Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Arejeshwa Nchini

$
0
0
Balozi  Radhia Msuya
Rais Dk. John Magufuli, amemrudisha nyumbani aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, pamoja na watumishi wengine watano, baada ya muda wao kumalizika.

Hii ni mara ya pili kwa Rais Dk. Magufuli kuwarejesha nyumbani Mabalozi wa Tanzania walioko nchi za nje baada ya muda wao wa mkataba kumalizika.

Ikumbukwe kuwa Januari 25, mwaka huu, Rais Magufuli alimrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Peter Kallaghe, kuja kufanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dk. James Msekela na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Dk. Batilda Buriani, baada ya mikataba yao kumalizika.

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga, amesema kurudhishwa nyumbani kwa Balozi Msuya, ni jambo la kawaida kwa sababu bado kazi ya kuwarudisha nyumbani Mabalozi waliomaliza mikataba yao linaendelea.

Alisema kwa sasa serikali inachofanya ni kuwarudisha nyumbani Mabalozi ambao mikataba yao imemalizika na kuwapeleka watumishi wengine wakapate uzoefu nje ya nchi.

Alisema kuna makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni watumishi wa idara ambao muda wao wa miaka mitano umemalizika ambao wanarudishwa nyumbani ama kuhamishiwa kituo kingine cha kazi.

Alisema kundi la pili ni la Mabalozi ambao siyo watumishi wa wizara, lakini waliteuliwa na Rais kwa mkataba, hivyo mikataba yao ikimalizika Rais mwenyewe ndiye anayeamua kama ni kuwaongezea au kusitisha na kurudi nyumbani.

Dk. Mahiga alitaja kundi la tatu kuwa ni Mabalozi ambao muda wao wa kukaa nje umemalizika au umri wao wa kustaafu umefika, lakini mikataba yao bado haijamalizika, hivyo Rais anaamua kuwarudisha nchini ili wapumzike na wengine wakashike nafasi zao.

Alisema kuna Mabalozi ambao mikataba yao ya kufanya kazi nje ya nchi ni miaka mitano, lakini wamekaa zaidi ya miaka 10, hivyo serikali iko katika mchakato wa kuwarudisha nyumbani.

Waziri Mahiga alisema kuna vituo zaidi ya 35 ambavyo vinatakiwa kuwa na Mabalozi, hivyo serikali itahakikisha inawarudisha nyumbani mabalozi waliomaliza muda wao wa kazi na kupangiwa majukumu mengine.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akabidhiwa zana ya ‘Kisukuma’ Kukabili MAJIPU......Pia Kapewa Jina Jipya ambalo ni Masanja Mkusanyaji

$
0
0

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amepewa jina jipya la Kisukuma na kukabidhiwa zana nyingine muhimu katika vita ya kupambana na ufisadi nchini maarufu kwa jina la kutumbua majipu.

Kuanzia juzi, Waziri Mkuu Majaliwa atakuwa akifahamika kwa jina lingine la Masanja, alilopewa na Wazee wa Kisukuma wa Lamadi wilayani Busega katika mkoa wa Simiyu. 

Kabla ya kuwahutubia maelfu ya wakazi wa Lamadi juzi jioni, wazee hao walimvisha Waziri Mkuu vazi la kijadi la Kisukuma akiwa katika kigoda, wakamkabidhi usinga, ng’ombe wawili na mkuki ambao walimueleza kuwa kazi yake ni kuendeleza vita ya ufisadi kwa kuutumia kutumbua majipu.

“Tunakukabidhi usinga na huu mkuki utumike kutumbua majipu kwa sababu kazi hii unaifanya vizuri hadi sasa, kwa hiyo uendelee kutumbua majipu. Na kwa kuanzia sasa, tunakupa jina la kwetu, kwa sababu wewe ni kijana wetu, utaitwa Masanja,” alisema Mchele Malale kwa niaba ya wazee wenzake.

Kwa mujibu wa wenyeji, jina la Masanja lina maana ya kuingia kokote, hali inayomaanisha kuwa Waziri Mkuu Majaliwa aendelee kutumbua majipu kila mahali.

Alipoanza kuhutubia, Waziri Mkuu alikiri kuwa amepata mapokezi makubwa kwa wananchi wa Lamadi, na zaidi, makubwa kuliko sehemu nyingi alizokwenda tangu ashike wadhifa wake huo.

“Kwa kweli nimefurahishwa na mapokezi yenu hapa…tangu nilipotoka Mwanza hadi kufika kwenu (Busega) mapokezi yamekuwa mazuri, na hapa Lamadi mmetisha. Mmenitia faraja sana,” alisema Waziri Mkuu na kuongeza: 

“Lakini nimefurahi kwa zawadi mlizonipa na pia jina jipya la Masanja.Nimeandika pale kwenye diary (shajala) yangu. Mmenipa pia mkuki, mmesema nitumie kama sindano kuendeleza ile kazi,” alisema Waziri Mkuu na kushangiliwa na maelfu ya wakazi wa Lamadi.

Akiwa Bariadi jana, Waziri Mkuu alisema jina lake sasa ni Masanja Mkusanyaji, na kwamba ataendelea kukabiliana na wakwepa kodi na mafisadi ili Watanzania wapate huduma stahiki.

Taarifa Fupi Kuhusu Ziara Ya Rais Wa Vietnam Nchini Tanzania Tarehe 9-10 Machi 2016

$
0
0
Utangulizi
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Mheshimiwa Truong Tan Sang anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini tarehe 9 Machi 2016.  

Madhumuni ya  ziara hiyo ni kukuza uhusiano baina ya Vietnam na Tanzania mbao umedumu kwa zaidi ya miaka hamsini tangu kuanzishwa kwake pamoja ‎Kufungua maeneo mapya ya Ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Vietnam. 

Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo Barani Afrika tangu aingie madarakani mwaka 2011, ambapo nchi nyingine anayotarajiwa kutembelea ni Mozambique. 

Rais Truong anatarajiwa kufuatana na mke wake Bi Mai Thi Hahn, mawaziri 4 wanaoshughulika na sekta za  Kilimo, Mawasiliano Uwekezaji, Afya,Viwanda na Biashara.  Aidha mgeni huyo atafuatana na ujumbe wa wafanyabiashara 30 kutoka Vietnam. 

Shughuli za msingi zitakazofanyika kwenye ziara
Wakati wa ziara hiyo Rais Truong Tang San atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar-es-Salaam.
 
Aidha, Rais Truong pia atapata fursa ya kutembelea eneo la EPZ la Ubungo kuangalia viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa za kuuza nje
 
Baada ya kutembelea EPZA Rais Truong atahudhuria mkutano wa biashara na uwekezaji katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na taasisi za umma na sekta binafsi kutoka Tanzania na Vietnam.
 
Rais Truong atamaliza ratiba yake kwa kuhudhuria dhifa ya Taifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.John Pombe Joseph Magufuli.

Wasifu wa Rais wa Vietnam‎
M‎heshimiwa Truong Tan Sang amezaliwa tarehe 21 January 1949 katika Jimbo la Long An nchini Vietnam. Amepata Elimu ya Juu kutoka taasisi ya national Academy of Public Administration ya Vietnam ambako alipata Shahada ya kwanza ya Sanaa na Sheria.
 
Kutokea mwaka 1966 hadi 1996 Mheshimiwa Truong ameshika nafasi mbalimbali za utendaji  katika Chama Tawala cha kikomunisti cha Vietnam.
 
Mwaka 1996 Mhe Truong alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Tawala na Katibu wa Chama hicho katika Jimbo la Ho Chi minh hadi mwaka 2000 ambapo aliachia wadhifa wa katibu Mkuu wa Jimbo na kuendelea na nafasi ya ujumbe wa Kamati kuu ya Chama tawala hadi tarehe 25 Julai 2011 alipochaguliwa na Bunge la Vietnam kuwa Rais wa Vietnam.
 
Mhe Truong amemuoa Bi mai Thi Hanh  na wamejaaliwa mtoto mmoja.

Taarifa Muhimu Kuhusu Vietnam‎

Historia fupi ya Vietnam
Vietnam ilifanya mapinduzi tarehe 14 Agosti 1945 na hatimaye kupata uhuru tarehe 2 Septemba 1945 ikijulikana kwa jina la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Vietnam. 

Pamoja na kupata uhuru nchi hiyo iliendelea kuwa na migongano baina ya Vietnam ya Kaskazini na Kusini iliyopelekea vita iliyodumu kwa muda mrefu na kuhusisha mataifa ya nje. 
 
Kufuatia kumalizika kwa vita, Vietnam ya Kaskazini na Kusini ziliungana tena na kuunda Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam tarehe 2 Julai 1976. 

Nchi hiyo yenye kilomita za mraba 329,560 iliyopo kusini mashariki mwa Asia ina watu milioni 91.7 na inaongozwa na Chama cha Kikomunisti cha Vietnam.

Mafanikio ya Uchumi ya Vietnam
‎Vietnam ni moja ya nchi zilizopiga hatua kubwa ya maendeleo barani Asia.

Mwaka 1986 Serikali ya Vietnam ilianzisha mageuzi makubwa ya uchumi yaliyopelekea kuitoa nchi hiyo kwenye kundi la nchi masikini yenye kipato cha Dola za Kimarekani 100 kwa kila mtu hadi kufikia kuwa nchi yenye uchumi wa kati yenye kipato cha Dola za kimarekani 2000 kwa kila mtu mwaka 2014. Katika mageuzi hayo,Vietnam imefanikiwa kupunguza umasikini wa wananchi wake kwa asilimia 50.

Mafanikio katika Sekta ya Kilimo
Sifa kuu ya Vietnam ni uthubutu na uwezo wa kusimamia mipango yake. Mfano mwaka 1980 nchi hiyo iliamua kuingia kwenye uzalishaji mkubwa wa kahawa. 

Ndani ya miaka 10 iliweza kufikia uzalishaji wa tani 300,000 kwa mwaka na hatimaye kuwa nchi inayoongoza ulimwenguni katika uzalishaji na uuzaji wa kahawa aina ya Robuster. 

Vilevile miaka ya 1990, Vietnam ilikuwa ikiagiza mchele kutoka nje, kufuatia hatua madhubuti walizochukua mwaka 2004 ilishika nafasi ya pili duniani katika uzalishaji wa mchele kwa kuwa na misimu mitatu ya mavuno.
 
Hivi sasa Vietnam imejiwekea malengo ya kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa sukari duniani ambapo mwaka 2015 uzalishaji wake umefikia tani milioni 2 kwa mwaka.‎ 

Mbali na mazao hayo, Vietnam inaongoza ulimwenguni kwa kuuza korosho na pilipili manga. Vilevile,Vietnam ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwenye kilimo cha muhogo na mpira. 
  ‎
Mafanikio makubwa ambayo Vietnam imeyapata katika kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo, yamekuwa chachu ya ukuaji wa sekta ya viwanda ambayo kwa sasa ndio imeshika hatamu ya uchumi wa Vietnam‎.
 
Mkakati wa Mageuzi ya Kijamii na Kiuchum 2011-2020
Aidha, Vietnam inatekeleza mkakati wake wa kuwezesha mageuzi ya kijamii na kiuchumi wa mwaka  2011-2020 ambao umejikita kwenye kuwapatia wananchi elimu na stadi za ufundi‎ kwa ajili ya kufanya kazi kwenye viwanda vinavyotumia teknolojia ya kisasa na ubunifu; kuboresha taasisi zinazoshughulika na masoko; na kuendelea na ujenzi wa miundombinu.
 
Mkakati huo unaendana na utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa nchi hiyo ambao kwa sasa umelenga kufanya mageuzi makubwa katika taasisi za kibenki ili kuwezesha wananchi kupata mitaji ya kufanya shughuli za uchumi na maendeleo; na mageuzi ya makapuni ya biashara ya Serikali ili yaweze kushindana katika uchumi wa soko ndani na nje ya nchi pasipo kutegemea ruzuku kutoka Serikalini.‎
 
Ni dhahiri kwamba yapo mambo ambayo Tanzania inaweza kujifunza kutoka Vietnam katika safari yake ya kuwa nchi ya uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025. Tanzania inayo nafasi kubwa ya kuongeza uzalishaji katika mazao ya miwa,mpunga na uvuvi kwa kupitia ushirikiano na Vietnam.

Mahusiano ya Vietnam na Tanzania‎
Mahusiano ya Tanzania na Vietnam yaliyojengwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kiongozi wa Vietnam Ho Chi Minh mwaka 1960 na kupelekea kuanzishwa rasmi kwa mahusiano ya kidiplomasia mwaka 1965. Kwa muda mrefu mahusiano hayo yalikuwa ya kisiasa zaidi ambapo Tanzania iliunga mkono harakati za Vietnam za kupinga uwepo wa majeshi ya kigeni kwenye ardhi yake.

Ziara za Kukuza Mahusiano za Viongozi Wakuu
Aidha katika kipindi cha miaka 50 ya mahusiano ya kidiplomasia baina ya Vietnam na Tanzania, viongozi wa kitaifa wa nchi hizi mbili wamefanya ziara za kudumisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Tarehe 25 Septemba 1973, Rais wa Vietnam Mheshimiwa Nguyen Huu Tho alifanya ziara nchini Tanzania. 
 
Kwa upande wa Tanzania, viongozi waliofanya ziara nchini Vietnam ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa (2004); Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (2014), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohamed Shein (2012); Mawaziri Wakuu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano‎ Mhe.Edward Lowassa (2006); na Mhe. Mizengo Kayanza Pinda (2010).

Mikataba ya Mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam
Katika jitihada za kuimarisha mahusiano, mwaka 2001 Tanzania na Vietnam zilisaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kuichumi na ufundi‎.  Mkataba huo uliainisha maeneo ya ushirikiano yafuatayo:
  1. Kubadilishana uzoefu katika sekta ya kilimo na maendeleo vijijini;
  2. Kubadilishana uzoefu katika matumizi ya sayansi na teknolojia katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, uvuvi na misitu;
  3. Kupeana taarifa za fursa za masoko ya bidhaa za kilimo
  4. Vietnam kuipata Tanzania utaalam na teknolojia ya uvunaji na utunzaji wa maji
  5. Mwaka 2014 Tanzania na Vietnam zilisaini Mkataba wa ushirikiano katika sekta ya mawasiliano ambapo kupitia mkataba huo kampuni ya Vietel  inayomilikiwa na Jeshi la Vietnam imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya mawasiliano nchini na kuzalisha ajira za moja kwa moja kwa watanzania 1600 na fursa za kujiajiri kwa watanzania 20,000. Vilevile,kampuni hiyo kupitia mkataba uliosainiwa,itatoa huduma za internet bure kwenye mashule na mahospitali ya Serikali vijijini.

-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dar es Salaam
03 Machi, 2016

Mizengo Pinda Awataka Watumishi wa Umma Wazingatie Maadili ili Wasitumbuliwe MAJIPU

$
0
0

Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Mizengo Pinda ametoa wito kwa watumishi wa Umma kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia sheria na taratibu ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya kuwahudimia wananchi na kukabiliana na umasikini.

Akizungumza wakati akifunga mkutano wa kikao cha ushauri cha mkoa wa Katavi(RCC), Pinda  amezishauri halmashauri kufuata taratibu za manunuzi na matumizi ya pesa kwa maslahi ya Umma ili kupiga hatua katika maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja.

Mhe. Pinda amesema licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa umma katika utendaji wao ila amewataka watanzania kujenga tabia ya kutokukubali kuwajibishwa kutokana na ukiukwaji wa utumishi wa Umma.

Aidha waziri Mkuu huyo Mstaafu amewataka viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Katavi kuumunga mkono na kumuombea rais Magufuli katika jitihada zake za kupambana na ufisadi ili kuleta maendeleo ambayo yalihodhiwa na watu wachache.

Mhe. Pinda ameongeza kuwa kwa mwendo wa Rais Magufuli anaamini kuwa ndani ya kipindi chake cha miaka kumi kama akifanikiwa kumaliza vipindi vyote basi kutokana na kasi yake Tanzania itakua imepiga hatua kubwa za kiuchumi na kuwa ni moja kati ya nchi zenye uchumi wa kati.

Meneja wa Yamoto Band Said Fella Ajipanga Kugombea Urais wa Tanzania Mwaka 2040

$
0
0

Meneja wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family Said Fella ‘Mkubwa Fella’ anajipanga kuogombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2040 akiwa na umri wa miaka 60.

Fella ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kilungule wilayani Temeke jijini Dar es salaam (CCM), amekiambia kipindi cha Enewz cha East Africa Television Jumatano hii kuwa  yeye ni mtu makini,  hivyo hawezi kushindwa kuiongoza nchi.

“Kama Mungu akinipa uhai mwaka huo nitakuwa na miaka 60 na nitakuwa nina uelewa wa kutosha na uwezo wa kuweza kuwaongoza watanzania kwa kujali maslahi yao ili kuwawezesha kujikwamua na umaskini” Alisema Fella.

Aidha Fella ametamba kuwa yeye anafanya kazi kwa vitendo ndiyo maana wananchi wa kata yake walimuamini na katika madiwani wote wa Dar es salaam yeye ndiye diwani pekee aliyeshinda kwa asilimia 89% katika uchaguzi mkuu wa October 2015.

Waziri Mkuu Asema Mtu Akiharibu Kazi Asitarajie Uhamisho.

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa(Pichani) amesema watumishi wa umma wako huru kuhamia kokote wapendako lakini wahakikishe wanaenda huko wakiwa safi na kamwe mtu asiharibu kazi kazi akitarajia kuwa atahamishiwa sehemu nyingine.

"Serikali hii haina utumishi kwa mtu aliyeharibu kazi,usije ukaharibu hapa Itilima ukadhani utaenda Bunda kuendelea na kazi. Serikali ya awamu hii haina nafasi na  watumishi wa aina hiyo," amesema.

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Ijumaa, Machi 4, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Itilima kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambao ameuzindua leo hii wilayani Itilima, mkoani Simiyu.

"Watumishi wenzangu huu ni wakati wa kubadilika na kuona mwelekeo wa Serikali hii ya awamu ya tano ukoje. Jukumu letu ni kuwatumikia Watanzania wote bila kujali itikadi zao, rangi wala dini zao," alisisitiza.

Waziri Mkuu aliwahakikishia watumishi hao kwamba Serikali inatambua changamoto walizonazo kutokana na upya wa wilaya hiyo na mkoa huo na akawaahidi kuwa itaboresha mazingira yenu. 

"Msiwaadhibu wananchi kwa kisingizio cha mazingira magumu ya kazi zenu, tunajua mnayo madai ya nauli, posho za mafunzo, kupandishwa madaraja na malimbikizo ya likizo," alisema huku akishangiliwa.

Alisema Serikali itayalipa madeni hayo japo haitamaliza yote kwa wakati mmoja ila ana uhakika wa kukamilisha walau kwa asilimia 80.

Mapema, akitoa taarifa ya wilaya hiyo, Mkuu wa wilaya hiyo, Bibi Georgina Bundala alisema wilaya hiyo iliyoanzishwa Machi 2012 na kupata Halmashauri Julai 2013 haina kituo cha polisi cha wilaya, haina gereza, Ofisi za TAKUKURU, mahakama ya wilaya wala benki.

Alisema wilaya hiyo haina hospitali ya wilaya ila akabainisha kuwa wamekwishatenga eneo la ekari 30 kwa ajili ya ujenzi huo.

 "Pia tumekwishapima viwanja 123 na eneo la kujenga  taasisi lenye ekari 143.8 limefanyiwa uthamini na fidia kukamilika," alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, MACHI 4, 2016.

Waziri Maghembe Awasimamisha Kazi Watumishi Watano wa Hifadhi ya Ngorongoro....15 Wahamishiwa Wizarani

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii  Mh.Profesa Jumanne Maghembe amewasimamisha kazi watumishi watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuwahamisha wengine 15 kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha na ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa Umma.
 
Mh.waziri Maghembe amechukua hatua hiyo baada ya  kutembelea na kukutana na wafanyakazi wa mamlaka hiyo na amesema hatua zingine zitafuata kwa watumishi hao ambao wote watano ni wa idara ya uhasibu.
Kuhusu  watumishi wanaohamishwa ambao ni wa idara mbalimbali ikiwemo uhandisi,utalii na ikolojia Mh.Prof.Maghembe amesema hatua hiyo inalenga kutoa nafasi ya kuendelea  kufanyika kwa uchunguzi zaidi juu ya tuhuma mbali mbali zinazowakabili.
Mhifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro Bw.Fredy Manongi pamoja na kukiri kuwa mamlaka inakabiliwa na changamoto mbalimbali amesema kwa sasa tatizo kubwa ni ujangili unaofanyika katika maeneo ya mipakani japo amesema wanaendelea kuzikabili. 
 
Hii ni ziara ya kwanza ya Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe katika mamlaka hiyo ambayo amesema ni mwendelezo wa utekelezaji wa azma ya serikali ya kuimarisha uwajibikaji,ukusanyaji wa mapato na kuimarisha  shughuli za uhifadhi.

Jamii Forums Wafungua Kesi Ya Kikatiba Mahakamani Kupinga Baadhi ya Vifungu vya Sheria ya Makosa ya Mtandao.

$
0
0

Septemba Mosi, 2015 Tanzania ilianza kutumia sheria ya Makosa ya Mtandao licha ya kuwepo kwa mvutano na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaotumia mitandao hiyo kwamba hawakushirikishwa kuijadili na kuichambua.

Leo March 4 2016 Kampuni ya Jamii Media inayoendesha JamiiForums.com na Fikrapevu.com imejitosa kutetea kile inachokiita ni kunyimwa haki ya wananchi kupata taarifa na kulindwa kwa uhuru wao wa maoni na kujieleza unaolindwa kwa mujibu wa katiba ya Nchi.

Jamii Media wameamua kufungua shauri Mahakama kuu kutaka kifungu cha 32 na 38 cha sheria ya Makosa ya Mtandao viangaliwe upya. Akizungumza kwa niaba ya Jamii Media,wakili Shukuru Mlwafu ameeleza…

"Baadhi ya vifungu vya sheria ya kimtandao vinakiuka masharti ambayo yamewekwa na katiba hasahasa vinaingilia haki ya faragha ambayo wateja wetu wanayo kikatiba.

"Njia pekee ni kufungua shauri la kikatiba kupinga vifungu hivyo na kuiomba mahakama ibatilishe na itamke kuwa vifungu hivyo ni batili kwa kuwa vinaenda kinyume na ibara 16 na 18 ya katiba" Amesema Shukuru Mlwafu

Hatua hiyo ya kufungua shauri Mahakamani imekuja baada ya kuwepo  na shinikizo kutoka Jeshi la polisi kuwataka Jamii Forum kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Maxence Melo amesema..

"Kuanzia uchaguzi october 2015 kumekuwa na barua kadha wa kadha zinazotaka kupata taarifa za siri za wanachama wa mtandao wa  jamii forum kitu ambacho tunahisi hata mitandao mingine ya kijamii wanafanyiwa na kumekuwa na mashinikizo kadha wakadha wakitaka tutoe IP Address za wateja, majina halisi na hata maeneo waliopo.Sasa tunaona hii itapekea kuvunjwa kwa  haki ya watumiaji wa Jamii forum":-Amesema Maxence Melo


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 5

Madiwani wa UKAWA Wavamia Ofisi ya Halmashauri ya Jiji La Dar Wakitaka Kuelezwa ni Lini Uchaguzi wa Meya Utafanyika

$
0
0

Zaidi ya madiwani 20 wanaotokana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), jana walivamia ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kumshinikiza Kaimu Mkurugenzi wake, Sarah Yohana kuitisha Baraza la madiwani kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa meya na naibu wake.

Madiwani hao waliovamia ofisi hiyo jana, walisema kikao hicho kinatakiwa kuitishwa ndani ya siku saba kikiwa na ajenda moja ambayo ni uchaguzi wa meya na naibu wake, ambao umekwama mara kadhaa kwa kile walichodai kuwa ni hila na hujuma.

Uchaguzi huo umeahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali, Januari 23 uliahirishwa kutokana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene kutoa muda kwa mameya wa manispaa zinazounda Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam; Kinondoni, Temeke na Ilala kuandaa mfumo bora wa kuwapata wajumbe watatu watakaounda Baraza la Jiji.

Februari 8, uliahirishwa kutokana na kubainika kwa nyongeza ya majina 14 yaliyopenyezwa kutoka halmashauri za Kinondoni na Ilala ambao hawakustahili kushiriki kikao hicho, pia Februari 27 uliahirishwa kutokana na zuio feki la mahakama.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana baada ya kukaa zaidi ya saa tatu bila kuonana na Yohana, madiwani hao na wabunge walisema wamechoshwa na uongozi wa jiji kuwahadaa kama watoto wadogo. 

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alisema wamechoka kupigwa danadana na kwamba wanachohitaji ni uchaguzi wa Meya wa Dar es Salaam kufanyika ndani ya siku saba siyo vinginevyo.

“Tumekaa zaidi ya saa tatu wametwambia Yohana hayupo, sasa akija mfikishieni taarifa kuwa Ukawa hatuna maelezo na Jumatatu tutatia timu tena hapa ofisini kwake,” alisema Mdee akimpa maagizo Ofisa Utawala wa Dar es Salaam, Iman Kasagara.

“Narudi tena, mfikishieni salamu, Jumatatu hatutaki kusikia longolongo za aina yoyote kutoka kwake. Tunataka majibu ya kueleweka vinginevyo hatutamuelewa,” alisema Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha).

Kasagara aliahidi kufikisha ujumbe huo kwa mhusika ambaye ilidaiwa alikuwa nje ya ofisi kikazi.

Mwenyekiti wa Madiwani wa Ukawa Dar es Salaam, Manase Mjema alisema uvumilivu umewashinda kutokana na figufigisu zinazofanywa na Jiji la Dar es Salaam kuhusu uchaguzi huo.

Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara alisema ajenda kuu ya Ukawa ni uchaguzi wa meya na wameacha shughuli zote hadi suala hilo lipatiwe ufumbuzi.

“Sasa hivi wakurugenzi akiwamo wa Dar es Salaam, wamepeleka bajeti zao hazina bila kushirikiana na meya kwa sababu hajapatikana, hivi hapo kuna maendeleo kweli?” alihoji Waitara.

“Kimsingi utaratibu wa kisheria ulishapita, sasa tunaelekea siku 90 bila meya tumechoka na hali hii,” alisema Waitara.

Rais Magufuli Ampongeza Francis Cheka kwa Kutwaa ubingwa wa Mabara wa Uzito wa Super-Middle

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amempongeza bondia Francis “SMG” Cheka kwa kutwaa ubingwa wa Mabara wa uzito wa Super-Middle wa chama cha WBF baada ya kumtwanga kwa pointi bondia Mserbia, Geard Ajetovic.

Cheka alimchapa Ajetovic kwa ushindi wa majaji wote wa tatu katika pambano gumu lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club.

Akitoa pongezi hizo jana, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema kuwa Rais amefuraishwa sana na ushindi wa Cheka ambao umeipa heshima nchi katika medani ya michezo ndani na nje ya mipaka yake.

Waziri Nnauye alisema kuwa serikali imeweka utaratibu wa kuwapongeza wanamichezo wanaofanya vyema kimataifa ili kuleta hamasa kwa wengine na wale wanoafanya vizuri kuongeza bidii.

“Cheka umefanya mambo makubwa sana, umeiletea sifa Tanzania na Rais amefuraishwa sana, naomba kuongeza bidii na wengine kufuata nyayo zako, nimefurahi kusikia kuwa mdogo wako, Cosmas naye ameshinda ubingwa wa Afrika, nampongeza sana,” alisema Nnauye.

Katika hafla hiyo, Serikali ilimpa cheti cha pongezi Francis Cheka na kumtaka kuzidi kuitangaza nchi kupitia mchezo huo ambao ni wa kwanza katika historia ya Tanzania kuleta heshima. “Serikali inaahidi kusaidia mchezo na mabondia ili kufikia maendeleo ya juu kabisa,” alisema.

Akizungumza katika hafla hiyo, Cheka aliipongeza serikali na kutambua mchango wake katika kuleta sifa ya nchi hii na kuahidi kuleta mikanda mingi ya ubingwa wa dunia.

“Nimefurahi kutambuliwa na serikali, nimepata hamasa kubwa sana, naahidi kufanya mambo makubwa katika mchezo huu,” alisema.
 
Mkurugenzi wa Advanced Security, Juma Ndambile ambaye ni meneja wa Cheka alisema kuwa wamefarijika sana kupata pongezi za serikali na kuahidi kuandaa mapambano mengi ya Cheka kwa mabondia wan je ya chi katika mapambano ya ubingwa wa Dunia.

Mkuu Wa Majeshi Aongoza Kuwaaga Maofisa Majenerali 16 Wa Jwtz Waliostaafu

$
0
0
MKUU wa Majeshi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange amewaongoza wanajeshi mbalimbali kuwaaga Majenerali 16 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambao wamemaliza muda wa utumishi wao.

Sherehe hizo zilifanyika Uwanja wa Kambi ya Jeshi wa Twalipo, Mgulani jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:30 mchana. Sherehe hizo ziliongozwa na bendi ya jeshi na gwaride maalumu.

Miongoni mwa waliomaliza muda wao ni Meja Jenerali Samuel Ndomba ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na hadi anastaafu alikuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ.

Wengine ni Luteni Jenerali Paul Mella ambaye alikuwa Kamanda wa Majeshi ya Kulinda Amani ya Darfur, Sudan na Brigedia Jenerali Harold Mziray ambaye alikuwa Mkuu wa Shule ya Infantria, Arusha.

Majenerali wengine walioagwa ni Brigedia Jenerali Martin Mwankanye aliyekuwa Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa jeshini, Brigedia Jenerali John Chacha aliyekuwa Kamanda wa Brigedi ya Tembo na Brigedia Jenerali Ezra Ngingwango aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Ndege na Usafirishaji jeshini.

Brigedia Jenerali Mrisho Abdallah aliyekuwa Mratibu Miradi ya Maendeleo jeshini naye ameagwa kama ilivyo kwa Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga aliyekuwa Mkuu, Tawi la Ukaguzi jeshini, Brigedia Augustino Gailanga aliyekuwa Mkuu wa Tawi Jeshi la Akiba, Brigedia Jenerali Luhindi Msangi aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Tiba Lugalo, Dar es Salaam na Meja Jenerali Raphael Muhuga wa JKT.

Wengine ni Meja Jenerali Charles Muzanila aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Mzinga Morogoro, Meja Jenerali Ezekiel Kyunga aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo Duluti mkoani Arusha, Meja Jenerali Joseph Kapwani aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Anga, Meja Jenerali Vincent Mritaba aliyekuwa Mkuu wa Utumishi jeshini na Meja Jenerali Salum Kijuu, Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu.
Brigedia Jenerali mstaafu, Msangi (kulia mbele), akikagua gwaride maalumu waliloandaliwa maofisa hao wastafu wakati wakiagwa rasmi baada ya kumaliza utumishi wao jeshini.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), mstaafu Meja Jenerali, Raphael Muhuga, akikagua gwaride hilo.

Mkuu wa Majeshi, Jenerali, Davis Mwamunyange (kushoto), akisalimiana na kumpongeza Mkuu wa Vikosi vya Kulinda Amani Umoja wa Mataifa, Luteni Jenerali mstaafu, Paul Ignas Meela katika hafla hiyo.

Bomu Lalipuka Maskani ya CCM Zanzibar

$
0
0
Kitu kinachosadikika kuwa bomu kimeripuka usiku wa kuamkia jana eneo la Michenzani mjini Unguja, eneo linalojulikana kama maskani maarufu ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mlipuko huo umezua taharuki na hofu kwa wananchi wa eneo hilo hususan wanachama wa CCM ambao hukutana kwa wingi eneo hilo na kujadili masuala mbalimbali ya chama chao kuelekea uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20 mwaka huu.

Naibu Katibu Mku wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alilaani tukio hilo na kulielezea kuwa  liliandaliwa makusudi kwa lengo la kuwavunja moyo wanachama wa chama hicho.

“Hili sio tukio la kwanza wala la pili katika eneo hili ambalo wanachama wetu walio msitari wa mbele wako wengi sana kwa kushirikiana na wanachama wengine. 

"Hili ni tukio ambalo unaweza kusema limeandaliwa kwa makusudi na watu wenye dhamira ya kuwavunja moyo wanachama wetu na wapenzi wa CCM,” Vuai aliwaambia waandishi wa habari.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibu, Mkadam Khamis Mkadam alieleza kuwa Jeshi hilo liliwasili katika eneo hilo usiku huo na kuimarisha ulinzi hadi asubuhi.

Kamanda Mkadam alisema kuwa walichukua vipande vya mlipuko huo na kuvipeleka sehemu husika kwa ajili ya kuchunguza kubaini aina ya mlipuko huo na vifaa vilivyotumika

Jinsi ya Kuandaa na Kutayarisha Dawa Lishe ya Kunenepesha,Kurutubisha na Kuongeza Mwili

$
0
0

Dawa-lishe  ya  kuongeza, kurutubisha  na  kunenepesha  mwili, ni  dawa  maalumu  kwa  watu  wenye  uzito  wa  chini  (  Under weight ) ambao  wanataka  kuongeza  mwili  na  uzito.


Dawa  hii  huwasaidia  watu  ambao  miili  yao  imedhoofu  kutokana  na  sababu  mbalimbali  kama  vile  kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali.

Na  kwa  wale  watu  wembamba  ambao  wanataka  kuongeza  miili  yao, dawa  hii  huwasaidia  vizuri  sana.

FAHAMU  JINSI NA  NAMNA  YA  KUANDAA NA  KUTAYARISHA   DAWA-LISHE  MAALUMU   YA  KUONGEZA, KURUTUBISHA  NA  KUNENEPESHA  MWILI.

MAHITAJI   YA  DAWA –LISHE

i.           Dawa –lishe vijiko  viwili vikubwa.

ii.         Asali  ya  tende  vijiko  vitano  vikubwa.

iii.       Tangawizi  ya  unga  vijiko  vikubwa  viwili

iv.       Unga  wa ufuta

v.         Maziwa  fresh nusu  lita

vi.       Maji  ya  moto  kiasi  cha  milimita  mia  mbili  na  hamsini  ( 250 mills  )


MATAYARISHO
i. Chukua  vijiko  vinne  vyenye  dawa  lishe  yako  kisha  chemsha  na  nusu  lita  ya  maji  hadi  mchanganyiko  wako  utokote  halafu  ipua, chuja , makapi  weka  pembeni  kisha  hifadhi  juisi  yako.

ii.Tayarisha  uji kwa  kutumia  unga  wa  ufuta  na maziwa  fresh

iii.Chukua  vijiko  viwili  vikubwa  vya tangawizi  ya  unga  kisha  changanya  kwenye  kikombe  cha  maji  ya  moto  chenye  ujazo  wa  milimita  mia  mbili  hamsini  (  250  mills )

MATUMIZI:
i. Tumia  kunywa  nusu  lita  ya  dawa –lishe  yako  kisha

ii.Tumia kula  vijiko  vinne  vikubwa  vya  asali  ya  tende

iii.Kisha tumia  kunywa  vikombe  vinne  vya  uji  wa  ufuta  ulio changanywa  na  maziwa  fresh

iv.Halafu  kunywa  glasi  moja  ya  moto  iliyo  changanywa  na  vijiko  viwili  vikubwa vya tangawizi  ya  unga.

UTAFANYA  HIVYO  MARA  MBILI  KWA  SIKU  KWA  MUDA  WA  SIKU  THELATHINI  MFULULIZO.

Baada  ya  siku  thelathini, utaangalia  na  kujitathmini  kiasi  ulicho  ongezeka. Kama  utataka  kuendelea  kuongezeka  zaidi, utaendelea  kutumia  dozi  hii  hadi hapo utakapo fikia kiwango  utakacho  rizika  nacho.

BEI  YA  DAWA-LISHE : Bei  ya  Dawa-Lishe  ni  SHILINGI  ELFU  HAMSINI  TU (TSHS.50,000/=)

JINSI  YA  KUIPATA  DAWA  LISHE:
Dawa  hii  inapatikana  katiuka  duka  la dawa  asilia  la  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAN  katika  eneo  la  TABATA  MAKOKA  karibu  na  SHULE  YA  SEKONDARI  YA  MT. ANNUARITE.

Unaweza  kufika  moja  kwa  moja  katika  ofisi  zetu  AU  unaweza  kuletewa  mahali popote  ulipo  jijini  Dar   Es  salaam.

Kwa  wakaazi  wa  ZANZIBAR  watatumiwa dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti  na  kwa  wateja  wetu  wa  ughaibuni watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

Kwa  mawasiliano  zaidi  wasiliana  nasi  kwa  simu

0766  53  83   84

Vile  vile  tunayo  dawa  ya  asili  iitwayo  JIKO  ambayo  inatibu  na  kuponyesha  kabisa  TATIZO  LA  UKOSEFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu  kuhusu  SAYANSI  YA  NGUVU  ZA  KIUME  pamoja  na  jinsi  dwa  ya  JIKO  inavyo  fanya  kazi  tafadhali  tembelea:

Maalim Seif Arejea Zanzibar Akitokea India Kwenye Matibabu......Mamia ya Wafuasi wake Wampokea, Asema Polisi Imegeuka tawi la CCM

$
0
0

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad jana aliwasili Zanzibar kutoka ughaibuni na kulilaumu Jeshi la Polisi nchini akisema, “hapana shaka yoyote sasa limegeuka tawi la CCM.”

Maalim Seif alisema hayo jana jioni wakati akizungumza na wafuasi wake waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume na baadaye kumsindikiza hadi nyumbani kwake Mbweni mjini hapa.

Baadhi ya viongozi wa CUF waliohudhuria mapokezi hayo ni pamoja na Mansour Yussuf Himid, Nassor Ahmed Mazrui, Fatma Abdulhabibi Ferej na aliyekuwa mgombea mwenza wa Chadema chini ya mwavuliwa wa Ukawa katika urais wa Muungano, Juma Duni Haji.

Maalim Seif aliyetokea India kupitia Falme za Kiarabu, alisema anaunga mkono kauli za Mazrui ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wake, zilizosababisha ahojiwe na polisi juzi, kuwa “sasa CUF wamechoka na uhuni dhidi ya mali na ofisi zao.”

“Nasikitika kuona hujuma, watu wakipigwa na kujeruhiwa na mazombi kila kukicha, polisi wapo wanayaona na hakuna aliyeitwa kuhojiwa kwa uchochezi. Sasa haitawezekana na haitakubalika tena...” alisema.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo jana, Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu alimtaka mwandishi kuzungumza na msemaji wa jeshi hilo, Advera Bulimba ambaye simu yake haikupatikana.

Hata hivyo, akizungumzia suala la mazombi hivi karibuni, Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar, Salum Msangi alisema taswira ya haraka wanayoipata ni kwamba inawezekana wanaotendewa vitendo hivyo ni wahalifu ambao wamekutana na wahalifu wenzao hivyo kuhofia kutoa taarifa ili uhalifu wao usibainike hali inayosababisha kunung’unika pembeni bila ya kufikisha taarifa maeneo sahihi ili zifanyiwe kazi.

“Kwa mujibu wa taratibu zilizopo ni kwamba mtu yeyote anayefanyiwa kitendo cha kihalifu anapaswa kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi ili hatua za uchunguzi au upelelezi zifanyike ili kubaini wahalifu hao,” alisema Msangi.

Katika hatua nyingine, Maalim Seif alimlaumu, Dk Ali Mohamed Shein kuwa si muungwana akidai kuwa amekataa kuondoka madarakani.

Alisema la kushangaza zaidi ni kuona aking’ang’ania uchaguzi wa marudio, ilihali hakuna mantiki wala kifungu chochote cha sheria kinachohalalisha hatua hiyo.

“Nasema sisi hatutambui uchaguzi huo wa marudio maana wameshindwa kututhibitishia ni wapi zilipo hizo dosari za uchaguzi uliokwishafanyika,” alisema.

Katika salamu hizo za takriban dakika 10, Maalim Seif alimtahadharisha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha asijaribu kulazimisha chama hicho kushiriki uchaguzi ‘batili’ wa marudio.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Aamuru Kukamatwa Papo hapo Walimu 8 Kwa Kujihusisha na Mapenzi na Wanafunzi

$
0
0

Walimu wanane wa Shule ya Sekondari Mihama, Kata ya Kitangili, Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wamesimamishwa kazi, watano kati yao wakishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na wanafunzi.

Pia, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo aliyetembelea shule hiyo jana, amevunja bodi ya shule hiyo baada ya kubainika kutofanya kikao hata kimoja tangu ilipoteuliwa Aprili 24, 2013.

Pamoja na Mkuu wa Shule, Joseph Malifedha, walimu wengine waliotiwa mbaroni jana ni Rodrick Uroki, Denis Sanga, Edmund Boaz, Steven Samuel.

Walimu watatu waliokuwa wakifundisha shuleni hapo, lakini wakahamishwa na hivi sasa wanasakwa na polisi kwa tuhuma hizo ni Joseph Lamongi na Joeza Mzava waliohamia Sekondari ya Sangabuye pamoja na Abdallah Mtelwe aliyehamia Tanga.

Malifedha anadaiwa kuwachangisha fedha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu kwa ajili ya picha za kuweka kwenye vitambulisho (passport size).

Akitangaza uamuzi huo, Mulongo alisema tume maalumu ya uchunguzi iliyoundwa Januari 27, kuchunguza tuhuma dhidi ya walimu hao kujihusisha na mapenzi na wanafunzi imebaini ukweli baada ya kuwahoji wanafunzi kadhaa.

“Ni fedheha na haivumiliki kuona walimu wakifanya mapenzi na wanafunzi wao. OCD wakamate walimu wote na uanze uchunguzi mara moja na kukusanya ushahidi utakaowezesha wahusika kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake,” aliagiza Mulongo.

Amri hiyo ilitekelezwa mara moja kwa walimu hao kuwekwa chini ya ulinzi.

Mulongo pia alimwagiza Katibu wa Idara ya Utumishi wa Walimu Mkoa wa Mwanza, Genzi Sahani kuwaandikia barua za onyo walimu wa kike shuleni hapo kwa kushindwa kulinda na kutetea masilahi ya wanafunzi wa kike waliokuwa wakidhulumiwa kingono na walimu wenzao kiasi cha baadhi yao kuathirika kisaikolojia.

Pia, alimwagiza Ofisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Khamisi Maulid kuangalia uwezekano wa kuwahamishia shule nyingine wanafunzi waliodhulumiwa kingono na walimu wao ili kuwaepusha na matatizo ya kisaikolojia.

Maulidi alisema wanafunzi walioathirika zaidi ni wale wa kidato cha nne.

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mkoa wa Mwanza, Said Mselem alisema kitendo hicho kimeifedhehesha taaluma ya ualimu na kuahidi kuwa ofisi yake itatanua wigo wa uchunguzi hadi kwenye shule nyingine. 

TRA Yamdai Profesa Tibaijuka Milioni 500 za Escrow

$
0
0

Hatima ya kesi ya Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka kupinga kuilipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zaidi ya Sh500 milioni kutoka katika mgawo wa Sh1.62 bilioni zinazohusishwa na fedha zilizochotwa Akaunti ya Tegeta Escrow, itajulikana Machi 29, wakati Bodi ya Rufaa za Kodi (Trab) itakapotoa uamuzi.

Tarehe hiyo imepangwa na Makamu Mwenyekiti wa Trab, Hakimu Agusta Mmbando baada ya kukamilika kwa hatua ya usikilizwaji pande zote mbili kwenye kesi hiyo.

Profesa Tibaijuka alikata rufaa Trab baada ya TRA kumpelekea madai ya malipo ya kodi ya Sh586 milioni kutokana na mgawo wa Sh1.62 bilioni anazodaiwa kupokea kutokana na fedha zilizochotwa kutoka akaunti hiyo iliyofunguliwa na Shirika la Umeme (Tanesco) na kampuni ya kufua nishati hiyo ya IPTL kwa ajili ya kuhifadhi fedha za malipo ya ununuzi wa umeme wakati mzozo wao ukiwa mahakamani, lakini zikachotwa kwa njia ambayo ilizua shaka.

Rufaa hiyo ilisikilizwa na Hakimu Mmbando Februari 17, 19 na 22 wakati Profesa Tibaijuka alipokuwa akitoa ushahidi.

Inadaiwa kuwa Profesa Tibaijuka, ambaye aliondolewa katika wadhifa wake wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutokana na sakata hilo, aliwekewa fedha hizo kwenye akaunti yake na James Rugemalira, Mkurugenzi wa VIP Engineering & Marketing Limited iliyokuwa kati ya wanahisa wa IPTL.

Kutokana na mgawo huo, Desemba 31, 2015, TRA ilimtaka alipe kodi hiyo, baada ya kushindwa kufanya marejesho kutokana na mgawo huo.

Hata hivyo, alipinga madai hayo na kisha akakata rufaa Trab kupinga hatua ya TRA kumtaka alipe kiasi hicho cha kodi, pamoja na mambo mengine akidai kuwa hajawahi kupokea fedha hizo kutoka kwa Rugemalira.

Katika rufaa hiyo namba 22 ya mwaka 2015, Profesa Tibaijuka anadai kuwa makadirio hayo ya TRA ya malipo ya kodi ni kinyume cha Sheria ya Kodi na hakupaswa kufanya marejesho kwa kuwa hakupokea kipato chochote katika muda huo uliotajwa.

Akiongozwa na wakili wake, Dk Nshalla Rugemeleza wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, Profesa Tibaijuka alidai kuwa fedha hizo zilikuwa ni mchango uliotolewa kwa Taasisi ya Joha Trust, kwa ajili ya Shule ya Wasichana ya Barbro Johansson inayomilikiwa na taasisi hiyo.

Profesa Tibaijuka alidai kuwa yeye si mwanahisa wa taasisi hiyo, bali ni mmoja wa wadhamini na kwamba TRA ilipuuza ushahidi wake kuwa VIP ilitoa mchango kwa Joha Trust na yeye kama mdhamini alizipeleka Joha Trust kupitia Bank M.

Aliongeza kuwa TRA haikuzingatia ukweli kwamba Joha Trust na yeye ni vitu viwili tofauti, huku akisisitiza kwamba fedha hizo zilikuwa ni kwa ajili ya Joha.

Hata hivyo, wakili wa TRA, Noah Tito ilipinga madai ya Profesa Tibaijuka akidai kuwa utetezi wake hauna msingi kwani fedha hizo ziliingia kwenye akaunti binafsi ya Profesa Tibaijuka na siyo ya Joha Trust.

Mkurugenzi Maswa Afariki Dunia Ghafla Kabla ya Ziara ya Waziri Mkuu

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekatisha ziara yake ya siku sita mkoani Simiyu, baada ya kifo cha ghafla  cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa (DED), Trasias Kagenzi kilichotokea juzi usiku.

Kaimu Katibu Tawala, Donatus Weginah alithibitisha kutokea kifo cha mkurugenzi huyo wakati Waziri Mkuu akiwa na ratiba ya kutembelea wilaya hiyo.

Weginah alisema juzi asubuhi Kagenzi alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia akiwa na mlinzi wake na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Rosemary Kirigini lakini alianza kujisikia vibaya.

“Mkurugenzi alikuwa akifanya mazoezi ‘jogging’ na DC Rosemary Kirigini, lakini baadaye alimwambia Kirigini najisikia pumzi zinabana, akamwambia aendelee… lakini mara mkuu wa wilaya alimuona amejiinamia, aliporudi kumuuliza akamwambia naona nakosa hewa, ndipo alipoamua kukimbia kuchukua gari kumpeleka hospitalini,”alisema.

Weginah alisema mkurugenzi huyo alipelekwa hospitali na majira ya saa tano asubuhi alionekana akiendelea vizuri, hata hivyo baadaye hali ikabadilika mchana na waliamua kumpeleka katika Hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi, lakini usiku wa saa saba alifariki dunia.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Tawala huyo, alisema mkurugenzi ana kama mwaka mmoja na nusu tangu alipohamia wilayani humo na kwamba familia yake iko Arusha.

Weginah alisema jana mchana mwili wa Kagenzi ulichukuliwa hospitalini Bugando na kuletwa wilayani Maswa ambapo leo asubuhi Waziri Mkuu Majaliwa ataongoza kuaga mwili wa mkurugenzi huyo, lakini baadaye wataangalia familia inaamuaje maana ilikuwa imebaki Arusha, kisha mambo mengine yatafuata.

Rais Magufuli Ahudhuria Mazishi Ya Kaka Wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Kijijini Msoga

$
0
0
RAIS John Magufuli jana ameshiriki maziko ya marehemu Selemani Kikwete ambaye ni kaka wa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, yaliyofanyika kijiji cha Msoga, wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani.

Selemani alifariki dunia Machi mosi, mwaka huu nchini India.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, Makamu wa Rais mstaafu Dk Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa zamani, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Mkuu mstaafu Samuel Malecela na Mufti Abubakary Zuberi.

Zitto Kabwe Amuomba Rais Magufuli Atengue Agizo la Jakaya Kikwete

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe anatafuta nafasi ya kukutana na Rais John Magufuli kumuomba atengue agizo la Rais Jakaya Kikwete la kuzuia ujenzi wa makazi katika Mlima wa Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Rais Kikwete alitoa agizo hilo mwaka 2006 kama moja ya hatua za kudhibiti mmomonyoko wa ardhi na kujaa mchanga kwa bandari ya Kigoma.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Kigoma Cinema mjini Kigoma, Mbunge huyo alisema ameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuamini kwamba taarifa alizopewa Rais Kikwete zilizosababisha kutoa agizo hilo hazikuwa sahihi.

Zitto alisema Rais Kikwete alipewa taarifa potofu kwamba mmomonyoko wa udongo kutoka katika eneo hilo ndiyo unaosababisha kujaza mchanga na kupunguza kina katika bandari ya Kigoma.

Mbunge huyo wa Kigoma Mjini alisema kuwa tafiti zilizofanyika na taarifa zilizopo zinaonesha kuwa kupanuliwa kwa Mto Lukuga kunafanya maji kutoka kwa wingi na kuingia bahari ya Atlantiki ndiko kulikochangia kupunguza kina cha maji katika maeneo mbalimbali ya mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa mwaka 2008 inaonyesha kuwa kiasi cha Sh bilioni tano kilikuwa kikihitajika kwa ajili ya kuwalipa fidia wakazi hao, fedha ambazo uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imesema haiwezi kuzilipa hivyo kutaka mamlaka za serikali kuona namna ya kutafuta fedha hizo na kugharamia kuwalipa watu hao.

Wakizungumzia kauli ya Zitto, baadhi ya wakazi wa eneo la Mlole ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa na agizo hilo la Rais Kikwete, walisema kuwa wameanza kupata matumaini ya kuona thamani ya nyumba zao kwani tangu kutolewa kwa agizo hilo nyumba zao zimekuwa hazina thamani mahali popote.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images