TBS Yawataka Wazalisha Nondo Kuanza Kuweka Lebo ( TBS steel bar ID & labelling )
↧
↧
Gavana Azindua Mwongozo Wa Kwanza Wa Kitaifa Wa Elimu Na Ulinzi Kwa Mtumiaji Wa Huduma Za Fedha (N-FEF).
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Huduma za Kifedha Tanzania (FSDT), imezindua Mwongozo wa taifa wenye lengo la kuongeza uelewa kuhusu elimu ya mambo ya fedha kwa wananchi.
Uelimishwaji wa wananchi kuhusu mambo ya fedha utatekelezwa kupitia “Mwongozo wa kwanza wa kitaifa wa elimu na ulinzi kwa mtumiaji wa huduma za fedha” (N-FEF).
Gavana Prof. Beno Ndulu ameuzindua rasmi mwongozo huu ambao utajikita katika kutatua changamoto zilizobainishwa katika utafiti uliopima uelewa wa mambo ya fedha kwa watu wazima nchini Tanzania. Utafiti huu unaitwa “Uwezo wa Kifedha Tanzania” wa mwaka 2014.
Utafiti huo umebainisha kuwa watanzania wengi hawana elimu na ujuzi mahususi wa masuala ya mambo ya fedha kwa ujumla, hivyo kuwanyima fursa ya kutumia huduma za kifedha kwa faida yao.
Katika utafiti huo imeonyeshwa kuwa upatikanaji wa huduma za fedha umekuwa na changamoto katika maeneo mengi huku zile zitolewazo kwa njia ya mitandao bado hazikidhi matarajio ingawa zinawafikia wateja wengi kwa sasa.
Sambamba na hilo kumekuwa na uhaba wa nyenzo na miundombinu ya kuhifadhi na kufikisha taarifa za fedha kwa watumiaji wa huduma hizo kwa kuzingatia namna sahihi ya kutoa taarifa, kuwaelimisha na kuwalinda.
Kutokana na utafiti wa “Uwezo wa Kifedha Tanzania” wa mwaka 2014 wananchi kutoka makundi mbalimbali katika jamii hawana ujuzi wa hesabu za kawaida ambao ndiyo msingi mkuu katika nadharia ya masuala yahusuyo mambo ya fedha.
Elimu msingi katika masuala ya fedha umekuwa kikwazo kwa waliowengi hasa katika uandaaji wa bajeti, kutunza kumbukumbu ya matumizi, kupanga fedha kwa matumizi yasiyotegemewa ama ya ziada na muhimu zaidi kutunza kiasi kwa ajili ya matumizi ya uzeeni (baada ya kustaafu).
Inaonekana kuwa upatikanaji wa taarifa za masuala ya fedha hutegemea zaidi vyombo vya habari kama redio, televisheni na magazeti lakini vyombo hivi kwa sehemu kubwa, hufikisha zaidi taarifa za biashara na masoko kuliko ambavyo vinaelimisha jamii kuhusu matumizi na upangaji wa mapato yao.
“Haya ndiyo masuala mahususi ambayo mwongozo huu wa taifa kuhusu elimu ya huduma za fedha unalenga kushughulika nayo,” alisema Prof Ndulu.
Pamoja na kuwepo ongezeko la upatikanaji wa huduma za kifedha, mpaka asilimia 58 mwaka 2013 kutoka kiwango cha asilimia 17 mwaka 2009, miongoni mwa watu wazima nchini, bado mwongozo huu ni muhimu ili kuleta mfumo imara wa sekta ya fedha na Zaidi sana ili kuleta ustawi wa maisha ya watanzania kwa ujumla.
Prof. Ndulu anasema kutatua changamoto za kielimu kwa ujumla na hususan elimu ya huduma za fedha italiwezesha taifa kuwa katika mwelekeo mzuri wa kukabiliana na umasikini na kufikia malengo ya kukuza uchumi.
“Tunapaswa kujiuliza: ni kwa namna gani wananchi hasa wale masikini na wasiokuwa na elimu za kifedha za wanapambana kuendeleza biashara zao katika mazingira ya soko huria na lenye ushindani kila uchwao” alisisitiza Prof. Ndulu.
Hivyo, mwongozo huu utahakikisha watanzania wapata elimu sahihi na ya uhakika ya huduma za kifedha pamoja na njia anazoweza nazo kujilinda katika ushindani huu.
Vilevile mwongozo huu umeundwa ili kutatua changamoto za kifedha zinazohusiana na maamuzi miongoni mwa watumiaji wa huduma hizi na kuwa jumuishi na wenye tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Mwongozo wa taifa kuhusu elimu ya huduma za fedha umeandaliwa kwa kujumisha washikadau kutoka Tanzania bara na Zanzibar.
Unabainisha changamoto zinazohusuana na uwezo wa kifedha ambazo zinahitaji kutatuliwa kwa uwepo wa elimu ya fedha. Pia, unatoa taratibu wakufanikisha utekelezaji wa elimu ya fedha, na mwongozo wa kitaifa wa kuratibu elimu ya fedha nchini.
Lengo la mwongozo wa elimu ya huduma za fedha ni kuwa na wananchi na kaya zenye uwezo kifedha nchini.
↧
Waziri Mkuu Majaliwa Awatembelea Waathirika Wa Mafuriko Iringa, Apokea Misaada Ya Maafa Ya Sh. Milioni 86/-
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. milioni 85.88/- kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko kwenye vijiji vya kata ya Mlenge, tarafa ya Pawaga, wilaya ya Iringa vijijini mkoa wa Iringa.
Misaada hiyo imetolewa na wadau mbalimbali kutokana na mafuriko ambayo yalibomoa nyumba 82 katika kitongoji cha Kilala, kijiji cha Kisanga na kuwaacha wananchi wake bila makazi.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kasanga ambako alikwenda kukagua athari za mafuriko na kuwapa pole wananchi hao jana mchana (Jumatatu, Februari 22, 2016), Waziri Mkuu aliwashukuru wadau wote waliojitolea kuwachangia watu waliopata maafa kutokana na mafuriko hayo.
Wadau waliotoa misaada hiyo ni Benki ya NMB mabati 500, mifuko ya saruji 500, kilo 820 za maharage, kilo 750 za unga wa mahindi na lita 250 za mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 20/-. Wengine ni Mfuko wa Pensheni wa PPF uliotoa mabati 200 na mifuko ya saruji 200 vyenye thamani ya sh. milioni 6.6/-.
Wengine ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) waliotoa mabati 200 na mifuko ya saruji 160 vyenye thamani ya sh. milioni 4.5/-; Kiwanda cha kusindika nyanya cha RedGold kimetoa mifuko ya saruji 100 na mabati 50 vyenye thamani ya sh. Milioni 3/-; mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Bi. Susan Chogisasa na wenzake wametoa mabati 150, mifuko 23 ya saruji, kilo 100 za maharage, kilo 50 za chumvi na nguo mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 1.3/-.
Madiwani wa Iringa Vijijini walitoa sh. 380,000/-, Wabunge wa Viti Maalum kupitia CCM walitoa vifaa vya sh. Milioni 1.7/-; ofisi ya CCM Mkoa wametoa vifaa vya sh. milioni 6.1/-, Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa, Bw. Salim Abri aliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Iringa sh. milioni 5/- ili wanunue vyakula vya waliopatwa na maafa.
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mbunge wa Isimani, Bw. William Lukuvi alitoa fedha taslim sh. milioni 20/- kati ya hizo sh. milioni 15 zikiwa ni zake na milioni 5/- ni za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Bw. George Simbachawene. Pia alikabidhi seti 251 za mashuka zenye thamani ya sh. milioni 4/- zikiwa ni mchango kutoka Benki ya CRDB.
Waziri Lukuvi ambaye alishatoa mabati 250, aliahidi kuongeza mabati mengine 250 (yote yana thamani ya sh. milioni 8), pia alikabidhi sh. milioni 1.5/- kwa diwani wa Mlenge ili ziwasaidie kukodi gari la kukarabati barabara yao ambayo imeharibika sana kutokana na mafuriko hayo.
Mapema, akitoa taarifa ya maafa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Amina Masenza alisema jumla ya kaya 82 zilikosa makazi kutokana na mvua zilizonyesha Februari 12 na kusababisha mafuriko. Kabla ya hapo, kaya nyingine 75 zenye wakazi 377ziliathirika kutokana na mvua zilizoanza Februari 3, mwaka huu.
Alisema miundombinu ya barabara na ya maji safi iliharibiwa vibaya na kusababisha hasara ya zaidi ya sh, milioni 250/-. Pia wakazi hao walikumbwa na ugonjwa wa kipindupindu kutokana na mto Mapogoro kufurika na kusomba baadhi ya vyoo vya wakazi hao.
“Tangu Februari mosi, wamekwishapokea wagonjwa wa kipindupinda 351 lakini walioko wodini hivi sasa ni wagonjwa 25 tu,“ alisema Mkuu huyo wa mkoa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 22, 2016.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwapa pole wanawake na watoto wakati alipotembelea makazi ya dharura waliyojengewa na serikali katika kijiji cha Kasanga wanapohifadhiwa waathirika wa mafuriko yaliyozikumba tarafa za Pawaga na Idodi , Iringa Februari 22, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya msaada kutoka kwa meneja uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mangele katika mkutano wa kuwapa pole wananchi wa tarafa za Pawaga na Idodi uliohutubiwa na Waziri Mkuu katika Kijiji cha Kasanga, Iringa Februari 22, 2016. Mfuko huo umetoa mabati 200 na saruji mifuko 200 vyote vikiwa na thamani ya sh. 6,600,000/=.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwapa pole kinamama na watoto wakati alipotembelea makazi ya dharura waliyojengewa na serikali katika kijiji cha Kasanga wanapohifadhiwa waathirika wa mafuriko yaliyozikumba tarafa za Pawaga na Idodi , Iringa Februari 22, 2016.
↧
Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Februari 23
↧
Wizara Ya Fedha Yasema Makusanyo Ya Fedha Kwa Mwezi Yamefika Trilioni 1.79........Mchanguo Wote Wa Matumizi wa Pesa Uko Hapa
SERIKALI imeendelea kupaa katika ukusanyaji wa mapato baada ya kukusanya hadi Sh trilioni 1.79, ambazo imezipeleka katika huduma za jamii, ikiwamo elimu, maji, miundombinu na miradi ya maendeleo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya hali ya mapato kwa kipindi cha Februari mwaka huu.
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata alisema makusanyo yameongeza kutoka Sh trilioni 1.2 Desemba hadi Sh trilioni 1.79 Januari.
Kabla ya Oktoba mwaka jana, makusanyo hayo hayakuzidi Sh bilioni 900 kwa mwezi.
Dk Likwelile alitaja maeneo ambayo fedha hizo zimeelekezwa ni kwa Mamlaka ya Elimu (TEA) iliyopewa Sh bilioni 23.078; Sh bilioni 18.7 zinatekeleza utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za awali, msingi hadi kidato cha nne kwa ajili ya ada, chakula na ruzuku.
Aidha, Sh bilioni 13 zimeelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu na Sh bilioni moja zitatumika kujengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao.
Pia Sh bilioni mbili zimeelekezwa kupanua udahili katika mkoa wa Dar es Salaam kama Rais John Magufuli alivyoahidi katika mkutano wake na wazee wa mkoa huo.
Dk Likwelile alitaja maeneo mengine yaliyonufaika na fedha hizo na shilingi kwenye mabano ni Mpango wa Maji Vijijini (bilioni 17.1), maendeleo ya ujenzi wa barabara (bilioni 58.8), miradi ya umeme vijijini (bilioni 20.2), reli (bilioni 2.034) Serikali za Mitaa (bilioni 4.5), na Mahakama zimepatiwa Sh bilioni 12.3.
Aidha, Dk Likwelile alisema ili kuwajengea uwezo walimu walio masomoni na wakufunzi wao, Wizara imetoa Sh bilioni 1.65 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
Kati ya fedha hizo, wakufunzi wamepatiwa Sh milioni 431.6, walimu walio masomoni wametengewa Sh milioni 249.2 kwa ajili ya vifaa vya kufundishia, posho na nauli.
Alisema kuwa fedha nyingine kati ya hizo, kiasi cha Sh bilioni 573.7 zimetolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa umma na ulipaji wa deni la taifa kwa mwezi huu zimetolewa Sh bilioni 842.1 na mifuko ya hifadhi za jamii Sh bilioni 81.13.
Aidha kiasi kilichotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ni Sh bilioni 166.2 huku Chuo kipya cha Sayansi ya Tiba kilicho katika hatua ya ujenzi cha Mloganzila huko Kibamba, nje ya Jiji la Dar es Salaam, kimepatiwa Sh bilioni 18 .
Kaimu kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Alfayo Kidata akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Tarishi Kibenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam jinsi Mamlaka hiyo ilivyofanikiwa kukusanya mapato kutoka trilioni 1.2 kwa mwezi Disemba mpaka trilioni 1 na bilioni 79 kwa mwezi Januari
↧
↧
Serikali Yapanga Bei Elekezi Kwa Hospitali Binafsi Ili Kupunguza Mzigo wa Gharama
SERIKALI imesema itatoa bei elekezi katika sekta ya afya hivi karibuni baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kubariki bei hizo kuanza kutumika kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wa gharama wananchi.
Bei elekezi kwa vituo vya afya zimeshasainiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na baadhi ya vituo vya afya vimeshaanza kutumia bei hiyo.
Aidha, serikali imepanga kuweka utaratibu wa wagonjwa kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni hatua ya kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hiyo.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Hamis Kigwangalla wakati akizungumza na waaandishi wa habari baada ya kuzindua Matokeo ya Utafiti wa Kutathimini utoaji wa huduma za afya nchini kwa mwaka 2014/2015.
“Bei elekezi ziko mbioni kutoka na baadhi ya vituo wameshaanza kuzitumia kwa sababu zimeshasainiwa na Waziri, sasa hivi tunasubiri Baraka za Waziri Mkuu akiziridhia tutazitangaza rasmi,” alisema Dk Kigwangalla.
↧
Meneja wa Shirika la Posta Tanzania Afikishwa Mahakamani Kwa Matumizi Mabaya Ya Ofisi
Meneja wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Mkoa wa Dar es Salaam, Lawrence Mwalumwelo na wenzake wawili wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Sophia Nyanda akishirikiana na Veronica Chimwanda mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Ofisa Tawala, Modester Fumbuka na Ofisa Manunuzi, Radecunda Massawe, wafanyakazi wa TPC.
Chimwanda alidai kuwa kati ya Agosti Mosi na Oktoba 31, 2010 washtakiwa hao walitumia vibaya madaraka yao kwa kuipa mkataba wa kutafuta vibarua kampuni ya Technical Merchantile Service bila kupata kibali kutoka bodi ya zabuni.
Vilevile ilidaiwa kuwa Septemba 26 ,2011 washtakiwa hao walitumia vibaya madaraka yao kwa kuiongezea kampuni hiyo mkataba wa kutafuta vibarua kutoka Septemba 30 hadi Desemba 31, 2011 bila ya kuishirikisha bodi hiyo.
Ilidaiwa kuwa Januari Mosi, 2012 washtakiwa hao waliiongezea tena kampuni hiyo mkataba wa kutafuta vibarua kutoka Januari Mosi, 2012 hadi Machi 30, 2014 bila ya kuishirikisha bodi hiyo. Washtakiwa hao walikana mashtaka.
Washtakiwa hao waliachiwa baada ya kutumiza masharti ya dhamana na kesi hiyo kuahirishwa hadi Machi 17.
↧
CCM Watuma Salamu za Pongezi Kwa Yoweri Museveni Kwa Ushindi wa Kiti cha Urais Uganda
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepongeza Chama cha National Resistance Movement (NRM) cha nchini Uganda kwa ushindi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Februari 18.
Kutokana na ushindi huo CCM inampongeza Rais mteule, Yoweri Museveni ambaye ndiye mwenyekiti wa NRM.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa CCM, Daniel Chongolo imeeleza kuwa wamefuatilia kwa ukaribu mchakato wa uchaguzi huo na walikuwa na imani kwamba NRM itaibuka mshindi dhidi ya waliokuwa wagombea wengine saba wa urais.
=====
↧
Mwanamkakati wa Maalim Seif Aswekwa Ndani Na Jeshi La Polisi Zanzibar
Mwanamkakati wa aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar, Mohamed Sultan Mugheiry, maarufu kwa jina la Eddy Riyami, amewekwa ndani na Jeshi la Polisi mjini Unguja kwa tuhuma za kumtukana Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Eddy Riyami ambaye ni mmoja wa wana mkakati wa timu ya ushindi wa aliyekuwa mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alikutwa na mkasa huo jana baada ya kuitwa polisi kutoa maelezo kutokana na tuhuma zinazomkabili.
Riyami ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, alikwenda Polisi Makao Makuu kuitikia wito wa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, SSP Simon Pasua, huku akiandamana na Mwanasheria wa CUF, Masoud Faki Masoud.
Mwanasheria huyo jana alisema Riyami anatuhumiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya kimtandao.
Alisema licha ya kuzikana tuhuma hizo, lakini Jeshi la Polisi bado lilimshikilia kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
“Ni kweli ameshikiliwa na polisi kwa ajili ya kupitisha uchunguzi na yupo Polisi Madema, eti Eddy kaambiwa kamtukana Dr. Shein kwenye ‘audio’ ambayo hata si sauti yake, lakini dhamana ipo wazi na tutamchukulia dhamana,” alisema Masoud.
Akizungumzia kukamatwa kwa Riyami, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, Salum Msangi, alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
“Kitu ninachoweza kuthibitisha ni kuwa tunamshikilia Riyami kwa ajili ya kupitisha uchunguzi,” alisema Naibu Kamishna Msangi.
Februari 15, mwaka huu Ofisi ya Mkurunzi na Makosa ya Jinai, ilimwandikia Riyami barua ya wito na kumtaka kufika ofisi ya upelelezi iliyopo Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.
Riyami alitii wito huo ambapo wiki iliyopita alikwenda lakini mmoja wa maofisa wa Jeshi la Polisi aliyemwandikia barua alikuwa nje ya Zanzibar kwa shughuli za kikazi na kumtaka kwenda jana jumatatu
Riyami si mwanachama wa CUF, lakini mara kadhaa amekuwa akitumiwa na chama hicho kwa ajili ya mikakati mbalimbali pamoja na ushauri.
↧
↧
Lipumba Amtaka Rais Magufuli Atangaze Mshahara Na Marupurupu Yake
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Rais John Magufuli atangaze mshahara na marupurupu yake, kwa kuwa amejivisha joho la kuwa Rais wa wanyonge.
Profesa Lipumba amelieleza gazeti la Mwananchi kuwa Rais Magufuli amejipambanua kuwa kiongozi anayeguswa na matatizo ya wanyonge, hapendi makuu, anahimiza ukusanyaji wa mapato ya Serikali na matumizi mazuri ya fedha za umma, lakini watanzania hawajui mshahara wake ni kiasi gani
Profesa huyo aliyejikita katika masuala ya uchumi, alirejea mijadala mbalimbali iliyowahi kuibuliwa kuhusu mshahara wa Rais, ikiwamo ule uliyowahi kuibuliwa mwaka 2013 na Zitto Kabwe, wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kuwa Rais analipwa Sh32 milioni kwa mwezi.
Pia alirejea taarifa iliyochapishwa na Mwananchi, Julai 27, 2015, iliyoandikwa kutoka katika mtandao wa African Review kuwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete ni wa nne miongoni mwa marais wa Afrika kwa kupata mshahara mkubwa wa dola za Marekani 192,000 kwa mwaka sawa na dola 16,000 kwa mwezi, ambayo ni sawa na Sh32 milioni kwa mwezi. Hadi jana jioni, dola moja ya Marekani ilikuwa sawa na Sh2,187.
“Taarifa ya Ikulu ilikanusha vikali habari zilizochapishwa na Mwananchi. Ikulu ilieleza kuwa habari hizo siyo za kweli. Hata hivyo, haikueleza mshahara wa Rais na marupurupu yake ni kiasi gani?
Pia, katika mjadala wa mshahara wa Rais, Naibu Spika wa Bunge lililopita ambaye ndiye Spika wa sasa, Job Ndugai alinukuliwa akieleza kuwa mshahara wa mtu ni siri yake.
Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma wa wakati huo, Celina Kombani (kwa sasa ni marehemu) alisema kuwa ni kosa kutangaza mshahara wa Rais.
“…Kwa hivi sasa Rais Magufuli atangaze mshahara na marupurupu yake na kama mapato yake ni Sh32 milioni kwa mwezi, basi ajitolee alau nusu ya mapato hayo kuchangia elimu na afya ya wanyonge. Hatua hii itaimarisha taswira inayojengeka barani Afrika kuwa yeye ni Rais wa wanyonge,” amesema Lipumba.
Wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam wiki iliyopita, Rais Magufuli aliwataka mawaziri, naibu mawaziri na makatibu wakuu wachangie Sh1 milioni katika mishahara yao kuchangia elimu.
Pia Rais alieleza kuwa yeye mwenyewe, makamu wake na waziri mkuu watachangia Sh6 milioni kila mmoja, ili zifike Sh100 milioni kusaidia changamoto za elimu bure Mkoa wa Dar es Salaam.
Kutokana na tangazo hilo, Profesa Lipumba alisema, “Ikiwa Sh6 milioni zitakatwa katika mshahara wake wa mwezi mmoja ni wazi mshahara wake na ule wa makamu wake na waziri mkuu ni zaidi ya Sh6 milioni kwa mwezi.
“Mishahara na marupurupu ya viongozi wa Tanzania hayako wazi. Watanzania hawajui kila mwezi Rais, Makamu wa Rais na viongozi wakuu wa Serikali wanalipwa kiasi gani? Malipo ya wabunge pia hayako wazi?” alihoji.
Profesa Lipumba ambaye amewahi kuwa msaidizi wa Rais katika masuala ya uchumi kati ya mwaka 1991 na 1993, alisema kwa kuwa Rais Magufuli amejivisha joho la kuwa Rais wa wanyonge, anawajibika kuwaeleza Watanzania mshahara na marupurupu yake.
“Ikiwa mshahara ni mkubwa sana achukue hatua za kuupunguza kama alivyofanya Mwalimu Nyerere mwaka 1965.”
Hata hivyo, alisema kifungu cha Katiba cha 43 (2) kinaeleza kuwa mshahara na malipo mengineyo yote ya Rais havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba.
Profesa Lipumba alisema Rais Magufuli akitaka kupunguza mshahara wake itabidi kwanza abadilishe kifungu hicho cha Katiba.
“Anaweza kujitolea mchango wa kudumu utakaokatwa kutoka kwenye mshahara wake kusaidia sekta ya afya au elimu,”alisema.
Profesa Lipumba ambaye ni mshauri wa Benki ya Dunia (WB) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika masuala ya uchumi, alisema ili kuimarisha utawala bora ni muhimu uongozi ulio madarakani utumie mamlaka waliopewa kwa manufaa ya Taifa.
“Mishahara na marupurupu ya viongozi yawe wazi na yaamuliwe na kupangwa na taasisi iliyo huru. Kuweka utaratibu ulio wazi wa kuamua mishahara na marupurupu ya viongozi wa umma wakiwamo Rais na makamu wake, mawaziri, wabunge, majaji, makatibu wakuu na viongozi wengine,”alisema.
Alisema ni muhimu katika ujenzi wa utawala bora, uwajibikaji na uwazi wa viongozi wa umma kwa wananchi wanao waongoza.
“ Inasemekana mshahara wa mbunge katika Bunge lililopita ulikuwa Sh3.4 milioni kila mwezi.Pia mbunge alilipwa Sh8.2 milioni, nyingine kama posho ya jimbo, gharama za ofisi, mafuta, malipo ya wasaidizi wake na dereva.
“Vile Vile, mbunge anapohudhuria kikao cha Bunge alilipwa posho ya Sh80,000 za kujikimu, Sh50,000 za mafuta ya gari na Sh200,00 za kuhudhuria kikao cha Bunge, jumla ni Sh330,000 kwa siku.
“Posho ya siku moja ya mbunge ni zaidi ya mara mbili ya kima cha chini cha mshahara wa Serikali kwa mwezi mzima ambacho ni Sh150,000. Mishahara inakatwa kodi, marupurupu hayakatwi kodi,”alisema.
↧
Magufuli Atinga GHAFLA Kivukoni na Magari yenye Namba za Kawaida
Rais John Magufuli ameendelea kufanya ziara za kushtukiza, baada ya kutembelea ofisi za Kivukoni Dar es Salaam kimyakimya juzi jioni kuangalia mwenendo wa utoaji huduma za vivuko.
Mashuhuda waliokuwepo eneo hilo Jumapili jioni wakati Rais anafanya ziara hiyo, walieleza mtindo alioingia nao Dk Magufuli ulikuwa ni wa kawaida na vigumu kwa mwananchi wa kawaida kung’amu uwapo wa Rais.
Mfanyabiashara wa eneo hilo, Sharif Mkamba alisema Rais Magufuli aliingia saa 11 jioni akiwa na msafara wa magari matatu ya kawaida yaliyokuwa na namba za kiraia.
“Hakukuwa na king’ora chochote kama tulivyozoea bali ulikuwa ni msafara wa kimya kimya. Aliingia moja kwa moja kwenye zile ofisi na alitumia kati ya dakika 10 hadi 15 kabla ya kutoka,” alisema Mkamba.
Said Likoko alisema kuwa baada ya kugundua kati ya magari matatu alikuwepo Rais, walisogea kufuatilia kwa kina kwa kuwa haijazoeleka na walitegemea huenda baadhi ya watumishi wangewajibishwa.
“Aliteremka na kumuuliza aliyemkusudia na taarifa tulizozipata jana zinadai hakumkuta huyo bosi, sijui ni meneja au ofisa sisi hatujui,” alisema Likoko ambaye hujishughulisha pia na biashara ndogondogo eneo la kivukoni.
Likoko alisema pamoja na kwamba aliingia kimya kimya, Rais Magufuli hakusita kuwasalimia wasafiri waliokuwa wakisubiri kivuko wakati alipofanya ziara hiyo.
Alieleza kuwa kama wananchi walifurahishwa na hatua hiyo ya Rais, kwa kuwa watendaji wengi hawafanyi kazi siku za wikiendi licha ya huduma zake kufanyika siku zote.
Tangu jana asubuhi kumekuwa na video inayosambaa ikimuonyesha Rais Magufuli akiwa Kivukoni akitembea kwa miguu ndani ya eneo hilo huku akishangiliwa na wasafiri waliokuwa wakingoja kivuko.
Hata hivyo, jitihada za kutafuta mamlaka husika kueleza kwa undani malengo ya ziara hiyo ziligonga mwamba baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue kutopokea simu.
Ofisa habari wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) Theresia Mwami, alitaka utafutwe uongozi wa juu kueleza yaliyojiri kwenye ziara hiyo kwa kuwa yeye yupo likizo.
↧
Rais Mugabe Atimiza miaka 92.....Wasaidizi wake Wasema Atawania Tena Urais Mwaka 2018
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimiza umri wa miaka 92 huku chama chake kikisema atawania tena urais 2018.
Mnadhimu wake mkuu alisema kiongozi huyo ambaye ameongoza nchi tangu mwaka 1980, bado ana uwezo kamili wa kuongoza Serikali licha ya tetesi kwamba hawezi kuongoza kutokana na umri.
Akizungumza na gazeti la Serikali Sunday Mail, Katibu Mkuu wa Rais Misheck Sibanda alisema tetesi hizo si za kweli na hazina msingi kwani Mugabe ana ratiba ya wiki nzima kutekeleza kazi za Serikali na chama.
Rais Mugabe ambaye aliapa kuongoza nchi hadi atakapokufa, alishinda kipindi kingine cha urais cha miaka mitano kwenye uchaguzi wa mwaka 2013 uliofanyika chini ya katiba mpya inayoweka ukomo wa kuongoza kwa vipindi viwili tu vya miaka mitano.
Chama chake tayari kimetangaza kumpitisha Mugabe kama mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2018.
Mugabe amekua kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Ni mwenyekiti wa chama tawala cha Zanu. 1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 Rais wa Zimbabwe.
Utawala wa Mugabe umeitwa wa kidikteta tangu mwaka 2002 kutokana na kudharau haki za binadamu nchi Zimbabwe.
↧
Uingereza Yammwagia Sifa Rais Magufuli Kwa Kasi Yake Ya Kukusanya Mapato na Kupambana Na Wala Rushwa
Nchi ya Uingereza imempongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wa serikali yake hususani katika kupambana na ubadhirifu wa mali za umma na ufisadi, kwa siku chache alizokaa madarakani.
Sifa hizo za Uingereza zimewasilishwa jana Ikulu jijini Dar es Salaam na Balozi wa nchi hiyo,, Balozi Dianna Melrose.
Balozi Melrose alieleza kuwa nchi yake imeridhishwa na juhudu za Rais Magufuli katika kulinda fedha za umma na kuahidi kushirikiana naye hususan katika kuimarisha idara ya Mahakama na Intelijensia nchini.
“Tunadhani ameonesha msimamo mkali dhidi ya rushwa na ufisadi, na miongoni mwa mambo ambayo tumezungumza ni namna ya kufanya kazi pamoja katika kupambana na rushwa. Tuna mazungumzo katika kuimarisha mifumo ya kiintelijensia na mahakama,” alisema Balozi Melrose.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alikutana na rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete Ikulu lakini mazumgumzo kati yao hayakuwekwa wazi.
↧
↧
TRA Yatoa Tamko ya Kuhusu Matumizi ya EFD Kwenye vituo vya Mafuta.
TANGAZO KWA UMMA
MATUMIZI YA MASHINE ZA EFD KATIKA VITUO VYOTE VYA MAFUTA NCHINI:
Kufuatia Tangazo kwa Umma lilitolewa kwenye vyombo vya Habari na kuchapishwa kwenye Magazeti, Uongozi wa Chama cha Wamiliki na Waendeshaji wa Vituo vya Mafuta Nchini (TAPSOA) ulikutana na Kaimu Kamishna Mkuu na kufanya majadiliano ya msingi kuhusu matumizi ya EFD na kufunga Mashine za EFD Maalum katika vituo vya mafuta kwa ajili ya kutolea risiti za mauzo. Makubaliano ya pamoja kutokana na majadiliano ni kwamba, agizo la Kaimu Kamishna Mkuu liendelee kutekelezwa katika utaratibu ufuatao;
- Wamiliki wote wenye vituo vya mafuta walio katika kundi la Makampuni makubwa wanaoagiza mafuta na kutumia Mawakala kusambaza/kuuza mafuta kwa wateja (CODO) wakamilishe kufunga Mashine za EFD katika vituo vyao vyote Nchini kama ilivyokubalika katika kikao hicho (yaani kufikia tarehe 15 Machi 2016).
- Wamiliki wote wenye vituo vya mafuta walio katika kundi la Makampuni wanaoagiza mafuta na kusambaza/ kuuza mafuta kwa wateja wao wenyewe (COCO) walioanza na wanaofunga Mashine za EFD kwenye pampu za vituo vyao waendelee kufanya hivyo wakati Mamlaka ya Mapato kwa kushirikiana na Wasambazaji na Uongozi wa TAPSOA wakiendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazojitokeza za kiufundi na gharama ya Mashine za EFD kwa ajili ya pampu husika.
- Wamiliki/Waendeshaji wote wenye vituo vya mafuta walio katika kundi la Makampuni ya watu binafsi wanaonunua mafuta kutoka kwa Makampuni mama na kusambaza/kuuza kwa wateja moja kwa moja (DODO) ambao hawajafunga Mashine za EFD kwenye pampu waendelee kutumia Mashine za EFD za kawaida (ETR) wakati changamoto za kiufundi, mtandao na bei za Mashine za EFD zikishughulikiwa.
Mamlaka ya Mapato kwa kushirikiana na uongozi wa TAPSOA kwa pamoja tutaendelea kuhimiza Matumizi ya Mashine za EFD katika vituo vya mafuta vyote Nchini.
Ni vyema kila Mfanyabiashara akatambua wajibu wake na kujenga utamaduni wa kutekeleza matakwa ya sheria kwa hiari bila kushurutishwa.
Pamoja Tunajenga Taifa Letu
KAIMU KAMISHNA MKUU
↧
Waziri Kitwanga Aagiza Mabadiliko Makubwa Idara Ya Uhamiaji
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga ameagiza yafanywe mabadiliko makubwa katika Vitengo mbalimbali vya Idara ya Uhamiaji ili kuboresha huduma na kuimarisha uadilifu katika Vitengo hivyo.
Mheshimiwa Kitwanga ametoa maagizo hayo leo wakati alipofanya kikao na Viongozi wa Idara ya Uhamiaji ambapo pia kilihudhuriwa na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwemo Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara. Kikao hicho kilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katika kikao hicho, Mheshimiwa Kitwanga ameagiza watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji walioko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, wahamishwe na kupelekwa maeneo mengine nchini, wakiwemo wale wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Wengine watakaohamishwa ni kutoka Kitengo cha Pasipoti, Uhasibu, Hati za Ukaazi na Kitengo cha Upelelezi, vyote vya Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.
Aidha ameagiza pia kuwa Wakuu wote wa Vitengo vya Upelelezi vya wilaya zilizopo jijini Dar es Salaam, na pia wale wa Vituo vya Tunduma, Mtukula, Holili na Kasumulo, wahamishiwe maeneo mengine, na pia watumishi wote waliokaa kwa zaidi ya miaka mitatu katika Vituo hivyo.
Amesema hatua hii inayochukuliwa sasa ni mwanzo tu wa mabadiliko makubwa yatakayofanywa katika Idara ya Uhamiaji ili kuboresha huduma zinazotolewa na Idara hii ambayo ni moja ya Idara muhimu za Serikali.
Amesema katika kuisafisha Idara hii, uangalifu mkubwa utachukuliwa ili kuhakikisha kuwa hakuna mtumishi anayeonewa wala kupendelewa, lakini lengo kubwa ni kuvunja mtandao wa wapokea rushwa na wale wasiowajibika.
Amesema kufuatana na utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa matatizo ya rushwa katika Idara ya Uhamiaji yanashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na asilimia 30, asilimia 20 ni uongozi mbovu na asilimia 20 ni matumizi mabaya ya madaraka. Asilimia 15 inahusisha vitendea kazi wa mifumo hafifu ya kufanya kazi, asilimia 10 huduma mbovu na asilimia 5 ukabila na upendeleo.
Amewataka Viongozi na watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya kazi na waepuke vitendo vya kupokea rushwa na kusaidia wahamiaji haramu na wauza madawa ya kulevya.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
23 Februari, 2016
↧
Makala : Fahamu Kuhusu Ndumba Za Kichawi Na Jinsi Ya Kujikinga Nazo.
FAHAMU KUHUSU NDUMBA ZA KICHAWI NA JINSI YA KUJIKINGA NAZO.
Mwandishi : Dokta. Mungwa Kabili….0744 000 473
Nimekuwa nikipokea barua pepe kutoka kwa watu mbalimbali, wakitaka kujua masuala mbalimbali kuhusu ulozi, uchawi na jinsi ya kujikinga dhidi ya uchawi na ulozi.
Kwa kuwa muda na nafasi haviniruhusu kumjibu kila mmoja kwa wakati wake, nitayajibu maswali yote hapa bloguni.
SWALI : NIMESIKIA KUWA WACHAWI HUWA HAWAFI UPESI.JE KUNA UKWELI WOWOTE KATIKA HILO ? NA KAMA NI UKWELI, JE NI KITU GANI HUWAPA UWEZO WA KUISHI MAISHA MAREFU ?
DOKTA. MUNGWA KABILI ANAJIBU :
Ni kweli kabisa wachawi wengi huwa hawafi upesi na zipo sababu kuu mbili zinazo wafanya wachawi waishi muda mrefu :
1.Kwanza : NDUMBA ZA KINGA: Wachawi wa nchi hutumia ndumba za kinga, ndumba hizo husaidia kuwakinga dhidi ya shari za wanadamu na majini wabaya na hivyo kuwafanya waishi siko zote walizo pangiwa na Mwenyezi Mungu. Ikitokea mchawi mwenye kinga hizo, amefariki dunia, basi anakuwa amefariki kwa mkono wa Mungu mwenyewe na si mwanadamu. Watu wengi hufa kwa mikono ya wanadamu waovu na shari za mapepo wabaya. Nitataja ndumba mbili zenye nguvu zinazo tumiwa na wachawi.
i. Kuna ndumba moja ya kichawi, ambayo kwa lugha za kisukuma na kinyamwezi hujulikana kama LUFAKALE.
Ndumba hii ya kichawi akichanjiwa mtu humkinga dhidi ya shari za wanadamu na mapepo wabaya. Humfanya aishi kwa kadri Mungu alivyop mkadiria. Humkinga na kumuepusha na shari kama ajali (hususani ajali za kichawi ), kufa kwa kurogwa nakadhalika.
Ndumba hii ina nguvu sana kiasi kwamba, mtu aliye chanjiwa , inapofika siku yake ya kufa roho yake huchukua muda mrefu sana kuacha mwili wake. Inaweza kumchukua mwaka mmoja hadi miaka kumi. Mtu anakuwa anonyesha dalili zote za kufa, au anakuwa ameisha kufa kabisa, lakini anakuwa bado anaongea. Nikipata nafasi siku zijazo nitaelezea kwa kina kuhusu ndumba hii.
ii. Ndumba ya pili, inatokana na mti unaitwa Msonihya . Huu ndio mti mkuu wa wachawi. Mtu huu una nguvu sana za kichawi. Mti huu hutumika kutengeneza hirizi ambayo huvaliwa mkononi kama bangili au kuwekwa nyumbani. Hakuna pepo, jinni wala kitu chochote kile kibaya kinaweza kumdhuru mtu aliye pewa hirizi hii.
Simba , nyoka wa kawaida pamoja na samba & nyoka wa kichawi au mnyama yoyote yule hawezi kumdhuru.
2. NDUMBA ZA KUWAWEZESHA KUONA MAMBO YATAKAYO TOKEA MBELENI.
Wachawi wa nchi wanazo ndumba zenye uwezo wa kuwasaidia kujua mambo yatakayo tokea mbeleni, hivyo basi kama kuna hatari yoyote ile inaenda kutokea kesho yake kama vile ajali au shari yoyote ile nakadhalika, wao wanakuwa wameshajua siku moja kabla na hivyo wanakuwa na nafasi ya kuchukua tahadhari mapema.
JINSI WANAVYO FANYA ILI KUWA NA UWEZO WA KUONA MAMBO YATAKAYO TOKEA.
Zipo njia mbalimbali wanazo tumia, ili kupata uwezo wa kuona mambo yatakayo tokea mbeleni, lakini kati ya njia hizo njia ifuatayo ni maarufu sana miongoni mwa wachawi na walozi.
i. Wanachukua ubongo wa fisi
ii. Wanachukua ubongo wa kunguru
iii. Wanachukua ubongo wa ndege anaitwa Mbesi. Ndege huyu hupatikana mtoni na chakula chake kikuu ni mizoga ya ndege, wadudu, samaki na wanyama. Katika ulimwengu wa wachawi, ndege huyu hujulikana kama mtaalamu wa kugundua mahali ilipo mizogo iliyo kufa.
Kwa mfano tuchukulie mkoa wote wa Dar Es Salaam ni pori, huyu ndege yupo mbagala halafu maeneo ya msasani kuna ndege,samaki,wadudu au mnyama amekufa, basi usiku wa siku hiyo ndege huyu ataota mahali ulipo mzoga huo, na kesho yake atapaa moja kwa moja hadi sehemu ulipo mzoga huo na kuufanya kuwa kitoweo chake.
Vitu vyote hivyo hapo juu hukaushwa na kusagwa kwa pamoja na kisha kuchanganywa na ndumba tatu za kichawi ambazo sitazitaja hapa kwa sababu maalumu.
Baada ya hapo, mchawi husika atachanjiwa ndumba hizo kichwani pamoja na kwenye zote nne za mwili.
Basi, mchawi huyo anakuwa na uwezo wa kuona ndotoni kila kitu kitakacho tokea kesho yake na kuendelea.
SWALI NAMBA MBILI : NASIKIA WATU WANAZUNGUMZA KUHUSU DUDUMIZI. JE DUDUMIZI NI NINI NA ANATUMIKAJE KATIKA UCHAWI
DR. MUNGWA KABILI ANAJIBU ;
Dudumizi ni ndege anaye patikana porini. Katika ukanda wa Pwani, ndege hawa wanapatikana kwa wingi sana katika mapori ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Kisarawe vijijini ( Hususani katika vijiji vya Mwaneromango, Nzenga na Msanga ) pamoja na wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
Ndege hawa wana macho mekundu, mkia mrefu pamoja na kucha ndefu sana.
Dudumizi hula wadudu, mijusi, nyoka, mayai,makinda, matunda, mizoga na wanyama wadogo pia.
Dudumizi wengi wana mabawa yenye rangi ya kahawia nyekundu na kichwa cheusi. Lakini pia wapo Dudumizi wenye mkia wa rangi ya shaba, Dudumizi weusi,Dudumizi wenye koo lenye rangi nyeusi, Dudumizi wenye kichwa chenye rangi ya buluu, pamoja na Dudumizi wenye nyushi nyeupe.
MAAJABU YA DUDUMIZI.
Dudumizi ni ndege mwenye maajabu mengi sana, kwa muwa muda hauturuhusu, leo nitataja mawili tu.
AJABU LA KWANZA : Ana uwezo wa kujifungua kamba mwenyewe. Kwa mfano, ukienda kwenye kiota cha Dudumizi, halafu ukawafunga makinda wa Dudumizi kamba kisha ukafunga na kwenye mti. Kesho yake asubuhi unakuta ile kamba imejifungua yenyewe . Ukimnchukua Dudumizi ukampeleka nyumbani kwako, ukamuweka kwenye banda, halafu ukamfunga kamba akiwa bandani, ukafunga banda halafu kamba hiyo ukaenda kuifunga kwenye mti au kitu chochote kile, kesho yake unakuta Dudumizi amefungua hiyo kamba na kuondoka, hata kama kamba hiyo itakuwa kubwa na nzito kwa kiasi gani.
AJABU LA PILI : Kwa kawaida Dudumizi hutaga mayai kati ya mawili hadi matano. Dume la Dudumizi ambalo huwa dogo kwa umbo kuliko jike, ndio linalo hatamia mayai na kutunza makinda.
JINSI WACHAWI WANAVYO MTUMIA NDEGE DUDUMIZI.
Katika ulimwengu wa wachawi, Dudumizi ana matumizi mengi sana kichawi. Leo nitataja mawili tu kwa sababu ya muda.
1.Kamba iliyo tumika kuwafunga Dudumizi na ikajifungua yenyewe, ikichanganya na ndumba za kichawi pmaoja na vizimba vyake, hutumika kuwafungua kichawi, watu walio katika vifungo mbalimbali vya kichawi kama vile vifungo katika biashara, vifungo katika mapenzi na ndoa, vifungo katika rizki , vifungo vya mizimu, nakadhalika.
2. Dudumizi hutumika, kutengeneza ndumba maalumu kwa wale wanawake wanao penda kuwa inamisha waume zao.
SWALI NAMBA TATU: JE NI KWELI KUWA WACHAWI WANA UWEZO WA KUMTIA MTU MIKOSI NA KUFUNGA RIZIKI YAKE?
DOKTA.MUNGWA KABILI ANAJIBU ;
Ni kweli kabisa,wachawi wana uwezo wa kumtia mtu mikosi . Zipo njia mbalimbali wanazo tumia wachawi katika kuwatia watu mikosi, ila kutokana na ufinyu wa nafasi, nitaelezea moja hapa ;
Katika njia hii, wachawi wakitaka kumtia mtu mikosi, hufanya mambo yafuatayo :
i. Wanachukua hela ambayo haitumiki
ii. Mavi ya mbwa mweusi ambayo ameyanya usiku
iii.Mkaa ulio kwisha tumika, ambao umetumika mahali ambapo watu hawalali kama vile kilioni au kwenye bara na migawaha inayo kesha lakini mara nyingi, huchukua mkaa wa kilioni.
iv. Mavi ya ndege anaitwa Mumbi. Huyu ndege aitwae Mumbi anapatikana porini. Anafanana sana na bata na ana puyanga la rangi nyekundu.
v.Shahidi la kaburini pamoja na ndumba zingine za kichawi
vi.Kitu chochote cha mtu aliye kusudiwa kutiwa mikosi kama vile picha yake, mchanga alipokanyagia, mate, kucha, au chochote kile.
Baada ya hapo, mchawi huyo atakwenda kaburini usiku wa manane na kuvizika vitu vyote nilivyo vieleza hapo juu, huku akisema maneno ya kichawi ambayo siwezi kuyataja hapa. Basi mtu aliye kusudiwa na uchawi huu, kama hana kinga, ata andamwa na mikosi mikubwa na mizito katika maisha yake yote.
SWALI NAMBA NNE : DOKTA, NINAPENDA KUJUA NINI KINGA DHIDI YA UCHAWI? NIFANYE NINI ILI UCHAWI USINIDHURU ?
DOKTA MUNGWA KABILI ANAJIBU:
Kama wewe ni Muislamu, uwe mtu wa swala sana, kufanya duwa na visomo ( Ruqiya) na kutoa Dhaka na swadaka kwa mola wako, na kama wewe ni Mkristo, basi uwe mtu wa kusali sana, kufunga na kuomba bila kusahau kutoa sadaka na fungu la kumi kwa Mungu wako.
Lakini kama unajijua, hauwezi kufanya mambo niliyo yataja hapo juu, basi unatakiwa kupata kinga ya mwili wako.
Zipo kinga nyingi zenye nguvu dhidi ya uchawi na ulozi. Zipo Kinga, mchawi akikutupia uchawi unamrudia mwenyewe ana kufa papo hapo au anapooza kwanza kwa muda mrefu kisha anakufa pia zipo kinga ambazo mchawi , akitaka kukutupia uchawi, anashindwa kukuona katika rada zake za kichawi.
Hii ni kinga muhimu sana na haiishii kukukinga mwili wako pekee.Inakinga nyumba, biashara, kiti cha ofisi nakadhalika.
KINGA HII HUJULIKANA, KAMA KINGA YA KUFICHA KIVULI CHAKO.
Inaitwa Kinga ya Kuficha kivuli, kwa sababu wachawi wanapo taka kumloga mtu, huchukua na hushambulia kivuli chake. ( HAPA SIZUNGUMZII KIVULI CHA JUANI, NAZUNGUMZIA KIVULI CHAKO CHA KIROHO, YAANI NAFSI YAKO )
Bila kuona kivuli chako, wachawi hawawezi kukuloga.
Kinga hii hukupa uwezo wa kutokuonekana kwenye rada za wachawi. Kwao unakuwa ni sawa na mtu aliye kufa tu, kwa sababu mtu aliye kufa kivuli chake hakionekani na pia hawezi kurogwa na uchawi wa aina yoyote ile.
JINSI YA KUFICHA KIVULI CHAKO KISIONEKANE NA WACHAWI.
i. Chukua nywele za saluni
ii. Chukua mzizi wa mti ulio katisha njia
iii. Chukua tawi la mti unaitwa Ututukanga. Huu mti wa Ututukanga unapatikana porini na huwa linaonekana shina lake na matawi yake tu, lakini mzizi wake huwa hauonekani.
iv. Unachukua mti unaitwa Msonihya
v. Unasaga pamoja na mti unaitwa mwavi.
vi. Baada ya hapo unachukua kuku mweusi, unamfunga kwenye kitambaa cheusi bila kumchinja, unachukua chungu cheusi, unamuunguza mpaka anakuwa mkaa, halafu unamsaga pamoja na miti iliyo tajwa hapo juu, unachanganya na mafuta ya simba.
vii. Unachukua buja ama dulya la ugali wa kilioni
viii. Kamba ya kitanda alicho lalia maiti, au kama maiti ipo kwenye nyumba ya nyasi, unachomoa nyasi wakati maiti imo ndani.
ix. Unachimba mzizi wa mti unaitwa mputika bila kivuli chako kugusa mti..
x. Unaunguza vyote kwa pamoja ukiwa na kaniki nyeusi bila kuvaa nguo yoyote usiku wa manane
xi. Unaipika njia panda pamoja na mafuta ya mti mmoja wa porini ambao jina lake linahifadhiwa hapa.
Baada ya hapo, mtu atachanjiwa na kuongeshwa pamoja na kufanyiwa tambiko maalumu.
Basi wachawi watakuwa wakijaribu kutaka kukutupia uchawi, wanakuwa hawakauoni kwenye rada zao za kichawi
SWALI NAMBA TANO : HABARI YAKO DOKTA. NASUMBULIWA SANA NA WIZI NYUMBANI KWANGU. JE IPO NDUMBA YA KUMKAMATA MWIZI ?
DOKTA MUNGWA KABILI ANAJIBU :
Zipo ndumba nyingi za kuwakamata wizi. Leo nitataja ndumba rahisi kabisa ya kumkata mwizi. Ukifanya ndumba hii, basi mwizi atajileta mwenyewe na kuomba msamaha.
i. Unachukua kinyonga akiwa mzima
ii. Unaponda majani ya kisamvu
iii.Unachukua na changarawe za njiani ambazo, hutembea mvua ikinyesha.
iv. Huyo kinyonga unamuweka kwenye hayo majani ya kisamvu pamoja na hizo changarawe, unafunga kwenye kitambaa cheusi halafu unafunga jikoni, kwenye sehemu inayo toka moshi. Utamuacha hapo kwa muda wa siku saba.
Baada ya siku sita, unamtoa hapo kwenye moshi, unasaga ukiwa umefumba macho halafu unaenda kuvifunga kwenye mti kwa muda wa siku saba. Kabla siku saba hazijaisha, mwizi wako atarudi mwenyewe. Na kama mwizi yumo humo humo ndani, atajisalimisha mwenyewe mara moja.
Hii dawa moja tu, lakini zipo nyingine nyingi.
SWALI NAMBA SITA : DOKTA NASIKIA WACHAWI WANA UWEZO WA KUTUMIA UCHAWI KUMSHIKA MWANAUME KIMAPENZI . JE NI KWELI? NA WANAFANYAJE FANYAJE ?
DOKTA. MUNGWA KABILI ANAJIBU.
Katika masuala ambayo uchawi una ishi na kutawala basi ni suala la mapenzi.
Asilimia kubwa ya watu wanao enda kwa waganga, huenda huko kwa sababu ya mapenzi au kwa sababu ya mambo yanayo sababishwa na mapenzi.
Uchawi wa mapenzi upo wa aina nyingi sana. Nikisema nianze kutaja na kuelezea kwa kila aina ya uchawi na ulozi katika mapenzi hapa, sitamaliza kwa sababu upo uchawi wa aina nyingi sana.
Nitataja na kuelezea kwa ufupi sana, aina chache za uchawi katika mapenzi, halafu nitaelezea aina moja ya uchawi wa mapenzi ambao ni uchawi hatari na wenye nguvu sana.
KUMSHIKA MWANAUME KATIKA MAPENZI ; Kumshika mwanaume katika mapenzi, wachawi huchukua njiwa wawili jike dume walio zaliwa kiota kimoja pamoja na kiota chawe, kisha njiwa hao huchinjwa , hupasuluwa na mioyo yao hunyofolewa, huchemshwa kwenye mafuta ya mti mmoja unapatikana porini, halafu husagwa hadi kuwa unga unga. Baada ya hapo huchukua njugu mawe nyeusi moja, huchanganya na mti unaitwa mlama, pamoja na miti mingine mitatu ya porini, kisha husagwa pamoja na ile mizoga ya njiwa.
Vyote hivi kwa pamoja, huchanganywa na vizimba vitatu vya ndumba za kichawi, halafu mwanaume huwekewa kwenye chakula, basi mwanaume huyo atakuwa hasemi chochote kwa mwanamke huyo.Mwanamke atakuwa mama ake atakuwa baba ake. Ni uchawi mbaya sana huu.
KUMFANYA MWANAUME ASIENDE NJE YA NDOA :
Kumfanya mwanaume asiende nje ya ndoa, wachawi huchukua kamba ya mbuzi, moyo wa kondoo, mti unaitwa INAMA NIKUCHUME ( Mti huu unapatikana Kigoma tu, na watu wa kigoma ndio huuita jina hilo), mti unaitwa Inyazya kisha vinasagwa kwa pamoja halafu vinachanganywa na nta ya nyuki, kisha wanatafuta kucha, au nywele, au ndevu, au uzi wa nguo yake yoyote, halafu vinakaangwa kwa chumvi ya mawe pamoja na vizimba vya zote \nilizo zitaja hapo juu, kisha vinafungwa kwenye kitambaa chekundu, halafu vinafukiwa mlangoni au kwenye mti wowote. Basi mwanaume huyu hawezi kwenda nje ya ndoa yake.
MWANAUME AKUONE WEWE TU KILA ANAPOKUWA NA MWANAMKE MWINGINE : Wachawi hutchukua maji ambayo mwanamke ametumia kunawa uso wake kisha huchanganya na ndumba 13 za kichawi pamoja na vizimba vyake kisha kutengeneza ndumba itakayo mfanya mume wa mwanamke huyo kuwa anaumuona mke wake wakati wote na pia kuwa anaona kama anatokewa na mke wake kila anapo kuwa na michepuko.
KUMFANYA MUME AKUPE MSHAHARA WAKE WOTE AU PESA ZAKE ZOTE KILA AKIZIPATA: Uchawi huu umewalostisha wanaume wengi sana. Hapa mchawi anacho chukua manii za mwanaume aliye mkusudia, ana changanya pamoja na baadhi ya vitu alivyo pewa na mwanaume huyo, halafu vinaenda kutengenezwa kichawi kwa kutumia ndumba za kichawi, basi mwanaume huyo atakuwa kila akipata mshahara wake anapeleka zote kwa mwanamke huyo. Asipojistukia mapema, anaweza uza kila kilicho chake.
KUMVUTA MPENZI : Ipo miti mitatu inapatikana porini, miti hutumika kumuita kichawi mwanamke au mwanaume aliye kusudiwa.
KUMTEGA DAWA ZA MAPENZI MWANAMKE AU MWANAUME.
Chaurembo kaenda kwa wachawi, na kuwaomba wampe msaada wa kichawi ili aweze kumteka kimapenzi Ndugu., Maridadi.
Wachawi watamchukua Chaurembo, watampa ndumba za aina tatu. Ndumba ya kwanza, atachanjiwa, kichwani na katika pembe zote za mwili wake. Ndumba ya pili atatumia kunywa, na ndumba ya tatu atatumia kuoga na kuchoma.
Sikui tatu baada ya kuanza kutumia ndumba hizo, Chaurembo atamuota Maridadi anapita katika sehemu ambayo Chaurembo anaifahamu. Chaurembo atatakiwa kuikariri ndumba hiyo.
Kesho yake, saa saba mchana, Chaurembo atatkiwa kwenda hadi mahali alipo muona Maridadi akiwa anapita,akifika katika eneo hilo, atatakiwa kumwaga dawa aliyo pewa.
Maridadi lazima atapita katika eneo hilo, na akipita tu, basi anakuwa amenasa kwenye penzi la Chaurembo.
Maridadi atamtafuta Chaurembo kwa udi na uvumba na atafanya kila kitu anacho kitaka Chaurembo.
Huu ni uchawi mbaya sana na hutumika hata katika mambo yasiyo ya mapenzi.
SIKU NYINGINE NITAELEZEA KWA UREFU SANA KUHUSU UCHAWI MBALIMBALI UNAO TUMIKA KATIKA MAPENZI.
SWALI NAMBA SABA : JE NI KWELI WACHAWI WANA UWEZO WA KUWAACHANISHA WAPENZI KWA KUTUMIA UCHAWI.
DOKTA MUNGWA KABILI ANAJIBU :
Ni kweli kabisa, wachawi wana uwezo wa kuwaachanisha wapenzi. Mke na mume walio ona kwa sherehe ya mamilioni wanaweza kuachana ndani ya wiki moja.
Zipo njia nyingi sana wanazo tumia, ila leo nitaitaja moja:
i.Wanachukua mti unaitwa mpuga mbu.
ii. Mkia wa ndege wa porini anaitwa katyente
iii. Picha ya mke na mume walio kusudiwa pamoja na majina yao.
iv. Wanachanganya na vizimba vyake.
v. Vitu vyote hivyo vinasagwa kwa pamoja, kisha vinakaangwa kwa kutumia chumvi ya mawe, halafu vinaen da kuchomwa jalalani.
Hata kama wanapendana vipi,wote wataachana.
Ndumba hii ndio inayo tumika pia kushusha thamani ya cheti cha mtu. Hata kama amesoma vipi, hawezi kupata kazi kama akifanyiwa uchawi huu.
Kwa leo naomba niishie hapo, kesho nitaendelea tena na makala haya.
MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA DOKTA. MUNGWA KABILI, MTALAAMU ALIYE BOBEA KATIKA MASUALA YA ULIMWENGU USIO ONEKANA. ANAPATIKANA JIJINI DAR ES SALAAM, KWA SIMU NAMBA 0744 000 473.
KWA HABARI ZAIDI KUHUSU ULIMWENGU USIO ONEKANA, TEMBELEA KILA SIKU ;
↧
Mkazi Wa Mafinga Aporwa Sh.milioni 12 Dar.
MKAZI wa Mafinga, David Isack ( 32) alivamiwa na majambazi na kuporwa sh.milioni 12 ambazo alikuwa akipeleka katika Benki ya DTB, ambapo alivamiwa na watu watano wanatuhumiwa kuwa ni majambazi wakiwa na usafiri wa pikipiki mbili aina ya boxer.
Akizungumza na waandishi wa habari ijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo lilitokea Februari 12 mwaka huu katika eneo la Uwanja Ndege , katika kurupushani za kutaka kuchukua fedha hizo walitokea askari na kuwazingira na kisha kuanza kukimbia na kuweza kudondosha bunduki aina ya SMG pamoja na risasi 24 ambazo zilitakiwa kutumika katika tukio hilo.
Amesema askari walipowakamata wananchi walikusanyika katika tukio hilo na kuanza kuwapiga watu wanaodaiwa kuwa majambazi mpaka kupoteza maisha kutokana kushambuliwa huko na wengine watatu waliweza kukimbia na kiasi hicho cha fedha.
Kamishna Sirro amesema Isac alikuwa akitokea benki ya NMB na kwenda kupeleka fedha hizo katika benki ya DTB iliyopo Quality Plaza.
Katika operesheni nyingine imefanikiwa kukamata bastola moja ambayo ilipatikana Februari 19 mwaka huu maeneo ya Kiwalani Kwa Gude kutokana na polisi kupata taarifa juu ya watu kujificha katika kichaka kwa ajili ya kufanya uhalifu na baada ya kugundua polisi wapo eneo hilo walikimbia na kuacha silaha hiyo na jeshi la polisi linafanyia kazi mmiliki wa silaha.
Hata hivyo Jedhi la Polisi Kanda Maalumu linawashikilia watu wane wanaodaiwa kuwa ni majambazi sugu waliowakamata eneo la Buguruni kwa Mnyamani ambao ni Mohamed Hassan maarufu kwa jina Kidali (21)Mkazi wa Vingunguti Speco,Hamis Alli (20) Mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani, Adam Salum (23) Mkazi wa Buguruni kwa Madenge, Bakari Hamis (19) Mkazi wa Buguruni.
Aidha amesema katika taarifa usalama Barabarani wameweza kukusanya zaidi ya Sh. Bilioni moja iliyotokana na makosa ya magari kuanzia Januari 02 hadi Februari 22 mwaka huu.
↧
↧
CUF Watoa Tamko Zito Kuhusiana Na Kukamatwa Kwa Mwanamkakati wa Maalim Seif
Wiki iliopita, mnamo tarehe 16 Februari, 2016, aliyekuwa mjumbe wa Timu ya Kampeni ya Chama Cha Wananchi (CUF), Ndugu Mohamed Ahmed Sultan Al-Mugheiry (maarufu kwa jina la Eddy Riyami), alipokea barua ya wito kutoka kwa Jeshi la Polisi Zanzibar ikimtaka kufika Makao Makuu ya Polisi, Ziwani, Zanzibar siku inayofuata, yaani tarehe 17 Februari, 2016, saa 2 asubuhi kwa kile kilichoelezwa kwamba “kuna mambo muhimu yanayomhusu” ambayo walitaka kuzungumza naye.
Bila ya kukosa, Eddy Riyami aliitikia wito huo na kufika Makao Makuu ya Polisi, Zanzibar na kuonana na SSP Simon S. Pasua wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID).
Hata hivyo, hakuhojiwa na badala yake alipewa simu na kutakiwa azungumze na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Bw. Salum Msangi ambaye alimwambia arudi tena Jumatatu, tarehe 22 Februari, 2016.
Hata hivyo, hakuhojiwa na badala yake alipewa simu na kutakiwa azungumze na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Bw. Salum Msangi ambaye alimwambia arudi tena Jumatatu, tarehe 22 Februari, 2016.
Eddy Riyami, akiwa raia mwema, alirudi tena jana kama alivyoagizwa. Alipofika hapo alihojiwa na Polisi na baadaye mwanasheria aliyefuatana naye akatakiwa kutafuta wadhamini wawili watakaomdhamini hadi atakapoitwa tena.
Wakati mwanasheria wake aliporudi na wadhamini, akaelezwa kwamba Polisi imebadili uamuzi wake na imeamua kumuweka ndani hadi leo, tarehe 23 Februari, 2016.
Mwanasheria na familia yake wakatakiwa kwenda tena Makao Makuu ya Polisi hiyo leo, saa 3 asubuhi. Walipofika leo asubuhi, wakaambiwa kwamba DCI kaacha maagizo kuwa suala la Eddy Riyami liachwe kwanza na wao warudi tena saa 6 mchana.
Wakati mwanasheria wake aliporudi na wadhamini, akaelezwa kwamba Polisi imebadili uamuzi wake na imeamua kumuweka ndani hadi leo, tarehe 23 Februari, 2016.
Mwanasheria na familia yake wakatakiwa kwenda tena Makao Makuu ya Polisi hiyo leo, saa 3 asubuhi. Walipofika leo asubuhi, wakaambiwa kwamba DCI kaacha maagizo kuwa suala la Eddy Riyami liachwe kwanza na wao warudi tena saa 6 mchana.
Hadi tunapotoa taarifa hii, hakujapatikana maelezo yoyote ya msingi juu ya kinachoendelea na wala Eddy Riyami hajafikishwa Mahakamani kusomewa mashtaka yoyote.
La ajabu zaidi, ni kwamba hata mke wake alipofika kituo cha polisi cha Madema anakoshikiliwa kwa ajili ya kwenda kumuona, hakuruhusiwa kumuona.
Kutokana na mwenendo huu, Chama Cha Wananchi (CUF) kinalichukulia suala hili kwamba ni mwendelezo wa vitendo vya unyanyasaji wa kisiasa dhidi ya wapinzani wa CCM, vitendo ambavyo tunaamini vinafanywa kwa shinikizo la wanasiasa.
La ajabu zaidi, ni kwamba hata mke wake alipofika kituo cha polisi cha Madema anakoshikiliwa kwa ajili ya kwenda kumuona, hakuruhusiwa kumuona.
Kutokana na mwenendo huu, Chama Cha Wananchi (CUF) kinalichukulia suala hili kwamba ni mwendelezo wa vitendo vya unyanyasaji wa kisiasa dhidi ya wapinzani wa CCM, vitendo ambavyo tunaamini vinafanywa kwa shinikizo la wanasiasa.
Itakumbukwa kwamba kwa muda mrefu tokea wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015 tumekuwa tukitoa tahadhari za kuwepo mipango ya kuwakamata viongozi wa CUF na wanaharakati wengine ili kufanikisha malengo ya kisiasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tuna kila sababu ya kuamini kwamba hatua ya kumkamata Eddy Riyami na kumuweka ndani bila ya kumfikisha Mahkamani ni utekelezaji wa mipango hiyo. La si hivyo, ikiwa Eddy Riyami ametenda kosa basi angelishafikishwa Mahkamani ndani ya muda wa saa 24 tokea kukamatwa kama sheria inavyotaka.
Tuna kila sababu ya kuamini kwamba hatua ya kumkamata Eddy Riyami na kumuweka ndani bila ya kumfikisha Mahkamani ni utekelezaji wa mipango hiyo. La si hivyo, ikiwa Eddy Riyami ametenda kosa basi angelishafikishwa Mahkamani ndani ya muda wa saa 24 tokea kukamatwa kama sheria inavyotaka.
Chama Cha Wananchi (CUF) kinalitaka Jeshi la Polisi kuacha kutumiwa na kutumika kisiasa kufanikisha malengo ya kisiasa ya CCM.
Tunashangazwa kwamba siku zote wanaoitwa kuhojiwa, kukamatwa na kuwekwa ndani ni wanasiasa wa vyama vya upinzani na wanaharakati wengine lakini hatujawahi kushuhudia viongozi wa CCM kuitwa kuhojiwa, kukamatwa na kuwekwa ndani.
CUF imetoa taarifa kadhaa kwa Jeshi la Polisi zinazohusu matamshi na vitendo vya viongozi wa CCM vyenye mwelekeo wa uhalifu lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Hizo ni dalili za waziwazi za Polisi kutumiwa na kukubali kutumika kisiasa.
Tunashangazwa kwamba siku zote wanaoitwa kuhojiwa, kukamatwa na kuwekwa ndani ni wanasiasa wa vyama vya upinzani na wanaharakati wengine lakini hatujawahi kushuhudia viongozi wa CCM kuitwa kuhojiwa, kukamatwa na kuwekwa ndani.
CUF imetoa taarifa kadhaa kwa Jeshi la Polisi zinazohusu matamshi na vitendo vya viongozi wa CCM vyenye mwelekeo wa uhalifu lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Hizo ni dalili za waziwazi za Polisi kutumiwa na kukubali kutumika kisiasa.
Tunalitaka Jeshi la Polisi iwapo kweli lina kesi dhidi ya Eddy Riyami basi limfikishe Mahkamani haraka ili hatua za kisheria zifuate mkondo wake.
Na iwapo hawana kesi, basi wamwachie huru mara moja. Umefika wakati wa Jeshi la Polisi kufanya kazi zake kitaalamu kama sheria na kanuni zao zinavyoagiza badala ya kuwatumikia wanasiasa wa CCM.
Na iwapo hawana kesi, basi wamwachie huru mara moja. Umefika wakati wa Jeshi la Polisi kufanya kazi zake kitaalamu kama sheria na kanuni zao zinavyoagiza badala ya kuwatumikia wanasiasa wa CCM.
HAKI SAWA KWA WOTE
HAMAD MASOUD HAMAD
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO NA UMMA – CUF
23 Februari 2016
↧
Rais Dr. Magufuli Ahakikishiwa Kuwa Hali Ya Burundi Ni Shwari.
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunziza amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hali ya Burundi ni shwari na kwamba tangu jana (Februari 22, 2016) nchi hiyo imepokea ugeni mkubwa wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki-moon na inatarajia kupokea marais watano kutoka nchi za Umoja wa Afrika tarehe 25 Februari, 2016.
Ujumbe wa Rais Nkurunziza umewasilishwa na Mjumbe maalum ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi, Mheshimiwa Leontina Nzeyimana leo tarehe 23 Februari, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, alipokutana na Rais Magufuli na kufanya nae Mazungumzo.
Pamoja na kumpa taarifa kuwa Burundi inaendelea vizuri, Mheshimiwa Nzeyimana pia amemueleza Rais Magufuli kuwa Burundi ipo tayari kupokea nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kwa Rwanda, ikiwa ni kwa mujibu wa Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaoelekeza kuwa nchi inayofuata kutoa Katibu Mkuu baada ya Katibu Mkuu wa sasa kumaliza muda wake, ni Burundi.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kufanya Mazungumzo na Mabalozi watatu wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.
Balozi wa Uholanzi hapa nchini Mheshimiwa Jaap Frederiks, amewasilisha salamu za Mfalme wa Uholanzi Mtukufu Willem-Alexander ambaye amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa alizoonesha katika mwanzo wa utawala wake, katika kusimamia Uadilifu serikalini na katika biashara na pia kuisaidia Mahakama. Amesema Uholanzi inaamini kuwa maeneo hayo ndio yamekuwa yakileta vikwazo vya maendeleo, biashara na uwekezaji.
Balozi Jaap Frederiks amemhakikishia Rais Magufuli kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo kama ilivyofanya katika miaka 45 iliyopita, huku akitaja baadhi ya maeneo ya ushirikiano kuwa ni Kilimo na Nishati.
Balozi wa India hapa nchini Mheshimiwa Sandeep Arya, amewasilisha salamu za Waziri Mkuu wa India Mheshimiwa Narendra Modi, ambaye pamoja na kuitaja Tanzania kuwa lango muhimu katika mpango wake wa ushirikiano na Afrika, amemhakikishia kuwa India itaendeleza uhusiano wake na Tanzania hususani katika biashara na uwekezaji ikiwemo kuunga mkono mpango wa ujenzi wa viwanda Tanzania.
Nae Balozi wa Zambia hapa nchini Mheshimiwa Judith Kangoma Kapijimpanga ameelezea matumaini makubwa ya kuendelezwa kwa ushirikiano na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Zambia na amemuomba Rais Magufuli aimarishe maeneo kadhaa ya kiushirikiano yakiwemo Reli ya TAZARA, Bomba la Mafuta la TAZAMA na taratibu za usafirishaji wa Mizigo katika bandari ya Dar es salaam na Mpaka wa Tanzania na Zambia.
Kwa upande wake Rais Magufuli amewahakikishia mabalozi hawa kuwa serikali yake ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi mahusiano kati ya Tanzania na nchi hizo na kwamba atafurahi kuona mahusiano na ushirikiano huo unaleta manufaa kwa wananchi.
Baadhi ya maeneo ambayo amezialika nchi hizo kuongeza ushirikiano na Tanzania ni katika ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge" kuwekeza katika viwanda vya kusindika mazao na kuzalisha bidhaa mbalimbali, Elimu na Afya.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya Mazungumzo na Jaji Mkuu wa Mahakama hapa nchini, Mheshimiwa Mohamed Chande Othman, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Imetolewa;
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
23 Februari, 2016
↧
Jengo la posta Dodoma lateketea kwa moto
JENGO Posta lililopo katika eneo la sabasaba katika Manispaa ya Dodoma jana limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa
Akizungumzia kutekeleza kwa jengo hilo Meneja wa Posta Mkoa wa Dodoma, Magreth Mlyomi alisema mpaka sasa kuna hasara kubwa kutokana na kutekeleza jengo hilo sambamba na vifaa vyote vya ofisi.
Mlyomi alisema licha ya kuwa hakuna mfanyakazi hata mmoja aliyepoteza maisha katika jengo hilo lakini mpaka sasa kuna vitendea kazi vingi vya ofisi pamoja na mizigo ya wateja imeteketea.
“Kuna mizigo mingi pamoja na vifaa vya kazi vyote vimeteketezwa na moto na kwa taarifa nilizopata kulikuwa na mizigo ya watu, inaonesha kuwa chanzo cha moto ni umeme,” alieleza Meneja huyo.
Akizungumzia kuhusu masuala ya miundombinu ya maeneo husika alisema ni mibovu na kutokana na changamoto hiyo suala hilo lipo katika mamlaka husika ya manispaa.
Kwa upande wake katibu wa wafanyabiashara katika soko la Sabasaba katika Manispaa ya Dodoma, Gergod Lugusi alisema jana saa nne asubuhi kulitokea moto mkali ambao uliunguza jengo hilo.
Alisema chanzo cha moto huo inasemakana kuwa ni tatizo la umeme na uongozi ulilazimika kutoa taarifa katika kikosi cha zima moto na bila kuchelewa walifika kwa wakati.
Hata hivyo alisema licha ya kufika kwa wakati katika tukio bado kikosi hicho kilikutana na kikwazo kwa kutokana na miundombinu kuwa mibovu na migumu kupitika.
↧
More Pages to Explore .....