Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli Atembelea Shule ya Msingi Mbuyuni na Kuwaaga Rasmi Walimu Wenzie na Wanafunzi Aliokuwa Akiwafundisha

$
0
0
LEO Feb 17 2016, Mke wa Rais John Pombe Magufuli  Janeth Magufuli amewasili katika shule ya msingi Mbuyuni, Dar  kwa  ajili  ya  kuagana  na  walimu wenzake  pamoja  na  wanafunzi  aliokuwa  akiwafundisha

Shule  ya  Msingi Mbuyuni ni  shule ambayo Mama Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza na baadaye mwaka 1995 kurudi tena kufundisha hapohapo  kwa miaka 17 hadi mumewe Rais Magufuli  alipochaguliwa  kuwa  Rais  wa  Tanzania.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi ya saa toka kwa mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza risala toka kwa mwanafunzi wa shule ya Msingi ya Mbuyuni Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi toka kwa Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni katika Shule ya msingi ya Mbuyuni Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza maelezo ya utangulizi ya mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo

Majipu Yaendelea Kutumbuliwa....Wakurugenzi Wanne wa Halmashauri Mkoani Kagera,Mtwara,Geita na Tunduma Wasimamishwa Kazi

$
0
0

WAZIRI nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne  kwa  tuhuma  za  kuwahonga wakaguzi wa fedha  kutoka katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa  Hesabu za  serikali (CAG) ili wapewe hati  safi huku Halmashauri hizi zikiwa na ufisadi .

Wakurugenzi  waliosimamishwa  kazi  ni   Elizabeth Chitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera, Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara  na  Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita.
 
Pia,Waziri Simbachawene   amemsimamisha kazi  mkurugenzi Halmashauri ya  Tunduma Mkoani  Mbeya Bi Halima Ajali  ili kupisha uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kuwatumia watoto wake katika shuguli za halmashauri na kuwalipa posho na kusababisha upotevu wa mapato.
 
Aidha, Waziri Simbachawane pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa ofisi ya mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini,CAG  waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe  hati safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na ubadilifu wa fedha za Umma.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Jijini Dar es Salaam,Waziri Simbachawene amesema Wakurugenzi hao wamegundulika  baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na wizara yake
 
Akibainisha makosa ya kila mkurugenzi,Waziri Simbachawene amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi, Bi Chitundu  alimwagiza  mweka hazina wake Majaliwa Bikwato atoe rushwa ya Milioni tatu kwa maafisa wa  ofisi ya CAG kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo  huku akijua ni kosa kisheria. Watumishi wa  wa ofisi ya CAG  waliopokea pesa hizo ni Stevin Buawa,John Elias pamoja na Kilembi Mkole
 
Katika Halmashauri ya Nanyumbu, Simbachawene amesema  kuwa  tarehe 26 Juni 2015, mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel Mugesa walimkabidhi fedha Milioni 3 na laki tano  afisa wa ofisi ya  CAG  kwa lengo la kutoa hati safi
 
Waziri Simbachawene amesema mwezi Novemba mwaka jana , Mkurugenzi wa Halmashauri  ya  Mbogwe mkoani Geita Abdalla Mfaume na mweka hazina wake waliwapatia milioni 16  maafisa wakaguzi wa ofisi ya CAG  ili wafiche ufisadi walioubaini
 
Amesema katika Halmashauri hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa ikiwemo malipo ya mishahara hewa pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadhi 

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Februari 18

Kasi Ya Rais Magufuli Yawagonganisha Waziri Wa Afya na Mkuu wa Wilaya Temeke

$
0
0

Siku mbili baada ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema Wilaya ya Temeke inaongoza mkoani Dar es Salaam kwa kuwa na wagonjwa sita wa kipindupindu, Mkuu wa wilaya hiyo (DC), Sophia Mjema amesema hadi jana hakukuwa na mgonjwa hata mmoja.

Baada ya DC huyo kukanusha, jana wizara hiyo ilitoa taarifa ikisisitiza kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na ugonjwa huo.

Kipindupindu ni moja ya vigezo vinne vilivyowekwa na Rais John Magufuli kupima utendaji kazi wa wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kabla ya kufanya uteuzi mpya.

Jumatatu iliyopita akiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Waziri Ummy alitoa takwimu za ugonjwa huo na kuitaja Temeke kuwa kinara lakini juzi, Mjema alisema kulikuwa na wagonjwa ambao hawakuwa wamethibitika kama wanaugua kipindupindu.

Jana, Ofisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, Joyce Msumba alisema juzi kulikuwa na mgonjwa mmoja wa kipindupindu lakini aliruhusiwa baada ya kupona.

“Kwa hiyo leo (jana) Manispaa ya Temeke haina hata mgonjwa mmoja na kambi ni nyeupe haina mtu,” alisema.

Alisema manispaa hiyo inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kanuni za afya ili kujikinga na ugonjwa huo baada ya kufanikiwa kuutokomeza.

“Hatutapumzika tutaendelea kuwakumbusha wananchi kutunza mazingira yao kuwa safi kwa sababu kipindupindu ni hatari,” alisema.

Wakati ofisa hiyo akisema hayo, Waziri Ummy alitoa taarifa akisema Mkoa wa Dar es Salaam kwa siku 10 zilizopita kuanzia Februari 7 hadi 16 kulikuwa na wagonjwa 16; Temeke 12 na Ilala wanne.

Alisema wizara yake ndiyo yenye dhamana ya kusimamia huduma za afya kwa jamii, hivyo wagonjwa hao walikidhi vigezo vya ainisho sanifu na kupata matibabu katika kambi ya kipindupindu kwa wagonjwa wa Temeke na Hospitali ya Amana kwa wagonjwa wa Ilala hivyo kulazimu kutolewa taarifa kwa mujibu wa mwongozo.

Barack Obama Asema Donald Trump Hawezi Kuwa Rais wa Marekani

$
0
0

Rais wa Marekani Barack Obama amesema anaamini mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump hatakuwa rais wa Marekani.

Rais Obama ameyasema hayo wakati wa mkutano mkuu wa kiuchumi wa nchi za kusini mashariki mwa Asia unaofanyika katika jimbo la California.

''Ninaendelea kuamini kwamba Bw Trump hatakuwa rais. Na sababu ni kwamba nina imani sana na Wamarekani,” amesema Bw Obama.

Kiongozi huyo amebainisha kuwa Wamarekani hawatampigia kura Bwn Trump kwa kuwa wanajua kazi ya urais ni kazi kubwa si kazi ya kuongea na kuonekana kwenye vyombo vya habari tuu.

Kwa upande wake Bwn Trump amemjibu Rais Obana na kusema kuwa hakuna mtu aliyeharibu nchi kama kipindi chake.

Mwanasiasa huyo anamchukia sana Obama na miaka ya nyuma alizoea kumtaka atoe stakabadhi za kuthibitisha kwamba alizaliwa Marekani.
 
Chanzo BBC

Afukuzwa CCM Kwa Kumfanyia Kampeni Edward Lowassa

$
0
0

Halmashauri ya CCM Mkoa wa Geita imemvua ujumbe wa Mkutano Mkuu, Peter Mwininga baada ya kudaiwa kukiuka maadili ya Umoja wa Vijana (UVCCM).

Licha ya kukiuka maadili ya umoja huo, Mwininga anadaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita kwa kuwatukana viongozi wa ngazi za juu kwa njia ya mtandao.

Akizungumza baada ya kikao hicho juzi, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoani hapa, Said Kalidushi alisema baada ya wajumbe wa halmashauri kuu kupokea malalamiko na mapendekezo kutoka UVCCM, waliamua kumvua nafasi ya ujumbe huo kutokana na kupungukiwa na sifa.

Kalidushi alisema wakati wa kampeni Mwininga alikihujumu chama chao na kumfanyia kampeni mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, huku akijua wazi kuwa ni kosa.

Katibu wa UVCCM mkoani hapa, Mashaka Mshola alisema kitendo cha Mwininga kuvuliwa nafasi aliyokuwa nayo kinatokana na usaliti na huo ni mwanzo wa chama hicho kuwafukuza wasaliti.

Mvutano Wa Sheria Watawala Kesi Ya Kamanda Kova na Nzowa......Makamanda Hawa Wanagombea Nyumba Ya Serikali Aliyouziwa Kova

$
0
0

Mahakama ya rufani jana imeanza kusikiliza kesi ya viongozi wawili waandamizi wa polisi, Kamishna mstaafu, Suleiman Kova na Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Godfrey Nzowa wanaogombea nyumba ya Serikali.

Katika rufani hiyo, Nzowa anapinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, kumpa haki ya kumiliki nyumba ya Serikali, Kova ambaye ni mlalamikiwa wa kwanza katika kesi hiyo. Mlalamikiwa wa pili ni Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA).

Nzowa anapinga nyumba ambayo anaishi hadi sasa, iliyokuwa na namba 203 na baadaye kubadilisha kuwa namba 140 kuuziwa Kova kwa kuwa wakati tangazo la kuuzwa nyumba za Serikali linatolewa yeye ndiye alikuwa akiishi katika nyumba hiyo.

Hata hivyo, TBA ilimuuzia Kova ambaye alikuwa amehamishiwa mkoani Kigoma.

Tangazo la kuuzwa nyumba hiyo, lilitolewa Mei Mosi, 2002, wakati Nzowa akiwa katika nyumba hiyo baada ya kuhamia Arusha Januari 8, 2002.

Nzowa ambaye ni Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za kulevya nchini na Kova ambaye amestaafu karibuni akiwa Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, waliwasili mahakamani jana saa tatu asubuhi.

Wa kwanza kufika alikuwa Kova akiwa anasindikizwa na watu kadhaa na baadaye Nzowa alifika akiwa ameongozana na familia yake.

Wakiwa mahakamani kila mmoja alikaa eneo lake, akifuatilia mabishano ya kisheria ya mawakili na baada ya shauri hilo kuahirishwa saa 6.25 mchana walitoka nje ya chumba cha Mahakama, kila mmoja akishauriana na wakili wake.

Pingamizi la rufani 
Kabla ya kuanza kusikilizwa rufani hiyo jana mbele ya majaji Mbarouk Salum, Benard Luanda na Mussa Kipenga, mawakili wa wajibu rufani katika kesi hiyo, wanaowatetea Kova na TBA, waliwasilisha pingamizi la kusikilizwa rufani hiyo kwa maelezo kuwa liliwasilishwa nje ya muda na lina upungufu wa kisheria.

Mawakili Dilip Kesaria na Pascal Qamala wanaomtetea Kamishna Kova na mawakili wa Serikali, Harun Matagane na Sylvester Mwakitalu wanaowakilisha TBA walieleza kuwa ni muhimu Mahakama ikaheshimu taratibu zake na kuhakikisha nyaraka zinazowasilishwa mbele yake zipo sahihi.

Wakili Kesaria alisema notisi ya kukata rufani ilitolewa Oktoba 3, 2013, lakini rufani iliwasilishwa rasmi mahakamani Januari 2, 2015 nje ya muda wa kisheria.

Mawakili hao wa walalamikiwa walieleza mkanganyiko wa nyaraka zilizowasilishwa mahakamani na waliiomba mahakama kuitupa rufani hiyo kwa kuwa ina upungufu ya kisheria.

Hata hivyo, mawakili Mpaya Kamara na Neema Mtayangulwa walipinga hoja hiyo wakisema hakuna dosari za kisheria katika uwasilishaji wa rufani hiyo.

Kamara alisema rufani na notisi vimefikishwa mahakamani ndani ya muda na ndiyo sababu Msajili wa Mahakama alivipokea.

Alisema kama kulikuwa na upungufu katika nyaraka, wanaopaswa kulaumiwa siyo wao, bali maofisa wa Mahakama waliopokea nyaraka za rufani na akatoa vielelezo vya kesi kadhaa ambazo ziliendelea mahakamani licha ya kuwapo dosari ndogo.

Kamala aliwaomba majaji kutupa hoja za wajibu rufani na kama ikifikia uamuzi wa kulipa gharama za pingamizi hilo, basi wajibu maombi wa pili ambao ni TBA ndiyo wanaopaswa kufanya hivyo.

Baada ya pande zote kuwasilisha hoja hizo, Jaji Mbarouk aliahirisha shauri hilo hadi hapo watakapomaliza kuzipitia.

TTCL Yakanusha Mfumo wake wa Mawasiliano Kuingiliwa.

$
0
0

KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa mfumo wa mawasiliano wa kampuni hiyo umeingiliwa na wadukuzi. 

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Nicodemus Thomas Mushi alisema taarifa zinazotolewa si za kweli hivyo kuwataka wateja wao wazipuuze.

 “Tunapenda kuwathibithia Wateja wetu wote wa ndani na nje ya nchi, wadau wetu na Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizi si sahihi, na kwamba mifumo yetu ya Mawasiliano ya TTCL ipo salama, huduma zetu zote zipo thabiti na mpaka sasa tunapotoa taarifa hii, hakuna uhalifu wowote uliofanyika kwa sisi wenyewe kama Kampuni wala kwa mteja wetu yeyote,” alisema Thomas Mushi na kuongeza;

 "Aidha, tunapenda kuwathibitishia kuwa, taarifa za Wateja wetu wote ikiwemo Serikali , Idara, Wakala na Taasisi za Umma, Taasisi za fedha, Mashirika, Makampuni na Watu binafsi zipo salama kabisa. Ukweli huu unathibitishwa na Wateja wao pia kwani hadi sasa, hakuna hata mmoja aliyeleta taarifa za kukosa huduma ama kupata athari zozote kutokana na tetesi hizo."

 Hata hivyo, alisema pamoja na taarifa hizo, Wataalamu wa kampuni hiyo wanaendelea kuwa macho kwa muda wote, ili kuhakikisha kuwa, wanafanyia kazi kila taarifa ama tishio la kiusalama linaloweza kujitokeza katika mfumo wao.

 “TTCL inaendelea kuwaomba Umma na Wateja wetu wote kuendelea na majukumu yao kama kawaida bila wasiwasi wowote. TCCL inawaleta Karibu.” Alisema Thomas Mushi. 

Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Usalama Mifumo ya Mawasiliano ya TTCL, Lina Rujweka alisema kitengo chao baada ya tetesi hizo kimefanya uchunguzi wa kina na hakuna ashirio lolote la mifumo yao kuingiliwa (kudukuliwa) kama ilivyoelezwa.

 Alisema kitengo hicho kina wataalam ambao muda wote wapo kazini kufuatilia ufanisi wa mfumo wa mawasiliano wa kampuni yao hivyo kuwaondoa hofu wateja wao.

 “... Baada ya taarifa hizo Kitengo cha Usalama wa Mifumo ya Mawasiliano ya Kampuni ya TTCL kiliingia kazini ili kubaini ukweli wa taarifa hizo na kufanya majaribio ya kitaalamu ili kuthibitisha usalama wa mifumo yetu. Baada ya utafiti wa kina na majaribio ya kitaalamu, tunapenda kuwathibithia Wateja wetu wote wa ndani na nje ya nchi, wadau wetu na Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizi si sahihi...” alisema.

Breaking News: Matokeo Ya Mtihani Kidato Cha Nne -2015 Yametoka....Yatazame Hapa

Uchaguzi Mkuu Uganda: Mitandao Ya Kijamii Imefungwa Na Miamala Ya Simu Imezuiliwa

$
0
0

Waganda leo wanapiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge, unaofanyika huku kukiwa na malalamiko ya masanduku ya kupigia kura kufikakwa  kuchelewa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura na kufungwa kwa mitandao ya kijamii.

Leo asubuhi asubuhi misururu mirefu ya watu ilionekana katika vituo vya kupigia kura mjini Kampala ambapo zoezi la kupiga kura lilianza kwa kuchelewa kwa zaidi ya saa moja na nusu kufuatia maafisa wa uchaguzi kuendelea na matayarisho ya vifaa vya kupigia kura.

Zoezi hilo la upigaji kura linatazamiwa kukamilika saa kumi jioni saa .Bado hapajakuwa na taarifa zozote iwapo zoezi hilo litarefushwa kufuatia baadhi ya vituo kuanza shughuli hiyo kwa kuchelewa.

Mawasiliano ya yamitandao ya jamii yafungwa
Huku hayo yakiarifiwa mdhibiti wa mawasiliano wa serikali ametangaza kufungwa kwa mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter na kufunga mifumo ya kutuma pesa kupitia njia ya simu. 

Kwa majibu wa mkuu wa kamisheni ya mawasiliano nchini Uganda Godfrey Mutabaazi aliyezungumza na kituo cha radio cha CBS, hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama.

Msemaji wa wizara ya nje ya Marekani Mark Toner amesema Washington ina wasiwasi kuwa vikwazo hivyo vya mawasiliano huenda vikasababisha mivutano zaidi katika nchi ambayo tayari inakumbwa na joto kali la uchaguzi.

Kwa upande mwingine wanaharakati wa haki za binaadamu wameelezea wasiwasi wao pia juu ya madai ya kuundwa kwa makundi ya vijana wenye silaha wanaohusishwa na vyama pamoja na wanasiasa mbali mbali kwa ajili ya kulinda maslahi ya vyama vyao kwenye uchaguzi huu.

Museveni aliye na miaka 71 aliyechukua madaraka kwa mara ya kwanza nchini Uganda mwaka wa 1986 na aliyeshinda uchaguzi mara nne kuanzia mwaka wa 1996, anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea wawili kati ya wagombea saba waliopo katika kinyang'anyiro cha urais.

Kizza Besigye, aliye na miaka 59, aliyekuwa daktari wa Museveni ndiye mgombea wa kwanza anayempa tumbo joto Museveni. 

Besigye ameshashindwa mara tatu katika safari yake ya kuwania urais nchini Uganda. Mwingine anayeonekana kutoa ushindani mkali ni Waziri Mkuu wa zamani Amama Mbabazi aliye na miaka 67.

Rais Magufuli Akutana Na Baadhi Ya Makundi Yaliyoshiriki Naye Kwenye Kampeni Ya Uchaguzi Mkuu Mwaka 2015

$
0
0
Rais John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.

 Rais John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akisalimia katika mkutano wa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan  akisalimia katika mkutano wa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Msanii wa Kundi la Orijino Komedi, Lucas Mhavile, maarufu kwa jina la Joti katika mkutano kati ya Rais John Magufuli na Wasanii uliofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 18, 2016. 
PICHA NA IKULU

CUF Yatangaza Maandamano Makubwa Dar es Salaam

$
0
0

Wanawake wa chama cha wananchi CUF maarufu kama JUKECUF wametangaza kufanya maandamano ya Amani siku ya tarehe 22,mwezi huu wa pili Jijini Dar es salaam yenye adhma ya kupinga hali ya kisiasa inayoendelea visiwani Zanzibar.

Akizungumza na wanahabari mapema leo mwenyekiti wa jumuiya hiyo  Mh severena mwijage amewaambia wanahabari kuwa maandamano hayo yataanzia ofisi kuu za CUF buguruni kuelekea ofisi ya makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu

Amesema kuwa jumuiya hiyo inatambua kwamba hali ya Amani iliyopo Zanzibar ikivurugika kwa kiasi kikubwa watakaoathirika ni kina mama na watoto hivyo wameona  ni bora kufikisha kilo chao hicho kwa makamu wa Rais ambaye ni Mwanamke mwenzao awasaidie.

Maandamano hayo yatapita barabara ya uhuru,ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam,karume,kariakoo,mnazi mmoja,Central polisi,barabara ya sokoine ,Bandarini,mahakama kuu,mahakama ya ardhi,Hadi ofisi ya makamu wa Rais.

Maandamano hayo bado hayajaruhusiwa na polisi licha ya polisi kupata barua kutoka CUF.

Matokeo Kidato Cha Nne: Shule 10 Bora Kitaifa na Shule 10 za Mwisho Kitaifa Ziko Hapa......Aliyeongoza Kitaifa Ni Msichana

$
0
0
Baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2015 yanayoonesha kiwango cha ufaulu kushuka kwa asilimia 0.80.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Charles Msonde amesema kuwa jumla watahiniwa 272,947 sawa na 67.53% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne 2015 wamefaulu tofauti na mwaka 2014 ambapo ufaulu ulikuwa 68.33%.

Msonde amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 11,125 (64.84) na wavulana wakiwa 124,871 (71.09).

Amesema kwa upande wa watahiniwa wa shule, ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014.

Aidha kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, Dkt Msonde amesema watahiniwa 31,951 sawa na asilimia 64.80 wamefaulu ikilinganishwa na watahiniwa 29,162 (61.12) waliofaulu mwaka 2014.

Kwa upade wa ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, Msonde amesema waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawa na asilimia 2.77, daraja la pili ni 31,986 sawa na asilimia 9.01, daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56.

Aidha waliopata daraja la nne ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 na waliopata daraja la sifuri (waliofeli) ni 113,489 sawa na asilimia 32.09.

Watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa kati ya daraja la kwanza hadi la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73 wavulana wakiwa 56,603 sawa na 29.99 na wasichana 38,338 sawa na asilimia 19.63.

Amesema kwa upande wa ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule, ufaulu wa juu kabisa ni wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 77.63 wamefaulu huku ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 16.76 wamefaulu.

Baraza hilo limezuia matokeo ya watahiniwa 121 kutokana na sababu za kiafya na watahiniwa hao wataruhusiwa kufanya mitihani ambayo hawakuifanya katika mtihani wa kidato cha nne, mwaka 2016.

Aidha baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa 87 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani ambapo kati yao 25 ni wa kujitengemea na 52 ni watahiniwa wa shule wakati 10 ni wa mtihani wa maarifa (QT)

Amezitaja shule 10 zenye watahiniwa zaidi ya 40 zilizofanya vizuri zaidi kuwa ni Kaizerege ya mkoani Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, St. Francis Girls ya Mbeya, Canossa ya Dar es salaam, Marian Boys ya Pwani, Alliance Rock Army ya Mwanza, Feza Girls Dar es salaam, Feza Boys ya Dar es salaam na Uru Seminary ya Kilimanjaro.

Shule 10 zilizofanya vibaya zaidi kwa watainiwa zaidi ya 40 ni pamoja na Pande ya mkoani Lindi, Igawa ya Morogoro, Korona ya Arusha, Sofi ya Morogoro, Kurui ya mkoani Pwani, Patema ya Tanga, Saviak ya Dar es salaam, Gubali ya Dodoma, Kichangani ya Morogoro na Malinyi ya Morogoro.

Kwa upande wa watahiniwa, Dkt Msonde amesema kati ya watahiniwa 10 waliofanya vizuri zaidi, wanne na wasichana na sita ni wavulana.

Mwanafunzi aliyeongoza ni msichana Butogwa Charles Shija wa Canossa, akifuatiwa na msichana mwingine Congcong Wang wa Feza Girls na wa tatu ni mvulana Innocent Lawrence wa Feza Boys.

Wengine ni Dominick Marco Aidano wa Msolwa, Sang'udi E Sang'udi wa Ilboru, Asteria Herbert Chilambo waCanossa, Belinda Jackson Magere wa Canossa, Humfrey Martine Kimanya wa Msolwa, Bright B Mwang'onda wa Marian Boys na wa 10 ni Erick R Mwang'ingo wa Marian Boys.

Matokeo hayo yamepangwa katika mfumo wa madaraja (Division) badala ya ule wa wasatani wa alama (GPA) kama ambavyo iliagizwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi hivi karibuni.


Rais Magufuli Apiga Marufuku Uingizwaji wa Sukari toka Ng'ambo ili Kulinda viwanda vya Ndani na kuvutia wawekezaji

$
0
0

RAIS John Magufuli amesema amedhamiria kwa dhati kufufua viwanda vya ndani na kama mfano amepiga marufuku kwa kiongozi yeyote wa serikali, kutoa kibali cha kuagiza sukari kutoka nje ya nchi zaidi yake.

Aidha, amesisitiza kwamba ataendelea kutumbua majipu ya viongozi mafisadi na wala rushwa, kwa kuwa yeye na viongozi wenzake sio wakatili, ila ni kutokana na nchi kuoza.

Amesema yupo radhi kuchukiwa na Watanzania wachache, ambao wamekuwa wakihusika na vitendo vya ufisadi, vinavyoathiri maisha ya Watanzania wengi ili kuiwezesha nchi kusonga mbele kuelekea kwenye uchumi wa kati kwa kasi.

Rais Magufuli alisema hayo Ikulu Dar es Salaam jana, alipokutana na makundi mbalimbali ya wadau walioshiriki kwenye kampeni zake kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana na kuibuka na ushindi uliomuwezesha kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano.

Akizungumzia ufufuaji wa viwanda ikiwa ni moja ya eneo alilolitilia msisitizo mkubwa wakati wa kampeni, Rais Magufuli alisema nia yake ya kufufua viwanda ipo pale pale na kusema tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa.

Akitoa mfano, Rais alisema wakati yapo maeneo ambayo wakulima wanajishughulisha na kilimo cha miwa na zao hilo kuwa tegemeo lao katika kuinua uchumi wao, wapo wafanyabiashara wanaojali maslahi yao binafsi ambao wamekuwa wakiagiza sukari kutoka nje hatua inayosababisha kufa kwa viwanda vya sukari vya ndani.

“Mtu anaagiza sukari kutoka nje, tena wakati mwingine ni sukari ambayo muda wake wa kuisha matumizi umekaribia kumalizika. 

"Huyu mfanyabiashara anaingiza sukari hiyo na kuifungasha upya ili isijulikane kuwa inakaribia kuharibika na kuwauzia wananchi masikini.

 “Kitendo hiki kinasababisha sukari inayozalishwa na viwanda vya ndani kukosa soko, wakulima wanakosa soko la miwa yao, na serikali nayo inakosa mapato ya ushuru. 

"Kwa vile bahati nzuri Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) na Makamu wa Rais (Samia Suluhu Hassan) mpo hapa, nasema kuanzia sasa asiwepo mtu wa kutoa kibali cha mtu kuagiza sukari kutoka nje hadi ruhusa hiyo itoke kwangu,” alisema Rais Magufuli.

Alisema mkakati kama huo hautaishia kwenye sukari pekee, bali ni mkakati ambao utahusu maeneo yote ya uzalishaji ili wananchi wa kipato cha chini waneemeke na nchi yao. 

“Nimekuwa nasema nchi yetu si masikini. Hii nchi ni tajiri sana, lakini wapo watu wamekuwa wanajinufaisha wao. Wapo tayari wapokee virushwa ili waneemeke wao huku Watanzania wengi wakiumia na kuteseka. 

“Ndio maana nasisitiza kwamba nitaendelea kutumbua majipu ya viongozi mafisadi na wala rushwa.

"Tunapotumbua majipu si kwamba sisi ni wakatili hapana, ila ni kutokana na nchi yetu kuoza. Kila unapotupia jicho pameoza, hadi wakati mwingine unashindwa kuamua uanze na jipu lipi na lipi ulitumbue kesho, yapo majipu mengine hayasikii dawa. 

“Hawa watu wanaolalamika sana sasa ni wachache ambao walikuwa wananufaika na ufisadi na rushwa. Ni bora ukachukiwa na watu 1,000 ili upendwe na watu milioni 50.Kama nitaboresha maisha ya Watanzania milioni 50, hata kwa Mungu tutapokelewa,” alisema Rais Magufuli.

Alisema serikali yake itaendelea kuchukua hatua katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya neema na ya uchumi wa kati na kuwa umoja, mshikamano na uzalendo usioambatana na tofauti za kidini, ukabila na itikadi za kisiasa ni nyenzo kubwa katika kufikia mafanikio hayo.

==>Tazama  Video  hii  kumsikiliza  Rais  akitoa  amri  ya  kupiga  marufu  uagizaji  Sukari

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Februari 19


Jeshi la Polisi Latua Bandarini Kuimarisha Ulinzi.....Waziri Kitwanga Atoa Onyo Kwa Polisi Wanaowabambika Kesi Wananchi

$
0
0

Jeshi la Polisi limeweka ulinzi katika Bandari ya Dar es Salaam, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kuwa ilindwe na vyombo vya dola badala ya kampuni binafsi za ulinzi.

Akizungumza kwenye kikao cha kazi kilichowahusisha makamanda wa mikoa na vikosi vya polisi nchini, Mkuu wa jeshi hilo (IGP), Ernest Mangu, alisema tayari  wamepeleka askari bandarini ambao wanafanya kazi kwa muda wakishirikiana na walinzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Mangu alisema askari hao wanakwenda kulinda kwa muda wakitokea Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.

Alisema amewaomba TPA wajenge kituo cha polisi bandarini hapo, ili askari wawepo muda wote.

“Tumetekeleza agizo la waziri, kwa sasa bado tunamalizia logistics fulani ili tuwe pale bandarini permanently (muda wote). Tunahitaji ushirikiano wa watendaji wote ili kuimarisha ulinzi wa mali za wananchi,” alisema Mangu.

Alisema polisi wamejipanga vyema kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa kurudisha nidhamu ya utendaji, kupambana na uhalifu, dawa za kulevya, ujangili na ujambazi.

Mkuu huyo wa polisi alisisitiza kwamba, kuanzia Juni Mosi, mwaka huu wataanza utaratibu mpya wa utendaji chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) ili kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kulinda mali na maisha yao.

“Kaulimbiu yetu ni ‘badilika kifikra, acha kufanya kazi kwa mazoea’. Kaulimbiu hii ni kielelezo cha jinsi tulivyodhamiria kubadilika kiutendaji,” alisema.

Awali, akifungua kikao hicho, Waziri Kitwanga aliwapongeza makamanda hao kuandaa kikao ili kuelekezana nini cha kufanya kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na Taifa.

“Serikali haitafumbia macho askari au ofisa yeyote atakayeomba na kupokea rushwa, kuchelewesha upepelezi, kutowajali wateja, kubambikia wananchi kesi na mambo mengineyo. Tutachukua hatua bila kujali cheo chake,” alisisitiza.

Kitwanga alisema Serikali imejipanga kuboresha maisha ya askari na mazingira yao ya kazi.

Alisema Serikali imeagiza magari na kupanga kujenga nyumba 3,500 kwa ajili ya makazi ya askari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker ambayo pia imedhamini kikao hicho alipendekeza matumizi ya fedha kielektroniki kwa kuwa ndiyo njia salama ya kutumia huduma za kibenki.

Kambi ya Upinzani bungeni Yaendelea Kumgomea Spika Ndugai

$
0
0

Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu amesema kambi hiyo haitaongoza kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac) hadi ofisi ya Spika itakapobadilisha uteuzi wa wajumbe wa kamati hizo.

Kwa mujibu wa mabunge ya Jumuiya za Madola, kamati hizo huongozwa na wapinzani, lakini tangu Spika wa Bunge, Job Ndugai afanye uteuzi wa wajumbe, kambi hiyo imesusia kushiriki uchaguzi kwa kile wanachokiita “kupangiwa wajumbe”.

Jana, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema mazungumzo kati ya ofisi ya spika na kambi hiyo bado yanaendelea na kusisitiza kwamba uteuzi huo unaweza kutenguliwa au kuachwa kama ulivyo. 

Katika maelezo yake, Lissu alisema licha ya kambi hiyo kuwa katika mazungumzo na ofisi ya spika, suluhisho halijapatikana na kusisitiza kuwa msimamo wao upo palepale. 

“Hatujafika popote. Msimamo wetu uko palepale na hatutakubali kuchaguliwa viongozi wa hizo kamati na CCM, kama wanafikiria ni lazima iwe wanavyotaka sisi hatutakubali,” alisema.

Joel aliwahi kunukuliwa na na vyombo vya habari  akisema kuwa kama kambi hiyo itasusia uchaguzi, shughuli za kamati zitafanywa na makamu wenyeviti ambao wanatokea CCM.

“Ni bora tusiziongoze kabisa kamati hizi. Ukifuatilia utabaini kuwa katika PAC na Laac tuna wajumbe sita kila kamati kati ya wajumbe 23, wakati huohuo kamati ya Ukimwi tumepewa wajumbe 12 kati ya wote 23,” alisema Lissu.

Alisema wajumbe sita waliopo katika kamati ya Laac na PAC wameteuliwa na CCM na kama kamati hizo zinaongozwa na upinzani ni lazima wapinzani wajichagulie wajumbe wao, wakiwamo watakaochaguliwa kuwa wenyeviti. Alisema wabunge wana haki sawa, lakini hawana uwezo sawa.

Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alisema uamuzi wa spika kuwapangia wajumbe katika kamati hizo hauna nia nzuri na kwamba, huenda ni mkakati wa ofisi hiyo kuifanya Serikali iwe inapitisha mambo yasiyofaa bungeni.

Februari Mosi mwaka huu, Kambi ya Upinzani bungeni ilisusia uchaguzi wa viongozi wa kamati hizo kwa maelezo kuwa Spika Ndugai alifanya uteuzi ‘kiholela’ na kuahidi kutoshiriki mpaka pale watakapopewa idhini ya kupendekeza wenyeviti.

Waziri Mbarawa Awakamua MAJIPU Wakurugenzi TCRA na TEMESA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Makame Mbarawa ameagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, kusitisha mara moja mkataba wa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa mamlaka hiyo, Elizabeth Nzagi, kwa kushindwa kusimamia ufungwaji wa kifaa cha kufuatilia mapato ya simu ya ndani katika mitambo ya kuchunguza mapato katika mitandao ya simu (TTMS).

Waziri Mbarawa amesema kutokufungwa kwa kifaa hicho kumeisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 400/= hivyo ameiagiza pia bodi hiyo ya TCRA kuwasimamisha kazi mara moja, Kaimu Mkurugenzi anayesimamia mfumo wa uhakiki na usimamiaji huduma za mawasiliano, mhandisi Sunday Richard na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Modestus Ndunguru ili kupisha uchugnuzi dhidi ya uhusika wao katika kusababisha kifaa hicho kutokufungwa.

Aidha, Waziri Mbarawa ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRCA, Ally Simba kwa kutokuwa makini katika utendaji huo huku akimwagiza kuhakikisha kuwa kifaa hicho kinafungwa ndani ya siku saba. 

Profesa  Mbarawa  pia  ametengua  uteuzi  wa  Mtendaji  mkuu  wa  Wakala  wa  Umeme  na  Ufundi  Tanzania  (Temesa),Mhandisi  Marcellin Magesa  kwa  kushindwa  kusimamia  matengenezo  ya  magari  ya  serikali, mitambo  na  vivuko.

Kadhalika, ametengua  uteuzi  wa  Mkurugenzi  wa  matengenezo  ya  magari  ya  serikali,Prisca  Mukama  na  Meneja  wa  Karakana   ya   magari  ya  Serikali  John Mushina  ambao  watapangiwa  majukumu mengine.

Askari Hifadhi ya Kinapa Watuhumiwa Kuwadhalilisha Wanawake kwa Kuwapiga, Kuwabaka na Kuwakalisha Juu ya Siafu

$
0
0

Serikali mkoani Kilimanjaro imeuagiza uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa), kuwachukulia hatua askari wanaodaiwa kuwanyanyasa wanawake wanaoingia katika Misitu ya Nusu Maili kukata nyasi na kuokota kuni.

Mkuu wa mkoa huo, Amos Makala alitoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mshiri wilayani hapa.

Alisema katika ziara aliyofanya kwenye vijiji vinavyozunguka msitu huo, wanawake wamekuwa wakilalamika kufanyiwa vitendo vya ukatili, ikiwamo ubakaji nakupigwa wanapokutwa na askari hao wakikata nyasi kwa ajili kulisha ng’ombe na kuokota kuni za kupikia.

“Kinapa najua wapo baadhi ya askari wenu ambao siyo waaminifu, wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya kikatili na vya kinyama wanawake wanaoingia katika Msitu wa Nusu Maili. Kwa hiyo nawaagiza kuwachukulia hatua za kisheria mara moja,” alisema Makala Mkuu huyo wa mkoa alisema vitendo hivyo ni vya aibu na vya kusikitisha kwa taasisi kubwa ya umma.

“Mtu mzima hawezi kusimama kwenye hadhara ya watu wengi namna hii na kusema uongo katika mambo makubwa kama kubakwa na kutembezwa kwenye hifadhi siku nzima, kupigwa na kukalishwa kwenye siafu,” alisema Makalla.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Veronica Mlay alisema wamekuwa wakiingia katika hifadhi hiyo siku za Jumatano na Jumamosi ambazo wameruhusiwa kukata nyasi na kuokota kuni, lakini baadhi ya askari wa Kinapa wanapowakuta huwafanyia vitendo vya unyanyasaji.

Kaimu mhifadhi wa hifadhi hiyo, Charles Ngendo alisema vitendo hivyo viliwahi kulalamikiwa miaka ya nyuma katika ofisi yake na kuvishughulikia.

Papa Francis, Donald Trump wavutana kuhusu ukristo wa Mgombea huyo

$
0
0
Papa Francis na mgombea wa Republican mwenye matamshi tata, Donald Trump wameingia kwenye mvutano kuhusu ukristo wa mgombea huyo kufuatia matamshi yake kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa Marekani atajenga ukuta mpakani mwa Mexico na Marekani ili kuzuia wahamiaji kuingia nchini humo.

Trump alieleza hivi karibuni kuwa atachukua hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya jitihada za kulinda usalama wa Marekani ikiwa ni pamoja na kuzuia Watu wenye imani ya Kiislamu kuingia nchini humo.

Kauli hiyo ya Trump imeonekana kumkwaza Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ambaye amesema kuwa mtu anayepanga kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico badala ya kujenga daraja ‘sio Mkristo’.

“Mtu anayefikiria kujenga ukuta, kokote walipo, na sio kujenga madaraja, sio mkristo. Hii sio injili,” Papa Francis aliwaambia waandishi wa habari.

Papa Francis alitoa kauli hiyo katika siku yake ya mwisho ya ziara ya Mexico. Alisema kuwa hawalazimishi wakristo kumchagua au kutomchagua mtu fulani, lakini wampime kauli zake kabla ya kufanya maamuzi katika sanduku la kura.

Trump amejibu kauli hiyo ya Papa akieleza kuwa Kiongozi huyo hana haki ya kumhukumu mtu yeyote kuwa ni Mkristo au sio Mkristo.

“Hakuna kiongozi, hususan kiongozi wa dini, mwenye haki ya ya kuhoji  imani ya kidini ya mtu mwingine,” Trump alisema.

“Kama Vatican itashambuliwa na ISIS, ambapo kila mmoja anajua kuwa ni tuzo muhimu ya ISIS, ninawaahidi kuwa Papa atatamani na kuomba kuwa Donald Trump angekuwa Rais,” aliongeza Trump.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images