Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Atoa Ufafanuzi Kuhusu Kauli Yake Ya Kupiga Marufuku Mikutano Ya Vyama Vya Siasa

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo amefafanua kauli yake ya kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa nchini  kuwashukuru wananchi hasa kwa wale wagombea walioshindwa uchaguzi  kwa kusema  kuwa mwandishi aliyeripoti tukio hilo alimnukuu vibaya.

“.......na tumesema, siasa tumeshazimaliza. Sasa tunataka tufanye kazi za maendeleo. Hatuhitaji tena watu kuja kutuvuruga. Mikutano ya shukrani itafanywa na wale tu walioshinda kwenye maeneo yao. Wengine watulie.

“Vyama sasa viache wale tu waliochaguliwa kwenye maeneo yao washukuru, wengine hawa watakuja kuleta maneno ambayo yatatuvuruga. "
Waziri Mkuu alinukuliwa akiyasema hayo Wilayani Ruangwa mkoani Lindi

Akijibu Swali la Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni Mhe. Freeman Mbowe  leo asubuhi kuhusiana na kauli hiyo, Waziri Mkuu alisema kuwa serikali inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na katiba hivyo inatambua kuwa katika mfumo wa vyama vingi,  vyama vya siasa vinaruhusiwa kufanya mikutano ila kwa utaratibu maalumu.

Waziri Majaliwa alisema  mwandishi aliyemnukuu kuhusiana na kauli hiyo hakumtendea haki kwa kuwa aliitoa kauli hiyo  akiwa kama mbunge wa kawaida na si Waziri mkuu na yalikuwa ni makubaliano ya vyama vya siasa katika jimbo lake  na kwamba halikuwa agizo kwa nchi nzima.

Waziri Mkuu huyo aliongeza kuwa kauli hiyo aliitoa wakati alipokutana na madiwani na viongozi wengine wa mkoa wake ambapo walikubaliana kuweka siasa pembeni na kufanya kazi kwa pamoja katika kuleta maendeleo.

Breaking News: CUF Wagoma Kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar

$
0
0
Azimio La Baraza Kuu La Uongozi La Taifa Kuhusu Tangazo La Mwenyekiti Wa Tume Ya Uchaguzi Ya Zanzibar La Kuitisha Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi), likiwa ndiyo chombo cha juu cha maamuzi katika Chama baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa, limefanya kikao cha dharura leo, tarehe 28 Januari, 2016, katika Ofisi Kuu ya CUF, mjini Dar es Salaam. 

Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja tu, ambayo ni kufanya maamuzi kuhusiana na tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar la kuitisha uchaguzi wa marudio.

Baada ya kujadili kwa kina tamko hilo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, la kuitisha uchaguzi wa marudio tarehe 20 Machi, 2016 na mwenendo mzima wa hali ya kisiasa Zanzibar tokea alipotoa tamko lake batili la tarehe 28 Oktoba, 2015 kudai kwamba amefuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matokeo yake, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

1. KWAMBA Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umeshafanyika tarehe 25 Oktoba, 2015, ambapo kwa upande wa uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani ulikwisha kamilika na washindi wote kupewa shahada za kuwathibitisha na kuwatambua kama washindi halali. 

Kwa upande wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, matokeo yalikwisha bandikwa nje ya vituo vya majumuisho vya majimbo yote 54. Kilichokuwa kinaendelea baada ya hapo ni kuhakiki matokeo hayo kutoka majimboni na kazi hiyo ilikwishakamilika kwa majimbo 40 na katika hayo, matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa majimbo 31 yalikwishatangazwa kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jecha Salum Jecha, kutangaza isivyo halali kwamba ameufuta uchaguzi huo.

2. KWAMBA Chama Cha Wananchi (CUF) hakitoshiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 kwa sababu uchaguzi huo si halali kwani uchaguzi halali ulishafanyika.

3. KWAMBA linatoa wito kwa Wazanzibari wote wanaoipenda nchi yao na ambao wanaamini katika utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu Katiba na Sheria za nchi yetu kutoshiriki katika uchaguzi huo usio halali wa marudio.

4. KWAMBA sababu kuu ya Baraza Kuu kufikia maamuzi haya ni kutokana na matamko yote mawili ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, kutokuwa halali na kwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984. 

Hakuna kifungu chochote cha Katiba ya Zanzibar au Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar kinachotoa uwezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na hata kwa Tume yenyewe kufuta uchaguzi au kuitisha uchaguzi wa marudio.

5. KWAMBA linazipongeza na limetiwa moyo sana na taasisi na jumuiya zote za kimataifa na kikanda zikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa Afrika (African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi za Marekani na Uingereza kwa msimamo wao wa kuungana na Wazanzibari na kutetea haki yao ya kidemokrasia na maamuzi halali waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kutaka mchakato wa uchaguzi huo ukamilishwe na matokeo yake kutangazwa.

6. KWAMBA linazipongeza na kutiwa moyo pia na taasisi za hapa nchini zikiwemo taasisi na jumuiya za kidini, taasisi za haki za binadamu, vyombo huru vya habari, vyama vyengine vya siasa na Wazanzibari na Watanzania wote wanaopenda amani na demokrasia kwa msimamo wao wa kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kuendelea kusisitiza haja ya kuheshimu na kufuata Katiba na Sheria za nchi yetu na pia haja na umuhimu wa kutunza amani ya nchi yetu kwa kutaka haki itendeke. 

Baraza Kuu linazihakikishia taasisi na jumuiya hizo zote na pia kuwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwamba CUF itaendelea kusimama kidete katika kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi yetu na pia kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.

7. KWAMBA limesikitishwa na kushangazwa na kitendo cha Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuandika barua na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kutaka vyama vya siasa vishiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 bila ya kujali kwamba uchaguzi huo ni haramu na unakiuka matakwa ya Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984.

 Baraza Kuu halikutarajia mtu mwenye hadhi ya Ujaji kufanya kazi ya kutumikia maslahi ya watawala ambao wameamua kuvunja Katiba na Sheria za nchi yetu na kukanyanga misingi ya haki na demokrasia huku akishindwa kukemea uhuni mkubwa uliofanywa wa kubaka demokrasia na haki za watu.

8. KWAMBA limesikitishwa na kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli, kukwepa dhamana na wajibu wake kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuiacha njiani kazi aliyoianza ya kutafuta ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi Zanzibar.

 Baraza Kuu linamtaka Rais Magufuli kujitathmini na kujiuliza anajiweka vipi na kutoa taswira gani mbele ya macho ya Watanzania na jumuiya ya kimataifa kutokana na kutosimamia ahadi yake aliyoitoa mbele ya Watanzania wakati akilizindua Bunge jipya kwamba atafanya kazi na vyama vya CUF na CCM ili kuupatia ufumbuzi mkwamo huu.

9. KWAMBA linalaani matumizi ya nguvu kubwa ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Muungano na Vikosi vya SMZ dhidi ya wananchi wasio na hatia na ambao wamekuwa watulivu licha ya vitendo vingi vya uchokozi wa makusudi na hata mashambulizi ya hujuma dhidi yao yanayofanywa na makundi ya vijana wa CCM waliowekwa katika makambi kadhaa kisiwani Unguja.

10. KWAMBA linaitaka jumuiya ya kimataifa na hasa taasisi zinazosimamia haki za binadamu na zinazopambana na makosa ya jinai kimataifa ikiwemo Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (International Criminal Court – ICC) kufanya uchunguzi wa kauli na matendo ya uhalifu, uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu na ubaguzi ambao umekuwa ukifanywa dhidi ya wananchi wa Zanzibar na kuchukua hatua dhidi ya watu walio nyuma ya maamuzi na utekelezaji wa matukio hayo.

11. KWAMBA linawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu na kuwa watulivu licha ya machungu makubwa waliyoyapitia na wanayoendelea kuyapitia tokea pale maamuzi yao yalipopinduliwa na CCM kwa kumtumia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha. 

Baraza Kuu linatoa wito kwa Wazanzibari wote kuungana pamoja chini ya chama chao cha CUF walichokipa ridhaa halali kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kutetea maamuzi yao waliyoyafanya kupitia sanduku la kura kwa njia za amani.

Baraza Kuu linawasisitiza tena Wazanzibari kwamba waendelee kutunza amani ya nchi yetu na kutambua kwamba kutunza amani si udhaifu bali ni jambo linaloipa nguvu jumuiya ya kimataifa kufuatilia haki za kidemokrasia za wananchi wa Zanzibar.

12. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawatahadharisha CCM na watawala wasiowajali na kuwaheshimu wananchi kwamba zama za utawala wa mabavu usioheshimu Katiba na Sheria za nchi hazina nafasi tena katika dunia ya leo. Baraza Kuu lina imani kwamba HAKI ITASHINDA.

LIMETOLEWA NA:
BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)
DAR ES SALAAM
28 JANUARI, 2016

Serikali Yatangaza Mkakati wa Kuwafilisi Mafisadi na Wahujumu Uchumi

$
0
0

SERIKALI kupitia vyombo vyake vya dola, imetangaza kuzitaifisha mali za wote waliopatikana na hatia ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi na kueleza kuwa utaratibu huo ndio utakaoendelea kwa watuhumiwa ambao bado kesi zao hazijamalizika au hazijapelekwa mahakamani.
 
Tangazo hilo la serikali limetolewa leo Januari 28, 2016 na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, DPP, Bw. Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi(DCI), Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani na Mkurugenzi wa Upeleelzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), wakati wa mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
 
Katika kuhakikisha kuwa jukumu hilo linatekelezwa, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai amesema, mwaka 2012 idara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kwa pamoja walikubaliana kufanya kazi ya ufuatiliaji wa mali zinazohusiana na uhalifu kama sheria inavyotaka na kwa upande wa jeshi hilo tayari kitengo chake cha upelelezi wa makosa ya uhalifu wa kifedha (Money laundering) kiko kazini.
 
“Katika kutekeleza mkakatihuo, Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi wa kesi 23 ambazo ziliwasilishwa kwa DPP na kati ha hizo ,kesi tatu (3) zimetolewa uamuzi na nyingine ishirini ziko katika hatua ya maombi ya kupata amri ya Mahakama ili ziweze kuzuiwa au kutaifishwa (Restraint or confiscation).” Alifafanua Kamishna Diwani Athumani
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Upelelezi kutoka TAKUKURU, Bw. Alex Mfungo, yeye amesema, taasisi yake imeona hakuna maana yoyote kwa mhalifu wa Ufisadi na uhujumu uchumi ukamfunga gerezani na kisha kumuachia baada ya kifungo halafu aendelee kutumia mali alizochuma kwa njia za haramu.

“Tumeona njia mbadala ya kudhibiti hali hiyo na kwa mujibu wa sheria ni kumfilisi mhusika hata kama atatumikia kifungo.” Alibainisha Bw. Alex

Naye Mkurugenzi wa Mashtaka, DPP, Bw. Biswalo Mganga, yeye amesema ili kuendana na dhana ya Hapa Kazi Tu, ni lazima kukabiliana na wahujumu uchumi na Mafisadi ili hatimaye Wananchi walio wengi waweze kunufaika na rasilimali zao. 

“Natoa wito kwa nyie waandishi wa habari muujulishe umma wa Watanzania kuwa kama mtu anayo taarifa au anajua mali zinazomilikiwa na mtu isivyo halali hususan watumishi wa umma basi atoe taarifa.” Alisema
 Mkurugezni wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga
DCI Kamishna wa Polisi Diwani Athumani
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, Bw. Alex Mfungo
DCI Kamishna wa Polisi Diwani Athumani
Bw. Mfungo, (kulia), akiwa na DPP, Mganga (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

Rais Dkt Magufuli Afanya Uteuzi Wa Naibu Gavana Wa Benki Kuu Ya Tanzania

$
0
0

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amemteua Ndugu Julian Banzi Raphael, kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Kabla ya uteuzi huu Ndugu Julian Banzi Raphael alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Viwanda, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


Ndugu Julian Banzi Raphael anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Juma RELI ambaye muda wake umemalizika tarehe 12 Julai, 2015.

Chadema Waungana na ACT -Wazalendo........Wadai Serikali ya Magufuli ni ya kidikteta

$
0
0

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekosa imani na serikali ya awamu ya tano kwa kuwa na matendo ya kidikteta na kwenda kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kwa kuminya uhuru wa wananchi wa kupata habari.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam, na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari ambapo amesema kuwa serikali imekuwa ikijinadi kwa kauli mbiu ya hapa kazi huku ikiwa mstari wa mbele kwa kuwanyima haki ya msingi wananchi ya kupata habari.

Amesema kuwa matendo hayo ni pamoja na kuzuia Shirikia la Utangazaji la Tanzania(TBC), kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mikutano ya bunge inayoendelea ,kufutwa kwa Gazeti la Mawio pasi na sababu za msingi,kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara, na kuunda kamati dhaifu bungeni.

Amesema kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye ametoa sababu zisizokuwa za msingi ambapo alidai kuwa serikali inaepuka gharama za kurusha matangazo hayo moja kwa moja na baadala yake kurekodi vikao hivyo vya bunge kwa  kurushwa saa nne usiku.

Amesema inaonekana Waziri huyo hajafanya utafiti na kwamba ikiwa  tatizo lipo kwenye gharama alizotaja chadema ipo tayari kuchangia gharama hizo kwa kuanzisha harambee maalumu pamoja kuwataka chama cha wamiliki wa vyombo vya Habari (Moat) na Baraza la Vyombo vya Habari (MCT) kulisimamia suala hilo.

“Nape ataje gharama hizo tutachangishana ......mwenye mia moja mia mbili ili wananchi wajue mambo muhimu yanayoendela kwa wakilishi wake”,amesema Mwalimu.

Amesema Nape alikuwa anayumba kwa kuwa na ndimi mbili kwa kuongeza sababu nyingine ya kuzuia kurusha kwa matangazo hayo ni kuwa muda huo ni wa kazi na kwamba watu watakuwa hawafanyi kazi kutokana na kuangalia bunge.

Amesema kuwa hoja ya watu kutofanya kazi haina mashiko kutokana na watu huwa wanafanya kazi ilhali bunge linaendelea ambapo kama kuna hoja muhimu watu huzisikia bila kuathiri shuguli zao lakini kuna wengine muda huo sio wa kazi kwao.

Amesema kuwa serikali imekusudia kuminya uhuru wa habari kutokana na matukio yaliyofuatana ya kushugulikia vyombo vya habari.

Amesema kuwa serikali imezuia mikutano ya siasa ambapo Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa na Nape Mnauye walitoa kauli hizo walipokuwa Mkoani Lindi na baadaye Jeshi la Polisi kuweka mkazo wa suala hilo.

Amesema suala hilo hawawezi kulikubali kutokana na chama kuwa na mikutano yao kila baada ya muda na kwamba muda wa kuratibu mikutano hiyo watafanya vikao vyao.

Amesema serikali imeunda kamati dhaifu bungeni  kwa nia ya kudhoofisha shughuli za utendaji bungeni na maendeleo ya nchi kwa kuwaweka wabunge wageni kwenye kamati muhimu ilhali hawana uwezo kuzisimamia ambapo kamati ambazo hazina umuhimu kupangiwa watu wenye uwezo.

Jifunze Kutengeneza Pipi Za Kihindi ,uongeze Kipato Chako.

$
0
0

 ==>Wewe  ni  kijana  wa  kitanzania ?
 ==>Unataka  kuongeza  kipato  chako ?
Kama  jibu  lako  ni NDIO  basi   hii  ni  HABARI NJEMA  SANA  KWAKO. Taasisi  ya  NEEMA  INSTITUTE  OF  N.G.O  MANAGEMENT  kupitia MRADI  WA  UANZISHAJI, UENDESHAJI  NA USIMAMIZI  WA BIASHARA  NDOGONDOGO  inatangaza  nafasi  za  kushiriki  katika  SEMINA  YA  UJASIRIAMALI.   Somo  litakalo fundishwa  ni

 UTENGENEZAJI  WA  PIPI  ZA  KIHINDI.
Pipi  za  Kihindi  ni  bidhaa  inayo  pendwa  sana  na  watoto  wa  shule  ya  msingi  na  hata  sekondari.
 
Washiriki  katika  Semina  hii, watapewa nafasi  za  biashara  katika  shule mbalimbali  za  msingi  zilizopo  jijini  Dar  Es  Salaam.

ADA  YA  KUSHIRIKI  KATIKA  SEMINA  HII    NI  SHILINGI  ELFU   HAMSINI    TU (Tshs.50,000/=)

Fomu  za  kujiunga  katika  semina  hii, zinapatikana  ofisini  kwetu  kwa gharama  ya  Shilingi  ELFU  KUMI  NA  TANO  TU( Tshs.15,000/=).

Tunapatikana  UBUNGO   Dar  Es  Salaam, jirani  na  Shule  Ya  Msingi  Ubungo  National  Housing  nyuma  ya  jengo  la  Ubungo  Plaza.

Mwisho  wa  kuchukua  fomu  ni  tarehe  30  JANUARY 2016  saa  nane  kamili  mchana.

Semina   itafanyika  kwa  siku  tano,  kuanzia  tarehe  01  Februari 2016  hadi  tarehe  05  February 2016.

Kwa  maelezo  zaidi  kuhusu  semina  hii , wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766  53  83  84    AU   Tembelea  blogu  yetu :www.neemainstitute.blogspot.com

FAIDA   ZA  KUSHIRIKI  KWENYE  SEMINA  KUHUSU  MAFUNZO  YA  UTENGENEZAJI WA  PIPI  ZA  KIHINDI.
Taasisi   ya  Neema  Institute  Of  N.G.O  Management  yenye  ofisi  zake  jijini  Dar  Es  Salaam, katika  eneo  la  Ubungo  imeandaa    SEMINA  KUHUSU   UTENGENEZAJI  WA  PIPI   ZA  KIHINDI  ambayo  itafanyika  kwa  muda  wa  siku  tano, kuanzia  tarehe  01  FEBRUARY  2016  hadi  tarehe  05 FEBRUARI 2016.

Lengo  la  semina  hii  ni  kuwasaidia  wajasiriamali  wadogo  wadogo  na  wale  wa  kati, kupata  ujuzi  utakao  wasaidia  kuongeza  vipato  vyao.

Zifuatazo  ni   faida   za  kushiriki  katika  semina  hii:
1.Mafunzo  yanafundishwa  kwa  njia  ya  nadharia  na  vitendo  ( Theory  and  Practical )kila  siku  kwa  siku  zote  tano  za  mafunzo .  Katika  siku  zote  tano  utakazo  hudhuria  mafunzo  haya, utapata  kujifunza  kwa  vitendo  jinsi  ya  kutengeneza  pipi  za  kihindi. Lengo  letu  ni  kuhakikisha  kila  anaye shiriki  katika  semina  hii, anatoka  akiwa  amewiva  katika  suala  zima  la  utengenezaji  wa  pipi.

2.     NI    BIDHAA  YENYE  SOKO  LA  UHAKIKA :
Pipi   za  kihindi  ni  pipi  zinazo  tengenezwa  kwa  kutumia  malighafi  iitwayo   sukari  guru  pamoja  na   viambatano  (ingredients )  vingine .   Pipi  hizi  ni  bidhaa  inayo pendwa  sana  na  watoto  wanao  soma  katika  shule  za  msingi  na  sekondari .  Kwa  muda  mrefu sasa, wahindi  wanajulikana  dunia  nzima  kwa  kuwa   na  umahiri  mkubwa  wa  kutengeneza   vitu  vitamu  tamu pamoja  na  vyakula  vizuri  kwa  ujumla.  Hivyo  basi  suala  la  pipi  za  kihindi.

Utafiti  wetu  umetuwezesha  kugundua, kwa  biashara  ya  kuuza  pipi  za  kihindi   mashuleni, unaweza  kuingiza  faida  ya  kati  ya  shilingi  Elfu Thelathini  ( Tshs.30,000/=)  hadi   Shilingi  Elfu  Themanini  (Tshs.80,000/=)  kwa siku, kutegemeana  na  kiwango  cha  uzalishaji  wako.
 
 Na  kama  utapata  nafasi  katika  shule  zaidi  ya  moja, kipato  chako  kitakuwa  kikubwa  maradufu.

3.UHAKIKA  WA  KUPATA  NAFASI  YA  BIASHARA  KWENYE  SOKO  LA  UHAKIKA .
Baada  ya  kuhitimu  mafunzo,  kila  mshiriki, atapewa  nafasi  ya  biashara    katika  shule  ya  msingi  yenye  idadi  kubwa  ya  wanafunzi iliyopo  jijini  Dar  Es  Salaam  na  hivyo  kumuwezesha  kutengeneza  kipato  cha  uhakika, kupitia  biashara  ya  pipi za  kihindi. Sisi  kama  Taasisi  tunazo  nafasi  zaidi ya  mia ( 100 ) katika  shule  mbalimbali  za  msingi  zilizopo  jijini  Dar  Es  Salaam zenye  idadi  ya  wanafunzi  kati  ya  mia  nne  (400)  hadi  elfu  moja  (1000).
Nafasi  hizi  za  biashara  tutazitoa  kwa   watakao  hitimu  mafunzo  yetu.
 
Nafasi  hii  utaipata  baada  ya  kumaliza  mafunzo. Mafunzo  yanaanza  Jumatatu na  kuisha  Ijumaa. Siku  hiyo  hiyo  ya  Ijumaa  unapewa  details  za  shule  utakayo  enda  kufanyia  biashara  yako, Jumamosi  na  Jumapili, unazitumia  kufanya  maandalizi  ya  kutengeneza  pipi  zako, na  Jumatatu  unaanza  kuingiza  pesa  kupitia  shughuli  ya  kuuza  pipi  kwenye  shule  ambayo  tutakuwa  tumekupangia.

(  FURSA  YA  KUPATA  NAFASI  YA  BIASHARA  INAWAHUSU  WALIOPO  DAR  ES  SALAAM  TU  )

4.MTAJI  MDOGO  WA  BIASHARA :  Mradi  wa  kutengeneza  na  kuuza  pipi za kihindi  mashuleni, hauhitaji kiasi  kikubwa  cha  fedha  za  mtaji. Hata  kwa  wajasiriamali  ambao  ndio  kwanza  wanaanza  ujasiriamali na  hawana uwezo mkubwa wa  kifedha  wanaweza  kumudu.

5.UTAPATA  FURSA  YA  KUUNGANISHWA  NA  WAJASIRIAMALI  WENZAKO  NA  KUUNDA  TAASISI  ISIYO  KUWA  YA  KISERIKALI.

Washiriki  wa  mafunzo  haya, wataunganishwa  pamoja  na  kuunda  Taasisi  isiyo  kuwa  ya  kiserikali ( N.G.O ), ambapo  wata saidiwa  kuanzisha  VICOBA  pamoja  na  kufundishwa  utengenezaji  wa  bidhaa  nyinginezo  zinazo  pendwa  sana  na  watoto  mashuleni  kama  vile  Ubuyu  wa  Zanzibar  nakadhalika.

6.SEMINA  INATOLEWA  KWA  MUDA  AMBAO  HAUWEZI KUHARIBU  RATIBA  YAKO.
Kutakuwa  na  madarasa  ya  asubuhi  pamoja  na  madarasa  ya  jioni. Madarasa  ya  asubuhi  yanaanza  saa  nne  hadi  saa  sita. Na  madarasa  ya  jioni  yanaanza  saa  kumi  hadi  saa kumi  na  mbili  Hivyo  basi  kama  wewe  ni  muajiriwa  na   hauna  nafasi  muda  wa  asubuhi, unaweza  kupata  fursa  ya  kushiriki  katika  semina hii wakati  wa   jioni  kuanzia  saa  kumi  hadi  saa  kumi  na  mbili.

7.UNAWEZA KUJIFUNZA  KUTENGENEZA  PIPI  ZA  KIHINDI  NA  UKAAJIRI  VIJANA WENGI  WA  KAZI  NA  KUTENGENEZA  FEDHA  MARADUFU.

Unaweza  kujifunza  kutengeneza  pipi  hizi, halafu  ukatafuta  nafasi  ya  biashara  kwenye  shule  mbalimbali  za  msingi   na  kuwaweka  vijana  wa kazi.   Ukipata  nafasi  katika  shule  nyingi, maana  yake  hata  kipato  chako  kitaongezeka  mara  dufu.

Hizo  ni  baadhi  ya  faida  za  kushiriki  katika  mafunzo  haya.

KWA   WALIOPO   NJE   YA  MKOA  WA  DAR  ES  SALAAM.
Kwa  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam, mafunzo   haya yatatolewa  kwa  njia  ya  Posta. Utapatiwa  DVD  na  VITABU  vinavyo  elezea  STEP  by  STEP  kuhusu namna  ya  KUTENGENEZA  PIPI  ZA KIHINDI.

JINSI   YA  KUJIUNGA  NA  MAFUNZO  HAYA  KWA  WAOMBAJI  KUTOKA  NJE  YA  DAR  ES  SALAAM.
Kama  upo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam, na  unataka  kushiriki  katika  mafunzo  haya, tuandikie  barua  pepe  ya  maombi  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya. Barua  pepe  yetu  ni :  neemainstitute@gmail.com
 
Mwisho  wa  kupokea  maombi  ni  tarehe  30 JANUARY  2016.

EWE  MZAZI !  EWE  MLEZI ! UNA NGOJA  NINI ?
MLETE  KIJANA  WAKO  APATE   MAFUNZO  YATAKAYO  MSAIDIA   KUINGIZA  KIPATO  CHAKE.

EWE  KIJANA!  ZAMA  ZA  KUAJIRIWA  ZIMEPITWA  NA  WAKATI. USISUBIRI  KUAJIRIWA.  NJOO  UPATE  UJUZI  UTAKAO  KUSAIDIA  KUINGIZA  KIPATO KIZURI

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Januari 29

January Makamba Atetea Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar.......Asema Watakaoleta Vurugu Damu Za Wazanzibar Zitawalilia

$
0
0

Serikali  imesema uamuzi wa kurudia uchaguzi wa urais Zanzibar ni halali na wa kisheria na kwamba wanaotafuta suluhu nje ya Katiba, wanakosea.

 Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, January Makamba alipokuwa akihitimisha majadiliano ya kuchangia hotuba ya Rais John Magufuli.

Alisema uchaguzi ulifutwa kisheria na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa Tangazo la Serikali Namba 6587. Makamba alisema Katiba ya Zanzibar, imeeleza wazi kuwa hakuna mamlaka ambayo itahoji uamuzi wa tume, hata kama ni Mahakama. Alisema akidi ilitimia wakati tume inafikia hatua hiyo.

Waziri huyo alisema wanaotaka kutumia suala hilo kuleta vurugu Zanzibar, damu za Watanzania zitawalilia. Alisema viongozi wakuu wa nchi, wamefanya kazi kubwa katika kulitafutia ufumbuzi suala hilo na hivyo ieleweke kuwa ZEC na NEC ni tume zinazojitegemea.

Alisisitiza NEC haiwezi kuingilia uamuzi wa ZEC, kwani uchaguzi wa rais uliofanyika kwa siku moja Tanzania Bara na Zanzibar, umekuwa ukiendeshwa na Tume mbili tofauti. Alisema uchaguzi huo, ulifanywa na tume tofauti na hata wino uliotumika katika chaguzi hizo ni tofauti .

Alisema wajibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuhakikisha kuwa amani na utulivu, vinalindwa Zanzibar katika marudio ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu.

Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, alitoa “Taarifa Kwa Umma ya Kufuta Uchaguzi wa Zanzibar”.

Katika taarifa hiyo, Jecha Salim Jecha alisema “Mimi nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, nimeridhika kwamba uchaguzi huu haukuwa wa haki na kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za uchaguzi. Hivyo, kwa uwezo nilionao natangaza rasmi kwamba uchaguzi huu na matokeo yake yote yamefutwa na kwamba kuna haja ya kurudia uchaguzi huu”.

Bunge: Hatutazuia Tv Binafsi Kurusha Live Matangazo ya Bunge

$
0
0

Wakati Bunge likieleza kuwa haliwezi kuzuia vituo vya televisheni nchini kuonyesha moja kwa moja matangazo ya shughuli za vikao vya Bunge, Serikali imetoa sababu tatu za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupunguza matangazo hayo ya shughuli za chombo hicho chenye mamlaka ya kutunga sheria.

Uamuzi wa Serikali kuhusu TBC ulizua sintofahamu bungeni na kusababisha polisi kutumika kuwatoa katika Ukumbi wa Bunge, wabunge wa upinzani waliokuwa wakishinikiza kusitishwa kwa mjadala wa hotuba ya Rais John Magufuli, badala yake lijadiliwe suala hilo la shirika hilo.

Naibu Katibu wa Bunge, John Joel alisema jana kuwa hakuna televisheni yenye mkataba na Bunge kurusha moja kwa moja matangazo hayo, zote zinazorusha zinatumia gharama zao wenyewe.

Baada ya TBC kupunguza matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge, televisheni zilizobaki ambazo zinarusha moja kwa moja matangazo hayo, ni Star TV kupitia chaneli yake ya Star Bunge pamoja na Azam TV.

 “Sisi hatuna mkataba nao, wao wanarusha kwa gharama zao na Bunge haliwezi kuwazuia, labda waulizwe wenyewe kama wataendelea kurusha matangazo hayo ama laa,” alisema Joel huku akisisitiza kuwa hakuna zuio lolote.

Juzi jioni Waziri wa Habari, Nape Nnauye alizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma na kueleza sababu tatu za kupunguzwa kwa matangazo hayo.

Nape aliitaja sababu ya kwanza kuwa ni kupunguza gharama za uendeshaji, “Kwa mwaka TBC ilikuwa inatumia Sh4.2 bilioni kurusha moja kwa moja matangazo haya. Fedha hizi hazilipwi na Bunge wala Serikali, zinatokana na matangazo madogo ya TBC, sasa pia hesabu tangu 2005 mpaka sasa zimetumika kiasi gasi.”

Alisema sababu nyingine ya kupunguza kurushwa kwa Bunge ni kutaka wafanyakazi wa Serikali kufanya kazi kikamilifu, kwa madai kuwa wengi badala ya kufanya kazi walikuwa wakifuatilia vipindi hivyo.

Alisema utafiti uliofanywa na Serikali umebaini kuwa waendesha bodaboda, mamalishe, wamachinga, wakulima, wafugaji na watu wenye shughuli nyingi wanashindwa kufuatilia vipindi vya Bunge asubuhi na mchana kutokana na kubanwa na shughuli zao.

Waziri Mpango: Hatutawaonea Huruma Wakwepa Kodi

$
0
0

Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa  mapato ya ndani ya kodi na ambayo siyo kodi ni lazima yakusanywe kikamilifu kwa mujibu wa sheria bila upendeleo na kuwaonea huruma wakwepa kodi nchini.

Mhe. Mpango ameyasema hayo kwenye mkutano wa pili kikao cha tatu Bungeni Mjini Dodoma alipokua akijibu hoja mbalimbali za wabunge walizochangia na kujadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa siku ya ufunguzi wa Bunge la kumi na moja tarehe 20 Novemba 2015 .

Dkt. amesema ni lazima watumishi na walipa kodi kufanya majukumu yao kikamilifu ili kupata fedha ambazo zitawasaidi wananchi wa vijijini kupata maendeleo kwa kupata huduma muhimu.

Waziri Mkuu: Tutahakikisha Nidhamu Inarudi Serikalini

$
0
0

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa,amesema serikali imeweka msisitizo katika kuhakikisha inarudisha nidhamu kwa watumishi wa umma kwa kuweka mkazo katika uadilifu, uwajibikaji, kutoa huduma kwa wakati.

Waziri mkuu Majaliwa ameyasema hayo  katika mkutano wa pili kikao cha tatu Bungeni Mjini Dodoma alipokua akihitimisha hoja ya kujadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa siku ya ufunguzi wa Bunge la kumi na moja tarehe 20 Novemba 2015 

Amesema  kuwa serikali itakuwa inawakumbusha watanzania na watendaji wa serikali  kufanya majukumu yao kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za haraka dhidi ya watumishi wanaokwenda kinyume na misingi ya utendaji kazi serikali kwa kuzingatia kauli mbiu ya hapa kazi tuu.

Pia amesema kuwa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge ambazo utekelezaji wake utahitaji kutengewa fedha za uandalizi wa kutenga fedha za serikali na utendaji wake utafanyika kwa haraka kwa kuzingatia maombi na hoja za wabunge kwakusimamia mapato ya Taifa ili yaongezeke kwa kiwango kikubwa.

Zitto Kabwe: "Serikali Imekurupuka, Kuongoza Nchi Sio Kutumbua Majipu Tu"

$
0
0
Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kuonesha masikitiko yake kwa kitendo cha serikali kushindwa kuleta Bungeni mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano.

Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameweka wazi jambo ambalo serikali inapaswa kufanya baada ya uchaguzi na kusema ni kuwasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano.

"Shughuli ya kwanza ya serikali baada ya uchaguzi ni kuwasilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano ( kutafsiri ilani yake kwenda kwenye mpango wa utekelezaji) . Bunge linapaswa kujadili na kuidhinisha Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 na kisha Mpango wa mwaka mmoja kuanza kutekeleza Mpango huo wa miaka 5. Kwa mujibu wa Katiba ya JMT Ibara ya 63(3)(c), Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 hutungiwa sheria kwa ajili ya utekelezaji." Alisema Zitto Kabwe

"Leo Serikali ya Rais John Magufuli ilipangiwa kuwasilisha Mpango huo wa Maendeleo wa miaka 5. Imeshindwa. Imeleta mwelekeo wa Mpango. Haikuleta sheria na Kamati ya Bajeti Imeleta maelezo yake kuhusu Mpango wa Maendeleo wa mwaka mmoja ilhali hakuna Mpango wa Miaka 5. 

"Mwenyekiti Chenge alitaka wabunge wajadili kwa mujibu wa kanuni ya 94 ambayo kimsingi ni Kanuni inayohusu Mpango wa mwaka mmoja. Serikali imejichanganya. Uongozi wa Bunge umechanganyikiwa." Aliongeza Zitto Kabwe

Zitto Kabwe alimaliza kwa kusema kuwa ni aibu kubwa kwa serikali inayojinasibu kwa kauli ya "Hapa kazi tu"

"Bunge linapaswa kuagiza Serikali ikalete Mpango wa Maendeleo wa miaka 5 ili uidhinishwe na utungiwe Sheria kabla ya kuanza kujadili mipango ya mwaka mmoja mmoja.

"Ni aibu kubwa kwa Serikali ya ‪#‎HapaKaziTu‬ kushindwa kuleta Bungeni Mpango wake wa Maendeleo wa miaka 5 na hata ule wa mwaka wake wa kwanza. Itapangaje bajeti zake? Itatekeleza vipi ilani yake? Kuongoza nchi sio kutumbua majipu tu, ni kuendesha nchi." Alimaliza Zitto Kabwe.

Shughuli ya kwanza ya Serikali baada ya uchaguzi ni kuwasilisha Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano ( kutafsiri ilani...
Posted by Zitto Kabwe on Friday, January 29, 2016

Chenge Awapa Somo Wabunge Kuhusu Matumizi ya Kanuni Za Bunge....Ni Baada ya Saed Kubenea Kuomba Mwongozo kuhusu Wabunge wa Kike Kuvuliwa Nguo

$
0
0

Mwenyekiti wa kikao cha Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge maarufu kwa jina la Mtemi amewataka wabunge kujifunza kwa umakini namna bora ya kutumia kanuni za Bunge.

Mwenyekiti Chenge amefanya hivyo mara kadhaa alipokuwa akijibu miongozo ya wabunge kutoka vyama vya upinzani wakiwamo Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (CHADEMA), Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT) pamoja na Mbunge wa Singida Magharibi Tundu Lissu (CHADEMA).

Kwa upande wa kubenea aliomba muongozo kuhusu mbwa walioingizwa Bungeni, askari polisi kuwavua nguo za ndani wabunge wa kike pamoja na shanga na Hereni zao  jambo ambalo haliruhusiwi ambapo Mwenyekiti wa Bunge alimtaka mbunge huyo kutafuta kanuni nyingine ya kupeleka ombi lake kama anadhani hoja yake ni ya msingi.

Kwa upande wa Lissu pamoja na Zitto wenyewe waliomba miongozo kuhusu mpango wa serikali wa miaka mitano uliowasilishwa na serikali kupitia wizara ya fedha,kwamba umekiuka kanuni za bunge,ambapo mwenyekiti aliwajibu kwamba mpango haujakiuka na si mara ya kwanza kufanya hivyo na akaahidi kutoa  majibu baadae.

Aidha Mwenyekiti  huyo wa Bunge alitoa rai kwa wabunge wote kuzisoma kanuni za bunge na kuzielewa na mipaka yake katika namna bora ya kuendesha vikao hivyo vya Bunge.

Hata hivyo Kikao cha bunge kimeendelea kama kawaida na shughuli zake huku wabunge wa kambi rasmi ya upinzani wakirejea baada ya kugoma kushiriki katika mjadala wa kuijadili hotuba ya Rais kwa kigezo cha shirika la utangazaji la Taifa kutorusha matangazo ya moja kwa moja kuhusiana na mijadala hiyo.

BAWATA Waunga Mkono Tamko la Serikali

$
0
0

Baraza la Waganga Tanzania (BAWATA) wameunga mkono tamko la Serikali la kukataza waganga wa tiba asili kujitangaza katika vyombo vya habari.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Waganga Tanzania Shaka Mohamed Shaka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji huduma ya tiba asili nchini.

‘’Sisi kama Baraza la Waganga Tanzania tukishirikiana na Serikali tunatoa wito kwa vyombo vya habari wasitoe matangazo ya waganga wa tiba asili kwakua jambo hili ni kosa kwa mujibu wa sheria”alisema Shaka.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza hilo David Witekye ameiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania (SHIVYATIATA) Abdulraham Lutenga kwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari bila kushirikiana na kamati yake tendaji wala vyama vinavyounda shirikisho hilo na kuwatetea wafanyabiashara wa tiba asili ambao wamejivika kilemba cha utabibu asili.

“Kwa niaba ya BAWATA, tunaiomba radhi Serikali kutokana na tamko la Mwenyekiti wa SHIVYATIATA kupinga tamko la Serikali, tunaamini lile ni tamko lake binafsi na sio la shirikisho”. alisema Wiketye.

Ameongeza kuwa,wameafiki tamko la Serikali kuhusu upimaji na usajili wa dawa asili na  kupendekeza  zoezi hili kuangaliwa upya ili kuwezesha watabibu asilia kumudu gharama hizo.

Tamko hilo lilitolewa baada ya kujitokeza kwa changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoa huduma wa tiba za  asili kutozingatia Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali inayohusu afya ya jamii.

LHRC Yaitaka Serikali Kuheshimu Haki ya Watanzania Kupata Taarifa, Yalaani Wabunge Kudhalilishwa na Mbwa wa Polisi

$
0
0

Serikali imetakiwa kuheshimu haki ya kikatiba ya kuwapa wananchi habari na taarifa muhimu zinazowahusu bila ya kujali gharama za taarifa hizo kwa kuwa ni jukumu lake kufanya hivyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na kituo cha sheria na haki za binadamu kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wake Bi. Imelda Urio na kuongeza kuwa kusitishwa baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge kwa kisingizio cha gharama ni kitendo cha makusudi kwa kuwanyima wananchi taarifa muhimu toka kwa wawakilishi wao ambao ni wabunge.

Bi Imelda Urio ameongeza kuwa muhimili wa bunge na viongozi wake lazima wafanye kazi kiueledi na kuzuia mianya ya kuingiliwa na mihimili mingine hususani serikali.

Aidha LHRC imelaani vikali kitengo cha kuzalilishwa kwa wabunge kwa kutolewa bungeni na mbwa wa jeshi la polisi,

Kwa upande wa kaimu mkurugenzi wa utetezi na maboresho Bi. Anna Henga yeye amesema kuwa haki yoyote haina gharama na ni jukumu la serikali kulipia gharama hizo za matangazo ya bunge.

TRA Yasitisha Upokeaji Wa Maombi Ya Nafasi Za Kazi

$
0
0

ISO 9001:2008 CERTIFIED
KUSITISHWA KWA MUDA UWASILISHWAJI WA MAOMBI YA KAZI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitoa tangazo la nafasi za kazi katika magazeti mbalimbali ambapo waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi kupitia tovuti ya TRA.
 
Kutokana na maombi ya nafasi za kazi kuingiliana na shughuli za kulipa kodi mwisho wa mwezi kupitia tovuti, TRA inasitisha kwa muda upokeaji wa maombi ya kazi kupitia tovuti hadi Jumanne tarehe mbili Februari 2016 ili kuruhusu ulipaji wa kodi uendelee bila usumbufu.
 
Pia TRA imeongeza muda wa kupokea maombi hadi tarehe 17 Februari 2016.
 
Waombaji wote wa nafasi za kazi zilizotangazwa wanaombwa kutuma maombi yao kuanzia Jumanne tarehe mbili Februari 2016.
 
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya.
 
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:
kituo cha huduma kwa wateja- 
08000780078, 0800750075, 0713800333

Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA-Makao Makuu

Rais Magufuli Amteua Paul Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi

$
0
0
==>Paul Chagonja

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wawili wa mikoa ya Mwanza na Katavi ili kujaza nafasi za Makatibu Tawala wa mikoa hiyo.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Rais amemteua Kamishna wa Polisi, Clodwing Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Faisal Issa ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Mtweve alikuwa Kamishna wa fedha na Utawala wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Balozi Sefue amesema Rais Magufuli pia amemteua Kamishna wa polisi Paul Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi ambako anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Madeni Kipande ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Kabla ya Uteuzi huo, Kamishna Chagonja alikuwa Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Aidha, Balozi Ombeni Sefue amesema Rais Magufuli ameamua kuwateua Makamishna hawa wa Polisi kama alivyowateua Majenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania kuwa Makatibu Wakuu wa Wizara, kwa lengo la kujenga nidhamu katika utumishi wa umma.

Makamishna Clodwing Mtweve na Paul Chagonja pamoja na Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim ambaye ameteuliwa kuwa Balozi Mpya wa Kuwait, wataapishwa kesho Jumamosi tarehe 30 Januari, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, saa nne asubuhi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam.
29 Januari, 2016

Serikali Yakubaliana na Hoja ya Zitto Kabwe......Yauondoa Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano Bungeni

$
0
0

Serikali imeamua kuondoa hoja yake ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano iliyokuwa imeuawasilisha mapema leo bungeni baada ya kudaiwa kuwa kilichowasilishwa hakikuwa mpango wa miaka mitano bali mwelekeo wa mpango wa mwaka mmoja.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya wabunge Tundu Lissu na Zitto Kabwe kupinga mjadala wa hoja hiyo katika kikao cha leo mchana kuwa hakuna haja ya kuendelea na mjadala hadi serikali ipeleke mpango wa miaka mitano ukiambatana na muswada wa sheria husika.

Katika kikao hicho, ilipelekea mwenyekiti wa bunge Andrew Chenge kuahirisha kikao baada ya kambi ya upinzani kugoma kutoa maoni yake kupitia kwa mbunge David Silinde, na kupangwa kikao hicho kingeendelea jioni.

Katika kikao cha jioni, Mwenyekiti wa bunge alilazimika kuahirisha bunge hadi Jumatatu ijayo baada serikali kukubali kuondoa hoja yake kwa ajili ya kujipanga upya.

Umoja wa Vijana Chadema Wampa siku Tatu Rais Magufuli

$
0
0

BARAZA la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kwa kushirikiana na Umoja wa wanafunzi wa vyuo vikuu Chadema (Chaso) wametoa siku tatu kwa Rais John Magufuli kufuta agizo la Shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) kutokurusha moja kwa moja mikutano ya Bunge inayoendelea Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi Taifa Bavicha Edward Simbeyi amesema, kitendo kilichofanywa na Serikali ni udikteta na kwamba, inawanyima wananchi kupata haki yao ya msingi.

“Tunajiuliza maswali mengi, ni vitu gani wanataka kuficha? Hadi wananchi wasivijue? Wakati Bunge linatakiwa kuwa masaa matano na dakika 45 sasa kwanini wanataka kurusha ndani ya saa moja? Haya masaa manne yanaenda wapi? Amehoji Simbeyi."

Amesema hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara yake ya 18 inatoa uhuru wa kila raia kupata au kupewa habari bila ya mashariti kama haya tunayoletewa leo.

“Wanaiogopa mijala inayoendelea Bungeni, Serikali yoyote inayoogopa kukosolewa lazima itakuwa na mapungufu yake, tunachohitaji ni mikutano uoneshwe live kila mtu ajue kinachoendelea” amesema Simbeyi.

Mbali na hilo, wameitaka serikali kutotumia ubabe ndani ya Bunge kwa lengo la kutaka kuwadhalilisha wabunge wa upinzani, pia Jeshi la polisi lizingatie maadili katika utendaji wao wa kazi na wasikubaliane na kila wanalotumwa na CCM hata kama linavunja sheria.

Amesema kitendo cha Jeshi la polisi kujiingiza katika masuala ya kisiasa ni kujidhalilisha wao wenyewe na ni hali inayoendelea kuwafanya kupoteza uaminifu wao ndani ya jamii.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Januari 30

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images