na runinga kila alipoonekana, hasa kutokana na wananchi kutarajia kusikia habari za kutumbuliwa kwa majipu ambao umekuwa ukifanywa na Serikali tangu Rais aapishwe Novemba 5, 2015.

Alianza kuchukuliwa na wengi kuwa ni mchapakazi na muadilifu na angeweza kwenda na kasi ya Rais Magufuli, ambaye amekuwa akihimiza mambo hayo na kusisitiza kuwa mtu asiyeweza kwenda na kasi yake, hatamvumilia.

Hakuna aliyekuwa na shaka na Balozi Sefue. Hata gazeti la Dira lilipotoa habari mfululizo kwenye matoleo mawili likimuhusisha na ushauri mbaya kwa Rais na pia utafutaji wa mjenzi wa daraja la Kigamboni, wengi hawakuweza kuamini, hasa kutokana na kuonekana kuwa karibu na Rais.

Lakini uamuzi wa Rais kumteua Balozi Kijazi kushika nafasi yake, unaweza kuibua mjadala mpya kuhusu ujenzi wa daraja hilo na mabadiliko yanayofanywa na Rais.

Uteuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi mpya umekuja siku 67 tangu Rais Magufuli atangaze kuteua makatibu wakuu 29 wapya Desemba 30, 2015 huku Sefue akihakikishiwa kuendelea kukaa Ikulu kwa mwaka mmoja zaidi.

Uteuzi huo pia umekuja siku chache baada ya gazeti la Dira kuanza kuandika jinsi Ikulu ilivyoshauriwa vibaya kuhusu uteuzi wa mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Madawa (MSD), ingawa Idara ya Habari (Maelezo) ilitoa tamko kali la kukanusha na kulitaka gazeti hilo liombe radhi, kitu ambacho hakijafanyika.

Uteuzi huo pia umekuja wakati kukiwa na sarakasi ya uteuzi wa Carina Wangwe kuwa kaimu mkurugenzi mkuu wa NSSF na uamuzi huo kutenguliwa saa tano baadaye (kutangazwa saa 11:150 jioni na kutenguliwa saa 4:15 usiku).

Katika sakata hilo, Sefue hakutangaza uteuzi huo ila alisema kuwa mamlaka ya kuteua ni ya Rais lakini ya kukaimu kuna taratibu zake, ambazo hakuzitaja. Alisema Wangwe alitakiwa kuwa mwangalizi.

Pia Balozi Kijazi, ambaye anamrithi Sefue kwenye nafasi ya Katibu Mkuu Kiongozi, ndiye aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu wakati pendekezo la ujenzi wa daraja la Kigamboni lilipotolewa na baadaye kupitishwa huku likikumbana na upinzani mkali toka kwa Kijazi na Magufuli ambaye wakati huo alikuwa ni Waziri  wa JK.

Balozi Kijazi aliondolewa wizara hiyo na kupelekwa ubalozini nchini India mwaka 2007 huku  Magufuli  akihamishiwa Wizara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo mwaka 2008.
Balozi Sefue alizaliwa Agosti 26, 1954 wilayani Same, Kilimanjaro. Alisomea Utawala na Sera za Umma kwenye Chuo cha Uongozi cha Mzumbe, ambacho sasa kinaitwa Chuo Kikuu cha Mzumbe.

Baadaye alipata shahada ya uzamili katika fani hiyo kwenye Chuo Kikuu cha Masomo ya Kijamii cha The Hague nchini Uholanzi mwaka 1981.

Pia ana astashahada ya uzamili ya masuala ya uhusiano wa kimataifa aliyoipata Chuo cha Diplomasia kilichopo Dar es Salaam.

Pia ana cheti cha usuluhishi wa kimataifa, matatizo ya kiuchumi na kijamii ya nchi zinazoendelea. Balozi Sefue na mkewe Anita wana watoto wawili, wa kiume na kike.

Amekuwa balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2007. Kabla ya hapo, alikuwa balozi wa Tanzania nchini Canada (2005-07).

Balozi Sefue aliachana na kazi ya udiplomasia mwaka 1993 na kwenda kufanya kazi ya kuandika hotuba za rais na pia kuwa msaidizi binafsi wa Rais Ali Hassan Mwinyi. Baada ya uchaguzi wa mwaka 1995, Rais Benjamin Mkapa aliendelea naye hadi mwaka 2005 wakati alipoachia ngazi.

Balozi Sefue alifanya kazi kwa karibu na Mkapa wakati akiwa Kamisheni ya Afrika (maarufu kama kamisheni ya Blair) ambayo ilitengeneza ripoti iliyojulikana kwa jina la “Our Common Interest: Report of the Commission for Africa in March 2005”, na kushiriki naye kwenye kikao cha marais wa nchi nane tajiri duniani (G8) ambacho kilijadili ripoti hiyo.

Pia alifanya kazi kwa karibu na Mkapa wakati akiwa mwenyekiti mwenza wa kamati iliyochambua athari za utandawazi kijamii ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) kati ya mwaka 2002-2004.

Rais Kikwete alimteua kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Desemba 31, 2011 na amedumu na wadhifa huo mpaka jana, huku akifanya kazi na Rais wa Awamu ya Tano, Dk Magufuli kwa siku 67 tu licha ya kuwa aliongezewa mwaka moja.

Rais wa Vietnam Kutua Nchini Kesho Saa Mbili Usiku

$
0
0

RAIS wa Vietnam, Truong Tan Sang anatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ziara rasmi ya kiserikali akifuatana na mke wake Mai Thi, mawaziri watano na wafanyabiashara 51. 

Hii ni ziara ya kwanza ya Mkuu wa nchi kuzuru nchini tangu Rais John Magufuli aingie Ikulu, lakini pia itakuwa ziara ya kwanza kwa Rais Truong kuzuru Afrika na Tanzania na baadaye ataelekea Msumbiji.

Pamoja na kuwa na mazungumzo na Rais Magufuli, Rais Truong atakutana na Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Spika wa Bunge Job Ndugai na kushiriki dhifa ya kitaifa Ikulu. 

Atakapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam saa 2.30 usiku kesho, Rais Truong atapokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk Augustine Mahiga.

Mapokezi rasmi kwa Rais huyo yatafanyika Jumatano Ikulu, Dar es Salaam ambapo kama zilivyo taratibu za kidiplomasia duniani, atapigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi la Majeshi ya Ulinzi na Usalama. 

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Mahiga alisema baada ya kupokelewa Ikulu na Rais Magufuli, kupigiwa mizinga na kukagua gwaride, Rais Truong atakuwa na mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake Rais Magufuli.

“Baada ya mazungumzo waheshimiwa marais watahudhuria hafla ya utiaji saini Mkataba wa masuala ya Kodi. Mkataba huu lengo lake ni kuchochea biashara baina ya Vietnam na Tanzania ambapo wafanyabiashara wa nchi zetu mbili hawatatozwa kodi mara mbili kwa biashara na uwekezaji watakaoufanya,” alisema Balozi Dk Mahiga. 

Alisema saa tano kesho, Rais Truong na ujumbe wake watakwenda katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba kwa ajili ya kukutana na Kikwete na kufanya mazungumzo, hasa kutokana na Rais Truong kuwa pia ni mmoja wa viongozi waandamizi wa Chama cha Kikomunisti cha Vietnam ambacho kina uhusiano wa muda mrefu na CCM.

Kwa kuzingatia mabadiliko makubwa katika uhusiano wa kimataifa ambapo dunia sasa inatupia macho zaidi kwenye diplomasia ya uchumi, baada ya kutoka Lumumba, Rais huyo atakwenda katika eneo maalumu la uwekezaji la EPZA Ubungo ambapo atapata fursa ya kutembelea viwanda na kupata taarifa za fursa za uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini.

“Saa 9:00 kamili jioni, Rais Truong na ujumbe wake watahudhuria Mkutano wa Biashara na Uwekezaji baina ya Vietnam na Tanzania.

"Saa 11 jioni atakutana na Spika wa Bunge Ndugai, saa 12.30 atakutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein na saa 1 jioni atahudhuria Dhifa ya Taifa, itakayoandaliwa kwa heshima yake na Rais Magufuli,” alisema Dk Mahiga.

Kwa mujibu wa Dk Mahiga, Alhamisi Machi 10, Rais Truong na ujumbe wake watakuwa na ratiba ya kutembelea mbuga za wanyama kati ya Saadani na Serengeti na Ijumaa Machi 11, Rais Truong na ujumbe wake wataondoka nchini kuelekea Msumbiji.

Katika ujumbe wake, Rais huyo atafuatana na mawaziri watano; wa Viwanda, Kilimo, Mawasiliano, Afya na Maji. 

Uhusiano wa Tanzania na Vietnam 
Balozi Mahiga alisema uhusiano wa Tanzania na Vietnam ulianza miaka ya 1960 wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere wakati Vietnam ikiwa chini ya chama tawala cha Kikomunisti na Tanzania chini ya TANU (baadaye CCM) na kufanya kwa kiasi kikubwa nchi hizo kuwa na mambo yanayofanana kichama na kiserikali.

Alisema ikiwa nchi masikini kama Tanzania, Vietnam ilianzisha mapinduzi makubwa ya kuuhuisha uchumi wake ili kufikia uchumi wa kati, na katika miaka 15, uchumi wa nchi hiyo ulizaa miujiza, baada ya pato la mwananchi kutoka Dola 100 kwa mwaka hadi kufikia Dola 2,000 na kuwa mfano wa kuigwa kwa mataifa yanayoendelea Asia na Afrika. 

Ikiwa na ukubwa wa mita za mraba 330,000 ambao ni sawa na theluthi ya ukubwa wa Tanzania, ina idadi kubwa ya watu wanaofikia milioni 91 lakini Vietnam imefanikiwa kuwa nchi ya juu kabisa kwa uuzaji wa kahawa aina ya Robusta na korosho duniani na inaongoza kwa ufugaji wa samaki.

“Kinacholeta upekee hapa ni kwamba mbegu ya kahawa ya wa-Vietnam waliichukua hapa Tanzania mkoani Kagera, halafu mbegu ya korosho waliichukua Mtwara na mbegu ya samaki wanaotamba nao aina ya tilapia walichukua katika Ziwa Victoria,” anasema Waziri Mahiga.

Waziri Mahiga akizungumzia maendeleo katika mawasiliano anaitaja kampuni ya Viatel ambayo imepiga hatua kubwa ya mawasiliano duniani, Tanzania ikiendesha huduma zake kupitia mtandao wa mawasiliano wa Hallotel ambao ni maarufu zaidi katika maeneo ya vijijini kutokana na kutoa huduma za intaneti bure.

Vita ya Vietnam na Marekani 
Pengine jambo la haraka sana la kuwawezesha Watanzania kuifahamu Vietnam ni kuzungumzia vita ya Vietnam na Marekani, hasa kutokana na mabanda mengi yanayoonesha mikanda inayohusiana na vita jijini Dar es Salaam na katika miji mingi nchini kupenda zaidi kuonesha vita ya Vietnam na Marekani.

Chimbuko la vita ya Vietnam na Marekani, lilitokana na hatua ya nchi hiyo kugawanyika Kaskazini na Kusini mara baada ya Uhuru wake mwaka 1945, ambapo waasi wa Kusini walitaka kujitenga, hatua iliyosababisha serikali ya Kikomunisti kuamua kupigana ili kurejesha taifa moja.

Kutokana na kuzuka kwa vita hiyo ya wenyewe kwa wenyewe, Marekani iliamua kuingilia kati ili kuwasaidia waasi wa Vietnam Kusini wakijulikana zaidi kama Saigon, kabla ya kukumbana na kichapo kikali kutoka kwa Serikali ya Kikomunisti chini ya Jenerali maarufu Giap Nguyen huku askari wake 56,000 wakiuawa.

Waziri Mahiga alisema nidhamu, juhudi, maarifa na kutokubali kushindwa kama inavyoonesha katika mkanda huo wa vita, ndio chimbuko la mafanikio makubwa katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi hiyo.

“Tunajifunza mambo matatu makubwa kutoka Vietnam; Moja uwezo mkubwa wa kufanya kazi kwa bidii hata iwe katika mazingira magumu ikiwemo vita au amani. 

“Pili; ni watu wa utekelezaji na tatu ni uwezo wa kujibu swali; kwamba kama unataka kuendelea unahitaji nini, kwanza ni elimu ya ufundi, halafu miundombinu kama vile barabara, umeme, reli, maghala na mwisho mitaji ya kifedha, na hasa mapinduzi makubwa katika sekta ya benki ili kupata mikopo,” alisema Waziri Mahiga.

January Makamba Hatihati Kutumbuliwa Jipu Kwa Ufisadi......Mange Kimambi Aapa Kupeleka Ushahidi TAKUKURU

$
0
0
Sakata la Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba na Mdogo wake Mwamvita kudaiwa kupokea rushwa kutoka kwa raia wa Italia, Vincenzo Cozzolino ili wamsaidie kupata zabuni ya ujenzi limechukua sura mpya.

Sauti na jumbe mbalimbali zilizosambazwa na kuwekwa kwenye mtandao na mtu maarufu kwenye mitandao ya kijamii na mmiliki wa tovuti ya U-Turn, Mange Kimambi, raia wa Tanzania aishie Marekani, zinaonesha mazungumzo kati ya watatu hao, mwaka 2011. Jana, Mwamvita na Makamba walikiri kuwa sauti hizo ni za kweli.

Muitaliano huyo ambaye anadaiwa kumpa Mange Kimambe ushahidi wote wa mawasiliano kati yake na Ndugu hao, amejitokeza na kuwasafisha akidai kuwa hakuwahi kuwapa rushwa wala kuhusiana na January kibiashara.

Cozzolino ameandika ujumbe akidai kuwa ingawa yeye na Mwamvita walikuwa na uhusiano wa mapenzi mwaka 2011 na baadae kujiingiza katika biashara binafsi ambayo ilipelekea kugombana kwao, hawakumhusisha January kwa aina yoyote katika biashara yao.

“Sikuwahi kumuomba [January] kunisaidia katika biashara zangu. Sikuwahi kumpa fedha. Mara chache nilizokutana naye ilikuwa ni mazungumzo ya kawaida ya kijamii. Nilikuwa na uhusiano na Mwamvita. Uhusiano wetu ulikuwa bomba mwanzoni lakini ukawa na mwisho mbaya,” ameandika Cozzolino.

Awali, sauti ya January na mwandishi wa habari iliyosambazwa, January anasikika akieleza kuwa aliwahi kukutana mara moja Dubai na Muitaliano huyo na kwamba alitambulishwa kama mpenzi wa dada yake. 

Alisema baadae dada yake alimwambia wameanza kufanya biashara ya kahawa na Muitaliano huyo na baadae biashara hiyo kufa huku ikiwaacha katika mzozo. 

Kwa mujibu wa Kamamba, Muitaliano aliyekuwa ameweka nusu ya mtaji ambayo ni dola milioni 50, alianza kudai kiasi hicho cha fedha na sio vinginevyo. 

Alisema kuwa awali, muitaliano huyo alikuwa anajaribu kumshawishi Mwamvita amkutanishe na viongozi wakubwa wa serikali ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu.

Hata hivyo, Mange Kimambe ambaye ndiye anayeeleza kuwa na nyaraka zote za ushahidi aliokabidhiwa na Muitaliano huyo na kwamba hivi sasa Muitaliano amelipwa na kukubaliana kumsafisha Mbunge huyo wa Bumbuli.

Mange amesisitiza kuwa ana ushahidi wote wa January na dada yake kupokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara huyo na yuko tayari kuwakabidhi Takukuru.

Yes it is indeed the biggest punishment ever. . . Jamani sina ushirikiano wa Muitaliano anymore Ila Muitaliano alishanipa enough to take them down anyways. . . Niko tayari kuwapa Takukuru email hii nzima waone Enzo alichomwandikia Mwamvita kuhusu January Makamba na kumtishia kuanika! Mpaka Mwamvita amjibu Hivi......In short it's about January Accepting a huge amount of cash from Avery questionable character . . Sito publish hapa sabbau pia nitakuwa nawasidia wao ku over their tracks. Hata Kama wahusika wakidelete hizi email , serikali still ina uwezo wa kuomba records zooote za email hawa hawa wahusika wooooote. Hii email Ndo jamaa alikuwa anawatishia cha mwisho mwisho wampe pesa zake kabla hajaanika issue wakadhani anatania! Kesho yake ndo akaja kwangu. . . Ila dah binadamu wabaya sana, hamuwezi mkaamini mnajua Muitaliano Sasa Hivi eti ananiomba niache kuposti? Ananiambia niachane na issue And respect his decision. Imagine, now ananiomba niwaprotect Makambas especially January. Ananiambia kabisa leave January alone 😂😂😂😂😂😂... Yani ukisoma messages zake wakati kadhulimiwa alivyokuwa anatia huruma and now unaweza shangaa.. Eti just stop Na huna ruhusa ya ku publish vitu nilivyokutumia in private . Ila nime mjibu vizuri nime mwambia I'm glad nimekusaidia Sasa niache niwasaidie Watanzania. I swear next time kabla sijamsaidia Mtu nitawasainisha mikataba mpaka! But nilichoelewa Ni kwamba I think kawaambia Kuwa hakuna vitu vingine alivyonitumia Au alivyoniambia so Sasa wanavurugana. . . You guys know what? Hata Kama serikali ikiangalia pembeni but guess what 2020 is not far tunasubiria CCM watuambie eti January Makamba ndo mgombea wao waone Kama hatutompa nchi Halima Mdee!! 😂😂😂😂😂😂. . . Oh yeah just to add, ile Safari ya Dubai, hata Mwamvita pia alikuwepo. In short it's a family affair. Ja Ja Ja Ja.... . . Basi immediately baada ya kumalizana Na Muitaliano Mwamvita akaenda kuweka caption eti NEXT?
A photo posted by @mangekimambi_ on

Ofisi 5 za CUF Zachomwa Moto Zanzibar

$
0
0
HALI ya kisiasa visiwani Zanzibar, inazidi kuwa tete huku siasa za visasi, chuki na uhasama zikionekana kurejea kwa kasi.

Hali hiyo imejitokeza baada ya ofisi za matawi matano ya Chama cha Wananchi (CUF) zilizopo Pemba na moja  Unguja kuchomwa moto na watu wasiojulikana.

Matukio ya kuchomwa moto kwa ofisi hizo yamekuja siku mbili baada ya watu wasiojulikana kuchoma moto maskani ya CCM ya Sauti ya Kisonge iliyopo mjini Unguja.

Hata hivyo Jeshi la Polisi visiwani humo limetangaza kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini watu waliohusika na matukio hayo.

Uchomaji huo ulifanyika usiku wa kuamkia jana saa 8 usiku, ambapo watu hao walichoma moto na kuteketeza nyaraka za chama hicho.

Matawi yaliyochomwa moto ni Kilimahewa mjini Unguja Wilaya ya Magharibi, Mkanyageni, Kiwapwa, Kiuyu Minungwini, Wingwi na Kinowe yote ya Kisiwani Pemba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir, amethibitisha kutokeo kwa matukio hayo.

Amesema kutokana na hali hiyo tayari ameagiza askari wake kuanza uchunguzi wa tukio hilo haraka ili waliohusika watiwe nguvuni na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

“Ni kweli kuna hilo tukio ingawa kwa sasa nipo safari kuelekea Unguja na tayari nimeagiza kuanza kwa uchunguzi wa matukio haya ili wahusika waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

“…siwezi kusema kama matukio haya yana uhusiano wa masuala ya kisiasa ingawa huu ni uhalifu kama uhalifu mwingine,” alisema Kamanda Nassir.

Akizungumzia tukio hilo, Mbunge wa Wingwi, Juma Kombo Hamad (CUF), alilaani tukio hilo huku akiwatuhumu wafuasi wa CCM kuhusika nalo.

Alisema hatua ya CUF kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu imekuwa ikiwaumiza CCM.

“Haya mambo yapo wazi tumeumizwa vya kutosha lakini katika hilo mimi binafsi wala sifichi hapa kuna mkono wa CCM  na sisi hatutarudi nyuma tunaendelea na msimamo wa chama,” alisema Hamad.

Kauli ya Maalim Seif
Machi 4, mwaka huu, Akizungumza na wafuasi wake waliomtembelea nyumbani kwake, Katibu Mkuu wa CUF,  Maalim Seif Sharif Hamad, alisema yuko tayari kukamatwa kutokana na msimamo wake wa kutotambua uchaguzi wa marudio.

“Msidhani kuwa mtatupiga shavu la kulia tukawageuzia la kushoto. Kila mara tunaibiwa, tunapigwa, tunafanywa kila kitu. Tukisema kuwa watu wajilinde, inakuwa nongwa.

“…basi tunawaambia kuwa kuitwa polisi, kuwekwa ndani, kufunguliwa mashtaka ya bandia, hata kuteswa, hayo ni mambo yamekuwa yakitutokea tangu 1992 tumeshayazoea,” alisema Maalim Seif.

Alisema udhalilishwaji kama huo haujawahi kukirudisha nyuma chama chake, zaidi ya kukiongezea umashuhuri na ufuasi mkubwa visiwani Zanzibar, huku akilituhumu Jeshi la Polisi kwa kuwa ‘tawi la CCM’ ambalo litakuwa dhamana wa machafuko yoyote yatakayotokea.

Katika hatua nyengine, Maalim Seif ambaye alikuwa mgombea urais katika Uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana  alirudia msimamo wa chama chake wa kutoshiriki kile alichodai uchaguzi wa marudio ulioitishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha, Machi 20, mwaka huu.

Alisema yeye alishashiriki uchaguzi na kushinda na hahusiki kabisa na uchaguzi mwengine. “Ninamwambia Jecha kuwa uchaguzi huo ni wenu peke yenu,” alisema Maalim Seif.

Rais Magufuli Amuapisha Balozi Eng. John William Kijazi Kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Eng. John William Herbert Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​ 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Hafla ya kuapishwa Balozi Kijazi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu wakuu na Naibu Katibu Wakuu. 

Balozi Kijazi ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India, anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine. 

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameagana na Mwakilishi wa Shirika Ia Umoja wa Mataifa Ia kuhudumia wakimbizi hapa nchini (UNHCR) anayemaliza muda wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amemshukuru kwa kazi kubwa ya kuhudumia wakimbizi kwa kipindi chote alichokuwepo hapa nchini. 

Kwa upande wake Bi. Joyce Mends-Cole amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri inayofanywa na Tanzania kuzisaidia nchi zenye matatizo, hususani migogoro ya kisiasa ambayo husababisha watu wake kuwa wakimbizi. 

Pia amepongeza kuteuliwa kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kusaidia usuluhishi wa mgogoro wa Burundi ambao umesababisha idadi kubwa ya wakimbizi kukimbilia Tanzania.

Hata hivyo amesema idadi ya wa kimbizi wanao kimbilia Tanzania imepungua kutoka wakimbizi 3,000 waliokuwa wakiingia hapa nchini kwa wiki, wakati Mgogoro wa Burundi ulipoanza hadi kufikia wakimbizi takribani 1,000 wanaingia hapa nchini kwa wiki hivi sasa. 

Aidha, Bi. Joyce Mends-Cole amewashukuru watanzania kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi cha miaka mitatu aliyofanya kazi hapa nchini, na ameahidi kuwa Balozi wa kuitangaza vyema Tanzania. 
 
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam 07 Machi, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi wa kwanza kushoto na Wa mwisho kulia ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja na viongozi Wakuu wa Ulinzi na Usalama nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

Moto Wateketeza Mabweni Mawili katika Shule ya Sekondari ya Iyunga jijini Mbeya Mchana huu

$
0
0

Mabweni mengine  mawili  ya  shule  ya  Sekondari  Iyunga  iliyoko  jijini  Mbeya  yameteketea  kwa  moto  mchana  huu.

Hii  ni mara ya pili sasa moto kuzuka katika shule hiyo .Wiki kadhaa zilizopita moto ulizuka na kuteketeza bweni moja la Mkwawa(‪Pichani‬) huku sababu zikielezwa ni hitilafu  ya  umeme  kutokana  na  uchakavu  wa  miundo  mbinu  shuleni  hapo.

Jeshi  la  Zimamoto  liko  eneo  la  tukio  kuukabili  moto  huo

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images