Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais John Pombe Joseph Magufuli Alaani Mauaji Ya Rubani Wa Helikopta Iliyotunguliwa Na Majangili Wa Tembo Mkoani Simiyu

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelaani kitendo cha watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili kumuua kwa kumpiga risasi Rubani wa helkopta Kepteni Roger Gower, raia wa Uingereza na kisha kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wakati alipoungana na Askari wa wanyamapori waliokuwa wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.

Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa sana na tukio hilo na ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha waliomuua Kepteni Gower na kuidondosha helkopta aliyokuwa akiiendesha wanakamatwa na wanafikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria.

Amemtumia salamu za pole, Balozi wa Uingereza hapa nchini kwa kumpoteza raia wake ambaye alikuwa akitoa mchango mkubwa katika kuhifadhi wanyamapori wa hapa nchini Tanzania.

Aidha, Rais Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zake zote na kuwataka wananchi na wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori, kutokatishwa tamaa na tukio hili na watoe ushirikiano wa kutosha kuwafichua watu wote wanaojihusisha na ujangili ama biashara ya bidhaa zitokanazo na ujangili.

Katika tukio hilo, pamoja na kumuua Kepteni Roger Gower watu hao wanaosadikiwa kuwa majangili wamemjeruhi Askari wanyama pori mmoja na wamewaua tembo watatu.

Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
31 Januari, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Februari 1

Dr. Shein Azindua Miaka 39 ya Kuzaliwa CCM.....Asisitiza Chama Chake Kiko Tayari Kwa Uhaguzi wa Marudio Zanzibar

$
0
0

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema chama hicho kipo tayari kwa uchaguzi wa marudio Machi 20 kwa lengo la kuhakikisha kinashika dola na waliochukua uamuzi wa kususa ni maamuzi yao binafsi.

Aidha, amesema Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad ndiye aliyekiuka makubaliano ya mazungumzo ya mwafaka na kukimbilia katika vyombo vya habari.

Akihutubia mamia ya wanachama wa CCM katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa kuzindua maadhimisho ya miaka 39 ya CCM, Dk Shein alisema maamuzi ya kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu yamefanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ambayo ndiyo chombo halali kwa mujibu wa Katiba cha kushughulikia masuala yote ya uchaguzi nchini.

Aliwataka wanachama na wafuasi wao kujipanga vizuri na kushiriki uchaguzi huo kikamilifu kwani kwa mujibu wa Katiba ya CCM ni kushinda uchaguzi zote zinazofanyika nchini ili kushika dola na kuwatumikia wananchi.

“Hayo ndiyo maamuzi ya chama chetu tuliyokubaliana kushiriki Uchaguzi Mkuu wa marudio baada ya kufutwa kwa ule wa Oktoba 25 mwaka jana kwa hivyo wanachama na wafuasi jitayarisheni kushiriki kikamilifu kwa ajili ya kushika dola,” alisema Dk Shein.

Dk Shein ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, alisema amesikitishwa na uamuzi pamoja na kauli za Katibu Mkuu wa CUF ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif za kujitoa katika mazungumzo yaliyokuwa yakifanyika, ambayo wote kwa jumla walikubaliana kwamba yawe siri kwa muda wote.

Huku akishangiliwa na wafuasi na wanachama wa CCM, Dk Shein alisema ni Maalim Seif ndiye aliyemuandikia barua kukutana na kufanya mazungumzo kwa ajili ya mustakabali wa wananchi wa Zanzibar, ombi ambalo yeye alikubaliana nalo na kuliwasilisha kwa wenzake na hapo mazungumzo yalianza.

Alifahamisha kwamba moja ya masharti ya mazungumzo yao ni kuheshimu na kutunza siri hadi muafaka utakapopatikana kwa kutoa taarifa ya pamoja kwa wananchi, lakini Dk Shein alisema kwa masikitiko makubwa Maalim alishindwa masharti hayo na kujitoa katika mazungumzo.

“Nasikitika sana aliyejitoa katika mazungumzo ni mwenzangu Maalim Seif ambaye alikiuka makubaliano yetu na kuamua kwenda mbele ya vyombo vya habari kuzungumza....... mimi ni muungwana bwana naheshimu makubaliano na ndiyo maana nimekaa kimya,”
alisema.

Aliwataka wananchi na wafuasi wa CCM kujiandaa na uchaguzi wa Machi 20, akitamba kuwa wembe ni ule ule wa kuhakikisha wanashinda uchaguzi huo na kurudisha na kujenga imani ya wananchi walio wengi ambao anaamini kwamba CCM ndiyo chama kitakacholinda amani na utulivu.

Aidha, alisema SMZ haipo tayari kuona kwamba watu wachache wanavuruga amani ya nchi kwa maslahi yao binafsi na uroho wa madaraka na kuwataka wananchi kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa marudio Machi 20.

“Nasisitiza tena Zanzibar itabakia kuwa na amani katika kipindi cha uchaguzi wa marudio na atakayejaribu kuleta fujo, vyombo vya sheria vitachukua mkondo wake na hakuna sababu ya wananchi kuogopa kwenda kupiga kura kwani suala la uchaguzi wa marudio ni la kawaida ambalo linatokana na matakwa ya kisheria,” alisema.

Mapema, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliwataka wanachama na viongozi kwa ujumla kujipanga kuhakikisha kwamba CCM inashinda, akisema uchaguzi ni kujipanga na kuweka mikakati pamoja na mahesabu.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatimiza miaka 39 tangu kilipozaliwa Februari 5, 1977 baada ya kuvunjwa kwa vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa kwa chama hicho kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano na mapenzi ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kilele cha sherehe kitakuwa mjini Singida Jumamosi wiki hii.

Jinsi Rubani Rodgers Gower Alivyouawa Na Majangili

$
0
0

Siku moja baada ya kifo cha rubani Rodgers Gower (37) aliyekuwa anaendesha helikopta inayomilikiwa na Mwiba Holdings, baadhi vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti kuwa huenda bunduki iliyomuua ni ile iliyokuwa inatumika kuulia tembo.

Miongoni mwa vyombo hivyo ni magazeti ya Uingereza ya Daily Mail, The Guardian, The Sun, The Telegram, The Independent, Shirika la Habari la Ufaransa AFP na Shirika la Utangazaji la Marekani CNN.

Mbali na vyombo hivyo, jana asubuhi mwili huo ulifanyiwa uchunguzi ambao ulionyesha matundu manne ya risasi, moja kwenye mguu, mawili begani na jingine kwenye paji la uso ambako risasi iliingilia kichwani na haikuwa imetoka. 

Chanzo cha habari katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, ulikopelekwa mwili huo kilisema walipewa maagizo kuhakikisha hauondolewi hadi risasi iliyopo kichwani imeondolewa.

“Unajua huyu aliyefariki ni Mzungu, hata kama amefanyiwa postmoterm hapa anaweza kufanyiwa nyingine Aga Khan, Dar es Salaam na akifikishwa kwao Uingereza anafanyiwa tena, ndivyo walivyo wenzetu,” alisema.

Ijumaa iliyopita, Gower aliuawa kwa risasi wakati akiendesha helikopta hiyo kwenye doria dhidi ya majangili katika Pori la Akiba la Maswa, mkoani Simiyu akiwa pamoja na raia wa Afrika Kusini, Nicky Bester ambaye alinusurika kifo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema Serikali inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini majangili waliohusika. 

Alivyouawa 
Daily Mail lilisema jana kuwa inawezekana hata bunduki iliyomuua Gower ni ile waliyokuwa wanatumia majangili hao kuua tembo. Lilieleza kuwa wakati Gower akiwa katika doria, aliona mabaki ya tembo wawili chini.

Gazeti hilo lilimnukuu Pra tik Patel, mmoja wa marafiki wa karibu marehemu, akisema wakati anaendelea na doria aliona tembo mwingine ambaye hakuwa ameuawa muda mrefu.

“Baada ya kuona hivyo, akataka ageuze ili wakamwangalie yule tembo, huku akijaribu kuona kama kuna majangili, ndipo mwanamume mmoja alitokea akiwa na bunduki na kupiga kwenye uvungu wa helikopta,” alisema Patel ambaye pia ni mfanyakazi mwenzake.

“Ile risasi ilitoboa uvungu wa helikopta na kupenya ndani, ikampiga rubani kwenye mguu na sehemu ya bega na uso kisha kutoboa paa la helikopta na kutoka nje … kutokana na uzito wa silaha iliyotumika kumuua, pengine ndiyo ileile ambayo majangili walitumia kuua tembo.”

Hata hivyo, gazeti la The Telegram, lilieleza kuwa bunduki iliyotumika kumuua Gower ni AK47.

“Alipokuwa anamkaribia tembo mmoja aliyeuawa, ndipo akapigwa risasi na kufariki kabla ya timu ya waokoaji kufika katika eneo hilo,” ilisema sehemu ya habari hiyo.

Mwanzilishi wa Mfuko wa Hifadhi wa Friedkin (FCF) aliyetoa taarifa kwa vyombo vya habari, Dan Friedkin ambaye aliwahi kufanya kazi na Gower alisema ni jambo la kusikitisha kuona rubani huyo, aliyekuwa katika operesheni ya kusaidia Tanzania kupambana na majangili ameuawa na haohao majangili.

The Guardian liliripoti kuwa jukumu kubwa la marehemu ambaye pia alikuwa mhasibu kitaaluma, lilikuwa kusafirisha watalii kwenye kambi mbalimbali za hifadhi.

Gower ambaye pia alihitimu masomo ya urubani wa helikopta mwaka 2004 London, Uingereza amekuwa akifanya doria kwa kushirikiana na wahifadhi kwa ajili ya kupambana na majangili kwenye hifadhi.

Akizungumzia mipango ya mazishi, Patel alisema jana kuwa suala hilo bado linajadiliwa na familia ya marehemu.

Hata hivyo, taarifa nyingine zilieleza kuwa mwili huo unatarajiwa kusafirishwa kwenda Uingereza kwa mazishi.

Chanzo cha kuaminika katika Mount Meru kilisema muda mfupi baada ya mwili huo kufikishwa, wakala wa kusafirisha miili ya raia wa kigeni alifika na kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Mwiba Holdings, iliyokuwa inamiliki helikopta hiyo.

Serikali Yakataa Maombi Yote Ya Shule Binafsi Kupandisha Ada Mwaka Huu

$
0
0
Kamishna wa Elimu nchini amekataa maombi yote ya shule za msingi na sekondari zisizo za Serikali kupandisha ada katika mwaka huu wa masomo na ameagiza shule zilizopandisha ada kinyume cha tamko la Serikali kusitisha ada hizo mpya.

Kutokana na uamuzi huo, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imeziagiza shule zote za binafsi ambazo zimepandishia ada kiholela bila kupata kibali cha wizara hiyo, kurejesha ada waliyokuwa wanatoza mwaka jana, la sivyo hatua kali zitachukuliwa kwa shule itakayokaidi.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ithibati ya Shule, Hadija Mcheka amesema baada ya tangazo la wizara hiyo kuzitaka shule binafsi zinazotaka kupandisha ada kuwasilisha maombi kwa Kamishna wa Elimu na kutoa sababu za kupandisha ada, ni shule 45 tu zilipeleka maombi ya kupandisha ada wakati shule zingine 900 ziliomba ziendelee kutoza ada ya mwaka jana.

“Hizi shule 45 hazikupata kibali cha kupandisha ada maana sababu walizozitoa hazikumridhisha Kamishna wa Elimu hivyo akaamuru zibakie na ada ya mwaka jana,” alisema Mcheka. 

Tanzania ina jumla ya shule za msingi 14,000 na kati ya hizo shule binafsi ni 1,000.

Kwa upande wa sekondari, shule binafsi ziko zaidi ya 1,400 kati ya sekondari 4,000. Mcheka alifafanua kuwa baadhi ya shule zilitoa sababu kuwa wanapandisha ada kwa sababu wana ujenzi, jambo ambalo kamishna aliona halimhusu mzazi.

“Mwingine anasema anataka kupandisha ada kwa vile anataka kuajiri walimu kutoka nje ya nchi, hili nalo halimhusu mzazi ndio maana tumewanyima kibali cha kupandisha ada,” alieleza.

Pia alisema shule zingine zilinyimwa ruhusa ya kupandisha ada kwa sababu hazikutoa sababu yoyote zaidi ya kueleza kuwa wanataka kupandisha ada kutokana na gharama za uendeshaji.

“Sababu zote hizi hazikumridhisha kamishna ndio maana tumewataka watii agizo la Serikali hadi hapo baadaye.” Alifafanua. 

Mcheka alisema hatua ya kuzitaka shule zote zibaki na ada ya mwaka jana ni kutokana na wizara hiyo kumwajiri mtaalamu mwelekezi anayefanya kazi ya kujua gharama za kumsomesha kila mwanafunzi ili kuisaidia Serikali kuweka ada elekezi.

Alisema ada elekezi hiyo ndio itakayoisaidia wizara kupanga ada elekezi kwa shule binafsi. 

Aliwaonya wamiliki wa shule binafsi ambao wamepuuza agizo hilo kwa kisingizio kuwa hawajapelekewa barua na wizara husika kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria zilizoainishwa wakati shule inaposajiliwa.

Alisema Serikali inafanya kazi kupitia waraka, matamko na maagizo ambayo lazima wahusika wanaohusika kuyatiii na sio kusubiri kuandikiwa barua. 

“Katika hili hatutanii kama zipo shule ambazo hazikutii tamko lile la Serikali na wakapandisha ada naomba wasitishe ada hizo mpya,” alionya.

Mcheka aliwataka wazazi na walezi walioanza kulipa ada hiyo mpya kusitisha malipo hayo mara moja na kwamba wahakikishe kuwa ada yote watakayolipa kwa mwaka huu ifanane na ile iliyolipwa mwaka jana na sio vinginevyo.

“Kama mwaka jana alilipa Sh milioni 1.5 na mwaka huu amepandishiwa hadi Sh milioni 1.8, na kwa kuwa mzazi analipa kwa term (muhula)na tayari ameshalipa term ya kwanza, naomba atakapolipa muhula wa pili alipe pesa pungufu ya kile alicholipa term (muhula) ya kwanza ili zitimie Sh milioni 1.5 na sio Sh milioni 1.8,” alisema Mcheka.

Aliwataka wazazi na walezi kutoa taarifa wizarani na ofisi za elimu za wilaya kwa shule ambazo zitakaidi agizo hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa. 

Mkoa wa Dar es Salaam Kuwa na Wilaya 5

$
0
0

Rais Dk. John Magufuli ameidhinisha kuwepo kwa wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam, badala ya tatu zilizokuwepo awali, ili kuleta maendeleo ya haraka hususan katika elimu.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, alisema juzi kuwa, waliwasilisha ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke kwa rais, ambapo ameshaliidhinisha.

“Hatua hii ya kuwepo kwa wilaya tano italiwezesha jiji la Dar es Salaam, kupata maendeleo ya haraka kwa kugawanywa kwa wilaya hizo, ambapo kutakuwa na usimamizi thabiti na hakutakuwa na kisingizio cha kuelemewa kwa majukumu kwa watendaji,”alisema.

Aliomba katika ugawaji wa wilaya hizo, rasilimali zilizopo na mipaka igawanywe kwa manufaa ya wananchi wa wilaya hizo. 

Aidha, alisema kinachosubiriwa ni ugawaji wa mipaka na kutangazwa rasmi kuongezeka wilaya mbili ya Kigamboni na Ubungo na kufikisha idadi ya wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam.

Akizungumzia ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke, Sadiki alisema hadi kufikia juzi, ombi hilo lilishaidhinishwa na rais, hivyo Kinondoni itakuwa na wilaya mbili za Kinondoni na Ubungo huku wilaya ya Temeke ikiwa na wilaya za Temeke na Kigamboni

Jaji Mkuu: Maharti ya Dhamana Mahakama za Mwanzo Kupunguzwa

$
0
0

Jaji mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed Othman Chande amesema idara ya mahakama ipo katika mchakato wa kuangalia upya masharti ya dhamana yanayotolewa katika mahakama za mwanzo baada ya kubainika kuwa ni magumu hali inayochangia mlrundikano wa mahabusu katika magereza yote nchini.

Jaji Chande aliyasema hayo jana jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa wiki ya elimu ya sheria nchini katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo alisema sharti la dhamana sio adhabu kwa mtuhumiwa na kusisitiza kuwa tayari mahakimu katika ngazi za Mahakama za Mwanzo, Wilaya na mikoa wameanza kutafuta njia ya kupunguza idadi ya mahabusu.

Aidha katika uzinduzi huo idara ya mahakama imesema inaangalia uwezekano wa kutoa adhabu mbadala kwa wafungwa waliohukumiwa kifungo cha chini ya miaka mitatu ikiwemo vifungo vya nje kwa kufanya kazi za kijamii zinazosimamiwa na idara ya ustawi wa jamii.

Askofu Mpya KKKT Aonya Utumbuaji MAJIPU.......Amtahadharisha Rais Kutumbua Majipu kwa Haki, Asema Bunge Halipaswi Kulindwa na Jeshi

$
0
0
(Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo (kulia) na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu Alex Malasusa baada ya ibada ya kumuingiza kazini Askofu Shoo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016. )
***

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick Shoo ameitahadharisha Serikali kuhusu zoezi la Utumbuaji Majipu linaloendelea akiitaka kuzingatia misingi ya haki na busara ya Ki-mungu ili kutowapa nafasi watu wasio waaminifu kuitumia vibaya kufanya ukandamizaji.

Askofu Shoo aliyasema hayo jana  mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, katika ibada maalum ya kuingizwa kazini iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Alisema kuwa Kanisa lina imani na Serikali ya Awamu ya Tano na kupongeza juhudi zake katika kupambana na watumishi wa wanaojihusisha na ubadhirifu wa mali za umma pamoja na mafisadi, lakini zoezi la kutumbua majipu linapaswa kuchukuliwa kwa uangalifu mkubwa ili kuepuka uonevu.

“Utumbuaji huu ufanyike katika misingi ya haki na kwa busara kwani watu wengine wanaweza kutumia mwanya huu kuonea wenzao wasiokuwa na hatia,” alisema Askofu Shoo.

Katika hatua nyingine, Askofu Shayo alielezwa kusikitishwa na vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyofanywa na baadhi ya wabunge wanapokuwa Bungeni.

“Tunahitaji kuona Bunge linajadili vikao vyake kwa uwazi na kwa kuzingatia misingi ya demokrasia. Kanisa linasikitishwa sana na vitendo vya utovu wa nidhamu vinavyoendelea bungeni. Tunapenda kuona hoja zinajadiliwa kwa ustaarabu,” alieleza.

Kadhalika, Askofu Shayo aliionya matumizi ya jeshi la Polisi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kueleza kuwa Bunge ni sehemu ya Demokrasia na kamwe haipaswi kulindwa na jeshi. Aliongeza kuwa Bunge linapaswa kuendeshwa kwa kufuata misingi ya kidemokrasia na uwazi.

Aliihakikishia serikali kuwa Kanisa litaendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo ikiwa ni pamoja ikiwemo sekta ya elimu na afya. Aliishauri Serikali kuangalia upya sera ya elimu bure na kuboresha utoaji wa elimu hiyo.

Naye Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alizishukuru taasisi za dini kwa kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo kupitia sekta mbalimbali na kuzihimiza kuendelea kuwekeza katika maeneo muhimu yakiwemo ya Afya na elimu.

“Napenda kutumia fursa hii kuyashukuru madhehebu ya dini ambayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia Serikali katika kufikisha huduma hizi za afya karibu zaidi na wananch. Wito wangu kwa hili, naombeni mjitahidi kutoa huduma hizi kwa gharama nafuu ili wananchi wengi waweze kuzitumia,” Waziri Mkuu Majaliwa ananukuliwa.

Ibada hiyo maalum ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Mahakama Yashusha Rungu kwa Majangili........Yawapiga Kifungo cha Miaka 20 na Faini ya Milioni 270

$
0
0

Mahakama ya Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida, imewahukumu mtu na kaka yake, kutumikia kifungu cha miaka 20 kila mmoja na kulipa fidia ya sh. milioni 270, baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya kukutwa na meno ya tembo, silaha na risasi kinyume cha sheria.

Washitakiwa hao ni Nicodem Mchongareli na Festol Mchongareli, ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 13 ya mwaka jana. 

Wanadaiwa kukutwa na meno ya tembo mawili yenye thamani ya sh. milioni 27, bunduki tatu zikiwemo za aina ya Riffle, risasi 25 na maganda yake 15.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Joyce Minde, baada ya upande wa Jamhuri uliokuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Salim Msemo na ule wa utetezi kufunga ushahidi.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Joyce alisema wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, upande wa jamhuri ulileta mashahidi watano na washitakiwa baada ya kuonekana wana kesi ya kujibu walijitetea wenyewe.

“Mahakama imewaona washitakiwa hao wana hatia baada ya upande wa Jamhuri kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi na kuacha shaka yoyote,” alisema.

Hakimu huyo aliwapa adhabu washitakiwa hao kwa kukutwa na meno ya tembo, kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja na kulipa serikali sh. milioni 270. 

Pia shitaka la pili wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya sh. milioni 333 na makosa mengine kutumilia kifungo cha miaka miwili au kulipa faini ya sh. milioni mbili kwa kila shitaka.

Adhabu za vifungo zinakwenda sambamba, hivyo washitakiwa hao watatumikia kifungo cha miaka 20 kila mmoja

UKAWA Wapinduliwa....Kamati Iliyoibua Sakata la Escrow Yakabidhiwa Kwa Wabunge wa CCM

$
0
0

Wabunge wa upinzani, wakiwamo wanaootoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamepata pigo la aina yake baada ya jukumu mojawapo muhimu la kamati wanayopaswa kuiongoza kuondolewa kwao, imefahamika.

Kamati hiyo ni ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC) ambayo imehamishiwa kwenye kamati mpya inayoongozwa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Majukumu hayo muhimu yaliyohamishwa PAC ni yale yanayohusiana na hesabu za mashirika ya umma.

Majukumu hayo sasa yamehamishiwa kwenye kamati mpya ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Jimbo la Sumve (CCM), Richard Ndasa, huku makamu mwenyekiti akiwa Lolesia Bukwimba (Busanda-CCM).

Naibu Katibu wa Bunge anayeshughulikia masuala ya Bunge, John Joel, amethibitisha  juu ya kuwapo kwa mabadiliko hayo, akisema kwamba ni kweli PIC imepewa jukumu la kusimamia hesabu za mashirika ya umma kutokana na kanuni za Bunge, toleo la Januari 2016.

Alisema uamuzi wa kupeleka jukumu hilo PIC, umetokana na pendekezo la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kutokana na PAC iliyopita kushindwa kutimiza majukumu yake iliyopewa.

Katika mabunge yaliyotangulia, hesabu za mashirika ya umma zilikuwa zikisimamiwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia (Chadema), Zitto Kabwe. Hivi sasa, Zitto ni Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo.

Kamati hiyo pia iliwahi kuongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mara zote PAC ndiyo iliyokuwa mstari wa mbele katika kuibua ‘madudu’ mbalimbali yanayohusiana na rushwa na ufisadi bungeni na kuilazimu serikali kubadili mawaziri wake mara kadhaa.

Baadhi ya mambo yaliyowahi kuibuliwa na PAC ni pamoja na kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow ambayo ripoti yake ilisababisha mawaziri wawili wa serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete na maofisa wengine kadhaa wa juu kuachia ngazi. 

Taarifa ya PAC kuhusiana na ripoti ya CAG mwaka 2012 pia ilisababisha vigogo kadhaa, wakiwamo mawaziri, kung’olewa.

Zitto Atoa ufafanuzi
Aliyekuwa Mwenyekiti wa PAC kwenye Bunge la 10, Zitto, amesema si kweli kwamba kuna jukumu walilopewa na kushindwa kulitimiza.

 “Kwa kweli tulitimiza majukumu yetu yote. Na ili tufanye kazi yetu kwa ufanisi, tuliigawa kamati, eneo moja likawa chini ya Makamu Mwenyekiti (Deo Filikunjombe) na moja chini yangu. Deo mashirika na mimi serikali.

"Hata hivyo, kazi ilikuwa kubwa na muhimu kugawa PAC kuwa na PIAC na PAC. Isipokuwa, PIC ya sasa haina mamlaka ya kushughulikia hesabu za mashirika ya umma kwa mujibu wa kanuni. Kamati za mahesabu ni mbili tu, PAC na LAAC,” alisema Zitto.

Aliongeza kuwa iwapo Bunge linataka PIC ishughulike na hesabu za mashirika ya umma, itabidi iitwe Public Investments Account Committee (PIAC) na itabidi iongozwe na mbunge wa upinzani na siyo wa CCM.

“Kanuni za Bunge za sasa hazielekezi PIC kushughulikia taarifa ya CAG kuhusu mahesabu ya mashirika ya umma. Pia kanuni haziipi PAC mamlaka hayo pia. Kikanuni, hivi sasa mahesabu ya mashirika ya umma hayana kamati,” alisema Zitto.

Vurugu: Watu Walioficha Nyuso Zao Wavamia na Kuvunja Vibanda vya Biashara na Msikiti Huko Zanzibar

$
0
0

Watu  wasiojulikana wamevamia katika makazi ya watu eneo la Msumbiji mjini Unguja na kuvunja mabanda na msikiti.

Watu hao maarufu kama mazombi, walifanya uhalifu huo usiku wa kuamkia jana, ambapo walivamia eneo hilo wakiwa wamejifunika nyuso zao na soksi maalumu, huku wakiwa na silaha za jadi.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, amesema  kuwa watu hao walivamia eneo hilo saa 10 alfajiri.

Alisema watu hao baada ya kufika katika eneo hilo ambalo linadaiwa kukusanya mashabiki wa vyama vya upinzani, walianza kuvunja mabanda ya mafundi seremala.

“Lilikuwa kundi la watu, tena wote ni mazombi, wakiwa na silaha za moto pamoja na zile za kijadi kama mapanga, marungu, mikuki na mashoka.

“Wamefanya uharibifu mkubwa wa mali zetu yakiwamo mabanda ya mbao, msikiti wa mabati wa hapa Msumbiji ambao tumekuwa tukiutumia kama msikiti wa muda wakati  huu wa kisasa ukiendelea kujengwa.

“Vurugu hizi wamefanya zimekuwa kubwa sana na uharibifu, huu kwa kweli ni uonevu wa hali ya juu, wameharibu mabanda karibu yote kama unavyoona  na mengine ya biashara yaliyopo kando ya barabara hadi kufikia eneo la mabati,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Jeshi la Polisi lipo katika uchunguzi.

“Tumepata taarifa za tukio la kuvunja vibanda katika eneo la Msumbiji na Jeshi la Polisi tumeanza msako wa kuwabaini watu waliohusika na tukio hili, ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema Kamanda Mukadam.

Kundi La Mziki La Navy Kenzo Latoa Wimbo Na Video Mpya-kamati

$
0
0
THE INDUSTRY MUSIC LABEL
Baada ya kutamba Mwaka Jana Africa nzima na wimbo unaoitwa ‘Game’, Kundi la Navy Kenzo limeanza mwaka vizuri baada ya kutoa wimbo mpya pamoja na video yake unaoitwa “Kamatia” .

 Wimbo huo umeshaanza kuwa gumzo sehemu mbali mbali na kuonyeshwa kwenye TV za kimataifa siku mbili tu baada ya kutoka.

 Uzinduzi wa Wimbo Huo ulifanyika Kiaina yake kwa Staili ya ‘Flash Mob’ Kwenye Club ya Rhapsody kwa kuwasuprise waliokuwa ndani ya Club hiyo.
 
Kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Aika na Nahreel ,mpaka sasa wameshatoa nyimbo kadhaa zilizotamba sana kama Moyoni, Bokodo, Visa na nyingine nyingi.
 
Navy Kenzo wameamua kutoa Wimbo pamoja na Video yake moja kwa moja kutokana na ushindani uliopo kwa sasa kwenye Music wa Bongo Flava.

Video imefanyika nchini South Africa na Muongozaji wa Video wa kimataifa anayeitwa Justin Campos.
 
==>Bonyeza Link ifuatayo Kudownload Wimbo huo ;DOWNLOAD AUDIO

==>Au Angalia Video Hapa;VIDEO

Toka Bungeni: Nyumba 3500 Kujengwa kwa Ajili ya askari Polisi

$
0
0

Serikali inakamilisha taratibu zakupata mkopo toka serikali ya China bilioni 500 kwaajili ya ujenzi wa nyumba 3500 za askari wa jeshi la polisi nchini kufikia mwaka 2025.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Masauni Yusufu Masauni ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka aliyetaka ufafanuzi wa lini serikali itaboresha na kuongeza nyumba za askari polisi nchini.

Naibu Waziri Masauni amesema kuwa ni dhamira ya serikali kuhakikisha jeshi la polisi linaboresha makazi na kuwa na ofisi ili kuwezesha utoaji wa huduma kwa wananchi kuwa mzuri na pindi mkopo huo utakapo kamilika ujenzi utaanza kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa kwa sasa wapo katika mpango wa awali wa kujenga nyumba 350 nchi nzima ambazo zitatatua tatizo hilo la walinzi wa raia na mali za wa Tanzania kukosa makazi bora na ya kudumu.

Toka Bungeni: Serikali Yaahidi Kuboresha Huduma Za Afya.......Wauguzi Wanaotoa Lugha Chafu Kwa Wagonjwa Kuchukuliwa Hatua Kali

$
0
0

Serikali imejipanga kutoa huduma bora za afya kwa wananchi kwa kuwawezesha kila mwananchi kupata Bima ya Afya itakayosaidia kupata huduma bora za afya katika zahanati na hospitali mbalimbali.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee Mhe.Hamis Adrea Kigwangalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Faida Mohammed Bakar(CCM) 

Mh. Faida alitaka kujua namna serikali ilivyojipanga kutokomeza tabia mbaya ya wahudumu wa afya hasa kutoa lugha chafu kwa wagonjwa hususani kwa kinamama wajawazito na kwamba  bado kuna ukiukwaji wa huduma za afya, haki za afya na haki za uzazi katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya  hapa nchini.

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kingwala alisema  katika kuhakikisha kuwa haki hizo za mgonjwa zinapatikana,Serikali kwa kupitia mifumo yake, ikiwa ni pamoja na mabaraza ya weledi, kurugenzi ya uhakiki na ubora wa huduma za afya na idara mbalimbali zilizo chini ya Waziri zinatoa mafunzo kwa watoa huduma za afya kuhusiana na haki za wateja.

Mhe. Hamis Adrea Kigwangalla amesema katika kutekeleza hili vituo vyote vya kutolea huduma za afya vina masanduku ya maoni na ofisi za malalamiko ambazo ni sehemu muhimu ambapo wateja wanaweza kupeleka malalamiko yao ili hatua zaidi zichukuliwe kukomesha na kutokomeza ukiukwaji wowote wa haki za wateja.

“ Tutawachukulia hatua wale wote watakaobainika kukiuka haki za wateja kwa kupitia baraza la wauguzi na wakunga ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazostahili ili kuokoa maisha ya wananchi hasa maisha ya mama na mtoto” Alisema Mhe.Kigwangalla na kuongeza;

''Ni marufuku kwa wauguzi kutoa lugha chafu kwa wagonjwa na wana bodi zao za taaluma zao hivyo kila mgonjwa anaehudumiwa aangalie anahudumiwa na nani na atoe maoni yake katika eneo husika ili sheria ichukue mkondo wake''

Aidha Mhe. Hamis Adrea Kigwangalla amesema Wizara yake imeandaa rasimu ya Sheria ya Bima ya Afya ambayo itamuwezesha kila mwananchi kupata bima ya afya itakayomsaidia kupata huduma bora za afya katika maeneo yao.

Serikali kupitia Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee inatoa mafunzo kwa  Wakunga wa Jadi ambao wamekuwa wakitumika sana sehemu ambazo huduma za afya zipo mbali ili kuwezesha wananchi hao kupata huduma bora za afya kutoka kwa wakunga hao hasa katika afya ya mama na mtoto.

Toka Bungeni : Bunge Latengua Kanuni Ya 94 (1)

$
0
0

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limetengua kanuni ya 94 (1) ya kanuni za kudumu za bunge za mwaka 2006 ili kuliwezesha bunge  kujadili mpango wa serikali utakaotaumika kwa muda wa mwaka wa fedha 2016 & 2017.

Akitengua kanuni hiyo, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu katika Serikali ya Awamu ya Tano, Jenista Mhagama amesema kwamba bunge lilitakiwa likae kama kamati mwezi Nonemba ili liweze kujadili mpango wa serikali lakini kutokana na uchaguzi mkuu uliokuwepo nchini kazi hiyo ilishindikana.

Kwa msingi huo kutokana na uwezo wa bunge kupitia ibara ya 63 (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayowezesha bunge kujadili mipango ya serikali,kwa muda muafaka serikali imeamua kutengua kanuni ili bunge likae kama kamati kwa muda wa siku 5 ili kujadili mpango wa serikali ili wabunge waweze kuishauri serikali kabla ya bunge la bajeti.

Aidha mpango huo ulishindwa kujadiliwa bungeni Ijumaa iliyopita kutokana na kanuni za bunge kukiukwa kwa kusomwa bila kutengua kanuni ya 94(1).

Kutoka Bungeni: Serikali Kujenga Vyuo Vya VETA kila Wilaya

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi  inatarajia kujenga Vyuo vya Ufundi (VETA) kwa kila wilaya ili kutoa fursa kwa wananchi wengi hususani vijana kupata mafunzo mbalimbali ya ufundi  yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kujenga taifa.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziriwa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi  Mhe. Mhandisi Stella Manyanya  wakati akijibu swali la Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Kilasike Mwambalaswa (CCM) kuhusu ujenzi wa vyuo vya VETA  kwa kila Wilaya ambapo Wilaya ya Chunya ni moja kati ya Wilaya kumi za mwanzo zilizo katika mpango wa ujenzi wa vyuo hivyo .

Naibu Waziri huyo amesema Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa na Chuo hicho  Cha VETA , tayari maandalizi ya awali ya ujenzi wa chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya utambuzi wa stadi zinazohitajika  yamekamilika.

“Natoa wito kwa wabunge katika majimbo yao kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya zote watafute ardhi kwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivi ili hata mipango ya ujenzi ikikamilka ikute eneo lipo tayari kwa kuanza utekelezaji wake”Alisema  Mhe.Manyanya.

Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amesema katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 Wizara hiyo kupitia Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeshateua wataalamu elekezi watakaoshindanishwa kutayarisha andiko la jinsi ya kuifanya kazi ya kubuni majengo na kupata gharama ya kazi hiyo ili kuanza ujenzi mara moja.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi  kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imejipanga kutoa elimu bora ya ufundi yenye kuleta ufanisi katika maendeleo ya ufundi stadi nchini ili kuwawezesha  wahitimu kupata ujuzi ulio bora kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Toka Bungeni: Hatimaye Bunge Laanza Kujadili Mpango wa Maendeleo Uliokwama Kuwasilishwa Bungeni Wiki Iliyopita

$
0
0

Hatimaye leo Bunge limeanza kujadili mpango wa maendeleo ya mwaka 2016/2017, baada ya bunge hilo kutengua kanuni ili kupitisha mpango huo ambao ulikataliwa wa baadhi ya wabunge wiki iliyopita.

Akiwasilisha Mpango huo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema mpango huo umeweka kipaumbe cha kuanzisha na kuendeleza viwanda vinavyotokana na rasilimali zinazopatikana nchini pamoja na viwanda vya kuzalisha bidhaa zinazotumiwa na watu wengi.

Dkt. Mpango amesema katika mapango huo serikali imepanga kukusanya shilingi trilioni 14.16 kutokana na mapato ya kodi katika mwaka wa fedha 2016/2017 ambayo ni ongezeko la asilimia 15 ikilinganishwa na mapato ya kodi ya fedha yaliyokusanywa mwaka uliopita.

Aidha katika mwaka wa fedha 2016/2017, serikali imepanga kutumia shilingi trilioni 22 .99 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo ambapo kati ya hizo trilioni 16.80 itakuwa ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 6.18 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Amesema kati ya trilion 16.80 za matumizi ya kawaida, shilingi trilion 6.65 zitakuwa ni kwa ajili ya mishahara.

Aidha amesema kuwa kati ya trilion 6.18 za miradi ya maendeleo, takriban trilion 4 sawa na asilimia 77.8 zitakuwa ni fedha za ndani.

Bunge litakaa kama kamati kujadili na kutoka mapendekezo kwa ajili ya kuboresha mpango huo kwa  siku tano kuanzia leo.

Mpango huo uliingia dosari wiki iliyopita baada ya wabunge wa upinzani kukataa kuujadili kwa madai kuwa serikali ilikiuka kanuni na taratibu za kuuwasilisha bungeni.

Kikwete Apata Uteuzi mwingine Mzito wa Kimataifa

$
0
0

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa na Mheshimiwa  Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (kulia) kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika  katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
 
Kufuatia uteuzi huo uliotangazwa rasmi na AU jana katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika, Rais Mstaafu Kikwete leo asubuhi amekutana na Dkt. Zuma makao makuu ya AU leo na kufanya nae mazungumzo kuhusu jukumu alilokabidhiwa.
 
Mheshimiwa Dkt. Kikwete amemshukuru Dkt. Zuma na Wakuu wa Nchi za AU kwa imani kubwa waliyoonyesha kwake kwa kukabidhiwa jukumu hilo zito.  Amewashukuru pia wadau wa siasa nchini Libya kwa kuridhia uteuzi wake.
 
Naye Dkt. Zuma amemshukuru Dkt. Kikwete kwa kukubali uteuzi huo na  kuwa tayari kubeba jukumu hilo.

 Amemueleza kuwa Umoja wa Afrika na Afrika nzima inayo matarajio makubwa juu yake na iko nyuma yake. 

Amemuhakikishia kumpa kila aina ya ushirikiano atakaouhitaji kukamilisha katika kutekeleza majukumu yake.

Rais Magufuli Afanya Mazungumzo Na Mwenyekiti Wa Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi ....Wameongelea Uhuru wa Tume na Swala la Zanzibar

$
0
0
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi hapa nchini Mheshimiwa Jaji Damian Lubuva amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa tume hiyo ipo huru na haijawahi kuingiliwa kimaamuzi na Rais wala kiongozi yoyote.

Jaji Lubuva amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli ambapo alikuwa akimpa taarifa juu ya yaliyojiri katika kikao cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika Mjini Kampala, Uganda na kujadili kuhusu uchaguzi Mkuu wa Uganda unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu.

Amesema katika kikao hicho ambacho yeye alikuwa mwenyekiti, wamezungumzia umuhimu wa tume ya uchaguzi kuwa huru huku wakichukulia mfano wa Tanzania ambayo imetoka katika uchaguzi mkuu miezi michache iliyopita.

Jaji Lubuva amefafanua kuwa tume ya uchaguzi inapaswa kuwa huru katika maamuzi yake na kwamba jambo hili limekuwa likifanyika wakati wote hapa nchini.

Amebainisha kuwa wanaosema Rais anapaswa kuingilia kati masuala ya uchaguzi iwe Tanzania bara ama Zanzibar wanafanya makosa, kwani kwa namna yoyote Rais hana mamlaka hayo na hivyo hawezi kuingilia maamuzi ya tume hizo

“Unaposikia kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano aingilie hilo suala la uchaguzi wa Zanzibar, yeye kwa kweli hana mamlaka kabisa. Pili ni kama kujikanganya, huku unasema tuwe na tume huru isiyoingiliwa halafu huku unasema aingilie kati maamuzi ya tume” alisema Jaji Lubuva

Jaji Lubuva amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikatiba hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar na hata huku bara pia hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya tume.

Mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi amewasihi Watanzania kuwa uchaguzi umekwisha, na kuwaomba waungane na viongozi waliochaguliwa kuchapa kazi ili kujiletea maendeleo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam.
01 Februari, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Ramadhan Kailima Februari 01,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya mazungumzo

Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman Atoa Siku 7 Kwa Mahakimu 508 Watoe Maelezo Kwanini Wasifunguliwe Mashitaka Kwa Kufanya Kazi Chini Ya Kiwango.

$
0
0
 JAJI Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othuman  ametoa siku saba kwa mahakimu 508 watoe maelezo ni kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa, baada ya kufanya kazi chini ya kiwango.

Jaji Mkuu Chande ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Mnanzi Mmoja jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Sheria.

Alisema kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ni 250, ambapo Mahakimu Wakazi 121 kwenye mahakama hizo wameamua kesi chini  100 mwaka jana.
 
Alibainisha kuwa kiwango cha kwa kila Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ni 260, ambapo mahakimu Wakazi na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo 387 wameamua kesi chini ya 100 mwaka jana.

"Ukiondoa wale ambao wameajiriwa karibuni, wanaofanya kazi kwenye mahakama za mwanzo zisizokua na mashauri mengi au waliokwenda masomoni katikati ya mwaka au likizo za ujauzito hawatahusika katika sakata la kujieleza.
 
"Majaji Wafawidhi nimewaagiza wachambue na kuainisha mahakimu wote walioshindwa kufikia kiwango cha kesi walizopaswa kuamua kesi 250 na kesi 260 kwa mwaka jana na kuwataka watoe maelezo ndani ya siku saba kwa nini wasichukuliwe hatua," alisema Jaji Chande

Jaji Chande alitoa muda wa kukamilika kwa mchakato huo, ambapo walizitaka idara husika ndani ya siku 21 kila kitu kiwe kimekamilika ili ijulikane ni hatua gani wanachukuliwe.
 
"Mahakama haikubali hakimu ambaye anabembeleza kesi. Hakimu hatakiwi kufanya hivyo anatakiwa asikilize kesi hizo naazimalize. Haiwezekani katika mahakama moja hakimu mmoja anamaliza kesi 800 mwingine anamalizia chini ya 100 hilo halitakubalika kutokana na kasi ambayo tunayo," alisema

Jaji Mkuu Chande alisema mahakimu hao watapelekwa katika kamati zao kwa hatua ya kujieleza. Kazi kuu ya kamati hizo ni kupeleleza, kuchunguza na kushughulikia mashtaka yote ya nidhamu ya mahakimu.

"Mahakimu wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi na kushindwa kutoa sababu za kuridhisha kwa nini wameamua idadi ndogo ya kesi kuliko walivyopaswa, ambapo itashughulikiwa haraka na Kamati za Maadili za Mahakimu kwa mujibu wa sheria na taratibu za haki," alisema

Hata hivyo, Jaji Mkuu Chande alitoa pongezi kwa mahakimu ambao wamevuka kiwango, ambapo mahakimu 14 wameamua zaidi ya kesi 700 kwa mwaka jana na mahakimu wengine wamesikiliza kesi 915,789 na 778.

Alisema mkakati wao ni kuanza kesi sifuri mwaka unapoanza, kwa sababu kuna baadhi ya mahakama za mwanzo zimekuwa zikimaliza kesi na kuanza mwaka upya.
 
Jaji Mkuu Chande alisema Januari 1, 2015 mahakama za mwanzo zilianza na kesi 34,126 na mwaka huu Januari 1 zilianza na kesi 20,431. Kiwango cha kumaliza kesi ukilinganisha na idadi ya kesi zilizosajiliwa 2015 ni zaidi ya asilimia 100. Mahakama ya Mkuranga asilimia 141, Rufiji asilimia 121 na Bukoba Mjini asilimia 224.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images