Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya yateketea kwa moto

$
0
0
Askari wa Kikosi cha Zimamoto Jijini Mbeya, akiendelea na jitihada za kuuzima moto unaoendelea kuwaka na kuteketeza Mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga jijini humo, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa, na jitihada za kuuzima zinaendelea.
Kikosi cha Zimamoto Jijini Mbeya, kikiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya, wakiwa nje ya Shule yao wakiangalia bila kujua cha kufanya wakati Mabweni yao yakiteketea kwa moto.

Jeshi la Polisi Zanzibar Latoa Ufafanuzi Kuhusu Madai ya CCM Kutaka Maalim Seif Akamatwe

$
0
0

Jeshi la Polisi Zanzibar limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa jeshi hilo linapanga kumkamata Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Taarifa zinazosambaa kwa kasi mitandaoni  zinasema Maalim Seif anatakiwa kukamatwa kwa tuhuma zinazohusiana na kujitangazia ushindi katika uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 kama inavyoshinikizwa na Chama cha Mapinduzi Zanzibar. 
 
Akiongea  na mwandishi wa Dw, Issac Gamba, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishina Mkadam Khamis Mkadam, amesema yeye hajapata taarifa yoyote toka kwa wakubwa wake inayomtaka amkamate Maalim Seif.

Amesema jeshi la polisi ni taasisi kubwa inayohusisha viongozi mbalimbali, hivyo yaweza  kuwa amri kama hiyo imetolewa kwa viongozi wengine

==>Zaidi, bonyeza hapo chini kumsikiliza

Waziri Mkuu Aagiza Daktari Hospitali ya Ligula Mtwara Asimamishwe Kazi Kwa Kuomba Rushwa Ya Sh. 100,000

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kusimamishwa kazi kwa Dk. Fortunatus Namahala wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Ligula ambayo ni hospitali mkoa wa Mtwara kutokana na tuhuma za kumdai mgonjwa rushwa ya sh. 100,000/-.
 
Pia ametoa agizo la kufungwa kwa maduka yote ya dawa yaliyo nje ya hospitali hiyo kuanzia leo na kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Alfred Luanda asimamie zoezi hilo mara moja.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Februari 29, 2016) kwenye kikao cha watumishi wa hospitali hiyo alichokiitisha baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya hospitali hiyo na kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa na ndugu wenye wagonjwa waliolazwa.

Mara baada ya kuwasili, Waziri Mkuu aliamua kwenda mojamoja mapokezi badala ya wodini kama alivyopangiwa na kuuliza maswali ni kwa nini wana dirisha moja la kupokelea wagonjwa wote. “Dirisha la wazee lipo?” akajibiwa hakuna. “Dirisha wa watu wa Bima ya Afya (NHIF) lipo” nalo pia akajibiwa halipo. “Je wazee wana daktari wao”, hakupata jibu.

“Mganga Mkuu ni kwa nini hujatenga dirisha la wazee wakati haya maelekezo yalishatolewa siku nyingi? Tengeni dirisha la wazee  na uhakikishe wana daktari wao. Siyo kuwaleta huku ili waje kusukumana na wagonjwa vijana,”  alisema wakati akimwagiza Mgaga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Shaibu Maarifa.

Akiwa njiani kuelekea wodi aliyopangiwa kuiona, Waziri Mkuu alikutana na kundi la wagonjwa waliokuwa wakiimba “tuna jambo, tuna jambo” wakiashiria kutaka kusikilizwa. Kati ya wauguzaji watatu aliowasikiliza, Waziri Mkuu alipokea kero za kuuziwa dawa kwa bei za juu kwenye maduka ya dawa binafsi, lugha mbaya za madaktari na wauguzi, uchafu wa vyoo na uhaba wa maji.

Lakini kero ya Bi. Tatu Abdallah aliyelazimika kuuza shamba la baba yake ekari 2.5 ili apate fedha za kulipa gharama za kufanya upasuaji kwenye hospitali binafsi baada ya baba huyo kutimuliwa kutoka hospitali ya Ligula ndiyo ilimgusa zaidi Waziri Mkuu.
 
“Februari mosi nilimleta baba yangu hapa nikaambiwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji. Nikaandikiwa ninunuue dawa za sh. 85,000/- hapo nje (pharmacy haikumbuki jina) pia uzi wa kushonea kwa sh. 25,000/-. Lakini pia daktari akasema anataka sh. 100,000/- ya kwake. Lakini hadi Februari 7 hakufanyiwa huo upasuaji.”

“Tarehe 12 Februari  baba alitolewa wodini na kuambiwa arudi tarehe 16 Februari. Niliumia sababu kijiji tunachotoka ni mbali na hali ya baba ilizidi kuzorota. Ndipo baba akaniambia nirudi kijijini kwetu Kilomba nikauze ekari 2.5 za shamba lake ili tulipie matibabu. Niliuza na kumpeleka baba katika zahanati ya Sajora. Huko nililipa sh. 560,000/- na baba akafanyiwa upasuaji sasa hivi yuko nyumbani”.

“Leo nataka huyu daktari aje achukue boksi hili la dawa alizoniandikia na pia anirudishie hela yangu iliyopotea bure. Mie sijazitumia, ni kwa nini aliniandikia wakati baba hajampa huduma yoyote?” Alipoulizwa kama anaweza kumtambua akimuona, mama huyo alikiri kuwa anaweza.

Waziri Mkuu alitembelea pia wodi ya akinamama waliojifungua na kukuta wakiwa wametandikiwa shuka moja na wagonjwa kulazimika kuweka khanga juu ya mipira wanayolalia wodini ambayo pia wanaambiwa wajinunulie kabla ya kwenda hospitali kujifungua.

Akiwa njiani kuelekea theatre, Waziri Mkuu alipata kilio cha wagonjwa wengine ambao walisema hospitali hiyo haina maji, choo kinachotumika ni kimoja na kwamba usafi umefanyika leo waliposikia kuwa atatembelea hospitali hiyo.

Akiwa katika kikao na watumishi hao, Waziri Mkuu aliwainua madaktari wote ili wajitambulishe ndipo akamuomba mama aliyedaiwa rushwa aende kumshika mkono daktari mhusika.
 
“Gwaride la utambuzi ni jambo la kawaida. RPC hakikisha huyu mama hasumbuliwi. Lakini leo nitaanza na huyu Daktari kwa sababu rushwa haivumiliki. RAS simamia suala lake lakini pia shirikiana na TAKUKURU na Polisi kufanya uchunguzi wa jambo hili hadi mwisho,” alisema.

Kuhusu madai na stahili za watumishi, Waziri Mkuu amemwagiza RAS, RMO na Afisa Utumishi wa mkoa wafanye kikao na watumishi wote wa hospitali hiyo leo saa 9 alasiri na kisha wamletee taarifa.

Kabla ya kufikia uamuzi wa kumsimamisha Dk. Namahala, Waziri Mkuu alitumia muda mwingi kuwaelezea watumishi hao jinsi walivyo na umuhimu katika huduma zao na kwamba nafasi yao ni nyeti kwa maisha ya binadamu hivyo wanapaswa kuwa na huruma na siyo kuwaumiza wananchi wa kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

Aliwataka waache tabia ya kuwatoza fedha watoto wanaolazwa hospitalini hapo na wanawake wanaojifungua kwani wanapaswa kutibiwa bure kwa mujibu wa sera ya Serikali.

Sakata la hospitali ya Ligula lilianza juzi (Jumamosi, Februari 27, 2016) wakati Waziri Mkuu akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa ambapo baadhi yao walikuwa wakichomekea kuwa aende hospitalini hapo kwa kuwa kuna majipu ya kutumbua.

Waziri Mkuu aliwajibu kuwa amesikia ujumbe wao na ataenda huko lakini alishindwa kutokana na ratiba za siku hiyo kumalizika jioni sana.

Waziri Mkuu amerejea Jijini Dar es Salaam mchana leo.

Taarifa ya Bodi ya Utalii Nchini Kupinga Taarifa Zinazosambaa Kwamba Olduvai Gorge iko Kenya

$
0
0

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kufuatia video iliyotumwa katika YouTube
https://www.youtube.com/watch?=iveX49WE7fw na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba iko Kenya.

Video hii imeibua majadiliano katika mitandao ya kijamii baina ya watanzania na watu wengine ambao wanaitakia mema Tanzania na wanaoelewa vizuri kuwa Olduvai Gorge iko Tanzania.

Bodi ya Utalii Tanzania kama taasisi ya Umma yenye jukumu la kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii imeshtushwa na video hii iliyojaa upotoshwaji mkubwa ambao tunaamini mbali ya malengo mengine inalenga kuchafua kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau wengine katika kutamgaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge.

Tunapenda kuchukua fursa hii kupinga vikali upotoshwaji huu uliofanywa na mtu huyo wakati akihutubia mkutano ambao tumeambiwa ulikuwa ni wa Vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Amerika mwezi Agosti mwaka jana. 

Tunapenda dunia ifahamu kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zanzibar n.k Olduvai Gorge mahali panapoaminika kuwa ndipo binadamu wa kwanza duniani aliishi na ambako Dr. Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 2 iliyopita iko pia Tanzania na si mahali pengine popote duniani. Eneo hili la Olduvai Gorge liko katika bonde la ufa katikati ya bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Manyara nchini Tanzania.

Tunatoa wito kwa watanzania mahali popote walipo kuendelea kuunga mkono juhudi za Bodi ya Utalii Tanzania za kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii kwa kujibu na kusahihisha papo hapo bila woga mara tu taarifa ya upotoshaji kuhusu nchi yetu inapotolewa iwe ni kwenye mikutano ya ndani ya nchi au ya Kimataifa. 

Tunaamini kuwa ni jukumu la kila mtanzania kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii badala ya kuiachia TTB kazi hii peke yake.

Yawezekana katika mkutano huo wa vijana ambao mjumbe huyo wa nchi jirani alipata fursa ya kuzungumza na kufanya upotoshaji huzo, wajumbe wa Tanzania pia walikuwepo ambao wangweza kukosoa upotoshaji huo papo hapo na kuelezea ukweli na usahihi wa mahali ilipo Olduvai Gorge.

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano

BODI YA UTALII TANZANIA

Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti ya Uingereza-Jumanne March 1

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya KENYA Jumanne ya March 1

TANESCO Yawasilisha Maombi ya Kushusha Bei ya Umeme

$
0
0
SHIRIKA la Umeme (Tanesco) limewasilisha katika Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) maombi ya kushusha bei ya umeme kwa asilimia 1.1 pamoja na kuondoa kabisa gharama za maombi ya awali ya wateja wapya na gharama za huduma kwa wateja wa majumbani.

Gharama za maombi hayo ya awali ambayo pia yanajulikana kama gharama za fomu ni Sh 5,900 na gharama za huduma (service charges) ni Sh 5,520 kwa mwezi kwa wateja wa majumbani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanseco,  Felichesmi Mramba alisema kuwa kisheria maombi hayo yanatakiwa kujibiwa ndani ya siku 24 ambapo wanaamini kuwa watapata majibu mazuri.

Mramba alisema gharama za huduma zimekuwa zikiathiri sana watumiaji wa umeme wa majumbani tofauti na wanaotumia viwandani.

Mramba alisema kuwa maombi hayo yamewasilishwa baada ya Tanesco kufanya tathimini ya kina kimahesabu pamoja na kubuni namna ambayo wateja wao wataweza kupata ahueni ya gharama kwa kuzingatia mazingira ya sasa.

Alisema punguzo hilo la asilimia 1.1 ni kwa mwaka wa kwanza na matarajio ni kwamba mwaka wa pili, watapunguza kwa asilimia 7.9.

“Baadhi ya vyombo vya habari viitunukuu vibaya,hatuna mpango wa kupandisha bei ya umeme na wala serikali haijatulazimisha kushusha bei. Tunawahakikishia wananchi kuwa maombi yaliyotumwa Ewura ni kuondoa usumbufu wanaoupata watumiaji wa umeme wa majumbani,’’ alisema Mramba.

Alisema kwa mujibu wa sheria, Tanesco inapotaka kubadilisha bei, iwe ni kushusha au kupandisha ni lazima iwasilishe maombi hayo Ewura kwani ndiyo yenye mamlaka ya kisheria ya kubadilisha bei hizo.

Alifafanua kuwa Tanseco huwasilisha maombi yake pamoja na takwimu halisi zinazoshawishi mantiki ya kubadilishwa kwa bei hizo na kwamba maombi yaliyowasilishwa Ewura hivi sasa, ndio ilivyotakiwa.

Aliongeza kuwa baadhi ya mambo yanayoendana na mazingira ya sasa, ni pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme wa gesi, tofauti na ilivyokuwa hapo kabla. Pia alisema kuongezeka kwa ujazo wa maji katika mabwawa makubwa hasa Mtera, kunachangia Tanesco kushusha bei hizo.

Akizungumzia madeni ya Tanesco, Mramba alisema kuwa kiasi cha madeni yaliyotajwa na vyombo vya habari sio sahihi.

Alifafanua kwamba madeni hayo yamezingatiwa kikamilifu katika mapendekezo ya kushusha bei hivyo na si kweli kwamba kushuka kwa bei kutasababisha Tanesco kufilisika.

“Sio sahihi kusema kwamba serikali imeilazimisha Tanesco kushusha bei ya umeme na kwamba kwa kufanya hivyo shirika litafilisika. Tathimini tulioifanya ni ya kitaalamu na pia kwa mujibu wa sheria ya Ewura itafanya tathimini yake kabla ya kuidhinisha bei mpya,’’ alifafanua.

Wasaliti Ndani ya CCM Waanza Kutumbuliwa MAJIPU

$
0
0

Huku kukiwa na taarifa kuwa wasaliti wa CCM wanaotarajiwa kutimuliwa wengi ni watu maarufu hasa viongozi wa ngazi za mkoa, tayari viongozi 21 wa Manyara, wameshatumbuliwa majipu bila ganzi.

Jumla ya viongozi 21, watatu wakiwa ni wa CCM Wilaya ya Babati Mjini mkoani Manyara na wengine 18 wa ngazi ya kata, wameshaadhibiwa na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete alichokiita kutumbua majipu bila aibu.

Inadaiwa kuwa viongozi hao walikuwa wanamshabikia aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Imedaiwa ushabiki ulisababisha CCM ipoteze jimbo na kata tano kati ya nane za Babati Mjini.

Katibu wa CCM mkoani Manyara, Ndeng’aso Ndekubali aliwataja waliofukuzwa uanachama kuwa ni wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, Cosmas Masauda, Zulekha Mohamed na mjumbe wa mkoa, Felix Kivuyo.

“Hawa wamefutwa uanachama baada ya kudaiwa kukisaliti chama kwa kuwapigia kampeni wagombea wa vyama vya upinzani na kuwaombea kura kwenye Uchaguzi Mkuu,” alidai Ndekubali.

Februari 24, mwaka huu, Kikwete alipokuwa akizindua nyumba ya chama hicho Kibaha mkoani Pwani, alisema mwanachama yeyote aliyekihujumu chama chao kwenye uchaguzi wa mwaka jana, atatumbuliwa jipu bila aibu.

Kikwete alikaririwa akisema tayari CCM ina majina ya wasaliti wote na mchakato wa kuwaadhibu unaendelea kuanzia ngazi ya matawi, kata, wilaya mkoa na Taifa. Alisema viongozi hao wamekiuka ibara ya 93, kifungu cha 14 ya Katiba ya CCM.

“Halmashauri Kuu ya CCM mkoa, imewavua nyadhifa viongozi 18 wa ngazi za kata wilayani Babati Mjini kwa kukiuka maadili, kushiriki ubadhirifu wa fedha na kukosa uaminifu,” alisema Ndekubali.

Alisema viongozi 18 wa ngazi ya kata ambao walivuliwa nyadhifa zao na kubaki kuwa wanachama wa kawaida, ni makatibu wa kata tisa, wenyeviti wa kata nane na katibu mwenezi mmoja wa kata, wote wa Wilaya ya Babati Mjini.

Wafanyabiashara Wanaopandisha bei ya sukari kukiona

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala amewaonya wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda wanaoficha sukari na kupandisha bei, akisema watachukuliwa hatua za kisheria.

Makala alitoa onyo hilo jana alipotembelea Kiwanda cha Sukari cha TPC na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro.

“Kamati imejiridhisha kwa kuona uzalishaji na wingi wa sukari iliyopo.Watakaobainika kuagiza sukari nje ya nchi watachukuliwa hatua,” alisema Makala.

Aliwataka wafanyabiashara wasifiche sukari kwa kuwa TPC inazalisha ya kutosha kwa mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Alisema ni vyema kiwanda hicho kikafanyiwa upanuzi ili kuongeza uzalishaji ambao utasaidia kuongeza mahitaji ya sukari nchini.

Alisema uzalishaji mkubwa utaondoa mianya ya uingizwaji wa sukari za magendo.

Makala alisema Serikali ilikataza uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ili viwanda vya ndani viuze kwa wingi.

Meneja Uhusiano wa TPC, Jafary Ally alisema hawajapandisha bei na kwamba bei ya jumla kwa wasambazaji ni Sh1,750 kwa kilo huku wafanyabiashara wakubwa wakiuziwa Sh1,807.

“Kwa sasa uzalishaji unaendelea kwa kiwango kikubwa na hakuna uhaba wa sukari katika maeneo tunayohudumia na maghala yetu yamejaa kutokana na hapo nyuma soko lilinyumba.

“Sukari ilikuwa ikitoka nje bila kulipiwa kibali hali iliyosababisha tuuze chini ya kiwango cha uzalishaji,” alisema Ally.

Alisema kiwanda hicho kikipanuliwa kinatarajia kuzalisha tani 100,000 kwa mwezi tofauti na tani 95,000 wanazozalisha.

Polisi Yaua Majambazi Watatu....Baada ya Kupekeliwa Walikutwa na Ujumbe wa Kamanda Suleiman Kova

$
0
0

Watu watatu wanaosadikiwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi na ujambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na polisi.

Watu hao walikutwa na karatasi yenye ujumbe kwa aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ulioandikwa:

“Nasaha kwa Kova, mzee andaa kamati ya mazishi ya vipolisi vyako tukiwamaliza tutakufikia wewe.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema jana kuwa tukio hilo, lilitokea Jumamosi iliyopita, eneo la Fire, jijini Arusha wakati mtuhumiwa Athumani Kassim alipokamatwa eneo la Engosheraton akiwa na silaha na aliwataja wenzake.

Kamanda Sabas alisema walipopata taarifa kutoka kwa raia wema walio tilia shaka mwenendo wa mtuhumiwa huyo ambaye alipokamatwa, alikutwa na milipuko, makoti makubwa mawili na kofia ya kuficha uso.

“Baada ya mahojiano, alituambia kuna wenzake wawili anashirikiana nao kufanya uhalifu na tuliweka mtego.

“Saa 5 usiku, askari wetu wakiwa wameambatana na Kassim, walipofika jirani kabisa na nyumba hiyo eneo la Fire, alitoa ishara na wenzake wakaanza kuwashambulia polisi kwa risasi,” alidai kamanda huyo.

Hata hivyo, Sabas alisema polisi waliwazidi nguvu na kuwajeruhi wawili kati yao.

Hata hivyo, magaidi hao walimpiga mwenzao risasi na wao walifariki dunia walipokuwa wakipelekwa hospitali.

Alisema kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi, walikuta vitu mbalimbali ikiwamo sare tano za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kofia tano za kuficha nyuso, vazi moja la karate, pikipiki moja iliyobomolewa na imebandikwa namba bandia.

Alivitaja vitu vingine kuwa ni bendera mbili nyeusi zenye maandishi ya Kiarabu zinazotumiwa na makundi ya kigaidi.

Vitu vingine ni kisanduku cha chuma na hati ya kusafiria ya Abrahaman Athuman Kangaa, iliyotolewa Aprili 2, 2013, simu tano za mkononi na kati ya hizo, moja ilitambulika kuwa ni ya marehemu Mary Joseph aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Februari 20, mwaka huu, eneo la Engosheratoni pamoja na kifurushi cha unga wa baruti na jambia moja.

Miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa ajili ya utambuzi. 

Rufaa ya Babu Seya na Mwanaye Kuanza Kusikilizwa March 11 Mwaka Huu.

$
0
0

Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) katika kikao chake kilichoanza jijini Arusha, itapitia maombi ya rufani ya mwanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking na John Viking dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo jana, ilieleza kuwa kesi hiyo namba 006/2015 iliyopangwa kusikilizwa Machi 11 haitasikilizwa katika mahakama ya wazi.

Ni kesi mbili pekee kati ya 50 zitakazosikilizwa kwenye mahakama ya wazi, ikiwamo inayomhusu mwanasiasa maarufu wa Rwanda, Victoire Ingabire aliyoifungua kupinga ukiukwaji wa haki anaofanyiwa na Serikali yake.

Pia, mahakama ilieleza kuwa kikao hicho cha 40 cha kawaida kitakamilika Machi 18 na kutoa uamuzi wa mashauri manne.

Kesi ya Ingabire inayotarajiwa kuvuta hisia za watu wengi ikizingatiwa upinzani ambao amekuwa akiuonyesha dhidi ya serikali yake, itasikilizwa Machi 4.

Katika kesi hiyo, Ingabire pamoja na mambo mengine anadai haki zake kuvunjwa ambazo zinatajwa kwenye Mkataba wa Mahakama hiyo Ibara ya 7, 10 na 18 hivyo anaitaka itoe uamuzi.

Pia, Taasisi ya Action Pour la Protection des Droits de I’Homme (APDH) inaishtaki Serikali ya Ivory Coast kuvunja mkataba wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu Ibara ya 3 na 17 katika kesi namba 001/2014, iliyopangwa kusikilizwa Machi 3.

Mahakama hiyo inaundwa na majaji 11 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na inakuwa na vikao vinne kwa mwaka, kufikia Januari 31 tayari ilikuwa imepokea kesi 74 kati ya hizo 25 imetolewa uamuzi.

Maombi manne yamepelekwa  kwa uamuzi zaidi kwenye Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu.

Waziri Mkuu Kutua Jijini Mwanza Leo

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa leo anatarajia kuanza ziara ya siku 14 katika mikoa ya Kanda Ziwa kukagua shughuli na miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema Waziri Mkuu anayetarajiwa kufika Mwanza saa nane mchana, atatembelea mikoa ya Simiyu, Kigoma, Geita na Kagera.

“Ingawa hakuna ratiba ya kutembelea eneo lolote mkoani Mwanza, tumejipanga kila idara endapo atafanya ziara ya kushtukiza, tuko tayari,” alisema.

Wakati huohuo; Mulongo alisema mke wa Rais, Janet Magufuli anatarajiwa kutembelea Kituo cha Kulea Wazee Bukumbi kilichopo wilayani Misungwi.

“Ziara hii ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8, kila mwaka,” alisema Mulongo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Tanzania Jumanne ya March 1

Halima Mdee Atupwa Rumande......Mahakama yakana kuzuia uchaguzi wa Meya Dar

$
0
0

Wakati mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee akilala rumande akihusishwa na vurugu zilizotokea Jumapili wakati uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam ulipokwama, Mahakama ya Kisutu imelikana zuio lililotumika kuzuia shughuli hizo. 

Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Januari 23, mwaka huu, lakini uliahirishwa ili kuandaa mfumo bora wa upatikanaji wajumbe kutokana na CCM kutaka kuingiza wapigakura nje ya waliotakiwa.

Ulikwama tena Februari 8, baada ya Halmashauri ya Jiji la Dar kubaini kasoro ya nyongeza ya majina 14 ya wajumbe kutoka manispaa za Ilala na Kinondoni.

Jumapili iliyopita ilikuwa ni mara ya tatu, kukwama tena kutokana na zuio lililosababishwa na kesi iliyofungiliwa na Saad Kimji na Suzan Masawe.

Hata hivyo, zuio hilo la muda la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu lililotumika kuahirisha uchaguzi wa meya na naibu meya wa Jiji, uliopaswa kufanyika Februari 27, 2016 limebainika kuwa ni batili.

Jana, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Waliarwande Lema alisema Saad Kimji na Suzan Massawe walifungua kesi Februari 5, 2016 wakizuia uchaguzi wa meya na naibu wake ambao ulipaswa kufanyika Februari 8,2016.

Hakimu Lema alibainisha baada ya kufungua shauri hilo, Mahakama ya Kisutu iliweka zuio la muda ili kesi hiyo ianze kusikilizwa Februari 15, 2016 lakini walalamikaji hawakutokea mahakamani hivyo mahakama ikapanga kusikiliza kesi hiyo Februari 23, lakini hawakutokea pia.

Alisema kutokana na hali hiyo, aliliondoa shauri hilo mahakamani hapo na hivyo zuio hilo likawa limekufa. 

Aliongeza kuwa aliyesema Mahakama ya Kisutu imetoa zuio ni muongo na kwamba zuio halali ni lazima liwe na jina la Hakimu pamoja na sahihi.

Kukamatwa kwa Mdee 
Katika sakata la jana, Mdee na madiwani wengine watatu walilazwa rumande kutokana na kutuhumiwa kumshambulia Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando 

Wanatuhumiwa kufanya kosa hilo baada ya vuta nikuvute kutokea Jumapili iliyopita wakati shughuli ya kuwasaka viongozi hao wa jiji zilipokwaa kisiki kwa mara ya tatu, na CCM kuamua kukimbilia mahakamani.

Hali hiyo, ilizua tafrani kati ya madiwani na wananchama wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) baada ya uchaguzi huo kuahirishwa kwa zuio la muda la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. 

Tafrani hiyo ndiyo iliyosababisha vurugu ambazo inadaiwa kuwa katika purukushani hizo Mdee alimshambulia Mmbando mara baada ya kutangaza kuahirisha uchaguzi huo.

Polisi waliokuwa wanalinda usalama kwenye ukumbi wa Karimjee ambako uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika, walimtoa nje Mmbando.

Akitoa maelezo mafupi kwa waandishi wa habari jana baada ya Mdee kuhojiwa kwa takriban saa sita, wakili wake , Profesa Abdalah Safari alisema mbunge huyo anashikiliwa kwa kosa hilo na atalala rumande.

“Kimsingi nilikuja kumsikiliza akitoa maelezo yake, ameshatoa lakini hakuna ushahidi wowote wa kosa analodaiwa kufanya la kushambulia Theresia,” alisema. 

Hata hiyo, Profesa Safari alisema kutokana na kosa hilo Mdee alikuwa na haki ya kuwekewa dhamana lakini polisi wamekataa.

“Mdee angeweza kujidhamini hata mwenyewe lakini wamekataa na kutokana na kosa hili anatakiwa kulala rumande kwa saa 48, zikizidi ina maana atapelekwa mahakamani,” alisema.

Profesa Safari, ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Chadema Bara, alisema mbali na Mdee pia madiwani watatu wanashikiliwa na polisi kwa kosa hilo.

Madiwani hao ni Humphrey Sambo wa kata ya Mbezi, Ephraim Kinyafu (Saranga), wakati hakumtaja jina diwani wa tatu.

Awali wakati mahojiano hayo yalipoanza saa 7:00 mchana, taarifa kutoka kwa mmoja wa makada wa chama hicho zilieleza kuwa Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara pia alitakiwa kufika kituoni hapo kutoa maelezo na anatarajiwa kuwasili leo.

Wakati wa polisi wakimhoji Mdee, wanachama wa Chadema walifika kituoni hapo, akiwapo Ester Bulaya, ambaye ni mbunge wa Bunda Mjini, Esther Matiko (Bunga Vijijini) na Henry Kilewo ambaye ni kanda wa Chadema.

Mapema jana mchana kabla ya Mdee kufikishwa kituoni hapo, ilielezwa kuwa polisi walizingira nyumba yake na kumtaka aende kituoni. 

Hata hivyo, mbunge huyo hakutoka hadi alipowasiliana na wakili wake ambaye alienda naye kituoni kwa ajili ya mahojiano.

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu za Kiume

$
0
0

Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  

Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :

Ukisoma  vizuri  kuhusu  mfumo  wa  nguvu  za  kiume, utagundua  kuwa   Suala  la  nguvu  za  kiume  ni  suala  la  kimfumo.  Ili  mwanaume  awe na nguvu  za  kiume, aendelee  kuwa  na  nguvu  za  kiume na  azilinde  nguvu  zake za  kiume, ni  lazima  ogani  zote zinazo  husika  na  mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ziwe  na  afya  njema  na  ziwe  na  ushirikiano   thabiti  na  wenye  afya.

Vile  vile , utagundua  kuwa , mambo  makuu  muhimu  katika   mfumo  wa  nguvu  za  kiume  ni  kama  ifuatavyo:

i.Mishipa  imara  ya  ubongo  na  yenye  afya  njema

ii. Mishipa  imara  ya  uti  wa  mgongo  (  spinal  cords )

iii.Mishipa  imara  itumikayo  kusafirisha  damu  mwilini  (  Blood Vessels )

iv. Mfumo  imara  wa  usafirishaji  damu  mwilini

v. Mishipa  ya  uume  iliyo  imara  na  yenye  afya  njema

vi. Uhusiano  imara  na  wenye  afya  kati  ya  mishipa  ya  fahamu  iliyopo  katika  ubongo, mishipa  ya  kwenye  uti  wa  mgongo  pamoja  na  misuli & mishipa  ya  kwenye  uume.

Hivyo  basi, ili  mwanaume  aweze  kuwa  na  nguvu  imara  za  kiume, na  aendelee  kuwa  na  nguvu  hizo ni  lazima  mambo  yote  muhimu  katika  mfumo  wa  nguvu za  kiume  yawe  imara  pasi na  hitilafu  yoyote.

Hitilafu  yoyote  katika  mambo  hayo, itasababisha  ukosefu na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume  kwa  mwanaume  huyo.  Pale inapotokea    hitilafu  ama  mapungufu  katika  ogani  zaidi  ya  moja  kati  ya  zilizo  tajwa hapo  juu, basi  tatizo  kwa  muhusika  huwa  kubwa  mara  dufu.

JINSI  PUNYETO  INAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU &  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
Mwanaume   anapopatwa na  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, ubongo  hutoa  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti  wa  mgongo  ambayo  nayo  husafirisha  taarifa  hadi  kwenye  mishipa &  misuli  ya  uume.

Mishipa  ya  uume inapopokea  taarifa  hiyo, hutanuka. Na  mishipa  ya  uume  inapotanuka, hufanya  mambo  mawili  muhimu  sana :

i.Husababisha  mishipa  ya  ateri  kupanuka  na  hivyo  kuruhusu  damu  kuingia kwa  kasi  sana   ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuufanya  uume  usimame  na  kuwa  imara  bara bara.

ii. Huibinya na  kuiziba  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kuzuia  kunyonya  ama  kufyonza  damu  iliyo  ingia  ndani  ya  mishipa ya  uume.  (  KAZI  KUBWA  YA  MISHIPA  YA  VENA  ILIYO  KARIBU NA  MISHIPA  YA  UUME  NI KUHAKIKISHA  HAKUNA  DAMU NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME. HIVYO  BASI  DAMU  INAPOINGIA  NDANI YA  MISHIPA  YA  UUME, MISHIPA  YA  VENA  HU “SENSE” JAMBO  HILO  KWA  HARAKA  NA HIVYO  KUIFYONZA  DAMU  HIYO  KUTOKA KWENYE MISHIPA  YA UUME  YA  KUITOA  NJE YA MISHIPA  YA  UUME.  NA  DAMU INAPOKOSEKANA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME, HUUFANYA  UUME  KUSINYAA  NA  KULEGEA )

Mtu  anayepiga  punyeto  husababisha  mambo  yafuatayo  katika  mwili  wake :

1. Huuwa  nguvu  ya  mishipa  & misuli ya  uume ambayo  ndio  inayo husika  na  kusimama  kwa  uume

2. Mishipa  ya   uume  inapo  sinyaa  na  kukosa  nguvu  yake  ya  asili, husababisha  mambo  yafuatayo :

i.Huondoa  uwezo  wa  mishipa  &  misuli  ya  uume  kutanuka, na  hii  ndio  sababu  inayo  wafanya  waathirika  wa  punyeto  kutumia  nguvu  nyingi  sana  katika  kuufanya  uume  usimame.

ii.Huondoa  uwezo  wa  mishipa &  misuli  ya  uume  kuibana  na  kuiziba  mishipa  ya  vena, na  hii ndio  sababu  inayo  fanya  waathirika  wa  punyeto  kufika  kileleni  haraka  sana, kwani damu  inayo  ingia  kwenye misuli  ya  uume   hufyonzwa  ndani ya  muda  mfupi sana. 
 
 Hii  hutokea  kwa  sababu  mishipa na  misuli  ya  uume inakuwa  imelegea,na  mishipa  ya  vena inakuwa  imepwaya, hivyo  msuguano wowote ule  hufanya  mishipa  ya  vena  kufunguka  na  kufyonza  damu  kutoka  kwenye mishipa  ya  uume  na hivyo  kuufanya  uume  kusinyaa  ndani ya dakika ama sekunde  chache sana.

3. Vile  vile  punyeto  hufanya  uume  kusinyaa na  kurudi ndani  na  kuufanya  uonekane kama  uume  wa  motto mdogo.

Kwa  ufupi  punyeto  husababisha  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume  kwa  sababu  kuu  zifuatazo :

i.Kwanza   hudhoofisha  na  kuharibu  mishipa  ya  uume,  ambayo  ndio  hufanya  uume kusimama.

ii.Pili  hudhoofisha  utendaji  kazi  wa  mishipa  ya  ateri, ambayo  ndio  hutumika  kama  njia  ya  kusafirisha  damu kupeleka kwenye  misuli  ya  uume  na  ivyo  kuufanya  uume  usimame

iii. Tatu, punyeto  hupelekea  kuvuja  kwa  mishipa  ya  vena  na  hivyo  kusababisha  damu  kufyonzwa  kwa  haraka  sana  kila  iingiapo ndani  ya  misuli ya  uume  na  matokeo  yake  ni  uume   kusimama  kwa  muda  mfupi  sana  wakati wa  tendo  la  ndoa.

iv. Punyeto  huathiri  mtiririko  wa  damu  kwenda  kwenye  mishipa  ya  uume, kwa  sababu  hudhoofisha  misuli &  mishipa  ya  uume  pamoja  na mishipa ya  ateri  ambayo  ndio  hutumika  katika  kusafirisha  damu kwenda  kwenye  uume

DALILI  ZA  MTU  ALIYE  ATHIRIWA  NA  PUNYETO
Dalili  kuu  za  mtu  aliye athiriwa  na  punyeto  ni  kama  ifuatavyo:

i.           Uume  kusinyaa  na  kuwa  kama  wa  mtoto
ii.         Uume kurudi  ndani
iii.       Uume  kusimama  ukiwa  legelege
iv.       Kufika  kileleni  haraka  wakati  wa  tendo  la  ndoa.

TIBA   YA   NGUVU  ZA  KIUME  KWA MTU  ALIYE  ATHIRIKA  NA  PUNYETO.
Dawa   asilia  ya  nguvu  za  kiume iitwayo JIKO  ni tiba  bora  na  ya  uhakika  kabisa  kwa  mtu  aliye  athiriwa   na  punyeto.  Dawa  hii, pamoja  na  mambo  mengine  mengi, husaidia  kufanya  mambio  yafuatayo  katika  mwili  wa  mwanaume  aliye  athiriwa  na  punyeto :

i.Kuimarisha  mishipa  & misuli  ya  uume  ulio  legea na  hivyo  kuurejeshea  uwezo wake wa  asili

ii. Hutibu   tatizo  la  uume  kurudi  ndani

iii.Humaliza  tatizo  la  kusimama  kwa  uume  ukiwa  legelege

iv.Hutibu  na  kuponya  kabisa  tatizo  la  kufika  kieleleni  haraka.

BEI  YA  DAWA  :  Dawa  hii  inapatikana  kwa  gharama  ya  SHILINGI  ELFU  THEMANINI  TU (Tsh. 80,000/=)

MAHALI  INAPOPATIKANA :  Dawa  hii  inapatikana  katika  duka  la  dawa  asilia  liitwalo  NEEMA  HERBALIST  &  NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC  lililopo  jijini  DAR  ES  SALAAM  katika  eneo  la  UBUNGO   nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA   karibu  na SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING.

Kwa  wateja  wasio  weza  kufika  ofisini  kwetu. Watafikishiwa  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  DAR  ES  SALAAM.

Kwa   wateja  waliopo  mikoani  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  MABASI

Kwa  wateja  waliopo   Zanzibar  wata fikishiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa boti.

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  ama  DHL.

MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee kila  siku  kwenye  blogu  yetu :


January Makamba Aikosoa Serikali ya Kikwete

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba ametofautisha nyakati za utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne iliyoongozwa na Dk. Jakaya Kikwete na zilizopita na huu wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli, huku akiitoa kasoro iliyopita.

Makamba ameeleza kuwa wakati tawala zilizopita, watu walikuwa wakionewa haya na na kujuana kulichukua nafasi tofauti na awamu hii inayochukua hatua stahiki bila kujali.

“Nadhani moja ya changamoto zilizosababisha huko nyuma tusifanikiwe sana katika suala la uwajibikaji, ni hili suala la kuoneana haya. Suala la kujuana kidogo na kusitiriana,” Makamba aliliambia Gazeti la Mwananchi hivi karibuni.

Alisema kuwa utamaduni huo unapoendelea na kuota mizizi, suala la uwajibikaji huwa kikwazo na hatua stahiki dhidi ya watu wanaofanya makosa hushindwa kuchukuliwa.

Makamba ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia katika Serikali ya Awamu ya Nne, alieleza kuwa hatua za utumbuaji majipu zinazochukuliwa hivi sasa dhidi ya wakwepa kodi na watumishi wanaovunja sheria na kutowajibika ni sahihi na kwamba kama kuna mtu anaona anaonewa bado anayo nafasi ya kutafuta haki yake kwenye vyombo vya kisheria.

“Kikubwa tu ambacho mimi ninaamini ni kwamba kunahitajika kujenga utamaduni mpya wa watu kuogopa na kuheshimu wajibu wao, na kwamba hizi kazi si kazi zetu za kudumu. Wakati wote unapofanya makosa basi kuna Mamlaka ya kukuchukulia hatua,” alisema.

Makamba alisisitiza kuwa ni sahihi kuchukua hatua hivi sasa dhidi ya makosa yaliyofanyika katika utawala uliopita, “Kama huko nyuma hakukuwa na utashi wa mfumo wa kuwezesha makosa hayo kubainika, lakini utashi huo upo sasa, basi hatua zichukuliwe.”

Serikali Yalitaka Gazeti la DIRA Limuombe Radhi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue

$
0
0

1. Utangulizi:

Gazeti la Dira ya Mtanzania, Toleo Na.404 la Februari, 29 - Machi 6, 2016 liliandika taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho "Uchafu wa Ombeni Sefue Ikulu".  Taarifa hiyo, ambayo ni muendelezo wa makala nyingine kwenye toleo la gazeti hilo la wiki iliyopita, ilimtuhumu Katibu Mkuu Kiongozi kushawishi juu ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD pamoja na Kampuni za "CRJE" na "UGG" kupewa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma, Daraja la Kigamboni na Reli ya Dar es Salaam - Kigali. Taarifa zote hizi ni za uongo na za kupotosha wananchi.

2. Kuhusu uteuzi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD,

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, hakuhusika kwa namna yoyote kushawishi uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD.

Uteuzi huo ulitekelezwa kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa. Nafasi hiyo ilitangazwa na Bodi tarehe 20 Novemba, 2013.

Usaili ulifanywa na kampuni huru iliyopewa jukumu hilo na Bodi. Mapendekezo ya majina matatu yalipelekwa kwa Mhe. Rais na Waziri wa Afya, kwa ajili ya uteuzi.

Balozi Sefue alikuwa hamjui aliyeteuliwa na wala hakuwahi kuwa na uhusiano naye. Alichofanya Balozi Sefue ni kutangaza tu uteuzi baada ya Rais kuteua.

Gazeti hilo pia limeandika uwongo kuwa MSD haijawahi kuongozwa na Mkurugenzi Mkuu asiye Mfamasia.

Tangu MSD ianzishwe mwaka 1993 hadi sasa, ni Mkurugenzi Mkuu mmoja tu, Rino Meyers (1996-1999), ndiye alikuwa Mfamasia. Wakurugenzi wengine kama Peter Mellon (1993-1995), Jay Drosin (2001-2004) na Joseph Mgaya (2004-2013) hawakuwa Wafamasia.

3. Kuhusu Kampuni ya CRJE kuhusishwa na Balozi Ombeni Y. Sefue

Suala la kumhusisha Katibu Mkuu Kiongozi na kampuni hii nalo ni uzushi na uongo wa kupindukia.

Wakati kampuni hii ikipewa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma mwezi Oktoba 2007, Balozi Ombeni Y. Sefue hakuwa Katibu Mkuu Kiongozi; alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

Kadhalika mchakato wa kumpata mkandarasi wa daraja la Kigamboni, ulipoanza mwezi Machi, 2011, Balozi Sefue hakuwa Katibu Mkuu Kiongozi; alikuwa Balozi wa Tanzania, Umoja wa Mataifa, New York.

Hata mkataba wa ujenzi wa Daraja hilo uliposainiwa tarehe 9 Januari, 2012, Balozi Sefue alikuwa na wiki moja tu ya kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kufuatia kuteuliwa tarehe 30 Disemba, 2011.

Aidha, Kampuni iliyoshinda tenda hiyo wala siyo CRJE kama ilivyoandikwa na gazeti hilo bali ni China Major Bridges Engineering Company (BCEC) kwa kushirikiana na Kampuni ya China Railway Construction (CRCEG).

4. Kuhusu tuhuma kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kuipigia Chapuo Kampuni ya UGG:

Katibu Mkuu Kiongozi hajawahi kuipigia chapuo kampuni yoyote ile pahala popote. Isitoshe, hakuna kampuni yenye jina la "UGG" iliyowahi kuonesha nia ya kujenga reli ya kati.

Hii ni moja ya uthibitisho kwamba gazeti hili linatoa taarifa za kuokoteza zisizo na ukweli kama vile walivyopotosha kuhusu jina la Katibu Mkuu Kiongozi kwenye makala yao ya pili kwenye ukurasa wa tisa wa gazeti hilo yenye kichwa cha habari "Magufuli anaishi na jipu Ikulu" ambapo walimpachika Katibu Mkuu Kiongozi jina la Sifuni, jina ambalo hajawahi kuwa nalo.

Balozi Sefue hajahusika, hahusiki na wala hatahusika katika kuchagua wa kupewa tenda hiyo kwa sababu yeye si sehemu ya wenye mamlaka ya kutoa tenda.

5. Kuhusu Eliachim Maswi:

Gazeti la Dira ya Mtanzania limeandika kuwa moja ya "madudu" aliyofanya Balozi Sefue ni walichoita kumsafisha Bwana Eliachim Maswi.

Wanadai hivyo wakati wamekiri kuwa alichofanya Balozi Sefue ni kusoma matokeo ya uchunguzi, ambao hakuufanya yeye.

Waliomsafisha Maswi ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali; Sekretarieti ya Maadili ya Umma; na hatimaye kamati ya uchunguzi iliyoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu. Kwa hiyo, kwa maoni ya gazeti hili, Balozi Sefue asingepaswa kusoma matokeo ya uchunguzi
uliofanywa  na  vyombo  hivyo  huru.     Kwa  maoni  yao  kusoma  taarifa  ya
uchunguzi ni "madudu".

6. Hitimisho:

Kwa kuwa habari hizo hazina chembe yoyote ya ukweli, na wao wenyewe ndani ya gazeti wamekiri hawana ushahidi, ni wazi kuwa habari hizo ni za kubuni na zimetungwa.

Kwa sababu hiyo, Serikali inalitaka Gazeti  la  Dira ya Mtanzania  kukanusha uongo na uzushi wao na kumuomba radhi Balozi Ombeni Sefue, kuiomba radhi Serikali na kuwaomba radhi wote walioumizwa na uzushi huo kwa uzito ule ule uliotumika kuchapisha taarifa hiyo.

Vinginevyo iwapo gazeti la Dira ya Mtanzania lina ushahidi wa huo "uchafu" wa Katibu Mkuu Kiongozi, waupeleke mara moja kwenye vyombo vinavyohusika ikiwamo Sekretarieti ya Maadili na TAKUKURU.

Vinginevyo, hatua zikichukuliwa dhidi yao wasiseme Serikali inavibana vyombo vya habari.

Aidha Serikali inashauri wenye vyombo vya habari, wachapishaji, wahariri na waandishi wa habari wajikite kwenye weledi na ukweli, wafanye utafiti na kuandika mambo waliyo na uhakika nayo, na kamwe wasikubali kutumiwa kuendeleza agenda za watu wengine.

Imetolewa na Idara ya Habari - MAELEZO.
01 Machi, 2016

Rais Dkt. Magufuli amtumia salamu za Rambirambi, Rais Mstaafu Dkt. Kikwete kufuatia kifo cha Kaka yake

$
0
0
Mzee Seleman Kikwete enzi za uhai wake

EWURA yatangaza kushuka kwa bei ya mafuta

$
0
0


Mkurugenzi wa Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi amesema ‘kuanzia tarehe 2 Machi bei za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la Februari 2016.

Kwa Machi 2016 bei ya rejareja za petroli imepungua Tsh 31 kwa lita sawa na 1.70%, Diesel imepungua Tsh 114 kwa lita sawa na 7.10% na mafuta ya taa yamepungua kwa Tsh 234 kwa lita sawa na 13.75%’

‘kwa kiasi kikubwa, kupungua huku kwa bei za mafuta kwenye soko la ndani kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia


Rais Magufuli akutana na kuzungumza na Rais Museveni wa Uganda

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, amekutana na kufanya Mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Tanga nchini Tanzania hadi nchini Uganda.

Rais Museveni alimtembelea Rais Magufuli katika Ikulu ndogo ya Arusha jana jioni mara baada ya kuwasili hapa nchini akitokea nchini Uganda, ambapo leo atahudhuria Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, utakaofanyika katika Hoteli ya Ngurudoto Jijini Arusha.

Akizungumza baada ya viongozi hao kufanya mazungumzo ya faragha, Rais Magufuli alisema wamekubaliana kutekeleza mradi huo wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanga hadi Uganda, kwa manufaa ya nchi zote mbili na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Alisema bomba hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1,120 na kwamba mradi huo utazalisha ajira za watu zaidi ya 15,000.

Rais Magufuli aliongeza kuwa pamoja na kujengwa kwa bomba la mafuta, pia walizungumzia kuongeza biashara ndani ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, kujenga viwanda na kuzalisha ajira zaidi kupitia sekta mbalimbali za uzalishaji mali.

Aidha, Rais Magufuli alisema katika Mkutano huu nchi wanachama watajadili maombi ya nchi ya Sudan Kusini kupata uanachama ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alibainisha kuwa, kwa Sudan Kusini kuwa mwanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki, itakuwa na uwezo wa kufanya biashara katika eneo lenye takribani watu milioni 150 na hivyo kupata manufaa makubwa zaidi.

Kwa upande wake Rais Yoweri Kaguta Museven pamoja na kuunga mkono yaliyosemwa na Rais Magufuli alimpongeza kwa kasi yake nzuri aliyoanza nayo katika uongozi, na alisema ni matumaini yake kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, sasa zitakuwa katika nafasi nzuri ya kwenda kwa kasi ya Rais Magufuli katika maendeleo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha
01 Machi, 2016

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images