Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Profesa Muhongo apinga Tanesco kununua transfoma kampuni binafsi

0
0

Waziri wa Nishati ya Madini, Profesa Sospeter Muhongo amepinga uamuzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kutumia zaidi ya Sh15 milioni kununua transfoma katika kampuni binafsi badala ya kwenye Kiwanda cha Tanalec Limited ambacho shirika hilo lina hisa zake.

Profesa Muhongo alitoa uamuzi huo baada ya kutembelea kiwanda hicho jana akiongozana na maofisa wa Tanesco, Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) na maofisa wa wizara hiyo.

Katika ziara hiyo walibaini kuwa Tanesco hainunui transfoma katika kiwanda hicho.

“Kuacha kununua Transfoma Tanalec hakuna sababu nyingine zaidi ya rushwa na siyo kweli kuwa Sheria ya Manunuzi inawabana. Kama kweli inawazuia, suala hili nitalifikisha kwa Rais (John Magufuli) na katika ngazi nyingine za uamuzi,” alisema Profesa Muhongo.

Katika kiwanda hicho, Tanesco inamiliki asilimia 20 ya hisa, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) asilimia 10 na Kampuni ya Transcentury ya Kenya inamiliki asilimia 70.

Awali, kabla ya ubinafishaji Serikali ilikuwa ikimiliki asilimia 80 za hisa.

Kaimu Meneja Mwandamizi wa Manunuzi wa Tanesco, Jasson Katule alisema shirika hilo linashindwa kununua transfoma Tanalec kutokana na sheria kuwabana kwa kuwa inawalazimisha kutangaza zabuni.

Alisema katika zabuni, Tanalec ilishindwa na kampuni za Quality Group na Intertrade ya India.

Kampuni ya Quality Group itanunua transfoma za zaidi ya Dola 3 milioni za Marekani na Intertrade imeshinda zabuni ya Dola5 milioni za Marekani.

Awali, Meneja Mkuu wa Tanalec, Zahir Saleh alisema kiwanda hicho kwa sasa kina uwezo wa kuzalisha transfoma 10,000, lakini kinazalisha 7,000 kutokana na udogo wake.

Pia, alisema wanakabiliwa na changamoto za kukosa soko la ndani huku wateja wakubwa yakiwa ni mashirika ya umeme ya Kenya, Uganda na Zambia.

Kikwete akubali kuwa balozi wa chanjo Afrika

0
0

RAIS mstaafu Jakaya Kikwete amekubali uteuzi wa kuwa Balozi wa Heshima wa kuhamasisha masuala ya afya na kuwataka Wakuu wa Nchi za Afrika kuweka kipaumbele katika upatikanaji wa huduma za afya katika jamii.


Kikwete aliyasema hayo mjini Addis Ababa nchini Ethiopia juzi, wakati akitoa salamu zake baada ya kukubali kuwa Balozi wa Heshima wa ‘Africa United’ kupitia Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Gavi.

United Africa ni mpango uliobuniwa kusaidia uhamasishaji wa masuala ya afya ukiongozwa na Gavi, CAF, Umoja wa Afrika, Benki ya Dunia na CDC Foundation na wameamua kutumia michezo kama nyenzo mojawapo ya kufanya kampeni ya kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa masuala ya afya yanayolikabili bara la Afrika.

Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Jopo la watu mashuhuri la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya namna bora ya kuendeleza na kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu hususani katika afya ya uzazi ya mama na mtoto, alisema upatikanaji wa chanjo utasaidia kuokoa vifo vingi vya watoto Afrika.

Uteuzi huo umekuja huku Rais huyo mstaafu akiteuliwa pia kuwa Mjumbe Maalumu wa AU nchini Libya.

Dr. Bana: CCM Iheshimu Mfumo wa vyama Vingi

0
0

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mambo ya kijamii Dk Benson Bana amesema chama tawala nchini CCM lazima kikubali utamaduni na kanuni za kukubali mfumo wa vingi vya siasa.


Ameyasema hayo alipokuwa akizungumzia suala la upatikanaji wa Meya wa jiji la Dar es salaam ambapo limegubikwa na mambo ya siasa zizizofaa kwa maendeleo ya wananchi na wapenda demokrasia nchini.

''Kauli za mvutano na malumbano ya UKAWA na chama cha mapinduzi havitasaidia wananchi kwanza wanajidhalilisha, kinachotakiwa ni upinzani kutumia busara lakini chama tawala pia watambue kwamba walipokubali mfumo wa vyama vingi lazima wakubali mabadiliko na kuheshimu mfumo wa vyama vingi

"Hakuna sababu ya msingi ya kuwepo malumbano hadi watu wengine wapigwe na wengine kuwekwa rumande kwanza kazi kubwa ya umeya ni kuongoza vikao ingelikuwa tunatafuta mkurugenzi hapo sawa lakini hili wanakosea kwa kweli''-Amesema Dkt. Bana

Meya wa jiji la Dar es salaam ameshindwa kuchaguliwa mara kadhaa pamoja na kuwepo kwa uhalali wa kufanyika uchaguzi huo jambo ambalo limesababisha malumbano makali na kushikiliwa kwa wabunge wawili wa Chadema Saed Kubenea na Halima Mdee.

CHADEMA Kususia ziara na Vikao vya Maendeleo Dar es Salaam

0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesusia ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika manispaa za Temeke, Kinondoni na Ilala na kuthibitisha kutoshiriki katika kikao cha bodi ya barabara kinachotarajiwa kufanyika leo kwa kile wanachodai kushinikiza kuachiwa kwa madiwani na mbunge ambao wanaeshikiliwa na jeshi la polisi.

Akielezsea hatua hiyo jana, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob alisema kuwa hawaoni sababu ya kuendelea na vikao mbalimbali vya jiji wakati hawajui hatma ya wenzao ambao mpaka sasa wanashikiliwa na polisi na wengine wanaitwa kufika kituoni hapo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kusababisha fujo katika zoezi la uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Kikao kikubwa cha kujadili mipango ya maendeleo ya jiji la Dar es Salaam kinatarajiwa kufanyika leo  ambapo mada kuu itakuwa ni ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Polisi Wafanya Upekuzi Nyumbani Kwa Halima Mdee

0
0

Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam jana lilifanya upekuzi mkubwa katika nyumba ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) baada ya kumtilia shaka kuwa na nyaraka muhimu za vikao vya uchaguzi wa Meya wa Jiji hilo.

Kikosi cha jeshi hilo kilifika katika nyumba ya mbunge huyo majira ya saa tisa alasiri na kufanya mazungumzo na Mwanasheria wake, John Mallya ambapo baada ya kukamilisha taratibu za kisheria walianza zoezi la upekuzi uliochukua zaidi ya saa moja.

Kiongozi wa kikosi hicho cha Polisi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa walilazimika kufanya upekuzi katika nyumba hiyo baada ya kusadikika kuwa wakati wa vurugu zilizotokea katika ukumbi wa Karimjee jijini humo wikendi iliyopita kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji, Mdee aliondoka na faili muhimu lenye madokezo yanayohusu uchaguzi huo.

Hata hivyo, baada ya kukamilisha upekuzi huo, Polisi walijiridhisha kuwa hakukuwa na nyaraka hizo ndani ya nyumba hiyo wala kitu chochote ambacho wangekitilia shaka licha ya kukuta nyaraka nyingi za mbunge huyo. Hivyo, walitoa cheti maalum cha kuthibitisha kuwa hakuwa na nyaraka zozote kinyume cha sheria.

“Wamekagua nyaraka zote. Madai yao ni kuwa Halima alimpora au alichukua nyaraka za kiongozi wa Jiji, lakini wamekuta hakuna jambo lolote ambalo linatiliwa shaka. Na wametoa Certificate inayoonesha kwamba hakuna chochote ambacho kimechukuliwa,” alisema Mwanasheria wa Mbunge huyo, John Mallya.

Mdee alishikiliwa na Polisi na kulala rumande juzi kutokana na tuhuma za kushiriki katika vurugu zilizotokea katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Jumamosi, Februari 27.

Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi ni Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

Lowassa Azidi Kuipasua CCM

0
0

Uamuzi wa Edward Lowassa kujiondoa CCM na kujiunga Chadema, bado unakitesa chama hicho tawala baada ya mikoa kuanza kuwashughulikia viongozi waliomuunga mkono wakati wa Uchaguzi Mkuu, huku baadhi wakisema wako tayari kupambana na wanaowatuhumu kusaliti chama.

Lowassa alijiengua CCM Julai mwaka jana baada ya jina lake kuondolewa kwenye mbio za urais kwa tiketi ya chama hicho, na baadaye kufuatwa na mawaziri, wabunge, wenyeviti wa mikoa na madiwani na hivyo kufanya Uchaguzi Mkuu kuwa na ushindani mkubwa.

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, viongozi na wanachama wa CCM walioonekana kuwa karibu na waziri huyo mkuu wa zamani, walituhumiwa kukihujumu chama kwa kumpigia kampeni Lowassa wakati wa usiku, huku mchana wakijionyesha kuwa wanaunga mkono wagombea wa CCM.

Tuhuma hizo ziliongezewa nguvu na mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete takriban wiki mbili zilizopita alipotangazakuwa waliosaliti chama hicho watatumbuliwa bila ya aibu, na tayari mkoa wa Manyara umeshatangaza kuwatimua uanachama viongozi 21 wanaotuhumiwa kushabikia upinzani.

Viongozi wa mikoa  wamekanusha tuhuma zinazoelekezwa kwao kuwa walisaidia upinzani wakati wa uchaguzi wa mwaka jana.

Miongoni mwa wanaotuhumiwa ni mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu ambaye aliangushwa kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho na Frederick Mwakalebela, ambaye pia alishindwa na Mchungaji Peter Msigwa kwenye kinyang’anyiro cha ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini.

Mwenyekiti huyo anatuhumiwa kubadili timu yake ya kampeni na kuifanya iwe ya kumpigia debe mgombea huyo wa Chadema.

Lakini Msambatavangu, ambaye pia anadaiwa kutoa gari zake zitumike kwenye kampeni za wapinzani, alisema yupo tayari kuhojiwa ili ajibu tuhuma dhidi yake ambazo tayari zimewasilishwa kwenye chama hicho.

Alisema anasubiri ahojiwe ili aeleze ukweli kuhusu suala hilo.
Mwakalebela alifungua kesi Mahakama Kuu akidai kuwa taratibu zilikiukwa wakati wa kuhesabu kura.

Mwingine anayezungumzwa ni mwenyekiti wa CCM wa Simiyu, Dk Titus Kamani, ambaye alikuwa Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo katika Serikali iliyopita, ambaye amezielezea tuhuma dhidi yake kuwa ni majungu ya wasiompenda ambao wanataka avuliwe uongozi.

Dk Kamani anadaiwa kuwawezesha kwa hali na mali baadhi ya wagombea wa upinzani, kama kutoa vyombo vya matangazo na gari lake wakati wa kampeni.

Ilidaiwa kuwa kutokana na msaada huo, wagombea wa upinzani walishinda katika kata ya Lamadi na Mkula.

“Matokeo ya uchaguzi yanaonyesha wazi kuwa wanaCCM kwa ujumla walikuwa na umoja,” alisema Dk Kamani.

“Majimbo mawili kati ya saba kwenye mkoa huu yalikuwa yanashikiliwa na upinzani, lakini tumefanikiwa kuyakomboa. Hata kata nyingi zilikuwa ngome ya upinzani, lakini tumezikomboa. Sasa kama zilizopotea hizo mbili, mimi nahusika vipi?”

Tuhuma kama hizo zilielekezwa kwa Profesa Juma Kapuya, ambaye licha ya kupitishwa na CCM kugombea ubunge wa Jimbo la Kaliua, anatuhumiwa kujinadi yeye na Magufuli, lakini akatumia usiku kumuombea kura Lowassa aliyegombea urais kwa tiketi ya Chadema.

Profesa Kapuya, ambaye aliangushwa kwenye jimbo hilo na Magdalena Sakaya wa CUF, alisema anaijua vyema CCM, hivyo asingeweza kufanya usaliti na kuendelea kubaki ndani ya chama hicho.

“Mungu pekee ndiye anayejua jinsi nilivyojituma kumuombea kura Dk Magufuli aliyekuwa mgombea wetu ambaye ameshinda na kuwa Rais. Sijui wanaonituhumu wanaanzia wapi,” alisema Profesa Kapuya.

Alisema hakukuwa na muda wa kufanya usaliti kwa sababu alikuwa anaachana na kamati ya kampeni usiku mara baada ya kumaliza vikao vya tathmini ya mikutano ya hadhara.

“Mtu kama mimi nitawezaje kufanya usaliti kama huo. (Nikifanya) Basi hapo shule itakuwa haijanisaidia,” alisema Profesa Kapuya ambaye amebobea kwenye elimu ya mimea.

“Pia ninaijua vyema CCM. Huwezi kuwa msaliti ukabaki kuwa salama huku ukiendelea kubaki hivyo. Ningejitoa mwenyewe.”

Tayari viongozi 21 wa Manyara wametimuliwa kwa tuhuma hizo.Kati ya waliotimuliwa, watatu ni kutoka Babati Mjini na wengine 18 wa ngazi ya kata.

Inadaiwa kuwa viongozi waliotimuliwa walikuwa wanamshabikia Lowassa na kusababisha CCM kupoteza jimbo na kata tano kati ya nane za Babati Mjini, kwa mujibu wa katibu wa CCM wa Manyara, Ndeng’aso Ndekubali.

Wauguzi sita Temeke wasimamishwa Kazi kwa kuuza gloves

0
0

Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamis Kigwangalla amewasimamishwa kazi wauguzi sita katika hospitali  ya  Temeke kwa kosa la kuomba rushwa.

Wauguzi waliosimamishwa ni Hadija Salum, Beatrice Temba, Agnes Mwampashe, Elizabeth Mwilawa, Mariam Mohamed na Marion Said, ambao walikuwa zamu katika wodi ya wajawazito wakati wa tukio hilo.

“Nimewasimamisha kazi wauguzi wote waliokuwa zamu jana (juzi) asubuhi, nakuagiza Msajili wa Baraza la Wauguzi uwasimamishe hadi utakapowasafisha kupitia kamati ya msajili,” alisema Dk Kigwangalla.

Mmoja wa wajawazito, Loshan Seif alisema alipowasili juzi asubuhi kwa ajili ya kujifungua, muuguzi mmoja wa zamu alimtaka kulipia Sh5,000 za gloves.

“Siku zote huwa natumia bima lakini jana (juzi) wakaniambia hawatumii, nitoe Sh5,000 za gloves, baadaye niliambiwa natakiwa kuwa na uzi wa mshono, sindano na vingine hivyo kama sina nitoe fedha,” Seif.

Dk Kigwangalla alifanya ziara ya ghafla hospitalini hapo jana saa 9.00 alasiri.

Akizungumza jana alasiri baada ya kufanya ziara ya ghafla Hospitalini hapo na kupata malalamiko hayo kutoka kwa wanawake waliojifungua.

“Mama anaambiwa atoe fedha ya gloves Sh5,000 wakati dukani zinauzwa Sh1,000, nataka liwe fundisho kwa wote wanaotuongezea vifo vya wajawazito kwa tamaa ndogondogo,” alisema Kigwangalla.

Katika ziara hiyo, Dk Kigwangalla alishuhudia ubovu wa vyumba viwili vya upasuaji na kutoa maelekezo kwamba, virekebishwe ndani ya miezi sita.

“Hali ni mbaya ndani ya hizi ‘theater’ zote mbili zifanyiwe ukarabati iwapo itashindikana nitazifunga, lazima ziwe na hadhi yake na nitakuja kukagua,” alisema.

Seleiman Jafo Amemvua Madaraka Meneja wa Mamlaka ya Maji Mji Mdogo wa Kisarawe

0
0

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleiman Jafo amemvua madaraka Meneja wa Mamlaka ya Maji Mji Mdogo wa Kisarawe mkoani Pwani, Listen Materu kwa kile alichodai ameshindwa kusimamia majukumu yake kikamilifu.

Pia, Jafo ameuagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuondoa kero zinazolalamikiwa na wananchi hasa idara za ardhi, afya na elimu.

Akisikiliza kero za wapigakura wake juzi, Jafo alisema uchunguzi alioufanya ameubaini kwa miaka mitano iliyopita kuwa baadhi ya watendaji wa vitengo na idara wa halmashauri hiyo walikuwa hawawajibiki kwa makusudi, lengo lao lilikiwa ni kujenga chuki baina ya mbunge na wananchi jambo ambalo limefikia kikomo.

“Kuna watu waligeuza wilaya hii kama shamba la bibi, walikuwa wanatumia mali za umma kwa kufanya ubadhirifu sasa wasiseme kuwa wamesalimika, kama wamehama au wamehamishwa tutawafuata kokote walipo na watawajibishwa kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Naibu waziri huyo alisema, kuwavua madaraka na kuwawajibisha watendaji wabovu hakutaishia kwa watumishi waliopo wilayani hapa, bali hata waliofanya ubadhirifu na kuhama au kuhamishiwa maeneo mengine.

Katika kuboresha wilaya hiyo na kuharakisha maendeleo, Jafo alisema ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha inatenga maeneo ya ujenzi wa stendi, machinjio na utekelezaji wake ufanyike haraka na kuwataka iwapo watakabiliwa na changamoto za kukwamishwa mpango huo wasisite kuwasiliana naye.

Kiwanda cha Vipodozi Feki chanaswa Kigamboni Dar

0
0

Mamlaka ya chakula na dawa nchini Tanzania TFDA imebaini kuwepo kwa kiwanda bubu kinachozalisha bidhaa za vipodozi nchini Tanzania zenye lebo ya SAME inayoonesha kutengenezwa nchini Uturuki kinyume na sheria na taratibu za kuanzisha kiwanda na bila kukaguliwa na mamlaka hiyo kama ni salama kwa matumizi ya binaadamu.

Akiongea hii leo mkurugenzi wa TFDA Hiti Silo amesema kuwa awali walikamata shehena ya chupa 5,350 za pafyumu zenye thamani ya shilingi milioni 107 na walipomuuliza mmiliki wa duka hilo Dr Mohamed Gwao akasema bidhaa hizo zimeagizwa toka nchini Uturuki lakini walipofuatilia wakagundua zinazalishwa hapa nchini maeneo ya Mbagala Tuangoma

Aidha mamlaka hiyo ilipotembelea eneo hilo ilibaini mitambo mikubwa ya kuzalisha pafyumu hizo na kuchukua vifaa vyote kwa ajili ya kuvifanyia uchunguzi zaidi na watuhumiwa wamefikishwa kituo cha polisi.

Mamlaka ya chakula na dawa nchini inawatahadharisha watumiaji wote wa pafyumu hizo kuacha kutumia mara moja kwani bidhaa hizo hazijasajiliwa na TFDA na hivyo ubora na usalama wake haufahamiki.

Mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali Akamatwa..

0
0
Picha ya maktaba
 
Jeshi la Polisi  Mkoani Morogoro, wilayani Kilombero  jana  lilimkamata mbunge wa jimbo la Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali kwa madai ya kutaka kuingia katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kuapisha na kuchagua mwenyekiti na makamu wake wakati si mpigakura.

Lijualikali alikamatwa nje ya ukumbi wa halmashauri na polisi na kuswekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Kilombero saa 3.48 asubuhi wakati akiingia kwenye ukumbi huo kama mmoja wa mashuhuda.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilombero, Shabaan Mikongolo alisema mbunge huyo hakutendewa haki na polisi kwa kuwa alifika eneo hilo kushuhudia matukio ya kuapishwa kwa madiwani.

“Ni kama kuna maelekezo yalitolewa kwa polisi kuwazuia wabunge, Lijualikali na Devotha Minja (Viti Maalumu – Chadema) na mwakilishi wa Katibu Mkuu Chadema kutoingia ukumbini lakini viongozi wengine wa Serikali ngazi ya mkoa na wilaya waliruhusiwa." Alisema Mikongolo

Pia, polisi walizuia waandishi wa habari na kutaka kuwanyang’anya kamera zao kwa sababu ambazo hazikuwekwa bayana.

Katika uchaguzi huo, Diwani wa Sanje (CCM), David Ligazo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombero kwa kura 19 dhidi ya Godfrey Lwena ( CHADEMA)  aliyepata kura 18

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 2

Polisi ,UKAWA Ngoma Nzito........Naibu Katibu Mkuu CUF Nassor Ahmed Mazrui Naye Atakiwa 'Kujisalimisha' Polisi Kwa Mahojiano

0
0

Jeshi la Polisi limeendelea na kamatakamata ya wapinzani wa vyama vinavyounda Ukawa katika maeneo mbalimbali likieleza sababu tofauti za kijinai zinazohusishwa na masuala ya kisiasa.

Mpaka sasa wabunge wa upinzani waliokamatwa ni; Halima Mdee (Kawe), Mwita Waitara (Ukonga) na Peter Lijualikali (Kilombero), wote wa Chadema na baadhi ya madiwani wa chama hicho katika Jiji la Dar es Salaam.

Vilevile, imeelezwa kuwa Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alikuwa anatafutwa kuunguanishwa na wenzake.

Pia, baadhi ya wanasiasa wa CUF Zanzibar wamekamatwa na kuhojiwa kwa madai ya kuwatusi viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). 

Viongozi wa CUF waliohojiwa na polisi mpaka sasa ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Omar Ali Shehe na Kiongozi wa Mkakati wa Ushindi, Mohamed Sultan Mugheir ‘Eddy Riyami’ ambaye yuko nje kwa dhamana.  

Mbali na viongozi hao, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui  jana  amepatiwa barua ya wito  na Polisi Zanzibar  ikielezwa kuna mambo yanamhusu.

Hii ni mara ya pili kwa Mazrui kuitwa polisi tangu kufutwa kwa uchaguzi wa Oktoba 25, huku CUF ikidai kuwa huo ni mwendelezo wa mkakati maalumu dhidi ya viongozi wa chama hicho. 
 
Jana, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma wa CUF, Maalim Hamad Masoud Hamad alidai kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya kisiasa ya kutaka kumkamata kila kiongozi wa juu wa CUF kuelekea uchaguzi wa marudio.

“Kwa viongozi wa CUF hili halishangazi, nahisi ingelikuwa ni hatua ya kushangaza sana iwapo wanaoitwa kuhojiwa na polisi ni viongozi wa vyama vingine.

"Sisi upande wetu hili ni jambo la kawaida mno na watu wasishangae,” alisema.

Mazrui ambaye pia alikuwa Waziri wa Biashara na Uwekezaji, ametakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi, Ofisi ya Upelelezi Ziwani mjini hapa kesho saa 2.00 asubuhi na kuonana na mkurugenzi wa makosa ya jinai Zanzibar.

Polisi Zanzibar imethibitisha kuwapo wito huo ikisema kuna mambo muhimu yanayomhusu mwanasiasa huyo.


Halima Mdee (Kawe) na Mwita Waitara (Ukonga) na Makada Wengine Watatu Wafikishwa Mahakamani Leo

0
0

Mbunge wa Kawe Halima Mdee na wenzake wanne  wamefikishwa mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam na kusomewa  shitaka moja la kumjeruhi katibu tawala wa mkoa wa Dar es salaam

Halima Mdee akiwa na mbunge mwenzie Mwita Waitara wa jimbo la Ukonga  pamoja na makada wengine watatu wa Chadema  wamekana shitaka hilo na wametakiwa kujidhamini wenyewe kwa kiasi cha Shilingi Milioni mbili kila mmoja.

Mahakama hiyo imewaachia kwa dhamana baada ya kuweza kujidhamini

TCRA Yakunjua makucha......Yazifungia na Kuzipiga Faini Kampuni za Azam Marine na RIFARO AFRICA Kwa kuendesha Biashara Bila Leseni

0
0

MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imeipiga faini ya milioni 10 kampuni ya biashara ya mtandao – RIFARO AFRICA na pia  imeizuia kuendelea na huduma kwa madai ya kutokuwa na leseni.

Aidha TCRA imeeleza kushangazwa na taarifa zinazotangazwa katika vyombo vya habari na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, kampuni hiyo inafanya shughuli zake kutokana na leseni namba 178933 pamoja na cheti cha TCRA namba 15420.

Akizungumza hii leo Makao Makuu ya TCRA Dk. Ally Yahaya Simba Mkurugenzi, Mkuu wa TCRA amesema, baada ya TCRA kuona taarifa hizo za upotoshaji, iliamua kuihoji kampuni ya RIFARO na kuifanyia uchunguzi ambapo walibaini kwamba haina uhalali.

“28 Julai 2014 TCRA ilitoa cheti cha matumizi ya rasilimali masafa kwa ajili ya huduma ya ziada za mawasiliano kupitia SMS namba 15420 ili kutengeneza mfumo wa kuunganisha taarifa za mawakala wao kuuza na kusambaza muda wa maongezi kupitia wavuti.

“Cheti hicho kilimalizika 27 Julai 2015 na kampuni hiyo haikuomba kibali tena cha kuendesha biashara yoyote na hivyo inachokifanya sasa hivi ni kinyume na kanuni ya 17(1) ya Mamlaka ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011,” ameeleza Dk. Simba.

Ameongeza kuwa, TCRA ilitumia sheria yake sura ya 172 kama ilivyorekebishwa na kifungu cha 179 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta na kuitaka kampuni hiyo ijitetee kwanini ischukuliwe hatua, ambapo ilikiri makosa yake yote.

Makosa ambayo RIFARO AFRICA imekiri katika shauri baina yake na TCRA mnamo 24 Februari 2016 ilipohojiwa ni pamoja na kufanya biashara bila kuwa na kibali, kwani cheti namba 15420 kilikuwa kimeisha muda wake tangu Julai 2015.

Lakini pia RIFARO imekiri kuingia mkataba wa kibiashara na kampuni ya Zanzibar Telecom Limited (ZANTEL) kwaajili ya huduma ya Ezzy Pesa kama mtoa huduma mkubwa “mobile money super dealer” kinyume na sheria.

“Kutokana na makosa hayo tunaitaka RIFARO isitishe mara moja biashara inayoiendesha kwa kutumia rasilimali namba 15420 kwani haina kibali lakini pia tunaipiga faini ya shilingi milioni 10 za kitanzania kwa kuendesha shughuli zake bila kibali”. Amesema  Dk. Simba.

Mbali na kampuni hiyo, TCRA pia  imeshusha rungu kwa Kampuni ya Azam Marine Company Limited  ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara Saed Salim Bakhresa kwa kuitaka kuacha mara moja kuendesha shughuli za kiposta za kusafirisha vifurushi na vipeto baada ya kubainika wanafanya hivyo bila kuwa na leseni na kibali cha TCRA, hivyo kuikoseha serikali mapato

Vilevile TCRA imeipiga faini ya shilingi milioni 5 kampuni hiyo kutokana na kufanya shughuli hizo kinyume cha sheria

Vodacom, Tigo, Airtel, Smart na Zantel Zapigwa Faini ya Mamilioni ya Pesa Na TCRA Kwa Kutoa Huduma Mbovu za Mawasiliano

0
0

Kufuatia malalamiko kuhusu huduma duni za mitandao ya simu nchini, Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imezitoza faini kampuni kwa kushindwa kuwajibika katika huduma zao.
 
Kampuni za simu zilizopigwa faini kutokana na kutoa huduma mbovu ni pamoja na Airtel, Smart, Tigo, Vodacom na Zantel. Pamoja na hivyo, zimetakiwa kuboresha huduma zake ndani ya miezi sita.

TCRA imefanya tathimini juu ya ubora wa huduma za mawasiliano ikiwemo sauti na data zinazotolewa na kampuni hizo ambapo imebainika kutowatendea haki watumiaji wake.

“TCRA inazipiga faini kampuni hizi zinazoanzia milioni 12.5 mpaka milioni 27.5 na inazitaka kuboresha huduma zao, miezi sita tangu siku ya kutolewa kwa tangazo hili,” imeeleza sehemu ya taarifa ya TCRA kwa vyombo vya habari.

Usumbufu unaotajwa na TCRA ambao unafanywa na mitandao hiyo ni pamoja na kudai namba haipatikani ilihali ipo hewani, kudai namba inatumika ilihali sivyo, kukata salio la mteja pasipo ridhaa yake na kukatika kwa mawasiliano mara kwa mara.

Kampuni ya Vodacom ndiyo iliyopigwa faini kubwa zaidi (milioni 27.5) huku Kampuni ya Smart ikipigwa faini ndogo zaidi (milioni 12.5), faini hizo zimetozwa kulingana na ukubwa wa makosa ambayo kampuni husika imekuwa ikiyafanya katika utoaji wa huduma zake.

Kampuni ya Airtel imepigwa faini ya Sh. 22.5 milioni, Zantel Sh. 25 milioni na Tigo Sh. 25 milioni. TCRA imezitaka kampuni hizo kulipa faini hizo haraka iwezekanavyo na kuboresha huduma zao kabla ya mamlaka hiyo kuchukua hatua kali zaidi.

Kwa mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Sura ya 306 mamlaka hiyo hapa nchini inayo mamlaka ya kutoa adhabu kwa kampuni yoyote inayokiuka masharti ya leseni ya utoaji huduma.

Rais Wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein Ashiriki Mkutano Wa 17 Wa EAC Arusha

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Museven baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC,(kulia) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC.

Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki wakisimama wakati wimbo wa umoja wa nchi hizo ukipigwa katika mkutano wa 17 wa EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto mkoani Arusha.
 
Miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania walioalikwa katika mkutano wa 17 wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto Hotel Mkoani Arusha,(katikati) Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini,akiwa na Mawaaziri wa Nchi za Jumuiya hiyo, (Picha na Ikulu.)

Rais Magufuli akutana na kufanya Mazungumzo na Rais Kenyatta na Rais Kagame

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kando ya Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Mkoani Arusha, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha mahusiano hususani katika masuala ya kiuchumi.

Baadhi ya maeneo waliyokubaliana kutilia mkazo katika mahusiano hayo, ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo inayounganisha nchi mbili ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kukuza biashara na kuzalisha ajira kupitia viwanda.

Rais Uhuru Kenyatta amesema amefurahishwa sana kuona Rais Magufuli yupo tayari kuhakikisha nchi ya Kenya na Tanzania zinakuwa karibu, na miradi ya maendeleo inaharakishwa.

"Kwa sababu nia yetu sisi ni kuona maendeleo ambayo yatagusa mwananchi wa kawaida, tumalize umasikini, uchumi ukue, na hivyo hatuwezi kufanya tukiwa tumetengana" Amesisitiza Rais Kenyatta.

Kwa upande wake Rais John Pombe Magufuli, amesema Tanzania na Kenya zina kila sababu ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara hasa katika ujenzi wa viwanda utakaozalisha ajira kwa kuwa watu wake ni wamoja.

"Wazee wetu Mzee Kenyatta na Mzee Nyerere walijenga mazingira mazuri ya kuwa na nchi hizi mbili wakati wakipigania uhuru, sasa sisi vijana wao ni wakati wetu kwenda mbele kwa ajili ya maendeleo" amebainisha Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amebainisha kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinajenga mahusiano na ushirikiano zinalenga kupata manufaa hayo ya kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake.

Ameutaja mradi mmojawapo kuwa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tanzania kwenda nchini Kenya kupitia Namanga, na akaongeza kuwa Tanzania itakapoongeza uzalishaji wa umeme na kuanza kuvuna gesi, itaiuzia pia Kenya, halikadhalika Kenya nayo itauza bidhaa zake Tanzania.

Kabla ya kukutana na Rais Kenyatta, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuzidisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda ambapo Rais Magufuli amemhakikishia kuwa serikali yake itakamilisha ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge" ili kurahisha usafirishaji wa bidhaa na watu.

Rais Kagame amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake bora uliolenga kuimarisha uchumi, ikiwemo kuimarisha bandari ya Dar es salaam ambayo Rwanda inaitegemea na ujenzi wa Reli ya Kati ambayo pia ni tegemeo kubwa kwa uchumi wa Rwanda.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiano, IKULU
Arusha- 02 Machi, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.

Sudani Kusini Yakubaliwa Kuwa Mwanachama Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.....Liberate Mfumukeko Ateuliwa Kuwa Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya Hiyo

0
0

Wakuu wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameikubalia Sudan Kusini kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo ya kikanda.

Mkutano wa kilele wa Jumuiya hiyo jijini Arushaleo  Jumatano (Machi 2) umepitisha  pendekezo la baraza la mawaziri juu ya uwanachama wa Sudan Kusini na pia hali ya usalama nchini Burundi.

Kikao hicho kilichodumu kwa muda wa takribani masaa matano kimelikubalia taifa hilo changa kabisa barani Afrika kuwa mwanachama wake wa sita, kuungana na Tanzania, Rwanda, Burundi , Uganda na Kenya.

Rais  Magufuli  ambaye ndiye  mwenyekiti wa kikao hicho, amewaambia wajumbe wa mkutano huo wa kilele kwamba sasa "Sudan ya Kusini ni mwanachama halali wa jumuiya" hiyo.

Mkutano huo pia umezungumzia kwa kina masuala ya maendeleo ndani ya jumuiya ikiwemo mipango ya kujengwa kwa viwanda vya nguo na bidhaa za ngozi ili kuondoa kabisa biashara ya uagizaji wa nguo kuukuu, maarufu kama mitumba, katika nchi hizo katika miaka michachache ijayo

Mkutano huo pia umeshuhudia uzinduzi wa pasi ya kusafiria ya kielektroniki itakayotumiwa katika eneo la Afrika Mashariki pamoja na mwongozo maalum wa kimaaadili katika biashara kwenye nchi wanachama wa jumiya hiyo.

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya jumuiya hiyo, Katibu Mkuu anayemaliza muda wake, Dk. Richard Sezibera, amesema kuwa jumiya hiyo inasonga mbele kwani itifaki mbalimbali zimepitishwa kuanzia ushirikiano katika soko la pamoja, ushuru wa forodha na sasa wanaelekea kufikia hatua ya Afrika Mashariki kuwa na sarafu moja itakayotumika katika nchi zote wanachama.

Amesema kuwa tayari jitihada zinaendelea katika kuondoa vikwazo mbalimbali katika sekta za mawasiliano, biashara na usafiri "ili kuwapa wananchi wa Afrika Mashariki fursa ya kuufurahia na kufaidi muungano" huo.

Katika mkutano huo, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi hakuhudhuria na badala yake alimtuma makamu wake wa pili, Joseph Butore, huku serikali ya Sudan Kusini ikiwakilishwa pia na makamu wa pili wa rais, James Waniiga.

Na katika hatua nyingine kikao hicho kimepitisha jina la Liberate Mfumukeko kutoka Burundi kuwa katibu mkuu mpya wa jumuiya  hiyo kuanzia Aprili 1 mwaka huu.

Waziri Mkuu Aanza Kutumbua MAJIPU Mkoani Simiyu

0
0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza kutafutwa kwa Ofisa Ardhi wilayani Busega aliyetoa hati na kibali cha kumuuzia Mtanzania mmoja mwenye asili ya Asia majengo yaliyokuwa yakitumiwa kwa ujenzi wa barabara ambayo yaligeuzwa shule.
 
Katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita mkoani Simiyu, Waziri Mkuu ameanza kusaka majipu kwa kuagiza kusakwa kwa mtumishi huyo wa umma.
 
Kwa mujibu wa Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni, majengo hayo yaliyokuwa yakitumiwa na kampuni ya ujenzi ya SK Investment Company Limited, yamebadilishwa hati na kuuzwa kinyemela kwa mtu aliyemtaja kuwa ni Mtanzania mwenye asili ya Asia.
 
Dk Chegeni alisema majengo hayo yalikuwa yakitumika na yanaendelea kutumika kama shule ya sekondari.
 
Akizungumzia sakata hilo, Waziri Mkuu Majaliwa aliagiza kusakwa kwa ofisa huyo ili aeleze kwa nini alitoa kibali na hati hiyo kinyume cha taratibu.
 
“Wacha hilo la mahakama likamilike, lakini huyu ofisa ardhi aliyetoa kibali na hati ya kumilikisha aradhi hiyo kwa Mhindi, asakwe ili aje aeleze nani amempa mamlaka hayo ya kutoa kibali na hatimiliki,” aliagiza Waziri Mkuu.

Meya wa Zamani wa Ilemela Henry Matata Afikishwa Mahakamani Kwa Matumizi Mabaya ya Ofisi

0
0

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mwanza, imemfikisha mahakamani aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata (63) na wenzake wawili wakikabiliwa na mashitaka ya kutumia vibaya madaraka.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo waliofikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Nyamagana ni aliyekuwa Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Justine Lukaza (42) na mfanyabiashara Hemedi Hamad (54).

Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Mwema Mella, alidai mbele ya hakimu Greyson Sumaye kwamba kati ya Juni mosi na Julai 31, mwaka 2014, washitakiwa hao walitumia vibaya madaraka kwa kutoa zabuni ya kutoza ushuru katika Kituo cha Mabasi cha Buzuruga kinyume cha utaratibu.

Alifafanua kuwa makosa waliofanya ni kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mamba 11/2007 na pia walikiuka sheria ya manunuzi ya umma namba 7/2011

 Wakati kesi hiyo inafikishwa mahakamani jana, mshitakiwa Lukaza hakuwepo, hatua iliyomfanya Mwendesha Mashitaka kuomba mahakama hati ya kumkamata.

Hakimu aliridhia ombi hilo na kesi hiyo ilioahirishwa hadi Machi 29 mwaka huu. Washitakiwa wawili waliokuwepo mahakamani walikana mashitaka hayo na wako nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images