Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Aapa Kuwatumbua MAJIPU Viongozi wa Sekretarieti ya EAC.......Asema Pesa Walizotumia Kuandaa Mkutano ni Nyingi Sana

$
0
0

WAKUU wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameazimia Rais John Magufuli awe Mwenyekiti wa jumuiya, kwa maana kwamba Tanzania iendelee mwaka mwingine kuongoza kipindi ambacho Burundi ndiyo ilipaswa kushika wadhifa.

Dk Magufuli ambaye anaongoza jumuiya hiyo ambayo imepata mwanachama mwingine, Sudan Kusini, ameanza kwa kasi kubwa huku akipenyeza msimamo na falsafa yake ya ‘kutumbua majipu’ kuhakikisha nchi wanachama wanakwenda pamoja na kuleta maendeleo ya wananchi.

Hayo yalifanyika katika mkutano wa kawaida wa 17 wa Jumuiya, ambapo wakuu hao wa nchi pia walikubaliana kwa pamoja Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kushirikiana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kutatua mgogoro wa Burundi.

Magufuli aliahidi atafuatilia Sekretarieti ya EAC, kuhakikisha inafanya kazi kwa maslahi ya wananchi wa nchi wanachama na si kuwanyonya.

Rais Magufuli alihimiza viongozi wakuu wa umoja huo, kutoa kipaumbele katika ujenzi wa viwanda. Alisisitiza msimamo wake kupitia Sekretarieti ya jumuiya hiyo, kubana matumizi kuhakikisha malengo ya kuleta maendeleo katika nchi wanachama yanatimia.

Akizungumzia gharama za ukumbi waliotumia kwa ajili ya mkutano huo wa 17 kwenye Hoteli ya Ngurdoto, Magufuli alisema dola 45 kwa kichwa zilizotumika ni nyingi ambazo kama zingebanwa, zingeokoa fedha ambazo zingenunua madawati na kwenda kusaidia mahali pengine.

“Mwito wangu kwa sekretarieti, muwe cost conscious (macho na gharama),” alisema. 

“Tubane sana matumizi iwezekanavyo, tukahudumie watu masikini na si kuwa na Sekretarieti inayokuwa parasite (nyonyaji),” aliendelea kusema.

Sekretarieti hiyo inaongozwa na Liberal Mfumukeko kutoka Burundi, aliyeteuliwa na wakuu hao wa nchi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitano baada ya Dk Richard Ssezibera wa Rwanda, muda wake kumalizika.

Magufuli katika hotuba yake ya kufunga mkutano huo, alisema amepiga hesabu ukumbi huo ni ghali. Alitoa mwito kwa sekretarieti na watumishi wote kwamba ni lazima wafahamu kwamba wako kwa watu masikini na wanahudumia watu masikini katika nchi wanachama.

“Nataka niiambie Sekretarieti, Marais wamefanya kosa sana kunichagua mimi kuwa mwenyekiti. Nitahakikisha nawafuatilia kweli. Kwa hiyo mjipange vizuri na kama patakuwapo mmoja wa wafanyakazi anakwenda sehemu isiyotakiwa, nitaripoti kwa nchi anakotoka ili atumbuliwe jipu,” alisema.

Alisisitiza ifanye kazi kwa niaba ya nchi zao kwa kutengeneza sheria na mambo yatakayozisaidia. Alihimiza sekretarieti isiwe sehemu ya walalamikaji, bali wawe watatuzi wa matatizo ya jumuiya. 

Alisema nchi wanachama wanapaswa kubadilika, kuwa na mtazamo wa kuhakikisha wananchi wake wananufaika na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Tunapaswa kutembea pamoja kwa maslahi ya jumuiya,” alisema. Rais Magufuli anaongoza jumuiya hiyo kwa mwaka mmoja, nafasi ambayo ilipaswa sasa ichukuliwe na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza. 

Hali hiyo inatokana na nchi hiyo kuomba kuachia nafasi hiyo ili kuelekeza nguvu zake katika kushughulikia matatizo yake ya ndani, lakini ilipewa nafasi ya kutoa Katibu.

Jumuiya ya Afrika Mashariki inaundwa na nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi huku Sudan Kusini ikiwa imekidhi vigezo na kukubaliwa kuwa mwanachama mpya wa jumuiya hiyo katika mkutano huo wa 17.

Watumishi 3 Ghala la Chakula Arusha Wasimamishwa kazi

$
0
0

Watumishi  watatu wa Ghala la Taifa la Hifadhi Chakula wamesimamishwa kazi, wakidaiwa kuchanganya kwa makusudi mahindi mabovu na mazuri na kuwapelekea wananchi.

Uamuzi huo ulichukuliwa mjini Arushajana na Naibu Waziri wa Mifugo, Kilimo na Ushirika, William Ole Nasha baada ya kufanya ziara kwenye ghala mkoani hapa.

Waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi ni Meneja Brightone Mollel ambaye ni msimamizi mkuu wa ghala na maofisa wawili kutoka Makao Makuu Dar es Salaam ambao ni Dunia Mlokozi na Silvano Mwakinyela.

Wanatuhumiwa pia kuuza mahindi hayo ya serikali kwa wafanyabiashara mbalimbali mkoani Arusha na nje ya nchi. 

Imedaiwa kutokana na vitendo hivyo, wamejinufaisha na kuwa mamilionea huku wananchi wakinyanyasika kwa kula chakula kibovu.

Hata hivyo, Meneja huyo, Mollel alimweleza waziri kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake si za kweli, kwani hajawahi kufanya unyama huo wala kuuza mahindi ya serikali.

Akifafanua kwa waandishi wa habari baada ya kufanya ziara ya ghafla katika ghala hilo, Naibu Waziri Nasha alisema hujuma ya kuwalisha watanzania chakula kibovu, imefanyika kwa miaka mingi na amekuwa akipata malalamiko mengi mkoani Arusha na nje ya mkoa.

Nasha alisema serikali haiwezi kuwaachia kirahisi watumishi wa aina hiyo wenye uchu wa utajiri kwa kuwaangamiza wananchi kwa maslahi yao. Alikielezea kitendo hicho kuwa si cha huruma.

Kwa mujibu wa naibu waziri huyo, mahindi mabovu ambayo yametengwa, huchanganywa na mahindi mazuri na kusambazwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu huku wahusika wakijua wazi kuwa hayafai kwa matumizi hayo.

‘’Angalia ubovu wa mahindi haya, lakini vigogo wa ghala hili wakishirikiana na wafanyabiashara, wanachanganya na mahindi mazima na kisha wanapeleka wilayani kwenye uhaba wa chakula. 

"Wananchi wamekuwa wakilalamika kila mara kuwa mahindi yanayopelekwa huko hayafai kuliwa na hata na mbuzi au ng’ombe hawali, hali iliyonifanya kufuatilia kwa karibu na kuja kujionea mwenyewe bila kuambiwa,’’ alisena Nasha.

"Hawa watu nimewasimamisha kazi kuanzia leo (jana) mpaka uchunguzi upite ni kwa nini wanafanya hivyo, hii haikubaliki,’’ alisema Nasha.

Baadhi ya wafanyakazi wa ghala hilo na wabeba mizigo, walikiri kwamba hali ya kuchanganya mahindi mabovu na mazuri iko katika ghala hilo kwa muda mrefu na wamekuwa wakilazimishwa kufanya hivyo kwa maslahi ya baadhi ya watumishi.

Mmoja wa wafanyakazi hao, aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alisema watendaji hao wakuu wa ghala, wana utajiri mkubwa unaohusishwa na hujuma hiyo ya mahindi.

“Kuna kigogo mmoja alimpa mtoto wake wa kike zawadi ya gari V8 VX yenye thamani ya zaidi ya Shmilioni themanini siku yake ya kuzaliwa. Baadhi ya watumishi wa serikali katika ghala hili wanaishi kama wapo peponi kwa kuwapa watanzania chakula kibovu.

"Mahindi ya serikali huuzwa na mengine kusafirishwa nchi jirani ya Kenya bila ya kubughudhiwa,” alisema mfanyakazi huyo. Mfanyakazi mwingine alisema kuna mtandao mkubwa wa kuuza mahindi ya serikali.

"Kibaya zaidi watanzania wanalishwa chakula kibovu chenye hatari kwa afya huku wao wakijitajirisha kwa mahindi mazuri yanayoenda nje ya nchi kwa njia za panya," alisema mfanyakazi mwingine aliyeomba jina lihifadhiwe.

Alisema, "Naomba Waziri unilinde kwani ninaweza kuuawa, hata nikifukuzwa kazi sioni tatizo, lakini roho inauma sana ninapoambiwa nichanganye mahindi mabovu yenye sumu na mahindi mazuri ili yakaliwe na watanzania, hiyo ilituuma sana wabeba mizigo wote’’.

Alisema malalamiko hayo waliyafikisha ofisi ya mkuu wa wilaya siku nyingi kuelezea hujuma hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu alikiri kuwa na taarifa hiyo na alisema ndio maana amekuja na waziri husika, anayeshughulika na sekta hiyo.

Nkurlu alisema pia Waziri mwenyewe amekiri kupata malalamiko katika wilaya za Karatu, Ngorongoro na Simanjiro kuwa mahindi ya misaada yanayopelekwa huko, hayafai kuliwa na binadamu kwani hata mifugo inakataa kula.

Binti wa Raila Odinga Aomba Radhi Watanzania kwa kauli yake kwamba Olduvai Gorge iko nchini Kenya

$
0
0

Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary amewaomba radhi Watanzania kwa kauli yake kwamba Olduvai Gorge iko nchini humo.

Rosemary alisema hakuwa na nia mbaya alipotoa kauli hiyo, bali aliitoa kwa bahati mbaya akimaanisha eneo jingine lililoko Kenya linaloitwa Olorgesalile.

Alifafanua kuwa matamshi hayo hayakulenga kupotosha ukweli, bali ulimi uliteleza.

Katika maelezo aliyotoa kupitia akaunti yake ya Facebook, Rosemary aliandika:

“Habari za jioni. Nimekuwa nikikumbushwa kuhusu tukio lililotokea wakati nahudhuria kongamano la vijana New York, miezi saba iliyopita.

Niliteleza ulimi kwani sikumaanisha Olduvai Gorge badala yake nilitaka kumaanisha Olorgesalile,” alisema na kuongeza:

“Nawapa pole Watanzania kutokana na usumbufu uliojitokeza, kaka zangu na dada zangu poleni sana na Olduvai Gorge yenu bado iko salama.”

Binti huyo alihitimisha kwa kuweka hotuba yake aliyoitoa kwenye kongamano hilo akisema ililenga kuleta umoja na mshikamano.

Tangu kutolewa kwa kauli hiyo, kumekuwa na mlolongo wa shutuma zinazoelekezwa kwa binti huyo wa Odinga huku baadhi ya Watanzania wakisaini azimio maalumu kumtaka ombe radhi ambalo waliosaini wamefikia 17,000.

Tangu wiki iliyopita, kumekuwapo na mkanda wa video unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Rosemary akihutubia mkutano jijini New York huku akidai Bonde hilo lililogunduliwa mtu wa kale la Olduvai Gorge linapatikana nchini Kenya.

Mapema, Serikali ya Tanzania imesema itachukua hatua za kidiplomasia endapo ungepatikana uhakika juu ya taarifa zinazoenezwa na mitandao ya kijamii kuwa raia wa Kenya huzitaja baadhi ya tunu za Tanzania kuwa zinamilikiwa na nchi yao.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambeni alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana akisema Serikali inafanya uchunguzi juu ya taarifa hizo.

Hata hivyo, alisema hali hiyo inaonyesha ni jinsi gani nchi Tanzania inazidi kuwa maarufu kwa mazuri yake mpaka majirani wanatamani miliki zake.

Mwambene alikuwa anazungumzia taarifa za mitandao zilizowahusisha raia wa Kenya kutamba kuwa Mlima Kilimanjaro, Olduvai Gorge na Mbuga ya Serengeti vipo nchini Kenya na ripoti za hivi karibuni kuwa mwanasoka wa kimataifa, Mbwana Samatta na mwanamuziki Diamond Platinumz ni raia wa Kenya.

Mbunge wa Kinondoni (CUF) Maulid Mtulia Apinga Mpango wa DC Makonda Kuwaruhusu Walimu Wasafiri Bure Kwenye Daladala

$
0
0

Mbunge wa Kinondoni, (CUF), Maulid Mtulia amepinga mpango wa walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam kusafiri bure kwenye daladala akisema utawashushia heshima.

Badala yake, alitaka Manispaa ya Kinondoni iweke utaratibu wa kuwaongezea walimu fedha za usafiri kwenye mishahara yao ili wajilipie wenyewe.

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya hiyo, Paul Makonda kutangaza kuwa walimu wa shule za Serikali za Dar es Salaam watasafiri bila kulipa nauli kwenye daladala.

Katika mpango huo ambao umepangwa kuanza Jumatatu ijayo unaozigusa pia manispaa za Temeke na Ilala, walimu watapatiwa vitambulisho maalumu vyenye saini ya Makonda.

Akizungumza katika mahojiano maalumu juzi, Mtulia alisema licha ya kuwa wazo lililenga kuwasaidia walimu, lakini litawasababishia dhihaka.

Alisema kinachopaswa kufanyika ni kutafuta suluhisho la kudumu la kero zinazowakabili walimu ambazo zinachangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.

“Itafika hatua kondakta atamsimamisha mwalimu kwenye kiti kama ilivyo kwa wanafunzi kwa sababu tu halipi nauli… Wazo hili ni zuri lakini lilipaswa kuboreshwa kama kweli nia ni kumsaidia mwalimu,” alisema. 

Alisema ikiwa kweli nia ni kuwasaidia walimu, basi halmashauri zina wajibu wa kuhesabu siku za kazi na kiasi ambacho mwalimu atalipia nauli ili fedha hizo ziongezwe kwenye mshahara wake.

Alisema njia hiyo itakuwa ya heshima zaidi kuliko walimu kusafiri bure kwa kutumia vitambulisho kama walivyo wanafunzi wao. 

Hata hivyo, alisema ipo haja kwa viongozi wa manispaa hiyo kukaa meza moja na walimu ili kujua changamoto zinazohitaji suluhu ya haraka, akisema huenda nauli ikawa si ya msingi kwao.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya March 3

NSSF Haina Mkurugenzi wala Kaimu kwa Wiki Mbili Sasa

$
0
0

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linamaliza siku ya 15 likiwa halina kiongozi baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu, Dk Ramadhan Dau kuteuliwa kuwa balozi na kuacha mara moja shughuli za kila siku za taasisi hiyo kubwa, hali iliyofanya shughuli zake kudorora.

Rais John Magufuli alimteua Dk Dau kuwa balozi Februari 15, sambamba na makada wengine wawili wa CCM, Dk Asha Rose Migiro na Mathias Chikawe, akisema vituo vyao vya kazi vitajulikana baada ya taratibu za kidiplomasia kukamilika.

Tangu wakati huo, NSSF imekuwa ikijiendesha bila ya kiongozi mkuu na habari kutoka ndani ya shirika hilo zinasema kuwa shughuli za shirika hilo kubwa kuliko yote yanayojihusisha na hifadhi ya jamii nchini, haziendi kutokana na kutokuwapo na mtu aliyepewa jukumu la kukaimu nafasi hiyo.

Miongoni mwa mambo hayo ni ufunguzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam ambalo lilitakiwa lianze rasmi kutumika Machi Mosi, ununuzi wa magari ya ofisi za mikoa, mkutano wa wanachama wa mwaka pamoja na wiki ya NSSF ambayo hujumuisha mambo mbalimbali, kama shughuli za kijamii, maonyesho ya huduma za NSSF na michezo.

Juhudi za kumpata Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama, anayehusika na mifuko ya hifadhi ya jamii hazikufanikiwa. Pia, Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue, ambaye amekuwa akitoa taarifa za uteuzi unaofanywa na Rais, hakupatikana jana.

Wiki iliyopita, Balozi Sefue alisema maswali kuhusu uteuzi wa kaimu yaelekezwe kwa Mhagama, ambaye alieleza wakati huo kuwa utaratibu wa kuimpata kaimu unaendelea.

 Kwa mujibu wa ripoti ya fedha ya mwaka 2011, shirika hilo lilikuwa na wanachama 501,218, kati yao wafanyakazi waliosajiliwa waliongezeka kutoka 17,666 hadi 18,779, sawa na ongezeko la asilimia 6, huku michango ikiongezeka kutoka Sh300.08 bilioni hadi Sh356.5 bilioni kwa mwaka, ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.8.

Kwa mujibu wa muundo wa uongozi wa NSSF, Mkurugenzi Mkuu ndiye kiongozi mkuu wa shirika akiwa na wakurugenzi wanane chini yake. 

Wakurugenzi hao wanahusika na uendeshaji (DO); utawala na rasilimali watu (DHRA); mipango, uwekezaji na miradi (DPIP); fedha (DF); teknohama (DIT); ukaguzi wa ndani (DIA); uthibiti na usalama wa mali (DARM) na huduma za kisheria (DLS).

Dr Slaa Afunga Ndoa na Josephine Mushumbusi Ughaibuni

$
0
0

Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi.

Wawili hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa  moja, lakini  habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita. 

Ndoa hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu  za Dr Slaa ambaye mwaka 2010 aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani  akidai bado anamtambua Josephine  kuwa ni mke wake wake halali.

Mume huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama  impatie haki  yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa.


Misukosuko ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa  mke wake, Rose Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50.

Dr Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini lakini wakashindwa kutokana na mapingamizi hayo.

Zuio la Uchaguzi Meya wa Dar Lageuka Kaa la Moto..... Aliyelisoma asema Hakujua kama ni Halali au Feki

$
0
0

Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kulikana zuio llilotumika kuahirisha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, suala hilo limekuwa sawa na kaa la moto na hakuna mtu anayetaka kulishika.

Jana Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, ambaye alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita,  jana alisema hajui lilikotoka zuio hilo kwa  kuwa alipewa tu na wanasheria wa jiji ili alisome kama lilivyo.

“Baada ya kufika eneo la tukio (kwenye ukumbi wa Karimjee), nilikabidhiwa zuio hilo nilisome. Suala la kujua kama limeisha muda wake au la naomba uwasiliane na mwanasheria wa jiji au mwanasheria wa mkoa, wao ndio walikuwa nalo na hata nilivyopoteza vitu vyangu vingine, hilo (zuio) wao wanalo,” alisema Mmbando.

Baada ya kutimiza wajibu wake, kama alivyotakiwa na wanasheria hao, alisema ndipo zilipozuka vurugu na yeye kupoteza nyaraka zake ikiwa pamoja na ajenda na miongozo ya kikao hicho.

Kwa upande wake, Mwanasheria wa Jiji la Dar es Salaam, Jackline Mosha, alisema hakupitia tamko hilo kabla ya kumpa aliyekuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo na kwamba alilikuta kwenye ukumbi huo bila kujua limetoka wapi.

Alisema walijua kuna zuio hilo baada ya kufika katika viwanja vya Karimjee siku hiyo ya uchaguzi.

“Zuio lilitoka Februari 5, sisi tulijua siku ya tukio, tulimkabidhi mwenyekiti Mmbando alisome, hatukufahamu kama limeisha muda wake.

“Hatukupata muda wa kulipitia na kujiridhisha kwa sababu haikuwa siku ya kazi kwa mahakama. Hata hivyo zuio hili hatukupewa mapema, wangetupa mapema tungejiridhisha na yote hayo tungeyajua kabla ya siku ile,” alisema.

Kuhusu madai kuwa walitumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya hivyo, alisema wao ni wanasheria na kwamba wanafanya kazi kitaalamu.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene, amesema kuwa tayari ameagiza apelekewe taarifa rasmi na Theresia Mmbando, ili kubaini ukweli kuhusu zuio hilo kama lilikuwa la kweli au la.

Waziri Simbachawene alitoa kauli hiyo juzi na kusisitiza kuwa kwa wakati huo hakuwa na taarifa zinazothibitisha  zuio la kuahirishwa kwa uchaguzi huo lililosomwa na Mmbando kama ni la kweli au la.

“Kwa sasa kama wizara hatuna cha kusema kuhusiana na tukio zima lililitokea siku ile. Kama mnavyojua Katibu Tawala alipigwa anaumwa, yeye ndiye aliyesoma zuio hilo hivyo tunasubiri apone atuandalie taarifa kamili,” alisema na kuongeza:

“Kama Waziri sijapokea taarifa zozote zinazosema zuio hilo lilikuwa halali au la. Tusubiri kwanza atuandikie hiyo taarifa yake ili tufanye ulinganisho ndipo wizara itapata cha kusema,” alisema.

Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika kwanza Desemba, mwaka jana, ukapangwa kufanyika Januari 23, mwaka huu lakini na baadaye kupangwa kuwa Februari 8.

Februari 8, mwaka huu, madiwani baada ya kufika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya uchaguzi, walikabidhiwa barua ambazo hazikueleza sababu za kuahirishwa kwake bali utafanyika utakapopangwa tena na ndipo ulipopangwa kufanyika Jumamosi iliyopita.

Jumatatu wiki hii, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Warialwande Lema, alikanusha taarifa kwamba   mahakama hiyo imetoa zuio la uchaguzi huo.

“Mahakama ilitoa amri ya zuio la muda Februari 5, mwaka huu la kuzuia uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 8 na ilipanga kusikiliza maombi hayo Februari 15 lakini walalamikaji hawakufika mahakamani,” alisema na kuongeza:

“Mahakama ilipanga tena maombi hayo kusikilizwa Februari 23, mwaka huu, lakini pia walalamikaji hawakutokea mahakamani.”

Walalamikaji katika shauri hilo walikuwa Susan Massawe na Saad Khimji, dhidi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam.

Akiendelea kufafanua, Hakimu Lema alisema baada ya walalamikaji kushindwa kufika, mahakama iliondoa maombi ya zuio yaliyokuwa yamewasilishwa  mbele yake na walalamikaji pamoja na zuio lililokuwa limetolewa awali.

“Aliyesema mahakama imetoa zuio ni uongo kwa kuwa walitumia amri ambayo ilipitwa na wakati. Sijui chochote kuhusu zuio la Februari 27, mwaka huu,” alisema Hakimu Lema.

Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Cyprian Mkeha, alisema baada ya maombi hayo kuondolewa mahakamani, hajapokea maombi mengine kuhusu kuzuia uchaguzi huo.

Wassira Amvaa January Makamba...... Asema Huenda Yeye ndo Alibebwa Tano Bora ya Urais CCM

$
0
0
 
MWANASIASA mkongwe aliyekuwa waziri katika Serikali ya awamu nne, Stephen Wasira, amemshangaa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, January Makamba aliposema kuwa uwajibikaji katika utawala wa awamu ya nne ulikuwa ni wa kuleana.

Kauli ya Wasira imekuja siku moja baada ya gazeti la Mwananchi kumnukuu Makamba akisema uwajibikaji katika Serikali ya awamu hiyo haukuwa wa kuridhisha kwasababu kulikuwa na utamaduni wa kuoneana haya, kujuana na kusitiriana.

Akizungumza  katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam jana, Wasira alieleza kushangazwa na kauli hiyo ya Makamba akisema yawezekana aliyelelewa ni yeye.

“Labda alilelewa yeye…kama rafiki yangu Makamba anasema kulikuwa na kuleana, mimi kwa upande wangu sikulelewa nilifanya kazi na nikatimiza wajibu wangu kama nilivyopewa na Rais.

“Sasa kama aliona kulikuwa kuna kuleana mimi sijui yeye ndiye anajua maana mimi sikulelewa. Kama unafanya makosa halafu unaachwa huondolewi hapo ni kuleana.

“Na yeye inawezekana alilelewa maana kuna watu wanasema kuingia kwake tano bora ya urais alipendelewa labda huko ndio kulelewa ndio maana akasema hivyo,”alisema Wasira.

Wasira ambaye aliongoza kamati iliyoandaa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, alisema kasi ya utumbuaji majipu aliyoanza nayo Rais Dk. John Magufuli ipo katika ilani ya chama hicho tawala na kwamba walipanga hivyo.

Mwanasiasa huyo ambaye alikuwa waziri katika kipindi chote cha miaka 10 ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, alisema si kweli kama ambavyo baadhi ya watu wanasema kwamba Serikali ya awamu ya nne haikufanya kitu, bali ilikuwa ikitumbua majipu kwa mtindo wa kimya kimya.

Alisema kila awamu inayoingia madarakani inakuwa na mtindo wake wa kufanya kazi na kwamba ni vigumu kulinganisha na awamu nyingine.

“Kila kiongozi ana ‘style’ yake, huwezi kulinganisha wakati wa Magufuli na Nyerere, Mwinyi, Mkapa au Kikwete hawa ni watu ‘individuals’ kila mtu ana mtazamo wake wa kuongoza na kila mtu ana ilani kwa wakati wake.

“ Wengine mara wanasema hatukuwa na Serikali awamu iliyopita wakidai kwamba haikufanya kitu, si kweli kabisa, Serikali ilikuwepo, lakini ili concentrate (kujielekeza) kwenye nini…lazima tufanye tathimini. Kila Serikali ina mazuri na mabaya.

“Ukitaka kufanya tathimini unawezaje kusema Jakaya Kikwete hakufanya kitu? Wakati alijenga shule nyingi za kata, barabara zilizojengwa wakati Magufuli akiwa waziri wa ujenzi hazikuwa zake bali ni mpango wa Serikali ya awamu ya Kikwete.

“Hakuna Serikali iliyo perfect (kamilika)na huku inaongozwa na wanadamu. Kila Serikali ina style yake na awamu ya nne ilikuwa ya kimya kimya kama nilivyoeleza. Ilifanya vizuri, mengine haijafanya sana na mengine haikufanya kabisa.

“Ukifanya uchunguzi Serikali zote utakuta kuna mazuri na mabaya. Mwalimu Nyerere alikuwa anaipenda Tanzania na Watanzania kutoka moyoni mwake na alikuwa tayari kufanya kazi bila kulipwa na wakati anastaafu akasema chukueni mambo mazuri tuliyofanya, mabaya acheni…hapo aliona kabisa Serikali haikuweza kutimiza yote,”alisema Wasira.

Kutokana na hilo, Wasira alisema popote duniani hakuna Serikali ambayo inaweza ikafanya kila kitu kwasababu hakuna binadamu aliye malaika.

“Hakuna Serikali itakayofanya kila kitu hata Magufuli ataacha mengine na mwingine atayakuta. Hakuna Serikali inayoongozwa na malaika bali inaongozwa na wanadamu. Kuendesha nchi si jambo dogo kwasababu ina mambo mengi.

“Matatizo ya bandari yalikuwepo na si kwamba yameisha. Mfano hivi sasa wamebadili jina la rushwa kuwa posho…kwa hiyo hivi sasa wamegeuza rushwa kuwa posho.

“Kwa kasi hii sasa wafanyakazi watarudi nyuma na kufanya kazi kwa nidhamu zaidi, lakini vichwa maji nao watatumia ‘style’ nyingine tu kama hiyo ya kugeuza rushwa kuwa posho,”alisema Wasira.

Wasira ambaye alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitokeza kutaka kuteuliwa na chama hicho kuwania urais, akizungumzia uteuzi huo alisema hakukuwa na namna kwasababu waliojitokeza walikuwa wengi.

“Walikuwepo watu 38 waliochukua fomu na kurudisha, wakateuliwa watano si kwamba walikata majina bali waliteua. Kanuni ya CCM ndiyo inasema hivyo sasa hivi hata nikisema haki haikutendeka itasaidia nini wakati uchaguzi ulishapita?

“Kanuni ya chama haisemi lazima waitwe ndio wahojiwe bali Kamati Kuu inajadili jina moja moja… kwa kuwa mimi sikuwepo ndani ya kikao hicho sijui kama nilijadiliwa… sielewi.

“Lakini nilisikitika kama binadamu na sikufanya chochote zaidi ya kusikitika maana ndio utaratibu wa chama inawataka watano,”alisema mwanasiasa huyo.

Akizugumzia kuhusu hali ya kisiasa visiwani Zanzibar, Wasira alikishauri Chama cha Wananchi (CUF) kikubali kushiriki uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20, mwaka huu kwasababu wapiga kura ni wale wale.

Alisema amani ya Zanzibar ipo mikononi mwa Wazanzibari kwa kushiriki uchaguzi huo.

“Ili kuwe na amani Zazinzibar CUF waende kwenye uchaguzi kwasababu wapiga kura ni walewale, kama wanajua walishinda hofu yao nini?…hata wakirudia watashinda.

“Ushauri wangu kwa Wazanzibari wasaidie katika kuleta amani, wapige kura…wanaoipigia CUF au CCM na vyama vingine wafanye hivyo halafu kura zihesabiwe mshindi atangazwe kwa sababu hakuna namna kwa vile Mwenyekiti wa ZEC alisema uchaguzi uliopita ulikuwa na kasoro,”alisema.

Wasira ambaye alikuwa Mbunge wa Bunda kwa muda mrefu, akielezea kuhusu namna alivyoshindwa na upinzani katika uchaguzi wa mwaka jana katika jimbo hilo, alisema uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.

“Uchaguzi ule uligubikwa na corruption (rushwa), ulikuwa na kasoro nyingi sana…hakukuwa na uchaguzi pale, lakini kwa kuwa bado suala hili liko mahakamani tuliache kwanza,”alisema.

Credit:Mtanzania

Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti ya Uingereza Ijumaa ya Leo March 4

Habari Zilizotawala Magazeti ya KENYA Ijumaa hii Ni Matokeo ya Mtihani wa KCSE 2015.........Karibu Ujionee

Rais Magufuli Awaongoza Wakuu Wa Nchi Za Jumuiya Ya Afrika Mashariki (EAC ) Kushiriki Katika Uzinduzi Wa Barabara Ya Arusha-Holili/Taveta-Voi Km 234.3 Marchi 3,2016

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Muigai Kenyatta, wameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Arusha - Holili - Taveta - Voi, yenye urefu wa kilometa 234.3 ambayo inaunganisha nchi za Tanzania na Kenya.

Hafla ya uwekaji wa jiwe hilo la Msingi imefanyika jana  katika eneo la Tengeru Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na viongozi wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ni Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Makamu wa pili wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Dkt. Joseph Butore, Mwakilishi wa Rais Paul Kagame wa Jamhuri ya Rwanda ambaye ni Waziri wa Afrika Mashariki wa Rwanda Mheshimiwa Valentine Rwabiza na Makamu wa Pili wa Rais Sudan Kusini Mheshimiwa James Wan Iga.

Uzinduzi huo pia umehudhuriwa  na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.

Kwa upande wa Tanzania ujenzi wa barabara hiyo unatakelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Arusha hadi Tengeru yenye urefu wa kilometa 14.1, na ujenzi wa barabara ya mzunguko yaani "Bypass" yenye urefu wa kilometa 42.4. 

Awamu ya pili itahusisha ujenzi wa barabara ya njia nne kuanzia Tengeru hadi Usa River yenye urefu wa kilometa 8.2 na Kutoka Usa River hadi Holili mpakani mwa Kenya na Tanzania yenye urefu wa kilometa 100.2

Gharama za upanuzi wa barabara ya Arusha - Tengeru na barabara ya kuzunguka nje ya jiji la Arusha kwa upande wa Tanzania ni shilingi bilioni 209.6, ambapo kati ya fedha hizo Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) itatoa mkopo wa shilingi bilioni 190.2 na serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 19.4.

Aidha Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ipo kwenye mazungumzo na serikali ya Japan ili kupata mkopo wa ujenzi wa awamu ya pili inayoanzia Tengeru hadi Holili.

Kwa upande wa Kenya, mradi huu unahusisha ujenzi wa barabara mpya kwa sehemu ya Taveta hadi Mwatate yenye urefu wa kilometa 100. Sehemu ya Mwatate hadi Voi ujenzi wake umekamilika.

Akizungumza katika hafla hii, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, amesema wananchi wa Afrika Mashari hawapaswi kuwa masikini na kueleza kuwa mradi huo na mingine itakayotekelezwa chini ya ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki itasaidia kuinua hali ya maisha ya wananchi.

Kwa upande wao Marais Uhuru Muigai Kenyatta wa Kenya, Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na wawakilishi wa marais wa Burundi, Rwanda, Sudani Kusini wameuelezea mradi huo kuwa ni moja ya miradi muhimu ya kuimarisha uchumi wa jumuiya ya Afrika Mashariki na wametoa wito kwa nchi zote wanachama wa jumuiya hiyo kushirikiana kukuza biashara baina yake.

Viongozi hao wote wamekiri kuwa Jumuiya hii yenye watu zaidi ya milioni 160, inayo nafasi ya kupiga hatua kubwa za kiuchumi na kuondokana na umasikini, ikiwa italitumia vizuri soko la pamoja kwa kubadilisha bidhaa kutoka nchi moja hadi nyingine na kujenga viwanda vingi badala ya kuendelea kutegemea bidhaa kutoka nje.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha
03 Machi, 2016

Waziri Nchemba Awafuta Kazi Viongozi Wote wa Wakulima wa Miwa Kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Taifa

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo na mtafiti wa mbegu kutoka mmoja ya maafisa wa juu wa wakala mkuu wa ghala la mbegu za ASA (Agricultural Seed Agency) Mkoani Morogoro.

Mhe. Mwigulu Nchemba akikagua mbegu zilizopo kwenye ghala la ASA mkoani Morogoro.

Mwigulu Nchemba akizungumza na watumishi wa ASA (Agricultural Seeds Agency) wakati wa ziara hiyo. Kubwa alilosisitiza ni uzalendo na kufanya kazi kwa kujituma.
Mhe. Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kuhusu malisho ya ng'ombe yanayopatikana kwenye kituo cha utafiti wa mifugo Morogoro(LITA).
Mhe. Waziri akiangalia baadhi ya ndama wa ng'ombe waliopo kwenye shamba la utafiti kwenye kituo cha LITA - Morogoro.
Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza na Makamu Mkuu wa chuo za SUA(Sokoine University of Agriculture) alipofika kwaajili ya kukutana na wataalam,na uongozi wa SUA kwaajili ya kupokea maoni yao kuelekea kilimo,ufugaji na uvuvi wa kisasa. "Transformation of Agriculture".

Katika kikao hicho, wataalam kutoka SUA walisisitiza kuwa ili Tanzania iweze kuondokana na kilimo holela,ni wakati muafaka sasa kama nchi kuamua kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji na kuondoakana na kilimo cha mvua,pia kuachana na jembe la mkono na wakati huo huo kuimarisha vituo vya utafiti na kuzalisha mbegu kikanda.
Akiwa njiani kuelekea Ifakara, Mwigulu Nchemba akaamua kufanya mkutao Jimbo la Mikumi kijiji cha Tungu kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi dhidi ya uongozi wa miwa wilaya, Mkoa na Taifa, mahusiano mabaya ya kibiashara kati ya wakulima wa miwana kiwanda cha Ilovo na utitiri wa vyama vya wakulima kwa eneo la Kilombero.
 
Baada ya kusikiliza kero kutoka kwa wananchi na kusoma baadhi ya ripoti za serikali ya wilaya na mkoa na zile za tume mbalimbali zilizoundaw kujua kiini cha matatizo ya wakulima wa miwa Kilombero, Mwigulu Nchemba akiwa ndiye Waziri mwenye dhamana na kilimo akaamua kufuta uongozi wote kwa wakulima wa miwa kuanzia ngazi ya Wilaya ya Mikumi hadi Taifa kwa kosa la ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule (Prof. Jay) wakati wa mkutano huo
Mhe. Mwigulu Nchemba akiangalia mfereji ulioandaliwa kwaajili ya kusambaza maji kwenye shamba la utafiti wa mbegu za Mpunga-Kilombero. Matumizi ya mifereji kwenye kilimo yanaondoa mfumo wa kutegemea mvua ili mimea kupata maji na kukua kwa wakati.

Mwigulu Nchemba anatarajia kuendelea na ziara ya kukagua vituo vya utafiti na uzalishaji wa mbegu nchi nzima, lakini wakati huo huo atatembelea mashamba ya mifugo na maeneo ya uvuvi wa samaki.
  • Picha/maelezo na festo Sanga Jr

Waziri Jenista Mhagama Amteua Dr. Wangwe Kuwa Kaimu Mkurugenzi wa NSSF ....Hata Hivyo Uteuzi Huo UMETENGULIWA Mpaka Utakapotangazwa Tena

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dkt. Carina Wangwe akifafanua jambo kwa wajumbe wa bodi wa shirika hilo (hawapo pichani ) kabla ya uteuzi huo kutenguliwa.

Masaa  kadhaa baada  ya  uteuzi huo, Waziri mhagama alitangaza  kutengua uteuzi huo kwa madai kwamba kuna baadhi ya taratibu hazijamilika

Paul Makonda Amkataa Hakimu Anayesikiliza Kesi ya Kuwakashfu Makada Wenzake wa CCM.....Kubenea Naye Akutwa na Kesi Ya Kujibu Sakala la Kumtusi Makonda

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda jana alitinga mahakamani na kumkataa hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi iliyofunguliwa dhidi yake na makada wawili wa zamani wa CCM wanaodai aliwakashifu.

Kesi dhidi ya Makonda, ambayo awali ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Hellen Liwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilishafikia hatua ya utetezi na Makonda alitakiwa kuanza kujitetea jana, baada ya mahakama hiyo kumuona kuwa ana kesi ya kujibu.

Hata hivyo, jana Makonda ambaye alifika mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kesi hiyo ilipofunguliwa, alishikilia msimamo wa kutokuwa na imani na hakimu huyo na hivyo kuomba apangiwe hakimu mwingine.

Makonda alifikia msimamo huo kutokana na maneno aliyoelezwa na wakili wake, ambayo kwa mtazamo yalionyesha kuwa hakimu atakuwa anawapendelea wadai na hivyo asingemtendea haki.

Kutokana na madai ya Makonda, Hakimu Liwa amejitoa kwenye kesi hiyo na amepanga ianze kusikiliza upande wa mashtaka Machi 23.

Kesi dhidi ya Kubenea 
Wakati Makonda akimkataa hakimu, mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, Saed Kubenea ameonekana ana kesi ya kujibu katika kesi inayomkabili ya tuhuma za kumtukana mkuu huyo wa wilaya. 

Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu anayesikiliza kesi hiyo, ikiwa ni siku chache baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake.

Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Simba alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka uliotolewa na mashahidi watatu, aliridhika kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu.

Baada ya uamuzi huo wakili wa Kubenea, Peter Kibatala aliieleza mahakama kuwa mteja wake atajitetea kwa kiapo na kwamba watakuwa na mashahidi wanne na wanakusudia kuwaita wote mahakamani siku ya kujitetea.

Hakimu Simba alipanga mshtakiwa huyo aanze kujitetea Machi 7, mwaka huu.

Kubenea, ambaye alipandishwa kizimbani, mahakamani hapo Desemba 15, mwaka jana, anadaiwa kumtolea DC huyo lugha ya matusi Desemba 14 mwaka jana wakati wakiwa kiwanda cha Tooku Garments kilichoko Mabibo External, Kinondoni, jambo ambalo lingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Anadaiwa kuwa siku hiyo alimuita Makonda kuwa ni “kibaka, mpumbavu na mjinga” na kwamba cheo chenyewe cha ukuu wa wilaya ni cha kupewa.

Wakati wa ushahidi wake, Makonda aliieleza mahakama kuwa alitumia nafasi yake ya ukuu wa wilaya kwenda kiwandani kwa lengo la kuzungumza na wafanyakazi waliokuwa wamegoma.

Mashahidi wengine wa upande wa mashtaka walikuwa ni maofisa wa polisi waliokuwapo eneo la tukio siku hiyo.

Alisema alipomaliza kuzungumza na wafanyakazi hao na kufunga kikao hicho, wakati anageuka alishangaa kumsikia mshtakiwa akimtukana.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazrui Ahojiwa na Jeshi la Polisi Zanzibar Na Kuachiwa Kwa Dhamana

$
0
0
Wakati polisi visiwani Zanzibar wakimhoji Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui jana, ulinzi uliimarishwa mjini Unguja huku askari wenye silaha na magari ya deraya wakifanya doria mitaani.

Mazrui, ambaye alifika makao makuu ya jeshi hilo saa 2:00 asubuhi akiambatana na wakili wake, ndiye aliyekuwa mkuu wa timu ya kampeni ya mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, katika uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, ambao chama chake kinaamini kuwa kilishinda.

Barabara zinazoelekea makao makuu ya polisi kutokea Jang’ombe, Kilimani na Bomani zilifungwa huku vikosi vya ulinzi na usalama vikiwa vimetapakaa maeneo hayo na mitaa mbalimbali mjini Unguja.

Wakazi wa Zanzibar wanaojiandaa kwa uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, kuanzia Jumatano mchana walishuhudia askari wenye sare wakiwa katika magari maalumu ya kijeshi wakirandaranda kwenye barabara za Unguja, hususan mitaa ya Ng’ambo kupitia Mnazi Mmoja, Darajani, Amani, Chumbuni na Mtoni kuelekea Bububu.

Wakati hali ikionekana hivyo mitaani, Mazrui alikuwa ndani ya Ofisi ya Upelelezi ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ziwani mjini Unguja ambamo alihojiwa kwa saa tatu na nusu.

Alianza kuhojiwa tangu saa 2.00 asubuhi kama alivyotakiwa na jeshi hilo kuripoti kupitia barua ya wito aliyotumiwa hivi karibuni, hadi saa 5.30

Hata baada ya kumaliza kuhojiwa, Mazrui aliyekuwa waziri wa biashara, alilazimika kubaki kituoni hapo akisubiri kukamilika kwa taratibu za dhamana. Aliruhusiwa kuondoka saa 6.40 mchana.

Pamoja na ulinzi kuimarishwa, mamia ya wananchi, hasa wapenzi, wanachama na wafuasi wa CUF, walifika makao makuu ya chama hicho yaliyoko Mtendeni ili kumpokea Mazrui akitokea polisi.

Baada ya kuachiwa kwa dhamana, Mazrui alisema alihojiwa na polisi kuhusu kauli aliyoitoa hivi karibuni alipokuwa Dunga Kiembeni, Wilaya ya Kati mkoani Kusini Unguja kwamba chama chake cha CUF kimechoshwa na vitendo vya hujuma na vya kihuni dhidi ya mali na ofisi zao.

“Naam, nimewaambia kwamba hiyo ni kauli yangu na niliyesema hayo ni mimi kuwa CUF tumechoshwa na uhuni huo,” alisisitiza Mazrui mara baada ya kuachiwa kwa dhamana ya masharti ya kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja wao kutakiwa kuweka hapo Sh500,000.

“Wamesema nimetoa kauli za uchochezi hivyo watanishtaki mahakamani na wamenitaka niripoti polisi Jumanne na Alhamisi.” Alisema

Naibu Waziri wa Afya Dr Kigwangala Azindua Wodi Mpya Ya Wagonjwa Mahututi Muhimbili.....Kasema Serikali ina Mpango wa Kuacha Kupeleka Wagonjwa Nje ya Nchi Kutibiwa

$
0
0
Serikali imesema ina mpango wa kusitisha kupeleka wagonjwa nje ya nchi kupatiwa matibabu na kuhakikisha kila kitengo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kinakuwa na chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).

Serikali imechukua uamuzi huo, wakati taarifa ndani ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto zikieleza inadaiwa deni la Sh.28.74 bilioni za malimbikizo kutokana na ongezeko la wagonjwa wanaopelekwa nje kwa matibabu.

Akizungumza jana wakati wa kuzindua chumba cha ICU kilichopo jengo la Mwaisela hospitalini hapo, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk Hamis Kigwangalla alisema lengo la Serikali ni kuanzisha vyumba hivyo kwa kila kitengo ili kupunguza vifo.

Alisema hospitali hiyo ina vitanda 25 vya ICU, lakini lengo ni kuwa na vitanda 150 vya wagonjwa mahututi na wataalamu wa kutosha.

Alisema Serikali ina mpango wa kutoa mafunzo kwa madaktari na wauguzi watakaokuwa wamebobea katika fani ya vyumba hivyo.

Madaktari na wauguzi hao watapata mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha Cairo na mengine yatatolewa kupitia Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (Muhas).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru alisema kuzinduliwa kwa ICU hiyo kunaifanya hospitali hiyo kuwa na vyumba vya aina hiyo viwili vyenye vitanda 25, kutoka chumba cha awali kilichokuwa na vitanda vinane.

Alisema uwapo wa vitanda hivyo ni ongezeko la asilimia 200 ikilinganishwa na uwezo wa awali.

“Fedha za ndani zilizotumika kwa ajili ya ukarabati wa chumba hiki ni Sh230 milioni ikiwa ni pamoja na kutafuta ufadhili kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya Ujerumani iliyowekeza vifaatiba vya Sh600 milioni.

‘‘Mfadhili huyu ndiye aliyetununulia vifaa vyenye thamani ya Dola 800,000 za Marekani,” alisema Profesa Mseru. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisisitiza jambo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi ya wodi ya ICU ilizopo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hosptitali ya Taifa ya Muhimbili MNH, Profesa Lawrence  Museru (katikati) akitoa maelezo mafupi jana Jijini Dar es Salaam kwa  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya  Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) wakati wa sherehe za uzinduzi wa wodi ya ICU iliyopo kwenye jengo la Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH)
Rais wa Shirika lisilo la Kiserikali la Madaktari wanaohusika na magonjwa ya ini na tumbo(Gastrenterology) kutoka Munich Ujerumani(kulia) akiteta jambo na  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya  Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa uzinduzi wa ICU Muhimbili.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya March 4

Madaktari 2 na Wauguzi 4 Wasimamishwa kazi Jijini Mwanza Kwa Kukataa Kumzalisha Mjamzito Ambaye Alijifungua Mapacha Wawili Chooni Wakafariki

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Baraka Konisaga, amemwamuru Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Adam Mgoyi kuwasimamisha kazi madaktari wawili na wauguzi wanne katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana iliyopo Kata ya Butimba kwa kushindwa kumuhudumia mama mjamzito aliyefikishwa hospitalini hapo na kusababisha kujifungua watoto mapacha na baadaye kufariki.

Hatua hiyo imesababishwa na tukio la mgonjwa Suzana John (27) mkazi wa Kata ya Mkolani kufikishwa na ndugu zake katika Hospitali hiyo, aliyekuwa mjamzito na kupokelewa na Dk Norin Magesa na Muuguzi, Janet Foya waliokuwa zamu ya usiku siku ya Machi Mosi, mwaka huu majira ya saa 4:00 usiku na kushindwa kumuhudumia zaidi ya kutoa lugha isiyoridhisha, pamoja na uzembe.

Akielezea tukio hilo, mwanamke huyo ( Suzan John ) alidai kuwa alianza kusikia uchungu na kuomba msaada kutoka kwa madaktari na wahudumu wa afya waliokuwa hospitalini hapo bila mafanikio.
 
“Nilifika nikiwa hoi, nikawaambia muda wangu tayari  lakini hawakunisaidia zaidi ya kunitolea maneno machafu.

"Wakati muda ukizidi  kwenda huku nikiwa sipewi huduma yoyote, nilihisi kubanwa haja ndogo hivyo nikaamua kwenda chooni .

Kule chooni mambo yakabadilika ghafla, mtoto wa kwanza akawa keshaanza kutoka.Bahati nzuri mle chooni kulikuwa na beseni

"Nililichukua lile beseni kwa ajili ya kuwaweka watoto huku niwakaita manesi.Manesi hao walikuja wakanichungulia halafu wakarudi. Akaja Nesi mmoja mwanafunzi, akakata kitovu akawaweka kwenye nguo, wakawa wamefariki,”Bi. Suzan alieleza kwa uchungu huku akilia.

Baada  ya mapacha hao kufariki, ndugu wa mwanamke huyo pamoja na wagonjwa wengine walioshuhudia mkasa huo walipandwa na hasira huku wakitaka kuwapiga wauguzi hao.

Taarifa za vurugu hizo zilimfikia DC Konisaga ambaye alifika hospitalini hapo  na kukutana kwa dharula na Mkurugenzi wa Jiji, Adamu Mgoyi, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Nyamagana, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa, Uongozi wa Hospitali na baadhi ya ndugu wa mgonjwa Suzana John aliyejifungua watoto mapach.

Katika kikao hicho cha dharura, walipokea maelezo ya pande mbili, kutoka kwa wauguzi na familia ya mgonjwa Suzana, na kupitia taarifa zilizokuwa zimeandikwa na Madaktari wawili waliomuona mgonjwa huyo, ndipo DC Konisaga akamuagiza Mkurugenzi Mgoyi na Kaimu Mganga Mkuu kuwasimamisha kazi madaktari wawili na wauguzi wanne ili kupisha uchunguzi wa kitaalamu juu ya tukio hilo.

Konisaga aliwataja wanaotakiwa kusimamishwa kazi kuwa ni Dk Magesa na muuguzi Foya waliompokea mgonjwa wakiwa zamu ya usiku wa Machi Mosi, mwaka huu na kushindwa kumpatia huduma zaidi ya kumtolea lugha chafu na uzembe huku wakishindwa kutoa maelezo wakati wa kukabidhi majukumu kwa madaktari na wauguzi walioingia zamu ya asubuhi ya Machi 2, mwaka huu.

DC Konisaga pia alieleza kuwa pamoja na kuingia kwa madaktari na wauguzi wa zamu ya asubuhi ya Machi 2, bado hawakumjali na kumhudumia mgonjwa huyo huku baadhi wakitoa lugha zisizo za faraja kwa ndugu wa mgonjwa. 

Hata alipozidiwa na kupewa taarifa na ndugu wa mgonjwa huyo, hawakufika na mara kadhaa walikuwa wakifika na kutoka bila kumudumia pamoja na kumsikiliza akilalamika.

Aliwataja wengine wanaotakiwa kusimamishwa kazi mara moja ni Dk Emiliana Mvungi, wauguzi ni Maria Mkankule, Suzana Sindano na Bibiana Moshi ambao walikuwa zamu na kutomhudumia mgonjwa ambaye alijifungua katika mazingira hatarishi akiwa Hospitalini hapo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo amemwagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk Rweyendela Onesmo ambaye ni Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa ya Sekou -Toure kupewa maelezo ya kina kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Nangi William na Mganga Mkuu wa Jiji, Dk John Andrew juu ya kushindwa kuchukua hatua pamoja na kupewa taarifa hizo.

Mulongo pia amemuagiza Dk Onesmo kuunda tume ya uchunguzi itakayoshughulikia suala la tukio hilo na kisha kukamilisha kazi hiyo kwa siku moja na kumpatia taarifa ili hatua kali za maadili ya utumishi wa umma zichukue mkondo wake ili pia kuwezesha kusaidia jinsi ya kuboresha utendaji wa kitaalamu na kitabibu katika hospitali hiyo ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kutokuwa na huduma nzuri kwa wagonjwa.

Magufuli Asema Mafisadi Wakimshinda Asiitwe Rais

$
0
0

Rais Dk. John Magufuli amesema amejitolea kuwa sadaka kwa  Tanzania katika vita dhidi ya mafisadi na kwamba akishindwa kufanya hivyo, hakuna sababu ya yeye kuitwa rais.

Pia amesema wote waliotumbuliwa majipu watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Akizungumza jana katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika sehemu ya barabara ya Sakina hadi  Tengeru yenye urefu wa kilomita 14.1, itakayokuwa na njia nne, alisema ataendelea  kutumbua majipu kwa kuwa wanaonufaika na kudidimiza uchumi wa nchi ni wachache.

“Tumeanza kuchukua hatua ndogo ndogo, tunatumbua majipu. Mpaka sasa waliotumbuliwa si wengi kiasi hicho, hawajafika hata 2,000. Juzi juzi nimesikia baadhi ya watu wameanza kuwatetea wanaotumbuliwa, nasema hao wanaowatetea washindwe na walegee,” alisema.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya, Makamu wa Pili wa Rais wa Burundi, Dk. Joseph Butore, Makamu wa Pili wa Rais wa Sudan Kusini, James Wani Igga, Balozi wa Japan nchini na mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Alisema wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida na taabu kutokana na wachache kufilisi mali na rasilimali za nchi.

“Ifike mahali mmoja lazima ajitolee kufanya kazi hii. Mimi nimeamua kuwa sadaka kwa Tanzania, lazima tufanye kazi ya kutumbua majipu na kuwaletea maendeleo wananchi.

“Nisipofanya hivyo, hakuna sababu ya mimi kuitwa Rais. Hii  nasema kwa dhati kabisa kutoka moyoni mwangu, naomba Watanzania waniombee,”alisema.

Alisema kwa mfano yapo mambo ya hovyo ambayo hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeisababishia serikali upotevu wa fedha za matumizi ya simu nje ya nchi husika (roaming) kiasi cha Sh. bilioni 200.

Alisema watu wote wanaojihusisha na ufisadi watafukuzwa na kufikishwa mahakamani mwishowe kufungwa ili nao wakapate machungu.

“Hii nchi ilifika mahali ikawa kama  shamba la bibi vile,” alisema na kusisitiza kuwa katika kuwaletea wananchi maendeleo hatafanya ubaguzi wowote kwa kuzingatia vyama, dini, kabila ila atachapa kazi tu.

“Nawaomba Arusha tujenge umoja wetu, tusibaguane. Tukianza kujenga umoja wa Tanzania na tukaunganishaa na umoja wa Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini, Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa na maendeleo ya kasi," alisema Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Aliongeza kuwa: "Tukiamua tunaweza kubadilika na kuwaletea wananchi wa jumuiya hii maendeleo makubwa.”
 
Alisema wananchi wa EAC wanachohitaji si vyama ila kazi, maendeleo na maisha mazuri na si kuwafanya wachache wawe wanafaidi kuliko wengine.

Awali, alimpongeza Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), kwamba ni mtu mchapakazi.

“Nampongeza sana Nassari, ni kijana safi anachotaka ni kazi na ameweza kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo lake.

"Sipendi kuwa mnafiki, nampongeza sana Nassari. Ukimtazama usoni Nassari ni Chadema lakini kwa kweli moyo wake uko CCM,” alisema na kufanya umati wa watu kulipuka kwa shangwe.

Mapema Rais Museveni alisema: “Tukiwa tunazungumzia uchumi wa kisasa, Afrika hakuna umaskini, ina utajiri mwingi wa raslimali isipokuwa inakosa maendeleo tu.

“Ardhi ipo, madini yapo, lakini tunashindwa kuzitumia, hivyo tunakosa maendeleo, tunakosa elimu na tuna afya duni,” alisema.

Aliwataka wananchi kujikita katika kilimo cha kisasa badala ya kulimia tumbo peke yake.

Museveni alisema sekta ya kilimo, viwanda, huduma na ICT, ndizo zinazoweza kuleta maendeleo kwa nchi za EAC.

Hata hivyo, alisema shida ya Waafrika ni kulala na kwamba wanalala huku kukiwa kumekucha na kusisitiza kuwa: 
 
“Tukiamka sisi sote tutakuwa na maendeleo kutokana na uzalishaji mkubwa utakaokuwapo," alisema.

Aliwaondoa wananchi hofu ya kupatikana kwa soko pale aliposema jumuiya hiyo ina watu zaidi ya milioni 160, hivyo idadi hiyo ni soko kubwa kwa bidhaa zitakazokuwa zikizalishwa na wananchi.

Kwa upande wake, Rais Kenyatta, alisema, viongozi wa jumuiya hiyo ndio waliofanya kazi ya kulala wakati kumekucha.
Alisema kazi kubwa waliyonayo wao ni kuwaletea maendeleo wananchi kwa kujenga miundombinu.

Aliwataka viongozi wenzake kubadilika badala ya kuwa na maneno mengi na kwamba sasa wawe watu wa kazi ambayo itawawezesha wananchi kupata maendeleo na kuyafurahia.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images